Iran na Urusi kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi nje ya Bahari ya Oman.
Iran na Urusi zinatarajiwa kuanza mazoezi ya pamoja ya kijeshi kesho Alhamisi katika maeneo ya nje ya Bahari ya Oman na kaskazini mwa Bahari ya Hindi, hatua inayotafsiriwa kama ishara ya kuimarika kwa ushirikiano wa kiusalama kati ya mataifa hayo mawili.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, tangazo hilo limekuja siku chache baada ya Kikosi Maalum cha Walinzi wa Mapinduzi wa Iran kufanya mazoezi ya kijeshi katika mlango wa bahari wa Hormuz, eneo nyeti linalopitisha sehemu kubwa ya usafirishaji wa mafuta duniani.
Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran, Hassan Maghsoodloo, ameeleza madhumuni ya mazoezi hayo kwa kusema: “Lengo la mazoezi haya ni kuunda nguvu za pamoja na kuimarisha uratibu wa hatua za pamoja ili kukabiliana na vitisho vinavyoathiri usalama wa majini na usalama wa nchi zetu mbili.”
Ameongeza kuwa: "Mazoezi haya pia yanalenga kupambana na ugaidi na kuimarisha utulivu katika eneo la kimkakati la bahari.”
Kauli hiyo inaonesha kuwa Tehran na Moscow zinaangazia zaidi usalama wa bahari na kulinda maslahi yao ya kiuchumi na kijeshi katika njia kuu za usafirishaji wa kimataifa.
Hatua hizi zinakuja wakati wa mvutano unaoendelea kati ya Marekani na Iran. Washington imetishia hatua za kijeshi dhidi ya Tehran, ikiishutumu kwa kile ilichodai kuwa ni ukiukwaji wa haki za Waandamanaji pamoja na kushindwa kufikia makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia.
Kwa upande wake, Iran imekuwa ikisisitiza mara kwa mara uwezekano wa kuufunga mlango wa bahari wa Hormuz wakati wa mvutano mkali na Marekani. Hata hivyo, hadi sasa, haijawahi kuchukua hatua ya kulifunga rasmi lango hilo muhimu la kimataifa.
Mazoezi haya yanaonekana kuwa na ujumbe wa wazi wa kisiasa na kijeshi kuonesha mshikamano wa Iran na Urusi katika kukabiliana na shinikizo la Magharibi, huku yakituma ishara kwa mataifa mengine kuhusu uwezo wao wa pamoja katika kulinda maslahi ya kimkakati katika Bahari ya Hindi na Ghuba ya Oman.
Wachambuzi wa masuala ya ulinzi wanaona kuwa ushirikiano huu unaweza kuathiri mizania ya nguvu katika eneo hilo, hasa katika kipindi ambacho diplomasia ya nyuklia bado haijafikia muafaka wa kudumu.
Toa maoni yako
#Habari