• Social Pop @socialpop Asante kwa Bluetick Tupo pamoja
    [Socialpop1] @socialpop Asante kwa Bluetick Tupo pamoja 👊
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·19 Views
  • Chukua hii.

    Kama utakwenda Nchini Japan na kusikia neno "Johatsu" (じょうはつ) tambua kuwa ni Mtu au Watu waliotoweka (kupotea) kutoka kwenye familia zao kutokana na sababu mbalimbali kama vile migogoro kwenye Ndoa, kushindwa kuoa, kukimbia madeni, kufukuzwa kazi na kadhalika. Watu hao huacha maisha yao na kuishi bila kujulikana wapi walipo kwa muda fulani na inaweze kuwa ni ndani ya Nchi ya Japan au nje Nchi yaani mataifa mengine kama vile Tanzania DR Congo , Burundi , Marekani , Mexico , Kenya ,....

    Pamoja na Watu hao kupotea, lakini wanasaidiwa na Makampuni ambayo yamebobea katika kazi hiyo yaani Watu au Mtu anayehitaji huduma hiyo unalipia kisha kuhamishwa usiku. Makampuni hayo maalumu yanajulikana kwa jina la "Wahamishaji Usiku" huwasaidia Watu kupotea (unaweza kusema kujiteka, kujipoteza,...).

    Haya Mashirika au Makampuni husaidia Watu kutoweka kwa kuwahamisha kwa siri sana na mara nyingi kazi hii hufanyika usiku na wanapokupeleka inakuwa ni siri kubwa yaani kuanzia mahali pa kulala, utakula nini, vitambulisho vipya vya kusafiria Kampuni hizo ndizo zinafanya kila kitu kwa mujibu wa mkataba wenu.

    Pia Kampuni hizi zitahakikisha zinasafisha kumbukumbu zote za Mteja na kusahaulika kwenye Jamii, Nyumbani na Nchi kwa ujumla kisha unaanza mwanzo mpya wa kuanzisha maisha mengine kwenye Nchi au mahali walipo kupeleka.

    Chukua hii. Kama utakwenda Nchini Japan 🇯🇵 na kusikia neno "Johatsu" (じょうはつ) tambua kuwa ni Mtu au Watu waliotoweka (kupotea) kutoka kwenye familia zao kutokana na sababu mbalimbali kama vile migogoro kwenye Ndoa, kushindwa kuoa, kukimbia madeni, kufukuzwa kazi na kadhalika. Watu hao huacha maisha yao na kuishi bila kujulikana wapi walipo kwa muda fulani na inaweze kuwa ni ndani ya Nchi ya Japan au nje Nchi yaani mataifa mengine kama vile Tanzania 🇨🇩 DR Congo 🇨🇩, Burundi 🇧🇮, Marekani 🇺🇸, Mexico 🇲🇽, Kenya 🇰🇪,.... Pamoja na Watu hao kupotea, lakini wanasaidiwa na Makampuni ambayo yamebobea katika kazi hiyo yaani Watu au Mtu anayehitaji huduma hiyo unalipia kisha kuhamishwa usiku. Makampuni hayo maalumu yanajulikana kwa jina la "Wahamishaji Usiku" huwasaidia Watu kupotea (unaweza kusema kujiteka, kujipoteza,...). Haya Mashirika au Makampuni husaidia Watu kutoweka kwa kuwahamisha kwa siri sana na mara nyingi kazi hii hufanyika usiku na wanapokupeleka inakuwa ni siri kubwa yaani kuanzia mahali pa kulala, utakula nini, vitambulisho vipya vya kusafiria Kampuni hizo ndizo zinafanya kila kitu kwa mujibu wa mkataba wenu. Pia Kampuni hizi zitahakikisha zinasafisha kumbukumbu zote za Mteja na kusahaulika kwenye Jamii, Nyumbani na Nchi kwa ujumla kisha unaanza mwanzo mpya wa kuanzisha maisha mengine kwenye Nchi au mahali walipo kupeleka.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·89 Views
  • Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·15 Views
  • Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·15 Views
  • Vinicius Junior amegoma kusaini mkataba mpya ndani ya klabu ya Real Madrid. Klabu hiyo imepanga kukutana nae ili kumshawishi zaidi huku mshahara ukiboresha hadi kufikia Euro milioni (15€) karibu na ule wa Mbappé. Pamoja na ongezeko hilo la mshahara lakini Vinicius Junior amepangua mkataba huo.

    Klabu Real Madrid imeomba kukutana nae ili kuangalia namna ya kufanya maboresho zaidi.
    (The Athletic).

    Vinicius Junior amegoma kusaini mkataba mpya ndani ya klabu ya Real Madrid. Klabu hiyo imepanga kukutana nae ili kumshawishi zaidi huku mshahara ukiboresha hadi kufikia Euro milioni (15€) karibu na ule wa Mbappé. Pamoja na ongezeko hilo la mshahara lakini Vinicius Junior amepangua mkataba huo. Klabu Real Madrid imeomba kukutana nae ili kuangalia namna ya kufanya maboresho zaidi. (The Athletic).
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·81 Views
  • Jux na Mchumba wake Priscilla (kutoka Nchini Nigeria ) wamefunga pingu ya maisha (Ndoa) leo hii.

    Jux na Mchumba wake Priscilla (kutoka Nchini Nigeria 🇳🇬) wamefunga pingu ya maisha (Ndoa) leo hii.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·64 Views
  • Miaka ya 90, Ukraine alikuwa mbabe sana. Taifa hili lilikuwa lina nguvu za kijeshi ambazo ziliwafanya majirani zake kusita hata kufikiria kulivamia.

    Sababu?

    Lilikuwa na zaidi ya mabomu 1,000 ya nyuklia. Haya si mabomu ya kawaida, ni silaha za maangamizi ambazo zingeweza kuifuta dunia katika sekunde chache.

    Lakini kama ilivyo kwa kila hadithi ya usaliti, Ukraine alifanya kosa moja kubwa, aliamini watu wengine badala ya kujilinda mwenyewe.

    Marekani, Urusi na Uingereza walimfuata kwa heshima kubwa, wakampigia magoti na kumwambia.

    "Tafadhali, haribu mabomu yako. Dunia itakuwa mahali salama zaidi, na sisi tutakuwa walinzi wako. Hatutakuacha."
    Ukraine akakubali. Akayaangamiza mabomu yake yote ya nyuklia. Mikataba iliwekwa. Ahadi zikaandikwa kwa kalamu na kutiwa muhuri.

    Ukraine akaamini kabisa kuwa usalama wake hauwezi kutikiswa tena.
    Miaka ya 90, Ukraine alikuwa mbabe sana. Taifa hili lilikuwa lina nguvu za kijeshi ambazo ziliwafanya majirani zake kusita hata kufikiria kulivamia. Sababu? Lilikuwa na zaidi ya mabomu 1,000 ya nyuklia. Haya si mabomu ya kawaida, ni silaha za maangamizi ambazo zingeweza kuifuta dunia katika sekunde chache. Lakini kama ilivyo kwa kila hadithi ya usaliti, Ukraine alifanya kosa moja kubwa, aliamini watu wengine badala ya kujilinda mwenyewe. Marekani, Urusi na Uingereza walimfuata kwa heshima kubwa, wakampigia magoti na kumwambia. "Tafadhali, haribu mabomu yako. Dunia itakuwa mahali salama zaidi, na sisi tutakuwa walinzi wako. Hatutakuacha." Ukraine akakubali. Akayaangamiza mabomu yake yote ya nyuklia. Mikataba iliwekwa. Ahadi zikaandikwa kwa kalamu na kutiwa muhuri. Ukraine akaamini kabisa kuwa usalama wake hauwezi kutikiswa tena.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·74 Views
  • Muda ukasonga. Dunia ikabadilika. Mataifa yakaanza kuweka mbele maslahi yao, na Ukraine akajikuta akilia peke yake kwenye uwanja wa vita.

    Aliyeahidi kumlinda Urusi ndiye huyo anayemshambulia kwa mabomu, vifaru na ndege za kivita.

    Kwa miaka mingi, Vladimir Putin alikuwa anaangalia ramani ya dunia akijiuliza, "Mbona Crimea na Donbas zipo nje ya milki yangu?"

    Halafu, ghafla mwaka 2014, Urusi ikaamua kumng'ata Ukraine kwa mara ya kwanza.

    Crimea ikachukuliwa, na dunia ikakaa kimya. Hakukuwa na hatua kubwa zilizochukuliwa na Marekani wala Uingereza. Ukraine akaanza kuona dalili za usaliti.

    Mwaka 2022, Urusi ikarudi tena, safari hii kwa nguvu kubwa zaidi.
    Tishio la silaha za nyuklia lililomfanya Ukraine kuwa mbabe, halikuwepo tena. Hakuwa na kinga tena, alikuwa mtu mwepesi wa kushambuliwa.

    Na hapa ndipo Ukraine alipogundua kosa lake kubwa aliamini makaratasi kuliko mabavu.
    Muda ukasonga. Dunia ikabadilika. Mataifa yakaanza kuweka mbele maslahi yao, na Ukraine akajikuta akilia peke yake kwenye uwanja wa vita. Aliyeahidi kumlinda Urusi ndiye huyo anayemshambulia kwa mabomu, vifaru na ndege za kivita. Kwa miaka mingi, Vladimir Putin alikuwa anaangalia ramani ya dunia akijiuliza, "Mbona Crimea na Donbas zipo nje ya milki yangu?" Halafu, ghafla mwaka 2014, Urusi ikaamua kumng'ata Ukraine kwa mara ya kwanza. Crimea ikachukuliwa, na dunia ikakaa kimya. Hakukuwa na hatua kubwa zilizochukuliwa na Marekani wala Uingereza. Ukraine akaanza kuona dalili za usaliti. Mwaka 2022, Urusi ikarudi tena, safari hii kwa nguvu kubwa zaidi. Tishio la silaha za nyuklia lililomfanya Ukraine kuwa mbabe, halikuwepo tena. Hakuwa na kinga tena, alikuwa mtu mwepesi wa kushambuliwa. Na hapa ndipo Ukraine alipogundua kosa lake kubwa aliamini makaratasi kuliko mabavu.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·129 Views
  • Marekani, Alitoa msaada wa miezi mitatu tu, kisha akaanza kulegeza kamba. Kwa sasa, Marekani imechoshwa na vita vya Ukraine.

    Wameona haina faida ya kuendelea kutoa silaha zisizoleta matokeo ya haraka.

    Uingereza, Ipo kama haipo. Iliahidi mengi, lakini imetulia kimya huku Waukraine wakiteketea kwenye moto wa kivita.

    Ulaya, Inajifanya ina wasiwasi, lakini ukweli ni kwamba kila nchi inajitazama yenyewe kwanza.

    Ukraine yuko peke yake.

    Na hapa ndipo tujiulize. Je, kweli Ukraine aliangamiza kila kitu?

    Inawezekana hana mabomu ya nyuklia tena, lakini ana akili, ana wataalamu, ana formula za kuyatengeneza.

    Na kama historia ni mwalimu, basi ni suala la muda tu kabla ya Ukraine kuamua kuchukua mkondo mpya.
    Vita vya Ukraine vimekuwa mzigo mzito kwa Urusi. Jeshi lake limepoteza askari wengi, uchumi wake umebanwa, na nguvu yake ya kijeshi imetetereka.
    Marekani, Alitoa msaada wa miezi mitatu tu, kisha akaanza kulegeza kamba. Kwa sasa, Marekani imechoshwa na vita vya Ukraine. Wameona haina faida ya kuendelea kutoa silaha zisizoleta matokeo ya haraka. Uingereza, Ipo kama haipo. Iliahidi mengi, lakini imetulia kimya huku Waukraine wakiteketea kwenye moto wa kivita. Ulaya, Inajifanya ina wasiwasi, lakini ukweli ni kwamba kila nchi inajitazama yenyewe kwanza. Ukraine yuko peke yake. Na hapa ndipo tujiulize. Je, kweli Ukraine aliangamiza kila kitu? Inawezekana hana mabomu ya nyuklia tena, lakini ana akili, ana wataalamu, ana formula za kuyatengeneza. Na kama historia ni mwalimu, basi ni suala la muda tu kabla ya Ukraine kuamua kuchukua mkondo mpya. Vita vya Ukraine vimekuwa mzigo mzito kwa Urusi. Jeshi lake limepoteza askari wengi, uchumi wake umebanwa, na nguvu yake ya kijeshi imetetereka.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·84 Views
  • Putin sasa anazunguka huku na kule akitafuta suluhu ya amani, lakini Ukraine naye amegoma kusalimu amri.

    Katika ramani ya dunia, mababe wawili wamebaki, Marekani na China.

    Marekani bado inatawala masoko ya dunia, ina silaha za kisasa, na inafanya kila kitu kuhakikisha inabaki juu.

    China inakuja kwa kasi, ikitumia siasa za uchumi badala ya vita. Wanajua kuwa kushinda vita vya sasa, sio kwa mabomu tu bali kwa pesa na teknolojia.

    Urusi? Imebanwa. Vita na Ukraine imeichosha. Mipango ya kupanua mipaka imekufa. Na sasa dunia inajiuliza Putin anaweza kushindwa?

    Hii dunia ina kanuni moja kubwa, Usimwamini mtu. Na hata kama ukimwamini mtu, basi huyo mtu awe wewe mwenyewe.

    Ukraine alifanya kosa ambalo sasa linamgharimu. Aliamini ahadi za mataifa makubwa bila kuhakikisha ana kinga yake mwenyewe. Akasahau kuwa siasa za dunia haziongozwi na ahadi, bali na nguvu.

    Hili liwe somo kwa kila taifa linalotegemea misaada kutoka nje. Leo wanakupenda, kesho wakishapata wanachotaka, wanakusahau.

    Na dunia ilivyo sasa, muda wowote inaweza kulipuka. Mataifa yanapimana nguvu, migogoro inaongezeka, na tunakaribia kuona enzi mpya ya vita vya madaraka kati ya Marekani na China.

    Ukraine, Anajifunza kwa uchungu kuwa historia haimsahau mjinga.
    Putin sasa anazunguka huku na kule akitafuta suluhu ya amani, lakini Ukraine naye amegoma kusalimu amri. Katika ramani ya dunia, mababe wawili wamebaki, Marekani na China. Marekani bado inatawala masoko ya dunia, ina silaha za kisasa, na inafanya kila kitu kuhakikisha inabaki juu. China inakuja kwa kasi, ikitumia siasa za uchumi badala ya vita. Wanajua kuwa kushinda vita vya sasa, sio kwa mabomu tu bali kwa pesa na teknolojia. Urusi? Imebanwa. Vita na Ukraine imeichosha. Mipango ya kupanua mipaka imekufa. Na sasa dunia inajiuliza Putin anaweza kushindwa? Hii dunia ina kanuni moja kubwa, Usimwamini mtu. Na hata kama ukimwamini mtu, basi huyo mtu awe wewe mwenyewe. Ukraine alifanya kosa ambalo sasa linamgharimu. Aliamini ahadi za mataifa makubwa bila kuhakikisha ana kinga yake mwenyewe. Akasahau kuwa siasa za dunia haziongozwi na ahadi, bali na nguvu. Hili liwe somo kwa kila taifa linalotegemea misaada kutoka nje. Leo wanakupenda, kesho wakishapata wanachotaka, wanakusahau. Na dunia ilivyo sasa, muda wowote inaweza kulipuka. Mataifa yanapimana nguvu, migogoro inaongezeka, na tunakaribia kuona enzi mpya ya vita vya madaraka kati ya Marekani na China. Ukraine, Anajifunza kwa uchungu kuwa historia haimsahau mjinga.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·147 Views