• Nchi ya Kenya yakemea vitendo vya kuwapeleka Vijana wake kwenye vita Nchini Ukraine.

    Serikali ya Kenya imekemea vikali vitendo vya baadhi ya Mawakala wanaodanganya Vijana kwa ahadi za ajira, kisha kuwapeleka moja kwa moja kwenye vita vinavyoendelea nchini Ukraine.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Musalia Mudavadi, amesema: “Tunatarajia kufanya ziara rasmi mjini Moscow kwa mazungumzo na Serikali ya Urusi, lengo likiwa kusitisha kabisa matumizi ya raia wa Kenya katika mapambano haya.”

    Mudavadi alibainisha kuwa tayari Wakenya kadhaa wamefariki dunia, huku wengine wakijeruhiwa vibaya baada ya kudanganywa kuingia mikataba ya kijeshi. Amesema: “Hatukubali upotevu wa maisha ya raia wetu. Hatua za kudumu lazima zichukuliwe.”

    Serikali ya Kenya imelaumu Mawakala wa ajira wanaoshawishi vijana kwa ahadi za mishahara mikubwa, kisha kuwapeleka mstari wa mbele vitani. Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la habari la Ufaransa, Agence France-Presse, imethibitisha kuwepo kwa mtandao wa udanganyifu unaowaingiza vijana wasiokuwa na historia ya kijeshi kusaini mikataba na Jeshi la Urusi, kisha kupelekwa haraka kwenye Uwanja wa mapambano.

    Mudavadi amesisitiza kuwa Kenya itafuatilia pia suala la kuachiliwa kwa Wakenya waliokamatwa kama wafungwa wa kivita nchini Ukraine. Amesema hatua hizi ni muhimu ili kulinda maisha ya Raia wake.

    Toa maoni yako
    #Habari
    #Russia #Ukraine #MusaliaMudavadi #Moscow #BreakingNews #WorldNews #VitaUkraine #KenyaAbroad #HumanRights #AfricaNews
    Nchi ya Kenya yakemea vitendo vya kuwapeleka Vijana wake kwenye vita Nchini Ukraine. Serikali ya Kenya imekemea vikali vitendo vya baadhi ya Mawakala wanaodanganya Vijana kwa ahadi za ajira, kisha kuwapeleka moja kwa moja kwenye vita vinavyoendelea nchini Ukraine. Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Musalia Mudavadi, amesema: “Tunatarajia kufanya ziara rasmi mjini Moscow kwa mazungumzo na Serikali ya Urusi, lengo likiwa kusitisha kabisa matumizi ya raia wa Kenya katika mapambano haya.” Mudavadi alibainisha kuwa tayari Wakenya kadhaa wamefariki dunia, huku wengine wakijeruhiwa vibaya baada ya kudanganywa kuingia mikataba ya kijeshi. Amesema: “Hatukubali upotevu wa maisha ya raia wetu. Hatua za kudumu lazima zichukuliwe.” Serikali ya Kenya imelaumu Mawakala wa ajira wanaoshawishi vijana kwa ahadi za mishahara mikubwa, kisha kuwapeleka mstari wa mbele vitani. Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la habari la Ufaransa, Agence France-Presse, imethibitisha kuwepo kwa mtandao wa udanganyifu unaowaingiza vijana wasiokuwa na historia ya kijeshi kusaini mikataba na Jeshi la Urusi, kisha kupelekwa haraka kwenye Uwanja wa mapambano. Mudavadi amesisitiza kuwa Kenya itafuatilia pia suala la kuachiliwa kwa Wakenya waliokamatwa kama wafungwa wa kivita nchini Ukraine. Amesema hatua hizi ni muhimu ili kulinda maisha ya Raia wake. Toa maoni yako #Habari #Russia #Ukraine #MusaliaMudavadi #Moscow #BreakingNews #WorldNews #VitaUkraine #KenyaAbroad #HumanRights #AfricaNews
    0 Yorumlar 2 hisse senetleri 63 Views