• #PART5

    Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite.

    Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo.

    Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba.

    Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay.

    April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha.

    March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.

    Kumekua na jitihada mbalimbali za kumaliza mgogoro wa DRC kwa njia za kidiplomasia ikiwemo mkutano wa viongozi wakuu wa SADC na EAC uliofanyika leo jijini Dar.

    #MyaTake:
    1. Congo imeponzwa na ukarimu wake. Wakati wa vita vya Rwanda, Congo ilipokea Watutsi wengi na kuwapa hifadhi, akiwemo Kagame. Baada ya utawala wa Habyarimana kuangushwa Wahutu nao wakakimbilia Congo na kupewa hifadhi. Sasa hicho kimekua kigezo cha Rwanda kuingiza majeshi Congo kila mara kwa madai ya kuwatafuta Wahutu wa FDLR. Kwa lugha rahisi vita ya ndugu wawili (Wahutu na Watutsi) iliyopaswa kupiganwa Rwanda sasa inapiganwa Congo.

    2. Congo inateswa na mipaka ya kikoloni. Laiti wakati wa kuchora mipaka jamii yote ya Watutsi ingewekwa Rwanda, leo kusingekuwa na Banyamulenge Congo, kwahiyo Watutsi wasingepata sababu ya kuishi Congo na kujifanya raia. Ni sawa na kukuta Wamasai 1,000 pale Longido, halafu uambiwe kati yao wapo wa Kenya. Utawajuaje? Utawatofautishaje?

    3. Congo inateswa na rasilimali zake. Kama eneo la Kivu lisingekuwa na utajiri, mgogoro usingekuwa mkubwa kama ulivyo. Rejea #Part1 kujua utajiri uliopo Kivu. Kumbuka bila Kivu dunia haina laptop wala smartphones kwa sababu 80% ya coltan yote duniani inatoka Kivu.

    4. Rwanda na Uganda ni Keyplayers kwenye mgogoro wa Congo. Kwa miaka mingi majeshi yao yameigeuza Congo shamba la bibi. Waondoe majeshi yao Congo.

    5. Viongozi wengi wa M23 ni Wanyarwanda. Huu ni udhibitisho kuwa Rwanda ni kinara kwenye mgogoro huu.

    6. Congo ni kubwa sana na hivyo inakosa jeshi imara la kutosha kulinda mipaka yake yote. Congo ni kubwa mara 90 ya Rwanda. Wapo wanaoshauri igawanywe kama njia ya kutatua mgogoro. Kama ambavyo Yugoslavia iligawanywa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

    7. Kiongozi wa sasa wa M23 Corneille Nangaa alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi 2019 na ndiye aliyemtangaza Tshisekedi kuwa Rais kwa ushindi wa 38%. Lakini alilaumiwa kupunguza kura za Martin Fayulu aliyepata 34%. Huenda kuna ahadi alipewa haikutimizwa ndio maana akaungana na Waasi.

    Sababu hizo hapo juu zikifanyiwa kazi, mgogoro wa Congo unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Mnaopenda kujifunza zaidi, naandika Kitabu. Get ready to have your copy. MWISHO.!

    (Malisa GJ )

    #PART5 Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite. Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo. Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba. Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay. April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha. March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa. Kumekua na jitihada mbalimbali za kumaliza mgogoro wa DRC kwa njia za kidiplomasia ikiwemo mkutano wa viongozi wakuu wa SADC na EAC uliofanyika leo jijini Dar. #MyaTake: 1. Congo imeponzwa na ukarimu wake. Wakati wa vita vya Rwanda, Congo ilipokea Watutsi wengi na kuwapa hifadhi, akiwemo Kagame. Baada ya utawala wa Habyarimana kuangushwa Wahutu nao wakakimbilia Congo na kupewa hifadhi. Sasa hicho kimekua kigezo cha Rwanda kuingiza majeshi Congo kila mara kwa madai ya kuwatafuta Wahutu wa FDLR. Kwa lugha rahisi vita ya ndugu wawili (Wahutu na Watutsi) iliyopaswa kupiganwa Rwanda sasa inapiganwa Congo. 2. Congo inateswa na mipaka ya kikoloni. Laiti wakati wa kuchora mipaka jamii yote ya Watutsi ingewekwa Rwanda, leo kusingekuwa na Banyamulenge Congo, kwahiyo Watutsi wasingepata sababu ya kuishi Congo na kujifanya raia. Ni sawa na kukuta Wamasai 1,000 pale Longido, halafu uambiwe kati yao wapo wa Kenya. Utawajuaje? Utawatofautishaje? 3. Congo inateswa na rasilimali zake. Kama eneo la Kivu lisingekuwa na utajiri, mgogoro usingekuwa mkubwa kama ulivyo. Rejea #Part1 kujua utajiri uliopo Kivu. Kumbuka bila Kivu dunia haina laptop wala smartphones kwa sababu 80% ya coltan yote duniani inatoka Kivu. 4. Rwanda na Uganda ni Keyplayers kwenye mgogoro wa Congo. Kwa miaka mingi majeshi yao yameigeuza Congo shamba la bibi. Waondoe majeshi yao Congo. 5. Viongozi wengi wa M23 ni Wanyarwanda. Huu ni udhibitisho kuwa Rwanda ni kinara kwenye mgogoro huu. 6. Congo ni kubwa sana na hivyo inakosa jeshi imara la kutosha kulinda mipaka yake yote. Congo ni kubwa mara 90 ya Rwanda. Wapo wanaoshauri igawanywe kama njia ya kutatua mgogoro. Kama ambavyo Yugoslavia iligawanywa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe. 7. Kiongozi wa sasa wa M23 Corneille Nangaa alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi 2019 na ndiye aliyemtangaza Tshisekedi kuwa Rais kwa ushindi wa 38%. Lakini alilaumiwa kupunguza kura za Martin Fayulu aliyepata 34%. Huenda kuna ahadi alipewa haikutimizwa ndio maana akaungana na Waasi. Sababu hizo hapo juu zikifanyiwa kazi, mgogoro wa Congo unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Mnaopenda kujifunza zaidi, naandika Kitabu. Get ready to have your copy. MWISHO.! (Malisa GJ ✍️)
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·1K Views
  • #PART6

    Alipoingia Ikulu Kabila alifuta jina Zaire na kurudisha Congo (Jamhuri ya kidemokrasia). Baadae alifikiria kuiachia Kivu, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini adimu duniani. Akasema "to hell with Lemera Agreement" akautupilia mbali mkataba wa Lemera. Akasema Kivu itabaki Congo na madini ya Kivu yatajenga Congo. Full stop. Ashakuwa Rais utamfanya nini?

    Kagame hakuamini macho yake. Alishawaza jinsi ambavyo Rwanda ingekuwa Dubai ya Afrika kwa rasilimali za Congo. Lakini ghafla aligeukwa na mshirika wake Laurent Désiré Kabila. Akamfuata "Godfather" wake mzee Museveni. Mzee akasema kama katugeuka tumpige. Wakatafuta kikundi cha Waasi wakiunge mkono. Wakapata Rassemblement Congolais pour la Démocratie (RCD), kilichoongozwa na Jenerali Ernest Wamba dia Wamba. Kikundi kikapewa silaha na fedha kikaanza kumshughulikia Kabila.

    RCD ikaanza kuchapana na jeshi la Congo (FARDC) ikiwa na backup ya Rwanda na Uganda. Vita vikapamba moto. Rwanda na Uganda nao wakaingiza majeshi Congo kusaidia waasi wa RCD. Kabila akaona anazidiwa, akaomba msaada Angola na Chad. Nchi hizo zikaleta vikosi vyake Congo. Mapigano yakawa makali sana. Eneo la mashariki mwa Congo likageuka machinjioni. Watu walikufa kwa wingi, mpaka maiti zikatapakaa barabarani bila kuzikwa, zikawa zinadonolewa na ndege.

    Hii iliitwa Vita ya Pili ya Congo (1998–2002), iliyokua mbaya zaidi katika historia ya vita zote Afrika. Imebatizwa jina "Vita Kuu ya Afrika". Inakadiriwa watu laki tano walipoteza maisha huku mamilioni wakikimbia nchi. Mapigano yaliendelea, huku vikosi vya Rwanda na Uganda vikichota madini. Katikati ya mapigano mgongano wa kimaslahi ukajitokeza.

    Jasin Stearns, katika kitabu chake Dancing in the Glory of Monsters, anasema Kagame alishindwa kuelewana na "godfather" wake Museveni juu ya mgawanyo wa mali. Hali hiyo ilifanya kikundi cha RCD kipasuke na kuzaliwa vikundi viwili. Cha kwanza kikajiita RCD-Goma kikiongozwa na Kanali Emile Ilunga (hiki kilisaidiwa na Rwanda) na cha pili kikajiita RCD-Kisangani, kikiongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi (kikisaidiwa na Uganda).
    (Malisa GJ)

    #PART6 Alipoingia Ikulu Kabila alifuta jina Zaire na kurudisha Congo (Jamhuri ya kidemokrasia). Baadae alifikiria kuiachia Kivu, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini adimu duniani. Akasema "to hell with Lemera Agreement" akautupilia mbali mkataba wa Lemera. Akasema Kivu itabaki Congo na madini ya Kivu yatajenga Congo. Full stop. Ashakuwa Rais utamfanya nini? Kagame hakuamini macho yake. Alishawaza jinsi ambavyo Rwanda ingekuwa Dubai ya Afrika kwa rasilimali za Congo. Lakini ghafla aligeukwa na mshirika wake Laurent Désiré Kabila. Akamfuata "Godfather" wake mzee Museveni. Mzee akasema kama katugeuka tumpige. Wakatafuta kikundi cha Waasi wakiunge mkono. Wakapata Rassemblement Congolais pour la Démocratie (RCD), kilichoongozwa na Jenerali Ernest Wamba dia Wamba. Kikundi kikapewa silaha na fedha kikaanza kumshughulikia Kabila. RCD ikaanza kuchapana na jeshi la Congo (FARDC) ikiwa na backup ya Rwanda na Uganda. Vita vikapamba moto. Rwanda na Uganda nao wakaingiza majeshi Congo kusaidia waasi wa RCD. Kabila akaona anazidiwa, akaomba msaada Angola na Chad. Nchi hizo zikaleta vikosi vyake Congo. Mapigano yakawa makali sana. Eneo la mashariki mwa Congo likageuka machinjioni. Watu walikufa kwa wingi, mpaka maiti zikatapakaa barabarani bila kuzikwa, zikawa zinadonolewa na ndege. Hii iliitwa Vita ya Pili ya Congo (1998–2002), iliyokua mbaya zaidi katika historia ya vita zote Afrika. Imebatizwa jina "Vita Kuu ya Afrika". Inakadiriwa watu laki tano walipoteza maisha huku mamilioni wakikimbia nchi. Mapigano yaliendelea, huku vikosi vya Rwanda na Uganda vikichota madini. Katikati ya mapigano mgongano wa kimaslahi ukajitokeza. Jasin Stearns, katika kitabu chake Dancing in the Glory of Monsters, anasema Kagame alishindwa kuelewana na "godfather" wake Museveni juu ya mgawanyo wa mali. Hali hiyo ilifanya kikundi cha RCD kipasuke na kuzaliwa vikundi viwili. Cha kwanza kikajiita RCD-Goma kikiongozwa na Kanali Emile Ilunga (hiki kilisaidiwa na Rwanda) na cha pili kikajiita RCD-Kisangani, kikiongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi (kikisaidiwa na Uganda). (Malisa GJ)
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·731 Views
  • DRC SAGA - PART 1

    (TAHADHARI: kama wwe ni mpenzi wa udaku au story fupifupi usisome. Hii ni kwa ajili ya watu wenye "solid mind" na wanaopenda kujifunza).
    ______
    Mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umebeba historia ndefu inayohitaji muda mrefu kuielezea, lakini nitajaribu kuifupisha kwa kuangazia mambo machache muhimu.

    Mpelelezi wa Kiingereza, John Speke, katika kitabu chake Journal of the Discovery of the Source of the Nile (1863), aliandika kuwa asili ya Watutsi ni Pembe ya Afrika (Ethiopia, Somalia, Djibouti), na kwamba walihama katika karne ya 12 wakielekea eneo la Maziwa Makuu. Walifanya makazi yao katika maeneo ya kaskazini-magharibi mwa Ziwa Tanganyika, eneo ambalo kwa sasa ni Rwanda, Burundi, na Congo. Walipowasili, walikuta wenyeji ambao Wahutu na Watwa, ambao waliishi nao kwa amani. Wahutu na Watwa walikuwa wakulima, huku Watutsi wakiwa wafugaji.

    Karne ya 18, wakoloni walipofika, waligawa maeneo ya kiutawala bila kuzingatia mipaka ya kijamii iliyokuwepo. Badala yake, walizingatia maslahi yao binafsi, jambo lililosababisha baadhi ya jamii kugawanyika katika mataifa mawili tofauti. Kwa mfano, jamii ya Wamasai iligawanywa kati ya Kenya na Tanganyika. Wahutu waligawanyika kati ya Rwanda na Burundi, huku Watutsi wakigawanyika Rwanda, Burundi na Congo maeneo ya Kivu kusini.

    Watutsi pamoja na kuwa wachache kwa idadi lakini walijikuta wameathirika zaidi kwa kugawanyika maeneo mengi. Waligawanyika katika mataifa matatu tofauti ingawa walikuwa watu wa jamii moja, walioongea lugha moja, wenye mila na desturi zinazofanana.

    Baada ya mipaka kuwekwa Watutsi waliojikuta katika eneo la Kivu (Congo) walitengwa na jamii nyingine za watu wa eneo hilo kama Wabembe, Wavira, na Wanyindu. Kwa kuwa sehemu kubwa ya Watutsi ilikua Rwanda, wale waliojikuta Congo walionekana kama wageni (externals) maana walikua 6% tu ya watu wa Kivu.

    Walishauriwa kuhamia Rwanda, lakini hawakua wanyarwanda. Ni Wakongomani waliozaliwa hapo. Babu zao walifika hapo karne ya 12 kama nilivyoeleza juu. Kabla ya ukoloni Watutsi wote walikua jamii moja. Lakini baada ya mipaka ya wakoloni wakajikuta wamegawanywa katika nchi 3 tofauti. Sasa wafanjeje?
    (Malisa GJ)

    DRC SAGA - PART 1 (TAHADHARI: kama wwe ni mpenzi wa udaku au story fupifupi usisome. Hii ni kwa ajili ya watu wenye "solid mind" na wanaopenda kujifunza). ______ Mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umebeba historia ndefu inayohitaji muda mrefu kuielezea, lakini nitajaribu kuifupisha kwa kuangazia mambo machache muhimu. Mpelelezi wa Kiingereza, John Speke, katika kitabu chake Journal of the Discovery of the Source of the Nile (1863), aliandika kuwa asili ya Watutsi ni Pembe ya Afrika (Ethiopia, Somalia, Djibouti), na kwamba walihama katika karne ya 12 wakielekea eneo la Maziwa Makuu. Walifanya makazi yao katika maeneo ya kaskazini-magharibi mwa Ziwa Tanganyika, eneo ambalo kwa sasa ni Rwanda, Burundi, na Congo. Walipowasili, walikuta wenyeji ambao Wahutu na Watwa, ambao waliishi nao kwa amani. Wahutu na Watwa walikuwa wakulima, huku Watutsi wakiwa wafugaji. Karne ya 18, wakoloni walipofika, waligawa maeneo ya kiutawala bila kuzingatia mipaka ya kijamii iliyokuwepo. Badala yake, walizingatia maslahi yao binafsi, jambo lililosababisha baadhi ya jamii kugawanyika katika mataifa mawili tofauti. Kwa mfano, jamii ya Wamasai iligawanywa kati ya Kenya na Tanganyika. Wahutu waligawanyika kati ya Rwanda na Burundi, huku Watutsi wakigawanyika Rwanda, Burundi na Congo maeneo ya Kivu kusini. Watutsi pamoja na kuwa wachache kwa idadi lakini walijikuta wameathirika zaidi kwa kugawanyika maeneo mengi. Waligawanyika katika mataifa matatu tofauti ingawa walikuwa watu wa jamii moja, walioongea lugha moja, wenye mila na desturi zinazofanana. Baada ya mipaka kuwekwa Watutsi waliojikuta katika eneo la Kivu (Congo) walitengwa na jamii nyingine za watu wa eneo hilo kama Wabembe, Wavira, na Wanyindu. Kwa kuwa sehemu kubwa ya Watutsi ilikua Rwanda, wale waliojikuta Congo walionekana kama wageni (externals) maana walikua 6% tu ya watu wa Kivu. Walishauriwa kuhamia Rwanda, lakini hawakua wanyarwanda. Ni Wakongomani waliozaliwa hapo. Babu zao walifika hapo karne ya 12 kama nilivyoeleza juu. Kabla ya ukoloni Watutsi wote walikua jamii moja. Lakini baada ya mipaka ya wakoloni wakajikuta wamegawanywa katika nchi 3 tofauti. Sasa wafanjeje? (Malisa GJ)
    0 Comments ·0 Shares ·507 Views
  • Kaka 2003 Alitua Malpesa Airpot Milan akiwa amevaa mewani ya mwanafunzi, Nywele zake amechana vizuri kama mwanafunzi, kitu pekee alichokosa ili awe mwanafunzi kamili ni vitabu na lunchbox, "nikasema" Mungu wangu tumefanya nini hiki? hivi huyu ataweza kucheza professional football kwa kiwango kinachotakiwa?

    Sikuwahi kumuona Ricardo Kaka kabla hiyo ndo ilikua mara ya kwanza, hata video yake yoyote sikuiona kwahiyo nilikua na wasiwasi.

    Hatimae siku ilifika Kaka akaja kwenye mazoezi kitu cha kwanza nilichotaka kumuuliza ni "Umewaambia wazazi wako kuwa haujaenda shule leo?", Walinzi wa Milanello(uwanja wa mazoezi) walikua na kila sababu ya kumuuliza iko wapi leseni yako ya udereva kabla ya kumruhusu kuingia ila unajua ni nini kilitokea? Ni hiki...

    Aliposimama uwanjani kwa mara ya kwanza niliskia kwaya na tarumbeta kutoka mbinguni kweli Kaka alikua ni Genius alieteremshwa kutoka mbinguni asante Mungu.

    Alipogusa tu mpira alikua na uwezo wa ajabu niliacha kuongea maana hakuna neno la kuelezea hisia zangu, hakuna neno kwenye kamusi linaloweza kuelezea ni nini niliona.

    Nilimpenda sana Kaka, kweli nilimpenda, sana, Aliweka chini mewani yake akavaa tracksuit na akawa kitu ambacho sikutegemea "mchezaji mwenye viwango vya dunia".

    Hayo ni Maneno aliyoandika Carlo Ancelotti kwenye kitabu chake "The beautiful Game of an Ordinary Genius", akielezea nini kilitokea alipokua kocha wa Ac Milan na walipomsajili Ricardo Izecson dos Santos Leite maarufu Ricardo Kaka.
    Kaka 2003 Alitua Malpesa Airpot Milan akiwa amevaa mewani ya mwanafunzi, Nywele zake amechana vizuri kama mwanafunzi, kitu pekee alichokosa ili awe mwanafunzi kamili ni vitabu na lunchbox, "nikasema" Mungu wangu tumefanya nini hiki? hivi huyu ataweza kucheza professional football kwa kiwango kinachotakiwa? Sikuwahi kumuona Ricardo Kaka kabla hiyo ndo ilikua mara ya kwanza, hata video yake yoyote sikuiona kwahiyo nilikua na wasiwasi. Hatimae siku ilifika Kaka akaja kwenye mazoezi kitu cha kwanza nilichotaka kumuuliza ni "Umewaambia wazazi wako kuwa haujaenda shule leo?", Walinzi wa Milanello(uwanja wa mazoezi) walikua na kila sababu ya kumuuliza iko wapi leseni yako ya udereva kabla ya kumruhusu kuingia ila unajua ni nini kilitokea? Ni hiki... Aliposimama uwanjani kwa mara ya kwanza niliskia kwaya na tarumbeta kutoka mbinguni kweli Kaka alikua ni Genius alieteremshwa kutoka mbinguni asante Mungu. Alipogusa tu mpira alikua na uwezo wa ajabu niliacha kuongea maana hakuna neno la kuelezea hisia zangu, hakuna neno kwenye kamusi linaloweza kuelezea ni nini niliona. Nilimpenda sana Kaka, kweli nilimpenda, sana, Aliweka chini mewani yake akavaa tracksuit na akawa kitu ambacho sikutegemea "mchezaji mwenye viwango vya dunia". Hayo ni Maneno aliyoandika Carlo Ancelotti kwenye kitabu chake "The beautiful Game of an Ordinary Genius", akielezea nini kilitokea alipokua kocha wa Ac Milan na walipomsajili Ricardo Izecson dos Santos Leite maarufu Ricardo Kaka.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·669 Views
  • Chukua hii tumia Hizi “Sheria 20 za 2025 kuelekea mafanikio yako..

    1. Hakuna ngono. Epuka kitu chochote kitakachokuchochea kuitazama.

    2. Fanya mazoezi mara tatu hadi nne kila wiki.

    3. Soma kurasa 10 za kitabu cha kujiboresha au kitabu cha historia kila siku.

    4. Hasira si rafiki yako. Idhibiti kabla ya kukudhibiti.

    5. kila wakati jitahidi kukaa nadhifu 80% ya wakati.

    6. Usiwe mcheshi ili kumvutia mtu yeyote. Hasa w0m£n.

    7. Fanya kazi kabla ya Burudani. Fanya kile unachohitaji kufanya kabla ya kwenda kwa kile unachotaka kufanya.

    8. Uvutaji sigara hudhuru zaidi kuliko inavyopenda. Achana nayo.

    9.samehe lakini usisahau somo ulilojifunza.

    10. Kuwa na Maono. Kuwa na kusudi. Pambana kuelekea hilo.

    11. Usikubali Kudharauliwa.

    12. Usifanye mzaha na maisha yako ya kifedha.

    13. Pesa inayotumika kununulia mapenzi, itaendelea kutumika kudumisha upendo huo. Usijihusishe na kitendo kama hicho.

    14.usijitambulishe kama "mwanaume halisi", hakuna kitu kama "mwanaume halisi". SIMP pekee ndizo zinazoitwa hivyo. Wewe ni wa thamani kubwa au huna.

    15. Jifunze jinsi ya kujitetea.

    16. Haijalishi umeanguka mara ngapi, pumua kwa kina na uinuke tena.

    17.dakika sh£ inakukataa, misheni imefutwa. Usiamue kuwa rafiki wa h£r. Songa mbele haraka iwezekanavyo. Kuna wanawake bilioni 3.97 duniani.

    18. Marafiki zako watakujenga au watakuvunja. Chagua kwa busara.

    19. Waheshimu na wapende wazazi wako. Walikuleta kwenye ulimwengu huu.

    20.anza 2025 na Mungu. Maliza na Mungu. Kaa Savage”.

    Plz like & follow
    Chukua hii tumia Hizi “Sheria 20 za 2025 kuelekea mafanikio yako.. 1. Hakuna ngono. Epuka kitu chochote kitakachokuchochea kuitazama. 2. Fanya mazoezi mara tatu hadi nne kila wiki. 3. Soma kurasa 10 za kitabu cha kujiboresha au kitabu cha historia kila siku. 4. Hasira si rafiki yako. Idhibiti kabla ya kukudhibiti. 5. kila wakati jitahidi kukaa nadhifu 80% ya wakati. 6. Usiwe mcheshi ili kumvutia mtu yeyote. Hasa w0m£n. 7. Fanya kazi kabla ya Burudani. Fanya kile unachohitaji kufanya kabla ya kwenda kwa kile unachotaka kufanya. 8. Uvutaji sigara hudhuru zaidi kuliko inavyopenda. Achana nayo. 9.samehe lakini usisahau somo ulilojifunza. 10. Kuwa na Maono. Kuwa na kusudi. Pambana kuelekea hilo. 11. Usikubali Kudharauliwa. 12. Usifanye mzaha na maisha yako ya kifedha. 13. Pesa inayotumika kununulia mapenzi, itaendelea kutumika kudumisha upendo huo. Usijihusishe na kitendo kama hicho. 14.usijitambulishe kama "mwanaume halisi", hakuna kitu kama "mwanaume halisi". SIMP pekee ndizo zinazoitwa hivyo. Wewe ni wa thamani kubwa au huna. 15. Jifunze jinsi ya kujitetea. 16. Haijalishi umeanguka mara ngapi, pumua kwa kina na uinuke tena. 17.dakika sh£ inakukataa, misheni imefutwa. Usiamue kuwa rafiki wa h£r. Songa mbele haraka iwezekanavyo. Kuna wanawake bilioni 3.97 duniani. 18. Marafiki zako watakujenga au watakuvunja. Chagua kwa busara. 19. Waheshimu na wapende wazazi wako. Walikuleta kwenye ulimwengu huu. 20.anza 2025 na Mungu. Maliza na Mungu. Kaa Savage”. Plz like & follow🙏
    Like
    2
    · 1 Comments ·0 Shares ·810 Views
  • "Faida ya kwanza ya Eng. Hersi na ACA ni kuwa sauti ya VILABU kwenye Mkutano wa Kamati Tendaji ya CAF

    Na moja ya Kilio kikubwa cha VILABU hapa Afrika ni kukosa Hela ya maandalizi kushiriki LIGI YA MABINGWA na KOMBE LA SHIRIKISHO

    Unapambana kupata nafasi kwenye Ligi, kisha upambane wapi utapata Hela ili ukashiriki HATUA 2 ZA AWALI ili baadae ukapate hela ya CAF kuanzia Hatua ya Makundi

    Timu nyingi ndogo Tanzania zilipata Tabu ya kushiriki michuano hii, Mfano wa wazi BIASHARA UNITED Kutoka Mara

    ENG Hersi amefika na kuhakikisha Timu zote za Hatua ya awali zinapata Fedha.

    Msimu huu ZAIDI YA BILIONI 13 kutoka CAF zimetoka kwa VILABU vilivyoshiriki Hatua ya awali.

    Makofi Mengi kwa Eng. Hersi Said" - Ally Kamwe, Msemaji wa klabu ya Yanga SC.

    "Faida ya kwanza ya Eng. Hersi na ACA ni kuwa sauti ya VILABU kwenye Mkutano wa Kamati Tendaji ya CAF Na moja ya Kilio kikubwa cha VILABU hapa Afrika ni kukosa Hela ya maandalizi kushiriki LIGI YA MABINGWA na KOMBE LA SHIRIKISHO Unapambana kupata nafasi kwenye Ligi, kisha upambane wapi utapata Hela ili ukashiriki HATUA 2 ZA AWALI ili baadae ukapate hela ya CAF kuanzia Hatua ya Makundi Timu nyingi ndogo Tanzania zilipata Tabu ya kushiriki michuano hii, Mfano wa wazi BIASHARA UNITED Kutoka Mara ENG Hersi amefika na kuhakikisha Timu zote za Hatua ya awali zinapata Fedha. Msimu huu ZAIDI YA BILIONI 13 kutoka CAF zimetoka kwa VILABU vilivyoshiriki Hatua ya awali. Makofi Mengi kwa Eng. Hersi Said👏👏" - Ally Kamwe, Msemaji wa klabu ya Yanga SC.
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·306 Views
  • "Faida ya kwanza ya Eng. Hersi na ACA ni kuwa sauti ya VILABU kwenye Mkutano wa Kamati Tendaji ya CAF

    Na moja ya Kilio kikubwa cha VILABU hapa Afrika ni kukosa Hela ya maandalizi kushiriki LIGI YA MABINGWA na KOMBE LA SHIRIKISHO

    Unapambana kupata nafasi kwenye Ligi, kisha upambane wapi utapata Hela ili ukashiriki HATUA 2 ZA AWALI ili baadae ukapate hela ya CAF kuanzia Hatua ya Makundi

    Timu nyingi ndogo Tanzania zilipata Tabu ya kushiriki michuano hii, Mfano wa wazi BIASHARA UNITED Kutoka Mara

    ENG Hersi amefika na kuhakikisha Timu zote za Hatua ya awali zinapata Fedha.

    Msimu huu ZAIDI YA BILIONI 13 kutoka CAF zimetoka kwa VILABU vilivyoshiriki Hatua ya awali.

    Makofi Mengi kwa Eng. Hersi Said" - Ally Kamwe, Msemaji wa klabu ya Yanga SC.

    "Faida ya kwanza ya Eng. Hersi na ACA ni kuwa sauti ya VILABU kwenye Mkutano wa Kamati Tendaji ya CAF Na moja ya Kilio kikubwa cha VILABU hapa Afrika ni kukosa Hela ya maandalizi kushiriki LIGI YA MABINGWA na KOMBE LA SHIRIKISHO Unapambana kupata nafasi kwenye Ligi, kisha upambane wapi utapata Hela ili ukashiriki HATUA 2 ZA AWALI ili baadae ukapate hela ya CAF kuanzia Hatua ya Makundi Timu nyingi ndogo Tanzania zilipata Tabu ya kushiriki michuano hii, Mfano wa wazi BIASHARA UNITED Kutoka Mara ENG Hersi amefika na kuhakikisha Timu zote za Hatua ya awali zinapata Fedha. Msimu huu ZAIDI YA BILIONI 13 kutoka CAF zimetoka kwa VILABU vilivyoshiriki Hatua ya awali. Makofi Mengi kwa Eng. Hersi Said👏👏" - Ally Kamwe, Msemaji wa klabu ya Yanga SC.
    0 Comments ·0 Shares ·286 Views
  • Jose mourinho : "Naweza kusema kazi ngumu niliyokuwa nayo ni Messi, nikikuta kitabu kimeandikwa kwenye jalada lake "How to stop Messi" ningenunua vitabu vyote vya kusoma na kuwapa wachezaji wangu, nilifanya hivyo. sikumtafutia suluhu nikiwa Real Madrid ningenunua mabeki bora na mwisho ningewakuta wanaanguka chini na Messi anakimbia na kujisemea

    "kuna bora zaidi ya hawa wachezaji? Hakuna, kwa hiyo tatizo halipo kwangu wala kwao, tatizo ni kwamba hakuna namna ya kumzuia" Naomba tu Mungu afanye muujiza kwa muujiza huu wa soka maana masuluhisho ya dunia hayatafanya kazi naye, Nataka kumwambia kocha yeyote ambaye hajakutana na Messi “una bahati sana kwani unalala vizuri kwani timu unazocheza nazo hazina Messi”, makocha watakaokutana naye nataka kusema “Usijisumbue na usijaribu kumzuia, furahia tu au utajikuta umekaa ukiwaza usiku wa manane"

    Jose mourinho 🗣️ : "Naweza kusema kazi ngumu niliyokuwa nayo ni Messi, nikikuta kitabu kimeandikwa kwenye jalada lake "How to stop Messi" ningenunua vitabu vyote vya kusoma na kuwapa wachezaji wangu, nilifanya hivyo. sikumtafutia suluhu nikiwa Real Madrid ningenunua mabeki bora na mwisho ningewakuta wanaanguka chini na Messi anakimbia na kujisemea "kuna bora zaidi ya hawa wachezaji? Hakuna, kwa hiyo tatizo halipo kwangu wala kwao, tatizo ni kwamba hakuna namna ya kumzuia" Naomba tu Mungu afanye muujiza kwa muujiza huu wa soka maana masuluhisho ya dunia hayatafanya kazi naye, Nataka kumwambia kocha yeyote ambaye hajakutana na Messi “una bahati sana kwani unalala vizuri kwani timu unazocheza nazo hazina Messi”, makocha watakaokutana naye nataka kusema “Usijisumbue na usijaribu kumzuia, furahia tu au utajikuta umekaa ukiwaza usiku wa manane"
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·412 Views
  • KILA SAFARI KUBWA INAANZA NA HATUA...

    Kuna vita vya utulivu ambavyo hupigana ndani ya moyo wa kila mtu anayesimama kwenye ukingo wa mwanzo mpya. Ni vita kati ya hofu na matumaini, shaka na uwezekano. Katika ukingo huo, mara nyingi sauti hunong’ona: “Itakuwaje nikishindwa? Nini kama mimi si mzuri vya kutosha?" Lakini wacha nikuulize, "nini ikiwa hautawahi kujaribu?" Hofu ya kushindwa imerudisha nyuma ndoto zaidi kuliko kushindwa yenyewe. Makaburi mengi yamejawa na mwangwi wa “kile ambacho kingekuwako.” tafadhali, usiogope kuanza. Kuwa na hofu ya kamwe kujaribu. Kila safari kubwa huanza na hatua moja. Hatua hiyo inaweza kuwa ya kutetereka, isiyo na uhakika, hata ndogo, lakini ndilo jambo lenye nguvu zaidi utakalowahi kuchukua. Kwa sababu katika wakati huo, unajiondoa kutoka kwa minyororo ya kusitasita. Inafungua milango ambayo hukuwahi kujua kuwa iko na njia ambazo haujawahi kufikiria unaweza kutembea.

    Usisahau kwamba sio makosa unayofanya njiani ambayo yanakufafanua. Ni kukataa kwako kuacha. Kila hatua mbaya, kila kushindwa, ni hatua tu. Watu waliofanikiwa zaidi ulimwenguni sio wale ambao hawakuwahi kushindwa, lakini wale ambao hawakukata tamaa. Mbegu iliyozikwa kwenye udongo haionekani sana. Lakini chini ya ardhi, bila kuonekana na ulimwengu, hupasuka na kusukuma juu. Na siku moja, inapasuka kama mti mkubwa. Unaweza kuhisi umezikwa leo, lakini kumbuka, haukuzikwa ili kusahaulika. Unapandwa kukua. Majuto makubwa utakayobeba maishani sio nyakati ulizoanguka bali ni nyakati ulizokataa kuinuka, ndoto ulizoziacha zifie kwenye pembe tulivu za moyo wako. Kwa hivyo chukua hatua hiyo ya kwanza. Andika kitabu. Anzisha biashara. Piga simu. Zungumza maneno. Hebu ujasiri uwe mkubwa kuliko hofu. Kwa sababu mwisho wa siku zako, hutakumbuka mambo yaliyokuogopesha. Utakumbuka nyakati ulizothubutu kuanza. Na hapo ndipo maisha yanapoanzia, marafiki zangu.

    KILA SAFARI KUBWA INAANZA NA HATUA... Kuna vita vya utulivu ambavyo hupigana ndani ya moyo wa kila mtu anayesimama kwenye ukingo wa mwanzo mpya. Ni vita kati ya hofu na matumaini, shaka na uwezekano. Katika ukingo huo, mara nyingi sauti hunong’ona: “Itakuwaje nikishindwa? Nini kama mimi si mzuri vya kutosha?" Lakini wacha nikuulize, "nini ikiwa hautawahi kujaribu?" Hofu ya kushindwa imerudisha nyuma ndoto zaidi kuliko kushindwa yenyewe. Makaburi mengi yamejawa na mwangwi wa “kile ambacho kingekuwako.” tafadhali, usiogope kuanza. Kuwa na hofu ya kamwe kujaribu. Kila safari kubwa huanza na hatua moja. Hatua hiyo inaweza kuwa ya kutetereka, isiyo na uhakika, hata ndogo, lakini ndilo jambo lenye nguvu zaidi utakalowahi kuchukua. Kwa sababu katika wakati huo, unajiondoa kutoka kwa minyororo ya kusitasita. Inafungua milango ambayo hukuwahi kujua kuwa iko na njia ambazo haujawahi kufikiria unaweza kutembea. Usisahau kwamba sio makosa unayofanya njiani ambayo yanakufafanua. Ni kukataa kwako kuacha. Kila hatua mbaya, kila kushindwa, ni hatua tu. Watu waliofanikiwa zaidi ulimwenguni sio wale ambao hawakuwahi kushindwa, lakini wale ambao hawakukata tamaa. Mbegu iliyozikwa kwenye udongo haionekani sana. Lakini chini ya ardhi, bila kuonekana na ulimwengu, hupasuka na kusukuma juu. Na siku moja, inapasuka kama mti mkubwa. Unaweza kuhisi umezikwa leo, lakini kumbuka, haukuzikwa ili kusahaulika. Unapandwa kukua. Majuto makubwa utakayobeba maishani sio nyakati ulizoanguka bali ni nyakati ulizokataa kuinuka, ndoto ulizoziacha zifie kwenye pembe tulivu za moyo wako. Kwa hivyo chukua hatua hiyo ya kwanza. Andika kitabu. Anzisha biashara. Piga simu. Zungumza maneno. Hebu ujasiri uwe mkubwa kuliko hofu. Kwa sababu mwisho wa siku zako, hutakumbuka mambo yaliyokuogopesha. Utakumbuka nyakati ulizothubutu kuanza. Na hapo ndipo maisha yanapoanzia, marafiki zangu.
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·427 Views
  • DUNIA NA MAAJABU YAKE
    (Muundo wa Dunia na Maajabu Yaliyomo)

    1. UMRI WA DUNIA

    HII Dunia yetu ina historia ndefu mno tangu ilipojiunda angani, miaka takribani bilioni 4.5 iliyopita.

    Tarakimu za umri huo wa miaka bilioni 4.5 ni 4,500,000,000, yaani miaka milioni elfu nne na mia tano iliyopita.

    Dunia ambayo kwa lugha ya Kiingereza inafahamika vyema kwa jina la 'Earth', pia hujulikana kama 'the World', ikimaanishwa ulimwengu.

    Aidha, Dunia ni sayari pekee kwenye himaya ya sayari zilizopo chini ya jua ambayo jina lake halitokani na majina ya "Miungu wa Dola" ya Kigiriki au ya Kirumi.

    Asili ya jina la 'earth' ni 'erde' lenye asili ya nchini Ujerumani, na maana yake ni udongo au ardhi.

    Mpaka kuweza kupata umri huo wa dunia wanasayansi walifanya kazi ya kutafiti na kisha kuwasilisha matokeo yao kwenye makongamano ya kisayansi duniani, ambapo matokeo hayo yalijadiliwa kwa kina na hatimaye kukubalika kama hivi.

    Kumbuka katika majadiliano hayo huwepo mivutano mikali miongoni mwa wanasayansi waalikwa, ambapo pia jopo la wanasayansi wanaowasilisha utafiti husika hujikuta wakitakiwa kujibu hoja mbalimbali za wanasayansi wenzao.

    Kuna wakati baadhi ya matokeo ya tafiti kadhaa hukataliwa, huku watafiti husika wakitakiwa kurejea upya tafiti zao.

    Wanasayansi hupata umri wa sayari kwa kupima umri wa miamba ya sayari husika, ambapo mwamba wenye umri mkubwa zaidi kuliko miamba yote ndiyo huchukuliwa kuwa umri wa sayari husika.

    Itakumbukwa kuwa Msahafu wa Biblia (Sura ya Mwanzo 1) husimulia jinsi Mwenyezi Mungu alivyoumba "mbingu na nchi na vyote vilivyomo kwa siku 6," lakini pia Msahafu huohuo kwenye aya zingine hueleza kuwa miaka elfu moja ya duniani yaweza kuwa sawa na siku moja kwenye ya Makazi ya Mwenyezi Mungu.

    Ni dhahiri kuwa binadamu tukiwa hatuna hoja sahihi kwa maelezo ya aina hiyo, ndipo tunaona ni vyema mambo ya Mwenyezi Mungu kumwachia Yeye Mwenyewe Mwenyezi Mungu.

    2. KUUMBIKA DUNIA, SAYARI, JUA, NYOTA

    Kimsingi, Dunia kama zilivyo sayari zingine zote ilijiunda kutokana na mabaki ya vitu vilivyotumika kuunda Jua.

    Jua ambalo ni nyota kama zilivyo nyota zote angani, lilijiunda lenyewe kwenye eneo la anga lijulikanalo kama 'Pillars of Creation' (nguzo za uumbaji) katika ukanda wa anga wenye upana ambao huonekana kutokuwa na mwisho.

    Ukanda huo ujulikanao kama 'Solar Nebula,' umegubikwa na mawingu ya vumbi la huko angani pamoja na aina mbalimbali za gesi na hewa, ikiwemo haidrojeni na heliumu.

    'Solar' ni jina la nishati itokanayo na joto la jua, na 'Nebula' kwa lugha ya Kilatini ni "wingu" au vumbi la gesi asilia mithili ya ukungu.

    Hivyo, 'Solar Nebula' ni ukanda katika anga ya mbali wenye mawingu yaliyosheheni nishati yenye joto, sawa na nishati ya joto la jua.

    Sasa basi, tunafahamu vyema kuwa jua hutoa mionzi hatari yenye joto kali mithili ya moto mkali, na ambayo ikiboreshwa kisayansi pia huweza kutoa nishati ya umeme.

    Hivyo, kwa muktadha huo, hebu ngoja sasa tuleta pamoja hewa za gesi, zikiwemo haidrojeni na heliumu, mawingu yenye nishati ya umeme wa jua, vumbi la angani na tufani itokanayo na mchafuko mbaya wa hali ya hewa huko anga za mbali.

    Na ili kuweza kupata matokeo yanayotakiwa, hebu pia tutambue uwepo wa nguvu kubwa ya asili katika kiwango kijulikanacho kwa jina la "Supernatural Power", ambayo ndiyo huwa kisababishi cha mambo yote.

    Kisayansi, "Supernatural Power" ni nguvu kubwa ya asili ambayo huendesha mifumo mbalimbali ya asili, ambapo duniani nguvu hiyo hujulikana kama Nguvu ya Mungu.

    Nguvu asili hiyo, yaani Supernatural Power, husababisha tufani ambayo huvurumisha kwa pamoja vitu vyote hivyo, (gesi, hewa, mawingu yenye nishati ya joto na vumbi la angani) ili kuunda tufani yenye umbo la duara.

    Duara hiyo ni kama ile itokanayo na kimbunga kikali duniani, na ambacho sasa tutaona kikifungamanisha pamoja vitu vyote hivyo katika mchafuko mkubwa wa hali mbaya ya hewa.

    Natumia maneno ya msisitizo kuelezea "ukubwa" wa mchafuko huo wa hali ya hewa katika eneo hilo la anga, kwani katika kuunda sayari au nyota nguvuasili kubwa hutumika.

    Aidha, tufani hiyo ya duara itakayoanza kidogo kidogo kama kimbunga kikali, itazidi kukua hadi kuwa na kipenyo cha takribani kilomita 10 hadi 200 au zaidi na kwendelea.

    Tufani hiyo ndiyo itavurumisha kwa pamoja gesi na hewa za naitrojeni na heliumu, mawingu ya nishati ya joto na vumbi la angani (kama kifanyavyo kimbunga kikali katika eneo tambarare la duniani).

    Pia, wakati mchafuko huo wa hali mbaya ya hewa ukiendelea, hebu ngoja sisi watazamaji tujibanze mahali fulani kwa mbali kushuhudia duara hiyo ya tufani ikijizungusha yenyewe bila kukoma kwa kipindi cha miaka mingi.

    Kitakachofuata ni kuanza kuona kiini cha moto kikianza kujiunda katikati ya duara hiyo ya tufani kali, huku pia nje ya duara hiyo vitu kibao vikivutwa kujiunga na mzunguko wa hiyo tufani ya duara.

    Vitu hivyo ni pamoja na vumbi zaidi la angani, na gesi zaidi zenye joto kali.

    Wakati huohuo kipenyo na mzingo wa duara hiyo vitazidi kuongezeka upana na ukubwa, mfano wa duara yenye umbo sawa na la mpira mkubwa wa miguu.

    Hivyo, baada ya miaka takribani milioni moja tutashangaa kuona lile vumbi likigeuka taratibu kuwa miamba ya moto ndani ya kiini cha tufani hiyo ya duara.

    Miamba hiyo ni kutokana na lile vumbi la angani ambalo hatimaye limeshikamana pamoja mithili ya zege, na hatimaye kuwa miamba ndani ya tufani ya duara.

    Sanjari na kuundika huko ndani ya kitovu cha hiyo tufani ya duara, pia kwelekea nje ya duara hiyo utaundika udongo ambao ardhi, mchanga na mawe.

    Kimsingi, vitu hivyo pia ni matokeo ya lile vumbi la angani ambalo lilikusanywa pamoja na kuvutwa na kasi ya mzunguko wa tufani.

    Hatua hiyo mpya inatokana na kuwepo mshikamano na mgandamizo wa zile chembechembe za lile vumbivumbi ndani ya tufani.

    Vurumai hiyo ya mzunguko wa hiyo tufani ya duara yenye vumbi, itazidi kukua hadi kuunda sumaku ya asili ndani ya kile kitovu cha duara ya tufani.

    Kutokana na duara hiyo ya tufani kuongezeka ukubwa, hatimaye sumaku iliyopo kwenye kitovu cha duara hiyo itaishiwa nguvu ya kwendelea kunasa vumbi zaidi kuja kwenye mzingo wa hiyo duara ya tufani.

    Kumbuka kuwa wakati huo hiyo duara pia itaunda kimo kutoka kwenye usawa wa ardhi yake kwenda ndani kwenye kitovu chake, na hivyo kuwa duara ya mviringo kama umbo mfano wa mpira mchezo wa miguu.

    Baada ya kupita maelfu ya miaka mingi, duara hiyo ambayo hapo awali ilianza kama umbo la tufani na kuzidi kukua huko angani, sasa itakuwa na joto kali kupita kiasi na kuanza kung'aa kama jua.

    Jua hilo, ndiyo nyota mojawapo ya zile ambazo huonekana usiku ziking'aa angani.

    Lakini pia wakati wa kujiunda nyota hiyo, kama tulivyoona hapo awali, baadhi ya mabaki yake yaliyokuwa yakitawanyika angani wakati ile tufani ya duara ikijizungusha, huweza kujikusanya pamoja na kuunda sayari ambazo huzunguka baadhi ya hizo nyota.

    Hivyo ndivyo zilivyojiunda sayari zote ambazo huelea kwa kulizunguka jua letu.

    Mathalani, sayari zote ambazo hulizunguka jua, ikiwemo dunia zilijiunda kutokana na mabaki ya vitu kama gesi, michanga na mawe ambavyo vilitawanyika angani wakati jua likijiunda (kama ambavyo imeelezwa hapo awali).

    3. KIINI CHA DUNIA

    Dunia yetu ambayo wastani wa nusu kipenyo cha umbo lake la duara ni kilomita 6,371, mzingo wake ni kilomita takribani 40,041.

    Kama zilivyo sayari zote katika himaya ya jua, dunia nayo ilijiunda wakati jua likijiunda lenyewe.

    Yaani kwamba sayari ni mabaki ya vitu vilivyotumika kuliunda jua.

    Kadhalika kama zilivyo sayari zingine zote, dunia nayo ina kiini chake ambacho kipo katikati ya ardhi yake.

    Kiini hicho kina nguvu kubwa ya sumaku ambayo, pamoja na mambo mengineyo, 'huvuta' umbo hilo la duara kutoka juu ya ardhi kwenda katikati ya kiini hicho.

    Muundo huo ndio hulifungamanisha pamoja umbo la duara la dunia, na hivyo kuzuia umbo hilo lisifumke kutoka ardhini na kusambaratika.

    Hiyo ni sawa na mpira wa miguu unavyoweza kupasuka na kusambaratika, kama utajazwa upepo kupita kiasi chake.

    Kiini hicho ambacho kipo katikati kabisa ya dunia, kinajulikanacho kwa jina la kisayansi la 'Inner Core.'

    Kiini hicho kina joto kali la sentigredi 6,230 ambacho ndio kiasi cha joto la jua.

    Kiini hicho kina umbo la duara lenye nusu kipenyo cha kilomita 1,250.

    Kama ingetokea kuchimba ardhi wima kwenda kwenye kiini hicho, mchimbaji angeanza kukutana na joto la kiini hicho kuanzia kimo cha umbali wa kilomita 5,150 kutoka usawa wa juu ya ardhi tunayotembea.

    Katika historia ya uchimbaji ardhi, kina kirefu kilichowahi kuchimbwa ardhini ni mita 12,345 (kilomita 12.345) huko Sakhalini, nchini Urusi, kwa ajili ya uvunaji wa mafuta ya petroli.

    Kiini cha dunia kinaundwa na madini mchanganyiko wa nikeli (nickle), chuma (iron) na dhahabu.

    Kwa mujibu wa utafiti, inakadiriwa kuwa kama dhahabu hiyo ingechimbwa na kuchomwa mpaka kuwa kimiminika sawa na uji na kisha kumwagwa chini, ingeweza kuifunika dunia yote kwa unene wa sentimeta 45.

    Kiini hicho muhimu kwa uhai wa sayari hii ya dunia kiligunduliwa mwaka 1936 na mtaalamu wa matetemeko ya ardhi wa nchini Denmark, mwanamama Dkt. Inge Lehmann.

    Dkt. Lehmann alihitimu shahada yake ya kwanza katika fani ya Hisabati mwaka 1910, ya Uzamili mwaka 1920 (zote kutoka Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini mwake), na ile ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza.

    Alifariki kwa uzee mwaka 1993 akiwa na umri wa miaka 104.

    4. MAJI DUNIANI

    Kupatikana maji kwenye dunia yetu, ni mojawapo ya miundo ambayo haipo katika sayari zingine ambazo tuna taarifa za kitafiti kuzuhusu.

    Maji ni muhimili muhimu kwa ajili ya uhai wa viumbe wote na mimea, ambavyo kwa pamoja havipo katika sayari zingine za himaya ya jua.

    Kwa mujibu wa tafiti nyingi ambazo zimefanyika kwa miongo mingi ya miaka kujaribu kubaini nini chanzo cha kuwepo maji duniani, hakuna hata utafiti mmoja ulioonesha kwa usahihi matokeo ya kuridhisha.

    Miongoni mwa tafiti hizo ni pamoja na ule wa mwaka 2005, ambapo Mkuu wa Idara ya Masomo ya Sayari na Mwezi katika Chuo Kikuu cha Arizona nchini Marekani, Profesa Michael Julian Drake, na mwenzake ambaye ni mtaalamu wa Vimondo, Dkt. Huberto Campins, wa Chuo Kikuu cha Central Florida, walitafiti nini chanzo cha kuwepo maji duniani.

    Katika mawasilisho yao kwenye kongamano la kisayansi la Chama cha Wanataaluma wa Maarifa ya Anga za Juu (IAU), watafiti hao walikanusha madai ya uwezekano wa dunia hapo kale kugongwa na kimondo kikubwa na kusababisha maji kulipuka kutoka ardhini.

    Wakiwasilisha matokeo ya utafiti wao kwenye mkutano wa kongamano hilo, magwiji hao wa masuala ya sayari walieleza kwenye waraka wao uitwao "Origin of water on the terrestial planets" (chanzo cha kuwepo maji kwenye sayari).

    Walidai kuwa maji yaliyopo duniani yaliumbika kwenye ardhi ya dunia tangu mwanzo, wakati ikijiunda angani.

    Ikumbukwe kuwa eneo la uso wa dunia likiwa ni jumla ya kilomita za mraba milioni 510, asilimia 70.8 ya eneo hilo imefunikwa na maji na asilimia 29.2 ni nchi kavu, ikiwemo milima, mabonde na ardhi tambarare.

    5. HEWA YA OKSIJENI

    Muundo mwingine muhimu katika sayari hii ya dunia ni hewa ambazo ni tawala, yaani Naitrojeni ambayo kwa usahihi imeenea kwa asilimia 78.08 ya hewa yote ya dunia, Oksijeni asilimia 20.95, 'Argon' asilimia 0.93, hewa ya Ukaa (Carbon dioxide) asilimia 0.039, na asilimia moja ni hewa mithili ya mvuke wa maji (water vapour).

    Hewa ya Oksijeni ambayo ni nguzo muhimu kwa ajili ya uhai wa viumbe wote na pia haipatikani kwenye sayari nyingine chini ya jua, inadhaniwa ilianza kupatikana duniani miaka takribani bilioni 2.5 iliyopita kufuatia "kukomaa kwa kiini cha dunia."

    Kwa mujibu wa matokeo ya tafiti mbalimbali na nadharia za kisayansi, inaoneshwa kuwa kukomaa kwa kiini hicho cha dunia hatimaye ndiko kulisababisha kuzuka duniani milipuko ya volikano ambayo pia ilisababisha kuzuka mabonde na milima.

    Inaoneshwa kuwa tayari wakati huo maji yaliishakuwepo duniani, na kuwezesha kuzuka chembechembe ndogo sana za kibakteria zijulikanazo kwa jina la kisayansi la 'cyanobacteria' au 'blue-green algae'.

    Kwa kutumia mwanga wa jua, maji na hewa ya ukaa, chembechembe hizo ziliweza kuzalisha hewa mbalimbali, ikiwemo 'Carbonhydrates' na Oksijeni.

    Kwa kuwa hizo chembechembe ndogo za kibakteria huishi baharini, ilikuwa rahisi kwa oksijeni kutokea baharini kupepea na kuenea katika anga ya dunia na kuzuiliwa hapo na nguvu asili ya uvutano ya dunia ili pia ibaki ikienea pote duniani.

    Mpaka wakati wa kuzuka duniani mimea na viumbe hai miaka takribani bilioni 3.5 iliyopita, tayari oksijeni ilikwa ni tele duniani; na hivyo kutumika kudumisha uhai wa viumbe hadi wakati huu.

    6. UKANDA WA 'OZONE'

    Muundo mwingie muhimu wa asili kwa dunia ni ukanda wa anga ujulikanao kwa jina la 'ozone' ambao umetanda kama 'mwavuli' kwenye anga ya dunia, na kuikinga isidhuriwe na mionzi hatari ya sumu kutoka kwenye Jua.

    Ukanda huo maarufu kama 'ozone layer' umetanda kuanzia usawa wa kilometa 15 kutoka ardhini kwenda juu angani mpaka ukomo wa kilomita takribani 50, ambapo huchuja asilimia kati ya 97 na 99 ya mionzi hatari kwenye miale ya joto la jua.

    Miongoni mwa matatizo yanayosababishwa na mionzi hiyo hatari kutoka kwenye jua, ni pamoja na magonjwa ya saratani ya ngozi kwa bianadamu.

    Pia juu ya ukanda wa tabaka la ozone kuna ukanda mwingine uitwao "atmosphere" ambao ni madhubuti kiasi kwamba vitu vinavyotoka anga za juu na kujaribu kuupenya ili kufika duniani, hukumbana na joto kali na kusambaratishwa kwa kuunguzwa.

    Si kwamba tabaka hilo lina joto, isipokuwa kasi ya "kuanguka" vitu hivyo kutoka juu angani kuja dunia husababisha msuguano na chembechembe za gesi katika eneo hilo na kuzalisha joto mithili ya ndimi za moto.

    Picha za video za vyombo vya 'Apollo' vikirejea duniani kutoka mwezini vikiwa na wanaanga ndani yake na kupenya tabaka hilo kwa kasi ya kilomita 39,000 kwa saa, huonekana kughubikwa na ndimi za moto wa rangi ya njano na bluu.

    Rangi hizo ni ishara ya ukali wa moto huo, lakini kutokana na waundaji wa vyombo hivyo kutumia mchanganyiko wa mabati na plastiki ngumu visivyopenywa na joto, Apollo huonekana kulichana tabaka hilo na kutokea upande wa pili ambao ni anga ya dunia.

    Hivyo basi, mfano huo mdogo unaonesha uimara wa tabaka hilo la 'ozone', ambalo kama ambavyo tumeona huchuja mionzi ya sumu kutoka kwenye mwanga wa jua ili kutolete madhara kwa viumbe duniani.

    Mwanga huo ukisafiri kutoka juani umbali wa kilomita milioni 150 kwa kasi ya kilomita 299,793, hutua duniani ndani ya dakika 8 na sekunde 19 ukiwa tayari umechujwa wakati ukipenya tabaka hilo.

    'Ozone' iligunduliwa mwaka 1913 na wanasayansi wawili wa nchini Ufaransa, Charlest Fabry na Henri Buisson, ambapo kipimo cha kasi ya mwanga kiligunduliwa na mwanasayansia wa anga za juu wa nchini Denmark, Ole Roemer, mwaka 1676.

    7. NGUVU ASILI YA UVUTANO

    Muundo mwingine wa dunia ni nguvu ya asili ya uvutano ya dunia, maarufu kama 'gravitation', ambayo huvuta vitu kuvirejesha chini duniani pale vinaporushwa kwenda juu au vile vinavyoanguka kutoka juu angani.

    Nguvu hiyo ina manufaa makubwa, kwani bila kuwepo duniani binadamu na viumbe wengine wangepeperuka kama karatasi kwenda juu wakati wakitembea juu ya ardhi ya hii.

    Kadhalika, nguvu hiyo husaidia kuvuta hewa ya oksijeni na kuiweka karibu na ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

    Pia, nguvu hiyo husaidia kuiweka dunia, mwezi, jua na sayari zingine katika uwiano wa umbali usio na madhara kutoka kila moja.

    Nguvu hiyo ya asili ndiyo huliweka joto la jua duniani na kubaki kuwa katika kiwango kinachotakiwa, na hivyo kuwezesha viumbe kupata joto la wastani na pia katika kiwango mwanana.

    Nguvu hiyo huvuta mvua kuja duniani na kuwezesha maji ya bahari, maziwa na mito kutulia duniani.

    Mathalani, bila nguvu asili hiyo kuwepo duniani, maji 'yangemwagika' kutoka duniani kwa kutawanyika kama upepo na kupaa kwenda juu angani na kutoweka kabisa.

    Na ndio maana ukirusha maji kwenda juu, hurudi chini ardhini.

    Hebu angalia mfano huu kwamba wanaanga waliokwenda mwenzini walilazimika kuvaa mavazi yenye uzito wa kilo 80 hapa duniani, lakini mavazi hayo kule mwezini yakawa na uzito wa kilo 3.

    Mavazi hayo, yaani viatu, koti, suruali, na kofia nzito yenye miwani maalumu ya kukinga macho dhidi ya mionzi hatari ya jua, vyote kwa pamoja viliunganishwa na kuwa mfano wa sare za 'ovaroli' za mafundi wa magari.

    Mavazi hayo pia mgongoni yakiwa yameunganishwa kwa pamoja na mtungi wa hewa ya oksijeni kwa ajili ya kupumua, yalivaaliwa mahsusi muda mfupi baada ya chombo kutua mwezini.

    Hivyo, msomaji wangu tafakari nini kilisababisha mavazi kuwa mazito hapa duniani, lakini yawe mepesi kule mwezini?

    Jibu ni kwamba nguvu asili ya uvutano hapa duniani ni kubwa kuliko ya kule mwezini.

    Na ndipo tunaona umuhimu wa muundo huo wa nguvu asili ya uvutano, ambapo hapa duniani huvuta vitu kuja chini kwa kasi ya mita 9.81 kwa sekunde, lakini kwa kuwa nguvu ya mwezi ni hafifu, huvuta vitu kwa kasi ndogo ya mita 1.62 kwa sekunde.

    Ingawa nguvu hiyo ya asili iligunduliwa kuwepo duniani miaka mingi iliyopta, mwanafizikia bingwa wa Uingereza, Sir Isaac Newton (1642-1727), ndiye anatambulika kama mgunduzi wa hesabu hizo za nguvu asili hiyo.

    Anaeleza kuwa vitu vyote vyenye maumbo asili, ikiwemo jua, sayari, dunia, mwezi, na vimondo, kila kimoja kina nguvu hiyo katika viwango tofauti.

    Kanuni hiyo, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wake, hueleza kuwa nguvu hiyo ndiyo hufanya jua kuvuta sayari zake ili kulizunguka, huku pia kila sayari ikitumia nguvu 'binafsi' (na kwa uwiano maalumu) kujihami isivutwe hadi kwenda kuligonga jua au kugongana na sayari zingine au vimondo.

    Nguvuasili ya jua ni mita 274 kwa sekunde, ikiwa ni zaidi ya kiasi cha nguvuasili ya kila sayari.

    Muundo huo wa kila sayari kujihami kivyake katika mstari wa njia yake hufahamika kisayansi kama "sayari kuhami mazingira ya njia yake"; yaani kwamba 'a planet has to clear the neighbourhood around its orbit.'

    Newton akiwa amezaliwa 'mtoto-njiti' na baadaye kuibuka kuwa mwenye akili nyingi kiasi cha kukaribia kuwa sawa na mtu wa miujiza, hakuwahi kuoa kutokana na kinachoelezwa kuwa ni " kutokana na kutingwa na shughuli za kimasomo."

    Huoneshwa kuwa muda mwingi alikuwa maabara akifanya tafiti mbalimbali za kisayansi, au akiwa maktaba akijisomea, ama akiandika kitabu, au akifundisha wanafunzi wake.

    Alikuwa bingwa mwenye kipaji cha taaluma nyingi, ikiwemo Fizikia, Kemia, Hisabati, Maarifa ya Anga za Juu, Uchumi, Falsafa, na Theolojia ambayo ni taaluma ya masuala ya kiroho.

    Kwa mujibu wa historia, mwanasayansi huyo gwiji wa kuigwa alihitimu shahada zake zote mbili za sayansi, yaani 'Bachelor' na 'Masters', mwaka 1665 na 1668 katika Chuo Kikuu cha Cambridge, nchini Uingereza.

    Akiwa na umri wa miaka 84, mwanasayansi huyo anayedhaniwa na wengi kuwa bingwa wa hesabu za kisayansi kuliko wote duniani, alifariki mwaka 1727 akiwa usingizini.

    Ripoti ya uchunguzi wa mwili wake huonesha kuwa alikuwa na tatizo la figo, lakini pia alikutwa na kiasi kingi cha zebaki.

    Zebaki hiyo, yamkini, ni kutokana na kudumu mno kwenye maabara za Kemia na Fizikia, ambazo hutumia kemikali aina mbalimbali, zikiwemo hewa za gesi, katika kufanya majaribio ya kisayansi.
    DUNIA NA MAAJABU YAKE (Muundo wa Dunia na Maajabu Yaliyomo) 1. UMRI WA DUNIA HII Dunia yetu ina historia ndefu mno tangu ilipojiunda angani, miaka takribani bilioni 4.5 iliyopita. Tarakimu za umri huo wa miaka bilioni 4.5 ni 4,500,000,000, yaani miaka milioni elfu nne na mia tano iliyopita. Dunia ambayo kwa lugha ya Kiingereza inafahamika vyema kwa jina la 'Earth', pia hujulikana kama 'the World', ikimaanishwa ulimwengu. Aidha, Dunia ni sayari pekee kwenye himaya ya sayari zilizopo chini ya jua ambayo jina lake halitokani na majina ya "Miungu wa Dola" ya Kigiriki au ya Kirumi. Asili ya jina la 'earth' ni 'erde' lenye asili ya nchini Ujerumani, na maana yake ni udongo au ardhi. Mpaka kuweza kupata umri huo wa dunia wanasayansi walifanya kazi ya kutafiti na kisha kuwasilisha matokeo yao kwenye makongamano ya kisayansi duniani, ambapo matokeo hayo yalijadiliwa kwa kina na hatimaye kukubalika kama hivi. Kumbuka katika majadiliano hayo huwepo mivutano mikali miongoni mwa wanasayansi waalikwa, ambapo pia jopo la wanasayansi wanaowasilisha utafiti husika hujikuta wakitakiwa kujibu hoja mbalimbali za wanasayansi wenzao. Kuna wakati baadhi ya matokeo ya tafiti kadhaa hukataliwa, huku watafiti husika wakitakiwa kurejea upya tafiti zao. Wanasayansi hupata umri wa sayari kwa kupima umri wa miamba ya sayari husika, ambapo mwamba wenye umri mkubwa zaidi kuliko miamba yote ndiyo huchukuliwa kuwa umri wa sayari husika. Itakumbukwa kuwa Msahafu wa Biblia (Sura ya Mwanzo 1) husimulia jinsi Mwenyezi Mungu alivyoumba "mbingu na nchi na vyote vilivyomo kwa siku 6," lakini pia Msahafu huohuo kwenye aya zingine hueleza kuwa miaka elfu moja ya duniani yaweza kuwa sawa na siku moja kwenye ya Makazi ya Mwenyezi Mungu. Ni dhahiri kuwa binadamu tukiwa hatuna hoja sahihi kwa maelezo ya aina hiyo, ndipo tunaona ni vyema mambo ya Mwenyezi Mungu kumwachia Yeye Mwenyewe Mwenyezi Mungu. 2. KUUMBIKA DUNIA, SAYARI, JUA, NYOTA Kimsingi, Dunia kama zilivyo sayari zingine zote ilijiunda kutokana na mabaki ya vitu vilivyotumika kuunda Jua. Jua ambalo ni nyota kama zilivyo nyota zote angani, lilijiunda lenyewe kwenye eneo la anga lijulikanalo kama 'Pillars of Creation' (nguzo za uumbaji) katika ukanda wa anga wenye upana ambao huonekana kutokuwa na mwisho. Ukanda huo ujulikanao kama 'Solar Nebula,' umegubikwa na mawingu ya vumbi la huko angani pamoja na aina mbalimbali za gesi na hewa, ikiwemo haidrojeni na heliumu. 'Solar' ni jina la nishati itokanayo na joto la jua, na 'Nebula' kwa lugha ya Kilatini ni "wingu" au vumbi la gesi asilia mithili ya ukungu. Hivyo, 'Solar Nebula' ni ukanda katika anga ya mbali wenye mawingu yaliyosheheni nishati yenye joto, sawa na nishati ya joto la jua. Sasa basi, tunafahamu vyema kuwa jua hutoa mionzi hatari yenye joto kali mithili ya moto mkali, na ambayo ikiboreshwa kisayansi pia huweza kutoa nishati ya umeme. Hivyo, kwa muktadha huo, hebu ngoja sasa tuleta pamoja hewa za gesi, zikiwemo haidrojeni na heliumu, mawingu yenye nishati ya umeme wa jua, vumbi la angani na tufani itokanayo na mchafuko mbaya wa hali ya hewa huko anga za mbali. Na ili kuweza kupata matokeo yanayotakiwa, hebu pia tutambue uwepo wa nguvu kubwa ya asili katika kiwango kijulikanacho kwa jina la "Supernatural Power", ambayo ndiyo huwa kisababishi cha mambo yote. Kisayansi, "Supernatural Power" ni nguvu kubwa ya asili ambayo huendesha mifumo mbalimbali ya asili, ambapo duniani nguvu hiyo hujulikana kama Nguvu ya Mungu. Nguvu asili hiyo, yaani Supernatural Power, husababisha tufani ambayo huvurumisha kwa pamoja vitu vyote hivyo, (gesi, hewa, mawingu yenye nishati ya joto na vumbi la angani) ili kuunda tufani yenye umbo la duara. Duara hiyo ni kama ile itokanayo na kimbunga kikali duniani, na ambacho sasa tutaona kikifungamanisha pamoja vitu vyote hivyo katika mchafuko mkubwa wa hali mbaya ya hewa. Natumia maneno ya msisitizo kuelezea "ukubwa" wa mchafuko huo wa hali ya hewa katika eneo hilo la anga, kwani katika kuunda sayari au nyota nguvuasili kubwa hutumika. Aidha, tufani hiyo ya duara itakayoanza kidogo kidogo kama kimbunga kikali, itazidi kukua hadi kuwa na kipenyo cha takribani kilomita 10 hadi 200 au zaidi na kwendelea. Tufani hiyo ndiyo itavurumisha kwa pamoja gesi na hewa za naitrojeni na heliumu, mawingu ya nishati ya joto na vumbi la angani (kama kifanyavyo kimbunga kikali katika eneo tambarare la duniani). Pia, wakati mchafuko huo wa hali mbaya ya hewa ukiendelea, hebu ngoja sisi watazamaji tujibanze mahali fulani kwa mbali kushuhudia duara hiyo ya tufani ikijizungusha yenyewe bila kukoma kwa kipindi cha miaka mingi. Kitakachofuata ni kuanza kuona kiini cha moto kikianza kujiunda katikati ya duara hiyo ya tufani kali, huku pia nje ya duara hiyo vitu kibao vikivutwa kujiunga na mzunguko wa hiyo tufani ya duara. Vitu hivyo ni pamoja na vumbi zaidi la angani, na gesi zaidi zenye joto kali. Wakati huohuo kipenyo na mzingo wa duara hiyo vitazidi kuongezeka upana na ukubwa, mfano wa duara yenye umbo sawa na la mpira mkubwa wa miguu. Hivyo, baada ya miaka takribani milioni moja tutashangaa kuona lile vumbi likigeuka taratibu kuwa miamba ya moto ndani ya kiini cha tufani hiyo ya duara. Miamba hiyo ni kutokana na lile vumbi la angani ambalo hatimaye limeshikamana pamoja mithili ya zege, na hatimaye kuwa miamba ndani ya tufani ya duara. Sanjari na kuundika huko ndani ya kitovu cha hiyo tufani ya duara, pia kwelekea nje ya duara hiyo utaundika udongo ambao ardhi, mchanga na mawe. Kimsingi, vitu hivyo pia ni matokeo ya lile vumbi la angani ambalo lilikusanywa pamoja na kuvutwa na kasi ya mzunguko wa tufani. Hatua hiyo mpya inatokana na kuwepo mshikamano na mgandamizo wa zile chembechembe za lile vumbivumbi ndani ya tufani. Vurumai hiyo ya mzunguko wa hiyo tufani ya duara yenye vumbi, itazidi kukua hadi kuunda sumaku ya asili ndani ya kile kitovu cha duara ya tufani. Kutokana na duara hiyo ya tufani kuongezeka ukubwa, hatimaye sumaku iliyopo kwenye kitovu cha duara hiyo itaishiwa nguvu ya kwendelea kunasa vumbi zaidi kuja kwenye mzingo wa hiyo duara ya tufani. Kumbuka kuwa wakati huo hiyo duara pia itaunda kimo kutoka kwenye usawa wa ardhi yake kwenda ndani kwenye kitovu chake, na hivyo kuwa duara ya mviringo kama umbo mfano wa mpira mchezo wa miguu. Baada ya kupita maelfu ya miaka mingi, duara hiyo ambayo hapo awali ilianza kama umbo la tufani na kuzidi kukua huko angani, sasa itakuwa na joto kali kupita kiasi na kuanza kung'aa kama jua. Jua hilo, ndiyo nyota mojawapo ya zile ambazo huonekana usiku ziking'aa angani. Lakini pia wakati wa kujiunda nyota hiyo, kama tulivyoona hapo awali, baadhi ya mabaki yake yaliyokuwa yakitawanyika angani wakati ile tufani ya duara ikijizungusha, huweza kujikusanya pamoja na kuunda sayari ambazo huzunguka baadhi ya hizo nyota. Hivyo ndivyo zilivyojiunda sayari zote ambazo huelea kwa kulizunguka jua letu. Mathalani, sayari zote ambazo hulizunguka jua, ikiwemo dunia zilijiunda kutokana na mabaki ya vitu kama gesi, michanga na mawe ambavyo vilitawanyika angani wakati jua likijiunda (kama ambavyo imeelezwa hapo awali). 3. KIINI CHA DUNIA Dunia yetu ambayo wastani wa nusu kipenyo cha umbo lake la duara ni kilomita 6,371, mzingo wake ni kilomita takribani 40,041. Kama zilivyo sayari zote katika himaya ya jua, dunia nayo ilijiunda wakati jua likijiunda lenyewe. Yaani kwamba sayari ni mabaki ya vitu vilivyotumika kuliunda jua. Kadhalika kama zilivyo sayari zingine zote, dunia nayo ina kiini chake ambacho kipo katikati ya ardhi yake. Kiini hicho kina nguvu kubwa ya sumaku ambayo, pamoja na mambo mengineyo, 'huvuta' umbo hilo la duara kutoka juu ya ardhi kwenda katikati ya kiini hicho. Muundo huo ndio hulifungamanisha pamoja umbo la duara la dunia, na hivyo kuzuia umbo hilo lisifumke kutoka ardhini na kusambaratika. Hiyo ni sawa na mpira wa miguu unavyoweza kupasuka na kusambaratika, kama utajazwa upepo kupita kiasi chake. Kiini hicho ambacho kipo katikati kabisa ya dunia, kinajulikanacho kwa jina la kisayansi la 'Inner Core.' Kiini hicho kina joto kali la sentigredi 6,230 ambacho ndio kiasi cha joto la jua. Kiini hicho kina umbo la duara lenye nusu kipenyo cha kilomita 1,250. Kama ingetokea kuchimba ardhi wima kwenda kwenye kiini hicho, mchimbaji angeanza kukutana na joto la kiini hicho kuanzia kimo cha umbali wa kilomita 5,150 kutoka usawa wa juu ya ardhi tunayotembea. Katika historia ya uchimbaji ardhi, kina kirefu kilichowahi kuchimbwa ardhini ni mita 12,345 (kilomita 12.345) huko Sakhalini, nchini Urusi, kwa ajili ya uvunaji wa mafuta ya petroli. Kiini cha dunia kinaundwa na madini mchanganyiko wa nikeli (nickle), chuma (iron) na dhahabu. Kwa mujibu wa utafiti, inakadiriwa kuwa kama dhahabu hiyo ingechimbwa na kuchomwa mpaka kuwa kimiminika sawa na uji na kisha kumwagwa chini, ingeweza kuifunika dunia yote kwa unene wa sentimeta 45. Kiini hicho muhimu kwa uhai wa sayari hii ya dunia kiligunduliwa mwaka 1936 na mtaalamu wa matetemeko ya ardhi wa nchini Denmark, mwanamama Dkt. Inge Lehmann. Dkt. Lehmann alihitimu shahada yake ya kwanza katika fani ya Hisabati mwaka 1910, ya Uzamili mwaka 1920 (zote kutoka Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini mwake), na ile ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza. Alifariki kwa uzee mwaka 1993 akiwa na umri wa miaka 104. 4. MAJI DUNIANI Kupatikana maji kwenye dunia yetu, ni mojawapo ya miundo ambayo haipo katika sayari zingine ambazo tuna taarifa za kitafiti kuzuhusu. Maji ni muhimili muhimu kwa ajili ya uhai wa viumbe wote na mimea, ambavyo kwa pamoja havipo katika sayari zingine za himaya ya jua. Kwa mujibu wa tafiti nyingi ambazo zimefanyika kwa miongo mingi ya miaka kujaribu kubaini nini chanzo cha kuwepo maji duniani, hakuna hata utafiti mmoja ulioonesha kwa usahihi matokeo ya kuridhisha. Miongoni mwa tafiti hizo ni pamoja na ule wa mwaka 2005, ambapo Mkuu wa Idara ya Masomo ya Sayari na Mwezi katika Chuo Kikuu cha Arizona nchini Marekani, Profesa Michael Julian Drake, na mwenzake ambaye ni mtaalamu wa Vimondo, Dkt. Huberto Campins, wa Chuo Kikuu cha Central Florida, walitafiti nini chanzo cha kuwepo maji duniani. Katika mawasilisho yao kwenye kongamano la kisayansi la Chama cha Wanataaluma wa Maarifa ya Anga za Juu (IAU), watafiti hao walikanusha madai ya uwezekano wa dunia hapo kale kugongwa na kimondo kikubwa na kusababisha maji kulipuka kutoka ardhini. Wakiwasilisha matokeo ya utafiti wao kwenye mkutano wa kongamano hilo, magwiji hao wa masuala ya sayari walieleza kwenye waraka wao uitwao "Origin of water on the terrestial planets" (chanzo cha kuwepo maji kwenye sayari). Walidai kuwa maji yaliyopo duniani yaliumbika kwenye ardhi ya dunia tangu mwanzo, wakati ikijiunda angani. Ikumbukwe kuwa eneo la uso wa dunia likiwa ni jumla ya kilomita za mraba milioni 510, asilimia 70.8 ya eneo hilo imefunikwa na maji na asilimia 29.2 ni nchi kavu, ikiwemo milima, mabonde na ardhi tambarare. 5. HEWA YA OKSIJENI Muundo mwingine muhimu katika sayari hii ya dunia ni hewa ambazo ni tawala, yaani Naitrojeni ambayo kwa usahihi imeenea kwa asilimia 78.08 ya hewa yote ya dunia, Oksijeni asilimia 20.95, 'Argon' asilimia 0.93, hewa ya Ukaa (Carbon dioxide) asilimia 0.039, na asilimia moja ni hewa mithili ya mvuke wa maji (water vapour). Hewa ya Oksijeni ambayo ni nguzo muhimu kwa ajili ya uhai wa viumbe wote na pia haipatikani kwenye sayari nyingine chini ya jua, inadhaniwa ilianza kupatikana duniani miaka takribani bilioni 2.5 iliyopita kufuatia "kukomaa kwa kiini cha dunia." Kwa mujibu wa matokeo ya tafiti mbalimbali na nadharia za kisayansi, inaoneshwa kuwa kukomaa kwa kiini hicho cha dunia hatimaye ndiko kulisababisha kuzuka duniani milipuko ya volikano ambayo pia ilisababisha kuzuka mabonde na milima. Inaoneshwa kuwa tayari wakati huo maji yaliishakuwepo duniani, na kuwezesha kuzuka chembechembe ndogo sana za kibakteria zijulikanazo kwa jina la kisayansi la 'cyanobacteria' au 'blue-green algae'. Kwa kutumia mwanga wa jua, maji na hewa ya ukaa, chembechembe hizo ziliweza kuzalisha hewa mbalimbali, ikiwemo 'Carbonhydrates' na Oksijeni. Kwa kuwa hizo chembechembe ndogo za kibakteria huishi baharini, ilikuwa rahisi kwa oksijeni kutokea baharini kupepea na kuenea katika anga ya dunia na kuzuiliwa hapo na nguvu asili ya uvutano ya dunia ili pia ibaki ikienea pote duniani. Mpaka wakati wa kuzuka duniani mimea na viumbe hai miaka takribani bilioni 3.5 iliyopita, tayari oksijeni ilikwa ni tele duniani; na hivyo kutumika kudumisha uhai wa viumbe hadi wakati huu. 6. UKANDA WA 'OZONE' Muundo mwingie muhimu wa asili kwa dunia ni ukanda wa anga ujulikanao kwa jina la 'ozone' ambao umetanda kama 'mwavuli' kwenye anga ya dunia, na kuikinga isidhuriwe na mionzi hatari ya sumu kutoka kwenye Jua. Ukanda huo maarufu kama 'ozone layer' umetanda kuanzia usawa wa kilometa 15 kutoka ardhini kwenda juu angani mpaka ukomo wa kilomita takribani 50, ambapo huchuja asilimia kati ya 97 na 99 ya mionzi hatari kwenye miale ya joto la jua. Miongoni mwa matatizo yanayosababishwa na mionzi hiyo hatari kutoka kwenye jua, ni pamoja na magonjwa ya saratani ya ngozi kwa bianadamu. Pia juu ya ukanda wa tabaka la ozone kuna ukanda mwingine uitwao "atmosphere" ambao ni madhubuti kiasi kwamba vitu vinavyotoka anga za juu na kujaribu kuupenya ili kufika duniani, hukumbana na joto kali na kusambaratishwa kwa kuunguzwa. Si kwamba tabaka hilo lina joto, isipokuwa kasi ya "kuanguka" vitu hivyo kutoka juu angani kuja dunia husababisha msuguano na chembechembe za gesi katika eneo hilo na kuzalisha joto mithili ya ndimi za moto. Picha za video za vyombo vya 'Apollo' vikirejea duniani kutoka mwezini vikiwa na wanaanga ndani yake na kupenya tabaka hilo kwa kasi ya kilomita 39,000 kwa saa, huonekana kughubikwa na ndimi za moto wa rangi ya njano na bluu. Rangi hizo ni ishara ya ukali wa moto huo, lakini kutokana na waundaji wa vyombo hivyo kutumia mchanganyiko wa mabati na plastiki ngumu visivyopenywa na joto, Apollo huonekana kulichana tabaka hilo na kutokea upande wa pili ambao ni anga ya dunia. Hivyo basi, mfano huo mdogo unaonesha uimara wa tabaka hilo la 'ozone', ambalo kama ambavyo tumeona huchuja mionzi ya sumu kutoka kwenye mwanga wa jua ili kutolete madhara kwa viumbe duniani. Mwanga huo ukisafiri kutoka juani umbali wa kilomita milioni 150 kwa kasi ya kilomita 299,793, hutua duniani ndani ya dakika 8 na sekunde 19 ukiwa tayari umechujwa wakati ukipenya tabaka hilo. 'Ozone' iligunduliwa mwaka 1913 na wanasayansi wawili wa nchini Ufaransa, Charlest Fabry na Henri Buisson, ambapo kipimo cha kasi ya mwanga kiligunduliwa na mwanasayansia wa anga za juu wa nchini Denmark, Ole Roemer, mwaka 1676. 7. NGUVU ASILI YA UVUTANO Muundo mwingine wa dunia ni nguvu ya asili ya uvutano ya dunia, maarufu kama 'gravitation', ambayo huvuta vitu kuvirejesha chini duniani pale vinaporushwa kwenda juu au vile vinavyoanguka kutoka juu angani. Nguvu hiyo ina manufaa makubwa, kwani bila kuwepo duniani binadamu na viumbe wengine wangepeperuka kama karatasi kwenda juu wakati wakitembea juu ya ardhi ya hii. Kadhalika, nguvu hiyo husaidia kuvuta hewa ya oksijeni na kuiweka karibu na ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Pia, nguvu hiyo husaidia kuiweka dunia, mwezi, jua na sayari zingine katika uwiano wa umbali usio na madhara kutoka kila moja. Nguvu hiyo ya asili ndiyo huliweka joto la jua duniani na kubaki kuwa katika kiwango kinachotakiwa, na hivyo kuwezesha viumbe kupata joto la wastani na pia katika kiwango mwanana. Nguvu hiyo huvuta mvua kuja duniani na kuwezesha maji ya bahari, maziwa na mito kutulia duniani. Mathalani, bila nguvu asili hiyo kuwepo duniani, maji 'yangemwagika' kutoka duniani kwa kutawanyika kama upepo na kupaa kwenda juu angani na kutoweka kabisa. Na ndio maana ukirusha maji kwenda juu, hurudi chini ardhini. Hebu angalia mfano huu kwamba wanaanga waliokwenda mwenzini walilazimika kuvaa mavazi yenye uzito wa kilo 80 hapa duniani, lakini mavazi hayo kule mwezini yakawa na uzito wa kilo 3. Mavazi hayo, yaani viatu, koti, suruali, na kofia nzito yenye miwani maalumu ya kukinga macho dhidi ya mionzi hatari ya jua, vyote kwa pamoja viliunganishwa na kuwa mfano wa sare za 'ovaroli' za mafundi wa magari. Mavazi hayo pia mgongoni yakiwa yameunganishwa kwa pamoja na mtungi wa hewa ya oksijeni kwa ajili ya kupumua, yalivaaliwa mahsusi muda mfupi baada ya chombo kutua mwezini. Hivyo, msomaji wangu tafakari nini kilisababisha mavazi kuwa mazito hapa duniani, lakini yawe mepesi kule mwezini? Jibu ni kwamba nguvu asili ya uvutano hapa duniani ni kubwa kuliko ya kule mwezini. Na ndipo tunaona umuhimu wa muundo huo wa nguvu asili ya uvutano, ambapo hapa duniani huvuta vitu kuja chini kwa kasi ya mita 9.81 kwa sekunde, lakini kwa kuwa nguvu ya mwezi ni hafifu, huvuta vitu kwa kasi ndogo ya mita 1.62 kwa sekunde. Ingawa nguvu hiyo ya asili iligunduliwa kuwepo duniani miaka mingi iliyopta, mwanafizikia bingwa wa Uingereza, Sir Isaac Newton (1642-1727), ndiye anatambulika kama mgunduzi wa hesabu hizo za nguvu asili hiyo. Anaeleza kuwa vitu vyote vyenye maumbo asili, ikiwemo jua, sayari, dunia, mwezi, na vimondo, kila kimoja kina nguvu hiyo katika viwango tofauti. Kanuni hiyo, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wake, hueleza kuwa nguvu hiyo ndiyo hufanya jua kuvuta sayari zake ili kulizunguka, huku pia kila sayari ikitumia nguvu 'binafsi' (na kwa uwiano maalumu) kujihami isivutwe hadi kwenda kuligonga jua au kugongana na sayari zingine au vimondo. Nguvuasili ya jua ni mita 274 kwa sekunde, ikiwa ni zaidi ya kiasi cha nguvuasili ya kila sayari. Muundo huo wa kila sayari kujihami kivyake katika mstari wa njia yake hufahamika kisayansi kama "sayari kuhami mazingira ya njia yake"; yaani kwamba 'a planet has to clear the neighbourhood around its orbit.' Newton akiwa amezaliwa 'mtoto-njiti' na baadaye kuibuka kuwa mwenye akili nyingi kiasi cha kukaribia kuwa sawa na mtu wa miujiza, hakuwahi kuoa kutokana na kinachoelezwa kuwa ni " kutokana na kutingwa na shughuli za kimasomo." Huoneshwa kuwa muda mwingi alikuwa maabara akifanya tafiti mbalimbali za kisayansi, au akiwa maktaba akijisomea, ama akiandika kitabu, au akifundisha wanafunzi wake. Alikuwa bingwa mwenye kipaji cha taaluma nyingi, ikiwemo Fizikia, Kemia, Hisabati, Maarifa ya Anga za Juu, Uchumi, Falsafa, na Theolojia ambayo ni taaluma ya masuala ya kiroho. Kwa mujibu wa historia, mwanasayansi huyo gwiji wa kuigwa alihitimu shahada zake zote mbili za sayansi, yaani 'Bachelor' na 'Masters', mwaka 1665 na 1668 katika Chuo Kikuu cha Cambridge, nchini Uingereza. Akiwa na umri wa miaka 84, mwanasayansi huyo anayedhaniwa na wengi kuwa bingwa wa hesabu za kisayansi kuliko wote duniani, alifariki mwaka 1727 akiwa usingizini. Ripoti ya uchunguzi wa mwili wake huonesha kuwa alikuwa na tatizo la figo, lakini pia alikutwa na kiasi kingi cha zebaki. Zebaki hiyo, yamkini, ni kutokana na kudumu mno kwenye maabara za Kemia na Fizikia, ambazo hutumia kemikali aina mbalimbali, zikiwemo hewa za gesi, katika kufanya majaribio ya kisayansi.
    0 Comments ·0 Shares ·1K Views
  • SAKATA LA JASUSI SERGEI SKRIPAL NA MWANAE NI UTEKELEZAJI WA OPERATION SARLISBURY ILIYOTEKELEZWA NA RUSSIA, KIMSIMGI NI VITA KATI YA URUSI NA NATO KUJIBU MAPIGO YA UCHAGUZI WA MAREKANI MWAKA 2016.

    Na mhariri wako Comred Mbwana Allyamtu

    Sakata la jaribio la mauaji ya jasusi au mpelelezi, ndumilakuwili wa Urusi na Uingereza, Sergei Skripal na binti yake Yulia katika kitongoji cha Salisbury jijini London nchini Uingereza linachukua sura mpya kila siku.

    Wawili hao walipatikana wakiwa hawajitambui katika eneo la maduka liitwalo Maltings mwanzoni mwa Machi.

    Taarifa kutoka kwa polisi wa Uingereza ambao hushughulikia matukio ya kigaidi wanaamini kuwa jasusi huyo na mwanaye, walivuta hewa iliyokuwa na kemikali yenye sumu iitwayo novichok.

    Kemikali hii hushambulia mfumo wa mfahamu na inasemekana ilitengenezwa katika maabara moja huko Urusi na ilitumika wakati wa Vita vya Pili vya Dunia mwaka 1935 hadi 1945. Kemikali hiyo iliachwa mlangoni mwa nyumba ambayo amekuwa akiishi jasusi huyo na mwanaye katika eneo hilo la Salisbury.

    Mashirika makubwa ya habari nchini Uingereza yameipa umuhimu habari hii ambapo Machi 30, yalitangaza kuwa binti wa Skripal, Yulia hakuwa katika hali tete kiafya.

    Kufuatia tukio hilo Serikali ya Uingereza chini ya Waziri Mkuu, Theresa May iliitupia lawama Serikali ya Urusi kwa kuhusika na uovu huo na ili kuonyesha kuwa imechukia iliamua kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi wapatao 23.

    Urusi imekanusha kuhusika na uovu huo na ikaahidi kuwa kwa kila hukumu itakayotolewa nayo itajibu kwa ukubwa huohuo au zaidi ya hapo, na ikajibu kwa kutoa hukumu ya kisasi kwa kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza na kufunga kituo cha Lugha na Utamaduni cha Uingereza, British Council na imeitaka Uingereza kuwaondoa wanadiplomasia wake wengine wapatao 50 katika kipindi cha mwezi mmoja.
    Ili kuonyesha mshikamano na Uingereza nchi nyingine za Ulaya Magharibi na Australia zimewafukuza wanadiplomasia wa Urusi wanaofikia 150 huku Marekani ikiongoza kwa kufunga ubalozi mdogo wa Urusi katika Jiji la Seattle na kuwafukuza wanadiplomasia 60 kutoka nchi hiyo.

    Urusi nayo haikubaki kimya, Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov ametangaza kuwafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani na vilevile kufunga ubalozi wa Marekani katika mji wa Saint Petersburg na kuahidi kuwa kila nchi iliyohusika na kufukuza wanadiplomasia wake itaadhibiwa vilivyo.

    Kwa ujumla nchi karibu 23 na Umoja wa Kujihami wa nchi za Ulaya Magharibi (Nato) kote ulimwenguni zimeonyesha kukerwa na vitendo vya Urusi kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi tofautitofauti, kama vile kuvamia Ukraine na kulichukua jimbo la Krimea, kuitungua ndege ya Malaysia na kuingilia uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka 2016.
    Siyo mara ya kwanza nchi hizi kuingia katika mzozo wa kidiplomasia kwani mwaka 1986 Ronald Reagan aliyekuwa Rais wa Marekani, aliamuru wanadiplomasia 80 wa Shirikisho la Urusi (USSR) wafukuzwe nchini humo na mwaka 2016, Rais Barak Obama aliwatimua wanadiplomasia 35 kutoka nchi hiyo kwa tuhuma za kudukua kompyuta za chama cha Democratic kwa nia ya kumhujumu mgombea wake wa Rais, Hillary Clinton.

    Mwaka 2006 Skripal alihukumiwa kifungo cha miaka 13, nchini Urusi katika kesi ambayo iliendeshwa katika mahakama ya siri, alipewa haki ya ukimbizi na ukazi nchini Uingereza mwaka 2010 baada ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa katika mtindo ambao ulitumika enzi za vita baridi kuhusiana na shughuli za kijasusi.

    Kulingana na nyaraka za kumbukumbu ambazo vyombo vya habari vya Uingereza vilizipata kutoka makumbusho ya taifa ya Uingereza mwaka 2015, zinaonyesha kuwa Serikali ya Urusi imekuwa ikiichunguza Uingereza muda mrefu lakini kisa kinachojulikana sana ni kile kilichopewa jina la Cambridge Four, ambapo kitengo cha ujasusi cha shirikisho la Urusi (USSR), KGB, katika miaka ya 1930 kabla ya vita vya pili vya dunia kiligundua kuwa Serikali ya Uingereza ilikuwa ikitumia Chuo Kikuu cha Cambridge kama sehemu maalumu ya kuwapata majasusi wachanga wakiwa masomoni. KGB waliwafuata wanafunzi wanne wa wakati huo ambao ni Anthony Blunt, Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess.
    Wasomi hao ambao kwa bahati nzuri kwao KGB walipomaliza masomo yao waliingia kufanya kazi katika Mashirika ya Ujasusi ya Uingereza, MI5 na MI6, na wakawa ni majasusi ndumilakuwili.

    Walifanya kazi yao hadi mwaka 1964 ambapo Anthony Blunt ambaye alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Ujasusi wa ndani, MI5, alikiri kuwa jasusi ndumilakuwili ili asishtakiwe na habari hiyo ilikuja kutolewa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo, Magreth Thatcher alipokuwa akihutubia Bunge mwaka 1979. Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess wao walitimkia Urusi na Serikali ya Uingereza ikawa imekubali yaiishe.

    Kwa hiyo Urusi imekuwa hailali usingizi wakati wote wa miaka ya vita baridi kati ya nchi za Ulaya Mashariki na Magharibi miaka ya 1945 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990, imekuwa ikiingiza wapelelezi wake maeneo mbalimbali katika nchi hizo ili kupata habari nyeti kuhusiana na masuala mbalimbali katika nyanja za uchumi, biashara hasa ya silaha na teknolojia yake na hivi karibuni kuingilia mambo ya siasa za uchaguzi huko Marekani.
    Ukiangalia kisa cha safari hii hakina tofauti sana kile alichofanyiwa Jasusi mwingine wa Urusi Novemba 2006, Alexander Litvinenko ambaye aliwekewa kemikali iitwayo Polonium 210 katika kikombe cha chai katika mgahawa mmoja jijini London.

    Litvinenko alitoroka Urusi baada ya kutofautiana na wenzake katika shirika la kijasusi la nchi hiyo FSB, ambapo aliutuhumu uongozi wa juu wa nchi hiyo kuigeuza nchi hiyo kuwa Taifa la kimafia. akiwa nchini Uingereza, alifanya kazi kama mwandishi wa habari, vitabu na mshauri wa mambo ya usalama.
    Akiwa Uingereza aliandika vitabu viwili, Blowing up Russia: Terror from within na Lubyanka Criminal Group ambapo aliituhumu idara hiyo ya kijasusi kwa vitendo vya mauaji na matumizi ya mabomu na mauaji ya mwandishi wa habari, Anna Politkovskaya kwa amri kutoka kwa Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin.

    Litvinenko akiwa mahututi kitandani hospitalini jijini London aliwatamkia ndugu zake kuwa alikuwa na uhakika kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin ndiye aliyeamuru auawe.
    Serikali ya Uingereza ya wakati huo chini ya Waziri Mkuu, Tony Blair ilifanya upelelezi na kugundua kuwa jasusi huyo siku chache kabla ya kupata mkasa huo alikuwa ametembelewa na jasusi mwingine mstaafu wa FSB ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara, Andrey Lugovoy.
    Serikali ya Uingereza iliitaka Urusi imsalimishe kwake ili afanyiwe mahojiano lakini Urusi ilikataa kwa maelezo kuwa Katiba ya nchi hiyo inakataza raia wake kupelekwa nchi nyingine kufanyiwa mashtaka ya jinai. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulififia kwa muda.

    Serikali ya Uingereza kwa matukio yote haya imekuwa ikiituhumu serikali ya Urusi kwa kile inachoeleza kuwa kemikali hizo haziwezi kuwa mikononi mwa mtu binafsi bila kuwa na kibari cha mamlaka za juu za nchi hiyo.

    Wakati Kim Phillby alipokimbilia Urusi baada ya kushtukia kuwa wenzake walikuwa wanaelekea kumgundua kuwa ni ndumilakuwili, Ofisa mmoja wa ngazi ya juu ndani ya KGB wakati huo alimsifu kuwa alikuwa jasusi mwenye thamani kubwa wa karne iliyopita.

    Urusi imekuwa ikitoa ulinzi wa kiwango cha juu kwa majasusi ndumilakuwili ambao wamefanikiwa kuingia nchini humo baada ya mambo kwenda kombo huko kwao.

    Marekani nayo haikuwahi kupona kwa taasisi zake za kijasusi kuingiliwa na wenzao wa Urusi. Mwaka 2001 Shirika la Ujasusi wa Ndani, FBI, lilimkamata Robert Hanssen ambaye alikuwa mtumishi wake kwa kupeleka taarifa za siri za nchi hiyo kwa Urusi tangu mwaka 1979 kwa kulipwa fedha na almasi.

    Kwa sehemu kubwa shughuli za ujasusi zimekuwa zikifanywa kwa njia ya teknolojia (Artificial Intelligence) ambapo mitambo ya kompyuta na setelaiti na kamera zenye nguvu za kunasa picha hutumika na pale ambapo haiwezekani, inabidi kutumia binadamu (human intelligence) ili kupata habari ambazo ni siri na mataifa karibu yote duniani yameuweka ujasusi kama ni kosa la uhaini kwa yeyote atakayejihusisha nao.
    SAKATA LA JASUSI SERGEI SKRIPAL NA MWANAE NI UTEKELEZAJI WA OPERATION SARLISBURY ILIYOTEKELEZWA NA RUSSIA, KIMSIMGI NI VITA KATI YA URUSI NA NATO KUJIBU MAPIGO YA UCHAGUZI WA MAREKANI MWAKA 2016. Na mhariri wako Comred Mbwana Allyamtu Sakata la jaribio la mauaji ya jasusi au mpelelezi, ndumilakuwili wa Urusi na Uingereza, Sergei Skripal na binti yake Yulia katika kitongoji cha Salisbury jijini London nchini Uingereza linachukua sura mpya kila siku. Wawili hao walipatikana wakiwa hawajitambui katika eneo la maduka liitwalo Maltings mwanzoni mwa Machi. Taarifa kutoka kwa polisi wa Uingereza ambao hushughulikia matukio ya kigaidi wanaamini kuwa jasusi huyo na mwanaye, walivuta hewa iliyokuwa na kemikali yenye sumu iitwayo novichok. Kemikali hii hushambulia mfumo wa mfahamu na inasemekana ilitengenezwa katika maabara moja huko Urusi na ilitumika wakati wa Vita vya Pili vya Dunia mwaka 1935 hadi 1945. Kemikali hiyo iliachwa mlangoni mwa nyumba ambayo amekuwa akiishi jasusi huyo na mwanaye katika eneo hilo la Salisbury. Mashirika makubwa ya habari nchini Uingereza yameipa umuhimu habari hii ambapo Machi 30, yalitangaza kuwa binti wa Skripal, Yulia hakuwa katika hali tete kiafya. Kufuatia tukio hilo Serikali ya Uingereza chini ya Waziri Mkuu, Theresa May iliitupia lawama Serikali ya Urusi kwa kuhusika na uovu huo na ili kuonyesha kuwa imechukia iliamua kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi wapatao 23. Urusi imekanusha kuhusika na uovu huo na ikaahidi kuwa kwa kila hukumu itakayotolewa nayo itajibu kwa ukubwa huohuo au zaidi ya hapo, na ikajibu kwa kutoa hukumu ya kisasi kwa kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza na kufunga kituo cha Lugha na Utamaduni cha Uingereza, British Council na imeitaka Uingereza kuwaondoa wanadiplomasia wake wengine wapatao 50 katika kipindi cha mwezi mmoja. Ili kuonyesha mshikamano na Uingereza nchi nyingine za Ulaya Magharibi na Australia zimewafukuza wanadiplomasia wa Urusi wanaofikia 150 huku Marekani ikiongoza kwa kufunga ubalozi mdogo wa Urusi katika Jiji la Seattle na kuwafukuza wanadiplomasia 60 kutoka nchi hiyo. Urusi nayo haikubaki kimya, Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov ametangaza kuwafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani na vilevile kufunga ubalozi wa Marekani katika mji wa Saint Petersburg na kuahidi kuwa kila nchi iliyohusika na kufukuza wanadiplomasia wake itaadhibiwa vilivyo. Kwa ujumla nchi karibu 23 na Umoja wa Kujihami wa nchi za Ulaya Magharibi (Nato) kote ulimwenguni zimeonyesha kukerwa na vitendo vya Urusi kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi tofautitofauti, kama vile kuvamia Ukraine na kulichukua jimbo la Krimea, kuitungua ndege ya Malaysia na kuingilia uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka 2016. Siyo mara ya kwanza nchi hizi kuingia katika mzozo wa kidiplomasia kwani mwaka 1986 Ronald Reagan aliyekuwa Rais wa Marekani, aliamuru wanadiplomasia 80 wa Shirikisho la Urusi (USSR) wafukuzwe nchini humo na mwaka 2016, Rais Barak Obama aliwatimua wanadiplomasia 35 kutoka nchi hiyo kwa tuhuma za kudukua kompyuta za chama cha Democratic kwa nia ya kumhujumu mgombea wake wa Rais, Hillary Clinton. Mwaka 2006 Skripal alihukumiwa kifungo cha miaka 13, nchini Urusi katika kesi ambayo iliendeshwa katika mahakama ya siri, alipewa haki ya ukimbizi na ukazi nchini Uingereza mwaka 2010 baada ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa katika mtindo ambao ulitumika enzi za vita baridi kuhusiana na shughuli za kijasusi. Kulingana na nyaraka za kumbukumbu ambazo vyombo vya habari vya Uingereza vilizipata kutoka makumbusho ya taifa ya Uingereza mwaka 2015, zinaonyesha kuwa Serikali ya Urusi imekuwa ikiichunguza Uingereza muda mrefu lakini kisa kinachojulikana sana ni kile kilichopewa jina la Cambridge Four, ambapo kitengo cha ujasusi cha shirikisho la Urusi (USSR), KGB, katika miaka ya 1930 kabla ya vita vya pili vya dunia kiligundua kuwa Serikali ya Uingereza ilikuwa ikitumia Chuo Kikuu cha Cambridge kama sehemu maalumu ya kuwapata majasusi wachanga wakiwa masomoni. KGB waliwafuata wanafunzi wanne wa wakati huo ambao ni Anthony Blunt, Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess. Wasomi hao ambao kwa bahati nzuri kwao KGB walipomaliza masomo yao waliingia kufanya kazi katika Mashirika ya Ujasusi ya Uingereza, MI5 na MI6, na wakawa ni majasusi ndumilakuwili. Walifanya kazi yao hadi mwaka 1964 ambapo Anthony Blunt ambaye alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Ujasusi wa ndani, MI5, alikiri kuwa jasusi ndumilakuwili ili asishtakiwe na habari hiyo ilikuja kutolewa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo, Magreth Thatcher alipokuwa akihutubia Bunge mwaka 1979. Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess wao walitimkia Urusi na Serikali ya Uingereza ikawa imekubali yaiishe. Kwa hiyo Urusi imekuwa hailali usingizi wakati wote wa miaka ya vita baridi kati ya nchi za Ulaya Mashariki na Magharibi miaka ya 1945 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990, imekuwa ikiingiza wapelelezi wake maeneo mbalimbali katika nchi hizo ili kupata habari nyeti kuhusiana na masuala mbalimbali katika nyanja za uchumi, biashara hasa ya silaha na teknolojia yake na hivi karibuni kuingilia mambo ya siasa za uchaguzi huko Marekani. Ukiangalia kisa cha safari hii hakina tofauti sana kile alichofanyiwa Jasusi mwingine wa Urusi Novemba 2006, Alexander Litvinenko ambaye aliwekewa kemikali iitwayo Polonium 210 katika kikombe cha chai katika mgahawa mmoja jijini London. Litvinenko alitoroka Urusi baada ya kutofautiana na wenzake katika shirika la kijasusi la nchi hiyo FSB, ambapo aliutuhumu uongozi wa juu wa nchi hiyo kuigeuza nchi hiyo kuwa Taifa la kimafia. akiwa nchini Uingereza, alifanya kazi kama mwandishi wa habari, vitabu na mshauri wa mambo ya usalama. Akiwa Uingereza aliandika vitabu viwili, Blowing up Russia: Terror from within na Lubyanka Criminal Group ambapo aliituhumu idara hiyo ya kijasusi kwa vitendo vya mauaji na matumizi ya mabomu na mauaji ya mwandishi wa habari, Anna Politkovskaya kwa amri kutoka kwa Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin. Litvinenko akiwa mahututi kitandani hospitalini jijini London aliwatamkia ndugu zake kuwa alikuwa na uhakika kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin ndiye aliyeamuru auawe. Serikali ya Uingereza ya wakati huo chini ya Waziri Mkuu, Tony Blair ilifanya upelelezi na kugundua kuwa jasusi huyo siku chache kabla ya kupata mkasa huo alikuwa ametembelewa na jasusi mwingine mstaafu wa FSB ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara, Andrey Lugovoy. Serikali ya Uingereza iliitaka Urusi imsalimishe kwake ili afanyiwe mahojiano lakini Urusi ilikataa kwa maelezo kuwa Katiba ya nchi hiyo inakataza raia wake kupelekwa nchi nyingine kufanyiwa mashtaka ya jinai. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulififia kwa muda. Serikali ya Uingereza kwa matukio yote haya imekuwa ikiituhumu serikali ya Urusi kwa kile inachoeleza kuwa kemikali hizo haziwezi kuwa mikononi mwa mtu binafsi bila kuwa na kibari cha mamlaka za juu za nchi hiyo. Wakati Kim Phillby alipokimbilia Urusi baada ya kushtukia kuwa wenzake walikuwa wanaelekea kumgundua kuwa ni ndumilakuwili, Ofisa mmoja wa ngazi ya juu ndani ya KGB wakati huo alimsifu kuwa alikuwa jasusi mwenye thamani kubwa wa karne iliyopita. Urusi imekuwa ikitoa ulinzi wa kiwango cha juu kwa majasusi ndumilakuwili ambao wamefanikiwa kuingia nchini humo baada ya mambo kwenda kombo huko kwao. Marekani nayo haikuwahi kupona kwa taasisi zake za kijasusi kuingiliwa na wenzao wa Urusi. Mwaka 2001 Shirika la Ujasusi wa Ndani, FBI, lilimkamata Robert Hanssen ambaye alikuwa mtumishi wake kwa kupeleka taarifa za siri za nchi hiyo kwa Urusi tangu mwaka 1979 kwa kulipwa fedha na almasi. Kwa sehemu kubwa shughuli za ujasusi zimekuwa zikifanywa kwa njia ya teknolojia (Artificial Intelligence) ambapo mitambo ya kompyuta na setelaiti na kamera zenye nguvu za kunasa picha hutumika na pale ambapo haiwezekani, inabidi kutumia binadamu (human intelligence) ili kupata habari ambazo ni siri na mataifa karibu yote duniani yameuweka ujasusi kama ni kosa la uhaini kwa yeyote atakayejihusisha nao.
    0 Comments ·0 Shares ·2K Views
  • *VATICAN CITY......
    Nchi? Mji? Serikali au Kampuni?*

    Nadhani moja kati ya maeneo ambayo yamekuwa tata zaidi kuyaelewa basi ni mji wa Vatican… tukiachilia mbali kuhusu utata/ugumu wa kuelewa mfumo wake wa uendeshaji na historia yake lakini swali jepesi zaidi ambalo kila mtu huwa anahisi analifahamu jawabu lake ni kuhusu utambulisho wa Vatican.!! Ni swali jepesi ambalo karibia kila mtu anadhani ana jawabu sahihi lakini uhalisia ni kwamba asilimia kubwa ya watu wana jawabu lisilo sahihi… kila mtu atakueleza kwamba Vatican ni nchi inayojitegemea lakini hii ni robo tu au thelethi ya jawabu…

    Leo nami niandike kidogo kuhusu eneo hili… na kwenye andishi hili fupi nitaeleza utambulisho wa Vatican ukoje kwa usahihi wake kabisa!

    *Muhimu:* andishi hili halilengi kukosoa au kupinga imani ya mtu yeyote. Tahadhali zote zinazingatiwa ili kulinda heshima ya imani ya kila mtu.

    Tuendelee…

    Vatican City, ndio makao makuu ya Kanisa Katoliki na nyumba ya maisha ya Papa, kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki.
    Vatican ndio nchi ndogo zaidi duniani kiasi kwamba unaweza kuizunguka yote kwa mzingo (circumference) kwa muda wa dakika arobaini tu kwa kutembea kwa miguu.

    Ni ajabu sana kwa namna gani nchi ndogo kiasi hiki imetokea na je ni nchi kama nchi nyingine???

    Jibu la swali hili ni refu sana kiaisi kwamba unaweza hata kusoma darasani kwa mwaka mzima lakini nitajaribu kuweka katika maneno machache sana ya kueleweka kwa wepesi…

    Miaka ya kale sana Papa wa Kanisa Katoliki alikuwa ni mtawala wa nchi ambayo ilikuwa inajiita *Himaya ya Papa (Papal State)* ambayo inarandana kabisa na eneo la sasa la nchi nzima ya Italia. Hii ilikuwa takribani miaka ya 754 mpaka miaka ya 1870.
    Ni katika kipindi hiki ambacho Papa aliteua eneo ndani ya nchi yake Papal State ambalo likajengwa *St. Peters Basilica*, kanisa kubwa zaidi duniani na lenye nakshi adhimu zaidi. Eneo hili ambalo St. Peters Basilica ilijengwa ni eneo fulani hivi la muinuko ambako hapo hapo pia yalijengwa makazi ya Papa kuishi.

    Ikumbukwe kwamba katika kipindi hiki hiki cha uwepo wa himaya ya Papal State pia ilikuwa inapakana na Ufalme wa Italy (Kingdom of Italy) japo kila moja ilikuwa inajitegemea.

    Japokuwa himaya hizi mbili zilikuwa jirani lakini kulikuwa na uhasama fulani kati yao. Hii ilifanya Papa kujenga ukuta mkubwa kuzunguka makazi yake ya kuishi na kanisa la St. Peters Basilica.

    Kadiri miaka ilivyozidi kwenda uhasama kati ya Italy Kingdom na Papal State ulipanuka zaidi na ilifikia hatua Kingdom of Italy wakafanya uamuzi wa kuiteka Papal State na kuifanya makao makuu ya nchi yake (Rome ya sasa).

    Wakati na baada ya uvamizi huu wa Kingdom of Italy kuteka Papal State, Papa mwenyewe alikuwa amejificha ndani ya makazi yake yaliyozungushiwa ukuta ambao nimeeleza awali.
    Ikumbukwe kwamba hata kipindi hiki Kanisa Katoliki tayari lilikuwa na ushawishi mkubwa duniani kwa hiyo Kingdom of Italy walihofia kuingiza majeshi kwa nguvu ndani ya makazi ya Papa na kumkamata kuogopa umaarufu wao kimataifa kudondoka.

    Kwa hiyo majeshi ya Kingdom of Italy yalibakia nje mwa kuta za Vatican kwa miaka mingi sana wakiamini kwamba iko siku Papa atakata tamaa na kujisalimisha.
    Lakini hii haikufua dafu kwani miongo ilipita na Papa hakujisalimisha kwa kutoka nje ya kuta za Vatican. Takribani Mapapa watano kwa muda wa karibia miaka sitini waliishi ndani ya kuta za Vatican katika hali hii. Mapapa hao kwa majina yao walikuwa ni Papa Pius IX, Papa Leo XIII, Papa Pius X, Papa Benedict XV na Papa Pius XI.

    Hali hii ilisababisha Mapapa kutotambua Kingdom of Italy na pia kulalamika mara kwa mara kwa jamii ya kimataifa kwamba wanaishi kama wafungwa ndani ya kuta za Vatican kutokana na ukandamizaji wa Kingdom of Italy na hofu waliyonayo kutoka nje ya kuta za Vatican.

    Hii inatufikisha mpaka miaka ya 1920s wakati wa utawala wa Benito Mussolini akiwa Waziri Mkuu wa Italy.
    Mussolini alichoshwa na malalamiko haya ya Papa na majibizano ya kila mara huku Papa bado akishikilia msimamo wa kutoitambua Italy

    Mussolini mwanasiasa mahiri kama ajulikanavyo akaona fursa hapa ya kuandika jina lake kwenye vitabu vya historia.
    Akapendekeza makubaliano maalumu kwa Papa. Kwamba atafanya yafuatayo;

    1. Italy itatoa ardhi ya Vatican kwa Papa na iwe himaya/nchi iliyo chini ya utawala wa Papa.

    2. Italy itatoa fedha kama fidia kwa Papa kutokana na manyanyaso ya miaka yote.

    Mussolini alihitaji Papa kufanya yafuatayo;

    1. Papa atambue Italy kuwa ni nchi.

    2. Papa asijihusishe wala kutoa maoni yoyote kuhusu masuala ya kisiasa na vita.

    Papa na Mussolini wakafikia makubaliano na mikataba ikasainiwa na hapa ndipo taifa dogo zaidi duniani likazaliwa, Vatican.

    Vatican ikaanza kujiendesha kama taifa linalojitegemea kwa kuwa na sarafu yake, serikali yake, Polisi wake, jela yake (ndio kuna jela Vatican), Posta yake, Plate number zake, Passport zake na kadhalika na kadhalika.

    Vatican si kama nchi nyingine duniani kwa hiyo usidhani kwamba tayari umeielewa Vatican, hicho nilichoeleza ni theluthi tu mkanganyiko wa kuielewa Vatican kama nchi… kunywa tena glass ya maji and relax!! Nitaeleza tena kidogo…

    Ili kuielewa Vatican walau kiduchu kuna watu wawili tunapaswa kuwafahamu;

    1. Papa

    2. Mfalme wa Vatican

    Na pia kuna vitu viwili vya kuvielewa;

    1. The Holy See

    2. Vatican City

    Tuanze kimoja kimoja…

    *1. Papa*
    Hii sihitaji kueleza sana karibia wote tunafahamu. Lakini kwa msingi wa awali kabisa, Papa ni askofu wa Wakatoliki wote waliopo Rome/Vatican lakini kwa kuwa yeye pia ndiye kiongozi wa Wakatoliki wote duniani ndio sababu ya Uaskofu wake kuwa Papa.

    *2. The Holy See*
    Kabla sijaeleza chochote kuhusu Mfalme wa Vatican kwanza nieleze kuhusu The Holy See. Hili ni moja ya mambo magumu zaidi kuyaelewa kuhusu Vatican. Nitaeleza kwa lugha nyepesi na uchache ili tusipasue vichwa kwa mikanganyiko.

    Kwa tafsiri nyepesi Holy See ni 'Throne' ya Papa (nakosa neno zuri la kiswahili, sipendezwi sana na tafsiri ya 'Kiti cha Enzi').

    Ni kwamba, maaskofu wote ndani ya kanisa Katoliki wanakuwa na 'throne' lakini kwa kuwa 'throne' ya Papa ni maalumu (kiongozi wa Wakatoliki wote duniani) kwa hiyo throne yake inakuwa muhimu zaidi na inaitwa 'The Holy See'.
    Mapapa wanabadilika lakini The Holy See iko na itaendelea kuwepo siku zote.

    Yaani kwa mfano Papa anapofariki au kustaafu kama tulivyoona mwaka juzi, Makadinali wanapokusanyika Vatican kwa uhalisia wanaenda kumchagua Kadinali mwenzao ambaye atakalia 'throne' ya 'Holy See'.

    Kwa 'angle' nyingine tunaweza kusema kwamba 'The Holy See' ndiyo sheria na mamlaka yote inayofanya kanisa Katoliki kuwa namna lilivyo. Pia sheria zote za kanisa Katoliki na mfumo wake unatengenezwa na The Holy See (sio Papa).

    Pia tunaweza kusema kwamba Benito Mussolini alipofanya makubaliano na Vatican aliingia mkataba ule na 'The Holy See'.

    Pia unaweza usiamini lakini katika nyanja za sheria za kimataifa 'The Holy See' inatambulika kama mtu/kampuni halisi ambaye amesajiliwa kisheria.

    Labda nitumie lugha nyepesi zaidi ya mfano… ukitaka kuelewa The Holy See, chukulia mfano huu kwamba Holy See ni "Catholic Church Inc." alafu Papa ndiye CEO.

    Nimejitahidi kueleza kwa kifupi na kwa wepesi niwezavyo, kuielewa kwa undani zaidi The Holy See labda tunapaswa kuandaa andishi maalumu mahususi kwa ajili yake tu.

    *3. Mfalme wa Vatican*
    Mfalme wa Vatican ni mtawala mwenye mamlaka yote juu ya nchi ya Vatican na hii inaifanya Vatican kuwa moja kati ya nchi sita pekee duniani zenye wafalme wenye mamlaka kamili (absolute monarchy). Nchi nyingine tano ni Saudi Arabia, Brunei, Oman, Qatar, Oman na Swaziland.

    Hii ndio sababu kwanini Vatican hawawezi kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa sababu EU wanakubali nchi zenye mfumo wa kidemokrasia pekee.
    Japokuwa Vatican ina tawi la 'bunge' ambalo linaundwa na makadinali wa Vatican ambayo wanatunga sheria za 'nchi' lakini bado mfalme wa Vatican anauwezo wa kuveto maamuzi yoyote ambayo wamefikia.

    *Swali: Kwanini hatusikii chochote kuhusu Mfalme wa Vatican??*

    Ni kwa sababu Mfalme wa Vatican na Papa ni wajibu na mamlaka mbili tofauti lakini zinakaliwa na mtu mmoja, Papa wa Kanisa Katoliki.

    Hii inatupa kitu kingine cha kipekee kuhusu Vatican.

    Papa anachaguliwa na makadinali wenzake - Demokrasia.
    Lakini Mfalme hachaguliwi.

    Hii inafanya Vatican kuwa nchi pekee kwenye historia ya dunia kuwa na Mfalme mwenye mamlaka kamili ambaye si wa kurithi na anapatikana kidemokrasia (Elected non-heridetary absolute Monarchy).

    Kwa hiyo Papa kulingana na muktadha na mazingira ya suala husika kuna muda anatumia mamlaka yake kama Papa na muda mwingine inampasa kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Vatican.

    Bado kuna mkanganyiko???

    Zingatia mfano huu rahisi; tuseme kwamba kuna kampuni fulani kubwa ya kimataifa inaitwa Aman Enterprises (The Holy See kwa mada yetu). Aman Enterprises wakafanikiwa kuishwishi Tanzania kuwapatia kisiwa cha Mbudya na Bold Enterprises wanakibadilisha kisiwa cha Mbudya kuwa nchi inayojitegemea, labda iitwe Aman Land (Vatican City kwa mfano wetu).
    Sasa CEO wa kampuni Bwana Aman (Papa kwa mada yetu) anahamishiamanya makao makuu ya kampuni mpaka Aman Land. Kwa kuwa Aman Land sasa ni nchi, CEO wa kampuni anakuwa pia mtawala wa nchi hii, Mfalme.

    .
    Kwa hiyo kwa manufaa ya kampuni kutumia 'connection' zake za kimataifa kunufaisha taifa lake la Aman Land ni vyema kutumia mamlaka kama CEO wa Bold Enterprises na kuna muda akihitaji nchi yake ya Aman Land kutunga sheria na taratibu ambazo zitanufaisha kampuni izidi kushamiri ni vyema kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Aman Land.

    Haya ndio mamlaka mawili yaliyo chini ya mtu mmoja ndani ya vatican, Papa na Mfalme wa Vatican.

    Bado kuna mkanganyiko???

    Kama haujaelewa sawia usihofu kwa maana bado kuna hata nchi nyingine duniani bado hawaelewi sawa sawa mfumo mzima wa Vatican.

    Mfano, Umoja wa Mataifa wamekubali The Holy See (corporation) kama mwanachama wake lakini sio Vatican City nchi yenyewe.

    Passports za raia wa Vatican zinatolewa na The Holy See na sio Vatican na zinakubalika kwenye nchi nyingine japokuwa The Holy See kimataifa inatambulika kisheria kama Kampuni inayojitegemea.

    Na hapa tuongee kiduchu pia kuhusu raia wa Vatican. Katika nchi nyingine raia wa wanaongezeka kutokana na kuzaliana lakini hapa Vatican hakuna hilo kutokana na idadi ndogo ya wanaweka kiasi kwamba karibia ni asilimia sufuri. Namna pekee ya kuwa raia wa Vatican ni kwa kupewa uraia na Mfalme wa Vatican ili uishi Vatican kama moja wa wasaidizi wa Papa (ambaye ndiye mfalme). Kwa hiyo siku ukiacha kazi, yaani usaidizi wako kwa Papa ukifikia kikomo, Mfalme wa Vatican (ambayr ndiye Papa) anaondoa uraia wako na unarudi kwenu.

    Katika muda wowote ule raia wa nchi ya Vatican wanakadiriwa kuwa jumla karibia ya 500 ambao ndio idadi ndogo zaidi ya raia kwa nchi na ndogo kushinda hata idadi ya watu wanaoishi kwenye ghorofa moja kwenye nchi nyingi.
    Na raia wote hawa ni wafanyakazi wa Papa/The Holy See ambao wanapewa uraia na Mfalme (ambaye ndiye Papa) ambapo wanafanya kazi kama Makadinali, Wanadiplomasia, walinzi au kazi nyingine za kikanisa.

    Kwa ufupi sana hii ndio picha halisi ya nchi ya Vatican… na hapa ndipo ambapo maisha ya kiroho ya wafuasi zaidi ya Billioni 2 yanapoendeshwa…

    *VATICAN CITY...... Nchi? Mji? Serikali au Kampuni?* Nadhani moja kati ya maeneo ambayo yamekuwa tata zaidi kuyaelewa basi ni mji wa Vatican… tukiachilia mbali kuhusu utata/ugumu wa kuelewa mfumo wake wa uendeshaji na historia yake lakini swali jepesi zaidi ambalo kila mtu huwa anahisi analifahamu jawabu lake ni kuhusu utambulisho wa Vatican.!! Ni swali jepesi ambalo karibia kila mtu anadhani ana jawabu sahihi lakini uhalisia ni kwamba asilimia kubwa ya watu wana jawabu lisilo sahihi… kila mtu atakueleza kwamba Vatican ni nchi inayojitegemea lakini hii ni robo tu au thelethi ya jawabu… Leo nami niandike kidogo kuhusu eneo hili… na kwenye andishi hili fupi nitaeleza utambulisho wa Vatican ukoje kwa usahihi wake kabisa! *Muhimu:* andishi hili halilengi kukosoa au kupinga imani ya mtu yeyote. Tahadhali zote zinazingatiwa ili kulinda heshima ya imani ya kila mtu. Tuendelee… Vatican City, ndio makao makuu ya Kanisa Katoliki na nyumba ya maisha ya Papa, kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki. Vatican ndio nchi ndogo zaidi duniani kiasi kwamba unaweza kuizunguka yote kwa mzingo (circumference) kwa muda wa dakika arobaini tu kwa kutembea kwa miguu. Ni ajabu sana kwa namna gani nchi ndogo kiasi hiki imetokea na je ni nchi kama nchi nyingine??? Jibu la swali hili ni refu sana kiaisi kwamba unaweza hata kusoma darasani kwa mwaka mzima lakini nitajaribu kuweka katika maneno machache sana ya kueleweka kwa wepesi… Miaka ya kale sana Papa wa Kanisa Katoliki alikuwa ni mtawala wa nchi ambayo ilikuwa inajiita *Himaya ya Papa (Papal State)* ambayo inarandana kabisa na eneo la sasa la nchi nzima ya Italia. Hii ilikuwa takribani miaka ya 754 mpaka miaka ya 1870. Ni katika kipindi hiki ambacho Papa aliteua eneo ndani ya nchi yake Papal State ambalo likajengwa *St. Peters Basilica*, kanisa kubwa zaidi duniani na lenye nakshi adhimu zaidi. Eneo hili ambalo St. Peters Basilica ilijengwa ni eneo fulani hivi la muinuko ambako hapo hapo pia yalijengwa makazi ya Papa kuishi. Ikumbukwe kwamba katika kipindi hiki hiki cha uwepo wa himaya ya Papal State pia ilikuwa inapakana na Ufalme wa Italy (Kingdom of Italy) japo kila moja ilikuwa inajitegemea. Japokuwa himaya hizi mbili zilikuwa jirani lakini kulikuwa na uhasama fulani kati yao. Hii ilifanya Papa kujenga ukuta mkubwa kuzunguka makazi yake ya kuishi na kanisa la St. Peters Basilica. Kadiri miaka ilivyozidi kwenda uhasama kati ya Italy Kingdom na Papal State ulipanuka zaidi na ilifikia hatua Kingdom of Italy wakafanya uamuzi wa kuiteka Papal State na kuifanya makao makuu ya nchi yake (Rome ya sasa). Wakati na baada ya uvamizi huu wa Kingdom of Italy kuteka Papal State, Papa mwenyewe alikuwa amejificha ndani ya makazi yake yaliyozungushiwa ukuta ambao nimeeleza awali. Ikumbukwe kwamba hata kipindi hiki Kanisa Katoliki tayari lilikuwa na ushawishi mkubwa duniani kwa hiyo Kingdom of Italy walihofia kuingiza majeshi kwa nguvu ndani ya makazi ya Papa na kumkamata kuogopa umaarufu wao kimataifa kudondoka. Kwa hiyo majeshi ya Kingdom of Italy yalibakia nje mwa kuta za Vatican kwa miaka mingi sana wakiamini kwamba iko siku Papa atakata tamaa na kujisalimisha. Lakini hii haikufua dafu kwani miongo ilipita na Papa hakujisalimisha kwa kutoka nje ya kuta za Vatican. Takribani Mapapa watano kwa muda wa karibia miaka sitini waliishi ndani ya kuta za Vatican katika hali hii. Mapapa hao kwa majina yao walikuwa ni Papa Pius IX, Papa Leo XIII, Papa Pius X, Papa Benedict XV na Papa Pius XI. Hali hii ilisababisha Mapapa kutotambua Kingdom of Italy na pia kulalamika mara kwa mara kwa jamii ya kimataifa kwamba wanaishi kama wafungwa ndani ya kuta za Vatican kutokana na ukandamizaji wa Kingdom of Italy na hofu waliyonayo kutoka nje ya kuta za Vatican. Hii inatufikisha mpaka miaka ya 1920s wakati wa utawala wa Benito Mussolini akiwa Waziri Mkuu wa Italy. Mussolini alichoshwa na malalamiko haya ya Papa na majibizano ya kila mara huku Papa bado akishikilia msimamo wa kutoitambua Italy Mussolini mwanasiasa mahiri kama ajulikanavyo akaona fursa hapa ya kuandika jina lake kwenye vitabu vya historia. Akapendekeza makubaliano maalumu kwa Papa. Kwamba atafanya yafuatayo; 1. Italy itatoa ardhi ya Vatican kwa Papa na iwe himaya/nchi iliyo chini ya utawala wa Papa. 2. Italy itatoa fedha kama fidia kwa Papa kutokana na manyanyaso ya miaka yote. Mussolini alihitaji Papa kufanya yafuatayo; 1. Papa atambue Italy kuwa ni nchi. 2. Papa asijihusishe wala kutoa maoni yoyote kuhusu masuala ya kisiasa na vita. Papa na Mussolini wakafikia makubaliano na mikataba ikasainiwa na hapa ndipo taifa dogo zaidi duniani likazaliwa, Vatican. Vatican ikaanza kujiendesha kama taifa linalojitegemea kwa kuwa na sarafu yake, serikali yake, Polisi wake, jela yake (ndio kuna jela Vatican), Posta yake, Plate number zake, Passport zake na kadhalika na kadhalika. Vatican si kama nchi nyingine duniani kwa hiyo usidhani kwamba tayari umeielewa Vatican, hicho nilichoeleza ni theluthi tu mkanganyiko wa kuielewa Vatican kama nchi… kunywa tena glass ya maji and relax!! Nitaeleza tena kidogo… Ili kuielewa Vatican walau kiduchu kuna watu wawili tunapaswa kuwafahamu; 1. Papa 2. Mfalme wa Vatican Na pia kuna vitu viwili vya kuvielewa; 1. The Holy See 2. Vatican City Tuanze kimoja kimoja… *1. Papa* Hii sihitaji kueleza sana karibia wote tunafahamu. Lakini kwa msingi wa awali kabisa, Papa ni askofu wa Wakatoliki wote waliopo Rome/Vatican lakini kwa kuwa yeye pia ndiye kiongozi wa Wakatoliki wote duniani ndio sababu ya Uaskofu wake kuwa Papa. *2. The Holy See* Kabla sijaeleza chochote kuhusu Mfalme wa Vatican kwanza nieleze kuhusu The Holy See. Hili ni moja ya mambo magumu zaidi kuyaelewa kuhusu Vatican. Nitaeleza kwa lugha nyepesi na uchache ili tusipasue vichwa kwa mikanganyiko. Kwa tafsiri nyepesi Holy See ni 'Throne' ya Papa (nakosa neno zuri la kiswahili, sipendezwi sana na tafsiri ya 'Kiti cha Enzi'). Ni kwamba, maaskofu wote ndani ya kanisa Katoliki wanakuwa na 'throne' lakini kwa kuwa 'throne' ya Papa ni maalumu (kiongozi wa Wakatoliki wote duniani) kwa hiyo throne yake inakuwa muhimu zaidi na inaitwa 'The Holy See'. Mapapa wanabadilika lakini The Holy See iko na itaendelea kuwepo siku zote. Yaani kwa mfano Papa anapofariki au kustaafu kama tulivyoona mwaka juzi, Makadinali wanapokusanyika Vatican kwa uhalisia wanaenda kumchagua Kadinali mwenzao ambaye atakalia 'throne' ya 'Holy See'. Kwa 'angle' nyingine tunaweza kusema kwamba 'The Holy See' ndiyo sheria na mamlaka yote inayofanya kanisa Katoliki kuwa namna lilivyo. Pia sheria zote za kanisa Katoliki na mfumo wake unatengenezwa na The Holy See (sio Papa). Pia tunaweza kusema kwamba Benito Mussolini alipofanya makubaliano na Vatican aliingia mkataba ule na 'The Holy See'. Pia unaweza usiamini lakini katika nyanja za sheria za kimataifa 'The Holy See' inatambulika kama mtu/kampuni halisi ambaye amesajiliwa kisheria. Labda nitumie lugha nyepesi zaidi ya mfano… ukitaka kuelewa The Holy See, chukulia mfano huu kwamba Holy See ni "Catholic Church Inc." alafu Papa ndiye CEO. Nimejitahidi kueleza kwa kifupi na kwa wepesi niwezavyo, kuielewa kwa undani zaidi The Holy See labda tunapaswa kuandaa andishi maalumu mahususi kwa ajili yake tu. *3. Mfalme wa Vatican* Mfalme wa Vatican ni mtawala mwenye mamlaka yote juu ya nchi ya Vatican na hii inaifanya Vatican kuwa moja kati ya nchi sita pekee duniani zenye wafalme wenye mamlaka kamili (absolute monarchy). Nchi nyingine tano ni Saudi Arabia, Brunei, Oman, Qatar, Oman na Swaziland. Hii ndio sababu kwanini Vatican hawawezi kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa sababu EU wanakubali nchi zenye mfumo wa kidemokrasia pekee. Japokuwa Vatican ina tawi la 'bunge' ambalo linaundwa na makadinali wa Vatican ambayo wanatunga sheria za 'nchi' lakini bado mfalme wa Vatican anauwezo wa kuveto maamuzi yoyote ambayo wamefikia. *Swali: Kwanini hatusikii chochote kuhusu Mfalme wa Vatican??* Ni kwa sababu Mfalme wa Vatican na Papa ni wajibu na mamlaka mbili tofauti lakini zinakaliwa na mtu mmoja, Papa wa Kanisa Katoliki. Hii inatupa kitu kingine cha kipekee kuhusu Vatican. Papa anachaguliwa na makadinali wenzake - Demokrasia. Lakini Mfalme hachaguliwi. Hii inafanya Vatican kuwa nchi pekee kwenye historia ya dunia kuwa na Mfalme mwenye mamlaka kamili ambaye si wa kurithi na anapatikana kidemokrasia (Elected non-heridetary absolute Monarchy). Kwa hiyo Papa kulingana na muktadha na mazingira ya suala husika kuna muda anatumia mamlaka yake kama Papa na muda mwingine inampasa kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Vatican. Bado kuna mkanganyiko??? Zingatia mfano huu rahisi; tuseme kwamba kuna kampuni fulani kubwa ya kimataifa inaitwa Aman Enterprises (The Holy See kwa mada yetu). Aman Enterprises wakafanikiwa kuishwishi Tanzania kuwapatia kisiwa cha Mbudya na Bold Enterprises wanakibadilisha kisiwa cha Mbudya kuwa nchi inayojitegemea, labda iitwe Aman Land (Vatican City kwa mfano wetu). Sasa CEO wa kampuni Bwana Aman (Papa kwa mada yetu) anahamishiamanya makao makuu ya kampuni mpaka Aman Land. Kwa kuwa Aman Land sasa ni nchi, CEO wa kampuni anakuwa pia mtawala wa nchi hii, Mfalme. . Kwa hiyo kwa manufaa ya kampuni kutumia 'connection' zake za kimataifa kunufaisha taifa lake la Aman Land ni vyema kutumia mamlaka kama CEO wa Bold Enterprises na kuna muda akihitaji nchi yake ya Aman Land kutunga sheria na taratibu ambazo zitanufaisha kampuni izidi kushamiri ni vyema kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Aman Land. Haya ndio mamlaka mawili yaliyo chini ya mtu mmoja ndani ya vatican, Papa na Mfalme wa Vatican. Bado kuna mkanganyiko??? Kama haujaelewa sawia usihofu kwa maana bado kuna hata nchi nyingine duniani bado hawaelewi sawa sawa mfumo mzima wa Vatican. Mfano, Umoja wa Mataifa wamekubali The Holy See (corporation) kama mwanachama wake lakini sio Vatican City nchi yenyewe. Passports za raia wa Vatican zinatolewa na The Holy See na sio Vatican na zinakubalika kwenye nchi nyingine japokuwa The Holy See kimataifa inatambulika kisheria kama Kampuni inayojitegemea. Na hapa tuongee kiduchu pia kuhusu raia wa Vatican. Katika nchi nyingine raia wa wanaongezeka kutokana na kuzaliana lakini hapa Vatican hakuna hilo kutokana na idadi ndogo ya wanaweka kiasi kwamba karibia ni asilimia sufuri. Namna pekee ya kuwa raia wa Vatican ni kwa kupewa uraia na Mfalme wa Vatican ili uishi Vatican kama moja wa wasaidizi wa Papa (ambaye ndiye mfalme). Kwa hiyo siku ukiacha kazi, yaani usaidizi wako kwa Papa ukifikia kikomo, Mfalme wa Vatican (ambayr ndiye Papa) anaondoa uraia wako na unarudi kwenu. Katika muda wowote ule raia wa nchi ya Vatican wanakadiriwa kuwa jumla karibia ya 500 ambao ndio idadi ndogo zaidi ya raia kwa nchi na ndogo kushinda hata idadi ya watu wanaoishi kwenye ghorofa moja kwenye nchi nyingi. Na raia wote hawa ni wafanyakazi wa Papa/The Holy See ambao wanapewa uraia na Mfalme (ambaye ndiye Papa) ambapo wanafanya kazi kama Makadinali, Wanadiplomasia, walinzi au kazi nyingine za kikanisa. Kwa ufupi sana hii ndio picha halisi ya nchi ya Vatican… na hapa ndipo ambapo maisha ya kiroho ya wafuasi zaidi ya Billioni 2 yanapoendeshwa…
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·832 Views
  • MAANA YA 'HANSARD' ZA BUNGE

    NENO "Hansard" ni maarufu sana katika shughuli za Bunge nchini Tanzania, na pia katika nchi zote za Jumuiya ya Madola (Commonwealth Countries). Hutamkwa kwa haraka, "han-sadi."

    Maana yake ni Kumbukumbu Rasmi za Majadiliano katika mijadala na hoja kati ya Wabunge na Serikali , ambayo hufanyika ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri.

    Kimsingi, ni mtiririko wa nukuu mbalimbali za hoja za wabunge (ambao ni wawakilishi wa wananchi) na Mawaziri (ambao ni Serikali), katika mijadala yao kwa ruksa ya Spika wa Bunge.

    Ni mtiririko wa nukuu ya majadiliano ya wabunge wakati wote wa vikao vya Bunge la Jamhuri, ambapo kila baada ya vikao husika majadiliano hayo huchapishwa na huhifadhiwa kama kumbukumbu mahsusi, hususan kwa ajili ya matumizi katika kumbukumbu za historia.

    Aidha, Hansard ni jina la heshima kutokana na kazi ya mwandishi na mchapishaji wa nyaraka na vitabu wa nchini Uingereza, Thomas Curson Hansard, ambaye alikuwa mwandishi na mchapishaji wa kwanza wa kumbukumbu za Bunge la Uingereza kule Westminster, mjini London.

    Kutokana na kazi hiyo ya mwandishi huyo, Thomas Hansard, ndipo majadiliano ya wabunge wa Uingereza yakapewa jina la Hansard.

    Hiyo ni kwa vile kila baada ya vikao husika vya wabunge, majadiliano yao yalikuwa tayari yamechapishwa na kusomwa na wao wenyewe, na pia watu wengine, kuhusiana na kile kilichokuwa kinajadiliwa na wabunge ndani ya Bunge.

    PICHA: Thomas Curson Hansard, ambaye alifariki mwaka 1833 akiwa na umri wa miaka 57.
    MAANA YA 'HANSARD' ZA BUNGE NENO "Hansard" ni maarufu sana katika shughuli za Bunge nchini Tanzania, na pia katika nchi zote za Jumuiya ya Madola (Commonwealth Countries). Hutamkwa kwa haraka, "han-sadi." Maana yake ni Kumbukumbu Rasmi za Majadiliano katika mijadala na hoja kati ya Wabunge na Serikali , ambayo hufanyika ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri. Kimsingi, ni mtiririko wa nukuu mbalimbali za hoja za wabunge (ambao ni wawakilishi wa wananchi) na Mawaziri (ambao ni Serikali), katika mijadala yao kwa ruksa ya Spika wa Bunge. Ni mtiririko wa nukuu ya majadiliano ya wabunge wakati wote wa vikao vya Bunge la Jamhuri, ambapo kila baada ya vikao husika majadiliano hayo huchapishwa na huhifadhiwa kama kumbukumbu mahsusi, hususan kwa ajili ya matumizi katika kumbukumbu za historia. Aidha, Hansard ni jina la heshima kutokana na kazi ya mwandishi na mchapishaji wa nyaraka na vitabu wa nchini Uingereza, Thomas Curson Hansard, ambaye alikuwa mwandishi na mchapishaji wa kwanza wa kumbukumbu za Bunge la Uingereza kule Westminster, mjini London. Kutokana na kazi hiyo ya mwandishi huyo, Thomas Hansard, ndipo majadiliano ya wabunge wa Uingereza yakapewa jina la Hansard. Hiyo ni kwa vile kila baada ya vikao husika vya wabunge, majadiliano yao yalikuwa tayari yamechapishwa na kusomwa na wao wenyewe, na pia watu wengine, kuhusiana na kile kilichokuwa kinajadiliwa na wabunge ndani ya Bunge. PICHA: Thomas Curson Hansard, ambaye alifariki mwaka 1833 akiwa na umri wa miaka 57.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·457 Views
  • PICHANI anaonekana aliyekuwa kiongozi wa Ujerumani bwana Adolf Hitler akipiga saluti. Hiyo inaitwa saluti ya kinazi, au kwa kingereza *'Nazi Salute'* ambayo ilikuwa ikipigwa na wananchi wa ujerumani kama ishara ya kutoa heshima kwa kiongozi wao.

    Saluti hiyo hupigwa kwa kunyoosha mkono wa kulia mbele usawa wa uso, huku vidole vikiwa vimenyooka....Na Mara zote, saluti hiyo huenda sanjari na maneno ..'''Heil Hitler..Heil, mein Führer""..yaani "Salaam Hitler, Salaam kiongozi wangu"

    Saluti hii ilianza kutumika katika miaka ya 1930, wakati wa kipindi cha Adolf Hitler na chama chake cha *Nazi Party.* Saluti hii ilikuwa ikifanywa na raia wa wajerumani, hususani wanajeshi, katika kutoa salamu na heshima kwa Hitler pamoja na kulitukuza taifa la ujerumani.

    Tarehe 13 Julai 1933, Serikali ilitoa Agizo kuwaamuru wafanyakazi wote wa serikali ya ujerumani kutumia saluti hiyo. Pia agizo hilo liliwataka watu wote kupiga saluti hiyo wakati wa kuimba wimbo wa taifa au wimbo wa chama...Na yeyote atakayekaidi, adhabu kali itatolewa juu yake.

    Mwaka 1934, tulishuhudia kuanzishwa kwa mahakama maalumu kwa ajili ya kuwahukumu wale wanaopinga saluti hiyo. Bwana mmoja aliyejulikana kwa jina la Paul Schneider, alipokea kipigo kikali kutoka kwa wafuasi wa itikadi za kiNazi baada ya kugoma kupiga saluti hiyo. Kwa ufupi niseme kwamba saluti hiyo ilikuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku ambapo Watu walikuwa wakisalimiana kwa saluti hiyo au kwa kutamka 'Hail Hilter'.

    Kama nilivyosema hapo awali kwamba, Saluti hii ilikuwa ikitumika wakati wa Adolf Hitler tuu, kwani baada ya kuanguka kwa utawala wake, saluti hii ilikomeshwa.

    Leo hii, ni kosa kubwa sana kutumia saluti hii. Na mtu yeyote atakayebainika kuonesha ishara hii, adhabu kali itatolewa dhidi yake. Mfano, Mwaka 2007 kuna mtu mmoja aliyeitwa Horst Mahler, alihukumiwa miezi sita jela baada ya kuonekana kutumia ishara hii.

    Pia mwaka 2013, mchezaji wa klabu ya soka ya AEK Athens FC, alifungiwa kucheza soka katika timu yake ya taifa ya Ugiriki, baada ya kutumia saluti hiyo wakati akishangilia goli aliloshinda katika mechi dhidi ya klabu ya Veria F.C.

    Naam!..Na hiyo ndio 'Nazi Salute' ambayo Mara nyingine huitwa Hitler Salute, ambayo Leo hii ni marufuku kutumika, na endapo utakamatwa umenyoosha mkono hivyo, Utapata tabu sana!!

    ***

    PICHANI anaonekana aliyekuwa kiongozi wa Ujerumani bwana Adolf Hitler akipiga saluti. Hiyo inaitwa saluti ya kinazi, au kwa kingereza *'Nazi Salute'* ambayo ilikuwa ikipigwa na wananchi wa ujerumani kama ishara ya kutoa heshima kwa kiongozi wao. Saluti hiyo hupigwa kwa kunyoosha mkono wa kulia mbele usawa wa uso, huku vidole vikiwa vimenyooka....Na Mara zote, saluti hiyo huenda sanjari na maneno ..'''Heil Hitler..Heil, mein Führer""..yaani "Salaam Hitler, Salaam kiongozi wangu" Saluti hii ilianza kutumika katika miaka ya 1930, wakati wa kipindi cha Adolf Hitler na chama chake cha *Nazi Party.* Saluti hii ilikuwa ikifanywa na raia wa wajerumani, hususani wanajeshi, katika kutoa salamu na heshima kwa Hitler pamoja na kulitukuza taifa la ujerumani. Tarehe 13 Julai 1933, Serikali ilitoa Agizo kuwaamuru wafanyakazi wote wa serikali ya ujerumani kutumia saluti hiyo. Pia agizo hilo liliwataka watu wote kupiga saluti hiyo wakati wa kuimba wimbo wa taifa au wimbo wa chama...Na yeyote atakayekaidi, adhabu kali itatolewa juu yake. Mwaka 1934, tulishuhudia kuanzishwa kwa mahakama maalumu kwa ajili ya kuwahukumu wale wanaopinga saluti hiyo. Bwana mmoja aliyejulikana kwa jina la Paul Schneider, alipokea kipigo kikali kutoka kwa wafuasi wa itikadi za kiNazi baada ya kugoma kupiga saluti hiyo. Kwa ufupi niseme kwamba saluti hiyo ilikuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku ambapo Watu walikuwa wakisalimiana kwa saluti hiyo au kwa kutamka 'Hail Hilter'. Kama nilivyosema hapo awali kwamba, Saluti hii ilikuwa ikitumika wakati wa Adolf Hitler tuu, kwani baada ya kuanguka kwa utawala wake, saluti hii ilikomeshwa. Leo hii, ni kosa kubwa sana kutumia saluti hii. Na mtu yeyote atakayebainika kuonesha ishara hii, adhabu kali itatolewa dhidi yake. Mfano, Mwaka 2007 kuna mtu mmoja aliyeitwa Horst Mahler, alihukumiwa miezi sita jela baada ya kuonekana kutumia ishara hii. Pia mwaka 2013, mchezaji wa klabu ya soka ya AEK Athens FC, alifungiwa kucheza soka katika timu yake ya taifa ya Ugiriki, baada ya kutumia saluti hiyo wakati akishangilia goli aliloshinda katika mechi dhidi ya klabu ya Veria F.C. Naam!..Na hiyo ndio 'Nazi Salute' ambayo Mara nyingine huitwa Hitler Salute, ambayo Leo hii ni marufuku kutumika, na endapo utakamatwa umenyoosha mkono hivyo, Utapata tabu sana!! ***
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·467 Views
  • UGOMVI WA PALESTINA NA ISRAEL NI WA MAPACHA WAWILI TOKA WAKIWA TUMBONI KABLA YA KUZALIWA.

    Nini sababu ya ugomvi ? Siyo tatizo la kugombania ardhi wala kugombania mji wa Yerusalem kunakosababisha ugomvi kati ya mataifa haya mawili ni kwamba kila taifa halitaki kutambulika kwa taifa jingine kama taifa huru.

    Hii inamaanisha kwamba hata kama taifa la Palestina litahamia katika bara jingine au Israel kuhamia bara jingine bado ugomvi na vita ingeendelea kati ya mataifa haya mawili ,ugomvi kati ya mataifa haya unakwenda mbali zaidi tangu watoto wawili mapacha wakiwa tumboni kabla ya kuzaliwa.

    Katika kitabu cha (Mwanzo 25:22) inasomeka;"Bwana akamwambia ,Mataifa mawili yamo tumboni mwako ,Na Kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako, Kabila moja litakuwa hodari Kuliko la pili na mkubwa atamtumikia mdogo."

    Alizaliwa kwanza Esau ambaye baadae aliitwa Edom kisha akafuatia Yakobo ambaye baadae aliitwa Israel. Wakati Edom ni taifa la Palestina, Israel ni taifa la Israeli, hakuna ubishi kwamba Israel ni hodari zaidi ya Palestina.

    Miaka ya 50 iliyopita, yaani mwaka 1967 ,kulitokea vita kati ya Israel na mataifa jirani zake, Vita hii ilipiganwa kwa siku 6 tu(Juni 5---Juni 10,1967) lakini madhara yake yapo mpaka leo ,ilikuwa ni miaka michache kupita baada ya wa--NAZI wa Hitler,kuwaua wayahudi milioni 6 ,ndoto ya kuanzishwa kwa Taifa la Israeli kama ilivyotabiriwa kwenye biblia ilitimia.

    Mwishoni mwa mwaka 1948 ikiwa ni miaka 3 tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia ,Mataifa ya kiarabu majirani mwa Israel yaliivamia Israel yakijaribu kuliangamiza Taifa changa ambalo muda mfupi tu lilikuwa limetangazwa na Umoja wa Mataifa kuwa Taifa huru, lakini hayakufanikiwa.

    Jeshi la misri lilipigwa lakini askari waliokuwa kwenye eneo dogo linalojulikana kama Falluja walikataa kusalimu amri ,kundi la askari wa Misri na Israeli walipambana vikali ,Miongoni mwa askari Vijana waliokuwa kwenye kikosi cha jeshi la Israel alikuwa ni Yitzhak Rabin ambaye alikuwa na umri wa miaka 26 wakati huo, Pamoja na Meja Gamal Abdel Nasser wa jeshi la Misri aliyekuwa na miaka 30.

    Wapalestina wanauita mwaka 1948 kuwa ni "al--Nakba" yaani 'Janga' .Zaidi ya wapalestina 750,000 walifukuzwa kutoka kwenye eneo ambalo sasa linajulikana kama Taifa la Israel na hawakuruhusiwa kurudi tena mahali hapo.

    Mataifa ya Misri, Jordani, na Syria yaliungana pamoja kuishambulia Israel ambayo hata hivyo ndiyo kwanza ilikuwa imepewa hadhi ya kuwa taifa huru. Lakini kwasababu Mungu alikuwa amesema kwamba "Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili" ni wazi kuwa Israel ,likiwa taifa changa ,bado lilifanikiwa kuwashinda majirani zake tena ndani ya siku 6 tu.

    Ingawa vita kati ya Israel na Palestina ilianzia tumboni ,lakini vita nyingi hutengenezwa na wajenzi huru kwa faida yao, Februari 17 mwaka 1950 James Paul Warburg mwenye asili ya kiyahudi alihutubia Baraza la Senate la Marekani na kusema " Government creates a crisis for which the public demands a solution.
    That solution instigates the changes that the government initially wanted but which the people would have been unwilling to accept.

    It is order out of chaos !!! Worldwide chaos will lead to worldwide solutions which will establish the one world order " yaani; Serikali hutengeneza migogoro ambayo umma hutaka pawepo na suruhisho.
    Suruhisho hilo hulazimisha mabadiliko ambayo awali Serikali iliyataka lakini umma ulikuwa hauyataki, ni utaratibu unaopatikana Kutokana na machafuko !! Machafuko ya kidunia yataleta suruhisho la kidunia ambalo litaanzisha utaratibu mmoja wa ulimwengu.

    Katika hotuba yake inayojulikana kama "Urbi et Orbi ", Papa Francis alisema ;" Pepo za vita zinavuma katika ulimwengu wetu na maendeleo yanaendelea kusababisha mmomonyoko wa maadili na uharibifu wa mazingira " Urbi et Orbi ni maneno yanayomaanisha " To the city and to the world" yaani " kwenda kwa mji na kwenda kwa ulimwengu" kumaanisha kwamba hotuba za Papa Francis zinakwenda kwa wakazi wa mji wa Vatican city na wakazi wa ulimwenguni kote.

    Tishio la silaha za nyuklia kutoka Korea kaskazini ,mgogoro wa peninsula ya Korea pamoja na mgogoro wa mji wa Yerusalem baada ya Rais Trump kutangaza kuwa Yerusalem ni mji Mkuu wa Israel na tangazo hilo kupingwa na Umoja wa Mataifa, ni pepo zinazoonyesha dalili ya kufumka kwa vita duniani kote.

    Katika hotuba hiyo papa Francis alipendekeza kutambuliwa kwa mataifa mawili yaani Israel na Palestina, kama suruhisho la mgogoro wa Mashariki ya kati pamoja na kutatua mgogoro wa Korea kaskazini kwa njia ya kidiplomasia.

    Itakumbukwa kwamba, Mwanasayansi mashuhuri aliyejulikana kama Albert Einstein alitoa tafsiri ya neno " Insanity" yaani " kuchanganyikiwa au uwendawazimu " akisema ;"wakati mtu anapojaribu kutumia kanuni ya zamani ambayo ilishindwa kwa wakati na wakati mwingine tena, akiamini kwamba ,kwa vyovyote atapata matokeo tofauti mtu huyo amechanganyikiwa au ana uwendawazimu.

    Israel, Palestina, Marekani na Umoja wa Mataifa kwa zaidi ya miaka 50 wamekuwa wakijadili uwezekano wa kuleta suluhu kwa kuifanya Palestina kuwa Taifa huru pamoja na Israeli. Hata hivyo ,wapalestina wamekuwa wakijiondoa kwenye suruhisho hilo kwa sababu mpango huo unaifanya Israel iendelee kuwa Taifa huru ,wapalestina wamekuwa wakipinga wazo kwamba Israel ina haki ya kuwepo na kuishi kama Taifa.

    Lengo ni kuwafutilia mbali wayahudi wote, jambo ambalo hata Adolf Hitler alikuwa nalo lakini hakuweza ,kwa mujibu wa Mwanasayansi Albert Einstein " suruhisho la mataifa mawili ( two state solution) limeshindwa kufanya kazi na wale wanaoendelea kupendekeza suruhisho hilo, ama wamechanganyikiwa na ni wendawazimu au wanafanya kwa makusudi wakiwa wanafahamu matokeo yake.

    Raia wa mataifa yote mawili wanamtambua Ibrahimu kama Baba wa Mataifa yao, Ibrahimu aliishi miaka 4000 iliyopita akisafiri Kwenye eneo la Taifa linalojulikana leo kama Iraqi, na akafika Kwenye eneo la taifa linalojulikana leo kama Israeli.

    Ibrahimu aliahidiwa na Mungu Kwamba atapata mtoto Katika uzee wake .Akiwa amesubiri utimilifu wa ahadi hii kwa muda mrefu bila kupata mtoto ,alimchukua kijakazi wake na akafanikiwa kuzaa naye mtoto aliyeitwa ishmail. Lakini mungu hakuwa amepanga kumpatia Ibrahim mtoto kwa njia hiyo, bado aliendelea kumhakikishia kwamba atapata mtoto kupitia kwa mkewe. Kwa sababu alikuwa na imani ,alifanikiwa kumpata mtoto aliyepewa jina la Isaka.

    Kisha Mungu akamuagiza kwenda kwenye mlima Moria, ili akamtoe kafara mtoto wake Isaka ambaye alikuwa amemsubiri Kwa muda mrefu. Huu mlima Moria upo wapi? Ingawa wakati wa siku za Ibrahimu ,miaka 2000KK ,eneo kubwa lilikuwa jangwa ,miaka 1000KK baadae Mfalme Daudi alijenga mji wa Yerusalem katika eneo hilo na mtoto wake aliyejulikana kama Mfalme Sulemani alijenga hekalu la kwanza kwenye eneo hilo la mlima Moria .

    Imeandikwa " ndipo Sulemani akaanza kuijenga nyumba ya bwana huko Yerusalem ,juu ya mlima Moria ..." (2 Nyakati 3:1). Lakini kwa Ibrahimu Mungu anamwambia : " umchukue mwanao ,mwana wako wa pekee, umpendaye ,Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka, ..." ( Mzo. 22:2) Hivyo basi mji wa Yerusalem anajulikana kama nchi ya Moria au mlima wa Moria au mji wa Daudi mahali palepale alipoambiwa nabii Ibrahimu kwenda kutoa kafara ,ndipo Hapo hapo Mfalme Sulemani alipojenga hekalu la kumuabudia Mungu na kumtolea kafara za wanyama.

    Lakini zaidi ni katika mji wa Yerusalem ndipo yesu aliposulubiwa msalabani na hapo ndipo lilipo chimbuko la dini ya ukristo iliyoanzishwa kwa ujumla uzao wa Ibrahimu ndio chimbuko la dini kubwa tatu ,yaani uyahudi, uislamu ,na ukristo.

    Dini zingine zote zimetokana na dini hizi tatu ,Kutokana na ukweli huu ,wajenzi huru wamefanikiwa kuwashawishi viongozi wa dini zote na kuziunganisha kuwa dini moja. Ingawa majina ya dini hizi yanaendelea kutumika kiasi cha kuonekana kwamba hakuna tofauti ,lakini matunda ya dini hizi yanaonyesha wazi kuwa yanatokea kwenye mti mmoja.

    Katika mambo ya kiroho jina la dini ya mtu au dhehebu lake haliwezi kumfanya muumini afike mbinguni bali kitu muhimu ni matunda ya dini hiyo au dhehebu hilo. Kwa kujua hili mwanzilishi wa illuminati Dkt Adam Weishaupt aliandika akisema , The great strength of our order lies in its concealment " yaani nguvu kubwa ya Utaratibu wetu Iko katika kuficha na kufanya kazi zetu kwa siri kubwa " Hata huu muunganiko wa dini umefanywa kwa siri kubwa kiasi kwamba waumini wengi hawajui kinachoendelea.

    Weishaupt akaendelea kusema, " let it never appear in any place in its own name, but always covered by another name and another occupation " yaani; " hebu isionekane mahali popote kwa jina lake, lakini daima ifanyike kwa jina lingine na kwa namna nyingine." ( Robin's Proofs of a Conspiracy, P. 195).
    UGOMVI WA PALESTINA NA ISRAEL NI WA MAPACHA WAWILI TOKA WAKIWA TUMBONI KABLA YA KUZALIWA. Nini sababu ya ugomvi ? Siyo tatizo la kugombania ardhi wala kugombania mji wa Yerusalem kunakosababisha ugomvi kati ya mataifa haya mawili ni kwamba kila taifa halitaki kutambulika kwa taifa jingine kama taifa huru. Hii inamaanisha kwamba hata kama taifa la Palestina litahamia katika bara jingine au Israel kuhamia bara jingine bado ugomvi na vita ingeendelea kati ya mataifa haya mawili ,ugomvi kati ya mataifa haya unakwenda mbali zaidi tangu watoto wawili mapacha wakiwa tumboni kabla ya kuzaliwa. Katika kitabu cha (Mwanzo 25:22) inasomeka;"Bwana akamwambia ,Mataifa mawili yamo tumboni mwako ,Na Kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako, Kabila moja litakuwa hodari Kuliko la pili na mkubwa atamtumikia mdogo." Alizaliwa kwanza Esau ambaye baadae aliitwa Edom kisha akafuatia Yakobo ambaye baadae aliitwa Israel. Wakati Edom ni taifa la Palestina, Israel ni taifa la Israeli, hakuna ubishi kwamba Israel ni hodari zaidi ya Palestina. Miaka ya 50 iliyopita, yaani mwaka 1967 ,kulitokea vita kati ya Israel na mataifa jirani zake, Vita hii ilipiganwa kwa siku 6 tu(Juni 5---Juni 10,1967) lakini madhara yake yapo mpaka leo ,ilikuwa ni miaka michache kupita baada ya wa--NAZI wa Hitler,kuwaua wayahudi milioni 6 ,ndoto ya kuanzishwa kwa Taifa la Israeli kama ilivyotabiriwa kwenye biblia ilitimia. Mwishoni mwa mwaka 1948 ikiwa ni miaka 3 tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia ,Mataifa ya kiarabu majirani mwa Israel yaliivamia Israel yakijaribu kuliangamiza Taifa changa ambalo muda mfupi tu lilikuwa limetangazwa na Umoja wa Mataifa kuwa Taifa huru, lakini hayakufanikiwa. Jeshi la misri lilipigwa lakini askari waliokuwa kwenye eneo dogo linalojulikana kama Falluja walikataa kusalimu amri ,kundi la askari wa Misri na Israeli walipambana vikali ,Miongoni mwa askari Vijana waliokuwa kwenye kikosi cha jeshi la Israel alikuwa ni Yitzhak Rabin ambaye alikuwa na umri wa miaka 26 wakati huo, Pamoja na Meja Gamal Abdel Nasser wa jeshi la Misri aliyekuwa na miaka 30. Wapalestina wanauita mwaka 1948 kuwa ni "al--Nakba" yaani 'Janga' .Zaidi ya wapalestina 750,000 walifukuzwa kutoka kwenye eneo ambalo sasa linajulikana kama Taifa la Israel na hawakuruhusiwa kurudi tena mahali hapo. Mataifa ya Misri, Jordani, na Syria yaliungana pamoja kuishambulia Israel ambayo hata hivyo ndiyo kwanza ilikuwa imepewa hadhi ya kuwa taifa huru. Lakini kwasababu Mungu alikuwa amesema kwamba "Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili" ni wazi kuwa Israel ,likiwa taifa changa ,bado lilifanikiwa kuwashinda majirani zake tena ndani ya siku 6 tu. Ingawa vita kati ya Israel na Palestina ilianzia tumboni ,lakini vita nyingi hutengenezwa na wajenzi huru kwa faida yao, Februari 17 mwaka 1950 James Paul Warburg mwenye asili ya kiyahudi alihutubia Baraza la Senate la Marekani na kusema " Government creates a crisis for which the public demands a solution. That solution instigates the changes that the government initially wanted but which the people would have been unwilling to accept. It is order out of chaos !!! Worldwide chaos will lead to worldwide solutions which will establish the one world order " yaani; Serikali hutengeneza migogoro ambayo umma hutaka pawepo na suruhisho. Suruhisho hilo hulazimisha mabadiliko ambayo awali Serikali iliyataka lakini umma ulikuwa hauyataki, ni utaratibu unaopatikana Kutokana na machafuko !! Machafuko ya kidunia yataleta suruhisho la kidunia ambalo litaanzisha utaratibu mmoja wa ulimwengu. Katika hotuba yake inayojulikana kama "Urbi et Orbi ", Papa Francis alisema ;" Pepo za vita zinavuma katika ulimwengu wetu na maendeleo yanaendelea kusababisha mmomonyoko wa maadili na uharibifu wa mazingira " Urbi et Orbi ni maneno yanayomaanisha " To the city and to the world" yaani " kwenda kwa mji na kwenda kwa ulimwengu" kumaanisha kwamba hotuba za Papa Francis zinakwenda kwa wakazi wa mji wa Vatican city na wakazi wa ulimwenguni kote. Tishio la silaha za nyuklia kutoka Korea kaskazini ,mgogoro wa peninsula ya Korea pamoja na mgogoro wa mji wa Yerusalem baada ya Rais Trump kutangaza kuwa Yerusalem ni mji Mkuu wa Israel na tangazo hilo kupingwa na Umoja wa Mataifa, ni pepo zinazoonyesha dalili ya kufumka kwa vita duniani kote. Katika hotuba hiyo papa Francis alipendekeza kutambuliwa kwa mataifa mawili yaani Israel na Palestina, kama suruhisho la mgogoro wa Mashariki ya kati pamoja na kutatua mgogoro wa Korea kaskazini kwa njia ya kidiplomasia. Itakumbukwa kwamba, Mwanasayansi mashuhuri aliyejulikana kama Albert Einstein alitoa tafsiri ya neno " Insanity" yaani " kuchanganyikiwa au uwendawazimu " akisema ;"wakati mtu anapojaribu kutumia kanuni ya zamani ambayo ilishindwa kwa wakati na wakati mwingine tena, akiamini kwamba ,kwa vyovyote atapata matokeo tofauti mtu huyo amechanganyikiwa au ana uwendawazimu. Israel, Palestina, Marekani na Umoja wa Mataifa kwa zaidi ya miaka 50 wamekuwa wakijadili uwezekano wa kuleta suluhu kwa kuifanya Palestina kuwa Taifa huru pamoja na Israeli. Hata hivyo ,wapalestina wamekuwa wakijiondoa kwenye suruhisho hilo kwa sababu mpango huo unaifanya Israel iendelee kuwa Taifa huru ,wapalestina wamekuwa wakipinga wazo kwamba Israel ina haki ya kuwepo na kuishi kama Taifa. Lengo ni kuwafutilia mbali wayahudi wote, jambo ambalo hata Adolf Hitler alikuwa nalo lakini hakuweza ,kwa mujibu wa Mwanasayansi Albert Einstein " suruhisho la mataifa mawili ( two state solution) limeshindwa kufanya kazi na wale wanaoendelea kupendekeza suruhisho hilo, ama wamechanganyikiwa na ni wendawazimu au wanafanya kwa makusudi wakiwa wanafahamu matokeo yake. Raia wa mataifa yote mawili wanamtambua Ibrahimu kama Baba wa Mataifa yao, Ibrahimu aliishi miaka 4000 iliyopita akisafiri Kwenye eneo la Taifa linalojulikana leo kama Iraqi, na akafika Kwenye eneo la taifa linalojulikana leo kama Israeli. Ibrahimu aliahidiwa na Mungu Kwamba atapata mtoto Katika uzee wake .Akiwa amesubiri utimilifu wa ahadi hii kwa muda mrefu bila kupata mtoto ,alimchukua kijakazi wake na akafanikiwa kuzaa naye mtoto aliyeitwa ishmail. Lakini mungu hakuwa amepanga kumpatia Ibrahim mtoto kwa njia hiyo, bado aliendelea kumhakikishia kwamba atapata mtoto kupitia kwa mkewe. Kwa sababu alikuwa na imani ,alifanikiwa kumpata mtoto aliyepewa jina la Isaka. Kisha Mungu akamuagiza kwenda kwenye mlima Moria, ili akamtoe kafara mtoto wake Isaka ambaye alikuwa amemsubiri Kwa muda mrefu. Huu mlima Moria upo wapi? Ingawa wakati wa siku za Ibrahimu ,miaka 2000KK ,eneo kubwa lilikuwa jangwa ,miaka 1000KK baadae Mfalme Daudi alijenga mji wa Yerusalem katika eneo hilo na mtoto wake aliyejulikana kama Mfalme Sulemani alijenga hekalu la kwanza kwenye eneo hilo la mlima Moria . Imeandikwa " ndipo Sulemani akaanza kuijenga nyumba ya bwana huko Yerusalem ,juu ya mlima Moria ..." (2 Nyakati 3:1). Lakini kwa Ibrahimu Mungu anamwambia : " umchukue mwanao ,mwana wako wa pekee, umpendaye ,Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka, ..." ( Mzo. 22:2) Hivyo basi mji wa Yerusalem anajulikana kama nchi ya Moria au mlima wa Moria au mji wa Daudi mahali palepale alipoambiwa nabii Ibrahimu kwenda kutoa kafara ,ndipo Hapo hapo Mfalme Sulemani alipojenga hekalu la kumuabudia Mungu na kumtolea kafara za wanyama. Lakini zaidi ni katika mji wa Yerusalem ndipo yesu aliposulubiwa msalabani na hapo ndipo lilipo chimbuko la dini ya ukristo iliyoanzishwa kwa ujumla uzao wa Ibrahimu ndio chimbuko la dini kubwa tatu ,yaani uyahudi, uislamu ,na ukristo. Dini zingine zote zimetokana na dini hizi tatu ,Kutokana na ukweli huu ,wajenzi huru wamefanikiwa kuwashawishi viongozi wa dini zote na kuziunganisha kuwa dini moja. Ingawa majina ya dini hizi yanaendelea kutumika kiasi cha kuonekana kwamba hakuna tofauti ,lakini matunda ya dini hizi yanaonyesha wazi kuwa yanatokea kwenye mti mmoja. Katika mambo ya kiroho jina la dini ya mtu au dhehebu lake haliwezi kumfanya muumini afike mbinguni bali kitu muhimu ni matunda ya dini hiyo au dhehebu hilo. Kwa kujua hili mwanzilishi wa illuminati Dkt Adam Weishaupt aliandika akisema , The great strength of our order lies in its concealment " yaani nguvu kubwa ya Utaratibu wetu Iko katika kuficha na kufanya kazi zetu kwa siri kubwa " Hata huu muunganiko wa dini umefanywa kwa siri kubwa kiasi kwamba waumini wengi hawajui kinachoendelea. Weishaupt akaendelea kusema, " let it never appear in any place in its own name, but always covered by another name and another occupation " yaani; " hebu isionekane mahali popote kwa jina lake, lakini daima ifanyike kwa jina lingine na kwa namna nyingine." ( Robin's Proofs of a Conspiracy, P. 195).
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·946 Views
  • Necronomicon
    Hiki ni Kitabu cha Imani ya Kishetani na Kina Mambo Mengi ya Kuogopesha na Ukikisoma Mambo hayo Hutokea Kweli!!
    Ni Mambo ya Mizimu na Mauzauza, Ukiwa Unasoma Kinakupeleka Kukiona Kweli Unachosoma Kupitia Hisia!, Kuna Imani ya Ajabu inakuingia.
    Kinakadiriwa Kuandikwa Tangu Miaka ya 800 A.D Kwa Lugha ya Ajabu na Kumekuwa Kukitajwa Waandishi Wengi Walioandika Kitabu hiki Miaka hiyo ya Kale na Mmoja Wapo ni 'Abdul Alhazred' Raia wa YEMEN.
    Kitabu hiki Kilikuja Kutafsiriwa na Kuandikwa Upya na Mmarekani H.P. Lovecraft Aliyekua Mtaalamu wa Kutafsiri Mambo ya Kimiujiza Mwaka 1927 na Kutolewa Rasmi Mwaka 1938. Hakuna Mtu Mwingine Aliyeweza Kukielewa Kiufasaha Zaidi yake tuu.
    Necronomicon Hiki ni Kitabu cha Imani ya Kishetani na Kina Mambo Mengi ya Kuogopesha na Ukikisoma Mambo hayo Hutokea Kweli!! Ni Mambo ya Mizimu na Mauzauza, Ukiwa Unasoma Kinakupeleka Kukiona Kweli Unachosoma Kupitia Hisia!, Kuna Imani ya Ajabu inakuingia. Kinakadiriwa Kuandikwa Tangu Miaka ya 800 A.D Kwa Lugha ya Ajabu na Kumekuwa Kukitajwa Waandishi Wengi Walioandika Kitabu hiki Miaka hiyo ya Kale na Mmoja Wapo ni 'Abdul Alhazred' Raia wa YEMEN. Kitabu hiki Kilikuja Kutafsiriwa na Kuandikwa Upya na Mmarekani H.P. Lovecraft Aliyekua Mtaalamu wa Kutafsiri Mambo ya Kimiujiza Mwaka 1927 na Kutolewa Rasmi Mwaka 1938. Hakuna Mtu Mwingine Aliyeweza Kukielewa Kiufasaha Zaidi yake tuu.
    0 Comments ·0 Shares ·380 Views
  • Mrs Feodol Vasslyev alizaliwa mwaka 1707 Shurya nchini Urusi. Ni mwanamke aliyeshika rekodi ya kuzaa watoto wengi zaidi duniani watoto 69 na ameingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia GUINNESS
    Alizaa mapacha wawili Mara 16, watatu ×7 na wanne ×4

    Mrs Feodol Vasslyev alizaliwa mwaka 1707 Shurya nchini Urusi. Ni mwanamke aliyeshika rekodi ya kuzaa watoto wengi zaidi duniani watoto 69 na ameingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia GUINNESS Alizaa mapacha wawili Mara 16, watatu ×7 na wanne ×4
    0 Comments ·0 Shares ·215 Views
  • MJUE ALIYECHAPISHA BIBLIA KWA MARA YA KWANZA
    .Johannes Gutenberg. Gutenberg , anayejulikana kifupi kama
    Johannes Gutenberg , (mnamo 1398 - 3 Februari 1468 ) alikuwa fundi dhahabu na
    mvumbuzi kutoka Ujerumani anayekumbukwa hasa kama mbunifu wa
    uchapaji vitabu kwa herufi za kusogezeka
    Alitengeneza mashine ya kwanza ya kuchapa vitabu,
    Kabla ya Gutenberg vitabu vingi viliandikwa kwa mkono. Kunakili kitabu kimoja kama Biblia kwa mkono kulichukua muda kama mwaka mmoja.. Hivyo dunia leo inamtambua Gutenberg kama mtu wa kwanza kuchapisha biblia .. kwa mashine ya aliyoigundua na kuitengeneza mwenyewe ...#like_page_&_sharee
    MJUE ALIYECHAPISHA BIBLIA KWA MARA YA KWANZA .Johannes Gutenberg. Gutenberg , anayejulikana kifupi kama Johannes Gutenberg , (mnamo 1398 - 3 Februari 1468 ) alikuwa fundi dhahabu na mvumbuzi kutoka Ujerumani anayekumbukwa hasa kama mbunifu wa uchapaji vitabu kwa herufi za kusogezeka Alitengeneza mashine ya kwanza ya kuchapa vitabu, Kabla ya Gutenberg vitabu vingi viliandikwa kwa mkono. Kunakili kitabu kimoja kama Biblia kwa mkono kulichukua muda kama mwaka mmoja.. Hivyo dunia leo inamtambua Gutenberg kama mtu wa kwanza kuchapisha biblia .. kwa mashine ya aliyoigundua na kuitengeneza mwenyewe ...#like_page_&_sharee
    0 Comments ·0 Shares ·253 Views
  • BAPHOMET: SANAMU LA SHETANI LILILOLETA UTATA NCHINI MAREKANI.

    Binadamu tangu zama za kale amekuwa akijenga, kuchonga na kuweka sanamu za aina nyingi kwa sababu mbalimbali.
    Baadhi hutumiwa kuwaenzi watu maarufu na kuwakumbuka, na nyingine huabudiwa kama miungu. Kwa muda mrefu hata hivyo imekuwa ni nadra kuona sanamu ambayo moja kwa moja inahusishwa na shetani au ibilisi. Lakini ukifika Marekani, mambo ni tofauti. Kuna sanamu moja kubwa ya shaba ambayo inahusishwa na ushetani. Ni sanamu ya, Baphomet ni kiumbe mwenye kichwa kinachofanana na cha mbuzi lakini ameongezwa maungo ya ajabu. Ni kiumbe mwenye mabawa, na kwenye sanamu hiyo inayotumiwa kwa sasa huoneshwa akiwa na watoto wawili wanaotabasamu.

    Sanamu inayotumiwa kwa sasa ina urefu wa karibu futi 9, na iligharimu $100,000 (£64,000) kuitengeneza. Sanamu hii imekuwa ikitumiwa kuwapiga vita wale walio na imani za Kikristo kiislamu na imani nyingine zenye kumcha Mungu mmoja. Ni sanamu hii ambayo imekuwa ikitumiwa kuendesha vita dhidi ya kuwekwa kwa sanamu za Kikristo na dini nyingine katika majengo maarufu, bustani na maeneo ya umma nchini Marekani. Agosti 17, sanamu hiyo ya kiumbe anayefahamika kama Baphomet ilipelekwa katika jimbo la Arkansas anakotoka Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton. Wanaotumia sanamu hiyo ni watu wa kundi linalofahamika kama Satanic Temple (Hekalu la Shetani) ambalo ni kundi la 'kidini' na kisiasa ambalo hupinga kuingizwa kwa dini katika masuala ya Serikali.

    Kundi hilo liliandaa maandamano ya watu 150 waliyojumuisha waabudu shetani, watu wasioamini Mungu yupo, na Wakristo pia.
    Maandamano hayo yalifanyika nje ya jengo lililo Makao Makuu ya jimbo la Arkansas katika mji wa Little Rock. Walikuwa wamekerwa na hatua ya kuweka sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu katika uwanja wa Makao Makuu hayo. Satanic Temple walisema sanamu hiyo inakiuka Sheria ya Kwanza ya Marekebisho ya Katiba nchini Marekani ambayo huzungumzia uhuru na haki za kidini. "Ikiwa utakubaliana na kuwepo kwa sanamu ya dini moja basi kunafaa kuwa na uhuru kwa wengine kuweka sanamu za kidini, na ukizuia basi kusiwe na sanamu yoyote ile," mwanzilishi mwenza wa tawi la Satanic Temple katika jimbo la Arkansas, Ivy Forrester, alinukuliwa na wanahabari siku hiyo ya maandamano.

    Ndoto yao ni kuwa na sanamu ya kudumu, lakini siku hiyo hawakuruhusiwa na sheria kuiweka kwa muda mrefu. Kuna sheria ya Arkansas ya mwaka 2017 inayohitaji sanamu ya kuwekwa maeneo ya Serikali iwe na udhamini wa Mbunge ambaye atawasilisha mswada iidhinishwe kupitia Bunge. Sanamu hiyo ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilidhaminiwa na mwanasiasa wa Republican, Seneta Jason Rapert. Hata hivyo, chini ya saa 24 baada ya kuwekwa, mwanamume mmoja alivurumisha gari na kuugonga mnara huo na kuubomoa. Maandamano ya Satanic Temple Arkansas yalisababisha kuandaliwa kwa maandamano mengine ya kuwapinga yaliyoandaliwa na makundi ya Kikristo na Wanachama wa Republican. Wakristo walikuwa wamebeba karatasi zilizokuwa na ujumbe kutoka kwenye Biblia. Satanic Temple waliwasilisha ombi la kushirikishwa kwenye kesi ya kupinga mnara huo wa Amri Kumi za Mungu iliyowasilishwa na shirika la haki za kiraia la American Civil Liberties Union, lakini kundi hilo limewasilisha ombi kutaka wasishirikishwe kwenye kesi hiyo.

    Sanamu hiyo ya Baphomet ilizinduliwa mara ya kwanza katika mji wa Detroit, Michigan. Mipango ya kuuweka nje ya Makao Makuu ya jimbo la Oklahoma ambapo kulikuwa kumewekwa mnara mwingine wa Amri Kumi za Mungu mwaka 2015. Mnara huo ulizinduliwa Julai 25 Mwaka huo, ambapo kupitia taarifa yao, Satanic temple walisema: "Tulichagua Baphomet kwa sababu ni kiumbe ambaye huhusishwa na Shetani na maana inayohusishwa naye inafaa sana akiwekwa kando na Sanamu inayowakilisha dini nyingine." Sherehe ya kuizindua ilikuwa ya faragha, na ukumbi uliotumiwa uliwekwa siri kubwa kwani Wakristo walikuwa wameandamana awali kuipinga mjini. Picha zilizopakiwa kwenye Facebook zilionyesha uzinduzi wake ulifanyika karibu na Mto wa Detroit. Kabla ya uzinduzi huo kufanyika, waumini takriban 200 walihudhuria ibada ya misa katika kanisa la St. Joseph mjini humo kupinga sanamu hiyo. Wengine 50 walifanya maombi mjini katika eneo ambalo awali Satanic Temple walikuwa wamepanga kuuzindulia mnara huo hapo.

    Mwanamume yule yule aliyeuharibu mnara wa Arkansas anadaiwa kufanya vivyo hivyo na kuubomoa mnara mwingine kama huo wa Amri Kumi za Mungu nje ya Makao Makuu ya jimbo la Oklahoma.
    Satanic Temple walisitisha juhudi zao za kutaka kuweka sanamu ya Baphomet huko baada ya Mahakama ya Juu ya Oklahoma kuamua kwamba Sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilikuwa imewekwa kinyume cha sheria, hivyo wakawa wameshinda vita bila kupigana. Mahakama ilisema ni kinyume cha sheria kutumia mali ya umma kwa manufaa ya dini yoyote ile.

    Jina hili Baphomet, asili yake ni enzi ya kukomesha uasi katika Kanisa Katoliki katika miaka ya 1100, kwa Kiingereza "Inquisition", na kuteswa kwa wapiganaji wa kidini kwa jina la "Knights Templar" waliokuwa wanateswa ili wafichue siri zao na wakubali kuifuata dini kwa mujibu wa viongozi wa kanisa wa wakati huo. Kwa mujibu wa waandishi wa enzi za vita vya kidini maarufu kama Crusade, wapiganaji hao walikiri kumuabudu Mungu wa wapagani kwa jina la Baphometh.

    Baadhi ya wasomi hata hivyo huamini kwamba "Baphometh" ni upotoshaji wa jina "Mahomet" - ambalo hutumiwa kumrejelea Nabii Muhammad, jambo linalozua utata zaidi. Lakini kadiri miaka ilivyosonga na mafumbo na siri kuhusu Utata wa Knights Templar kuzidi, ndivyo ufafanuzi wa neno hilo na maana yake ulivyozidi kutofautiana. Moja ya tafsiri ya neno hilo inapatikana katika kitabu cha "Da Vinci Code" cha ,Dan Brown, ambapo, neno Baphomet limefafanuliwa na kutafsiriwa kama "Sophia" au busara.

    Picha maarufu zaidi ya Baphomet ilichorwa na mzungu wa Ufaransa aitwaye , Eliphas Levi, mwaka 1856 katika kitabu chake cha Transcendental Magic: Its Doctrine and Ritual. Alichora kiumbe mwenye mabawa na mwenye pembe na mwenge ulio katikati ya pembe hizo kichwani. Kuna mchoro pia wa pembe nane kwenye paji la uso. Mikononi kumeandikwa maneno ya Kilatino SOLVE (tenganishwa) na COAGULA (fungamanisha) - ambazo ni nguvu za kuunganisha na kutenganisha ambazo zilitwaliwa kutoka kwa Mungu. Mchoro wa Levi ulihamasisha zaidi sanamu inayotumiwa na Satanic Temple.

    Ni jinsia mbili kwa pamoja, nusu mnyama na nusu binadamu.anapiga saluti ya vidole viwili Sanamu hiyo ina vidole viwili vilivyoelekezwa juu mkono wa kulia na viwili vinavyoelekezwa chini mkono wa kushoto, maana yake "kama ilivyo juu, na chini iwe pia". Maneno hayo na ishara hiyo ya vidole ni maarufu miongoni mwa wenye kuamini katika mizungu na mafumbo. Chanzo chake ni kazi za kale za msomi Hermes Trismegistus, ambaye vitabu vyake vilikuwa maarufu sana enzi ya Kipindi cha mwamko wa sanaa na mageuzi ya kidini, maarufu kama "Renaissance and Reformation" barani Ulaya. Maneno hayo pia hutumiwa kuhusiana na sayansi, vitu vyote na Mungu, lakini Levi aliandika kwamba kwa kutumia ishara hiyo, Baphomet wake alikuwa anaashiria kuwiana sawa kwa fadhila na haki. Lakini maana yake halisi ni kwamba ,shetani anatawala duniani na Mungu anatawala juu.

    Lucien Greaves, msemaji wa Satanic Temple anasema "lengo lao ni kwamba watoto watatazama kazi hiyo ya sanaa kama kwa usalama, ni sanamu isiyofaa kuzua wasiwasi wowote. "Sura ya mbuzi huyo haioneshi chochote. Si ya kishetani wala ya kutisha - kama wanavyodai baadhi ya watu - ukiitazama bila kuongozwa na mzigo wa utamaduni."
    "Sifikiri watoto wanaokutana na sanamu hii watatiwa hofu na propaganda wanaweza wasione chochote cha kuwatia wasiwasi," anasema Greaves. "Lakini si kwamba tunapinga kuwaingiza watoto kwenye mitazamo ya kidini. Mara nyingi watoto hulazimishwa kuingia kwenye dini. Hilo ni jambo hatutaki kulifanya kamwe."

    Kwenye tumbo la Baphomet kuna ishara ya kale ya Kigiriki ya nyoka wawili walio kwenye fimbo - fimbo ambayo ilibebwa na Hermes na maafisa wa kueneza matangazo au kutoa matangazo rasmi waliotumiwa kutoa matamko rasmi. Ishara hiyo kwenye sanamu hiyo inaashiria biashara, mashauriano na kutendeana, na iliingizwa kwenye Baphomet na Levi. "Kwetu ni ishara ya maridhiano ya vitu viwili tofauti - kwa mfano kuwa na sanamu ya Kishetani karibu na sanamu ya Kikristo," anasema Greaves. "Tunafikiri ni ujumbe wenye nguvu sana kuwa na sanamu hii ikiwa karibu na sanamu ya Amri Kumi za Mungu. Unaweza kuwa na mambo mawili tofauti kwa pamoja bila mzozo." Baphomet wa Levi alikuwa ni mwenye maziwa, lakini "tuliyaondoa maziwa hayo" anasema Greaves. Anasema hatukutaka wajipachike kwenye mdahalo kuhusu jinsia ya kiumbe huyo wao jambo ambalo lingewafanya watu kupoteza maana halisi. Badala yake anasema watoto wawili, mvulana na msichana, ndio wanaowakilisha jinsia. Kwa maana iliyojificha Greaves anashindwa kusema kwamba watoto hao wawili wa kike na kiume wanawakilisha ulimwengu wote na hawa ni Adam na Hawa,

    Kwenye paji la uso la Baphomet na kwenye kiti cha enzi alichokikalia kuna mchoro wa nyota ya pembe tano, ishara ambayo mara nyingi hutambuliwa kama ishara ya shetani. Mara nyingi huonekana ikiwa imepinduliwa. Msalaba wa Peter pia hupinduliwa. Greaves anasema lengo lao ni kuwafanya watu wabadilishe mtazamo wao na kuacha kuongozwa na waliyofunzwa na utamaduni wao. Waangazie mambo kwa kuzingatia ushahidi uliopo. Anasema mtazamo huo huwazuia watu kuchukua msimamo huru kuhusu masuala kama vile ndoa za wapenzi wa jinsia moja na haki za kutoa mimba pamoja na huduma nyingine za uzazi wa mpango. "Mwenge wa maarifa ndio kama upembe wa kati na inatukuza juhudi za kutafuta elimu na maarifa. Tunathamini hilo sana," anasema Greaves.

    Levi mwenyewe aliandika kwamba mwenge wa maarifa uolikuwa unawaka katikati ya pembe za Baphomet ni mwanga wa kusawazisha vitu vyote. Ni taswira ya roho iliyo juu ya vitu vyote vinavyoonekana, kama zilivyo ndimi za moto, ingawa bado imeunganishwa na vitu hivyo, mfano moto unavyoendelea kung'aa juu ya mafuta au kijiti. Kulikuwa na mpango wa kuongeza maandiko kwenye mchoro wa nyota ya pembe tano ya moja ya nguzo saba kuu za Satanic Temple: "moyo wa huruma, busara na haki unafaa daima kuongoza zaidi ya neno lililoandikwa au kutamkwa." Nyuma ya sanamu hiyo, kutakuwa na nukuu kutoka kwa kitabu cha Cain chake Lord Byron unaosema: "Kisha, nani alikuwa Ibilisi? Yule hangekuruhusu wewe uishi milele, au yule ambaye angelikuumba uishi milele, katika raha na nguvu za elimu na maarifa?"

    Kwa mujibu wa tovuti yao Satanic Temple wanaamini kwamba "kimsingi watu kuteseka au kuumia ni vibaya, na chochote kile kinachopunguza madhila na mateso ni kizuri." Hawaamini katika kutenda mabaya. Wanasema: "Huwa tunakumbatia kukufuru kama njia halali ya kujieleza na kuonyesha uhuru wa mtu binafsi dhidi ya imani za kitamaduni zisizo na tija." "Msimamo wa Satanic Temple ni kwamba dini inaweza, na inafaa kutenganishwa na ushirikina. Hivyo basi, huwa hawaendelezi imani katika Shetani binafsi. "Kukumbatia jina la Shetani ni kukumbatia mtazamo wa kutumia fikira na kujiondoa kutoka katika mfumo wa kuamini katika nguvu za kipekee za kutoka nje ya dunia na utamaduni uliopitwa na wakati wenye msingi wake katika ushirikina."
    BAPHOMET: SANAMU LA SHETANI LILILOLETA UTATA NCHINI MAREKANI. Binadamu tangu zama za kale amekuwa akijenga, kuchonga na kuweka sanamu za aina nyingi kwa sababu mbalimbali. Baadhi hutumiwa kuwaenzi watu maarufu na kuwakumbuka, na nyingine huabudiwa kama miungu. Kwa muda mrefu hata hivyo imekuwa ni nadra kuona sanamu ambayo moja kwa moja inahusishwa na shetani au ibilisi. Lakini ukifika Marekani, mambo ni tofauti. Kuna sanamu moja kubwa ya shaba ambayo inahusishwa na ushetani. Ni sanamu ya, Baphomet ni kiumbe mwenye kichwa kinachofanana na cha mbuzi lakini ameongezwa maungo ya ajabu. Ni kiumbe mwenye mabawa, na kwenye sanamu hiyo inayotumiwa kwa sasa huoneshwa akiwa na watoto wawili wanaotabasamu. Sanamu inayotumiwa kwa sasa ina urefu wa karibu futi 9, na iligharimu $100,000 (£64,000) kuitengeneza. Sanamu hii imekuwa ikitumiwa kuwapiga vita wale walio na imani za Kikristo kiislamu na imani nyingine zenye kumcha Mungu mmoja. Ni sanamu hii ambayo imekuwa ikitumiwa kuendesha vita dhidi ya kuwekwa kwa sanamu za Kikristo na dini nyingine katika majengo maarufu, bustani na maeneo ya umma nchini Marekani. Agosti 17, sanamu hiyo ya kiumbe anayefahamika kama Baphomet ilipelekwa katika jimbo la Arkansas anakotoka Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton. Wanaotumia sanamu hiyo ni watu wa kundi linalofahamika kama Satanic Temple (Hekalu la Shetani) ambalo ni kundi la 'kidini' na kisiasa ambalo hupinga kuingizwa kwa dini katika masuala ya Serikali. Kundi hilo liliandaa maandamano ya watu 150 waliyojumuisha waabudu shetani, watu wasioamini Mungu yupo, na Wakristo pia. Maandamano hayo yalifanyika nje ya jengo lililo Makao Makuu ya jimbo la Arkansas katika mji wa Little Rock. Walikuwa wamekerwa na hatua ya kuweka sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu katika uwanja wa Makao Makuu hayo. Satanic Temple walisema sanamu hiyo inakiuka Sheria ya Kwanza ya Marekebisho ya Katiba nchini Marekani ambayo huzungumzia uhuru na haki za kidini. "Ikiwa utakubaliana na kuwepo kwa sanamu ya dini moja basi kunafaa kuwa na uhuru kwa wengine kuweka sanamu za kidini, na ukizuia basi kusiwe na sanamu yoyote ile," mwanzilishi mwenza wa tawi la Satanic Temple katika jimbo la Arkansas, Ivy Forrester, alinukuliwa na wanahabari siku hiyo ya maandamano. Ndoto yao ni kuwa na sanamu ya kudumu, lakini siku hiyo hawakuruhusiwa na sheria kuiweka kwa muda mrefu. Kuna sheria ya Arkansas ya mwaka 2017 inayohitaji sanamu ya kuwekwa maeneo ya Serikali iwe na udhamini wa Mbunge ambaye atawasilisha mswada iidhinishwe kupitia Bunge. Sanamu hiyo ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilidhaminiwa na mwanasiasa wa Republican, Seneta Jason Rapert. Hata hivyo, chini ya saa 24 baada ya kuwekwa, mwanamume mmoja alivurumisha gari na kuugonga mnara huo na kuubomoa. Maandamano ya Satanic Temple Arkansas yalisababisha kuandaliwa kwa maandamano mengine ya kuwapinga yaliyoandaliwa na makundi ya Kikristo na Wanachama wa Republican. Wakristo walikuwa wamebeba karatasi zilizokuwa na ujumbe kutoka kwenye Biblia. Satanic Temple waliwasilisha ombi la kushirikishwa kwenye kesi ya kupinga mnara huo wa Amri Kumi za Mungu iliyowasilishwa na shirika la haki za kiraia la American Civil Liberties Union, lakini kundi hilo limewasilisha ombi kutaka wasishirikishwe kwenye kesi hiyo. Sanamu hiyo ya Baphomet ilizinduliwa mara ya kwanza katika mji wa Detroit, Michigan. Mipango ya kuuweka nje ya Makao Makuu ya jimbo la Oklahoma ambapo kulikuwa kumewekwa mnara mwingine wa Amri Kumi za Mungu mwaka 2015. Mnara huo ulizinduliwa Julai 25 Mwaka huo, ambapo kupitia taarifa yao, Satanic temple walisema: "Tulichagua Baphomet kwa sababu ni kiumbe ambaye huhusishwa na Shetani na maana inayohusishwa naye inafaa sana akiwekwa kando na Sanamu inayowakilisha dini nyingine." Sherehe ya kuizindua ilikuwa ya faragha, na ukumbi uliotumiwa uliwekwa siri kubwa kwani Wakristo walikuwa wameandamana awali kuipinga mjini. Picha zilizopakiwa kwenye Facebook zilionyesha uzinduzi wake ulifanyika karibu na Mto wa Detroit. Kabla ya uzinduzi huo kufanyika, waumini takriban 200 walihudhuria ibada ya misa katika kanisa la St. Joseph mjini humo kupinga sanamu hiyo. Wengine 50 walifanya maombi mjini katika eneo ambalo awali Satanic Temple walikuwa wamepanga kuuzindulia mnara huo hapo. Mwanamume yule yule aliyeuharibu mnara wa Arkansas anadaiwa kufanya vivyo hivyo na kuubomoa mnara mwingine kama huo wa Amri Kumi za Mungu nje ya Makao Makuu ya jimbo la Oklahoma. Satanic Temple walisitisha juhudi zao za kutaka kuweka sanamu ya Baphomet huko baada ya Mahakama ya Juu ya Oklahoma kuamua kwamba Sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilikuwa imewekwa kinyume cha sheria, hivyo wakawa wameshinda vita bila kupigana. Mahakama ilisema ni kinyume cha sheria kutumia mali ya umma kwa manufaa ya dini yoyote ile. Jina hili Baphomet, asili yake ni enzi ya kukomesha uasi katika Kanisa Katoliki katika miaka ya 1100, kwa Kiingereza "Inquisition", na kuteswa kwa wapiganaji wa kidini kwa jina la "Knights Templar" waliokuwa wanateswa ili wafichue siri zao na wakubali kuifuata dini kwa mujibu wa viongozi wa kanisa wa wakati huo. Kwa mujibu wa waandishi wa enzi za vita vya kidini maarufu kama Crusade, wapiganaji hao walikiri kumuabudu Mungu wa wapagani kwa jina la Baphometh. Baadhi ya wasomi hata hivyo huamini kwamba "Baphometh" ni upotoshaji wa jina "Mahomet" - ambalo hutumiwa kumrejelea Nabii Muhammad, jambo linalozua utata zaidi. Lakini kadiri miaka ilivyosonga na mafumbo na siri kuhusu Utata wa Knights Templar kuzidi, ndivyo ufafanuzi wa neno hilo na maana yake ulivyozidi kutofautiana. Moja ya tafsiri ya neno hilo inapatikana katika kitabu cha "Da Vinci Code" cha ,Dan Brown, ambapo, neno Baphomet limefafanuliwa na kutafsiriwa kama "Sophia" au busara. Picha maarufu zaidi ya Baphomet ilichorwa na mzungu wa Ufaransa aitwaye , Eliphas Levi, mwaka 1856 katika kitabu chake cha Transcendental Magic: Its Doctrine and Ritual. Alichora kiumbe mwenye mabawa na mwenye pembe na mwenge ulio katikati ya pembe hizo kichwani. Kuna mchoro pia wa pembe nane kwenye paji la uso. Mikononi kumeandikwa maneno ya Kilatino SOLVE (tenganishwa) na COAGULA (fungamanisha) - ambazo ni nguvu za kuunganisha na kutenganisha ambazo zilitwaliwa kutoka kwa Mungu. Mchoro wa Levi ulihamasisha zaidi sanamu inayotumiwa na Satanic Temple. Ni jinsia mbili kwa pamoja, nusu mnyama na nusu binadamu.anapiga saluti ya vidole viwili Sanamu hiyo ina vidole viwili vilivyoelekezwa juu mkono wa kulia na viwili vinavyoelekezwa chini mkono wa kushoto, maana yake "kama ilivyo juu, na chini iwe pia". Maneno hayo na ishara hiyo ya vidole ni maarufu miongoni mwa wenye kuamini katika mizungu na mafumbo. Chanzo chake ni kazi za kale za msomi Hermes Trismegistus, ambaye vitabu vyake vilikuwa maarufu sana enzi ya Kipindi cha mwamko wa sanaa na mageuzi ya kidini, maarufu kama "Renaissance and Reformation" barani Ulaya. Maneno hayo pia hutumiwa kuhusiana na sayansi, vitu vyote na Mungu, lakini Levi aliandika kwamba kwa kutumia ishara hiyo, Baphomet wake alikuwa anaashiria kuwiana sawa kwa fadhila na haki. Lakini maana yake halisi ni kwamba ,shetani anatawala duniani na Mungu anatawala juu. Lucien Greaves, msemaji wa Satanic Temple anasema "lengo lao ni kwamba watoto watatazama kazi hiyo ya sanaa kama kwa usalama, ni sanamu isiyofaa kuzua wasiwasi wowote. "Sura ya mbuzi huyo haioneshi chochote. Si ya kishetani wala ya kutisha - kama wanavyodai baadhi ya watu - ukiitazama bila kuongozwa na mzigo wa utamaduni." "Sifikiri watoto wanaokutana na sanamu hii watatiwa hofu na propaganda wanaweza wasione chochote cha kuwatia wasiwasi," anasema Greaves. "Lakini si kwamba tunapinga kuwaingiza watoto kwenye mitazamo ya kidini. Mara nyingi watoto hulazimishwa kuingia kwenye dini. Hilo ni jambo hatutaki kulifanya kamwe." Kwenye tumbo la Baphomet kuna ishara ya kale ya Kigiriki ya nyoka wawili walio kwenye fimbo - fimbo ambayo ilibebwa na Hermes na maafisa wa kueneza matangazo au kutoa matangazo rasmi waliotumiwa kutoa matamko rasmi. Ishara hiyo kwenye sanamu hiyo inaashiria biashara, mashauriano na kutendeana, na iliingizwa kwenye Baphomet na Levi. "Kwetu ni ishara ya maridhiano ya vitu viwili tofauti - kwa mfano kuwa na sanamu ya Kishetani karibu na sanamu ya Kikristo," anasema Greaves. "Tunafikiri ni ujumbe wenye nguvu sana kuwa na sanamu hii ikiwa karibu na sanamu ya Amri Kumi za Mungu. Unaweza kuwa na mambo mawili tofauti kwa pamoja bila mzozo." Baphomet wa Levi alikuwa ni mwenye maziwa, lakini "tuliyaondoa maziwa hayo" anasema Greaves. Anasema hatukutaka wajipachike kwenye mdahalo kuhusu jinsia ya kiumbe huyo wao jambo ambalo lingewafanya watu kupoteza maana halisi. Badala yake anasema watoto wawili, mvulana na msichana, ndio wanaowakilisha jinsia. Kwa maana iliyojificha Greaves anashindwa kusema kwamba watoto hao wawili wa kike na kiume wanawakilisha ulimwengu wote na hawa ni Adam na Hawa, Kwenye paji la uso la Baphomet na kwenye kiti cha enzi alichokikalia kuna mchoro wa nyota ya pembe tano, ishara ambayo mara nyingi hutambuliwa kama ishara ya shetani. Mara nyingi huonekana ikiwa imepinduliwa. Msalaba wa Peter pia hupinduliwa. Greaves anasema lengo lao ni kuwafanya watu wabadilishe mtazamo wao na kuacha kuongozwa na waliyofunzwa na utamaduni wao. Waangazie mambo kwa kuzingatia ushahidi uliopo. Anasema mtazamo huo huwazuia watu kuchukua msimamo huru kuhusu masuala kama vile ndoa za wapenzi wa jinsia moja na haki za kutoa mimba pamoja na huduma nyingine za uzazi wa mpango. "Mwenge wa maarifa ndio kama upembe wa kati na inatukuza juhudi za kutafuta elimu na maarifa. Tunathamini hilo sana," anasema Greaves. Levi mwenyewe aliandika kwamba mwenge wa maarifa uolikuwa unawaka katikati ya pembe za Baphomet ni mwanga wa kusawazisha vitu vyote. Ni taswira ya roho iliyo juu ya vitu vyote vinavyoonekana, kama zilivyo ndimi za moto, ingawa bado imeunganishwa na vitu hivyo, mfano moto unavyoendelea kung'aa juu ya mafuta au kijiti. Kulikuwa na mpango wa kuongeza maandiko kwenye mchoro wa nyota ya pembe tano ya moja ya nguzo saba kuu za Satanic Temple: "moyo wa huruma, busara na haki unafaa daima kuongoza zaidi ya neno lililoandikwa au kutamkwa." Nyuma ya sanamu hiyo, kutakuwa na nukuu kutoka kwa kitabu cha Cain chake Lord Byron unaosema: "Kisha, nani alikuwa Ibilisi? Yule hangekuruhusu wewe uishi milele, au yule ambaye angelikuumba uishi milele, katika raha na nguvu za elimu na maarifa?" Kwa mujibu wa tovuti yao Satanic Temple wanaamini kwamba "kimsingi watu kuteseka au kuumia ni vibaya, na chochote kile kinachopunguza madhila na mateso ni kizuri." Hawaamini katika kutenda mabaya. Wanasema: "Huwa tunakumbatia kukufuru kama njia halali ya kujieleza na kuonyesha uhuru wa mtu binafsi dhidi ya imani za kitamaduni zisizo na tija." "Msimamo wa Satanic Temple ni kwamba dini inaweza, na inafaa kutenganishwa na ushirikina. Hivyo basi, huwa hawaendelezi imani katika Shetani binafsi. "Kukumbatia jina la Shetani ni kukumbatia mtazamo wa kutumia fikira na kujiondoa kutoka katika mfumo wa kuamini katika nguvu za kipekee za kutoka nje ya dunia na utamaduni uliopitwa na wakati wenye msingi wake katika ushirikina."
    0 Comments ·0 Shares ·1K Views
  • MUONEKANO WA NABII ISSA MIAKA HIYO ULIKUWAJE ?

    Karibu kila mtu ana dhana fulani kuhusu muonekano wa Yesu Kristo.
    Ndiye mtu aliyechorwa zaidi katika sanaa ya Magharibi. Picha zake hutambuliwa kwa urahisi, ambapo huoneshwa akiwa na nywele na ndevu, akiwa amevalia vazi lefu lenye mikono mirefu linalofanana na kanzu ( la rangi nyeupe), na pia akiwa amejifunga joho (la rangi ya samawati). Muonekano wa Yesu umefahamika sana na wengi kiasi kwamba unaweza kutambuliwa ukiwa hata kwenye mikate au biskuti.

    Picha za sasa za Yesu zinatokana na enzi ya Byzantine, himaya iliyokuwa na mji mkuu wake Constantinople. Ni picha iliyoanza kutumika karne ya nne hivi. Michoro ya Yesu ya wakati wa utawala wa Byzantine ilikuwa ya ishara, na si muonekano wake. Wasanii waliangazia zaidi maana na si kumfananisha na Yesu mwenyewe.
    Picha zao ziliongozwa na dhana ya Yesu kama mtawala, kwenye kiti cha enzi, kama anavyoonyeshwa kwenye mchoro ulio kwenye altari ya kanisa la Santa Pudenziana jijini Roma.

    Yesu anaoneshwa akiwa amevalia mgolole wa rangi ya dhahabu.
    Ndiye mtawala wa dunia yote aliyetoka mbinguni, mfanano wa picha yake ni ule wa sanamu ya Zeus wa Olympus anayeonyeshwa akiwa na nywele ndefu za ndevu kwenye kiti cha enzi. Ni sanamu iliyokuwa maarufu sana wakati huo kiasi kwamba Mfalme Augustus wa Roma alishurutisha naye atengenezewe sanamu kama hiyo, lakini yake ikiwa bila nywele ndefu na ndevu, Wasanii wa Byzantine, walitaka kumuonyesha Kristo kama mtawala kutoka mbinguni, mfalme wa aina yake, na hivyo wakachora wakimuonyesha kama Zeus, lakini akiwa mdogo kidogo wa umri.

    Kilichotokea kadiri miaka ilivyosonga ni kwamba kuonyeshwa huku kwa Kristo kama mtawala kutoka mbinguni - ambapo wakati mwingine ameonyeshwa hata akiwa kama 'hippie' au 'superstar' (kama ilivyo kwenye mchoro huu hapa chini) - ndiko kumekuwa kama kigezo chetu cha Yesu alivyokuwa. Hebu tuchanganue kutoka kichwani hadi vidole vya miguuni. Wakristo wa nyakati za kwanza wakati walipokuwa wanamwonyesha Kristo si kama mtawala kutoka mbinguni, walimuonyesha kama binadamu wa kawaida tu - akiwa hana ndevu na hana nywele ndefu.

    Lakini pengine, kama msomi wa aina yake aliyekuwa akisafiri kutoka eneo moja hadi jingine, Yesu pengine alikuwa na ndevu, kwa sababu hakuwa akienda kwa vinyozi. Kwa kawaida, kuwa mchafu kiasi na kuwa na ndevu ndefu ni sifa ambazo zilihusishwa na wanafalsafa, wasomi wa ngazi ya juu, na kuwatenganisha na watu wa kawaida.
    Mwanafalsafa maarufu wa kundi la Stoic (Wanafalsafa wa Kigiriki waliofuata mafundisho ya mwanzilishi wao Zeno wa Citium mjini Athens mapema karne ya 3 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu) Epictetus aliamini "ilifaa hivyo kwa mujibu wa maumbile." Mambo yalibadilika katika karne ya 1 baada ya kuzaliwa kwa Yesu, wakati wa enzi za Warumi na Wagiriki, ambapo kuwa na nywele fupi na kunyoa ndefu ndiyo mambo yaliyochukuliwa kuwa yafaayo na ya kistaarabu.

    Kuwa na nywele ndefu na ndevu ni mambo ambayo yaliachiwa miungu pekee, si ya watu wa kawaida. Hata wanafalsafa enzi hizo walikuwa na nywele fupi. Ndevu pia hazikuwa sifa za kuwatambulisha Wayahudi enzi hizo. Ukweli ni kwamba moja ya changamoto ambazo waliotaka kuwatesa Wayahudi vipindi mbalimbali katika historia walihangaika sana kuwatofautisha na watu wengine. Hii ni kwa sababu wote walifanana (jambo ambalo limegusiwa katika kitabu cha Wamakabayo). Hata hivyo, picha za wanaume wa Kiyahudi zilizokuwa kwenye sarafu za Judea Capta ambazo zilitolewa na utawala wa Roma baada ya kutekwa kwa mji wa Yerusalemu mwaka 70 baada ya kuzaliwa kwa Yesu zinawaonesha wanaume wakiwa na ndevu, lakini nywele zao si ndefu.

    Kwa hivyo, Yesu, kama mwanafalsafa wa muonekano wa kawaida, kuna uwezekano alikuwa na ndevu lakini si ndefu sana, sawa na wanaume hao walioonyeshwa kwenye sarafu za Judaea Capta, lakini nywele zake basi hazikuwa ndefu sana pia.
    Kama ingetokea kwamba awe na nywele ndefu hata kidogo tu kuliko kawaida, basi angezua mtafaruku Wanaume wa Kiyahudi waliokuwa na ndevu ambazo hazikuwa zimetunzwa vyema na nywele ambazo zilikuwa ndefu kidogo kuliko kawaida walitambulika mara moja kama watu waliokuwa wamekula kiapo cha kuwa Wanazari (Nazarite).

    Hii ilikuwa na maana kwamba wangejitoa wakfu kwa Mungu kwa kipindi fulani, ambapo hawangekunywa vileo wala kuzikata nywele zao. Mwisho wa kipindi hicho, wangenyolewa nywele zao katika sherehe maalum hekaluni Jerusalem (kama inavyoelezwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Sura ya 21, aya ya 24).
    Lakini Yesu hakuwa amekula kiapo cha kuwa Mnazari, kwa sababu mara nyingi tunamsikia kwenye Biblia akinywa divai - wakosoaji wake hata wakati mwingine wanamshutumu kwa kunywa divai sana, kupita kiasi (Matayo Sura ya 11, aya ya 19). Kama angekuwepo na nywele ndefu, na kuonekana kama Mnazari, tungelitarajia basi kuwepo na tamko pahala fulani kuhusu tofauti ya muonekano wake na matendo aliyokuwa akiyafanya ambayo hayakuendana na Unazari. Hali kwamba alikuwa akinywa divai yenyewe ingekuwa tatizo kubwa.

    Wakati Yesu alipoishi, matajiri walizoea kuvalia kanzu na majoyo ya vitambaa vya thamani, kuonyesha hadhi yao katika jamii. Katika moja ya mahubiri yake, Yesu anasema : "Jihadharini na walimu wa sheria (waandishi). Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu (stolai), na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Pia wao hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kupewa nafasi za heshima katika karamu." Mafundisho haya ya Yesu kwa kawaida huchukuliwa kama yenye maelezo ya kuaminika zaidi kwenye Injili, hivyo tunaweza kuwa na msingi kuamini kwamba Yesu hakuvalia mavazi kama hayo marefu. Kwa jumla, mwanamume wakati huo wa Yesu angevalia gwanda au kanzu fupi hivi, na mwanamke angevalia vazi lililomfika kwenye kifundo cha mguu.

    Kwa hivyo, katika karne ya 2 kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume, Paul na Thecla, inapotokea kwamba Thecla ambaye ni mwanamke anavalia kanzu fupi kama mwanamume, hilo ni jambo linaloshangaza sana. Kanzu hizi kwa kawaida zingekuwa na ukanda au mstari wa rangi tofauti kutoka kwenye bega hadi kwenye pindo sehemu ya chini. Ni vazi ambalo lingeshonwa au kufumwa kama kipande kimoja cha vazi. Juu ya kanzu hiyo, ungejifunga joho au vazi jingine la nje, na tunajua kwamba Yesu alivalia vazi kama hilo kwa sababu ndilo lililoguswa na mwanamke aliyetaka kuponywa naye. (Marko 5:27): Alikuwa amesikia habari za Yesu, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, kwa maana alisema moyoni mwake, 'Kama nikiweza kuligusa vazi lake tu, nitaponywa.') Vazi hilo la nje lilifumwa kwa manyoya, lakini halikuwa zito sana na ndipo ili uhisi joto ingemlazimu mtu kuvalia mavazi mawili kama hayo.

    Vazi hilo lingevaliwa kwa njia nyingi, na wakati mwingine lingening'inia hadi chini ya magoti na kulifunika lile kanzu fupi la ndani. (Baadhi ya wanafalsafa walizoea kuvalia vazi hilo la nje pekee bila kuvalia ile kanzu ya ndani na kuacha sehemu ya bega au kifua ikiwa wazi). Mamlaka na hadhi ya mtu ni vitu ambavyo vilidhihirishwa kupitia ubora, ukubwa na rangi ya mavazi hayo ya nje. Rangi ya zambarau na baadhi ya aina za rangi ya buluu (samawati) ni rangi zilizoashiria utajiri, hadhi na kujionea fahari. Zilikuwa ni rangi za kifahari kwa sababu viungo vya kutengeneza rangi hizo vilikuwa adimu na ghali sana.

    Lakini rangi pia huashiria kitu kingine tofauti. Mwanahistoria Josephus, anawaeleza walokole waliofahamika kama Zealots (kundi la Wayahudi wa itikadi kali waliotaka kuwafurusha Warumi kutoka Judea) kama kundi la wahalifu wauaji waliovalia mavazi ya nje yaliyopakwa rangi kwa jina - mavazi anayoyaita chlanidia - kuashiria kwamba yalikuwa ni kama mavazi yaliyovaliwa na wanawake. Hii inaashiria kwamba wanaume kamili, kama hawakuwa na cheo cha juu zaidi katika jamii, walifaa kuvalia mavazi yasiyopakwa rangi.
    Yesu hakuvalia mavazi meupe hata hivyo. Haya yalikuwa mavazi ya kipekee na yalihitaji kupaushwa mara kwa mara (kufanywa meupe tena) au kupakwa chokaa. Judea, mavazi kama hayo meupe yalihusishwa na kundi lililofahamika kama Essenes - ambao ni watu waliofuata ufasiri mkali wa sheria za Kiyahudi. Tofauti kati ya mavazi ya Yesu na mavazi mengine ya rangi nyeupe ya kung'aa inaelezwa kwenye sura ya 9 ya Marko ambapo anaandamana na mitume watatu mlimani.

    Yesu aliwachukua "Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao. Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angaliweza kuyangʼarisha. Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu." Marko anaeleza kwamba mavazi ya Yesu yaligeuka rangi yakawa meupe sana, hapa anarejelea vazi la ndani na si la nje. Kabla ya kugeuka sura huku kwa Yesu, anaoneshwa na Marko kama mwanamume wa kawaida, aliyevalia mavazi ya kawaida, ambayo ni ya rangi ambayo haijapaushwa. Katika hali ambayo ndipo yang'ae na kuangaza unahitaji kumpelekea fundi.

    Tunaelezwa zaidi kuhusu mavazi ya Yesu wakati wa kusulubiwa kwake, pale wanajeshi wa Kirumi wanapoyakata mavazi yake ya nje vipande vinne (Yohana19:23: Askari walipokwisha kumsulubisha Yesu, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini.) Kuna uwezekano mavazi hayo ya nje yalikuwa mavazi mawili.

    Moja ya vazi hili huenda lilikuwa ni tallith, ambalo ni vazi la kujifunga Kiyahudi wakati wa maombi. Vazi hili lenye shada (tzitzith) limetajwa moja kwa moja na Yesu katika kitabu cha Mathayo 23:5 anapozungumza kuhusu walimu wa sheria na Mafarisayo (Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao). Lilikuwa ni vazi la nje lisilo zito, ambalo kawaida lilitengenezwa kwa kitambaa cha manyoya na lilikuwa la rangi ya malai hivi (krimu), na pengine lilikuwa na ukanda au mstari wa rangi ya nili (bluu iliyoiva).

    Miguuni, Yesu angevalia ndara (kandambili au malapa). Kila mtu wakati huo alivalia ndara. Katika mapango yaliyo jangwani karibu na Bahari ya Chumvi (Bahari Mfu) na Masada, ndara za wakati alipoishi Yesu zimegunduliwa, na tunaweza kutazama ndara ambazo huenda alivaa zilivyoonekana. Zilikuwa hazijafanyiwa kazi nyingi sana ya kiufundi. Soli (nyayo au kikanyagio) zake zilikuwa vipande vigumu vya ngozi vilivyoshonwa pamoja, na juu kulikuwa ni kanda za ngozi ambazo mbele zingeingizwa katikati ya vidole, kama malapa tu ya siku hizi.

    Yesu (Nabii Issa) Alikuwa Myahudi, na uso wake pia bila shaka ungefanana na Wayahudi wa wakati huo. Hali kwamba Yesu alikuwa Myahudi (au Mjudea) ni jambo linalorejelewa katika vitabu vingi, zikiwemo barua za Mtume Paulo. Na katika barua yake kwa Waebrania, anaandika: "Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda" (Sura ya 7:14) Kwa hivyo, Myahudi wa wakati huo, mwanamume wa miaka 30 hivi alipoanza kueneza Injili kwa mujibu wa Luka 3, pia akiwa ni mwenye ngozi nyeusi kama ilivyokuwa kwa wayahudi wengi zama zile waliokuwa wakitembeleana na ndugu zao wa Misri (Kushi) kemet.

    Mwaka 2001 mwanaantholopojia (mtaalamu wa elimu ya binadamu hasa elimu ihusuyo habari zinazohusu asili na maendeleo yake ya awali) Richard Neave alitengeneza mfano wa mwanamume wa Galilaya wa zama za Yesu ambao ulitumiwa kwa jina Son of God (Mwana wa Mungu). Alitumia fuvu lililopatikana katika eneo hilo. Hakusema kwamba huo ulikuwa muonekano wa uso wa Yesu. Mfano ulikuwa tu wa kuchochea hisia na kuwafanya watu kumfikiria Yesu kama mwanamume wa zama hizo na eneo hilo, kwa sababu hakuna mchoro wala maelezo yaliyopo ya kina kuhusu muonekano wake halisi.

    Ingawa tunaweza kupata viashiria kutoka kwa teknolojia na kutumia mifupa ya watu wa kale, kiashiria cha karibu sana kuhusu pengine Yesu alionekana vipi labda kinaweza kutokana na mchoro wa Musa kwenye ukuta wa sinagogi ya karne ya 3 ya Dura-Europos, kwani mchoro huo unaonesha jinsi Myahudi wa hekima alidhaniwa kuwa wakati wa utawala wa Wagiriki na Warumi. Musa anaoneshwa akiwa na mavazi ambayo hayajapaushwa, na moja ya vazi lake la nje ni tallith.

    Katika mchoro huo wa Dura wa Musa akitenganisha maji kwenye Bahari ya Sham ili Waisraeli wapite, unaweza kuziona shada (tzitzith) kwenye kona za vazi hilo. Kwa kiwango kikubwa, picha hiyo pengine inatoa msingi bora zaidi wa kumfikiria Yesu alivyokuwa badala ya picha za sasa zinazoongozwa na busara na mawazo ya enzi ya Byzantine - alikuwa na nywele fupi, ndevu fupi, na alikuwa amevalia kanzu fupi lenye mikono mifupi, na alikuwa na joho au vazi la nje.

    Makala hii chimbuko lake ni makala ya Kiingereza ya Joan Taylor ambaye ni profesa wa kitivo cha Asili ya Ukristo na Hekalu la Pili la Wayahudi katika Chuo Kikuu cha King's College London na ndiye mwandishi wa kitabu kwa jina The Essenes, the Scrolls and the Dead Sea.
    MUONEKANO WA NABII ISSA MIAKA HIYO ULIKUWAJE ? Karibu kila mtu ana dhana fulani kuhusu muonekano wa Yesu Kristo. Ndiye mtu aliyechorwa zaidi katika sanaa ya Magharibi. Picha zake hutambuliwa kwa urahisi, ambapo huoneshwa akiwa na nywele na ndevu, akiwa amevalia vazi lefu lenye mikono mirefu linalofanana na kanzu ( la rangi nyeupe), na pia akiwa amejifunga joho (la rangi ya samawati). Muonekano wa Yesu umefahamika sana na wengi kiasi kwamba unaweza kutambuliwa ukiwa hata kwenye mikate au biskuti. Picha za sasa za Yesu zinatokana na enzi ya Byzantine, himaya iliyokuwa na mji mkuu wake Constantinople. Ni picha iliyoanza kutumika karne ya nne hivi. Michoro ya Yesu ya wakati wa utawala wa Byzantine ilikuwa ya ishara, na si muonekano wake. Wasanii waliangazia zaidi maana na si kumfananisha na Yesu mwenyewe. Picha zao ziliongozwa na dhana ya Yesu kama mtawala, kwenye kiti cha enzi, kama anavyoonyeshwa kwenye mchoro ulio kwenye altari ya kanisa la Santa Pudenziana jijini Roma. Yesu anaoneshwa akiwa amevalia mgolole wa rangi ya dhahabu. Ndiye mtawala wa dunia yote aliyetoka mbinguni, mfanano wa picha yake ni ule wa sanamu ya Zeus wa Olympus anayeonyeshwa akiwa na nywele ndefu za ndevu kwenye kiti cha enzi. Ni sanamu iliyokuwa maarufu sana wakati huo kiasi kwamba Mfalme Augustus wa Roma alishurutisha naye atengenezewe sanamu kama hiyo, lakini yake ikiwa bila nywele ndefu na ndevu, Wasanii wa Byzantine, walitaka kumuonyesha Kristo kama mtawala kutoka mbinguni, mfalme wa aina yake, na hivyo wakachora wakimuonyesha kama Zeus, lakini akiwa mdogo kidogo wa umri. Kilichotokea kadiri miaka ilivyosonga ni kwamba kuonyeshwa huku kwa Kristo kama mtawala kutoka mbinguni - ambapo wakati mwingine ameonyeshwa hata akiwa kama 'hippie' au 'superstar' (kama ilivyo kwenye mchoro huu hapa chini) - ndiko kumekuwa kama kigezo chetu cha Yesu alivyokuwa. Hebu tuchanganue kutoka kichwani hadi vidole vya miguuni. Wakristo wa nyakati za kwanza wakati walipokuwa wanamwonyesha Kristo si kama mtawala kutoka mbinguni, walimuonyesha kama binadamu wa kawaida tu - akiwa hana ndevu na hana nywele ndefu. Lakini pengine, kama msomi wa aina yake aliyekuwa akisafiri kutoka eneo moja hadi jingine, Yesu pengine alikuwa na ndevu, kwa sababu hakuwa akienda kwa vinyozi. Kwa kawaida, kuwa mchafu kiasi na kuwa na ndevu ndefu ni sifa ambazo zilihusishwa na wanafalsafa, wasomi wa ngazi ya juu, na kuwatenganisha na watu wa kawaida. Mwanafalsafa maarufu wa kundi la Stoic (Wanafalsafa wa Kigiriki waliofuata mafundisho ya mwanzilishi wao Zeno wa Citium mjini Athens mapema karne ya 3 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu) Epictetus aliamini "ilifaa hivyo kwa mujibu wa maumbile." Mambo yalibadilika katika karne ya 1 baada ya kuzaliwa kwa Yesu, wakati wa enzi za Warumi na Wagiriki, ambapo kuwa na nywele fupi na kunyoa ndefu ndiyo mambo yaliyochukuliwa kuwa yafaayo na ya kistaarabu. Kuwa na nywele ndefu na ndevu ni mambo ambayo yaliachiwa miungu pekee, si ya watu wa kawaida. Hata wanafalsafa enzi hizo walikuwa na nywele fupi. Ndevu pia hazikuwa sifa za kuwatambulisha Wayahudi enzi hizo. Ukweli ni kwamba moja ya changamoto ambazo waliotaka kuwatesa Wayahudi vipindi mbalimbali katika historia walihangaika sana kuwatofautisha na watu wengine. Hii ni kwa sababu wote walifanana (jambo ambalo limegusiwa katika kitabu cha Wamakabayo). Hata hivyo, picha za wanaume wa Kiyahudi zilizokuwa kwenye sarafu za Judea Capta ambazo zilitolewa na utawala wa Roma baada ya kutekwa kwa mji wa Yerusalemu mwaka 70 baada ya kuzaliwa kwa Yesu zinawaonesha wanaume wakiwa na ndevu, lakini nywele zao si ndefu. Kwa hivyo, Yesu, kama mwanafalsafa wa muonekano wa kawaida, kuna uwezekano alikuwa na ndevu lakini si ndefu sana, sawa na wanaume hao walioonyeshwa kwenye sarafu za Judaea Capta, lakini nywele zake basi hazikuwa ndefu sana pia. Kama ingetokea kwamba awe na nywele ndefu hata kidogo tu kuliko kawaida, basi angezua mtafaruku Wanaume wa Kiyahudi waliokuwa na ndevu ambazo hazikuwa zimetunzwa vyema na nywele ambazo zilikuwa ndefu kidogo kuliko kawaida walitambulika mara moja kama watu waliokuwa wamekula kiapo cha kuwa Wanazari (Nazarite). Hii ilikuwa na maana kwamba wangejitoa wakfu kwa Mungu kwa kipindi fulani, ambapo hawangekunywa vileo wala kuzikata nywele zao. Mwisho wa kipindi hicho, wangenyolewa nywele zao katika sherehe maalum hekaluni Jerusalem (kama inavyoelezwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Sura ya 21, aya ya 24). Lakini Yesu hakuwa amekula kiapo cha kuwa Mnazari, kwa sababu mara nyingi tunamsikia kwenye Biblia akinywa divai - wakosoaji wake hata wakati mwingine wanamshutumu kwa kunywa divai sana, kupita kiasi (Matayo Sura ya 11, aya ya 19). Kama angekuwepo na nywele ndefu, na kuonekana kama Mnazari, tungelitarajia basi kuwepo na tamko pahala fulani kuhusu tofauti ya muonekano wake na matendo aliyokuwa akiyafanya ambayo hayakuendana na Unazari. Hali kwamba alikuwa akinywa divai yenyewe ingekuwa tatizo kubwa. Wakati Yesu alipoishi, matajiri walizoea kuvalia kanzu na majoyo ya vitambaa vya thamani, kuonyesha hadhi yao katika jamii. Katika moja ya mahubiri yake, Yesu anasema : "Jihadharini na walimu wa sheria (waandishi). Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu (stolai), na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Pia wao hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kupewa nafasi za heshima katika karamu." Mafundisho haya ya Yesu kwa kawaida huchukuliwa kama yenye maelezo ya kuaminika zaidi kwenye Injili, hivyo tunaweza kuwa na msingi kuamini kwamba Yesu hakuvalia mavazi kama hayo marefu. Kwa jumla, mwanamume wakati huo wa Yesu angevalia gwanda au kanzu fupi hivi, na mwanamke angevalia vazi lililomfika kwenye kifundo cha mguu. Kwa hivyo, katika karne ya 2 kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume, Paul na Thecla, inapotokea kwamba Thecla ambaye ni mwanamke anavalia kanzu fupi kama mwanamume, hilo ni jambo linaloshangaza sana. Kanzu hizi kwa kawaida zingekuwa na ukanda au mstari wa rangi tofauti kutoka kwenye bega hadi kwenye pindo sehemu ya chini. Ni vazi ambalo lingeshonwa au kufumwa kama kipande kimoja cha vazi. Juu ya kanzu hiyo, ungejifunga joho au vazi jingine la nje, na tunajua kwamba Yesu alivalia vazi kama hilo kwa sababu ndilo lililoguswa na mwanamke aliyetaka kuponywa naye. (Marko 5:27): Alikuwa amesikia habari za Yesu, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, kwa maana alisema moyoni mwake, 'Kama nikiweza kuligusa vazi lake tu, nitaponywa.') Vazi hilo la nje lilifumwa kwa manyoya, lakini halikuwa zito sana na ndipo ili uhisi joto ingemlazimu mtu kuvalia mavazi mawili kama hayo. Vazi hilo lingevaliwa kwa njia nyingi, na wakati mwingine lingening'inia hadi chini ya magoti na kulifunika lile kanzu fupi la ndani. (Baadhi ya wanafalsafa walizoea kuvalia vazi hilo la nje pekee bila kuvalia ile kanzu ya ndani na kuacha sehemu ya bega au kifua ikiwa wazi). Mamlaka na hadhi ya mtu ni vitu ambavyo vilidhihirishwa kupitia ubora, ukubwa na rangi ya mavazi hayo ya nje. Rangi ya zambarau na baadhi ya aina za rangi ya buluu (samawati) ni rangi zilizoashiria utajiri, hadhi na kujionea fahari. Zilikuwa ni rangi za kifahari kwa sababu viungo vya kutengeneza rangi hizo vilikuwa adimu na ghali sana. Lakini rangi pia huashiria kitu kingine tofauti. Mwanahistoria Josephus, anawaeleza walokole waliofahamika kama Zealots (kundi la Wayahudi wa itikadi kali waliotaka kuwafurusha Warumi kutoka Judea) kama kundi la wahalifu wauaji waliovalia mavazi ya nje yaliyopakwa rangi kwa jina - mavazi anayoyaita chlanidia - kuashiria kwamba yalikuwa ni kama mavazi yaliyovaliwa na wanawake. Hii inaashiria kwamba wanaume kamili, kama hawakuwa na cheo cha juu zaidi katika jamii, walifaa kuvalia mavazi yasiyopakwa rangi. Yesu hakuvalia mavazi meupe hata hivyo. Haya yalikuwa mavazi ya kipekee na yalihitaji kupaushwa mara kwa mara (kufanywa meupe tena) au kupakwa chokaa. Judea, mavazi kama hayo meupe yalihusishwa na kundi lililofahamika kama Essenes - ambao ni watu waliofuata ufasiri mkali wa sheria za Kiyahudi. Tofauti kati ya mavazi ya Yesu na mavazi mengine ya rangi nyeupe ya kung'aa inaelezwa kwenye sura ya 9 ya Marko ambapo anaandamana na mitume watatu mlimani. Yesu aliwachukua "Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao. Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angaliweza kuyangʼarisha. Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu." Marko anaeleza kwamba mavazi ya Yesu yaligeuka rangi yakawa meupe sana, hapa anarejelea vazi la ndani na si la nje. Kabla ya kugeuka sura huku kwa Yesu, anaoneshwa na Marko kama mwanamume wa kawaida, aliyevalia mavazi ya kawaida, ambayo ni ya rangi ambayo haijapaushwa. Katika hali ambayo ndipo yang'ae na kuangaza unahitaji kumpelekea fundi. Tunaelezwa zaidi kuhusu mavazi ya Yesu wakati wa kusulubiwa kwake, pale wanajeshi wa Kirumi wanapoyakata mavazi yake ya nje vipande vinne (Yohana19:23: Askari walipokwisha kumsulubisha Yesu, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini.) Kuna uwezekano mavazi hayo ya nje yalikuwa mavazi mawili. Moja ya vazi hili huenda lilikuwa ni tallith, ambalo ni vazi la kujifunga Kiyahudi wakati wa maombi. Vazi hili lenye shada (tzitzith) limetajwa moja kwa moja na Yesu katika kitabu cha Mathayo 23:5 anapozungumza kuhusu walimu wa sheria na Mafarisayo (Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao). Lilikuwa ni vazi la nje lisilo zito, ambalo kawaida lilitengenezwa kwa kitambaa cha manyoya na lilikuwa la rangi ya malai hivi (krimu), na pengine lilikuwa na ukanda au mstari wa rangi ya nili (bluu iliyoiva). Miguuni, Yesu angevalia ndara (kandambili au malapa). Kila mtu wakati huo alivalia ndara. Katika mapango yaliyo jangwani karibu na Bahari ya Chumvi (Bahari Mfu) na Masada, ndara za wakati alipoishi Yesu zimegunduliwa, na tunaweza kutazama ndara ambazo huenda alivaa zilivyoonekana. Zilikuwa hazijafanyiwa kazi nyingi sana ya kiufundi. Soli (nyayo au kikanyagio) zake zilikuwa vipande vigumu vya ngozi vilivyoshonwa pamoja, na juu kulikuwa ni kanda za ngozi ambazo mbele zingeingizwa katikati ya vidole, kama malapa tu ya siku hizi. Yesu (Nabii Issa) Alikuwa Myahudi, na uso wake pia bila shaka ungefanana na Wayahudi wa wakati huo. Hali kwamba Yesu alikuwa Myahudi (au Mjudea) ni jambo linalorejelewa katika vitabu vingi, zikiwemo barua za Mtume Paulo. Na katika barua yake kwa Waebrania, anaandika: "Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda" (Sura ya 7:14) Kwa hivyo, Myahudi wa wakati huo, mwanamume wa miaka 30 hivi alipoanza kueneza Injili kwa mujibu wa Luka 3, pia akiwa ni mwenye ngozi nyeusi kama ilivyokuwa kwa wayahudi wengi zama zile waliokuwa wakitembeleana na ndugu zao wa Misri (Kushi) kemet. Mwaka 2001 mwanaantholopojia (mtaalamu wa elimu ya binadamu hasa elimu ihusuyo habari zinazohusu asili na maendeleo yake ya awali) Richard Neave alitengeneza mfano wa mwanamume wa Galilaya wa zama za Yesu ambao ulitumiwa kwa jina Son of God (Mwana wa Mungu). Alitumia fuvu lililopatikana katika eneo hilo. Hakusema kwamba huo ulikuwa muonekano wa uso wa Yesu. Mfano ulikuwa tu wa kuchochea hisia na kuwafanya watu kumfikiria Yesu kama mwanamume wa zama hizo na eneo hilo, kwa sababu hakuna mchoro wala maelezo yaliyopo ya kina kuhusu muonekano wake halisi. Ingawa tunaweza kupata viashiria kutoka kwa teknolojia na kutumia mifupa ya watu wa kale, kiashiria cha karibu sana kuhusu pengine Yesu alionekana vipi labda kinaweza kutokana na mchoro wa Musa kwenye ukuta wa sinagogi ya karne ya 3 ya Dura-Europos, kwani mchoro huo unaonesha jinsi Myahudi wa hekima alidhaniwa kuwa wakati wa utawala wa Wagiriki na Warumi. Musa anaoneshwa akiwa na mavazi ambayo hayajapaushwa, na moja ya vazi lake la nje ni tallith. Katika mchoro huo wa Dura wa Musa akitenganisha maji kwenye Bahari ya Sham ili Waisraeli wapite, unaweza kuziona shada (tzitzith) kwenye kona za vazi hilo. Kwa kiwango kikubwa, picha hiyo pengine inatoa msingi bora zaidi wa kumfikiria Yesu alivyokuwa badala ya picha za sasa zinazoongozwa na busara na mawazo ya enzi ya Byzantine - alikuwa na nywele fupi, ndevu fupi, na alikuwa amevalia kanzu fupi lenye mikono mifupi, na alikuwa na joho au vazi la nje. Makala hii chimbuko lake ni makala ya Kiingereza ya Joan Taylor ambaye ni profesa wa kitivo cha Asili ya Ukristo na Hekalu la Pili la Wayahudi katika Chuo Kikuu cha King's College London na ndiye mwandishi wa kitabu kwa jina The Essenes, the Scrolls and the Dead Sea.
    0 Comments ·0 Shares ·808 Views
More Results