• MTAKATIFU ANAYE ISHI PART TWO.

    MTAZAMO CHANYA KUHUSU UTAKATIFU.

    1.*UTAKATIFU NI KUTENGWA*(KUKUBALI KUACHA)

    Dunia inamtazamo wake kuhusu utakatifu na Mbingu pia ina mtazamo wake kuhusu utakatifu.

    *Kitendo cha biblia kukufahamu kama mtakatifu ni lazima Mungu awe amekutenga kwa kusudi maalamu.*

    Kila aliye okoka ni kiungo katika kuukamilisha mwili wa Kristo katika eneo alilo itiwa .inaweza kuwa uchungaji ,ualimu ,uinjiristi ,,biashara ,siasa , utumishi wa uma nk .

    *Na nieleweke zaidi ninapo sema "Kutengwa" au "kuitwa '' simahanishi kuwa muhudumu wa madhabau peke yake hapana na maanisha kila jambo unalo lifanya ukiokoka na ukafanya sawa sawa na mapenzi ya Mungu ndio wito wako wengine wameitwa kuwa wafanya biashara ,wengine watawala ,wengine wachungaji ,wengine ni wasomi na washauri ko kila mmoja katika gield yake anapaswa kujua ametengwa na "Mungu kuwa mtakatifu"*

    Warumi 1:1 *Paulo, mtumishi wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu*

    Paulo yeye alitengwa kwa ajiri ya injiri ya mataifa ,mimi sijui wewe umeitwa katika karia gani ila najenga msingi kuwa katika field uliyo itwa Bwana amekutenga uwe mtakatifu.

    Warumi 12:2. *Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.*

    Kumbuka kuwa Mungu alimuumba mwanadamu ili awe mkamirifu .

    Ndo mana ni rahisi sana kwa mtucasite jua wokovu kuona kama utakatifu unapaswa kuzingatiwa na makuhani peke yake ,

    *Lakini uhalisia utakatifu ni maisha ya mwamini kila wakati na mwamini lazima ujue wewe ni barua unasomwa na wengi*

    Mifano ya watu ambao hawakuwa makuhani wala manabii ila waliupendeza moyo wa Mungu .

    *-Daudi alipendezwa na Mungu na akuwa kuhani wala nabii alikuwa mwanasiasa (mfalme) wa nchi lakini kiwango cha unyenyekevu wake kilimpendeza Mungu.*

    -Daniel akuwa nabii lakini alikuwa mwanasiasa kwa maana ya (ukuu wa wilaya) lugha nyepesi kada wa mlengo wa mfalme (mwanasiasa) lakini alisimama na kukubali kutengwa na kutimiza kusudi la Mungu ata katika ugenini.

    Danieli 10:12. *Aliitwa apendwaye sana sibahati bali ni kwa sababu alikubali kujitenga na kuishi utakatifu , ni wewe tu mwokovu wa leo unaona kama kuishi utakatifu haiwezekani .*

    -Yusuph alikuwa si muhubiri pia wala kuhani lakini alichagua kujitenga na uharibifu wa zinaa na alikuwa mwanasiasa karsmatic leader ko ni wewe tu blaza unatumia ushawishi wako vibaya .

    *Ok nataka kusema hivi kama kila mtu ataamua kuwa barua ya kristo katika eneo alilo itiwa basi jua kabisa tutmpendeza Mungu cna baraka zitatufuata duniani kisha uzima wa milele .*

    Utakatifu ni maisha siyo tukio ukiweza kujua hilo basi utakuwa uleishu kadiri roho apendavyo.

    Ok naitwa sylvester kutoka (build new eden ) kwa mafundisho zaidi unaweza nitafuta kwa namba 0622625340 ni ku add kwenye mfululizo wa mafundisho .

    #build new eden
    #restore men position
    MTAKATIFU ANAYE ISHI PART TWO. MTAZAMO CHANYA KUHUSU UTAKATIFU. 1.*UTAKATIFU NI KUTENGWA*(KUKUBALI KUACHA) Dunia inamtazamo wake kuhusu utakatifu na Mbingu pia ina mtazamo wake kuhusu utakatifu. *Kitendo cha biblia kukufahamu kama mtakatifu ni lazima Mungu awe amekutenga kwa kusudi maalamu.* Kila aliye okoka ni kiungo katika kuukamilisha mwili wa Kristo katika eneo alilo itiwa .inaweza kuwa uchungaji ,ualimu ,uinjiristi ,,biashara ,siasa , utumishi wa uma nk . *Na nieleweke zaidi ninapo sema "Kutengwa" au "kuitwa '' simahanishi kuwa muhudumu wa madhabau peke yake hapana na maanisha kila jambo unalo lifanya ukiokoka na ukafanya sawa sawa na mapenzi ya Mungu ndio wito wako wengine wameitwa kuwa wafanya biashara ,wengine watawala ,wengine wachungaji ,wengine ni wasomi na washauri ko kila mmoja katika gield yake anapaswa kujua ametengwa na "Mungu kuwa mtakatifu"* Warumi 1:1 *Paulo, mtumishi wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu* Paulo yeye alitengwa kwa ajiri ya injiri ya mataifa ,mimi sijui wewe umeitwa katika karia gani ila najenga msingi kuwa katika field uliyo itwa Bwana amekutenga uwe mtakatifu. Warumi 12:2. *Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.* Kumbuka kuwa Mungu alimuumba mwanadamu ili awe mkamirifu . Ndo mana ni rahisi sana kwa mtucasite jua wokovu kuona kama utakatifu unapaswa kuzingatiwa na makuhani peke yake , *Lakini uhalisia utakatifu ni maisha ya mwamini kila wakati na mwamini lazima ujue wewe ni barua unasomwa na wengi* Mifano ya watu ambao hawakuwa makuhani wala manabii ila waliupendeza moyo wa Mungu . *-Daudi alipendezwa na Mungu na akuwa kuhani wala nabii alikuwa mwanasiasa (mfalme) wa nchi lakini kiwango cha unyenyekevu wake kilimpendeza Mungu.* -Daniel akuwa nabii lakini alikuwa mwanasiasa kwa maana ya (ukuu wa wilaya) lugha nyepesi kada wa mlengo wa mfalme (mwanasiasa) lakini alisimama na kukubali kutengwa na kutimiza kusudi la Mungu ata katika ugenini. Danieli 10:12. *Aliitwa apendwaye sana sibahati bali ni kwa sababu alikubali kujitenga na kuishi utakatifu , ni wewe tu mwokovu wa leo unaona kama kuishi utakatifu haiwezekani .* -Yusuph alikuwa si muhubiri pia wala kuhani lakini alichagua kujitenga na uharibifu wa zinaa na alikuwa mwanasiasa karsmatic leader ko ni wewe tu blaza unatumia ushawishi wako vibaya . *Ok nataka kusema hivi kama kila mtu ataamua kuwa barua ya kristo katika eneo alilo itiwa basi jua kabisa tutmpendeza Mungu cna baraka zitatufuata duniani kisha uzima wa milele .* Utakatifu ni maisha siyo tukio ukiweza kujua hilo basi utakuwa uleishu kadiri roho apendavyo. Ok naitwa sylvester kutoka (build new eden ) kwa mafundisho zaidi unaweza nitafuta kwa namba 0622625340 ni ku add kwenye mfululizo wa mafundisho . #build new eden #restore men position
    0 Comments 0 Shares 169 Views
  • 4/21.Tumia biblia kuomba ulinzi wa Mungu.

    *Maisha ya mwanadamu hayako mikononi mwa mwanadamu bali yako mikononi mwake mwokozi Mungu wetu.*

    *Ukijua kuwa uweponi mwa bwana jukumu la kujilinda linakuwa siyo lako.*

    Zaburi 127:1-2
    *BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure. Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi."*

    Kumbe lazima Bwana akulinde kwani kujilnda uwezi hata siku moja.

    1.Mfanye Bwana kuwa mlinzi wako

    Mithali18:10. *Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama*

    Zaburi 27:1.BHN *Mwenyezi-Mungu ni mwanga wangu na wokovu wangu, ni nani nitakayemwogopa? Mwenyezi-Mungu ni ngome ya maisha yangu, sitamwogopa mtu yeyote*

    Kumbe lazima ifike mahara bwana awe ngome yako na kimbilio lako na uo ndio wakovu mkuu.

    2.Bwana atakulinda dhidi ya mabaya

    Zaburi 91:4
    *Bwana atakufunika chini ya mbawa zake*
    Zaburi 121:1-4

    Zaburi 34:7
    *Malaika wa Mwenyezi-Mungu huwalinda wote wamchao, na kuwaokoa katika hatari.*

    Kumbe kama tu ukiamua kuokoka Bwana anaanza kuwa mtetezi wako .

    *Kiwango chako cha kumjua Mungu kinaamua kiwango gani Mungu awa mtetezi wako .*
    Ayubu 22:21

    *Mjue sana Mungu ili uwe na amani, ndipo mema yatakapokujia*

    Kumbe mema yako ni uwezo wako wa kumjua Mungu.

    Kutoka 14;14 SUV
    *BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.*

    Zaburi 23:4
    *Nijapopita katika bonde la giza kuu la kifo, sitaogopa hatari yoyote, maana wewe ee Mwenyezi-Mungu u pamoja nami; gongo lako na fimbo yako vyanilinda*

    *Wokovu ndio siri inayo kukutaniisha na Mungu na kuwa mlinzi wa karibu*

    *Mtafute sana Mungu ndipo atakuzidishia ulinzi kiasi cha kuweza kukuandalia meza katikati ya watesi wako.*

    *Mungu akiwa mlinzi wako ndivyo anavyo weza kuwa kimbilio lako na ngome yako na mtetezi wako.*

    #build new eden
    #restore men position
    4/21.Tumia biblia kuomba ulinzi wa Mungu. *Maisha ya mwanadamu hayako mikononi mwa mwanadamu bali yako mikononi mwake mwokozi Mungu wetu.* *Ukijua kuwa uweponi mwa bwana jukumu la kujilinda linakuwa siyo lako.* Zaburi 127:1-2 *BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure. Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi."* Kumbe lazima Bwana akulinde kwani kujilnda uwezi hata siku moja. 1.Mfanye Bwana kuwa mlinzi wako Mithali18:10. *Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama* Zaburi 27:1.BHN *Mwenyezi-Mungu ni mwanga wangu na wokovu wangu, ni nani nitakayemwogopa? Mwenyezi-Mungu ni ngome ya maisha yangu, sitamwogopa mtu yeyote* Kumbe lazima ifike mahara bwana awe ngome yako na kimbilio lako na uo ndio wakovu mkuu. 2.Bwana atakulinda dhidi ya mabaya Zaburi 91:4 *Bwana atakufunika chini ya mbawa zake* Zaburi 121:1-4 Zaburi 34:7 *Malaika wa Mwenyezi-Mungu huwalinda wote wamchao, na kuwaokoa katika hatari.* Kumbe kama tu ukiamua kuokoka Bwana anaanza kuwa mtetezi wako . *Kiwango chako cha kumjua Mungu kinaamua kiwango gani Mungu awa mtetezi wako .* Ayubu 22:21 *Mjue sana Mungu ili uwe na amani, ndipo mema yatakapokujia* Kumbe mema yako ni uwezo wako wa kumjua Mungu. Kutoka 14;14 SUV *BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.* Zaburi 23:4 *Nijapopita katika bonde la giza kuu la kifo, sitaogopa hatari yoyote, maana wewe ee Mwenyezi-Mungu u pamoja nami; gongo lako na fimbo yako vyanilinda* *Wokovu ndio siri inayo kukutaniisha na Mungu na kuwa mlinzi wa karibu* *Mtafute sana Mungu ndipo atakuzidishia ulinzi kiasi cha kuweza kukuandalia meza katikati ya watesi wako.* *Mungu akiwa mlinzi wako ndivyo anavyo weza kuwa kimbilio lako na ngome yako na mtetezi wako.* #build new eden #restore men position
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 210 Views
  • Habari ya jion wapendwa leo ni siku yetu ya mwisho kabisa kwa fasiri ya ndoto japo nipo naandaa kitabu cha kutafsiri ndoto zipo 100+ plus kikitoka nitawajuza .

    *Tunamalizia ndoto hii leo je umewai ota umeachwa na gari kwa kujizungusha ?*

    Nini maana yake kiroho .
    *Kumbuka ndoto ni mlango (portal ambayo Mungu anaitumia sana katimka kufikisha ujumbe hata shetani pia anatumia ku attack*

    Maana
    1.Unaupoteza msimu wako mpya

    2. Malango yako ya kimataifa yanakuwa yamefungwa
    3.
    3. *Gari pia inatafsirika kama huduma au wito ko unaweza kuwa umeachwa na huduma au karama yako*

    Naombaje ? Namna ya kuomba .

    1.Omba toba haraka ya kufungua mlango .

    2.Omba urejeshewe nyakati na majira.

    *Watu hawa wameibiwa hakuna asemaye rejesha*

    3.Muone kuhani haraka sana

    Naitwa sylvester kutoka build new eden.
    Pia nawakaribisha kwa maombi ya siku 21 za kumlingana Mungu na kumkumbusha ahadi zake kwetu .

    Twende kaka yangi ,dada yangu tukadai karama zetu ,tukadai mafanikio yetu .
    Tunaanza tar 28.04.2025. - 18.05.2025

    #build new eden
    Habari ya jion wapendwa leo ni siku yetu ya mwisho kabisa kwa fasiri ya ndoto japo nipo naandaa kitabu cha kutafsiri ndoto zipo 100+ plus kikitoka nitawajuza . *Tunamalizia ndoto hii leo je umewai ota umeachwa na gari kwa kujizungusha ?* Nini maana yake kiroho . *Kumbuka ndoto ni mlango (portal ambayo Mungu anaitumia sana katimka kufikisha ujumbe hata shetani pia anatumia ku attack* Maana 1.Unaupoteza msimu wako mpya 2. Malango yako ya kimataifa yanakuwa yamefungwa 3. 3. *Gari pia inatafsirika kama huduma au wito ko unaweza kuwa umeachwa na huduma au karama yako* Naombaje ? Namna ya kuomba . 1.Omba toba haraka ya kufungua mlango . 2.Omba urejeshewe nyakati na majira. *Watu hawa wameibiwa hakuna asemaye rejesha* 3.Muone kuhani haraka sana Naitwa sylvester kutoka build new eden. Pia nawakaribisha kwa maombi ya siku 21 za kumlingana Mungu na kumkumbusha ahadi zake kwetu . Twende kaka yangi ,dada yangu tukadai karama zetu ,tukadai mafanikio yetu . Tunaanza tar 28.04.2025. - 18.05.2025 #build new eden
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 296 Views
  • Habari ya usiku ndugu zangu ni siku ya nne leo japo kwa kuchelewe tunaendelea na mwendelezo wa fasiri za ndoto kiblia .

    *Ungana nami Sylvester Mwakabende kwa ufafanuzi zaidi kadiri roho wa Bwana Atakavyo niongoza*

    *Je umewai kuota unafukuzwa na mbwa ? nini maana yake*? .


    Zaburi 22:16
    *[16]Kwa maana mbwa wamenizunguka Kusanyiko la waovu wamenisonga;
    Wamenizua mikono na miguu*
    For dogs have compassed me: the assembly of the wicked have inclosed me: they pierced my hands and my feet.

    1.Kufuatiliwa na roho chafu kama zinaa na uasherati

    Mithali26:11 SUV

    *Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena.*

    Kutoka 22:31 BHN
    *Nyinyi mtakuwa watu waliowekwa wakfu kwangu. Kwa hiyo hamtakula nyama ya mnyama aliyeuawa na mnyama wa porini. Nyama hiyo mtawatupia mbwa.*

    Chochote kile kilicho kichafu upaswi kukila .

    Torati 23:18 BHN
    *Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yoyote; kwani haya ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako, yote mawili.*
    2wafalme 9;10

    Zaburi 22;20 BHN
    *Iokoe nafsi yangu mbali na upanga, yaokoe maisha yangu makuchani mwa mbwa hao!*

    *Mbwa ana nguvu maana yake mbwa anawakilisha roho chafu za zinaa, uasherati na machafu yote ya shetani .*
    .
    2.kuiacha njia ya bwana kama kuhani.

    Isaya 56:11 BHN
    *Hao ni kama mbwa wenye uchu sana, wala hawawezi kamwe kutoshelezwa. Wachungaji hao hawana akili yoyote; kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe.*

    Naombaje ?NAMNA YA KUOMBA

    1.Toba ya kweli kwa sababu ya kufungua mlango .

    2.kuhalibu kila njia ya uovu inayo kufuatilia

    3.Muone kuhani kwa ajiri ya ukombozi .

    4.kataa kabisa roho za uharibifu kwa kusimamisha madhabau ya Mungu kwa sadaka.

    Zingatia :Ndoto ni mlango Mungu anao utumia kupitisha ujumbe wake na shetani naye anatumia hivyo hivyo jifunze kuomba uongozi wa roho mtakatifu katika fasiri sahiii japo zingine uja kwa uchovu na shughuli nyingi.

    Ok naitwa Sylvester Mwakabende wa (Build new eden)
    Unaweza share somo hili kwa rafiki wengine.
    Simu no :0622625340
    Habari ya usiku ndugu zangu ni siku ya nne leo japo kwa kuchelewe tunaendelea na mwendelezo wa fasiri za ndoto kiblia . *Ungana nami Sylvester Mwakabende kwa ufafanuzi zaidi kadiri roho wa Bwana Atakavyo niongoza* *Je umewai kuota unafukuzwa na mbwa ? nini maana yake*? . Zaburi 22:16 *[16]Kwa maana mbwa wamenizunguka Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenizua mikono na miguu* For dogs have compassed me: the assembly of the wicked have inclosed me: they pierced my hands and my feet. 1.Kufuatiliwa na roho chafu kama zinaa na uasherati Mithali26:11 SUV *Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena.* Kutoka 22:31 BHN *Nyinyi mtakuwa watu waliowekwa wakfu kwangu. Kwa hiyo hamtakula nyama ya mnyama aliyeuawa na mnyama wa porini. Nyama hiyo mtawatupia mbwa.* Chochote kile kilicho kichafu upaswi kukila . Torati 23:18 BHN *Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yoyote; kwani haya ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako, yote mawili.* 2wafalme 9;10 Zaburi 22;20 BHN *Iokoe nafsi yangu mbali na upanga, yaokoe maisha yangu makuchani mwa mbwa hao!* *Mbwa ana nguvu maana yake mbwa anawakilisha roho chafu za zinaa, uasherati na machafu yote ya shetani .* . 2.kuiacha njia ya bwana kama kuhani. Isaya 56:11 BHN *Hao ni kama mbwa wenye uchu sana, wala hawawezi kamwe kutoshelezwa. Wachungaji hao hawana akili yoyote; kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe.* Naombaje ?NAMNA YA KUOMBA 1.Toba ya kweli kwa sababu ya kufungua mlango . 2.kuhalibu kila njia ya uovu inayo kufuatilia 3.Muone kuhani kwa ajiri ya ukombozi . 4.kataa kabisa roho za uharibifu kwa kusimamisha madhabau ya Mungu kwa sadaka. Zingatia :Ndoto ni mlango Mungu anao utumia kupitisha ujumbe wake na shetani naye anatumia hivyo hivyo jifunze kuomba uongozi wa roho mtakatifu katika fasiri sahiii japo zingine uja kwa uchovu na shughuli nyingi. Ok naitwa Sylvester Mwakabende wa (Build new eden) Unaweza share somo hili kwa rafiki wengine. Simu no :0622625340
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 443 Views
  • Habari ya jion tena .leo tunaendelea tena na tafsiri ya ndoto kiroho kwa kutumia biblia .

    Ukiota ndoto umekaa na viongozi wakuu wanchi ,unawawakilisha au hata unashare nao majukumu au company ywko ndotoni nini maana yake.?

    Mithali 18:16

    1.Ndoto hii inaashiria karama au kibali kinacho kuja mbele yako au uwezo wako wa ndani rohoni jinsi unavyo tizamwa.

    2.Inawakilisha kuwa kuna msimu mpya unakuja na nafasi mpya njema katika maisha yako.

    3. Inaonyesha pia unaweza ukawa unashare naye destiny huyo kiongozi yaani rohoni mko level moja sasa inategemea huyo uongozi wake msingi wake ni upi?


    Mwanzo 40:9-23 wote waliota ndoto zinazo elekeana lakini hazikufanana

    4.Unaukuu ndani yako wa kiuongozi ni vile tu umejisahau sana .anza kuliishi kusudi lako ili uifikie hatma yako.
    Zaburi 113:7-8

    Maana ya jumla .
    Viongozi katika ndotocwanawakilisha roho yenye mamlaka ya kutawala na yenye nguvu wakutawala na kumiliki juu ya nchi.

    Unapo wakilisha wakuu au kuona nafasi ya ukuu ndani yako wanawakikisha kutiwa mafuta kwa nafsi yako ili upate kuwa mtu fulani katika nchi.

    Ndoto za ukuu mara nyingi zinakuwaga na vita sana zinataka kusimama sana na Mungu kwani ukitaka kuona msome yusuph katika mwanzo 37

    NB .Kuota swala moja na kutimia swala moja ili litimie lazima ujifunze namna ya kuomba Mungu.

    Namna ya kuomba .

    1.kuwa mtu wa imani amini anza kuomba rehema na shukrani.

    2.Omba Mungu aifanikishe isibaki kuwa ndoto tu (ndoto iliyo zuiwa rohoni)

    3.Chuchumilia mbele za Mungu mpaka itimie kwa mifungo mingi na maombi mengi sana.

    4.Kama kuna nafasi chuku hatua ya kuomba Mungu akusogezee watu sahii ambao wanaweza kuwa wakuu.

    Ok naitwa sylvester kutoka (build new eden.
    Habari ya jion tena .leo tunaendelea tena na tafsiri ya ndoto kiroho kwa kutumia biblia . Ukiota ndoto umekaa na viongozi wakuu wanchi ,unawawakilisha au hata unashare nao majukumu au company ywko ndotoni nini maana yake.? Mithali 18:16 1.Ndoto hii inaashiria karama au kibali kinacho kuja mbele yako au uwezo wako wa ndani rohoni jinsi unavyo tizamwa. 2.Inawakilisha kuwa kuna msimu mpya unakuja na nafasi mpya njema katika maisha yako. 3. Inaonyesha pia unaweza ukawa unashare naye destiny huyo kiongozi yaani rohoni mko level moja sasa inategemea huyo uongozi wake msingi wake ni upi? Mwanzo 40:9-23 wote waliota ndoto zinazo elekeana lakini hazikufanana 4.Unaukuu ndani yako wa kiuongozi ni vile tu umejisahau sana .anza kuliishi kusudi lako ili uifikie hatma yako. Zaburi 113:7-8 Maana ya jumla . Viongozi katika ndotocwanawakilisha roho yenye mamlaka ya kutawala na yenye nguvu wakutawala na kumiliki juu ya nchi. Unapo wakilisha wakuu au kuona nafasi ya ukuu ndani yako wanawakikisha kutiwa mafuta kwa nafsi yako ili upate kuwa mtu fulani katika nchi. Ndoto za ukuu mara nyingi zinakuwaga na vita sana zinataka kusimama sana na Mungu kwani ukitaka kuona msome yusuph katika mwanzo 37 NB .Kuota swala moja na kutimia swala moja ili litimie lazima ujifunze namna ya kuomba Mungu. Namna ya kuomba . 1.kuwa mtu wa imani amini anza kuomba rehema na shukrani. 2.Omba Mungu aifanikishe isibaki kuwa ndoto tu (ndoto iliyo zuiwa rohoni) 3.Chuchumilia mbele za Mungu mpaka itimie kwa mifungo mingi na maombi mengi sana. 4.Kama kuna nafasi chuku hatua ya kuomba Mungu akusogezee watu sahii ambao wanaweza kuwa wakuu. Ok naitwa sylvester kutoka (build new eden.
    Share on WhatsApp
    w.app
    WhatsApp Messenger: More than 2 billion people in over 180 countries use WhatsApp to stay in touch with friends and family, anytime and anywhere. WhatsApp is free and offers simple, secure, reliable messaging and calling, available on phones all over the world.
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 403 Views
  • Hakuna siku ambayo hupita nisipokufikiria, Mama.
    Ninakukosa kwa kila sehemu yangu—moyo wangu unauma kwa nyakati ambazo hatutawahi kuwa nazo, mambo ambayo hatutawahi kupata kushiriki.
    Lakini hata katika maumivu haya, najua bado uko pamoja nami.
    Upendo wako huishi ndani yangu, katika masomo uliyonifundisha, kwa jinsi ninavyojaribu kuishi kila siku kwa nguvu, neema, na upendo.
    Unaweza kuwa mbali na macho yangu, lakini kamwe kutoka kwa nafsi yangu.
    Siku zote nitakubeba moyoni mwangu.
    Nimekukumbuka, Mama. Sana.
    #mama
    Hakuna siku ambayo hupita nisipokufikiria, Mama. Ninakukosa kwa kila sehemu yangu—moyo wangu unauma kwa nyakati ambazo hatutawahi kuwa nazo, mambo ambayo hatutawahi kupata kushiriki. Lakini hata katika maumivu haya, najua bado uko pamoja nami. Upendo wako huishi ndani yangu, katika masomo uliyonifundisha, kwa jinsi ninavyojaribu kuishi kila siku kwa nguvu, neema, na upendo. Unaweza kuwa mbali na macho yangu, lakini kamwe kutoka kwa nafsi yangu. Siku zote nitakubeba moyoni mwangu. Nimekukumbuka, Mama. Sana. #mama
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 339 Views
  • Rais wa zamani wa Marekani , Barack Obama katika mahojiano na chuo cha Hamilton College Nchini humo aliongea kuhusu hali ya Nchi chini ya muhula wa pili wa Rais wa sasa Donald Trump na alikosoa vikali hatua za hivi karibuni za utawala huo.

    Rais huyo Mstaafu ambaye alitangulia muhula wa kwanza wa Trump, alimkosoa vikali Trump kwa juhudi zake za kubadilisha mfumo wa Serikali ya Shirikisho, kukandamiza uhamiaji na upinzani, pamoja na kuwatisha Wanahabari na Taasisi ya sheria.

    “Hivyo basi, hii ndio mara yangu ya kwanza kuzungumza hadharani kwa muda sasa,” Obama alisema wakati wa mahojiano jukwaani katika Chuo cha Hamilton. “Nimekuwa nikitazama kwa muda.”

    "Hebu fikiria kama ningekuwa nimefanya chochote kati ya haya,”

    “Ni jambo lisilowezekana kufikirika kwamba vyama vilevile vinavyonyamaza sasa vingevumilia tabia kama hiyo kutoka kwangu, au hata kutoka kwa baadhi ya walionitangulia.” alisema Obama

    Obama aliendelea kusema kuwa haamini tangazo jipya la ushuru lililotolewa na Trump “litakuwa zuri kwa Marekani.” Hata hivyo, alieleza kuwa anahofia zaidi kile alichokiita kama uvunjaji wa haki unaofanywa na Ikulu.

    Rais wa zamani wa Marekani 馃嚭馃嚫, Barack Obama katika mahojiano na chuo cha Hamilton College Nchini humo aliongea kuhusu hali ya Nchi chini ya muhula wa pili wa Rais wa sasa Donald Trump na alikosoa vikali hatua za hivi karibuni za utawala huo. Rais huyo Mstaafu ambaye alitangulia muhula wa kwanza wa Trump, alimkosoa vikali Trump kwa juhudi zake za kubadilisha mfumo wa Serikali ya Shirikisho, kukandamiza uhamiaji na upinzani, pamoja na kuwatisha Wanahabari na Taasisi ya sheria. “Hivyo basi, hii ndio mara yangu ya kwanza kuzungumza hadharani kwa muda sasa,” Obama alisema wakati wa mahojiano jukwaani katika Chuo cha Hamilton. “Nimekuwa nikitazama kwa muda.” "Hebu fikiria kama ningekuwa nimefanya chochote kati ya haya,” “Ni jambo lisilowezekana kufikirika kwamba vyama vilevile vinavyonyamaza sasa vingevumilia tabia kama hiyo kutoka kwangu, au hata kutoka kwa baadhi ya walionitangulia.” alisema Obama Obama aliendelea kusema kuwa haamini tangazo jipya la ushuru lililotolewa na Trump “litakuwa zuri kwa Marekani.” Hata hivyo, alieleza kuwa anahofia zaidi kile alichokiita kama uvunjaji wa haki unaofanywa na Ikulu.
    Love
    Like
    3
    0 Comments 0 Shares 559 Views
  • Rais wa Marekani , DonaldTrump, ameibua mjadala mkali baada ya kusema kuwa kuna uwezekano wa yeye kuwania muhula wa tatu, licha ya Katiba ya Marekani kupiga marufuku jambo hilo kupitia Marekebisho ya 22. Katika mahojiano na NBCNews, Rais huyo hakutaka kufuta uwezekano wa kuwania tena Urais baada ya kumaliza mihula miwili, akidai kuwa kuna njia za kufanya hilo kutokea. Alisisitiza kuwa "hakuwa anatania," jambo ambalo limeibua hofu miongoni mwa Wachambuzi wa siasa na Wanaharakati wa demokrasia Nchini humo.

    Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, Rais haruhusiwi kutawala kwa zaidi ya mihula miwili ya miaka minne minne. Marekebisho ya 22 yaliwekwa ili kuzuia Mtu mmoja kuwa na mamlaka ya muda mrefu kama ilivyokuwa kwa Franklin D. Roosevelt, ambaye altawala kwa zaidi ya mihula miwili kabla ya marekebisho hayo kuidhinishwa mwaka 1951.

    Kauli ya Trump imeibua maswali kuhusu mbinu anazoweza kutumia kutafuta muhula wa tatu. Wachambuzi wa sheria wanabainisha kuwa ili hilo litokee, ama katiba ibadilishwe rasmi kwa marekebisho mapya, au ipatikane tafsiri mpya ya kisheria inayomruhusu kugombea tena. Hata hivyo, mchakato wa kubadili katiba ni mgumu na unahitaji ridhaa ya Bunge pamoja na Majimbo mengi ya Marekani.

    Baadhi ya Wafuasi wa Donald Trump wameunga mkono kauli yake, wakidai kuwa anastahili muda zaidi wa kuongoza Nchi. Hata hivyo, Wakosoaji wake wanasema kuwa hatua yoyote ya kupindua Marekebisho ya 22 inaweza kuwa tishio kwa demokrasia ya Marekani na kuweka msingi wa uongozi wa kiimla.

    Rais wa Marekani 馃嚭馃嚫, DonaldTrump, ameibua mjadala mkali baada ya kusema kuwa kuna uwezekano wa yeye kuwania muhula wa tatu, licha ya Katiba ya Marekani kupiga marufuku jambo hilo kupitia Marekebisho ya 22. Katika mahojiano na NBCNews, Rais huyo hakutaka kufuta uwezekano wa kuwania tena Urais baada ya kumaliza mihula miwili, akidai kuwa kuna njia za kufanya hilo kutokea. Alisisitiza kuwa "hakuwa anatania," jambo ambalo limeibua hofu miongoni mwa Wachambuzi wa siasa na Wanaharakati wa demokrasia Nchini humo. Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, Rais haruhusiwi kutawala kwa zaidi ya mihula miwili ya miaka minne minne. Marekebisho ya 22 yaliwekwa ili kuzuia Mtu mmoja kuwa na mamlaka ya muda mrefu kama ilivyokuwa kwa Franklin D. Roosevelt, ambaye altawala kwa zaidi ya mihula miwili kabla ya marekebisho hayo kuidhinishwa mwaka 1951. Kauli ya Trump imeibua maswali kuhusu mbinu anazoweza kutumia kutafuta muhula wa tatu. Wachambuzi wa sheria wanabainisha kuwa ili hilo litokee, ama katiba ibadilishwe rasmi kwa marekebisho mapya, au ipatikane tafsiri mpya ya kisheria inayomruhusu kugombea tena. Hata hivyo, mchakato wa kubadili katiba ni mgumu na unahitaji ridhaa ya Bunge pamoja na Majimbo mengi ya Marekani. Baadhi ya Wafuasi wa Donald Trump wameunga mkono kauli yake, wakidai kuwa anastahili muda zaidi wa kuongoza Nchi. Hata hivyo, Wakosoaji wake wanasema kuwa hatua yoyote ya kupindua Marekebisho ya 22 inaweza kuwa tishio kwa demokrasia ya Marekani na kuweka msingi wa uongozi wa kiimla.
    0 Comments 0 Shares 609 Views
  • "Marekani mpaka sasa hawajasaini mkataba wa kuilinda Congo mchakato umekuwa mrefu. Jiulize vile vikwazo vya Magharibi walivyoiwekea Rwanda vimeishia wapi

    Kagame anajua anachokifanya ndio maana licha ya ripoti za UN , US na EU kuonyesha Rwanda wanaifadhili M23 plus Vikwazo hakuna kilichobadilika Congo

    Wanachokifanya wanaoibia Congo na Africa ni ile ile mbinu ya wakati wa ukoloni inaitwa "Divided and Rule " yaani wagawanywe uwatawale nakumbuka hii mbinu pia enzi hizo ndio iliyozaa utani wa jadi wa Yanga na Simba

    Oooh Africa " - Zungu, Mchambuzi wa Siasa na Mtangazaji.

    "Marekani mpaka sasa hawajasaini mkataba wa kuilinda Congo mchakato umekuwa mrefu. Jiulize vile vikwazo vya Magharibi walivyoiwekea Rwanda vimeishia wapi 馃榾馃榾馃榾馃榾 Kagame anajua anachokifanya ndio maana licha ya ripoti za UN , US na EU kuonyesha Rwanda wanaifadhili M23 plus Vikwazo hakuna kilichobadilika Congo 馃槶馃槶馃槶馃槶 Wanachokifanya wanaoibia Congo na Africa ni ile ile mbinu ya wakati wa ukoloni inaitwa "Divided and Rule " yaani wagawanywe uwatawale nakumbuka hii mbinu pia enzi hizo ndio iliyozaa utani wa jadi wa Yanga na Simba Oooh Africa馃實 馃槶" - Zungu, Mchambuzi wa Siasa na Mtangazaji.
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 704 Views
  • Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa , N’Golo Kanté, ameonyesha moyo wa upendo kwa jamii kwa kujenga hospitali ya kisasa yenye thamani ya dola milioni tano (5) Nchini Mali, ikiwa ni msaada kwa Watoto na familia zisizojiweza kupata huduma bora za afya.

    Kanté, ambaye alizaliwa Jijini Paris, Ufaransa, ana asili ya Mali, Wazazi wake wakiwa Wahamiaji waliotoka Nchini Mali mwaka 1980. Jina lake N’Golo linatokana na Mfalme wa zamani wa Mali aliyewahi kutawala. Katika ziara yake Mali, Kanté alitumia muda na familia yake huku akitoa heshima kwa Baba yake na Kaka yake Marehemu.

    Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa 馃嚝馃嚪, N’Golo Kanté, ameonyesha moyo wa upendo kwa jamii kwa kujenga hospitali ya kisasa yenye thamani ya dola milioni tano (5) Nchini Mali, ikiwa ni msaada kwa Watoto na familia zisizojiweza kupata huduma bora za afya. Kanté, ambaye alizaliwa Jijini Paris, Ufaransa, ana asili ya Mali, Wazazi wake wakiwa Wahamiaji waliotoka Nchini Mali mwaka 1980. Jina lake N’Golo linatokana na Mfalme wa zamani wa Mali aliyewahi kutawala. Katika ziara yake Mali, Kanté alitumia muda na familia yake huku akitoa heshima kwa Baba yake na Kaka yake Marehemu.
    0 Comments 0 Shares 578 Views
  • Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa , N’Golo Kanté, ameonyesha moyo wa upendo kwa jamii kwa kujenga hospitali ya kisasa yenye thamani ya dola milioni tano (5) Nchini Mali, ikiwa ni msaada kwa Watoto na familia zisizojiweza kupata huduma bora za afya.

    Kanté, ambaye alizaliwa Jijini Paris, Ufaransa, ana asili ya Mali, Wazazi wake wakiwa Wahamiaji waliotoka Nchini Mali mwaka 1980. Jina lake N’Golo linatokana na Mfalme wa zamani wa Mali aliyewahi kutawala. Katika ziara yake Mali, Kanté alitumia muda na familia yake huku akitoa heshima kwa Baba yake na Kaka yake Marehemu.
    Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa 馃嚝馃嚪, N’Golo Kanté, ameonyesha moyo wa upendo kwa jamii kwa kujenga hospitali ya kisasa yenye thamani ya dola milioni tano (5) Nchini Mali, ikiwa ni msaada kwa Watoto na familia zisizojiweza kupata huduma bora za afya. Kanté, ambaye alizaliwa Jijini Paris, Ufaransa, ana asili ya Mali, Wazazi wake wakiwa Wahamiaji waliotoka Nchini Mali mwaka 1980. Jina lake N’Golo linatokana na Mfalme wa zamani wa Mali aliyewahi kutawala. Katika ziara yake Mali, Kanté alitumia muda na familia yake huku akitoa heshima kwa Baba yake na Kaka yake Marehemu.
    0 Comments 0 Shares 590 Views
  • PICHA YA SIMBA HUYU NI FUNZO MAISHANI:
    ------------------------------------------------------

    Hivi ndivyo mfalme wa pori anavyoonekana akiwa kwenye siku za mwisho za maisha yake. Jinsi alivyokonda, kujua idadi ya mbavu zake hata huitaji msaada wa calculator.

    Hii picha ilipigwa na "Larry Pannell."

    Alifanikiwa kupata picha ya Simba aliyekuwa kwenye hitimisho la kuvuta pumzi za mwisho. Katika huu ulimwengu wenye mafungamano na dhambi.

    "Larry Pannell" anasema:

    Nilimkuta huyu simba amelala kwenye majani. Akiwa amechoka, miguu ikionekana kumnyima ushirikiano wa kutembea.

    Sikuwa na lakufanya zaidi ya kusimama mita kadhaa. Macho yakifanya ushuhuda wa kutazama, "King of savannah" akipoteza uhai chini ya kivuli cha mti.

    Nikiwa nimesimama kimya. Nilishusha chini camera yangu. Tulitazamana na simba, tukafumba macho yetu pamoja.

    Jinsi mfalme wa nyika alivyokuwa akihangaika kuhema. Pumzi zilionekana kuwa bidhaa hadimu kwenye duka la mapafu yake.

    Kifua chake kilikuwa kikipanda na kushuka. Ishara ya kuonyesha anavuta pumzi za mwisho, kabla ya kukipa ruhusa kifo kiondoke na roho yake.

    Ghafla eneo alilolala Simba ukazaliwa ukimya. Mfalme wa pori akawa haemi wala kutikisika. Mauti ikawa imehitimisha simulizi ya ubabe wake mbugani.

    Hakika maisha ya binadamu na wanyama ni simulizi fupi sana."

    Haijalishi una nguvu kiasi gani. Kuna nyakati zitafika nguvu zitafanya mgomo wa kuishi mwilini mwako. Zitaupisha udhaifu uchukue nafasi ya kukutawala. Udhaifu nao ukikutawala, utayaita maradhi. Bila hiyari utajikuta umekigeuza kitanda kuwa rafiki."

    Kuna shule ya bure hapa: Nguvu tulizonazo ni kitu cha kupita. Hata uzuri umpao kiburi mwanamke una ukomo. Licha ya kujidanganya kwa make up na wanja. Lakini hawezi kuzuia muanguko wa mashavu, uzee unapoanza kumuondoa kwenye kundi la warembo.

    "Chini ya jua kila kitu kina mwanzo na mwisho."

    Hivyo katika maisha tusisahau kuvipa kipaumbele vitu hivi. Utu, wema, ukarimu, heshima, na unyenyekevu.

    Tusaidie wenye maradhi, tuwajali wasiojiweza, na viongozi tusitumie madaraka vibaya.

    Tutende mema tukiamini. Kuna siku pumzi zitamaliza mkataba wa kuishi ndani ya matundu ya pua zetu. Baada ya hapo sisi wote tutalala mauti."

    Imeandikwa na Green Osward
    PICHA YA SIMBA HUYU NI FUNZO MAISHANI: ------------------------------------------------------ Hivi ndivyo mfalme wa pori anavyoonekana akiwa kwenye siku za mwisho za maisha yake. Jinsi alivyokonda, kujua idadi ya mbavu zake hata huitaji msaada wa calculator. Hii picha ilipigwa na "Larry Pannell." Alifanikiwa kupata picha ya Simba aliyekuwa kwenye hitimisho la kuvuta pumzi za mwisho. Katika huu ulimwengu wenye mafungamano na dhambi. "Larry Pannell" anasema: Nilimkuta huyu simba amelala kwenye majani. Akiwa amechoka, miguu ikionekana kumnyima ushirikiano wa kutembea. Sikuwa na lakufanya zaidi ya kusimama mita kadhaa. Macho yakifanya ushuhuda wa kutazama, "King of savannah" akipoteza uhai chini ya kivuli cha mti. Nikiwa nimesimama kimya. Nilishusha chini camera yangu. Tulitazamana na simba, tukafumba macho yetu pamoja. Jinsi mfalme wa nyika alivyokuwa akihangaika kuhema. Pumzi zilionekana kuwa bidhaa hadimu kwenye duka la mapafu yake. Kifua chake kilikuwa kikipanda na kushuka. Ishara ya kuonyesha anavuta pumzi za mwisho, kabla ya kukipa ruhusa kifo kiondoke na roho yake. Ghafla eneo alilolala Simba ukazaliwa ukimya. Mfalme wa pori akawa haemi wala kutikisika. Mauti ikawa imehitimisha simulizi ya ubabe wake mbugani. Hakika maisha ya binadamu na wanyama ni simulizi fupi sana." Haijalishi una nguvu kiasi gani. Kuna nyakati zitafika nguvu zitafanya mgomo wa kuishi mwilini mwako. Zitaupisha udhaifu uchukue nafasi ya kukutawala. Udhaifu nao ukikutawala, utayaita maradhi. Bila hiyari utajikuta umekigeuza kitanda kuwa rafiki." Kuna shule ya bure hapa: Nguvu tulizonazo ni kitu cha kupita. Hata uzuri umpao kiburi mwanamke una ukomo. Licha ya kujidanganya kwa make up na wanja. Lakini hawezi kuzuia muanguko wa mashavu, uzee unapoanza kumuondoa kwenye kundi la warembo. "Chini ya jua kila kitu kina mwanzo na mwisho." Hivyo katika maisha tusisahau kuvipa kipaumbele vitu hivi. Utu, wema, ukarimu, heshima, na unyenyekevu. Tusaidie wenye maradhi, tuwajali wasiojiweza, na viongozi tusitumie madaraka vibaya. Tutende mema tukiamini. Kuna siku pumzi zitamaliza mkataba wa kuishi ndani ya matundu ya pua zetu. Baada ya hapo sisi wote tutalala mauti." Imeandikwa na Green Osward
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 991 Views
  • EPUKA MAISHA FEKI YA KIJAMII...

    Tunaishi katika zama ambazo watu hawafanyi kazi tena ili kufanikiwa; wanafanya kazi ili waonekane wamefanikiwa. Ambapo watu hawatafuti tena uzuri wa kweli, lakini udanganyifu wa uzuri. Na ambapo mahusiano hayahusu tena upendo, bali kuhusu kuonyesha toleo lililohaririwa kwa uangalifu la upendo. Shida ni kwamba wanaume wa kisasa hutumia mitandao ya kijamii kughushi mafanikio yao. Wanawake wa kisasa hutumia mitandao ya kijamii kudanganya uzuri wao. Na wawili hawa wanapoingia kwenye uhusiano, wote wawili hutumia mitandao ya kijamii kughushi furaha yao. Hii ina maana gani? Inamaanisha kwamba tunaishi katika ulimwengu wa udanganyifu. Ulimwengu ambao wengi hawajaribu kujenga utajiri wa kweli, wanajaribu tu kuonekana matajiri. Ulimwengu ambapo wanawake wengi hawafanyi kazi juu ya tabia zao, wanafanya kazi tu kwenye vichungi. Ulimwengu ambao uhusiano hauhusu upendo na uaminifu, lakini ni nani anayechapisha picha bora za 'malengo ya wanandoa'. Mafanikio si utendaji wa hadhira. Haipimwi kwa magari, saa, au likizo zilizochapishwa mtandaoni. Mafanikio ni safari, sio post. Walakini, wanaume wa kisasa wanadanganya. Wanaazima magari ili kupiga picha, hukodisha vyumba vya bei ghali ili kuwavutia watu wasiowajua, na kuvaa chapa ambazo hawawezi kumudu. Katika mchakato huo, wanajipoteza. Wanazingatia zaidi kuonekana tajiri kuliko kuwa tajiri.

    Ulimwengu hautoi thawabu kwa kuonekana; inatuza vitu. Unaweza kudanganya watu mtandaoni, lakini huwezi kudanganya ukweli. Ukijifanya kuwa umefanikiwa bila msingi wa bidii, nidhamu na hekima, muda utakuweka wazi. Anasa iliyokodishwa haiwezi kudumisha mawazo duni. Wanawake wa kisasa, pia, wameanguka katika mtego huu. Uzuri sio asili tena; sasa ni bandia. Wengi hutegemea vichungi, upasuaji, na uhariri mzito. Badala ya kuimarisha roho zao, wanaboresha picha zao. Badala ya kujenga akili zao, wanajenga udanganyifu. Lakini nini kinatokea wakati ukweli unakutana na udanganyifu? Ni nini hufanyika wakati kichujio kinapozimwa? Mwanamke ambaye ni mrembo tu mtandaoni lakini hana tabia katika maisha halisi atawavutia wanaume wanaopenda udanganyifu tu, si uhalisia. Wanaume halisi hawatafuti vichungi; wanatafuta wema, wema, akili, kwa mwanamke ambaye uzuri wake si usoni tu bali moyoni. Kwangu mimi, mitandao ya kijamii ni chombo, si kioo cha maisha. Haipaswi kufafanua wewe ni nani. Mafanikio ya mwanamume hayatokani na jinsi mtindo wake wa maisha unavyoonekana ghali mtandaoni, lakini katika uhalisia jinsi alivyo na nidhamu, uchapakazi na kuwajibika. Uzuri wa mwanamke sio jinsi uso wake unavyoonekana kwenye Instagram, lakini kwa jinsi roho, akili na tabia yake ilivyo nzuri katika maisha halisi. Furaha ya uhusiano haiko katika idadi ya likes na maoni inayopata, lakini kwa amani, upendo na umoja watu hao wawili hushiriki bila milango.

    Kuwa halisi. Fanyia kazi mafanikio yako ya kweli, sio picha yako ya mtandaoni. Kuza uzuri wako halisi, si tu uso wako uliochujwa. Jenga uhusiano wa kweli, sio hadithi ya hadithi ya Instagram. Kwa sababu mwisho wa siku ukweli utafichua udanganyifu kila wakati.

    Credit
    Rev.Albert Nwosu
    EPUKA MAISHA FEKI YA KIJAMII... Tunaishi katika zama ambazo watu hawafanyi kazi tena ili kufanikiwa; wanafanya kazi ili waonekane wamefanikiwa. Ambapo watu hawatafuti tena uzuri wa kweli, lakini udanganyifu wa uzuri. Na ambapo mahusiano hayahusu tena upendo, bali kuhusu kuonyesha toleo lililohaririwa kwa uangalifu la upendo. Shida ni kwamba wanaume wa kisasa hutumia mitandao ya kijamii kughushi mafanikio yao. Wanawake wa kisasa hutumia mitandao ya kijamii kudanganya uzuri wao. Na wawili hawa wanapoingia kwenye uhusiano, wote wawili hutumia mitandao ya kijamii kughushi furaha yao. Hii ina maana gani? Inamaanisha kwamba tunaishi katika ulimwengu wa udanganyifu. Ulimwengu ambao wengi hawajaribu kujenga utajiri wa kweli, wanajaribu tu kuonekana matajiri. Ulimwengu ambapo wanawake wengi hawafanyi kazi juu ya tabia zao, wanafanya kazi tu kwenye vichungi. Ulimwengu ambao uhusiano hauhusu upendo na uaminifu, lakini ni nani anayechapisha picha bora za 'malengo ya wanandoa'. Mafanikio si utendaji wa hadhira. Haipimwi kwa magari, saa, au likizo zilizochapishwa mtandaoni. Mafanikio ni safari, sio post. Walakini, wanaume wa kisasa wanadanganya. Wanaazima magari ili kupiga picha, hukodisha vyumba vya bei ghali ili kuwavutia watu wasiowajua, na kuvaa chapa ambazo hawawezi kumudu. Katika mchakato huo, wanajipoteza. Wanazingatia zaidi kuonekana tajiri kuliko kuwa tajiri. Ulimwengu hautoi thawabu kwa kuonekana; inatuza vitu. Unaweza kudanganya watu mtandaoni, lakini huwezi kudanganya ukweli. Ukijifanya kuwa umefanikiwa bila msingi wa bidii, nidhamu na hekima, muda utakuweka wazi. Anasa iliyokodishwa haiwezi kudumisha mawazo duni. Wanawake wa kisasa, pia, wameanguka katika mtego huu. Uzuri sio asili tena; sasa ni bandia. Wengi hutegemea vichungi, upasuaji, na uhariri mzito. Badala ya kuimarisha roho zao, wanaboresha picha zao. Badala ya kujenga akili zao, wanajenga udanganyifu. Lakini nini kinatokea wakati ukweli unakutana na udanganyifu? Ni nini hufanyika wakati kichujio kinapozimwa? Mwanamke ambaye ni mrembo tu mtandaoni lakini hana tabia katika maisha halisi atawavutia wanaume wanaopenda udanganyifu tu, si uhalisia. Wanaume halisi hawatafuti vichungi; wanatafuta wema, wema, akili, kwa mwanamke ambaye uzuri wake si usoni tu bali moyoni. Kwangu mimi, mitandao ya kijamii ni chombo, si kioo cha maisha. Haipaswi kufafanua wewe ni nani. Mafanikio ya mwanamume hayatokani na jinsi mtindo wake wa maisha unavyoonekana ghali mtandaoni, lakini katika uhalisia jinsi alivyo na nidhamu, uchapakazi na kuwajibika. Uzuri wa mwanamke sio jinsi uso wake unavyoonekana kwenye Instagram, lakini kwa jinsi roho, akili na tabia yake ilivyo nzuri katika maisha halisi. Furaha ya uhusiano haiko katika idadi ya likes na maoni inayopata, lakini kwa amani, upendo na umoja watu hao wawili hushiriki bila milango. Kuwa halisi. Fanyia kazi mafanikio yako ya kweli, sio picha yako ya mtandaoni. Kuza uzuri wako halisi, si tu uso wako uliochujwa. Jenga uhusiano wa kweli, sio hadithi ya hadithi ya Instagram. Kwa sababu mwisho wa siku ukweli utafichua udanganyifu kila wakati. Credit Rev.Albert Nwosu
    0 Comments 0 Shares 988 Views
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili hali ya usalama na kibinadamu Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku hali ikizidi kuzorota. Mwakilishi Maalum wa Umoja huo (UN) Nchini DR Congo, Bintou Keita, amesema Waasi wa kundi la M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda sasa wanadhibiti maeneo makubwa ya Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini na kutishia kupanua mashambulizi yao hadi Mkoani Tshopo na Maniema.

    "Hivi karibuni M23 imesimika utawala wake kwa kuteua gavana, makamu gavana na meya huko Bukavu, Kivu Kusini," amesema Keita.

    Ameeleza kuwa mgogoro huo unahusiana na unyonyaji wa madini mashariki mwa DR Congo na kuzua wasiwasi wa kikanda. Pia amegusia hali mbaya ya kibinadamu, akisema kumekuwa na ongezeko la ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara na ajira ya kulazimishwa kwa Vijana, wakiwemo Watoto.

    Licha ya makubaliano ya hivi karibuni kati ya Marais wa Rwanda na DR Congo Nchini Qatar , amani bado haijapatikana. Keita ametoa wito wa kuteuliwa kwa mpatanishi wa Umoja wa Afrika ili kuongoza juhudi za kusitisha mapigano.

    Balozi wa DR Congo katika Baraza la Umoja wa kimataifa (UN), Zénon Mukongo Ngay, ameishutumu Rwanda kwa kutotekeleza usitishaji mapigano, huku Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, akisema Nchi yake itaendelea kuchukua "hatua za ulinzi" mpaka kuwe na mfumo wa kudumu wa usalama.

    Wakati huo huo, imeripotiwa kuwa DR Congo inakabiliwa na janga kubwa zaidi la njaa kuwahi kutokea, ambapo Watu zaidi ya milioni 27.7 wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na vita na ukosefu wa utulivu mashariki mwa Nchi hiyo.

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili hali ya usalama na kibinadamu Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 馃嚚馃嚛 huku hali ikizidi kuzorota. Mwakilishi Maalum wa Umoja huo (UN) Nchini DR Congo, Bintou Keita, amesema Waasi wa kundi la M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda 馃嚪馃嚰 sasa wanadhibiti maeneo makubwa ya Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini na kutishia kupanua mashambulizi yao hadi Mkoani Tshopo na Maniema. "Hivi karibuni M23 imesimika utawala wake kwa kuteua gavana, makamu gavana na meya huko Bukavu, Kivu Kusini," amesema Keita. Ameeleza kuwa mgogoro huo unahusiana na unyonyaji wa madini mashariki mwa DR Congo na kuzua wasiwasi wa kikanda. Pia amegusia hali mbaya ya kibinadamu, akisema kumekuwa na ongezeko la ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara na ajira ya kulazimishwa kwa Vijana, wakiwemo Watoto. Licha ya makubaliano ya hivi karibuni kati ya Marais wa Rwanda na DR Congo Nchini Qatar 馃嚩馃嚘, amani bado haijapatikana. Keita ametoa wito wa kuteuliwa kwa mpatanishi wa Umoja wa Afrika ili kuongoza juhudi za kusitisha mapigano. Balozi wa DR Congo katika Baraza la Umoja wa kimataifa (UN), Zénon Mukongo Ngay, ameishutumu Rwanda kwa kutotekeleza usitishaji mapigano, huku Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, akisema Nchi yake itaendelea kuchukua "hatua za ulinzi" mpaka kuwe na mfumo wa kudumu wa usalama. Wakati huo huo, imeripotiwa kuwa DR Congo inakabiliwa na janga kubwa zaidi la njaa kuwahi kutokea, ambapo Watu zaidi ya milioni 27.7 wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na vita na ukosefu wa utulivu mashariki mwa Nchi hiyo.
    0 Comments 0 Shares 670 Views
  • VITABU VYENYE NGUVU DUNIANI AMBAVYO HAUTAFUNDISHWA SHULENI: SIRI KUBWA YA UTAJIRI WA ULIMWENGU!

    Je, umefundishwa katika dini yako kuwa Biblia na Quran ndio vitabu pekee vyenye nguvu na maajabu? Ni kweli vitabu hivi ni miongoni mwa vitabu vyenye maajabu, ila kuna baddhi ya vitabu vinavyofichwa kutokana na nguvu zake za kubadili maisha ya watu, kwa utajiri ama wakawa masikini wa kutupwa na hata kuwa wenye mikosi mikubwa.

    Dunia imejawa siri ambazo wachache wanazitumia kujinufaisha na kujitajirisha, huku wakiwadanganya wengine Kuwa ili ufanikiwe basi wafaa upate muda wa kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa, uwe mvumilivu, Ufanye kazi kwa bidii na mambo mengine mengi,
    lakini hawakuambii mambo ya siri wanayoyafanya na vitabu vya siri wanavyosoma ili kukuza utajiri wao na mvuto wao katika ulimwengu.

    Leo hii nimekuletea vitabu vya siri zaidi ya Biblia na Quran, vyenye nguvu sana, na vinavyotumika kubadili maisha ya Matajiri wa dunia hii, na imebakia kuwa siri kwao, wakiificha kwa nguvu zote na kuhakikisha wachache wanaifahamu, huku wengi wakitiwa hofu ya kuiogopa siri hii na kuviona vitabu hivi kama vya mashetani.

    1. The Book of Abramelin the Mage – Kitabu cha kale cha uchawi kinachoeleza njia za kuwasiliana na malaika na nguvu za kichawi. Kitabu hiki kina nguvu za kukufundisha ushirikina na upeo wa juu unaopita uwezo wa kawaida wa mwanadamu.

    2.The Lesser Key of Solomon (Lemegeton) – Kitabu cha uchawi kinachodaiwa kuwa na mafundisho ya mfalme Sulemani kuhusu majini na roho. Ni kitabu kinachosadikika kuandikwa na mfalme wa Israel ajulikanaye kama sulemani, kikiwa kimejaa elimu ya kiroho, na namna ya kuyatumia majini katika shughuli za kila siku bila kutumia nguvu kubwa.

    3.Picatrix – Kitabu cha uchawi wa Kiarabu kinachoeleza jinsi ya kutumia nyota na sayari kwa utajiri. Masomo mengi yanayohusiana na nyota pamoja na bahati, hutolewa katika kitabu hiki cha ajabu. Kuna matamshi ya kiarabu katika kitabu hiki yenye nguvu ya kuleta maajabu usiyotarajia, ambayo sitayasema katika makala hii kwa kuwa sifundishi uchawi, nafunua siri zilizofichwa na mabeberu wachache ili waendelee kuitawala dunia hii kiuchumi na kuwa na nguvu ya ushawishi.

    4.The Kybalion – Kitabu cha Hermeticism kinachofundisha sheria saba za ulimwengu zinazodaiwa kuwa na nguvu za kimetafizikia, zinazoleta mvuto kwa watu wanaokutazama, ushawishi kwa wanaokusikiliza na Nguvu ya fedha.

    5. The Secret (Rhonda Byrne) – Kitabu kinachoelezea sheria ya mvutano (Law of Attraction) na jinsi ya kutumia mawazo kuvutia mafanikio na utajiri. Kitabu hiki ni cha ajabu maana kimejawa na siri zenye uwezo wa Kubadili uchumi wako.

    6. Necronomicon – Ingawa ni kitabu cha kubuniwa na H.P. Lovecraft, kimekuwa na hadithi nyingi zinazodai kuwa kina maelezo ya siri za ulimwengu. Usisome kitabu hiki maana kinaweza kuleta shida maishani mwako bila kupata mwongozo kamili.

    7.The Voynich Manuscript – Kitabu cha ajabu kilichoandikwa kwa lugha isiyojulikana na hakijafasiriwa hadi sasa. Kimekosa tafsiri yake kutokana na ukweli kuwa kiliandikwa katika lugha ambayo haipo hapa duniani, ama ilikuwapo ila imepotea.

    Vitabu hivi ndivyo vinavyowafanya watu kuwa na mvuto, na utajiri mkubwa duniani. Kwa kweli huwezi kuwa na mvuto mkubwa ama utajiri mkubwa duniani pasina kusoma vitabu hivi na kufuata kanuni zake, wenda kama utakuwa tajiri kijijini kwenu lakini si duniani.

    Nikiwa namalizia, kuna Vitabu vyenye nguvu ya kukutajirisha, vyenye nguvu ya kukulaani na hata kukuletea mikosi isiyokoma, ambavyo vimekuwa vikihifadhiwa kwa siri sana, ili kutumiwa na wachache kwa malengo mahususi. Wapo watu kadhaa wanaopinga nguvu ya maandishi katika vitabu wakiidharau na kuyaona maandishi kama herufi za kawaida sana, lakini ukweli ni kuwa kuna nguvu katika vitabu, kuna maajabu katika vitabu na kuna watu waliofunga maisha yao kwa kusoma vifungu fulani kimakosa katika vitabu. Hebu kuwa makini na kila kitabu unachosoma. Hakikisha kwanza kitabu usomacho ni salama, maana kuna vitabu kama vile "Necronomicon, The book of Soyga, The grand Grimoire, n.k" vinavyoweza kukuletea shida na hata mikosi maishani mwako.
    VITABU VYENYE NGUVU DUNIANI AMBAVYO HAUTAFUNDISHWA SHULENI: SIRI KUBWA YA UTAJIRI WA ULIMWENGU! Je, umefundishwa katika dini yako kuwa Biblia na Quran ndio vitabu pekee vyenye nguvu na maajabu? Ni kweli vitabu hivi ni miongoni mwa vitabu vyenye maajabu, ila kuna baddhi ya vitabu vinavyofichwa kutokana na nguvu zake za kubadili maisha ya watu, kwa utajiri ama wakawa masikini wa kutupwa na hata kuwa wenye mikosi mikubwa. Dunia imejawa siri ambazo wachache wanazitumia kujinufaisha na kujitajirisha, huku wakiwadanganya wengine Kuwa ili ufanikiwe basi wafaa upate muda wa kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa, uwe mvumilivu, Ufanye kazi kwa bidii na mambo mengine mengi, lakini hawakuambii mambo ya siri wanayoyafanya na vitabu vya siri wanavyosoma ili kukuza utajiri wao na mvuto wao katika ulimwengu. Leo hii nimekuletea vitabu vya siri zaidi ya Biblia na Quran, vyenye nguvu sana, na vinavyotumika kubadili maisha ya Matajiri wa dunia hii, na imebakia kuwa siri kwao, wakiificha kwa nguvu zote na kuhakikisha wachache wanaifahamu, huku wengi wakitiwa hofu ya kuiogopa siri hii na kuviona vitabu hivi kama vya mashetani. 1. The Book of Abramelin the Mage – Kitabu cha kale cha uchawi kinachoeleza njia za kuwasiliana na malaika na nguvu za kichawi. Kitabu hiki kina nguvu za kukufundisha ushirikina na upeo wa juu unaopita uwezo wa kawaida wa mwanadamu. 2.The Lesser Key of Solomon (Lemegeton) – Kitabu cha uchawi kinachodaiwa kuwa na mafundisho ya mfalme Sulemani kuhusu majini na roho. Ni kitabu kinachosadikika kuandikwa na mfalme wa Israel ajulikanaye kama sulemani, kikiwa kimejaa elimu ya kiroho, na namna ya kuyatumia majini katika shughuli za kila siku bila kutumia nguvu kubwa. 3.Picatrix – Kitabu cha uchawi wa Kiarabu kinachoeleza jinsi ya kutumia nyota na sayari kwa utajiri. Masomo mengi yanayohusiana na nyota pamoja na bahati, hutolewa katika kitabu hiki cha ajabu. Kuna matamshi ya kiarabu katika kitabu hiki yenye nguvu ya kuleta maajabu usiyotarajia, ambayo sitayasema katika makala hii kwa kuwa sifundishi uchawi, nafunua siri zilizofichwa na mabeberu wachache ili waendelee kuitawala dunia hii kiuchumi na kuwa na nguvu ya ushawishi. 4.The Kybalion – Kitabu cha Hermeticism kinachofundisha sheria saba za ulimwengu zinazodaiwa kuwa na nguvu za kimetafizikia, zinazoleta mvuto kwa watu wanaokutazama, ushawishi kwa wanaokusikiliza na Nguvu ya fedha. 5. The Secret (Rhonda Byrne) – Kitabu kinachoelezea sheria ya mvutano (Law of Attraction) na jinsi ya kutumia mawazo kuvutia mafanikio na utajiri. Kitabu hiki ni cha ajabu maana kimejawa na siri zenye uwezo wa Kubadili uchumi wako. 6. Necronomicon – Ingawa ni kitabu cha kubuniwa na H.P. Lovecraft, kimekuwa na hadithi nyingi zinazodai kuwa kina maelezo ya siri za ulimwengu. Usisome kitabu hiki maana kinaweza kuleta shida maishani mwako bila kupata mwongozo kamili. 7.The Voynich Manuscript – Kitabu cha ajabu kilichoandikwa kwa lugha isiyojulikana na hakijafasiriwa hadi sasa. Kimekosa tafsiri yake kutokana na ukweli kuwa kiliandikwa katika lugha ambayo haipo hapa duniani, ama ilikuwapo ila imepotea. Vitabu hivi ndivyo vinavyowafanya watu kuwa na mvuto, na utajiri mkubwa duniani. Kwa kweli huwezi kuwa na mvuto mkubwa ama utajiri mkubwa duniani pasina kusoma vitabu hivi na kufuata kanuni zake, wenda kama utakuwa tajiri kijijini kwenu lakini si duniani. Nikiwa namalizia, kuna Vitabu vyenye nguvu ya kukutajirisha, vyenye nguvu ya kukulaani na hata kukuletea mikosi isiyokoma, ambavyo vimekuwa vikihifadhiwa kwa siri sana, ili kutumiwa na wachache kwa malengo mahususi. Wapo watu kadhaa wanaopinga nguvu ya maandishi katika vitabu wakiidharau na kuyaona maandishi kama herufi za kawaida sana, lakini ukweli ni kuwa kuna nguvu katika vitabu, kuna maajabu katika vitabu na kuna watu waliofunga maisha yao kwa kusoma vifungu fulani kimakosa katika vitabu. Hebu kuwa makini na kila kitabu unachosoma. Hakikisha kwanza kitabu usomacho ni salama, maana kuna vitabu kama vile "Necronomicon, The book of Soyga, The grand Grimoire, n.k" vinavyoweza kukuletea shida na hata mikosi maishani mwako.
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 889 Views
  • Ahmed Ally, Msemaji wa klabu ya Simba SC

    Anatokea mwehu mmoja anamdhihaki huyu Rais au kikundi cha vijana wa hovyo wanadhihaki Mamlaka za mpira wetu, Hii Nchi uhuru umepitiliza sana

    Wallace Karia, TFF na Bodi ya Ligi Wanapaswa kuheshimiwa, kuenziwa, kutunzwa na kulindwa maana wamefanya kazi kubwa na wanaendelea kufanya kazi kubwa kwenye mpira wetu

    Yote tuliyokua tunayaota kwenye mpira sasa hivi yanatokea, yale tuliyodhani ni magumu kwa Karia yamewezekana

    Na kama haitoshi tunaiona kesho njema ya mpira wa Tanzania chini ya Karia na wenzake

    President @wallacekaria na Uongozi wako wa TFF na Bodi ya ligi msirudi nyuma na msikubali mtu akaturudisha nyuma sasa hivi tunawaza World Cup tunawaza Utawala wa AFCON na Ubingwa Afrika ngazi klabu

    KAMA HUMPENDI KARIA PENDA MAFANIKIO YAKE"

    Ahmed Ally, Msemaji wa klabu ya Simba SC 鉁嶏笍 Anatokea mwehu mmoja anamdhihaki huyu Rais au kikundi cha vijana wa hovyo wanadhihaki Mamlaka za mpira wetu, Hii Nchi uhuru umepitiliza sana Wallace Karia, TFF na Bodi ya Ligi Wanapaswa kuheshimiwa, kuenziwa, kutunzwa na kulindwa maana wamefanya kazi kubwa na wanaendelea kufanya kazi kubwa kwenye mpira wetu Yote tuliyokua tunayaota kwenye mpira sasa hivi yanatokea, yale tuliyodhani ni magumu kwa Karia yamewezekana Na kama haitoshi tunaiona kesho njema ya mpira wa Tanzania chini ya Karia na wenzake President @wallacekaria na Uongozi wako wa TFF na Bodi ya ligi msirudi nyuma na msikubali mtu akaturudisha nyuma sasa hivi tunawaza World Cup tunawaza Utawala wa AFCON na Ubingwa Afrika ngazi klabu KAMA HUMPENDI KARIA PENDA MAFANIKIO YAKE"
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 576 Views
  • Kwenye barua ambayo Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imewajibu Yanga yenye kumbukumbu namba TPLB/2024/625 ya Machi 16,2025 imewaambia Yanga hawawezi kupewa alama tatu kutokana na kuwa hakuna KANUNI ya Ligi Kuu inayoamuru jambo hilo ambapo TPLB imewapa sababu takribani 10, nitazielezea kwa uchache.

    1. Mchezo ulighairishwa na Bodi majira ya saa8 Mchana ambapo baada ya Bodi huo hapakuwa na Afisa yoyote wa mchezo zaidi ya Watu wa Usalama.

    2. Hakuna taratibu zozote za mchezo zilizofanyika uwanjani kwa mujibu wa Kanuni ya 17 ikiwemo timu kukaguliwa na ili timu ipewe alama tatu na mabao matatu ilipaswa ukaguzi kufanyika na Maafisa ww Mchezo.

    3. Bodi ilishindwa kuruhusu mchezo uchezwe sio kwasababu Simba ALIGOMEA mechi bali kupitia Kamati ya Masaa 72 ikaamuru kupitia sababu mbalimbali za Kikanuni kughairisha mchezo huo baada ya kupokea pia ripoti mbalimbali kutoka Maafisa wa mchezo huo.

    4. Yanga SC wameambiwa kwamba hakuna Kanuni inasema Klabu Mgeni anapaswa kuwataarifu wao kwamba wanakuja kufanya mazoezi, hivyo suala la mawasiliano ni MWONGOZO tu wa Bodi hivyo Simba haikuvunja Kanuni kutowasiliana bali ilivunja MIONGOZO.

    5. Yanga SC wamejibiwa kuwa haitowapa alama tatu kwakuwa sababu za kughairisha mchezo zilikuwa ni za kiusalama, ambapo kulikuwa na tuhuma za rushwa, vitisho na kasoro za Kiusalama hivyo ingekuwa ngumu kuruhusu mchezo uendelee ambao ungeleta kasoro, kabla, wakati na baada ya mchezo.

    6. Yanga SC wanalaumiwa na Bodi kitendo cha kupeleka timu uwanjani wakati mechi imeshaghairishwa ni kinyume na Kanuni ya 47(18) na imeonesha kupingana na Mamlaka.

    7. Kuhusu gharama za mchezo ambazo Yanga wameziingia Bodi inasema itazighulikia Kikanuni.

    8. Bodi imewatakia Yanga maandalizi mema ya mchezo ujao wa Derby ambapo watawapangia rasmi tarehe.
    Etc.

    Kwenye barua ambayo Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imewajibu Yanga yenye kumbukumbu namba TPLB/2024/625 ya Machi 16,2025 imewaambia Yanga hawawezi kupewa alama tatu kutokana na kuwa hakuna KANUNI ya Ligi Kuu inayoamuru jambo hilo ambapo TPLB imewapa sababu takribani 10, nitazielezea kwa uchache. 1. Mchezo ulighairishwa na Bodi majira ya saa8 Mchana ambapo baada ya Bodi huo hapakuwa na Afisa yoyote wa mchezo zaidi ya Watu wa Usalama. 2. Hakuna taratibu zozote za mchezo zilizofanyika uwanjani kwa mujibu wa Kanuni ya 17 ikiwemo timu kukaguliwa na ili timu ipewe alama tatu na mabao matatu ilipaswa ukaguzi kufanyika na Maafisa ww Mchezo. 3. Bodi ilishindwa kuruhusu mchezo uchezwe sio kwasababu Simba ALIGOMEA mechi bali kupitia Kamati ya Masaa 72 ikaamuru kupitia sababu mbalimbali za Kikanuni kughairisha mchezo huo baada ya kupokea pia ripoti mbalimbali kutoka Maafisa wa mchezo huo. 4. Yanga SC wameambiwa kwamba hakuna Kanuni inasema Klabu Mgeni anapaswa kuwataarifu wao kwamba wanakuja kufanya mazoezi, hivyo suala la mawasiliano ni MWONGOZO tu wa Bodi hivyo Simba haikuvunja Kanuni kutowasiliana bali ilivunja MIONGOZO. 5. Yanga SC wamejibiwa kuwa haitowapa alama tatu kwakuwa sababu za kughairisha mchezo zilikuwa ni za kiusalama, ambapo kulikuwa na tuhuma za rushwa, vitisho na kasoro za Kiusalama hivyo ingekuwa ngumu kuruhusu mchezo uendelee ambao ungeleta kasoro, kabla, wakati na baada ya mchezo. 6. Yanga SC wanalaumiwa na Bodi kitendo cha kupeleka timu uwanjani wakati mechi imeshaghairishwa ni kinyume na Kanuni ya 47(18) na imeonesha kupingana na Mamlaka. 7. Kuhusu gharama za mchezo ambazo Yanga wameziingia Bodi inasema itazighulikia Kikanuni. 8. Bodi imewatakia Yanga maandalizi mema ya mchezo ujao wa Derby ambapo watawapangia rasmi tarehe. Etc.
    0 Comments 0 Shares 585 Views
  • Rais wa Nchi ya Rwanda , Paul Kagame ameionya Nchi ya Ubelgiji kuacha kutoa maagizo kwa Nchi yake na kuipangia cha kufanya utadhani kwamba Mungu amewapa jukumu na haki ya kuwasimamia ambapo amesema Rwanda haitokubali kutawaliwa tena na Wabelgji bali itapambana nao na itawashinda.

    Hayo ameyasema jana Jumapili Machi 16,2025 katika ukumbi wa BK Arena Nchini Rwanda, Kagame alinunuliwa akisema:

    “Nawaonya Wabelgi , Wabelgiji wameiharibu Rwanda, Wameua Wanyarwanda, tuliwaonya zamani na tunawaonya leo, wanasema ‘hawatuwaruhusu kufanya hiki na kile’ na sisi tunawauliza nyinyi ni nani?, nani kawapa jukumu la kutusimamia sisi?”

    “Wanyarwanda wanamuamini Mungu, mnaamini Mungu amewapa Wabelgiji jukumu la kuisimamia Rwanda?, kwa uwezo huu mdogo tulionao, tutapambana nao wote wanaotumia muda wao kututukana, kujaribu kututesa na hawatoweza kutushinda, watuache tuishi kwa amani, baada ya miaka yote tuliyotumia kupambana kuijenga Nchi yetu tunataka kuwa Wanyarwanda hatutaki kuwa Wabelgiji”

    “Rwanda kwa bahati mbaya tulitawaliwa na ka-nchi kadogo (Ubelgiji) ambayo ilienda mbali zaidi na kuigawa nchi yetu ili iwe ndogo kama nchi yao, sijawahi kusita kulieleza hili, tulilaani hili zamani na tutaendelea kulaani jambo hilo leo, hakuna kitu kibaya kitatokea kwetu kushinda majanga tuliyopitia huko nyuma, ndio maana hatupaswi kuogopa kusema na kujipambania sisi wenyewe dhidi ya wale wanaotaka kutuangamiza”

    Katika hatua nyingine, Serekali ya Rwanda imeawaamuru Wanadiplomasia wote wa Ubelgiji Nchini humo kuondoka ndani ya saa 48. Rwanda imesema kuwa itahakikisha ulinzi wa majengo, mali, na kumbukumbu za ubalozi wa Ubelgiji Jijini Kigali.

    Serikali ya Rwanda imesema kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na ubelgiji imefikiwa baada ya kuzingatia kwa makini mambo kadhaa, yote yakihusishwa na hatua za kusikitisha za Ubelgiji kuendeleza udanganyifu wake wa ukoloni mamboleo.

    Rais wa Nchi ya Rwanda 馃嚪馃嚰 , Paul Kagame ameionya Nchi ya Ubelgiji 馃嚙馃嚜 kuacha kutoa maagizo kwa Nchi yake na kuipangia cha kufanya utadhani kwamba Mungu amewapa jukumu na haki ya kuwasimamia ambapo amesema Rwanda haitokubali kutawaliwa tena na Wabelgji bali itapambana nao na itawashinda. Hayo ameyasema jana Jumapili Machi 16,2025 katika ukumbi wa BK Arena Nchini Rwanda, Kagame alinunuliwa akisema: “Nawaonya Wabelgi , Wabelgiji wameiharibu Rwanda, Wameua Wanyarwanda, tuliwaonya zamani na tunawaonya leo, wanasema ‘hawatuwaruhusu kufanya hiki na kile’ na sisi tunawauliza nyinyi ni nani?, nani kawapa jukumu la kutusimamia sisi?” “Wanyarwanda wanamuamini Mungu, mnaamini Mungu amewapa Wabelgiji jukumu la kuisimamia Rwanda?, kwa uwezo huu mdogo tulionao, tutapambana nao wote wanaotumia muda wao kututukana, kujaribu kututesa na hawatoweza kutushinda, watuache tuishi kwa amani, baada ya miaka yote tuliyotumia kupambana kuijenga Nchi yetu tunataka kuwa Wanyarwanda hatutaki kuwa Wabelgiji” “Rwanda kwa bahati mbaya tulitawaliwa na ka-nchi kadogo (Ubelgiji) ambayo ilienda mbali zaidi na kuigawa nchi yetu ili iwe ndogo kama nchi yao, sijawahi kusita kulieleza hili, tulilaani hili zamani na tutaendelea kulaani jambo hilo leo, hakuna kitu kibaya kitatokea kwetu kushinda majanga tuliyopitia huko nyuma, ndio maana hatupaswi kuogopa kusema na kujipambania sisi wenyewe dhidi ya wale wanaotaka kutuangamiza” Katika hatua nyingine, Serekali ya Rwanda imeawaamuru Wanadiplomasia wote wa Ubelgiji Nchini humo kuondoka ndani ya saa 48. Rwanda imesema kuwa itahakikisha ulinzi wa majengo, mali, na kumbukumbu za ubalozi wa Ubelgiji Jijini Kigali. Serikali ya Rwanda imesema kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na ubelgiji imefikiwa baada ya kuzingatia kwa makini mambo kadhaa, yote yakihusishwa na hatua za kusikitisha za Ubelgiji kuendeleza udanganyifu wake wa ukoloni mamboleo.
    0 Comments 0 Shares 491 Views
  • Taasisi ya dini ya Kiislamu ya Al-Hikma Foundation imetangaza kuwalipia mahari vijana 200 ambao wapo tayari kuoa.

    Akizungumza katika mashindano ya 25 ya kimataifa ya uhifadhi wa Qur'an yaliyofanyika leo Jumapili, Machi 16, 2023, katika Uwanja wa Mkapa na Uhuru, jijini Dar es Salaam, Sheikh Nurdin Kishki, ambaye ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo, amesema kuwa mwaka huu Vijana 200 watakaolipiwa mahari 100 watatoka Tanzania , na wengine 100 kutoka Nchini Burundi .

    "Kutokana na idadi ya watu wasiokuwa kwenye ndoa, mwaka huu tutaozesha vijana 200. Ndoa 100 zitafungwa Tanzania na 100 nyingine kwa ndugu zetu wa Burundi. Mahari na gharama nyingine za ndoa tutatoa sisi, Al-Hikma Foundation,"

    Pia, Sheikh Kishki ameeleza kuwa taasisi hiyo itawalipia gharama za tohara kwa watoto wa kiume 1000 Nchini Tanzania. Amesema mambo hayo yanafanyika kupitia programu maalumu iliyoanzishwa na taasisi hiyo ya kurejesha kwa jamii kupitia mashindano hayo.

    Taasisi ya dini ya Kiislamu ya Al-Hikma Foundation imetangaza kuwalipia mahari vijana 200 ambao wapo tayari kuoa. Akizungumza katika mashindano ya 25 ya kimataifa ya uhifadhi wa Qur'an yaliyofanyika leo Jumapili, Machi 16, 2023, katika Uwanja wa Mkapa na Uhuru, jijini Dar es Salaam, Sheikh Nurdin Kishki, ambaye ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo, amesema kuwa mwaka huu Vijana 200 watakaolipiwa mahari 100 watatoka Tanzania 馃嚬馃嚳, na wengine 100 kutoka Nchini Burundi 馃嚙馃嚠. "Kutokana na idadi ya watu wasiokuwa kwenye ndoa, mwaka huu tutaozesha vijana 200. Ndoa 100 zitafungwa Tanzania na 100 nyingine kwa ndugu zetu wa Burundi. Mahari na gharama nyingine za ndoa tutatoa sisi, Al-Hikma Foundation," Pia, Sheikh Kishki ameeleza kuwa taasisi hiyo itawalipia gharama za tohara kwa watoto wa kiume 1000 Nchini Tanzania. Amesema mambo hayo yanafanyika kupitia programu maalumu iliyoanzishwa na taasisi hiyo ya kurejesha kwa jamii kupitia mashindano hayo.
    0 Comments 0 Shares 404 Views
  • Jumatano ya Machi 17, 2021, Nchi ya Tanzania iligubikwa na simanzi zito ya kumpoteza Rais wao aliyekuwa madarakani, Dk John Pombe Magufuli maarufu JPM. Ni kwa mara ya kwanza Taifa hili la Afrika Mashariki kushuhudia Rais aliyekuwa madarakani akifariki dunia. Kifo chake kilitangazwa na Samia Suluhu Hassan, aliyekuwa Makamu wa Rais.

    Dk Magufuli aliyezaliwa Chato Mkoani Geita, Oktoba 29, 1959 alihitimisha utawala wake wa miaka mitano na miezi minne aliouanza Novemba 5, 2015 katika Hospitali ya Mzena, Kijitonyoma Jijini Dar es Salaam kwa maradhi ya moyo.

    Leo Jumatatu Machi 17, 2025, ndugu, jamaa na marafiki watamkumbuka kwa Ibada itakayofanyikia Chato ambayo imeandaliwa na familia yake.

    Jumatano ya Machi 17, 2021, Nchi ya Tanzania 馃嚬馃嚳 iligubikwa na simanzi zito ya kumpoteza Rais wao aliyekuwa madarakani, Dk John Pombe Magufuli maarufu JPM. Ni kwa mara ya kwanza Taifa hili la Afrika Mashariki kushuhudia Rais aliyekuwa madarakani akifariki dunia. Kifo chake kilitangazwa na Samia Suluhu Hassan, aliyekuwa Makamu wa Rais. Dk Magufuli aliyezaliwa Chato Mkoani Geita, Oktoba 29, 1959 alihitimisha utawala wake wa miaka mitano na miezi minne aliouanza Novemba 5, 2015 katika Hospitali ya Mzena, Kijitonyoma Jijini Dar es Salaam kwa maradhi ya moyo. Leo Jumatatu Machi 17, 2025, ndugu, jamaa na marafiki watamkumbuka kwa Ibada itakayofanyikia Chato ambayo imeandaliwa na familia yake.
    0 Comments 0 Shares 378 Views
More Results