• Katika siasa za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), jina la Corneille Nangaa limepita katika nyanja tofauti.

    Kutoka kuwa msomi wa uchumi, mtumishi wa Umoja wa Mataifa (UNDP), msimamizi wa uchaguzi mkuu.

    Hadi sasa kuwa mmoja wa watu wanaoitikisa nchi hiyo kwa kiwango kikubwa.

    Mwanaume huyu ambaye aliwahi kuwa miongoni mwa watendaji wakubwa wa serikali, sasa anatajwa kuwa nyuma ya moja ya harakati hatari zaidi zinazoendelea katika ardhi ya Congo.

    Akiwa na historia ndefu ya kushika nafasi za juu serikalini, alifikia hatua ya kuanzisha chama chake cha kisiasa, Action for Change (AFC).

    Lakini hatua zake zilizoibua taharuki kubwa ni uhusiano wake wa karibu na kundi la waasi la M23, ambalo hivi sasa linatajwa kuwa jeshi lake binafsi.

    Lakini vipi msomi huyu wa uchumi alihamia kutoka kuongoza uchaguzi hadi kusimamia jeshi la waasi?

    Corneille Nangaa alianza kama msomi wa uchumi, akipata elimu yake kutoka Chuo Kikuu cha Kinshasa.
    Katika siasa za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), jina la Corneille Nangaa limepita katika nyanja tofauti. Kutoka kuwa msomi wa uchumi, mtumishi wa Umoja wa Mataifa (UNDP), msimamizi wa uchaguzi mkuu. Hadi sasa kuwa mmoja wa watu wanaoitikisa nchi hiyo kwa kiwango kikubwa. Mwanaume huyu ambaye aliwahi kuwa miongoni mwa watendaji wakubwa wa serikali, sasa anatajwa kuwa nyuma ya moja ya harakati hatari zaidi zinazoendelea katika ardhi ya Congo. Akiwa na historia ndefu ya kushika nafasi za juu serikalini, alifikia hatua ya kuanzisha chama chake cha kisiasa, Action for Change (AFC). Lakini hatua zake zilizoibua taharuki kubwa ni uhusiano wake wa karibu na kundi la waasi la M23, ambalo hivi sasa linatajwa kuwa jeshi lake binafsi. Lakini vipi msomi huyu wa uchumi alihamia kutoka kuongoza uchaguzi hadi kusimamia jeshi la waasi? Corneille Nangaa alianza kama msomi wa uchumi, akipata elimu yake kutoka Chuo Kikuu cha Kinshasa.
    0 Commentarii ·0 Distribuiri ·870 Views
  • Akiwa na uelewa mkubwa wa masuala ya kifedha na uchumi wa dunia, alijiunga na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika la Maendeleo (UNDP), ambako alifanya kazi kwa miaka kadhaa.

    Kupitia UNDP, alihusika katika miradi mbalimbali ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Congo, jambo lililompatia uzoefu mkubwa wa utawala.

    Ndiye aliyekuwa kiungo kati ya mashirika ya kimataifa na serikali ya Congo, akisimamia miradi ya maendeleo katika nchi iliyojaa changamoto za kisiasa na kiusalama.

    Uwezo wake wa kusimamia taasisi na kuelewa siasa za ndani ulimfanya kuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa serikalini, jambo lililomfungulia milango ya nafasi kubwa zaidi.

    Mwaka 2015, Corneille Nangaa aliteuliwa kuwa Rais wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI), moja ya nafasi zenye ushawishi mkubwa nchini Congo.
    Hili lilimpa mamlaka ya kusimamia uchaguzi mkuu wa 2018, uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa kati ya wapinzani wa Joseph Kabila na viongozi wa upinzani.

    Katika uchaguzi huo, Corneille Nangaa alisimamia na hatimaye kutangaza ushindi wa Félix Tshisekedi kuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
    Akiwa na uelewa mkubwa wa masuala ya kifedha na uchumi wa dunia, alijiunga na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika la Maendeleo (UNDP), ambako alifanya kazi kwa miaka kadhaa. Kupitia UNDP, alihusika katika miradi mbalimbali ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Congo, jambo lililompatia uzoefu mkubwa wa utawala. Ndiye aliyekuwa kiungo kati ya mashirika ya kimataifa na serikali ya Congo, akisimamia miradi ya maendeleo katika nchi iliyojaa changamoto za kisiasa na kiusalama. Uwezo wake wa kusimamia taasisi na kuelewa siasa za ndani ulimfanya kuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa serikalini, jambo lililomfungulia milango ya nafasi kubwa zaidi. Mwaka 2015, Corneille Nangaa aliteuliwa kuwa Rais wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI), moja ya nafasi zenye ushawishi mkubwa nchini Congo. Hili lilimpa mamlaka ya kusimamia uchaguzi mkuu wa 2018, uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa kati ya wapinzani wa Joseph Kabila na viongozi wa upinzani. Katika uchaguzi huo, Corneille Nangaa alisimamia na hatimaye kutangaza ushindi wa Félix Tshisekedi kuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
    0 Commentarii ·0 Distribuiri ·348 Views
  • Wow
    1
    · 0 Commentarii ·0 Distribuiri ·116 Views
  • 0 Commentarii ·0 Distribuiri ·119 Views
  • Nchi ya Kenya imetuma Askari wengine 144 Nchini Haïti, kwa ajili ya kulinda amani na kurejesha utulivu Nchini humo ambao imepotea kwa miaka kadhaa sasa. Askari hao, ambao ni Wanaume 120 na Wanawake 24, wameelekea Haiti asubuhi ya Februari 6, 2025 baada ya kuagwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Kipchumba Murkomen.

    Idadi ya Askari hao kutoka Nchini Kenya inafikisha jumla ya Askari Polisi 744 waliotumwa Nchini Haiti kwa ajili ya kupambana na magenge ya kihalifu yaliyokithiri Nchini humo pamoja na uvunjwaji wa amani.

    Nchi ya Kenya 🇰🇪 imetuma Askari wengine 144 Nchini Haïti🇭🇹, kwa ajili ya kulinda amani na kurejesha utulivu Nchini humo ambao imepotea kwa miaka kadhaa sasa. Askari hao, ambao ni Wanaume 120 na Wanawake 24, wameelekea Haiti asubuhi ya Februari 6, 2025 baada ya kuagwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Kipchumba Murkomen. Idadi ya Askari hao kutoka Nchini Kenya inafikisha jumla ya Askari Polisi 744 waliotumwa Nchini Haiti kwa ajili ya kupambana na magenge ya kihalifu yaliyokithiri Nchini humo pamoja na uvunjwaji wa amani.
    Like
    1
    · 0 Commentarii ·0 Distribuiri ·659 Views
  • 0 Commentarii ·0 Distribuiri ·120 Views
  • Uamuzi huo ulizua sintofahamu kubwa, kwani upinzani ulidai kuwa matokeo hayo yalikuwa na mizengwe.

    Wapo waliodai kuwa Nangaa alihusika moja kwa moja kuhakikisha Tshisekedi anashinda ili kumaliza utawala wa muda mrefu wa Joseph Kabila.

    Lakini wakati watu walidhani kuwa jukumu lake katika siasa za Congo limeishia hapo, mambo yalibadilika ghafla.

    Badala ya kustaafu kwenye siasa, Corneille Nangaa aliibuka na Action for Change (AFC), chama kipya cha kisiasa ambacho kilionekana kuja na ajenda tofauti.

    Alianza kujenga ushawishi mkubwa ndani na nje ya Congo, huku akijitokeza kama mpinzani wa utawala wa Tshisekedi aliyechangia kumuweka madarakani.

    Lakini hatua iliyotikisa Congo ni pale ilipogundulika kuwa Nangaa sasa alikuwa na uhusiano wa karibu na kundi la waasi la M23, ambalo linajulikana kwa mapigano yake dhidi ya serikali ya Congo.

    Kwa muda mrefu, kundi la M23 limekuwa likipambana na serikali, likidai haki kwa jamii ya Watutsi wa Congo.

    Lakini sasa, kulikuwa na mabadiliko makubwa M23, haikuwa tu kundi la waasi, bali lilionekana kama jeshi binafsi la Corneille Nangaa.

    Uamuzi huo ulizua sintofahamu kubwa, kwani upinzani ulidai kuwa matokeo hayo yalikuwa na mizengwe. Wapo waliodai kuwa Nangaa alihusika moja kwa moja kuhakikisha Tshisekedi anashinda ili kumaliza utawala wa muda mrefu wa Joseph Kabila. Lakini wakati watu walidhani kuwa jukumu lake katika siasa za Congo limeishia hapo, mambo yalibadilika ghafla. Badala ya kustaafu kwenye siasa, Corneille Nangaa aliibuka na Action for Change (AFC), chama kipya cha kisiasa ambacho kilionekana kuja na ajenda tofauti. Alianza kujenga ushawishi mkubwa ndani na nje ya Congo, huku akijitokeza kama mpinzani wa utawala wa Tshisekedi aliyechangia kumuweka madarakani. Lakini hatua iliyotikisa Congo ni pale ilipogundulika kuwa Nangaa sasa alikuwa na uhusiano wa karibu na kundi la waasi la M23, ambalo linajulikana kwa mapigano yake dhidi ya serikali ya Congo. Kwa muda mrefu, kundi la M23 limekuwa likipambana na serikali, likidai haki kwa jamii ya Watutsi wa Congo. Lakini sasa, kulikuwa na mabadiliko makubwa M23, haikuwa tu kundi la waasi, bali lilionekana kama jeshi binafsi la Corneille Nangaa.
    Like
    1
    · 0 Commentarii ·0 Distribuiri ·801 Views
  • Mtoto wa Lionel Messi, Thiago Messi amefunga mabao (11) kwenye mchezo ulioikutanisha klabu yake ya Inter Miami ya Watoto wenye umri chini ya miaka (13) dhidi ya klabu ya Atlanta United ambapo mchezo umemaliza kwa ushindi Inter Miami wa mabao (12-0).

    Thiago Messi amefanya hivyo kwa kufunga mabao hayo (11) ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu Mtoto wa Cristiano Ronaldo, Cristiano Junior kuifungia klabu yake ya Al Nasr (Watoto) mabao matano (5) kwenye mchezo mmoja.

    Mtoto wa Lionel Messi, Thiago Messi amefunga mabao (11) kwenye mchezo ulioikutanisha klabu yake ya Inter Miami ya Watoto wenye umri chini ya miaka (13) dhidi ya klabu ya Atlanta United ambapo mchezo umemaliza kwa ushindi Inter Miami wa mabao (12-0). Thiago Messi amefanya hivyo kwa kufunga mabao hayo (11) ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu Mtoto wa Cristiano Ronaldo, Cristiano Junior kuifungia klabu yake ya Al Nasr (Watoto) mabao matano (5) kwenye mchezo mmoja.
    Like
    1
    · 1 Commentarii ·0 Distribuiri ·457 Views
  • Mwaka 2017, Program hii ya aina ya CHATGPT kabla haijaanza kuitwa Akili bandia, Mfanyabiashara Tajiri na maarufu Duniani, Bill Gates alisema kuwa Tekinolojia hii inaweza kuwa tishio baadaye. Kwa sasa inaonyesha jinsi gani Teknolojia za AI zinavyoshika kasi Duniani kote.

    Mwanzilishi huyo wa kampuni ya Microsoft, Bill gates alisema kuwa kampuni ambazo zinaunda Maroboti kwa ajili ya kuchukua ajira za Watu wanatakiwa kulipia kodi ya kuhusu mashine (Roboti) hizo kama wanavyofanya kwa Wanadamu wanavyolipa kodi.

    Kutokana na maendeleo ya Tekinolojia ya AI inavyokwenda kwa kasi na inatishia kuchukua kazi za Watu mbalimbali basi, inapaswa wale Wamiliki wa maroboti kulipa kodi ya mashine zao ili kuwepo na usawa huo kati ya mashine hizo na Binadamu (Watu) kwa sababu Watu wanalipa kodi kwa ajili ya kazi zao ila maroboti hayo hayalipi kodi kwa kufanya kazi hizo za Kibinadamu.

    Mwaka 2017, Program hii ya aina ya CHATGPT kabla haijaanza kuitwa Akili bandia, Mfanyabiashara Tajiri na maarufu Duniani, Bill Gates alisema kuwa Tekinolojia hii inaweza kuwa tishio baadaye. Kwa sasa inaonyesha jinsi gani Teknolojia za AI zinavyoshika kasi Duniani kote. Mwanzilishi huyo wa kampuni ya Microsoft, Bill gates alisema kuwa kampuni ambazo zinaunda Maroboti kwa ajili ya kuchukua ajira za Watu wanatakiwa kulipia kodi ya kuhusu mashine (Roboti) hizo kama wanavyofanya kwa Wanadamu wanavyolipa kodi. Kutokana na maendeleo ya Tekinolojia ya AI inavyokwenda kwa kasi na inatishia kuchukua kazi za Watu mbalimbali basi, inapaswa wale Wamiliki wa maroboti kulipa kodi ya mashine zao ili kuwepo na usawa huo kati ya mashine hizo na Binadamu (Watu) kwa sababu Watu wanalipa kodi kwa ajili ya kazi zao ila maroboti hayo hayalipi kodi kwa kufanya kazi hizo za Kibinadamu.
    0 Commentarii ·0 Distribuiri ·856 Views
  • Ripoti mbalimbali zilionesha kuwa Nangaa alikuwa akilitumia kundi hilo kama silaha yake ya kisiasa na kijeshi.

    Huku akipewa misaada ya kifedha na baadhi ya mataifa ya nje yenye maslahi katika siasa za Congo.

    Sasa Congo iko njia panda. Corneille Nangaa, ambaye miaka michache iliyopita alihusika katika kuleta utawala wa sasa, sasa anatajwa kama mmoja wa watu wanaotaka kuipindua serikali.

    Je, anataka kuwa Rais?
    Au ana ajenda nyingine ya siri?

    Wakati serikali ya Tshisekedi ikifanya kila juhudi kuhakikisha Nangaa na jeshi lake wanadhibitiwa, ukweli unabaki kuwa Congo imeingia katika mgogoro mpya

    Jeshi la M23 likiwa linazidi kuimarika, na Nangaa akiwa nyuma ya harakati hizo, taifa linakabiliwa na changamoto kubwa ya usalama na utulivu wa kisiasa.

    Ikiwa hatua hazitachukuliwa haraka, huenda Congo ikajikuta kwenye mgogoro mkubwa zaidi wa kisiasa na kijeshi na jina la Corneille Nangaa litakuwa miongoni mwa majina yatakayotajwa kwa historia ndefu katika taifa hilo.

    Ripoti mbalimbali zilionesha kuwa Nangaa alikuwa akilitumia kundi hilo kama silaha yake ya kisiasa na kijeshi. Huku akipewa misaada ya kifedha na baadhi ya mataifa ya nje yenye maslahi katika siasa za Congo. Sasa Congo iko njia panda. Corneille Nangaa, ambaye miaka michache iliyopita alihusika katika kuleta utawala wa sasa, sasa anatajwa kama mmoja wa watu wanaotaka kuipindua serikali. Je, anataka kuwa Rais? Au ana ajenda nyingine ya siri? Wakati serikali ya Tshisekedi ikifanya kila juhudi kuhakikisha Nangaa na jeshi lake wanadhibitiwa, ukweli unabaki kuwa Congo imeingia katika mgogoro mpya Jeshi la M23 likiwa linazidi kuimarika, na Nangaa akiwa nyuma ya harakati hizo, taifa linakabiliwa na changamoto kubwa ya usalama na utulivu wa kisiasa. Ikiwa hatua hazitachukuliwa haraka, huenda Congo ikajikuta kwenye mgogoro mkubwa zaidi wa kisiasa na kijeshi na jina la Corneille Nangaa litakuwa miongoni mwa majina yatakayotajwa kwa historia ndefu katika taifa hilo.
    0 Commentarii ·0 Distribuiri ·334 Views