0 Comments
·0 Shares
·14 Views
-
Kuna gereza, na kuna Guantanamo Bay.
Hili si gereza la kawaida. Ni shimo la mateso, mahali ambapo sheria za haki za binadamu zinaonekana kama hadithi za kufikirika.
Lipo Cuba, lakini linamilikiwa na Marekani.
Wanasema gereza ni sehemu ya kutumikia adhabu, lakini Guantanamo ni sehemu ambapo unatakiwa kusahau kama ulikuwa binadamu.
Kama umewekwa hapa, ni ishara kwamba dunia imeshakusahau.
Na hata kama hauna hatia, hutaweza kuthibitisha chochote.
Marekani ni taifa la haki, Ndio! angalau kwenye makaratasi.
Lakini hata Wamarekani wenyewe walikuwa hawapendi Guantanamo.
Kila mwaka, wanaharakati wa haki za binadamu walikuwa wakiandamana, wakitaka gereza hilo lifungwe.
Ilipofika mwaka 2008, Barack Obama alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha urais, akaahidi jambo moja kubwa.
"Nikichaguliwa kuwa Rais, gereza la Guantanamo litafungwa mara moja!"
Ilionekana kama ahadi ya kweli.
Wamarekani wakashangilia, wakaamini kwamba hatimaye heshima ya taifa lao itarudi.
Kuna gereza, na kuna Guantanamo Bay. Hili si gereza la kawaida. Ni shimo la mateso, mahali ambapo sheria za haki za binadamu zinaonekana kama hadithi za kufikirika. Lipo Cuba, lakini linamilikiwa na Marekani. Wanasema gereza ni sehemu ya kutumikia adhabu, lakini Guantanamo ni sehemu ambapo unatakiwa kusahau kama ulikuwa binadamu. Kama umewekwa hapa, ni ishara kwamba dunia imeshakusahau. Na hata kama hauna hatia, hutaweza kuthibitisha chochote. Marekani ni taifa la haki, Ndio! angalau kwenye makaratasi. Lakini hata Wamarekani wenyewe walikuwa hawapendi Guantanamo. Kila mwaka, wanaharakati wa haki za binadamu walikuwa wakiandamana, wakitaka gereza hilo lifungwe. Ilipofika mwaka 2008, Barack Obama alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha urais, akaahidi jambo moja kubwa. "Nikichaguliwa kuwa Rais, gereza la Guantanamo litafungwa mara moja!" Ilionekana kama ahadi ya kweli. Wamarekani wakashangilia, wakaamini kwamba hatimaye heshima ya taifa lao itarudi.0 Comments ·0 Shares ·2 Views -
Na kweli, wakampigia kura, Obama akaingia madarakani.
Mwaka wa kwanza ukapita.
Mwaka wa pili ukapita.
Mwaka wa tatu ukapita.
Gereza bado liko palepale.
Kila alipoulizwa juu ya ahadi yake, alitoa majibu yasiyoeleweka.
Ndani ya miaka yake minane madarakani, Guantanamo Bay liliendelea kuwepo.
Ndipo Wamarekani wakagundua kitu.
Hata Rais hana nguvu juu ya gereza hili.
Wakati Trump akaingia madarakani, yeye hakutumia Guantanamo kama njia ya kuombea kura.
Hakusema atalifunga.
Hakusema atalifungua.
Lakini alipoingia, akatoa amri ya kuhamisha wafungwa zaidi ya 30,000.
Lengo lake lilikuwa moja tu.
"Tuhakikishe gereza linajaa wale ambao kweli wanastahili kuwepo humo."
Na kweli, wakampigia kura, Obama akaingia madarakani. Mwaka wa kwanza ukapita. Mwaka wa pili ukapita. Mwaka wa tatu ukapita. Gereza bado liko palepale. Kila alipoulizwa juu ya ahadi yake, alitoa majibu yasiyoeleweka. Ndani ya miaka yake minane madarakani, Guantanamo Bay liliendelea kuwepo. Ndipo Wamarekani wakagundua kitu. Hata Rais hana nguvu juu ya gereza hili. Wakati Trump akaingia madarakani, yeye hakutumia Guantanamo kama njia ya kuombea kura. Hakusema atalifunga. Hakusema atalifungua. Lakini alipoingia, akatoa amri ya kuhamisha wafungwa zaidi ya 30,000. Lengo lake lilikuwa moja tu. "Tuhakikishe gereza linajaa wale ambao kweli wanastahili kuwepo humo."0 Comments ·0 Shares ·1 Views -
Hivyo, wale waliokuwa hawana ushahidi wa moja kwa moja wakaanza kuhamishwa.
Lakini wale waliokuwa na rekodi ya ugaidi wa kiwango cha juu, wakabaki.
Kwa Trump, Guantanamo lilikuwa muhimu.
Lilikuwa sehemu ya kuhakikisha magaidi hawana sehemu ya kujificha.
Hapa hakuna kesi.
Hakuna mawakili.
Hakuna upendeleo.
Ukiingia, unasahau kama kuna dunia nje.
Mateso yanayotokea ndani ya gereza hili ni siri kubwa ya Marekani.
Lakini waliowahi kutoka, au maafisa wa zamani wa CIA na FBI, wamesema kwamba mateso ya Guantanamo yanaweza kumfanya mtu mwenye msimamo mkali wa kidini aseme Yesu alikuwa Muislam na Muhammad alikuwa Myahudi.
Hivyo, wale waliokuwa hawana ushahidi wa moja kwa moja wakaanza kuhamishwa. Lakini wale waliokuwa na rekodi ya ugaidi wa kiwango cha juu, wakabaki. Kwa Trump, Guantanamo lilikuwa muhimu. Lilikuwa sehemu ya kuhakikisha magaidi hawana sehemu ya kujificha. Hapa hakuna kesi. Hakuna mawakili. Hakuna upendeleo. Ukiingia, unasahau kama kuna dunia nje. Mateso yanayotokea ndani ya gereza hili ni siri kubwa ya Marekani. Lakini waliowahi kutoka, au maafisa wa zamani wa CIA na FBI, wamesema kwamba mateso ya Guantanamo yanaweza kumfanya mtu mwenye msimamo mkali wa kidini aseme Yesu alikuwa Muislam na Muhammad alikuwa Myahudi.0 Comments ·0 Shares ·1 Views -
Wanasema kwamba ukiingizwa kwenye chumba cha mateso, unaweza kuanza kuongea kabla hata hawajauliza maswali.
Ule ukali wa "Sitawataja washikaji wangu" unayeyuka ndani ya saa moja.
Gereza hili linawafanya hata magaidi waliokuwa na imani kali kuwa wepesi kama karatasi.
Ndiyo maana wanasema,
"Magaidi wengi wanaoingizwa humo, hawachukui muda kutaja mnyororo mzima wa washikaji zao."
Kwa kifupi, Guantanamo ni gereza ambalo lina mlango wa kuingilia, lakini hauna mlango wa kutokea.
Ni jela ambayo ukishaingia, unaishi kwa maombi hata kama wewe si mtu wa dini.
Wanasema kwamba ukiingizwa kwenye chumba cha mateso, unaweza kuanza kuongea kabla hata hawajauliza maswali. Ule ukali wa "Sitawataja washikaji wangu" unayeyuka ndani ya saa moja. Gereza hili linawafanya hata magaidi waliokuwa na imani kali kuwa wepesi kama karatasi. Ndiyo maana wanasema, "Magaidi wengi wanaoingizwa humo, hawachukui muda kutaja mnyororo mzima wa washikaji zao." Kwa kifupi, Guantanamo ni gereza ambalo lina mlango wa kuingilia, lakini hauna mlango wa kutokea. Ni jela ambayo ukishaingia, unaishi kwa maombi hata kama wewe si mtu wa dini.0 Comments ·0 Shares ·1 Views -
-