• IMANI KUBWA.

    Imani ni uhakika wa jambo bayana ya lile lisilo onekana.

    #Waebrania 11:1
    [1]Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

    Imani kubwa ni imani ya kulitazama neno na kutokea kwenye neno kila jawabu lako unaliona hapo.

    Mfano uhalisia madaktari wanasema huwezi kupona kisukari lakini neno linasema alichukua magonjwa yetu ,madhaifu yetu hivyo basi lwa kupigwa kwake sisi tumepona.

    Imani kubwa ni kuvuka mstari wa wanayo onekana na kisha kutazama neno na kuliishi.

    Akida alikuwa mfano wa jambo hili.

    #Luka 7:7
    [7]kwa hiyo nilijiona sistahili mwenyewe kuja kwako; lakini, sema neno tu, na mtumwa wangu atapona.

    Huyu akida akuhitaji kabisa hata Yesu aende eneo lile badala yake aliitaji alitume neno tu na yule mtumwa wake apone.

    Hii ndiyo imani kubwa ni wakati uhalisia unakataa lakini ndo kipindi ambacho unaona jibu hapo hapo.

    #Luka 7:7,9
    [7]kwa hiyo nilijiona sistahili mwenyewe kuja kwako; lakini, sema neno tu, na mtumwa wangu atapona.

    [9]Yesu aliposikia hayo alimstaajabia, akaugeukia mkutano uliokuwa ukimfuata, akasema, Nawaambia, hata katika Israeli sijaona imani kubwa namna hii.

    Wanao pokea wote kwa ukubwa lazima wawe na imani kubwa sana na chanzo cha imani kubwa ni kusikia neno la Mungu na kuligeuza kuwa lako la maisha.

    Kwa sababu Mungu huwa ana asili ya kulituma neno lake lake kisha likabadilisha yote.

    #Zaburi 107:20
    [20]Hulituma neno lake, huwaponya,
    Huwatoa katika maangamizo yao.

    Ko kama huamini neno Mungu hawezi kulituma neno ni lazima ufike kipindi uamue kulituma neno ili kutokea kwenye neno libadilishe yote.

    Mfano mwingine .

    Petro alipo kiuhalisia petro alikuwa mtaalamu wa uvuvi na kiasi cha kuwa amekesha kabisa kutafuta samaki .

    Na kanuni ya uvuvi samaki wanapatikana usiku , Yesu ameenda muda ambao hualisia wa kawaida haukubali kuvua.

    Na anamwambia Petro shusha nyavu kilindini,
    Petro sababu ya imani kubwa alimwambia kwa neno lako nashusha nyavu.

    #Luka 5:5
    [5]Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.

    Na kutokea kushusha nyavu walipata samaki wengi kiasi cha nyavu kukatika.

    #Luka 5:6-7
    [6]Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;
    .
    [7]wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama.

    Kumbe hata wewe upati majibu sababu utaki kujenga imani kubwa katika jambo unalo lifanya.

    Mfano moyoni mwako kila ukiwaza unasikia kuwa na real estate na uhalisia uoni lakini una kakiwanja mahali au unapo ishi kumbe imani kubwa ni kuanza hata na vyumba viwili ndo vitabadilisha maisha yako.

    Ni neno la uzima peke yake ndilo Lina badilishaga yote .

    Jifunze kutii kile unacho kiona kwenye neno na kutokea hapo maisha yako yote yatabadilika.

    Jitahidi sana kuomba kwa Mungu neno la uzima linabdailishaga yote.

    Imani inabadilisha yote kabisa na ukiamua kumfuata Yesu na ukalipenda neno maisha yako yatabadilika kabisa.

    Kuwa na imani kubwa harafu uone matokeo makubwa

    NAKUOMBEA MUNGU WANGU AKUPE NEEMA YA KUWA NA IMANI KUBWA KTIKA NENO LAKE NA KUTOKEA HAPO JANA YAKO IBADILIKE KABISA NA KUWA KESHO NJEMA KWA JINA LA YESU.

    Nikutakie asubui njema na siku njema .

    Naitwa sylvester Mwakabende
    Build new eden ministry
    0622625340

    #build new eden
    #restore men position
    IMANI KUBWA. Imani ni uhakika wa jambo bayana ya lile lisilo onekana. #Waebrania 11:1 [1]Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Imani kubwa ni imani ya kulitazama neno na kutokea kwenye neno kila jawabu lako unaliona hapo. Mfano uhalisia madaktari wanasema huwezi kupona kisukari lakini neno linasema alichukua magonjwa yetu ,madhaifu yetu hivyo basi lwa kupigwa kwake sisi tumepona. Imani kubwa ni kuvuka mstari wa wanayo onekana na kisha kutazama neno na kuliishi. Akida alikuwa mfano wa jambo hili. #Luka 7:7 [7]kwa hiyo nilijiona sistahili mwenyewe kuja kwako; lakini, sema neno tu, na mtumwa wangu atapona. Huyu akida akuhitaji kabisa hata Yesu aende eneo lile badala yake aliitaji alitume neno tu na yule mtumwa wake apone. Hii ndiyo imani kubwa ni wakati uhalisia unakataa lakini ndo kipindi ambacho unaona jibu hapo hapo. #Luka 7:7,9 [7]kwa hiyo nilijiona sistahili mwenyewe kuja kwako; lakini, sema neno tu, na mtumwa wangu atapona. [9]Yesu aliposikia hayo alimstaajabia, akaugeukia mkutano uliokuwa ukimfuata, akasema, Nawaambia, hata katika Israeli sijaona imani kubwa namna hii. Wanao pokea wote kwa ukubwa lazima wawe na imani kubwa sana na chanzo cha imani kubwa ni kusikia neno la Mungu na kuligeuza kuwa lako la maisha. Kwa sababu Mungu huwa ana asili ya kulituma neno lake lake kisha likabadilisha yote. #Zaburi 107:20 [20]Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao. Ko kama huamini neno Mungu hawezi kulituma neno ni lazima ufike kipindi uamue kulituma neno ili kutokea kwenye neno libadilishe yote. Mfano mwingine . Petro alipo kiuhalisia petro alikuwa mtaalamu wa uvuvi na kiasi cha kuwa amekesha kabisa kutafuta samaki . Na kanuni ya uvuvi samaki wanapatikana usiku , Yesu ameenda muda ambao hualisia wa kawaida haukubali kuvua. Na anamwambia Petro shusha nyavu kilindini, Petro sababu ya imani kubwa alimwambia kwa neno lako nashusha nyavu. #Luka 5:5 [5]Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. Na kutokea kushusha nyavu walipata samaki wengi kiasi cha nyavu kukatika. #Luka 5:6-7 [6]Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika; . [7]wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama. Kumbe hata wewe upati majibu sababu utaki kujenga imani kubwa katika jambo unalo lifanya. Mfano moyoni mwako kila ukiwaza unasikia kuwa na real estate na uhalisia uoni lakini una kakiwanja mahali au unapo ishi kumbe imani kubwa ni kuanza hata na vyumba viwili ndo vitabadilisha maisha yako. Ni neno la uzima peke yake ndilo Lina badilishaga yote . Jifunze kutii kile unacho kiona kwenye neno na kutokea hapo maisha yako yote yatabadilika. Jitahidi sana kuomba kwa Mungu neno la uzima linabdailishaga yote. Imani inabadilisha yote kabisa na ukiamua kumfuata Yesu na ukalipenda neno maisha yako yatabadilika kabisa. Kuwa na imani kubwa harafu uone matokeo makubwa NAKUOMBEA MUNGU WANGU AKUPE NEEMA YA KUWA NA IMANI KUBWA KTIKA NENO LAKE NA KUTOKEA HAPO JANA YAKO IBADILIKE KABISA NA KUWA KESHO NJEMA KWA JINA LA YESU. Nikutakie asubui njema na siku njema . Naitwa sylvester Mwakabende Build new eden ministry 0622625340 #build new eden #restore men position
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·32 Visualizações
  • Luka 22:31-32
    [31]
    Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano;
    :
    [32]lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.

    Hii ina maana kubwa sana kumbe kuba wakati imani zetu huwa zinashindwa na kuishiwa nguvu kutokana na changamoto ambazo shetani anaweza kuwapitisha watoto wa Mungu.
    .
    Kama Yesu alimuombea petro kuhusu imani yake na sisi tunapaswa kuombea imani zetu ziwe na nguvu nyingi ili zisiyumbe kipindi cha majaribio .

    Kwa mantiki hiyo kama ukuwa mtu wa kuomba na kuiombea imani siku ikiguswa kidogo tu inakutoa kwenye njia.

    Kwanini tunapaswa kuombea imani zetu ziiwe na nguvu kubwa

    1.Imani ndiyo inayo tuokoa roho zetu..

    Roho ya mtu itapoke muujiza wa sawa sawa na imani yetu.

    Mara nyingi sehemu ambazo Yesu alifanya miujiza wengi walipokea sawa sawa na imani zao.

    Imarisha imani yako juu ya Mungu uanze kuishi na kupokea yale Mungu amekuhaidi kuyafanya.

    Kimani zetu ndizo zinaamua aina ya majibu juu maombi yetu.

    Wenye nguvu za Mungu ndio wenye imani juu ya matendo ua Mungu.

    Watu wa Mungu lengo la Kristo ni kanisa liwe na imani kubwa na ndio mna hata baada ya shetani kupata kibali ya kuwajaribu wanafunzi wake aliona ipo sababu ya kumuombea Petro awe na imani kubwa.

    Waebrania 11:8
    [8]Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako

    Na alienda asiko kujua lakini sababu imani yale ilijengwa kiasi cha kuto tikisika sababu yake Ubaba wa imani duniani alipewa yeye na familia yake ikafanywa kuwa taifa na Mungu akaitazama mpaka leo.

    Sijui kama utaona iko haja ya kuimalisha imani zetu kiasi cha shetani kusema kuwa bila wewe Mungu kiuniruhusu mimi siwezi mana umezingira kila kitu chake.

    Maombi ni moja silaha watu wa rohoni wanaitumia kuimalisha imani zao .

    Kama imani yako ilifika kipindi sababu ya kuomba bilz kupokea au majaribu ukaona Mungu amekuacha nataka nikwambie kuw wewe unapendwa na Mungu kuliko unavyo jidhania.

    Kili leo maneno hayakuwa HAKUNA KITAKACHO NITENGA NA UPENDO WA KRISTO YAWE MAISHA MAGUMU ,UMASKINI ,TAABU ,NJAA ,ADHA,UCHI,NA KILA JAMBO LILILOKUWA LINANIRUDISHA NYUMA KIASI CHA KUIASI IMANI NAOMBA BWANA UNIREHEMU NA KUNINYANYUA IMANI YANGU IWE IMARA ZAIDI YA YULE MAMA ALIYE ADHIMIA KUGUSA PINDO LAKO TU NA KUWA MZIMA.

    BWANA YESU NISAIDIE IMANI YANGU ISIYUMBE MIMI NIWE PETRO KWENYE HUDUMA NA WITO WANGU MJARIBU AJAPO KUJA KUNIPEPETA KAMA NGANO IMANI YANGU ISIYUMBE BADALA YAKE IWE IMARA KULIKO JANA NA JUZI.

    BWANA ATAKUPIGANIA NA WEWE UTANYAMAZA KIMYA .
    AMINA ....

    Naitwa mwl sylvester Mwakabende kutoka build
    new eden .

    Karibu kwa mafundisho zaidi unaweza jiunga na sisi katika group letu la watsap.

    https://chat.whatsapp.com/HhjVJc0bcdY5i5LCZnjHZ6

    #build new eden
    #restore men position
    Luka 22:31-32 [31] Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; : [32]lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako. Hii ina maana kubwa sana kumbe kuba wakati imani zetu huwa zinashindwa na kuishiwa nguvu kutokana na changamoto ambazo shetani anaweza kuwapitisha watoto wa Mungu. . Kama Yesu alimuombea petro kuhusu imani yake na sisi tunapaswa kuombea imani zetu ziwe na nguvu nyingi ili zisiyumbe kipindi cha majaribio . Kwa mantiki hiyo kama ukuwa mtu wa kuomba na kuiombea imani siku ikiguswa kidogo tu inakutoa kwenye njia. Kwanini tunapaswa kuombea imani zetu ziiwe na nguvu kubwa 1.Imani ndiyo inayo tuokoa roho zetu.. Roho ya mtu itapoke muujiza wa sawa sawa na imani yetu. Mara nyingi sehemu ambazo Yesu alifanya miujiza wengi walipokea sawa sawa na imani zao. Imarisha imani yako juu ya Mungu uanze kuishi na kupokea yale Mungu amekuhaidi kuyafanya. Kimani zetu ndizo zinaamua aina ya majibu juu maombi yetu. Wenye nguvu za Mungu ndio wenye imani juu ya matendo ua Mungu. Watu wa Mungu lengo la Kristo ni kanisa liwe na imani kubwa na ndio mna hata baada ya shetani kupata kibali ya kuwajaribu wanafunzi wake aliona ipo sababu ya kumuombea Petro awe na imani kubwa. Waebrania 11:8 [8]Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako Na alienda asiko kujua lakini sababu imani yale ilijengwa kiasi cha kuto tikisika sababu yake Ubaba wa imani duniani alipewa yeye na familia yake ikafanywa kuwa taifa na Mungu akaitazama mpaka leo. Sijui kama utaona iko haja ya kuimalisha imani zetu kiasi cha shetani kusema kuwa bila wewe Mungu kiuniruhusu mimi siwezi mana umezingira kila kitu chake. Maombi ni moja silaha watu wa rohoni wanaitumia kuimalisha imani zao . Kama imani yako ilifika kipindi sababu ya kuomba bilz kupokea au majaribu ukaona Mungu amekuacha nataka nikwambie kuw wewe unapendwa na Mungu kuliko unavyo jidhania. Kili leo maneno hayakuwa HAKUNA KITAKACHO NITENGA NA UPENDO WA KRISTO YAWE MAISHA MAGUMU ,UMASKINI ,TAABU ,NJAA ,ADHA,UCHI,NA KILA JAMBO LILILOKUWA LINANIRUDISHA NYUMA KIASI CHA KUIASI IMANI NAOMBA BWANA UNIREHEMU NA KUNINYANYUA IMANI YANGU IWE IMARA ZAIDI YA YULE MAMA ALIYE ADHIMIA KUGUSA PINDO LAKO TU NA KUWA MZIMA. BWANA YESU NISAIDIE IMANI YANGU ISIYUMBE MIMI NIWE PETRO KWENYE HUDUMA NA WITO WANGU MJARIBU AJAPO KUJA KUNIPEPETA KAMA NGANO IMANI YANGU ISIYUMBE BADALA YAKE IWE IMARA KULIKO JANA NA JUZI. BWANA ATAKUPIGANIA NA WEWE UTANYAMAZA KIMYA . AMINA .... Naitwa mwl sylvester Mwakabende kutoka build new eden . Karibu kwa mafundisho zaidi unaweza jiunga na sisi katika group letu la watsap. https://chat.whatsapp.com/HhjVJc0bcdY5i5LCZnjHZ6 #build new eden #restore men position
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·1KB Visualizações
  • Damu ya Yesu kama damu ya Agano.

    Waebrania 8:6
    *[6]Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora*.

    Agano ni muunganiko wa uhai baina ya Mungu na watu wake.

    Agano pia ni kiapo au makubaliano yaliyoandikwa au ahadi kwa kawaida chini ya muhuri kati ya pande mbili au zaidi hasa kwa ajili ya utekelezaji wa hatua fulani

    Mwanzo 22:16
    *[16]akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,*

    Agano lazima liambatane na kiapo chenye kushuhudiwa na vitu au watu.

    50 Ukiwatesa binti zangu, na ukitwaa wake zaidi ya binti zangu, wala hapana mtu pamoja nasi, tazama, Mungu ni shahidi kati ya mimi na wewe

    Ziko aina nyinyi za agano yaweza kuwa

    1.MTU NA MTU
    2.MTU NA VITU
    3.MTU NA SHETANI
    4.MTU NA MUNGU
    5.MUNGU NA VIUMBE VYAKE .
    6.MUNGU NA MTU
    7.MTU NA UZAO WAKE

    Aina zote hizi ili zitamatike au kutimia lazima ziandikwe katika vipokeleo vya sadaka au wengine wanaita vitunza kumbukumbu.

    Yaweza kuwa 1.ARDHI 2.ANGA 3.MAJI 4.MOTO

    Agano lazima liambatane na madhabau kwa maana ya ibada na sadaka.

    Watu wengi sana wanaishi maisha ya mateso pasipo kujua kumbe ni kwa sababu wanaishi ndani ya agano ambalo pengine hata wao hawalijui.

    Sifa za agano
    Agano lenye nguvu huwa lazima liwe la damu.

    Agano lazima libebe matokeo yaneweza kuwa mema(baraka) au mabaya (laana).

    Agano lazima liambatane na maneno au maandishi.

    *Agano huvunjwa na agano*

    Na ahsante Yesu kwa kuwa yeye ndiye bwana wa agano jipya.

    Lengo la Mungu kuja kuleta agano jipya ambalo linamuhusisha Kristo ni kutupa ushindi dhidi ya adui.

    Wagalatia 3:29
    [29]Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.

    Lazima tujue kuomba namna ya kutoka katika masgano ambayo siyo mazuri kwetu na tuyakimbie kabisa.

    Inawezekana kabisa wala usiogope mana maandiko yanasema
    Na imekuwa mtu akiwa ndani ya kristo na amekuwa kiumbe kipya kweli ya kale yote yamesha kwisha kupita

    Natumai umejifunza Mungu akituongoza tunaendelea na sehemu ya pili hapa hapa.

    Naitwa sylvester Mwakabende kutoka ( build new eden)

    #build new eden
    #restore men position
    Damu ya Yesu kama damu ya Agano. Waebrania 8:6 *[6]Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora*. Agano ni muunganiko wa uhai baina ya Mungu na watu wake. Agano pia ni kiapo au makubaliano yaliyoandikwa au ahadi kwa kawaida chini ya muhuri kati ya pande mbili au zaidi hasa kwa ajili ya utekelezaji wa hatua fulani Mwanzo 22:16 *[16]akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,* Agano lazima liambatane na kiapo chenye kushuhudiwa na vitu au watu. 50 Ukiwatesa binti zangu, na ukitwaa wake zaidi ya binti zangu, wala hapana mtu pamoja nasi, tazama, Mungu ni shahidi kati ya mimi na wewe Ziko aina nyinyi za agano yaweza kuwa 1.MTU NA MTU 2.MTU NA VITU 3.MTU NA SHETANI 4.MTU NA MUNGU 5.MUNGU NA VIUMBE VYAKE . 6.MUNGU NA MTU 7.MTU NA UZAO WAKE Aina zote hizi ili zitamatike au kutimia lazima ziandikwe katika vipokeleo vya sadaka au wengine wanaita vitunza kumbukumbu. Yaweza kuwa 1.ARDHI 2.ANGA 3.MAJI 4.MOTO Agano lazima liambatane na madhabau kwa maana ya ibada na sadaka. Watu wengi sana wanaishi maisha ya mateso pasipo kujua kumbe ni kwa sababu wanaishi ndani ya agano ambalo pengine hata wao hawalijui. Sifa za agano Agano lenye nguvu huwa lazima liwe la damu. Agano lazima libebe matokeo yaneweza kuwa mema(baraka) au mabaya (laana). Agano lazima liambatane na maneno au maandishi. *Agano huvunjwa na agano* Na ahsante Yesu kwa kuwa yeye ndiye bwana wa agano jipya. Lengo la Mungu kuja kuleta agano jipya ambalo linamuhusisha Kristo ni kutupa ushindi dhidi ya adui. Wagalatia 3:29 [29]Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi. Lazima tujue kuomba namna ya kutoka katika masgano ambayo siyo mazuri kwetu na tuyakimbie kabisa. Inawezekana kabisa wala usiogope mana maandiko yanasema Na imekuwa mtu akiwa ndani ya kristo na amekuwa kiumbe kipya kweli ya kale yote yamesha kwisha kupita Natumai umejifunza Mungu akituongoza tunaendelea na sehemu ya pili hapa hapa. Naitwa sylvester Mwakabende kutoka ( build new eden) #build new eden #restore men position
    Yay
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·758 Visualizações
  • MUONEKANO WA NABII ISSA MIAKA HIYO ULIKUWAJE ?

    Karibu kila mtu ana dhana fulani kuhusu muonekano wa Yesu Kristo.
    Ndiye mtu aliyechorwa zaidi katika sanaa ya Magharibi. Picha zake hutambuliwa kwa urahisi, ambapo huoneshwa akiwa na nywele na ndevu, akiwa amevalia vazi lefu lenye mikono mirefu linalofanana na kanzu ( la rangi nyeupe), na pia akiwa amejifunga joho (la rangi ya samawati). Muonekano wa Yesu umefahamika sana na wengi kiasi kwamba unaweza kutambuliwa ukiwa hata kwenye mikate au biskuti.

    Picha za sasa za Yesu zinatokana na enzi ya Byzantine, himaya iliyokuwa na mji mkuu wake Constantinople. Ni picha iliyoanza kutumika karne ya nne hivi. Michoro ya Yesu ya wakati wa utawala wa Byzantine ilikuwa ya ishara, na si muonekano wake. Wasanii waliangazia zaidi maana na si kumfananisha na Yesu mwenyewe.
    Picha zao ziliongozwa na dhana ya Yesu kama mtawala, kwenye kiti cha enzi, kama anavyoonyeshwa kwenye mchoro ulio kwenye altari ya kanisa la Santa Pudenziana jijini Roma.

    Yesu anaoneshwa akiwa amevalia mgolole wa rangi ya dhahabu.
    Ndiye mtawala wa dunia yote aliyetoka mbinguni, mfanano wa picha yake ni ule wa sanamu ya Zeus wa Olympus anayeonyeshwa akiwa na nywele ndefu za ndevu kwenye kiti cha enzi. Ni sanamu iliyokuwa maarufu sana wakati huo kiasi kwamba Mfalme Augustus wa Roma alishurutisha naye atengenezewe sanamu kama hiyo, lakini yake ikiwa bila nywele ndefu na ndevu, Wasanii wa Byzantine, walitaka kumuonyesha Kristo kama mtawala kutoka mbinguni, mfalme wa aina yake, na hivyo wakachora wakimuonyesha kama Zeus, lakini akiwa mdogo kidogo wa umri.

    Kilichotokea kadiri miaka ilivyosonga ni kwamba kuonyeshwa huku kwa Kristo kama mtawala kutoka mbinguni - ambapo wakati mwingine ameonyeshwa hata akiwa kama 'hippie' au 'superstar' (kama ilivyo kwenye mchoro huu hapa chini) - ndiko kumekuwa kama kigezo chetu cha Yesu alivyokuwa. Hebu tuchanganue kutoka kichwani hadi vidole vya miguuni. Wakristo wa nyakati za kwanza wakati walipokuwa wanamwonyesha Kristo si kama mtawala kutoka mbinguni, walimuonyesha kama binadamu wa kawaida tu - akiwa hana ndevu na hana nywele ndefu.

    Lakini pengine, kama msomi wa aina yake aliyekuwa akisafiri kutoka eneo moja hadi jingine, Yesu pengine alikuwa na ndevu, kwa sababu hakuwa akienda kwa vinyozi. Kwa kawaida, kuwa mchafu kiasi na kuwa na ndevu ndefu ni sifa ambazo zilihusishwa na wanafalsafa, wasomi wa ngazi ya juu, na kuwatenganisha na watu wa kawaida.
    Mwanafalsafa maarufu wa kundi la Stoic (Wanafalsafa wa Kigiriki waliofuata mafundisho ya mwanzilishi wao Zeno wa Citium mjini Athens mapema karne ya 3 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu) Epictetus aliamini "ilifaa hivyo kwa mujibu wa maumbile." Mambo yalibadilika katika karne ya 1 baada ya kuzaliwa kwa Yesu, wakati wa enzi za Warumi na Wagiriki, ambapo kuwa na nywele fupi na kunyoa ndefu ndiyo mambo yaliyochukuliwa kuwa yafaayo na ya kistaarabu.

    Kuwa na nywele ndefu na ndevu ni mambo ambayo yaliachiwa miungu pekee, si ya watu wa kawaida. Hata wanafalsafa enzi hizo walikuwa na nywele fupi. Ndevu pia hazikuwa sifa za kuwatambulisha Wayahudi enzi hizo. Ukweli ni kwamba moja ya changamoto ambazo waliotaka kuwatesa Wayahudi vipindi mbalimbali katika historia walihangaika sana kuwatofautisha na watu wengine. Hii ni kwa sababu wote walifanana (jambo ambalo limegusiwa katika kitabu cha Wamakabayo). Hata hivyo, picha za wanaume wa Kiyahudi zilizokuwa kwenye sarafu za Judea Capta ambazo zilitolewa na utawala wa Roma baada ya kutekwa kwa mji wa Yerusalemu mwaka 70 baada ya kuzaliwa kwa Yesu zinawaonesha wanaume wakiwa na ndevu, lakini nywele zao si ndefu.

    Kwa hivyo, Yesu, kama mwanafalsafa wa muonekano wa kawaida, kuna uwezekano alikuwa na ndevu lakini si ndefu sana, sawa na wanaume hao walioonyeshwa kwenye sarafu za Judaea Capta, lakini nywele zake basi hazikuwa ndefu sana pia.
    Kama ingetokea kwamba awe na nywele ndefu hata kidogo tu kuliko kawaida, basi angezua mtafaruku Wanaume wa Kiyahudi waliokuwa na ndevu ambazo hazikuwa zimetunzwa vyema na nywele ambazo zilikuwa ndefu kidogo kuliko kawaida walitambulika mara moja kama watu waliokuwa wamekula kiapo cha kuwa Wanazari (Nazarite).

    Hii ilikuwa na maana kwamba wangejitoa wakfu kwa Mungu kwa kipindi fulani, ambapo hawangekunywa vileo wala kuzikata nywele zao. Mwisho wa kipindi hicho, wangenyolewa nywele zao katika sherehe maalum hekaluni Jerusalem (kama inavyoelezwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Sura ya 21, aya ya 24).
    Lakini Yesu hakuwa amekula kiapo cha kuwa Mnazari, kwa sababu mara nyingi tunamsikia kwenye Biblia akinywa divai - wakosoaji wake hata wakati mwingine wanamshutumu kwa kunywa divai sana, kupita kiasi (Matayo Sura ya 11, aya ya 19). Kama angekuwepo na nywele ndefu, na kuonekana kama Mnazari, tungelitarajia basi kuwepo na tamko pahala fulani kuhusu tofauti ya muonekano wake na matendo aliyokuwa akiyafanya ambayo hayakuendana na Unazari. Hali kwamba alikuwa akinywa divai yenyewe ingekuwa tatizo kubwa.

    Wakati Yesu alipoishi, matajiri walizoea kuvalia kanzu na majoyo ya vitambaa vya thamani, kuonyesha hadhi yao katika jamii. Katika moja ya mahubiri yake, Yesu anasema : "Jihadharini na walimu wa sheria (waandishi). Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu (stolai), na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Pia wao hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kupewa nafasi za heshima katika karamu." Mafundisho haya ya Yesu kwa kawaida huchukuliwa kama yenye maelezo ya kuaminika zaidi kwenye Injili, hivyo tunaweza kuwa na msingi kuamini kwamba Yesu hakuvalia mavazi kama hayo marefu. Kwa jumla, mwanamume wakati huo wa Yesu angevalia gwanda au kanzu fupi hivi, na mwanamke angevalia vazi lililomfika kwenye kifundo cha mguu.

    Kwa hivyo, katika karne ya 2 kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume, Paul na Thecla, inapotokea kwamba Thecla ambaye ni mwanamke anavalia kanzu fupi kama mwanamume, hilo ni jambo linaloshangaza sana. Kanzu hizi kwa kawaida zingekuwa na ukanda au mstari wa rangi tofauti kutoka kwenye bega hadi kwenye pindo sehemu ya chini. Ni vazi ambalo lingeshonwa au kufumwa kama kipande kimoja cha vazi. Juu ya kanzu hiyo, ungejifunga joho au vazi jingine la nje, na tunajua kwamba Yesu alivalia vazi kama hilo kwa sababu ndilo lililoguswa na mwanamke aliyetaka kuponywa naye. (Marko 5:27): Alikuwa amesikia habari za Yesu, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, kwa maana alisema moyoni mwake, 'Kama nikiweza kuligusa vazi lake tu, nitaponywa.') Vazi hilo la nje lilifumwa kwa manyoya, lakini halikuwa zito sana na ndipo ili uhisi joto ingemlazimu mtu kuvalia mavazi mawili kama hayo.

    Vazi hilo lingevaliwa kwa njia nyingi, na wakati mwingine lingening'inia hadi chini ya magoti na kulifunika lile kanzu fupi la ndani. (Baadhi ya wanafalsafa walizoea kuvalia vazi hilo la nje pekee bila kuvalia ile kanzu ya ndani na kuacha sehemu ya bega au kifua ikiwa wazi). Mamlaka na hadhi ya mtu ni vitu ambavyo vilidhihirishwa kupitia ubora, ukubwa na rangi ya mavazi hayo ya nje. Rangi ya zambarau na baadhi ya aina za rangi ya buluu (samawati) ni rangi zilizoashiria utajiri, hadhi na kujionea fahari. Zilikuwa ni rangi za kifahari kwa sababu viungo vya kutengeneza rangi hizo vilikuwa adimu na ghali sana.

    Lakini rangi pia huashiria kitu kingine tofauti. Mwanahistoria Josephus, anawaeleza walokole waliofahamika kama Zealots (kundi la Wayahudi wa itikadi kali waliotaka kuwafurusha Warumi kutoka Judea) kama kundi la wahalifu wauaji waliovalia mavazi ya nje yaliyopakwa rangi kwa jina - mavazi anayoyaita chlanidia - kuashiria kwamba yalikuwa ni kama mavazi yaliyovaliwa na wanawake. Hii inaashiria kwamba wanaume kamili, kama hawakuwa na cheo cha juu zaidi katika jamii, walifaa kuvalia mavazi yasiyopakwa rangi.
    Yesu hakuvalia mavazi meupe hata hivyo. Haya yalikuwa mavazi ya kipekee na yalihitaji kupaushwa mara kwa mara (kufanywa meupe tena) au kupakwa chokaa. Judea, mavazi kama hayo meupe yalihusishwa na kundi lililofahamika kama Essenes - ambao ni watu waliofuata ufasiri mkali wa sheria za Kiyahudi. Tofauti kati ya mavazi ya Yesu na mavazi mengine ya rangi nyeupe ya kung'aa inaelezwa kwenye sura ya 9 ya Marko ambapo anaandamana na mitume watatu mlimani.

    Yesu aliwachukua "Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao. Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angaliweza kuyangʼarisha. Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu." Marko anaeleza kwamba mavazi ya Yesu yaligeuka rangi yakawa meupe sana, hapa anarejelea vazi la ndani na si la nje. Kabla ya kugeuka sura huku kwa Yesu, anaoneshwa na Marko kama mwanamume wa kawaida, aliyevalia mavazi ya kawaida, ambayo ni ya rangi ambayo haijapaushwa. Katika hali ambayo ndipo yang'ae na kuangaza unahitaji kumpelekea fundi.

    Tunaelezwa zaidi kuhusu mavazi ya Yesu wakati wa kusulubiwa kwake, pale wanajeshi wa Kirumi wanapoyakata mavazi yake ya nje vipande vinne (Yohana19:23: Askari walipokwisha kumsulubisha Yesu, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini.) Kuna uwezekano mavazi hayo ya nje yalikuwa mavazi mawili.

    Moja ya vazi hili huenda lilikuwa ni tallith, ambalo ni vazi la kujifunga Kiyahudi wakati wa maombi. Vazi hili lenye shada (tzitzith) limetajwa moja kwa moja na Yesu katika kitabu cha Mathayo 23:5 anapozungumza kuhusu walimu wa sheria na Mafarisayo (Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao). Lilikuwa ni vazi la nje lisilo zito, ambalo kawaida lilitengenezwa kwa kitambaa cha manyoya na lilikuwa la rangi ya malai hivi (krimu), na pengine lilikuwa na ukanda au mstari wa rangi ya nili (bluu iliyoiva).

    Miguuni, Yesu angevalia ndara (kandambili au malapa). Kila mtu wakati huo alivalia ndara. Katika mapango yaliyo jangwani karibu na Bahari ya Chumvi (Bahari Mfu) na Masada, ndara za wakati alipoishi Yesu zimegunduliwa, na tunaweza kutazama ndara ambazo huenda alivaa zilivyoonekana. Zilikuwa hazijafanyiwa kazi nyingi sana ya kiufundi. Soli (nyayo au kikanyagio) zake zilikuwa vipande vigumu vya ngozi vilivyoshonwa pamoja, na juu kulikuwa ni kanda za ngozi ambazo mbele zingeingizwa katikati ya vidole, kama malapa tu ya siku hizi.

    Yesu (Nabii Issa) Alikuwa Myahudi, na uso wake pia bila shaka ungefanana na Wayahudi wa wakati huo. Hali kwamba Yesu alikuwa Myahudi (au Mjudea) ni jambo linalorejelewa katika vitabu vingi, zikiwemo barua za Mtume Paulo. Na katika barua yake kwa Waebrania, anaandika: "Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda" (Sura ya 7:14) Kwa hivyo, Myahudi wa wakati huo, mwanamume wa miaka 30 hivi alipoanza kueneza Injili kwa mujibu wa Luka 3, pia akiwa ni mwenye ngozi nyeusi kama ilivyokuwa kwa wayahudi wengi zama zile waliokuwa wakitembeleana na ndugu zao wa Misri (Kushi) kemet.

    Mwaka 2001 mwanaantholopojia (mtaalamu wa elimu ya binadamu hasa elimu ihusuyo habari zinazohusu asili na maendeleo yake ya awali) Richard Neave alitengeneza mfano wa mwanamume wa Galilaya wa zama za Yesu ambao ulitumiwa kwa jina Son of God (Mwana wa Mungu). Alitumia fuvu lililopatikana katika eneo hilo. Hakusema kwamba huo ulikuwa muonekano wa uso wa Yesu. Mfano ulikuwa tu wa kuchochea hisia na kuwafanya watu kumfikiria Yesu kama mwanamume wa zama hizo na eneo hilo, kwa sababu hakuna mchoro wala maelezo yaliyopo ya kina kuhusu muonekano wake halisi.

    Ingawa tunaweza kupata viashiria kutoka kwa teknolojia na kutumia mifupa ya watu wa kale, kiashiria cha karibu sana kuhusu pengine Yesu alionekana vipi labda kinaweza kutokana na mchoro wa Musa kwenye ukuta wa sinagogi ya karne ya 3 ya Dura-Europos, kwani mchoro huo unaonesha jinsi Myahudi wa hekima alidhaniwa kuwa wakati wa utawala wa Wagiriki na Warumi. Musa anaoneshwa akiwa na mavazi ambayo hayajapaushwa, na moja ya vazi lake la nje ni tallith.

    Katika mchoro huo wa Dura wa Musa akitenganisha maji kwenye Bahari ya Sham ili Waisraeli wapite, unaweza kuziona shada (tzitzith) kwenye kona za vazi hilo. Kwa kiwango kikubwa, picha hiyo pengine inatoa msingi bora zaidi wa kumfikiria Yesu alivyokuwa badala ya picha za sasa zinazoongozwa na busara na mawazo ya enzi ya Byzantine - alikuwa na nywele fupi, ndevu fupi, na alikuwa amevalia kanzu fupi lenye mikono mifupi, na alikuwa na joho au vazi la nje.

    Makala hii chimbuko lake ni makala ya Kiingereza ya Joan Taylor ambaye ni profesa wa kitivo cha Asili ya Ukristo na Hekalu la Pili la Wayahudi katika Chuo Kikuu cha King's College London na ndiye mwandishi wa kitabu kwa jina The Essenes, the Scrolls and the Dead Sea.
    MUONEKANO WA NABII ISSA MIAKA HIYO ULIKUWAJE ? Karibu kila mtu ana dhana fulani kuhusu muonekano wa Yesu Kristo. Ndiye mtu aliyechorwa zaidi katika sanaa ya Magharibi. Picha zake hutambuliwa kwa urahisi, ambapo huoneshwa akiwa na nywele na ndevu, akiwa amevalia vazi lefu lenye mikono mirefu linalofanana na kanzu ( la rangi nyeupe), na pia akiwa amejifunga joho (la rangi ya samawati). Muonekano wa Yesu umefahamika sana na wengi kiasi kwamba unaweza kutambuliwa ukiwa hata kwenye mikate au biskuti. Picha za sasa za Yesu zinatokana na enzi ya Byzantine, himaya iliyokuwa na mji mkuu wake Constantinople. Ni picha iliyoanza kutumika karne ya nne hivi. Michoro ya Yesu ya wakati wa utawala wa Byzantine ilikuwa ya ishara, na si muonekano wake. Wasanii waliangazia zaidi maana na si kumfananisha na Yesu mwenyewe. Picha zao ziliongozwa na dhana ya Yesu kama mtawala, kwenye kiti cha enzi, kama anavyoonyeshwa kwenye mchoro ulio kwenye altari ya kanisa la Santa Pudenziana jijini Roma. Yesu anaoneshwa akiwa amevalia mgolole wa rangi ya dhahabu. Ndiye mtawala wa dunia yote aliyetoka mbinguni, mfanano wa picha yake ni ule wa sanamu ya Zeus wa Olympus anayeonyeshwa akiwa na nywele ndefu za ndevu kwenye kiti cha enzi. Ni sanamu iliyokuwa maarufu sana wakati huo kiasi kwamba Mfalme Augustus wa Roma alishurutisha naye atengenezewe sanamu kama hiyo, lakini yake ikiwa bila nywele ndefu na ndevu, Wasanii wa Byzantine, walitaka kumuonyesha Kristo kama mtawala kutoka mbinguni, mfalme wa aina yake, na hivyo wakachora wakimuonyesha kama Zeus, lakini akiwa mdogo kidogo wa umri. Kilichotokea kadiri miaka ilivyosonga ni kwamba kuonyeshwa huku kwa Kristo kama mtawala kutoka mbinguni - ambapo wakati mwingine ameonyeshwa hata akiwa kama 'hippie' au 'superstar' (kama ilivyo kwenye mchoro huu hapa chini) - ndiko kumekuwa kama kigezo chetu cha Yesu alivyokuwa. Hebu tuchanganue kutoka kichwani hadi vidole vya miguuni. Wakristo wa nyakati za kwanza wakati walipokuwa wanamwonyesha Kristo si kama mtawala kutoka mbinguni, walimuonyesha kama binadamu wa kawaida tu - akiwa hana ndevu na hana nywele ndefu. Lakini pengine, kama msomi wa aina yake aliyekuwa akisafiri kutoka eneo moja hadi jingine, Yesu pengine alikuwa na ndevu, kwa sababu hakuwa akienda kwa vinyozi. Kwa kawaida, kuwa mchafu kiasi na kuwa na ndevu ndefu ni sifa ambazo zilihusishwa na wanafalsafa, wasomi wa ngazi ya juu, na kuwatenganisha na watu wa kawaida. Mwanafalsafa maarufu wa kundi la Stoic (Wanafalsafa wa Kigiriki waliofuata mafundisho ya mwanzilishi wao Zeno wa Citium mjini Athens mapema karne ya 3 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu) Epictetus aliamini "ilifaa hivyo kwa mujibu wa maumbile." Mambo yalibadilika katika karne ya 1 baada ya kuzaliwa kwa Yesu, wakati wa enzi za Warumi na Wagiriki, ambapo kuwa na nywele fupi na kunyoa ndefu ndiyo mambo yaliyochukuliwa kuwa yafaayo na ya kistaarabu. Kuwa na nywele ndefu na ndevu ni mambo ambayo yaliachiwa miungu pekee, si ya watu wa kawaida. Hata wanafalsafa enzi hizo walikuwa na nywele fupi. Ndevu pia hazikuwa sifa za kuwatambulisha Wayahudi enzi hizo. Ukweli ni kwamba moja ya changamoto ambazo waliotaka kuwatesa Wayahudi vipindi mbalimbali katika historia walihangaika sana kuwatofautisha na watu wengine. Hii ni kwa sababu wote walifanana (jambo ambalo limegusiwa katika kitabu cha Wamakabayo). Hata hivyo, picha za wanaume wa Kiyahudi zilizokuwa kwenye sarafu za Judea Capta ambazo zilitolewa na utawala wa Roma baada ya kutekwa kwa mji wa Yerusalemu mwaka 70 baada ya kuzaliwa kwa Yesu zinawaonesha wanaume wakiwa na ndevu, lakini nywele zao si ndefu. Kwa hivyo, Yesu, kama mwanafalsafa wa muonekano wa kawaida, kuna uwezekano alikuwa na ndevu lakini si ndefu sana, sawa na wanaume hao walioonyeshwa kwenye sarafu za Judaea Capta, lakini nywele zake basi hazikuwa ndefu sana pia. Kama ingetokea kwamba awe na nywele ndefu hata kidogo tu kuliko kawaida, basi angezua mtafaruku Wanaume wa Kiyahudi waliokuwa na ndevu ambazo hazikuwa zimetunzwa vyema na nywele ambazo zilikuwa ndefu kidogo kuliko kawaida walitambulika mara moja kama watu waliokuwa wamekula kiapo cha kuwa Wanazari (Nazarite). Hii ilikuwa na maana kwamba wangejitoa wakfu kwa Mungu kwa kipindi fulani, ambapo hawangekunywa vileo wala kuzikata nywele zao. Mwisho wa kipindi hicho, wangenyolewa nywele zao katika sherehe maalum hekaluni Jerusalem (kama inavyoelezwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Sura ya 21, aya ya 24). Lakini Yesu hakuwa amekula kiapo cha kuwa Mnazari, kwa sababu mara nyingi tunamsikia kwenye Biblia akinywa divai - wakosoaji wake hata wakati mwingine wanamshutumu kwa kunywa divai sana, kupita kiasi (Matayo Sura ya 11, aya ya 19). Kama angekuwepo na nywele ndefu, na kuonekana kama Mnazari, tungelitarajia basi kuwepo na tamko pahala fulani kuhusu tofauti ya muonekano wake na matendo aliyokuwa akiyafanya ambayo hayakuendana na Unazari. Hali kwamba alikuwa akinywa divai yenyewe ingekuwa tatizo kubwa. Wakati Yesu alipoishi, matajiri walizoea kuvalia kanzu na majoyo ya vitambaa vya thamani, kuonyesha hadhi yao katika jamii. Katika moja ya mahubiri yake, Yesu anasema : "Jihadharini na walimu wa sheria (waandishi). Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu (stolai), na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Pia wao hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kupewa nafasi za heshima katika karamu." Mafundisho haya ya Yesu kwa kawaida huchukuliwa kama yenye maelezo ya kuaminika zaidi kwenye Injili, hivyo tunaweza kuwa na msingi kuamini kwamba Yesu hakuvalia mavazi kama hayo marefu. Kwa jumla, mwanamume wakati huo wa Yesu angevalia gwanda au kanzu fupi hivi, na mwanamke angevalia vazi lililomfika kwenye kifundo cha mguu. Kwa hivyo, katika karne ya 2 kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume, Paul na Thecla, inapotokea kwamba Thecla ambaye ni mwanamke anavalia kanzu fupi kama mwanamume, hilo ni jambo linaloshangaza sana. Kanzu hizi kwa kawaida zingekuwa na ukanda au mstari wa rangi tofauti kutoka kwenye bega hadi kwenye pindo sehemu ya chini. Ni vazi ambalo lingeshonwa au kufumwa kama kipande kimoja cha vazi. Juu ya kanzu hiyo, ungejifunga joho au vazi jingine la nje, na tunajua kwamba Yesu alivalia vazi kama hilo kwa sababu ndilo lililoguswa na mwanamke aliyetaka kuponywa naye. (Marko 5:27): Alikuwa amesikia habari za Yesu, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, kwa maana alisema moyoni mwake, 'Kama nikiweza kuligusa vazi lake tu, nitaponywa.') Vazi hilo la nje lilifumwa kwa manyoya, lakini halikuwa zito sana na ndipo ili uhisi joto ingemlazimu mtu kuvalia mavazi mawili kama hayo. Vazi hilo lingevaliwa kwa njia nyingi, na wakati mwingine lingening'inia hadi chini ya magoti na kulifunika lile kanzu fupi la ndani. (Baadhi ya wanafalsafa walizoea kuvalia vazi hilo la nje pekee bila kuvalia ile kanzu ya ndani na kuacha sehemu ya bega au kifua ikiwa wazi). Mamlaka na hadhi ya mtu ni vitu ambavyo vilidhihirishwa kupitia ubora, ukubwa na rangi ya mavazi hayo ya nje. Rangi ya zambarau na baadhi ya aina za rangi ya buluu (samawati) ni rangi zilizoashiria utajiri, hadhi na kujionea fahari. Zilikuwa ni rangi za kifahari kwa sababu viungo vya kutengeneza rangi hizo vilikuwa adimu na ghali sana. Lakini rangi pia huashiria kitu kingine tofauti. Mwanahistoria Josephus, anawaeleza walokole waliofahamika kama Zealots (kundi la Wayahudi wa itikadi kali waliotaka kuwafurusha Warumi kutoka Judea) kama kundi la wahalifu wauaji waliovalia mavazi ya nje yaliyopakwa rangi kwa jina - mavazi anayoyaita chlanidia - kuashiria kwamba yalikuwa ni kama mavazi yaliyovaliwa na wanawake. Hii inaashiria kwamba wanaume kamili, kama hawakuwa na cheo cha juu zaidi katika jamii, walifaa kuvalia mavazi yasiyopakwa rangi. Yesu hakuvalia mavazi meupe hata hivyo. Haya yalikuwa mavazi ya kipekee na yalihitaji kupaushwa mara kwa mara (kufanywa meupe tena) au kupakwa chokaa. Judea, mavazi kama hayo meupe yalihusishwa na kundi lililofahamika kama Essenes - ambao ni watu waliofuata ufasiri mkali wa sheria za Kiyahudi. Tofauti kati ya mavazi ya Yesu na mavazi mengine ya rangi nyeupe ya kung'aa inaelezwa kwenye sura ya 9 ya Marko ambapo anaandamana na mitume watatu mlimani. Yesu aliwachukua "Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao. Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angaliweza kuyangʼarisha. Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu." Marko anaeleza kwamba mavazi ya Yesu yaligeuka rangi yakawa meupe sana, hapa anarejelea vazi la ndani na si la nje. Kabla ya kugeuka sura huku kwa Yesu, anaoneshwa na Marko kama mwanamume wa kawaida, aliyevalia mavazi ya kawaida, ambayo ni ya rangi ambayo haijapaushwa. Katika hali ambayo ndipo yang'ae na kuangaza unahitaji kumpelekea fundi. Tunaelezwa zaidi kuhusu mavazi ya Yesu wakati wa kusulubiwa kwake, pale wanajeshi wa Kirumi wanapoyakata mavazi yake ya nje vipande vinne (Yohana19:23: Askari walipokwisha kumsulubisha Yesu, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini.) Kuna uwezekano mavazi hayo ya nje yalikuwa mavazi mawili. Moja ya vazi hili huenda lilikuwa ni tallith, ambalo ni vazi la kujifunga Kiyahudi wakati wa maombi. Vazi hili lenye shada (tzitzith) limetajwa moja kwa moja na Yesu katika kitabu cha Mathayo 23:5 anapozungumza kuhusu walimu wa sheria na Mafarisayo (Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao). Lilikuwa ni vazi la nje lisilo zito, ambalo kawaida lilitengenezwa kwa kitambaa cha manyoya na lilikuwa la rangi ya malai hivi (krimu), na pengine lilikuwa na ukanda au mstari wa rangi ya nili (bluu iliyoiva). Miguuni, Yesu angevalia ndara (kandambili au malapa). Kila mtu wakati huo alivalia ndara. Katika mapango yaliyo jangwani karibu na Bahari ya Chumvi (Bahari Mfu) na Masada, ndara za wakati alipoishi Yesu zimegunduliwa, na tunaweza kutazama ndara ambazo huenda alivaa zilivyoonekana. Zilikuwa hazijafanyiwa kazi nyingi sana ya kiufundi. Soli (nyayo au kikanyagio) zake zilikuwa vipande vigumu vya ngozi vilivyoshonwa pamoja, na juu kulikuwa ni kanda za ngozi ambazo mbele zingeingizwa katikati ya vidole, kama malapa tu ya siku hizi. Yesu (Nabii Issa) Alikuwa Myahudi, na uso wake pia bila shaka ungefanana na Wayahudi wa wakati huo. Hali kwamba Yesu alikuwa Myahudi (au Mjudea) ni jambo linalorejelewa katika vitabu vingi, zikiwemo barua za Mtume Paulo. Na katika barua yake kwa Waebrania, anaandika: "Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda" (Sura ya 7:14) Kwa hivyo, Myahudi wa wakati huo, mwanamume wa miaka 30 hivi alipoanza kueneza Injili kwa mujibu wa Luka 3, pia akiwa ni mwenye ngozi nyeusi kama ilivyokuwa kwa wayahudi wengi zama zile waliokuwa wakitembeleana na ndugu zao wa Misri (Kushi) kemet. Mwaka 2001 mwanaantholopojia (mtaalamu wa elimu ya binadamu hasa elimu ihusuyo habari zinazohusu asili na maendeleo yake ya awali) Richard Neave alitengeneza mfano wa mwanamume wa Galilaya wa zama za Yesu ambao ulitumiwa kwa jina Son of God (Mwana wa Mungu). Alitumia fuvu lililopatikana katika eneo hilo. Hakusema kwamba huo ulikuwa muonekano wa uso wa Yesu. Mfano ulikuwa tu wa kuchochea hisia na kuwafanya watu kumfikiria Yesu kama mwanamume wa zama hizo na eneo hilo, kwa sababu hakuna mchoro wala maelezo yaliyopo ya kina kuhusu muonekano wake halisi. Ingawa tunaweza kupata viashiria kutoka kwa teknolojia na kutumia mifupa ya watu wa kale, kiashiria cha karibu sana kuhusu pengine Yesu alionekana vipi labda kinaweza kutokana na mchoro wa Musa kwenye ukuta wa sinagogi ya karne ya 3 ya Dura-Europos, kwani mchoro huo unaonesha jinsi Myahudi wa hekima alidhaniwa kuwa wakati wa utawala wa Wagiriki na Warumi. Musa anaoneshwa akiwa na mavazi ambayo hayajapaushwa, na moja ya vazi lake la nje ni tallith. Katika mchoro huo wa Dura wa Musa akitenganisha maji kwenye Bahari ya Sham ili Waisraeli wapite, unaweza kuziona shada (tzitzith) kwenye kona za vazi hilo. Kwa kiwango kikubwa, picha hiyo pengine inatoa msingi bora zaidi wa kumfikiria Yesu alivyokuwa badala ya picha za sasa zinazoongozwa na busara na mawazo ya enzi ya Byzantine - alikuwa na nywele fupi, ndevu fupi, na alikuwa amevalia kanzu fupi lenye mikono mifupi, na alikuwa na joho au vazi la nje. Makala hii chimbuko lake ni makala ya Kiingereza ya Joan Taylor ambaye ni profesa wa kitivo cha Asili ya Ukristo na Hekalu la Pili la Wayahudi katika Chuo Kikuu cha King's College London na ndiye mwandishi wa kitabu kwa jina The Essenes, the Scrolls and the Dead Sea.
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·2KB Visualizações
  • Je, Ni Sahihi Kuombea Marehemu/Mtu Aliyekufa?

    = Mtu akishakufa huwezi tena kumwombea chochote, haifai hata kumwombea apumzike kwa amani au awekwe mahala pema peponi. Hiyo nafasi haipo kabisa maana mara baada ya kufa ni hukumu.

    = Mara mtu akifa, hukumu hufanyika halafu wafu huwekwa eneo la mangojeo yaani kuzimu Kwa wenye dhambi na peponi kwa watakatifu wakingojea ujio wa Yesu Kristo. Baada ya hapo kutakuwa na mauti ya pili kwa wenye dhambi, yaani kutupwa kwenye ziwa la moto.

    >> Waebrania 9:27
    Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;

    = Kwa hiyo, mtu asipotengeneza maisha yake akiwa hai asitarajie kuombewa aende peponi akiisha kufa. Pia waliokufa hata kama waliishi maisha matakatifu hatuwezi kuwaomba watuombee maana tutakuwa tunaomba wafu. Ibada ya wafu ni chukizo kwa Mungu.

    >> Kumbukumbu la Torati 18:10-11
    10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,

    11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.

    = Tunao waombezi wawili wakuu kule mbinguni; Yesu Kristo na Roho Mtakatifu.

    = Mtu akishakufa mawasiliano hukatwa kati ya walio hai na waliokufa. Hakuna namna unaweza kumwombea chochote ili kubadilisha chochote wala huwezi kumwomba akuombee.

    >> Mhubiri 9:5
    5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

    = Mfano sahihi angalia kwa tajiri na masikini Lazaro;
    >>Luka 16: 20-30
    19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.

    20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,

    21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.

    22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.

    23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.

    24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.

    25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.

    26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.

    27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,

    28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.

    29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.

    30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.

    31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.
    Je, Ni Sahihi Kuombea Marehemu/Mtu Aliyekufa? = Mtu akishakufa huwezi tena kumwombea chochote, haifai hata kumwombea apumzike kwa amani au awekwe mahala pema peponi. Hiyo nafasi haipo kabisa maana mara baada ya kufa ni hukumu. = Mara mtu akifa, hukumu hufanyika halafu wafu huwekwa eneo la mangojeo yaani kuzimu Kwa wenye dhambi na peponi kwa watakatifu wakingojea ujio wa Yesu Kristo. Baada ya hapo kutakuwa na mauti ya pili kwa wenye dhambi, yaani kutupwa kwenye ziwa la moto. >> Waebrania 9:27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; = Kwa hiyo, mtu asipotengeneza maisha yake akiwa hai asitarajie kuombewa aende peponi akiisha kufa. Pia waliokufa hata kama waliishi maisha matakatifu hatuwezi kuwaomba watuombee maana tutakuwa tunaomba wafu. Ibada ya wafu ni chukizo kwa Mungu. >> Kumbukumbu la Torati 18:10-11 10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. = Tunao waombezi wawili wakuu kule mbinguni; Yesu Kristo na Roho Mtakatifu. = Mtu akishakufa mawasiliano hukatwa kati ya walio hai na waliokufa. Hakuna namna unaweza kumwombea chochote ili kubadilisha chochote wala huwezi kumwomba akuombee. >> Mhubiri 9:5 5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. = Mfano sahihi angalia kwa tajiri na masikini Lazaro; >>Luka 16: 20-30 19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. 20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, 21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. 22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. 23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. 24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. 25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. 26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. 27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, 28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. 29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. 30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu. 31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.
    Love
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·1KB Visualizações