• Msanii wa Bongo Fleva, @officialzuchu , ataandika historia mpya leo akiwa kama msanii mkuu atakayetoa burudani katika Fainali za African Nation Champion League (CHAN) 2024.

    Zuchu atatoa burudani ya kipekee katika Tamasha hilo kubwa ambalo litafanyika leo Jumamosi, tarehe 30 Agosti 2025, katika Uwanja wa Kasarani jijini Nairobi, Kenya, likiwakutanisha Madagascar dhidi ya Morocco.

    Wakati macho ya wapenzi wa soka yakiwa kwa fainali hiyo, masikio na mioyo ya mashabiki wa muziki yataelekezwa kwa Zuchu, ambaye atapanda jukwaani kuonyesha uwezo wake na kuwakilisha Tanzania katika anga ya kimataifa.

    | @errymars_

    #ManaraTV
    #ManaraTVUpdates
    Msanii wa Bongo Fleva, @officialzuchu , ataandika historia mpya leo akiwa kama msanii mkuu atakayetoa burudani katika Fainali za African Nation Champion League (CHAN) 2024. Zuchu atatoa burudani ya kipekee katika Tamasha hilo kubwa ambalo litafanyika leo Jumamosi, tarehe 30 Agosti 2025, katika Uwanja wa Kasarani jijini Nairobi, Kenya, likiwakutanisha Madagascar dhidi ya Morocco. Wakati macho ya wapenzi wa soka yakiwa kwa fainali hiyo, masikio na mioyo ya mashabiki wa muziki yataelekezwa kwa Zuchu, ambaye atapanda jukwaani kuonyesha uwezo wake na kuwakilisha Tanzania 馃嚬馃嚳 katika anga ya kimataifa. 鉁嶏笍| @errymars_ #ManaraTV #ManaraTVUpdates
    0 Comments 0 Shares 44 Views
  • Mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Victor Boniface, anayeichezea Bayer Leverkusen ya Ujerumani, ameachana na mpenzi wake, Rikke Hermine, raia wa Norway. Wawili hao walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa miaka minne, lakini wameamua kuvunja uhusiano wao kutokana na kugundua kuwa Victor kwenye mali zake ameandika majina ya mama yake tu.

    Chanzo cha habari kinaeleza kuwa uamuzi wa Rikke kuachana na Victor ulitokana na kugundua kuwa katika mali zote za mshambuliaji huyo, majina ya mama yake mzazi pekee ndiyo yaliyoandikwa. Hali hii ilimfanya Rikke kuhisi kuwa hakuwa na nafasi ya kutosha katika maisha ya Victor, jambo lililomfanya kuchukua hatua hiyo.

    Aidha, inadaiwa kuwa Rikke alikuwa akishinikiza kufunga ndoa baada ya kuwa wapenzi kwa muda mrefu, huku Victor akiwa tayari kufunga naye ndoa lakini kwa sharti la kusaini mkataba wa awali (prenup).

    Prenup ni Mkataba wa awali kabla ya kufunga ndoa ambao unalenga kulinda mali za pande zote mbili endapo itatokea mkaachana kila mmoja anabaki na alichokuja nacho katika ndoa na sio kugawana mali, ila bibie Rikkie amekuwa mgumu kukubali hilo hivyo kuachana.

    | @errymars_

    #ManaraTV
    #manaratvupdates
    Mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Victor Boniface, anayeichezea Bayer Leverkusen ya Ujerumani, ameachana na mpenzi wake, Rikke Hermine, raia wa Norway. Wawili hao walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa miaka minne, lakini wameamua kuvunja uhusiano wao kutokana na kugundua kuwa Victor kwenye mali zake ameandika majina ya mama yake tu. Chanzo cha habari kinaeleza kuwa uamuzi wa Rikke kuachana na Victor ulitokana na kugundua kuwa katika mali zote za mshambuliaji huyo, majina ya mama yake mzazi pekee ndiyo yaliyoandikwa. Hali hii ilimfanya Rikke kuhisi kuwa hakuwa na nafasi ya kutosha katika maisha ya Victor, jambo lililomfanya kuchukua hatua hiyo. Aidha, inadaiwa kuwa Rikke alikuwa akishinikiza kufunga ndoa baada ya kuwa wapenzi kwa muda mrefu, huku Victor akiwa tayari kufunga naye ndoa lakini kwa sharti la kusaini mkataba wa awali (prenup). Prenup ni Mkataba wa awali kabla ya kufunga ndoa ambao unalenga kulinda mali za pande zote mbili endapo itatokea mkaachana kila mmoja anabaki na alichokuja nacho katika ndoa na sio kugawana mali, ila bibie Rikkie amekuwa mgumu kukubali hilo hivyo kuachana. 鉁嶏笍| @errymars_ #ManaraTV #manaratvupdates
    Love
    1
    1 Comments 0 Shares 1K Views