• #PART4

    Wakati hayo yakiendelea Congo, kule Rwanda, kikundi cha waasi cha RPF chini ya Paul Kagame kilifanikiwa kuyashinda majeshi ya serikali na kuchukua dola baada ya yale mauaji ya kimbari. Askari wa jeshi la Rwanda, ambao wengi walikuwa Wahutu (Itarahamwe), walikimbilia Congo. Walipofika kule, wakaanzisha kikundi cha waasi cha kupigana na serikali ya Rwanda kilichoitwa FDLR. Kikundi hicho kikaungwa mkono na serikali ya Mobutu. Hivyo Mobutu akawa anawapa silaha wapigane na serikali ya Kagame ili kurudisha utawala wa Wahutu madarakani.

    Wakati Mobutu akisaidia waasi kuangusha serikali ya Rwanda, kulikia na vikundi vya waasi zaidi ya 40 vinapigana na jeshi lake. Moja kati ya vikundi hivyo ni Alliance of Democratic Forces for the Liberation (AFDL) kilichokuwa kinaongozwa na Mzee Laurent Kabila, ambaye ni Mluba wa Katanga, kusini mashariki mwa Congo karibu na Ziwa Tanganyika.

    Baada ya miaka karibu 30 ya kupigana msituni, hatimaye nguvu zikapungua. Akawa haendi tena mstari wa mbele. Mara kwa mara alikuja kupumzika nyumbani kwake Msasani jijini DSM, akimuachia Kanali Reuben Um-Nyobe kuongoza kikosi msituni.

    Mobutu alipoamua kuwasaidia askari wa FDLR (Intarahamwe) kupigana na serikali ya Rwanda, Kagame nae akaamua kumuunga mkono Laurent Kabila na kikundi chake cha AFDL ili wamng'oe Mobutu. Yaani, serikali ya Rwanda ikaunga mkono waasi wa Congo kwa sababu serikali ya Congo inaunga mkono waasi wa Rwanda. ‘Scratch my back, and I will scratch yours’.

    Wakati huo, inadaiwa serikali ya Rwanda ilikuwa imepata silaha nyingi kutoka Ufaransa na UK, kwa hiyo Kagame alijipima akaona ana nguvu za kupigana na Mobutu. Wakati huo Kagame alikuwa Makamu wa Rais chini ya Pasteur Bizimungu, lakini yeye ndiye aliyeongoza kila kitu. Sababu za kumuunga mkono Kabila;
    1. Ethnicity (Waluba na Watutsi wanaelewana)
    2. Mobutu kuunga mkono FDLR (Intarahamwe)
    3. Uwepo wa rasilimali nyingi sana eneo la Kivu, hasa madini.
    (Malisa GJ)

    #PART4 Wakati hayo yakiendelea Congo, kule Rwanda, kikundi cha waasi cha RPF chini ya Paul Kagame kilifanikiwa kuyashinda majeshi ya serikali na kuchukua dola baada ya yale mauaji ya kimbari. Askari wa jeshi la Rwanda, ambao wengi walikuwa Wahutu (Itarahamwe), walikimbilia Congo. Walipofika kule, wakaanzisha kikundi cha waasi cha kupigana na serikali ya Rwanda kilichoitwa FDLR. Kikundi hicho kikaungwa mkono na serikali ya Mobutu. Hivyo Mobutu akawa anawapa silaha wapigane na serikali ya Kagame ili kurudisha utawala wa Wahutu madarakani. Wakati Mobutu akisaidia waasi kuangusha serikali ya Rwanda, kulikia na vikundi vya waasi zaidi ya 40 vinapigana na jeshi lake. Moja kati ya vikundi hivyo ni Alliance of Democratic Forces for the Liberation (AFDL) kilichokuwa kinaongozwa na Mzee Laurent Kabila, ambaye ni Mluba wa Katanga, kusini mashariki mwa Congo karibu na Ziwa Tanganyika. Baada ya miaka karibu 30 ya kupigana msituni, hatimaye nguvu zikapungua. Akawa haendi tena mstari wa mbele. Mara kwa mara alikuja kupumzika nyumbani kwake Msasani jijini DSM, akimuachia Kanali Reuben Um-Nyobe kuongoza kikosi msituni. Mobutu alipoamua kuwasaidia askari wa FDLR (Intarahamwe) kupigana na serikali ya Rwanda, Kagame nae akaamua kumuunga mkono Laurent Kabila na kikundi chake cha AFDL ili wamng'oe Mobutu. Yaani, serikali ya Rwanda ikaunga mkono waasi wa Congo kwa sababu serikali ya Congo inaunga mkono waasi wa Rwanda. ‘Scratch my back, and I will scratch yours’. Wakati huo, inadaiwa serikali ya Rwanda ilikuwa imepata silaha nyingi kutoka Ufaransa na UK, kwa hiyo Kagame alijipima akaona ana nguvu za kupigana na Mobutu. Wakati huo Kagame alikuwa Makamu wa Rais chini ya Pasteur Bizimungu, lakini yeye ndiye aliyeongoza kila kitu. Sababu za kumuunga mkono Kabila; 1. Ethnicity (Waluba na Watutsi wanaelewana) 2. Mobutu kuunga mkono FDLR (Intarahamwe) 3. Uwepo wa rasilimali nyingi sana eneo la Kivu, hasa madini. (Malisa GJ)
    0 Комментарии ·0 Поделились ·54 Просмотры
  • #PART5
    Eneo la Kivu ni eneo la kimkakati sana na mabepari wote duniani wanalitolea macho kutokana na utajiri wake. Kivu ina madini ya Coltan ambayo yanatumika kutengeneza simu na laptop. 80% ya coltan yote duniani inatoka Congo (unaweza kugoogle kama huamini). Yani kwa kifupi bila Congo hakuna smartphones wala laptop duniani.

    Kivu pia kuna madini ya tin yanayotumika kutengenezea solder za kuchomelea vifaa vya kielektroniki kama radio, TV, simu, nk. Kuna madini ya Tungsten yanayotumika kutengenezea silaha. Na pia kuna Cobalt inayotumika kutengeneza betri mbalimbali zikiwemo za magari. Kama haitoshi Kivu kuna dhahabu nyingi mno. Eneo la Kivu ni eneo lenye dhahabu nyingi zaidi duniani ambayo bado haijachimbwa (The most unexplored gold site globally).

    Kagame aliona fursa. Wakati huo Rwanda ilikuwa imetoka kwenye vita na machafuko ya muda mrefu. Akataka rasilimali za jirani. Lakini atazipataje wakati yeye na Mobutu hawaelewani? Akakaamua kumuunga mkono mzee Laurent Kabila. Lakini akaweka masharti. Nikikusaidia kumng'oa Mobutu, eneo la Kivu Kusini, lenye Watutsi wengi (Banyamulenge), litajitenga na Congo na kuwa nchi inayojitegemea.

    Alishapiga hesabu za mbali za kuifanya Kivu kuwa sehemu ya Rwanda baada ya kujitenga DRC. Kabila akasema poa tu. Ashapigana miaka 30 msituni bila mafanikio? Sasa kapata "kamserereko" ka kwenda Ikulu akatae? Kagame nyuma yake walikuwepo Ufaransa na Uingereza akasema twende kwa maandishi. Mkataba ukasainiwa mji mdogo wa Lemera, Kivu Kusini. AFDL ikapewa support ya silaha na pesa, ikaamsha dude kupigana na majeshi ya serikali (FARDC).

    Wakati Mobutu anajaribu kupambana na AFDL, vikaibuka vikundi vingine vya waasi zaidi ya 40 kupigana na majeshi ya serikali. Vita ikiwa imepamba moto, Rwanda ikajitosa rasmi kupigana na serikali ya Mobutu kwa kisingizio cha kuwatafuta wanamgambo wa Intarahamwe waliokimbilia Congo. Uganda nayo ikaingiza jeshi kuwatafuta waasi wa LRA. Mobutu kaona "nini cha kufia" akadaka chopa akatokomea zake Moroco. Kesho yake tar.17 Mei 1997, Laurent Kabila akatangazwa Rais mpya wa Congo. Vita hii ikabatizwa jina vita vya kwanza vya Congo (1996-1997).
    (Malisa GJ)

    #PART5 Eneo la Kivu ni eneo la kimkakati sana na mabepari wote duniani wanalitolea macho kutokana na utajiri wake. Kivu ina madini ya Coltan ambayo yanatumika kutengeneza simu na laptop. 80% ya coltan yote duniani inatoka Congo (unaweza kugoogle kama huamini). Yani kwa kifupi bila Congo hakuna smartphones wala laptop duniani. Kivu pia kuna madini ya tin yanayotumika kutengenezea solder za kuchomelea vifaa vya kielektroniki kama radio, TV, simu, nk. Kuna madini ya Tungsten yanayotumika kutengenezea silaha. Na pia kuna Cobalt inayotumika kutengeneza betri mbalimbali zikiwemo za magari. Kama haitoshi Kivu kuna dhahabu nyingi mno. Eneo la Kivu ni eneo lenye dhahabu nyingi zaidi duniani ambayo bado haijachimbwa (The most unexplored gold site globally). Kagame aliona fursa. Wakati huo Rwanda ilikuwa imetoka kwenye vita na machafuko ya muda mrefu. Akataka rasilimali za jirani. Lakini atazipataje wakati yeye na Mobutu hawaelewani? Akakaamua kumuunga mkono mzee Laurent Kabila. Lakini akaweka masharti. Nikikusaidia kumng'oa Mobutu, eneo la Kivu Kusini, lenye Watutsi wengi (Banyamulenge), litajitenga na Congo na kuwa nchi inayojitegemea. Alishapiga hesabu za mbali za kuifanya Kivu kuwa sehemu ya Rwanda baada ya kujitenga DRC. Kabila akasema poa tu. Ashapigana miaka 30 msituni bila mafanikio? Sasa kapata "kamserereko" ka kwenda Ikulu akatae? Kagame nyuma yake walikuwepo Ufaransa na Uingereza akasema twende kwa maandishi. Mkataba ukasainiwa mji mdogo wa Lemera, Kivu Kusini. AFDL ikapewa support ya silaha na pesa, ikaamsha dude kupigana na majeshi ya serikali (FARDC). Wakati Mobutu anajaribu kupambana na AFDL, vikaibuka vikundi vingine vya waasi zaidi ya 40 kupigana na majeshi ya serikali. Vita ikiwa imepamba moto, Rwanda ikajitosa rasmi kupigana na serikali ya Mobutu kwa kisingizio cha kuwatafuta wanamgambo wa Intarahamwe waliokimbilia Congo. Uganda nayo ikaingiza jeshi kuwatafuta waasi wa LRA. Mobutu kaona "nini cha kufia" akadaka chopa akatokomea zake Moroco. Kesho yake tar.17 Mei 1997, Laurent Kabila akatangazwa Rais mpya wa Congo. Vita hii ikabatizwa jina vita vya kwanza vya Congo (1996-1997). (Malisa GJ)
    0 Комментарии ·0 Поделились ·74 Просмотры
  • #PART6

    Alipoingia Ikulu Kabila alifuta jina Zaire na kurudisha Congo (Jamhuri ya kidemokrasia). Baadae alifikiria kuiachia Kivu, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini adimu duniani. Akasema "to hell with Lemera Agreement" akautupilia mbali mkataba wa Lemera. Akasema Kivu itabaki Congo na madini ya Kivu yatajenga Congo. Full stop. Ashakuwa Rais utamfanya nini?

    Kagame hakuamini macho yake. Alishawaza jinsi ambavyo Rwanda ingekuwa Dubai ya Afrika kwa rasilimali za Congo. Lakini ghafla aligeukwa na mshirika wake Laurent Désiré Kabila. Akamfuata "Godfather" wake mzee Museveni. Mzee akasema kama katugeuka tumpige. Wakatafuta kikundi cha Waasi wakiunge mkono. Wakapata Rassemblement Congolais pour la Démocratie (RCD), kilichoongozwa na Jenerali Ernest Wamba dia Wamba. Kikundi kikapewa silaha na fedha kikaanza kumshughulikia Kabila.

    RCD ikaanza kuchapana na jeshi la Congo (FARDC) ikiwa na backup ya Rwanda na Uganda. Vita vikapamba moto. Rwanda na Uganda nao wakaingiza majeshi Congo kusaidia waasi wa RCD. Kabila akaona anazidiwa, akaomba msaada Angola na Chad. Nchi hizo zikaleta vikosi vyake Congo. Mapigano yakawa makali sana. Eneo la mashariki mwa Congo likageuka machinjioni. Watu walikufa kwa wingi, mpaka maiti zikatapakaa barabarani bila kuzikwa, zikawa zinadonolewa na ndege.

    Hii iliitwa Vita ya Pili ya Congo (1998–2002), iliyokua mbaya zaidi katika historia ya vita zote Afrika. Imebatizwa jina "Vita Kuu ya Afrika". Inakadiriwa watu laki tano walipoteza maisha huku mamilioni wakikimbia nchi. Mapigano yaliendelea, huku vikosi vya Rwanda na Uganda vikichota madini. Katikati ya mapigano mgongano wa kimaslahi ukajitokeza.

    Jasin Stearns, katika kitabu chake Dancing in the Glory of Monsters, anasema Kagame alishindwa kuelewana na "godfather" wake Museveni juu ya mgawanyo wa mali. Hali hiyo ilifanya kikundi cha RCD kipasuke na kuzaliwa vikundi viwili. Cha kwanza kikajiita RCD-Goma kikiongozwa na Kanali Emile Ilunga (hiki kilisaidiwa na Rwanda) na cha pili kikajiita RCD-Kisangani, kikiongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi (kikisaidiwa na Uganda).
    (Malisa GJ)

    #PART6 Alipoingia Ikulu Kabila alifuta jina Zaire na kurudisha Congo (Jamhuri ya kidemokrasia). Baadae alifikiria kuiachia Kivu, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini adimu duniani. Akasema "to hell with Lemera Agreement" akautupilia mbali mkataba wa Lemera. Akasema Kivu itabaki Congo na madini ya Kivu yatajenga Congo. Full stop. Ashakuwa Rais utamfanya nini? Kagame hakuamini macho yake. Alishawaza jinsi ambavyo Rwanda ingekuwa Dubai ya Afrika kwa rasilimali za Congo. Lakini ghafla aligeukwa na mshirika wake Laurent Désiré Kabila. Akamfuata "Godfather" wake mzee Museveni. Mzee akasema kama katugeuka tumpige. Wakatafuta kikundi cha Waasi wakiunge mkono. Wakapata Rassemblement Congolais pour la Démocratie (RCD), kilichoongozwa na Jenerali Ernest Wamba dia Wamba. Kikundi kikapewa silaha na fedha kikaanza kumshughulikia Kabila. RCD ikaanza kuchapana na jeshi la Congo (FARDC) ikiwa na backup ya Rwanda na Uganda. Vita vikapamba moto. Rwanda na Uganda nao wakaingiza majeshi Congo kusaidia waasi wa RCD. Kabila akaona anazidiwa, akaomba msaada Angola na Chad. Nchi hizo zikaleta vikosi vyake Congo. Mapigano yakawa makali sana. Eneo la mashariki mwa Congo likageuka machinjioni. Watu walikufa kwa wingi, mpaka maiti zikatapakaa barabarani bila kuzikwa, zikawa zinadonolewa na ndege. Hii iliitwa Vita ya Pili ya Congo (1998–2002), iliyokua mbaya zaidi katika historia ya vita zote Afrika. Imebatizwa jina "Vita Kuu ya Afrika". Inakadiriwa watu laki tano walipoteza maisha huku mamilioni wakikimbia nchi. Mapigano yaliendelea, huku vikosi vya Rwanda na Uganda vikichota madini. Katikati ya mapigano mgongano wa kimaslahi ukajitokeza. Jasin Stearns, katika kitabu chake Dancing in the Glory of Monsters, anasema Kagame alishindwa kuelewana na "godfather" wake Museveni juu ya mgawanyo wa mali. Hali hiyo ilifanya kikundi cha RCD kipasuke na kuzaliwa vikundi viwili. Cha kwanza kikajiita RCD-Goma kikiongozwa na Kanali Emile Ilunga (hiki kilisaidiwa na Rwanda) na cha pili kikajiita RCD-Kisangani, kikiongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi (kikisaidiwa na Uganda). (Malisa GJ)
    0 Комментарии ·0 Поделились ·26 Просмотры
  • 0 Комментарии ·0 Поделились ·10 Просмотры
  • 0 Комментарии ·0 Поделились ·10 Просмотры
  • Mo Salah amebakisha mabao 83 kuivunja rekodi ya ufungaji bora wa muda wote ya ligi kuu ya England inayoshikiliwa na muingereza Alan Shearer.

    Kwa sasa Salah yupo nafasi ya 6 akiwa na mabao 178, na anayo nafasi ya kupanda hadi nafasi ya 5 na kumshusha Sergio Kun-Aguero mwenye mabao 184, endapo atafunga mabao 7 katika mechi 15 zilizobaki. Na kama itakuwa hivyo basi atakuwa amebakisha mabao 76 ili kuvunja kabisa ya muda wote.

    Kwa rekodi ya ufungaji ya Salah, atahitaji misimu angalau minne kuifikia rekodi hii. Hii ni kwa sababu tangu ajiunge Liverpool 2016/18 amekuwa na wastani wa kufunga mabao 22 kwa msimu.

    2024/25 - 21
    2023/24 - 18
    2022/23 - 19
    2021/22 - 23
    2020/21 - 22
    2019/20 - 19
    2018/19 - 22
    2017/18 - 32

    Mkataba wa Mo Salah utaisha mwishoni mwa msimu huu na mazungumzo ya mkataba mpya yanasuasua. Salah mwenye miaka 32 amesema anatamani kubaki Liverpool, akini apewe mkataba wa miaka mitatu hadi 2028.

    Ila wamiliki wa klabu hiyo, kampuni ya FSG, wanasita kutoa mkataba mrefu namna hiyo kwa hofu ya umri wake.

    Mo Salah amebakisha mabao 83 kuivunja rekodi ya ufungaji bora wa muda wote ya ligi kuu ya England inayoshikiliwa na muingereza Alan Shearer. Kwa sasa Salah yupo nafasi ya 6 akiwa na mabao 178, na anayo nafasi ya kupanda hadi nafasi ya 5 na kumshusha Sergio Kun-Aguero mwenye mabao 184, endapo atafunga mabao 7 katika mechi 15 zilizobaki. Na kama itakuwa hivyo basi atakuwa amebakisha mabao 76 ili kuvunja kabisa ya muda wote. Kwa rekodi ya ufungaji ya Salah, atahitaji misimu angalau minne kuifikia rekodi hii. Hii ni kwa sababu tangu ajiunge Liverpool 2016/18 amekuwa na wastani wa kufunga mabao 22 kwa msimu. 2024/25 - 21 2023/24 - 18 2022/23 - 19 2021/22 - 23 2020/21 - 22 2019/20 - 19 2018/19 - 22 2017/18 - 32 Mkataba wa Mo Salah utaisha mwishoni mwa msimu huu na mazungumzo ya mkataba mpya yanasuasua. Salah mwenye miaka 32 amesema anatamani kubaki Liverpool, akini apewe mkataba wa miaka mitatu hadi 2028. Ila wamiliki wa klabu hiyo, kampuni ya FSG, wanasita kutoa mkataba mrefu namna hiyo kwa hofu ya umri wake.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·12 Просмотры
  • 0 Комментарии ·0 Поделились ·11 Просмотры
  • 0 Комментарии ·0 Поделились ·9 Просмотры
  • 0 Комментарии ·0 Поделились ·9 Просмотры
  • 0 Комментарии ·0 Поделились ·10 Просмотры