• Binti wa Kim Jong Un aonekana kwenye Gwaride la Kijeshi, azua maswali kuhusu uongozi wa baadaye.

    Binti wa Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, ameonekana hadharani wakati wa gwaride la kijeshi lililofanyika katika Mji Mkuu wa Pyongyang, jambo ambalo limeongeza uvumi kuwa huenda anaandaliwa kuwa Mrithi wa baadaye wa uongozi wa taifa hilo.

    Msichana huyo kijana anayejulikana kwa jina la Ju Ae alihudhuria tukio hilo kubwa lililofanyika kuhitimisha Kongamano la Tisa la Chama Tawala cha Workers' Party of Korea, tukio ambalo ni mojawapo ya muhimu zaidi katika ratiba ya kisiasa ya North Korea.

    Wachambuzi wa siasa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mkutano huo wakitarajia kuona mabadiliko ya sera au ishara za mwelekeo wa uongozi wa baadaye.

    Picha iliyochapishwa na shirika la habari la serikali, KCNA, ilimuonesha Ju Ae akiwa amesimama karibu na Baba yake pamoja na viongozi waandamizi wa kijeshi huku wakipongeza gwaride hilo.

    Ingawa KCNA haikutoa maelezo ya wazi kuhusu jukumu la Binti huyo katika shughuli za gwaride, uwepo wake unaonekana kuongeza mjadala kuhusu suala la urithi wa uongozi katika mfumo wa kisiasa unaotegemea uhalali wa kifamilia wa nasaba ya Kim.

    Kwa sasa, hakuna tamko rasmi lililotolewa kuhusu nafasi yake ya baadaye, lakini kuonekana kwake mara kwa mara katika matukio ya kitaifa kunaendelea kuchukuliwa na wengi kama ishara yenye uzito wa kisiasa.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Binti wa Kim Jong Un aonekana kwenye Gwaride la Kijeshi, azua maswali kuhusu uongozi wa baadaye. Binti wa Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, ameonekana hadharani wakati wa gwaride la kijeshi lililofanyika katika Mji Mkuu wa Pyongyang, jambo ambalo limeongeza uvumi kuwa huenda anaandaliwa kuwa Mrithi wa baadaye wa uongozi wa taifa hilo. Msichana huyo kijana anayejulikana kwa jina la Ju Ae alihudhuria tukio hilo kubwa lililofanyika kuhitimisha Kongamano la Tisa la Chama Tawala cha Workers' Party of Korea, tukio ambalo ni mojawapo ya muhimu zaidi katika ratiba ya kisiasa ya North Korea. Wachambuzi wa siasa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mkutano huo wakitarajia kuona mabadiliko ya sera au ishara za mwelekeo wa uongozi wa baadaye. Picha iliyochapishwa na shirika la habari la serikali, KCNA, ilimuonesha Ju Ae akiwa amesimama karibu na Baba yake pamoja na viongozi waandamizi wa kijeshi huku wakipongeza gwaride hilo. Ingawa KCNA haikutoa maelezo ya wazi kuhusu jukumu la Binti huyo katika shughuli za gwaride, uwepo wake unaonekana kuongeza mjadala kuhusu suala la urithi wa uongozi katika mfumo wa kisiasa unaotegemea uhalali wa kifamilia wa nasaba ya Kim. Kwa sasa, hakuna tamko rasmi lililotolewa kuhusu nafasi yake ya baadaye, lakini kuonekana kwake mara kwa mara katika matukio ya kitaifa kunaendelea kuchukuliwa na wengi kama ishara yenye uzito wa kisiasa. Toa maoni yako #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 107 مشاهدة
  • Binti wa Kim Jong Un aonekana kwenye Gwaride la Kijeshi, azua maswali kuhusu uongozi wa baadaye.

    Binti wa Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, ameonekana hadharani wakati wa gwaride la kijeshi lililofanyika katika Mji Mkuu wa Pyongyang, jambo ambalo limeongeza uvumi kuwa huenda anaandaliwa kuwa Mrithi wa baadaye wa uongozi wa taifa hilo.

    Msichana huyo kijana anayejulikana kwa jina la Ju Ae alihudhuria tukio hilo kubwa lililofanyika kuhitimisha Kongamano la Tisa la Chama Tawala cha Workers' Party of Korea, tukio ambalo ni mojawapo ya muhimu zaidi katika ratiba ya kisiasa ya North Korea.

    Wachambuzi wa siasa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mkutano huo wakitarajia kuona mabadiliko ya sera au ishara za mwelekeo wa uongozi wa baadaye.

    Picha iliyochapishwa na shirika la habari la serikali, KCNA, ilimuonesha Ju Ae akiwa amesimama karibu na Baba yake pamoja na viongozi waandamizi wa kijeshi huku wakipongeza gwaride hilo.

    Ingawa KCNA haikutoa maelezo ya wazi kuhusu jukumu la Binti huyo katika shughuli za gwaride, uwepo wake unaonekana kuongeza mjadala kuhusu suala la urithi wa uongozi katika mfumo wa kisiasa unaotegemea uhalali wa kifamilia wa nasaba ya Kim.

    Kwa sasa, hakuna tamko rasmi lililotolewa kuhusu nafasi yake ya baadaye, lakini kuonekana kwake mara kwa mara katika matukio ya kitaifa kunaendelea kuchukuliwa na wengi kama ishara yenye uzito wa kisiasa.
    Binti wa Kim Jong Un aonekana kwenye Gwaride la Kijeshi, azua maswali kuhusu uongozi wa baadaye. Binti wa Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, ameonekana hadharani wakati wa gwaride la kijeshi lililofanyika katika Mji Mkuu wa Pyongyang, jambo ambalo limeongeza uvumi kuwa huenda anaandaliwa kuwa Mrithi wa baadaye wa uongozi wa taifa hilo. Msichana huyo kijana anayejulikana kwa jina la Ju Ae alihudhuria tukio hilo kubwa lililofanyika kuhitimisha Kongamano la Tisa la Chama Tawala cha Workers' Party of Korea, tukio ambalo ni mojawapo ya muhimu zaidi katika ratiba ya kisiasa ya North Korea. Wachambuzi wa siasa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mkutano huo wakitarajia kuona mabadiliko ya sera au ishara za mwelekeo wa uongozi wa baadaye. Picha iliyochapishwa na shirika la habari la serikali, KCNA, ilimuonesha Ju Ae akiwa amesimama karibu na Baba yake pamoja na viongozi waandamizi wa kijeshi huku wakipongeza gwaride hilo. Ingawa KCNA haikutoa maelezo ya wazi kuhusu jukumu la Binti huyo katika shughuli za gwaride, uwepo wake unaonekana kuongeza mjadala kuhusu suala la urithi wa uongozi katika mfumo wa kisiasa unaotegemea uhalali wa kifamilia wa nasaba ya Kim. Kwa sasa, hakuna tamko rasmi lililotolewa kuhusu nafasi yake ya baadaye, lakini kuonekana kwake mara kwa mara katika matukio ya kitaifa kunaendelea kuchukuliwa na wengi kama ishara yenye uzito wa kisiasa.
    0 التعليقات 0 المشاركات 107 مشاهدة
  • PSG ilitoa Ofa ya €250 milioni kwa Lamine Yamal, Barcelona wakataa - Laporta afunguka.

    Rais wa klabu ya FC Barcelona, Joan Laporta, ameweka wazi kuwa klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) iliwahi kuwasilisha ofa nono ya euro milioni 250 kwa ajili ya kinda nyota Lamine Yamal lakini Barca waliikataa bila kusita.

    Akizungumza kuhusu tukio hilo, Laporta amesema ofa hiyo iliwasilishwa takribani miaka miwili iliyopita wakati Yamal akiwa na umri wa miaka 17 pekee.

    “Lamine alikuwa na miaka 17, miaka miwili iliyopita… PSG walituma pendekezo la euro milioni 250 na tulisema hapana. Nakumbuka baadhi ya watu walifikiri tulikuwa tumepoteza akili,” ameeleza Laporta.

    Kwa mujibu wa Kiongozi huyo wa Barcelona, uamuzi wa kuikataa ofa hiyo haukuwa wa kifedha bali wa kimkakati na kihistoria. Klabu hiyo inaamini Yamal ni sehemu ya mradi wa muda mrefu wa kurejesha enzi za mafanikio Camp Nou.

    “Kwa sisi, amekuwa asiyeuzwa. Hagusiki,” alisisitiza Laporta.

    Kwa kuzingatia ukubwa wa ofa hiyo, wengi walihoji kama Barcelona walipaswa kukubali kiasi hicho kikubwa cha fedha, hasa katika kipindi ambacho klabu hiyo ilikuwa inapitia changamoto za kifedha. Hata hivyo, maendeleo ya haraka ya Yamal ndani ya kikosi cha kwanza na mchango wake katika mafanikio ya timu yameanza kuhalalisha msimamo wa uongozi.

    Yamal ameonekana kuwa moja ya vipaji adimu vilivyotoka "Akademi" ya La Masia, akionesha utulivu, ubunifu na ujasiri mkubwa licha ya umri wake mdogo.

    Kauli ya Laporta inaashiria wazi kwamba Barcelona haioni thamani ya Yamal kwa mizani ya fedha pekee. Kwao, ni Mrithi wa kizazi kipya cha Nyota wa klabu hiyo, Mchezaji wa kujengwa kuzunguka mradi wa baadaye.

    Katika soko la sasa la uhamisho, euro milioni 250 ni kiwango kinachoweza kubadilisha historia ya klabu yoyote. Lakini kwa Barcelona, Lamine Yamal si bidhaa ya kuuzwa ni alama ya mustakabali wao.

    Toa maoni yako
    #Sports
    PSG ilitoa Ofa ya €250 milioni kwa Lamine Yamal, Barcelona wakataa - Laporta afunguka. Rais wa klabu ya FC Barcelona, Joan Laporta, ameweka wazi kuwa klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) iliwahi kuwasilisha ofa nono ya euro milioni 250 kwa ajili ya kinda nyota Lamine Yamal lakini Barca waliikataa bila kusita. Akizungumza kuhusu tukio hilo, Laporta amesema ofa hiyo iliwasilishwa takribani miaka miwili iliyopita wakati Yamal akiwa na umri wa miaka 17 pekee. “Lamine alikuwa na miaka 17, miaka miwili iliyopita… PSG walituma pendekezo la euro milioni 250 na tulisema hapana. Nakumbuka baadhi ya watu walifikiri tulikuwa tumepoteza akili,” ameeleza Laporta. Kwa mujibu wa Kiongozi huyo wa Barcelona, uamuzi wa kuikataa ofa hiyo haukuwa wa kifedha bali wa kimkakati na kihistoria. Klabu hiyo inaamini Yamal ni sehemu ya mradi wa muda mrefu wa kurejesha enzi za mafanikio Camp Nou. “Kwa sisi, amekuwa asiyeuzwa. Hagusiki,” alisisitiza Laporta. Kwa kuzingatia ukubwa wa ofa hiyo, wengi walihoji kama Barcelona walipaswa kukubali kiasi hicho kikubwa cha fedha, hasa katika kipindi ambacho klabu hiyo ilikuwa inapitia changamoto za kifedha. Hata hivyo, maendeleo ya haraka ya Yamal ndani ya kikosi cha kwanza na mchango wake katika mafanikio ya timu yameanza kuhalalisha msimamo wa uongozi. Yamal ameonekana kuwa moja ya vipaji adimu vilivyotoka "Akademi" ya La Masia, akionesha utulivu, ubunifu na ujasiri mkubwa licha ya umri wake mdogo. Kauli ya Laporta inaashiria wazi kwamba Barcelona haioni thamani ya Yamal kwa mizani ya fedha pekee. Kwao, ni Mrithi wa kizazi kipya cha Nyota wa klabu hiyo, Mchezaji wa kujengwa kuzunguka mradi wa baadaye. Katika soko la sasa la uhamisho, euro milioni 250 ni kiwango kinachoweza kubadilisha historia ya klabu yoyote. Lakini kwa Barcelona, Lamine Yamal si bidhaa ya kuuzwa ni alama ya mustakabali wao. Toa maoni yako #Sports
    0 التعليقات 0 المشاركات 201 مشاهدة
  • Kesi ya uhaini dhidi ya Tundu Lissu yaahirishwa tena Mahakamani.

    Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, imeahirishwa hadi kesho baada ya Mahakama kushindwa kuendelea na usikilizwaji wake kufuatia mjadala mzito wa kisheria. Chanzo cha mvutano huo ni notisi iliyowasilishwa na upande wa Jamhuri ikieleza nia ya kuleta ushahidi mpya Mahakamani.

    Jamhuri: Notisi Iliwasilishwa kwa mujibu wa sheria.

    Upande wa Mashtaka umeeleza kuwa uliwasilisha notisi hiyo tarehe 20 Februari 2026 kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Wakili wa Serikali alidai kuwa notisi hiyo ina maudhui ya ushahidi unaokusudiwa kuongezwa kama nyongeza ya ushahidi uliowasilishwa awali na ACP Amini Mahamba.

    Kwa hoja ya Jamhuri:

    - Kifungu cha 308(1) kinatoa mwongozo wa kuwasilisha ushahidi wa ziada.

    - Kifungu cha 308(4) kinahusu ushahidi uliopo katika jalada la kesi.

    - ACP Mahamba alikuwa Mchunguzi wa matukio yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025.

    Kwa mtazamo wa Jamhuri, ushahidi huo ni wa kuimarisha hoja zao na unafuata taratibu za kisheria.

    Lissu apinga: “Si shahidi mpya”

    Hata hivyo, Tundu Lissu alipinga vikali notisi hiyo akisema haikidhi matakwa ya kisheria.

    Kwa mujibu wa hoja yake:

    - Kifungu cha 308(1) kinahusu shahidi mpya ambaye ushahidi wake haukusomwa wakati wa hatua ya awali (committal proceedings).

    - Upande wa Jamhuri hauleti shahidi mpya, bali unataka kuongeza ushahidi wa shahidi ambaye tayari alishatoa ushahidi wake.

    - Notisi hiyo haimtaji shahidi mpya kama sheria inavyotaka.

    Lissu alisisitiza kuwa hatua hiyo ni kinyume cha utaratibu wa kisheria na inalenga kupanua wigo wa kesi nje ya hati ya mashtaka.

    Aidha, Lissu alieleza kuwa maelezo yanayohusu matukio ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 hayamo kwenye hati ya mashtaka.

    Alidai kuwa:

    - Serikali inaonekana kutaka kubadilisha hati ya mashtaka bila kufuata utaratibu.

    - Wakati wa matukio hayo, yeye alikuwa mahabusu kwa miezi sita na nusu.

    - Kuruhusu notisi hiyo ni sawa na kufungua “sanduku la Pandora” kwa kuingiza masuala mapya yasiyo kwenye mashtaka ya awali.

    Kutokana na mvutano huo wa kisheria, Mahakama ililazimika kuahirisha kesi hiyo hadi kesho ili kutoa mwongozo au uamuzi kuhusu uhalali wa notisi ya Jamhuri.

    Uamuzi utakaotolewa unaweza kuwa na athari kubwa katika mwelekeo wa kesi hiyo, hasa kuhusu tafsiri na matumizi ya kifungu cha 308 katika mazingira ya ushahidi wa ziada.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Kesi ya uhaini dhidi ya Tundu Lissu yaahirishwa tena Mahakamani. Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, imeahirishwa hadi kesho baada ya Mahakama kushindwa kuendelea na usikilizwaji wake kufuatia mjadala mzito wa kisheria. Chanzo cha mvutano huo ni notisi iliyowasilishwa na upande wa Jamhuri ikieleza nia ya kuleta ushahidi mpya Mahakamani. Jamhuri: Notisi Iliwasilishwa kwa mujibu wa sheria. Upande wa Mashtaka umeeleza kuwa uliwasilisha notisi hiyo tarehe 20 Februari 2026 kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Wakili wa Serikali alidai kuwa notisi hiyo ina maudhui ya ushahidi unaokusudiwa kuongezwa kama nyongeza ya ushahidi uliowasilishwa awali na ACP Amini Mahamba. Kwa hoja ya Jamhuri: - Kifungu cha 308(1) kinatoa mwongozo wa kuwasilisha ushahidi wa ziada. - Kifungu cha 308(4) kinahusu ushahidi uliopo katika jalada la kesi. - ACP Mahamba alikuwa Mchunguzi wa matukio yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025. Kwa mtazamo wa Jamhuri, ushahidi huo ni wa kuimarisha hoja zao na unafuata taratibu za kisheria. Lissu apinga: “Si shahidi mpya” Hata hivyo, Tundu Lissu alipinga vikali notisi hiyo akisema haikidhi matakwa ya kisheria. Kwa mujibu wa hoja yake: - Kifungu cha 308(1) kinahusu shahidi mpya ambaye ushahidi wake haukusomwa wakati wa hatua ya awali (committal proceedings). - Upande wa Jamhuri hauleti shahidi mpya, bali unataka kuongeza ushahidi wa shahidi ambaye tayari alishatoa ushahidi wake. - Notisi hiyo haimtaji shahidi mpya kama sheria inavyotaka. Lissu alisisitiza kuwa hatua hiyo ni kinyume cha utaratibu wa kisheria na inalenga kupanua wigo wa kesi nje ya hati ya mashtaka. Aidha, Lissu alieleza kuwa maelezo yanayohusu matukio ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 hayamo kwenye hati ya mashtaka. Alidai kuwa: - Serikali inaonekana kutaka kubadilisha hati ya mashtaka bila kufuata utaratibu. - Wakati wa matukio hayo, yeye alikuwa mahabusu kwa miezi sita na nusu. - Kuruhusu notisi hiyo ni sawa na kufungua “sanduku la Pandora” kwa kuingiza masuala mapya yasiyo kwenye mashtaka ya awali. Kutokana na mvutano huo wa kisheria, Mahakama ililazimika kuahirisha kesi hiyo hadi kesho ili kutoa mwongozo au uamuzi kuhusu uhalali wa notisi ya Jamhuri. Uamuzi utakaotolewa unaweza kuwa na athari kubwa katika mwelekeo wa kesi hiyo, hasa kuhusu tafsiri na matumizi ya kifungu cha 308 katika mazingira ya ushahidi wa ziada. Toa maoni yako #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 151 مشاهدة
  • Familia ya Kiongozi wa upinzani wa Uganda Bobi Wine yafunguka kukimbia Nchi kufuatia matukio ya siasa na usalama.

    Katika taarifa iliyotolewa, Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kama Bobi Wine, amethibitisha mbele ya Wakaguzi wa haki za binadamu Mjini Geneva kwamba Mke wake, Barbie Itungo Kyagulanyi, na Watoto wao wametoka Uganda kwa sababu za hofu ya maisha yao kufuatia hali tete inayojitokeza nchini mwao baada ya uchaguzi wa Rais.

    Katika hotuba yake kupitia video mbele ya Geneva Summit for Human Rights and Democracy, Bobi Wine alisema wazi: “Mke wangu na Watoto walilazimika kukimbia nchi kwa hofu ya maisha yao.” - Bobi Wine.

    Alifafanua kuwa usalama wa familia yake uliathirika sana kutokana na operesheni za vikosi vya usalama zilizoendelea mara tu baada ya uchaguzi wa 15 Januari 2026, ambapo serikali ilitangaza ushindi wa Rais Yoweri Museveni ambayo Bobi Wine ameipinga kwa madai ya udanganyifu wa kura na ukandamizaji wa upinzani.

    Bobi Wine pia alidai kwamba vikosi vya usalama: “Vilivamia nyumba yangu, vikamtesa Mke wangu, kumfanya asiwe na chaguo ila kuondoka na Watoto wakiwa nje ya nchi.” amesema

    Habari kwamba familia yake imeondoka Uganda na si tu kutoroka nyumba yao ya Magere imetolewa mara tu baada ya miezi ya mvutano mkali, ikiwa ni pamoja na madai ya mashambulizi, ulinzi mkali wa nyumba yao na vitisho vilivyowekwa na baadhi ya Afisa wa usalama.

    Katika maneno yake Mjini Geneva, Bobi Wine pia alijumuisha ombi kwa Jumuiya ya kimataifa kuhusu hatua za kulinda haki za binadamu na kuzuia ukandamizaji wa upinzani nchini Uganda.

    Taarifa hii inakuja katika wakati ambapo Uganda iko chini ya uangalizi wa kimataifa kufuatia ripoti za ghasia, mashambulizi dhidi ya wapinzani wa kisiasa, na madai ya upendeleo wa vyombo vya usalama kuelekea chama tawala.

    Kwa sasa, bado haijafahamika kwa umma ni nchi gani hasa Barbie Itungo Kyagulanyi na Watoto hao wamekwenda, ila uamuzi wao wa kukimbia unachukuliwa kama hatua ya kulinda usalama wa familia katika mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Uganda.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Familia ya Kiongozi wa upinzani wa Uganda Bobi Wine yafunguka kukimbia Nchi kufuatia matukio ya siasa na usalama. Katika taarifa iliyotolewa, Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kama Bobi Wine, amethibitisha mbele ya Wakaguzi wa haki za binadamu Mjini Geneva kwamba Mke wake, Barbie Itungo Kyagulanyi, na Watoto wao wametoka Uganda kwa sababu za hofu ya maisha yao kufuatia hali tete inayojitokeza nchini mwao baada ya uchaguzi wa Rais. Katika hotuba yake kupitia video mbele ya Geneva Summit for Human Rights and Democracy, Bobi Wine alisema wazi: “Mke wangu na Watoto walilazimika kukimbia nchi kwa hofu ya maisha yao.” - Bobi Wine. Alifafanua kuwa usalama wa familia yake uliathirika sana kutokana na operesheni za vikosi vya usalama zilizoendelea mara tu baada ya uchaguzi wa 15 Januari 2026, ambapo serikali ilitangaza ushindi wa Rais Yoweri Museveni ambayo Bobi Wine ameipinga kwa madai ya udanganyifu wa kura na ukandamizaji wa upinzani. Bobi Wine pia alidai kwamba vikosi vya usalama: “Vilivamia nyumba yangu, vikamtesa Mke wangu, kumfanya asiwe na chaguo ila kuondoka na Watoto wakiwa nje ya nchi.” amesema Habari kwamba familia yake imeondoka Uganda na si tu kutoroka nyumba yao ya Magere imetolewa mara tu baada ya miezi ya mvutano mkali, ikiwa ni pamoja na madai ya mashambulizi, ulinzi mkali wa nyumba yao na vitisho vilivyowekwa na baadhi ya Afisa wa usalama. Katika maneno yake Mjini Geneva, Bobi Wine pia alijumuisha ombi kwa Jumuiya ya kimataifa kuhusu hatua za kulinda haki za binadamu na kuzuia ukandamizaji wa upinzani nchini Uganda. Taarifa hii inakuja katika wakati ambapo Uganda iko chini ya uangalizi wa kimataifa kufuatia ripoti za ghasia, mashambulizi dhidi ya wapinzani wa kisiasa, na madai ya upendeleo wa vyombo vya usalama kuelekea chama tawala. Kwa sasa, bado haijafahamika kwa umma ni nchi gani hasa Barbie Itungo Kyagulanyi na Watoto hao wamekwenda, ila uamuzi wao wa kukimbia unachukuliwa kama hatua ya kulinda usalama wa familia katika mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Uganda. Toa maoni yako #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 359 مشاهدة
  • Facebook yatangaza rasmi kufunga App ya Messenger kuanzia April.

    Kampuni ya teknolojia ya META imetangaza rasmi kuwa itafunga programu yake ya ujumbe, Messenger, kuanzia mwezi April mwaka huu.

    Kwa mujibu wa tangazo hilo, hatua za kwanza za mabadiliko zitaanza kwa Watumiaji wa kompyuta za Mac na Windows, ambapo toleo la desktop la Messenger litafungwa rasmi. Kampuni hiyo imeeleza pia kuwa mwakani inapanga kuiondoa kabisa Messenger kama app huru na kubaki na Facebook kama jukwaa moja lenye sehemu ya ujumbe (messages) ndani yake.

    Messenger haikuanza kwa jina hilo. Mwaka 2008, huduma hiyo ilizinduliwa kwa jina la Facebook Chat, ikiwa ni sehemu ya mawasiliano ya moja kwa moja ndani ya Facebook.

    Mwaka 2011, huduma hiyo iliboreshwa na kubadilishwa jina rasmi kuwa Messenger, ikiwa ni app inayojitegemea kwa simu na baadaye kwa kompyuta.

    Katika kipindi cha ukuaji wake, Messenger ilitumika kama silaha ya ushindani dhidi ya majukwaa mengine makubwa ya mawasiliano kama:

    - WhatsApp
    - iMessage
    - WeChat
    - Skype

    Lengo lilikuwa ni kuimarisha mawasiliano ya Watumiaji wa Facebook bila kulazimika kuondoka ndani ya mfumo wa kampuni hiyo.

    Baada ya kufutwa kwa Messenger kama app ya pekee, Facebook itabaki kama mtandao mmoja wenye sehemu ya ujumbe ndani yake. Hii ina maana kuwa Watumiaji wataendelea kutuma na kupokea meseji, lakini kupitia mfumo wa moja kwa moja ndani ya Facebook badala ya app tofauti.

    Hatua hii inaashiria mabadiliko makubwa katika mkakati wa kidijitali wa Facebook, hasa katika kipindi ambacho kampuni nyingi za teknolojia zinaelekea kurahisisha huduma zao na kupunguza gharama za uendeshaji.

    Zaidi ya muongo mmoja baada ya kuzinduliwa kwake, Messenger sasa inaingia rasmi katika historia kama app iliyowahi kuwa moja ya majukwaa makubwa ya mawasiliano duniani.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Facebook yatangaza rasmi kufunga App ya Messenger kuanzia April. Kampuni ya teknolojia ya META imetangaza rasmi kuwa itafunga programu yake ya ujumbe, Messenger, kuanzia mwezi April mwaka huu. Kwa mujibu wa tangazo hilo, hatua za kwanza za mabadiliko zitaanza kwa Watumiaji wa kompyuta za Mac na Windows, ambapo toleo la desktop la Messenger litafungwa rasmi. Kampuni hiyo imeeleza pia kuwa mwakani inapanga kuiondoa kabisa Messenger kama app huru na kubaki na Facebook kama jukwaa moja lenye sehemu ya ujumbe (messages) ndani yake. Messenger haikuanza kwa jina hilo. Mwaka 2008, huduma hiyo ilizinduliwa kwa jina la Facebook Chat, ikiwa ni sehemu ya mawasiliano ya moja kwa moja ndani ya Facebook. Mwaka 2011, huduma hiyo iliboreshwa na kubadilishwa jina rasmi kuwa Messenger, ikiwa ni app inayojitegemea kwa simu na baadaye kwa kompyuta. Katika kipindi cha ukuaji wake, Messenger ilitumika kama silaha ya ushindani dhidi ya majukwaa mengine makubwa ya mawasiliano kama: - WhatsApp - iMessage - WeChat - Skype Lengo lilikuwa ni kuimarisha mawasiliano ya Watumiaji wa Facebook bila kulazimika kuondoka ndani ya mfumo wa kampuni hiyo. Baada ya kufutwa kwa Messenger kama app ya pekee, Facebook itabaki kama mtandao mmoja wenye sehemu ya ujumbe ndani yake. Hii ina maana kuwa Watumiaji wataendelea kutuma na kupokea meseji, lakini kupitia mfumo wa moja kwa moja ndani ya Facebook badala ya app tofauti. Hatua hii inaashiria mabadiliko makubwa katika mkakati wa kidijitali wa Facebook, hasa katika kipindi ambacho kampuni nyingi za teknolojia zinaelekea kurahisisha huduma zao na kupunguza gharama za uendeshaji. Zaidi ya muongo mmoja baada ya kuzinduliwa kwake, Messenger sasa inaingia rasmi katika historia kama app iliyowahi kuwa moja ya majukwaa makubwa ya mawasiliano duniani. Toa maoni yako #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 266 مشاهدة
  • Trump aahidi kufungua mafaili ya siri kuhusu “Aliens” baada ya kauli ya Obama.

    Mjadala kuhusu uwepo wa viumbe wa angani umechukua sura mpya baada ya kauli ya aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama, na kufuatiwa na ahadi ya Rais wa sasa, Donald Trump, ya kuweka wazi mafaili ya siri yanayohusiana na suala hilo.

    Katika maelezo yake ya hivi karibuni, Obama aligusia uwepo wa viumbe wa angani, akionesha kuwa suala hilo si la kubezwa. Kauli hiyo imeamsha hisia na mijadala mikubwa miongoni mwa Wananchi na Wachambuzi wa masuala ya usalama na sayansi.

    Ingawa hakutoa ushahidi wa moja kwa moja hadharani, kauli yake imechukuliwa kama ishara kwamba kuna taarifa ambazo bado hazijawekwa wazi kwa umma.

    Kupitia ujumbe wake rasmi, Trump ameahidi kuchukua hatua. Katika ujumbe huo ameandika: “Kutokana na hamasa kubwa iliyooneshwa na Wananchi juu ya kutaka kutambua ukweli kuhusu Aliens, nimezielekeza wizara na taasisi husika kuanza mchakato wa kubaini na kutoa hadharani nyaraka za serikali zinazohusiana na maisha ya viumbe wa anga (Aliens), matukio ya vitu visivyojulikana angani (UAP), vitu vinavyoruka visivyojulikana (UFO), pamoja na taarifa nyingine zote zinazohusiana na masuala haya ambayo ni magumu lakini ya kuvutia na muhimu sana.”

    Kauli hiyo imezua maswali mengi: Je, serikali ya Marekani iko tayari kufungua mafaili yote ya siri? Au kutakuwa na taarifa chache tu zitakazowekwa wazi kwa umma?

    Katika miaka ya karibuni, taasisi za ulinzi za Marekani zimekiri kuchunguza matukio ya UAP (Unidentified Aerial Phenomena) na UFO (Unidentified Flying Objects). Baadhi ya video na taarifa tayari zimewahi kutolewa, lakini bado kuna madai kwamba sehemu kubwa ya taarifa hizo imebaki kuwa siri ya serikali.

    Ahadi ya Trump inaweza kuwa hatua mpya katika historia ya uwazi wa taarifa za usalama wa taifa au inaweza kuwa mkakati wa kisiasa unaolenga kuvutia umma.

    Je, Siri zitafunguliwa Kweli?

    Kihistoria, masuala yanayohusiana na usalama wa taifa yamekuwa yakilindwa kwa uangalifu mkubwa. Hivyo, hata kama mchakato utaanza, Wachambuzi wanaamini kuwa kuna uwezekano wa kuwepo kwa uchujaji wa taarifa kabla ya kutolewa hadharani.

    Kwa sasa, macho ya dunia yanaelekezwa Washington kusubiri kama ahadi hiyo itatekelezwa kikamilifu.

    Unadhani Serikali ya Marekani itatoa kweli siri hizi zote? Na wewe binafsi, unaamini kweli kuna viumbe wa angani wanaoishi nje ya sayari yetu?

    Toa maoni yako
    #Habari
    Trump aahidi kufungua mafaili ya siri kuhusu “Aliens” baada ya kauli ya Obama. Mjadala kuhusu uwepo wa viumbe wa angani umechukua sura mpya baada ya kauli ya aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama, na kufuatiwa na ahadi ya Rais wa sasa, Donald Trump, ya kuweka wazi mafaili ya siri yanayohusiana na suala hilo. Katika maelezo yake ya hivi karibuni, Obama aligusia uwepo wa viumbe wa angani, akionesha kuwa suala hilo si la kubezwa. Kauli hiyo imeamsha hisia na mijadala mikubwa miongoni mwa Wananchi na Wachambuzi wa masuala ya usalama na sayansi. Ingawa hakutoa ushahidi wa moja kwa moja hadharani, kauli yake imechukuliwa kama ishara kwamba kuna taarifa ambazo bado hazijawekwa wazi kwa umma. Kupitia ujumbe wake rasmi, Trump ameahidi kuchukua hatua. Katika ujumbe huo ameandika: “Kutokana na hamasa kubwa iliyooneshwa na Wananchi juu ya kutaka kutambua ukweli kuhusu Aliens, nimezielekeza wizara na taasisi husika kuanza mchakato wa kubaini na kutoa hadharani nyaraka za serikali zinazohusiana na maisha ya viumbe wa anga (Aliens), matukio ya vitu visivyojulikana angani (UAP), vitu vinavyoruka visivyojulikana (UFO), pamoja na taarifa nyingine zote zinazohusiana na masuala haya ambayo ni magumu lakini ya kuvutia na muhimu sana.” Kauli hiyo imezua maswali mengi: Je, serikali ya Marekani iko tayari kufungua mafaili yote ya siri? Au kutakuwa na taarifa chache tu zitakazowekwa wazi kwa umma? Katika miaka ya karibuni, taasisi za ulinzi za Marekani zimekiri kuchunguza matukio ya UAP (Unidentified Aerial Phenomena) na UFO (Unidentified Flying Objects). Baadhi ya video na taarifa tayari zimewahi kutolewa, lakini bado kuna madai kwamba sehemu kubwa ya taarifa hizo imebaki kuwa siri ya serikali. Ahadi ya Trump inaweza kuwa hatua mpya katika historia ya uwazi wa taarifa za usalama wa taifa au inaweza kuwa mkakati wa kisiasa unaolenga kuvutia umma. Je, Siri zitafunguliwa Kweli? Kihistoria, masuala yanayohusiana na usalama wa taifa yamekuwa yakilindwa kwa uangalifu mkubwa. Hivyo, hata kama mchakato utaanza, Wachambuzi wanaamini kuwa kuna uwezekano wa kuwepo kwa uchujaji wa taarifa kabla ya kutolewa hadharani. Kwa sasa, macho ya dunia yanaelekezwa Washington kusubiri kama ahadi hiyo itatekelezwa kikamilifu. Unadhani Serikali ya Marekani itatoa kweli siri hizi zote? Na wewe binafsi, unaamini kweli kuna viumbe wa angani wanaoishi nje ya sayari yetu? Toa maoni yako #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 330 مشاهدة
  • Vatican yakataa mwaliko wa Trump kujiunga na “Bodi ya Amani”.

    Mvutano mpya wa kidiplomasia umeibuka baada ya Vatican kukataa rasmi mwaliko wa Rais wa Marekani kujiunga na kile kilichoelezwa kama “Bodi ya Amani”, mpango ambao umekuwa ukizua mjadala mkali katika duru za kimataifa.

    Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Katibu wa Jimbo la Vatican, Cardinal Pietro Parolin, Taasisi ya Kiti Kitakatifu haitashiriki katika mpango huo, ikitaja sababu za kimsingi zinazohusiana na mwelekeo na uhalali wa jukwaa hilo.

    Katika kauli yake, Kardinali Parolin alisema: “Kuna masuala nyeti na hoja ambazo zinatuacha katika mshangao mkubwa.”

    Alisisitiza kuwa masuala ya migogoro ya kimataifa, ikiwemo hali ya Gaza, yanapaswa kushughulikiwa ndani ya mfumo wa kimataifa uliopo badala ya kuanzishwa kwa chombo mbadala kinachoongozwa na taifa moja.

    Kwa mujibu wa Vatican,
    “Migogoro ya kimataifa kama wa Gaza inapaswa kushughulikiwa chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa, si kupitia jukwaa mbadala linaloongozwa na Marekani.”

    Hatua hiyo inatajwa kama pigo la kidiplomasia kwa Ikulu ya White House, hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya washirika wa Magharibi tayari wameonesha kusita au kujiondoa katika mpango huo kabla hata ya mkutano wake wa kwanza mkubwa.

    Uamuzi huo kutoka Vatican ya Pope Leo XIV unaongeza shinikizo kwa mpango wa Rais huyo wa Marekani, ambao ulikusudiwa kuonesha dira mpya ya uongozi wa kimataifa katika kutafuta amani.

    Kwa sasa, jicho la dunia linaelekezwa kuona hatua inayofuata ya Washington, huku Vatican ikiweka msimamo wazi: haitashiriki katika bodi hiyo mpya.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Vatican yakataa mwaliko wa Trump kujiunga na “Bodi ya Amani”. Mvutano mpya wa kidiplomasia umeibuka baada ya Vatican kukataa rasmi mwaliko wa Rais wa Marekani kujiunga na kile kilichoelezwa kama “Bodi ya Amani”, mpango ambao umekuwa ukizua mjadala mkali katika duru za kimataifa. Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Katibu wa Jimbo la Vatican, Cardinal Pietro Parolin, Taasisi ya Kiti Kitakatifu haitashiriki katika mpango huo, ikitaja sababu za kimsingi zinazohusiana na mwelekeo na uhalali wa jukwaa hilo. Katika kauli yake, Kardinali Parolin alisema: “Kuna masuala nyeti na hoja ambazo zinatuacha katika mshangao mkubwa.” Alisisitiza kuwa masuala ya migogoro ya kimataifa, ikiwemo hali ya Gaza, yanapaswa kushughulikiwa ndani ya mfumo wa kimataifa uliopo badala ya kuanzishwa kwa chombo mbadala kinachoongozwa na taifa moja. Kwa mujibu wa Vatican, “Migogoro ya kimataifa kama wa Gaza inapaswa kushughulikiwa chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa, si kupitia jukwaa mbadala linaloongozwa na Marekani.” Hatua hiyo inatajwa kama pigo la kidiplomasia kwa Ikulu ya White House, hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya washirika wa Magharibi tayari wameonesha kusita au kujiondoa katika mpango huo kabla hata ya mkutano wake wa kwanza mkubwa. Uamuzi huo kutoka Vatican ya Pope Leo XIV unaongeza shinikizo kwa mpango wa Rais huyo wa Marekani, ambao ulikusudiwa kuonesha dira mpya ya uongozi wa kimataifa katika kutafuta amani. Kwa sasa, jicho la dunia linaelekezwa kuona hatua inayofuata ya Washington, huku Vatican ikiweka msimamo wazi: haitashiriki katika bodi hiyo mpya. Toa maoni yako #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 330 مشاهدة
  • Iran na Urusi kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi nje ya Bahari ya Oman.

    Iran na Urusi zinatarajiwa kuanza mazoezi ya pamoja ya kijeshi kesho Alhamisi katika maeneo ya nje ya Bahari ya Oman na kaskazini mwa Bahari ya Hindi, hatua inayotafsiriwa kama ishara ya kuimarika kwa ushirikiano wa kiusalama kati ya mataifa hayo mawili.

    Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, tangazo hilo limekuja siku chache baada ya Kikosi Maalum cha Walinzi wa Mapinduzi wa Iran kufanya mazoezi ya kijeshi katika mlango wa bahari wa Hormuz, eneo nyeti linalopitisha sehemu kubwa ya usafirishaji wa mafuta duniani.

    Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran, Hassan Maghsoodloo, ameeleza madhumuni ya mazoezi hayo kwa kusema: “Lengo la mazoezi haya ni kuunda nguvu za pamoja na kuimarisha uratibu wa hatua za pamoja ili kukabiliana na vitisho vinavyoathiri usalama wa majini na usalama wa nchi zetu mbili.”

    Ameongeza kuwa: "Mazoezi haya pia yanalenga kupambana na ugaidi na kuimarisha utulivu katika eneo la kimkakati la bahari.”

    Kauli hiyo inaonesha kuwa Tehran na Moscow zinaangazia zaidi usalama wa bahari na kulinda maslahi yao ya kiuchumi na kijeshi katika njia kuu za usafirishaji wa kimataifa.

    Hatua hizi zinakuja wakati wa mvutano unaoendelea kati ya Marekani na Iran. Washington imetishia hatua za kijeshi dhidi ya Tehran, ikiishutumu kwa kile ilichodai kuwa ni ukiukwaji wa haki za Waandamanaji pamoja na kushindwa kufikia makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia.

    Kwa upande wake, Iran imekuwa ikisisitiza mara kwa mara uwezekano wa kuufunga mlango wa bahari wa Hormuz wakati wa mvutano mkali na Marekani. Hata hivyo, hadi sasa, haijawahi kuchukua hatua ya kulifunga rasmi lango hilo muhimu la kimataifa.

    Mazoezi haya yanaonekana kuwa na ujumbe wa wazi wa kisiasa na kijeshi kuonesha mshikamano wa Iran na Urusi katika kukabiliana na shinikizo la Magharibi, huku yakituma ishara kwa mataifa mengine kuhusu uwezo wao wa pamoja katika kulinda maslahi ya kimkakati katika Bahari ya Hindi na Ghuba ya Oman.

    Wachambuzi wa masuala ya ulinzi wanaona kuwa ushirikiano huu unaweza kuathiri mizania ya nguvu katika eneo hilo, hasa katika kipindi ambacho diplomasia ya nyuklia bado haijafikia muafaka wa kudumu.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Iran na Urusi kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi nje ya Bahari ya Oman. Iran na Urusi zinatarajiwa kuanza mazoezi ya pamoja ya kijeshi kesho Alhamisi katika maeneo ya nje ya Bahari ya Oman na kaskazini mwa Bahari ya Hindi, hatua inayotafsiriwa kama ishara ya kuimarika kwa ushirikiano wa kiusalama kati ya mataifa hayo mawili. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, tangazo hilo limekuja siku chache baada ya Kikosi Maalum cha Walinzi wa Mapinduzi wa Iran kufanya mazoezi ya kijeshi katika mlango wa bahari wa Hormuz, eneo nyeti linalopitisha sehemu kubwa ya usafirishaji wa mafuta duniani. Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran, Hassan Maghsoodloo, ameeleza madhumuni ya mazoezi hayo kwa kusema: “Lengo la mazoezi haya ni kuunda nguvu za pamoja na kuimarisha uratibu wa hatua za pamoja ili kukabiliana na vitisho vinavyoathiri usalama wa majini na usalama wa nchi zetu mbili.” Ameongeza kuwa: "Mazoezi haya pia yanalenga kupambana na ugaidi na kuimarisha utulivu katika eneo la kimkakati la bahari.” Kauli hiyo inaonesha kuwa Tehran na Moscow zinaangazia zaidi usalama wa bahari na kulinda maslahi yao ya kiuchumi na kijeshi katika njia kuu za usafirishaji wa kimataifa. Hatua hizi zinakuja wakati wa mvutano unaoendelea kati ya Marekani na Iran. Washington imetishia hatua za kijeshi dhidi ya Tehran, ikiishutumu kwa kile ilichodai kuwa ni ukiukwaji wa haki za Waandamanaji pamoja na kushindwa kufikia makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia. Kwa upande wake, Iran imekuwa ikisisitiza mara kwa mara uwezekano wa kuufunga mlango wa bahari wa Hormuz wakati wa mvutano mkali na Marekani. Hata hivyo, hadi sasa, haijawahi kuchukua hatua ya kulifunga rasmi lango hilo muhimu la kimataifa. Mazoezi haya yanaonekana kuwa na ujumbe wa wazi wa kisiasa na kijeshi kuonesha mshikamano wa Iran na Urusi katika kukabiliana na shinikizo la Magharibi, huku yakituma ishara kwa mataifa mengine kuhusu uwezo wao wa pamoja katika kulinda maslahi ya kimkakati katika Bahari ya Hindi na Ghuba ya Oman. Wachambuzi wa masuala ya ulinzi wanaona kuwa ushirikiano huu unaweza kuathiri mizania ya nguvu katika eneo hilo, hasa katika kipindi ambacho diplomasia ya nyuklia bado haijafikia muafaka wa kudumu. Toa maoni yako #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 407 مشاهدة
  • Kylian Mbappé amshambulia Gianluca Prestianni kabla ya mechi marudiano huko Bernabéu.

    Mvutano umeibuka kabla ya pambano kubwa linalotarajiwa kupigwa katika dimba la Santiago Bernabéu Stadium, baada ya mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Kylian Mbappé kutoa kauli nzito dhidi ya kijana Gianluca Prestianni kisa sakata lake na Vini.

    Katika mahojiano aliyofanya na TNT Sports Brazil, Mbappé hakusita kueleza msimamo wake kuhusu uwezekano wa Prestianni kucheza katika mechi hiyo muhimu.

    “Natumaini sitamuona Prestianni katika Uwanja wa Bernabéu wiki ijayo… kwa hakika hapaswi kucheza katika Uwanja bora zaidi duniani, hastahili kuwa sehemu ya mchezo huo.”

    Kauli hiyo imezua mjadala mpana miongoni mwa mashabiki wa soka, hasa ikizingatiwa ukubwa wa mechi hiyo inayotarajiwa kuzikutanisha klabu mbili zenye historia kubwa barani Ulaya.

    Mbappé aliendelea kusisitiza kuwa, licha ya matarajio yake ya kushuhudia mechi bora, anaamini Prestianni hapaswi kupewa nafasi ya kushiriki.

    “Nina uhakika utakuwa mchezo wa kuvutia sana, klabu mbili za kihistoria zikiwa Uwanjani, lakini kwa mtazamo wangu Prestianni anapaswa kuwa nje.”

    Kauli yake ya mwisho ndiyo imeongeza moto zaidi katika sakata hilo, akitoa maoni yanayoashiria kuwa anatamani hatua kali zichukuliwe.

    “Haya ni maoni yangu, natumaini atafungiwa.”

    Hadi sasa hakuna tamko rasmi kutoka upande wa Prestianni au klabu yake kujibu kauli hizo. Hata hivyo, presha imeongezeka kuelekea mchezo huo, huku mashabiki wakisubiri kuona kama maneno hayo yatageuka kuwa chachu ya ushindani mkali zaidi Uwanjani.

    Toa maoni yako
    #Sports
    #Habari
    Kylian Mbappé amshambulia Gianluca Prestianni kabla ya mechi marudiano huko Bernabéu. Mvutano umeibuka kabla ya pambano kubwa linalotarajiwa kupigwa katika dimba la Santiago Bernabéu Stadium, baada ya mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Kylian Mbappé kutoa kauli nzito dhidi ya kijana Gianluca Prestianni kisa sakata lake na Vini. Katika mahojiano aliyofanya na TNT Sports Brazil, Mbappé hakusita kueleza msimamo wake kuhusu uwezekano wa Prestianni kucheza katika mechi hiyo muhimu. “Natumaini sitamuona Prestianni katika Uwanja wa Bernabéu wiki ijayo… kwa hakika hapaswi kucheza katika Uwanja bora zaidi duniani, hastahili kuwa sehemu ya mchezo huo.” Kauli hiyo imezua mjadala mpana miongoni mwa mashabiki wa soka, hasa ikizingatiwa ukubwa wa mechi hiyo inayotarajiwa kuzikutanisha klabu mbili zenye historia kubwa barani Ulaya. Mbappé aliendelea kusisitiza kuwa, licha ya matarajio yake ya kushuhudia mechi bora, anaamini Prestianni hapaswi kupewa nafasi ya kushiriki. “Nina uhakika utakuwa mchezo wa kuvutia sana, klabu mbili za kihistoria zikiwa Uwanjani, lakini kwa mtazamo wangu Prestianni anapaswa kuwa nje.” Kauli yake ya mwisho ndiyo imeongeza moto zaidi katika sakata hilo, akitoa maoni yanayoashiria kuwa anatamani hatua kali zichukuliwe. “Haya ni maoni yangu, natumaini atafungiwa.” Hadi sasa hakuna tamko rasmi kutoka upande wa Prestianni au klabu yake kujibu kauli hizo. Hata hivyo, presha imeongezeka kuelekea mchezo huo, huku mashabiki wakisubiri kuona kama maneno hayo yatageuka kuwa chachu ya ushindani mkali zaidi Uwanjani. Toa maoni yako #Sports #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 169 مشاهدة
  • Wakili Craig Kitambala aomba ridhaa ya Fally Ipupa kufungua kesi dhidi ya Mwanahabari Gautier Sey.

    Hatua mpya ya kisheria imeibuka katika tasnia ya burudani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya Wakili Craig Kitambala kuomba ruhusa rasmi kutoka kwa Msanii maarufu Fally Ipupa ili kuanzisha mashitaka dhidi ya Mwanahabari Gautier Sey kwa tuhuma za kumchafulia jina.

    Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Wakili Kitambala anataka kuchukua hatua za kisheria kufuatia kauli na maudhui yaliyotolewa na Gautier Sey ambayo yanaelezwa kuwa yamelenga kumdhalilisha au kumharibia taswira Msanii huyo mbele ya umma.

    Katika maelezo yake, Wakili Kitambala ameeleza kuwa anasubiri kibali cha moja kwa moja kutoka kwa Fally Ipupa kabla ya kuwasilisha rasmi malalamiko Mahakamani.

    “Ninaomba idhini ya Fally Ipupa ili niweze kuanzisha rasmi mashitaka ya kashfa dhidi ya Mwanahabari Gautier Sey,” imeelezwa katika ujumbe unaohusishwa na Wakili huyo.

    Hatua hiyo inakuja wakati mijadala mikali ikiendelea mtandaoni kuhusu uhuru wa vyombo vya habari dhidi ya heshima na hadhi ya watu maarufu. Ikiwa kibali hicho kitatolewa, kesi hiyo inaweza kufungua mjadala mpana kuhusu mipaka ya maoni ya Wanahabari na wajibu wao katika kuripoti habari zinazowahusu watu mashuhuri.

    Kwa sasa, Fally Ipupa hajatoa tamko rasmi hadharani kuhusu iwapo atatoa ruhusa hiyo au la. Vivyo hivyo, Gautier Sey naye hajajibu moja kwa moja tuhuma zinazomkabili.

    Endapo shauri hilo litafunguliwa, linaweza kuwa miongoni mwa kesi zinazovuta hisia kubwa katika tasnia ya muziki na vyombo vya habari nchini DR Congo.

    Toa maoni yako
    #Music
    Wakili Craig Kitambala aomba ridhaa ya Fally Ipupa kufungua kesi dhidi ya Mwanahabari Gautier Sey. Hatua mpya ya kisheria imeibuka katika tasnia ya burudani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya Wakili Craig Kitambala kuomba ruhusa rasmi kutoka kwa Msanii maarufu Fally Ipupa ili kuanzisha mashitaka dhidi ya Mwanahabari Gautier Sey kwa tuhuma za kumchafulia jina. Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Wakili Kitambala anataka kuchukua hatua za kisheria kufuatia kauli na maudhui yaliyotolewa na Gautier Sey ambayo yanaelezwa kuwa yamelenga kumdhalilisha au kumharibia taswira Msanii huyo mbele ya umma. Katika maelezo yake, Wakili Kitambala ameeleza kuwa anasubiri kibali cha moja kwa moja kutoka kwa Fally Ipupa kabla ya kuwasilisha rasmi malalamiko Mahakamani. “Ninaomba idhini ya Fally Ipupa ili niweze kuanzisha rasmi mashitaka ya kashfa dhidi ya Mwanahabari Gautier Sey,” imeelezwa katika ujumbe unaohusishwa na Wakili huyo. Hatua hiyo inakuja wakati mijadala mikali ikiendelea mtandaoni kuhusu uhuru wa vyombo vya habari dhidi ya heshima na hadhi ya watu maarufu. Ikiwa kibali hicho kitatolewa, kesi hiyo inaweza kufungua mjadala mpana kuhusu mipaka ya maoni ya Wanahabari na wajibu wao katika kuripoti habari zinazowahusu watu mashuhuri. Kwa sasa, Fally Ipupa hajatoa tamko rasmi hadharani kuhusu iwapo atatoa ruhusa hiyo au la. Vivyo hivyo, Gautier Sey naye hajajibu moja kwa moja tuhuma zinazomkabili. Endapo shauri hilo litafunguliwa, linaweza kuwa miongoni mwa kesi zinazovuta hisia kubwa katika tasnia ya muziki na vyombo vya habari nchini DR Congo. Toa maoni yako #Music
    0 التعليقات 0 المشاركات 185 مشاهدة
  • Ushirikiano wa RDC – Monaco unakabiliwa na changamoto?

    Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na klabu ya AS Monaco unaweza kuwa kwenye hatari, ikizingatiwa taarifa zilizotolewa na Gazeti la L’Équipe la Nchini Ufaransa.

    Taarifa hizo zinaonyesha kwamba malalamiko ya "kuficha fedha", "kufurushwa fedha za umma" (Wizi) na "ufisadi" yamewasilishwa katika Tume ya Ufilisi wa Kifedha ya Taifa (PNF) mnamo Septemba 2025.

    Malalamiko haya yanahusu mkataba uliosainiwa kati ya Wizara ya Michezo ya RDC na AS Monaco mwezi Juni mwaka jana.

    Baada ya miezi kadhaa ya uchambuzi, PNF imetuma ripoti rasmi kwa mamlaka za Monaco. Hivyo, sasa kesi hiyo ipo mikononi mwa Mahakama ya Dola la Nchi ya Monaco.

    Hali hii inachukua sura mpya katika uhusiano wa michezo na uwekezaji kati ya RDC na Monaco, huku mashabiki na wanasiasa wakilenga kuona matokeo ya kesi hii.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Ushirikiano wa RDC – Monaco unakabiliwa na changamoto? Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na klabu ya AS Monaco unaweza kuwa kwenye hatari, ikizingatiwa taarifa zilizotolewa na Gazeti la L’Équipe la Nchini Ufaransa. Taarifa hizo zinaonyesha kwamba malalamiko ya "kuficha fedha", "kufurushwa fedha za umma" (Wizi) na "ufisadi" yamewasilishwa katika Tume ya Ufilisi wa Kifedha ya Taifa (PNF) mnamo Septemba 2025. Malalamiko haya yanahusu mkataba uliosainiwa kati ya Wizara ya Michezo ya RDC na AS Monaco mwezi Juni mwaka jana. Baada ya miezi kadhaa ya uchambuzi, PNF imetuma ripoti rasmi kwa mamlaka za Monaco. Hivyo, sasa kesi hiyo ipo mikononi mwa Mahakama ya Dola la Nchi ya Monaco. Hali hii inachukua sura mpya katika uhusiano wa michezo na uwekezaji kati ya RDC na Monaco, huku mashabiki na wanasiasa wakilenga kuona matokeo ya kesi hii. Toa maoni yako #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 142 مشاهدة
  • Gianluca Prestianni ajibu baada ya kudaiwa kumtukana Vinicius Jr.

    Gianluca Prestianni ametoa taarifa rasmi baada ya kudaiwa kumkosea heshima Vinicius Jr. Prestianni ameeleza wazi: “Nataka kufafanua kwamba, sikuwahi kumtukana Mchezaji wa Real Madrid wowote ule, Vinicius Jr, kwa bahati mbaya alikosea kuelewa yale aliyoamini akinisikia nikisema.”

    Aidha, Mchezaji huyo wa Argentina ameongeza: “Sijawahi kumchukia Mtu kwa rangi na ninajuta kwa vitisho nilivyopokea kutoka kwa Wachezaji wa Real Madrid.”

    Taarifa hii inakuja baada ya kashfa ya madai ya ubaguzi wa rangi iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, na Prestianni ameonekana kujaribu kuondoa kashfa hiyo kwa uwazi wake.

    Hii ni hatua muhimu kwa Mchezaji huyo ili kulinda heshima yake na kuweka wazi msimamo wake dhidi ya ubaguzi wa rangi.

    Toa maoni yako
    #Sports
    #Habari
    Gianluca Prestianni ajibu baada ya kudaiwa kumtukana Vinicius Jr. Gianluca Prestianni ametoa taarifa rasmi baada ya kudaiwa kumkosea heshima Vinicius Jr. Prestianni ameeleza wazi: “Nataka kufafanua kwamba, sikuwahi kumtukana Mchezaji wa Real Madrid wowote ule, Vinicius Jr, kwa bahati mbaya alikosea kuelewa yale aliyoamini akinisikia nikisema.” Aidha, Mchezaji huyo wa Argentina ameongeza: “Sijawahi kumchukia Mtu kwa rangi na ninajuta kwa vitisho nilivyopokea kutoka kwa Wachezaji wa Real Madrid.” Taarifa hii inakuja baada ya kashfa ya madai ya ubaguzi wa rangi iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, na Prestianni ameonekana kujaribu kuondoa kashfa hiyo kwa uwazi wake. Hii ni hatua muhimu kwa Mchezaji huyo ili kulinda heshima yake na kuweka wazi msimamo wake dhidi ya ubaguzi wa rangi. Toa maoni yako #Sports #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 140 مشاهدة
  • Msanii wa Afrobeats Simi aibua mjadala mzito kuhusu adhabu kwa Wabakaji wa Watoto.

    Msanii wa muziki wa Afrobeats, Simisola Kosoko maarufu kama Simi, amezua mjadala mkubwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii baada ya kutoa wito wa kuchukuliwa hatua kali dhidi ya Wanaume wanaobaka Watoto na Wasichana.

    Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Nigeria, nchi hiyo kwa sasa inapitia kipindi kigumu kutokana na ongezeko la matukio ya ukatili wa kijinsia. Visa vya ubakaji dhidi ya Wanawake na Watoto vimeripotiwa katika maeneo tofauti ndani ya wiki za hivi karibuni, jambo lililoibua hasira na maumivu miongoni mwa Wananchi.

    Kupitia ujumbe aliouchapisha katika mtandao wa X usiku wa Jumanne, tarehe 17 Februari 2026, Simi alionyesha wazi ghadhabu yake dhidi ya vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, hasa vinavyowalenga Watoto wa kike. Msanii huyo aliitaka serikali pamoja na jamii kwa ujumla kuchukua hatua madhubuti kukomesha uhalifu huo.

    Katika ujumbe wake, aliandika: "Nimechoka na nimekasirika sana. Acheni kubaka Wanawake na Watoto. Wanaume wanaobaka Watoto na Wasichana wanapaswa kuhasiwa na kuchomwa moto wakiwa hai.”

    Kauli hiyo imeibua mjadala mpana mtandaoni, huku baadhi ya watu wakimuunga mkono kwa kuonesha uchungu na hasira juu ya matukio ya ubakaji, na wengine wakipinga aina ya adhabu aliyoipendekeza wakisisitiza umuhimu wa kufuata misingi ya sheria na haki za binadamu.

    Wachambuzi wa masuala ya kijamii wanasema kauli ya Simi inaakisi hisia kali za Wananchi wengi wanaohisi mfumo wa haki jinai haujachukua hatua za kutosha kukabiliana na ongezeko la uhalifu wa kijinsia. Hata hivyo, wanasisitiza kuwa mapambano dhidi ya ubakaji yanahitaji mchanganyiko wa hatua za kisheria, elimu ya jamii, pamoja na ulinzi madhubuti kwa waathirika.

    Mjadala unaoendelea unaweka shinikizo kwa mamlaka husika kuimarisha sheria, kuharakisha mashauri ya kesi za ubakaji, na kuhakikisha Wahusika wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

    Toa maoni yako
    #Music
    #Habari
    Msanii wa Afrobeats Simi aibua mjadala mzito kuhusu adhabu kwa Wabakaji wa Watoto. Msanii wa muziki wa Afrobeats, Simisola Kosoko maarufu kama Simi, amezua mjadala mkubwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii baada ya kutoa wito wa kuchukuliwa hatua kali dhidi ya Wanaume wanaobaka Watoto na Wasichana. Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Nigeria, nchi hiyo kwa sasa inapitia kipindi kigumu kutokana na ongezeko la matukio ya ukatili wa kijinsia. Visa vya ubakaji dhidi ya Wanawake na Watoto vimeripotiwa katika maeneo tofauti ndani ya wiki za hivi karibuni, jambo lililoibua hasira na maumivu miongoni mwa Wananchi. Kupitia ujumbe aliouchapisha katika mtandao wa X usiku wa Jumanne, tarehe 17 Februari 2026, Simi alionyesha wazi ghadhabu yake dhidi ya vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, hasa vinavyowalenga Watoto wa kike. Msanii huyo aliitaka serikali pamoja na jamii kwa ujumla kuchukua hatua madhubuti kukomesha uhalifu huo. Katika ujumbe wake, aliandika: "Nimechoka na nimekasirika sana. Acheni kubaka Wanawake na Watoto. Wanaume wanaobaka Watoto na Wasichana wanapaswa kuhasiwa na kuchomwa moto wakiwa hai.” Kauli hiyo imeibua mjadala mpana mtandaoni, huku baadhi ya watu wakimuunga mkono kwa kuonesha uchungu na hasira juu ya matukio ya ubakaji, na wengine wakipinga aina ya adhabu aliyoipendekeza wakisisitiza umuhimu wa kufuata misingi ya sheria na haki za binadamu. Wachambuzi wa masuala ya kijamii wanasema kauli ya Simi inaakisi hisia kali za Wananchi wengi wanaohisi mfumo wa haki jinai haujachukua hatua za kutosha kukabiliana na ongezeko la uhalifu wa kijinsia. Hata hivyo, wanasisitiza kuwa mapambano dhidi ya ubakaji yanahitaji mchanganyiko wa hatua za kisheria, elimu ya jamii, pamoja na ulinzi madhubuti kwa waathirika. Mjadala unaoendelea unaweka shinikizo kwa mamlaka husika kuimarisha sheria, kuharakisha mashauri ya kesi za ubakaji, na kuhakikisha Wahusika wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria za nchi. Toa maoni yako #Music #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 281 مشاهدة
  • Pitbull ataka kuweka rekodi ya Dunia kupitia Guinness World Records.

    Rapa maarufu duniani, Pitbull, ametangaza mpango wa kuandika historia mpya katika Guinness World Records akishirikiana na mashabiki wake watakaohudhuria tamasha lake Jijini London, Uingereza.

    Msanii huyo mwenye umri wa miaka 45, anayejulikana pia kwa jina la kisanii Mr. Worldwide, anataka kuweka rekodi ya dunia kwa kuwa na “kundi kubwa zaidi la watu waliovaa kofia maalum zinazoiga kipara (bald caps)” katika tukio moja.

    Jaribio hilo linatarajiwa kufanyika wakati wa tamasha kubwa la muziki la BST Hyde Park, litakalofanyika tarehe 10 Julai 2026 Jijini London, ambapo Pitbull atakuwa Msanii mkuu wa siku hiyo.

    Wazo hilo limechochewa na utamaduni ulioenea katika maonyesho yake ya hivi karibuni, ambapo mashabiki wengi hujitokeza wakiwa wamevaa bald caps, miwani mikubwa aina ya aviators, pamoja na suti au makoti yanayokaa mwilini kwa umaridadi, mtindo unaoiga mwonekano rasmi wa Pitbull anapokuwa jukwaani.

    Akizungumza kuhusu mpango huo, Pitbull ameeleza kuwa “tunataka kuonyesha nguvu ya mashabiki na kuandika historia pamoja.”

    Mpango huo ulipata nguvu zaidi baada ya kuungwa mkono na Mtangazaji wa BBC Radio 1 Breakfast, Greg James, ambaye alihamasisha hadhira kuunga mkono jaribio hilo la kuvunja rekodi ya dunia.

    Kwa mujibu wa Waandaaji, endapo idadi ya mashabiki watakaovaa kofia hizo itafikia kiwango kinachotakiwa na Waamuzi wa Guinness World Records, basi Pitbull ataingia rasmi kwenye vitabu vya historia kama Msanii aliyeongoza tukio la kipekee zaidi la aina yake.

    Iwapo jaribio hilo litafanikiwa, litakuwa si tu ushindi kwa Pitbull binafsi, bali pia kwa mashabiki wake wanaojulikana kwa ubunifu na mshikamano mkubwa katika matamasha yake duniani.

    Toa maoni yako
    #Music
    #Habari
    Pitbull ataka kuweka rekodi ya Dunia kupitia Guinness World Records. Rapa maarufu duniani, Pitbull, ametangaza mpango wa kuandika historia mpya katika Guinness World Records akishirikiana na mashabiki wake watakaohudhuria tamasha lake Jijini London, Uingereza. Msanii huyo mwenye umri wa miaka 45, anayejulikana pia kwa jina la kisanii Mr. Worldwide, anataka kuweka rekodi ya dunia kwa kuwa na “kundi kubwa zaidi la watu waliovaa kofia maalum zinazoiga kipara (bald caps)” katika tukio moja. Jaribio hilo linatarajiwa kufanyika wakati wa tamasha kubwa la muziki la BST Hyde Park, litakalofanyika tarehe 10 Julai 2026 Jijini London, ambapo Pitbull atakuwa Msanii mkuu wa siku hiyo. Wazo hilo limechochewa na utamaduni ulioenea katika maonyesho yake ya hivi karibuni, ambapo mashabiki wengi hujitokeza wakiwa wamevaa bald caps, miwani mikubwa aina ya aviators, pamoja na suti au makoti yanayokaa mwilini kwa umaridadi, mtindo unaoiga mwonekano rasmi wa Pitbull anapokuwa jukwaani. Akizungumza kuhusu mpango huo, Pitbull ameeleza kuwa “tunataka kuonyesha nguvu ya mashabiki na kuandika historia pamoja.” Mpango huo ulipata nguvu zaidi baada ya kuungwa mkono na Mtangazaji wa BBC Radio 1 Breakfast, Greg James, ambaye alihamasisha hadhira kuunga mkono jaribio hilo la kuvunja rekodi ya dunia. Kwa mujibu wa Waandaaji, endapo idadi ya mashabiki watakaovaa kofia hizo itafikia kiwango kinachotakiwa na Waamuzi wa Guinness World Records, basi Pitbull ataingia rasmi kwenye vitabu vya historia kama Msanii aliyeongoza tukio la kipekee zaidi la aina yake. Iwapo jaribio hilo litafanikiwa, litakuwa si tu ushindi kwa Pitbull binafsi, bali pia kwa mashabiki wake wanaojulikana kwa ubunifu na mshikamano mkubwa katika matamasha yake duniani. Toa maoni yako #Music #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 249 مشاهدة
  • Saudi Arabia thibitisha kuonekana kwa Mwezi wa Ramadhani 1447 AH, kufunga kuanza Kesho.

    Mamlaka nchini Saudi Arabia yamethibitisha rasmi kwamba mwezi wa Ramadhani umeonekana, jambo linalothibitisha kuanza kwa mwezi mtukufu wa kufunga. Kwa mujibu wa tamko rasmi na kuthibitishwa kuonekana kwa Mwezi, na hivyo kesho, Jumatano, tarehe 18 Februari 2026, itakuwa siku ya kwanza ya Ramadhani 1447 Hijiria

    Ramadhani, mwezi ni wa tisa katika kalenda ya Kiislamu, hufungwa na Waislamu duniani kote kwa kuswali, kufanya ibada, na kufunga (kujizuia) kuanzia alfajiri hadi machweo ya jua. Kuonekana kwa mwezi wa Ramadhani ni kiashiria cha kuanza kwa ibada hii ya kiroho.

    Mamlaka za kidini katika mataifa mengine ya GCC pia zimethibitisha uamuzi huu, huku baadhi ya nchi zikitarajiwa kuanza kufunga siku moja baadae, kulingana na muda na mahali ambapo mwezi umeonekana. Hii ni kuonyesha umuhimu wa kalenda ya Kiislamu (Hijiria) katika kuamua siku za ibada na sherehe za kidini.

    Waislamu wanashauriwa kujiandaa kwa siku ya kwanza ya kufunga, kuimarisha imani na kufanya matendo mema, huku wakizingatia tamko la mamlaka husika.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Saudi Arabia thibitisha kuonekana kwa Mwezi wa Ramadhani 1447 AH, kufunga kuanza Kesho. Mamlaka nchini Saudi Arabia yamethibitisha rasmi kwamba mwezi wa Ramadhani umeonekana, jambo linalothibitisha kuanza kwa mwezi mtukufu wa kufunga. Kwa mujibu wa tamko rasmi na kuthibitishwa kuonekana kwa Mwezi, na hivyo kesho, Jumatano, tarehe 18 Februari 2026, itakuwa siku ya kwanza ya Ramadhani 1447 Hijiria Ramadhani, mwezi ni wa tisa katika kalenda ya Kiislamu, hufungwa na Waislamu duniani kote kwa kuswali, kufanya ibada, na kufunga (kujizuia) kuanzia alfajiri hadi machweo ya jua. Kuonekana kwa mwezi wa Ramadhani ni kiashiria cha kuanza kwa ibada hii ya kiroho. Mamlaka za kidini katika mataifa mengine ya GCC pia zimethibitisha uamuzi huu, huku baadhi ya nchi zikitarajiwa kuanza kufunga siku moja baadae, kulingana na muda na mahali ambapo mwezi umeonekana. Hii ni kuonyesha umuhimu wa kalenda ya Kiislamu (Hijiria) katika kuamua siku za ibada na sherehe za kidini. Waislamu wanashauriwa kujiandaa kwa siku ya kwanza ya kufunga, kuimarisha imani na kufanya matendo mema, huku wakizingatia tamko la mamlaka husika. Toa maoni yako #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 152 مشاهدة
  • FARDC yaishutumu AFC/M23 kwa wizi wa lami ya ujenzi wa barabara ya Mudaka.

    Mvutano mpya umezuka katika eneo la Sud-Kivu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya Jeshi la Serikali, Forces Armées de la République Démocratique du Congo (FARDC), kuishutumu kundi la Waasi la Alliance Fleuve Congo/M23 kwa kuiba lami iliyokuwa imekusudiwa kwa ajili ya kazi za ujenzi wa barabara katika eneo la Mudaka.

    Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi hilo, tukio hilo limetokea wakati mamlaka za serikali zikiendelea na maandalizi ya kuboresha miundombinu ya barabara katika eneo hilo, lengo likiwa ni kurahisisha usafiri na shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa Mudaka na maeneo jirani.

    Katika taarifa yake, FARDC imesema, “Kundi la AFC/M23 limehusika katika wizi wa lami iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara Mudaka, hatua inayolenga kuhujumu juhudi za serikali za kuboresha miundombinu.”

    Jeshi hilo limeongeza kuwa kitendo hicho ni sehemu ya mikakati ya makundi yenye silaha kuvuruga utulivu na maendeleo katika Mkoa wa Sud-Kivu.

    Kwa upande wake, hadi sasa AFC/M23 haijatoa tamko rasmi kujibu tuhuma hizo. Hata hivyo, kundi hilo limekuwa likitajwa mara kwa mara katika matukio ya mapigano na mivutano ya kiusalama katika maeneo mbalimbali ya mashariki mwa DRC.

    Wachambuzi wa masuala ya usalama wanaeleza kuwa miundombinu kama barabara imekuwa ikilengwa mara kwa mara katika maeneo yenye migogoro, kwani hudhoofisha uwezo wa serikali kufikisha huduma na kuimarisha ushawishi wake kwa wananchi.

    Hali ya usalama katika Mkoa wa Sud-Kivu inaendelea kuwa tete, huku jamii ya kimataifa ikiendelea kutoa wito wa mazungumzo na suluhisho la kudumu la kisiasa ili kumaliza mzozo wa muda mrefu katika eneo hilo.

    Kwa sasa, mamlaka za kijeshi zimesema zinaendelea kufuatilia tukio hilo na kuchukua hatua stahiki dhidi ya wahusika.

    Toa maoni yako
    #Habari
    FARDC yaishutumu AFC/M23 kwa wizi wa lami ya ujenzi wa barabara ya Mudaka. Mvutano mpya umezuka katika eneo la Sud-Kivu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya Jeshi la Serikali, Forces Armées de la République Démocratique du Congo (FARDC), kuishutumu kundi la Waasi la Alliance Fleuve Congo/M23 kwa kuiba lami iliyokuwa imekusudiwa kwa ajili ya kazi za ujenzi wa barabara katika eneo la Mudaka. Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi hilo, tukio hilo limetokea wakati mamlaka za serikali zikiendelea na maandalizi ya kuboresha miundombinu ya barabara katika eneo hilo, lengo likiwa ni kurahisisha usafiri na shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa Mudaka na maeneo jirani. Katika taarifa yake, FARDC imesema, “Kundi la AFC/M23 limehusika katika wizi wa lami iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara Mudaka, hatua inayolenga kuhujumu juhudi za serikali za kuboresha miundombinu.” Jeshi hilo limeongeza kuwa kitendo hicho ni sehemu ya mikakati ya makundi yenye silaha kuvuruga utulivu na maendeleo katika Mkoa wa Sud-Kivu. Kwa upande wake, hadi sasa AFC/M23 haijatoa tamko rasmi kujibu tuhuma hizo. Hata hivyo, kundi hilo limekuwa likitajwa mara kwa mara katika matukio ya mapigano na mivutano ya kiusalama katika maeneo mbalimbali ya mashariki mwa DRC. Wachambuzi wa masuala ya usalama wanaeleza kuwa miundombinu kama barabara imekuwa ikilengwa mara kwa mara katika maeneo yenye migogoro, kwani hudhoofisha uwezo wa serikali kufikisha huduma na kuimarisha ushawishi wake kwa wananchi. Hali ya usalama katika Mkoa wa Sud-Kivu inaendelea kuwa tete, huku jamii ya kimataifa ikiendelea kutoa wito wa mazungumzo na suluhisho la kudumu la kisiasa ili kumaliza mzozo wa muda mrefu katika eneo hilo. Kwa sasa, mamlaka za kijeshi zimesema zinaendelea kufuatilia tukio hilo na kuchukua hatua stahiki dhidi ya wahusika. Toa maoni yako #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 217 مشاهدة
  • Zambia Yawafukuza Zaidi ya Raia 80 wa Congo kwa tuhuma za kukaa kinyume cha sheria.

    Serikali ya Zambia imewafukuza zaidi ya Raia 80 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika operesheni maalum iliyolenga watu wanaodaiwa kuishi nchini humo bila vibali halali.

    Kwa mujibu wa mamlaka za Zambia, hatua hiyo ni sehemu ya zoezi pana la kukagua Wahamiaji wanaoshukiwa kuwa katika hali isiyo halali ndani ya mipaka ya taifa hilo. Vyanzo vya kiusalama vinaeleza kuwa operesheni hiyo ilifanyika baada ya uchunguzi wa kina kubaini kuwepo kwa idadi kubwa ya watu wasiokuwa na nyaraka sahihi.

    Afisa wa Zambia wamesema kuwa, "Zaidi ya watu 170 wa mataifa mbalimbali wanashukiwa kuwa katika hali isiyo halali nchini Zambia."

    Taarifa hiyo inaashiria kuwa si Raia wa Congo pekee waliolengwa katika msako huo, bali pia watu kutoka mataifa mengine ambao wanadaiwa kukiuka sheria za uhamiaji.

    Hatua ya kufukuzwa kwa Raia hao wa Congo inaelezwa kuwa ni utekelezaji wa sheria za uhamiaji za Zambia, ambazo zinataka Wageni wote kuwa na vibali halali vya kuishi au kufanya kazi nchini humo.

    Wachambuzi wa masuala ya kikanda wanasema kuwa operesheni za aina hii mara nyingi huibua mjadala kuhusu haki za Wahamiaji, hasa katika ukanda wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambako harakati za watu kuvuka mipaka ni jambo la kawaida kwa sababu za kiuchumi na kijamii.

    Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi kuhusu iwapo hatua hiyo itaathiri uhusiano wa kidiplomasia kati ya Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Serikali ya Zambia imeweka wazi kuwa itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kukaa nchini humo bila kufuata taratibu za kisheria.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Zambia Yawafukuza Zaidi ya Raia 80 wa Congo kwa tuhuma za kukaa kinyume cha sheria. Serikali ya Zambia imewafukuza zaidi ya Raia 80 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika operesheni maalum iliyolenga watu wanaodaiwa kuishi nchini humo bila vibali halali. Kwa mujibu wa mamlaka za Zambia, hatua hiyo ni sehemu ya zoezi pana la kukagua Wahamiaji wanaoshukiwa kuwa katika hali isiyo halali ndani ya mipaka ya taifa hilo. Vyanzo vya kiusalama vinaeleza kuwa operesheni hiyo ilifanyika baada ya uchunguzi wa kina kubaini kuwepo kwa idadi kubwa ya watu wasiokuwa na nyaraka sahihi. Afisa wa Zambia wamesema kuwa, "Zaidi ya watu 170 wa mataifa mbalimbali wanashukiwa kuwa katika hali isiyo halali nchini Zambia." Taarifa hiyo inaashiria kuwa si Raia wa Congo pekee waliolengwa katika msako huo, bali pia watu kutoka mataifa mengine ambao wanadaiwa kukiuka sheria za uhamiaji. Hatua ya kufukuzwa kwa Raia hao wa Congo inaelezwa kuwa ni utekelezaji wa sheria za uhamiaji za Zambia, ambazo zinataka Wageni wote kuwa na vibali halali vya kuishi au kufanya kazi nchini humo. Wachambuzi wa masuala ya kikanda wanasema kuwa operesheni za aina hii mara nyingi huibua mjadala kuhusu haki za Wahamiaji, hasa katika ukanda wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambako harakati za watu kuvuka mipaka ni jambo la kawaida kwa sababu za kiuchumi na kijamii. Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi kuhusu iwapo hatua hiyo itaathiri uhusiano wa kidiplomasia kati ya Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Serikali ya Zambia imeweka wazi kuwa itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kukaa nchini humo bila kufuata taratibu za kisheria. Toa maoni yako #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 171 مشاهدة
  • Koffi Olomide atangaza tamasha kubwa Ubelgiji baada ya kufutwa matamasha yake Ufaransa.

    Mwanamuziki Nguli wa rumba ya Congo, Koffi Olomide, ametangaza rasmi kufanya tamasha kubwa katika Ubelgiji, baada ya kukumbana na changamoto ya kufutwa kwa matamasha kadhaa nchini Ufaransa.

    Tamasha hilo limepangwa kufanyika tarehe 11 Julai 2026 katika Uwanja maarufu wa Stade Roi Baudouin uliopo Jijini Brussels. Tangazo hili limeibua msisimko mkubwa miongoni mwa mashabiki wa muziki wa Congo na rumba kwa ujumla barani Ulaya na Afrika.

    Kupitia matangazo yake ya moja kwa moja kwenye TikTok, Msanii huyo alieleza dhamira yake ya kuifanya siku hiyo kuwa ya kipekee katika maisha yake ya muziki.

    Amesema kuwa anataka tarehe hiyo iwe tukio la kihistoria, akisherehekea miaka yake 70 ya kuzaliwa akiwa pamoja na mashabiki wake.

    Tamasha hilo linatajwa kuwa uzalishaji mkubwa (grande production) unaotarajiwa kuvuta maelfu ya watu katika Uwanja huo wenye historia ya kuandaa matukio makubwa ya kimataifa ya michezo na burudani.

    Hatua hii inakuja baada ya kufutwa kwa matamasha kadhaa ya Msanii huyo nchini Ufaransa, jambo lililozua mjadala mpana katika tasnia ya muziki. Hata hivyo, tangazo la Brussels linaonekana kama kurejea kwa nguvu kwa Gwiji huyo wa rumba, akionyesha kuwa bado ana ushawishi mkubwa na soko imara barani Ulaya.

    Kwa wapenzi wa rumba na muziki wa Congo, tukio hili tayari linaonekana kuwa miongoni mwa matamasha makubwa zaidi ya mwaka 2026. Kwa historia ndefu ya Koffi Olomide katika muziki, tamasha hili linatarajiwa kuwa zaidi ya burudani bali ni sherehe ya urithi, mafanikio na mchango wake katika kukuza rumba ya Kongo kimataifa.

    Mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu maandalizi rasmi, mauzo ya tiketi na orodha ya Wasanii watakaoshiriki katika usiku huo unaotarajiwa kuwa wa kipekee.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Koffi Olomide atangaza tamasha kubwa Ubelgiji baada ya kufutwa matamasha yake Ufaransa. Mwanamuziki Nguli wa rumba ya Congo, Koffi Olomide, ametangaza rasmi kufanya tamasha kubwa katika Ubelgiji, baada ya kukumbana na changamoto ya kufutwa kwa matamasha kadhaa nchini Ufaransa. Tamasha hilo limepangwa kufanyika tarehe 11 Julai 2026 katika Uwanja maarufu wa Stade Roi Baudouin uliopo Jijini Brussels. Tangazo hili limeibua msisimko mkubwa miongoni mwa mashabiki wa muziki wa Congo na rumba kwa ujumla barani Ulaya na Afrika. Kupitia matangazo yake ya moja kwa moja kwenye TikTok, Msanii huyo alieleza dhamira yake ya kuifanya siku hiyo kuwa ya kipekee katika maisha yake ya muziki. Amesema kuwa anataka tarehe hiyo iwe tukio la kihistoria, akisherehekea miaka yake 70 ya kuzaliwa akiwa pamoja na mashabiki wake. Tamasha hilo linatajwa kuwa uzalishaji mkubwa (grande production) unaotarajiwa kuvuta maelfu ya watu katika Uwanja huo wenye historia ya kuandaa matukio makubwa ya kimataifa ya michezo na burudani. Hatua hii inakuja baada ya kufutwa kwa matamasha kadhaa ya Msanii huyo nchini Ufaransa, jambo lililozua mjadala mpana katika tasnia ya muziki. Hata hivyo, tangazo la Brussels linaonekana kama kurejea kwa nguvu kwa Gwiji huyo wa rumba, akionyesha kuwa bado ana ushawishi mkubwa na soko imara barani Ulaya. Kwa wapenzi wa rumba na muziki wa Congo, tukio hili tayari linaonekana kuwa miongoni mwa matamasha makubwa zaidi ya mwaka 2026. Kwa historia ndefu ya Koffi Olomide katika muziki, tamasha hili linatarajiwa kuwa zaidi ya burudani bali ni sherehe ya urithi, mafanikio na mchango wake katika kukuza rumba ya Kongo kimataifa. Mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu maandalizi rasmi, mauzo ya tiketi na orodha ya Wasanii watakaoshiriki katika usiku huo unaotarajiwa kuwa wa kipekee. Toa maoni yako #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 105 مشاهدة
  • Trump aonyesha utayari wa kukutana na Kiongozi wa Mapinduzi ya Iran.

    Mvutano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Iran unaendelea kuchukua sura mpya, huku Washington ikionesha ishara za kutaka kufungua ukurasa wa mazungumzo mapya na Tehran.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, amesema kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump, yuko tayari kukutana na Kiongozi wa Mapinduzi ya Iran iwapo upande wa Iran utaonesha nia ya kufanya hivyo.

    Akizungumza kuhusu msimamo wa Marekani, Rubio alisema: “Trump ameonesha utayari wake kukutana na Kiongozi wa Mapinduzi ya Iran ikiwa atapenda kufanya hivyo.”

    Kauli hiyo inaonekana kufungua uwezekano wa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili ambazo kwa muda mrefu zimekuwa katika mvutano wa kisiasa, kiusalama na kiuchumi.

    Kwa mujibu wa Rubio, Marekani inaendelea kufanya kazi kwa lengo la kufikia makubaliano mapya na Iran, hasa katika masuala yanayohusu usalama wa kikanda na mpango wa nyuklia wa Tehran.

    Rubio aliongeza kuwa: "Tunafanya kazi kufikia makubaliano na Iran, na mikutano ijayo itaonesha kama maendeleo yanaweza kupatikana.”

    Kauli hiyo inaashiria kuwa mazungumzo ya ngazi za juu yanatarajiwa kufanyika katika siku zijazo, huku macho ya jumuiya ya kimataifa yakielekezwa kwenye iwapo juhudi hizo zitazaa matunda au la.

    Uhusiano kati ya Washington na Tehran yamekuwa ya misukosuko kwa miaka kadhaa, hasa baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 na kurejesha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran.

    Hatua yoyote ya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Viongozi wa juu inaweza kuwa hatua muhimu katika kupunguza mvutano uliodumu kwa muda mrefu.

    Kwa sasa, dunia inasubiri kuona iwapo utayari huo wa kukutana utageuka kuwa mkutano rasmi na kama makubaliano mapya yanaweza kufikiwa kati ya mataifa hayo mawili yenye ushawishi mkubwa katika siasa za kimataifa.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Trump aonyesha utayari wa kukutana na Kiongozi wa Mapinduzi ya Iran. Mvutano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Iran unaendelea kuchukua sura mpya, huku Washington ikionesha ishara za kutaka kufungua ukurasa wa mazungumzo mapya na Tehran. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, amesema kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump, yuko tayari kukutana na Kiongozi wa Mapinduzi ya Iran iwapo upande wa Iran utaonesha nia ya kufanya hivyo. Akizungumza kuhusu msimamo wa Marekani, Rubio alisema: “Trump ameonesha utayari wake kukutana na Kiongozi wa Mapinduzi ya Iran ikiwa atapenda kufanya hivyo.” Kauli hiyo inaonekana kufungua uwezekano wa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili ambazo kwa muda mrefu zimekuwa katika mvutano wa kisiasa, kiusalama na kiuchumi. Kwa mujibu wa Rubio, Marekani inaendelea kufanya kazi kwa lengo la kufikia makubaliano mapya na Iran, hasa katika masuala yanayohusu usalama wa kikanda na mpango wa nyuklia wa Tehran. Rubio aliongeza kuwa: "Tunafanya kazi kufikia makubaliano na Iran, na mikutano ijayo itaonesha kama maendeleo yanaweza kupatikana.” Kauli hiyo inaashiria kuwa mazungumzo ya ngazi za juu yanatarajiwa kufanyika katika siku zijazo, huku macho ya jumuiya ya kimataifa yakielekezwa kwenye iwapo juhudi hizo zitazaa matunda au la. Uhusiano kati ya Washington na Tehran yamekuwa ya misukosuko kwa miaka kadhaa, hasa baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 na kurejesha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran. Hatua yoyote ya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Viongozi wa juu inaweza kuwa hatua muhimu katika kupunguza mvutano uliodumu kwa muda mrefu. Kwa sasa, dunia inasubiri kuona iwapo utayari huo wa kukutana utageuka kuwa mkutano rasmi na kama makubaliano mapya yanaweza kufikiwa kati ya mataifa hayo mawili yenye ushawishi mkubwa katika siasa za kimataifa. Toa maoni yako #Habari
    0 التعليقات 0 المشاركات 330 مشاهدة
الصفحات المعززة