Upgrade to Pro

Ilinichukua miezi sita kutulia Man Utd - Onana


Kipa wa Manchester United Andre Onana anasema ilimchukua miezi sita "kutulia" Old Trafford.

United walilipa £47.2m kumsajili Onana kutoka Inter Milan mwezi Julai kuchukuwa nafasi ya kipa Mhispania David de Gea.

Hata hivyo, licha ya matarajio makubwa juu ya ujio wake, mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon alifungwa kwa umbali wa yadi 50 katika mechi yake ya kwanza Old Trafford dhidi ya Lens na kisha akafanya makosa kadhaa ambayo yalichangia klabu hiyo kutofanya vizuri katika Ligi Kuu na kuondolewa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.

Uchezaji wa Onana haukuimarika sana hadi aliporejea kutoka Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Februari na ingawa amefanya makosa ya ajabu, sasa anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji wa kutegemewa wa kikosi cha meneja Erik ten Hag watakapoelekea Jumamosi

Fainali ya Kombe la FA dhidi ya wapinzani Manchester City (15:00 BST). “Nilifika nikiwa kipa bora zaidi duniani na ‘boom’ ilishuka.

Ilikuwa kama ‘nini kilitokea?’,” alisema kijana huyo mwenye umri wa miaka 28. “Lakini hivyo ndivyo soka linavyokuwa gumu wakati mwingine.

Inategemea kama unataka kukaa chini na kulia au kusimama na kupigana.

Najua nilichokifanya kufika hapa. Najua mimi ni nani. Niliamua kusimama na kupigana.”
#Sports view
🩸Ilinichukua miezi sita kutulia Man Utd - Onana Kipa wa Manchester United Andre Onana anasema ilimchukua miezi sita "kutulia" Old Trafford. United walilipa £47.2m kumsajili Onana kutoka Inter Milan mwezi Julai kuchukuwa nafasi ya kipa Mhispania David de Gea. Hata hivyo, licha ya matarajio makubwa juu ya ujio wake, mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon alifungwa kwa umbali wa yadi 50 katika mechi yake ya kwanza Old Trafford dhidi ya Lens na kisha akafanya makosa kadhaa ambayo yalichangia klabu hiyo kutofanya vizuri katika Ligi Kuu na kuondolewa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa. Uchezaji wa Onana haukuimarika sana hadi aliporejea kutoka Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Februari na ingawa amefanya makosa ya ajabu, sasa anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji wa kutegemewa wa kikosi cha meneja Erik ten Hag watakapoelekea Jumamosi Fainali ya Kombe la FA dhidi ya wapinzani Manchester City (15:00 BST). “Nilifika nikiwa kipa bora zaidi duniani na ‘boom’ ilishuka. Ilikuwa kama ‘nini kilitokea?’,” alisema kijana huyo mwenye umri wa miaka 28. “Lakini hivyo ndivyo soka linavyokuwa gumu wakati mwingine. Inategemea kama unataka kukaa chini na kulia au kusimama na kupigana. Najua nilichokifanya kufika hapa. Najua mimi ni nani. Niliamua kusimama na kupigana.” #Sports view
Like
Love
8
1 Comments ·146 Views