*VATICAN CITY......
Nchi? Mji? Serikali au Kampuni?*
Nadhani moja kati ya maeneo ambayo yamekuwa tata zaidi kuyaelewa basi ni mji wa Vatican… tukiachilia mbali kuhusu utata/ugumu wa kuelewa mfumo wake wa uendeshaji na historia yake lakini swali jepesi zaidi ambalo kila mtu huwa anahisi analifahamu jawabu lake ni kuhusu utambulisho wa Vatican.!! Ni swali jepesi ambalo karibia kila mtu anadhani ana jawabu sahihi lakini uhalisia ni kwamba asilimia kubwa ya watu wana jawabu lisilo sahihi… kila mtu atakueleza kwamba Vatican ni nchi inayojitegemea lakini hii ni robo tu au thelethi ya jawabu…
Leo nami niandike kidogo kuhusu eneo hili… na kwenye andishi hili fupi nitaeleza utambulisho wa Vatican ukoje kwa usahihi wake kabisa!
*Muhimu:* andishi hili halilengi kukosoa au kupinga imani ya mtu yeyote. Tahadhali zote zinazingatiwa ili kulinda heshima ya imani ya kila mtu.
Tuendelee…
Vatican City, ndio makao makuu ya Kanisa Katoliki na nyumba ya maisha ya Papa, kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki.
Vatican ndio nchi ndogo zaidi duniani kiasi kwamba unaweza kuizunguka yote kwa mzingo (circumference) kwa muda wa dakika arobaini tu kwa kutembea kwa miguu.
Ni ajabu sana kwa namna gani nchi ndogo kiasi hiki imetokea na je ni nchi kama nchi nyingine???
Jibu la swali hili ni refu sana kiaisi kwamba unaweza hata kusoma darasani kwa mwaka mzima lakini nitajaribu kuweka katika maneno machache sana ya kueleweka kwa wepesi…
Miaka ya kale sana Papa wa Kanisa Katoliki alikuwa ni mtawala wa nchi ambayo ilikuwa inajiita *Himaya ya Papa (Papal State)* ambayo inarandana kabisa na eneo la sasa la nchi nzima ya Italia. Hii ilikuwa takribani miaka ya 754 mpaka miaka ya 1870.
Ni katika kipindi hiki ambacho Papa aliteua eneo ndani ya nchi yake Papal State ambalo likajengwa *St. Peters Basilica*, kanisa kubwa zaidi duniani na lenye nakshi adhimu zaidi. Eneo hili ambalo St. Peters Basilica ilijengwa ni eneo fulani hivi la muinuko ambako hapo hapo pia yalijengwa makazi ya Papa kuishi.
Ikumbukwe kwamba katika kipindi hiki hiki cha uwepo wa himaya ya Papal State pia ilikuwa inapakana na Ufalme wa Italy (Kingdom of Italy) japo kila moja ilikuwa inajitegemea.
Japokuwa himaya hizi mbili zilikuwa jirani lakini kulikuwa na uhasama fulani kati yao. Hii ilifanya Papa kujenga ukuta mkubwa kuzunguka makazi yake ya kuishi na kanisa la St. Peters Basilica.
Kadiri miaka ilivyozidi kwenda uhasama kati ya Italy Kingdom na Papal State ulipanuka zaidi na ilifikia hatua Kingdom of Italy wakafanya uamuzi wa kuiteka Papal State na kuifanya makao makuu ya nchi yake (Rome ya sasa).
Wakati na baada ya uvamizi huu wa Kingdom of Italy kuteka Papal State, Papa mwenyewe alikuwa amejificha ndani ya makazi yake yaliyozungushiwa ukuta ambao nimeeleza awali.
Ikumbukwe kwamba hata kipindi hiki Kanisa Katoliki tayari lilikuwa na ushawishi mkubwa duniani kwa hiyo Kingdom of Italy walihofia kuingiza majeshi kwa nguvu ndani ya makazi ya Papa na kumkamata kuogopa umaarufu wao kimataifa kudondoka.
Kwa hiyo majeshi ya Kingdom of Italy yalibakia nje mwa kuta za Vatican kwa miaka mingi sana wakiamini kwamba iko siku Papa atakata tamaa na kujisalimisha.
Lakini hii haikufua dafu kwani miongo ilipita na Papa hakujisalimisha kwa kutoka nje ya kuta za Vatican. Takribani Mapapa watano kwa muda wa karibia miaka sitini waliishi ndani ya kuta za Vatican katika hali hii. Mapapa hao kwa majina yao walikuwa ni Papa Pius IX, Papa Leo XIII, Papa Pius X, Papa Benedict XV na Papa Pius XI.
Hali hii ilisababisha Mapapa kutotambua Kingdom of Italy na pia kulalamika mara kwa mara kwa jamii ya kimataifa kwamba wanaishi kama wafungwa ndani ya kuta za Vatican kutokana na ukandamizaji wa Kingdom of Italy na hofu waliyonayo kutoka nje ya kuta za Vatican.
Hii inatufikisha mpaka miaka ya 1920s wakati wa utawala wa Benito Mussolini akiwa Waziri Mkuu wa Italy.
Mussolini alichoshwa na malalamiko haya ya Papa na majibizano ya kila mara huku Papa bado akishikilia msimamo wa kutoitambua Italy
Mussolini mwanasiasa mahiri kama ajulikanavyo akaona fursa hapa ya kuandika jina lake kwenye vitabu vya historia.
Akapendekeza makubaliano maalumu kwa Papa. Kwamba atafanya yafuatayo;
1. Italy itatoa ardhi ya Vatican kwa Papa na iwe himaya/nchi iliyo chini ya utawala wa Papa.
2. Italy itatoa fedha kama fidia kwa Papa kutokana na manyanyaso ya miaka yote.
Mussolini alihitaji Papa kufanya yafuatayo;
1. Papa atambue Italy kuwa ni nchi.
2. Papa asijihusishe wala kutoa maoni yoyote kuhusu masuala ya kisiasa na vita.
Papa na Mussolini wakafikia makubaliano na mikataba ikasainiwa na hapa ndipo taifa dogo zaidi duniani likazaliwa, Vatican.
Vatican ikaanza kujiendesha kama taifa linalojitegemea kwa kuwa na sarafu yake, serikali yake, Polisi wake, jela yake (ndio kuna jela Vatican), Posta yake, Plate number zake, Passport zake na kadhalika na kadhalika.
Vatican si kama nchi nyingine duniani kwa hiyo usidhani kwamba tayari umeielewa Vatican, hicho nilichoeleza ni theluthi tu mkanganyiko wa kuielewa Vatican kama nchi… kunywa tena glass ya maji and relax!! Nitaeleza tena kidogo…
Ili kuielewa Vatican walau kiduchu kuna watu wawili tunapaswa kuwafahamu;
1. Papa
2. Mfalme wa Vatican
Na pia kuna vitu viwili vya kuvielewa;
1. The Holy See
2. Vatican City
Tuanze kimoja kimoja…
*1. Papa*
Hii sihitaji kueleza sana karibia wote tunafahamu. Lakini kwa msingi wa awali kabisa, Papa ni askofu wa Wakatoliki wote waliopo Rome/Vatican lakini kwa kuwa yeye pia ndiye kiongozi wa Wakatoliki wote duniani ndio sababu ya Uaskofu wake kuwa Papa.
*2. The Holy See*
Kabla sijaeleza chochote kuhusu Mfalme wa Vatican kwanza nieleze kuhusu The Holy See. Hili ni moja ya mambo magumu zaidi kuyaelewa kuhusu Vatican. Nitaeleza kwa lugha nyepesi na uchache ili tusipasue vichwa kwa mikanganyiko.
Kwa tafsiri nyepesi Holy See ni 'Throne' ya Papa (nakosa neno zuri la kiswahili, sipendezwi sana na tafsiri ya 'Kiti cha Enzi').
Ni kwamba, maaskofu wote ndani ya kanisa Katoliki wanakuwa na 'throne' lakini kwa kuwa 'throne' ya Papa ni maalumu (kiongozi wa Wakatoliki wote duniani) kwa hiyo throne yake inakuwa muhimu zaidi na inaitwa 'The Holy See'.
Mapapa wanabadilika lakini The Holy See iko na itaendelea kuwepo siku zote.
Yaani kwa mfano Papa anapofariki au kustaafu kama tulivyoona mwaka juzi, Makadinali wanapokusanyika Vatican kwa uhalisia wanaenda kumchagua Kadinali mwenzao ambaye atakalia 'throne' ya 'Holy See'.
Kwa 'angle' nyingine tunaweza kusema kwamba 'The Holy See' ndiyo sheria na mamlaka yote inayofanya kanisa Katoliki kuwa namna lilivyo. Pia sheria zote za kanisa Katoliki na mfumo wake unatengenezwa na The Holy See (sio Papa).
Pia tunaweza kusema kwamba Benito Mussolini alipofanya makubaliano na Vatican aliingia mkataba ule na 'The Holy See'.
Pia unaweza usiamini lakini katika nyanja za sheria za kimataifa 'The Holy See' inatambulika kama mtu/kampuni halisi ambaye amesajiliwa kisheria.
Labda nitumie lugha nyepesi zaidi ya mfano… ukitaka kuelewa The Holy See, chukulia mfano huu kwamba Holy See ni "Catholic Church Inc." alafu Papa ndiye CEO.
Nimejitahidi kueleza kwa kifupi na kwa wepesi niwezavyo, kuielewa kwa undani zaidi The Holy See labda tunapaswa kuandaa andishi maalumu mahususi kwa ajili yake tu.
*3. Mfalme wa Vatican*
Mfalme wa Vatican ni mtawala mwenye mamlaka yote juu ya nchi ya Vatican na hii inaifanya Vatican kuwa moja kati ya nchi sita pekee duniani zenye wafalme wenye mamlaka kamili (absolute monarchy). Nchi nyingine tano ni Saudi Arabia, Brunei, Oman, Qatar, Oman na Swaziland.
Hii ndio sababu kwanini Vatican hawawezi kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa sababu EU wanakubali nchi zenye mfumo wa kidemokrasia pekee.
Japokuwa Vatican ina tawi la 'bunge' ambalo linaundwa na makadinali wa Vatican ambayo wanatunga sheria za 'nchi' lakini bado mfalme wa Vatican anauwezo wa kuveto maamuzi yoyote ambayo wamefikia.
*Swali: Kwanini hatusikii chochote kuhusu Mfalme wa Vatican??*
Ni kwa sababu Mfalme wa Vatican na Papa ni wajibu na mamlaka mbili tofauti lakini zinakaliwa na mtu mmoja, Papa wa Kanisa Katoliki.
Hii inatupa kitu kingine cha kipekee kuhusu Vatican.
Papa anachaguliwa na makadinali wenzake - Demokrasia.
Lakini Mfalme hachaguliwi.
Hii inafanya Vatican kuwa nchi pekee kwenye historia ya dunia kuwa na Mfalme mwenye mamlaka kamili ambaye si wa kurithi na anapatikana kidemokrasia (Elected non-heridetary absolute Monarchy).
Kwa hiyo Papa kulingana na muktadha na mazingira ya suala husika kuna muda anatumia mamlaka yake kama Papa na muda mwingine inampasa kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Vatican.
Bado kuna mkanganyiko???
Zingatia mfano huu rahisi; tuseme kwamba kuna kampuni fulani kubwa ya kimataifa inaitwa Aman Enterprises (The Holy See kwa mada yetu). Aman Enterprises wakafanikiwa kuishwishi Tanzania kuwapatia kisiwa cha Mbudya na Bold Enterprises wanakibadilisha kisiwa cha Mbudya kuwa nchi inayojitegemea, labda iitwe Aman Land (Vatican City kwa mfano wetu).
Sasa CEO wa kampuni Bwana Aman (Papa kwa mada yetu) anahamishiamanya makao makuu ya kampuni mpaka Aman Land. Kwa kuwa Aman Land sasa ni nchi, CEO wa kampuni anakuwa pia mtawala wa nchi hii, Mfalme.
.
Kwa hiyo kwa manufaa ya kampuni kutumia 'connection' zake za kimataifa kunufaisha taifa lake la Aman Land ni vyema kutumia mamlaka kama CEO wa Bold Enterprises na kuna muda akihitaji nchi yake ya Aman Land kutunga sheria na taratibu ambazo zitanufaisha kampuni izidi kushamiri ni vyema kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Aman Land.
Haya ndio mamlaka mawili yaliyo chini ya mtu mmoja ndani ya vatican, Papa na Mfalme wa Vatican.
Bado kuna mkanganyiko???
Kama haujaelewa sawia usihofu kwa maana bado kuna hata nchi nyingine duniani bado hawaelewi sawa sawa mfumo mzima wa Vatican.
Mfano, Umoja wa Mataifa wamekubali The Holy See (corporation) kama mwanachama wake lakini sio Vatican City nchi yenyewe.
Passports za raia wa Vatican zinatolewa na The Holy See na sio Vatican na zinakubalika kwenye nchi nyingine japokuwa The Holy See kimataifa inatambulika kisheria kama Kampuni inayojitegemea.
Na hapa tuongee kiduchu pia kuhusu raia wa Vatican. Katika nchi nyingine raia wa wanaongezeka kutokana na kuzaliana lakini hapa Vatican hakuna hilo kutokana na idadi ndogo ya wanaweka kiasi kwamba karibia ni asilimia sufuri. Namna pekee ya kuwa raia wa Vatican ni kwa kupewa uraia na Mfalme wa Vatican ili uishi Vatican kama moja wa wasaidizi wa Papa (ambaye ndiye mfalme). Kwa hiyo siku ukiacha kazi, yaani usaidizi wako kwa Papa ukifikia kikomo, Mfalme wa Vatican (ambayr ndiye Papa) anaondoa uraia wako na unarudi kwenu.
Katika muda wowote ule raia wa nchi ya Vatican wanakadiriwa kuwa jumla karibia ya 500 ambao ndio idadi ndogo zaidi ya raia kwa nchi na ndogo kushinda hata idadi ya watu wanaoishi kwenye ghorofa moja kwenye nchi nyingi.
Na raia wote hawa ni wafanyakazi wa Papa/The Holy See ambao wanapewa uraia na Mfalme (ambaye ndiye Papa) ambapo wanafanya kazi kama Makadinali, Wanadiplomasia, walinzi au kazi nyingine za kikanisa.
Kwa ufupi sana hii ndio picha halisi ya nchi ya Vatican… na hapa ndipo ambapo maisha ya kiroho ya wafuasi zaidi ya Billioni 2 yanapoendeshwa…