• PART 7

    Saa 4:28 asubuhi, Mnara wa Kaskazini wa WTC ulianguka, dakika 102 baada ya athari iliyosababishwa na ndege ya shirika la ndege la American Airlines. Mamia ya watu, ambao hawakuweza kuondolewa, ikiwa ni pamoja na waokoaji waliokuwa katika ghorofa, walifukiwa na vifusi vya jengo hilo.
    Minara hiyo inayoanguka pia ilisababisha uharibifu mkubwa kwa majengo yaliyo kuwa karibu, kama mnara wa 7 wa WTC, ambao ulidondoka saa 11:20 jioni.
    PART 7 Saa 4:28 asubuhi, Mnara wa Kaskazini wa WTC ulianguka, dakika 102 baada ya athari iliyosababishwa na ndege ya shirika la ndege la American Airlines. Mamia ya watu, ambao hawakuweza kuondolewa, ikiwa ni pamoja na waokoaji waliokuwa katika ghorofa, walifukiwa na vifusi vya jengo hilo. Minara hiyo inayoanguka pia ilisababisha uharibifu mkubwa kwa majengo yaliyo kuwa karibu, kama mnara wa 7 wa WTC, ambao ulidondoka saa 11:20 jioni.
    0 Comments ·0 Shares ·72 Views
  • PART 6

    Saa 3:59 asubuhi, Mnara wa Kusini wa kituo cha Biashara cha World Trade Center (WTC) ulidondoka wenyewe, dakika 55 matukio hayo ya kwanza.
    Ndege ya nne, ya shirika la ndege la United Airlines Flight 93, ilianguka saa 10: 03 asubuhi kwenye chamba moja karibu na Pittsburg, huko Pennsylvania, ikiwa na watu 44, wakiwemo magaidi wanne. Abiria kwenye ndege hiyo waliripotiwa kupigana na watekaji nyara baada ya kuambiwa juu ya mkasa huo kwenye simu zao za rununu. Inaaminika kwamba ndege hii, iliyokuwa ikielekea Washington,ilienda kushambulia Capitol, makao makuu ya Bunge la Marekani.
    PART 6 Saa 3:59 asubuhi, Mnara wa Kusini wa kituo cha Biashara cha World Trade Center (WTC) ulidondoka wenyewe, dakika 55 matukio hayo ya kwanza. Ndege ya nne, ya shirika la ndege la United Airlines Flight 93, ilianguka saa 10: 03 asubuhi kwenye chamba moja karibu na Pittsburg, huko Pennsylvania, ikiwa na watu 44, wakiwemo magaidi wanne. Abiria kwenye ndege hiyo waliripotiwa kupigana na watekaji nyara baada ya kuambiwa juu ya mkasa huo kwenye simu zao za rununu. Inaaminika kwamba ndege hii, iliyokuwa ikielekea Washington,ilienda kushambulia Capitol, makao makuu ya Bunge la Marekani.
    0 Comments ·0 Shares ·70 Views
  • PART 5

    Lakini saa 3:37 asubuhi huko Virginia, ndege ya tatu, ya shirika la ndege la American Airlines Flight 77, ilianguka katika sehemu ya magharibi ya Pentagon, makao makuu ya wizara ya Ulinzi ya Marekani, ikiwa na watu 64, wakiwemo watu watano wa kujitoa mhanga.
    PART 5 Lakini saa 3:37 asubuhi huko Virginia, ndege ya tatu, ya shirika la ndege la American Airlines Flight 77, ilianguka katika sehemu ya magharibi ya Pentagon, makao makuu ya wizara ya Ulinzi ya Marekani, ikiwa na watu 64, wakiwemo watu watano wa kujitoa mhanga.
    0 Comments ·0 Shares ·68 Views
  • PART 4

    2:46 asubuhi, ulimwengu wapigwa na bumbuwazi

    Ilikuwa saa 2:46 asubuhi, saa zahuko New York, wakati Boeing 767 kutoka shirika la ndege la American Airlines Flight 11 ilipoanguka kwenye Mnara wa Kaskazini wa kituo cha Biashara cha World Trade Center , ikiwa na watu 92 , wakiwemo magaidi watano.
    Dakika kumi na saba baadaye, saa 3:03 asubuhi, vituo kadhaa vya televisheni vilikuwa vikitangaza tukio hilo, watu waliona ndege ya shirika la ndege la United Airlines Flight 175 ikigonga Mnara wa Kusini wa jengo hilo la kibiashara. Watu 65 walikuemo, ikiwa ni pamoja na watekaji nyara watano. Wakati moto ukiharibu sakafu za juu za minara hiyo miwili, Andrew Card, mkurugenzi katika ofisi ya rais, alimfahamisha rais George W. Bush: “Ndege ya pili imegonga mnara mwingine na Marekani sasa inashambuliwa. "
    PART 4 2:46 asubuhi, ulimwengu wapigwa na bumbuwazi Ilikuwa saa 2:46 asubuhi, saa zahuko New York, wakati Boeing 767 kutoka shirika la ndege la American Airlines Flight 11 ilipoanguka kwenye Mnara wa Kaskazini wa kituo cha Biashara cha World Trade Center , ikiwa na watu 92 , wakiwemo magaidi watano. Dakika kumi na saba baadaye, saa 3:03 asubuhi, vituo kadhaa vya televisheni vilikuwa vikitangaza tukio hilo, watu waliona ndege ya shirika la ndege la United Airlines Flight 175 ikigonga Mnara wa Kusini wa jengo hilo la kibiashara. Watu 65 walikuemo, ikiwa ni pamoja na watekaji nyara watano. Wakati moto ukiharibu sakafu za juu za minara hiyo miwili, Andrew Card, mkurugenzi katika ofisi ya rais, alimfahamisha rais George W. Bush: “Ndege ya pili imegonga mnara mwingine na Marekani sasa inashambuliwa. "
    0 Comments ·0 Shares ·71 Views
  • "MFUMO ULIOANGUSHA B737MAX"

    Mara baada ya uchunguzi wa awali kutoa ripoti inayoonesha kuwa ajali ya ndege ya Ethiopia Airline na Lion Air B737 Max iliyotokea mapema miezi michache iliyopita haikusababishwa na makosa ya kiurubani bali ni mfumo wao mpya wa"Software" iitwayo 'MCAS' waliouweka katika ndege hiyo kwa lengo la kuzuia ndege ku'STALL.
    'STALL' ni kitendo ambacho hutokea pale mbawa za ndege zinapobinuka na kufikia 'angle' ambayo hushindwa kuendelea kuzalisha 'lift' ya kutosha na kupelekea ndege kushindwa kuendelea kupaa na kurudi chini (mda mwengine mithili ya jiwe).
    'Stall' mara nyingi inatokea pale ambapo ndege inapokuwa inapaa na kunyanyua pua yake juu kupita kiasi na katika mwendo mdogo isivyo kawaida na kupelekea hewa inayopita kwenye mbawa zake ili kuipaisha ndege kuvurugika.
    Software hii mpya ya "MCAS' (Inayosemekana kuwa na makosa) imewekwa kwenye B737Max ili kuzuia ndege hizo ku'stall na inafanya kazi 'automatic' ya kuinamisha pua ya ndege chini ili kuipa kasi na kurudisha hewa iliyovurugika kwenye mbawa katika hali yake ya kawaida ili ndege iendelee kupaa.
    Lakini wachambuzi wanasema, software hii mda mwengine inafanya kazi kimakosa pale inapoinamisha pua ya ndege chini hata kama ndege haikuwa katika ya hali hiyo ya kunyanyua pua yake hivyo kuanza kushindana na Rubani na kupelekea ndege kudaivu kurudi ardhini mithili ya mkuki.
    Inasemekana Boeing wameweka Software hii mpya kwenye B737Max ili kuzuia tabia hiyo mpya ya ndege hizo ya kunyanyua pua yake juu zaidi pale inapokuwa inapaa hali inayosababishwa na kubachikwa kwa injini nyengine kubwa mpya ambazo zilishindwa kufiti katika sehemu yake ya kawaida kutokana na ndege hizo kuwa chichini hivyo waka'modify kwa kuzisogeza mbele na kuzipandisha juu kidogo ya mbawa.
    Modification' hiyo inapelekea ndege kuwa na tabia hiyo ya kunyanyua pua yake yenyewe wakati wa urukaji hivyo kujitofautisha na Boeing 737 nyengine za awali katika urukaji hivyo Boeing wakaamua kuweka mfumo huu ili kuepuka gharama za kufundisha marubani upya juu ya hali hiyo.
    (Picha kwa hisani ya mtandao)
    #Ndege #Ajali #Boeing #Max #Ethiopian #Airline #Lion #Air #MCAS
    "MFUMO ULIOANGUSHA B737MAX" Mara baada ya uchunguzi wa awali kutoa ripoti inayoonesha kuwa ajali ya ndege ya Ethiopia Airline na Lion Air B737 Max iliyotokea mapema miezi michache iliyopita haikusababishwa na makosa ya kiurubani bali ni mfumo wao mpya wa"Software" iitwayo 'MCAS' waliouweka katika ndege hiyo kwa lengo la kuzuia ndege ku'STALL. 'STALL' ni kitendo ambacho hutokea pale mbawa za ndege zinapobinuka na kufikia 'angle' ambayo hushindwa kuendelea kuzalisha 'lift' ya kutosha na kupelekea ndege kushindwa kuendelea kupaa na kurudi chini (mda mwengine mithili ya jiwe). 'Stall' mara nyingi inatokea pale ambapo ndege inapokuwa inapaa na kunyanyua pua yake juu kupita kiasi na katika mwendo mdogo isivyo kawaida na kupelekea hewa inayopita kwenye mbawa zake ili kuipaisha ndege kuvurugika. Software hii mpya ya "MCAS' (Inayosemekana kuwa na makosa) imewekwa kwenye B737Max ili kuzuia ndege hizo ku'stall na inafanya kazi 'automatic' ya kuinamisha pua ya ndege chini ili kuipa kasi na kurudisha hewa iliyovurugika kwenye mbawa katika hali yake ya kawaida ili ndege iendelee kupaa. Lakini wachambuzi wanasema, software hii mda mwengine inafanya kazi kimakosa pale inapoinamisha pua ya ndege chini hata kama ndege haikuwa katika ya hali hiyo ya kunyanyua pua yake hivyo kuanza kushindana na Rubani na kupelekea ndege kudaivu kurudi ardhini mithili ya mkuki. Inasemekana Boeing wameweka Software hii mpya kwenye B737Max ili kuzuia tabia hiyo mpya ya ndege hizo ya kunyanyua pua yake juu zaidi pale inapokuwa inapaa hali inayosababishwa na kubachikwa kwa injini nyengine kubwa mpya ambazo zilishindwa kufiti katika sehemu yake ya kawaida kutokana na ndege hizo kuwa chichini hivyo waka'modify kwa kuzisogeza mbele na kuzipandisha juu kidogo ya mbawa. Modification' hiyo inapelekea ndege kuwa na tabia hiyo ya kunyanyua pua yake yenyewe wakati wa urukaji hivyo kujitofautisha na Boeing 737 nyengine za awali katika urukaji hivyo Boeing wakaamua kuweka mfumo huu ili kuepuka gharama za kufundisha marubani upya juu ya hali hiyo. (Picha kwa hisani ya mtandao) #Ndege #Ajali #Boeing #Max #Ethiopian #Airline #Lion #Air #MCAS
    0 Comments ·0 Shares ·514 Views