UCHAMBUZI WA FILAMU 📽
THE DA VINCI CODE (2006)
-----‐-----------------------------
Kwa desturi tunapotazama filamu yoyote ile, tunalenga kuziburudisha nafsi zetu.
Sio kazi rahisi mtu akae chini kwa saa moja mpaka mawili amekodolea skrini yake kutazama filamu.
Kila mtu ana machaguo yake binafsi ya filamu anazozipendelea sana. Zipo mpaka zile zinazotisha sana lakini bado zinapendwa.
Filamu ni kama darasa pia. Hutoa mafundisho mengi ambayo yanaweza kuwa na manufaa mema au hata kupotosha pia. Inategemeana na mapokezi ya mtu anayeitazama.
Leo hii nataka kalamu yangu iandike juu ya hii filamu ambayo huenda itaweza kukushawishi wewe msomaji kukubaliana na kile ambacho ubongo wangu umekitafsiri baada ya kuitazama.
`THE DA VINCI CODE`
Kama wewe ni mkristo mwenye imani iliyoota mizizi, nakushauri usiitazame filamu hii kwa kukamia sana.
Maana matukio yaliyomo humo yanaweza kuzua sintofahamu, au hata kukupotosha kutoka kwenye mafundisho ya imani yako. Na waandaaji wa filamu hii hawakukusudia hayo yatokee,
Wao walifanya kwa ajili ya burudani tu. Naam, burudani tu na wala sio kukuondoa kwenye imani yako.
Unajua ni matukio gani hayo yanayoweza kukuchanganya?
Hebu fikiria kuwa leo hii mtu anakueleza kuwa Yesu Kristo alikuwa na mke na baadae akawa baba wa mtoto mmoja.
Sio rahisi kusadiki eeh? Sasa kaa nami hapa ndani, usome niliyokuandalia leo kuihusu hii filamu.
`THE DA VINCI CODE`, ni filamu ambayo chimbuko lake ni kazi ya riwaya iliyoandikwa kwa mkono wa bwana Dan Brown.
Ni hadithi ya kusisimua juu ya siri kubwa iliyokuwa imefichwa kwenye michoro mashuhuri ya yule anayejulikana kama mchoraji bora wa muda wote, Leonardo Da Vinci.
Siri hii ilifichwa kwa muda mrefu sana tangu karne ya kwanza. Na ikalindwa kwa nguvu zote na wanachama wa kikundi cha siri, (secret society) kilichoitwa THE PRIORY OF SION.
Inasemekana kikundi hiki kilitengenezwa na watu wenye uwezo mkubwa sana wa maarifa na akili, Leonardo da Vinci akiikamilisha namba ya kama mmoja wa wanachama wa jumuiya hio ya siri.
Jukumu lao likiwa moja tu kuulindaa ukweli wote juu ya historia na maisha ya halisi ya Yesu Kristo.
Walipambana kuulinda kweli huu ili usiharibiwe na mtu au taasisi yoyote ile..badala yake ujulikane na watu wote duniani.
Ukweli walioulinda dhidi ya uharibifu, ulikuwa ni kwamba Yesu Kristo; licha ya kuwa Mungu-mtu alikuwa pia na mchumba. Yule Maria Magdalene anayejulikana na wengi kama mmoja kati ya wale thenashara.
Hawa walimfahamu kama mchumba na baadaye akawa mke mpenzi wa Yesu Kristo.
Na akamwacha na ujauzito kabla hajauawa pale msalabani.
Kwa maana hio baada ya kifo cha bwana Yesu Kristo, aliacha mtoto wake haoa duniani.
Mtoto akakua akajenga familia na kuendeleza kizazi.
Damu ya kristo ikaendelea kutalii hapa kwenye sayari yetu, kwa vizazi vingi.
Ikawa kwa karne nyingi, ukweli huu unapingwa na taasisi mbalimbali za kidini, na wale wanachama wote wa PRIORY OF SION wanatafutwa kuuawa. Ili tu, wasiwahamishe watu kutoka kwenye mafundisho na imani ambayo imejengwa tayari mioyoni mwao kwa muda mrefu.
Kikaanzishwa kikundi kingine kutoka katika kanisa katoliki kilichoitwa OPUS DEI,
Hiki kilianzishwa maalumu ili kulinda mafundisho ya kanisa katoliki na utamaduni wake wote. Na kikawa tayari kwenda umbali wowote ule kumuangamiza mtu yeyote yule ambaye anataka kuukengeusha umma wa waamini. Hasahasa hawa PRIORY OF SION.
OPUS DEI wakajenga utamaduni wa kuwatafuta watoto wote wenye vinasaba au ukabila wa aina yoyote ile na Yesu Kristo, yaan wale vilembwe na vilembwekeza wakawa wanauawa ili kuuficha ukweli kuwa Kristo aliacha vinasaba vyake hapa duniani kabla hajarudi kwa baba yake mbinguni.
Ndipo filamu yetu ikaanzia hapo,
Ni baada ya kifo cha professa mmoja katika jengo la makumbusho yenye michoro ya kale, michoro ya thamani iliochorwa na Leonardo Da Vinci.
Alikutwa ameuawa kikatili lakini ameacha alama juu ya mwili wake.
Alama ambayo iliwachanganya askari polisi. Wakaamua kuutafuta msaada wa professa Robert Langdon, genius wa kung'amua michoro na alama za kale. Ubongo wake ulimiliki utajiri mkubwa sana wa akili yenye utambuzi wa mafumbo na vitendawili vyote vigumu, kama tu vinahusisha alama.
Robert Langdon alifika eneo la tukio, kitendo tu cha macho yake kutazama ile alama kwenye tumbo la maiti, akagundua kuwa ule ni mchoro wa Da Vinci.
Kwenye kufukua makaburi ya sintofahamu, hapa na pale akiutafuta ukweli nyuma ya kifo cha ajabu cha professa yule, akajikuta amejiingiza kwenye vita kali sana kati ya vikundi viwili hatari vinavyowindana tangu enzi.
Akaugundua ukweli ulioko nyuma ya pazia, kuwa kuna vifo vinavyoendelea na vyote vinawahusisha watu wanaofahamu siri fulani.
Robert Langdon akaingia kazini, kufungua vitabu vyake vya historia ili kugundua kuwa ni code zipi za siri zimefichwa kwenye picha za Leornado Da Vinci.
Akaja kuufahamu ukweli juu ya uhusiano kati ya Maria Magdalene na Kristo, baada ya kuitafsiri ile picha ya *'The last supper'*.
(Nitaweka uchambuzi wa picha hii hapo chini baada ya makala hii )
Na akagundua uhasama wa muda mrefu uliopo kati ya OPUS DEI na PRIORY OF SION.
Akagundua kuwa kuna roho ya mtu inatafutwa ili itolewe na kizazi za Kristo kifutwe hapa duniani.
Ikambidi sasa afanye kazi ya kumtafuta mtu wa mwisho kwenye ukoo wa damu ya Kristo, ambaye ameachwa hapa duniani na amlinde ili asiuawe na wadhalimu.
Filamu hii ni nzuri sana, ina mafunzo mengi sana juu ya ujasusi na historia za kale,
Umakini na utulivu mkubwa unahitajika kichwani mwako ili kuitazama.
Mradi tu uiangalie kwa macho ya kutegemea burudani na sio kuutaka ukweli wa mambo.
Imetoka mwaka 2006...✍️🏻
UCHAMBUZI WA FILAMU 📽🎬