0 Comments
·0 Shares
·18 Views
-
Kuna gereza, na kuna Guantanamo Bay.
Hili si gereza la kawaida. Ni shimo la mateso, mahali ambapo sheria za haki za binadamu zinaonekana kama hadithi za kufikirika.
Lipo Cuba, lakini linamilikiwa na Marekani.
Wanasema gereza ni sehemu ya kutumikia adhabu, lakini Guantanamo ni sehemu ambapo unatakiwa kusahau kama ulikuwa binadamu.
Kama umewekwa hapa, ni ishara kwamba dunia imeshakusahau.
Na hata kama hauna hatia, hutaweza kuthibitisha chochote.
Marekani ni taifa la haki, Ndio! angalau kwenye makaratasi.
Lakini hata Wamarekani wenyewe walikuwa hawapendi Guantanamo.
Kila mwaka, wanaharakati wa haki za binadamu walikuwa wakiandamana, wakitaka gereza hilo lifungwe.
Ilipofika mwaka 2008, Barack Obama alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha urais, akaahidi jambo moja kubwa.
"Nikichaguliwa kuwa Rais, gereza la Guantanamo litafungwa mara moja!"
Ilionekana kama ahadi ya kweli.
Wamarekani wakashangilia, wakaamini kwamba hatimaye heshima ya taifa lao itarudi.
Kuna gereza, na kuna Guantanamo Bay. Hili si gereza la kawaida. Ni shimo la mateso, mahali ambapo sheria za haki za binadamu zinaonekana kama hadithi za kufikirika. Lipo Cuba, lakini linamilikiwa na Marekani. Wanasema gereza ni sehemu ya kutumikia adhabu, lakini Guantanamo ni sehemu ambapo unatakiwa kusahau kama ulikuwa binadamu. Kama umewekwa hapa, ni ishara kwamba dunia imeshakusahau. Na hata kama hauna hatia, hutaweza kuthibitisha chochote. Marekani ni taifa la haki, Ndio! angalau kwenye makaratasi. Lakini hata Wamarekani wenyewe walikuwa hawapendi Guantanamo. Kila mwaka, wanaharakati wa haki za binadamu walikuwa wakiandamana, wakitaka gereza hilo lifungwe. Ilipofika mwaka 2008, Barack Obama alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha urais, akaahidi jambo moja kubwa. "Nikichaguliwa kuwa Rais, gereza la Guantanamo litafungwa mara moja!" Ilionekana kama ahadi ya kweli. Wamarekani wakashangilia, wakaamini kwamba hatimaye heshima ya taifa lao itarudi.0 Comments ·0 Shares ·8 Views -
Na kweli, wakampigia kura, Obama akaingia madarakani.
Mwaka wa kwanza ukapita.
Mwaka wa pili ukapita.
Mwaka wa tatu ukapita.
Gereza bado liko palepale.
Kila alipoulizwa juu ya ahadi yake, alitoa majibu yasiyoeleweka.
Ndani ya miaka yake minane madarakani, Guantanamo Bay liliendelea kuwepo.
Ndipo Wamarekani wakagundua kitu.
Hata Rais hana nguvu juu ya gereza hili.
Wakati Trump akaingia madarakani, yeye hakutumia Guantanamo kama njia ya kuombea kura.
Hakusema atalifunga.
Hakusema atalifungua.
Lakini alipoingia, akatoa amri ya kuhamisha wafungwa zaidi ya 30,000.
Lengo lake lilikuwa moja tu.
"Tuhakikishe gereza linajaa wale ambao kweli wanastahili kuwepo humo."
Na kweli, wakampigia kura, Obama akaingia madarakani. Mwaka wa kwanza ukapita. Mwaka wa pili ukapita. Mwaka wa tatu ukapita. Gereza bado liko palepale. Kila alipoulizwa juu ya ahadi yake, alitoa majibu yasiyoeleweka. Ndani ya miaka yake minane madarakani, Guantanamo Bay liliendelea kuwepo. Ndipo Wamarekani wakagundua kitu. Hata Rais hana nguvu juu ya gereza hili. Wakati Trump akaingia madarakani, yeye hakutumia Guantanamo kama njia ya kuombea kura. Hakusema atalifunga. Hakusema atalifungua. Lakini alipoingia, akatoa amri ya kuhamisha wafungwa zaidi ya 30,000. Lengo lake lilikuwa moja tu. "Tuhakikishe gereza linajaa wale ambao kweli wanastahili kuwepo humo."0 Comments ·0 Shares ·8 Views -
Hivyo, wale waliokuwa hawana ushahidi wa moja kwa moja wakaanza kuhamishwa.
Lakini wale waliokuwa na rekodi ya ugaidi wa kiwango cha juu, wakabaki.
Kwa Trump, Guantanamo lilikuwa muhimu.
Lilikuwa sehemu ya kuhakikisha magaidi hawana sehemu ya kujificha.
Hapa hakuna kesi.
Hakuna mawakili.
Hakuna upendeleo.
Ukiingia, unasahau kama kuna dunia nje.
Mateso yanayotokea ndani ya gereza hili ni siri kubwa ya Marekani.
Lakini waliowahi kutoka, au maafisa wa zamani wa CIA na FBI, wamesema kwamba mateso ya Guantanamo yanaweza kumfanya mtu mwenye msimamo mkali wa kidini aseme Yesu alikuwa Muislam na Muhammad alikuwa Myahudi.
Hivyo, wale waliokuwa hawana ushahidi wa moja kwa moja wakaanza kuhamishwa. Lakini wale waliokuwa na rekodi ya ugaidi wa kiwango cha juu, wakabaki. Kwa Trump, Guantanamo lilikuwa muhimu. Lilikuwa sehemu ya kuhakikisha magaidi hawana sehemu ya kujificha. Hapa hakuna kesi. Hakuna mawakili. Hakuna upendeleo. Ukiingia, unasahau kama kuna dunia nje. Mateso yanayotokea ndani ya gereza hili ni siri kubwa ya Marekani. Lakini waliowahi kutoka, au maafisa wa zamani wa CIA na FBI, wamesema kwamba mateso ya Guantanamo yanaweza kumfanya mtu mwenye msimamo mkali wa kidini aseme Yesu alikuwa Muislam na Muhammad alikuwa Myahudi.0 Comments ·0 Shares ·6 Views -
Wanasema kwamba ukiingizwa kwenye chumba cha mateso, unaweza kuanza kuongea kabla hata hawajauliza maswali.
Ule ukali wa "Sitawataja washikaji wangu" unayeyuka ndani ya saa moja.
Gereza hili linawafanya hata magaidi waliokuwa na imani kali kuwa wepesi kama karatasi.
Ndiyo maana wanasema,
"Magaidi wengi wanaoingizwa humo, hawachukui muda kutaja mnyororo mzima wa washikaji zao."
Kwa kifupi, Guantanamo ni gereza ambalo lina mlango wa kuingilia, lakini hauna mlango wa kutokea.
Ni jela ambayo ukishaingia, unaishi kwa maombi hata kama wewe si mtu wa dini.
Wanasema kwamba ukiingizwa kwenye chumba cha mateso, unaweza kuanza kuongea kabla hata hawajauliza maswali. Ule ukali wa "Sitawataja washikaji wangu" unayeyuka ndani ya saa moja. Gereza hili linawafanya hata magaidi waliokuwa na imani kali kuwa wepesi kama karatasi. Ndiyo maana wanasema, "Magaidi wengi wanaoingizwa humo, hawachukui muda kutaja mnyororo mzima wa washikaji zao." Kwa kifupi, Guantanamo ni gereza ambalo lina mlango wa kuingilia, lakini hauna mlango wa kutokea. Ni jela ambayo ukishaingia, unaishi kwa maombi hata kama wewe si mtu wa dini.0 Comments ·0 Shares ·5 Views -
-
-
"Kazi bado ni ngumu katika mzozo wa Drc ukitazama maoni ya Marais wa Afrika mashariki utagundua kuwa hii ngoma bado ngumu!!
Marais wengi wanashauri Tshsekedi afanye mazungumzo na M23 ili kufikia makubaliano na hatimaye amani, ugumu ni kuwa Rais Tshsekedi na serikali yake ya Congo imeapa kamwe haitazungumza na waasi na kufanya hivyo ni kitu ambacho Congo hawataki
Ugumu ni kuwa tayari M23 imejitangazia serikali yake huko Goma kitendo ambacho ni sawa na uhaini kwa serikali ya Tshsekedi na Tshsekedi hataki kuzungumza na wahaini wa serikali yake
Hivyo kwa sasa fahamu kuwa sio M23 wanaokataa mazungumzo bali serikali ya Congo ambayo inaona kufanya hivyo ni kuwapa nguvu zaidi waasi
Ni wazi kuwa njia pekee anayoitaka Tshsekedi ni kutumia mtutu wa silaha dhidi ya M23 kitu ambacho kwa sasa ni kigumu kwa sababu jeshi la Congo ni dhaifu, na hawezi bila msaada wa majeshi mengine.. Congo bado ngoma ni ngumu!!" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.
"Kazi bado ni ngumu katika mzozo wa Drc ukitazama maoni ya Marais wa Afrika mashariki utagundua kuwa hii ngoma bado ngumu!! Marais wengi wanashauri Tshsekedi afanye mazungumzo na M23 ili kufikia makubaliano na hatimaye amani, ugumu ni kuwa Rais Tshsekedi na serikali yake ya Congo imeapa kamwe haitazungumza na waasi na kufanya hivyo ni kitu ambacho Congo hawataki Ugumu ni kuwa tayari M23 imejitangazia serikali yake huko Goma kitendo ambacho ni sawa na uhaini kwa serikali ya Tshsekedi na Tshsekedi hataki kuzungumza na wahaini wa serikali yake Hivyo kwa sasa fahamu kuwa sio M23 wanaokataa mazungumzo bali serikali ya Congo ambayo inaona kufanya hivyo ni kuwapa nguvu zaidi waasi Ni wazi kuwa njia pekee anayoitaka Tshsekedi ni kutumia mtutu wa silaha dhidi ya M23 kitu ambacho kwa sasa ni kigumu kwa sababu jeshi la Congo ni dhaifu, na hawezi bila msaada wa majeshi mengine.. Congo bado ngoma ni ngumu!!" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.0 Comments ·0 Shares ·5 Views -
#PART12
Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite.
Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo.
Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba.
Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay.
April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha.
March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.!
(Malisa GJ)
#PART12 Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite. Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo. Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba. Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay. April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha. March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.! (Malisa GJ)0 Comments ·0 Shares ·8 Views -
Kwenye kikao cha pamoja kati ya Jumuiya mbili za SADC na ile ya EAC, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo , Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, ambaye alihudhuria kwa njia ya Mtandao, aliweka wazi matakwa yake kwenye mkutano huo ambapo alisema baadhi ya mambo yakiwemo yafuatayo:
- Nchi ya Rwanda iambiwe ukweli, ionywe na iachane na uvamizi wake huko Mjini Goma.
- Vikosi vya Rwanda viondoke mara moja kwenye maeneo ya DR Congo ambayo wanayamiliki pasipo uhalali.
- Kufunguliwa kwa Uwanja wa Ndege wa Mjini Goma kwa ajili ya misaada ya kibinadamu.
- Kurejesha Mji wa Goma kwa Mamlaka ya Serikali ya DR Congo.
Kwenye kikao cha pamoja kati ya Jumuiya mbili za SADC na ile ya EAC, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo 🇨🇩, Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, ambaye alihudhuria kwa njia ya Mtandao, aliweka wazi matakwa yake kwenye mkutano huo ambapo alisema baadhi ya mambo yakiwemo yafuatayo: - Nchi ya Rwanda 🇷🇼 iambiwe ukweli, ionywe na iachane na uvamizi wake huko Mjini Goma. - Vikosi vya Rwanda viondoke mara moja kwenye maeneo ya DR Congo ambayo wanayamiliki pasipo uhalali. - Kufunguliwa kwa Uwanja wa Ndege wa Mjini Goma kwa ajili ya misaada ya kibinadamu. - Kurejesha Mji wa Goma kwa Mamlaka ya Serikali ya DR Congo.0 Comments ·0 Shares ·5 Views