• Love
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·110 Views
  • 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·109 Views
  • #PART5

    Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite.

    Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo.

    Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba.

    Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay.

    April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha.

    March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.

    Kumekua na jitihada mbalimbali za kumaliza mgogoro wa DRC kwa njia za kidiplomasia ikiwemo mkutano wa viongozi wakuu wa SADC na EAC uliofanyika leo jijini Dar.

    #MyaTake:
    1. Congo imeponzwa na ukarimu wake. Wakati wa vita vya Rwanda, Congo ilipokea Watutsi wengi na kuwapa hifadhi, akiwemo Kagame. Baada ya utawala wa Habyarimana kuangushwa Wahutu nao wakakimbilia Congo na kupewa hifadhi. Sasa hicho kimekua kigezo cha Rwanda kuingiza majeshi Congo kila mara kwa madai ya kuwatafuta Wahutu wa FDLR. Kwa lugha rahisi vita ya ndugu wawili (Wahutu na Watutsi) iliyopaswa kupiganwa Rwanda sasa inapiganwa Congo.

    2. Congo inateswa na mipaka ya kikoloni. Laiti wakati wa kuchora mipaka jamii yote ya Watutsi ingewekwa Rwanda, leo kusingekuwa na Banyamulenge Congo, kwahiyo Watutsi wasingepata sababu ya kuishi Congo na kujifanya raia. Ni sawa na kukuta Wamasai 1,000 pale Longido, halafu uambiwe kati yao wapo wa Kenya. Utawajuaje? Utawatofautishaje?

    3. Congo inateswa na rasilimali zake. Kama eneo la Kivu lisingekuwa na utajiri, mgogoro usingekuwa mkubwa kama ulivyo. Rejea #Part1 kujua utajiri uliopo Kivu. Kumbuka bila Kivu dunia haina laptop wala smartphones kwa sababu 80% ya coltan yote duniani inatoka Kivu.

    4. Rwanda na Uganda ni Keyplayers kwenye mgogoro wa Congo. Kwa miaka mingi majeshi yao yameigeuza Congo shamba la bibi. Waondoe majeshi yao Congo.

    5. Viongozi wengi wa M23 ni Wanyarwanda. Huu ni udhibitisho kuwa Rwanda ni kinara kwenye mgogoro huu.

    6. Congo ni kubwa sana na hivyo inakosa jeshi imara la kutosha kulinda mipaka yake yote. Congo ni kubwa mara 90 ya Rwanda. Wapo wanaoshauri igawanywe kama njia ya kutatua mgogoro. Kama ambavyo Yugoslavia iligawanywa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

    7. Kiongozi wa sasa wa M23 Corneille Nangaa alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi 2019 na ndiye aliyemtangaza Tshisekedi kuwa Rais kwa ushindi wa 38%. Lakini alilaumiwa kupunguza kura za Martin Fayulu aliyepata 34%. Huenda kuna ahadi alipewa haikutimizwa ndio maana akaungana na Waasi.

    Sababu hizo hapo juu zikifanyiwa kazi, mgogoro wa Congo unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Mnaopenda kujifunza zaidi, naandika Kitabu. Get ready to have your copy. MWISHO.!

    (Malisa GJ )

    #PART5 Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite. Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo. Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba. Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay. April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha. March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa. Kumekua na jitihada mbalimbali za kumaliza mgogoro wa DRC kwa njia za kidiplomasia ikiwemo mkutano wa viongozi wakuu wa SADC na EAC uliofanyika leo jijini Dar. #MyaTake: 1. Congo imeponzwa na ukarimu wake. Wakati wa vita vya Rwanda, Congo ilipokea Watutsi wengi na kuwapa hifadhi, akiwemo Kagame. Baada ya utawala wa Habyarimana kuangushwa Wahutu nao wakakimbilia Congo na kupewa hifadhi. Sasa hicho kimekua kigezo cha Rwanda kuingiza majeshi Congo kila mara kwa madai ya kuwatafuta Wahutu wa FDLR. Kwa lugha rahisi vita ya ndugu wawili (Wahutu na Watutsi) iliyopaswa kupiganwa Rwanda sasa inapiganwa Congo. 2. Congo inateswa na mipaka ya kikoloni. Laiti wakati wa kuchora mipaka jamii yote ya Watutsi ingewekwa Rwanda, leo kusingekuwa na Banyamulenge Congo, kwahiyo Watutsi wasingepata sababu ya kuishi Congo na kujifanya raia. Ni sawa na kukuta Wamasai 1,000 pale Longido, halafu uambiwe kati yao wapo wa Kenya. Utawajuaje? Utawatofautishaje? 3. Congo inateswa na rasilimali zake. Kama eneo la Kivu lisingekuwa na utajiri, mgogoro usingekuwa mkubwa kama ulivyo. Rejea #Part1 kujua utajiri uliopo Kivu. Kumbuka bila Kivu dunia haina laptop wala smartphones kwa sababu 80% ya coltan yote duniani inatoka Kivu. 4. Rwanda na Uganda ni Keyplayers kwenye mgogoro wa Congo. Kwa miaka mingi majeshi yao yameigeuza Congo shamba la bibi. Waondoe majeshi yao Congo. 5. Viongozi wengi wa M23 ni Wanyarwanda. Huu ni udhibitisho kuwa Rwanda ni kinara kwenye mgogoro huu. 6. Congo ni kubwa sana na hivyo inakosa jeshi imara la kutosha kulinda mipaka yake yote. Congo ni kubwa mara 90 ya Rwanda. Wapo wanaoshauri igawanywe kama njia ya kutatua mgogoro. Kama ambavyo Yugoslavia iligawanywa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe. 7. Kiongozi wa sasa wa M23 Corneille Nangaa alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi 2019 na ndiye aliyemtangaza Tshisekedi kuwa Rais kwa ushindi wa 38%. Lakini alilaumiwa kupunguza kura za Martin Fayulu aliyepata 34%. Huenda kuna ahadi alipewa haikutimizwa ndio maana akaungana na Waasi. Sababu hizo hapo juu zikifanyiwa kazi, mgogoro wa Congo unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Mnaopenda kujifunza zaidi, naandika Kitabu. Get ready to have your copy. MWISHO.! (Malisa GJ ✍️)
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·2χλμ. Views
  • Rwanda inalichukulia jeshi la Burundi kama tishio jingine la usalama katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya demokrasi ya Congo (DRC).

    Nchi inayopakana na Rwanda na DRC imekuwa na maelfu ya wanajeshi huko kwa miaka mingi.

    Walikwenda kuwafuatilia waasi wa Burundi lakini sasa wanasaidia jeshi la Kinshasa katika vita dhidi ya M23.

    Uhusiano kati ya Rwanda na Burundi ni mbaya.

    Nchi hizi mbili zina muundo wa kikabila unaofanana lakini kinyume na Rwanda, Hutu ndiyo wanaoshikilia madaraka nchini Burundi.

    Nchi zote mbili zimekashifiana kwa kudai kujaribu kuangusha serikali zao.

    Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, ametoa onyo kali kwenye mitandao ya kijamii.

    "Ikizidi, Rwanda itaendelea na mashambulizi," aliandika, "Najua vita vitafika Burundi… Siku moja atataka kuingia Burundi - hatutakubaliana na hilo. Vita vitapanuka."

    Tishio hili litakuwa kubwa zaidi ikiwa M23 itaendelea na mashambulizi kutoka Goma kuelekea mkoa wa Kivu kusini karibu na mpaka wa Burundi, ambapo vikosi vyake viko.

    "Kile kinachotafutwa na Burundi hapa ni kuokoa utawala wake," alisema Bw. Stearns.

    "Burundi inahofia kuwa kama vikosi vya Rwanda vitaimarisha ushawishi wao katika eneo la Kivu kusini, inaweza kuteteresha serikali ya Bujumbura. Kile kilicho hatarini hapa ni kuzima uasi huu kabla haujaingilia karibu zaidi."

    Wengine wanahofia kurudi kwa vita mbili zilizoshambulia eneo hilo mwishoni mwa miaka ya 1990, ambazo zilihusisha nchi tisa na kusababisha vifo vya mamilioni ya watu.

    Mara hii, mapigano ya moja kwa moja kati ya majeshi mawili yanaweza kupelekea mgogoro wa DRC kuvuka nje ya mipaka yake.
    (BBC Swahili)

    Rwanda inalichukulia jeshi la Burundi kama tishio jingine la usalama katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya demokrasi ya Congo (DRC). Nchi inayopakana na Rwanda na DRC imekuwa na maelfu ya wanajeshi huko kwa miaka mingi. Walikwenda kuwafuatilia waasi wa Burundi lakini sasa wanasaidia jeshi la Kinshasa katika vita dhidi ya M23. Uhusiano kati ya Rwanda na Burundi ni mbaya. Nchi hizi mbili zina muundo wa kikabila unaofanana lakini kinyume na Rwanda, Hutu ndiyo wanaoshikilia madaraka nchini Burundi. Nchi zote mbili zimekashifiana kwa kudai kujaribu kuangusha serikali zao. Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, ametoa onyo kali kwenye mitandao ya kijamii. "Ikizidi, Rwanda itaendelea na mashambulizi," aliandika, "Najua vita vitafika Burundi… Siku moja atataka kuingia Burundi - hatutakubaliana na hilo. Vita vitapanuka." Tishio hili litakuwa kubwa zaidi ikiwa M23 itaendelea na mashambulizi kutoka Goma kuelekea mkoa wa Kivu kusini karibu na mpaka wa Burundi, ambapo vikosi vyake viko. "Kile kinachotafutwa na Burundi hapa ni kuokoa utawala wake," alisema Bw. Stearns. "Burundi inahofia kuwa kama vikosi vya Rwanda vitaimarisha ushawishi wao katika eneo la Kivu kusini, inaweza kuteteresha serikali ya Bujumbura. Kile kilicho hatarini hapa ni kuzima uasi huu kabla haujaingilia karibu zaidi." Wengine wanahofia kurudi kwa vita mbili zilizoshambulia eneo hilo mwishoni mwa miaka ya 1990, ambazo zilihusisha nchi tisa na kusababisha vifo vya mamilioni ya watu. Mara hii, mapigano ya moja kwa moja kati ya majeshi mawili yanaweza kupelekea mgogoro wa DRC kuvuka nje ya mipaka yake. (BBC Swahili)
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·700 Views
  • Maazimio (22) ya Marais wa Nchi Wanachama wa SADC na EAC kwenye mkutano uliofanyika leo hii Jijini Dar Es Salaam, Tanzania , Azimio la (12) limewataka Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Nchi zote Wanachama kukutana ndani ya siku tano (5) na kutoa mwelekeo wa kitalaam kuhusu mambo yafuatayo:

    - Kusitisha mara moja mapigano huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo .

    - Kutoa misaada ya Kibinadamu na kuwasaidia Wahanga wa vita.

    - Kutoa mpango kazi wa ulinzi ndani ya Mji wa Goma na maeneo Jirani.

    - Kuzifungua njia muhimu za mawasiliano kwenye Miji ya Goma - Kibumba- Rumangambo - Kalengera- Rutshuru na Goma - Kiwanja- Rwindi lakini pia matumizi ya Ziwa Kivu kwa ajili ya usafiri.

    - Kuufungua Uwanja wa Ndege wa Mji Goma mara moja.

    Maazimio (22) ya Marais wa Nchi Wanachama wa SADC na EAC kwenye mkutano uliofanyika leo hii Jijini Dar Es Salaam, Tanzania 🇹🇿, Azimio la (12) limewataka Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Nchi zote Wanachama kukutana ndani ya siku tano (5) na kutoa mwelekeo wa kitalaam kuhusu mambo yafuatayo: - Kusitisha mara moja mapigano huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo 🇨🇩. - Kutoa misaada ya Kibinadamu na kuwasaidia Wahanga wa vita. - Kutoa mpango kazi wa ulinzi ndani ya Mji wa Goma na maeneo Jirani. - Kuzifungua njia muhimu za mawasiliano kwenye Miji ya Goma - Kibumba- Rumangambo - Kalengera- Rutshuru na Goma - Kiwanja- Rwindi lakini pia matumizi ya Ziwa Kivu kwa ajili ya usafiri. - Kuufungua Uwanja wa Ndege wa Mji Goma mara moja.
    Like
    2
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·493 Views
  • #PART1

    Katika maisha, kuna mafanikio, kuna mapenzi, na kuna maumivu.

    Lakini maumivu gani yanaweza kuwa makali zaidi ya baba kugombana na damu yake mwenyewe?

    Hii ni stori ya 50 Cent, mwanamuziki, mfanyabiashara, na mtu aliye role model wa mamilioni ya wanaume duniani.

    Jamaa aliinuka kutoka mitaa ya ghetto, akapambana, akawa milionea. Lakini pamoja na pesa zote, hakununua upendo wa mtoto wake wa kwanza.

    Miaka ya nyuma, 50 Cent alikuwa baba mwenye furaha. Alikuwa anampenda mtoto wake kupita maelezo.

    Ilikuwa siyo tu kwa sababu ni damu yake, bali pia alitaka kuhakikisha kijana wake anakuwa na maisha bora zaidi.

    Aliamua kumuandalia mtoto wake maisha mazuri. Akampeleka kwenye shule nzuri ya mpira wa kikapu. Akalipia kila kitu, kutoka ada mpka mavazi.

    Mtoto akapewa kila alichohitaji, maisha ya kifahari yakawa sehemu yake ya kila siku.

    Lakini kitu kimoja hakikumpenda. Mpira wa kikapu haukumpenda.

    Dogo akaamua kuachana na basketball. Baba yake hakukasirika, akamwambia

    "Sawa mwanangu, kama siyo mpira, basi komaa na shule."

    #PART1 Katika maisha, kuna mafanikio, kuna mapenzi, na kuna maumivu. Lakini maumivu gani yanaweza kuwa makali zaidi ya baba kugombana na damu yake mwenyewe? Hii ni stori ya 50 Cent, mwanamuziki, mfanyabiashara, na mtu aliye role model wa mamilioni ya wanaume duniani. Jamaa aliinuka kutoka mitaa ya ghetto, akapambana, akawa milionea. Lakini pamoja na pesa zote, hakununua upendo wa mtoto wake wa kwanza. Miaka ya nyuma, 50 Cent alikuwa baba mwenye furaha. Alikuwa anampenda mtoto wake kupita maelezo. Ilikuwa siyo tu kwa sababu ni damu yake, bali pia alitaka kuhakikisha kijana wake anakuwa na maisha bora zaidi. Aliamua kumuandalia mtoto wake maisha mazuri. Akampeleka kwenye shule nzuri ya mpira wa kikapu. Akalipia kila kitu, kutoka ada mpka mavazi. Mtoto akapewa kila alichohitaji, maisha ya kifahari yakawa sehemu yake ya kila siku. Lakini kitu kimoja hakikumpenda. Mpira wa kikapu haukumpenda. Dogo akaamua kuachana na basketball. Baba yake hakukasirika, akamwambia "Sawa mwanangu, kama siyo mpira, basi komaa na shule."
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·1χλμ. Views
  • #PART 2

    Na kweli dogo akasoma kwa bidii. Ila kumbe kwa nyuma kulikuwa na mpango wa siri.

    Ilikuwa ni siku ya furaha kwa kila mzazi ambaye mtoto wake amemaliza chuo. Siku ya mahafali.

    50 Cent alikuwa na mipango mikubwa kwa kijana wake. Alikuwa tayari kumpa zawadi ya maisha, gari la kifahari ambalo lingemfungulia milango ya mafanikio zaidi.

    Lakini kilichotokea siku hiyo kilimvunja moyo.

    Hakupewa hata mwaliko wa mahafali.

    Fikiria baba ambaye amehangaika kuhakikisha mtoto wake anapata elimu bora, amemlipia kila kitu, amempa maisha ya ndoto, lakini siku kubwa kama hii hatakiwi hata kufika.

    Habari za mahafali alipewa na washikaji wa dogo. Walikuwa wanataka kumuona 50 Cent siku hiyo ili wapige naye picha.

    Lakini dogo mwenyewe? Hakumwambia chochote

    Hii haikuwa bahati mbaya, ilikuwa ni mpango wa makusudi.

    50 Cent hakuelewa nini kilichotokea, akapiga simu chuoni kuuliza.

    "Leo kuna mahafali, si ndiyo?"

    Wakamwambia ndiyo!

    Lilikuwa ni pigo lisilopimika kwa baba aliyetoa kila kitu kwa mwanawe.

    Lakini kilichomvunja moyo zaidi hakikuwa kutoalikwa tu kwenye mahafali.
    #PART 2 Na kweli dogo akasoma kwa bidii. Ila kumbe kwa nyuma kulikuwa na mpango wa siri. Ilikuwa ni siku ya furaha kwa kila mzazi ambaye mtoto wake amemaliza chuo. Siku ya mahafali. 50 Cent alikuwa na mipango mikubwa kwa kijana wake. Alikuwa tayari kumpa zawadi ya maisha, gari la kifahari ambalo lingemfungulia milango ya mafanikio zaidi. Lakini kilichotokea siku hiyo kilimvunja moyo. Hakupewa hata mwaliko wa mahafali. Fikiria baba ambaye amehangaika kuhakikisha mtoto wake anapata elimu bora, amemlipia kila kitu, amempa maisha ya ndoto, lakini siku kubwa kama hii hatakiwi hata kufika. Habari za mahafali alipewa na washikaji wa dogo. Walikuwa wanataka kumuona 50 Cent siku hiyo ili wapige naye picha. Lakini dogo mwenyewe? Hakumwambia chochote Hii haikuwa bahati mbaya, ilikuwa ni mpango wa makusudi. 50 Cent hakuelewa nini kilichotokea, akapiga simu chuoni kuuliza. "Leo kuna mahafali, si ndiyo?" Wakamwambia ndiyo! Lilikuwa ni pigo lisilopimika kwa baba aliyetoa kila kitu kwa mwanawe. Lakini kilichomvunja moyo zaidi hakikuwa kutoalikwa tu kwenye mahafali.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·794 Views
  • #PART3

    Dogo alianza kupiga picha na maadui wa baba yake.

    Unajua maana yake? Kijana wako, damu yako mwenyewe, anashirikiana na watu waliotaka kukuangusha.

    Hii haikuwa tu ishu ya "Hana time na baba yake," hii ilikuwa ni chuki ya makusudi.

    Na chuki hiyo haikutoka kwa mtoto mwenyewe, bali ilitengenezwa na mama yake.

    Mama ambaye baada ya kuachwa alitaka pesa nyingi kutoka kwa 50 Cent lakini ikashindikana.

    Mama ambaye hakuwa na njia ya kumkomoa baba, akaamua kutumia mtoto kama silaha.

    Na mtoto, bila kujua anatumika kama chess piece, akaingia kwenye mchezo wa mama.

    Huu ni ukweli mchungu. Katika ndoa au mahusiano yanayovunjika, asilimia kubwa ya wanawake hutumia watoto kama njia ya kulipiza kisasi.

    Ni wachache sana watakaoruhusu baba wa mtoto wao aendelee kuwa na uhusiano mzuri na mwanawe baada ya kutengana.
    #PART3 Dogo alianza kupiga picha na maadui wa baba yake. Unajua maana yake? Kijana wako, damu yako mwenyewe, anashirikiana na watu waliotaka kukuangusha. Hii haikuwa tu ishu ya "Hana time na baba yake," hii ilikuwa ni chuki ya makusudi. Na chuki hiyo haikutoka kwa mtoto mwenyewe, bali ilitengenezwa na mama yake. Mama ambaye baada ya kuachwa alitaka pesa nyingi kutoka kwa 50 Cent lakini ikashindikana. Mama ambaye hakuwa na njia ya kumkomoa baba, akaamua kutumia mtoto kama silaha. Na mtoto, bila kujua anatumika kama chess piece, akaingia kwenye mchezo wa mama. Huu ni ukweli mchungu. Katika ndoa au mahusiano yanayovunjika, asilimia kubwa ya wanawake hutumia watoto kama njia ya kulipiza kisasi. Ni wachache sana watakaoruhusu baba wa mtoto wao aendelee kuwa na uhusiano mzuri na mwanawe baada ya kutengana.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·841 Views
  • #PART4

    Lakini cha kushangaza, wanaume wengi hawafanyi hivi.

    Kwa nini?

    Kwa sababu mwanaume hapendi kuonekana amefeli.

    Dogo akimuuliza baba yake, "Kwanini ulimuacha mama?" baba atapata kigugumizi.

    Hakuna mwanaume anayependa aonekane alishindwa kufanya kitu sahihi.

    Ndiyo maana wanaume wengi husema mambo mazuri kuhusu mama wa mtoto wao, hata kama waliachana kwa mabaya.

    Lakini wanawake wengi hawawezi kufanya hivyo. Wengi hujaza chuki kwa mtoto. Wanaangalia maisha yao kwa sasa, wanasahau mtoto atakua na atagundua ukweli wenyewe.

    50 Cent ni role model wa wanaume wengi kwa sababu moja kubwa, anajua dunia ilivyo.

    Ndiyo maana hata Chris Brown, kabla ya kuingia kwenye ndoa, alikwenda kwa 50 Cent kumuuliza ushauri.

    50 Cent alimwambia USITHUBUTU!
    #PART4 Lakini cha kushangaza, wanaume wengi hawafanyi hivi. Kwa nini? Kwa sababu mwanaume hapendi kuonekana amefeli. Dogo akimuuliza baba yake, "Kwanini ulimuacha mama?" baba atapata kigugumizi. Hakuna mwanaume anayependa aonekane alishindwa kufanya kitu sahihi. Ndiyo maana wanaume wengi husema mambo mazuri kuhusu mama wa mtoto wao, hata kama waliachana kwa mabaya. Lakini wanawake wengi hawawezi kufanya hivyo. Wengi hujaza chuki kwa mtoto. Wanaangalia maisha yao kwa sasa, wanasahau mtoto atakua na atagundua ukweli wenyewe. 50 Cent ni role model wa wanaume wengi kwa sababu moja kubwa, anajua dunia ilivyo. Ndiyo maana hata Chris Brown, kabla ya kuingia kwenye ndoa, alikwenda kwa 50 Cent kumuuliza ushauri. 50 Cent alimwambia USITHUBUTU!
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·803 Views
  • #PART5

    Alimwambia, "Siku hizi wanawake hawana mapenzi ya kweli, Wanachoangalia ni pesa. Wanakuja kuchukua na kuondoka."

    Chris Brown aliposikia hivyo, mpaka leo hajataka ndoa.

    Ukitaka kuzaa na mtu, hakikisha unamjua kwa undani.

    Maana unaweza ukadhani unazaa mtoto, kumbe unazaa silaha ya kukushambulia baadaye.

    Na mwisho wa siku, mtoto akikua, atapambanua mwenyewe nani alikuwa na nia njema naye na nani alitumia chuki kama mtaji.

    50 Cent alijua mwanaye atakua na kuona ukweli mwenyewe.

    Na kweli, siku hizi mtoto ameanza kurudi kwa baba yake, maana ameanza kugundua kuwa mama yake alimtumia.

    Siku zote, ukweli hauwezi kufichika milele.
    #PART5 Alimwambia, "Siku hizi wanawake hawana mapenzi ya kweli, Wanachoangalia ni pesa. Wanakuja kuchukua na kuondoka." Chris Brown aliposikia hivyo, mpaka leo hajataka ndoa. Ukitaka kuzaa na mtu, hakikisha unamjua kwa undani. Maana unaweza ukadhani unazaa mtoto, kumbe unazaa silaha ya kukushambulia baadaye. Na mwisho wa siku, mtoto akikua, atapambanua mwenyewe nani alikuwa na nia njema naye na nani alitumia chuki kama mtaji. 50 Cent alijua mwanaye atakua na kuona ukweli mwenyewe. Na kweli, siku hizi mtoto ameanza kurudi kwa baba yake, maana ameanza kugundua kuwa mama yake alimtumia. Siku zote, ukweli hauwezi kufichika milele.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·655 Views