UEFA kufungua uchunguzi wa tuhuma za ubaguzi wa rangi katika kesi ya Vinicius na Prestianni.

UEFA imetangaza kuwa iko tayari kufungua uchunguzi rasmi kuhusiana na tuhuma za ubaguzi wa rangi zinazomhusisha Mchezaji wa Real Madrid, Vinícius Júnior, na wa Benfica, Gianluca Prestianni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na kituo cha redio cha Hispania, Cadena SER kupitia kipindi cha michezo cha El Larguero, uchunguzi huo unatarajiwa kuanza kwa kuhoji Wachezaji wote waliokuwepo Uwanjani wakati wa tukio hilo.

Chanzo hicho kimenukuliwa kikisema, “Kesi itafunguliwa kwa kuwaita Wachezaji wote ili waripoti mambo yote waliyosikia na kuyaona Uwanjani.”

Hata hivyo, taarifa hiyo imeonya kuwa mchakato huo unaweza kuwa mgumu iwapo ushahidi wa moja kwa moja hautapatikana. Chanzo hicho kimeongeza kwa kusema, “Itakuwa vigumu kutoa uamuzi ikiwa tusi la kibaguzi na matusi ya moja kwa moja hayawezi kuthibitishwa.”

Kwa mujibu wa taratibu za kinidhamu za UEFA, uchunguzi wa aina hii hulenga kukusanya ushahidi wa sauti, picha, pamoja na ushuhuda wa mashahidi ili kubaini iwapo kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni za maadili na nidhamu za mashindano ya Ulaya.

Tukio hilo limeibua mjadala mpana katika ulimwengu wa soka, hasa katika kipindi ambacho juhudi za kupambana na ubaguzi wa rangi Viwanjani zimekuwa zikipewa kipaumbele katika mashindano ya kimataifa.

Uamuzi wa mwisho wa UEFA utategemea uzito wa ushahidi utakao wasilishwa katika uchunguzi huo.

Toa maoni yako
#Sports
#Habari
UEFA kufungua uchunguzi wa tuhuma za ubaguzi wa rangi katika kesi ya Vinicius na Prestianni. UEFA imetangaza kuwa iko tayari kufungua uchunguzi rasmi kuhusiana na tuhuma za ubaguzi wa rangi zinazomhusisha Mchezaji wa Real Madrid, Vinícius Júnior, na wa Benfica, Gianluca Prestianni. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na kituo cha redio cha Hispania, Cadena SER kupitia kipindi cha michezo cha El Larguero, uchunguzi huo unatarajiwa kuanza kwa kuhoji Wachezaji wote waliokuwepo Uwanjani wakati wa tukio hilo. Chanzo hicho kimenukuliwa kikisema, “Kesi itafunguliwa kwa kuwaita Wachezaji wote ili waripoti mambo yote waliyosikia na kuyaona Uwanjani.” Hata hivyo, taarifa hiyo imeonya kuwa mchakato huo unaweza kuwa mgumu iwapo ushahidi wa moja kwa moja hautapatikana. Chanzo hicho kimeongeza kwa kusema, “Itakuwa vigumu kutoa uamuzi ikiwa tusi la kibaguzi na matusi ya moja kwa moja hayawezi kuthibitishwa.” Kwa mujibu wa taratibu za kinidhamu za UEFA, uchunguzi wa aina hii hulenga kukusanya ushahidi wa sauti, picha, pamoja na ushuhuda wa mashahidi ili kubaini iwapo kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni za maadili na nidhamu za mashindano ya Ulaya. Tukio hilo limeibua mjadala mpana katika ulimwengu wa soka, hasa katika kipindi ambacho juhudi za kupambana na ubaguzi wa rangi Viwanjani zimekuwa zikipewa kipaumbele katika mashindano ya kimataifa. Uamuzi wa mwisho wa UEFA utategemea uzito wa ushahidi utakao wasilishwa katika uchunguzi huo. Toa maoni yako #Sports #Habari
0 Comments 0 Shares 13 Views