• "Marekani mpaka sasa hawajasaini mkataba wa kuilinda Congo mchakato umekuwa mrefu. Jiulize vile vikwazo vya Magharibi walivyoiwekea Rwanda vimeishia wapi

    Kagame anajua anachokifanya ndio maana licha ya ripoti za UN , US na EU kuonyesha Rwanda wanaifadhili M23 plus Vikwazo hakuna kilichobadilika Congo

    Wanachokifanya wanaoibia Congo na Africa ni ile ile mbinu ya wakati wa ukoloni inaitwa "Divided and Rule " yaani wagawanywe uwatawale nakumbuka hii mbinu pia enzi hizo ndio iliyozaa utani wa jadi wa Yanga na Simba

    Oooh Africa " - Zungu, Mchambuzi wa Siasa na Mtangazaji.

    "Marekani mpaka sasa hawajasaini mkataba wa kuilinda Congo mchakato umekuwa mrefu. Jiulize vile vikwazo vya Magharibi walivyoiwekea Rwanda vimeishia wapi 😀😀😀😀 Kagame anajua anachokifanya ndio maana licha ya ripoti za UN , US na EU kuonyesha Rwanda wanaifadhili M23 plus Vikwazo hakuna kilichobadilika Congo 😭😭😭😭 Wanachokifanya wanaoibia Congo na Africa ni ile ile mbinu ya wakati wa ukoloni inaitwa "Divided and Rule " yaani wagawanywe uwatawale nakumbuka hii mbinu pia enzi hizo ndio iliyozaa utani wa jadi wa Yanga na Simba Oooh Africa🌍 😭" - Zungu, Mchambuzi wa Siasa na Mtangazaji.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·199 مشاهدة
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili hali ya usalama na kibinadamu Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku hali ikizidi kuzorota. Mwakilishi Maalum wa Umoja huo (UN) Nchini DR Congo, Bintou Keita, amesema Waasi wa kundi la M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda sasa wanadhibiti maeneo makubwa ya Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini na kutishia kupanua mashambulizi yao hadi Mkoani Tshopo na Maniema.

    "Hivi karibuni M23 imesimika utawala wake kwa kuteua gavana, makamu gavana na meya huko Bukavu, Kivu Kusini," amesema Keita.

    Ameeleza kuwa mgogoro huo unahusiana na unyonyaji wa madini mashariki mwa DR Congo na kuzua wasiwasi wa kikanda. Pia amegusia hali mbaya ya kibinadamu, akisema kumekuwa na ongezeko la ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara na ajira ya kulazimishwa kwa Vijana, wakiwemo Watoto.

    Licha ya makubaliano ya hivi karibuni kati ya Marais wa Rwanda na DR Congo Nchini Qatar , amani bado haijapatikana. Keita ametoa wito wa kuteuliwa kwa mpatanishi wa Umoja wa Afrika ili kuongoza juhudi za kusitisha mapigano.

    Balozi wa DR Congo katika Baraza la Umoja wa kimataifa (UN), Zénon Mukongo Ngay, ameishutumu Rwanda kwa kutotekeleza usitishaji mapigano, huku Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, akisema Nchi yake itaendelea kuchukua "hatua za ulinzi" mpaka kuwe na mfumo wa kudumu wa usalama.

    Wakati huo huo, imeripotiwa kuwa DR Congo inakabiliwa na janga kubwa zaidi la njaa kuwahi kutokea, ambapo Watu zaidi ya milioni 27.7 wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na vita na ukosefu wa utulivu mashariki mwa Nchi hiyo.

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili hali ya usalama na kibinadamu Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 huku hali ikizidi kuzorota. Mwakilishi Maalum wa Umoja huo (UN) Nchini DR Congo, Bintou Keita, amesema Waasi wa kundi la M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda 🇷🇼 sasa wanadhibiti maeneo makubwa ya Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini na kutishia kupanua mashambulizi yao hadi Mkoani Tshopo na Maniema. "Hivi karibuni M23 imesimika utawala wake kwa kuteua gavana, makamu gavana na meya huko Bukavu, Kivu Kusini," amesema Keita. Ameeleza kuwa mgogoro huo unahusiana na unyonyaji wa madini mashariki mwa DR Congo na kuzua wasiwasi wa kikanda. Pia amegusia hali mbaya ya kibinadamu, akisema kumekuwa na ongezeko la ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara na ajira ya kulazimishwa kwa Vijana, wakiwemo Watoto. Licha ya makubaliano ya hivi karibuni kati ya Marais wa Rwanda na DR Congo Nchini Qatar 🇶🇦, amani bado haijapatikana. Keita ametoa wito wa kuteuliwa kwa mpatanishi wa Umoja wa Afrika ili kuongoza juhudi za kusitisha mapigano. Balozi wa DR Congo katika Baraza la Umoja wa kimataifa (UN), Zénon Mukongo Ngay, ameishutumu Rwanda kwa kutotekeleza usitishaji mapigano, huku Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, akisema Nchi yake itaendelea kuchukua "hatua za ulinzi" mpaka kuwe na mfumo wa kudumu wa usalama. Wakati huo huo, imeripotiwa kuwa DR Congo inakabiliwa na janga kubwa zaidi la njaa kuwahi kutokea, ambapo Watu zaidi ya milioni 27.7 wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na vita na ukosefu wa utulivu mashariki mwa Nchi hiyo.
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·208 مشاهدة
  • Rais wa Nchi ya Burundi , Evariste Ndayishimiye anasema kuwa Nchi ya Rwanda ina mpango wa kuivamia Burundi kupitia Congo ambapo anasema Nchi hiyo itakuwa imekosea sana.

    “Tunajua kwamba Rwanda inajaribu kutushambulia kupitia eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kupitia vuguvugu la Red-Tabara. Lakini tunawaambia kwamba ikiwa wanataka kushambulia Bujumbura kupitia Congo na sisi Kigali hatuko mbali kupitia Kirundo,” alisema Rais Evariste Ndayishimiye

    Baada ya kauli hiyo, Msemaji wa Serikali ya Rwanda Yolande Makolo amesema kuwa, ameshangazwa na kauli ya Rais Evariste Ndayishimiye huku akihoji Rais Ndayishimiye anaeleza kuwa ana taarifa za kuaminika kuwa Rwanda ina mpango wa kushambulia Burundi ?. Msemaji huyo alisema pia endapo hali hiyo ikitokea basi migogoro inaweza kuwa na maafa kwani inaweza kusambaa katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki na kati.

    Rais Ndayishimiye amemalizia kwa kusema kuwa tayari ameshatuma Wajumbe kadhaa kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame wa kumtaka atekeleze makubaliano ambayo yatazileta pamoja Nchi hizo mbili pamoja lakini hadi leo hii hakuna majibu yoyote yaliyotolewa na bado anayasubiri pia.

    Rais wa Nchi ya Burundi 🇧🇮, Evariste Ndayishimiye anasema kuwa Nchi ya Rwanda 🇷🇼 ina mpango wa kuivamia Burundi kupitia Congo ambapo anasema Nchi hiyo itakuwa imekosea sana. “Tunajua kwamba Rwanda inajaribu kutushambulia kupitia eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kupitia vuguvugu la Red-Tabara. Lakini tunawaambia kwamba ikiwa wanataka kushambulia Bujumbura kupitia Congo na sisi Kigali hatuko mbali kupitia Kirundo,” alisema Rais Evariste Ndayishimiye Baada ya kauli hiyo, Msemaji wa Serikali ya Rwanda Yolande Makolo amesema kuwa, ameshangazwa na kauli ya Rais Evariste Ndayishimiye huku akihoji Rais Ndayishimiye anaeleza kuwa ana taarifa za kuaminika kuwa Rwanda ina mpango wa kushambulia Burundi ?. Msemaji huyo alisema pia endapo hali hiyo ikitokea basi migogoro inaweza kuwa na maafa kwani inaweza kusambaa katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki na kati. Rais Ndayishimiye amemalizia kwa kusema kuwa tayari ameshatuma Wajumbe kadhaa kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame wa kumtaka atekeleze makubaliano ambayo yatazileta pamoja Nchi hizo mbili pamoja lakini hadi leo hii hakuna majibu yoyote yaliyotolewa na bado anayasubiri pia.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·154 مشاهدة
  • "Najisikia vibaya namna watu wanavyoniona na kuanza kuniita Yesu, wanafikia hata kutundika picha zangu katika nyumba zao, mimi ni mwigizaji tu, mimi ni mtu" - Jonathan Roumie(50), mwigizaji wa Marekani

    Aidha, Jonathan Roumie katika mahojiano amesema maisha yake binafsi alikuwa na hali mbaya kiuchumi hakuwa na uhakika siku inayofuata atakula nini, alikuwa mwigizaji ila kiuchumi alikuwa bado hajafanikiwa. Baada ya mambo kuzidi kuwa magumu siku moja ni kama alikuwa anamuomba Mungu kuhusu hali anayopitia ili mambo yake yakae sawa

    Baada ya miezi kama mitatu ndio akapata nafasi ya kuigiza kama Yesu katika series ya "The Chosen" iliyoanza kuoneshwa 2017 ambayo imejipatia umaarufu mkubwa sana hadi sasa imetazamwa na watu zaidi ya milioni 250 na misimu mipya inafuata huku ikipongezwa kwa kinachoonekana kuigizwa

    Umaarufu wa uhusika wake kama Yesu umempa umaarufu mkubwa na fursa nyingi ikiwemo katika mikutano na makongamano makubwa ya kidini na app za dini ya kikiristo

    Jonathan ambaye ni mkatoliki, alipoulizwa na New York Times, je ni tukio gani gumu analokumbuka ambalo alishakutana nalo baada ya kuigiza kama Yesu, amejibu kwa kusema kuna kipindi alikuwa katika mkutano kwenye uwanja wenye watu takribani 40,000 baadaye alishuka stejini akaenda kwenye chumba fulani uwanjani hapo, mmoja wa walinzi alikuja akamwambia nje kuna mwanamke ana mtoto kwenye kiti cha magurudumu anaomba kusalimiana na wewe

    Jonathan alitoka akaonana na mwanamke husika na mwanae ambaye kwa ufupi alieleza jinsi Yesu alivyoponya mtu katika hiyo series ya "The Chosen" na kusema angependa mwanae pia apone yaani akimtaka Jonathan amponye mtoto wake. Ilibidi Jonathan amueleze ukweli kwamba yeye sio mponyaji wala mhubiri bali ni mwigizaji tu.

    Jonathan akamueleza wafanye maombi wote ilichukua kama dakika moja, walipomaliza maombi wakafurahi na kushukuru kisha Jonathan akarudi alipokuwa huku akitokwa na machozi akihisi amewaangusha matarajio waliyokuwa nayo kwake ila amesema ni bora waujue ukweli kuwa yeye sio Yesu wala mponyaji bali ni mwigizaji tu

    Ukiacha hayo ya uhusika wake wa Yesu na dini, Jonathan Roumie amegusia pia kwamba alishafika Tanzania na Rwanda sababu kuna watoto kadhaa wanaoishi katika mazingira magumu huwa anawasaidia na familia zao

    Jonathan Roumie pia ameweka wazi kwamba anatamani watu pia wawe wanamuona katika nyuma ya pazia(behind the scene) anayopitia katika kujiandaa na uigizaji wake kama Yesu ili watu wengine waelewe wajue kumtofautisha katika maisha halisi na kisanaa

    KUMBUKA, zipo filamu nyingine miaka ya nyuma kuhusu Yesu zilizohusisha waigizaji wengine kabla ya sasa Jonathan Roumie kupata umaarufu na uhusika wa Yesu katika series maarufu ya "The Chosen"
    (Swahili Word)

    "Najisikia vibaya namna watu wanavyoniona na kuanza kuniita Yesu, wanafikia hata kutundika picha zangu katika nyumba zao, mimi ni mwigizaji tu, mimi ni mtu" - Jonathan Roumie(50), mwigizaji wa Marekani Aidha, Jonathan Roumie katika mahojiano amesema maisha yake binafsi alikuwa na hali mbaya kiuchumi hakuwa na uhakika siku inayofuata atakula nini, alikuwa mwigizaji ila kiuchumi alikuwa bado hajafanikiwa. Baada ya mambo kuzidi kuwa magumu siku moja ni kama alikuwa anamuomba Mungu kuhusu hali anayopitia ili mambo yake yakae sawa Baada ya miezi kama mitatu ndio akapata nafasi ya kuigiza kama Yesu katika series ya "The Chosen" iliyoanza kuoneshwa 2017 ambayo imejipatia umaarufu mkubwa sana hadi sasa imetazamwa na watu zaidi ya milioni 250 na misimu mipya inafuata huku ikipongezwa kwa kinachoonekana kuigizwa Umaarufu wa uhusika wake kama Yesu umempa umaarufu mkubwa na fursa nyingi ikiwemo katika mikutano na makongamano makubwa ya kidini na app za dini ya kikiristo Jonathan ambaye ni mkatoliki, alipoulizwa na New York Times, je ni tukio gani gumu analokumbuka ambalo alishakutana nalo baada ya kuigiza kama Yesu, amejibu kwa kusema kuna kipindi alikuwa katika mkutano kwenye uwanja wenye watu takribani 40,000 baadaye alishuka stejini akaenda kwenye chumba fulani uwanjani hapo, mmoja wa walinzi alikuja akamwambia nje kuna mwanamke ana mtoto kwenye kiti cha magurudumu anaomba kusalimiana na wewe Jonathan alitoka akaonana na mwanamke husika na mwanae ambaye kwa ufupi alieleza jinsi Yesu alivyoponya mtu katika hiyo series ya "The Chosen" na kusema angependa mwanae pia apone yaani akimtaka Jonathan amponye mtoto wake. Ilibidi Jonathan amueleze ukweli kwamba yeye sio mponyaji wala mhubiri bali ni mwigizaji tu. Jonathan akamueleza wafanye maombi wote ilichukua kama dakika moja, walipomaliza maombi wakafurahi na kushukuru kisha Jonathan akarudi alipokuwa huku akitokwa na machozi akihisi amewaangusha matarajio waliyokuwa nayo kwake ila amesema ni bora waujue ukweli kuwa yeye sio Yesu wala mponyaji bali ni mwigizaji tu Ukiacha hayo ya uhusika wake wa Yesu na dini, Jonathan Roumie amegusia pia kwamba alishafika Tanzania na Rwanda sababu kuna watoto kadhaa wanaoishi katika mazingira magumu huwa anawasaidia na familia zao Jonathan Roumie pia ameweka wazi kwamba anatamani watu pia wawe wanamuona katika nyuma ya pazia(behind the scene) anayopitia katika kujiandaa na uigizaji wake kama Yesu ili watu wengine waelewe wajue kumtofautisha katika maisha halisi na kisanaa KUMBUKA, zipo filamu nyingine miaka ya nyuma kuhusu Yesu zilizohusisha waigizaji wengine kabla ya sasa Jonathan Roumie kupata umaarufu na uhusika wa Yesu katika series maarufu ya "The Chosen" (Swahili Word)
    Love
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·296 مشاهدة
  • Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , Felix Tshisekedi amesema Nchi yake iko tayari kuingia mkataba wa madini na Nchi Marekani kwa mabadilishano ya kupatiwa uwezo wa kujilinda dhidi ya Makundi ya Wapiganaji mashariki mwa taifa hilo kama vile kundi la M23 na mengineyo.

    Akizungumza na kituo cha Televisheni cha Fox News leo asubuhi, Rais huyo amesema makubaliano ya aina hiyo yataiwezesha Nchi ya DR Congo kuchimba madini yake kupitia Kampuni za Marekani huku yenyewe ikinufaika kwa kuimarisha mifumo yake ya ulinzi na usalama. Nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa madini ikiwemo kobalti na urani imekuwa inapambana na Kundi la Waasi wa M23 linadaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda ambalo limefanikiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu kuchukua udhibiti wa maeneo makubwa upande wa mashariki mwa Nchi hiyo.

    Hapo jana, kundi hilo la Waasi wa M23 limeendelea kufanya mashambulizi na kuingia Mji mdogo wenye utajiri wa madini wa Walikale licha ya mwito wa kusitishwa mapigano uliotolewa na Rais Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame walipokutana Nchini Qatar mapema wiki hii.

    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, Felix Tshisekedi amesema Nchi yake iko tayari kuingia mkataba wa madini na Nchi Marekani 🇺🇸 kwa mabadilishano ya kupatiwa uwezo wa kujilinda dhidi ya Makundi ya Wapiganaji mashariki mwa taifa hilo kama vile kundi la M23 na mengineyo. Akizungumza na kituo cha Televisheni cha Fox News leo asubuhi, Rais huyo amesema makubaliano ya aina hiyo yataiwezesha Nchi ya DR Congo kuchimba madini yake kupitia Kampuni za Marekani huku yenyewe ikinufaika kwa kuimarisha mifumo yake ya ulinzi na usalama. Nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa madini ikiwemo kobalti na urani imekuwa inapambana na Kundi la Waasi wa M23 linadaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda 🇷🇼 ambalo limefanikiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu kuchukua udhibiti wa maeneo makubwa upande wa mashariki mwa Nchi hiyo. Hapo jana, kundi hilo la Waasi wa M23 limeendelea kufanya mashambulizi na kuingia Mji mdogo wenye utajiri wa madini wa Walikale licha ya mwito wa kusitishwa mapigano uliotolewa na Rais Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame walipokutana Nchini Qatar 🇶🇦 mapema wiki hii.
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·189 مشاهدة
  • "Paul Kagame the Rock from East Africa leo kawajibu Belgium kwa kumfukuza balozi wao Rwanda, kiufupi hakuna tena kwa sasa mahusiano kati ya Rwanda na Belgium

    Kagame anaishtumu Belgium kuwa ni kimbelembele yaani ana kamdomo cha kumchongea Rwanda kwa wakubwa ambao ni Uingereza na Marekani ndio maana Rwanda kapigwa vikwazo

    The Rock kagame kayatibua na Belgium huku tayari ana vikwazo kutoka Marekani na Uingereza na hajali wala nini, yeye siku zote anasema kuwa Rwanda haihusiki na M23 hivyo basi hivyo vikwazo yeye anaona kuwa Rwanda inaonewa tu!

    Huyo ndiye Kagame the Rock from East Africa hanaga unafiki Ukijichanganya tu anaruka na wewe, wewe muulize Museveni licha ya kuwa marafiki wa kitambo na kuhaso pamoja lakini Kagame haonagi haya kumsema Museveni akijichanganya, ... Yeye Kagame kwake ni kitu cha kawaida kuingia katika migogoro na kiongozi yeyote kutoka eneo lolote li mradi tu anatetea maslahi ya Rwanda ama Misimamo yake binafsi!!!

    Niwaache na swali je ni nchi gani ya Afrika mashariki ambayo Kagame hajawahi kuingia kwenye mgogoro nayo?" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa siasa.

    "Paul Kagame the Rock from East Africa leo kawajibu Belgium kwa kumfukuza balozi wao Rwanda, kiufupi hakuna tena kwa sasa mahusiano kati ya Rwanda na Belgium Kagame anaishtumu Belgium kuwa ni kimbelembele yaani ana kamdomo cha kumchongea Rwanda kwa wakubwa ambao ni Uingereza na Marekani ndio maana Rwanda kapigwa vikwazo The Rock kagame kayatibua na Belgium huku tayari ana vikwazo kutoka Marekani na Uingereza na hajali wala nini, yeye siku zote anasema kuwa Rwanda haihusiki na M23 😃 hivyo basi hivyo vikwazo yeye anaona kuwa Rwanda inaonewa tu! Huyo ndiye Kagame the Rock from East Africa hanaga unafiki Ukijichanganya tu anaruka na wewe, wewe muulize Museveni licha ya kuwa marafiki wa kitambo na kuhaso pamoja lakini Kagame haonagi haya kumsema Museveni akijichanganya, ... Yeye Kagame kwake ni kitu cha kawaida kuingia katika migogoro na kiongozi yeyote kutoka eneo lolote li mradi tu anatetea maslahi ya Rwanda ama Misimamo yake binafsi!!! Niwaache na swali je ni nchi gani ya Afrika mashariki ambayo Kagame hajawahi kuingia kwenye mgogoro nayo?" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa siasa.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·188 مشاهدة
  • Baada ya kutangaza kuwa hawatashiriki mazungumzo ya amani huko Mjini Luanda Nchini Angola , Waasi wa kundi la M23 wamesema kuwa Umoja wa Ulaya (EU) ni moja ya Taasisi inayokwamisha mazungumzo hayo kufuatia kuwekewa vikwazo na Umoja huo Viongozi wake Wakuu akiwemo Bertrand Bisimwa.

    Hata hivyo, Serikali ya Kinshasa kupitia Msemaji wake Tina Salama, imesema itashiriki mazungumzo hayo licha ya Kundi la Waasi wa M23 kujiweka pembeni. Pia Serikali ya Angola vile vile imetangaza kwamba mazungumzo hayo yataendelea kama ilivyokuwa imepangwa. Wakizungumzia vikwazo hivyo vya moja wa Ulaya, Waasi hao wa M23 wamesema Taasisi kadhaa za kimataifa zinakwamisha juhudi za kutafuta amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo .

    Ikumbukwe kwamba hapo jana, Umoja wa Ulaya ulitangaza kuwawekea vikwazo Makamanda watatu (3) wa Jeshi la Rwanda na Mkuu wa Shirika lake la uchimbaji madini kwa madai ya kuwaunga mkono Wapiganaji wanaovuruga amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Pia Umoja huo ulimuwekea vikwazo Mkuu wa kundi la M23, Bertrand Bisimwa.

    Baada ya kutangaza kuwa hawatashiriki mazungumzo ya amani huko Mjini Luanda Nchini Angola 🇦🇴, Waasi wa kundi la M23 wamesema kuwa Umoja wa Ulaya (EU) ni moja ya Taasisi inayokwamisha mazungumzo hayo kufuatia kuwekewa vikwazo na Umoja huo Viongozi wake Wakuu akiwemo Bertrand Bisimwa. Hata hivyo, Serikali ya Kinshasa kupitia Msemaji wake Tina Salama, imesema itashiriki mazungumzo hayo licha ya Kundi la Waasi wa M23 kujiweka pembeni. Pia Serikali ya Angola vile vile imetangaza kwamba mazungumzo hayo yataendelea kama ilivyokuwa imepangwa. Wakizungumzia vikwazo hivyo vya moja wa Ulaya, Waasi hao wa M23 wamesema Taasisi kadhaa za kimataifa zinakwamisha juhudi za kutafuta amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Ikumbukwe kwamba hapo jana, Umoja wa Ulaya ulitangaza kuwawekea vikwazo Makamanda watatu (3) wa Jeshi la Rwanda 🇷🇼 na Mkuu wa Shirika lake la uchimbaji madini kwa madai ya kuwaunga mkono Wapiganaji wanaovuruga amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Pia Umoja huo ulimuwekea vikwazo Mkuu wa kundi la M23, Bertrand Bisimwa.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·168 مشاهدة
  • Rais wa Nchi ya Rwanda , Paul Kagame ameionya Nchi ya Ubelgiji kuacha kutoa maagizo kwa Nchi yake na kuipangia cha kufanya utadhani kwamba Mungu amewapa jukumu na haki ya kuwasimamia ambapo amesema Rwanda haitokubali kutawaliwa tena na Wabelgji bali itapambana nao na itawashinda.

    Hayo ameyasema jana Jumapili Machi 16,2025 katika ukumbi wa BK Arena Nchini Rwanda, Kagame alinunuliwa akisema:

    “Nawaonya Wabelgi , Wabelgiji wameiharibu Rwanda, Wameua Wanyarwanda, tuliwaonya zamani na tunawaonya leo, wanasema ‘hawatuwaruhusu kufanya hiki na kile’ na sisi tunawauliza nyinyi ni nani?, nani kawapa jukumu la kutusimamia sisi?”

    “Wanyarwanda wanamuamini Mungu, mnaamini Mungu amewapa Wabelgiji jukumu la kuisimamia Rwanda?, kwa uwezo huu mdogo tulionao, tutapambana nao wote wanaotumia muda wao kututukana, kujaribu kututesa na hawatoweza kutushinda, watuache tuishi kwa amani, baada ya miaka yote tuliyotumia kupambana kuijenga Nchi yetu tunataka kuwa Wanyarwanda hatutaki kuwa Wabelgiji”

    “Rwanda kwa bahati mbaya tulitawaliwa na ka-nchi kadogo (Ubelgiji) ambayo ilienda mbali zaidi na kuigawa nchi yetu ili iwe ndogo kama nchi yao, sijawahi kusita kulieleza hili, tulilaani hili zamani na tutaendelea kulaani jambo hilo leo, hakuna kitu kibaya kitatokea kwetu kushinda majanga tuliyopitia huko nyuma, ndio maana hatupaswi kuogopa kusema na kujipambania sisi wenyewe dhidi ya wale wanaotaka kutuangamiza”

    Katika hatua nyingine, Serekali ya Rwanda imeawaamuru Wanadiplomasia wote wa Ubelgiji Nchini humo kuondoka ndani ya saa 48. Rwanda imesema kuwa itahakikisha ulinzi wa majengo, mali, na kumbukumbu za ubalozi wa Ubelgiji Jijini Kigali.

    Serikali ya Rwanda imesema kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na ubelgiji imefikiwa baada ya kuzingatia kwa makini mambo kadhaa, yote yakihusishwa na hatua za kusikitisha za Ubelgiji kuendeleza udanganyifu wake wa ukoloni mamboleo.

    Rais wa Nchi ya Rwanda 🇷🇼 , Paul Kagame ameionya Nchi ya Ubelgiji 🇧🇪 kuacha kutoa maagizo kwa Nchi yake na kuipangia cha kufanya utadhani kwamba Mungu amewapa jukumu na haki ya kuwasimamia ambapo amesema Rwanda haitokubali kutawaliwa tena na Wabelgji bali itapambana nao na itawashinda. Hayo ameyasema jana Jumapili Machi 16,2025 katika ukumbi wa BK Arena Nchini Rwanda, Kagame alinunuliwa akisema: “Nawaonya Wabelgi , Wabelgiji wameiharibu Rwanda, Wameua Wanyarwanda, tuliwaonya zamani na tunawaonya leo, wanasema ‘hawatuwaruhusu kufanya hiki na kile’ na sisi tunawauliza nyinyi ni nani?, nani kawapa jukumu la kutusimamia sisi?” “Wanyarwanda wanamuamini Mungu, mnaamini Mungu amewapa Wabelgiji jukumu la kuisimamia Rwanda?, kwa uwezo huu mdogo tulionao, tutapambana nao wote wanaotumia muda wao kututukana, kujaribu kututesa na hawatoweza kutushinda, watuache tuishi kwa amani, baada ya miaka yote tuliyotumia kupambana kuijenga Nchi yetu tunataka kuwa Wanyarwanda hatutaki kuwa Wabelgiji” “Rwanda kwa bahati mbaya tulitawaliwa na ka-nchi kadogo (Ubelgiji) ambayo ilienda mbali zaidi na kuigawa nchi yetu ili iwe ndogo kama nchi yao, sijawahi kusita kulieleza hili, tulilaani hili zamani na tutaendelea kulaani jambo hilo leo, hakuna kitu kibaya kitatokea kwetu kushinda majanga tuliyopitia huko nyuma, ndio maana hatupaswi kuogopa kusema na kujipambania sisi wenyewe dhidi ya wale wanaotaka kutuangamiza” Katika hatua nyingine, Serekali ya Rwanda imeawaamuru Wanadiplomasia wote wa Ubelgiji Nchini humo kuondoka ndani ya saa 48. Rwanda imesema kuwa itahakikisha ulinzi wa majengo, mali, na kumbukumbu za ubalozi wa Ubelgiji Jijini Kigali. Serikali ya Rwanda imesema kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na ubelgiji imefikiwa baada ya kuzingatia kwa makini mambo kadhaa, yote yakihusishwa na hatua za kusikitisha za Ubelgiji kuendeleza udanganyifu wake wa ukoloni mamboleo.
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·208 مشاهدة
  • Nchi ya Ujerumani imepanda kusitisha misaada kwa Nchi ya Rwanda kutokana na kujihusisha kwao na Kundi la Waasi wa M23 ambao limefanikiwa kuiteka Miji ya Goma na Bukavu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo . Tayari Rwanda imeshafahamishwa na Ujerumani kuhusu mpango huo.

    Aidha, Nchi ya Rwanda imekuwa ikinufaika na misaada kutoka Nchini Ujerumani inayokadiriwa kufikia thamani ya wastani wa Dola za Kimarekani milioni 53 kwa mwaka ambayo imekuwa ikitolewa katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, uzalishaji wa chanjo na mabadiliko ya tabia Nchi.

    Nchi ya Ujerumani 🇩🇪 imepanda kusitisha misaada kwa Nchi ya Rwanda 🇷🇼 kutokana na kujihusisha kwao na Kundi la Waasi wa M23 ambao limefanikiwa kuiteka Miji ya Goma na Bukavu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Tayari Rwanda imeshafahamishwa na Ujerumani kuhusu mpango huo. Aidha, Nchi ya Rwanda imekuwa ikinufaika na misaada kutoka Nchini Ujerumani inayokadiriwa kufikia thamani ya wastani wa Dola za Kimarekani milioni 53 kwa mwaka ambayo imekuwa ikitolewa katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, uzalishaji wa chanjo na mabadiliko ya tabia Nchi.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·273 مشاهدة
  • Uingereza imesitisha kutoa baadhi ya misaada ya moja kwa moja kwa Nchi ya Rwanda kufuatia kuendelea kwa machafuko ya yanayosababishwa na Vikundi huko Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kikiwemo Kikundi cha Waasi cha M23 ambacho kinadaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda.

    Uamuzi huo unakuja baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Lammy kukutana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame Jijini Kigali, Rwanda na Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi Jijini Kinshasa, DR Congo.

    Uingereza 🇬🇧 imesitisha kutoa baadhi ya misaada ya moja kwa moja kwa Nchi ya Rwanda 🇷🇼 kufuatia kuendelea kwa machafuko ya yanayosababishwa na Vikundi huko Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 kikiwemo Kikundi cha Waasi cha M23 ambacho kinadaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda. Uamuzi huo unakuja baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Lammy kukutana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame Jijini Kigali, Rwanda na Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi Jijini Kinshasa, DR Congo.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·318 مشاهدة
  • "Naona Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amefunga safari hadi Congo kumuona Rais Tshisekedi, sijui ni kipi hasa kinaendelea katika jumuiya ya Afrika mashariki lakini ni kama kuna muungano ndani ya muungano, eeeh kuna muungano kati ya Congo na Burundi ambao unalenga kupambana dhidi ya Rwanda

    Yaani ukiwatazama Congo na Burundi ni kama wameungana kupambana na Rwanda na M23 eeeh ipo wazi na tayari mapigano kati ya majeshi ya Congo Burundi dhidi ya Rwanda na M23 yameshuhudiwa, EAC wasipodhibiti hali ya Congo mzozo huu utaenda kutanuka na kuwa wa kikanda

    Ngoja tuone ila yajayo sio mazuri kwa diplomasia ya EAC , kiufupi ziara ya Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, nchini Congo inalenga kuonana na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi, huku lengo kuu ikiwa na mazungumzo kuhusu mzozo unaolikumba eneo la mashariki mwa Kongo" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.

    "Naona Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amefunga safari hadi Congo kumuona Rais Tshisekedi, sijui ni kipi hasa kinaendelea katika jumuiya ya Afrika mashariki lakini ni kama kuna muungano ndani ya muungano, eeeh kuna muungano kati ya Congo na Burundi ambao unalenga kupambana dhidi ya Rwanda Yaani ukiwatazama Congo na Burundi ni kama wameungana kupambana na Rwanda na M23 eeeh ipo wazi na tayari mapigano kati ya majeshi ya Congo Burundi dhidi ya Rwanda na M23 yameshuhudiwa, EAC wasipodhibiti hali ya Congo mzozo huu utaenda kutanuka na kuwa wa kikanda 😭 Ngoja tuone ila yajayo sio mazuri kwa diplomasia ya EAC , kiufupi ziara ya Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, nchini Congo inalenga kuonana na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi, huku lengo kuu ikiwa na mazungumzo kuhusu mzozo unaolikumba eneo la mashariki mwa Kongo" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·413 مشاهدة
  • Maskari wa Jeshi la Ulinzi la Afrika Kusini (SANDF) waliojeruhiwa katika mapigano Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , limeanza kurejea nyumbani kupitia Jijini Kigali, Rwanda baada ya kukwama katika kambi zao kwa takriban mwezi mmoja DR Congo.

    Wanajeshi hao ni miongoni mwa Askari wa (SANDF) walioko chini ya Kikosi cha Walinda Amani wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SAMIDRC), wanaoimarisha ulinzi Mashariki mwa DR Congo pamoja na kukabiliana na uovu wa Waasi wa kundi la M23 dhidi ya Raia wa DR Congo.

    Televisheni ya Afrika Kusini ya SABC imesema, Wanajeshi hao ambao walishindwa kupambana na Waasi wa kundi la M23 ambao waliitwaa Miji ya mashariki mwa Nchi hiyo, walionekana wakiondoka Mjini Goma kuanzia juzi jioni kwa barabara bila vifaa na sare zao za Kijeshi. Ripoti ya Jarida la Afrika Kusini la Rapport iliyochapishwa Jumapili ilieleza kuwa Wanajeshi wa Afrika Kusini waliojeruhiwa ni zaidi ya 189.

    Kwa mujibu wa Jarida hilo, miongoni mwa waliojeruhiwa ni Wanajeshi wawili (2) ambao ni Wajawazito, huku idadi ya Wanajeshi wa (SANDF) wanaoendelea kukwama Nchini DR Congo ikikadiriwa kuwa kati ya elfu moja (1,000) na elfu mbili (2,000).

    Maskari wa Jeshi la Ulinzi la Afrika Kusini 🇿🇦 (SANDF) waliojeruhiwa katika mapigano Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, limeanza kurejea nyumbani kupitia Jijini Kigali, Rwanda 🇷🇼 baada ya kukwama katika kambi zao kwa takriban mwezi mmoja DR Congo. Wanajeshi hao ni miongoni mwa Askari wa (SANDF) walioko chini ya Kikosi cha Walinda Amani wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SAMIDRC), wanaoimarisha ulinzi Mashariki mwa DR Congo pamoja na kukabiliana na uovu wa Waasi wa kundi la M23 dhidi ya Raia wa DR Congo. Televisheni ya Afrika Kusini ya SABC imesema, Wanajeshi hao ambao walishindwa kupambana na Waasi wa kundi la M23 ambao waliitwaa Miji ya mashariki mwa Nchi hiyo, walionekana wakiondoka Mjini Goma kuanzia juzi jioni kwa barabara bila vifaa na sare zao za Kijeshi. Ripoti ya Jarida la Afrika Kusini la Rapport iliyochapishwa Jumapili ilieleza kuwa Wanajeshi wa Afrika Kusini waliojeruhiwa ni zaidi ya 189. Kwa mujibu wa Jarida hilo, miongoni mwa waliojeruhiwa ni Wanajeshi wawili (2) ambao ni Wajawazito, huku idadi ya Wanajeshi wa (SANDF) wanaoendelea kukwama Nchini DR Congo ikikadiriwa kuwa kati ya elfu moja (1,000) na elfu mbili (2,000).
    Sad
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·283 مشاهدة
  • Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo , Felix Tshisekedi ameitaka Nchi ya Marekani kununua madini moja kwa moja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiitaja ndio "mmiliki halisi" wa rasilimali hizo na sio Nchi Rwanda .

    Tshisekedi amesema kuwa anaanza kwa kutoa ofa hiyo kwa Marekani kwanza huku akitoa pendekezo hilo pia liko wazi kwa mataifa ya Umoja Ulaya (EU) na wanunuzi wengine wanaotafuta na kununua madini kutoka Nchini Rwanda kwa sasa.

    Rais huyo amewaonya Mataifa yanayonunua madini kutoka Nchini Rwanda kuwa wanachukua madini yaliyoibwa kutoka Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, kwahiyo wanatakiwa kununua kwa mmiliki halali. Ikumbukwe kwamba Nchi ya Rwanda ni moja ya kati ya Nchi zinauza madini mengi barani Afrika kwa Mataifa ya Ulaya, Marekani na Asia.

    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo 🇨🇩, Felix Tshisekedi ameitaka Nchi ya Marekani 🇺🇸 kununua madini moja kwa moja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiitaja ndio "mmiliki halisi" wa rasilimali hizo na sio Nchi Rwanda 🇷🇼. Tshisekedi amesema kuwa anaanza kwa kutoa ofa hiyo kwa Marekani kwanza huku akitoa pendekezo hilo pia liko wazi kwa mataifa ya Umoja Ulaya (EU) na wanunuzi wengine wanaotafuta na kununua madini kutoka Nchini Rwanda kwa sasa. Rais huyo amewaonya Mataifa yanayonunua madini kutoka Nchini Rwanda kuwa wanachukua madini yaliyoibwa kutoka Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, kwahiyo wanatakiwa kununua kwa mmiliki halali. Ikumbukwe kwamba Nchi ya Rwanda ni moja ya kati ya Nchi zinauza madini mengi barani Afrika kwa Mataifa ya Ulaya, Marekani na Asia.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·233 مشاهدة
  • Zambia wana Laptop zao zinaitwa NEO, Rwanda wana MARA Phones na Satelite , Uganda wana Simu zao zinaitwa SIMI, Kenya wana Laptop zao zinaitwa TAIFA Wana Starlink pia wana Satelite yao, Tanzania tuna nini ?
    Zambia wana Laptop zao zinaitwa NEO, Rwanda wana MARA Phones na Satelite , Uganda wana Simu zao zinaitwa SIMI, Kenya wana Laptop zao zinaitwa TAIFA Wana Starlink pia wana Satelite yao, Tanzania tuna nini ?
    Like
    Wow
    2
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·538 مشاهدة
  • Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeomba msaada wa kijeshi kutoka Nchini Chad katika jitihada zake za kupambana na Waasi wa kundi la M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda . Waziri anayeshughulikia masuala ya kikanda wa DR Congo alikutana na Rais wa Chad, Mahamat Idriss Deby Itno, Jumanne akimuwakilisha Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi, kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Rais wa Chad na kusasishwa kwenye wa mtandao wa Facebook.

    Maelezo ya kina ya mazungumzo yao hajawekwa wazi. Mmoja wa Maafisa wa Chad anayeyefahamu mazungumzo hayo alisema Chad inalibeba ombi la kuombwa msaada na DR Congo, lakini bado haijafanya maamuzi kuhusu ombi hilo. Chanzo kutoka Ofisi ya Rais DR Congo C kimeiambia BBC kuwa kuwa Nchi hiyo imeomba msaada wa kijeshi na kidiplomasia kutoka Nchini Chad.

    Hata hivyo chanzo hicho ambacho hakijataka kutambulishwa kwa sababu za ndani, hakijatoa maelezo zaidi. Msemaji wa Serikali ya Chad, Gassim Cherif, hakujibu ombi la kutoa maoni yake kuhusu hili, kwa mujibu wa Reuters. Kwa upande wake, Msemaji wa Rais Tshisekedi, Tina Salama, alisema hana taarifa yoyote kuhusu suala hilo.

    Wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad aliiambia Reuters kuwa kupeleka msaada wa kijeshi DR Congo ni "taarifa za tetesi" bado haijathibitishwa rasmi.
    (BBC)

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 imeomba msaada wa kijeshi kutoka Nchini Chad 🇹🇩 katika jitihada zake za kupambana na Waasi wa kundi la M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda 🇷🇼. Waziri anayeshughulikia masuala ya kikanda wa DR Congo alikutana na Rais wa Chad, Mahamat Idriss Deby Itno, Jumanne akimuwakilisha Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi, kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Rais wa Chad na kusasishwa kwenye wa mtandao wa Facebook. Maelezo ya kina ya mazungumzo yao hajawekwa wazi. Mmoja wa Maafisa wa Chad anayeyefahamu mazungumzo hayo alisema Chad inalibeba ombi la kuombwa msaada na DR Congo, lakini bado haijafanya maamuzi kuhusu ombi hilo. Chanzo kutoka Ofisi ya Rais DR Congo C kimeiambia BBC kuwa kuwa Nchi hiyo imeomba msaada wa kijeshi na kidiplomasia kutoka Nchini Chad. Hata hivyo chanzo hicho ambacho hakijataka kutambulishwa kwa sababu za ndani, hakijatoa maelezo zaidi. Msemaji wa Serikali ya Chad, Gassim Cherif, hakujibu ombi la kutoa maoni yake kuhusu hili, kwa mujibu wa Reuters. Kwa upande wake, Msemaji wa Rais Tshisekedi, Tina Salama, alisema hana taarifa yoyote kuhusu suala hilo. Wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad aliiambia Reuters kuwa kupeleka msaada wa kijeshi DR Congo ni "taarifa za tetesi" bado haijathibitishwa rasmi. (BBC)
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·489 مشاهدة
  • Rais wa Rwanda , Paul Kagame ameweka wazi kuwa hana hofu na vitisho vya vikwazo vinavyotolewa na Mataifa ya Magharibi dhidi ya Nchi yake akisisitiza kuwa Rwanda itachukua hatua zozote zinazohitajika kulinda maslahi yake, akizungumza na Gazeti la Jeune Afrique, Kagame amezungumzia kwa kina mzozo kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na shinikizo kutoka Ulaya na Marekani .

    Kagame amesisitiza kuwa hatakubali mashinikizo yanayoelekezwa kwa Rwanda kwa lengo la kuidhoofisha akisema Nchi yake inayo haki ya kujilinda dhidi ya vitisho vyovyote vya nje ambapo Mataifa ya Magharibi yanaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono kundi la Waasi wa M23 wanaopigana mashariki mwa DR Congo jambo ambalo Rwanda imekanusha mara kadhaa.

    Kauli Kagame inakuja wakati mvutano kati ya Rwanda na DR Congo ukiendelea huku mataifa ya Magharibi yakitoa wito wa mazungumzo ya amani lakini licha ya hivyo Rwanda imeendelea kusisitiza kuwa haitakubali kushinikizwa kwa njia yoyote ikibainisha kuwa hatua zake zitalenga kulinda usalama wa Taifa lake kwa gharama yoyote.
    (DW Swahili)

    Rais wa Rwanda 🇷🇼, Paul Kagame ameweka wazi kuwa hana hofu na vitisho vya vikwazo vinavyotolewa na Mataifa ya Magharibi dhidi ya Nchi yake akisisitiza kuwa Rwanda itachukua hatua zozote zinazohitajika kulinda maslahi yake, akizungumza na Gazeti la Jeune Afrique, Kagame amezungumzia kwa kina mzozo kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 pamoja na shinikizo kutoka Ulaya na Marekani 🇺🇸. Kagame amesisitiza kuwa hatakubali mashinikizo yanayoelekezwa kwa Rwanda kwa lengo la kuidhoofisha akisema Nchi yake inayo haki ya kujilinda dhidi ya vitisho vyovyote vya nje ambapo Mataifa ya Magharibi yanaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono kundi la Waasi wa M23 wanaopigana mashariki mwa DR Congo jambo ambalo Rwanda imekanusha mara kadhaa. Kauli Kagame inakuja wakati mvutano kati ya Rwanda na DR Congo ukiendelea huku mataifa ya Magharibi yakitoa wito wa mazungumzo ya amani lakini licha ya hivyo Rwanda imeendelea kusisitiza kuwa haitakubali kushinikizwa kwa njia yoyote ikibainisha kuwa hatua zake zitalenga kulinda usalama wa Taifa lake kwa gharama yoyote. (DW Swahili)
    Love
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·351 مشاهدة
  • Wapiganaji wa kundi la Waasi wa M23 na Askari wanaodhaniwa kuwa ni Rwanda wameendelea kusonga mbele katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo . Hayo ni kwa mujibu wa vyanzo vya eneo hilo pamoja na vya mashirika ya kibinadamu. Miji iliyotekwa ni Ihusi na Kalehe, iliyoko karibu kiliomita sitini (60) kutoka Mji wa Bukavu.

    Katika taarifa, Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeitisha mkutano wa dharura wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutathmini hali hiyo na "kutathmini hali na matokeo ya kitendo hiki kipya cha uchokozi", ikitoa wito wa vikwazo.

    Rais wa Burundi , Evariste Ndayishimiye amesema yeyote atakayeishambulia Nchi yake naye atashambuliwa. Wakati huo huo, Viongozi wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Nchini DR Congo na ule wa Kanisa la Kristo la DR Congo umekutana na kundi la Waasi wa M23 Mjini Goma katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kusaka amani na mazungumzo. Walikutana na kiongozi wa kisiasa wa kundi la M23 Corneille Nangaa.
    (DW Swahili)

    Wapiganaji wa kundi la Waasi wa M23 na Askari wanaodhaniwa kuwa ni Rwanda 🇷🇼 wameendelea kusonga mbele katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Hayo ni kwa mujibu wa vyanzo vya eneo hilo pamoja na vya mashirika ya kibinadamu. Miji iliyotekwa ni Ihusi na Kalehe, iliyoko karibu kiliomita sitini (60) kutoka Mji wa Bukavu. Katika taarifa, Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeitisha mkutano wa dharura wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutathmini hali hiyo na "kutathmini hali na matokeo ya kitendo hiki kipya cha uchokozi", ikitoa wito wa vikwazo. Rais wa Burundi 🇧🇮, Evariste Ndayishimiye amesema yeyote atakayeishambulia Nchi yake naye atashambuliwa. Wakati huo huo, Viongozi wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Nchini DR Congo na ule wa Kanisa la Kristo la DR Congo umekutana na kundi la Waasi wa M23 Mjini Goma katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kusaka amani na mazungumzo. Walikutana na kiongozi wa kisiasa wa kundi la M23 Corneille Nangaa. (DW Swahili)
    Love
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·480 مشاهدة
  • "Unajua hadithi hiyo, sihitaji kuirudia. Tuna
    angalau makubaliano matano na serikali za Congo tangu Mwaka 2007 na hakuna hata mmoja wao ambaye ameheshimu toka DRC. Wanamgambo wa mauaji ya kimbari bado wanaishi Congo. Kuifanya Rwanda kuwa tatizo ni njia ya kuficha tatizo halisi na kuandika upya historia kwa kumbadilisha mhasiriwa kuwa Mnyongaji“

    "Halafu kuna kutokubaliana kwa wazi na udanganyifu kwa upande wa nchi , kama Ubelgiji, ambazo ni sehemu ya historia na tatizo. Serikali ya DRC inaajiri mamluki, kama kila mtu anavyojua.Wanatoka wapi? Kutoka Ulaya. Je, umewahi kusikia kuhusu nchi moja ya Ulaya wanalaumu wale raia wao ambao wanahusika, pamoja na serikali pia. Nani aliwaajiri?Hakuna. Na bado wanaendelea kurudia kwamba kila kitu ni makosa ya Rwanda. ” - Paul Kagame, Rais wa Rwanda kupitia AJ

    "Unajua hadithi hiyo, sihitaji kuirudia. Tuna angalau makubaliano matano na serikali za Congo tangu Mwaka 2007 na hakuna hata mmoja wao ambaye ameheshimu toka DRC. Wanamgambo wa mauaji ya kimbari bado wanaishi Congo. Kuifanya Rwanda kuwa tatizo ni njia ya kuficha tatizo halisi na kuandika upya historia kwa kumbadilisha mhasiriwa kuwa Mnyongaji“ "Halafu kuna kutokubaliana kwa wazi na udanganyifu kwa upande wa nchi , kama Ubelgiji, ambazo ni sehemu ya historia na tatizo. Serikali ya DRC inaajiri mamluki, kama kila mtu anavyojua.Wanatoka wapi? Kutoka Ulaya. Je, umewahi kusikia kuhusu nchi moja ya Ulaya wanalaumu wale raia wao ambao wanahusika, pamoja na serikali pia. Nani aliwaajiri?Hakuna. Na bado wanaendelea kurudia kwamba kila kitu ni makosa ya Rwanda. ” - Paul Kagame, Rais wa Rwanda 🇷🇼 kupitia AJ
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·278 مشاهدة
  • Mahakama ya ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) imeanza kusikiliza shauri la Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo dhidi ya Nchi ya Rwanda , ambalo limefunguliwa kwenye mahakama hiyo iliyoko Jijini Arusha Nchini Tanzania .

    Aidha, DR Congo ilifungua kesi dhidi ya Rwanda, Agosti 21 2023, ikiituhumu Nchi hiyo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu. Kupitia kesi namba 007/2023, DR Congo inadai kuwa Nchi ya Rwanda inahusika na mgogoro unaeondelea Mashariki mwa Nchi hiyo hasa Mkoa wa Sud-Kivu.

    Mahakama ya ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) imeanza kusikiliza shauri la Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 dhidi ya Nchi ya Rwanda 🇷🇼, ambalo limefunguliwa kwenye mahakama hiyo iliyoko Jijini Arusha Nchini Tanzania 🇹🇿. Aidha, DR Congo ilifungua kesi dhidi ya Rwanda, Agosti 21 2023, ikiituhumu Nchi hiyo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu. Kupitia kesi namba 007/2023, DR Congo inadai kuwa Nchi ya Rwanda inahusika na mgogoro unaeondelea Mashariki mwa Nchi hiyo hasa Mkoa wa Sud-Kivu.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·409 مشاهدة
  • Rais wa Nchi ya Rwanda , Paul Kagame ameendelea kukanusha madai kuwa wao kuwa ndiyo chanzo cha mgogoro wa Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kusema kuwa huo ni mgogoro wa ndani ya DR Congo na hautoki nje ya Congo na suluhu lazima itoke kwa Serikali ya Nchi hiyo.

    Ikumbukwe kwamba Rais Paul Kagame alihudhuria mkutano wa Marais wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Febuari 8,2025 uliojadili namna gani ya kurudisha usalama Nchini DR Congo ambapo Waasi wa kundi la M23 wameiteka Mkoa wa Kivu Kaskazini.

    Rais wa Nchi ya Rwanda 🇷🇼, Paul Kagame ameendelea kukanusha madai kuwa wao kuwa ndiyo chanzo cha mgogoro wa Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 kwa kusema kuwa huo ni mgogoro wa ndani ya DR Congo na hautoki nje ya Congo na suluhu lazima itoke kwa Serikali ya Nchi hiyo. Ikumbukwe kwamba Rais Paul Kagame alihudhuria mkutano wa Marais wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Febuari 8,2025 uliojadili namna gani ya kurudisha usalama Nchini DR Congo ambapo Waasi wa kundi la M23 wameiteka Mkoa wa Kivu Kaskazini.
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·262 مشاهدة
الصفحات المعززة