Passa a Pro

  • OPERATION ENTEBBE -4

    Katika sehemmu iliyopita nilieleza namna ambavyo baada ya madege ya kivita ya Lockheed Harcules C-130 kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe na moja ya ndege hizo kwenda moja kwa moja karibu na geti la Terminal huku mlango wa nyuma ukiwa wazi na kutoka gari aina na Mercides pamoja na Land Rover kufanana kabisa na msafara wa Idd Amin atembeleapo uwanja wa ndege, la kini ajabu ni kwamba walijikuta wakinyooshewa bunduki na wanajeshi waliokuwa wanalinda getini…
    Walikuwa hawana taarifa kuwa Amin alikuwa amebadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda nyeupe kabla ya safari yake ya kwenda Mauritius kwenye kikao cha O.A.U.
    Tuendelee…
    SEHEMU TA NNE
    Wanajeshi hawa wawili wa Uganda waliokuwa getini walinyanyua bunduki zao aina ya Kalashnikov na hawakuonyesha dalili kwamba labda walikuwa wanataka kufanya ukaguzi wa kawaida tu kabla ya kuwaruhusu, walionyesha dhahiri kabisa kwamba walikuwa wanataka kufanya shambulio.
    Kabla wanajeshi hao wa Uganda kufanya lolote lile, Netanyahu na komando mwingine ambao walikuwa ndani ya gari walitumia weledi wao kufanya uamuzi makini wa haraka kwa kufyatua risasi kutoka kwenye bastola zao zenye ‘silencer’ na mara moja wale wanajeshi wawili wa Uganda walienda chini.
    Lakini moja ya wale wanajeshi wa Uganda waliodondoka chini baada ya kufyatuliwa risasi, hakufa mara moja na alikuwa anajitahidi kuinuka. Hii ilisababisha komando mwingine wa Israel kufyatua risasi lakini safari hii huyu komando wa Israel alifyatua risasi kutoka kwenye bunduki ambayo haina ‘silencer’. Hii iliwashitua wanajeshi wengine wa Uganda waliokuwa nje ya Terminal na kuanza kukimbilia walipokuwa wanasikia milio ya risasi inatokea huku wanafyatua risasi.
    Kwa maneno mengine ilikuwa kwa kiasi fulani walichokuwa wamekipanga makomando wa Israel, kufanya shambulio la kushitukiza lakini mpaka muda huu tayari ile ‘element of surprise’ ilikuwa haipo tena, jeshi la Uganda lilikuwa limeshitukia ‘mchezo’.
    Bila kuchelewa sana, makomando wote walikuwa kwenye zile gari mbili (Mercedes na Land Rover) waliruka nje ya gari na kukimbia kuelekea ndani ya terminal.
    Vichwani mwao walikuwa bado hawajaondokewa na kumbukumbu ya oparesheni kama hii iliyotokea miaka miwili iliyopita nchini Israel kwenye mji wa Ma’a lot ambapowatekaji wa KIpalestina baada ya kushituka kuwa kulikuwa na makomando wa Israel wamefika kufanya uokozi, waliwapiga risasi mateka wao 25 ambao kati yao 22 walikuwa ni watoto wadogo.
    Hivyo Netanyahu na wenzake hawakutaka kitu kama hiki kjitokeze tena… Netenyahu na makomando wenzake wa Syeret Matkal kwa ustadi wa hali ya juu walikimbia na kuingia ndani ya terminal na kuwaacha vile vikosi vingine kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliopo nje ya terminal (kama nilivyoeleza juzi namna kikosi kilivyogawanywa kwenye vikundi vidogo kila kimoja kikipewa jukumu lake).
    Mateka wanaeleza kwamba baada ya mpambano ya risasi kuanza huko nje ya terminal waliwaona watekaji kadhaa wakiongozwa na yule aliyeonekana kama kiongozi wao, Wilfred Bose waliingia ndani ya terminal wakiwa wanahaha kama wamechanganyikiwa wasijue wafanye nini, ilionekana dhahiri kuwa walikuwa hawajajiandaa kwa hili shambulio la ghafla, ilionekana dhahiri kwamba katika akili yao walikuwa wanasubiria Israel kutimiza masharti yao ili waweze kuachia mateka.
    Kuna muda Wilfred Bose alionekana kunyoonya bunduki yake kwa mateka kama vile anawataka kuwamininia risasi lakini alikuwa anashindwa kufanya uamuzi huo. Bose aligeuka ghafla baada ya kusikia kishindo cha mlango wa terminal ukifunguliwa.
    Makomando wa Israel walikuwa wametumia weledi na ustadi wao wa hali ya juu kuingia ndani ya terminal kwa muda sahihi kabla ya Wilfred Bose na wenzake kufanya uamuzi wowote wa kuua mateka.
    Makomando wa Israel walipoingia tu ndani ya terminal, mmoja wao mkononi walikuwa na kipaza sauti aina ya ‘megaphone’ na alikuwa anaongeea kwa nguvu kwa lugha ya kihebrania, “Lay down, Lay down. We are Israel soldiers. Lay down. Lay down!!”.
    Mateka wote wa kiisrael hata wale waliokuwa wamekaa kitako walilala chini, hivyo ndani ya sekunde chache tu kila mtu ambaye alibakia amesimama alikuwa ni halali yao kumtandika risasi.
    Kwa bahati mbaya kulikuwa na mateka kadhaa ambao wwalikuwa hawajui kihebreania sawia na hii iliwagharimu sana. Kwa mfano kulikuwa na kijana wa mika 19 aliyeitwa Jean-Jacques Maimoni, huyu alikuwa amehamia Israel siku si nyingi sana kutokea nchini ufaransa. Lilipotolewa tangazo hilo la kila mtu kulala chini hakuelewa na alibakia akiwa amesimama na alitandikwa risasi na makomando wa Israel pamoja na wale watekaji. Kijana huyu hakuwa peke yake, lakini pia kulikuwa na mateka mwingine aliyeitwa Ida Borochovitch, ambaye alihamia Israel kutoka nchini Urusi.
    Risasi zilirindima kwa takribani dakika mbili nzima na baadae ukimya wa kama sekunde 15 ukatawala na moja wa makomando wa kiisrael akauliza kwa kiebrania, “where are the rest of them?” (“wako wapi wengine?”). Mateka wakaonyesha kidole kwenye chumba kidogo kilichopo pembeni.
    Makomando wakarusha mabomu kadhaa ya kutupa kwa mkono na kisha kuingia ndani ya chumba hicho na kuwamiminia risasi wote ambao walikuwa humo.
    Milio ya risasi ndani ya terminal hatimaye ilikuwa imekoma japo bado huko nje walisikia majibizano ya risasi. Mwanajeshi mmoja wa Israel kati ya wale waliopo ndani ya terminal, kwa sauti ya utulivu kabisa na katika lugha ya kihebrania aliwatangazia mateka, “listen guys, we’ve come to take you home!” (“sikilizeni, tumekuja kuwachukua kuwarudisha nyumbani!”).
    Baada ya hapo makomando walianza kuwatoa mateka kutoka kwenye terminal na kuwapakia kwenye ndege kwa tahadhari kubwa huku wale wenzao wengine wakiendelea kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanarusha risasi kutoka kwenye maeneo ya kujificha ndani ya uwanja wa ndege.
    Wakiwa wanaendelea kuwapakia mateka waliowaokoa kwenye ndege, kumbe kulikuwa na mwanajeshi wa Uganda amebakia juu kwenye mnara wa uongozaji (airport control tower). Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibunui kutoka kwa mtoto wa Idd Amin anasema kwamba mwanajeshi huyu alikuwa ni binamu wa Idd Amin. Kutokea hapo kwenye mnara alimimina risasi mfululizo kwa makomando wa Israel na moja ya risasi hizi ilimpaka Koamando Yonatan Netanyahu ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Matkal iliyopo hapoa na alipoteza uhai pale pale.
    Wanajeshi wa Isarel walijibu mapigo kwa kurusha bomu la roketi ndogo ya begani na kusambaratisha kabisa kiota cha mnara na kumuua mwanajeshi wa Uganda aliyekuwa anawashambulia.
    Baada ya hapo waliwapakia kwenye ndege mateka wote ambao waliokolewa pamoja na miili ya Waisrael ambao walifariki kwenye majibizano hayo ya risasi.
    Kisha ili kuhakikisha kuwa hakuna ndege itakayowafuatia nyuma wakiondoka au kushambuliwa, walilipua ndege zote za jeshi la Uganda ambazo zilikuwa uwanjani hapo.
    Oparesheni yote hii ilichukua takribani dakika 53 ambapo dakika 30 pekee ndio zilikuwa za mapigano na 23 zilizosalia zilikuwa za kupakia mateka walio okolewa na kuondoka.
    Mpaka kufikia mwishio mwa oparesheni, jumla ya watekaji wote 7 walikuwa wameuwawa, pia wanajeshi 45 wa jeshi la Uganda walikuwa wameuwawa pia. Lakini pia ndege za kijeshi 11 aina ya MiG-17 na Mig-21 zililipuliwa na makomando wa Isarel. Ikumbukwe kwamba ndege hizi ndizo zilikuwa ni ndege zote za kijeshi ambazo zilikuwa zinamilikiwa na jeshi la anga la Uganda. Hii inaonyesha moja kati ya mapungufu makubwa ya kiuongozi ya Amin. Hakukuwa na busara yoyote au faida yoyote ya kimkakati kuweka ndege zote za jeshi lako la anga kwenye uwanja wa ndege wa kiraia ili kulinda mateka wa tukio ambalo wengine walikuwa wanaweza kuliona kama tukio la kigaidi na kwa namna Fulani kama ugomvi ambao ulikuwa haumuhusu moja kwa moja.
    Katika mateka wote 106 waliobakia (kumbuka nilieleza kuwa kulikuwa na mikupuo miwili ya mateka wasio wa Kiisrael au asili ya Kiyahudi waliachiwa kwa kupelekwa na ndege ufaransa nchini), kwahiyo kati ya wale 106 waliobakio, mateka watatu waliuwawa muda wa mapambano (hawa ndio wale ambao walikuwa hawaelewi kihebrania kwa ufasaha na kwa hiyo hawakulalala chini kama ilivyoamrishwa na makomando wa Israel), na mateka mmoja bibi wa miaka 74 aliyeitwa Dora Bloch aliachwa akiwa Hospitali mjini Entebbe ambako alipelekwa na Amin siku kadhaa nyuma kutokana na kuhitaji uangalizi maalumu wa kidaktari.
    Kati ya Makomando wa Isarel, ni mmoja tu ndiye aliuwawa tena dakika za mwisho (Yonatan Netanyahu) japo pia kuna makomando wengine kama watano ambao walijeruhiwa. Kifo cha kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Mitkal, Yonatan Netanyahu katika oparesheni hii ndio iliyofanya siku kadhaa baadae oparesheni hii pia kubatizwa jina la OPERATION YONATAN kwa heshima yake na ushujaa wake wa kutoa maisha yake ili kutetea na kuooa roho za raia alioapa kuwalinda.
    Baada ya kila kitu kuwekwa sawa na watu wote kupanda ndani ya ndege, waliruka mpaka Nairobi Kenya kwa mapumziko mafupi ili kutibia wale ambao walijeruhiwa (kama ambavyo nilieleza kuwa ile moja ya Boeing 707 iliyotengwa kama ‘hospitali’ ilibaki Nairobi).
    Baada ya matibabu hapo Nairobi, madege yote yaliruka kurudi Israel. Kwa kifupi operation hii was a big SUCCESS.!
    Japokuwa baada ya ulimwengu mzima kutangaziwa juu ya kilichotokea, juu ya ‘umafia’ uliofanywa na Israel, ulimwengu uligawanyika kila nchi ukiunga mkono upande fulani, lakini nchi nyingi ziliunga mkono Israel kwa matumizi ya jeshi katika nchi nyingine, wengi walimlaumu Amin kwa kushindwa kutumia diplomasia kumaliza mzozo huu. Ajabu ni kwamba mwezi huo wa July, Mkuu wa Majeshi wa Iran moja wa mahsimu wa siku zote wa Israel aliandika barua kwa Waziri mkuu wa Israel kumpongeza kuhusu Oparation hiyo na kumpa pole kwa kifo cha Yonatan Netanyahu akimuita Yonatan kumsifu kuwa ni ‘martyr’.
    Vyovyote vile ambavyo unaweza kuitazama oparesheni hii kwenye jicho la kisiasa ua kidiplomasia, kwamba kama ilikuwa ni sahihi au si sahihi lakini katika jicho la kijeshi na ujasusi hii ni moja ya oparesheni murua kabisa kuwahi kufanyika katika historia ya majeshi duniani. Moja ya manguli wa “ulimwengu wa giza”, Bw. Henry Kissinger aliwahi kutamka kuwa hii ilikuwa ni “an immposible mission”!
    Umaridadi wa oparesheni hii umefanya hata vitengo kadhaa vya weledi vya majeshi mbali mbali kutaka kuiga mfano wake lakini bila mafanikio yoyote. Kwa mfano Wamarekani walijaribu kuiga umaridadi wa Oparesheni hii na kufanya ya kwao iliyoitwa Oparation Eagle Claw baada ya kutokea kwa utekeaji kwenye ubalozi wa Iran lakini oparesheni hiyo ilifeli vibaya.
    Sasa hivi kama wewe ni mwanajeshi katika jeshi fulani kwenye kitengo cha weledi (special force) au labda ni jasusi maalumu, lazima katika hatua fulani ya japo hata ‘darasani’ kwenye makaratasi utafundwa kuhusu Oparetion Entebbe na namna ilivyo tekelezwa.
    Oparesheni hii ilimuacha Amin na aibu kubwa kiasi kwamba akaendelea kufanya vitu ambavyo vilidhihirisha udhaifu wake wa kiungozi. Kwa mfano, yule bibi wa miaka 74 aliyeachwa hospitali mjini Entebbe, aliamuru auwawe kinyama. Lakini pia Amin alisimami kuwawa kwa McKenzie yule waziri wa kilimo wa Kenya ambaye alimsaidia Ehud Barak kumshinikiza Mzee Jomo Kenyetta kuruhusu ndege za jeshi la Israel kutumia viwanja vya ndege vya Kenya wakati wa utekelezaji wa OParesheni hiyo na pia kumsaidi kukusanya Intelijensia kwa kutumia ndege yake binafsi.
    McKenzie aliuwawa kwa bomu lililotegwa kwenye gari yake.
    Pia Amin alisimamia ulipuaji kwa bomu moja ya hoteli kubwa Nairobi kipindi hicho ambayo ilikuwa inaitwa The Norfolk Hotel, ambayo ilimilikiwa na moja ya wayahudi mashuhuri nchini Kenya.
    [6/12, 13:48] The Bold: Licha ya ‘fujo’ zote hizi ambazo Amin alizifanya baada ya jeshi lake kudhalilika kutokana na Oeration Entebbe lakini hatupawsi kusahau kwamba chini ya miaka mitatu baadae, yaani baada ya utekelezaji wa opareshini hii, Idd Amin aliondolewa kwa aibu madarakani na majeshi ya Tanzania na kumfanya akimbie nchi yake.

    ......................MWISHO..............
    #TheBOLD_JF
    OPERATION ENTEBBE -4 Katika sehemmu iliyopita nilieleza namna ambavyo baada ya madege ya kivita ya Lockheed Harcules C-130 kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe na moja ya ndege hizo kwenda moja kwa moja karibu na geti la Terminal huku mlango wa nyuma ukiwa wazi na kutoka gari aina na Mercides pamoja na Land Rover kufanana kabisa na msafara wa Idd Amin atembeleapo uwanja wa ndege, la kini ajabu ni kwamba walijikuta wakinyooshewa bunduki na wanajeshi waliokuwa wanalinda getini… Walikuwa hawana taarifa kuwa Amin alikuwa amebadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda nyeupe kabla ya safari yake ya kwenda Mauritius kwenye kikao cha O.A.U. Tuendelee… SEHEMU TA NNE Wanajeshi hawa wawili wa Uganda waliokuwa getini walinyanyua bunduki zao aina ya Kalashnikov na hawakuonyesha dalili kwamba labda walikuwa wanataka kufanya ukaguzi wa kawaida tu kabla ya kuwaruhusu, walionyesha dhahiri kabisa kwamba walikuwa wanataka kufanya shambulio. Kabla wanajeshi hao wa Uganda kufanya lolote lile, Netanyahu na komando mwingine ambao walikuwa ndani ya gari walitumia weledi wao kufanya uamuzi makini wa haraka kwa kufyatua risasi kutoka kwenye bastola zao zenye ‘silencer’ na mara moja wale wanajeshi wawili wa Uganda walienda chini. Lakini moja ya wale wanajeshi wa Uganda waliodondoka chini baada ya kufyatuliwa risasi, hakufa mara moja na alikuwa anajitahidi kuinuka. Hii ilisababisha komando mwingine wa Israel kufyatua risasi lakini safari hii huyu komando wa Israel alifyatua risasi kutoka kwenye bunduki ambayo haina ‘silencer’. Hii iliwashitua wanajeshi wengine wa Uganda waliokuwa nje ya Terminal na kuanza kukimbilia walipokuwa wanasikia milio ya risasi inatokea huku wanafyatua risasi. Kwa maneno mengine ilikuwa kwa kiasi fulani walichokuwa wamekipanga makomando wa Israel, kufanya shambulio la kushitukiza lakini mpaka muda huu tayari ile ‘element of surprise’ ilikuwa haipo tena, jeshi la Uganda lilikuwa limeshitukia ‘mchezo’. Bila kuchelewa sana, makomando wote walikuwa kwenye zile gari mbili (Mercedes na Land Rover) waliruka nje ya gari na kukimbia kuelekea ndani ya terminal. Vichwani mwao walikuwa bado hawajaondokewa na kumbukumbu ya oparesheni kama hii iliyotokea miaka miwili iliyopita nchini Israel kwenye mji wa Ma’a lot ambapowatekaji wa KIpalestina baada ya kushituka kuwa kulikuwa na makomando wa Israel wamefika kufanya uokozi, waliwapiga risasi mateka wao 25 ambao kati yao 22 walikuwa ni watoto wadogo. Hivyo Netanyahu na wenzake hawakutaka kitu kama hiki kjitokeze tena… Netenyahu na makomando wenzake wa Syeret Matkal kwa ustadi wa hali ya juu walikimbia na kuingia ndani ya terminal na kuwaacha vile vikosi vingine kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliopo nje ya terminal (kama nilivyoeleza juzi namna kikosi kilivyogawanywa kwenye vikundi vidogo kila kimoja kikipewa jukumu lake). Mateka wanaeleza kwamba baada ya mpambano ya risasi kuanza huko nje ya terminal waliwaona watekaji kadhaa wakiongozwa na yule aliyeonekana kama kiongozi wao, Wilfred Bose waliingia ndani ya terminal wakiwa wanahaha kama wamechanganyikiwa wasijue wafanye nini, ilionekana dhahiri kuwa walikuwa hawajajiandaa kwa hili shambulio la ghafla, ilionekana dhahiri kwamba katika akili yao walikuwa wanasubiria Israel kutimiza masharti yao ili waweze kuachia mateka. Kuna muda Wilfred Bose alionekana kunyoonya bunduki yake kwa mateka kama vile anawataka kuwamininia risasi lakini alikuwa anashindwa kufanya uamuzi huo. Bose aligeuka ghafla baada ya kusikia kishindo cha mlango wa terminal ukifunguliwa. Makomando wa Israel walikuwa wametumia weledi na ustadi wao wa hali ya juu kuingia ndani ya terminal kwa muda sahihi kabla ya Wilfred Bose na wenzake kufanya uamuzi wowote wa kuua mateka. Makomando wa Israel walipoingia tu ndani ya terminal, mmoja wao mkononi walikuwa na kipaza sauti aina ya ‘megaphone’ na alikuwa anaongeea kwa nguvu kwa lugha ya kihebrania, “Lay down, Lay down. We are Israel soldiers. Lay down. Lay down!!”. Mateka wote wa kiisrael hata wale waliokuwa wamekaa kitako walilala chini, hivyo ndani ya sekunde chache tu kila mtu ambaye alibakia amesimama alikuwa ni halali yao kumtandika risasi. Kwa bahati mbaya kulikuwa na mateka kadhaa ambao wwalikuwa hawajui kihebreania sawia na hii iliwagharimu sana. Kwa mfano kulikuwa na kijana wa mika 19 aliyeitwa Jean-Jacques Maimoni, huyu alikuwa amehamia Israel siku si nyingi sana kutokea nchini ufaransa. Lilipotolewa tangazo hilo la kila mtu kulala chini hakuelewa na alibakia akiwa amesimama na alitandikwa risasi na makomando wa Israel pamoja na wale watekaji. Kijana huyu hakuwa peke yake, lakini pia kulikuwa na mateka mwingine aliyeitwa Ida Borochovitch, ambaye alihamia Israel kutoka nchini Urusi. Risasi zilirindima kwa takribani dakika mbili nzima na baadae ukimya wa kama sekunde 15 ukatawala na moja wa makomando wa kiisrael akauliza kwa kiebrania, “where are the rest of them?” (“wako wapi wengine?”). Mateka wakaonyesha kidole kwenye chumba kidogo kilichopo pembeni. Makomando wakarusha mabomu kadhaa ya kutupa kwa mkono na kisha kuingia ndani ya chumba hicho na kuwamiminia risasi wote ambao walikuwa humo. Milio ya risasi ndani ya terminal hatimaye ilikuwa imekoma japo bado huko nje walisikia majibizano ya risasi. Mwanajeshi mmoja wa Israel kati ya wale waliopo ndani ya terminal, kwa sauti ya utulivu kabisa na katika lugha ya kihebrania aliwatangazia mateka, “listen guys, we’ve come to take you home!” (“sikilizeni, tumekuja kuwachukua kuwarudisha nyumbani!”). Baada ya hapo makomando walianza kuwatoa mateka kutoka kwenye terminal na kuwapakia kwenye ndege kwa tahadhari kubwa huku wale wenzao wengine wakiendelea kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanarusha risasi kutoka kwenye maeneo ya kujificha ndani ya uwanja wa ndege. Wakiwa wanaendelea kuwapakia mateka waliowaokoa kwenye ndege, kumbe kulikuwa na mwanajeshi wa Uganda amebakia juu kwenye mnara wa uongozaji (airport control tower). Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibunui kutoka kwa mtoto wa Idd Amin anasema kwamba mwanajeshi huyu alikuwa ni binamu wa Idd Amin. Kutokea hapo kwenye mnara alimimina risasi mfululizo kwa makomando wa Israel na moja ya risasi hizi ilimpaka Koamando Yonatan Netanyahu ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Matkal iliyopo hapoa na alipoteza uhai pale pale. Wanajeshi wa Isarel walijibu mapigo kwa kurusha bomu la roketi ndogo ya begani na kusambaratisha kabisa kiota cha mnara na kumuua mwanajeshi wa Uganda aliyekuwa anawashambulia. Baada ya hapo waliwapakia kwenye ndege mateka wote ambao waliokolewa pamoja na miili ya Waisrael ambao walifariki kwenye majibizano hayo ya risasi. Kisha ili kuhakikisha kuwa hakuna ndege itakayowafuatia nyuma wakiondoka au kushambuliwa, walilipua ndege zote za jeshi la Uganda ambazo zilikuwa uwanjani hapo. Oparesheni yote hii ilichukua takribani dakika 53 ambapo dakika 30 pekee ndio zilikuwa za mapigano na 23 zilizosalia zilikuwa za kupakia mateka walio okolewa na kuondoka. Mpaka kufikia mwishio mwa oparesheni, jumla ya watekaji wote 7 walikuwa wameuwawa, pia wanajeshi 45 wa jeshi la Uganda walikuwa wameuwawa pia. Lakini pia ndege za kijeshi 11 aina ya MiG-17 na Mig-21 zililipuliwa na makomando wa Isarel. Ikumbukwe kwamba ndege hizi ndizo zilikuwa ni ndege zote za kijeshi ambazo zilikuwa zinamilikiwa na jeshi la anga la Uganda. Hii inaonyesha moja kati ya mapungufu makubwa ya kiuongozi ya Amin. Hakukuwa na busara yoyote au faida yoyote ya kimkakati kuweka ndege zote za jeshi lako la anga kwenye uwanja wa ndege wa kiraia ili kulinda mateka wa tukio ambalo wengine walikuwa wanaweza kuliona kama tukio la kigaidi na kwa namna Fulani kama ugomvi ambao ulikuwa haumuhusu moja kwa moja. Katika mateka wote 106 waliobakia (kumbuka nilieleza kuwa kulikuwa na mikupuo miwili ya mateka wasio wa Kiisrael au asili ya Kiyahudi waliachiwa kwa kupelekwa na ndege ufaransa nchini), kwahiyo kati ya wale 106 waliobakio, mateka watatu waliuwawa muda wa mapambano (hawa ndio wale ambao walikuwa hawaelewi kihebrania kwa ufasaha na kwa hiyo hawakulalala chini kama ilivyoamrishwa na makomando wa Israel), na mateka mmoja bibi wa miaka 74 aliyeitwa Dora Bloch aliachwa akiwa Hospitali mjini Entebbe ambako alipelekwa na Amin siku kadhaa nyuma kutokana na kuhitaji uangalizi maalumu wa kidaktari. Kati ya Makomando wa Isarel, ni mmoja tu ndiye aliuwawa tena dakika za mwisho (Yonatan Netanyahu) japo pia kuna makomando wengine kama watano ambao walijeruhiwa. Kifo cha kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Mitkal, Yonatan Netanyahu katika oparesheni hii ndio iliyofanya siku kadhaa baadae oparesheni hii pia kubatizwa jina la OPERATION YONATAN kwa heshima yake na ushujaa wake wa kutoa maisha yake ili kutetea na kuooa roho za raia alioapa kuwalinda. Baada ya kila kitu kuwekwa sawa na watu wote kupanda ndani ya ndege, waliruka mpaka Nairobi Kenya kwa mapumziko mafupi ili kutibia wale ambao walijeruhiwa (kama ambavyo nilieleza kuwa ile moja ya Boeing 707 iliyotengwa kama ‘hospitali’ ilibaki Nairobi). Baada ya matibabu hapo Nairobi, madege yote yaliruka kurudi Israel. Kwa kifupi operation hii was a big SUCCESS.! Japokuwa baada ya ulimwengu mzima kutangaziwa juu ya kilichotokea, juu ya ‘umafia’ uliofanywa na Israel, ulimwengu uligawanyika kila nchi ukiunga mkono upande fulani, lakini nchi nyingi ziliunga mkono Israel kwa matumizi ya jeshi katika nchi nyingine, wengi walimlaumu Amin kwa kushindwa kutumia diplomasia kumaliza mzozo huu. Ajabu ni kwamba mwezi huo wa July, Mkuu wa Majeshi wa Iran moja wa mahsimu wa siku zote wa Israel aliandika barua kwa Waziri mkuu wa Israel kumpongeza kuhusu Oparation hiyo na kumpa pole kwa kifo cha Yonatan Netanyahu akimuita Yonatan kumsifu kuwa ni ‘martyr’. Vyovyote vile ambavyo unaweza kuitazama oparesheni hii kwenye jicho la kisiasa ua kidiplomasia, kwamba kama ilikuwa ni sahihi au si sahihi lakini katika jicho la kijeshi na ujasusi hii ni moja ya oparesheni murua kabisa kuwahi kufanyika katika historia ya majeshi duniani. Moja ya manguli wa “ulimwengu wa giza”, Bw. Henry Kissinger aliwahi kutamka kuwa hii ilikuwa ni “an immposible mission”! Umaridadi wa oparesheni hii umefanya hata vitengo kadhaa vya weledi vya majeshi mbali mbali kutaka kuiga mfano wake lakini bila mafanikio yoyote. Kwa mfano Wamarekani walijaribu kuiga umaridadi wa Oparesheni hii na kufanya ya kwao iliyoitwa Oparation Eagle Claw baada ya kutokea kwa utekeaji kwenye ubalozi wa Iran lakini oparesheni hiyo ilifeli vibaya. Sasa hivi kama wewe ni mwanajeshi katika jeshi fulani kwenye kitengo cha weledi (special force) au labda ni jasusi maalumu, lazima katika hatua fulani ya japo hata ‘darasani’ kwenye makaratasi utafundwa kuhusu Oparetion Entebbe na namna ilivyo tekelezwa. Oparesheni hii ilimuacha Amin na aibu kubwa kiasi kwamba akaendelea kufanya vitu ambavyo vilidhihirisha udhaifu wake wa kiungozi. Kwa mfano, yule bibi wa miaka 74 aliyeachwa hospitali mjini Entebbe, aliamuru auwawe kinyama. Lakini pia Amin alisimami kuwawa kwa McKenzie yule waziri wa kilimo wa Kenya ambaye alimsaidia Ehud Barak kumshinikiza Mzee Jomo Kenyetta kuruhusu ndege za jeshi la Israel kutumia viwanja vya ndege vya Kenya wakati wa utekelezaji wa OParesheni hiyo na pia kumsaidi kukusanya Intelijensia kwa kutumia ndege yake binafsi. McKenzie aliuwawa kwa bomu lililotegwa kwenye gari yake. Pia Amin alisimamia ulipuaji kwa bomu moja ya hoteli kubwa Nairobi kipindi hicho ambayo ilikuwa inaitwa The Norfolk Hotel, ambayo ilimilikiwa na moja ya wayahudi mashuhuri nchini Kenya. [6/12, 13:48] The Bold: Licha ya ‘fujo’ zote hizi ambazo Amin alizifanya baada ya jeshi lake kudhalilika kutokana na Oeration Entebbe lakini hatupawsi kusahau kwamba chini ya miaka mitatu baadae, yaani baada ya utekelezaji wa opareshini hii, Idd Amin aliondolewa kwa aibu madarakani na majeshi ya Tanzania na kumfanya akimbie nchi yake. ......................MWISHO.............. #TheBOLD_JF
    ·327 Views
  • SAKATA LA JASUSI SERGEI SKRIPAL NA MWANAE NI UTEKELEZAJI WA OPERATION SARLISBURY ILIYOTEKELEZWA NA RUSSIA, KIMSIMGI NI VITA KATI YA URUSI NA NATO KUJIBU MAPIGO YA UCHAGUZI WA MAREKANI MWAKA 2016.

    Na mhariri wako Comred Mbwana Allyamtu

    Sakata la jaribio la mauaji ya jasusi au mpelelezi, ndumilakuwili wa Urusi na Uingereza, Sergei Skripal na binti yake Yulia katika kitongoji cha Salisbury jijini London nchini Uingereza linachukua sura mpya kila siku.

    Wawili hao walipatikana wakiwa hawajitambui katika eneo la maduka liitwalo Maltings mwanzoni mwa Machi.

    Taarifa kutoka kwa polisi wa Uingereza ambao hushughulikia matukio ya kigaidi wanaamini kuwa jasusi huyo na mwanaye, walivuta hewa iliyokuwa na kemikali yenye sumu iitwayo novichok.

    Kemikali hii hushambulia mfumo wa mfahamu na inasemekana ilitengenezwa katika maabara moja huko Urusi na ilitumika wakati wa Vita vya Pili vya Dunia mwaka 1935 hadi 1945. Kemikali hiyo iliachwa mlangoni mwa nyumba ambayo amekuwa akiishi jasusi huyo na mwanaye katika eneo hilo la Salisbury.

    Mashirika makubwa ya habari nchini Uingereza yameipa umuhimu habari hii ambapo Machi 30, yalitangaza kuwa binti wa Skripal, Yulia hakuwa katika hali tete kiafya.

    Kufuatia tukio hilo Serikali ya Uingereza chini ya Waziri Mkuu, Theresa May iliitupia lawama Serikali ya Urusi kwa kuhusika na uovu huo na ili kuonyesha kuwa imechukia iliamua kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi wapatao 23.

    Urusi imekanusha kuhusika na uovu huo na ikaahidi kuwa kwa kila hukumu itakayotolewa nayo itajibu kwa ukubwa huohuo au zaidi ya hapo, na ikajibu kwa kutoa hukumu ya kisasi kwa kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza na kufunga kituo cha Lugha na Utamaduni cha Uingereza, British Council na imeitaka Uingereza kuwaondoa wanadiplomasia wake wengine wapatao 50 katika kipindi cha mwezi mmoja.
    Ili kuonyesha mshikamano na Uingereza nchi nyingine za Ulaya Magharibi na Australia zimewafukuza wanadiplomasia wa Urusi wanaofikia 150 huku Marekani ikiongoza kwa kufunga ubalozi mdogo wa Urusi katika Jiji la Seattle na kuwafukuza wanadiplomasia 60 kutoka nchi hiyo.

    Urusi nayo haikubaki kimya, Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov ametangaza kuwafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani na vilevile kufunga ubalozi wa Marekani katika mji wa Saint Petersburg na kuahidi kuwa kila nchi iliyohusika na kufukuza wanadiplomasia wake itaadhibiwa vilivyo.

    Kwa ujumla nchi karibu 23 na Umoja wa Kujihami wa nchi za Ulaya Magharibi (Nato) kote ulimwenguni zimeonyesha kukerwa na vitendo vya Urusi kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi tofautitofauti, kama vile kuvamia Ukraine na kulichukua jimbo la Krimea, kuitungua ndege ya Malaysia na kuingilia uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka 2016.
    Siyo mara ya kwanza nchi hizi kuingia katika mzozo wa kidiplomasia kwani mwaka 1986 Ronald Reagan aliyekuwa Rais wa Marekani, aliamuru wanadiplomasia 80 wa Shirikisho la Urusi (USSR) wafukuzwe nchini humo na mwaka 2016, Rais Barak Obama aliwatimua wanadiplomasia 35 kutoka nchi hiyo kwa tuhuma za kudukua kompyuta za chama cha Democratic kwa nia ya kumhujumu mgombea wake wa Rais, Hillary Clinton.

    Mwaka 2006 Skripal alihukumiwa kifungo cha miaka 13, nchini Urusi katika kesi ambayo iliendeshwa katika mahakama ya siri, alipewa haki ya ukimbizi na ukazi nchini Uingereza mwaka 2010 baada ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa katika mtindo ambao ulitumika enzi za vita baridi kuhusiana na shughuli za kijasusi.

    Kulingana na nyaraka za kumbukumbu ambazo vyombo vya habari vya Uingereza vilizipata kutoka makumbusho ya taifa ya Uingereza mwaka 2015, zinaonyesha kuwa Serikali ya Urusi imekuwa ikiichunguza Uingereza muda mrefu lakini kisa kinachojulikana sana ni kile kilichopewa jina la Cambridge Four, ambapo kitengo cha ujasusi cha shirikisho la Urusi (USSR), KGB, katika miaka ya 1930 kabla ya vita vya pili vya dunia kiligundua kuwa Serikali ya Uingereza ilikuwa ikitumia Chuo Kikuu cha Cambridge kama sehemu maalumu ya kuwapata majasusi wachanga wakiwa masomoni. KGB waliwafuata wanafunzi wanne wa wakati huo ambao ni Anthony Blunt, Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess.
    Wasomi hao ambao kwa bahati nzuri kwao KGB walipomaliza masomo yao waliingia kufanya kazi katika Mashirika ya Ujasusi ya Uingereza, MI5 na MI6, na wakawa ni majasusi ndumilakuwili.

    Walifanya kazi yao hadi mwaka 1964 ambapo Anthony Blunt ambaye alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Ujasusi wa ndani, MI5, alikiri kuwa jasusi ndumilakuwili ili asishtakiwe na habari hiyo ilikuja kutolewa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo, Magreth Thatcher alipokuwa akihutubia Bunge mwaka 1979. Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess wao walitimkia Urusi na Serikali ya Uingereza ikawa imekubali yaiishe.

    Kwa hiyo Urusi imekuwa hailali usingizi wakati wote wa miaka ya vita baridi kati ya nchi za Ulaya Mashariki na Magharibi miaka ya 1945 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990, imekuwa ikiingiza wapelelezi wake maeneo mbalimbali katika nchi hizo ili kupata habari nyeti kuhusiana na masuala mbalimbali katika nyanja za uchumi, biashara hasa ya silaha na teknolojia yake na hivi karibuni kuingilia mambo ya siasa za uchaguzi huko Marekani.
    Ukiangalia kisa cha safari hii hakina tofauti sana kile alichofanyiwa Jasusi mwingine wa Urusi Novemba 2006, Alexander Litvinenko ambaye aliwekewa kemikali iitwayo Polonium 210 katika kikombe cha chai katika mgahawa mmoja jijini London.

    Litvinenko alitoroka Urusi baada ya kutofautiana na wenzake katika shirika la kijasusi la nchi hiyo FSB, ambapo aliutuhumu uongozi wa juu wa nchi hiyo kuigeuza nchi hiyo kuwa Taifa la kimafia. akiwa nchini Uingereza, alifanya kazi kama mwandishi wa habari, vitabu na mshauri wa mambo ya usalama.
    Akiwa Uingereza aliandika vitabu viwili, Blowing up Russia: Terror from within na Lubyanka Criminal Group ambapo aliituhumu idara hiyo ya kijasusi kwa vitendo vya mauaji na matumizi ya mabomu na mauaji ya mwandishi wa habari, Anna Politkovskaya kwa amri kutoka kwa Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin.

    Litvinenko akiwa mahututi kitandani hospitalini jijini London aliwatamkia ndugu zake kuwa alikuwa na uhakika kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin ndiye aliyeamuru auawe.
    Serikali ya Uingereza ya wakati huo chini ya Waziri Mkuu, Tony Blair ilifanya upelelezi na kugundua kuwa jasusi huyo siku chache kabla ya kupata mkasa huo alikuwa ametembelewa na jasusi mwingine mstaafu wa FSB ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara, Andrey Lugovoy.
    Serikali ya Uingereza iliitaka Urusi imsalimishe kwake ili afanyiwe mahojiano lakini Urusi ilikataa kwa maelezo kuwa Katiba ya nchi hiyo inakataza raia wake kupelekwa nchi nyingine kufanyiwa mashtaka ya jinai. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulififia kwa muda.

    Serikali ya Uingereza kwa matukio yote haya imekuwa ikiituhumu serikali ya Urusi kwa kile inachoeleza kuwa kemikali hizo haziwezi kuwa mikononi mwa mtu binafsi bila kuwa na kibari cha mamlaka za juu za nchi hiyo.

    Wakati Kim Phillby alipokimbilia Urusi baada ya kushtukia kuwa wenzake walikuwa wanaelekea kumgundua kuwa ni ndumilakuwili, Ofisa mmoja wa ngazi ya juu ndani ya KGB wakati huo alimsifu kuwa alikuwa jasusi mwenye thamani kubwa wa karne iliyopita.

    Urusi imekuwa ikitoa ulinzi wa kiwango cha juu kwa majasusi ndumilakuwili ambao wamefanikiwa kuingia nchini humo baada ya mambo kwenda kombo huko kwao.

    Marekani nayo haikuwahi kupona kwa taasisi zake za kijasusi kuingiliwa na wenzao wa Urusi. Mwaka 2001 Shirika la Ujasusi wa Ndani, FBI, lilimkamata Robert Hanssen ambaye alikuwa mtumishi wake kwa kupeleka taarifa za siri za nchi hiyo kwa Urusi tangu mwaka 1979 kwa kulipwa fedha na almasi.

    Kwa sehemu kubwa shughuli za ujasusi zimekuwa zikifanywa kwa njia ya teknolojia (Artificial Intelligence) ambapo mitambo ya kompyuta na setelaiti na kamera zenye nguvu za kunasa picha hutumika na pale ambapo haiwezekani, inabidi kutumia binadamu (human intelligence) ili kupata habari ambazo ni siri na mataifa karibu yote duniani yameuweka ujasusi kama ni kosa la uhaini kwa yeyote atakayejihusisha nao.
    SAKATA LA JASUSI SERGEI SKRIPAL NA MWANAE NI UTEKELEZAJI WA OPERATION SARLISBURY ILIYOTEKELEZWA NA RUSSIA, KIMSIMGI NI VITA KATI YA URUSI NA NATO KUJIBU MAPIGO YA UCHAGUZI WA MAREKANI MWAKA 2016. Na mhariri wako Comred Mbwana Allyamtu Sakata la jaribio la mauaji ya jasusi au mpelelezi, ndumilakuwili wa Urusi na Uingereza, Sergei Skripal na binti yake Yulia katika kitongoji cha Salisbury jijini London nchini Uingereza linachukua sura mpya kila siku. Wawili hao walipatikana wakiwa hawajitambui katika eneo la maduka liitwalo Maltings mwanzoni mwa Machi. Taarifa kutoka kwa polisi wa Uingereza ambao hushughulikia matukio ya kigaidi wanaamini kuwa jasusi huyo na mwanaye, walivuta hewa iliyokuwa na kemikali yenye sumu iitwayo novichok. Kemikali hii hushambulia mfumo wa mfahamu na inasemekana ilitengenezwa katika maabara moja huko Urusi na ilitumika wakati wa Vita vya Pili vya Dunia mwaka 1935 hadi 1945. Kemikali hiyo iliachwa mlangoni mwa nyumba ambayo amekuwa akiishi jasusi huyo na mwanaye katika eneo hilo la Salisbury. Mashirika makubwa ya habari nchini Uingereza yameipa umuhimu habari hii ambapo Machi 30, yalitangaza kuwa binti wa Skripal, Yulia hakuwa katika hali tete kiafya. Kufuatia tukio hilo Serikali ya Uingereza chini ya Waziri Mkuu, Theresa May iliitupia lawama Serikali ya Urusi kwa kuhusika na uovu huo na ili kuonyesha kuwa imechukia iliamua kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi wapatao 23. Urusi imekanusha kuhusika na uovu huo na ikaahidi kuwa kwa kila hukumu itakayotolewa nayo itajibu kwa ukubwa huohuo au zaidi ya hapo, na ikajibu kwa kutoa hukumu ya kisasi kwa kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza na kufunga kituo cha Lugha na Utamaduni cha Uingereza, British Council na imeitaka Uingereza kuwaondoa wanadiplomasia wake wengine wapatao 50 katika kipindi cha mwezi mmoja. Ili kuonyesha mshikamano na Uingereza nchi nyingine za Ulaya Magharibi na Australia zimewafukuza wanadiplomasia wa Urusi wanaofikia 150 huku Marekani ikiongoza kwa kufunga ubalozi mdogo wa Urusi katika Jiji la Seattle na kuwafukuza wanadiplomasia 60 kutoka nchi hiyo. Urusi nayo haikubaki kimya, Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov ametangaza kuwafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani na vilevile kufunga ubalozi wa Marekani katika mji wa Saint Petersburg na kuahidi kuwa kila nchi iliyohusika na kufukuza wanadiplomasia wake itaadhibiwa vilivyo. Kwa ujumla nchi karibu 23 na Umoja wa Kujihami wa nchi za Ulaya Magharibi (Nato) kote ulimwenguni zimeonyesha kukerwa na vitendo vya Urusi kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi tofautitofauti, kama vile kuvamia Ukraine na kulichukua jimbo la Krimea, kuitungua ndege ya Malaysia na kuingilia uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka 2016. Siyo mara ya kwanza nchi hizi kuingia katika mzozo wa kidiplomasia kwani mwaka 1986 Ronald Reagan aliyekuwa Rais wa Marekani, aliamuru wanadiplomasia 80 wa Shirikisho la Urusi (USSR) wafukuzwe nchini humo na mwaka 2016, Rais Barak Obama aliwatimua wanadiplomasia 35 kutoka nchi hiyo kwa tuhuma za kudukua kompyuta za chama cha Democratic kwa nia ya kumhujumu mgombea wake wa Rais, Hillary Clinton. Mwaka 2006 Skripal alihukumiwa kifungo cha miaka 13, nchini Urusi katika kesi ambayo iliendeshwa katika mahakama ya siri, alipewa haki ya ukimbizi na ukazi nchini Uingereza mwaka 2010 baada ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa katika mtindo ambao ulitumika enzi za vita baridi kuhusiana na shughuli za kijasusi. Kulingana na nyaraka za kumbukumbu ambazo vyombo vya habari vya Uingereza vilizipata kutoka makumbusho ya taifa ya Uingereza mwaka 2015, zinaonyesha kuwa Serikali ya Urusi imekuwa ikiichunguza Uingereza muda mrefu lakini kisa kinachojulikana sana ni kile kilichopewa jina la Cambridge Four, ambapo kitengo cha ujasusi cha shirikisho la Urusi (USSR), KGB, katika miaka ya 1930 kabla ya vita vya pili vya dunia kiligundua kuwa Serikali ya Uingereza ilikuwa ikitumia Chuo Kikuu cha Cambridge kama sehemu maalumu ya kuwapata majasusi wachanga wakiwa masomoni. KGB waliwafuata wanafunzi wanne wa wakati huo ambao ni Anthony Blunt, Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess. Wasomi hao ambao kwa bahati nzuri kwao KGB walipomaliza masomo yao waliingia kufanya kazi katika Mashirika ya Ujasusi ya Uingereza, MI5 na MI6, na wakawa ni majasusi ndumilakuwili. Walifanya kazi yao hadi mwaka 1964 ambapo Anthony Blunt ambaye alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Ujasusi wa ndani, MI5, alikiri kuwa jasusi ndumilakuwili ili asishtakiwe na habari hiyo ilikuja kutolewa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo, Magreth Thatcher alipokuwa akihutubia Bunge mwaka 1979. Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess wao walitimkia Urusi na Serikali ya Uingereza ikawa imekubali yaiishe. Kwa hiyo Urusi imekuwa hailali usingizi wakati wote wa miaka ya vita baridi kati ya nchi za Ulaya Mashariki na Magharibi miaka ya 1945 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990, imekuwa ikiingiza wapelelezi wake maeneo mbalimbali katika nchi hizo ili kupata habari nyeti kuhusiana na masuala mbalimbali katika nyanja za uchumi, biashara hasa ya silaha na teknolojia yake na hivi karibuni kuingilia mambo ya siasa za uchaguzi huko Marekani. Ukiangalia kisa cha safari hii hakina tofauti sana kile alichofanyiwa Jasusi mwingine wa Urusi Novemba 2006, Alexander Litvinenko ambaye aliwekewa kemikali iitwayo Polonium 210 katika kikombe cha chai katika mgahawa mmoja jijini London. Litvinenko alitoroka Urusi baada ya kutofautiana na wenzake katika shirika la kijasusi la nchi hiyo FSB, ambapo aliutuhumu uongozi wa juu wa nchi hiyo kuigeuza nchi hiyo kuwa Taifa la kimafia. akiwa nchini Uingereza, alifanya kazi kama mwandishi wa habari, vitabu na mshauri wa mambo ya usalama. Akiwa Uingereza aliandika vitabu viwili, Blowing up Russia: Terror from within na Lubyanka Criminal Group ambapo aliituhumu idara hiyo ya kijasusi kwa vitendo vya mauaji na matumizi ya mabomu na mauaji ya mwandishi wa habari, Anna Politkovskaya kwa amri kutoka kwa Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin. Litvinenko akiwa mahututi kitandani hospitalini jijini London aliwatamkia ndugu zake kuwa alikuwa na uhakika kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin ndiye aliyeamuru auawe. Serikali ya Uingereza ya wakati huo chini ya Waziri Mkuu, Tony Blair ilifanya upelelezi na kugundua kuwa jasusi huyo siku chache kabla ya kupata mkasa huo alikuwa ametembelewa na jasusi mwingine mstaafu wa FSB ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara, Andrey Lugovoy. Serikali ya Uingereza iliitaka Urusi imsalimishe kwake ili afanyiwe mahojiano lakini Urusi ilikataa kwa maelezo kuwa Katiba ya nchi hiyo inakataza raia wake kupelekwa nchi nyingine kufanyiwa mashtaka ya jinai. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulififia kwa muda. Serikali ya Uingereza kwa matukio yote haya imekuwa ikiituhumu serikali ya Urusi kwa kile inachoeleza kuwa kemikali hizo haziwezi kuwa mikononi mwa mtu binafsi bila kuwa na kibari cha mamlaka za juu za nchi hiyo. Wakati Kim Phillby alipokimbilia Urusi baada ya kushtukia kuwa wenzake walikuwa wanaelekea kumgundua kuwa ni ndumilakuwili, Ofisa mmoja wa ngazi ya juu ndani ya KGB wakati huo alimsifu kuwa alikuwa jasusi mwenye thamani kubwa wa karne iliyopita. Urusi imekuwa ikitoa ulinzi wa kiwango cha juu kwa majasusi ndumilakuwili ambao wamefanikiwa kuingia nchini humo baada ya mambo kwenda kombo huko kwao. Marekani nayo haikuwahi kupona kwa taasisi zake za kijasusi kuingiliwa na wenzao wa Urusi. Mwaka 2001 Shirika la Ujasusi wa Ndani, FBI, lilimkamata Robert Hanssen ambaye alikuwa mtumishi wake kwa kupeleka taarifa za siri za nchi hiyo kwa Urusi tangu mwaka 1979 kwa kulipwa fedha na almasi. Kwa sehemu kubwa shughuli za ujasusi zimekuwa zikifanywa kwa njia ya teknolojia (Artificial Intelligence) ambapo mitambo ya kompyuta na setelaiti na kamera zenye nguvu za kunasa picha hutumika na pale ambapo haiwezekani, inabidi kutumia binadamu (human intelligence) ili kupata habari ambazo ni siri na mataifa karibu yote duniani yameuweka ujasusi kama ni kosa la uhaini kwa yeyote atakayejihusisha nao.
    ·324 Views
  • CHAGUA KINACHO FAIDA, SI KILE KINACHOSISIMUA...

    Maisha ni safari iliyojaa chaguzi, njia panda, na maamuzi ambayo yanaunda hatima yetu. Hata hivyo, katikati ya haya yote, moja ya majaribu makubwa tunayokabiliana nayo ni chambo cha kile kinachoonekana "kuvutia." Lakini wacha nikukumbushe kwamba sio kila kitu kinachovutia ambacho kinafaa kufuata, na sio kila kitu kitamu kinaongoza kwenye uzima. Tunaishi katika ulimwengu unaotukuza kufuatia raha, mvuto wa burudani, na msisimuko wa muda mfupi tu. Lakini kumbuka hili: "Labda ni ya kuvutia, lakini inaua." Sio nyakati za msisimko za muda mfupi ambazo hufafanua ubora wa maisha yako; ni maamuzi ya muda mrefu unayofanya ambayo ni muhimu sana. Kuna meza ambapo raha hutolewa kwenye sahani za fedha, meza ambapo anasa hupongezwa, na mipaka imefichwa. Jedwali hizi zinaweza kuonekana kuwa za kuvutia, lakini mara nyingi huficha vikombe vyenye sumu. Maisha mengi yameharibiwa na ladha tamu ya anasa. Kinywaji hicho cha ziada, tabia hiyo ya kutojali, tukio hilo lisilo na madhara, yote ya kuvutia kwa sasa, lakini wengi wamelipa kwa afya zao, amani yao, na hata maisha yao. Je! ni watu wangapi wamelala kwenye vitanda vya hospitali leo kwa sababu walifuata kile "kinachovutia"? Ni ndoto ngapi zimekatishwa kwa sababu mtu alifuata kile "kinachosisimua" bila kuzingatia matokeo? Kama vile mithali ya kale inavyosema, “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti” (Mithali 14:12).

    Jedwali lingine la kuepukwa ni meza ya uvumi. Lo, ni jambo la kupendeza kama nini kuketi na kusikiliza mtu akipasuliwa, jina lake likikokotwa kwenye tope! Lakini wacha nikuambie kitu: porojo hazina marafiki wa kudumu. Vinywa vile vile vinavyowachana wengine mbele yako ndivyo vitakugeukia wewe usipokuwepo. Usidanganywe na maoni ya uwongo ya urafiki ambayo porojo hutoa. Uvumi ni kama vampire, unalisha damu ya mahusiano, uaminifu, na sifa. Inavutia, lakini inaua. Inaua urafiki, familia, na jamii. Kama msemo unavyosema, "Mtu anayeondoa kaa linalowaka kutoka kwa paa la jirani yake atalipata peke yake." Unaposhiriki katika uvumi, unafungua mlango wa uharibifu kuingia katika maisha yako mwenyewe. Maisha si msururu wa starehe za kupita muda; ni zawadi takatifu inayokusudiwa kuishi kwa makusudi. Usiishi maisha yako kwa kuzingatia kile kinachovutia. Badala yake, iishi kulingana na kile ambacho kinafaa kwako kwa muda mrefu. Mambo yanayotutegemeza, nidhamu, kazi ngumu, uadilifu, na upendo, si mara zote "yanavutia" kwa sasa, lakini yanajenga maisha yenye thamani. Epuka meza ambapo vitu vya kupendeza tu hutolewa. Jizungushe na watu wanaokupa changamoto, wanaokuhimiza kukua, wanaokuita kwa viwango vya juu zaidi. Kama vile Mtakatifu Paulo anavyoandika, “Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vyenye faida” (1 Wakorintho 10:23). Chagua kile ambacho ni cha manufaa, sio tu kinachosisimua.

    Usiruhusu harakati zako za msisimko zikupoteze maisha ambayo Mungu alikusudia kwa ajili yako. Chagua maisha, chagua kusudi, na uchague njia inayoongoza kwa furaha ya kweli na amani ya kudumu.
    @Fr. Albert Nwosu'
    CHAGUA KINACHO FAIDA, SI KILE KINACHOSISIMUA... Maisha ni safari iliyojaa chaguzi, njia panda, na maamuzi ambayo yanaunda hatima yetu. Hata hivyo, katikati ya haya yote, moja ya majaribu makubwa tunayokabiliana nayo ni chambo cha kile kinachoonekana "kuvutia." Lakini wacha nikukumbushe kwamba sio kila kitu kinachovutia ambacho kinafaa kufuata, na sio kila kitu kitamu kinaongoza kwenye uzima. Tunaishi katika ulimwengu unaotukuza kufuatia raha, mvuto wa burudani, na msisimuko wa muda mfupi tu. Lakini kumbuka hili: "Labda ni ya kuvutia, lakini inaua." Sio nyakati za msisimko za muda mfupi ambazo hufafanua ubora wa maisha yako; ni maamuzi ya muda mrefu unayofanya ambayo ni muhimu sana. Kuna meza ambapo raha hutolewa kwenye sahani za fedha, meza ambapo anasa hupongezwa, na mipaka imefichwa. Jedwali hizi zinaweza kuonekana kuwa za kuvutia, lakini mara nyingi huficha vikombe vyenye sumu. Maisha mengi yameharibiwa na ladha tamu ya anasa. Kinywaji hicho cha ziada, tabia hiyo ya kutojali, tukio hilo lisilo na madhara, yote ya kuvutia kwa sasa, lakini wengi wamelipa kwa afya zao, amani yao, na hata maisha yao. Je! ni watu wangapi wamelala kwenye vitanda vya hospitali leo kwa sababu walifuata kile "kinachovutia"? Ni ndoto ngapi zimekatishwa kwa sababu mtu alifuata kile "kinachosisimua" bila kuzingatia matokeo? Kama vile mithali ya kale inavyosema, “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti” (Mithali 14:12). Jedwali lingine la kuepukwa ni meza ya uvumi. Lo, ni jambo la kupendeza kama nini kuketi na kusikiliza mtu akipasuliwa, jina lake likikokotwa kwenye tope! Lakini wacha nikuambie kitu: porojo hazina marafiki wa kudumu. Vinywa vile vile vinavyowachana wengine mbele yako ndivyo vitakugeukia wewe usipokuwepo. Usidanganywe na maoni ya uwongo ya urafiki ambayo porojo hutoa. Uvumi ni kama vampire, unalisha damu ya mahusiano, uaminifu, na sifa. Inavutia, lakini inaua. Inaua urafiki, familia, na jamii. Kama msemo unavyosema, "Mtu anayeondoa kaa linalowaka kutoka kwa paa la jirani yake atalipata peke yake." Unaposhiriki katika uvumi, unafungua mlango wa uharibifu kuingia katika maisha yako mwenyewe. Maisha si msururu wa starehe za kupita muda; ni zawadi takatifu inayokusudiwa kuishi kwa makusudi. Usiishi maisha yako kwa kuzingatia kile kinachovutia. Badala yake, iishi kulingana na kile ambacho kinafaa kwako kwa muda mrefu. Mambo yanayotutegemeza, nidhamu, kazi ngumu, uadilifu, na upendo, si mara zote "yanavutia" kwa sasa, lakini yanajenga maisha yenye thamani. Epuka meza ambapo vitu vya kupendeza tu hutolewa. Jizungushe na watu wanaokupa changamoto, wanaokuhimiza kukua, wanaokuita kwa viwango vya juu zaidi. Kama vile Mtakatifu Paulo anavyoandika, “Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vyenye faida” (1 Wakorintho 10:23). Chagua kile ambacho ni cha manufaa, sio tu kinachosisimua. Usiruhusu harakati zako za msisimko zikupoteze maisha ambayo Mungu alikusudia kwa ajili yako. Chagua maisha, chagua kusudi, na uchague njia inayoongoza kwa furaha ya kweli na amani ya kudumu. @Fr. Albert Nwosu'
    Love
    1
    ·152 Views
  • GEREZA LA GITARAMA: Jehenamu duniani!

    Jiji la Gitarama hupatikana katikati ya nchi ya Rwanda, kwa makadirio kilomita arobaini na tano toka kwenye jiji kubwa nchini humo; jiji la Kigali, jiji pekee lililoitangulia Gitarama kwa ukubwa.

    Kama haitoshi ni hapahapa katika jiji hili ndipo kuna historia kubwa ya makutano yaliyofanyika mwezi wa kwanza; mwaka 1961, Rwanda ikatangazwa rasmi kama jamhuri. Vilevile jiji hili (kipindi hicho mji) likatoa raisi wa kwanza wa Rwanda, bwana Gregoire Kayibanda, ambaye kumbukumbuye mpaka sasa imesimamishwa katikati ya eneo hili.

    Mazuri hayo hayakomei hapo, hapana! Bali pia hili jiji likabarikiwa na kutunukiwa vivutio kadha wa kadha vya utalii na taasisi lukuki za elimu ambazo aidha zaweza jaza ukumbi nikizianisha hapa. Na kwa namna moja ama nyingine nachelea kusema taasisi hizo zilijengwa (zimejengwa) kwa lengo chanya la kuwafanya watu wapate elimu na hatimaye kujikomboa kifikra na kimwili.

    Lakini mbali na taasisi hizo, na aidha vivutio na uzuri wa jiji hili, upande wa pili wa sarafu ukisikia jina hili ‘Gitarama’, yakupasa uhofie na hata kushikwa na huruma kwa namna binadamu kama wewe wanavyotendwa, tena bado wakiwa hai kabisa. Binadamu hao wakiwa wanaishi ndani ya eneo ambalo hakuna binadamu yeyote juu ya uso wa dunia angelipenda kuwamo kwa gharama yoyote ile!

    GITARAMA; ‘JEHANAMU DUNIANI’:

    Sehemu nyingi duniani zimewahi kuitwa jehanamu. Na jina hili lilishamiri zaidi baada ya vita vya pili vya dunia ambapo maeneo kadhaa yalipewa jina hili kuwakilisha maeneo yasiyokalika, hatari na yasiyo na afya stahiki kwa wanadamu. Maeneo hayo mathalani ni Blood Falls (Maanguko ya damu) huko Antarktika, Danakil Depression (bonde la Danakil) huko Ethiopia, Door to Hell (mlango wa kuzimu) huko Turkmenistan, Kamchatka Peninsula huko Russia na kadhalika, na kadhalika.

    Japokuwa sehemu hizo zipo nyingi zikipatikana maeneo mbalimbali, ni dhahiri kuna sifa ambazo hushirikiana na hivyo basi ndio maana huwekwa chini ya mwamvuli mmoja wa ‘jehanamu’.

    Upande wa kusini magharibi mwa jiji la Kigali, ndipo ilipo jela hii Gitarama. Kwa sasa inaitwa jela ya Muhanga ikichukua jina la wilaya ambayo ndiyo makazi yake mpaka sasa. Majengo ya jela hiyo yalikuwa yanamilikiwa na waingereza British housing complex mnamo mwaka 1960 yakiwa yamejengwa kama makazi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

    Pale kampuni ilipofungwa, eneo hilo likakodiwa na serikali ya kwanza ya Rwanda iliyokuwa imedhamiria kufanya majengo hayo kuwa jela ya kisiasa (political prison). Tangu hapo hakuna chochote kilichobadilika ndani ya jela hiyo isipokuwa tu serikali ya Rwanda ambapo kila serikali iliyoingia madarakani ilionekana kuipatia ama kuitafutia matumizi eneo hilo.

    Kwa mujibu wa gazeti la London Independent mwaka 1995, hii ndiyo jela mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani. Pia wanda za tovuti nyingi za mitandao, zinakiri na kuiweka jela hii kwenye kumi, ama tano, ama tatu bora zaidi ya jela hatari mno kuwahi kutokea duniani.

    Gitarama ilijengwa kwa ajili ya kumudu wafungwa mia nne tu, lakini mpaka sasa inabebelea wafungwa elfu saba! Mara kumi na nane kwa makadirio. Hali hii inapelekea mahesabu ya wafungwa wanne kurundikana katika eneo la hatua tatu (three feet). Hili laweza likawa la kawaida sana ukilisoma hapa, lakini ukijaribu kutoka nje ya bandiko hili na kujikuta ukiwa umekaa na watu wengine watatu ndani ya eneo la hatua tatu tu, kidogo waweza kuelewa.

    Hakuna mahali pa kulala, kujilaza, wala pa kuketi. Wafungwa husimama wakikung’utwa na jua na wakipoozwa na mvua kwakuwa jela hii kwa kiasi kikubwa haina paa la kuwakinga wafungwa na jua, mvua wala baridi.

    Kutokana na kutapakaa kwa wafungwa hao kwenye eneo hilo dogo, inakuwa ngumu sana kwa mfungwa kutaka kwenda chooni akafanikiwa kwa muda, hali hii inapelekea wafungwa kujisaidia popote pale na hivyo basi kujaza vinyesi, mikojo na harufu kila eneo. Wafungwa huozeshwa na kumomonywa miili na bakteria mpaka kufa kwasababu ya kujiweka karibu, aidha kwa kulala ama kusimama kwenye vinyesi na uchafu wa kila aina (gangrene).

    Wafungwa wengi hawana vidole, nyayo na miguu kwasababu ya kuoza wakiwa hai. Miguu hubadilika rangi na hata kutoa madonda. Ni kawaida kuona mtu ana wadudu miguuni huku wakitembea.

    Kati ya wafungwa kumi ndani ya jela hii, nane hufa kwa kukosa hewa ama magonjwa mbalimbali. Lakini wanapotoka kwenda kuzikwa, basi huingizwa wafungwa wengine ndani ya mlango mkubwa wenye kutu wenye kutoa malalamiko ya ukuukuu.

    Lakini ajabu na kweli ni kwamba, wafungwa waliomo humo ndani hakuna hata mmoja ambaye amepitia mahakamani akathibitishwa ya kwamba ana makosa na anastahili kufungwa.
    Wengi wao, kama si wote, ni wa Hutu. Na walianza kujazwa humo miaka ya 1990's wakituhumiwa kwa mauaji ya Kimbari yaliyokwapua maisha ya wana Rwanda zaidi ya milioni moja. Na hii huonekana ni sababu kubwa inayofanya serikali kutokujali kabisa jela hiyo achilia mbali aliye madarakani ni mtutsi.

    "Watu wanafanyana vitoweo."

    Si tu kwamba hakuna mahali pa kupumzikia, bali ndani ya jela hii kuna rekodi kadha wa kadha mfungwa kumuua mwenzake kisha kumla kama chakula.

    Mgawo wa chakula ni finyu sana. chakula na maji hutolewa mara moja tu kwa juma, tena kikiwa kibovu na hakitoshelezi; mara nyingine chakula kinakosekana kabisa na hivyo basi kuwalazimu wafungwa kumaliza siku kadha wa kadha pasipo kutia kitu tumboni.

    Kwakuwa kila mtu anataka kuishi, wafungwa wengine huamua kuchukua hatua ya kulinda uhai wao kwa kuwanyonga wenzao, kuwabamiza ukutani mpaka mauti kisha kuwatafuna wakiwa wabichi na wakivuja damu moto.

    Wengine hucheza kamari kabisa, ambapo wahusika huchaguliwa kwa kukurupushwa. Mwisho wa siku wahanga wa Kamari hiyo hupotea isijulikane wameenda wapi ndani ya jela, bali matumboni.

    Kumbuka kwamba yote haya yanawezekana tena kwa urahisi kwa sababu ndani ya jela hii hakuna hata mlinzi anayediriki kuingia, ni wafungwa wenyewe tu ndio ambao hujihudumia wenyewe. Chakula na maji vikiletwa, huachwa mlangoni kabla ya wafungwa wenyewe kunyakuwa na kuanza kujigawia. Ndio maana mtu anaweza akafa mpaka akaoza ndani ya jela hii kabla hajaja tolewa na kwenda kuzikwa kwenye makaburi ya pamoja.

    Kulana wenyewe kwa wenyewe si jambo geni wala la kushhtukiza kwa walinzi wa jela hiyo wala tawala husika.

    Juhudi za kubadilisha hali ya Gitarama:

    Kwa namna moja ama nyingine kuna watu na mashirika yaliyoguswa na hali ya kusikitisha kuhusu Gitarama. Japokuwa kweli waliomo humo wanaweza wakawa ni watu waliofanya makosa mbalimbali, ikiwemo hata kuua, lakini halibadilishi dhana ya kwamba na wao wanahitaji haki za binadamu kama wengineo.

    Shirika la Global Giving, likisukumwa na kiongozi wa projekti hii Karen Tse, ni moja ya shirika lisilonuwia faida lililoguswa na hata kuanzisha kampeni ya kutafuta pesa kwa ajili ya kuwasaidia wafungwa hao. Mpaka sasa shirika hili li wazi na unaweza ukawachangia.

    Pesa waliyoichangisha mpaka sasa ni dola za kimarekani 325 huku wakifadhiliwa na mashirika mawili fadhili na huu ukiwa ni mwaka wa sita sasa wapo moto (active).

    Mbali na hapo wanajitutumua kuwasaidia wafungwa hao kisheria ili kesi zao zipatwe kusikilizwa mahakamani. Japokuwa swala hili linaonekana ndoto zaidi ya uhalisia tangu mkono wa serikali unakuwa mzito sana kutingisha kidole.

    “Hiyo ndiyo Gitarama; jehanamu juu ya uso wa dunia. Ama tuseme tawi dogo la jehanamu duniani.”
    GEREZA LA GITARAMA: Jehenamu duniani! Jiji la Gitarama hupatikana katikati ya nchi ya Rwanda, kwa makadirio kilomita arobaini na tano toka kwenye jiji kubwa nchini humo; jiji la Kigali, jiji pekee lililoitangulia Gitarama kwa ukubwa. Kama haitoshi ni hapahapa katika jiji hili ndipo kuna historia kubwa ya makutano yaliyofanyika mwezi wa kwanza; mwaka 1961, Rwanda ikatangazwa rasmi kama jamhuri. Vilevile jiji hili (kipindi hicho mji) likatoa raisi wa kwanza wa Rwanda, bwana Gregoire Kayibanda, ambaye kumbukumbuye mpaka sasa imesimamishwa katikati ya eneo hili. Mazuri hayo hayakomei hapo, hapana! Bali pia hili jiji likabarikiwa na kutunukiwa vivutio kadha wa kadha vya utalii na taasisi lukuki za elimu ambazo aidha zaweza jaza ukumbi nikizianisha hapa. Na kwa namna moja ama nyingine nachelea kusema taasisi hizo zilijengwa (zimejengwa) kwa lengo chanya la kuwafanya watu wapate elimu na hatimaye kujikomboa kifikra na kimwili. Lakini mbali na taasisi hizo, na aidha vivutio na uzuri wa jiji hili, upande wa pili wa sarafu ukisikia jina hili ‘Gitarama’, yakupasa uhofie na hata kushikwa na huruma kwa namna binadamu kama wewe wanavyotendwa, tena bado wakiwa hai kabisa. Binadamu hao wakiwa wanaishi ndani ya eneo ambalo hakuna binadamu yeyote juu ya uso wa dunia angelipenda kuwamo kwa gharama yoyote ile! GITARAMA; ‘JEHANAMU DUNIANI’: Sehemu nyingi duniani zimewahi kuitwa jehanamu. Na jina hili lilishamiri zaidi baada ya vita vya pili vya dunia ambapo maeneo kadhaa yalipewa jina hili kuwakilisha maeneo yasiyokalika, hatari na yasiyo na afya stahiki kwa wanadamu. Maeneo hayo mathalani ni Blood Falls (Maanguko ya damu) huko Antarktika, Danakil Depression (bonde la Danakil) huko Ethiopia, Door to Hell (mlango wa kuzimu) huko Turkmenistan, Kamchatka Peninsula huko Russia na kadhalika, na kadhalika. Japokuwa sehemu hizo zipo nyingi zikipatikana maeneo mbalimbali, ni dhahiri kuna sifa ambazo hushirikiana na hivyo basi ndio maana huwekwa chini ya mwamvuli mmoja wa ‘jehanamu’. Upande wa kusini magharibi mwa jiji la Kigali, ndipo ilipo jela hii Gitarama. Kwa sasa inaitwa jela ya Muhanga ikichukua jina la wilaya ambayo ndiyo makazi yake mpaka sasa. Majengo ya jela hiyo yalikuwa yanamilikiwa na waingereza British housing complex mnamo mwaka 1960 yakiwa yamejengwa kama makazi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo. Pale kampuni ilipofungwa, eneo hilo likakodiwa na serikali ya kwanza ya Rwanda iliyokuwa imedhamiria kufanya majengo hayo kuwa jela ya kisiasa (political prison). Tangu hapo hakuna chochote kilichobadilika ndani ya jela hiyo isipokuwa tu serikali ya Rwanda ambapo kila serikali iliyoingia madarakani ilionekana kuipatia ama kuitafutia matumizi eneo hilo. Kwa mujibu wa gazeti la London Independent mwaka 1995, hii ndiyo jela mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani. Pia wanda za tovuti nyingi za mitandao, zinakiri na kuiweka jela hii kwenye kumi, ama tano, ama tatu bora zaidi ya jela hatari mno kuwahi kutokea duniani. Gitarama ilijengwa kwa ajili ya kumudu wafungwa mia nne tu, lakini mpaka sasa inabebelea wafungwa elfu saba! Mara kumi na nane kwa makadirio. Hali hii inapelekea mahesabu ya wafungwa wanne kurundikana katika eneo la hatua tatu (three feet). Hili laweza likawa la kawaida sana ukilisoma hapa, lakini ukijaribu kutoka nje ya bandiko hili na kujikuta ukiwa umekaa na watu wengine watatu ndani ya eneo la hatua tatu tu, kidogo waweza kuelewa. Hakuna mahali pa kulala, kujilaza, wala pa kuketi. Wafungwa husimama wakikung’utwa na jua na wakipoozwa na mvua kwakuwa jela hii kwa kiasi kikubwa haina paa la kuwakinga wafungwa na jua, mvua wala baridi. Kutokana na kutapakaa kwa wafungwa hao kwenye eneo hilo dogo, inakuwa ngumu sana kwa mfungwa kutaka kwenda chooni akafanikiwa kwa muda, hali hii inapelekea wafungwa kujisaidia popote pale na hivyo basi kujaza vinyesi, mikojo na harufu kila eneo. Wafungwa huozeshwa na kumomonywa miili na bakteria mpaka kufa kwasababu ya kujiweka karibu, aidha kwa kulala ama kusimama kwenye vinyesi na uchafu wa kila aina (gangrene). Wafungwa wengi hawana vidole, nyayo na miguu kwasababu ya kuoza wakiwa hai. Miguu hubadilika rangi na hata kutoa madonda. Ni kawaida kuona mtu ana wadudu miguuni huku wakitembea. Kati ya wafungwa kumi ndani ya jela hii, nane hufa kwa kukosa hewa ama magonjwa mbalimbali. Lakini wanapotoka kwenda kuzikwa, basi huingizwa wafungwa wengine ndani ya mlango mkubwa wenye kutu wenye kutoa malalamiko ya ukuukuu. Lakini ajabu na kweli ni kwamba, wafungwa waliomo humo ndani hakuna hata mmoja ambaye amepitia mahakamani akathibitishwa ya kwamba ana makosa na anastahili kufungwa. Wengi wao, kama si wote, ni wa Hutu. Na walianza kujazwa humo miaka ya 1990's wakituhumiwa kwa mauaji ya Kimbari yaliyokwapua maisha ya wana Rwanda zaidi ya milioni moja. Na hii huonekana ni sababu kubwa inayofanya serikali kutokujali kabisa jela hiyo achilia mbali aliye madarakani ni mtutsi. "Watu wanafanyana vitoweo." Si tu kwamba hakuna mahali pa kupumzikia, bali ndani ya jela hii kuna rekodi kadha wa kadha mfungwa kumuua mwenzake kisha kumla kama chakula. Mgawo wa chakula ni finyu sana. chakula na maji hutolewa mara moja tu kwa juma, tena kikiwa kibovu na hakitoshelezi; mara nyingine chakula kinakosekana kabisa na hivyo basi kuwalazimu wafungwa kumaliza siku kadha wa kadha pasipo kutia kitu tumboni. Kwakuwa kila mtu anataka kuishi, wafungwa wengine huamua kuchukua hatua ya kulinda uhai wao kwa kuwanyonga wenzao, kuwabamiza ukutani mpaka mauti kisha kuwatafuna wakiwa wabichi na wakivuja damu moto. Wengine hucheza kamari kabisa, ambapo wahusika huchaguliwa kwa kukurupushwa. Mwisho wa siku wahanga wa Kamari hiyo hupotea isijulikane wameenda wapi ndani ya jela, bali matumboni. Kumbuka kwamba yote haya yanawezekana tena kwa urahisi kwa sababu ndani ya jela hii hakuna hata mlinzi anayediriki kuingia, ni wafungwa wenyewe tu ndio ambao hujihudumia wenyewe. Chakula na maji vikiletwa, huachwa mlangoni kabla ya wafungwa wenyewe kunyakuwa na kuanza kujigawia. Ndio maana mtu anaweza akafa mpaka akaoza ndani ya jela hii kabla hajaja tolewa na kwenda kuzikwa kwenye makaburi ya pamoja. Kulana wenyewe kwa wenyewe si jambo geni wala la kushhtukiza kwa walinzi wa jela hiyo wala tawala husika. Juhudi za kubadilisha hali ya Gitarama: Kwa namna moja ama nyingine kuna watu na mashirika yaliyoguswa na hali ya kusikitisha kuhusu Gitarama. Japokuwa kweli waliomo humo wanaweza wakawa ni watu waliofanya makosa mbalimbali, ikiwemo hata kuua, lakini halibadilishi dhana ya kwamba na wao wanahitaji haki za binadamu kama wengineo. Shirika la Global Giving, likisukumwa na kiongozi wa projekti hii Karen Tse, ni moja ya shirika lisilonuwia faida lililoguswa na hata kuanzisha kampeni ya kutafuta pesa kwa ajili ya kuwasaidia wafungwa hao. Mpaka sasa shirika hili li wazi na unaweza ukawachangia. Pesa waliyoichangisha mpaka sasa ni dola za kimarekani 325 huku wakifadhiliwa na mashirika mawili fadhili na huu ukiwa ni mwaka wa sita sasa wapo moto (active). Mbali na hapo wanajitutumua kuwasaidia wafungwa hao kisheria ili kesi zao zipatwe kusikilizwa mahakamani. Japokuwa swala hili linaonekana ndoto zaidi ya uhalisia tangu mkono wa serikali unakuwa mzito sana kutingisha kidole. “Hiyo ndiyo Gitarama; jehanamu juu ya uso wa dunia. Ama tuseme tawi dogo la jehanamu duniani.”
    Like
    2
    ·220 Views
  • Orodha ya Marais waliofariki wakiwa bado wapo madarakani Barani Afrika.

    Ifuatayo ndiyo orodha ya maraisi kutoka nchi mbalimbali barani afrika waliofariki wakiwa bado wapo madarakani:

    Lansana Conte, Rais wa Guinea
    Baada ya miaka 24 Lansana Conte alifariki na ugonjwa usiojulikana akiwa na umri wa miaka 74. Alipambana na matatizo ya kisukari na maradhi ya moyo. Kuanzia Aprili 1984 mpaka kifo chake Desemba 2008 alikuwa ni rais wa pili kushika madaraka nchini Guinea. Mbali na matatizo ya afya aliyokuwa nayo aliweza kushinda uchaguzi.

    Omar Bongo, Rais wa Gabon
    Saratani ya tumbo iliosambaa ndio iliyosababisha kifo cha Rais Omar Bongo June 2009 mjini Barcelona, Uhispania, baada ya kuwa rais kwa miaka 42 mfululizo. Alifariki akiwa na umri wa miaka 72 na pia alikuwa ni kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu katika historia na alikuwa akiongoza katika mambo ya rushwa. Bongo alijikusanyia utajiri mkubwa huku akiiacha nchi yake katika hali ya umasikini.

    Joao Bernardo Vieira, Rais wa Guinea-Bissau
    Joao Bernardo Vieira rais wa Guinea-Bissau aliuwawa nchi mwake Machi 2009, akiwa na umri wa miaka 69. Alikuwa kiongozi wa nchi kwa muda wa miaka 31. 1978 alikuwa waziri mkuu na kuchukua madaraka 1980 na alitawala kwa miaka 19. Alibadilika na kuwa kiongozi wa umma na aliongoza miaka minne mingine zaidi. 2005 alishinda tena uchaguzi wa uraisi.

    Umaru Musa Yar’Adua, Rais wa Nigeria
    Umaru Musa Yar’Adua, alifariki akiwa na umri wa miaka 58 mwaka 2011 akisumbuliwa na matatizo ya moyo nchini Nigeria. Alikuwa madarakani kwa miaka mitatu pekee. Alikosekana katika kampeni za uchaguzi kwa sababu za kiafya. Baada ya kuchaguliwa kwake 2007, afya yake ilidhoofika kwa haraka.

    Muammar Gadhafi, kiongozi na mwana mapinduzi wa Libya
    Mwathirika wa mauaji, Muammar Gadhafi aliuawa akiwa na umri wa miaka 69 na vikosi vya waasi katika mazingira yasiyoeleweka nchini Libya, baada ya kuwa kiongozi wa taifa hilo kwa muda wa miaka 42. Aliuondoa uongozi wa kifalme bila ya kumwaga damu wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1969 lakini utawala wake ulifikia kikomo baada ya matokeo ya vuguvugu la mapinduzi ya uarabuni.

    Malam Bacai Sanha, Rais wa Guinea-Bissau
    Kiongozi huyu alifariki mwaka 2012 alikuwa ni Malam Bacai Sanha rais wa Guinea-Bissau. Aliugua ugonjwa wa kisukari na alifariki mjini Paris baada ya miaka minne kama rais akiwa na umri wa miaka 64. Katika kipindi chote cha utawala wake alisumbuliwa na matatizo kadhaa ya kiafya yalosababisha kwenda hospitali mara nyingi.

    Bingu wa Mutharika, Rais wa Malawi
    Rais mwingine aliyefariki mwaka 2012 ni Bingu wa Mutharika, rais wa Malawi. Alipata mshutuko wa moyo mwezi Aprili na kufariki siku mbili baadae akiwa na umri wa miaka 78. Uongozi wake ulikuwa ni wa miaka nane na alipata mafanikio makubwa katika sera zake za kilimo na chakula. Sifa yake iliharibika kufuatia maandamano makubwa yalopinga ununuzi wa ndege ya rais iliyogharimu Dola milioni 14

    John Atta Mills, Rais wa Ghana
    Pia mwaka 2012, John Atta Mills, rais wa Ghana alifariki akiwa nyumbani kwake kwa mshutuko wa moyo na saratani ya koo akiwa na umri wa miaka 68. Alishinda uchaguzi wa rais wa 2008 alishika madaraka kwa miaka mitatu pekee. Alianzisha mikakati mingi ya kiuchumi na mageuzi ya kiuchumi yalomletea sifa kutoka ndani na nje ya nchi.

    Meles Zenawi, Waziri Mkuu wa Ethiopia
    Meles Zenawi alifariki Agosti 2012 nchini Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 57 kwa maambukizi yasiyojulikana. Ameiongoza Ethiopia kwa miaka 5 kama rais kuanzia mwaka 1991 hadi 1995 na kama Waziri Mkuu kwa miaka 17 kuanzia 1995 hadi 2012. Anajulikana kwa kuanzisha mfumo wa siasa wa vyama vingi, lakini pia kwa ukandamizaji wa maandamano halali ya watu wa Oromia wa kaskazini mwa Ethiopia.

    Michael Sata, Rais wa Zambia
    Michael Sata ni kiongozi wa hivi karibuni aliyefariki madarakani akiwa na umri wa miaka 77 kwa maradhi ambayo hayakuwekwa wazi Oktoba 28 2014, nchini Uingereza. Baada ya uchaguzi wa 2011, uvumi juu ya afya yake ulisambaa nchini Zambia. Kukosekana kwake katika shughuli kubwa za kitaifa kuliibua wasiwasi wa afya yake ingawa msemaji wake alisema alikuwa katika afya nzuri.
    Orodha ya Marais waliofariki wakiwa bado wapo madarakani Barani Afrika. Ifuatayo ndiyo orodha ya maraisi kutoka nchi mbalimbali barani afrika waliofariki wakiwa bado wapo madarakani: Lansana Conte, Rais wa Guinea Baada ya miaka 24 Lansana Conte alifariki na ugonjwa usiojulikana akiwa na umri wa miaka 74. Alipambana na matatizo ya kisukari na maradhi ya moyo. Kuanzia Aprili 1984 mpaka kifo chake Desemba 2008 alikuwa ni rais wa pili kushika madaraka nchini Guinea. Mbali na matatizo ya afya aliyokuwa nayo aliweza kushinda uchaguzi. Omar Bongo, Rais wa Gabon Saratani ya tumbo iliosambaa ndio iliyosababisha kifo cha Rais Omar Bongo June 2009 mjini Barcelona, Uhispania, baada ya kuwa rais kwa miaka 42 mfululizo. Alifariki akiwa na umri wa miaka 72 na pia alikuwa ni kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu katika historia na alikuwa akiongoza katika mambo ya rushwa. Bongo alijikusanyia utajiri mkubwa huku akiiacha nchi yake katika hali ya umasikini. Joao Bernardo Vieira, Rais wa Guinea-Bissau Joao Bernardo Vieira rais wa Guinea-Bissau aliuwawa nchi mwake Machi 2009, akiwa na umri wa miaka 69. Alikuwa kiongozi wa nchi kwa muda wa miaka 31. 1978 alikuwa waziri mkuu na kuchukua madaraka 1980 na alitawala kwa miaka 19. Alibadilika na kuwa kiongozi wa umma na aliongoza miaka minne mingine zaidi. 2005 alishinda tena uchaguzi wa uraisi. Umaru Musa Yar’Adua, Rais wa Nigeria Umaru Musa Yar’Adua, alifariki akiwa na umri wa miaka 58 mwaka 2011 akisumbuliwa na matatizo ya moyo nchini Nigeria. Alikuwa madarakani kwa miaka mitatu pekee. Alikosekana katika kampeni za uchaguzi kwa sababu za kiafya. Baada ya kuchaguliwa kwake 2007, afya yake ilidhoofika kwa haraka. Muammar Gadhafi, kiongozi na mwana mapinduzi wa Libya Mwathirika wa mauaji, Muammar Gadhafi aliuawa akiwa na umri wa miaka 69 na vikosi vya waasi katika mazingira yasiyoeleweka nchini Libya, baada ya kuwa kiongozi wa taifa hilo kwa muda wa miaka 42. Aliuondoa uongozi wa kifalme bila ya kumwaga damu wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1969 lakini utawala wake ulifikia kikomo baada ya matokeo ya vuguvugu la mapinduzi ya uarabuni. Malam Bacai Sanha, Rais wa Guinea-Bissau Kiongozi huyu alifariki mwaka 2012 alikuwa ni Malam Bacai Sanha rais wa Guinea-Bissau. Aliugua ugonjwa wa kisukari na alifariki mjini Paris baada ya miaka minne kama rais akiwa na umri wa miaka 64. Katika kipindi chote cha utawala wake alisumbuliwa na matatizo kadhaa ya kiafya yalosababisha kwenda hospitali mara nyingi. Bingu wa Mutharika, Rais wa Malawi Rais mwingine aliyefariki mwaka 2012 ni Bingu wa Mutharika, rais wa Malawi. Alipata mshutuko wa moyo mwezi Aprili na kufariki siku mbili baadae akiwa na umri wa miaka 78. Uongozi wake ulikuwa ni wa miaka nane na alipata mafanikio makubwa katika sera zake za kilimo na chakula. Sifa yake iliharibika kufuatia maandamano makubwa yalopinga ununuzi wa ndege ya rais iliyogharimu Dola milioni 14 John Atta Mills, Rais wa Ghana Pia mwaka 2012, John Atta Mills, rais wa Ghana alifariki akiwa nyumbani kwake kwa mshutuko wa moyo na saratani ya koo akiwa na umri wa miaka 68. Alishinda uchaguzi wa rais wa 2008 alishika madaraka kwa miaka mitatu pekee. Alianzisha mikakati mingi ya kiuchumi na mageuzi ya kiuchumi yalomletea sifa kutoka ndani na nje ya nchi. Meles Zenawi, Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi alifariki Agosti 2012 nchini Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 57 kwa maambukizi yasiyojulikana. Ameiongoza Ethiopia kwa miaka 5 kama rais kuanzia mwaka 1991 hadi 1995 na kama Waziri Mkuu kwa miaka 17 kuanzia 1995 hadi 2012. Anajulikana kwa kuanzisha mfumo wa siasa wa vyama vingi, lakini pia kwa ukandamizaji wa maandamano halali ya watu wa Oromia wa kaskazini mwa Ethiopia. Michael Sata, Rais wa Zambia Michael Sata ni kiongozi wa hivi karibuni aliyefariki madarakani akiwa na umri wa miaka 77 kwa maradhi ambayo hayakuwekwa wazi Oktoba 28 2014, nchini Uingereza. Baada ya uchaguzi wa 2011, uvumi juu ya afya yake ulisambaa nchini Zambia. Kukosekana kwake katika shughuli kubwa za kitaifa kuliibua wasiwasi wa afya yake ingawa msemaji wake alisema alikuwa katika afya nzuri.
    Like
    2
    ·97 Views
  • MAMBO 8 YA KUSHANGAZA YANAYOFANYWA NA MWILI WAKO KUKULINDA PASIPO WEWE KUJUA.

    C&P

    Mwili wa binadamu unafanya mambo mengi ya kibaiolojia ambayo mara nyingi ni vigumu kuyaelewa.

    Mwili una mifumo mbalimbali ya ulinzi ambayo inatulinda na hatari zinazoweza kutudhuru. Mifumo hiyo inatulinda masaa 24 ya siku, Siku zote 7 za wiki, katika mambo yote yanayoweza kuhatarisha maisha yetu.

    Yafuatayo ni mambo yanayofanywa na mwili ambayo ni kati ya hiyo mifumo ya ulinzi wa mwili wa binadamu.

    1. KUPIGA MIAYO (YAWNING)
    Lengo kubwa la kupiga muayo ni kuupoza ubongo baada ya joto kuzidi kwenye ubongo au baada ya ubongo kuchoka kufanya kazi.

    Vile vile kama ukiwa umechoka au una njaa husabababisha oxygen kupungua kwenye damu na kwenye mapafu, hii hupelekea tatizo la kupumua, hivyo kupiga miayo husaidia kuingiza oxygen ya ziada mwilini ili irudishe mwili katika hali yake ya kawaida.

    2. KUPIGA CHAFYA (SNEEZING)
    Mara nyingi tunapiga chafya pale pua zetu zinapokua zimejaa bakteria wa magonjwa ambao hawahitajiki mwilini, Vumbi pamoja na takataka mbali mbali zilizoingia kupitia pua.

    Hivyo kupiga chafya ni kitenda cha mwili kujisafisha kwa kuyatoa hayo matakataka nje yaliyoingia mwilini.

    3. KUJINYOOSHA (STRETCHING)
    Kuninyoosha mwili ni kitendo kisicho cha hiari ambacho lengo lake ni kuuandaa mwili kwa ajili ya kazi mbalimbali za kutumia nguvu utakazokabiliana nazo kwa siku nzima. Lakini pia kujinyoosha kunaipa misuli ya mwili mazoezi na kuiweka sawa vilevile kunarudisha mzunguko wa damu katika hali yake ya kawaida na kumtoa mtu katika uchovu.

    4. KWIKWI (HICCUPING)
    Najua umewahi kupata kwikwi, na mara nyingi mara baada ya kumaliza kula chakula. Je umeshawahi kujiuliza ile sauti ya ajabu ya kwikwi inasababishwa na nini au kwa sabababu gani watu hushikwa na kwikwi?

    Hiyo yote husababishwa na DIAPHRAGM (tamka DAYA - FRAM) kiungo kinachopatikana ndani ya mwili wa binadamu chini kabisa ya kifua baada ya mapafu(lungs). Kazi kubwa ya diaphragm ni kusaidia katika upumuaji, (inhale) na (exhale). Pale unapoingiza hewa ndani (inhale) diaphragm hushuka chini ili kusaidia kuivuta hewa ifike kwenye mapafu. Na unapotoa hewa nje (exhale) diaphragm hutulia kwa kubakia sehem yake ili kuwezesha hewa chafu kutoka nje kupitia pua na mdomo.

    Sasa basi, kuna wakati diaphragm kubugudhiwa na kuisababisha kushuka chini kwa kasi sana jambo linalosababisha wewe kuvuta hewa (inhale) kwa kasi isiyo ya kawaida kupitia koromeo la sauti, hewa ikifika kwenye box la sauti (larynx), sehem hiyo hujifunga kwa haraka sana ili kuzuia hewa isipite huko na ndipo KWIKWI hutokea.

    Mambo mengine yanayoweza kuibugudhi diaphragm na kuisababisha kufanya kazi vibaya mpaka kupelekea kwikwi ni kitendo cha kula haraka haraka au kuvimbewa.

    5. KUJIKUNJA KWA NGOZI YA VIDOLE VYA MIKONO BAADA YA KULOWA AU KUKAA MUDA MREFU KWENYE MAJI.
    Je umewahi shuhudia jinsi ngozi ya vidole vyako inavyojikunja baada ya kufua nguo muda mrefu au kushika maji muda mrefu? Unajua ni kwa sababu gani ngozi hujikunja kama ya mtu aliyezeeka angali yu kijana mara baada ya kukaa sana kwenye maji?

    Watu wengi kabla walizani kwamba kujikunja kwa ngozi hiyo hutokana na maji kuingia kwenye ngozi na hivyo ngozi hujikunja baada ya kulowa.

    Lakini wanasayansi baada ya kufanya utafiti kwa muda merefu juu ya nini hasa hupelekea ngozi kujikunja? Walisema HAPANA si kwa sababu ya ngozi kulowana. Na walikuja na majibu haya.

    Mwili unapokutana na majimaji mara moja hupeleka taarifa na kutafsiri kwamba mazingira hayo yana UTELEZI (Slippery) hivyo kutasababisha mikono kushindwa kushika (Grip) au kukamata vitu kwa urahisi kutokana na utelezi huo. Hapo mwili huchukua hatua ya haraka kuikunja ngozi ya mikono yako ili kurahisisha ushikaji wa vitu vinavyoteleza ndani ya maji pamoja na kutembea kwenye utelezi.

    6. VIPELE VIPELE VYA BARIDI KWENYE NGOZI (GOOSEBUMPS)
    Kazi kubwa ya vipele hivi ni kupunguza kiasi cha joto la mwili linalopotea kupitia matundu ya ngozi. Hivyo kwa kufanya hivi humfanya binadamu kutunza joto la mwili hata katika mazingira ambayo hali yake ya hewa si rafiki kwa mwili wa mwanadamu au ni yenye baridi sana.

    7. MACHOZI (TEARS)
    Zaidi ya kuwa majimaji (MUCOUS MEMBRANE ) yanayopatikana kwenye Macho ambayo kazi zake ni kulilinda jicho dhidi ya kitu chochote kigeni kinachoingia jichoni (mfano unapokata vitunguu au mdudu anapoingia jichoni huwa unatoa machozi mengi eeeh!! Pia dhidi ya upepo na moshi) na pia hutumika kama kilainishi cha jicho pale linapokuwa linazunguka zunguka (blink).

    Vilevile machozi yana kazi ya kupunguza HISIA ZA HUDHUNI zinazozalishwa mwilini. Wanasayansi wanaamini kuwa mtu anapokua mwenye msongo wa mawazo (stress) mwili hutengeneza kitu kipya ili kwenda kubugudhi na kuharibu maumivu yote ambayo mtu anajisikia. Hivyo machozi yanayozalishwa hapa huwa na kemikali na yanafahamika kama NATURAL PAINKILLER. Machozi haya ni tofauti na machozi ya kawaida, lengo lake hasa la kuzalishwa ni kwa ajili ya kuondoa kabisa maumivu yaliyozalishwa mwilini

    Hivyo mpaka hapa tumeona kua kuna machozi ya aina tatu ambayo ni
    i. Basal tears (vilainishi)
    ii. Reflex tears (mlinzi)
    iii. Emotion tears (mtuliza maumivu)

    8. KUSHTUKA USINGIZINI (MYOCLONIC JERKS or HYPNIC JERK).
    Je! Ushawahi kutokewa na hali hii? umelala halafu ghafla unashtuka usingizini kwa mguvu nyingi kama umepigwa na shoti ya umeme na akili inakurudi ghafla huku mapigo ya moyo yakikuenda mbio? Na hali hii ikakutokea pasipo hata kuota ndoto yoyote?

    Basi usiogope au kuwasingizia watu uchawi, hii ni hali ya sayansi ya mwili.na ni njia moja wapo katika ile mifumo ya mwili kujilinda.

    Je hutokeaje?

    Hii ni hali ya ajabu sana isiyofanywa kwa hiari ambayo huwatokea watu mara tu wamejinyoosha kitandani na kupitiwa na usingizi, mwili hutetemeshwa na kusukumwa kwa nguvu na mtu hushtuka katika hali kama vile kapigwa na shoti ya umeme. Hali hii inaweza kupelekea mtu hata kuanguka kitandani na humwamsha mara moja kutoka usingizini.

    Wanasayansi wanatuambia kua, pale tu unapopata usingizi kiwango cha upumuaji kinashuka ghafla, mapigo ya moyo nayo taratibu yanapungua, misuli inatulia kwa ku-relax, Kitu cha AJABU hapa ubongo unatafsiri hali hii kama ni DALILI ZA KIFO (brain's misinterpretation of muscle relaxation), hivyo huchukua hatua za haraka za kuushtua mwili kwa kuutetemesha au kuuskuma kwa nguvu, hali ambayo humfanya mtu kuamka kutoka usingizini kwa KURUKA kitu ambacho ni hali isiyo ya kawaida.

    Hali hii ikimtokea mtu huambatana na kuongezeka kwa mapigo ya moyo (rapid heartbeat), kuhema haraka haraka, na wakati mwingine mtu hutokwa na jasho jingi.

    Wakati mwingine mtu huamka ametoa macho na kama ukimwangalia, nae huishia hukuangalia tu huku akikosa la kukujibu endapo utamuuliza vipi kuna tatizo gani?

    MWILI WAKO NI ZAIDI YA UNAVYOUJUA. JAMBO LA MSINGI NI KUONDOA HOFU KWANI MWILI WAKO UNAJUA NINI UFANYE NA WAKATI GANI ILI KUKULINDA USIKU NA MCHANA KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO.

    Share pia wengine wajue sio kila kitu ni uchawi
    MAMBO 8 YA KUSHANGAZA YANAYOFANYWA NA MWILI WAKO KUKULINDA PASIPO WEWE KUJUA. C&P Mwili wa binadamu unafanya mambo mengi ya kibaiolojia ambayo mara nyingi ni vigumu kuyaelewa. Mwili una mifumo mbalimbali ya ulinzi ambayo inatulinda na hatari zinazoweza kutudhuru. Mifumo hiyo inatulinda masaa 24 ya siku, Siku zote 7 za wiki, katika mambo yote yanayoweza kuhatarisha maisha yetu. Yafuatayo ni mambo yanayofanywa na mwili ambayo ni kati ya hiyo mifumo ya ulinzi wa mwili wa binadamu. 1. KUPIGA MIAYO (YAWNING) Lengo kubwa la kupiga muayo ni kuupoza ubongo baada ya joto kuzidi kwenye ubongo au baada ya ubongo kuchoka kufanya kazi. Vile vile kama ukiwa umechoka au una njaa husabababisha oxygen kupungua kwenye damu na kwenye mapafu, hii hupelekea tatizo la kupumua, hivyo kupiga miayo husaidia kuingiza oxygen ya ziada mwilini ili irudishe mwili katika hali yake ya kawaida. 2. KUPIGA CHAFYA (SNEEZING) Mara nyingi tunapiga chafya pale pua zetu zinapokua zimejaa bakteria wa magonjwa ambao hawahitajiki mwilini, Vumbi pamoja na takataka mbali mbali zilizoingia kupitia pua. Hivyo kupiga chafya ni kitenda cha mwili kujisafisha kwa kuyatoa hayo matakataka nje yaliyoingia mwilini. 3. KUJINYOOSHA (STRETCHING) Kuninyoosha mwili ni kitendo kisicho cha hiari ambacho lengo lake ni kuuandaa mwili kwa ajili ya kazi mbalimbali za kutumia nguvu utakazokabiliana nazo kwa siku nzima. Lakini pia kujinyoosha kunaipa misuli ya mwili mazoezi na kuiweka sawa vilevile kunarudisha mzunguko wa damu katika hali yake ya kawaida na kumtoa mtu katika uchovu. 4. KWIKWI (HICCUPING) Najua umewahi kupata kwikwi, na mara nyingi mara baada ya kumaliza kula chakula. Je umeshawahi kujiuliza ile sauti ya ajabu ya kwikwi inasababishwa na nini au kwa sabababu gani watu hushikwa na kwikwi? Hiyo yote husababishwa na DIAPHRAGM (tamka DAYA - FRAM) kiungo kinachopatikana ndani ya mwili wa binadamu chini kabisa ya kifua baada ya mapafu(lungs). Kazi kubwa ya diaphragm ni kusaidia katika upumuaji, (inhale) na (exhale). Pale unapoingiza hewa ndani (inhale) diaphragm hushuka chini ili kusaidia kuivuta hewa ifike kwenye mapafu. Na unapotoa hewa nje (exhale) diaphragm hutulia kwa kubakia sehem yake ili kuwezesha hewa chafu kutoka nje kupitia pua na mdomo. Sasa basi, kuna wakati diaphragm kubugudhiwa na kuisababisha kushuka chini kwa kasi sana jambo linalosababisha wewe kuvuta hewa (inhale) kwa kasi isiyo ya kawaida kupitia koromeo la sauti, hewa ikifika kwenye box la sauti (larynx), sehem hiyo hujifunga kwa haraka sana ili kuzuia hewa isipite huko na ndipo KWIKWI hutokea. Mambo mengine yanayoweza kuibugudhi diaphragm na kuisababisha kufanya kazi vibaya mpaka kupelekea kwikwi ni kitendo cha kula haraka haraka au kuvimbewa. 5. KUJIKUNJA KWA NGOZI YA VIDOLE VYA MIKONO BAADA YA KULOWA AU KUKAA MUDA MREFU KWENYE MAJI. Je umewahi shuhudia jinsi ngozi ya vidole vyako inavyojikunja baada ya kufua nguo muda mrefu au kushika maji muda mrefu? Unajua ni kwa sababu gani ngozi hujikunja kama ya mtu aliyezeeka angali yu kijana mara baada ya kukaa sana kwenye maji? Watu wengi kabla walizani kwamba kujikunja kwa ngozi hiyo hutokana na maji kuingia kwenye ngozi na hivyo ngozi hujikunja baada ya kulowa. Lakini wanasayansi baada ya kufanya utafiti kwa muda merefu juu ya nini hasa hupelekea ngozi kujikunja? Walisema HAPANA si kwa sababu ya ngozi kulowana. Na walikuja na majibu haya. Mwili unapokutana na majimaji mara moja hupeleka taarifa na kutafsiri kwamba mazingira hayo yana UTELEZI (Slippery) hivyo kutasababisha mikono kushindwa kushika (Grip) au kukamata vitu kwa urahisi kutokana na utelezi huo. Hapo mwili huchukua hatua ya haraka kuikunja ngozi ya mikono yako ili kurahisisha ushikaji wa vitu vinavyoteleza ndani ya maji pamoja na kutembea kwenye utelezi. 6. VIPELE VIPELE VYA BARIDI KWENYE NGOZI (GOOSEBUMPS) Kazi kubwa ya vipele hivi ni kupunguza kiasi cha joto la mwili linalopotea kupitia matundu ya ngozi. Hivyo kwa kufanya hivi humfanya binadamu kutunza joto la mwili hata katika mazingira ambayo hali yake ya hewa si rafiki kwa mwili wa mwanadamu au ni yenye baridi sana. 7. MACHOZI (TEARS) Zaidi ya kuwa majimaji (MUCOUS MEMBRANE ) yanayopatikana kwenye Macho ambayo kazi zake ni kulilinda jicho dhidi ya kitu chochote kigeni kinachoingia jichoni (mfano unapokata vitunguu au mdudu anapoingia jichoni huwa unatoa machozi mengi eeeh!! Pia dhidi ya upepo na moshi) na pia hutumika kama kilainishi cha jicho pale linapokuwa linazunguka zunguka (blink). Vilevile machozi yana kazi ya kupunguza HISIA ZA HUDHUNI zinazozalishwa mwilini. Wanasayansi wanaamini kuwa mtu anapokua mwenye msongo wa mawazo (stress) mwili hutengeneza kitu kipya ili kwenda kubugudhi na kuharibu maumivu yote ambayo mtu anajisikia. Hivyo machozi yanayozalishwa hapa huwa na kemikali na yanafahamika kama NATURAL PAINKILLER. Machozi haya ni tofauti na machozi ya kawaida, lengo lake hasa la kuzalishwa ni kwa ajili ya kuondoa kabisa maumivu yaliyozalishwa mwilini Hivyo mpaka hapa tumeona kua kuna machozi ya aina tatu ambayo ni i. Basal tears (vilainishi) ii. Reflex tears (mlinzi) iii. Emotion tears (mtuliza maumivu) 8. KUSHTUKA USINGIZINI (MYOCLONIC JERKS or HYPNIC JERK). Je! Ushawahi kutokewa na hali hii? umelala halafu ghafla unashtuka usingizini kwa mguvu nyingi kama umepigwa na shoti ya umeme na akili inakurudi ghafla huku mapigo ya moyo yakikuenda mbio? Na hali hii ikakutokea pasipo hata kuota ndoto yoyote? Basi usiogope au kuwasingizia watu uchawi, hii ni hali ya sayansi ya mwili.na ni njia moja wapo katika ile mifumo ya mwili kujilinda. Je hutokeaje? Hii ni hali ya ajabu sana isiyofanywa kwa hiari ambayo huwatokea watu mara tu wamejinyoosha kitandani na kupitiwa na usingizi, mwili hutetemeshwa na kusukumwa kwa nguvu na mtu hushtuka katika hali kama vile kapigwa na shoti ya umeme. Hali hii inaweza kupelekea mtu hata kuanguka kitandani na humwamsha mara moja kutoka usingizini. Wanasayansi wanatuambia kua, pale tu unapopata usingizi kiwango cha upumuaji kinashuka ghafla, mapigo ya moyo nayo taratibu yanapungua, misuli inatulia kwa ku-relax, Kitu cha AJABU hapa ubongo unatafsiri hali hii kama ni DALILI ZA KIFO (brain's misinterpretation of muscle relaxation), hivyo huchukua hatua za haraka za kuushtua mwili kwa kuutetemesha au kuuskuma kwa nguvu, hali ambayo humfanya mtu kuamka kutoka usingizini kwa KURUKA kitu ambacho ni hali isiyo ya kawaida. Hali hii ikimtokea mtu huambatana na kuongezeka kwa mapigo ya moyo (rapid heartbeat), kuhema haraka haraka, na wakati mwingine mtu hutokwa na jasho jingi. Wakati mwingine mtu huamka ametoa macho na kama ukimwangalia, nae huishia hukuangalia tu huku akikosa la kukujibu endapo utamuuliza vipi kuna tatizo gani? MWILI WAKO NI ZAIDI YA UNAVYOUJUA. JAMBO LA MSINGI NI KUONDOA HOFU KWANI MWILI WAKO UNAJUA NINI UFANYE NA WAKATI GANI ILI KUKULINDA USIKU NA MCHANA KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO. Share pia wengine wajue sio kila kitu ni uchawi
    ·199 Views
  • Nyumbu ( wildebeest) uzito 140 hadi 220 kulingana na afya yake, hupendelea kula nyasi ndogo ndogo zinazochipua, kama hatopata suluba huishi hadi miaka 17 na kidogo.uzee ukimzidi akishindwa kufanya safari kutafta malisho na wenzake basi hufa kwa njaa, eidha ufanywa kitoweo cha jioni na mtawala wa eneo hilo (simba)

    Kundi LA nyumbu huwa kati ya 10,000 hadi 90,000. Endapo majani yapo yakutosha nyumbu huongezeka idadi hadi kufikia 100,000 na zaidi.vipindi vya mvua nyingi ndipo nymbu huzaliana kwa kasi zaidi,

    Nyumbu wa Serengeti hula na kuzaliana nyakati za masika tu.endapo kiangazi kitaingia nyumbuwote hufunga safari na kuelekea hifadhi jilani ya Kenya (masaimar). Nyakati hizo huko kenya huwa kunamalisho yakutosha, nyumbu hukaa miezi isiyopungua 6 ndipo hufanya safari zao.

    Nyumbu ni mnyama wa tofauti kidogo na wanyama wengine kimaumbile, yaani nyumbu amebeba muonekano wa wanyama wasiopungua 7, ngoja nikujuze,

    Nywele za shingoni; SIMBA
    Mkia: FARASI
    Ndevu:MBUZI
    Mapaja ya nyuma; PUNDA MILIA
    Mgongo :ng'ombe
    Miguu ya mbele milefu yanyuma mifupi ; FISI

    Watu husema nyumbu ni mwoga na mzembe

    Nyumbu wakiwa katika kundi huwa ni waoga saaaana, yaani at a mtoto wa duma mwenye mwezi mmoja anaweza kutishia kundi LA nyumbu 20000 na wakakimbia, na asiwepo nyumbu wa kudinda ata kugeuka nyuma.

    Ila nyumbu akiwa mwenyew huwa haogopi .ni mala chache mno nyumbu aliye pekeake kumkimbia adui yake, nyumbu akiwa mwenyewe huwa anajiona kama tembo au kifaru, huwa ni hatari zaidi ata duma hutegea wawe kwenye kundi ndio wavamie.

    Nyumbu wakiwa safarini hawajawai kupisha kitu chochote kilichopo mbeleyao. Wakiwa katika mwendo wa mchaka mchaka wakiluka mabonde na mapolomoko, wakivuka mito mikubwa mithiri ya wanajeshi wakiwa mafunzoni.

    Katika safari yao nyumbu hawajawahi kumsubiri nyumbu mwezao aliyepata ajali, aliejisahau eidha alikuw anakul majan, aliyezaa wala aliyekamatwa na mnyama mlanyama, msafala wao huwa hausubiri kitu wala hauna fea.

    Pia nyumbu hawana mda wa kumtetea mwenzao aliyedhibitiwa na mnyama mla mnyama.
    Nyumbu ( wildebeest) uzito 140 hadi 220 kulingana na afya yake, hupendelea kula nyasi ndogo ndogo zinazochipua, kama hatopata suluba huishi hadi miaka 17 na kidogo.uzee ukimzidi akishindwa kufanya safari kutafta malisho na wenzake basi hufa kwa njaa, eidha ufanywa kitoweo cha jioni na mtawala wa eneo hilo (simba) Kundi LA nyumbu huwa kati ya 10,000 hadi 90,000. Endapo majani yapo yakutosha nyumbu huongezeka idadi hadi kufikia 100,000 na zaidi.vipindi vya mvua nyingi ndipo nymbu huzaliana kwa kasi zaidi, Nyumbu wa Serengeti hula na kuzaliana nyakati za masika tu.endapo kiangazi kitaingia nyumbuwote hufunga safari na kuelekea hifadhi jilani ya Kenya (masaimar). Nyakati hizo huko kenya huwa kunamalisho yakutosha, nyumbu hukaa miezi isiyopungua 6 ndipo hufanya safari zao. Nyumbu ni mnyama wa tofauti kidogo na wanyama wengine kimaumbile, yaani nyumbu amebeba muonekano wa wanyama wasiopungua 7, ngoja nikujuze, Nywele za shingoni; SIMBA Mkia: FARASI Ndevu:MBUZI Mapaja ya nyuma; PUNDA MILIA Mgongo :ng'ombe Miguu ya mbele milefu yanyuma mifupi ; FISI Watu husema nyumbu ni mwoga na mzembe Nyumbu wakiwa katika kundi huwa ni waoga saaaana, yaani at a mtoto wa duma mwenye mwezi mmoja anaweza kutishia kundi LA nyumbu 20000 na wakakimbia, na asiwepo nyumbu wa kudinda ata kugeuka nyuma. Ila nyumbu akiwa mwenyew huwa haogopi .ni mala chache mno nyumbu aliye pekeake kumkimbia adui yake, nyumbu akiwa mwenyewe huwa anajiona kama tembo au kifaru, huwa ni hatari zaidi ata duma hutegea wawe kwenye kundi ndio wavamie. Nyumbu wakiwa safarini hawajawai kupisha kitu chochote kilichopo mbeleyao. Wakiwa katika mwendo wa mchaka mchaka wakiluka mabonde na mapolomoko, wakivuka mito mikubwa mithiri ya wanajeshi wakiwa mafunzoni. Katika safari yao nyumbu hawajawahi kumsubiri nyumbu mwezao aliyepata ajali, aliejisahau eidha alikuw anakul majan, aliyezaa wala aliyekamatwa na mnyama mlanyama, msafala wao huwa hausubiri kitu wala hauna fea. Pia nyumbu hawana mda wa kumtetea mwenzao aliyedhibitiwa na mnyama mla mnyama.
    Like
    1
    ·100 Views
  • Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia Doto Maduhu Sita (32) mkazi wa Kishiri, Wilaya ya Nyamagana ambaye ni baba wa kambo wa mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi kwa tuhuma za kumbaka, kumlawiti na kumshambulia mtoto huyo.

    Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema mtoto huyo alikuwa akifanyiwa ukatili huo mara kwa mara na kupelekea hali yake ya kiafya kuwa dhaifu, hivyo kuwafanya raia wema kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto.
    #neliudcosiah
    Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia Doto Maduhu Sita (32) mkazi wa Kishiri, Wilaya ya Nyamagana ambaye ni baba wa kambo wa mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi kwa tuhuma za kumbaka, kumlawiti na kumshambulia mtoto huyo. Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema mtoto huyo alikuwa akifanyiwa ukatili huo mara kwa mara na kupelekea hali yake ya kiafya kuwa dhaifu, hivyo kuwafanya raia wema kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto. #neliudcosiah
    ·187 Views
  • WALAU UNAWEZA KUCHUKUA KITU KUELEKEA 2025

    1. Peleka watoto shule unazoweza kumudu ada yake, kimsingi shule kuwa na gharama kubwa hakumaanishi inakuhakikishia ufaulu mzuri Kwa watoto. Hakikisha tu wanahudhuria vizuri shule yoyote watafaulu tu.

    2. Panga nyumba au chumba ambacho utaweza kulipia kwa urahisi. Usiishi katika nyumba kubwa au eneo ambalo unahangaika kulipa kila mwaka Kwa jasho na damu.

    3. Panga maisha yako na uishi kulingana na uwezo weko. Weka akiba zaidi na utumie kidogo.

    4. Kuna wanawake mnanunua chakula cha watoto wenu kila asubuhi kabla ya kwenda shuleni au hata kwa familia nzima, hivi hamjui kuwa ni nafuu mno kupika nyumbani?

    5. Watu wengine hamna pesa nyingi, lakini mnalipia DSTV na AZAM TV nyumbani vifurushi vikubwa na hamshindi hapo, Lipia vifurushi vya kawaida na siyo lazima Kila mwezi, kama ni mlevi wa mpira wakati mwingine kaangalie mpira na washkaji bar au vibanda umiza.

    6. Kula milo yenye afya na linda familia yako dhidi ya mbu uepuke kwenda hospitali hovyo.

    7. Nunua Mahitaji ya chakula kwenye masoko makubwa Kwa bei nafuu na tumia vizuri msimu ya vyakula tofauti na matunda kwa kuwa ubunifu kuunda milo inayoendana na Chakula Cha msimu huo.

    8.Usiige maisha ya jirani yako, hujui kipato chake ni kikubwa kiasi gani na anapataje ama mume wake ni 'mtu mkubwa'

    9. Usifuatishe mitindo ya uvaaji kadiri inavyobadilika, nunua mavazi pale unapohitaji tu siyo style zinapokuhitaji. Weka nywele zako nadhifu, suka style rahisi inayokupendeza.

    10. Punguza idadi ya watu wanaokuzunguka... Chagua marafiki wa kweli wachache wenye mambo ya msingi na wewe.

    11. Juu ya vitu vyote tuweke hofu ya Mungu, uadilifu na tusiwe wavivu wa kusali na kumuomba Mwenyezi Mungu Jaalia.

    12. Kupanga ni ufunguo wa mambo mengi, UKIFELI KUPANGA UNAPANGA KUFELI

    13. Usifanye mambo yanayozidi bajeti yako safari hii, hakuna tuzo inayotolewa kwa Familia Bora iliyovaa nguo za gharama kubwa, iliyochangia michango mingi ya sherehe au iliyokula bata sana Kwa mwaka.

    14. Usifanye ushindani na mtu yeyote kwenye suala lolote bali shindana na mipango yako.

    HERI YA MWAKA MPYA
    WALAU UNAWEZA KUCHUKUA KITU KUELEKEA 2025 1. Peleka watoto shule unazoweza kumudu ada yake, kimsingi shule kuwa na gharama kubwa hakumaanishi inakuhakikishia ufaulu mzuri Kwa watoto. Hakikisha tu wanahudhuria vizuri shule yoyote watafaulu tu. 2. Panga nyumba au chumba ambacho utaweza kulipia kwa urahisi. Usiishi katika nyumba kubwa au eneo ambalo unahangaika kulipa kila mwaka Kwa jasho na damu. 3. Panga maisha yako na uishi kulingana na uwezo weko. Weka akiba zaidi na utumie kidogo. 4. Kuna wanawake mnanunua chakula cha watoto wenu kila asubuhi kabla ya kwenda shuleni au hata kwa familia nzima, hivi hamjui kuwa ni nafuu mno kupika nyumbani? 5. Watu wengine hamna pesa nyingi, lakini mnalipia DSTV na AZAM TV nyumbani vifurushi vikubwa na hamshindi hapo, Lipia vifurushi vya kawaida na siyo lazima Kila mwezi, kama ni mlevi wa mpira wakati mwingine kaangalie mpira na washkaji bar au vibanda umiza. 6. Kula milo yenye afya na linda familia yako dhidi ya mbu uepuke kwenda hospitali hovyo. 7. Nunua Mahitaji ya chakula kwenye masoko makubwa Kwa bei nafuu na tumia vizuri msimu ya vyakula tofauti na matunda kwa kuwa ubunifu kuunda milo inayoendana na Chakula Cha msimu huo. 8.Usiige maisha ya jirani yako, hujui kipato chake ni kikubwa kiasi gani na anapataje ama mume wake ni 'mtu mkubwa' 9. Usifuatishe mitindo ya uvaaji kadiri inavyobadilika, nunua mavazi pale unapohitaji tu siyo style zinapokuhitaji. Weka nywele zako nadhifu, suka style rahisi inayokupendeza. 10. Punguza idadi ya watu wanaokuzunguka... Chagua marafiki wa kweli wachache wenye mambo ya msingi na wewe. 11. Juu ya vitu vyote tuweke hofu ya Mungu, uadilifu na tusiwe wavivu wa kusali na kumuomba Mwenyezi Mungu Jaalia. 12. Kupanga ni ufunguo wa mambo mengi, UKIFELI KUPANGA UNAPANGA KUFELI 13. Usifanye mambo yanayozidi bajeti yako safari hii, hakuna tuzo inayotolewa kwa Familia Bora iliyovaa nguo za gharama kubwa, iliyochangia michango mingi ya sherehe au iliyokula bata sana Kwa mwaka. 14. Usifanye ushindani na mtu yeyote kwenye suala lolote bali shindana na mipango yako. HERI YA MWAKA MPYA
    Like
    Love
    Sad
    3
    ·400 Views
  • "Hii ya kupiga pass tatu goli hii sio nzuri Wananchi wala sio uungwana huu, hii ya kutamanisha Mpinzani unamwachia mpira anakushambulia halafu unamrudisha kwa counter wala sio ustaarabu Wananchi, hata hii ya kufunga mabao yanafuatana sio afya sana mnawchanganya Mashabiki hawajui washangilie lipi.

    Hii ya Clement Mzize kufunga ama kuassist sio nzuri sana maana hatuelewi yeye ni Striker ama Kiungo? Hii ya Pacome na Stephen Aziz Ki kucheza kama hawataki, kufunga kwa starehe na kuassist wanapojisikia sio njema sana, Yanga kama kiwanja cha mgogoro tu, utakataa kununua ila utatamani kukimiliki.

    Hii habari ya tano tano wala sio ngeni ndani ya NBC Premier League, labda kama wewe ni Mgeni wa Ligi, hii ishataka kuanza kuwa mbaya itaanza sasa hivi habari ya Udhamini hii" - Farhan JR, Mchambuzi.

    "Hii ya kupiga pass tatu goli hii sio nzuri Wananchi wala sio uungwana huu, hii ya kutamanisha Mpinzani unamwachia mpira anakushambulia halafu unamrudisha kwa counter wala sio ustaarabu Wananchi, hata hii ya kufunga mabao yanafuatana sio afya sana mnawchanganya Mashabiki hawajui washangilie lipi. Hii ya Clement Mzize kufunga ama kuassist sio nzuri sana maana hatuelewi yeye ni Striker ama Kiungo? Hii ya Pacome na Stephen Aziz Ki kucheza kama hawataki, kufunga kwa starehe na kuassist wanapojisikia sio njema sana, Yanga kama kiwanja cha mgogoro tu, utakataa kununua ila utatamani kukimiliki. Hii habari ya tano tano wala sio ngeni ndani ya NBC Premier League, labda kama wewe ni Mgeni wa Ligi, hii ishataka kuanza kuwa mbaya itaanza sasa hivi habari ya Udhamini hii😀" - Farhan JR, Mchambuzi.
    ·135 Views
  • MEMBERS NIPO TU HAPA HOME, AFYA NI NZURI KWA KULA NA KUNYWA CHOCHOTE, NAOMBENI MWALIKO
    MEMBERS NIPO TU HAPA HOME, AFYA NI NZURI KWA KULA NA KUNYWA CHOCHOTE, NAOMBENI MWALIKO 😊😊😊
    Like
    Love
    2
    2 Commenti ·251 Views
  • Profesa Jay amuombea afya Njema Chameleone.!
    Profesa Jay amuombea afya Njema Chameleone.!
    ·112 Views
  • *Idadi ya wagonjwa wa afya ya akili imeendelea kupungua katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe iliyoko Dodoma kwa mwaka 2023-24, kufuatia juhudi za kutoa elimu kuhusu msongo wa mawazo na njia za kukabiliana na changamoto hiyo.

    *Idadi ya wagonjwa wa afya ya akili imeendelea kupungua katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe iliyoko Dodoma kwa mwaka 2023-24, kufuatia juhudi za kutoa elimu kuhusu msongo wa mawazo na njia za kukabiliana na changamoto hiyo.
    ·110 Views
  • BREAKING
    *ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KAZINI MUDA HUU KUTOKA UTUMISHI KADA ZA AFYA, TAASISI MBALIMBALI.*


    > PAKUA PDF HAPA:- https://wananchiforum.com/threads/kuitwa-kazini-kada-za-afya-na-taasisi-mbalimbali-5-desemba-2024.320/
    BREAKING 🚨 *ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KAZINI MUDA HUU KUTOKA UTUMISHI KADA ZA AFYA, TAASISI MBALIMBALI.* > PAKUA PDF HAPA:- https://wananchiforum.com/threads/kuitwa-kazini-kada-za-afya-na-taasisi-mbalimbali-5-desemba-2024.320/
    WANANCHIFORUM.COM
    KUITWA KAZINI KADA ZA AFYA NA TAASISI MBALIMBALI 5 DESEMBA 2024
    TANGAZO LA KUITWA KAZINI Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 03-09-2024 na tarehe...
    Like
    2
    ·309 Views
  • Mlinda mlango Aishi Manula ameshindwa kuendelea na safari baada ya kupata hitilafu ya kiafya dakika chache kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini Algeria tukiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. #paulswai
    Mlinda mlango Aishi Manula ameshindwa kuendelea na safari baada ya kupata hitilafu ya kiafya dakika chache kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini Algeria tukiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. #paulswai
    Like
    Love
    4
    1 Commenti ·272 Views
  • Mkuu wa kitengo cha maudhui wa klabu ya Yanga SC, Privaldinho amjia juu Wilson Orumo.

    "Ukiniuliza miongoni mwa wachambuzi wenye uelewa mzuri wa soka nisipotaja jina la @wilsonoruma_ basi ulizia natumia kinywaji gani muda pengine nimepiga vyombo.

    Namfahamu Udom. Najua uwezo wake. Sijui shida gani imempata. Anyway twende kwenye hoja yake.

    Kwamba kumkejeli Pacome hujagusa biashara ya watu? Sijaona ukiongelea hili bali umejikita kwenye ishu ya mtengeneza jezi. Kuna nyakati tuliitwa maiti? Kuna nyakati walisema jezi zetu ni mbaya mno. Je mzee wangu ulikemea? Je Yanga tulisema chochote?

    Iko hivi

    Utani wa jadi ni mbwembwe za Makolo na mabingwa wa kihistoria. Ni kama mchezo wa ngumi tu. Mbwembwembwe na kejeli zeru ndio tambo zetu. Ipo hivo miaka na miaka. Kama hutaki kutaniwa usije kwenye hizi timu mbili. Pengine kauze suti za wanasheria huko kidogo kuna maadili.

    Uvumilivu wa utani wa jadi umegusa wengi. Huyu Oruma mwenyewe amewahi kuingia kwenye utani wa jadi. Mara kadhaa ametumia maneno makali dhidi ya Yanga na Yanga haijawahi kumgusa.

    Oruma ni bingwa kuitania Yanga ametuita gongo wazi. Hakuna mtu kutoka Yanga aliyewahi kwenda mahakamani. Gongo wazi ni neno la kejeli kwa Yanga.

    Pengine basi kwa kuwa anaharibu brand ya Yanga twende mahakamani na invoice? Mtu ambaye tulitegemea awe mchambuzi na mtenda haki anaingia kwenye utani na Yanga inaona sawa tu. Lakini walipohisi ally amemlenga mtu wao wanatoka na Mapanga.

    Oruma, ni mtu mwenye akili na uelewa mkubwa wa mambo. Kwa bahati mbaya hivi karibuni amechagua njia ambayo binafsi simwelewi. Ni kama anapigana na Yanga hadharani.

    Ni rafiki yangu na mara kadhaa huwa namwambia. Uwezo wake wa kuchanganua mambo ni hazina kubwa kwa taifa letu. Lakini matumizi yake amejikita kwenye siasa za mpira ambazo mara nyingi kwangu sioni kama zina afya.

    Moja kati ya wachambuzi ambao wangeamua kujikita kwenye tactically analysis angesaidia sana TAIFA hili. Leo hii anaita Yanga Gongowazi hivi na sisi tukiamua kuitafutia jina baya EFM atakaa kimya?

    Mimi nafikiri rafiki yangu huyu afanye tafakuri ya kutosha. Kwanza afaham kuwa taifa linamhitaji zaidi kuliko vijana wanaochipukia wanavyosaka comments na likes. Atafakari vyema njia zake.

    Shalom."
    Mkuu wa kitengo cha maudhui wa klabu ya Yanga SC, Privaldinho amjia juu Wilson Orumo. "Ukiniuliza miongoni mwa wachambuzi wenye uelewa mzuri wa soka nisipotaja jina la @wilsonoruma_ basi ulizia natumia kinywaji gani muda pengine nimepiga vyombo. Namfahamu Udom. Najua uwezo wake. Sijui shida gani imempata. Anyway twende kwenye hoja yake. Kwamba kumkejeli Pacome hujagusa biashara ya watu? Sijaona ukiongelea hili bali umejikita kwenye ishu ya mtengeneza jezi. Kuna nyakati tuliitwa maiti? Kuna nyakati walisema jezi zetu ni mbaya mno. Je mzee wangu ulikemea? Je Yanga tulisema chochote? Iko hivi Utani wa jadi ni mbwembwe za Makolo na mabingwa wa kihistoria. Ni kama mchezo wa ngumi tu. Mbwembwembwe na kejeli zeru ndio tambo zetu. Ipo hivo miaka na miaka. Kama hutaki kutaniwa usije kwenye hizi timu mbili. Pengine kauze suti za wanasheria huko kidogo kuna maadili. Uvumilivu wa utani wa jadi umegusa wengi. Huyu Oruma mwenyewe amewahi kuingia kwenye utani wa jadi. Mara kadhaa ametumia maneno makali dhidi ya Yanga na Yanga haijawahi kumgusa. Oruma ni bingwa kuitania Yanga ametuita gongo wazi. Hakuna mtu kutoka Yanga aliyewahi kwenda mahakamani. Gongo wazi ni neno la kejeli kwa Yanga. Pengine basi kwa kuwa anaharibu brand ya Yanga twende mahakamani na invoice? Mtu ambaye tulitegemea awe mchambuzi na mtenda haki anaingia kwenye utani na Yanga inaona sawa tu. Lakini walipohisi ally amemlenga mtu wao wanatoka na Mapanga. Oruma, ni mtu mwenye akili na uelewa mkubwa wa mambo. Kwa bahati mbaya hivi karibuni amechagua njia ambayo binafsi simwelewi. Ni kama anapigana na Yanga hadharani. Ni rafiki yangu na mara kadhaa huwa namwambia. Uwezo wake wa kuchanganua mambo ni hazina kubwa kwa taifa letu. Lakini matumizi yake amejikita kwenye siasa za mpira ambazo mara nyingi kwangu sioni kama zina afya. Moja kati ya wachambuzi ambao wangeamua kujikita kwenye tactically analysis angesaidia sana TAIFA hili. Leo hii anaita Yanga Gongowazi hivi na sisi tukiamua kuitafutia jina baya EFM atakaa kimya? Mimi nafikiri rafiki yangu huyu afanye tafakuri ya kutosha. Kwanza afaham kuwa taifa linamhitaji zaidi kuliko vijana wanaochipukia wanavyosaka comments na likes. Atafakari vyema njia zake. Shalom."
    ·443 Views
  • CHADO MASTA KITENGO; Huyu mwamba kanishangaza katoa movie nyingi tu na hatuna habari nae, ila kafyatua Goma la *MISSION IMPOSSIBLE* kama kaanza leo kilakona anaimbwa na vitoto vya miaka mi3 mpaka mi4 yaani kama una mtoto wa umri huu na hakusumbui weka CHADO MASTA nyosha kidole juuu.
    #sokachampions
    #soccersportstz
    #uefachampionsleague2024
    #tanzania
    #chadomasta
    CHADO MASTA KITENGO; Huyu mwamba kanishangaza katoa movie nyingi tu na hatuna habari nae, ila kafyatua Goma la *MISSION IMPOSSIBLE* kama kaanza leo kilakona anaimbwa na vitoto vya miaka mi3 mpaka mi4 yaani kama una mtoto wa umri huu na hakusumbui weka CHADO MASTA nyosha kidole juuu👆. #sokachampions #soccersportstz #uefachampionsleague2024 #tanzania #chadomasta
    Love
    Like
    4
    ·635 Views
  • Kuna baadhi ya wanawake wakipenda huwa wanapenda kweli yaani toka moyoni........
    Kwa hiyo kama mke wako anamchepuko ujue anaupenda mchepuko wake kweli kwelii......

    Habari zenu wanawake mlioko Ndoani Na mnamichepuko yenu..... Angalieni Furaha Na Upendo wenu ila msisahau kujali Afya zenu..
    Kuna baadhi ya wanawake wakipenda huwa wanapenda kweli yaani toka moyoni........ Kwa hiyo kama mke wako anamchepuko ujue anaupenda mchepuko wake kweli kwelii...... Habari zenu wanawake mlioko Ndoani Na mnamichepuko yenu..... Angalieni Furaha Na Upendo wenu ila msisahau kujali Afya zenu..
    Like
    1
    ·361 Views
  • Hello ndugu zangu natumaini muwazima wa afya napenda kuwatakia uck mwema
    Hello ndugu zangu natumaini muwazima wa afya napenda kuwatakia uck mwema 🙏
    Love
    Like
    3
    ·197 Views
  • Habari yangu ni nzuri sana kiafya
    Habari yangu ni nzuri sana kiafya
    ·267 Views
Pagine in Evidenza