• Stress-Free Airport Travel for Seniors

    Make every journey comfortable with our Senior Citizen Travel Support.
    We provide wheelchair assistance, meet & assist service, baggage help, and priority airport support for a smooth travel experience.

    Book Senior Travel Assistance Today!
    www.jodogoairportassist.com
    +1(325) 225 5550

    #SeniorTravelSupport #AirportAssist #WheelchairAssistance #SeniorFriendlyTravel
    #AirportAssistance #LHR #DXB #AUH #LAX #ICN #DFW #ORD #DEL #MIA #Jeddah #RUH #EWR #JFK #MobilitySupport #TravelWithCare #HassleFreeTravel #AirportSupport #JodogoAirportAssist
    ✈️ Stress-Free Airport Travel for Seniors Make every journey comfortable with our Senior Citizen Travel Support. We provide wheelchair assistance, meet & assist service, baggage help, and priority airport support for a smooth travel experience. Book Senior Travel Assistance Today! 🌐 www.jodogoairportassist.com 📞 +1(325) 225 5550 #SeniorTravelSupport #AirportAssist #WheelchairAssistance #SeniorFriendlyTravel #AirportAssistance #LHR #DXB #AUH #LAX #ICN #DFW #ORD #DEL #MIA #Jeddah #RUH #EWR #JFK #MobilitySupport #TravelWithCare #HassleFreeTravel #AirportSupport #JodogoAirportAssist ✈️
    0 Commentarios 0 Acciones 31 Views
  • Mapigano Kaskazini na Kusini mwa Kivu yazidi kupamba moto.

    Katika hali ya mzozo unaoendelea Kivu, Waasi wa M23 ARC/AFC-Alliance Fleuve Congo wamezindua operesheni ya kulipiza kisasi dhidi ya nafasi za FARDC na washirika wake wa Wazalendo. Ripoti zinaonyesha kuwa Waasi hao wamefanikiwa kuchukua udhibiti wa baadhi ya maeneo, ikiwemo Luke, Katobotobo na Kasenyi, huku mapigano yakiendelea huko Kasinga, Mkoani Sud-Kivu.

    Taarifa rasmi kutoka vyanzo vya ulinzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinaeleza kwamba, “Wanajeshi wetu wanatumia drones kushambulia Rugezi, eneo lililopo kwenye milima ya Minembwe, Kusini mwa Kivu.” Hii inathibitisha kuwa jeshi linajitahidi kudhibiti hali ya usalama katika maeneo tofauti, hasa kusini mwa mkoa wa Kivu, huku mashambulizi ya drone yakiendelea.

    Hali hii inaashiria ongezeko la ukali wa mapigano Kivu, ambapo pande zote zinajaribu kupata udhibiti wa maeneo muhimu, huku wananchi wakikabiliwa na hatari ya usalama wa maisha na mali zao.

    Mapigano Kaskazini na Kusini mwa Kivu yazidi kupamba moto. Katika hali ya mzozo unaoendelea Kivu, Waasi wa M23 ARC/AFC-Alliance Fleuve Congo wamezindua operesheni ya kulipiza kisasi dhidi ya nafasi za FARDC na washirika wake wa Wazalendo. Ripoti zinaonyesha kuwa Waasi hao wamefanikiwa kuchukua udhibiti wa baadhi ya maeneo, ikiwemo Luke, Katobotobo na Kasenyi, huku mapigano yakiendelea huko Kasinga, Mkoani Sud-Kivu. Taarifa rasmi kutoka vyanzo vya ulinzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinaeleza kwamba, “Wanajeshi wetu wanatumia drones kushambulia Rugezi, eneo lililopo kwenye milima ya Minembwe, Kusini mwa Kivu.” Hii inathibitisha kuwa jeshi linajitahidi kudhibiti hali ya usalama katika maeneo tofauti, hasa kusini mwa mkoa wa Kivu, huku mashambulizi ya drone yakiendelea. Hali hii inaashiria ongezeko la ukali wa mapigano Kivu, ambapo pande zote zinajaribu kupata udhibiti wa maeneo muhimu, huku wananchi wakikabiliwa na hatari ya usalama wa maisha na mali zao.
    0 Commentarios 0 Acciones 174 Views
  • Area Codes 305 & 786 cover Miami, FL and nearby cities. This guide breaks down their location, timezone (Eastern Time), major communities served, and what these area codes mean for calls and messages. Visit- https://www.messageblink.com/area-code-305-786-miami-florida/
    Area Codes 305 & 786 cover Miami, FL and nearby cities. This guide breaks down their location, timezone (Eastern Time), major communities served, and what these area codes mean for calls and messages. Visit- https://www.messageblink.com/area-code-305-786-miami-florida/
    0 Commentarios 0 Acciones 67 Views
  • PSG ilitoa Ofa ya €250 milioni kwa Lamine Yamal, Barcelona wakataa - Laporta afunguka.

    Rais wa klabu ya FC Barcelona, Joan Laporta, ameweka wazi kuwa klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) iliwahi kuwasilisha ofa nono ya euro milioni 250 kwa ajili ya kinda nyota Lamine Yamal lakini Barca waliikataa bila kusita.

    Akizungumza kuhusu tukio hilo, Laporta amesema ofa hiyo iliwasilishwa takribani miaka miwili iliyopita wakati Yamal akiwa na umri wa miaka 17 pekee.

    “Lamine alikuwa na miaka 17, miaka miwili iliyopita… PSG walituma pendekezo la euro milioni 250 na tulisema hapana. Nakumbuka baadhi ya watu walifikiri tulikuwa tumepoteza akili,” ameeleza Laporta.

    Kwa mujibu wa Kiongozi huyo wa Barcelona, uamuzi wa kuikataa ofa hiyo haukuwa wa kifedha bali wa kimkakati na kihistoria. Klabu hiyo inaamini Yamal ni sehemu ya mradi wa muda mrefu wa kurejesha enzi za mafanikio Camp Nou.

    “Kwa sisi, amekuwa asiyeuzwa. Hagusiki,” alisisitiza Laporta.

    Kwa kuzingatia ukubwa wa ofa hiyo, wengi walihoji kama Barcelona walipaswa kukubali kiasi hicho kikubwa cha fedha, hasa katika kipindi ambacho klabu hiyo ilikuwa inapitia changamoto za kifedha. Hata hivyo, maendeleo ya haraka ya Yamal ndani ya kikosi cha kwanza na mchango wake katika mafanikio ya timu yameanza kuhalalisha msimamo wa uongozi.

    Yamal ameonekana kuwa moja ya vipaji adimu vilivyotoka "Akademi" ya La Masia, akionesha utulivu, ubunifu na ujasiri mkubwa licha ya umri wake mdogo.

    Kauli ya Laporta inaashiria wazi kwamba Barcelona haioni thamani ya Yamal kwa mizani ya fedha pekee. Kwao, ni Mrithi wa kizazi kipya cha Nyota wa klabu hiyo, Mchezaji wa kujengwa kuzunguka mradi wa baadaye.

    Katika soko la sasa la uhamisho, euro milioni 250 ni kiwango kinachoweza kubadilisha historia ya klabu yoyote. Lakini kwa Barcelona, Lamine Yamal si bidhaa ya kuuzwa ni alama ya mustakabali wao.

    Toa maoni yako
    #Sports
    PSG ilitoa Ofa ya €250 milioni kwa Lamine Yamal, Barcelona wakataa - Laporta afunguka. Rais wa klabu ya FC Barcelona, Joan Laporta, ameweka wazi kuwa klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) iliwahi kuwasilisha ofa nono ya euro milioni 250 kwa ajili ya kinda nyota Lamine Yamal lakini Barca waliikataa bila kusita. Akizungumza kuhusu tukio hilo, Laporta amesema ofa hiyo iliwasilishwa takribani miaka miwili iliyopita wakati Yamal akiwa na umri wa miaka 17 pekee. “Lamine alikuwa na miaka 17, miaka miwili iliyopita… PSG walituma pendekezo la euro milioni 250 na tulisema hapana. Nakumbuka baadhi ya watu walifikiri tulikuwa tumepoteza akili,” ameeleza Laporta. Kwa mujibu wa Kiongozi huyo wa Barcelona, uamuzi wa kuikataa ofa hiyo haukuwa wa kifedha bali wa kimkakati na kihistoria. Klabu hiyo inaamini Yamal ni sehemu ya mradi wa muda mrefu wa kurejesha enzi za mafanikio Camp Nou. “Kwa sisi, amekuwa asiyeuzwa. Hagusiki,” alisisitiza Laporta. Kwa kuzingatia ukubwa wa ofa hiyo, wengi walihoji kama Barcelona walipaswa kukubali kiasi hicho kikubwa cha fedha, hasa katika kipindi ambacho klabu hiyo ilikuwa inapitia changamoto za kifedha. Hata hivyo, maendeleo ya haraka ya Yamal ndani ya kikosi cha kwanza na mchango wake katika mafanikio ya timu yameanza kuhalalisha msimamo wa uongozi. Yamal ameonekana kuwa moja ya vipaji adimu vilivyotoka "Akademi" ya La Masia, akionesha utulivu, ubunifu na ujasiri mkubwa licha ya umri wake mdogo. Kauli ya Laporta inaashiria wazi kwamba Barcelona haioni thamani ya Yamal kwa mizani ya fedha pekee. Kwao, ni Mrithi wa kizazi kipya cha Nyota wa klabu hiyo, Mchezaji wa kujengwa kuzunguka mradi wa baadaye. Katika soko la sasa la uhamisho, euro milioni 250 ni kiwango kinachoweza kubadilisha historia ya klabu yoyote. Lakini kwa Barcelona, Lamine Yamal si bidhaa ya kuuzwa ni alama ya mustakabali wao. Toa maoni yako #Sports
    0 Commentarios 0 Acciones 271 Views
  • Mnataka awe shabiki wa Yanga Africa mnamlipa? Mjibuni Diwani Kwanza hili Swali ,mnamlipa?

    Maana yake yeye ili awe Shabiki wa Simba Sports au Yanga Africa itategemea tu na wakati huo nani anamlipa??

    Sahauni Kabisa Kuhusu Kuwa baba yake ni Lijendi wa Yanga Africa ,yeye ushabiki wake ni Based on Sasampa tu

    Maana yake Kama Simba Sports wangeendelea Kumpa Mkataba na Kumlipa hakuna namna Leo angejiita Shabiki wa Yanga Africa.

    Tangu Siku ya Kwanza nilisema hapa Sababu iliyotumika Kumleta Yanga ilikuwa ni Makosa .

    Kuwa Shabiki na Mwanachama wa Yanga au Simba Sababu haiwezi Kuwa eti Kwasababu unaichukia Simba au una Mgogoro na Simba and Vice Versa.This is totally wrong.

    Sababu ya Kuwa Shabiki na Mwanachama wa Yanga au Simba Sports haiwezi Kuwa Kwasababu unafanya Kazi Yanga au GSM ,Simba Sports au METL.

    Nina msemo wangu maarufu huwezi Kuwa Shabiki wa Yanga ukiwa na miaka 50. Big Nooo

    Kuwa Shabiki na Mwanachama wa Yanga ni Safari ya Kuwekeza hisia zako. Ni uwajibikaji wa Maisha yako yako yote wakati wa shida na raha.

    So inawezekana Kuna hoja Kwenye baadhi ya Maneno ya Diwani,Lakini nikishasikia anasema yeye ni Shabiki wa Yanga naacha Kumsikiliza hapo hapo .

    Kimsingi Kwa mambo yanavyoelekea Ndugu Yangu Diwani mpaka Sasa hana timu .Manake kule Simba Sports tena nao hawataki hata Kumuona.

    Note; Na najua ndugu yangu mmemnyoa hana ofisi tena Pale Saramander. Kibaya zaidi Kwenye mnuso wa Mtoto wa tajiri napo mmemtosa. Imagine Futari ya Jana Kwa tajiri pia hayumo. I knew for sure he was coming for you .I Knew it

    - Wilson Oruma, Mchambuzi.

    Toa maoni yako
    Mnataka awe shabiki wa Yanga Africa mnamlipa? Mjibuni Diwani Kwanza hili Swali ,mnamlipa? Maana yake yeye ili awe Shabiki wa Simba Sports au Yanga Africa itategemea tu na wakati huo nani anamlipa?? Sahauni Kabisa Kuhusu Kuwa baba yake ni Lijendi wa Yanga Africa ,yeye ushabiki wake ni Based on Sasampa tu Maana yake Kama Simba Sports wangeendelea Kumpa Mkataba na Kumlipa hakuna namna Leo angejiita Shabiki wa Yanga Africa. Tangu Siku ya Kwanza nilisema hapa Sababu iliyotumika Kumleta Yanga ilikuwa ni Makosa . Kuwa Shabiki na Mwanachama wa Yanga au Simba Sababu haiwezi Kuwa eti Kwasababu unaichukia Simba au una Mgogoro na Simba and Vice Versa.This is totally wrong. Sababu ya Kuwa Shabiki na Mwanachama wa Yanga au Simba Sports haiwezi Kuwa Kwasababu unafanya Kazi Yanga au GSM ,Simba Sports au METL. Nina msemo wangu maarufu huwezi Kuwa Shabiki wa Yanga ukiwa na miaka 50. Big Nooo Kuwa Shabiki na Mwanachama wa Yanga ni Safari ya Kuwekeza hisia zako. Ni uwajibikaji wa Maisha yako yako yote wakati wa shida na raha. So inawezekana Kuna hoja Kwenye baadhi ya Maneno ya Diwani,Lakini nikishasikia anasema yeye ni Shabiki wa Yanga naacha Kumsikiliza hapo hapo . Kimsingi Kwa mambo yanavyoelekea Ndugu Yangu Diwani mpaka Sasa hana timu .Manake kule Simba Sports tena nao hawataki hata Kumuona. Note; Na najua ndugu yangu mmemnyoa hana ofisi tena Pale Saramander. Kibaya zaidi Kwenye mnuso wa Mtoto wa tajiri napo mmemtosa. Imagine Futari ya Jana Kwa tajiri pia hayumo. I knew for sure he was coming for you .I Knew it 😅🙌 - Wilson Oruma, Mchambuzi. Toa maoni yako
    0 Commentarios 0 Acciones 250 Views
  • Zelensky asema Putin ameanzisha vita ya tatu ya Dunia.

    Volodymyr Zelensky ametoa kauli nzito akidai kuwa Vladimir Putin tayari ameanzisha Vita ya tatu ya Dunia, akisisitiza kuwa suluhisho pekee ni kuiwekea Urusi shinikizo kali kijeshi na kiuchumi ili kuizuia isisambaze zaidi mgogoro huo.

    Katika mahojiano aliyofanya na BBC Mjini Kyiv, Kiongozi huyo wa Ukraine alieleza kuwa nchi yake haitaanguka mikononi mwa Urusi, bali itaibuka mshindi mwishoni mwa vita. Alisisitiza kuwa Ukraine haiwezi kutoa ardhi yake kama gharama ya amani, hasa ikizingatiwa kuwa majeshi ya Urusi hayajafanikiwa kuiteka kikamilifu licha ya kupeleka wanajeshi wengi vitani.

    “Nafikiri Putin tayari ameanzisha Vita ya Tatu ya Dunia. Swali si tu kwamba ameianzisha, bali ni wapi anaweza kufika na namna gani dunia inaweza kumzuia,” alisema Zelensky.

    Aliongeza kuwa Urusi inalenga kubadili mfumo wa kimataifa na kuwalazimisha watu kuishi katika mfumo ambao hawajauchagua wenyewe.

    Akizungumzia pendekezo la Urusi la kutaka Ukraine ikabidhi takribani asilimia 20 ya maeneo yake, ikiwemo sehemu za Mkoa wa Donetsk na maeneo ya kusini, Zelensky alikataa wazo hilo vikali.

    Kwa mujibu wake, suala hilo halihusu ardhi pekee, bali linahusu maisha ya Raia wa Ukraine na mustakabali wa taifa. Alisema kukubali masharti hayo kungekuwa sawa na kuwasaliti Wananchi na kuipokonya nchi hadhi yake.

    Zelensky ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Moscow pamoja na kuimarisha msaada wa kijeshi kwa Ukraine. Anaamini kuwa presha ya pamoja ndiyo njia pekee ya kuzuia mzozo huo kuenea zaidi na kuathiri usalama wa dunia kwa upana wake.

    Kauli yake inakuja wakati mapigano kati ya Ukraine na Urusi yakiendelea katika maeneo kadhaa ya mashariki na kusini mwa nchi hiyo, huku hali ya kisiasa na kiusalama ikiendelea kuwa tete katika ukanda wa Ulaya Mashariki.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Zelensky asema Putin ameanzisha vita ya tatu ya Dunia. Volodymyr Zelensky ametoa kauli nzito akidai kuwa Vladimir Putin tayari ameanzisha Vita ya tatu ya Dunia, akisisitiza kuwa suluhisho pekee ni kuiwekea Urusi shinikizo kali kijeshi na kiuchumi ili kuizuia isisambaze zaidi mgogoro huo. Katika mahojiano aliyofanya na BBC Mjini Kyiv, Kiongozi huyo wa Ukraine alieleza kuwa nchi yake haitaanguka mikononi mwa Urusi, bali itaibuka mshindi mwishoni mwa vita. Alisisitiza kuwa Ukraine haiwezi kutoa ardhi yake kama gharama ya amani, hasa ikizingatiwa kuwa majeshi ya Urusi hayajafanikiwa kuiteka kikamilifu licha ya kupeleka wanajeshi wengi vitani. “Nafikiri Putin tayari ameanzisha Vita ya Tatu ya Dunia. Swali si tu kwamba ameianzisha, bali ni wapi anaweza kufika na namna gani dunia inaweza kumzuia,” alisema Zelensky. Aliongeza kuwa Urusi inalenga kubadili mfumo wa kimataifa na kuwalazimisha watu kuishi katika mfumo ambao hawajauchagua wenyewe. Akizungumzia pendekezo la Urusi la kutaka Ukraine ikabidhi takribani asilimia 20 ya maeneo yake, ikiwemo sehemu za Mkoa wa Donetsk na maeneo ya kusini, Zelensky alikataa wazo hilo vikali. Kwa mujibu wake, suala hilo halihusu ardhi pekee, bali linahusu maisha ya Raia wa Ukraine na mustakabali wa taifa. Alisema kukubali masharti hayo kungekuwa sawa na kuwasaliti Wananchi na kuipokonya nchi hadhi yake. Zelensky ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Moscow pamoja na kuimarisha msaada wa kijeshi kwa Ukraine. Anaamini kuwa presha ya pamoja ndiyo njia pekee ya kuzuia mzozo huo kuenea zaidi na kuathiri usalama wa dunia kwa upana wake. Kauli yake inakuja wakati mapigano kati ya Ukraine na Urusi yakiendelea katika maeneo kadhaa ya mashariki na kusini mwa nchi hiyo, huku hali ya kisiasa na kiusalama ikiendelea kuwa tete katika ukanda wa Ulaya Mashariki. Toa maoni yako #Habari
    0 Commentarios 0 Acciones 349 Views
  • Trump kutoa hotuba ya Taifa: Je, Ni kipimo cha Chama cha Republican?

    Hii Jumanne, Marekani inatarajia kusikiliza hotuba ya Rais Donald Trump, hotuba ambayo wengi wanaiona kama kipimo cha namna chama chake cha Republican kitakavyoshikilia imani ya wapiga kura kuelekea uchaguzi wa katikati ya muhula.

    Hotuba hii siyo tu ni nafasi ya kuwasilisha mpango wa serikali, bali pia ni fursa ya Trump kuonyesha mwelekeo wa sera na jinsi anavyopanga kushawishi umaarufu wa chama chake katika majimbo yote ya nchi. Ushuru wa kimataifa, ambao ameeleza unaongezwa kutoka asilimia 10 hadi 15, ni moja ya hoja ambazo zitaangaziwa na zitakuwa kipimo cha sera zake za uchumi.

    Hata hivyo, kura za maoni zinaonesha kuwa imani ya wananchi katika baadhi ya majimbo imepungua, kutokana na namna rais Trump alivyosimamia serikali katika muhula wake wa kwanza tangu kurejea madarakani. Hii inafanya hotuba yake kuwa kipimo cha umakini wa umma na nguvu ya chama chake kushikilia uongozi wa Bunge na Seneti.

    Wakati hotuba hii kwa kawaida inatarajiwa kuzungumzia zaidi masuala ya ndani ya nchi, kitisho cha Iran kutokana na mpango wake wa nyuklia kinaweza kuigubika hotuba yote. Trump ameendelea kushinikiza hoja za kuishambulia Iran, jambo linalotarajiwa kuvutia hisia na mjadala mkali nchini na kimataifa.

    Kwa hakika, hotuba ya Jumanne sio tu taarifa kwa taifa, bali ni kioo cha mustakabali wa kisiasa wa Republican na jinsi Rais Trump anavyopanga kuendeleza sera zake katika muhula huu wa pili.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Trump kutoa hotuba ya Taifa: Je, Ni kipimo cha Chama cha Republican? Hii Jumanne, Marekani inatarajia kusikiliza hotuba ya Rais Donald Trump, hotuba ambayo wengi wanaiona kama kipimo cha namna chama chake cha Republican kitakavyoshikilia imani ya wapiga kura kuelekea uchaguzi wa katikati ya muhula. Hotuba hii siyo tu ni nafasi ya kuwasilisha mpango wa serikali, bali pia ni fursa ya Trump kuonyesha mwelekeo wa sera na jinsi anavyopanga kushawishi umaarufu wa chama chake katika majimbo yote ya nchi. Ushuru wa kimataifa, ambao ameeleza unaongezwa kutoka asilimia 10 hadi 15, ni moja ya hoja ambazo zitaangaziwa na zitakuwa kipimo cha sera zake za uchumi. Hata hivyo, kura za maoni zinaonesha kuwa imani ya wananchi katika baadhi ya majimbo imepungua, kutokana na namna rais Trump alivyosimamia serikali katika muhula wake wa kwanza tangu kurejea madarakani. Hii inafanya hotuba yake kuwa kipimo cha umakini wa umma na nguvu ya chama chake kushikilia uongozi wa Bunge na Seneti. Wakati hotuba hii kwa kawaida inatarajiwa kuzungumzia zaidi masuala ya ndani ya nchi, kitisho cha Iran kutokana na mpango wake wa nyuklia kinaweza kuigubika hotuba yote. Trump ameendelea kushinikiza hoja za kuishambulia Iran, jambo linalotarajiwa kuvutia hisia na mjadala mkali nchini na kimataifa. Kwa hakika, hotuba ya Jumanne sio tu taarifa kwa taifa, bali ni kioo cha mustakabali wa kisiasa wa Republican na jinsi Rais Trump anavyopanga kuendeleza sera zake katika muhula huu wa pili. Toa maoni yako #Habari
    0 Commentarios 0 Acciones 364 Views
  • Vita vya M23: Wiki ngumu kwa Waasi katika eneo la Masisi.

    Wiki hii imekuwa ya majaribu makubwa kwa Waasi wa M23 na washirika wao katika eneo la Masisi, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya ndani, makundi hayo yanadaiwa kupata hasara kubwa katika mapigano dhidi ya vikosi vya ndani vinavyopambana nao.

    Leo hii Jumatatu, 23 Februari 2026, Muungano unaojumuisha Wazalendo, CMPDN na Pareco-FF ulitangaza kuwa umefanikiwa kuwaondoa wapiganaji wa M23 katika eneo la Kaniro. Hatua hiyo inaelezwa kuwa ya kimkakati, kwani sasa inawakaribisha wapiganaji hao karibu na Katale-centre, eneo lililo jirani na Masisi-centre.

    Kwa mujibu wa taarifa hizo, mafanikio hayo yanatajwa kuwa sehemu ya operesheni pana inayolenga kuisukuma M23 kutoka katika maeneo wanayodhibiti.

    Wakati huo huo, Mji wa madini wa Rubaya unaripotiwa kuwa karibu kuzingirwa na Wazalendo. Inadaiwa kuwa makundi hayo sasa yanadhibiti barabara na njia kadhaa muhimu zinazoelekea Mjini humo, zikiwemo Kinigi, Kilonge na Kaniro.

    Rubaya inachukuliwa kuwa kitovu muhimu cha uchimbaji madini katika eneo hilo. Taarifa za makadirio zinaonesha kuwa uchimbaji wake huzalisha zaidi ya dola milioni 2.5 za Marekani kwa mwezi, kwa kiwango cha uzalishaji kinachokadiriwa kufikia tani 110 hadi 120 za madini kila mwezi.

    Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, Kamanda wa M23, Sultani Makenga, aliripotiwa kufika Rubaya mapema leo hii Jumatatu kwa lengo la kusimamia binafsi operesheni za kijeshi. Taarifa zinaeleza kuwa kikosi cha M23 kilichokuwa kimepelekwa Kinigi kilisukumwa nyuma hadi Kibabi.

    Kutokana na presha ya mashambulizi, Makenga anadaiwa kushuka mstari wa mbele ili kujaribu kupanga upya vikosi vilivyokuwa vinayumba.

    Hata hivyo, kasi ya Wazalendo inaelezwa kupungua kutokana na uwepo wa silaha nzito za msaada, zikiwemo vipande vya mizinga na chokaa ya milimita 120, zilizowekwa Kalonge. Silaha hizo zinaripotiwa kushambulia maeneo ya Chugi, Kinigi/Bisunzu na Kilonge, jambo linalozuia kusonga mbele kwa haraka kwa wapiganaji wa Wazalendo.

    Kuimarishwa kwa vikosi vya Waasi ndani ya Rubaya kunaonekana kulenga kulinda Mji huo wa kimkakati, hasa kutokana na umuhimu wake wa kiuchumi. Hali ya usalama katika eneo la Masisi bado ni tete, huku pande zote zikijaribu kudhibiti maeneo yenye umuhimu wa kijeshi na kiuchumi.

    Kadri mapigano yanavyoendelea, macho ya wengi yanaelekezwa katika mustakabali wa Rubaya na iwapo Muungano wa Wazalendo utafanikiwa kuudhibiti Mji huo au la.

    Toa maoni yako
    #Habari
    🇨🇩Vita vya M23: Wiki ngumu kwa Waasi katika eneo la Masisi. Wiki hii imekuwa ya majaribu makubwa kwa Waasi wa M23 na washirika wao katika eneo la Masisi, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya ndani, makundi hayo yanadaiwa kupata hasara kubwa katika mapigano dhidi ya vikosi vya ndani vinavyopambana nao. Leo hii Jumatatu, 23 Februari 2026, Muungano unaojumuisha Wazalendo, CMPDN na Pareco-FF ulitangaza kuwa umefanikiwa kuwaondoa wapiganaji wa M23 katika eneo la Kaniro. Hatua hiyo inaelezwa kuwa ya kimkakati, kwani sasa inawakaribisha wapiganaji hao karibu na Katale-centre, eneo lililo jirani na Masisi-centre. Kwa mujibu wa taarifa hizo, mafanikio hayo yanatajwa kuwa sehemu ya operesheni pana inayolenga kuisukuma M23 kutoka katika maeneo wanayodhibiti. Wakati huo huo, Mji wa madini wa Rubaya unaripotiwa kuwa karibu kuzingirwa na Wazalendo. Inadaiwa kuwa makundi hayo sasa yanadhibiti barabara na njia kadhaa muhimu zinazoelekea Mjini humo, zikiwemo Kinigi, Kilonge na Kaniro. Rubaya inachukuliwa kuwa kitovu muhimu cha uchimbaji madini katika eneo hilo. Taarifa za makadirio zinaonesha kuwa uchimbaji wake huzalisha zaidi ya dola milioni 2.5 za Marekani kwa mwezi, kwa kiwango cha uzalishaji kinachokadiriwa kufikia tani 110 hadi 120 za madini kila mwezi. Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, Kamanda wa M23, Sultani Makenga, aliripotiwa kufika Rubaya mapema leo hii Jumatatu kwa lengo la kusimamia binafsi operesheni za kijeshi. Taarifa zinaeleza kuwa kikosi cha M23 kilichokuwa kimepelekwa Kinigi kilisukumwa nyuma hadi Kibabi. Kutokana na presha ya mashambulizi, Makenga anadaiwa kushuka mstari wa mbele ili kujaribu kupanga upya vikosi vilivyokuwa vinayumba. Hata hivyo, kasi ya Wazalendo inaelezwa kupungua kutokana na uwepo wa silaha nzito za msaada, zikiwemo vipande vya mizinga na chokaa ya milimita 120, zilizowekwa Kalonge. Silaha hizo zinaripotiwa kushambulia maeneo ya Chugi, Kinigi/Bisunzu na Kilonge, jambo linalozuia kusonga mbele kwa haraka kwa wapiganaji wa Wazalendo. Kuimarishwa kwa vikosi vya Waasi ndani ya Rubaya kunaonekana kulenga kulinda Mji huo wa kimkakati, hasa kutokana na umuhimu wake wa kiuchumi. Hali ya usalama katika eneo la Masisi bado ni tete, huku pande zote zikijaribu kudhibiti maeneo yenye umuhimu wa kijeshi na kiuchumi. Kadri mapigano yanavyoendelea, macho ya wengi yanaelekezwa katika mustakabali wa Rubaya na iwapo Muungano wa Wazalendo utafanikiwa kuudhibiti Mji huo au la. Toa maoni yako #Habari
    0 Commentarios 0 Acciones 357 Views
  • Familia ya Kiongozi wa upinzani wa Uganda Bobi Wine yafunguka kukimbia Nchi kufuatia matukio ya siasa na usalama.

    Katika taarifa iliyotolewa, Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kama Bobi Wine, amethibitisha mbele ya Wakaguzi wa haki za binadamu Mjini Geneva kwamba Mke wake, Barbie Itungo Kyagulanyi, na Watoto wao wametoka Uganda kwa sababu za hofu ya maisha yao kufuatia hali tete inayojitokeza nchini mwao baada ya uchaguzi wa Rais.

    Katika hotuba yake kupitia video mbele ya Geneva Summit for Human Rights and Democracy, Bobi Wine alisema wazi: “Mke wangu na Watoto walilazimika kukimbia nchi kwa hofu ya maisha yao.” - Bobi Wine.

    Alifafanua kuwa usalama wa familia yake uliathirika sana kutokana na operesheni za vikosi vya usalama zilizoendelea mara tu baada ya uchaguzi wa 15 Januari 2026, ambapo serikali ilitangaza ushindi wa Rais Yoweri Museveni ambayo Bobi Wine ameipinga kwa madai ya udanganyifu wa kura na ukandamizaji wa upinzani.

    Bobi Wine pia alidai kwamba vikosi vya usalama: “Vilivamia nyumba yangu, vikamtesa Mke wangu, kumfanya asiwe na chaguo ila kuondoka na Watoto wakiwa nje ya nchi.” amesema

    Habari kwamba familia yake imeondoka Uganda na si tu kutoroka nyumba yao ya Magere imetolewa mara tu baada ya miezi ya mvutano mkali, ikiwa ni pamoja na madai ya mashambulizi, ulinzi mkali wa nyumba yao na vitisho vilivyowekwa na baadhi ya Afisa wa usalama.

    Katika maneno yake Mjini Geneva, Bobi Wine pia alijumuisha ombi kwa Jumuiya ya kimataifa kuhusu hatua za kulinda haki za binadamu na kuzuia ukandamizaji wa upinzani nchini Uganda.

    Taarifa hii inakuja katika wakati ambapo Uganda iko chini ya uangalizi wa kimataifa kufuatia ripoti za ghasia, mashambulizi dhidi ya wapinzani wa kisiasa, na madai ya upendeleo wa vyombo vya usalama kuelekea chama tawala.

    Kwa sasa, bado haijafahamika kwa umma ni nchi gani hasa Barbie Itungo Kyagulanyi na Watoto hao wamekwenda, ila uamuzi wao wa kukimbia unachukuliwa kama hatua ya kulinda usalama wa familia katika mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Uganda.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Familia ya Kiongozi wa upinzani wa Uganda Bobi Wine yafunguka kukimbia Nchi kufuatia matukio ya siasa na usalama. Katika taarifa iliyotolewa, Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kama Bobi Wine, amethibitisha mbele ya Wakaguzi wa haki za binadamu Mjini Geneva kwamba Mke wake, Barbie Itungo Kyagulanyi, na Watoto wao wametoka Uganda kwa sababu za hofu ya maisha yao kufuatia hali tete inayojitokeza nchini mwao baada ya uchaguzi wa Rais. Katika hotuba yake kupitia video mbele ya Geneva Summit for Human Rights and Democracy, Bobi Wine alisema wazi: “Mke wangu na Watoto walilazimika kukimbia nchi kwa hofu ya maisha yao.” - Bobi Wine. Alifafanua kuwa usalama wa familia yake uliathirika sana kutokana na operesheni za vikosi vya usalama zilizoendelea mara tu baada ya uchaguzi wa 15 Januari 2026, ambapo serikali ilitangaza ushindi wa Rais Yoweri Museveni ambayo Bobi Wine ameipinga kwa madai ya udanganyifu wa kura na ukandamizaji wa upinzani. Bobi Wine pia alidai kwamba vikosi vya usalama: “Vilivamia nyumba yangu, vikamtesa Mke wangu, kumfanya asiwe na chaguo ila kuondoka na Watoto wakiwa nje ya nchi.” amesema Habari kwamba familia yake imeondoka Uganda na si tu kutoroka nyumba yao ya Magere imetolewa mara tu baada ya miezi ya mvutano mkali, ikiwa ni pamoja na madai ya mashambulizi, ulinzi mkali wa nyumba yao na vitisho vilivyowekwa na baadhi ya Afisa wa usalama. Katika maneno yake Mjini Geneva, Bobi Wine pia alijumuisha ombi kwa Jumuiya ya kimataifa kuhusu hatua za kulinda haki za binadamu na kuzuia ukandamizaji wa upinzani nchini Uganda. Taarifa hii inakuja katika wakati ambapo Uganda iko chini ya uangalizi wa kimataifa kufuatia ripoti za ghasia, mashambulizi dhidi ya wapinzani wa kisiasa, na madai ya upendeleo wa vyombo vya usalama kuelekea chama tawala. Kwa sasa, bado haijafahamika kwa umma ni nchi gani hasa Barbie Itungo Kyagulanyi na Watoto hao wamekwenda, ila uamuzi wao wa kukimbia unachukuliwa kama hatua ya kulinda usalama wa familia katika mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Uganda. Toa maoni yako #Habari
    0 Commentarios 0 Acciones 433 Views
  • Uingereza yakataa ombi la Trump kutumia kambi zake za kijeshi kushambulia Iran.

    Serikali ya Uingereza imekataa rasmi ombi la Rais wa Marekani, Donald Trump, la kutaka kutumia kambi za kijeshi za Uingereza kama vituo vya kuanzishia mashambulizi yanayoweza kulenga Iran.

    Kwa mujibu wa taarifa za kidiplomasia, ombi hilo lilihusisha matumizi ya kambi muhimu zikiwemo Diego Garcia katika Bahari ya Hindi pamoja na RAF Fairford iliyoko Gloucestershire.

    Vyanzo vya serikali Mjini London vinaeleza kuwa uamuzi huo umechukuliwa kwa kuzingatia maslahi ya kitaifa na tahadhari dhidi ya kuongezeka kwa mvutano wa kijeshi Mashariki ya Kati.

    Msimamo huo unaonyesha kuwa Uingereza haitaki kuhusishwa moja kwa moja na operesheni yoyote ya kijeshi dhidi ya Iran bila mchakato mpana wa kidiplomasia na kibali cha kimataifa.

    Ingawa Marekani na Uingereza ni washirika wakubwa wa kijeshi kupitia Muungano wa NATO, London imeonekana kuchukua tahadhari kubwa katika suala linaloweza kusababisha vita pana katika eneo la Ghuba.

    Kisiwa cha Diego Garcia ni kituo cha kimkakati kinachotumiwa kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Marekani na Uingereza. Kimewahi kutumika kama kitovu cha operesheni za kijeshi katika Mashariki ya Kati, hasa wakati wa vita vya Iraq na Afghanistan.

    Kwa upande mwingine, RAF Fairford imekuwa ikitumika mara kadhaa kupokea ndege za kivita za Marekani, zikiwemo mabomu mazito ya masafa marefu kama B-52.

    Hatua ya Uingereza inaweza kuathiri kwa kiwango fulani uratibu wa kijeshi kati ya Washington na London, hasa wakati ambapo mvutano kati ya Marekani na Iran unaongezeka.

    Hadi sasa, Ikulu ya White House haijatoa tamko rasmi kuhusu msimamo wa Uingereza, huku Wachambuzi wa siasa za kimataifa wakitathmini iwapo uamuzi huo utaashiria tofauti ya kimkakati kati ya washirika hao wawili wa muda mrefu.

    Mvutano kati ya Marekani na Iran umeendelea kuwa tete, hasa katika masuala yanayohusu nyuklia na ushawishi wa kikanda.

    Je, uamuzi wa London utatuliza hali au utaongeza presha za kidiplomasia? Dunia inaendelea kufuatilia kwa karibu.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Uingereza yakataa ombi la Trump kutumia kambi zake za kijeshi kushambulia Iran. Serikali ya Uingereza imekataa rasmi ombi la Rais wa Marekani, Donald Trump, la kutaka kutumia kambi za kijeshi za Uingereza kama vituo vya kuanzishia mashambulizi yanayoweza kulenga Iran. Kwa mujibu wa taarifa za kidiplomasia, ombi hilo lilihusisha matumizi ya kambi muhimu zikiwemo Diego Garcia katika Bahari ya Hindi pamoja na RAF Fairford iliyoko Gloucestershire. Vyanzo vya serikali Mjini London vinaeleza kuwa uamuzi huo umechukuliwa kwa kuzingatia maslahi ya kitaifa na tahadhari dhidi ya kuongezeka kwa mvutano wa kijeshi Mashariki ya Kati. Msimamo huo unaonyesha kuwa Uingereza haitaki kuhusishwa moja kwa moja na operesheni yoyote ya kijeshi dhidi ya Iran bila mchakato mpana wa kidiplomasia na kibali cha kimataifa. Ingawa Marekani na Uingereza ni washirika wakubwa wa kijeshi kupitia Muungano wa NATO, London imeonekana kuchukua tahadhari kubwa katika suala linaloweza kusababisha vita pana katika eneo la Ghuba. Kisiwa cha Diego Garcia ni kituo cha kimkakati kinachotumiwa kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Marekani na Uingereza. Kimewahi kutumika kama kitovu cha operesheni za kijeshi katika Mashariki ya Kati, hasa wakati wa vita vya Iraq na Afghanistan. Kwa upande mwingine, RAF Fairford imekuwa ikitumika mara kadhaa kupokea ndege za kivita za Marekani, zikiwemo mabomu mazito ya masafa marefu kama B-52. Hatua ya Uingereza inaweza kuathiri kwa kiwango fulani uratibu wa kijeshi kati ya Washington na London, hasa wakati ambapo mvutano kati ya Marekani na Iran unaongezeka. Hadi sasa, Ikulu ya White House haijatoa tamko rasmi kuhusu msimamo wa Uingereza, huku Wachambuzi wa siasa za kimataifa wakitathmini iwapo uamuzi huo utaashiria tofauti ya kimkakati kati ya washirika hao wawili wa muda mrefu. Mvutano kati ya Marekani na Iran umeendelea kuwa tete, hasa katika masuala yanayohusu nyuklia na ushawishi wa kikanda. Je, uamuzi wa London utatuliza hali au utaongeza presha za kidiplomasia? Dunia inaendelea kufuatilia kwa karibu. Toa maoni yako #Habari
    0 Commentarios 0 Acciones 561 Views
  • Facebook yatangaza rasmi kufunga App ya Messenger kuanzia April.

    Kampuni ya teknolojia ya META imetangaza rasmi kuwa itafunga programu yake ya ujumbe, Messenger, kuanzia mwezi April mwaka huu.

    Kwa mujibu wa tangazo hilo, hatua za kwanza za mabadiliko zitaanza kwa Watumiaji wa kompyuta za Mac na Windows, ambapo toleo la desktop la Messenger litafungwa rasmi. Kampuni hiyo imeeleza pia kuwa mwakani inapanga kuiondoa kabisa Messenger kama app huru na kubaki na Facebook kama jukwaa moja lenye sehemu ya ujumbe (messages) ndani yake.

    Messenger haikuanza kwa jina hilo. Mwaka 2008, huduma hiyo ilizinduliwa kwa jina la Facebook Chat, ikiwa ni sehemu ya mawasiliano ya moja kwa moja ndani ya Facebook.

    Mwaka 2011, huduma hiyo iliboreshwa na kubadilishwa jina rasmi kuwa Messenger, ikiwa ni app inayojitegemea kwa simu na baadaye kwa kompyuta.

    Katika kipindi cha ukuaji wake, Messenger ilitumika kama silaha ya ushindani dhidi ya majukwaa mengine makubwa ya mawasiliano kama:

    - WhatsApp
    - iMessage
    - WeChat
    - Skype

    Lengo lilikuwa ni kuimarisha mawasiliano ya Watumiaji wa Facebook bila kulazimika kuondoka ndani ya mfumo wa kampuni hiyo.

    Baada ya kufutwa kwa Messenger kama app ya pekee, Facebook itabaki kama mtandao mmoja wenye sehemu ya ujumbe ndani yake. Hii ina maana kuwa Watumiaji wataendelea kutuma na kupokea meseji, lakini kupitia mfumo wa moja kwa moja ndani ya Facebook badala ya app tofauti.

    Hatua hii inaashiria mabadiliko makubwa katika mkakati wa kidijitali wa Facebook, hasa katika kipindi ambacho kampuni nyingi za teknolojia zinaelekea kurahisisha huduma zao na kupunguza gharama za uendeshaji.

    Zaidi ya muongo mmoja baada ya kuzinduliwa kwake, Messenger sasa inaingia rasmi katika historia kama app iliyowahi kuwa moja ya majukwaa makubwa ya mawasiliano duniani.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Facebook yatangaza rasmi kufunga App ya Messenger kuanzia April. Kampuni ya teknolojia ya META imetangaza rasmi kuwa itafunga programu yake ya ujumbe, Messenger, kuanzia mwezi April mwaka huu. Kwa mujibu wa tangazo hilo, hatua za kwanza za mabadiliko zitaanza kwa Watumiaji wa kompyuta za Mac na Windows, ambapo toleo la desktop la Messenger litafungwa rasmi. Kampuni hiyo imeeleza pia kuwa mwakani inapanga kuiondoa kabisa Messenger kama app huru na kubaki na Facebook kama jukwaa moja lenye sehemu ya ujumbe (messages) ndani yake. Messenger haikuanza kwa jina hilo. Mwaka 2008, huduma hiyo ilizinduliwa kwa jina la Facebook Chat, ikiwa ni sehemu ya mawasiliano ya moja kwa moja ndani ya Facebook. Mwaka 2011, huduma hiyo iliboreshwa na kubadilishwa jina rasmi kuwa Messenger, ikiwa ni app inayojitegemea kwa simu na baadaye kwa kompyuta. Katika kipindi cha ukuaji wake, Messenger ilitumika kama silaha ya ushindani dhidi ya majukwaa mengine makubwa ya mawasiliano kama: - WhatsApp - iMessage - WeChat - Skype Lengo lilikuwa ni kuimarisha mawasiliano ya Watumiaji wa Facebook bila kulazimika kuondoka ndani ya mfumo wa kampuni hiyo. Baada ya kufutwa kwa Messenger kama app ya pekee, Facebook itabaki kama mtandao mmoja wenye sehemu ya ujumbe ndani yake. Hii ina maana kuwa Watumiaji wataendelea kutuma na kupokea meseji, lakini kupitia mfumo wa moja kwa moja ndani ya Facebook badala ya app tofauti. Hatua hii inaashiria mabadiliko makubwa katika mkakati wa kidijitali wa Facebook, hasa katika kipindi ambacho kampuni nyingi za teknolojia zinaelekea kurahisisha huduma zao na kupunguza gharama za uendeshaji. Zaidi ya muongo mmoja baada ya kuzinduliwa kwake, Messenger sasa inaingia rasmi katika historia kama app iliyowahi kuwa moja ya majukwaa makubwa ya mawasiliano duniani. Toa maoni yako #Habari
    0 Commentarios 0 Acciones 330 Views
  • Trump aahidi kufungua mafaili ya siri kuhusu “Aliens” baada ya kauli ya Obama.

    Mjadala kuhusu uwepo wa viumbe wa angani umechukua sura mpya baada ya kauli ya aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama, na kufuatiwa na ahadi ya Rais wa sasa, Donald Trump, ya kuweka wazi mafaili ya siri yanayohusiana na suala hilo.

    Katika maelezo yake ya hivi karibuni, Obama aligusia uwepo wa viumbe wa angani, akionesha kuwa suala hilo si la kubezwa. Kauli hiyo imeamsha hisia na mijadala mikubwa miongoni mwa Wananchi na Wachambuzi wa masuala ya usalama na sayansi.

    Ingawa hakutoa ushahidi wa moja kwa moja hadharani, kauli yake imechukuliwa kama ishara kwamba kuna taarifa ambazo bado hazijawekwa wazi kwa umma.

    Kupitia ujumbe wake rasmi, Trump ameahidi kuchukua hatua. Katika ujumbe huo ameandika: “Kutokana na hamasa kubwa iliyooneshwa na Wananchi juu ya kutaka kutambua ukweli kuhusu Aliens, nimezielekeza wizara na taasisi husika kuanza mchakato wa kubaini na kutoa hadharani nyaraka za serikali zinazohusiana na maisha ya viumbe wa anga (Aliens), matukio ya vitu visivyojulikana angani (UAP), vitu vinavyoruka visivyojulikana (UFO), pamoja na taarifa nyingine zote zinazohusiana na masuala haya ambayo ni magumu lakini ya kuvutia na muhimu sana.”

    Kauli hiyo imezua maswali mengi: Je, serikali ya Marekani iko tayari kufungua mafaili yote ya siri? Au kutakuwa na taarifa chache tu zitakazowekwa wazi kwa umma?

    Katika miaka ya karibuni, taasisi za ulinzi za Marekani zimekiri kuchunguza matukio ya UAP (Unidentified Aerial Phenomena) na UFO (Unidentified Flying Objects). Baadhi ya video na taarifa tayari zimewahi kutolewa, lakini bado kuna madai kwamba sehemu kubwa ya taarifa hizo imebaki kuwa siri ya serikali.

    Ahadi ya Trump inaweza kuwa hatua mpya katika historia ya uwazi wa taarifa za usalama wa taifa au inaweza kuwa mkakati wa kisiasa unaolenga kuvutia umma.

    Je, Siri zitafunguliwa Kweli?

    Kihistoria, masuala yanayohusiana na usalama wa taifa yamekuwa yakilindwa kwa uangalifu mkubwa. Hivyo, hata kama mchakato utaanza, Wachambuzi wanaamini kuwa kuna uwezekano wa kuwepo kwa uchujaji wa taarifa kabla ya kutolewa hadharani.

    Kwa sasa, macho ya dunia yanaelekezwa Washington kusubiri kama ahadi hiyo itatekelezwa kikamilifu.

    Unadhani Serikali ya Marekani itatoa kweli siri hizi zote? Na wewe binafsi, unaamini kweli kuna viumbe wa angani wanaoishi nje ya sayari yetu?

    Toa maoni yako
    #Habari
    Trump aahidi kufungua mafaili ya siri kuhusu “Aliens” baada ya kauli ya Obama. Mjadala kuhusu uwepo wa viumbe wa angani umechukua sura mpya baada ya kauli ya aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama, na kufuatiwa na ahadi ya Rais wa sasa, Donald Trump, ya kuweka wazi mafaili ya siri yanayohusiana na suala hilo. Katika maelezo yake ya hivi karibuni, Obama aligusia uwepo wa viumbe wa angani, akionesha kuwa suala hilo si la kubezwa. Kauli hiyo imeamsha hisia na mijadala mikubwa miongoni mwa Wananchi na Wachambuzi wa masuala ya usalama na sayansi. Ingawa hakutoa ushahidi wa moja kwa moja hadharani, kauli yake imechukuliwa kama ishara kwamba kuna taarifa ambazo bado hazijawekwa wazi kwa umma. Kupitia ujumbe wake rasmi, Trump ameahidi kuchukua hatua. Katika ujumbe huo ameandika: “Kutokana na hamasa kubwa iliyooneshwa na Wananchi juu ya kutaka kutambua ukweli kuhusu Aliens, nimezielekeza wizara na taasisi husika kuanza mchakato wa kubaini na kutoa hadharani nyaraka za serikali zinazohusiana na maisha ya viumbe wa anga (Aliens), matukio ya vitu visivyojulikana angani (UAP), vitu vinavyoruka visivyojulikana (UFO), pamoja na taarifa nyingine zote zinazohusiana na masuala haya ambayo ni magumu lakini ya kuvutia na muhimu sana.” Kauli hiyo imezua maswali mengi: Je, serikali ya Marekani iko tayari kufungua mafaili yote ya siri? Au kutakuwa na taarifa chache tu zitakazowekwa wazi kwa umma? Katika miaka ya karibuni, taasisi za ulinzi za Marekani zimekiri kuchunguza matukio ya UAP (Unidentified Aerial Phenomena) na UFO (Unidentified Flying Objects). Baadhi ya video na taarifa tayari zimewahi kutolewa, lakini bado kuna madai kwamba sehemu kubwa ya taarifa hizo imebaki kuwa siri ya serikali. Ahadi ya Trump inaweza kuwa hatua mpya katika historia ya uwazi wa taarifa za usalama wa taifa au inaweza kuwa mkakati wa kisiasa unaolenga kuvutia umma. Je, Siri zitafunguliwa Kweli? Kihistoria, masuala yanayohusiana na usalama wa taifa yamekuwa yakilindwa kwa uangalifu mkubwa. Hivyo, hata kama mchakato utaanza, Wachambuzi wanaamini kuwa kuna uwezekano wa kuwepo kwa uchujaji wa taarifa kabla ya kutolewa hadharani. Kwa sasa, macho ya dunia yanaelekezwa Washington kusubiri kama ahadi hiyo itatekelezwa kikamilifu. Unadhani Serikali ya Marekani itatoa kweli siri hizi zote? Na wewe binafsi, unaamini kweli kuna viumbe wa angani wanaoishi nje ya sayari yetu? Toa maoni yako #Habari
    0 Commentarios 0 Acciones 395 Views
  • “Nimemsikia Rais wa Marekani akisema, kwa zaidi ya miaka 47, Marekani imeshindwa kuivunja Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Sasa namuambia kwamba: hamtokuja kufanikiwa kamwe”

    - Ayatollah Sayeed Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Iran.

    Toa maoni yako
    #Habari
    #Habari
    “Nimemsikia Rais wa Marekani akisema, kwa zaidi ya miaka 47, Marekani imeshindwa kuivunja Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Sasa namuambia kwamba: hamtokuja kufanikiwa kamwe” - Ayatollah Sayeed Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Iran. Toa maoni yako #Habari #Habari
    0 Commentarios 0 Acciones 218 Views
  • Pitbull ataka kuweka rekodi ya Dunia kupitia Guinness World Records.

    Rapa maarufu duniani, Pitbull, ametangaza mpango wa kuandika historia mpya katika Guinness World Records akishirikiana na mashabiki wake watakaohudhuria tamasha lake Jijini London, Uingereza.

    Msanii huyo mwenye umri wa miaka 45, anayejulikana pia kwa jina la kisanii Mr. Worldwide, anataka kuweka rekodi ya dunia kwa kuwa na “kundi kubwa zaidi la watu waliovaa kofia maalum zinazoiga kipara (bald caps)” katika tukio moja.

    Jaribio hilo linatarajiwa kufanyika wakati wa tamasha kubwa la muziki la BST Hyde Park, litakalofanyika tarehe 10 Julai 2026 Jijini London, ambapo Pitbull atakuwa Msanii mkuu wa siku hiyo.

    Wazo hilo limechochewa na utamaduni ulioenea katika maonyesho yake ya hivi karibuni, ambapo mashabiki wengi hujitokeza wakiwa wamevaa bald caps, miwani mikubwa aina ya aviators, pamoja na suti au makoti yanayokaa mwilini kwa umaridadi, mtindo unaoiga mwonekano rasmi wa Pitbull anapokuwa jukwaani.

    Akizungumza kuhusu mpango huo, Pitbull ameeleza kuwa “tunataka kuonyesha nguvu ya mashabiki na kuandika historia pamoja.”

    Mpango huo ulipata nguvu zaidi baada ya kuungwa mkono na Mtangazaji wa BBC Radio 1 Breakfast, Greg James, ambaye alihamasisha hadhira kuunga mkono jaribio hilo la kuvunja rekodi ya dunia.

    Kwa mujibu wa Waandaaji, endapo idadi ya mashabiki watakaovaa kofia hizo itafikia kiwango kinachotakiwa na Waamuzi wa Guinness World Records, basi Pitbull ataingia rasmi kwenye vitabu vya historia kama Msanii aliyeongoza tukio la kipekee zaidi la aina yake.

    Iwapo jaribio hilo litafanikiwa, litakuwa si tu ushindi kwa Pitbull binafsi, bali pia kwa mashabiki wake wanaojulikana kwa ubunifu na mshikamano mkubwa katika matamasha yake duniani.

    Toa maoni yako
    #Music
    #Habari
    Pitbull ataka kuweka rekodi ya Dunia kupitia Guinness World Records. Rapa maarufu duniani, Pitbull, ametangaza mpango wa kuandika historia mpya katika Guinness World Records akishirikiana na mashabiki wake watakaohudhuria tamasha lake Jijini London, Uingereza. Msanii huyo mwenye umri wa miaka 45, anayejulikana pia kwa jina la kisanii Mr. Worldwide, anataka kuweka rekodi ya dunia kwa kuwa na “kundi kubwa zaidi la watu waliovaa kofia maalum zinazoiga kipara (bald caps)” katika tukio moja. Jaribio hilo linatarajiwa kufanyika wakati wa tamasha kubwa la muziki la BST Hyde Park, litakalofanyika tarehe 10 Julai 2026 Jijini London, ambapo Pitbull atakuwa Msanii mkuu wa siku hiyo. Wazo hilo limechochewa na utamaduni ulioenea katika maonyesho yake ya hivi karibuni, ambapo mashabiki wengi hujitokeza wakiwa wamevaa bald caps, miwani mikubwa aina ya aviators, pamoja na suti au makoti yanayokaa mwilini kwa umaridadi, mtindo unaoiga mwonekano rasmi wa Pitbull anapokuwa jukwaani. Akizungumza kuhusu mpango huo, Pitbull ameeleza kuwa “tunataka kuonyesha nguvu ya mashabiki na kuandika historia pamoja.” Mpango huo ulipata nguvu zaidi baada ya kuungwa mkono na Mtangazaji wa BBC Radio 1 Breakfast, Greg James, ambaye alihamasisha hadhira kuunga mkono jaribio hilo la kuvunja rekodi ya dunia. Kwa mujibu wa Waandaaji, endapo idadi ya mashabiki watakaovaa kofia hizo itafikia kiwango kinachotakiwa na Waamuzi wa Guinness World Records, basi Pitbull ataingia rasmi kwenye vitabu vya historia kama Msanii aliyeongoza tukio la kipekee zaidi la aina yake. Iwapo jaribio hilo litafanikiwa, litakuwa si tu ushindi kwa Pitbull binafsi, bali pia kwa mashabiki wake wanaojulikana kwa ubunifu na mshikamano mkubwa katika matamasha yake duniani. Toa maoni yako #Music #Habari
    0 Commentarios 0 Acciones 293 Views
  • Zambia Yawafukuza Zaidi ya Raia 80 wa Congo kwa tuhuma za kukaa kinyume cha sheria.

    Serikali ya Zambia imewafukuza zaidi ya Raia 80 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika operesheni maalum iliyolenga watu wanaodaiwa kuishi nchini humo bila vibali halali.

    Kwa mujibu wa mamlaka za Zambia, hatua hiyo ni sehemu ya zoezi pana la kukagua Wahamiaji wanaoshukiwa kuwa katika hali isiyo halali ndani ya mipaka ya taifa hilo. Vyanzo vya kiusalama vinaeleza kuwa operesheni hiyo ilifanyika baada ya uchunguzi wa kina kubaini kuwepo kwa idadi kubwa ya watu wasiokuwa na nyaraka sahihi.

    Afisa wa Zambia wamesema kuwa, "Zaidi ya watu 170 wa mataifa mbalimbali wanashukiwa kuwa katika hali isiyo halali nchini Zambia."

    Taarifa hiyo inaashiria kuwa si Raia wa Congo pekee waliolengwa katika msako huo, bali pia watu kutoka mataifa mengine ambao wanadaiwa kukiuka sheria za uhamiaji.

    Hatua ya kufukuzwa kwa Raia hao wa Congo inaelezwa kuwa ni utekelezaji wa sheria za uhamiaji za Zambia, ambazo zinataka Wageni wote kuwa na vibali halali vya kuishi au kufanya kazi nchini humo.

    Wachambuzi wa masuala ya kikanda wanasema kuwa operesheni za aina hii mara nyingi huibua mjadala kuhusu haki za Wahamiaji, hasa katika ukanda wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambako harakati za watu kuvuka mipaka ni jambo la kawaida kwa sababu za kiuchumi na kijamii.

    Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi kuhusu iwapo hatua hiyo itaathiri uhusiano wa kidiplomasia kati ya Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Serikali ya Zambia imeweka wazi kuwa itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kukaa nchini humo bila kufuata taratibu za kisheria.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Zambia Yawafukuza Zaidi ya Raia 80 wa Congo kwa tuhuma za kukaa kinyume cha sheria. Serikali ya Zambia imewafukuza zaidi ya Raia 80 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika operesheni maalum iliyolenga watu wanaodaiwa kuishi nchini humo bila vibali halali. Kwa mujibu wa mamlaka za Zambia, hatua hiyo ni sehemu ya zoezi pana la kukagua Wahamiaji wanaoshukiwa kuwa katika hali isiyo halali ndani ya mipaka ya taifa hilo. Vyanzo vya kiusalama vinaeleza kuwa operesheni hiyo ilifanyika baada ya uchunguzi wa kina kubaini kuwepo kwa idadi kubwa ya watu wasiokuwa na nyaraka sahihi. Afisa wa Zambia wamesema kuwa, "Zaidi ya watu 170 wa mataifa mbalimbali wanashukiwa kuwa katika hali isiyo halali nchini Zambia." Taarifa hiyo inaashiria kuwa si Raia wa Congo pekee waliolengwa katika msako huo, bali pia watu kutoka mataifa mengine ambao wanadaiwa kukiuka sheria za uhamiaji. Hatua ya kufukuzwa kwa Raia hao wa Congo inaelezwa kuwa ni utekelezaji wa sheria za uhamiaji za Zambia, ambazo zinataka Wageni wote kuwa na vibali halali vya kuishi au kufanya kazi nchini humo. Wachambuzi wa masuala ya kikanda wanasema kuwa operesheni za aina hii mara nyingi huibua mjadala kuhusu haki za Wahamiaji, hasa katika ukanda wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambako harakati za watu kuvuka mipaka ni jambo la kawaida kwa sababu za kiuchumi na kijamii. Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi kuhusu iwapo hatua hiyo itaathiri uhusiano wa kidiplomasia kati ya Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Serikali ya Zambia imeweka wazi kuwa itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kukaa nchini humo bila kufuata taratibu za kisheria. Toa maoni yako #Habari
    0 Commentarios 0 Acciones 188 Views
  • Denis Mukwege ataka “Mazungumzo ya Kitaifa” kutatua tatizo la uongozi DRC.

    Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Dkt. Denis Mukwege, amesema kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inahitaji haraka “Mazungumzo ya Kitaifa” ili kupata suluhisho la kudumu kwa changamoto zinazoikabili nchi hiyo, hususan katika eneo la uongozi.

    Akizungumza kuhusu hali ya sasa ya nchi yake, Dkt. Mukwege alieleza kuwa kiini cha matatizo mengi yanayoikumba Congo ni ukosefu wa uongozi bora.

    “Iwapo leo Congo inapitia mateso yote tunayoshuhudia, ni kwa sababu tu ya uwepo wa uongozi mbovu. Kama kungekuwa na uongozi mzuri, kwa kawaida Congo ingeweza kulinda raia wake na kusimamia ipasavyo rasilimali zake za madini ambazo kwa sasa zinavunwa na kila aina ya walafi wanaozunguka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.”

    Kauli hiyo imekuja wakati nchi hiyo ikiendelea kukabiliwa na changamoto za kiusalama, migogoro ya silaha katika maeneo ya mashariki, pamoja na lawama za muda mrefu kuhusu usimamizi wa rasilimali asilia.

    Kwa mujibu wa Dkt. Mukwege, suluhisho la kweli halitapatikana kwa hatua za juu juu, bali kupitia mchakato mpana wa kitaifa utakaowaleta pamoja wadau wote muhimu—serikali, vyama vya siasa, Asasi za kiraia na Wawakilishi wa wananchi.

    Anaamini kuwa kupitia jukwaa hilo, taifa linaweza kujadili kwa uwazi matatizo ya kiutawala, uwajibikaji wa Viongozi, pamoja na namna bora ya kusimamia utajiri mkubwa wa madini uliopo nchini humo.

    DRC ni miongoni mwa mataifa yenye utajiri mkubwa wa madini duniani, ikiwemo cobalt, dhahabu na coltan. Hata hivyo, kwa miaka mingi, rasilimali hizo zimehusishwa na migogoro, rushwa na uingiliaji wa maslahi ya ndani na nje ya nchi.

    Kauli ya Dkt. Mukwege inachukuliwa na Wachambuzi wengi kama wito wa mageuzi ya kina katika mifumo ya uongozi na uwajibikaji, ili kuhakikisha rasilimali za taifa zinawanufaisha Wananchi badala ya makundi machache yenye nguvu.

    Kwa sasa, macho ya wengi yanaelekezwa kuona iwapo wito huo wa “Mazungumzo ya Kitaifa” utapokelewa na mamlaka husika na kuwa mwanzo wa mabadiliko yanayohitajika nchini Congo.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Denis Mukwege ataka “Mazungumzo ya Kitaifa” kutatua tatizo la uongozi DRC. Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Dkt. Denis Mukwege, amesema kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inahitaji haraka “Mazungumzo ya Kitaifa” ili kupata suluhisho la kudumu kwa changamoto zinazoikabili nchi hiyo, hususan katika eneo la uongozi. Akizungumza kuhusu hali ya sasa ya nchi yake, Dkt. Mukwege alieleza kuwa kiini cha matatizo mengi yanayoikumba Congo ni ukosefu wa uongozi bora. “Iwapo leo Congo inapitia mateso yote tunayoshuhudia, ni kwa sababu tu ya uwepo wa uongozi mbovu. Kama kungekuwa na uongozi mzuri, kwa kawaida Congo ingeweza kulinda raia wake na kusimamia ipasavyo rasilimali zake za madini ambazo kwa sasa zinavunwa na kila aina ya walafi wanaozunguka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.” Kauli hiyo imekuja wakati nchi hiyo ikiendelea kukabiliwa na changamoto za kiusalama, migogoro ya silaha katika maeneo ya mashariki, pamoja na lawama za muda mrefu kuhusu usimamizi wa rasilimali asilia. Kwa mujibu wa Dkt. Mukwege, suluhisho la kweli halitapatikana kwa hatua za juu juu, bali kupitia mchakato mpana wa kitaifa utakaowaleta pamoja wadau wote muhimu—serikali, vyama vya siasa, Asasi za kiraia na Wawakilishi wa wananchi. Anaamini kuwa kupitia jukwaa hilo, taifa linaweza kujadili kwa uwazi matatizo ya kiutawala, uwajibikaji wa Viongozi, pamoja na namna bora ya kusimamia utajiri mkubwa wa madini uliopo nchini humo. DRC ni miongoni mwa mataifa yenye utajiri mkubwa wa madini duniani, ikiwemo cobalt, dhahabu na coltan. Hata hivyo, kwa miaka mingi, rasilimali hizo zimehusishwa na migogoro, rushwa na uingiliaji wa maslahi ya ndani na nje ya nchi. Kauli ya Dkt. Mukwege inachukuliwa na Wachambuzi wengi kama wito wa mageuzi ya kina katika mifumo ya uongozi na uwajibikaji, ili kuhakikisha rasilimali za taifa zinawanufaisha Wananchi badala ya makundi machache yenye nguvu. Kwa sasa, macho ya wengi yanaelekezwa kuona iwapo wito huo wa “Mazungumzo ya Kitaifa” utapokelewa na mamlaka husika na kuwa mwanzo wa mabadiliko yanayohitajika nchini Congo. Toa maoni yako #Habari
    0 Commentarios 0 Acciones 131 Views
  • Nyota wa Soka Kaslin Soza atangaza kusilimu

    Mchezaji wa soka kutoka Brazil, Kaslin Soza, ametangaza rasmi kuwa amesilimu na kuanza maisha mapya ya imani ya Kiislamu.

    Kaslin, ambaye aliwahi kuitumikia klabu ya Wanawake ya Real Madrid Femenino nchini Hispania na kwa sasa anakipiga katika klabu ya Saudia ya Al-Nassr Women, alitoa taarifa hiyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

    Katika ujumbe wake, Kaslin aliandika kwa hisia na msisitizo akisema: “Nimechagua kuingia katika dini ya Uislamu kwa hiari yangu mwenyewe, nikiwa na amani moyoni na imani thabiti juu ya uamuzi huu.”

    Nyota huyo wa kandanda alieleza kuwa safari yake ya kiroho haikuwa ya ghafla, bali ni matokeo ya tafakari ya muda mrefu na kujifunza kwa kina kuhusu mafundisho ya dini hiyo.

    “Huu ni mwanzo wa ukurasa mpya katika maisha yangu, safari ya kujitambua zaidi na kumkaribia Mwenyezi Mungu,” aliongeza katika ujumbe wake.

    Hatua hiyo imeibua mjadala mpana mtandaoni, huku mashabiki wake na wadau wa soka wakitoa pongezi na salamu za heri kwa uamuzi wake. Wapo waliomsifu kwa ujasiri wa kusimama hadharani na kutangaza mabadiliko hayo ya kiimani.

    Kaslin Soza amekuwa miongoni mwa Wachezaji wa Brazil waliopata nafasi ya kucheza katika Ligi kubwa barani Ulaya kabla ya kuhamia Mashariki ya Kati, ambako soka la Wanawake linaendelea kukua kwa kasi.

    Kwa sasa, macho ya mashabiki wake yapo si tu kwenye kiwango chake Uwanjani, bali pia katika safari yake mpya ya maisha nje ya Uwanja.

    Toa maoni yako
    #Sports
    #Habari
    🇧🇷 Nyota wa Soka Kaslin Soza atangaza kusilimu Mchezaji wa soka kutoka Brazil, Kaslin Soza, ametangaza rasmi kuwa amesilimu na kuanza maisha mapya ya imani ya Kiislamu. Kaslin, ambaye aliwahi kuitumikia klabu ya Wanawake ya Real Madrid Femenino nchini Hispania na kwa sasa anakipiga katika klabu ya Saudia ya Al-Nassr Women, alitoa taarifa hiyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii. Katika ujumbe wake, Kaslin aliandika kwa hisia na msisitizo akisema: “Nimechagua kuingia katika dini ya Uislamu kwa hiari yangu mwenyewe, nikiwa na amani moyoni na imani thabiti juu ya uamuzi huu.” Nyota huyo wa kandanda alieleza kuwa safari yake ya kiroho haikuwa ya ghafla, bali ni matokeo ya tafakari ya muda mrefu na kujifunza kwa kina kuhusu mafundisho ya dini hiyo. “Huu ni mwanzo wa ukurasa mpya katika maisha yangu, safari ya kujitambua zaidi na kumkaribia Mwenyezi Mungu,” aliongeza katika ujumbe wake. Hatua hiyo imeibua mjadala mpana mtandaoni, huku mashabiki wake na wadau wa soka wakitoa pongezi na salamu za heri kwa uamuzi wake. Wapo waliomsifu kwa ujasiri wa kusimama hadharani na kutangaza mabadiliko hayo ya kiimani. Kaslin Soza amekuwa miongoni mwa Wachezaji wa Brazil waliopata nafasi ya kucheza katika Ligi kubwa barani Ulaya kabla ya kuhamia Mashariki ya Kati, ambako soka la Wanawake linaendelea kukua kwa kasi. Kwa sasa, macho ya mashabiki wake yapo si tu kwenye kiwango chake Uwanjani, bali pia katika safari yake mpya ya maisha nje ya Uwanja. Toa maoni yako #Sports #Habari
    0 Commentarios 0 Acciones 310 Views
  • Kim Jong Un azindua makaziapya Pyongyang kwa familia za Wanajeshi waliofariki dunia.

    Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, amefungua rasmi mradi mpya wa makazi katika Mji Mkuu wa Pyongyang, uliolengwa kuwahudumia familia za wanajeshi waliopoteza maisha wakilitumikia taifa hilo.

    Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya taifa, makazi hayo yamejengwa kwa hadhi ya juu kama ishara ya kutambua mchango na kujitoa kwa wanajeshi waliofariki vitani au katika majukumu ya kijeshi.

    Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Kim Jong Un alinukuliwa akisema: “Familia za mashujaa wetu waliolitoa uhai wao kwa ajili ya taifa hili zinastahili kuishi kwa heshima na utulivu.”

    Aliongeza kuwa: "Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa watoto na wake wa wanajeshi wetu wanaendelea kuishi maisha bora, wakiwa na makazi salama na ya kisasa.”

    Mradi huo ni sehemu ya mpango mpana wa maendeleo ya makazi unaoendelea nchini humo, hasa katika Mji wa Pyongyang, ambako serikali imekuwa ikiwekeza katika ujenzi wa majengo mapya ya kisasa kwa lengo la kuboresha ustawi wa raia wake.

    Wachambuzi wa masuala ya siasa za Korea Kaskazini wanasema hatua hiyo pia inalenga kuimarisha mshikamano wa kitaifa na kuonyesha umuhimu unaotolewa kwa Jeshi, ambalo lina nafasi kubwa katika mfumo wa uongozi wa nchi hiyo.

    Katika miaka ya karibuni, Pyongyang imekuwa ikishuhudia miradi kadhaa ya makazi ya ghorofa za kisasa, huku serikali ikisisitiza kuwa maendeleo ya Mji huo ni kielelezo cha mafanikio ya sera zake za kiuchumi na kijamii.

    Uzinduzi wa makazi haya mapya unatajwa kama ishara ya kutambua sadaka ya wanajeshi waliopoteza maisha, huku serikali ikiendelea kusisitiza msimamo wake wa kulinda na kuenzi waliolitumikia taifa kwa uaminifu.

    Toa maoni yako
    #Habari
    🇰🇵 Kim Jong Un azindua makaziapya Pyongyang kwa familia za Wanajeshi waliofariki dunia. Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, amefungua rasmi mradi mpya wa makazi katika Mji Mkuu wa Pyongyang, uliolengwa kuwahudumia familia za wanajeshi waliopoteza maisha wakilitumikia taifa hilo. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya taifa, makazi hayo yamejengwa kwa hadhi ya juu kama ishara ya kutambua mchango na kujitoa kwa wanajeshi waliofariki vitani au katika majukumu ya kijeshi. Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Kim Jong Un alinukuliwa akisema: “Familia za mashujaa wetu waliolitoa uhai wao kwa ajili ya taifa hili zinastahili kuishi kwa heshima na utulivu.” Aliongeza kuwa: "Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa watoto na wake wa wanajeshi wetu wanaendelea kuishi maisha bora, wakiwa na makazi salama na ya kisasa.” Mradi huo ni sehemu ya mpango mpana wa maendeleo ya makazi unaoendelea nchini humo, hasa katika Mji wa Pyongyang, ambako serikali imekuwa ikiwekeza katika ujenzi wa majengo mapya ya kisasa kwa lengo la kuboresha ustawi wa raia wake. Wachambuzi wa masuala ya siasa za Korea Kaskazini wanasema hatua hiyo pia inalenga kuimarisha mshikamano wa kitaifa na kuonyesha umuhimu unaotolewa kwa Jeshi, ambalo lina nafasi kubwa katika mfumo wa uongozi wa nchi hiyo. Katika miaka ya karibuni, Pyongyang imekuwa ikishuhudia miradi kadhaa ya makazi ya ghorofa za kisasa, huku serikali ikisisitiza kuwa maendeleo ya Mji huo ni kielelezo cha mafanikio ya sera zake za kiuchumi na kijamii. Uzinduzi wa makazi haya mapya unatajwa kama ishara ya kutambua sadaka ya wanajeshi waliopoteza maisha, huku serikali ikiendelea kusisitiza msimamo wake wa kulinda na kuenzi waliolitumikia taifa kwa uaminifu. Toa maoni yako #Habari
    0 Commentarios 0 Acciones 181 Views
  • Umoja wa Afrika wasisitiza “Hakuna kuvumilia kabisa” dhidi ya mapinduzi na mabadiliko yasiyo ya kikatiba.

    Umoja wa Afrika (AU) umetangaza msimamo mkali dhidi ya mabadiliko ya serikali yanayokiuka katiba katika nchi wanachama, ukisisitiza sera ya “Hakuna kuvumilia kabisa” kwa vitendo vinavyovuruga utawala wa kikatiba na utulivu wa bara la Afrika.

    Kauli hiyo imekuja wakati bara la Afrika likikabiliwa na changamoto za mapinduzi ya kijeshi, migogoro ya kisiasa na kuingiliwa kwa masuala ya ndani na nguvu za kigeni. Viongozi wa AU wamesema hatua madhubuti zinahitajika ili kuhakikisha silaha zinanyamaza na misingi ya demokrasia unalindwa.

    Akizungumza kwa niaba ya Umoja huo, Mwenyekiti wa sasa wa AU na Rais wa Burundi, Évariste Ndayishimiye, alisisitiza umuhimu wa kulinda mamlaka ya nchi za Afrika dhidi ya ushawishi wa nje.

    “Hakuna nchi ya Afrika inayopaswa kutawaliwa tena kikoloni, kuvamiwa au kulazimishwa kujisalimisha kwa mamlaka yoyote ya kigeni katika karne ya 21.”

    Kauli hiyo inaonesha msimamo wa wazi wa Umoja wa Afrika kupinga aina yoyote ya kuingiliwa kwa uhuru wa nchi wanachama, iwe kwa njia ya mapinduzi ya ndani au shinikizo la kimataifa.

    Kwa mujibu wa misingi ya AU, mabadiliko yoyote ya serikali yanapaswa kufuata katiba na taratibu za kisheria zilizowekwa. Umoja huo kwa muda mrefu umekuwa ukitoa adhabu kama kusimamisha uanachama kwa nchi zinazoshuhudia mapinduzi ya kijeshi au hatua nyingine zisizo za kikatiba.

    Tamko la “Zero Tolerance” linatafsiriwa kama onyo kwa vikundi vyote vinavyotaka kutumia nguvu kuchukua madaraka, pamoja na ujumbe kwa mataifa ya nje kuheshimu mamlaka ya bara la Afrika.

    Sera hiyo pia inaunganishwa na azma ya muda mrefu ya AU ya “Kuzinyamazisha silaha barani Afrika,” kampeni inayolenga kumaliza migogoro ya kivita na kuimarisha amani na usalama.

    Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema msimamo huo unaashiria jitihada za kuimarisha mshikamano wa bara na kulinda misingi ya uhuru, demokrasia na utawala wa sheria.

    Kwa ujumla, kauli ya Umoja wa Afrika inatoa ujumbe mzito: Bara haliko tayari kuvumilia mapinduzi, uvamizi au aina yoyote ya utawala wa kulazimishwa katika zama za sasa.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Umoja wa Afrika wasisitiza “Hakuna kuvumilia kabisa” dhidi ya mapinduzi na mabadiliko yasiyo ya kikatiba. Umoja wa Afrika (AU) umetangaza msimamo mkali dhidi ya mabadiliko ya serikali yanayokiuka katiba katika nchi wanachama, ukisisitiza sera ya “Hakuna kuvumilia kabisa” kwa vitendo vinavyovuruga utawala wa kikatiba na utulivu wa bara la Afrika. Kauli hiyo imekuja wakati bara la Afrika likikabiliwa na changamoto za mapinduzi ya kijeshi, migogoro ya kisiasa na kuingiliwa kwa masuala ya ndani na nguvu za kigeni. Viongozi wa AU wamesema hatua madhubuti zinahitajika ili kuhakikisha silaha zinanyamaza na misingi ya demokrasia unalindwa. Akizungumza kwa niaba ya Umoja huo, Mwenyekiti wa sasa wa AU na Rais wa Burundi, Évariste Ndayishimiye, alisisitiza umuhimu wa kulinda mamlaka ya nchi za Afrika dhidi ya ushawishi wa nje. “Hakuna nchi ya Afrika inayopaswa kutawaliwa tena kikoloni, kuvamiwa au kulazimishwa kujisalimisha kwa mamlaka yoyote ya kigeni katika karne ya 21.” Kauli hiyo inaonesha msimamo wa wazi wa Umoja wa Afrika kupinga aina yoyote ya kuingiliwa kwa uhuru wa nchi wanachama, iwe kwa njia ya mapinduzi ya ndani au shinikizo la kimataifa. Kwa mujibu wa misingi ya AU, mabadiliko yoyote ya serikali yanapaswa kufuata katiba na taratibu za kisheria zilizowekwa. Umoja huo kwa muda mrefu umekuwa ukitoa adhabu kama kusimamisha uanachama kwa nchi zinazoshuhudia mapinduzi ya kijeshi au hatua nyingine zisizo za kikatiba. Tamko la “Zero Tolerance” linatafsiriwa kama onyo kwa vikundi vyote vinavyotaka kutumia nguvu kuchukua madaraka, pamoja na ujumbe kwa mataifa ya nje kuheshimu mamlaka ya bara la Afrika. Sera hiyo pia inaunganishwa na azma ya muda mrefu ya AU ya “Kuzinyamazisha silaha barani Afrika,” kampeni inayolenga kumaliza migogoro ya kivita na kuimarisha amani na usalama. Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema msimamo huo unaashiria jitihada za kuimarisha mshikamano wa bara na kulinda misingi ya uhuru, demokrasia na utawala wa sheria. Kwa ujumla, kauli ya Umoja wa Afrika inatoa ujumbe mzito: Bara haliko tayari kuvumilia mapinduzi, uvamizi au aina yoyote ya utawala wa kulazimishwa katika zama za sasa. Toa maoni yako #Habari
    0 Commentarios 0 Acciones 187 Views
  • Koffi Olomide atangaza tamasha kubwa Ubelgiji baada ya kufutwa matamasha yake Ufaransa.

    Mwanamuziki Nguli wa rumba ya Congo, Koffi Olomide, ametangaza rasmi kufanya tamasha kubwa katika Ubelgiji, baada ya kukumbana na changamoto ya kufutwa kwa matamasha kadhaa nchini Ufaransa.

    Tamasha hilo limepangwa kufanyika tarehe 11 Julai 2026 katika Uwanja maarufu wa Stade Roi Baudouin uliopo Jijini Brussels. Tangazo hili limeibua msisimko mkubwa miongoni mwa mashabiki wa muziki wa Congo na rumba kwa ujumla barani Ulaya na Afrika.

    Kupitia matangazo yake ya moja kwa moja kwenye TikTok, Msanii huyo alieleza dhamira yake ya kuifanya siku hiyo kuwa ya kipekee katika maisha yake ya muziki.

    Amesema kuwa anataka tarehe hiyo iwe tukio la kihistoria, akisherehekea miaka yake 70 ya kuzaliwa akiwa pamoja na mashabiki wake.

    Tamasha hilo linatajwa kuwa uzalishaji mkubwa (grande production) unaotarajiwa kuvuta maelfu ya watu katika Uwanja huo wenye historia ya kuandaa matukio makubwa ya kimataifa ya michezo na burudani.

    Hatua hii inakuja baada ya kufutwa kwa matamasha kadhaa ya Msanii huyo nchini Ufaransa, jambo lililozua mjadala mpana katika tasnia ya muziki. Hata hivyo, tangazo la Brussels linaonekana kama kurejea kwa nguvu kwa Gwiji huyo wa rumba, akionyesha kuwa bado ana ushawishi mkubwa na soko imara barani Ulaya.

    Kwa wapenzi wa rumba na muziki wa Congo, tukio hili tayari linaonekana kuwa miongoni mwa matamasha makubwa zaidi ya mwaka 2026. Kwa historia ndefu ya Koffi Olomide katika muziki, tamasha hili linatarajiwa kuwa zaidi ya burudani bali ni sherehe ya urithi, mafanikio na mchango wake katika kukuza rumba ya Kongo kimataifa.

    Mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu maandalizi rasmi, mauzo ya tiketi na orodha ya Wasanii watakaoshiriki katika usiku huo unaotarajiwa kuwa wa kipekee.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Koffi Olomide atangaza tamasha kubwa Ubelgiji baada ya kufutwa matamasha yake Ufaransa. Mwanamuziki Nguli wa rumba ya Congo, Koffi Olomide, ametangaza rasmi kufanya tamasha kubwa katika Ubelgiji, baada ya kukumbana na changamoto ya kufutwa kwa matamasha kadhaa nchini Ufaransa. Tamasha hilo limepangwa kufanyika tarehe 11 Julai 2026 katika Uwanja maarufu wa Stade Roi Baudouin uliopo Jijini Brussels. Tangazo hili limeibua msisimko mkubwa miongoni mwa mashabiki wa muziki wa Congo na rumba kwa ujumla barani Ulaya na Afrika. Kupitia matangazo yake ya moja kwa moja kwenye TikTok, Msanii huyo alieleza dhamira yake ya kuifanya siku hiyo kuwa ya kipekee katika maisha yake ya muziki. Amesema kuwa anataka tarehe hiyo iwe tukio la kihistoria, akisherehekea miaka yake 70 ya kuzaliwa akiwa pamoja na mashabiki wake. Tamasha hilo linatajwa kuwa uzalishaji mkubwa (grande production) unaotarajiwa kuvuta maelfu ya watu katika Uwanja huo wenye historia ya kuandaa matukio makubwa ya kimataifa ya michezo na burudani. Hatua hii inakuja baada ya kufutwa kwa matamasha kadhaa ya Msanii huyo nchini Ufaransa, jambo lililozua mjadala mpana katika tasnia ya muziki. Hata hivyo, tangazo la Brussels linaonekana kama kurejea kwa nguvu kwa Gwiji huyo wa rumba, akionyesha kuwa bado ana ushawishi mkubwa na soko imara barani Ulaya. Kwa wapenzi wa rumba na muziki wa Congo, tukio hili tayari linaonekana kuwa miongoni mwa matamasha makubwa zaidi ya mwaka 2026. Kwa historia ndefu ya Koffi Olomide katika muziki, tamasha hili linatarajiwa kuwa zaidi ya burudani bali ni sherehe ya urithi, mafanikio na mchango wake katika kukuza rumba ya Kongo kimataifa. Mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu maandalizi rasmi, mauzo ya tiketi na orodha ya Wasanii watakaoshiriki katika usiku huo unaotarajiwa kuwa wa kipekee. Toa maoni yako #Habari
    0 Commentarios 0 Acciones 125 Views
Resultados de la búsqueda