Upgrade to Pro

  • "MFUMO ULIOANGUSHA B737MAX"

    Mara baada ya uchunguzi wa awali kutoa ripoti inayoonesha kuwa ajali ya ndege ya Ethiopia Airline na Lion Air B737 Max iliyotokea mapema miezi michache iliyopita haikusababishwa na makosa ya kiurubani bali ni mfumo wao mpya wa"Software" iitwayo 'MCAS' waliouweka katika ndege hiyo kwa lengo la kuzuia ndege ku'STALL.
    'STALL' ni kitendo ambacho hutokea pale mbawa za ndege zinapobinuka na kufikia 'angle' ambayo hushindwa kuendelea kuzalisha 'lift' ya kutosha na kupelekea ndege kushindwa kuendelea kupaa na kurudi chini (mda mwengine mithili ya jiwe).
    'Stall' mara nyingi inatokea pale ambapo ndege inapokuwa inapaa na kunyanyua pua yake juu kupita kiasi na katika mwendo mdogo isivyo kawaida na kupelekea hewa inayopita kwenye mbawa zake ili kuipaisha ndege kuvurugika.
    Software hii mpya ya "MCAS' (Inayosemekana kuwa na makosa) imewekwa kwenye B737Max ili kuzuia ndege hizo ku'stall na inafanya kazi 'automatic' ya kuinamisha pua ya ndege chini ili kuipa kasi na kurudisha hewa iliyovurugika kwenye mbawa katika hali yake ya kawaida ili ndege iendelee kupaa.
    Lakini wachambuzi wanasema, software hii mda mwengine inafanya kazi kimakosa pale inapoinamisha pua ya ndege chini hata kama ndege haikuwa katika ya hali hiyo ya kunyanyua pua yake hivyo kuanza kushindana na Rubani na kupelekea ndege kudaivu kurudi ardhini mithili ya mkuki.
    Inasemekana Boeing wameweka Software hii mpya kwenye B737Max ili kuzuia tabia hiyo mpya ya ndege hizo ya kunyanyua pua yake juu zaidi pale inapokuwa inapaa hali inayosababishwa na kubachikwa kwa injini nyengine kubwa mpya ambazo zilishindwa kufiti katika sehemu yake ya kawaida kutokana na ndege hizo kuwa chichini hivyo waka'modify kwa kuzisogeza mbele na kuzipandisha juu kidogo ya mbawa.
    Modification' hiyo inapelekea ndege kuwa na tabia hiyo ya kunyanyua pua yake yenyewe wakati wa urukaji hivyo kujitofautisha na Boeing 737 nyengine za awali katika urukaji hivyo Boeing wakaamua kuweka mfumo huu ili kuepuka gharama za kufundisha marubani upya juu ya hali hiyo.
    (Picha kwa hisani ya mtandao)
    #Ndege #Ajali #Boeing #Max #Ethiopian #Airline #Lion #Air #MCAS
    "MFUMO ULIOANGUSHA B737MAX" Mara baada ya uchunguzi wa awali kutoa ripoti inayoonesha kuwa ajali ya ndege ya Ethiopia Airline na Lion Air B737 Max iliyotokea mapema miezi michache iliyopita haikusababishwa na makosa ya kiurubani bali ni mfumo wao mpya wa"Software" iitwayo 'MCAS' waliouweka katika ndege hiyo kwa lengo la kuzuia ndege ku'STALL. 'STALL' ni kitendo ambacho hutokea pale mbawa za ndege zinapobinuka na kufikia 'angle' ambayo hushindwa kuendelea kuzalisha 'lift' ya kutosha na kupelekea ndege kushindwa kuendelea kupaa na kurudi chini (mda mwengine mithili ya jiwe). 'Stall' mara nyingi inatokea pale ambapo ndege inapokuwa inapaa na kunyanyua pua yake juu kupita kiasi na katika mwendo mdogo isivyo kawaida na kupelekea hewa inayopita kwenye mbawa zake ili kuipaisha ndege kuvurugika. Software hii mpya ya "MCAS' (Inayosemekana kuwa na makosa) imewekwa kwenye B737Max ili kuzuia ndege hizo ku'stall na inafanya kazi 'automatic' ya kuinamisha pua ya ndege chini ili kuipa kasi na kurudisha hewa iliyovurugika kwenye mbawa katika hali yake ya kawaida ili ndege iendelee kupaa. Lakini wachambuzi wanasema, software hii mda mwengine inafanya kazi kimakosa pale inapoinamisha pua ya ndege chini hata kama ndege haikuwa katika ya hali hiyo ya kunyanyua pua yake hivyo kuanza kushindana na Rubani na kupelekea ndege kudaivu kurudi ardhini mithili ya mkuki. Inasemekana Boeing wameweka Software hii mpya kwenye B737Max ili kuzuia tabia hiyo mpya ya ndege hizo ya kunyanyua pua yake juu zaidi pale inapokuwa inapaa hali inayosababishwa na kubachikwa kwa injini nyengine kubwa mpya ambazo zilishindwa kufiti katika sehemu yake ya kawaida kutokana na ndege hizo kuwa chichini hivyo waka'modify kwa kuzisogeza mbele na kuzipandisha juu kidogo ya mbawa. Modification' hiyo inapelekea ndege kuwa na tabia hiyo ya kunyanyua pua yake yenyewe wakati wa urukaji hivyo kujitofautisha na Boeing 737 nyengine za awali katika urukaji hivyo Boeing wakaamua kuweka mfumo huu ili kuepuka gharama za kufundisha marubani upya juu ya hali hiyo. (Picha kwa hisani ya mtandao) #Ndege #Ajali #Boeing #Max #Ethiopian #Airline #Lion #Air #MCAS
    ·146 Views