PICHA YA SIMBA HUYU NI FUNZO MAISHANI:
------------------------------------------------------
Hivi ndivyo mfalme wa pori anavyoonekana akiwa kwenye siku za mwisho za maisha yake. Jinsi alivyokonda, kujua idadi ya mbavu zake hata huitaji msaada wa calculator.
Hii picha ilipigwa na "Larry Pannell."
Alifanikiwa kupata picha ya Simba aliyekuwa kwenye hitimisho la kuvuta pumzi za mwisho. Katika huu ulimwengu wenye mafungamano na dhambi.
"Larry Pannell" anasema:
Nilimkuta huyu simba amelala kwenye majani. Akiwa amechoka, miguu ikionekana kumnyima ushirikiano wa kutembea.
Sikuwa na lakufanya zaidi ya kusimama mita kadhaa. Macho yakifanya ushuhuda wa kutazama, "King of savannah" akipoteza uhai chini ya kivuli cha mti.
Nikiwa nimesimama kimya. Nilishusha chini camera yangu. Tulitazamana na simba, tukafumba macho yetu pamoja.
Jinsi mfalme wa nyika alivyokuwa akihangaika kuhema. Pumzi zilionekana kuwa bidhaa hadimu kwenye duka la mapafu yake.
Kifua chake kilikuwa kikipanda na kushuka. Ishara ya kuonyesha anavuta pumzi za mwisho, kabla ya kukipa ruhusa kifo kiondoke na roho yake.
Ghafla eneo alilolala Simba ukazaliwa ukimya. Mfalme wa pori akawa haemi wala kutikisika. Mauti ikawa imehitimisha simulizi ya ubabe wake mbugani.
Hakika maisha ya binadamu na wanyama ni simulizi fupi sana."
Haijalishi una nguvu kiasi gani. Kuna nyakati zitafika nguvu zitafanya mgomo wa kuishi mwilini mwako. Zitaupisha udhaifu uchukue nafasi ya kukutawala. Udhaifu nao ukikutawala, utayaita maradhi. Bila hiyari utajikuta umekigeuza kitanda kuwa rafiki."
Kuna shule ya bure hapa: Nguvu tulizonazo ni kitu cha kupita. Hata uzuri umpao kiburi mwanamke una ukomo. Licha ya kujidanganya kwa make up na wanja. Lakini hawezi kuzuia muanguko wa mashavu, uzee unapoanza kumuondoa kwenye kundi la warembo.
"Chini ya jua kila kitu kina mwanzo na mwisho."
Hivyo katika maisha tusisahau kuvipa kipaumbele vitu hivi. Utu, wema, ukarimu, heshima, na unyenyekevu.
Tusaidie wenye maradhi, tuwajali wasiojiweza, na viongozi tusitumie madaraka vibaya.
Tutende mema tukiamini. Kuna siku pumzi zitamaliza mkataba wa kuishi ndani ya matundu ya pua zetu. Baada ya hapo sisi wote tutalala mauti."
Imeandikwa na Green Osward

0 Commenti
·0 condivisioni
·10 Views