HALI HALISI YA MAISHA HUKO MTAANI .
Baada ya kumaliza shule
Wale wote uliosoma nao wanaenda maeneo mbalimbali duniani.
Wengine wamemaliza chuo na sasa ni Madaktari, Wahandisi, Waalimu, Wanasheria, Wahasibu nk.
Wengine wameoa/kuolewa. Wengine wana watoto. Wengine ndo bado wanatafuta ajira. Wengine wamekufa, usisahau hilo pia. Wengine ni wagonjwa vitandani, wengine wameendelea na elimu ya juu zaidi nk. Wengine wanamiliki kampuni, wengine ni mabosi na wanamiliki hisa katika makampuni makubwa duniani.
Ila vipi wewe UNAJISIKIAJE unapokutana na wale uliosoma nao, ambao inaonekana wamefanikiwa katika NDOTO zao, wakati wewe bado unasuasua hata hujafanya chochote na hata kimshahara ulicho nacho hakikusogezi popote isipokuwa kula na kubadili nguo pamoja na kodi ya nyumba tu?
Ni mawazo mengi huja akilini, Je huwa unawaonea wivu? Na huo wivu wako ni wa aina gani? Je ni wa kuwachukia au ule wivu wa wewe kupambana ufikie mafanikio kama wao?
Kwanza watu wa namna hii huwa wanafikiria Mungu hawapendi kabisa.
Usisahau pia kuna wale waliofariki... Bado unafikiria vilevile na unawaonea wivu?
MY TAKE
Usiruhusu nafasi ya KUKATA TAMAA. Sisi ni tofauti na njia zetu za kufanikiwa ni tofauti.
Wengine wanafanikiwa haraka kabla yako na wengine baada yako na wewe unakuja kufanikiwa baada yao ndivyo ilivyo katika maisha. Ila katika hali yoyote unayojikuta upo sasa, tafadhali endelea kuvunja vizuizi na songa mbele huenda njia uliyo nayo ndiyo itakayo kutoa kamwe usijaribu kuishi maisha wanayoishi wengine kumbuka maisha ni vile unavyoamua kuishi wewe na si mwingine anavoishi.
Unapoona wengine wanafanikiwa basi jitume na wewe uweze kufanikiwa, kubwa ni kuongeza juhudi katika kazi zako.
Rafiki yako akinunua gari leo, furahi, kumbuka wakati utakaponunua la kwako litakuwa jipya zaidi kuliko la kwake na utatamba kwa wakati huo kiasi cha wao kukuonea wivu pia.
Hakuna washindi wa kudumu katika maisha, ila kuna washindi kwa muda.
Maisha siyo mashindano, usishindane na yoyote, kumbuka, kuwa maisha ni kama kitabu kwamba tunasoma kitabu kimoja lakini kurasa tofauti katika muda tofauti na kila mtu anafanikiwa kwa nafasi na wakati wake, inategemea unaanda mazingira yapi ya kufanikiwa...
Usiruhusu woga ndani yako kuuwa ndoto ndani yako, baki ukichochea matamanio yako pia jaribu kuthubutu kufanya usiwe mtu wa kuogopa hasara katika jambo la mafanikio kwani bila changamoto huwezi kutoboa.
Ni nini unatamani Leo...!?
Andika kwa sababu siku moja dunia itatamani kukusoma, na itakuwa ni sehemu ya historia yako ya mafanikio.
Hakuna mahali usipoweza kufika isipokuwa juani tu, jiamini, fanyia kazi malengo yako, tambua changamoto na zisikukatize tamaa. Usiumie kwa kuona wenzako wanafanikiwa, kumbuka anga ni pana sana na kila ndege anaweza kupaa bila kumgusa mwenzake.
Thamini kila jambo dogo ambalo linakujia katika maisha. Chini ya dunia kila kitu kinawezekana ukiamua epuka kupoteza muda mwingi kuumizwa na vitu visivyo na msingi katika maisha yako na pindi litokeapo jambo ambalo unaona litakurudisha nyuma basi weka pembeni jambo hilo kisha elekeza akili katika njia ya kutafuta mafanikio ipo siku utafanikiwa na mambo yote yataenda sawa.
Nahitimisha kwa kusema "Katika harakati za mafanikio kuna vitu vingi sana ambavyo huwa tunatamani viende kwa pamoja lakini kwa bahati mbaya kuna vingine huangukia njiani hivyo basi vyote ambavyo vinaonekana kukukwamisha fanya kuviweka kando kwa muda kisha chukua hata moja katika vingi hivyo lipeleke hadi mwisho kisha anza kuyarudia haya mengine baada ya mafanikio.