“Ukiwa Mwandishi wa Habari una vitu viwili muhimu vya kuchunga navyo ni Ulimi wako na Mikono yako, unapaswa kufahamu unaongea nini ama unaandika kitu gani, nyuma ya mauaji ya Kimbari yalikuwa ni matamshi ya Watangazaji pia ambao walieneza chuki, kwasasa kuna kazi mbili za hatari nazo ni Ualimu na Waandishi wa Habari, hawa wanaweza kutengeneza taifa la Wajinga ama Waelevu.
Nataka kusema nini? Nataka kusema juu ya kelele na shutuma za Yanga na Singida bado hakuna aliyetupa picha kamili zaidi ni kuwa Mashabiki wanalalamika kwa hisia, Waandishi tunalalamika kwa hisia ila hakuna anayekuja mbele kutoa usahihi, inaitwa Proving beyond reasonable doubt! Nimeona Wadau wanasema TFF haifanyi chochote, lakini wewe umewapa tip gani? Taasisi haifanyi maamuzi kwa hisia, the corporate world works differently from streets.
Bado kizazi chetu cha Uandishi kuna kitu kinamiss ni INVESTIGATIVE JOURNALISM, binafsi nakiri wazi TUMEFELI sana eneo hili, yaani sote tunalaumu Singida kufanya rotation tunaita kupanga matokeo, tangu lini duniani kubadili kikosi chako ni kupanga matokeo? Ikitokea Coastal kabadili kikosi, ikitokea Simba kabadili ama AZAM? Yani timu inalaumiwa kwa kutumia Wachezaji wake?
Tunaweza kuwa na hoja ila mpaka sasa hazina mashiko zaidi tunaonekana tunalalama ila tukipelekwa Mahakamani hakuna ambaye atathibitisha chochote, kama kufungwa ni kupanga matokeo mara ya mwisho Simba kumfunga Yanga ndani ya dakika 90 ni lini? Kama kufungwa ni kupanga matokeo lini Singida kamfunga Simba? Kama kufungwa ni kupanga lini Namungo kamfunga Simba lini?
Sisi WAANDISHI tuna homework tunapaswa kufanya, tutaharibu fikra za Watanzania! Wenzetu Ulaya walipoibua kashfa ya Casciopoli pale Italia walikuja na data, hata UEFA Heated Balls Scandal watu walikuwa na data! Yanga wakisema waende kisheria nani anaweza kuja na hoja za kueleweka? Kama hakuna taarifa sahihi, mifano hai basi tunaongelea hisia, TFF atareact endapo atajitokea Mtu akaattack matter not the subject" - Farhan JR, Mchambuzi.