• OFFICIAL Kocha Wa Real Madrid Xabi Alonso amesema Dean Huijsen, Trent Alexander-Arnold, Dani Carvajal na Dani Ceballos wote wako tayari kwa mchezo wa El Clasco.

    Alonso amesema wachezaji pekee wataukosa mchezo wa El Clasco ni Antonio Rudiger na David Alaba wengine wapo.
    🚨 OFFICIAL Kocha Wa Real Madrid Xabi Alonso amesema Dean Huijsen, Trent Alexander-Arnold, Dani Carvajal na Dani Ceballos wote wako tayari kwa mchezo wa El Clasco. Alonso amesema wachezaji pekee wataukosa mchezo wa El Clasco ni Antonio Rudiger na David Alaba wengine wapo.
    0 Comments ·0 Shares ·191 Views
  • Klabu ya Al Ahli SC wapo tayari kutoa kiasi cha euro milioni 15 ili kuipata saini ya mshambuliaji wa Pyramids, Fiston Mayele Kalala "Cyborg" .

    Klabu iyo kutokea nchini Saudia Arabia wapo tayari kumpa Mayele mshahara wa euro milioni 3 kwa mwaka !
    🚨 Klabu ya Al Ahli SC 🇸🇦 wapo tayari kutoa kiasi cha euro milioni 15 ili kuipata saini ya mshambuliaji wa Pyramids, Fiston Mayele Kalala "Cyborg" 🇨🇩. Klabu iyo kutokea nchini Saudia Arabia wapo tayari kumpa Mayele mshahara wa euro milioni 3 kwa mwaka ! 💵
    0 Comments ·0 Shares ·184 Views
  • 𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆: Ter Stegen huwenda akaondoka Barcelona January kwa mkopo , reports Sky Sports. 👋🏽
    🚨🚨 𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆: Ter Stegen huwenda akaondoka Barcelona January kwa mkopo , reports Sky Sports. 👋🏽💣
    0 Comments ·0 Shares ·175 Views
  • Nyota wa Real Madrid, Endrick ameomba kuondoka Real Madrid January kwa mkopo ili kulinda kiwango chake.

    Chini ya Xabi Alonso nyota huyo amekosa nafasi kabisa ya kucheza, mara ya mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa May 18 dhidi ya Sevilla.

    Source [ El Chiringuito TV ]
    Nyota wa Real Madrid, Endrick ameomba kuondoka Real Madrid January kwa mkopo ili kulinda kiwango chake. Chini ya Xabi Alonso nyota huyo amekosa nafasi kabisa ya kucheza, mara ya mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa May 18 dhidi ya Sevilla. Source [ El Chiringuito TV ]
    0 Comments ·0 Shares ·100 Views
  • OFFICIAL Beki Trent Alexander-Arnold na Dani Carvajal wote wamefanya mazoezi leo na Kikosi cha kwanza cha Real Madrid kwa ajili ya mchezo wa Kesho dhidi ya Juventus na El Clascoo..
    🚨OFFICIAL Beki Trent Alexander-Arnold na Dani Carvajal wote wamefanya mazoezi leo na Kikosi cha kwanza cha Real Madrid kwa ajili ya mchezo wa Kesho dhidi ya Juventus na El Clascoo..
    0 Comments ·0 Shares ·122 Views
  • "Nani alaumiwe? Anaweza kuwa Injinia Hersi Said mwenyewe. Yanga ilifika fainali za Shirikisho miaka ya karibuni. Yanga ilitolewa robo fainali. Yanga ilitolewa pia makundi. Hersi anajua ndoto za Wanayanga. Huwa wananyanyasika kwa mashabiki wa mtani zao kwa kutofanya vizuri katika michuano ya CAF. Ligi ya Mabingwa.
    .
    Wakati huu wakiwa wamesajili wachezaji wazuri huku akiendelea kumiliki wachezaji mafundi kama kina Pacome Zouzoua, Hersi akaitafutia Yanga kocha mwanafunzi.

    Ukitazama wasifu wa Folz, alikuwa amepita katika klabu kadhaa akiwa kama kocha msaidizi. Hersi na wenzake walikuwa wamecheza kamari kwa kumleta Folz. Hajawahi kuwa kocha mkuu wala kutwaa taji lolote muhimu katika maisha yake ya mpira.

    Unawezaje kutimiza ndoto zako ukiwa na kocha wa namna hii. Katika lugha ya mtaani ya Waingereza tunaweza kusema Hersi na wenzake walikuwa wamecheza kamari. ‘Gambling’. Haukuwa muda wa Yanga kucheza bahati nasibu.

    Ulikuwa muda wa wao kuwa na kocha ambaye ana uzoefu na anaweza kuishi katika falsafa zao. Matokeo yake Yanga wamejiweka katika hatari. Wameshafungwa ugenini na wageni wao wanaweza kuja na mbinu za ajabu. Injinia Hersi na wenzake ambao wanaongoza Yanga sasa hivi hawakufikiria kama wanaweza kuwa katika nafasi hii kwa sasa. Wakati wao wanaiwaza nusu fainali au fainali, tayari wapo hatarini kutofika hata makundi.

    - Edo Kumwembe, Mchambuzi.
    "Nani alaumiwe? Anaweza kuwa Injinia Hersi Said mwenyewe. Yanga ilifika fainali za Shirikisho miaka ya karibuni. Yanga ilitolewa robo fainali. Yanga ilitolewa pia makundi. Hersi anajua ndoto za Wanayanga. Huwa wananyanyasika kwa mashabiki wa mtani zao kwa kutofanya vizuri katika michuano ya CAF. Ligi ya Mabingwa. . Wakati huu wakiwa wamesajili wachezaji wazuri huku akiendelea kumiliki wachezaji mafundi kama kina Pacome Zouzoua, Hersi akaitafutia Yanga kocha mwanafunzi. 😀 Ukitazama wasifu wa Folz, alikuwa amepita katika klabu kadhaa akiwa kama kocha msaidizi. Hersi na wenzake walikuwa wamecheza kamari kwa kumleta Folz. Hajawahi kuwa kocha mkuu wala kutwaa taji lolote muhimu katika maisha yake ya mpira. Unawezaje kutimiza ndoto zako ukiwa na kocha wa namna hii. Katika lugha ya mtaani ya Waingereza tunaweza kusema Hersi na wenzake walikuwa wamecheza kamari. ‘Gambling’. Haukuwa muda wa Yanga kucheza bahati nasibu. Ulikuwa muda wa wao kuwa na kocha ambaye ana uzoefu na anaweza kuishi katika falsafa zao. Matokeo yake Yanga wamejiweka katika hatari. Wameshafungwa ugenini na wageni wao wanaweza kuja na mbinu za ajabu. Injinia Hersi na wenzake ambao wanaongoza Yanga sasa hivi hawakufikiria kama wanaweza kuwa katika nafasi hii kwa sasa. Wakati wao wanaiwaza nusu fainali au fainali, tayari wapo hatarini kutofika hata makundi. - Edo Kumwembe, Mchambuzi.
    0 Comments ·0 Shares ·193 Views
  • BREAKING:

    Wachezaji wa Atlético Madrid waliondoka kwenye uwanja wa Emirates bila kuoga kutokana na kukosekana kwa maji ya moto.

    Wachezaji walikuwa wametokwa jasho na wakakimbilia hotelini kuoga kwa sababu hakukuwa na maji ya moto baada ya kumaliza mazoezi rasmi.

    Msafara wa Atlético umekasirishwa sana na tayari umepeleka malalamiko UEFA kuhusu ukosefu wa huduma muhimu katika uwanja wa Emirates.

    Source [ Carusselderpotivo]

    BREAKING: Wachezaji wa Atlético Madrid waliondoka kwenye uwanja wa Emirates bila kuoga kutokana na kukosekana kwa maji ya moto. Wachezaji walikuwa wametokwa jasho na wakakimbilia hotelini kuoga kwa sababu hakukuwa na maji ya moto baada ya kumaliza mazoezi rasmi. Msafara wa Atlético umekasirishwa sana na tayari umepeleka malalamiko UEFA kuhusu ukosefu wa huduma muhimu katika uwanja wa Emirates. Source [ Carusselderpotivo]
    0 Comments ·0 Shares ·128 Views
  • Fc Barcelona wana nia ya dhati ya kumsajili nyota wa Marseille, Mason Greenwood na wameanza kufuatilia maendeleo yake tokea alipokuwa Getafe kwa mkopo .

    Taarifa zilizopo maskauti wa Fc Barcelona walikuwepo kwenye mchezo wa Marseille dhidi ya Le Havre uliopigwa weekend hii wakifuatilia kwa ukaribu maendeleo ya Mason Greenwood.

    Kwenye mchezo huo Greenwood aliisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa goli 6-2 huku akifunga magoli 4.

    #SportsElite
    Fc Barcelona wana nia ya dhati ya kumsajili nyota wa Marseille, Mason Greenwood na wameanza kufuatilia maendeleo yake tokea alipokuwa Getafe kwa mkopo . Taarifa zilizopo maskauti wa Fc Barcelona walikuwepo kwenye mchezo wa Marseille dhidi ya Le Havre uliopigwa weekend hii wakifuatilia kwa ukaribu maendeleo ya Mason Greenwood. Kwenye mchezo huo Greenwood aliisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa goli 6-2 huku akifunga magoli 4. #SportsElite
    0 Comments ·0 Shares ·168 Views
  • Nottingham Forest imefikia makubaliano kamili na Kocha Sean Dyche kuwa kocha wao mpya kwa mkataba hadi 2027. ✅️

    Source Fabrizio Romano
    🚨 Nottingham Forest imefikia makubaliano kamili na Kocha Sean Dyche kuwa kocha wao mpya kwa mkataba hadi 2027. ✅️ Source Fabrizio Romano
    0 Comments ·0 Shares ·56 Views
  • Iran yakataa mazungumzo na Trump, yakanusha madai ya uharibifu wa nyuklia.

    Katika kile kinachoonekana kuwa kuendelea kwa mvutano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Iran, Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameibuka hadharani na kukataa pendekezo la Rais wa Marekani, Donald Trump, la kurejea kwenye meza ya mazungumzo.

    Akizungumza kupitia vyombo vya habari vya Serikali, Khamenei alisema wazi kuwa pendekezo la Trump halikuwa la kweli, bali ni jaribio la kulazimisha makubaliano kwa njia ya vitisho.

    "Trump anasema yeye ni Mtaalamu wa kufanikisha makubaliano, lakini kama makubaliano hayo yanaambatana na shinikizo na matokeo yake tayari yameamuliwa, basi hiyo siyo makubaliano bali ni kulazimisha na vitisho," - Ayatollah Ali Khamenei.

    Kauli hiyo ya Khamenei imekuja kufuatia hotuba ya Trump wiki iliyopita, ambapo aliwaambia Wabunge wa Israel kwamba Marekani ingependa kufanikisha makubaliano ya amani na Tehran, hasa baada ya kutangazwa kwa usitishaji mapigano kati ya Israel na Hamas huko Gaza. Katika hotuba hiyo, Trump pia alidai kuwa:

    "Marekani imeharibu kabisa maeneo ya nyuklia ya Iran."

    Lakini Khamenei alikanusha vikali kauli hiyo, akisema:

    "Rais wa Marekani anajivunia kusema kuwa wamebomoa na kuharibu sekta ya nyuklia ya Iran. Vizuri, endeleeni kuota!"

    Kauli hizi zinaashiria kuwa uhusiano kati ya Tehran na Washington bado uko katika hali ya sintofahamu, huku Iran ikionekana kuchukua msimamo mkali dhidi ya kile inachokiona kama mbinu za mabeberu.

    Kwa sasa, haijafahamika kama juhudi za kidiplomasia zitaendelea, hasa ikizingatiwa kuwa Iran bado inashikilia haki yake ya kuendesha mpango wake wa nyuklia kama nchi huru.

    Je, unadhani mvutano huu unaweza kuzua mgogoro mpya wa kimataifa?

    Toa maoni yako
    Iran yakataa mazungumzo na Trump, yakanusha madai ya uharibifu wa nyuklia. Katika kile kinachoonekana kuwa kuendelea kwa mvutano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Iran, Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameibuka hadharani na kukataa pendekezo la Rais wa Marekani, Donald Trump, la kurejea kwenye meza ya mazungumzo. Akizungumza kupitia vyombo vya habari vya Serikali, Khamenei alisema wazi kuwa pendekezo la Trump halikuwa la kweli, bali ni jaribio la kulazimisha makubaliano kwa njia ya vitisho. "Trump anasema yeye ni Mtaalamu wa kufanikisha makubaliano, lakini kama makubaliano hayo yanaambatana na shinikizo na matokeo yake tayari yameamuliwa, basi hiyo siyo makubaliano bali ni kulazimisha na vitisho," - Ayatollah Ali Khamenei. Kauli hiyo ya Khamenei imekuja kufuatia hotuba ya Trump wiki iliyopita, ambapo aliwaambia Wabunge wa Israel kwamba Marekani ingependa kufanikisha makubaliano ya amani na Tehran, hasa baada ya kutangazwa kwa usitishaji mapigano kati ya Israel na Hamas huko Gaza. Katika hotuba hiyo, Trump pia alidai kuwa: "Marekani imeharibu kabisa maeneo ya nyuklia ya Iran." Lakini Khamenei alikanusha vikali kauli hiyo, akisema: "Rais wa Marekani anajivunia kusema kuwa wamebomoa na kuharibu sekta ya nyuklia ya Iran. Vizuri, endeleeni kuota!" Kauli hizi zinaashiria kuwa uhusiano kati ya Tehran na Washington bado uko katika hali ya sintofahamu, huku Iran ikionekana kuchukua msimamo mkali dhidi ya kile inachokiona kama mbinu za mabeberu. Kwa sasa, haijafahamika kama juhudi za kidiplomasia zitaendelea, hasa ikizingatiwa kuwa Iran bado inashikilia haki yake ya kuendesha mpango wake wa nyuklia kama nchi huru. Je, unadhani mvutano huu unaweza kuzua mgogoro mpya wa kimataifa? Toa maoni yako
    0 Comments ·0 Shares ·131 Views
  • GOLI LA KWANZA LA SIMBA SC

    ⚽️ Wilson Nangu

    Nsingizini 0-1 Simba SC
    GOLI LA KWANZA LA SIMBA SC ⚽️ Wilson Nangu 🇸🇿 Nsingizini 0-1 Simba SC 🇹🇿
    0 Comments ·0 Shares ·174 Views
  • Burkina Faso yatangaza utaratibu mpya wa kusimamia fedha za mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs).

    Serikali ya Burkina Faso imechukua hatua mpya ya kuhakikisha uwazi na usimamizi madhubuti wa fedha zinazotumiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) Nchini humo. Kuanzia sasa, mashirika yote yatahitajika kufungua akaunti katika Benki ya Kitaifa ya Amana ya Hazina (National Bank of Deposits of the Treasury).

    Uamuzi huo unalenga kufuatilia kwa karibu michakato ya kifedha ya mashirika hayo, na kuhakikisha kuwa fedha zinazotoka kwa wahisani zinatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa kwa uwazi na uwajibikaji wa hali ya juu.

    Hatua hii imezua mijadala kwenye majukwaa ya kijamii na ndani ya mashirika husika, ambapo baadhi wanaitazama kama njia ya kuimarisha nidhamu ya kifedha, huku wengine wakihofia kuingiliwa kwa uhuru wa mashirika ya kiraia.

    Serikali bado haijatoa taarifa ya kina kuhusu jinsi utekelezaji wa agizo hili utakavyofanyika, wala ikiwa kutakuwepo na muda maalum wa mpito kwa mashirika hayo kuhamia mfumo huo mpya wa kifedha.

    Toa maoni yako
    Burkina Faso yatangaza utaratibu mpya wa kusimamia fedha za mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs). Serikali ya Burkina Faso imechukua hatua mpya ya kuhakikisha uwazi na usimamizi madhubuti wa fedha zinazotumiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) Nchini humo. Kuanzia sasa, mashirika yote yatahitajika kufungua akaunti katika Benki ya Kitaifa ya Amana ya Hazina (National Bank of Deposits of the Treasury). Uamuzi huo unalenga kufuatilia kwa karibu michakato ya kifedha ya mashirika hayo, na kuhakikisha kuwa fedha zinazotoka kwa wahisani zinatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa kwa uwazi na uwajibikaji wa hali ya juu. Hatua hii imezua mijadala kwenye majukwaa ya kijamii na ndani ya mashirika husika, ambapo baadhi wanaitazama kama njia ya kuimarisha nidhamu ya kifedha, huku wengine wakihofia kuingiliwa kwa uhuru wa mashirika ya kiraia. Serikali bado haijatoa taarifa ya kina kuhusu jinsi utekelezaji wa agizo hili utakavyofanyika, wala ikiwa kutakuwepo na muda maalum wa mpito kwa mashirika hayo kuhamia mfumo huo mpya wa kifedha. Toa maoni yako
    0 Comments ·0 Shares ·258 Views
  • AYRA STARR AANDIKA HISTORIA KWENYE YOUTUBE KUPITIA WIMBO WAKE “RUSH”.

    Nyota wa muziki kutoka Nigeria, Ayra Starr, ameweka rekodi ya kipekee na kuandika jina lake kwenye vitabu vya historia ya burudani barani Afrika. Kupitia wimbo wake maarufu Rush, Ayra Starr amekuwa Msanii wa kwanza wa kike barani Afrika kufikisha zaidi ya Watazamaji milioni 500 kwenye mtandao wa YouTube kwa wimbo mmoja wa solo.

    Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Ayra alishiriki furaha yake kwa mafanikio hayo na kusema:

    “Sauti ya Gen-Z kutoka Afrika inasikika! Rush imefanya historia, na hii ni mwanzo tu.”

    Kwa mafanikio haya, Rush imejiunga na orodha ya video tano bora za muziki za Kiafrika zilizotazamwa zaidi kila wakati kwenye YouTube.

    - Calm Down : Rema
    - Jerusalema : Master KG ft. Nomcebo Zikode
    - Love Nwantiti : CKay
    - Magic In The Air : Magic System

    Kinachovutia zaidi ni kwamba, licha ya umaarufu wa Wasanii kama Burna Boy, Wizkid, Davido, pamoja na wakali wa kimataifa kama NBA YoungBoy, Polo G, Lil Tjay, NLE Choppa, na Lil Durk, hakuna hata mmoja wao ambaye amewahi kufikisha Watazamaji zaidi ya milioni 500 kwa wimbo mmoja wa solo kwenye jukwaa la YouTube tofauti na Ayra Starr.

    Rekodi hii inaendelea kuimarisha nafasi ya Ayra Starr kama sauti muhimu ya kizazi kipya cha muziki barani Afrika, hasa kwa kizazi cha Gen-Z, na kuonyesha ukuaji wa ushawishi wa Wanawake kwenye tasnia ya muziki wa kimataifa.

    “Rush is not just a song, it’s a movement.” - Ayra Starr

    Pongezi kwa Ayra kwa kuwakilisha Afrika kwa kishindo duniani!
    AYRA STARR AANDIKA HISTORIA KWENYE YOUTUBE KUPITIA WIMBO WAKE “RUSH”. Nyota wa muziki kutoka Nigeria, Ayra Starr, ameweka rekodi ya kipekee na kuandika jina lake kwenye vitabu vya historia ya burudani barani Afrika. Kupitia wimbo wake maarufu Rush, Ayra Starr amekuwa Msanii wa kwanza wa kike barani Afrika kufikisha zaidi ya Watazamaji milioni 500 kwenye mtandao wa YouTube kwa wimbo mmoja wa solo. Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Ayra alishiriki furaha yake kwa mafanikio hayo na kusema: “Sauti ya Gen-Z kutoka Afrika inasikika! Rush imefanya historia, na hii ni mwanzo tu.” Kwa mafanikio haya, Rush imejiunga na orodha ya video tano bora za muziki za Kiafrika zilizotazamwa zaidi kila wakati kwenye YouTube. - Calm Down : Rema - Jerusalema : Master KG ft. Nomcebo Zikode - Love Nwantiti : CKay - Magic In The Air : Magic System Kinachovutia zaidi ni kwamba, licha ya umaarufu wa Wasanii kama Burna Boy, Wizkid, Davido, pamoja na wakali wa kimataifa kama NBA YoungBoy, Polo G, Lil Tjay, NLE Choppa, na Lil Durk, hakuna hata mmoja wao ambaye amewahi kufikisha Watazamaji zaidi ya milioni 500 kwa wimbo mmoja wa solo kwenye jukwaa la YouTube tofauti na Ayra Starr. Rekodi hii inaendelea kuimarisha nafasi ya Ayra Starr kama sauti muhimu ya kizazi kipya cha muziki barani Afrika, hasa kwa kizazi cha Gen-Z, na kuonyesha ukuaji wa ushawishi wa Wanawake kwenye tasnia ya muziki wa kimataifa. “Rush is not just a song, it’s a movement.” - Ayra Starr Pongezi kwa Ayra kwa kuwakilisha Afrika kwa kishindo duniani!
    0 Comments ·0 Shares ·323 Views
  • Arnold Schwarzenegger awasilisha mpango wa kuokoa demokrasia Marekani.

    Mwigizaji Nguli wa Hollywood na Gavana wa zamani wa Jimbo la California, Arnold Schwarzenegger, ameibuka na pendekezo la kina la kuimarisha demokrasia Nchini Marekani. Katika mahojiano yake kwenye kipindi maarufu cha Real Time with Bill Maher, Schwarzenegger alifichua mpango wa hatua tatu ambao anauona kama njia ya “kupatanisha pande zote mbili” yaani Republican na Democratic. Katika maelezo yake rasmi, Schwarzenegger alisema:

    “Tunapaswa kutangaza Siku ya Uchaguzi kuwa likizo ya kitaifa, kuhakikisha kuwa ramani za kisiasa zinatengenezwa na tume huru zisizoegemea upande wowote, na kuimarisha mifumo ya utambulisho wa wapiga kura.”

    Mpango huu, ambao una lengo la kuhamasisha ushiriki mpana wa Wananchi na kulinda uadilifu wa chaguzi, umeungwa mkono na hoja za kisera zinazoegemea misingi ya haki, usawa na uwazi.

    Schwarzenegger pia hakusita kuelezea wasiwasi wake kuhusu Pendekezo la 50 la California, akiliona kama:

    “Hila kubwa ambayo inaweza kurudisha ramani za uchaguzi mikononi mwa Wanasiasa badala ya Wataalamu huru.”

    Kwa mujibu wake, hatua hiyo ya kuruhusu Wanasiasa kushiriki katika uundwaji wa ramani ya majimbo inaweza kuathiri vibaya uwakilishi wa haki kwa Wananchi.

    Mpango huu wa Schwarzenegger una mvuto wa kipekee kwa kuwa unachanganya ushawishi wa jina kubwa na hoja nzito za kisera. Hata hivyo, utekelezaji wake unategemea mabadiliko ya kisheria, mjadala wa kina wa kitaifa, na maridhiano kati ya vyama viwili vikuu vya siasa.

    Kwa mujibu wa Wachambuzi wa siasa za Marekani, hoja za Schwarzenegger zinaibua maswali mapana kuhusu:

    - Usawa katika chaguzi,
    - Usalama wa mfumo wa upigaji kura,
    - Na mwelekeo wa demokrasia ya Marekani kwa vizazi vijavyo.

    Mpaka sasa, bado haijajulikana iwapo pendekezo hili litaungwa mkono na Wabunge, lakini bila shaka, Schwarzenegger amejipambanua tena, safari hii siyo kwenye sinema au siasa za majimbo tu, bali kwenye uwanja mpana wa mustakabali wa kidemokrasia wa taifa lake.
    Arnold Schwarzenegger awasilisha mpango wa kuokoa demokrasia Marekani. Mwigizaji Nguli wa Hollywood na Gavana wa zamani wa Jimbo la California, Arnold Schwarzenegger, ameibuka na pendekezo la kina la kuimarisha demokrasia Nchini Marekani. Katika mahojiano yake kwenye kipindi maarufu cha Real Time with Bill Maher, Schwarzenegger alifichua mpango wa hatua tatu ambao anauona kama njia ya “kupatanisha pande zote mbili” yaani Republican na Democratic. Katika maelezo yake rasmi, Schwarzenegger alisema: “Tunapaswa kutangaza Siku ya Uchaguzi kuwa likizo ya kitaifa, kuhakikisha kuwa ramani za kisiasa zinatengenezwa na tume huru zisizoegemea upande wowote, na kuimarisha mifumo ya utambulisho wa wapiga kura.” Mpango huu, ambao una lengo la kuhamasisha ushiriki mpana wa Wananchi na kulinda uadilifu wa chaguzi, umeungwa mkono na hoja za kisera zinazoegemea misingi ya haki, usawa na uwazi. Schwarzenegger pia hakusita kuelezea wasiwasi wake kuhusu Pendekezo la 50 la California, akiliona kama: “Hila kubwa ambayo inaweza kurudisha ramani za uchaguzi mikononi mwa Wanasiasa badala ya Wataalamu huru.” Kwa mujibu wake, hatua hiyo ya kuruhusu Wanasiasa kushiriki katika uundwaji wa ramani ya majimbo inaweza kuathiri vibaya uwakilishi wa haki kwa Wananchi. Mpango huu wa Schwarzenegger una mvuto wa kipekee kwa kuwa unachanganya ushawishi wa jina kubwa na hoja nzito za kisera. Hata hivyo, utekelezaji wake unategemea mabadiliko ya kisheria, mjadala wa kina wa kitaifa, na maridhiano kati ya vyama viwili vikuu vya siasa. Kwa mujibu wa Wachambuzi wa siasa za Marekani, hoja za Schwarzenegger zinaibua maswali mapana kuhusu: - Usawa katika chaguzi, - Usalama wa mfumo wa upigaji kura, - Na mwelekeo wa demokrasia ya Marekani kwa vizazi vijavyo. Mpaka sasa, bado haijajulikana iwapo pendekezo hili litaungwa mkono na Wabunge, lakini bila shaka, Schwarzenegger amejipambanua tena, safari hii siyo kwenye sinema au siasa za majimbo tu, bali kwenye uwanja mpana wa mustakabali wa kidemokrasia wa taifa lake.
    0 Comments ·0 Shares ·259 Views
  • Vurugu mitandaoni! Ned Nwoko amvaa Regina Daniels, asema "ameharibu familia yetu".

    Mitandao ya kijamii imewaka moto kufuatia tuhuma nzito zilizotolewa na Bilionea na mwanasiasa mashuhuri kutoka Nigeria, Prince Ned Nwoko, dhidi ya Mke wake, Mwigizaji maarufu wa filamu za Nigeria (Nollywood) Regina Daniels. Kupitia chapisho la video kwenye ukurasa wake wa Instagram, Nwoko amemshutumu Regina kwa kile alichokiita "vurugu za kupindukia" pamoja na matumizi mabaya ya dawa za kulevya na pombe.

    Katika maneno yake, Ned aliandika: “Hakuwa hivi mwanzo… kile kinachotokea sasa kimeharibu kabisa utulivu wa familia yetu.”

    Nwoko alieleza kuwa ndani ya saa 48, Regina alifanya fujo kubwa nyumbani kwao akiwapiga Wafanyakazi watatu wa ndani, kuharibu mali, na kusababisha uharibifu mkubwa bila sababu ya msingi.

    Kwa mujibu wa chapisho hilo la Instagram: “Nimetoa masharti ya wazi kwake. Lazima akubali kwenda kwenye tiba ya kuacha dawa, iwe ndani au nje ya Nchi. Vinginevyo, naogopa kwa usalama wake.” - Prince Ned Nwoko.

    Katika tuhuma hizo, Ned alimtaja mtu aitwaye Sammy kama Muuzaji mkuu wa dawa kwa Regina, huku pia akilitaja jina la Ann, akisema anahusika katika kile alichokiita “mzunguko wa maovu.”

    Tukio hili limetikisa jamii ya mtandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakionesha mshangao, wengine wakimtetea Regina, na wengi wakitaka ukweli wa kina juu ya maisha ya kifahari ya wawili hao.

    Je, hii ni drama ya ndoa ya Mastaa au kuna jambo kubwa zaidi nyuma ya pazia?
    Vurugu mitandaoni! Ned Nwoko amvaa Regina Daniels, asema "ameharibu familia yetu". Mitandao ya kijamii imewaka moto kufuatia tuhuma nzito zilizotolewa na Bilionea na mwanasiasa mashuhuri kutoka Nigeria, Prince Ned Nwoko, dhidi ya Mke wake, Mwigizaji maarufu wa filamu za Nigeria (Nollywood) Regina Daniels. Kupitia chapisho la video kwenye ukurasa wake wa Instagram, Nwoko amemshutumu Regina kwa kile alichokiita "vurugu za kupindukia" pamoja na matumizi mabaya ya dawa za kulevya na pombe. Katika maneno yake, Ned aliandika: “Hakuwa hivi mwanzo… kile kinachotokea sasa kimeharibu kabisa utulivu wa familia yetu.” Nwoko alieleza kuwa ndani ya saa 48, Regina alifanya fujo kubwa nyumbani kwao akiwapiga Wafanyakazi watatu wa ndani, kuharibu mali, na kusababisha uharibifu mkubwa bila sababu ya msingi. Kwa mujibu wa chapisho hilo la Instagram: “Nimetoa masharti ya wazi kwake. Lazima akubali kwenda kwenye tiba ya kuacha dawa, iwe ndani au nje ya Nchi. Vinginevyo, naogopa kwa usalama wake.” - Prince Ned Nwoko. Katika tuhuma hizo, Ned alimtaja mtu aitwaye Sammy kama Muuzaji mkuu wa dawa kwa Regina, huku pia akilitaja jina la Ann, akisema anahusika katika kile alichokiita “mzunguko wa maovu.” Tukio hili limetikisa jamii ya mtandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakionesha mshangao, wengine wakimtetea Regina, na wengi wakitaka ukweli wa kina juu ya maisha ya kifahari ya wawili hao. Je, hii ni drama ya ndoa ya Mastaa au kuna jambo kubwa zaidi nyuma ya pazia?
    0 Comments ·0 Shares ·344 Views
  • Alloyce Nyanda

    Mtani wangu @gersonmsigwa mbona umekanusha kwa herufi kubwa hivyo ku likes Picha ya Mange

    Unajua acha nikusaidie Mtani ufahamu kuwa katika Hii Dunia Serikali zote Duniani huwa zinajaribu kuhakikisha zina “control information

    Uki Control Informatio utakuwa na nguvu ya kumuita Malaika-Shetani na shetani ukamuita Malaika na dunia itatii na haitahoji.

    Wenye nguvu za utoaji wa taarifa za dunia waliwahi ku control Information na kuuambia ulimwengu kuwa Muammar al-Gaddafi ni gaidi na dunia ikatii amri

    Waliandika kwa lugha zao nasi tukatafsiri kwa lugha yetu na tukamuita mwana wa Afrika Gadafi ni Gaidi.

    “Information is power”. Sasa wewe badala ya Kupambana ku Control Information wewe unapambana Kukanusha haitakusaidia wewe wala serikali yetu.

    Na Ku control Information huwa sio kuzima Internet au kufunga Mitandao kwa sababu wanaotaka taarifa wameshajua watapataje ndio wana VPN na wapo tayari Kulipia

    nataka nikushauri Msemaji ukifanyie kazi kwa haraka badala ya kukanusha na kulalamika jenga uwezo wa kumiliki nguvu ya Taarifa iliyokaribu na umma.

    Jitaidi Pages za serikali zenye kutoa taarifa zifanye ziwe na nguvu ili ziwe karibu na jamii yake sasa haiwezekani Mange Kimambi awe na ukaribu na jamii kiasi hicho kuliko serikali yenyewe.

    Unakuta wizara ya Afya badala ya kutengeneza maudhui yenye kuisogeza jamii karibu nayo wao wanaweza hata kupost picha waziri anasalimiana na Dkt na kuigeuza kuwa jambo la maana kupeleka kwa watu .

    Sasa kwa hulka hiyo utawezaje Ku control Power ya Taarifa? ukimkuta Mange amechapa Hospital X haina Vifaa wananchi wanaona huyu ndiye anatusaidia na wewe @gersonmsigwa unabakiza kazi ya kukanusha tu wakati unayo nafasi ya kueleza situation ya Hospital hata kabla ya wengine kupost

    Lazima idara za serikali zigeuzwe kuwa na uwezo wa kufanya Visibility kubwa , unadhani wewe Msigwa utaweza peke yako? Utachekwa tu

    Utakanusha ma ngapi na utapinga Ma ngapi? maana hata leo kuonekana umelikes page umehaha mbaya why? Wewe Pambana kuifanya Jamii kuiamini serikali zaidi ili wampuuze Mange

    Unataka kweli U contol Information kwa mbinu ya Mwijaku au Mzee wangu au Mafufu? (Utaishia kuchekesha tu)

    Power of Informations
    Alloyce Nyanda ✍️ Mtani wangu @gersonmsigwa mbona umekanusha kwa herufi kubwa hivyo ku likes Picha ya Mange Unajua acha nikusaidie Mtani ufahamu kuwa katika Hii Dunia Serikali zote Duniani huwa zinajaribu kuhakikisha zina “control information Uki Control Informatio utakuwa na nguvu ya kumuita Malaika-Shetani na shetani ukamuita Malaika na dunia itatii na haitahoji. Wenye nguvu za utoaji wa taarifa za dunia waliwahi ku control Information na kuuambia ulimwengu kuwa Muammar al-Gaddafi ni gaidi na dunia ikatii amri Waliandika kwa lugha zao nasi tukatafsiri kwa lugha yetu na tukamuita mwana wa Afrika Gadafi ni Gaidi. “Information is power”. Sasa wewe badala ya Kupambana ku Control Information wewe unapambana Kukanusha haitakusaidia wewe wala serikali yetu. Na Ku control Information huwa sio kuzima Internet au kufunga Mitandao kwa sababu wanaotaka taarifa wameshajua watapataje ndio wana VPN na wapo tayari Kulipia nataka nikushauri Msemaji ukifanyie kazi kwa haraka badala ya kukanusha na kulalamika jenga uwezo wa kumiliki nguvu ya Taarifa iliyokaribu na umma. Jitaidi Pages za serikali zenye kutoa taarifa zifanye ziwe na nguvu ili ziwe karibu na jamii yake sasa haiwezekani Mange Kimambi awe na ukaribu na jamii kiasi hicho kuliko serikali yenyewe. Unakuta wizara ya Afya badala ya kutengeneza maudhui yenye kuisogeza jamii karibu nayo wao wanaweza hata kupost picha waziri anasalimiana na Dkt na kuigeuza kuwa jambo la maana kupeleka kwa watu . Sasa kwa hulka hiyo utawezaje Ku control Power ya Taarifa? ukimkuta Mange amechapa Hospital X haina Vifaa wananchi wanaona huyu ndiye anatusaidia na wewe @gersonmsigwa unabakiza kazi ya kukanusha tu wakati unayo nafasi ya kueleza situation ya Hospital hata kabla ya wengine kupost Lazima idara za serikali zigeuzwe kuwa na uwezo wa kufanya Visibility kubwa , unadhani wewe Msigwa utaweza peke yako? Utachekwa tu Utakanusha ma ngapi na utapinga Ma ngapi? maana hata leo kuonekana umelikes page umehaha mbaya why? Wewe Pambana kuifanya Jamii kuiamini serikali zaidi ili wampuuze Mange Unataka kweli U contol Information kwa mbinu ya Mwijaku au Mzee wangu au Mafufu? (Utaishia kuchekesha tu) Power of Informations
    0 Comments ·0 Shares ·296 Views
  • Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, amesema amejificha “mahali salama” baada ya jaribio la kumuua, kufuatia wiki kadhaa za maandamano yanayomtaka ajiuzulu.

    Kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye Facebook, Rajoelina (51) alidai kuwa kundi la wanajeshi na wanasiasa lilipanga kumuua, bila kufichua alipo. Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinadai huenda alitoroka nchini kwa ndege ya kijeshi ya Ufaransa.

    Maandamano makubwa yanayoongozwa na vijana yamekuwa yakiendelea kote nchini, wakilalamikia hali ngumu ya kiuchumi na utawala wa kiimla. Serikali haijatoa tamko rasmi kuhusu jaribio hilo, huku hali ya taharuki ikiendelea katika mji mkuu, Antananarivo.

    Tufuatilie kupitia YouTube ya NIOKOE TV
    Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, amesema amejificha “mahali salama” baada ya jaribio la kumuua, kufuatia wiki kadhaa za maandamano yanayomtaka ajiuzulu. Kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye Facebook, Rajoelina (51) alidai kuwa kundi la wanajeshi na wanasiasa lilipanga kumuua, bila kufichua alipo. Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinadai huenda alitoroka nchini kwa ndege ya kijeshi ya Ufaransa. Maandamano makubwa yanayoongozwa na vijana yamekuwa yakiendelea kote nchini, wakilalamikia hali ngumu ya kiuchumi na utawala wa kiimla. Serikali haijatoa tamko rasmi kuhusu jaribio hilo, huku hali ya taharuki ikiendelea katika mji mkuu, Antananarivo. 🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya NIOKOE TV
    0 Comments ·0 Shares ·299 Views
  • Why Do More Shooters Choose the Atlas Bipod?

    The Atlas bipod is a top choice for many shooters. But what makes it stand out? It’s strong without being heavy. It locks in place fast. You can shift positions without losing your setup. That makes it great for field work or the range.
    The design suits many shooting styles. From prone to awkward angles, it stays stable. It gives you control and stays quick to adjust. Many shooters trust it for that reason. It works well with different rifles and adapts to changing ground.
    Delta Tactical stocks Atlas models made for real use. Each one is tested to handle tough conditions. They are strong, simple, and ready for the field. You can rely on them for repeated use in demanding settings.
    Need steady support without bulk? See why more shooters are going with Atlas. Your setup might be missing one piece.

    For more visit - https://www.deltatactical.com.au/shop-by-category/bipods-tripods/
    Why Do More Shooters Choose the Atlas Bipod? The Atlas bipod is a top choice for many shooters. But what makes it stand out? It’s strong without being heavy. It locks in place fast. You can shift positions without losing your setup. That makes it great for field work or the range. The design suits many shooting styles. From prone to awkward angles, it stays stable. It gives you control and stays quick to adjust. Many shooters trust it for that reason. It works well with different rifles and adapts to changing ground. Delta Tactical stocks Atlas models made for real use. Each one is tested to handle tough conditions. They are strong, simple, and ready for the field. You can rely on them for repeated use in demanding settings. Need steady support without bulk? See why more shooters are going with Atlas. Your setup might be missing one piece. For more visit - https://www.deltatactical.com.au/shop-by-category/bipods-tripods/
    Bipods & Tripods - Atlas Bipod Options
    www.deltatactical.com.au
    Explore a variety of bipods and tripods, including Atlas Bipod selections, for enhanced stability and accuracy at Delta Tactical.
    0 Comments ·0 Shares ·259 Views
  • Miaka mitatu iliyopita, Ancelotti alisafiri mpaka jijini Manchester kumfuata Pep Guardiola ili kumuuliza kuhusu sababu ya mafanikio yake na City.

    Guardiola alimuambia kuwa sababu ya mafanikio yake ni kwamba anafanya kazi na wachezaji wenye akili, kisha alimuita De Bruyne kuthibitisha kwa Ancelotti.

    Alimuuliza De Bruyne, "Ni nani mtoto wa wazazi wako, lakini siyo kaka au dada zako?"
    De Bruyne akajibu, "Mimi."

    Ancelotti aliporudi Madrid akamuita Mendy, akamuuliza swali lile lile "Ni nani mtoto wa wazazi wako lakini siyo kaka au dada zako?"

    Mendy akasema, "Ngoja kidogo," akaenda kumuuliza Modrić. Modrić akajibu, "Mimi."

    Mendy akarudi kwa Ancelotti na kumwambia jibu ni "Modrić."

    Ancelotti akasema, "Umekosa jibu ni ni De Bruyne."

    #SportsElite
    Miaka mitatu iliyopita, Ancelotti alisafiri mpaka jijini Manchester kumfuata Pep Guardiola ili kumuuliza kuhusu sababu ya mafanikio yake na City. Guardiola alimuambia kuwa sababu ya mafanikio yake ni kwamba anafanya kazi na wachezaji wenye akili, kisha alimuita De Bruyne kuthibitisha kwa Ancelotti. Alimuuliza De Bruyne, "Ni nani mtoto wa wazazi wako, lakini siyo kaka au dada zako?" De Bruyne akajibu, "Mimi." Ancelotti aliporudi Madrid akamuita Mendy, akamuuliza swali lile lile "Ni nani mtoto wa wazazi wako lakini siyo kaka au dada zako?" Mendy akasema, "Ngoja kidogo," akaenda kumuuliza Modrić. Modrić akajibu, "Mimi." Mendy akarudi kwa Ancelotti na kumwambia jibu ni "Modrić." Ancelotti akasema, "Umekosa jibu ni ni De Bruyne."🤣 😂 #SportsElite
    0 Comments ·0 Shares ·359 Views
  • Lamine Yamal ni mmoja wa mawinga bora kabisa wa kulia kwenye soka kwa sasa huku Nuno Mendes akiwa beki bora kabisa wa kushoto kwa sasa Duniani wakati wawili hawa wakikutana mara mbili hivi karibuni kwenye mchezo wa UEFA Nations League (Fainali, Ureno vs Uhispania) na kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL), (Barcelona vs PSG).

    Kwenye mechi zote mbili Yamal ameshindwa kutamba mbele ya Mreno huyo ambaye alifunga goli na kutoa 'assist' na kuwa nyota wa mchezo huku timu yake ikishinda mara zote wakati Yamal akitoka patupu bila goli huku timu yake ikipoteza.

    Je unadhani kuna winga anaweza kummudu Nuno Mendes kwa sasa?

    FAINALI: #UEFANATIONS LEAGUE
    Ureno 2-2 Uhispania (P 5-3)
    Mendes
    Ronaldo

    Zubimendi
    Oyarzabal

    #UCL
    Barcelona 1-2 PSG
    19' Torres
    38' Mayulu( Mendes)
    90' Ramos ( Hakimi)


    #SportsElite
    Lamine Yamal ni mmoja wa mawinga bora kabisa wa kulia kwenye soka kwa sasa huku Nuno Mendes akiwa beki bora kabisa wa kushoto kwa sasa Duniani wakati wawili hawa wakikutana mara mbili hivi karibuni kwenye mchezo wa UEFA Nations League (Fainali, Ureno vs Uhispania) na kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL), (Barcelona vs PSG). Kwenye mechi zote mbili Yamal ameshindwa kutamba mbele ya Mreno huyo ambaye alifunga goli na kutoa 'assist' na kuwa nyota wa mchezo huku timu yake ikishinda mara zote wakati Yamal akitoka patupu bila goli huku timu yake ikipoteza. ✍️ Je unadhani kuna winga anaweza kummudu Nuno Mendes kwa sasa? FAINALI: #UEFANATIONS LEAGUE Ureno 🇵🇹 2-2 🇪🇸 Uhispania (P 5-3) ⚽ Mendes ⚽ Ronaldo ⚽ Zubimendi ⚽ Oyarzabal #UCL Barcelona 🇪🇸 1-2 🇫🇷 PSG ⚽ 19' Torres ⚽ 38' Mayulu(🅰️ Mendes) ⚽ 90' Ramos (🅰️ Hakimi) #SportsElite
    0 Comments ·0 Shares ·553 Views
More Results