• Hi
    Hi
    0 Comments ·0 Shares ·168 Views
  • 0 Comments ·0 Shares ·164 Views
  • Hawa M23 Hawataki Utani..

    Waasi wa M23 wametangaza serikali mpya katika Jimbo la Kivu Kaskazini, DRC, baada ya kuuteka mji wa Goma wiki moja iliyopita.

    Kanali Bahati Musanga ameteuliwa kuwa Gavana, huku Willy Manzi na Shadary Bahati wakiwa Manaibu Gavana.
    Hawa M23 Hawataki Utani.. Waasi wa M23 wametangaza serikali mpya katika Jimbo la Kivu Kaskazini, DRC, baada ya kuuteka mji wa Goma wiki moja iliyopita. Kanali Bahati Musanga ameteuliwa kuwa Gavana, huku Willy Manzi na Shadary Bahati wakiwa Manaibu Gavana.
    Sad
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·244 Views
  • Hawa M23 Hawataki Utani..

    Waasi wa M23 wametangaza serikali mpya katika Jimbo la Kivu Kaskazini, DRC, baada ya kuuteka mji wa Goma wiki moja iliyopita.

    Kanali Bahati Musanga ameteuliwa kuwa Gavana, huku Willy Manzi na Shadary Bahati wakiwa Manaibu Gavana.
    Hawa M23 Hawataki Utani.. Waasi wa M23 wametangaza serikali mpya katika Jimbo la Kivu Kaskazini, DRC, baada ya kuuteka mji wa Goma wiki moja iliyopita. Kanali Bahati Musanga ameteuliwa kuwa Gavana, huku Willy Manzi na Shadary Bahati wakiwa Manaibu Gavana.
    0 Comments ·0 Shares ·250 Views

  • Katika uteuzi huo, pia wamemteua Meya wa Jiji la Goma pamoja na Wakuu wa Wilaya mbalimbali.

    Hatua hii inakuja wakati maeneo kama Walikale, Lubero, na Beni bado yako chini ya udhibiti wa serikali ya DRC inayoongozwa na Félix Tshisekedi.

    M23, kundi la waasi lenye silaha nzito na za kisasa, linadai kuwa linapigania haki za jamii ya Watutsi wa Congo.

    Jamii ya Watutsi waishio Congo mara nyingi hutengwa, huku serikali ya DRC ikiwatambua kama Wanyarwanda wanaoishi nchini humo.

    Taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa, zikiwemo Umoja wa Mataifa na serikali ya DRC, zinadai kuwa kundi hili linaungwa mkono na Rwanda kwa maslahi ya kiuchumi na kisiasa.

    Hata hivyo, M23 wamekanusha vikali tuhuma hizo, wakisisitiza kuwa hawapokei msaada wa kijeshi kutoka Rwanda na kwamba wanapigana kwa maslahi yao wenyewe..

    Katika uteuzi huo, pia wamemteua Meya wa Jiji la Goma pamoja na Wakuu wa Wilaya mbalimbali. Hatua hii inakuja wakati maeneo kama Walikale, Lubero, na Beni bado yako chini ya udhibiti wa serikali ya DRC inayoongozwa na Félix Tshisekedi. M23, kundi la waasi lenye silaha nzito na za kisasa, linadai kuwa linapigania haki za jamii ya Watutsi wa Congo. Jamii ya Watutsi waishio Congo mara nyingi hutengwa, huku serikali ya DRC ikiwatambua kama Wanyarwanda wanaoishi nchini humo. Taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa, zikiwemo Umoja wa Mataifa na serikali ya DRC, zinadai kuwa kundi hili linaungwa mkono na Rwanda kwa maslahi ya kiuchumi na kisiasa. Hata hivyo, M23 wamekanusha vikali tuhuma hizo, wakisisitiza kuwa hawapokei msaada wa kijeshi kutoka Rwanda na kwamba wanapigana kwa maslahi yao wenyewe..
    0 Comments ·0 Shares ·314 Views
  • Kutangazwa kwa serikali hii mpya kumepokelewa kwa tahadhari kubwa.

    Jumuiya za kimataifa zina wasiwasi kuhusu usalama wa raia na mali zao, huku zikiendelea kutoa mwito wa utulivu na mazungumzo ya amani.

    Mgogoro huu umeibua hofu ya kuzuka kwa janga kubwa la kibinadamu, linaloweza kusababisha vifo vingi na kuwalazimu maelfu ya watu kuyahama makazi yao.

    Serikali ya DRC imekosoa hatua hii, ikisisitiza kuwa itaendelea kupambana na waasi ili kurejesha mamlaka yake katika maeneo yote ya Kivu Kaskazini.

    Hali ya usalama katika Goma na maeneo jirani inazidi kuzorota, huku shughuli za kiuchumi zikidorora kwa kasi.

    Maelfu ya raia wameyakimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea. Mashirika ya misaada yanafanya juhudi kusaidia waathirika wa mgogoro huu..

    Kutangazwa kwa serikali hii mpya kumepokelewa kwa tahadhari kubwa. Jumuiya za kimataifa zina wasiwasi kuhusu usalama wa raia na mali zao, huku zikiendelea kutoa mwito wa utulivu na mazungumzo ya amani. Mgogoro huu umeibua hofu ya kuzuka kwa janga kubwa la kibinadamu, linaloweza kusababisha vifo vingi na kuwalazimu maelfu ya watu kuyahama makazi yao. Serikali ya DRC imekosoa hatua hii, ikisisitiza kuwa itaendelea kupambana na waasi ili kurejesha mamlaka yake katika maeneo yote ya Kivu Kaskazini. Hali ya usalama katika Goma na maeneo jirani inazidi kuzorota, huku shughuli za kiuchumi zikidorora kwa kasi. Maelfu ya raia wameyakimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea. Mashirika ya misaada yanafanya juhudi kusaidia waathirika wa mgogoro huu..
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·438 Views
  • Jumuiya ya kimataifa inafuatilia kwa karibu hali inayoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), huku mashirika ya haki za binadamu yakilaani uhalifu wa kivita unaofanywa na pande zote dhidi ya raia.

    Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa maelfu ya watu wamelazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea, huku ukatili dhidi ya wanawake na watoto ukiongezeka kwa kiwango cha kutisha.

    Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetangaza kuwa inafuatilia kwa karibu mzozo huu na imeonya kuwa yeyote anayehusika na uhalifu wa kivita, dhidi ya binadamu, au mauaji ya halaiki hatosazwa na mkono wa sheria.

    Mgogoro wa DRC ni wa muda mrefu na wenye mizizi mirefu. Tangu miaka ya 1990, taifa hili limepitia machafuko ya mara kwa mara, yakichochewa na rasilimali za madini,ukosefu wa utawala thabiti, na uhusiano tata wa kisiasa kati ya mataifa jirani, hususan Rwanda na Uganda.

    M23, kundi la waasi linalotajwa kupokea msaada kutoka nje, limeendelea kushikilia maeneo muhimu, hususan Goma, na hata kutishia kuuteka mji wa Kinshasa.

    Katika mazingira haya, kama ungekuwa Rais wa DRC, Félix Tshisekedi, ungefanya nini?

    Kwa mtazamo wangu, suluhisho pekee ni mazungumzo na diplomasia.

    Historia imeonyesha kuwa vita dhidi ya makundi ya waasi kama M23 si rahisi kushinda kwa nguvu za kijeshi pekee.

    Licha ya msaada wa kijeshi kutoka kwa MONUSCO (Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC) na majeshi ya kikanda kama vile EACRF (East African Community Regional Force), kundi hili limeendelea kuwa tishio kubwa kwa utawala wa Tshisekedi.

    Ikiwa Rais Tshisekedi ataendelea kulazimisha suluhisho la kijeshi bila mpango wa mazungumzo, hatari ipo kwamba mapigano yatapanuka zaidi, na hata kutishia utulivu wa taifa kwa ujumla.

    Hatua muhimu kwa sasa ni kuitisha mazungumzo ya dhati na kutafuta njia ya kidiplomasia ya kumaliza mgogoro huu kabla hali haijazidi kuwa mbaya.
    Jumuiya ya kimataifa inafuatilia kwa karibu hali inayoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), huku mashirika ya haki za binadamu yakilaani uhalifu wa kivita unaofanywa na pande zote dhidi ya raia. Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa maelfu ya watu wamelazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea, huku ukatili dhidi ya wanawake na watoto ukiongezeka kwa kiwango cha kutisha. Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetangaza kuwa inafuatilia kwa karibu mzozo huu na imeonya kuwa yeyote anayehusika na uhalifu wa kivita, dhidi ya binadamu, au mauaji ya halaiki hatosazwa na mkono wa sheria. Mgogoro wa DRC ni wa muda mrefu na wenye mizizi mirefu. Tangu miaka ya 1990, taifa hili limepitia machafuko ya mara kwa mara, yakichochewa na rasilimali za madini,ukosefu wa utawala thabiti, na uhusiano tata wa kisiasa kati ya mataifa jirani, hususan Rwanda na Uganda. M23, kundi la waasi linalotajwa kupokea msaada kutoka nje, limeendelea kushikilia maeneo muhimu, hususan Goma, na hata kutishia kuuteka mji wa Kinshasa. Katika mazingira haya, kama ungekuwa Rais wa DRC, Félix Tshisekedi, ungefanya nini? Kwa mtazamo wangu, suluhisho pekee ni mazungumzo na diplomasia. Historia imeonyesha kuwa vita dhidi ya makundi ya waasi kama M23 si rahisi kushinda kwa nguvu za kijeshi pekee. Licha ya msaada wa kijeshi kutoka kwa MONUSCO (Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC) na majeshi ya kikanda kama vile EACRF (East African Community Regional Force), kundi hili limeendelea kuwa tishio kubwa kwa utawala wa Tshisekedi. Ikiwa Rais Tshisekedi ataendelea kulazimisha suluhisho la kijeshi bila mpango wa mazungumzo, hatari ipo kwamba mapigano yatapanuka zaidi, na hata kutishia utulivu wa taifa kwa ujumla. Hatua muhimu kwa sasa ni kuitisha mazungumzo ya dhati na kutafuta njia ya kidiplomasia ya kumaliza mgogoro huu kabla hali haijazidi kuwa mbaya.
    0 Comments ·0 Shares ·995 Views
  • Je, nini kinaweza kuwa suluhisho la kudumu kwa Kivu Kaskazini na DRC kwa ujumla?

    Mazungumzo ya kina na makundi ya waasi – Kupitia majadiliano yanayojumuisha waasi, serikali, na wadau wa kikanda ili kufikia makubaliano ya amani.

    Kushughulikia mizizi ya mgogoro – Mgogoro wa DRC unahusiana na rasilimali, ukabila, na siasa za kikanda. Ni lazima kuwe na suluhisho la kisera linalozingatia haya yote.

    Msaada wa kimataifa wenye ufanisi – Umoja wa Mataifa na jumuiya za kikanda kama AU na EAC wanapaswa kushirikiana kuhakikisha kuwa msaada wa kijeshi na diplomasia unakwenda sambamba.

    Marekebisho ya kijeshi na kiuchumi – Kuimarisha jeshi la DRC na kupunguza utegemezi wa wanajeshi wa kigeni, pamoja na kuweka mikakati ya maendeleo ili wananchi wa Kivu Kaskazini wapate ajira na fursa badala ya kushawishika kujiunga na makundi ya waasi.

    Kwa sasa, swali kubwa linabaki:

    Je, Tshisekedi atachagua vita au diplomasia?

    Na je, nini kingekuwa suluhisho la kudumu kwa mgogoro wa Kivu Kaskazini na DRC kwa ujumla?
    Je, nini kinaweza kuwa suluhisho la kudumu kwa Kivu Kaskazini na DRC kwa ujumla? Mazungumzo ya kina na makundi ya waasi – Kupitia majadiliano yanayojumuisha waasi, serikali, na wadau wa kikanda ili kufikia makubaliano ya amani. Kushughulikia mizizi ya mgogoro – Mgogoro wa DRC unahusiana na rasilimali, ukabila, na siasa za kikanda. Ni lazima kuwe na suluhisho la kisera linalozingatia haya yote. Msaada wa kimataifa wenye ufanisi – Umoja wa Mataifa na jumuiya za kikanda kama AU na EAC wanapaswa kushirikiana kuhakikisha kuwa msaada wa kijeshi na diplomasia unakwenda sambamba. Marekebisho ya kijeshi na kiuchumi – Kuimarisha jeshi la DRC na kupunguza utegemezi wa wanajeshi wa kigeni, pamoja na kuweka mikakati ya maendeleo ili wananchi wa Kivu Kaskazini wapate ajira na fursa badala ya kushawishika kujiunga na makundi ya waasi. Kwa sasa, swali kubwa linabaki: Je, Tshisekedi atachagua vita au diplomasia? Na je, nini kingekuwa suluhisho la kudumu kwa mgogoro wa Kivu Kaskazini na DRC kwa ujumla?
    Wow
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·520 Views
  • Katika siasa za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), jina la Corneille Nangaa limepita katika nyanja tofauti.

    Kutoka kuwa msomi wa uchumi, mtumishi wa Umoja wa Mataifa (UNDP), msimamizi wa uchaguzi mkuu.

    Hadi sasa kuwa mmoja wa watu wanaoitikisa nchi hiyo kwa kiwango kikubwa.

    Mwanaume huyu ambaye aliwahi kuwa miongoni mwa watendaji wakubwa wa serikali, sasa anatajwa kuwa nyuma ya moja ya harakati hatari zaidi zinazoendelea katika ardhi ya Congo.

    Akiwa na historia ndefu ya kushika nafasi za juu serikalini, alifikia hatua ya kuanzisha chama chake cha kisiasa, Action for Change (AFC).

    Lakini hatua zake zilizoibua taharuki kubwa ni uhusiano wake wa karibu na kundi la waasi la M23, ambalo hivi sasa linatajwa kuwa jeshi lake binafsi.

    Lakini vipi msomi huyu wa uchumi alihamia kutoka kuongoza uchaguzi hadi kusimamia jeshi la waasi?

    Corneille Nangaa alianza kama msomi wa uchumi, akipata elimu yake kutoka Chuo Kikuu cha Kinshasa.
    Katika siasa za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), jina la Corneille Nangaa limepita katika nyanja tofauti. Kutoka kuwa msomi wa uchumi, mtumishi wa Umoja wa Mataifa (UNDP), msimamizi wa uchaguzi mkuu. Hadi sasa kuwa mmoja wa watu wanaoitikisa nchi hiyo kwa kiwango kikubwa. Mwanaume huyu ambaye aliwahi kuwa miongoni mwa watendaji wakubwa wa serikali, sasa anatajwa kuwa nyuma ya moja ya harakati hatari zaidi zinazoendelea katika ardhi ya Congo. Akiwa na historia ndefu ya kushika nafasi za juu serikalini, alifikia hatua ya kuanzisha chama chake cha kisiasa, Action for Change (AFC). Lakini hatua zake zilizoibua taharuki kubwa ni uhusiano wake wa karibu na kundi la waasi la M23, ambalo hivi sasa linatajwa kuwa jeshi lake binafsi. Lakini vipi msomi huyu wa uchumi alihamia kutoka kuongoza uchaguzi hadi kusimamia jeshi la waasi? Corneille Nangaa alianza kama msomi wa uchumi, akipata elimu yake kutoka Chuo Kikuu cha Kinshasa.
    0 Comments ·0 Shares ·747 Views
  • Akiwa na uelewa mkubwa wa masuala ya kifedha na uchumi wa dunia, alijiunga na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika la Maendeleo (UNDP), ambako alifanya kazi kwa miaka kadhaa.

    Kupitia UNDP, alihusika katika miradi mbalimbali ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Congo, jambo lililompatia uzoefu mkubwa wa utawala.

    Ndiye aliyekuwa kiungo kati ya mashirika ya kimataifa na serikali ya Congo, akisimamia miradi ya maendeleo katika nchi iliyojaa changamoto za kisiasa na kiusalama.

    Uwezo wake wa kusimamia taasisi na kuelewa siasa za ndani ulimfanya kuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa serikalini, jambo lililomfungulia milango ya nafasi kubwa zaidi.

    Mwaka 2015, Corneille Nangaa aliteuliwa kuwa Rais wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI), moja ya nafasi zenye ushawishi mkubwa nchini Congo.
    Hili lilimpa mamlaka ya kusimamia uchaguzi mkuu wa 2018, uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa kati ya wapinzani wa Joseph Kabila na viongozi wa upinzani.

    Katika uchaguzi huo, Corneille Nangaa alisimamia na hatimaye kutangaza ushindi wa Félix Tshisekedi kuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
    Akiwa na uelewa mkubwa wa masuala ya kifedha na uchumi wa dunia, alijiunga na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika la Maendeleo (UNDP), ambako alifanya kazi kwa miaka kadhaa. Kupitia UNDP, alihusika katika miradi mbalimbali ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Congo, jambo lililompatia uzoefu mkubwa wa utawala. Ndiye aliyekuwa kiungo kati ya mashirika ya kimataifa na serikali ya Congo, akisimamia miradi ya maendeleo katika nchi iliyojaa changamoto za kisiasa na kiusalama. Uwezo wake wa kusimamia taasisi na kuelewa siasa za ndani ulimfanya kuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa serikalini, jambo lililomfungulia milango ya nafasi kubwa zaidi. Mwaka 2015, Corneille Nangaa aliteuliwa kuwa Rais wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI), moja ya nafasi zenye ushawishi mkubwa nchini Congo. Hili lilimpa mamlaka ya kusimamia uchaguzi mkuu wa 2018, uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa kati ya wapinzani wa Joseph Kabila na viongozi wa upinzani. Katika uchaguzi huo, Corneille Nangaa alisimamia na hatimaye kutangaza ushindi wa Félix Tshisekedi kuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
    0 Comments ·0 Shares ·320 Views