• HOW TO DEPLOY WHATSAPP BOT FOR FREE ONLINE 24/7

    Watch this video
    https://m.youtube.com/watch?v=7NFWBdXHpw8


    Deployment Site
    https://host.talkdrove.com/auth/signup?ref=E565C590




    #DUDUU_MENDEZ
    #DML_TECH
    HOW TO DEPLOY WHATSAPP BOT FOR FREE ONLINE 24/7 Watch this video https://m.youtube.com/watch?v=7NFWBdXHpw8 Deployment Site https://host.talkdrove.com/auth/signup?ref=E565C590 #DUDUU_MENDEZ #DML_TECH
    0 Комментарии ·0 Поделились ·8 Просмотры
  • I real love you..
    I real love you..❤️❤️❤️❤️
    0 Комментарии ·0 Поделились ·5 Просмотры
  • "Ni kweli tunamshikilia Ali Kamwe ambaye ni Msemaji wa Klabu ya Yanga na tunamfanyia mahojiano kwa tuhuma za kutoa maneno machafu kwa Viongozi wa Serikali na tutatoa taarifa rasmi baada ya mahojiano kukamilika" - RPC Richard Abwao, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani wa Tabora.

    "Ni kweli tunamshikilia Ali Kamwe ambaye ni Msemaji wa Klabu ya Yanga na tunamfanyia mahojiano kwa tuhuma za kutoa maneno machafu kwa Viongozi wa Serikali na tutatoa taarifa rasmi baada ya mahojiano kukamilika" - RPC Richard Abwao, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani wa Tabora.
    Like
    1
    · 1 Комментарии ·0 Поделились ·12 Просмотры
  • Msemaji wa klabu ya Yanga SC, Ali Kamwe alikamatwa na Jeshi Polisi baada ya mchezo wao dhidi ya klabu ya Tabora United majira ya saa saba na nusu usiku wa kuamkia leo hii. Ali Kamwe alipelekwa kituo kikubwa cha Polisi cha Mkoa na amelala ndani hapo na hadi sasa bado hajaachiwa.

    Viongozi wa Yanga SC bado wanaendelea kufanya jitihada za kumtoa Ali Kamwe hapo haijawekwa bayana makosa aliyoyafanya Msemaji huyo. Taarifa iliyopo ni kuwa, inadaiwa Ali Kamwe alitoa kauli isiyokuwa nzuri kipindi anamjibu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha kabla ya mechi kama sehemu ya utani baada ya Mkuu huyo kutoa ahadi ya Shilingi milioni sitini (60) endapo klabu ya Tabora United ikimfunga Yanga SC ambapo mchezo ulimalizika kwa ushindi wa Yanga SC wa mabao matatu kwa bila (0-3).

    Msemaji wa klabu ya Yanga SC, Ali Kamwe alikamatwa na Jeshi Polisi baada ya mchezo wao dhidi ya klabu ya Tabora United majira ya saa saba na nusu usiku wa kuamkia leo hii. Ali Kamwe alipelekwa kituo kikubwa cha Polisi cha Mkoa na amelala ndani hapo na hadi sasa bado hajaachiwa. Viongozi wa Yanga SC bado wanaendelea kufanya jitihada za kumtoa Ali Kamwe hapo haijawekwa bayana makosa aliyoyafanya Msemaji huyo. Taarifa iliyopo ni kuwa, inadaiwa Ali Kamwe alitoa kauli isiyokuwa nzuri kipindi anamjibu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha kabla ya mechi kama sehemu ya utani baada ya Mkuu huyo kutoa ahadi ya Shilingi milioni sitini (60) endapo klabu ya Tabora United ikimfunga Yanga SC ambapo mchezo ulimalizika kwa ushindi wa Yanga SC wa mabao matatu kwa bila (0-3).
    0 Комментарии ·0 Поделились ·19 Просмотры
  • Muigizaji maarufu na Mkongwe Duniani, Jean-Claude Van Damme anakabiliwa na mashtaka ya kujibu baada ya kudaiwa kufanya ngono na Wanawake waliotekwa nyara Nchini Romania .

    Kwa mujibu wa CNN, Idara ya Romania ya Uchunguzi wa Uhalifu wa kupangwa na Ugaidi (DIICOT) imewasilisha malalamiko ya jinai dhidi ya Van Damme, ikidai alifanya ngono kwa kujua na Wanawake kadhaa waliokuwa wakitumiwa katika biashara haramu ya ngono.

    Kulingana na ripoti hiyo, Mwigizaji huyo Raia wa Ubelgiji anadaiwa kukutana na Watu kadhaa ambao pia wanachunguzwa kwa uhalifu wa usafirishaji wa Binadamu, ambao walimpa fursa ya kufanya ngono na Wanamitindo watano (5) wa Kiromania kama zawadi.

    Tukio hilo linaripotiwa kutokea Cannes Nchini Ufaransa hivyo, Serikali ya hiyo inapaswa kuidhinisha mashitaka hayo ya jinai lakini haikuwekwa wazi ni lini tukio hilo lilitokea hapo Ufaransa.

    Muigizaji maarufu na Mkongwe Duniani, Jean-Claude Van Damme anakabiliwa na mashtaka ya kujibu baada ya kudaiwa kufanya ngono na Wanawake waliotekwa nyara Nchini Romania 🇷🇴. Kwa mujibu wa CNN, Idara ya Romania ya Uchunguzi wa Uhalifu wa kupangwa na Ugaidi (DIICOT) imewasilisha malalamiko ya jinai dhidi ya Van Damme, ikidai alifanya ngono kwa kujua na Wanawake kadhaa waliokuwa wakitumiwa katika biashara haramu ya ngono. Kulingana na ripoti hiyo, Mwigizaji huyo Raia wa Ubelgiji 🇧🇪 anadaiwa kukutana na Watu kadhaa ambao pia wanachunguzwa kwa uhalifu wa usafirishaji wa Binadamu, ambao walimpa fursa ya kufanya ngono na Wanamitindo watano (5) wa Kiromania kama zawadi. Tukio hilo linaripotiwa kutokea Cannes Nchini Ufaransa 🇫🇷 hivyo, Serikali ya hiyo inapaswa kuidhinisha mashitaka hayo ya jinai lakini haikuwekwa wazi ni lini tukio hilo lilitokea hapo Ufaransa.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·12 Просмотры
  • "Simba SC wamepoteza lakini HII WANAVUKA, NO DOUBT. Sioni Al Masry wakileta ubishi kwa Mkapa, dhahiri watatii Sheria iwe kwa shuruti au bila shuruti. Heads up boys, come finish your job. TANZANIA KWANZA" - Jemedari Said, Mchambuzi.

    "Simba SC wamepoteza lakini HII WANAVUKA, NO DOUBT. Sioni Al Masry wakileta ubishi kwa Mkapa, dhahiri watatii Sheria iwe kwa shuruti au bila shuruti. Heads up boys, come finish your job. TANZANIA 🇹🇿 KWANZA" - Jemedari Said, Mchambuzi.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·29 Просмотры
  • “Kila siku Robo tu , Kocha naye amechangia Dakika ya kwanza tu toa Ateba weka Mukwala , Halftime toa Ngoma weka Mavambo mwarabu alikuwa anakufa” Mwisho wa kunukuu

    Kuna kibanda umiza nipo hapa nimenukuu maneno ya shabiki Ingawa sijafanikiwa kujua ni shabiki wa timu gani" - Shaffih Dauda, Mchambuzi

    “Kila siku Robo tu , Kocha naye amechangia Dakika ya kwanza tu toa Ateba weka Mukwala , Halftime toa Ngoma weka Mavambo mwarabu alikuwa anakufa” Mwisho wa kunukuu Kuna kibanda umiza nipo hapa nimenukuu maneno ya shabiki Ingawa sijafanikiwa kujua ni shabiki wa timu gani" - Shaffih Dauda, Mchambuzi ✍️
    0 Комментарии ·0 Поделились ·23 Просмотры
  • "Goli mbili ni nyingi kwenye soka la Africa,tena kwa bahati mbaya ni 2-0,hivyo kwenye mechi ya pili Simba wanatakiwa kufunga goli tatu huku wakipambana kutoruhusu goli lolote….huu ni mlima mkubwa sana.

    Kuna mtu atakwambia Simba wamecheza vizuri,walikuwa na on target 7 na total shots 18 ila mwisho wa Siku hakuna goli.

    Narudia tena mechi za mtoano watu hawaangalii umiliki wa mpira bali matokeo ya mwisho,ndio maana ushangai kuona Al ahly anapaki Bus kwenye mechi za ugenini.

    Ni kweli Simba walikuwa na umiliki mkubwa ila nyuma hawakuwa na nidhamu,Al Masry walikuwa tishio kwenye counter na hata goli la pili limetokana na counter.

    Haya ni makosa ya miaka yote ya Simba kutaka umiliki mkubwa kuliko matokeo ya kupita.

    Nilitarajia Simba kupaki bus na kupiga counter ila imekuwa tofauti na goli mbili wamefungwa baada ya kuingia kwenye mtego wa Masry

    Simba wametengeneza mlima mkubwa sana" - Hans Rafael, Mchambuzi.

    "Goli mbili ni nyingi kwenye soka la Africa,tena kwa bahati mbaya ni 2-0,hivyo kwenye mechi ya pili Simba wanatakiwa kufunga goli tatu huku wakipambana kutoruhusu goli lolote….huu ni mlima mkubwa sana. Kuna mtu atakwambia Simba wamecheza vizuri,walikuwa na on target 7 na total shots 18 ila mwisho wa Siku hakuna goli. Narudia tena mechi za mtoano watu hawaangalii umiliki wa mpira bali matokeo ya mwisho,ndio maana ushangai kuona Al ahly anapaki Bus kwenye mechi za ugenini. Ni kweli Simba walikuwa na umiliki mkubwa ila nyuma hawakuwa na nidhamu,Al Masry walikuwa tishio kwenye counter na hata goli la pili limetokana na counter. Haya ni makosa ya miaka yote ya Simba kutaka umiliki mkubwa kuliko matokeo ya kupita. Nilitarajia Simba kupaki bus na kupiga counter ila imekuwa tofauti na goli mbili wamefungwa baada ya kuingia kwenye mtego wa Masry🥲 Simba wametengeneza mlima mkubwa sana" - Hans Rafael, Mchambuzi.
    Like
    1
    · 0 Комментарии ·0 Поделились ·50 Просмотры
  • Mahakama Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imebatilisha hukumu ya kifo waliyopewa Raia watatu (3) wa Marekani kwa makosa ya jinai, ugaidi na kujaribu kuipindua Serikali ya Nchi hiyo.

    Shirika la Habari la Reuters, limeripoti leo Aprili 2,2025, kuwa taarifa ya Ikulu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeeleza watatu hao sasa hawatotumikia adhabu ya kifo badala yake watatumikia kifungo cha maisha jela. Walikuwa miongoni mwa Watu (37) waliohukumiwa kifo Septemba mwaka jana (2024) na Mahakama ya Kijeshi Nchini DR Congo katika mashitaka hayo ambayo hata hivyo waliyakanusha.

    Watatu hao ambao ni Mtoto wa Raia wa Marekani mwenye asili ya DR Congo, Christian Malanga, Marcel Malanga Malu, Rafiki zake Tylor Thomson na Zalman Polun Benjamin, walipewa msamaha kutoka kwa Rais Felix Tshisekedi. Walishtakiwa kwa kuongoza genge la uhalifu lililotekeleza shambulio dhidi ya ikulu na makazi ya Mshirika wa Rais wa Nchi nchi hiyo, Mei, 2024.

    Katika Taarifa iliyosomwa na Msemaji wa Rais Félix Tshisekedi, Tyna Salama kwenye Televisheni ya Taifa, imesema kuwa Rais Tshisekedi ametoa msamaha huo kwa kubatilisha hukumu ya kifo kwa Rais hao na kuwa ya kifungo cha maisha Jela kwa sababu ya kudumisha mahusiano mazuri kimataifa na Nchi ya Marekani.

    Kubatilishwa kwa hukumu hiyo kunakuja kabla ya ziara ya Mshauri mpya Mwandamizi wa Marekani barani Afrika, Massad Boulos. Ambapo ziara hiyo ililenga kwenda DR Congo.
    Mahakama Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 imebatilisha hukumu ya kifo waliyopewa Raia watatu (3) wa Marekani 🇺🇸 kwa makosa ya jinai, ugaidi na kujaribu kuipindua Serikali ya Nchi hiyo. Shirika la Habari la Reuters, limeripoti leo Aprili 2,2025, kuwa taarifa ya Ikulu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeeleza watatu hao sasa hawatotumikia adhabu ya kifo badala yake watatumikia kifungo cha maisha jela. Walikuwa miongoni mwa Watu (37) waliohukumiwa kifo Septemba mwaka jana (2024) na Mahakama ya Kijeshi Nchini DR Congo katika mashitaka hayo ambayo hata hivyo waliyakanusha. Watatu hao ambao ni Mtoto wa Raia wa Marekani mwenye asili ya DR Congo, Christian Malanga, Marcel Malanga Malu, Rafiki zake Tylor Thomson na Zalman Polun Benjamin, walipewa msamaha kutoka kwa Rais Felix Tshisekedi. Walishtakiwa kwa kuongoza genge la uhalifu lililotekeleza shambulio dhidi ya ikulu na makazi ya Mshirika wa Rais wa Nchi nchi hiyo, Mei, 2024. Katika Taarifa iliyosomwa na Msemaji wa Rais Félix Tshisekedi, Tyna Salama kwenye Televisheni ya Taifa, imesema kuwa Rais Tshisekedi ametoa msamaha huo kwa kubatilisha hukumu ya kifo kwa Rais hao na kuwa ya kifungo cha maisha Jela kwa sababu ya kudumisha mahusiano mazuri kimataifa na Nchi ya Marekani. Kubatilishwa kwa hukumu hiyo kunakuja kabla ya ziara ya Mshauri mpya Mwandamizi wa Marekani barani Afrika, Massad Boulos. Ambapo ziara hiyo ililenga kwenda DR Congo.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·67 Просмотры
  • Liziki za watu zipo mikononi mwa watu
    Maisha ni kutegemeana
    Liziki za watu zipo mikononi mwa watu Maisha ni kutegemeana
    Sad
    1
    · 0 Комментарии ·0 Поделились ·36 Просмотры
  • Pamoja na uwezo wa ugomvi wa Mashabiki ambao ulitokea kwenye mchezo wa jana kati ya Mamelodi Sundowns dhidi ya Esperence kwenye mchezo wa klabu bingwa barani Afrika (CAF Champions League) lakini hiki kitendo kimesisimua zaidi Mashabiki wengi.

    Picha hii inaeleza sababu milioni ya upendo ambao unatakiwa pindi Mashabiki wawapo Uwanjani. Mpira wa miguu unatufanya kuwa ndugu hii ndio maana unaitwa Football kwa kiingereza.

    Pamoja na uwezo wa ugomvi wa Mashabiki ambao ulitokea kwenye mchezo wa jana kati ya Mamelodi Sundowns 🇿🇦dhidi ya Esperence 🇹🇳 kwenye mchezo wa klabu bingwa barani Afrika (CAF Champions League) lakini hiki kitendo kimesisimua zaidi Mashabiki wengi. Picha hii inaeleza sababu milioni ya upendo ambao unatakiwa pindi Mashabiki wawapo Uwanjani. Mpira wa miguu unatufanya kuwa ndugu hii ndio maana unaitwa Football kwa kiingereza.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·62 Просмотры
  • Uongozi wa Ligi Kuu ya mpira wa miguu Nchini Marekani , Major League Soccer (MLS), umempiga marufuku Mlinzi binafsi (Bodyguard) wa Lionel Messi, Yassine Cheuko, kuwa kando na kuingia katikati ya Uwanja wakati wa mechi za Inter Miami kwa lengo lake la kumlinda Mwajiri wake Messi.

    Ikumbukwe kwamba Yassine Cheuko, ni Mwanajeshi wa zamani wa kikosi maalumu cha operesheni za kijeshi cha Jeshi la Majini la Marekani (U.S. Navy) kinachobobea katika vita visivyo vya kawaida, kupambana na ugaidi, mashambulizi ya moja kwa moja, na upelelezi wa kijeshi. Tangu Yessine Cheuko aanze kufanya kazi na Messi amejizolea umaarufu mkubwa Duniani kwani ameonekana mara nyingi akiwadhibiti Wavamizi mbalimbali ambao wengi lengo lao huwa sio baya, zaidi wanataka kupiga picha na Messi.

    Tayari uongozi wa Ligi hiyo umemzuia kuingia Uwanjani, sasa ataruhusiwa tu kuwa kwenye Vyumba vya kubadilishia nguo na maeneo ya Waandishi wa habari siku za mechi. Uamuzi huu ni sehemu ya mpango wa (MLS) wa kuchukua mamlaka kamili ya usalama wa mechi.

    Baada ya katazo, Yassine Cheuko ameonyesha kutoridhishwa na hatua hiyo, akisema kuwa Wavamizi wa Uwanja ni tatizo kubwa zaidi Nchini Marekani kuliko Ulaya. Kwa mujibu wake, katika miaka saba aliyofanya kazi Ulaya, kulikuwa na matukio sita pekee ya uvamizi Uwanjani, ilhali katika miezi 20 Nchini Marekani, tayari yameshuhudiwa matukio 16.

    Mlinzi huyo ameendelea kusema kuwa Uongozi wa Ligi Kuu ya Marekani haukutakiwa kumzuia kufanye kazi yake bali walitakiwa kumpa ushirikiano ili kazi hiyo waifanye kwa pamoja kwa sababu eti kipindi yupo barani Ulaya, alipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwenye Uongozi na alifanya kazi yake kwa uhuru. Pamoja na kuzuiliwa kuingia Uwanjani au kukaa kando ya Uwanja, Cheuko amesema kuwa ataendelea kufanya kazi yake kama kawaida bila kuvunja sheria au utaratibu uliopo kwenye mchezo wa mpira wa miguu.

    Uongozi wa Ligi Kuu ya mpira wa miguu Nchini Marekani 🇺🇸, Major League Soccer (MLS), umempiga marufuku Mlinzi binafsi (Bodyguard) wa Lionel Messi, Yassine Cheuko, kuwa kando na kuingia katikati ya Uwanja wakati wa mechi za Inter Miami kwa lengo lake la kumlinda Mwajiri wake Messi. Ikumbukwe kwamba Yassine Cheuko, ni Mwanajeshi wa zamani wa kikosi maalumu cha operesheni za kijeshi cha Jeshi la Majini la Marekani (U.S. Navy) kinachobobea katika vita visivyo vya kawaida, kupambana na ugaidi, mashambulizi ya moja kwa moja, na upelelezi wa kijeshi. Tangu Yessine Cheuko aanze kufanya kazi na Messi amejizolea umaarufu mkubwa Duniani kwani ameonekana mara nyingi akiwadhibiti Wavamizi mbalimbali ambao wengi lengo lao huwa sio baya, zaidi wanataka kupiga picha na Messi. Tayari uongozi wa Ligi hiyo umemzuia kuingia Uwanjani, sasa ataruhusiwa tu kuwa kwenye Vyumba vya kubadilishia nguo na maeneo ya Waandishi wa habari siku za mechi. Uamuzi huu ni sehemu ya mpango wa (MLS) wa kuchukua mamlaka kamili ya usalama wa mechi. Baada ya katazo, Yassine Cheuko ameonyesha kutoridhishwa na hatua hiyo, akisema kuwa Wavamizi wa Uwanja ni tatizo kubwa zaidi Nchini Marekani kuliko Ulaya. Kwa mujibu wake, katika miaka saba aliyofanya kazi Ulaya, kulikuwa na matukio sita pekee ya uvamizi Uwanjani, ilhali katika miezi 20 Nchini Marekani, tayari yameshuhudiwa matukio 16. Mlinzi huyo ameendelea kusema kuwa Uongozi wa Ligi Kuu ya Marekani haukutakiwa kumzuia kufanye kazi yake bali walitakiwa kumpa ushirikiano ili kazi hiyo waifanye kwa pamoja kwa sababu eti kipindi yupo barani Ulaya, alipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwenye Uongozi na alifanya kazi yake kwa uhuru. Pamoja na kuzuiliwa kuingia Uwanjani au kukaa kando ya Uwanja, Cheuko amesema kuwa ataendelea kufanya kazi yake kama kawaida bila kuvunja sheria au utaratibu uliopo kwenye mchezo wa mpira wa miguu.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·105 Просмотры
  • Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepanga kufanya mazungumzo na Kundi la Waasi wa M23, April 9 mwaka huu, Nchini Qatar , yenye nia ya kutafuta amani katika eneo la Mashariki mwa Nchi hiyo. Kikao hicho kitakachofanyika Jijini Doha n kitakuwa kikao cha kwanza kwa pande zote mbili kukaa na kuzungumza baada ya kuthibitisha kuwa watashiriki.

    Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 imepanga kufanya mazungumzo na Kundi la Waasi wa M23, April 9 mwaka huu, Nchini Qatar 🇶🇦, yenye nia ya kutafuta amani katika eneo la Mashariki mwa Nchi hiyo. Kikao hicho kitakachofanyika Jijini Doha n kitakuwa kikao cha kwanza kwa pande zote mbili kukaa na kuzungumza baada ya kuthibitisha kuwa watashiriki.
    Love
    1
    · 0 Комментарии ·0 Поделились ·67 Просмотры
  • Aliyetiwa hatiani kuwa Mhalifu wa kivita na Mahakama ya kimataifa ya (ICC) kwa makosa mbalimbali, Thomas Lubanga, ametangaza kuunda kundi jipya la Waasi lenye lengo la kuiangusha Serikali ya Jimbo la Ituri, lililopo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo .

    Nchi ya DR Congo imekuwa ikikabiliwa na tishio la kiusalama katika Mikoa ya mashariki ambapo makundi ya Waasi ikiwemo Muungano wa Waasi wa AFC/M23 unaoshikilia Miji ya Goma, Bukavu, Nyabibwe na Walikale.

    Hata hivyo, uamuzi wa Thomas Lubanga ambaye ni Mzaliwa wa Mkoa wa Ituri Nchini DR Congo na anayeishi Nchini Uganda , kutangaza kuanzisha Kundi lake la Waasi alilolipa jina Convention for the Popular Revolution (CPR) ambalo litaongeza hofu ya machafuko Nchini humo wakati huu ambao Serikali ya Rais Felix Tshisekedi inatafuta maridhiano na M23 kwa njia ya mazungumzo.

    Shirika la Habari la Reuters, limeripoti leo Jumanne Aprili Mosi, 2025, kuwa Lubanga ambaye ni Mzaliwa wa Ituri, alihukumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mwaka 2012 kwa makosa ya kuwasajili Watoto kama Askari na akapewa kifungo cha miaka 14 Gerezani, baadaye aliachiliwa mwaka 2020 na Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi kisha akamteua kuwa sehemu ya kikosi kazi cha kuleta amani Jimboni Ituri.

    Hata hivyo, mwaka 2022 alitekwa nyara kwa miezi miwili na kundi la Waasi, tukio analodai kupangwa na Serikali ya DR Congo kwa lengo kumpoteza ila kwa sasa anaishi Nchini Uganda.

    Aliyetiwa hatiani kuwa Mhalifu wa kivita na Mahakama ya kimataifa ya (ICC) kwa makosa mbalimbali, Thomas Lubanga, ametangaza kuunda kundi jipya la Waasi lenye lengo la kuiangusha Serikali ya Jimbo la Ituri, lililopo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Nchi ya DR Congo imekuwa ikikabiliwa na tishio la kiusalama katika Mikoa ya mashariki ambapo makundi ya Waasi ikiwemo Muungano wa Waasi wa AFC/M23 unaoshikilia Miji ya Goma, Bukavu, Nyabibwe na Walikale. Hata hivyo, uamuzi wa Thomas Lubanga ambaye ni Mzaliwa wa Mkoa wa Ituri Nchini DR Congo na anayeishi Nchini Uganda 🇺🇬, kutangaza kuanzisha Kundi lake la Waasi alilolipa jina Convention for the Popular Revolution (CPR) ambalo litaongeza hofu ya machafuko Nchini humo wakati huu ambao Serikali ya Rais Felix Tshisekedi inatafuta maridhiano na M23 kwa njia ya mazungumzo. Shirika la Habari la Reuters, limeripoti leo Jumanne Aprili Mosi, 2025, kuwa Lubanga ambaye ni Mzaliwa wa Ituri, alihukumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mwaka 2012 kwa makosa ya kuwasajili Watoto kama Askari na akapewa kifungo cha miaka 14 Gerezani, baadaye aliachiliwa mwaka 2020 na Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi kisha akamteua kuwa sehemu ya kikosi kazi cha kuleta amani Jimboni Ituri. Hata hivyo, mwaka 2022 alitekwa nyara kwa miezi miwili na kundi la Waasi, tukio analodai kupangwa na Serikali ya DR Congo kwa lengo kumpoteza ila kwa sasa anaishi Nchini Uganda.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·140 Просмотры
  • Keep Smille
    #socialpopvideo
    #Socialpopreels
    Keep Smille🤩 #socialpopvideo #Socialpopreels
    0 Комментарии ·0 Поделились ·230 Просмотры
  • Furaha yetu sio pesa ✌ vado
    Furaha yetu sio pesa ✌ vado
    Love
    1
    · 0 Комментарии ·0 Поделились ·114 Просмотры ·0
  • Mafinga town
    Mafinga town
    Like
    Love
    2
    · 0 Комментарии ·0 Поделились ·69 Просмотры
  • Mke wa Mchezaji wa kimataifa wa Burkina Faso n'a klabu ya Yanga SC, Hamisa Mobetto (Tanzania ) ameingia kwenye orodha ya WAGS (Wives And Girlfriends of Footballers) ambao ni Wake (Wapenzi au Wachumba) wa Wachezaji wenye Wafuasi (followers) wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram Duniani.

    1. @georginagio (Mrs. Ronaldo) :+65.5M
    2. antonelaroccuzzo (Mrs. Messi) : +39.9M
    3. @iambeckyg (Mrs. Sebastian) : +37.2M
    4. @victoriabeckham (Mrs. Beckham) : +32.9M
    5. @perrieedwards (Mrs. Alex) :+19M

    6. @alishalehmann7 (Mrs. Douglas Luiz) : +16.6M
    7. @brunabiancardi (Mrs. Neymar Jr) : +13.6M
    8. @hamisamobetto (Mrs. Aziz Ki) : +12.1M
    9. @pilarrubio (Mrs. Sergio Ramos) : +11.1M
    10. @leighannepinnock (Mrs. Andre Gray) : +10M

    Mke wa Mchezaji wa kimataifa wa Burkina Faso 🇧🇫 n'a klabu ya Yanga SC, Hamisa Mobetto (Tanzania 🇹🇿) ameingia kwenye orodha ya WAGS (Wives And Girlfriends of Footballers) ambao ni Wake (Wapenzi au Wachumba) wa Wachezaji wenye Wafuasi (followers) wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram Duniani. 1. @georginagio (Mrs. Ronaldo) :+65.5M 2. antonelaroccuzzo (Mrs. Messi) : +39.9M 3. @iambeckyg (Mrs. Sebastian) : +37.2M 4. @victoriabeckham (Mrs. Beckham) : +32.9M 5. @perrieedwards (Mrs. Alex) :+19M 6. @alishalehmann7 (Mrs. Douglas Luiz) : +16.6M 7. @brunabiancardi (Mrs. Neymar Jr) : +13.6M 8. @hamisamobetto (Mrs. Aziz Ki) : +12.1M 9. @pilarrubio (Mrs. Sergio Ramos) : +11.1M 10. @leighannepinnock (Mrs. Andre Gray) : +10M
    0 Комментарии ·0 Поделились ·216 Просмотры
  • Rais wa Nchi ya Burkina Faso , Kapteni Ibrahim Traoré ametoa msamaha kwa Wanajeshi (21) waliojaribu kufanya mapinduzi ya Serikali ya Septemba mwaka 2015. Katika amri iliyosainiwa Machi 24 na kuwekwa hadharani Jumapili hii, Kapteni Traore aliweka masharti ya msamaha huu, ambao ulipigiwa kura na Bunge la Nchi hiy Desemba iliyopita.

    Wanajeshi hao (21), wakiwemo Maafisa, Maafisa wasio na kamisheni na Vyeo vingine, walifikishwa mahakamani na kutiwa hatiani kwa matendo yaliyofanywa Septemba 15 na 16, 2015, inasema amri iliyotiwa saini na Rais wa Nchi hiyo Kapteni Ibrahim Traore. Amri hii iliyopitishwa na Bunge mwishoni mwa Desemba 2024 ya msamaha na masharti ya kutoa msamaha kwa Watu waliopatikana na hatia kuhusiana na mapinduzi yaliyofeli ya 2015.

    Sheria hii pia imeweka wazi kwamba Askari waliotiwa hatiani au kufunguliwa mashtaka kuhusiana na kesi hii, wakionyesha kujitolea katika mapambano dhidi ya ugaidi Nchini humo, wanaweza kupata fursa ya neema ya msamaha ili kupandishwa cheo kazini.

    Rais wa Nchi ya Burkina Faso 🇧🇫, Kapteni Ibrahim Traoré ametoa msamaha kwa Wanajeshi (21) waliojaribu kufanya mapinduzi ya Serikali ya Septemba mwaka 2015. Katika amri iliyosainiwa Machi 24 na kuwekwa hadharani Jumapili hii, Kapteni Traore aliweka masharti ya msamaha huu, ambao ulipigiwa kura na Bunge la Nchi hiy Desemba iliyopita. Wanajeshi hao (21), wakiwemo Maafisa, Maafisa wasio na kamisheni na Vyeo vingine, walifikishwa mahakamani na kutiwa hatiani kwa matendo yaliyofanywa Septemba 15 na 16, 2015, inasema amri iliyotiwa saini na Rais wa Nchi hiyo Kapteni Ibrahim Traore. Amri hii iliyopitishwa na Bunge mwishoni mwa Desemba 2024 ya msamaha na masharti ya kutoa msamaha kwa Watu waliopatikana na hatia kuhusiana na mapinduzi yaliyofeli ya 2015. Sheria hii pia imeweka wazi kwamba Askari waliotiwa hatiani au kufunguliwa mashtaka kuhusiana na kesi hii, wakionyesha kujitolea katika mapambano dhidi ya ugaidi Nchini humo, wanaweza kupata fursa ya neema ya msamaha ili kupandishwa cheo kazini.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·122 Просмотры
  • Rais wa Marekani , DonaldTrump, ameibua mjadala mkali baada ya kusema kuwa kuna uwezekano wa yeye kuwania muhula wa tatu, licha ya Katiba ya Marekani kupiga marufuku jambo hilo kupitia Marekebisho ya 22. Katika mahojiano na NBCNews, Rais huyo hakutaka kufuta uwezekano wa kuwania tena Urais baada ya kumaliza mihula miwili, akidai kuwa kuna njia za kufanya hilo kutokea. Alisisitiza kuwa "hakuwa anatania," jambo ambalo limeibua hofu miongoni mwa Wachambuzi wa siasa na Wanaharakati wa demokrasia Nchini humo.

    Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, Rais haruhusiwi kutawala kwa zaidi ya mihula miwili ya miaka minne minne. Marekebisho ya 22 yaliwekwa ili kuzuia Mtu mmoja kuwa na mamlaka ya muda mrefu kama ilivyokuwa kwa Franklin D. Roosevelt, ambaye altawala kwa zaidi ya mihula miwili kabla ya marekebisho hayo kuidhinishwa mwaka 1951.

    Kauli ya Trump imeibua maswali kuhusu mbinu anazoweza kutumia kutafuta muhula wa tatu. Wachambuzi wa sheria wanabainisha kuwa ili hilo litokee, ama katiba ibadilishwe rasmi kwa marekebisho mapya, au ipatikane tafsiri mpya ya kisheria inayomruhusu kugombea tena. Hata hivyo, mchakato wa kubadili katiba ni mgumu na unahitaji ridhaa ya Bunge pamoja na Majimbo mengi ya Marekani.

    Baadhi ya Wafuasi wa Donald Trump wameunga mkono kauli yake, wakidai kuwa anastahili muda zaidi wa kuongoza Nchi. Hata hivyo, Wakosoaji wake wanasema kuwa hatua yoyote ya kupindua Marekebisho ya 22 inaweza kuwa tishio kwa demokrasia ya Marekani na kuweka msingi wa uongozi wa kiimla.

    Rais wa Marekani 🇺🇸, DonaldTrump, ameibua mjadala mkali baada ya kusema kuwa kuna uwezekano wa yeye kuwania muhula wa tatu, licha ya Katiba ya Marekani kupiga marufuku jambo hilo kupitia Marekebisho ya 22. Katika mahojiano na NBCNews, Rais huyo hakutaka kufuta uwezekano wa kuwania tena Urais baada ya kumaliza mihula miwili, akidai kuwa kuna njia za kufanya hilo kutokea. Alisisitiza kuwa "hakuwa anatania," jambo ambalo limeibua hofu miongoni mwa Wachambuzi wa siasa na Wanaharakati wa demokrasia Nchini humo. Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, Rais haruhusiwi kutawala kwa zaidi ya mihula miwili ya miaka minne minne. Marekebisho ya 22 yaliwekwa ili kuzuia Mtu mmoja kuwa na mamlaka ya muda mrefu kama ilivyokuwa kwa Franklin D. Roosevelt, ambaye altawala kwa zaidi ya mihula miwili kabla ya marekebisho hayo kuidhinishwa mwaka 1951. Kauli ya Trump imeibua maswali kuhusu mbinu anazoweza kutumia kutafuta muhula wa tatu. Wachambuzi wa sheria wanabainisha kuwa ili hilo litokee, ama katiba ibadilishwe rasmi kwa marekebisho mapya, au ipatikane tafsiri mpya ya kisheria inayomruhusu kugombea tena. Hata hivyo, mchakato wa kubadili katiba ni mgumu na unahitaji ridhaa ya Bunge pamoja na Majimbo mengi ya Marekani. Baadhi ya Wafuasi wa Donald Trump wameunga mkono kauli yake, wakidai kuwa anastahili muda zaidi wa kuongoza Nchi. Hata hivyo, Wakosoaji wake wanasema kuwa hatua yoyote ya kupindua Marekebisho ya 22 inaweza kuwa tishio kwa demokrasia ya Marekani na kuweka msingi wa uongozi wa kiimla.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·158 Просмотры
Расширенные страницы