Uingereza yakataa ombi la Trump kutumia kambi zake za kijeshi kushambulia Iran.
Serikali ya Uingereza imekataa rasmi ombi la Rais wa Marekani, Donald Trump, la kutaka kutumia kambi za kijeshi za Uingereza kama vituo vya kuanzishia mashambulizi yanayoweza kulenga Iran.
Kwa mujibu wa taarifa za kidiplomasia, ombi hilo lilihusisha matumizi ya kambi muhimu zikiwemo Diego Garcia katika Bahari ya Hindi pamoja na RAF Fairford iliyoko Gloucestershire.
Vyanzo vya serikali Mjini London vinaeleza kuwa uamuzi huo umechukuliwa kwa kuzingatia maslahi ya kitaifa na tahadhari dhidi ya kuongezeka kwa mvutano wa kijeshi Mashariki ya Kati.
Msimamo huo unaonyesha kuwa Uingereza haitaki kuhusishwa moja kwa moja na operesheni yoyote ya kijeshi dhidi ya Iran bila mchakato mpana wa kidiplomasia na kibali cha kimataifa.
Ingawa Marekani na Uingereza ni washirika wakubwa wa kijeshi kupitia Muungano wa NATO, London imeonekana kuchukua tahadhari kubwa katika suala linaloweza kusababisha vita pana katika eneo la Ghuba.
Kisiwa cha Diego Garcia ni kituo cha kimkakati kinachotumiwa kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Marekani na Uingereza. Kimewahi kutumika kama kitovu cha operesheni za kijeshi katika Mashariki ya Kati, hasa wakati wa vita vya Iraq na Afghanistan.
Kwa upande mwingine, RAF Fairford imekuwa ikitumika mara kadhaa kupokea ndege za kivita za Marekani, zikiwemo mabomu mazito ya masafa marefu kama B-52.
Hatua ya Uingereza inaweza kuathiri kwa kiwango fulani uratibu wa kijeshi kati ya Washington na London, hasa wakati ambapo mvutano kati ya Marekani na Iran unaongezeka.
Hadi sasa, Ikulu ya White House haijatoa tamko rasmi kuhusu msimamo wa Uingereza, huku Wachambuzi wa siasa za kimataifa wakitathmini iwapo uamuzi huo utaashiria tofauti ya kimkakati kati ya washirika hao wawili wa muda mrefu.
Mvutano kati ya Marekani na Iran umeendelea kuwa tete, hasa katika masuala yanayohusu nyuklia na ushawishi wa kikanda.
Je, uamuzi wa London utatuliza hali au utaongeza presha za kidiplomasia? Dunia inaendelea kufuatilia kwa karibu.
Toa maoni yako
#Habari

0 Reacties
0 aandelen
32 Views