Обновить до Про

WAKALI WA MOVIE 🎬
WAKALI WA MOVIE 🎬

WAKALI WA MOVIE 🎬

Публичная группа 265 участники 322 Записей Movies and Animation
0 предпросмотр

1 ZINGATIA HAYA KABLA YA KUPOST:
1.POST ZA NGONO,KUHUSU NGONO
HAZIRUHUSIWI


2.BILA JINA LA MOVIE POST YAKO
HAITA RUHUSIWA

3.UKITAKA KUTANGAZA
BIASHARA YAKO YOYOTE
WASILIANA NA ADMINI
2 MATAMSHI MACHAFU NA
UDHALILISHAJI:
ZINGATIA KUTOKASHFU
POST YA MTU YOYOTE
AU COMMENT YA MTU
YOYOTE.MAONI YA KILA
MTU YAHESHIMIWE.

  • Jana Usiku nimeteseka sana kupata usingizi na hata baada ya kupata usingizi nimeota ndoto Za ajabu mnoo

    Mpaka nikajuta ni kwanini nimeangalia hii muvi wakuu hii movie inatisha mnoo Tena Sanaa in short ni kwamba kama ww ni muoga usiitazame hii sitaki lawama

    Uzuri ni kwamba umeshapewa onyo asanteni
    Jana Usiku nimeteseka sana kupata usingizi na hata baada ya kupata usingizi nimeota ndoto Za ajabu mnoo Mpaka nikajuta ni kwanini nimeangalia hii muvi wakuu hii movie inatisha mnoo Tena Sanaa in short ni kwamba kama ww ni muoga usiitazame hii sitaki lawama Uzuri ni kwamba umeshapewa onyo asanteni
    Like
    Love
    2
    ·13 Просмотры
  • Like
    Love
    2
    ·13 Просмотры
  • Like
    3
    1 Комментарии ·13 Просмотры
  • Like
    Love
    3
    ·13 Просмотры
  • Like
    3
    ·13 Просмотры
  • UCHAMBUZI WA FILAMU 📽
    THE DA VINCI CODE (2006)

    -----‐-----------------------------

    Kwa desturi tunapotazama filamu yoyote ile, tunalenga kuziburudisha nafsi zetu.
    Sio kazi rahisi mtu akae chini kwa saa moja mpaka mawili amekodolea skrini yake kutazama filamu.
    Kila mtu ana machaguo yake binafsi ya filamu anazozipendelea sana. Zipo mpaka zile zinazotisha sana lakini bado zinapendwa.

    Filamu ni kama darasa pia. Hutoa mafundisho mengi ambayo yanaweza kuwa na manufaa mema au hata kupotosha pia. Inategemeana na mapokezi ya mtu anayeitazama.

    Leo hii nataka kalamu yangu iandike juu ya hii filamu ambayo huenda itaweza kukushawishi wewe msomaji kukubaliana na kile ambacho ubongo wangu umekitafsiri baada ya kuitazama.

    `THE DA VINCI CODE`

    Kama wewe ni mkristo mwenye imani iliyoota mizizi, nakushauri usiitazame filamu hii kwa kukamia sana.
    Maana matukio yaliyomo humo yanaweza kuzua sintofahamu, au hata kukupotosha kutoka kwenye mafundisho ya imani yako. Na waandaaji wa filamu hii hawakukusudia hayo yatokee,
    Wao walifanya kwa ajili ya burudani tu. Naam, burudani tu na wala sio kukuondoa kwenye imani yako.
    Unajua ni matukio gani hayo yanayoweza kukuchanganya?

    Hebu fikiria kuwa leo hii mtu anakueleza kuwa Yesu Kristo alikuwa na mke na baadae akawa baba wa mtoto mmoja.
    Sio rahisi kusadiki eeh? Sasa kaa nami hapa ndani, usome niliyokuandalia leo kuihusu hii filamu.

    `THE DA VINCI CODE`, ni filamu ambayo chimbuko lake ni kazi ya riwaya iliyoandikwa kwa mkono wa bwana Dan Brown.

    Ni hadithi ya kusisimua juu ya siri kubwa iliyokuwa imefichwa kwenye michoro mashuhuri ya yule anayejulikana kama mchoraji bora wa muda wote, Leonardo Da Vinci.
    Siri hii ilifichwa kwa muda mrefu sana tangu karne ya kwanza. Na ikalindwa kwa nguvu zote na wanachama wa kikundi cha siri, (secret society) kilichoitwa THE PRIORY OF SION.
    Inasemekana kikundi hiki kilitengenezwa na watu wenye uwezo mkubwa sana wa maarifa na akili, Leonardo da Vinci akiikamilisha namba ya kama mmoja wa wanachama wa jumuiya hio ya siri.
    Jukumu lao likiwa moja tu kuulindaa ukweli wote juu ya historia na maisha ya halisi ya Yesu Kristo.
    Walipambana kuulinda kweli huu ili usiharibiwe na mtu au taasisi yoyote ile..badala yake ujulikane na watu wote duniani.

    Ukweli walioulinda dhidi ya uharibifu, ulikuwa ni kwamba Yesu Kristo; licha ya kuwa Mungu-mtu alikuwa pia na mchumba. Yule Maria Magdalene anayejulikana na wengi kama mmoja kati ya wale thenashara.
    Hawa walimfahamu kama mchumba na baadaye akawa mke mpenzi wa Yesu Kristo.
    Na akamwacha na ujauzito kabla hajauawa pale msalabani.

    Kwa maana hio baada ya kifo cha bwana Yesu Kristo, aliacha mtoto wake haoa duniani.
    Mtoto akakua akajenga familia na kuendeleza kizazi.
    Damu ya kristo ikaendelea kutalii hapa kwenye sayari yetu, kwa vizazi vingi.

    Ikawa kwa karne nyingi, ukweli huu unapingwa na taasisi mbalimbali za kidini, na wale wanachama wote wa PRIORY OF SION wanatafutwa kuuawa. Ili tu, wasiwahamishe watu kutoka kwenye mafundisho na imani ambayo imejengwa tayari mioyoni mwao kwa muda mrefu.

    Kikaanzishwa kikundi kingine kutoka katika kanisa katoliki kilichoitwa OPUS DEI,
    Hiki kilianzishwa maalumu ili kulinda mafundisho ya kanisa katoliki na utamaduni wake wote. Na kikawa tayari kwenda umbali wowote ule kumuangamiza mtu yeyote yule ambaye anataka kuukengeusha umma wa waamini. Hasahasa hawa PRIORY OF SION.

    OPUS DEI wakajenga utamaduni wa kuwatafuta watoto wote wenye vinasaba au ukabila wa aina yoyote ile na Yesu Kristo, yaan wale vilembwe na vilembwekeza wakawa wanauawa ili kuuficha ukweli kuwa Kristo aliacha vinasaba vyake hapa duniani kabla hajarudi kwa baba yake mbinguni.

    Ndipo filamu yetu ikaanzia hapo,
    Ni baada ya kifo cha professa mmoja katika jengo la makumbusho yenye michoro ya kale, michoro ya thamani iliochorwa na Leonardo Da Vinci.
    Alikutwa ameuawa kikatili lakini ameacha alama juu ya mwili wake.

    Alama ambayo iliwachanganya askari polisi. Wakaamua kuutafuta msaada wa professa Robert Langdon, genius wa kung'amua michoro na alama za kale. Ubongo wake ulimiliki utajiri mkubwa sana wa akili yenye utambuzi wa mafumbo na vitendawili vyote vigumu, kama tu vinahusisha alama.

    Robert Langdon alifika eneo la tukio, kitendo tu cha macho yake kutazama ile alama kwenye tumbo la maiti, akagundua kuwa ule ni mchoro wa Da Vinci.

    Kwenye kufukua makaburi ya sintofahamu, hapa na pale akiutafuta ukweli nyuma ya kifo cha ajabu cha professa yule, akajikuta amejiingiza kwenye vita kali sana kati ya vikundi viwili hatari vinavyowindana tangu enzi.
    Akaugundua ukweli ulioko nyuma ya pazia, kuwa kuna vifo vinavyoendelea na vyote vinawahusisha watu wanaofahamu siri fulani.

    Robert Langdon akaingia kazini, kufungua vitabu vyake vya historia ili kugundua kuwa ni code zipi za siri zimefichwa kwenye picha za Leornado Da Vinci.
    Akaja kuufahamu ukweli juu ya uhusiano kati ya Maria Magdalene na Kristo, baada ya kuitafsiri ile picha ya *'The last supper'*.

    (Nitaweka uchambuzi wa picha hii hapo chini baada ya makala hii )

    Na akagundua uhasama wa muda mrefu uliopo kati ya OPUS DEI na PRIORY OF SION.
    Akagundua kuwa kuna roho ya mtu inatafutwa ili itolewe na kizazi za Kristo kifutwe hapa duniani.

    Ikambidi sasa afanye kazi ya kumtafuta mtu wa mwisho kwenye ukoo wa damu ya Kristo, ambaye ameachwa hapa duniani na amlinde ili asiuawe na wadhalimu.

    Filamu hii ni nzuri sana, ina mafunzo mengi sana juu ya ujasusi na historia za kale,
    Umakini na utulivu mkubwa unahitajika kichwani mwako ili kuitazama.
    Mradi tu uiangalie kwa macho ya kutegemea burudani na sio kuutaka ukweli wa mambo.

    Imetoka mwaka 2006...✍️🏻
    UCHAMBUZI WA FILAMU 📽🎬 THE DA VINCI CODE (2006) -----‐----------------------------- Kwa desturi tunapotazama filamu yoyote ile, tunalenga kuziburudisha nafsi zetu. Sio kazi rahisi mtu akae chini kwa saa moja mpaka mawili amekodolea skrini yake kutazama filamu. Kila mtu ana machaguo yake binafsi ya filamu anazozipendelea sana. Zipo mpaka zile zinazotisha sana lakini bado zinapendwa. Filamu ni kama darasa pia. Hutoa mafundisho mengi ambayo yanaweza kuwa na manufaa mema au hata kupotosha pia. Inategemeana na mapokezi ya mtu anayeitazama. Leo hii nataka kalamu yangu iandike juu ya hii filamu ambayo huenda itaweza kukushawishi wewe msomaji kukubaliana na kile ambacho ubongo wangu umekitafsiri baada ya kuitazama. `THE DA VINCI CODE` Kama wewe ni mkristo mwenye imani iliyoota mizizi, nakushauri usiitazame filamu hii kwa kukamia sana. Maana matukio yaliyomo humo yanaweza kuzua sintofahamu, au hata kukupotosha kutoka kwenye mafundisho ya imani yako. Na waandaaji wa filamu hii hawakukusudia hayo yatokee, Wao walifanya kwa ajili ya burudani tu. Naam, burudani tu na wala sio kukuondoa kwenye imani yako. Unajua ni matukio gani hayo yanayoweza kukuchanganya? Hebu fikiria kuwa leo hii mtu anakueleza kuwa Yesu Kristo alikuwa na mke na baadae akawa baba wa mtoto mmoja. Sio rahisi kusadiki eeh? Sasa kaa nami hapa ndani, usome niliyokuandalia leo kuihusu hii filamu. `THE DA VINCI CODE`, ni filamu ambayo chimbuko lake ni kazi ya riwaya iliyoandikwa kwa mkono wa bwana Dan Brown. Ni hadithi ya kusisimua juu ya siri kubwa iliyokuwa imefichwa kwenye michoro mashuhuri ya yule anayejulikana kama mchoraji bora wa muda wote, Leonardo Da Vinci. Siri hii ilifichwa kwa muda mrefu sana tangu karne ya kwanza. Na ikalindwa kwa nguvu zote na wanachama wa kikundi cha siri, (secret society) kilichoitwa THE PRIORY OF SION. Inasemekana kikundi hiki kilitengenezwa na watu wenye uwezo mkubwa sana wa maarifa na akili, Leonardo da Vinci akiikamilisha namba ya kama mmoja wa wanachama wa jumuiya hio ya siri. Jukumu lao likiwa moja tu kuulindaa ukweli wote juu ya historia na maisha ya halisi ya Yesu Kristo. Walipambana kuulinda kweli huu ili usiharibiwe na mtu au taasisi yoyote ile..badala yake ujulikane na watu wote duniani. Ukweli walioulinda dhidi ya uharibifu, ulikuwa ni kwamba Yesu Kristo; licha ya kuwa Mungu-mtu alikuwa pia na mchumba. Yule Maria Magdalene anayejulikana na wengi kama mmoja kati ya wale thenashara. Hawa walimfahamu kama mchumba na baadaye akawa mke mpenzi wa Yesu Kristo. Na akamwacha na ujauzito kabla hajauawa pale msalabani. Kwa maana hio baada ya kifo cha bwana Yesu Kristo, aliacha mtoto wake haoa duniani. Mtoto akakua akajenga familia na kuendeleza kizazi. Damu ya kristo ikaendelea kutalii hapa kwenye sayari yetu, kwa vizazi vingi. Ikawa kwa karne nyingi, ukweli huu unapingwa na taasisi mbalimbali za kidini, na wale wanachama wote wa PRIORY OF SION wanatafutwa kuuawa. Ili tu, wasiwahamishe watu kutoka kwenye mafundisho na imani ambayo imejengwa tayari mioyoni mwao kwa muda mrefu. Kikaanzishwa kikundi kingine kutoka katika kanisa katoliki kilichoitwa OPUS DEI, Hiki kilianzishwa maalumu ili kulinda mafundisho ya kanisa katoliki na utamaduni wake wote. Na kikawa tayari kwenda umbali wowote ule kumuangamiza mtu yeyote yule ambaye anataka kuukengeusha umma wa waamini. Hasahasa hawa PRIORY OF SION. OPUS DEI wakajenga utamaduni wa kuwatafuta watoto wote wenye vinasaba au ukabila wa aina yoyote ile na Yesu Kristo, yaan wale vilembwe na vilembwekeza wakawa wanauawa ili kuuficha ukweli kuwa Kristo aliacha vinasaba vyake hapa duniani kabla hajarudi kwa baba yake mbinguni. Ndipo filamu yetu ikaanzia hapo, Ni baada ya kifo cha professa mmoja katika jengo la makumbusho yenye michoro ya kale, michoro ya thamani iliochorwa na Leonardo Da Vinci. Alikutwa ameuawa kikatili lakini ameacha alama juu ya mwili wake. Alama ambayo iliwachanganya askari polisi. Wakaamua kuutafuta msaada wa professa Robert Langdon, genius wa kung'amua michoro na alama za kale. Ubongo wake ulimiliki utajiri mkubwa sana wa akili yenye utambuzi wa mafumbo na vitendawili vyote vigumu, kama tu vinahusisha alama. Robert Langdon alifika eneo la tukio, kitendo tu cha macho yake kutazama ile alama kwenye tumbo la maiti, akagundua kuwa ule ni mchoro wa Da Vinci. Kwenye kufukua makaburi ya sintofahamu, hapa na pale akiutafuta ukweli nyuma ya kifo cha ajabu cha professa yule, akajikuta amejiingiza kwenye vita kali sana kati ya vikundi viwili hatari vinavyowindana tangu enzi. Akaugundua ukweli ulioko nyuma ya pazia, kuwa kuna vifo vinavyoendelea na vyote vinawahusisha watu wanaofahamu siri fulani. Robert Langdon akaingia kazini, kufungua vitabu vyake vya historia ili kugundua kuwa ni code zipi za siri zimefichwa kwenye picha za Leornado Da Vinci. Akaja kuufahamu ukweli juu ya uhusiano kati ya Maria Magdalene na Kristo, baada ya kuitafsiri ile picha ya *'The last supper'*. (Nitaweka uchambuzi wa picha hii hapo chini baada ya makala hii ) Na akagundua uhasama wa muda mrefu uliopo kati ya OPUS DEI na PRIORY OF SION. Akagundua kuwa kuna roho ya mtu inatafutwa ili itolewe na kizazi za Kristo kifutwe hapa duniani. Ikambidi sasa afanye kazi ya kumtafuta mtu wa mwisho kwenye ukoo wa damu ya Kristo, ambaye ameachwa hapa duniani na amlinde ili asiuawe na wadhalimu. Filamu hii ni nzuri sana, ina mafunzo mengi sana juu ya ujasusi na historia za kale, Umakini na utulivu mkubwa unahitajika kichwani mwako ili kuitazama. Mradi tu uiangalie kwa macho ya kutegemea burudani na sio kuutaka ukweli wa mambo. Imetoka mwaka 2006...✍️🏻
    Like
    Love
    3
    ·13 Просмотры
  • Like
    Love
    3
    ·12 Просмотры
  • Kama shule yako ina mashaka mashaka!!!!
    Ukiangalia hii movie utaishia kulaumu watu tu
    Kama shule yako ina mashaka mashaka!!!! Ukiangalia hii movie utaishia kulaumu watu tu😂😂
    Like
    Love
    3
    ·12 Просмотры
  • Is back
    TONY JAA
    NAONA ANATAKA KUFUNGA MWAKA UMU KUNA MKONO BALAA AFU ACTION YAKE IMEPANGILIWA SOUND YA KIBABE SANA
    Nazani mapkezi yataakuwa makubwa
    Is back TONY JAA NAONA ANATAKA KUFUNGA MWAKA UMU KUNA MKONO BALAA AFU ACTION YAKE IMEPANGILIWA SOUND YA KIBABE SANA Nazani mapkezi yataakuwa makubwa
    Like
    Love
    3
    ·12 Просмотры
  • Ukiongelea movie Kali ya ki..zombi..
    Hii mi naipa namba(1) movie gani ya kizombi...unaikubali...tukutane kwenye comment....
    Ukiongelea movie Kali ya ki..zombi.. Hii mi naipa namba(1) movie gani ya kizombi...unaikubali...tukutane kwenye comment👇....
    Like
    Love
    3
    1 Комментарии ·12 Просмотры
  • Like
    Love
    2
    ·12 Просмотры
  • Tuishi na hii

    Kifupi story ni kwamba mwamba aitwae Solomon alikua mpiga panga Hodari , kapigana vita nyingi sana na amechinja sana .
    Baadae aliamua kubadilisha maisha na kuwa mtu mwema baada Ya kukutana na mfalme wa kichawi aliyemwambia , kwamba yeye ni wa Motoni kutokana na uovu mwingi alioufanya .
    Aliamua kuwa mwema kujisafisha lakini shida ss uja pale Yule mchawi anapotaka kutawala , anachinja watu na kuamulisha wawe wafuasi wake .
    Jamaa anaamua tena kushika panga ili kufyeka mchawi na wafuasi wake wote wenye kazi yao Ya kishetani

    Enjoy
    Tuishi na hii 👇 Kifupi story ni kwamba mwamba aitwae Solomon alikua mpiga panga Hodari , kapigana vita nyingi sana na amechinja sana . Baadae aliamua kubadilisha maisha na kuwa mtu mwema baada Ya kukutana na mfalme wa kichawi aliyemwambia , kwamba yeye ni wa Motoni kutokana na uovu mwingi alioufanya . Aliamua kuwa mwema kujisafisha lakini shida ss uja pale Yule mchawi anapotaka kutawala , anachinja watu na kuamulisha wawe wafuasi wake . Jamaa anaamua tena kushika panga ili kufyeka mchawi na wafuasi wake wote wenye kazi yao Ya kishetani Enjoy 🙏
    Like
    2
    ·12 Просмотры
  • THE EXORCISM YA MWAKA (2024)
    KAMA UJAICHEK UNASUBILI NIN
    Plot: Walikuwa wanatengeneza sinema iliyolaaniwa. Walionywa wasifanye hivyo. Walipaswa kusikiliza. mwigizaji mwenye matatizo anaanza kufunguka huku akipiga filamu ya kutisha isiyo ya kawaida, na kumfanya binti yake aliyeachana naye kujiuliza ikiwa anarudi kwenye uraibu wake wa zamani au ikiwa kuna kitu kibaya zaidi kinachochezwa.

    GENRE: HORROR, TRILLER
    THE EXORCISM YA MWAKA (2024) KAMA UJAICHEK UNASUBILI NIN Plot: Walikuwa wanatengeneza sinema iliyolaaniwa. Walionywa wasifanye hivyo. Walipaswa kusikiliza. mwigizaji mwenye matatizo anaanza kufunguka huku akipiga filamu ya kutisha isiyo ya kawaida, na kumfanya binti yake aliyeachana naye kujiuliza ikiwa anarudi kwenye uraibu wake wa zamani au ikiwa kuna kitu kibaya zaidi kinachochezwa. GENRE: HORROR, TRILLER
    Like
    Love
    2
    ·12 Просмотры
  • Series inakwenda Kwa jina la The Midwich Cuckoos imetoka 2022.
    Inahusu Kijiji kidogo nchini England ambapo wanawake wa Kijiji icho bila kutegemea wanapata ujauzito wa kushangaza baada ya tukio la kushangaza linalosababisha Kijiji kupoteza fahamu Kwa muda.
    Shida inakuja Kwa hao watoto watakaozaliwa kisanga ndo kipo apo,,,,mzigo una episode 7 wale wapenzi wa series za kufikirisha hii itawafaa sana
    Series inakwenda Kwa jina la The Midwich Cuckoos imetoka 2022. Inahusu Kijiji kidogo nchini England ambapo wanawake wa Kijiji icho bila kutegemea wanapata ujauzito wa kushangaza baada ya tukio la kushangaza linalosababisha Kijiji kupoteza fahamu Kwa muda. Shida inakuja Kwa hao watoto watakaozaliwa💯🔥 kisanga ndo kipo apo,,,,mzigo una episode 7 wale wapenzi wa series za kufikirisha hii itawafaa sana
    Like
    Love
    2
    ·12 Просмотры
  • HEART ROBOTS YA MWAKA(2024)
    NDANI KUNA MACHETE UMO

    PLOT: Miaka kadhaa baada ya apocalypse ya roboti, Terra anajitosa kutoka kwa eneo lake lililojitenga ili kumchukua roboti mwenzake anayependwa Magharibi ili kuokoa ulimwengu uliobaki.

    GENRE: ACTION, ADVENTURE
    HEART ROBOTS YA MWAKA(2024) NDANI KUNA MACHETE UMO😁🍿🍿 PLOT: Miaka kadhaa baada ya apocalypse ya roboti, Terra anajitosa kutoka kwa eneo lake lililojitenga ili kumchukua roboti mwenzake anayependwa Magharibi ili kuokoa ulimwengu uliobaki. GENRE: ACTION, ADVENTURE
    Like
    Love
    2
    ·12 Просмотры
  • Hii movie ya Azrael kiukweli sijaelewa kabisa. Naona tu watu hawaongei. Na kule mwisho yule dada sterling kajikuta anarithi mtoto wa kishetani. Sa sijui nimeiangalia mara 2 sielewi. Ama kwa nikaangalie Wikipedia
    Hii movie ya Azrael kiukweli sijaelewa kabisa. Naona tu watu hawaongei. Na kule mwisho yule dada sterling kajikuta anarithi mtoto wa kishetani. Sa sijui nimeiangalia mara 2 sielewi. Ama kwa nikaangalie Wikipedia 🥲
    Like
    1
    ·12 Просмотры
  • ALIEN: ROMULUS YA (2024)

    NJAMA: Wakati wa kupekua ncha za kina za kituo cha anga cha mbali, kikundi cha wakoloni wachanga wa anga wanakutana ana kwa ana na aina ya maisha ya kutisha zaidi katika ulimwengu.

    AINA: VITENDO, VYA KUTISHA, SCI-FI, THRILLER...
    ALIEN: ROMULUS YA (2024) NJAMA: Wakati wa kupekua ncha za kina za kituo cha anga cha mbali, kikundi cha wakoloni wachanga wa anga wanakutana ana kwa ana na aina ya maisha ya kutisha zaidi katika ulimwengu. AINA: VITENDO, VYA KUTISHA, SCI-FI, THRILLER...
    Like
    Love
    2
    ·12 Просмотры
  • THE WILD ROBOT YA (2024)
    KWA WALE WANAO PENDA KATUNI HI IMEKAA POA...MWANADADA MKENYA
    (Lupita Nyong'o) NDIO SAUTI YA ROBOTI

    NJAMA: Baada ya ajali ya meli, roboti yenye akili iitwayo Roz imekwama kwenye kisiwa kisicho na watu. Ili kustahimili mazingira magumu, Roz hufungamana na wanyama wa kisiwa hicho na kumtunza mtoto ambaye ni yatima.

    AINA: UHUISHAJI, FAMILIA, SCI-F
    THE WILD ROBOT YA (2024) KWA WALE WANAO PENDA KATUNI HI IMEKAA POA...MWANADADA MKENYA (Lupita Nyong'o) NDIO SAUTI YA ROBOTI NJAMA: Baada ya ajali ya meli, roboti yenye akili iitwayo Roz imekwama kwenye kisiwa kisicho na watu. Ili kustahimili mazingira magumu, Roz hufungamana na wanyama wa kisiwa hicho na kumtunza mtoto ambaye ni yatima. AINA: UHUISHAJI, FAMILIA, SCI-F
    Like
    1
    ·12 Просмотры
  • Like
    2
    1 Комментарии ·47 Просмотры
  • Kazi ya mazombie ya wakorea , inaitwa ALIVE

    Story inamuhusu mwamba mmoja mcheza game za online , ambaye mwenyewe kutwa nzima anashinda ndani anacheza game tu ktk apartment ya wazazi wake .
    Ukatokea mlipuko wa mazombie wakati yeye akiwa ndani na kushuhudia yote yaliyotokea nje , kwa uwoga akaamua kubaki humo ndani kajifungia akiendelea kucheza game , akiamini atasurvive kwa mtindo huo .
    Shida ss binadamu anahitaji maji na chakula kuweza kuishi , kwa hiyo kwa namna yoyote ile kama anataka kuendelea kuishi lazima atoke nje .

    Uzuri anagundua gorofa ya pili kuna mtu mwingine pia aliyesurvive , anaanza kuwasiliana na mtu huyo na kuona kama kuna namna wanaweza kukutana , wakawa pamoja kuweza kujiokoa ktk mazingira hayo hatari .
    Shida ss ni kuweza kutoka nje kupata chakula , pili kuweza kukutana na huyo survivor mwingine lakini tatu pia ni kuweza kuokoka mazingira hayo yenye mazombie wenye njaa kali waliotapakaa kote .

    Enjoy
    Kazi ya mazombie ya wakorea , inaitwa ALIVE Story inamuhusu mwamba mmoja mcheza game za online , ambaye mwenyewe kutwa nzima anashinda ndani anacheza game tu ktk apartment ya wazazi wake . Ukatokea mlipuko wa mazombie wakati yeye akiwa ndani na kushuhudia yote yaliyotokea nje , kwa uwoga akaamua kubaki humo ndani kajifungia akiendelea kucheza game , akiamini atasurvive kwa mtindo huo . Shida ss binadamu anahitaji maji na chakula kuweza kuishi , kwa hiyo kwa namna yoyote ile kama anataka kuendelea kuishi lazima atoke nje . Uzuri anagundua gorofa ya pili kuna mtu mwingine pia aliyesurvive , anaanza kuwasiliana na mtu huyo na kuona kama kuna namna wanaweza kukutana , wakawa pamoja kuweza kujiokoa ktk mazingira hayo hatari . Shida ss ni kuweza kutoka nje kupata chakula , pili kuweza kukutana na huyo survivor mwingine lakini tatu pia ni kuweza kuokoka mazingira hayo yenye mazombie wenye njaa kali waliotapakaa kote . Enjoy 🙏
    ·48 Просмотры
  • Wazee wa horror

    Story ni kwamba truth or dare ni mchezo wa kuchagua , ambapo ukichagua truth utatakiwa kusema ukweli wako wa maisha ambao hujawahi kuusema mfano labda ulibaka/ulibakwa/uliiba/ulienda kwa mganga n.k , lakini ukichagua "dare" bas unayecheza nae huo mchezo anakuamulisha ufanye jambo ambalo linaweza kuwa gumu mfano utembee uchi , utupe simu yako n.k

    Tukirudi ktk muvi yetu hii ni kwamba kulikua na vijana marafiki , walienda mexico kula bata ambako huko wakajikuta wanarudi na laana ya mapepo inayotishia uhai wa maisha yao .
    Walipokua huko kuna kijana mmoja walimkuta huko , kijana huyo aliwachukua na kuwapeleka sehemu moja kucheza huo mchezo wa truth or dare .
    Kumbe kijana huyo aliwapeleka makusudi eneo lenye hiyo laana kusudi na yeye akatoe hiyo laana maana na yeye aliucheza huo mchezo , na ili kutoa laana lazima awachezeshe wengine .
    Hao vijana bila kujua wakacheza ktk hilo eneo , lakini kumbe wanaweka maagano na hayo mapepo wa huo mchezo .

    Shida ss wamerudi nchini kwao , mapepo yanaanza kuwaletea huo mchezo kupitia watu ambapo hatari yake inafikia steji ya wao kujidhalilisha maana truth inawafanya waseme ukweli wao wa maisha , lakini pia kuhatarisha maisha maana dare inawafanya wafanye mambo ya hatari kwa uhai wao .

    Enjoy
    Wazee wa horror 👇 Story ni kwamba truth or dare ni mchezo wa kuchagua , ambapo ukichagua truth utatakiwa kusema ukweli wako wa maisha ambao hujawahi kuusema mfano labda ulibaka/ulibakwa/uliiba/ulienda kwa mganga n.k , lakini ukichagua "dare" bas unayecheza nae huo mchezo anakuamulisha ufanye jambo ambalo linaweza kuwa gumu mfano utembee uchi , utupe simu yako n.k Tukirudi ktk muvi yetu hii 👇ni kwamba kulikua na vijana marafiki , walienda mexico kula bata ambako huko wakajikuta wanarudi na laana ya mapepo inayotishia uhai wa maisha yao . Walipokua huko kuna kijana mmoja walimkuta huko , kijana huyo aliwachukua na kuwapeleka sehemu moja kucheza huo mchezo wa truth or dare . Kumbe kijana huyo aliwapeleka makusudi eneo lenye hiyo laana kusudi na yeye akatoe hiyo laana maana na yeye aliucheza huo mchezo , na ili kutoa laana lazima awachezeshe wengine . Hao vijana bila kujua wakacheza ktk hilo eneo , lakini kumbe wanaweka maagano na hayo mapepo wa huo mchezo . Shida ss wamerudi nchini kwao , mapepo yanaanza kuwaletea huo mchezo kupitia watu ambapo hatari yake inafikia steji ya wao kujidhalilisha maana truth inawafanya waseme ukweli wao wa maisha , lakini pia kuhatarisha maisha maana dare inawafanya wafanye mambo ya hatari kwa uhai wao . Enjoy 🙏
    ·46 Просмотры
  • Kama hujatazama hii movie na unauchungu na bando lako Wala usijisumbue kuitafuta maskini bando langu

    Na hivi starling wa awamu hii ni mwanamke,nikajua kabisa kwisha habari yetu,mzigo tumeusubiri kwa hamu kuanzia 2019 halafu wanatuletea matango pori

    Baada ya quiet place day one hii pia ni muvi mbovu ndani ya mwaka huu ambayo ukimaliza kuitazama unaifuta hapo hapo huku unasonya na kutukana matusi kimya kimya
    👉Kama hujatazama hii movie na unauchungu na bando lako Wala usijisumbue kuitafuta 🥺 maskini bando langu 😭 Na hivi starling wa awamu hii ni mwanamke,nikajua kabisa kwisha habari yetu,mzigo tumeusubiri kwa hamu kuanzia 2019 halafu wanatuletea matango pori Baada ya quiet place day one hii pia ni muvi mbovu ndani ya mwaka huu ambayo ukimaliza kuitazama unaifuta hapo hapo huku unasonya na kutukana matusi kimya kimya✍️
    ·45 Просмотры
  • Kuna hili tambara apa awo machalii ni ma supernatural
    #GIFTED
    HALIUMIZI KICHWA ANGALIA ATA UKIWA UMELEWA KALI SANA
    Kuna hili tambara apa awo machalii ni ma supernatural #GIFTED HALIUMIZI KICHWA ANGALIA ATA UKIWA UMELEWA KALI SANA🔥🔥🔥🔥🔥🔥
    ·35 Просмотры
  • ·45 Просмотры
  • Love
    1
    ·45 Просмотры
Больше