• Margaret Nduta Macharia (37) ambaye ni Raia wa Kenya aliyekamatwa mwaka 2023 Nchini Vietnam na kilogramu mbili (2) za dawa za kulevya aina ya Cocaine, anatarajiwa kunyongwa hadi kufa kesho Jumatatu Machi 17, 2025.

    Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Nation, Margaret aliyepewa hukumu hiyo Machi 6, 2025 alisema alipewa mzigo huo wa dawa za kulevya na Mwanaume mmoja kutoka Nchini Kenya aliyemtaja kwa jina moja la John. Pia, taarifa hiyo inaeleza kuwa alifanikiwa kupita katika Viwanja vitatu (3) vya Ndege bila kukamatwa, kabla ya kugundulika Nchini Vietnam. Viwanja hivyo ni pamoja na Jomo Kenyatta (Kenya), Bole (Ethiopia) na Hamad (Qatar).

    Hata hivyo, Margaret akijitetea Mahakamani Nchini Vietnam alidai hakufahamu kama mzigo ule ulikuwa ni dawa za kulevya. Taarifa kutoka Nchini Vietnam, Margaret atakula chakula chake cha mwisho kesho saa 1:30 usiku na kisha kunyongwa saa 2:30 za usiku.

    Margaret Nduta Macharia (37) ambaye ni Raia wa Kenya 🇰🇪 aliyekamatwa mwaka 2023 Nchini Vietnam 🇻🇳 na kilogramu mbili (2) za dawa za kulevya aina ya Cocaine, anatarajiwa kunyongwa hadi kufa kesho Jumatatu Machi 17, 2025. Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Nation, Margaret aliyepewa hukumu hiyo Machi 6, 2025 alisema alipewa mzigo huo wa dawa za kulevya na Mwanaume mmoja kutoka Nchini Kenya aliyemtaja kwa jina moja la John. Pia, taarifa hiyo inaeleza kuwa alifanikiwa kupita katika Viwanja vitatu (3) vya Ndege bila kukamatwa, kabla ya kugundulika Nchini Vietnam. Viwanja hivyo ni pamoja na Jomo Kenyatta (Kenya), Bole (Ethiopia) na Hamad (Qatar). Hata hivyo, Margaret akijitetea Mahakamani Nchini Vietnam alidai hakufahamu kama mzigo ule ulikuwa ni dawa za kulevya. Taarifa kutoka Nchini Vietnam, Margaret atakula chakula chake cha mwisho kesho saa 1:30 usiku na kisha kunyongwa saa 2:30 za usiku.
    0 Commentaires ·0 Parts ·53 Vue