• #PART4

    Wanasema kwamba ukiingizwa kwenye chumba cha mateso, unaweza kuanza kuongea kabla hata hawajauliza maswali.

    Ule ukali wa "Sitawataja washikaji wangu" unayeyuka ndani ya saa moja.

    Gereza hili linawafanya hata magaidi waliokuwa na imani kali kuwa wepesi kama karatasi.

    Ndiyo maana wanasema,

    "Magaidi wengi wanaoingizwa humo, hawachukui muda kutaja mnyororo mzima wa washikaji zao."

    Kwa kifupi, Guantanamo ni gereza ambalo lina mlango wa kuingilia, lakini hauna mlango wa kutokea.

    Ni jela ambayo ukishaingia, unaishi kwa maombi hata kama wewe si mtu wa dini.
    #PART4 Wanasema kwamba ukiingizwa kwenye chumba cha mateso, unaweza kuanza kuongea kabla hata hawajauliza maswali. Ule ukali wa "Sitawataja washikaji wangu" unayeyuka ndani ya saa moja. Gereza hili linawafanya hata magaidi waliokuwa na imani kali kuwa wepesi kama karatasi. Ndiyo maana wanasema, "Magaidi wengi wanaoingizwa humo, hawachukui muda kutaja mnyororo mzima wa washikaji zao." Kwa kifupi, Guantanamo ni gereza ambalo lina mlango wa kuingilia, lakini hauna mlango wa kutokea. Ni jela ambayo ukishaingia, unaishi kwa maombi hata kama wewe si mtu wa dini.
    0 Comments ·0 Shares ·196 Views
  • #PART1

    Kuna gereza, na kuna Guantanamo Bay.

    Hili si gereza la kawaida. Ni shimo la mateso, mahali ambapo sheria za haki za binadamu zinaonekana kama hadithi za kufikirika.

    Lipo Cuba, lakini linamilikiwa na Marekani.

    Wanasema gereza ni sehemu ya kutumikia adhabu, lakini Guantanamo ni sehemu ambapo unatakiwa kusahau kama ulikuwa binadamu.

    Kama umewekwa hapa, ni ishara kwamba dunia imeshakusahau.
    Na hata kama hauna hatia, hutaweza kuthibitisha chochote.

    Marekani ni taifa la haki, Ndio! angalau kwenye makaratasi.
    Lakini hata Wamarekani wenyewe walikuwa hawapendi Guantanamo.

    Kila mwaka, wanaharakati wa haki za binadamu walikuwa wakiandamana, wakitaka gereza hilo lifungwe.

    Ilipofika mwaka 2008, Barack Obama alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha urais, akaahidi jambo moja kubwa.

    "Nikichaguliwa kuwa Rais, gereza la Guantanamo litafungwa mara moja!"

    Ilionekana kama ahadi ya kweli.

    Wamarekani wakashangilia, wakaamini kwamba hatimaye heshima ya taifa lao itarudi.
    #PART1 Kuna gereza, na kuna Guantanamo Bay. Hili si gereza la kawaida. Ni shimo la mateso, mahali ambapo sheria za haki za binadamu zinaonekana kama hadithi za kufikirika. Lipo Cuba, lakini linamilikiwa na Marekani. Wanasema gereza ni sehemu ya kutumikia adhabu, lakini Guantanamo ni sehemu ambapo unatakiwa kusahau kama ulikuwa binadamu. Kama umewekwa hapa, ni ishara kwamba dunia imeshakusahau. Na hata kama hauna hatia, hutaweza kuthibitisha chochote. Marekani ni taifa la haki, Ndio! angalau kwenye makaratasi. Lakini hata Wamarekani wenyewe walikuwa hawapendi Guantanamo. Kila mwaka, wanaharakati wa haki za binadamu walikuwa wakiandamana, wakitaka gereza hilo lifungwe. Ilipofika mwaka 2008, Barack Obama alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha urais, akaahidi jambo moja kubwa. "Nikichaguliwa kuwa Rais, gereza la Guantanamo litafungwa mara moja!" Ilionekana kama ahadi ya kweli. Wamarekani wakashangilia, wakaamini kwamba hatimaye heshima ya taifa lao itarudi.
    0 Comments ·0 Shares ·332 Views
  • Muda ukasonga. Dunia ikabadilika. Mataifa yakaanza kuweka mbele maslahi yao, na Ukraine akajikuta akilia peke yake kwenye uwanja wa vita.

    Aliyeahidi kumlinda Urusi ndiye huyo anayemshambulia kwa mabomu, vifaru na ndege za kivita.

    Kwa miaka mingi, Vladimir Putin alikuwa anaangalia ramani ya dunia akijiuliza, "Mbona Crimea na Donbas zipo nje ya milki yangu?"

    Halafu, ghafla mwaka 2014, Urusi ikaamua kumng'ata Ukraine kwa mara ya kwanza.

    Crimea ikachukuliwa, na dunia ikakaa kimya. Hakukuwa na hatua kubwa zilizochukuliwa na Marekani wala Uingereza. Ukraine akaanza kuona dalili za usaliti.

    Mwaka 2022, Urusi ikarudi tena, safari hii kwa nguvu kubwa zaidi.
    Tishio la silaha za nyuklia lililomfanya Ukraine kuwa mbabe, halikuwepo tena. Hakuwa na kinga tena, alikuwa mtu mwepesi wa kushambuliwa.

    Na hapa ndipo Ukraine alipogundua kosa lake kubwa aliamini makaratasi kuliko mabavu.
    Muda ukasonga. Dunia ikabadilika. Mataifa yakaanza kuweka mbele maslahi yao, na Ukraine akajikuta akilia peke yake kwenye uwanja wa vita. Aliyeahidi kumlinda Urusi ndiye huyo anayemshambulia kwa mabomu, vifaru na ndege za kivita. Kwa miaka mingi, Vladimir Putin alikuwa anaangalia ramani ya dunia akijiuliza, "Mbona Crimea na Donbas zipo nje ya milki yangu?" Halafu, ghafla mwaka 2014, Urusi ikaamua kumng'ata Ukraine kwa mara ya kwanza. Crimea ikachukuliwa, na dunia ikakaa kimya. Hakukuwa na hatua kubwa zilizochukuliwa na Marekani wala Uingereza. Ukraine akaanza kuona dalili za usaliti. Mwaka 2022, Urusi ikarudi tena, safari hii kwa nguvu kubwa zaidi. Tishio la silaha za nyuklia lililomfanya Ukraine kuwa mbabe, halikuwepo tena. Hakuwa na kinga tena, alikuwa mtu mwepesi wa kushambuliwa. Na hapa ndipo Ukraine alipogundua kosa lake kubwa aliamini makaratasi kuliko mabavu.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·381 Views
  • muda mwingi yeye yeye utamkuta anaiongoza camera drone (ndege isiyo na rubani) au anakuwa na peni na karatasi yako muda mwingi anaandika baadhi ya vitu

    huyu ndo mfungua code wa kocha fadlu davies , huyu ndo anampa mifumo na uwezo wa timu inayotarajiwa kucheza na SIMBA , huyu ndo humpa udhaifu na ubora wa timu pinzani inayotarajiwa kucheza na SIMBA huyu ndo anajifungia ndani na kocha fadlu kumpa mrejesho wa perfomance ya mchezaji mmoja mmoja wa SIMBA baada ya kumalizika mazoezi

    Ni bwanamdogo sana ila uwezo wake unatisha sana ukizungumzia mafanikio ya RAJA CASABLANCA msimu uliopita basi moja kati ya waliochangia ni huyu jamaa na raja ikamaliza msimu uliopita ligi ya moroco wakiwa mabingwa na walimaliza msimu bila kufungwa (unbeaten)

    anaitwa MUEEZKAJEE ni mchambuzi wa video wa SIMBA SPORTS CLUB ( video &perfomance analysis) ni kijana mzaliwa wa africa kusini ila uwezo mkubwa sana , hata ile siku anaenda kuuambia uongozi wa RAJA kuwa anaondoka na anamfata kocha fadlu viongozi wa RAJA waliumia sana

    wote kwa pamoja walikuwa raja na msimu uliopita na wakaipa ubingwa namsimu huu wapo SIMBA wanaendelea kuwapa furaha wanasimba.


    #paulswai
    muda mwingi yeye yeye utamkuta anaiongoza camera drone (ndege isiyo na rubani) au anakuwa na peni na karatasi yako muda mwingi anaandika baadhi ya vitu huyu ndo mfungua code wa kocha fadlu davies , huyu ndo anampa mifumo na uwezo wa timu inayotarajiwa kucheza na SIMBA , huyu ndo humpa udhaifu na ubora wa timu pinzani inayotarajiwa kucheza na SIMBA huyu ndo anajifungia ndani na kocha fadlu kumpa mrejesho wa perfomance ya mchezaji mmoja mmoja wa SIMBA baada ya kumalizika mazoezi Ni bwanamdogo sana ila uwezo wake unatisha sana ukizungumzia mafanikio ya RAJA CASABLANCA msimu uliopita basi moja kati ya waliochangia ni huyu jamaa na raja ikamaliza msimu uliopita ligi ya moroco wakiwa mabingwa na walimaliza msimu bila kufungwa (unbeaten) anaitwa MUEEZKAJEE ni mchambuzi wa video wa SIMBA SPORTS CLUB ( video &perfomance analysis) ni kijana mzaliwa wa africa kusini ila uwezo mkubwa sana , hata ile siku anaenda kuuambia uongozi wa RAJA kuwa anaondoka na anamfata kocha fadlu viongozi wa RAJA waliumia sana wote kwa pamoja walikuwa raja na msimu uliopita na wakaipa ubingwa namsimu huu wapo SIMBA wanaendelea kuwapa furaha wanasimba. 👍👍👍👍🦁🦁🦁🦁 #paulswai
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·602 Views
  • OPERATION ENTEBBE -2

    Tayari zilikuwa zimepita siku tatu tangu ndege ya Air France Flight 139 kuondoka Tel Aviv na hatimaye kutekwa baada ya kuruka jijini Athens iliposimama kuchukua abiria. Lakini pia zilikuwa zimepita siku mbili tangu ndege hii kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda. Katika siku zote mbili hizi tangu ndege hii itue uwanjani hapa, rais wa Uganda Idd Amin Nduli Dadaa alikuwa anafika uwanjani hapo kila siku “kuwajulia hali” mateka hao.
    Kwa muda wa siku hizi zote mbili tangu ndege itue uwanjani hapo, magaidi hawa walioiteka ndege kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kuchunguza majina ya kila abiria kama ambavyo yalikuwa yameandikwa kwenye pasport. Lengo lao la kufanya hivi ilikuwa ni kujaribu kufahamu uraia wa kila mateka waliye naye. Baada ya kufanya uchambuzi huu wa passport zote, hatimaye siku hii ya tatu, yaani tarehe 29 June 1976 kiongozi wa magaidi hawa Wilfred Bose akiwa na karatasi mkononi aliingi ndani ya terminal ambayo walikuwa wanaitumia kuwahifadhi mateka na kisha akaanza kusoma majina ya kila abiria. Alichokuwa anakifanya ni kusoma majina ya mateka ambao passport zao zilionyesha walikuwa ni raia wa Israel. Lakini pia alisoma majina ya mateka wengine ambao licha ya passport zao kuonyesha kuwa hawakuwa raia wa Israel lakini walikuwa na majina ya kiyahudi. Pamoja na hao pia mateka wote ambao walikuwa na uraia pacha na uraia huo mmojawapo ukiwa ni Israel basi nao waliunganishwa kwenye list hii.
    Baada ya kuwatenganisha raia wote wa Israel na kuwaweka kwenye chumba kingine peke yao hapo hapo kwenye terminal, kuna mwanadada raia wa Ufaransa aliyeitwa Jocelyne Monier yeye jina lake halikuitwa kwenye ile list ya wanaotakiwa kutengwa kwenye chumba kingine (Waisrael na Wayahudi). Lakini ‘boyfriend’ wake alikuwa ni Muisrael na aliitwa jina na kutengwa na wengine katika kile chumba kingine. Mwanadada huyu ili kuonyesha kumtia moyo mpenzi wake na kupinga huu ubaguzi uliokuwa unafanywa na hawa magaidi, kwa hiari yake alijipeleka kwenye chumba cha mateka wa Kiisrael. Si mwanadada huyu pekee ambaye alifanya kitendo hiki cha ushujaa, lakini pia kulikuwa na mwanamama mwingine aliitwa Janet Almog (rai wa Marekani) na mateka mwingine aliyeitwa Jean-Jacques Mimouni (raia wa Ufaransa) nao kwenye kuonyesha hali ya kuwaunga mkono wenzao waliotengwa kwenye chumba kingine na kupinga ubaguzi uliokuwa unafanywa na maharamia hawa, nao walijipeleka kwa hiari yao kwenye chumba ambacho mateka hao walikibatiza jina “Chumba cha Waisrael”, ambacho mateka wote walijua fika kwamba kuna jambo baya maharamia hao walikuwa wamepanga kulifanya.

    Licha ya maharamia kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kufanya uchambuzi huu wa kina kuhusu uraia wa kila mateka waliye naye, lakini walifanya kosa kubwa sana ambalo lilkuja kuwagharimu sana hapo baadae. Kwenye uchambuzi wao wote huu walioufanya walishindwa kumng’amua mateka mmoja mwanajeshi wa Israel ambaye alikuwa ana uraia pacha na siku hiyo alikuwa anatumia passport ambayo sio ya Israel. Mateka huyu alikuja kuwa muhimu sana huko mbeleni kuwapatia Mossad Intelijensia mujarabu kabisa kuhusu watekaji, jengo wanaloshikilia mateka, na namana wanavyoshirikiana na jeshi la Uganda.
    Siku iliyofuata yaani June 30, maharamia haya wakawaachia mkupuo wa kwanza wa mateka wasio raia wa Israel au wayahudi. Katika mkupuo huu wa kwanza waliachia mateka 48 ambao walikuwa ni wazee, watoto na akina mama wenye watoto wadogo.
    Baada ya mkupuo huu wa kwanza wa kuwaachia mateka hawa wachache, maharamia wakaweka wazi matakwa yao ili waweze kuachia mateka wengine. Kwanza kabisa walitaka walipwe fedha kiasi cha dola za Kimarekani milioni 5. Na pili walitakakuachiwa kwa wafungwa 53 wenye asili ya kipalestina wanaotuhumiwa kwa ugaidi, ambao kati yao 40 walikuwa kwenye jela za Israel na 13 katika nchi nyingine za Ulaya. Watekaji hawa wakatoa ‘ultimutum’ kwamba kama matakwa yao hayatatekelezwa ndani ya masaa ishirini na nne yajayo (mpaka tarehe 1 July saa 8 mchana) basi wataanza kuua raia wa Israel mmoja baada ya mwingine.
    Dunia nzima ni kama ilisimama kwa masaa kadhaa kutokana na sintofahamu iliyogubika kila mahali. Sintofahamu hii ililetwa na ukweli kwamba, ilikuwa inajulikana wazi kwa miaka yote kwamba Israel wana sera ya kutofanya mazungumzo au makubaliano na Magaidi. Kwahiyo kila mtu alikuwa nafahamu kuwa kuna uwezekano mkubwa ndani ya masaa 24 yajayo ulimwengu ukashuhidia watu zaidi ya 200 wakichinjwa kama kuku.

    NCHINI ISRAEL: KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI
    Nchini Israel kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kilikuwa kimeitishwa na waziri Mkuu Yitzhak Rabin kujadili kuhusu hatua za kuchukua kuokoa raia wake ambao wameshikiliwa mateka huko uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda.
    Hali ya kikao ilikuwa tete sana kutokana na kila dakika waliyokuwa wanaitumia kujadili ndivyo ambavyo walikuwa wanaikaribia saa 8 mchana ya tarehe 1 July. Walipowasilana na Ujerumani na Ufaransa ambao nao walikuwa na baadhi ya wafungwa wa Kipalestina ambao watekaji walitaka waachiwe… walipowaomba ushirikiano wao kuhusu kukabali kuachia hao wafungwa, Ujerumani na Ufaransa walikataa katakata kuachia hata mfungwa mmoja wa Kipalestina ambaye alikuwa kwenye magereza zao.
    Sintofahamu ilizidi kuongezeka. Masaa yalizidi kuyoyoma. Saa 8 mchana ya tarehe 1 July ilizidi kukaribia. Harufu ya damu ilikuwa inabisha hodi mlangoni kwao. Licha ya weledi wao wote walionao lakini mbele yao waliona giza.
    Inapaswa kukumbukwa kwamba Idd Amin aliwahi kupatiwa mafunzo ya weledi wa kijeshi nchini Isarel (Special Force Training). Kwa hiyo baraza la mawaziri likamuagiza Baruch Bar-Lev, kamanda mstaafu wa IDF ambaye alihusika kumpatia mafunzo ya kijeshi Amin kipindi yuko Israel na kufanikiwa kujenga naye ukaribu. Baraza la Mawaziri likamuagiza Baruck (marafiki zake humuita “Burka”) kufanya mawasiliano na Rais huyo wa Uganda ili kujaribu kumuomba awashawishi magaidi wanaoshikilia mateka kwenye uwanja wake wa ndege wa Entebbe wawaachie mateka hao bila masharti magumu.
    Kupitia kwa Burka, Israel ilifikia mpaka hatua ya kumuahidi Idd Amin kuwa kama atafanikisha kuachiwa kwa mateka hao basi watatumia ushawishi walionao kuhakikisha kuwa Amin anatunukiwa tuzo ya amani ya Nobel.
    Lakini Amin hakulegeza msimamo, akaendelea kuwasisitiza kuwa hakuna namna nyingine yeyote ambayo mateka hao wataachiwa bila masharti yaliyotolewa na watekaji kutimizwa.
    Baada ya juhudi hii ya kumuhonga ‘tuzo’ kugonga mwamba, Waziri Mkuu wa Israel akawasiliana na serikali ya Marekani na kuwaomba wamshawishi Rais wa Misri Anwar Sadat ambaye alikuwa anaheshimiana sana na Amin ili amshawishi kuwaamuru magaidi yaliyoko uwanjani kwake Entebbe waachiemateka bila masharti magumu.
    Amin bado akashikilia msimamo kwamba hakuna mateka atakayeachiwa pasipo masharti yaliyotolewa kutimizwa.
    Juhudi hizi za kumshawishi Amin zilikula muda mwingi sana na hatimaye wakajikuta tayari kulikuwa kumekucha asubuhi. Mbele yao kulikuwa kumebakia masaa chini ya manane kabla ya damu ya zaidi ya watu 200 kumwagika.
    Baraza la mawaziri la Israel likamuomba Amin aongee na watekaji wakubali kusogeza siku mbele ili kuipa serikali ya Israel muda wakutosha kushughulikia lojistiki na kushawishi Ujerumani na Ufaransa ili waweze kutimiza sharti la kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wanaotuhumiwa kwa ugaidi.
    Rais Idd Amin baada ya kushawishiwa sana akakubali ombi hili na akaieleza serikali ya Israel kwamba ni siku tatu tu pekee zinaongezwa, yaani ikimaanisha kwamba siku zitaongezwa mpaka tarehe 4 July, saa 8 mchana. Serikali ya Israel ikakubliana na hili.
    Mchana wa siku hiyo, serikali ilitoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari wakilaani vitendo vya kigaidi na hususani matukio ya utekeji wa raia wasio na hatia, na pia ikaendelea kusisitiza kuhusu sera yake ya kutojadili na magaidi. Lakini taarifa hii ikamalizia kwa kueleza kuwa kwa kujali zaidi uhai wa zaidi ya raia 200 ambao bado wanashikiliwa na magaidi hayo, na kujali maumivu ambayo familia zao na taifa zima linapitia, wamekubali kutimiza sharti la magaidi hao la kuwalipa fedha za kimarekani dola milioni tano pamoja na kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wenye tuhuma za ugaidi.
    Ilikuwa ni moja ya matukio machache ambayo yaliishangaza dunia kwa Israel kukubali kushindwa hadharani. Kwa upande wa maadui wa Israel hii ilikuwa ni sherehe kubwa kwao. Na kwa upande wa Isarel na maswahiba zake hii iikuwa ni maombolezo makubwa.
    Amin na wenzake kule Uganda walikuwa wanasherehekea baada ya taarifa hii kutolewa kwa vyombo vya habari. Walihsi kabisa harufu ya ushindi inanukia kwenye pua zao.
    Kitu ambacho walikuwa hawafahamu ilikuwa ni kwamba, Israel walikuwa wanawafanyia ‘mchezo’ wa kisaikolojia ili Amin, jeshi lake na watekaji wajiamini kwa kuona kuwa ushindi umeegemea upande wao na hatimaye wajisahau kutokana na kujiamini huku.

    NYUMA YA PAZIA
    Huko Tel aviv, makamanda wa IDF na maafisa wa Mossad walikuwa wamekusanyika katika conference room ya mako makuu ya wizara ya ulinzi kuweka mkakati wa oparesheni ya uokozi (rescue mission) wa mateka wanaoshikiliwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda.
    Kati ya watu muhimu ambao walikuwepo kwenye kikao hiki alikuwa ni Waziri Mkuu Rabin na Ehud Barak ambaye kipindi hicho alikuwa kamanda wa ngazi za juu kwenye jeshi anayeongoza kitengo cha Intelijensia ya jeshi (Military Intelligence).
    Moja kati ya vitu muhimu ambavyo viliwasaidia ilikuwa ni taarifa ya intelijensia iliyoletwa na Mossad kwamba uwanja wa ndege wa Entebbe ulijengwa na kampuni ya Kiisrael inayoitwa Solel Boneh.
    Kwahiyo muwakilishi kutoka katika kampuni hii ya ujenzi naye akaitwa kikaoni kwa ajili ya kuwasilisha michoro kuhusu jengo lote na uwanja wa ndege wa Entebbe ulivyo.
    Lakini pia wakati huo huo kulikuwa na maafisa wa Mossad ambao walikuwa ufaransa kuwahoji wale mateka ambao walikuwa wameachiwa awali. Mtu muhimu zaidi ambaye alitoa taarifa nzuri kwa Mossad alikuwa ni yule afisa wa jeshi niliyemuelezea awali kwamba alikuwa na uraia wan chi mbili (Israel na Ufaransa) na siku hii alikuwa ametumia passport ya nchi ya ufaransa hivyo watekaji walimuachia pamoja na wenzake wa kundi la kwanza lile la watu 48.
    Bwana huyu alitoa taarifa muhimu zaidi kuhusu kilichokuwa kinaendelea katika uwanja wa ndege wa Entebbe, kwa kuwa yeye tofauti na wenzake kutokana na uzoefu wake wa jeshi alikuwa aliweza kuwaeleza Mossad kuhusu ni salaha za namna gani watekaji walikuwa nazo, kulikuwa na ndege za aina gani za kijeshi pale uwanjani (Idd Amin aliamuru Air Force ya Uganda kulinda uwanja huo masaa 24), pia aliweza kuwaeleza kuhusu ‘rotation’ ya ulinzi ya jeshi la Uganda pamoja na taarifa nyingine muhimu ambazo abiria wengine wasingeweza kuzitilia maanani au kkuzieleza kwa ufasaha.
    Baada ya kupata intelijensia ya kutosha, mkakati wa awali ambao ulipendekezwa na jeshi ulikuwa ni kutumia ndege ya kijeshi na kisha kudondosha makomando kwenye ziwa Viktoria na kutoka hapo watatumia boti za mpira kuvuka mpaka nchi kavu na hatimaye kuelekea uwanja wa ndege ambao haukuwa mbali sana na ziwa Viktoria.
    Mkakati huu ulikuwa ni mzuri lakini ulihairishwa baada ya kupewa taarifa kuwa ziwa Viktoria lilikuwa na mamba wengi na ingeweza kuhatarisha uhai wa hawa makomando kabla hata ya kufika kwenye uwanja wa ndege. Kwahiyo ilikuwa dhahiri kwamba mkakati wowote ambao utawekwa ni lazima uwe wa kuvamia kutokea nchi kavu na ikiwezekana kutoka nchi jirani.
    Changamoto kubwa zaidi ilikuwa ni usafiri. Yaani kwamba oparesheni hii ilikuwa si tu kwamba makomando wanaotumwa kutekeleza wanaenda kupambana na magaidi wanne tu walioteka ndege, bali ilikuwa ni kana kwamba wanaenda kupambana na jeshi zima la Uganda. Kwa hiyo kikosi cha makomando ambacho kitatumwa kwenda huko lazima kiwe na watu wengi wa kutosha na pia lazima wachukue silaha nzito za kutosha. Ili kufaniskisha safari yenye makomando wengi hivi na vifaa vizito ilikuwa ni lazima kutumia ndege kubwa za kijeshi zenye uwezo mkubwa pia na hakukuwa na chaguo zuri zaid ya kutumia ndege za kijeshi za LOCKHEED C-130 HERCULES. Sasa changamoto ilikuwa inakuja kwamba huwezi kurusha dege kubwa kama hii kwenda na kurudi kutoka Israel mpaka Uganda bila kujaza mafuta tena japo mara moja.
    Katika kipindi hiki bado Israel walikuwa hawajawa na uwezo wa kufanya ‘Aerial Refuel’, yaani ndege kujazwa mafuta kwa kutumia ndege nyingine ikiwa angani. Lakini pia ilikuwa ni lazima madege hayo yakikaribia Uganda yaruke chini chini ili kukwepa kudunguliwa na kuikwepa rada ya kijeshi. Kwa hiyo ilikuwa ni lazima kupata nchi ndani ya afrika Mashariki ambao watakubali madege hayo ya kijeshi ya Israel kutua kwenye uwanja wake wa ndege na kujaza mafuta lakini pia kujiandaa na kuanzisha operation kutokea hapo na pia anga lao kutumika kuanzisha shambulizi la kijeshi kuelekea Uganda.
    Sasa japokuwa nchi zote za Afrika Mashariki zilikuwa hazikubaliana na kitendo cha Rais wa Uganda kushirikiana na watekaji, lakini hakukuwa na hata nchi moja ambayo ilikuwa iko tayari kuingia kwenye mzozo na Idd Amin kwa kuruhusu viwanja vya vya ndege kutumika na ndege za jeshi la Israel au wanajeshi kujiandaa kuvamia Entebbe au pia kuruhusu anga lao kutumia na jeshi la Israel.
    Ndipo hapa ambapo kwa haraka sana siku hiyo hiyo Waziri Mkuu Rabin akamtuma Ehud Barak na maafisa wachache wa Mossad kwenda Kenya kushawishi serikali ya Mzee Jomo Kenyatta iruhusu ndege za jeshi la Isarel kutumia kiwanja chao cha ndege. Ehud barak na wenzake hawakwenda tu moja kwa moja kwa Mzee Kenyatta, bali kwanza walienda kwa Waziri wa kilimo wa kipindi hicho Bw. Bruce McKenzie ambaye huyu aliwahi kuwa afisa wa Idara ya ujasusi ya Uingereza, MI6 na pia alikuwa swahiba mkubwa wa Ehud Barak.

    Kwa hiyo Israel ikamtumia Bruce McKenzie kumshawishi Mzee Jomo Kenyatta kuruhusu anga la Kenya na viwanjavya ndege kutumiwa na makomando wa Israel na ndege zao.
    Ehud Barak na maafisa wa Mossad hawakuishia hapa tu, bali pia walifanya vikao vya siri na wafanyabiashara wakubwa nchini Kenya wenye asili ya Israel na wale ambao walikuwa na ‘marafiki’ wa Israel kuwaomba watumie ushawishi wao wa kisiasa na kiuchumi wasaidie kumshawishi Kenyatta kukubali ombi la seriakli ya Israael viwanja vyao kutumika na ndege za kijeshi za Israel na makondo wake.
    Baada ya mashinikizo haya kutoka kila upande, Mzee Kenyatta hakuwa na chaguo linguine zaidi ya kukubali ombi lao.
    Bwana huyu McKenzie pia alikuwa na ndege yakebinafsi, na Ehud Barak akaona fursa. Walitumia ndege hii ya kiraia kuruka mpaka Uganda mijini Entebbe na kukatiza juu ya anga la uwanja wa ndege wa Entebbe na walipokuwa wanapita juu ya anga la uwanja wa ndege, Ehud Barak akatumia fursa hii kupiga picha kila eneo la uwanja. Kwa kuwa hii ilikuwa ni ndege ya kiraia, jeshi la Uganda hawakushughulika nayo.
    Picha hizi zilizopigwa na Ehud Barak zilikuja kuwa na umuhimumkubwa katika maandalizi ya mwisho ya oparesheni ya makomando wa Isarel Kuvamia uwanja huu.
    Mpaka kufikia hapa maandalizi yote muhimu yalikuwa yamekamilika.
    WAKATI HUO HUO
    Upande wa watekaji kule Uganda walikuwa wanasubria mifwedha yao dola milioni 5 za kimarekani.
    Rais Idd Amin naye baada ya kufikia makubaliano na Israel kuwa masharti ya fedha na wafungwa wa kipalestina kuachiwa tarehe 4 July, naye ‘akarelax’ na akaona huo ndio muda wa kutekeleza majukumu Mengine akisubiria tarehe 4 July ifike.
    Katika kipindi hiki Idd amin ndiye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa kuzingatia utaratibu wa uenyekiti kuzunguka kwa kila nchi kwa mwaka mmoja mmoja na wiki hii alikuwa anatakiwa kwenye kikao cha Umoja wa Afrika kilichokuwa kinafanyika Mauritius. Kwa hiyo Amin akafunga safari kuelekea Mauritius kwenda kukabidhi kijiti cha Uenyekiti.
    Ehud Barak aliposikia taarifa hii, kwa kutumia akili yake kubwa ya kuzaliwa aliyojaliwa na uzoefu wake wa ujasusi, aliona fursa adhimu kabisa hapa. Akawasiliana na walioko kikaoni huko Tel Aviv na kuwaeleza taarifa ambazo awali wote hawakuielewa.
    Ehud Barak: “Idd Amin akiwa ndani ya Uganda huwa anatumia Mercedes Limousine katika msafara wake”
    Waziri Mkuu Rabin: “Ok! Limefanyaje?’
    Ehud Barak: “Nataka mtafute gari kama hiyo… Mercedes Limousine”
    Waziri Mkuu Rabin: “la kazi gani?”
    Ehud Barak: “siku ambayo kikosi cha makomando wakipanda kwenye ndege kutoka huko Israel kwenda Uganda, gari hilo nataka pia lipakiwe ndani ya ndge!”
    Kwa dakika kadhaa wote ambao walikuwa wanamsikiliza pale kikaoni kupitia simu hakuna ambaye alielewa nini hasa Ehud Barak alikuwa anapendekeza.
    Yalikuwa yamebaki masaa machache tu ambapo, weledi, ushujaa na uzalendo uliotukuka ulikuwa unaedna kudhihirika.

    Itaendelea
    #TheBOLD_JF
    OPERATION ENTEBBE -2 Tayari zilikuwa zimepita siku tatu tangu ndege ya Air France Flight 139 kuondoka Tel Aviv na hatimaye kutekwa baada ya kuruka jijini Athens iliposimama kuchukua abiria. Lakini pia zilikuwa zimepita siku mbili tangu ndege hii kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda. Katika siku zote mbili hizi tangu ndege hii itue uwanjani hapa, rais wa Uganda Idd Amin Nduli Dadaa alikuwa anafika uwanjani hapo kila siku “kuwajulia hali” mateka hao. Kwa muda wa siku hizi zote mbili tangu ndege itue uwanjani hapo, magaidi hawa walioiteka ndege kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kuchunguza majina ya kila abiria kama ambavyo yalikuwa yameandikwa kwenye pasport. Lengo lao la kufanya hivi ilikuwa ni kujaribu kufahamu uraia wa kila mateka waliye naye. Baada ya kufanya uchambuzi huu wa passport zote, hatimaye siku hii ya tatu, yaani tarehe 29 June 1976 kiongozi wa magaidi hawa Wilfred Bose akiwa na karatasi mkononi aliingi ndani ya terminal ambayo walikuwa wanaitumia kuwahifadhi mateka na kisha akaanza kusoma majina ya kila abiria. Alichokuwa anakifanya ni kusoma majina ya mateka ambao passport zao zilionyesha walikuwa ni raia wa Israel. Lakini pia alisoma majina ya mateka wengine ambao licha ya passport zao kuonyesha kuwa hawakuwa raia wa Israel lakini walikuwa na majina ya kiyahudi. Pamoja na hao pia mateka wote ambao walikuwa na uraia pacha na uraia huo mmojawapo ukiwa ni Israel basi nao waliunganishwa kwenye list hii. Baada ya kuwatenganisha raia wote wa Israel na kuwaweka kwenye chumba kingine peke yao hapo hapo kwenye terminal, kuna mwanadada raia wa Ufaransa aliyeitwa Jocelyne Monier yeye jina lake halikuitwa kwenye ile list ya wanaotakiwa kutengwa kwenye chumba kingine (Waisrael na Wayahudi). Lakini ‘boyfriend’ wake alikuwa ni Muisrael na aliitwa jina na kutengwa na wengine katika kile chumba kingine. Mwanadada huyu ili kuonyesha kumtia moyo mpenzi wake na kupinga huu ubaguzi uliokuwa unafanywa na hawa magaidi, kwa hiari yake alijipeleka kwenye chumba cha mateka wa Kiisrael. Si mwanadada huyu pekee ambaye alifanya kitendo hiki cha ushujaa, lakini pia kulikuwa na mwanamama mwingine aliitwa Janet Almog (rai wa Marekani) na mateka mwingine aliyeitwa Jean-Jacques Mimouni (raia wa Ufaransa) nao kwenye kuonyesha hali ya kuwaunga mkono wenzao waliotengwa kwenye chumba kingine na kupinga ubaguzi uliokuwa unafanywa na maharamia hawa, nao walijipeleka kwa hiari yao kwenye chumba ambacho mateka hao walikibatiza jina “Chumba cha Waisrael”, ambacho mateka wote walijua fika kwamba kuna jambo baya maharamia hao walikuwa wamepanga kulifanya. Licha ya maharamia kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kufanya uchambuzi huu wa kina kuhusu uraia wa kila mateka waliye naye, lakini walifanya kosa kubwa sana ambalo lilkuja kuwagharimu sana hapo baadae. Kwenye uchambuzi wao wote huu walioufanya walishindwa kumng’amua mateka mmoja mwanajeshi wa Israel ambaye alikuwa ana uraia pacha na siku hiyo alikuwa anatumia passport ambayo sio ya Israel. Mateka huyu alikuja kuwa muhimu sana huko mbeleni kuwapatia Mossad Intelijensia mujarabu kabisa kuhusu watekaji, jengo wanaloshikilia mateka, na namana wanavyoshirikiana na jeshi la Uganda. Siku iliyofuata yaani June 30, maharamia haya wakawaachia mkupuo wa kwanza wa mateka wasio raia wa Israel au wayahudi. Katika mkupuo huu wa kwanza waliachia mateka 48 ambao walikuwa ni wazee, watoto na akina mama wenye watoto wadogo. Baada ya mkupuo huu wa kwanza wa kuwaachia mateka hawa wachache, maharamia wakaweka wazi matakwa yao ili waweze kuachia mateka wengine. Kwanza kabisa walitaka walipwe fedha kiasi cha dola za Kimarekani milioni 5. Na pili walitakakuachiwa kwa wafungwa 53 wenye asili ya kipalestina wanaotuhumiwa kwa ugaidi, ambao kati yao 40 walikuwa kwenye jela za Israel na 13 katika nchi nyingine za Ulaya. Watekaji hawa wakatoa ‘ultimutum’ kwamba kama matakwa yao hayatatekelezwa ndani ya masaa ishirini na nne yajayo (mpaka tarehe 1 July saa 8 mchana) basi wataanza kuua raia wa Israel mmoja baada ya mwingine. Dunia nzima ni kama ilisimama kwa masaa kadhaa kutokana na sintofahamu iliyogubika kila mahali. Sintofahamu hii ililetwa na ukweli kwamba, ilikuwa inajulikana wazi kwa miaka yote kwamba Israel wana sera ya kutofanya mazungumzo au makubaliano na Magaidi. Kwahiyo kila mtu alikuwa nafahamu kuwa kuna uwezekano mkubwa ndani ya masaa 24 yajayo ulimwengu ukashuhidia watu zaidi ya 200 wakichinjwa kama kuku. NCHINI ISRAEL: KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI Nchini Israel kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kilikuwa kimeitishwa na waziri Mkuu Yitzhak Rabin kujadili kuhusu hatua za kuchukua kuokoa raia wake ambao wameshikiliwa mateka huko uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda. Hali ya kikao ilikuwa tete sana kutokana na kila dakika waliyokuwa wanaitumia kujadili ndivyo ambavyo walikuwa wanaikaribia saa 8 mchana ya tarehe 1 July. Walipowasilana na Ujerumani na Ufaransa ambao nao walikuwa na baadhi ya wafungwa wa Kipalestina ambao watekaji walitaka waachiwe… walipowaomba ushirikiano wao kuhusu kukabali kuachia hao wafungwa, Ujerumani na Ufaransa walikataa katakata kuachia hata mfungwa mmoja wa Kipalestina ambaye alikuwa kwenye magereza zao. Sintofahamu ilizidi kuongezeka. Masaa yalizidi kuyoyoma. Saa 8 mchana ya tarehe 1 July ilizidi kukaribia. Harufu ya damu ilikuwa inabisha hodi mlangoni kwao. Licha ya weledi wao wote walionao lakini mbele yao waliona giza. Inapaswa kukumbukwa kwamba Idd Amin aliwahi kupatiwa mafunzo ya weledi wa kijeshi nchini Isarel (Special Force Training). Kwa hiyo baraza la mawaziri likamuagiza Baruch Bar-Lev, kamanda mstaafu wa IDF ambaye alihusika kumpatia mafunzo ya kijeshi Amin kipindi yuko Israel na kufanikiwa kujenga naye ukaribu. Baraza la Mawaziri likamuagiza Baruck (marafiki zake humuita “Burka”) kufanya mawasiliano na Rais huyo wa Uganda ili kujaribu kumuomba awashawishi magaidi wanaoshikilia mateka kwenye uwanja wake wa ndege wa Entebbe wawaachie mateka hao bila masharti magumu. Kupitia kwa Burka, Israel ilifikia mpaka hatua ya kumuahidi Idd Amin kuwa kama atafanikisha kuachiwa kwa mateka hao basi watatumia ushawishi walionao kuhakikisha kuwa Amin anatunukiwa tuzo ya amani ya Nobel. Lakini Amin hakulegeza msimamo, akaendelea kuwasisitiza kuwa hakuna namna nyingine yeyote ambayo mateka hao wataachiwa bila masharti yaliyotolewa na watekaji kutimizwa. Baada ya juhudi hii ya kumuhonga ‘tuzo’ kugonga mwamba, Waziri Mkuu wa Israel akawasiliana na serikali ya Marekani na kuwaomba wamshawishi Rais wa Misri Anwar Sadat ambaye alikuwa anaheshimiana sana na Amin ili amshawishi kuwaamuru magaidi yaliyoko uwanjani kwake Entebbe waachiemateka bila masharti magumu. Amin bado akashikilia msimamo kwamba hakuna mateka atakayeachiwa pasipo masharti yaliyotolewa kutimizwa. Juhudi hizi za kumshawishi Amin zilikula muda mwingi sana na hatimaye wakajikuta tayari kulikuwa kumekucha asubuhi. Mbele yao kulikuwa kumebakia masaa chini ya manane kabla ya damu ya zaidi ya watu 200 kumwagika. Baraza la mawaziri la Israel likamuomba Amin aongee na watekaji wakubali kusogeza siku mbele ili kuipa serikali ya Israel muda wakutosha kushughulikia lojistiki na kushawishi Ujerumani na Ufaransa ili waweze kutimiza sharti la kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wanaotuhumiwa kwa ugaidi. Rais Idd Amin baada ya kushawishiwa sana akakubali ombi hili na akaieleza serikali ya Israel kwamba ni siku tatu tu pekee zinaongezwa, yaani ikimaanisha kwamba siku zitaongezwa mpaka tarehe 4 July, saa 8 mchana. Serikali ya Israel ikakubliana na hili. Mchana wa siku hiyo, serikali ilitoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari wakilaani vitendo vya kigaidi na hususani matukio ya utekeji wa raia wasio na hatia, na pia ikaendelea kusisitiza kuhusu sera yake ya kutojadili na magaidi. Lakini taarifa hii ikamalizia kwa kueleza kuwa kwa kujali zaidi uhai wa zaidi ya raia 200 ambao bado wanashikiliwa na magaidi hayo, na kujali maumivu ambayo familia zao na taifa zima linapitia, wamekubali kutimiza sharti la magaidi hao la kuwalipa fedha za kimarekani dola milioni tano pamoja na kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wenye tuhuma za ugaidi. Ilikuwa ni moja ya matukio machache ambayo yaliishangaza dunia kwa Israel kukubali kushindwa hadharani. Kwa upande wa maadui wa Israel hii ilikuwa ni sherehe kubwa kwao. Na kwa upande wa Isarel na maswahiba zake hii iikuwa ni maombolezo makubwa. Amin na wenzake kule Uganda walikuwa wanasherehekea baada ya taarifa hii kutolewa kwa vyombo vya habari. Walihsi kabisa harufu ya ushindi inanukia kwenye pua zao. Kitu ambacho walikuwa hawafahamu ilikuwa ni kwamba, Israel walikuwa wanawafanyia ‘mchezo’ wa kisaikolojia ili Amin, jeshi lake na watekaji wajiamini kwa kuona kuwa ushindi umeegemea upande wao na hatimaye wajisahau kutokana na kujiamini huku. NYUMA YA PAZIA Huko Tel aviv, makamanda wa IDF na maafisa wa Mossad walikuwa wamekusanyika katika conference room ya mako makuu ya wizara ya ulinzi kuweka mkakati wa oparesheni ya uokozi (rescue mission) wa mateka wanaoshikiliwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda. Kati ya watu muhimu ambao walikuwepo kwenye kikao hiki alikuwa ni Waziri Mkuu Rabin na Ehud Barak ambaye kipindi hicho alikuwa kamanda wa ngazi za juu kwenye jeshi anayeongoza kitengo cha Intelijensia ya jeshi (Military Intelligence). Moja kati ya vitu muhimu ambavyo viliwasaidia ilikuwa ni taarifa ya intelijensia iliyoletwa na Mossad kwamba uwanja wa ndege wa Entebbe ulijengwa na kampuni ya Kiisrael inayoitwa Solel Boneh. Kwahiyo muwakilishi kutoka katika kampuni hii ya ujenzi naye akaitwa kikaoni kwa ajili ya kuwasilisha michoro kuhusu jengo lote na uwanja wa ndege wa Entebbe ulivyo. Lakini pia wakati huo huo kulikuwa na maafisa wa Mossad ambao walikuwa ufaransa kuwahoji wale mateka ambao walikuwa wameachiwa awali. Mtu muhimu zaidi ambaye alitoa taarifa nzuri kwa Mossad alikuwa ni yule afisa wa jeshi niliyemuelezea awali kwamba alikuwa na uraia wan chi mbili (Israel na Ufaransa) na siku hii alikuwa ametumia passport ya nchi ya ufaransa hivyo watekaji walimuachia pamoja na wenzake wa kundi la kwanza lile la watu 48. Bwana huyu alitoa taarifa muhimu zaidi kuhusu kilichokuwa kinaendelea katika uwanja wa ndege wa Entebbe, kwa kuwa yeye tofauti na wenzake kutokana na uzoefu wake wa jeshi alikuwa aliweza kuwaeleza Mossad kuhusu ni salaha za namna gani watekaji walikuwa nazo, kulikuwa na ndege za aina gani za kijeshi pale uwanjani (Idd Amin aliamuru Air Force ya Uganda kulinda uwanja huo masaa 24), pia aliweza kuwaeleza kuhusu ‘rotation’ ya ulinzi ya jeshi la Uganda pamoja na taarifa nyingine muhimu ambazo abiria wengine wasingeweza kuzitilia maanani au kkuzieleza kwa ufasaha. Baada ya kupata intelijensia ya kutosha, mkakati wa awali ambao ulipendekezwa na jeshi ulikuwa ni kutumia ndege ya kijeshi na kisha kudondosha makomando kwenye ziwa Viktoria na kutoka hapo watatumia boti za mpira kuvuka mpaka nchi kavu na hatimaye kuelekea uwanja wa ndege ambao haukuwa mbali sana na ziwa Viktoria. Mkakati huu ulikuwa ni mzuri lakini ulihairishwa baada ya kupewa taarifa kuwa ziwa Viktoria lilikuwa na mamba wengi na ingeweza kuhatarisha uhai wa hawa makomando kabla hata ya kufika kwenye uwanja wa ndege. Kwahiyo ilikuwa dhahiri kwamba mkakati wowote ambao utawekwa ni lazima uwe wa kuvamia kutokea nchi kavu na ikiwezekana kutoka nchi jirani. Changamoto kubwa zaidi ilikuwa ni usafiri. Yaani kwamba oparesheni hii ilikuwa si tu kwamba makomando wanaotumwa kutekeleza wanaenda kupambana na magaidi wanne tu walioteka ndege, bali ilikuwa ni kana kwamba wanaenda kupambana na jeshi zima la Uganda. Kwa hiyo kikosi cha makomando ambacho kitatumwa kwenda huko lazima kiwe na watu wengi wa kutosha na pia lazima wachukue silaha nzito za kutosha. Ili kufaniskisha safari yenye makomando wengi hivi na vifaa vizito ilikuwa ni lazima kutumia ndege kubwa za kijeshi zenye uwezo mkubwa pia na hakukuwa na chaguo zuri zaid ya kutumia ndege za kijeshi za LOCKHEED C-130 HERCULES. Sasa changamoto ilikuwa inakuja kwamba huwezi kurusha dege kubwa kama hii kwenda na kurudi kutoka Israel mpaka Uganda bila kujaza mafuta tena japo mara moja. Katika kipindi hiki bado Israel walikuwa hawajawa na uwezo wa kufanya ‘Aerial Refuel’, yaani ndege kujazwa mafuta kwa kutumia ndege nyingine ikiwa angani. Lakini pia ilikuwa ni lazima madege hayo yakikaribia Uganda yaruke chini chini ili kukwepa kudunguliwa na kuikwepa rada ya kijeshi. Kwa hiyo ilikuwa ni lazima kupata nchi ndani ya afrika Mashariki ambao watakubali madege hayo ya kijeshi ya Israel kutua kwenye uwanja wake wa ndege na kujaza mafuta lakini pia kujiandaa na kuanzisha operation kutokea hapo na pia anga lao kutumika kuanzisha shambulizi la kijeshi kuelekea Uganda. Sasa japokuwa nchi zote za Afrika Mashariki zilikuwa hazikubaliana na kitendo cha Rais wa Uganda kushirikiana na watekaji, lakini hakukuwa na hata nchi moja ambayo ilikuwa iko tayari kuingia kwenye mzozo na Idd Amin kwa kuruhusu viwanja vya vya ndege kutumika na ndege za jeshi la Israel au wanajeshi kujiandaa kuvamia Entebbe au pia kuruhusu anga lao kutumia na jeshi la Israel. Ndipo hapa ambapo kwa haraka sana siku hiyo hiyo Waziri Mkuu Rabin akamtuma Ehud Barak na maafisa wachache wa Mossad kwenda Kenya kushawishi serikali ya Mzee Jomo Kenyatta iruhusu ndege za jeshi la Isarel kutumia kiwanja chao cha ndege. Ehud barak na wenzake hawakwenda tu moja kwa moja kwa Mzee Kenyatta, bali kwanza walienda kwa Waziri wa kilimo wa kipindi hicho Bw. Bruce McKenzie ambaye huyu aliwahi kuwa afisa wa Idara ya ujasusi ya Uingereza, MI6 na pia alikuwa swahiba mkubwa wa Ehud Barak. Kwa hiyo Israel ikamtumia Bruce McKenzie kumshawishi Mzee Jomo Kenyatta kuruhusu anga la Kenya na viwanjavya ndege kutumiwa na makomando wa Israel na ndege zao. Ehud Barak na maafisa wa Mossad hawakuishia hapa tu, bali pia walifanya vikao vya siri na wafanyabiashara wakubwa nchini Kenya wenye asili ya Israel na wale ambao walikuwa na ‘marafiki’ wa Israel kuwaomba watumie ushawishi wao wa kisiasa na kiuchumi wasaidie kumshawishi Kenyatta kukubali ombi la seriakli ya Israael viwanja vyao kutumika na ndege za kijeshi za Israel na makondo wake. Baada ya mashinikizo haya kutoka kila upande, Mzee Kenyatta hakuwa na chaguo linguine zaidi ya kukubali ombi lao. Bwana huyu McKenzie pia alikuwa na ndege yakebinafsi, na Ehud Barak akaona fursa. Walitumia ndege hii ya kiraia kuruka mpaka Uganda mijini Entebbe na kukatiza juu ya anga la uwanja wa ndege wa Entebbe na walipokuwa wanapita juu ya anga la uwanja wa ndege, Ehud Barak akatumia fursa hii kupiga picha kila eneo la uwanja. Kwa kuwa hii ilikuwa ni ndege ya kiraia, jeshi la Uganda hawakushughulika nayo. Picha hizi zilizopigwa na Ehud Barak zilikuja kuwa na umuhimumkubwa katika maandalizi ya mwisho ya oparesheni ya makomando wa Isarel Kuvamia uwanja huu. Mpaka kufikia hapa maandalizi yote muhimu yalikuwa yamekamilika. WAKATI HUO HUO Upande wa watekaji kule Uganda walikuwa wanasubria mifwedha yao dola milioni 5 za kimarekani. Rais Idd Amin naye baada ya kufikia makubaliano na Israel kuwa masharti ya fedha na wafungwa wa kipalestina kuachiwa tarehe 4 July, naye ‘akarelax’ na akaona huo ndio muda wa kutekeleza majukumu Mengine akisubiria tarehe 4 July ifike. Katika kipindi hiki Idd amin ndiye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa kuzingatia utaratibu wa uenyekiti kuzunguka kwa kila nchi kwa mwaka mmoja mmoja na wiki hii alikuwa anatakiwa kwenye kikao cha Umoja wa Afrika kilichokuwa kinafanyika Mauritius. Kwa hiyo Amin akafunga safari kuelekea Mauritius kwenda kukabidhi kijiti cha Uenyekiti. Ehud Barak aliposikia taarifa hii, kwa kutumia akili yake kubwa ya kuzaliwa aliyojaliwa na uzoefu wake wa ujasusi, aliona fursa adhimu kabisa hapa. Akawasiliana na walioko kikaoni huko Tel Aviv na kuwaeleza taarifa ambazo awali wote hawakuielewa. Ehud Barak: “Idd Amin akiwa ndani ya Uganda huwa anatumia Mercedes Limousine katika msafara wake” Waziri Mkuu Rabin: “Ok! Limefanyaje?’ Ehud Barak: “Nataka mtafute gari kama hiyo… Mercedes Limousine” Waziri Mkuu Rabin: “la kazi gani?” Ehud Barak: “siku ambayo kikosi cha makomando wakipanda kwenye ndege kutoka huko Israel kwenda Uganda, gari hilo nataka pia lipakiwe ndani ya ndge!” Kwa dakika kadhaa wote ambao walikuwa wanamsikiliza pale kikaoni kupitia simu hakuna ambaye alielewa nini hasa Ehud Barak alikuwa anapendekeza. Yalikuwa yamebaki masaa machache tu ambapo, weledi, ushujaa na uzalendo uliotukuka ulikuwa unaedna kudhihirika. Itaendelea #TheBOLD_JF
    0 Comments ·0 Shares ·1K Views
  • OPERATION ENTEBBE -4

    Katika sehemmu iliyopita nilieleza namna ambavyo baada ya madege ya kivita ya Lockheed Harcules C-130 kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe na moja ya ndege hizo kwenda moja kwa moja karibu na geti la Terminal huku mlango wa nyuma ukiwa wazi na kutoka gari aina na Mercides pamoja na Land Rover kufanana kabisa na msafara wa Idd Amin atembeleapo uwanja wa ndege, la kini ajabu ni kwamba walijikuta wakinyooshewa bunduki na wanajeshi waliokuwa wanalinda getini…
    Walikuwa hawana taarifa kuwa Amin alikuwa amebadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda nyeupe kabla ya safari yake ya kwenda Mauritius kwenye kikao cha O.A.U.
    Tuendelee…
    SEHEMU TA NNE
    Wanajeshi hawa wawili wa Uganda waliokuwa getini walinyanyua bunduki zao aina ya Kalashnikov na hawakuonyesha dalili kwamba labda walikuwa wanataka kufanya ukaguzi wa kawaida tu kabla ya kuwaruhusu, walionyesha dhahiri kabisa kwamba walikuwa wanataka kufanya shambulio.
    Kabla wanajeshi hao wa Uganda kufanya lolote lile, Netanyahu na komando mwingine ambao walikuwa ndani ya gari walitumia weledi wao kufanya uamuzi makini wa haraka kwa kufyatua risasi kutoka kwenye bastola zao zenye ‘silencer’ na mara moja wale wanajeshi wawili wa Uganda walienda chini.
    Lakini moja ya wale wanajeshi wa Uganda waliodondoka chini baada ya kufyatuliwa risasi, hakufa mara moja na alikuwa anajitahidi kuinuka. Hii ilisababisha komando mwingine wa Israel kufyatua risasi lakini safari hii huyu komando wa Israel alifyatua risasi kutoka kwenye bunduki ambayo haina ‘silencer’. Hii iliwashitua wanajeshi wengine wa Uganda waliokuwa nje ya Terminal na kuanza kukimbilia walipokuwa wanasikia milio ya risasi inatokea huku wanafyatua risasi.
    Kwa maneno mengine ilikuwa kwa kiasi fulani walichokuwa wamekipanga makomando wa Israel, kufanya shambulio la kushitukiza lakini mpaka muda huu tayari ile ‘element of surprise’ ilikuwa haipo tena, jeshi la Uganda lilikuwa limeshitukia ‘mchezo’.
    Bila kuchelewa sana, makomando wote walikuwa kwenye zile gari mbili (Mercedes na Land Rover) waliruka nje ya gari na kukimbia kuelekea ndani ya terminal.
    Vichwani mwao walikuwa bado hawajaondokewa na kumbukumbu ya oparesheni kama hii iliyotokea miaka miwili iliyopita nchini Israel kwenye mji wa Ma’a lot ambapowatekaji wa KIpalestina baada ya kushituka kuwa kulikuwa na makomando wa Israel wamefika kufanya uokozi, waliwapiga risasi mateka wao 25 ambao kati yao 22 walikuwa ni watoto wadogo.
    Hivyo Netanyahu na wenzake hawakutaka kitu kama hiki kjitokeze tena… Netenyahu na makomando wenzake wa Syeret Matkal kwa ustadi wa hali ya juu walikimbia na kuingia ndani ya terminal na kuwaacha vile vikosi vingine kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliopo nje ya terminal (kama nilivyoeleza juzi namna kikosi kilivyogawanywa kwenye vikundi vidogo kila kimoja kikipewa jukumu lake).
    Mateka wanaeleza kwamba baada ya mpambano ya risasi kuanza huko nje ya terminal waliwaona watekaji kadhaa wakiongozwa na yule aliyeonekana kama kiongozi wao, Wilfred Bose waliingia ndani ya terminal wakiwa wanahaha kama wamechanganyikiwa wasijue wafanye nini, ilionekana dhahiri kuwa walikuwa hawajajiandaa kwa hili shambulio la ghafla, ilionekana dhahiri kwamba katika akili yao walikuwa wanasubiria Israel kutimiza masharti yao ili waweze kuachia mateka.
    Kuna muda Wilfred Bose alionekana kunyoonya bunduki yake kwa mateka kama vile anawataka kuwamininia risasi lakini alikuwa anashindwa kufanya uamuzi huo. Bose aligeuka ghafla baada ya kusikia kishindo cha mlango wa terminal ukifunguliwa.
    Makomando wa Israel walikuwa wametumia weledi na ustadi wao wa hali ya juu kuingia ndani ya terminal kwa muda sahihi kabla ya Wilfred Bose na wenzake kufanya uamuzi wowote wa kuua mateka.
    Makomando wa Israel walipoingia tu ndani ya terminal, mmoja wao mkononi walikuwa na kipaza sauti aina ya ‘megaphone’ na alikuwa anaongeea kwa nguvu kwa lugha ya kihebrania, “Lay down, Lay down. We are Israel soldiers. Lay down. Lay down!!”.
    Mateka wote wa kiisrael hata wale waliokuwa wamekaa kitako walilala chini, hivyo ndani ya sekunde chache tu kila mtu ambaye alibakia amesimama alikuwa ni halali yao kumtandika risasi.
    Kwa bahati mbaya kulikuwa na mateka kadhaa ambao wwalikuwa hawajui kihebreania sawia na hii iliwagharimu sana. Kwa mfano kulikuwa na kijana wa mika 19 aliyeitwa Jean-Jacques Maimoni, huyu alikuwa amehamia Israel siku si nyingi sana kutokea nchini ufaransa. Lilipotolewa tangazo hilo la kila mtu kulala chini hakuelewa na alibakia akiwa amesimama na alitandikwa risasi na makomando wa Israel pamoja na wale watekaji. Kijana huyu hakuwa peke yake, lakini pia kulikuwa na mateka mwingine aliyeitwa Ida Borochovitch, ambaye alihamia Israel kutoka nchini Urusi.
    Risasi zilirindima kwa takribani dakika mbili nzima na baadae ukimya wa kama sekunde 15 ukatawala na moja wa makomando wa kiisrael akauliza kwa kiebrania, “where are the rest of them?” (“wako wapi wengine?”). Mateka wakaonyesha kidole kwenye chumba kidogo kilichopo pembeni.
    Makomando wakarusha mabomu kadhaa ya kutupa kwa mkono na kisha kuingia ndani ya chumba hicho na kuwamiminia risasi wote ambao walikuwa humo.
    Milio ya risasi ndani ya terminal hatimaye ilikuwa imekoma japo bado huko nje walisikia majibizano ya risasi. Mwanajeshi mmoja wa Israel kati ya wale waliopo ndani ya terminal, kwa sauti ya utulivu kabisa na katika lugha ya kihebrania aliwatangazia mateka, “listen guys, we’ve come to take you home!” (“sikilizeni, tumekuja kuwachukua kuwarudisha nyumbani!”).
    Baada ya hapo makomando walianza kuwatoa mateka kutoka kwenye terminal na kuwapakia kwenye ndege kwa tahadhari kubwa huku wale wenzao wengine wakiendelea kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanarusha risasi kutoka kwenye maeneo ya kujificha ndani ya uwanja wa ndege.
    Wakiwa wanaendelea kuwapakia mateka waliowaokoa kwenye ndege, kumbe kulikuwa na mwanajeshi wa Uganda amebakia juu kwenye mnara wa uongozaji (airport control tower). Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibunui kutoka kwa mtoto wa Idd Amin anasema kwamba mwanajeshi huyu alikuwa ni binamu wa Idd Amin. Kutokea hapo kwenye mnara alimimina risasi mfululizo kwa makomando wa Israel na moja ya risasi hizi ilimpaka Koamando Yonatan Netanyahu ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Matkal iliyopo hapoa na alipoteza uhai pale pale.
    Wanajeshi wa Isarel walijibu mapigo kwa kurusha bomu la roketi ndogo ya begani na kusambaratisha kabisa kiota cha mnara na kumuua mwanajeshi wa Uganda aliyekuwa anawashambulia.
    Baada ya hapo waliwapakia kwenye ndege mateka wote ambao waliokolewa pamoja na miili ya Waisrael ambao walifariki kwenye majibizano hayo ya risasi.
    Kisha ili kuhakikisha kuwa hakuna ndege itakayowafuatia nyuma wakiondoka au kushambuliwa, walilipua ndege zote za jeshi la Uganda ambazo zilikuwa uwanjani hapo.
    Oparesheni yote hii ilichukua takribani dakika 53 ambapo dakika 30 pekee ndio zilikuwa za mapigano na 23 zilizosalia zilikuwa za kupakia mateka walio okolewa na kuondoka.
    Mpaka kufikia mwishio mwa oparesheni, jumla ya watekaji wote 7 walikuwa wameuwawa, pia wanajeshi 45 wa jeshi la Uganda walikuwa wameuwawa pia. Lakini pia ndege za kijeshi 11 aina ya MiG-17 na Mig-21 zililipuliwa na makomando wa Isarel. Ikumbukwe kwamba ndege hizi ndizo zilikuwa ni ndege zote za kijeshi ambazo zilikuwa zinamilikiwa na jeshi la anga la Uganda. Hii inaonyesha moja kati ya mapungufu makubwa ya kiuongozi ya Amin. Hakukuwa na busara yoyote au faida yoyote ya kimkakati kuweka ndege zote za jeshi lako la anga kwenye uwanja wa ndege wa kiraia ili kulinda mateka wa tukio ambalo wengine walikuwa wanaweza kuliona kama tukio la kigaidi na kwa namna Fulani kama ugomvi ambao ulikuwa haumuhusu moja kwa moja.
    Katika mateka wote 106 waliobakia (kumbuka nilieleza kuwa kulikuwa na mikupuo miwili ya mateka wasio wa Kiisrael au asili ya Kiyahudi waliachiwa kwa kupelekwa na ndege ufaransa nchini), kwahiyo kati ya wale 106 waliobakio, mateka watatu waliuwawa muda wa mapambano (hawa ndio wale ambao walikuwa hawaelewi kihebrania kwa ufasaha na kwa hiyo hawakulalala chini kama ilivyoamrishwa na makomando wa Israel), na mateka mmoja bibi wa miaka 74 aliyeitwa Dora Bloch aliachwa akiwa Hospitali mjini Entebbe ambako alipelekwa na Amin siku kadhaa nyuma kutokana na kuhitaji uangalizi maalumu wa kidaktari.
    Kati ya Makomando wa Isarel, ni mmoja tu ndiye aliuwawa tena dakika za mwisho (Yonatan Netanyahu) japo pia kuna makomando wengine kama watano ambao walijeruhiwa. Kifo cha kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Mitkal, Yonatan Netanyahu katika oparesheni hii ndio iliyofanya siku kadhaa baadae oparesheni hii pia kubatizwa jina la OPERATION YONATAN kwa heshima yake na ushujaa wake wa kutoa maisha yake ili kutetea na kuooa roho za raia alioapa kuwalinda.
    Baada ya kila kitu kuwekwa sawa na watu wote kupanda ndani ya ndege, waliruka mpaka Nairobi Kenya kwa mapumziko mafupi ili kutibia wale ambao walijeruhiwa (kama ambavyo nilieleza kuwa ile moja ya Boeing 707 iliyotengwa kama ‘hospitali’ ilibaki Nairobi).
    Baada ya matibabu hapo Nairobi, madege yote yaliruka kurudi Israel. Kwa kifupi operation hii was a big SUCCESS.!
    Japokuwa baada ya ulimwengu mzima kutangaziwa juu ya kilichotokea, juu ya ‘umafia’ uliofanywa na Israel, ulimwengu uligawanyika kila nchi ukiunga mkono upande fulani, lakini nchi nyingi ziliunga mkono Israel kwa matumizi ya jeshi katika nchi nyingine, wengi walimlaumu Amin kwa kushindwa kutumia diplomasia kumaliza mzozo huu. Ajabu ni kwamba mwezi huo wa July, Mkuu wa Majeshi wa Iran moja wa mahsimu wa siku zote wa Israel aliandika barua kwa Waziri mkuu wa Israel kumpongeza kuhusu Oparation hiyo na kumpa pole kwa kifo cha Yonatan Netanyahu akimuita Yonatan kumsifu kuwa ni ‘martyr’.
    Vyovyote vile ambavyo unaweza kuitazama oparesheni hii kwenye jicho la kisiasa ua kidiplomasia, kwamba kama ilikuwa ni sahihi au si sahihi lakini katika jicho la kijeshi na ujasusi hii ni moja ya oparesheni murua kabisa kuwahi kufanyika katika historia ya majeshi duniani. Moja ya manguli wa “ulimwengu wa giza”, Bw. Henry Kissinger aliwahi kutamka kuwa hii ilikuwa ni “an immposible mission”!
    Umaridadi wa oparesheni hii umefanya hata vitengo kadhaa vya weledi vya majeshi mbali mbali kutaka kuiga mfano wake lakini bila mafanikio yoyote. Kwa mfano Wamarekani walijaribu kuiga umaridadi wa Oparesheni hii na kufanya ya kwao iliyoitwa Oparation Eagle Claw baada ya kutokea kwa utekeaji kwenye ubalozi wa Iran lakini oparesheni hiyo ilifeli vibaya.
    Sasa hivi kama wewe ni mwanajeshi katika jeshi fulani kwenye kitengo cha weledi (special force) au labda ni jasusi maalumu, lazima katika hatua fulani ya japo hata ‘darasani’ kwenye makaratasi utafundwa kuhusu Oparetion Entebbe na namna ilivyo tekelezwa.
    Oparesheni hii ilimuacha Amin na aibu kubwa kiasi kwamba akaendelea kufanya vitu ambavyo vilidhihirisha udhaifu wake wa kiungozi. Kwa mfano, yule bibi wa miaka 74 aliyeachwa hospitali mjini Entebbe, aliamuru auwawe kinyama. Lakini pia Amin alisimami kuwawa kwa McKenzie yule waziri wa kilimo wa Kenya ambaye alimsaidia Ehud Barak kumshinikiza Mzee Jomo Kenyetta kuruhusu ndege za jeshi la Israel kutumia viwanja vya ndege vya Kenya wakati wa utekelezaji wa OParesheni hiyo na pia kumsaidi kukusanya Intelijensia kwa kutumia ndege yake binafsi.
    McKenzie aliuwawa kwa bomu lililotegwa kwenye gari yake.
    Pia Amin alisimamia ulipuaji kwa bomu moja ya hoteli kubwa Nairobi kipindi hicho ambayo ilikuwa inaitwa The Norfolk Hotel, ambayo ilimilikiwa na moja ya wayahudi mashuhuri nchini Kenya.
    [6/12, 13:48] The Bold: Licha ya ‘fujo’ zote hizi ambazo Amin alizifanya baada ya jeshi lake kudhalilika kutokana na Oeration Entebbe lakini hatupawsi kusahau kwamba chini ya miaka mitatu baadae, yaani baada ya utekelezaji wa opareshini hii, Idd Amin aliondolewa kwa aibu madarakani na majeshi ya Tanzania na kumfanya akimbie nchi yake.

    ......................MWISHO..............
    #TheBOLD_JF
    OPERATION ENTEBBE -4 Katika sehemmu iliyopita nilieleza namna ambavyo baada ya madege ya kivita ya Lockheed Harcules C-130 kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe na moja ya ndege hizo kwenda moja kwa moja karibu na geti la Terminal huku mlango wa nyuma ukiwa wazi na kutoka gari aina na Mercides pamoja na Land Rover kufanana kabisa na msafara wa Idd Amin atembeleapo uwanja wa ndege, la kini ajabu ni kwamba walijikuta wakinyooshewa bunduki na wanajeshi waliokuwa wanalinda getini… Walikuwa hawana taarifa kuwa Amin alikuwa amebadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda nyeupe kabla ya safari yake ya kwenda Mauritius kwenye kikao cha O.A.U. Tuendelee… SEHEMU TA NNE Wanajeshi hawa wawili wa Uganda waliokuwa getini walinyanyua bunduki zao aina ya Kalashnikov na hawakuonyesha dalili kwamba labda walikuwa wanataka kufanya ukaguzi wa kawaida tu kabla ya kuwaruhusu, walionyesha dhahiri kabisa kwamba walikuwa wanataka kufanya shambulio. Kabla wanajeshi hao wa Uganda kufanya lolote lile, Netanyahu na komando mwingine ambao walikuwa ndani ya gari walitumia weledi wao kufanya uamuzi makini wa haraka kwa kufyatua risasi kutoka kwenye bastola zao zenye ‘silencer’ na mara moja wale wanajeshi wawili wa Uganda walienda chini. Lakini moja ya wale wanajeshi wa Uganda waliodondoka chini baada ya kufyatuliwa risasi, hakufa mara moja na alikuwa anajitahidi kuinuka. Hii ilisababisha komando mwingine wa Israel kufyatua risasi lakini safari hii huyu komando wa Israel alifyatua risasi kutoka kwenye bunduki ambayo haina ‘silencer’. Hii iliwashitua wanajeshi wengine wa Uganda waliokuwa nje ya Terminal na kuanza kukimbilia walipokuwa wanasikia milio ya risasi inatokea huku wanafyatua risasi. Kwa maneno mengine ilikuwa kwa kiasi fulani walichokuwa wamekipanga makomando wa Israel, kufanya shambulio la kushitukiza lakini mpaka muda huu tayari ile ‘element of surprise’ ilikuwa haipo tena, jeshi la Uganda lilikuwa limeshitukia ‘mchezo’. Bila kuchelewa sana, makomando wote walikuwa kwenye zile gari mbili (Mercedes na Land Rover) waliruka nje ya gari na kukimbia kuelekea ndani ya terminal. Vichwani mwao walikuwa bado hawajaondokewa na kumbukumbu ya oparesheni kama hii iliyotokea miaka miwili iliyopita nchini Israel kwenye mji wa Ma’a lot ambapowatekaji wa KIpalestina baada ya kushituka kuwa kulikuwa na makomando wa Israel wamefika kufanya uokozi, waliwapiga risasi mateka wao 25 ambao kati yao 22 walikuwa ni watoto wadogo. Hivyo Netanyahu na wenzake hawakutaka kitu kama hiki kjitokeze tena… Netenyahu na makomando wenzake wa Syeret Matkal kwa ustadi wa hali ya juu walikimbia na kuingia ndani ya terminal na kuwaacha vile vikosi vingine kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliopo nje ya terminal (kama nilivyoeleza juzi namna kikosi kilivyogawanywa kwenye vikundi vidogo kila kimoja kikipewa jukumu lake). Mateka wanaeleza kwamba baada ya mpambano ya risasi kuanza huko nje ya terminal waliwaona watekaji kadhaa wakiongozwa na yule aliyeonekana kama kiongozi wao, Wilfred Bose waliingia ndani ya terminal wakiwa wanahaha kama wamechanganyikiwa wasijue wafanye nini, ilionekana dhahiri kuwa walikuwa hawajajiandaa kwa hili shambulio la ghafla, ilionekana dhahiri kwamba katika akili yao walikuwa wanasubiria Israel kutimiza masharti yao ili waweze kuachia mateka. Kuna muda Wilfred Bose alionekana kunyoonya bunduki yake kwa mateka kama vile anawataka kuwamininia risasi lakini alikuwa anashindwa kufanya uamuzi huo. Bose aligeuka ghafla baada ya kusikia kishindo cha mlango wa terminal ukifunguliwa. Makomando wa Israel walikuwa wametumia weledi na ustadi wao wa hali ya juu kuingia ndani ya terminal kwa muda sahihi kabla ya Wilfred Bose na wenzake kufanya uamuzi wowote wa kuua mateka. Makomando wa Israel walipoingia tu ndani ya terminal, mmoja wao mkononi walikuwa na kipaza sauti aina ya ‘megaphone’ na alikuwa anaongeea kwa nguvu kwa lugha ya kihebrania, “Lay down, Lay down. We are Israel soldiers. Lay down. Lay down!!”. Mateka wote wa kiisrael hata wale waliokuwa wamekaa kitako walilala chini, hivyo ndani ya sekunde chache tu kila mtu ambaye alibakia amesimama alikuwa ni halali yao kumtandika risasi. Kwa bahati mbaya kulikuwa na mateka kadhaa ambao wwalikuwa hawajui kihebreania sawia na hii iliwagharimu sana. Kwa mfano kulikuwa na kijana wa mika 19 aliyeitwa Jean-Jacques Maimoni, huyu alikuwa amehamia Israel siku si nyingi sana kutokea nchini ufaransa. Lilipotolewa tangazo hilo la kila mtu kulala chini hakuelewa na alibakia akiwa amesimama na alitandikwa risasi na makomando wa Israel pamoja na wale watekaji. Kijana huyu hakuwa peke yake, lakini pia kulikuwa na mateka mwingine aliyeitwa Ida Borochovitch, ambaye alihamia Israel kutoka nchini Urusi. Risasi zilirindima kwa takribani dakika mbili nzima na baadae ukimya wa kama sekunde 15 ukatawala na moja wa makomando wa kiisrael akauliza kwa kiebrania, “where are the rest of them?” (“wako wapi wengine?”). Mateka wakaonyesha kidole kwenye chumba kidogo kilichopo pembeni. Makomando wakarusha mabomu kadhaa ya kutupa kwa mkono na kisha kuingia ndani ya chumba hicho na kuwamiminia risasi wote ambao walikuwa humo. Milio ya risasi ndani ya terminal hatimaye ilikuwa imekoma japo bado huko nje walisikia majibizano ya risasi. Mwanajeshi mmoja wa Israel kati ya wale waliopo ndani ya terminal, kwa sauti ya utulivu kabisa na katika lugha ya kihebrania aliwatangazia mateka, “listen guys, we’ve come to take you home!” (“sikilizeni, tumekuja kuwachukua kuwarudisha nyumbani!”). Baada ya hapo makomando walianza kuwatoa mateka kutoka kwenye terminal na kuwapakia kwenye ndege kwa tahadhari kubwa huku wale wenzao wengine wakiendelea kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanarusha risasi kutoka kwenye maeneo ya kujificha ndani ya uwanja wa ndege. Wakiwa wanaendelea kuwapakia mateka waliowaokoa kwenye ndege, kumbe kulikuwa na mwanajeshi wa Uganda amebakia juu kwenye mnara wa uongozaji (airport control tower). Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibunui kutoka kwa mtoto wa Idd Amin anasema kwamba mwanajeshi huyu alikuwa ni binamu wa Idd Amin. Kutokea hapo kwenye mnara alimimina risasi mfululizo kwa makomando wa Israel na moja ya risasi hizi ilimpaka Koamando Yonatan Netanyahu ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Matkal iliyopo hapoa na alipoteza uhai pale pale. Wanajeshi wa Isarel walijibu mapigo kwa kurusha bomu la roketi ndogo ya begani na kusambaratisha kabisa kiota cha mnara na kumuua mwanajeshi wa Uganda aliyekuwa anawashambulia. Baada ya hapo waliwapakia kwenye ndege mateka wote ambao waliokolewa pamoja na miili ya Waisrael ambao walifariki kwenye majibizano hayo ya risasi. Kisha ili kuhakikisha kuwa hakuna ndege itakayowafuatia nyuma wakiondoka au kushambuliwa, walilipua ndege zote za jeshi la Uganda ambazo zilikuwa uwanjani hapo. Oparesheni yote hii ilichukua takribani dakika 53 ambapo dakika 30 pekee ndio zilikuwa za mapigano na 23 zilizosalia zilikuwa za kupakia mateka walio okolewa na kuondoka. Mpaka kufikia mwishio mwa oparesheni, jumla ya watekaji wote 7 walikuwa wameuwawa, pia wanajeshi 45 wa jeshi la Uganda walikuwa wameuwawa pia. Lakini pia ndege za kijeshi 11 aina ya MiG-17 na Mig-21 zililipuliwa na makomando wa Isarel. Ikumbukwe kwamba ndege hizi ndizo zilikuwa ni ndege zote za kijeshi ambazo zilikuwa zinamilikiwa na jeshi la anga la Uganda. Hii inaonyesha moja kati ya mapungufu makubwa ya kiuongozi ya Amin. Hakukuwa na busara yoyote au faida yoyote ya kimkakati kuweka ndege zote za jeshi lako la anga kwenye uwanja wa ndege wa kiraia ili kulinda mateka wa tukio ambalo wengine walikuwa wanaweza kuliona kama tukio la kigaidi na kwa namna Fulani kama ugomvi ambao ulikuwa haumuhusu moja kwa moja. Katika mateka wote 106 waliobakia (kumbuka nilieleza kuwa kulikuwa na mikupuo miwili ya mateka wasio wa Kiisrael au asili ya Kiyahudi waliachiwa kwa kupelekwa na ndege ufaransa nchini), kwahiyo kati ya wale 106 waliobakio, mateka watatu waliuwawa muda wa mapambano (hawa ndio wale ambao walikuwa hawaelewi kihebrania kwa ufasaha na kwa hiyo hawakulalala chini kama ilivyoamrishwa na makomando wa Israel), na mateka mmoja bibi wa miaka 74 aliyeitwa Dora Bloch aliachwa akiwa Hospitali mjini Entebbe ambako alipelekwa na Amin siku kadhaa nyuma kutokana na kuhitaji uangalizi maalumu wa kidaktari. Kati ya Makomando wa Isarel, ni mmoja tu ndiye aliuwawa tena dakika za mwisho (Yonatan Netanyahu) japo pia kuna makomando wengine kama watano ambao walijeruhiwa. Kifo cha kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Mitkal, Yonatan Netanyahu katika oparesheni hii ndio iliyofanya siku kadhaa baadae oparesheni hii pia kubatizwa jina la OPERATION YONATAN kwa heshima yake na ushujaa wake wa kutoa maisha yake ili kutetea na kuooa roho za raia alioapa kuwalinda. Baada ya kila kitu kuwekwa sawa na watu wote kupanda ndani ya ndege, waliruka mpaka Nairobi Kenya kwa mapumziko mafupi ili kutibia wale ambao walijeruhiwa (kama ambavyo nilieleza kuwa ile moja ya Boeing 707 iliyotengwa kama ‘hospitali’ ilibaki Nairobi). Baada ya matibabu hapo Nairobi, madege yote yaliruka kurudi Israel. Kwa kifupi operation hii was a big SUCCESS.! Japokuwa baada ya ulimwengu mzima kutangaziwa juu ya kilichotokea, juu ya ‘umafia’ uliofanywa na Israel, ulimwengu uligawanyika kila nchi ukiunga mkono upande fulani, lakini nchi nyingi ziliunga mkono Israel kwa matumizi ya jeshi katika nchi nyingine, wengi walimlaumu Amin kwa kushindwa kutumia diplomasia kumaliza mzozo huu. Ajabu ni kwamba mwezi huo wa July, Mkuu wa Majeshi wa Iran moja wa mahsimu wa siku zote wa Israel aliandika barua kwa Waziri mkuu wa Israel kumpongeza kuhusu Oparation hiyo na kumpa pole kwa kifo cha Yonatan Netanyahu akimuita Yonatan kumsifu kuwa ni ‘martyr’. Vyovyote vile ambavyo unaweza kuitazama oparesheni hii kwenye jicho la kisiasa ua kidiplomasia, kwamba kama ilikuwa ni sahihi au si sahihi lakini katika jicho la kijeshi na ujasusi hii ni moja ya oparesheni murua kabisa kuwahi kufanyika katika historia ya majeshi duniani. Moja ya manguli wa “ulimwengu wa giza”, Bw. Henry Kissinger aliwahi kutamka kuwa hii ilikuwa ni “an immposible mission”! Umaridadi wa oparesheni hii umefanya hata vitengo kadhaa vya weledi vya majeshi mbali mbali kutaka kuiga mfano wake lakini bila mafanikio yoyote. Kwa mfano Wamarekani walijaribu kuiga umaridadi wa Oparesheni hii na kufanya ya kwao iliyoitwa Oparation Eagle Claw baada ya kutokea kwa utekeaji kwenye ubalozi wa Iran lakini oparesheni hiyo ilifeli vibaya. Sasa hivi kama wewe ni mwanajeshi katika jeshi fulani kwenye kitengo cha weledi (special force) au labda ni jasusi maalumu, lazima katika hatua fulani ya japo hata ‘darasani’ kwenye makaratasi utafundwa kuhusu Oparetion Entebbe na namna ilivyo tekelezwa. Oparesheni hii ilimuacha Amin na aibu kubwa kiasi kwamba akaendelea kufanya vitu ambavyo vilidhihirisha udhaifu wake wa kiungozi. Kwa mfano, yule bibi wa miaka 74 aliyeachwa hospitali mjini Entebbe, aliamuru auwawe kinyama. Lakini pia Amin alisimami kuwawa kwa McKenzie yule waziri wa kilimo wa Kenya ambaye alimsaidia Ehud Barak kumshinikiza Mzee Jomo Kenyetta kuruhusu ndege za jeshi la Israel kutumia viwanja vya ndege vya Kenya wakati wa utekelezaji wa OParesheni hiyo na pia kumsaidi kukusanya Intelijensia kwa kutumia ndege yake binafsi. McKenzie aliuwawa kwa bomu lililotegwa kwenye gari yake. Pia Amin alisimamia ulipuaji kwa bomu moja ya hoteli kubwa Nairobi kipindi hicho ambayo ilikuwa inaitwa The Norfolk Hotel, ambayo ilimilikiwa na moja ya wayahudi mashuhuri nchini Kenya. [6/12, 13:48] The Bold: Licha ya ‘fujo’ zote hizi ambazo Amin alizifanya baada ya jeshi lake kudhalilika kutokana na Oeration Entebbe lakini hatupawsi kusahau kwamba chini ya miaka mitatu baadae, yaani baada ya utekelezaji wa opareshini hii, Idd Amin aliondolewa kwa aibu madarakani na majeshi ya Tanzania na kumfanya akimbie nchi yake. ......................MWISHO.............. #TheBOLD_JF
    0 Comments ·0 Shares ·2K Views
  • DUNIA NA MAAJABU YAKE
    (Muundo wa Dunia na Maajabu Yaliyomo)

    1. UMRI WA DUNIA

    HII Dunia yetu ina historia ndefu mno tangu ilipojiunda angani, miaka takribani bilioni 4.5 iliyopita.

    Tarakimu za umri huo wa miaka bilioni 4.5 ni 4,500,000,000, yaani miaka milioni elfu nne na mia tano iliyopita.

    Dunia ambayo kwa lugha ya Kiingereza inafahamika vyema kwa jina la 'Earth', pia hujulikana kama 'the World', ikimaanishwa ulimwengu.

    Aidha, Dunia ni sayari pekee kwenye himaya ya sayari zilizopo chini ya jua ambayo jina lake halitokani na majina ya "Miungu wa Dola" ya Kigiriki au ya Kirumi.

    Asili ya jina la 'earth' ni 'erde' lenye asili ya nchini Ujerumani, na maana yake ni udongo au ardhi.

    Mpaka kuweza kupata umri huo wa dunia wanasayansi walifanya kazi ya kutafiti na kisha kuwasilisha matokeo yao kwenye makongamano ya kisayansi duniani, ambapo matokeo hayo yalijadiliwa kwa kina na hatimaye kukubalika kama hivi.

    Kumbuka katika majadiliano hayo huwepo mivutano mikali miongoni mwa wanasayansi waalikwa, ambapo pia jopo la wanasayansi wanaowasilisha utafiti husika hujikuta wakitakiwa kujibu hoja mbalimbali za wanasayansi wenzao.

    Kuna wakati baadhi ya matokeo ya tafiti kadhaa hukataliwa, huku watafiti husika wakitakiwa kurejea upya tafiti zao.

    Wanasayansi hupata umri wa sayari kwa kupima umri wa miamba ya sayari husika, ambapo mwamba wenye umri mkubwa zaidi kuliko miamba yote ndiyo huchukuliwa kuwa umri wa sayari husika.

    Itakumbukwa kuwa Msahafu wa Biblia (Sura ya Mwanzo 1) husimulia jinsi Mwenyezi Mungu alivyoumba "mbingu na nchi na vyote vilivyomo kwa siku 6," lakini pia Msahafu huohuo kwenye aya zingine hueleza kuwa miaka elfu moja ya duniani yaweza kuwa sawa na siku moja kwenye ya Makazi ya Mwenyezi Mungu.

    Ni dhahiri kuwa binadamu tukiwa hatuna hoja sahihi kwa maelezo ya aina hiyo, ndipo tunaona ni vyema mambo ya Mwenyezi Mungu kumwachia Yeye Mwenyewe Mwenyezi Mungu.

    2. KUUMBIKA DUNIA, SAYARI, JUA, NYOTA

    Kimsingi, Dunia kama zilivyo sayari zingine zote ilijiunda kutokana na mabaki ya vitu vilivyotumika kuunda Jua.

    Jua ambalo ni nyota kama zilivyo nyota zote angani, lilijiunda lenyewe kwenye eneo la anga lijulikanalo kama 'Pillars of Creation' (nguzo za uumbaji) katika ukanda wa anga wenye upana ambao huonekana kutokuwa na mwisho.

    Ukanda huo ujulikanao kama 'Solar Nebula,' umegubikwa na mawingu ya vumbi la huko angani pamoja na aina mbalimbali za gesi na hewa, ikiwemo haidrojeni na heliumu.

    'Solar' ni jina la nishati itokanayo na joto la jua, na 'Nebula' kwa lugha ya Kilatini ni "wingu" au vumbi la gesi asilia mithili ya ukungu.

    Hivyo, 'Solar Nebula' ni ukanda katika anga ya mbali wenye mawingu yaliyosheheni nishati yenye joto, sawa na nishati ya joto la jua.

    Sasa basi, tunafahamu vyema kuwa jua hutoa mionzi hatari yenye joto kali mithili ya moto mkali, na ambayo ikiboreshwa kisayansi pia huweza kutoa nishati ya umeme.

    Hivyo, kwa muktadha huo, hebu ngoja sasa tuleta pamoja hewa za gesi, zikiwemo haidrojeni na heliumu, mawingu yenye nishati ya umeme wa jua, vumbi la angani na tufani itokanayo na mchafuko mbaya wa hali ya hewa huko anga za mbali.

    Na ili kuweza kupata matokeo yanayotakiwa, hebu pia tutambue uwepo wa nguvu kubwa ya asili katika kiwango kijulikanacho kwa jina la "Supernatural Power", ambayo ndiyo huwa kisababishi cha mambo yote.

    Kisayansi, "Supernatural Power" ni nguvu kubwa ya asili ambayo huendesha mifumo mbalimbali ya asili, ambapo duniani nguvu hiyo hujulikana kama Nguvu ya Mungu.

    Nguvu asili hiyo, yaani Supernatural Power, husababisha tufani ambayo huvurumisha kwa pamoja vitu vyote hivyo, (gesi, hewa, mawingu yenye nishati ya joto na vumbi la angani) ili kuunda tufani yenye umbo la duara.

    Duara hiyo ni kama ile itokanayo na kimbunga kikali duniani, na ambacho sasa tutaona kikifungamanisha pamoja vitu vyote hivyo katika mchafuko mkubwa wa hali mbaya ya hewa.

    Natumia maneno ya msisitizo kuelezea "ukubwa" wa mchafuko huo wa hali ya hewa katika eneo hilo la anga, kwani katika kuunda sayari au nyota nguvuasili kubwa hutumika.

    Aidha, tufani hiyo ya duara itakayoanza kidogo kidogo kama kimbunga kikali, itazidi kukua hadi kuwa na kipenyo cha takribani kilomita 10 hadi 200 au zaidi na kwendelea.

    Tufani hiyo ndiyo itavurumisha kwa pamoja gesi na hewa za naitrojeni na heliumu, mawingu ya nishati ya joto na vumbi la angani (kama kifanyavyo kimbunga kikali katika eneo tambarare la duniani).

    Pia, wakati mchafuko huo wa hali mbaya ya hewa ukiendelea, hebu ngoja sisi watazamaji tujibanze mahali fulani kwa mbali kushuhudia duara hiyo ya tufani ikijizungusha yenyewe bila kukoma kwa kipindi cha miaka mingi.

    Kitakachofuata ni kuanza kuona kiini cha moto kikianza kujiunda katikati ya duara hiyo ya tufani kali, huku pia nje ya duara hiyo vitu kibao vikivutwa kujiunga na mzunguko wa hiyo tufani ya duara.

    Vitu hivyo ni pamoja na vumbi zaidi la angani, na gesi zaidi zenye joto kali.

    Wakati huohuo kipenyo na mzingo wa duara hiyo vitazidi kuongezeka upana na ukubwa, mfano wa duara yenye umbo sawa na la mpira mkubwa wa miguu.

    Hivyo, baada ya miaka takribani milioni moja tutashangaa kuona lile vumbi likigeuka taratibu kuwa miamba ya moto ndani ya kiini cha tufani hiyo ya duara.

    Miamba hiyo ni kutokana na lile vumbi la angani ambalo hatimaye limeshikamana pamoja mithili ya zege, na hatimaye kuwa miamba ndani ya tufani ya duara.

    Sanjari na kuundika huko ndani ya kitovu cha hiyo tufani ya duara, pia kwelekea nje ya duara hiyo utaundika udongo ambao ardhi, mchanga na mawe.

    Kimsingi, vitu hivyo pia ni matokeo ya lile vumbi la angani ambalo lilikusanywa pamoja na kuvutwa na kasi ya mzunguko wa tufani.

    Hatua hiyo mpya inatokana na kuwepo mshikamano na mgandamizo wa zile chembechembe za lile vumbivumbi ndani ya tufani.

    Vurumai hiyo ya mzunguko wa hiyo tufani ya duara yenye vumbi, itazidi kukua hadi kuunda sumaku ya asili ndani ya kile kitovu cha duara ya tufani.

    Kutokana na duara hiyo ya tufani kuongezeka ukubwa, hatimaye sumaku iliyopo kwenye kitovu cha duara hiyo itaishiwa nguvu ya kwendelea kunasa vumbi zaidi kuja kwenye mzingo wa hiyo duara ya tufani.

    Kumbuka kuwa wakati huo hiyo duara pia itaunda kimo kutoka kwenye usawa wa ardhi yake kwenda ndani kwenye kitovu chake, na hivyo kuwa duara ya mviringo kama umbo mfano wa mpira mchezo wa miguu.

    Baada ya kupita maelfu ya miaka mingi, duara hiyo ambayo hapo awali ilianza kama umbo la tufani na kuzidi kukua huko angani, sasa itakuwa na joto kali kupita kiasi na kuanza kung'aa kama jua.

    Jua hilo, ndiyo nyota mojawapo ya zile ambazo huonekana usiku ziking'aa angani.

    Lakini pia wakati wa kujiunda nyota hiyo, kama tulivyoona hapo awali, baadhi ya mabaki yake yaliyokuwa yakitawanyika angani wakati ile tufani ya duara ikijizungusha, huweza kujikusanya pamoja na kuunda sayari ambazo huzunguka baadhi ya hizo nyota.

    Hivyo ndivyo zilivyojiunda sayari zote ambazo huelea kwa kulizunguka jua letu.

    Mathalani, sayari zote ambazo hulizunguka jua, ikiwemo dunia zilijiunda kutokana na mabaki ya vitu kama gesi, michanga na mawe ambavyo vilitawanyika angani wakati jua likijiunda (kama ambavyo imeelezwa hapo awali).

    3. KIINI CHA DUNIA

    Dunia yetu ambayo wastani wa nusu kipenyo cha umbo lake la duara ni kilomita 6,371, mzingo wake ni kilomita takribani 40,041.

    Kama zilivyo sayari zote katika himaya ya jua, dunia nayo ilijiunda wakati jua likijiunda lenyewe.

    Yaani kwamba sayari ni mabaki ya vitu vilivyotumika kuliunda jua.

    Kadhalika kama zilivyo sayari zingine zote, dunia nayo ina kiini chake ambacho kipo katikati ya ardhi yake.

    Kiini hicho kina nguvu kubwa ya sumaku ambayo, pamoja na mambo mengineyo, 'huvuta' umbo hilo la duara kutoka juu ya ardhi kwenda katikati ya kiini hicho.

    Muundo huo ndio hulifungamanisha pamoja umbo la duara la dunia, na hivyo kuzuia umbo hilo lisifumke kutoka ardhini na kusambaratika.

    Hiyo ni sawa na mpira wa miguu unavyoweza kupasuka na kusambaratika, kama utajazwa upepo kupita kiasi chake.

    Kiini hicho ambacho kipo katikati kabisa ya dunia, kinajulikanacho kwa jina la kisayansi la 'Inner Core.'

    Kiini hicho kina joto kali la sentigredi 6,230 ambacho ndio kiasi cha joto la jua.

    Kiini hicho kina umbo la duara lenye nusu kipenyo cha kilomita 1,250.

    Kama ingetokea kuchimba ardhi wima kwenda kwenye kiini hicho, mchimbaji angeanza kukutana na joto la kiini hicho kuanzia kimo cha umbali wa kilomita 5,150 kutoka usawa wa juu ya ardhi tunayotembea.

    Katika historia ya uchimbaji ardhi, kina kirefu kilichowahi kuchimbwa ardhini ni mita 12,345 (kilomita 12.345) huko Sakhalini, nchini Urusi, kwa ajili ya uvunaji wa mafuta ya petroli.

    Kiini cha dunia kinaundwa na madini mchanganyiko wa nikeli (nickle), chuma (iron) na dhahabu.

    Kwa mujibu wa utafiti, inakadiriwa kuwa kama dhahabu hiyo ingechimbwa na kuchomwa mpaka kuwa kimiminika sawa na uji na kisha kumwagwa chini, ingeweza kuifunika dunia yote kwa unene wa sentimeta 45.

    Kiini hicho muhimu kwa uhai wa sayari hii ya dunia kiligunduliwa mwaka 1936 na mtaalamu wa matetemeko ya ardhi wa nchini Denmark, mwanamama Dkt. Inge Lehmann.

    Dkt. Lehmann alihitimu shahada yake ya kwanza katika fani ya Hisabati mwaka 1910, ya Uzamili mwaka 1920 (zote kutoka Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini mwake), na ile ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza.

    Alifariki kwa uzee mwaka 1993 akiwa na umri wa miaka 104.

    4. MAJI DUNIANI

    Kupatikana maji kwenye dunia yetu, ni mojawapo ya miundo ambayo haipo katika sayari zingine ambazo tuna taarifa za kitafiti kuzuhusu.

    Maji ni muhimili muhimu kwa ajili ya uhai wa viumbe wote na mimea, ambavyo kwa pamoja havipo katika sayari zingine za himaya ya jua.

    Kwa mujibu wa tafiti nyingi ambazo zimefanyika kwa miongo mingi ya miaka kujaribu kubaini nini chanzo cha kuwepo maji duniani, hakuna hata utafiti mmoja ulioonesha kwa usahihi matokeo ya kuridhisha.

    Miongoni mwa tafiti hizo ni pamoja na ule wa mwaka 2005, ambapo Mkuu wa Idara ya Masomo ya Sayari na Mwezi katika Chuo Kikuu cha Arizona nchini Marekani, Profesa Michael Julian Drake, na mwenzake ambaye ni mtaalamu wa Vimondo, Dkt. Huberto Campins, wa Chuo Kikuu cha Central Florida, walitafiti nini chanzo cha kuwepo maji duniani.

    Katika mawasilisho yao kwenye kongamano la kisayansi la Chama cha Wanataaluma wa Maarifa ya Anga za Juu (IAU), watafiti hao walikanusha madai ya uwezekano wa dunia hapo kale kugongwa na kimondo kikubwa na kusababisha maji kulipuka kutoka ardhini.

    Wakiwasilisha matokeo ya utafiti wao kwenye mkutano wa kongamano hilo, magwiji hao wa masuala ya sayari walieleza kwenye waraka wao uitwao "Origin of water on the terrestial planets" (chanzo cha kuwepo maji kwenye sayari).

    Walidai kuwa maji yaliyopo duniani yaliumbika kwenye ardhi ya dunia tangu mwanzo, wakati ikijiunda angani.

    Ikumbukwe kuwa eneo la uso wa dunia likiwa ni jumla ya kilomita za mraba milioni 510, asilimia 70.8 ya eneo hilo imefunikwa na maji na asilimia 29.2 ni nchi kavu, ikiwemo milima, mabonde na ardhi tambarare.

    5. HEWA YA OKSIJENI

    Muundo mwingine muhimu katika sayari hii ya dunia ni hewa ambazo ni tawala, yaani Naitrojeni ambayo kwa usahihi imeenea kwa asilimia 78.08 ya hewa yote ya dunia, Oksijeni asilimia 20.95, 'Argon' asilimia 0.93, hewa ya Ukaa (Carbon dioxide) asilimia 0.039, na asilimia moja ni hewa mithili ya mvuke wa maji (water vapour).

    Hewa ya Oksijeni ambayo ni nguzo muhimu kwa ajili ya uhai wa viumbe wote na pia haipatikani kwenye sayari nyingine chini ya jua, inadhaniwa ilianza kupatikana duniani miaka takribani bilioni 2.5 iliyopita kufuatia "kukomaa kwa kiini cha dunia."

    Kwa mujibu wa matokeo ya tafiti mbalimbali na nadharia za kisayansi, inaoneshwa kuwa kukomaa kwa kiini hicho cha dunia hatimaye ndiko kulisababisha kuzuka duniani milipuko ya volikano ambayo pia ilisababisha kuzuka mabonde na milima.

    Inaoneshwa kuwa tayari wakati huo maji yaliishakuwepo duniani, na kuwezesha kuzuka chembechembe ndogo sana za kibakteria zijulikanazo kwa jina la kisayansi la 'cyanobacteria' au 'blue-green algae'.

    Kwa kutumia mwanga wa jua, maji na hewa ya ukaa, chembechembe hizo ziliweza kuzalisha hewa mbalimbali, ikiwemo 'Carbonhydrates' na Oksijeni.

    Kwa kuwa hizo chembechembe ndogo za kibakteria huishi baharini, ilikuwa rahisi kwa oksijeni kutokea baharini kupepea na kuenea katika anga ya dunia na kuzuiliwa hapo na nguvu asili ya uvutano ya dunia ili pia ibaki ikienea pote duniani.

    Mpaka wakati wa kuzuka duniani mimea na viumbe hai miaka takribani bilioni 3.5 iliyopita, tayari oksijeni ilikwa ni tele duniani; na hivyo kutumika kudumisha uhai wa viumbe hadi wakati huu.

    6. UKANDA WA 'OZONE'

    Muundo mwingie muhimu wa asili kwa dunia ni ukanda wa anga ujulikanao kwa jina la 'ozone' ambao umetanda kama 'mwavuli' kwenye anga ya dunia, na kuikinga isidhuriwe na mionzi hatari ya sumu kutoka kwenye Jua.

    Ukanda huo maarufu kama 'ozone layer' umetanda kuanzia usawa wa kilometa 15 kutoka ardhini kwenda juu angani mpaka ukomo wa kilomita takribani 50, ambapo huchuja asilimia kati ya 97 na 99 ya mionzi hatari kwenye miale ya joto la jua.

    Miongoni mwa matatizo yanayosababishwa na mionzi hiyo hatari kutoka kwenye jua, ni pamoja na magonjwa ya saratani ya ngozi kwa bianadamu.

    Pia juu ya ukanda wa tabaka la ozone kuna ukanda mwingine uitwao "atmosphere" ambao ni madhubuti kiasi kwamba vitu vinavyotoka anga za juu na kujaribu kuupenya ili kufika duniani, hukumbana na joto kali na kusambaratishwa kwa kuunguzwa.

    Si kwamba tabaka hilo lina joto, isipokuwa kasi ya "kuanguka" vitu hivyo kutoka juu angani kuja dunia husababisha msuguano na chembechembe za gesi katika eneo hilo na kuzalisha joto mithili ya ndimi za moto.

    Picha za video za vyombo vya 'Apollo' vikirejea duniani kutoka mwezini vikiwa na wanaanga ndani yake na kupenya tabaka hilo kwa kasi ya kilomita 39,000 kwa saa, huonekana kughubikwa na ndimi za moto wa rangi ya njano na bluu.

    Rangi hizo ni ishara ya ukali wa moto huo, lakini kutokana na waundaji wa vyombo hivyo kutumia mchanganyiko wa mabati na plastiki ngumu visivyopenywa na joto, Apollo huonekana kulichana tabaka hilo na kutokea upande wa pili ambao ni anga ya dunia.

    Hivyo basi, mfano huo mdogo unaonesha uimara wa tabaka hilo la 'ozone', ambalo kama ambavyo tumeona huchuja mionzi ya sumu kutoka kwenye mwanga wa jua ili kutolete madhara kwa viumbe duniani.

    Mwanga huo ukisafiri kutoka juani umbali wa kilomita milioni 150 kwa kasi ya kilomita 299,793, hutua duniani ndani ya dakika 8 na sekunde 19 ukiwa tayari umechujwa wakati ukipenya tabaka hilo.

    'Ozone' iligunduliwa mwaka 1913 na wanasayansi wawili wa nchini Ufaransa, Charlest Fabry na Henri Buisson, ambapo kipimo cha kasi ya mwanga kiligunduliwa na mwanasayansia wa anga za juu wa nchini Denmark, Ole Roemer, mwaka 1676.

    7. NGUVU ASILI YA UVUTANO

    Muundo mwingine wa dunia ni nguvu ya asili ya uvutano ya dunia, maarufu kama 'gravitation', ambayo huvuta vitu kuvirejesha chini duniani pale vinaporushwa kwenda juu au vile vinavyoanguka kutoka juu angani.

    Nguvu hiyo ina manufaa makubwa, kwani bila kuwepo duniani binadamu na viumbe wengine wangepeperuka kama karatasi kwenda juu wakati wakitembea juu ya ardhi ya hii.

    Kadhalika, nguvu hiyo husaidia kuvuta hewa ya oksijeni na kuiweka karibu na ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

    Pia, nguvu hiyo husaidia kuiweka dunia, mwezi, jua na sayari zingine katika uwiano wa umbali usio na madhara kutoka kila moja.

    Nguvu hiyo ya asili ndiyo huliweka joto la jua duniani na kubaki kuwa katika kiwango kinachotakiwa, na hivyo kuwezesha viumbe kupata joto la wastani na pia katika kiwango mwanana.

    Nguvu hiyo huvuta mvua kuja duniani na kuwezesha maji ya bahari, maziwa na mito kutulia duniani.

    Mathalani, bila nguvu asili hiyo kuwepo duniani, maji 'yangemwagika' kutoka duniani kwa kutawanyika kama upepo na kupaa kwenda juu angani na kutoweka kabisa.

    Na ndio maana ukirusha maji kwenda juu, hurudi chini ardhini.

    Hebu angalia mfano huu kwamba wanaanga waliokwenda mwenzini walilazimika kuvaa mavazi yenye uzito wa kilo 80 hapa duniani, lakini mavazi hayo kule mwezini yakawa na uzito wa kilo 3.

    Mavazi hayo, yaani viatu, koti, suruali, na kofia nzito yenye miwani maalumu ya kukinga macho dhidi ya mionzi hatari ya jua, vyote kwa pamoja viliunganishwa na kuwa mfano wa sare za 'ovaroli' za mafundi wa magari.

    Mavazi hayo pia mgongoni yakiwa yameunganishwa kwa pamoja na mtungi wa hewa ya oksijeni kwa ajili ya kupumua, yalivaaliwa mahsusi muda mfupi baada ya chombo kutua mwezini.

    Hivyo, msomaji wangu tafakari nini kilisababisha mavazi kuwa mazito hapa duniani, lakini yawe mepesi kule mwezini?

    Jibu ni kwamba nguvu asili ya uvutano hapa duniani ni kubwa kuliko ya kule mwezini.

    Na ndipo tunaona umuhimu wa muundo huo wa nguvu asili ya uvutano, ambapo hapa duniani huvuta vitu kuja chini kwa kasi ya mita 9.81 kwa sekunde, lakini kwa kuwa nguvu ya mwezi ni hafifu, huvuta vitu kwa kasi ndogo ya mita 1.62 kwa sekunde.

    Ingawa nguvu hiyo ya asili iligunduliwa kuwepo duniani miaka mingi iliyopta, mwanafizikia bingwa wa Uingereza, Sir Isaac Newton (1642-1727), ndiye anatambulika kama mgunduzi wa hesabu hizo za nguvu asili hiyo.

    Anaeleza kuwa vitu vyote vyenye maumbo asili, ikiwemo jua, sayari, dunia, mwezi, na vimondo, kila kimoja kina nguvu hiyo katika viwango tofauti.

    Kanuni hiyo, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wake, hueleza kuwa nguvu hiyo ndiyo hufanya jua kuvuta sayari zake ili kulizunguka, huku pia kila sayari ikitumia nguvu 'binafsi' (na kwa uwiano maalumu) kujihami isivutwe hadi kwenda kuligonga jua au kugongana na sayari zingine au vimondo.

    Nguvuasili ya jua ni mita 274 kwa sekunde, ikiwa ni zaidi ya kiasi cha nguvuasili ya kila sayari.

    Muundo huo wa kila sayari kujihami kivyake katika mstari wa njia yake hufahamika kisayansi kama "sayari kuhami mazingira ya njia yake"; yaani kwamba 'a planet has to clear the neighbourhood around its orbit.'

    Newton akiwa amezaliwa 'mtoto-njiti' na baadaye kuibuka kuwa mwenye akili nyingi kiasi cha kukaribia kuwa sawa na mtu wa miujiza, hakuwahi kuoa kutokana na kinachoelezwa kuwa ni " kutokana na kutingwa na shughuli za kimasomo."

    Huoneshwa kuwa muda mwingi alikuwa maabara akifanya tafiti mbalimbali za kisayansi, au akiwa maktaba akijisomea, ama akiandika kitabu, au akifundisha wanafunzi wake.

    Alikuwa bingwa mwenye kipaji cha taaluma nyingi, ikiwemo Fizikia, Kemia, Hisabati, Maarifa ya Anga za Juu, Uchumi, Falsafa, na Theolojia ambayo ni taaluma ya masuala ya kiroho.

    Kwa mujibu wa historia, mwanasayansi huyo gwiji wa kuigwa alihitimu shahada zake zote mbili za sayansi, yaani 'Bachelor' na 'Masters', mwaka 1665 na 1668 katika Chuo Kikuu cha Cambridge, nchini Uingereza.

    Akiwa na umri wa miaka 84, mwanasayansi huyo anayedhaniwa na wengi kuwa bingwa wa hesabu za kisayansi kuliko wote duniani, alifariki mwaka 1727 akiwa usingizini.

    Ripoti ya uchunguzi wa mwili wake huonesha kuwa alikuwa na tatizo la figo, lakini pia alikutwa na kiasi kingi cha zebaki.

    Zebaki hiyo, yamkini, ni kutokana na kudumu mno kwenye maabara za Kemia na Fizikia, ambazo hutumia kemikali aina mbalimbali, zikiwemo hewa za gesi, katika kufanya majaribio ya kisayansi.
    DUNIA NA MAAJABU YAKE (Muundo wa Dunia na Maajabu Yaliyomo) 1. UMRI WA DUNIA HII Dunia yetu ina historia ndefu mno tangu ilipojiunda angani, miaka takribani bilioni 4.5 iliyopita. Tarakimu za umri huo wa miaka bilioni 4.5 ni 4,500,000,000, yaani miaka milioni elfu nne na mia tano iliyopita. Dunia ambayo kwa lugha ya Kiingereza inafahamika vyema kwa jina la 'Earth', pia hujulikana kama 'the World', ikimaanishwa ulimwengu. Aidha, Dunia ni sayari pekee kwenye himaya ya sayari zilizopo chini ya jua ambayo jina lake halitokani na majina ya "Miungu wa Dola" ya Kigiriki au ya Kirumi. Asili ya jina la 'earth' ni 'erde' lenye asili ya nchini Ujerumani, na maana yake ni udongo au ardhi. Mpaka kuweza kupata umri huo wa dunia wanasayansi walifanya kazi ya kutafiti na kisha kuwasilisha matokeo yao kwenye makongamano ya kisayansi duniani, ambapo matokeo hayo yalijadiliwa kwa kina na hatimaye kukubalika kama hivi. Kumbuka katika majadiliano hayo huwepo mivutano mikali miongoni mwa wanasayansi waalikwa, ambapo pia jopo la wanasayansi wanaowasilisha utafiti husika hujikuta wakitakiwa kujibu hoja mbalimbali za wanasayansi wenzao. Kuna wakati baadhi ya matokeo ya tafiti kadhaa hukataliwa, huku watafiti husika wakitakiwa kurejea upya tafiti zao. Wanasayansi hupata umri wa sayari kwa kupima umri wa miamba ya sayari husika, ambapo mwamba wenye umri mkubwa zaidi kuliko miamba yote ndiyo huchukuliwa kuwa umri wa sayari husika. Itakumbukwa kuwa Msahafu wa Biblia (Sura ya Mwanzo 1) husimulia jinsi Mwenyezi Mungu alivyoumba "mbingu na nchi na vyote vilivyomo kwa siku 6," lakini pia Msahafu huohuo kwenye aya zingine hueleza kuwa miaka elfu moja ya duniani yaweza kuwa sawa na siku moja kwenye ya Makazi ya Mwenyezi Mungu. Ni dhahiri kuwa binadamu tukiwa hatuna hoja sahihi kwa maelezo ya aina hiyo, ndipo tunaona ni vyema mambo ya Mwenyezi Mungu kumwachia Yeye Mwenyewe Mwenyezi Mungu. 2. KUUMBIKA DUNIA, SAYARI, JUA, NYOTA Kimsingi, Dunia kama zilivyo sayari zingine zote ilijiunda kutokana na mabaki ya vitu vilivyotumika kuunda Jua. Jua ambalo ni nyota kama zilivyo nyota zote angani, lilijiunda lenyewe kwenye eneo la anga lijulikanalo kama 'Pillars of Creation' (nguzo za uumbaji) katika ukanda wa anga wenye upana ambao huonekana kutokuwa na mwisho. Ukanda huo ujulikanao kama 'Solar Nebula,' umegubikwa na mawingu ya vumbi la huko angani pamoja na aina mbalimbali za gesi na hewa, ikiwemo haidrojeni na heliumu. 'Solar' ni jina la nishati itokanayo na joto la jua, na 'Nebula' kwa lugha ya Kilatini ni "wingu" au vumbi la gesi asilia mithili ya ukungu. Hivyo, 'Solar Nebula' ni ukanda katika anga ya mbali wenye mawingu yaliyosheheni nishati yenye joto, sawa na nishati ya joto la jua. Sasa basi, tunafahamu vyema kuwa jua hutoa mionzi hatari yenye joto kali mithili ya moto mkali, na ambayo ikiboreshwa kisayansi pia huweza kutoa nishati ya umeme. Hivyo, kwa muktadha huo, hebu ngoja sasa tuleta pamoja hewa za gesi, zikiwemo haidrojeni na heliumu, mawingu yenye nishati ya umeme wa jua, vumbi la angani na tufani itokanayo na mchafuko mbaya wa hali ya hewa huko anga za mbali. Na ili kuweza kupata matokeo yanayotakiwa, hebu pia tutambue uwepo wa nguvu kubwa ya asili katika kiwango kijulikanacho kwa jina la "Supernatural Power", ambayo ndiyo huwa kisababishi cha mambo yote. Kisayansi, "Supernatural Power" ni nguvu kubwa ya asili ambayo huendesha mifumo mbalimbali ya asili, ambapo duniani nguvu hiyo hujulikana kama Nguvu ya Mungu. Nguvu asili hiyo, yaani Supernatural Power, husababisha tufani ambayo huvurumisha kwa pamoja vitu vyote hivyo, (gesi, hewa, mawingu yenye nishati ya joto na vumbi la angani) ili kuunda tufani yenye umbo la duara. Duara hiyo ni kama ile itokanayo na kimbunga kikali duniani, na ambacho sasa tutaona kikifungamanisha pamoja vitu vyote hivyo katika mchafuko mkubwa wa hali mbaya ya hewa. Natumia maneno ya msisitizo kuelezea "ukubwa" wa mchafuko huo wa hali ya hewa katika eneo hilo la anga, kwani katika kuunda sayari au nyota nguvuasili kubwa hutumika. Aidha, tufani hiyo ya duara itakayoanza kidogo kidogo kama kimbunga kikali, itazidi kukua hadi kuwa na kipenyo cha takribani kilomita 10 hadi 200 au zaidi na kwendelea. Tufani hiyo ndiyo itavurumisha kwa pamoja gesi na hewa za naitrojeni na heliumu, mawingu ya nishati ya joto na vumbi la angani (kama kifanyavyo kimbunga kikali katika eneo tambarare la duniani). Pia, wakati mchafuko huo wa hali mbaya ya hewa ukiendelea, hebu ngoja sisi watazamaji tujibanze mahali fulani kwa mbali kushuhudia duara hiyo ya tufani ikijizungusha yenyewe bila kukoma kwa kipindi cha miaka mingi. Kitakachofuata ni kuanza kuona kiini cha moto kikianza kujiunda katikati ya duara hiyo ya tufani kali, huku pia nje ya duara hiyo vitu kibao vikivutwa kujiunga na mzunguko wa hiyo tufani ya duara. Vitu hivyo ni pamoja na vumbi zaidi la angani, na gesi zaidi zenye joto kali. Wakati huohuo kipenyo na mzingo wa duara hiyo vitazidi kuongezeka upana na ukubwa, mfano wa duara yenye umbo sawa na la mpira mkubwa wa miguu. Hivyo, baada ya miaka takribani milioni moja tutashangaa kuona lile vumbi likigeuka taratibu kuwa miamba ya moto ndani ya kiini cha tufani hiyo ya duara. Miamba hiyo ni kutokana na lile vumbi la angani ambalo hatimaye limeshikamana pamoja mithili ya zege, na hatimaye kuwa miamba ndani ya tufani ya duara. Sanjari na kuundika huko ndani ya kitovu cha hiyo tufani ya duara, pia kwelekea nje ya duara hiyo utaundika udongo ambao ardhi, mchanga na mawe. Kimsingi, vitu hivyo pia ni matokeo ya lile vumbi la angani ambalo lilikusanywa pamoja na kuvutwa na kasi ya mzunguko wa tufani. Hatua hiyo mpya inatokana na kuwepo mshikamano na mgandamizo wa zile chembechembe za lile vumbivumbi ndani ya tufani. Vurumai hiyo ya mzunguko wa hiyo tufani ya duara yenye vumbi, itazidi kukua hadi kuunda sumaku ya asili ndani ya kile kitovu cha duara ya tufani. Kutokana na duara hiyo ya tufani kuongezeka ukubwa, hatimaye sumaku iliyopo kwenye kitovu cha duara hiyo itaishiwa nguvu ya kwendelea kunasa vumbi zaidi kuja kwenye mzingo wa hiyo duara ya tufani. Kumbuka kuwa wakati huo hiyo duara pia itaunda kimo kutoka kwenye usawa wa ardhi yake kwenda ndani kwenye kitovu chake, na hivyo kuwa duara ya mviringo kama umbo mfano wa mpira mchezo wa miguu. Baada ya kupita maelfu ya miaka mingi, duara hiyo ambayo hapo awali ilianza kama umbo la tufani na kuzidi kukua huko angani, sasa itakuwa na joto kali kupita kiasi na kuanza kung'aa kama jua. Jua hilo, ndiyo nyota mojawapo ya zile ambazo huonekana usiku ziking'aa angani. Lakini pia wakati wa kujiunda nyota hiyo, kama tulivyoona hapo awali, baadhi ya mabaki yake yaliyokuwa yakitawanyika angani wakati ile tufani ya duara ikijizungusha, huweza kujikusanya pamoja na kuunda sayari ambazo huzunguka baadhi ya hizo nyota. Hivyo ndivyo zilivyojiunda sayari zote ambazo huelea kwa kulizunguka jua letu. Mathalani, sayari zote ambazo hulizunguka jua, ikiwemo dunia zilijiunda kutokana na mabaki ya vitu kama gesi, michanga na mawe ambavyo vilitawanyika angani wakati jua likijiunda (kama ambavyo imeelezwa hapo awali). 3. KIINI CHA DUNIA Dunia yetu ambayo wastani wa nusu kipenyo cha umbo lake la duara ni kilomita 6,371, mzingo wake ni kilomita takribani 40,041. Kama zilivyo sayari zote katika himaya ya jua, dunia nayo ilijiunda wakati jua likijiunda lenyewe. Yaani kwamba sayari ni mabaki ya vitu vilivyotumika kuliunda jua. Kadhalika kama zilivyo sayari zingine zote, dunia nayo ina kiini chake ambacho kipo katikati ya ardhi yake. Kiini hicho kina nguvu kubwa ya sumaku ambayo, pamoja na mambo mengineyo, 'huvuta' umbo hilo la duara kutoka juu ya ardhi kwenda katikati ya kiini hicho. Muundo huo ndio hulifungamanisha pamoja umbo la duara la dunia, na hivyo kuzuia umbo hilo lisifumke kutoka ardhini na kusambaratika. Hiyo ni sawa na mpira wa miguu unavyoweza kupasuka na kusambaratika, kama utajazwa upepo kupita kiasi chake. Kiini hicho ambacho kipo katikati kabisa ya dunia, kinajulikanacho kwa jina la kisayansi la 'Inner Core.' Kiini hicho kina joto kali la sentigredi 6,230 ambacho ndio kiasi cha joto la jua. Kiini hicho kina umbo la duara lenye nusu kipenyo cha kilomita 1,250. Kama ingetokea kuchimba ardhi wima kwenda kwenye kiini hicho, mchimbaji angeanza kukutana na joto la kiini hicho kuanzia kimo cha umbali wa kilomita 5,150 kutoka usawa wa juu ya ardhi tunayotembea. Katika historia ya uchimbaji ardhi, kina kirefu kilichowahi kuchimbwa ardhini ni mita 12,345 (kilomita 12.345) huko Sakhalini, nchini Urusi, kwa ajili ya uvunaji wa mafuta ya petroli. Kiini cha dunia kinaundwa na madini mchanganyiko wa nikeli (nickle), chuma (iron) na dhahabu. Kwa mujibu wa utafiti, inakadiriwa kuwa kama dhahabu hiyo ingechimbwa na kuchomwa mpaka kuwa kimiminika sawa na uji na kisha kumwagwa chini, ingeweza kuifunika dunia yote kwa unene wa sentimeta 45. Kiini hicho muhimu kwa uhai wa sayari hii ya dunia kiligunduliwa mwaka 1936 na mtaalamu wa matetemeko ya ardhi wa nchini Denmark, mwanamama Dkt. Inge Lehmann. Dkt. Lehmann alihitimu shahada yake ya kwanza katika fani ya Hisabati mwaka 1910, ya Uzamili mwaka 1920 (zote kutoka Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini mwake), na ile ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza. Alifariki kwa uzee mwaka 1993 akiwa na umri wa miaka 104. 4. MAJI DUNIANI Kupatikana maji kwenye dunia yetu, ni mojawapo ya miundo ambayo haipo katika sayari zingine ambazo tuna taarifa za kitafiti kuzuhusu. Maji ni muhimili muhimu kwa ajili ya uhai wa viumbe wote na mimea, ambavyo kwa pamoja havipo katika sayari zingine za himaya ya jua. Kwa mujibu wa tafiti nyingi ambazo zimefanyika kwa miongo mingi ya miaka kujaribu kubaini nini chanzo cha kuwepo maji duniani, hakuna hata utafiti mmoja ulioonesha kwa usahihi matokeo ya kuridhisha. Miongoni mwa tafiti hizo ni pamoja na ule wa mwaka 2005, ambapo Mkuu wa Idara ya Masomo ya Sayari na Mwezi katika Chuo Kikuu cha Arizona nchini Marekani, Profesa Michael Julian Drake, na mwenzake ambaye ni mtaalamu wa Vimondo, Dkt. Huberto Campins, wa Chuo Kikuu cha Central Florida, walitafiti nini chanzo cha kuwepo maji duniani. Katika mawasilisho yao kwenye kongamano la kisayansi la Chama cha Wanataaluma wa Maarifa ya Anga za Juu (IAU), watafiti hao walikanusha madai ya uwezekano wa dunia hapo kale kugongwa na kimondo kikubwa na kusababisha maji kulipuka kutoka ardhini. Wakiwasilisha matokeo ya utafiti wao kwenye mkutano wa kongamano hilo, magwiji hao wa masuala ya sayari walieleza kwenye waraka wao uitwao "Origin of water on the terrestial planets" (chanzo cha kuwepo maji kwenye sayari). Walidai kuwa maji yaliyopo duniani yaliumbika kwenye ardhi ya dunia tangu mwanzo, wakati ikijiunda angani. Ikumbukwe kuwa eneo la uso wa dunia likiwa ni jumla ya kilomita za mraba milioni 510, asilimia 70.8 ya eneo hilo imefunikwa na maji na asilimia 29.2 ni nchi kavu, ikiwemo milima, mabonde na ardhi tambarare. 5. HEWA YA OKSIJENI Muundo mwingine muhimu katika sayari hii ya dunia ni hewa ambazo ni tawala, yaani Naitrojeni ambayo kwa usahihi imeenea kwa asilimia 78.08 ya hewa yote ya dunia, Oksijeni asilimia 20.95, 'Argon' asilimia 0.93, hewa ya Ukaa (Carbon dioxide) asilimia 0.039, na asilimia moja ni hewa mithili ya mvuke wa maji (water vapour). Hewa ya Oksijeni ambayo ni nguzo muhimu kwa ajili ya uhai wa viumbe wote na pia haipatikani kwenye sayari nyingine chini ya jua, inadhaniwa ilianza kupatikana duniani miaka takribani bilioni 2.5 iliyopita kufuatia "kukomaa kwa kiini cha dunia." Kwa mujibu wa matokeo ya tafiti mbalimbali na nadharia za kisayansi, inaoneshwa kuwa kukomaa kwa kiini hicho cha dunia hatimaye ndiko kulisababisha kuzuka duniani milipuko ya volikano ambayo pia ilisababisha kuzuka mabonde na milima. Inaoneshwa kuwa tayari wakati huo maji yaliishakuwepo duniani, na kuwezesha kuzuka chembechembe ndogo sana za kibakteria zijulikanazo kwa jina la kisayansi la 'cyanobacteria' au 'blue-green algae'. Kwa kutumia mwanga wa jua, maji na hewa ya ukaa, chembechembe hizo ziliweza kuzalisha hewa mbalimbali, ikiwemo 'Carbonhydrates' na Oksijeni. Kwa kuwa hizo chembechembe ndogo za kibakteria huishi baharini, ilikuwa rahisi kwa oksijeni kutokea baharini kupepea na kuenea katika anga ya dunia na kuzuiliwa hapo na nguvu asili ya uvutano ya dunia ili pia ibaki ikienea pote duniani. Mpaka wakati wa kuzuka duniani mimea na viumbe hai miaka takribani bilioni 3.5 iliyopita, tayari oksijeni ilikwa ni tele duniani; na hivyo kutumika kudumisha uhai wa viumbe hadi wakati huu. 6. UKANDA WA 'OZONE' Muundo mwingie muhimu wa asili kwa dunia ni ukanda wa anga ujulikanao kwa jina la 'ozone' ambao umetanda kama 'mwavuli' kwenye anga ya dunia, na kuikinga isidhuriwe na mionzi hatari ya sumu kutoka kwenye Jua. Ukanda huo maarufu kama 'ozone layer' umetanda kuanzia usawa wa kilometa 15 kutoka ardhini kwenda juu angani mpaka ukomo wa kilomita takribani 50, ambapo huchuja asilimia kati ya 97 na 99 ya mionzi hatari kwenye miale ya joto la jua. Miongoni mwa matatizo yanayosababishwa na mionzi hiyo hatari kutoka kwenye jua, ni pamoja na magonjwa ya saratani ya ngozi kwa bianadamu. Pia juu ya ukanda wa tabaka la ozone kuna ukanda mwingine uitwao "atmosphere" ambao ni madhubuti kiasi kwamba vitu vinavyotoka anga za juu na kujaribu kuupenya ili kufika duniani, hukumbana na joto kali na kusambaratishwa kwa kuunguzwa. Si kwamba tabaka hilo lina joto, isipokuwa kasi ya "kuanguka" vitu hivyo kutoka juu angani kuja dunia husababisha msuguano na chembechembe za gesi katika eneo hilo na kuzalisha joto mithili ya ndimi za moto. Picha za video za vyombo vya 'Apollo' vikirejea duniani kutoka mwezini vikiwa na wanaanga ndani yake na kupenya tabaka hilo kwa kasi ya kilomita 39,000 kwa saa, huonekana kughubikwa na ndimi za moto wa rangi ya njano na bluu. Rangi hizo ni ishara ya ukali wa moto huo, lakini kutokana na waundaji wa vyombo hivyo kutumia mchanganyiko wa mabati na plastiki ngumu visivyopenywa na joto, Apollo huonekana kulichana tabaka hilo na kutokea upande wa pili ambao ni anga ya dunia. Hivyo basi, mfano huo mdogo unaonesha uimara wa tabaka hilo la 'ozone', ambalo kama ambavyo tumeona huchuja mionzi ya sumu kutoka kwenye mwanga wa jua ili kutolete madhara kwa viumbe duniani. Mwanga huo ukisafiri kutoka juani umbali wa kilomita milioni 150 kwa kasi ya kilomita 299,793, hutua duniani ndani ya dakika 8 na sekunde 19 ukiwa tayari umechujwa wakati ukipenya tabaka hilo. 'Ozone' iligunduliwa mwaka 1913 na wanasayansi wawili wa nchini Ufaransa, Charlest Fabry na Henri Buisson, ambapo kipimo cha kasi ya mwanga kiligunduliwa na mwanasayansia wa anga za juu wa nchini Denmark, Ole Roemer, mwaka 1676. 7. NGUVU ASILI YA UVUTANO Muundo mwingine wa dunia ni nguvu ya asili ya uvutano ya dunia, maarufu kama 'gravitation', ambayo huvuta vitu kuvirejesha chini duniani pale vinaporushwa kwenda juu au vile vinavyoanguka kutoka juu angani. Nguvu hiyo ina manufaa makubwa, kwani bila kuwepo duniani binadamu na viumbe wengine wangepeperuka kama karatasi kwenda juu wakati wakitembea juu ya ardhi ya hii. Kadhalika, nguvu hiyo husaidia kuvuta hewa ya oksijeni na kuiweka karibu na ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Pia, nguvu hiyo husaidia kuiweka dunia, mwezi, jua na sayari zingine katika uwiano wa umbali usio na madhara kutoka kila moja. Nguvu hiyo ya asili ndiyo huliweka joto la jua duniani na kubaki kuwa katika kiwango kinachotakiwa, na hivyo kuwezesha viumbe kupata joto la wastani na pia katika kiwango mwanana. Nguvu hiyo huvuta mvua kuja duniani na kuwezesha maji ya bahari, maziwa na mito kutulia duniani. Mathalani, bila nguvu asili hiyo kuwepo duniani, maji 'yangemwagika' kutoka duniani kwa kutawanyika kama upepo na kupaa kwenda juu angani na kutoweka kabisa. Na ndio maana ukirusha maji kwenda juu, hurudi chini ardhini. Hebu angalia mfano huu kwamba wanaanga waliokwenda mwenzini walilazimika kuvaa mavazi yenye uzito wa kilo 80 hapa duniani, lakini mavazi hayo kule mwezini yakawa na uzito wa kilo 3. Mavazi hayo, yaani viatu, koti, suruali, na kofia nzito yenye miwani maalumu ya kukinga macho dhidi ya mionzi hatari ya jua, vyote kwa pamoja viliunganishwa na kuwa mfano wa sare za 'ovaroli' za mafundi wa magari. Mavazi hayo pia mgongoni yakiwa yameunganishwa kwa pamoja na mtungi wa hewa ya oksijeni kwa ajili ya kupumua, yalivaaliwa mahsusi muda mfupi baada ya chombo kutua mwezini. Hivyo, msomaji wangu tafakari nini kilisababisha mavazi kuwa mazito hapa duniani, lakini yawe mepesi kule mwezini? Jibu ni kwamba nguvu asili ya uvutano hapa duniani ni kubwa kuliko ya kule mwezini. Na ndipo tunaona umuhimu wa muundo huo wa nguvu asili ya uvutano, ambapo hapa duniani huvuta vitu kuja chini kwa kasi ya mita 9.81 kwa sekunde, lakini kwa kuwa nguvu ya mwezi ni hafifu, huvuta vitu kwa kasi ndogo ya mita 1.62 kwa sekunde. Ingawa nguvu hiyo ya asili iligunduliwa kuwepo duniani miaka mingi iliyopta, mwanafizikia bingwa wa Uingereza, Sir Isaac Newton (1642-1727), ndiye anatambulika kama mgunduzi wa hesabu hizo za nguvu asili hiyo. Anaeleza kuwa vitu vyote vyenye maumbo asili, ikiwemo jua, sayari, dunia, mwezi, na vimondo, kila kimoja kina nguvu hiyo katika viwango tofauti. Kanuni hiyo, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wake, hueleza kuwa nguvu hiyo ndiyo hufanya jua kuvuta sayari zake ili kulizunguka, huku pia kila sayari ikitumia nguvu 'binafsi' (na kwa uwiano maalumu) kujihami isivutwe hadi kwenda kuligonga jua au kugongana na sayari zingine au vimondo. Nguvuasili ya jua ni mita 274 kwa sekunde, ikiwa ni zaidi ya kiasi cha nguvuasili ya kila sayari. Muundo huo wa kila sayari kujihami kivyake katika mstari wa njia yake hufahamika kisayansi kama "sayari kuhami mazingira ya njia yake"; yaani kwamba 'a planet has to clear the neighbourhood around its orbit.' Newton akiwa amezaliwa 'mtoto-njiti' na baadaye kuibuka kuwa mwenye akili nyingi kiasi cha kukaribia kuwa sawa na mtu wa miujiza, hakuwahi kuoa kutokana na kinachoelezwa kuwa ni " kutokana na kutingwa na shughuli za kimasomo." Huoneshwa kuwa muda mwingi alikuwa maabara akifanya tafiti mbalimbali za kisayansi, au akiwa maktaba akijisomea, ama akiandika kitabu, au akifundisha wanafunzi wake. Alikuwa bingwa mwenye kipaji cha taaluma nyingi, ikiwemo Fizikia, Kemia, Hisabati, Maarifa ya Anga za Juu, Uchumi, Falsafa, na Theolojia ambayo ni taaluma ya masuala ya kiroho. Kwa mujibu wa historia, mwanasayansi huyo gwiji wa kuigwa alihitimu shahada zake zote mbili za sayansi, yaani 'Bachelor' na 'Masters', mwaka 1665 na 1668 katika Chuo Kikuu cha Cambridge, nchini Uingereza. Akiwa na umri wa miaka 84, mwanasayansi huyo anayedhaniwa na wengi kuwa bingwa wa hesabu za kisayansi kuliko wote duniani, alifariki mwaka 1727 akiwa usingizini. Ripoti ya uchunguzi wa mwili wake huonesha kuwa alikuwa na tatizo la figo, lakini pia alikutwa na kiasi kingi cha zebaki. Zebaki hiyo, yamkini, ni kutokana na kudumu mno kwenye maabara za Kemia na Fizikia, ambazo hutumia kemikali aina mbalimbali, zikiwemo hewa za gesi, katika kufanya majaribio ya kisayansi.
    0 Comments ·0 Shares ·1K Views
  • BAPHOMET: SANAMU LA SHETANI LILILOLETA UTATA NCHINI MAREKANI.

    Binadamu tangu zama za kale amekuwa akijenga, kuchonga na kuweka sanamu za aina nyingi kwa sababu mbalimbali.
    Baadhi hutumiwa kuwaenzi watu maarufu na kuwakumbuka, na nyingine huabudiwa kama miungu. Kwa muda mrefu hata hivyo imekuwa ni nadra kuona sanamu ambayo moja kwa moja inahusishwa na shetani au ibilisi. Lakini ukifika Marekani, mambo ni tofauti. Kuna sanamu moja kubwa ya shaba ambayo inahusishwa na ushetani. Ni sanamu ya, Baphomet ni kiumbe mwenye kichwa kinachofanana na cha mbuzi lakini ameongezwa maungo ya ajabu. Ni kiumbe mwenye mabawa, na kwenye sanamu hiyo inayotumiwa kwa sasa huoneshwa akiwa na watoto wawili wanaotabasamu.

    Sanamu inayotumiwa kwa sasa ina urefu wa karibu futi 9, na iligharimu $100,000 (£64,000) kuitengeneza. Sanamu hii imekuwa ikitumiwa kuwapiga vita wale walio na imani za Kikristo kiislamu na imani nyingine zenye kumcha Mungu mmoja. Ni sanamu hii ambayo imekuwa ikitumiwa kuendesha vita dhidi ya kuwekwa kwa sanamu za Kikristo na dini nyingine katika majengo maarufu, bustani na maeneo ya umma nchini Marekani. Agosti 17, sanamu hiyo ya kiumbe anayefahamika kama Baphomet ilipelekwa katika jimbo la Arkansas anakotoka Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton. Wanaotumia sanamu hiyo ni watu wa kundi linalofahamika kama Satanic Temple (Hekalu la Shetani) ambalo ni kundi la 'kidini' na kisiasa ambalo hupinga kuingizwa kwa dini katika masuala ya Serikali.

    Kundi hilo liliandaa maandamano ya watu 150 waliyojumuisha waabudu shetani, watu wasioamini Mungu yupo, na Wakristo pia.
    Maandamano hayo yalifanyika nje ya jengo lililo Makao Makuu ya jimbo la Arkansas katika mji wa Little Rock. Walikuwa wamekerwa na hatua ya kuweka sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu katika uwanja wa Makao Makuu hayo. Satanic Temple walisema sanamu hiyo inakiuka Sheria ya Kwanza ya Marekebisho ya Katiba nchini Marekani ambayo huzungumzia uhuru na haki za kidini. "Ikiwa utakubaliana na kuwepo kwa sanamu ya dini moja basi kunafaa kuwa na uhuru kwa wengine kuweka sanamu za kidini, na ukizuia basi kusiwe na sanamu yoyote ile," mwanzilishi mwenza wa tawi la Satanic Temple katika jimbo la Arkansas, Ivy Forrester, alinukuliwa na wanahabari siku hiyo ya maandamano.

    Ndoto yao ni kuwa na sanamu ya kudumu, lakini siku hiyo hawakuruhusiwa na sheria kuiweka kwa muda mrefu. Kuna sheria ya Arkansas ya mwaka 2017 inayohitaji sanamu ya kuwekwa maeneo ya Serikali iwe na udhamini wa Mbunge ambaye atawasilisha mswada iidhinishwe kupitia Bunge. Sanamu hiyo ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilidhaminiwa na mwanasiasa wa Republican, Seneta Jason Rapert. Hata hivyo, chini ya saa 24 baada ya kuwekwa, mwanamume mmoja alivurumisha gari na kuugonga mnara huo na kuubomoa. Maandamano ya Satanic Temple Arkansas yalisababisha kuandaliwa kwa maandamano mengine ya kuwapinga yaliyoandaliwa na makundi ya Kikristo na Wanachama wa Republican. Wakristo walikuwa wamebeba karatasi zilizokuwa na ujumbe kutoka kwenye Biblia. Satanic Temple waliwasilisha ombi la kushirikishwa kwenye kesi ya kupinga mnara huo wa Amri Kumi za Mungu iliyowasilishwa na shirika la haki za kiraia la American Civil Liberties Union, lakini kundi hilo limewasilisha ombi kutaka wasishirikishwe kwenye kesi hiyo.

    Sanamu hiyo ya Baphomet ilizinduliwa mara ya kwanza katika mji wa Detroit, Michigan. Mipango ya kuuweka nje ya Makao Makuu ya jimbo la Oklahoma ambapo kulikuwa kumewekwa mnara mwingine wa Amri Kumi za Mungu mwaka 2015. Mnara huo ulizinduliwa Julai 25 Mwaka huo, ambapo kupitia taarifa yao, Satanic temple walisema: "Tulichagua Baphomet kwa sababu ni kiumbe ambaye huhusishwa na Shetani na maana inayohusishwa naye inafaa sana akiwekwa kando na Sanamu inayowakilisha dini nyingine." Sherehe ya kuizindua ilikuwa ya faragha, na ukumbi uliotumiwa uliwekwa siri kubwa kwani Wakristo walikuwa wameandamana awali kuipinga mjini. Picha zilizopakiwa kwenye Facebook zilionyesha uzinduzi wake ulifanyika karibu na Mto wa Detroit. Kabla ya uzinduzi huo kufanyika, waumini takriban 200 walihudhuria ibada ya misa katika kanisa la St. Joseph mjini humo kupinga sanamu hiyo. Wengine 50 walifanya maombi mjini katika eneo ambalo awali Satanic Temple walikuwa wamepanga kuuzindulia mnara huo hapo.

    Mwanamume yule yule aliyeuharibu mnara wa Arkansas anadaiwa kufanya vivyo hivyo na kuubomoa mnara mwingine kama huo wa Amri Kumi za Mungu nje ya Makao Makuu ya jimbo la Oklahoma.
    Satanic Temple walisitisha juhudi zao za kutaka kuweka sanamu ya Baphomet huko baada ya Mahakama ya Juu ya Oklahoma kuamua kwamba Sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilikuwa imewekwa kinyume cha sheria, hivyo wakawa wameshinda vita bila kupigana. Mahakama ilisema ni kinyume cha sheria kutumia mali ya umma kwa manufaa ya dini yoyote ile.

    Jina hili Baphomet, asili yake ni enzi ya kukomesha uasi katika Kanisa Katoliki katika miaka ya 1100, kwa Kiingereza "Inquisition", na kuteswa kwa wapiganaji wa kidini kwa jina la "Knights Templar" waliokuwa wanateswa ili wafichue siri zao na wakubali kuifuata dini kwa mujibu wa viongozi wa kanisa wa wakati huo. Kwa mujibu wa waandishi wa enzi za vita vya kidini maarufu kama Crusade, wapiganaji hao walikiri kumuabudu Mungu wa wapagani kwa jina la Baphometh.

    Baadhi ya wasomi hata hivyo huamini kwamba "Baphometh" ni upotoshaji wa jina "Mahomet" - ambalo hutumiwa kumrejelea Nabii Muhammad, jambo linalozua utata zaidi. Lakini kadiri miaka ilivyosonga na mafumbo na siri kuhusu Utata wa Knights Templar kuzidi, ndivyo ufafanuzi wa neno hilo na maana yake ulivyozidi kutofautiana. Moja ya tafsiri ya neno hilo inapatikana katika kitabu cha "Da Vinci Code" cha ,Dan Brown, ambapo, neno Baphomet limefafanuliwa na kutafsiriwa kama "Sophia" au busara.

    Picha maarufu zaidi ya Baphomet ilichorwa na mzungu wa Ufaransa aitwaye , Eliphas Levi, mwaka 1856 katika kitabu chake cha Transcendental Magic: Its Doctrine and Ritual. Alichora kiumbe mwenye mabawa na mwenye pembe na mwenge ulio katikati ya pembe hizo kichwani. Kuna mchoro pia wa pembe nane kwenye paji la uso. Mikononi kumeandikwa maneno ya Kilatino SOLVE (tenganishwa) na COAGULA (fungamanisha) - ambazo ni nguvu za kuunganisha na kutenganisha ambazo zilitwaliwa kutoka kwa Mungu. Mchoro wa Levi ulihamasisha zaidi sanamu inayotumiwa na Satanic Temple.

    Ni jinsia mbili kwa pamoja, nusu mnyama na nusu binadamu.anapiga saluti ya vidole viwili Sanamu hiyo ina vidole viwili vilivyoelekezwa juu mkono wa kulia na viwili vinavyoelekezwa chini mkono wa kushoto, maana yake "kama ilivyo juu, na chini iwe pia". Maneno hayo na ishara hiyo ya vidole ni maarufu miongoni mwa wenye kuamini katika mizungu na mafumbo. Chanzo chake ni kazi za kale za msomi Hermes Trismegistus, ambaye vitabu vyake vilikuwa maarufu sana enzi ya Kipindi cha mwamko wa sanaa na mageuzi ya kidini, maarufu kama "Renaissance and Reformation" barani Ulaya. Maneno hayo pia hutumiwa kuhusiana na sayansi, vitu vyote na Mungu, lakini Levi aliandika kwamba kwa kutumia ishara hiyo, Baphomet wake alikuwa anaashiria kuwiana sawa kwa fadhila na haki. Lakini maana yake halisi ni kwamba ,shetani anatawala duniani na Mungu anatawala juu.

    Lucien Greaves, msemaji wa Satanic Temple anasema "lengo lao ni kwamba watoto watatazama kazi hiyo ya sanaa kama kwa usalama, ni sanamu isiyofaa kuzua wasiwasi wowote. "Sura ya mbuzi huyo haioneshi chochote. Si ya kishetani wala ya kutisha - kama wanavyodai baadhi ya watu - ukiitazama bila kuongozwa na mzigo wa utamaduni."
    "Sifikiri watoto wanaokutana na sanamu hii watatiwa hofu na propaganda wanaweza wasione chochote cha kuwatia wasiwasi," anasema Greaves. "Lakini si kwamba tunapinga kuwaingiza watoto kwenye mitazamo ya kidini. Mara nyingi watoto hulazimishwa kuingia kwenye dini. Hilo ni jambo hatutaki kulifanya kamwe."

    Kwenye tumbo la Baphomet kuna ishara ya kale ya Kigiriki ya nyoka wawili walio kwenye fimbo - fimbo ambayo ilibebwa na Hermes na maafisa wa kueneza matangazo au kutoa matangazo rasmi waliotumiwa kutoa matamko rasmi. Ishara hiyo kwenye sanamu hiyo inaashiria biashara, mashauriano na kutendeana, na iliingizwa kwenye Baphomet na Levi. "Kwetu ni ishara ya maridhiano ya vitu viwili tofauti - kwa mfano kuwa na sanamu ya Kishetani karibu na sanamu ya Kikristo," anasema Greaves. "Tunafikiri ni ujumbe wenye nguvu sana kuwa na sanamu hii ikiwa karibu na sanamu ya Amri Kumi za Mungu. Unaweza kuwa na mambo mawili tofauti kwa pamoja bila mzozo." Baphomet wa Levi alikuwa ni mwenye maziwa, lakini "tuliyaondoa maziwa hayo" anasema Greaves. Anasema hatukutaka wajipachike kwenye mdahalo kuhusu jinsia ya kiumbe huyo wao jambo ambalo lingewafanya watu kupoteza maana halisi. Badala yake anasema watoto wawili, mvulana na msichana, ndio wanaowakilisha jinsia. Kwa maana iliyojificha Greaves anashindwa kusema kwamba watoto hao wawili wa kike na kiume wanawakilisha ulimwengu wote na hawa ni Adam na Hawa,

    Kwenye paji la uso la Baphomet na kwenye kiti cha enzi alichokikalia kuna mchoro wa nyota ya pembe tano, ishara ambayo mara nyingi hutambuliwa kama ishara ya shetani. Mara nyingi huonekana ikiwa imepinduliwa. Msalaba wa Peter pia hupinduliwa. Greaves anasema lengo lao ni kuwafanya watu wabadilishe mtazamo wao na kuacha kuongozwa na waliyofunzwa na utamaduni wao. Waangazie mambo kwa kuzingatia ushahidi uliopo. Anasema mtazamo huo huwazuia watu kuchukua msimamo huru kuhusu masuala kama vile ndoa za wapenzi wa jinsia moja na haki za kutoa mimba pamoja na huduma nyingine za uzazi wa mpango. "Mwenge wa maarifa ndio kama upembe wa kati na inatukuza juhudi za kutafuta elimu na maarifa. Tunathamini hilo sana," anasema Greaves.

    Levi mwenyewe aliandika kwamba mwenge wa maarifa uolikuwa unawaka katikati ya pembe za Baphomet ni mwanga wa kusawazisha vitu vyote. Ni taswira ya roho iliyo juu ya vitu vyote vinavyoonekana, kama zilivyo ndimi za moto, ingawa bado imeunganishwa na vitu hivyo, mfano moto unavyoendelea kung'aa juu ya mafuta au kijiti. Kulikuwa na mpango wa kuongeza maandiko kwenye mchoro wa nyota ya pembe tano ya moja ya nguzo saba kuu za Satanic Temple: "moyo wa huruma, busara na haki unafaa daima kuongoza zaidi ya neno lililoandikwa au kutamkwa." Nyuma ya sanamu hiyo, kutakuwa na nukuu kutoka kwa kitabu cha Cain chake Lord Byron unaosema: "Kisha, nani alikuwa Ibilisi? Yule hangekuruhusu wewe uishi milele, au yule ambaye angelikuumba uishi milele, katika raha na nguvu za elimu na maarifa?"

    Kwa mujibu wa tovuti yao Satanic Temple wanaamini kwamba "kimsingi watu kuteseka au kuumia ni vibaya, na chochote kile kinachopunguza madhila na mateso ni kizuri." Hawaamini katika kutenda mabaya. Wanasema: "Huwa tunakumbatia kukufuru kama njia halali ya kujieleza na kuonyesha uhuru wa mtu binafsi dhidi ya imani za kitamaduni zisizo na tija." "Msimamo wa Satanic Temple ni kwamba dini inaweza, na inafaa kutenganishwa na ushirikina. Hivyo basi, huwa hawaendelezi imani katika Shetani binafsi. "Kukumbatia jina la Shetani ni kukumbatia mtazamo wa kutumia fikira na kujiondoa kutoka katika mfumo wa kuamini katika nguvu za kipekee za kutoka nje ya dunia na utamaduni uliopitwa na wakati wenye msingi wake katika ushirikina."
    BAPHOMET: SANAMU LA SHETANI LILILOLETA UTATA NCHINI MAREKANI. Binadamu tangu zama za kale amekuwa akijenga, kuchonga na kuweka sanamu za aina nyingi kwa sababu mbalimbali. Baadhi hutumiwa kuwaenzi watu maarufu na kuwakumbuka, na nyingine huabudiwa kama miungu. Kwa muda mrefu hata hivyo imekuwa ni nadra kuona sanamu ambayo moja kwa moja inahusishwa na shetani au ibilisi. Lakini ukifika Marekani, mambo ni tofauti. Kuna sanamu moja kubwa ya shaba ambayo inahusishwa na ushetani. Ni sanamu ya, Baphomet ni kiumbe mwenye kichwa kinachofanana na cha mbuzi lakini ameongezwa maungo ya ajabu. Ni kiumbe mwenye mabawa, na kwenye sanamu hiyo inayotumiwa kwa sasa huoneshwa akiwa na watoto wawili wanaotabasamu. Sanamu inayotumiwa kwa sasa ina urefu wa karibu futi 9, na iligharimu $100,000 (£64,000) kuitengeneza. Sanamu hii imekuwa ikitumiwa kuwapiga vita wale walio na imani za Kikristo kiislamu na imani nyingine zenye kumcha Mungu mmoja. Ni sanamu hii ambayo imekuwa ikitumiwa kuendesha vita dhidi ya kuwekwa kwa sanamu za Kikristo na dini nyingine katika majengo maarufu, bustani na maeneo ya umma nchini Marekani. Agosti 17, sanamu hiyo ya kiumbe anayefahamika kama Baphomet ilipelekwa katika jimbo la Arkansas anakotoka Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton. Wanaotumia sanamu hiyo ni watu wa kundi linalofahamika kama Satanic Temple (Hekalu la Shetani) ambalo ni kundi la 'kidini' na kisiasa ambalo hupinga kuingizwa kwa dini katika masuala ya Serikali. Kundi hilo liliandaa maandamano ya watu 150 waliyojumuisha waabudu shetani, watu wasioamini Mungu yupo, na Wakristo pia. Maandamano hayo yalifanyika nje ya jengo lililo Makao Makuu ya jimbo la Arkansas katika mji wa Little Rock. Walikuwa wamekerwa na hatua ya kuweka sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu katika uwanja wa Makao Makuu hayo. Satanic Temple walisema sanamu hiyo inakiuka Sheria ya Kwanza ya Marekebisho ya Katiba nchini Marekani ambayo huzungumzia uhuru na haki za kidini. "Ikiwa utakubaliana na kuwepo kwa sanamu ya dini moja basi kunafaa kuwa na uhuru kwa wengine kuweka sanamu za kidini, na ukizuia basi kusiwe na sanamu yoyote ile," mwanzilishi mwenza wa tawi la Satanic Temple katika jimbo la Arkansas, Ivy Forrester, alinukuliwa na wanahabari siku hiyo ya maandamano. Ndoto yao ni kuwa na sanamu ya kudumu, lakini siku hiyo hawakuruhusiwa na sheria kuiweka kwa muda mrefu. Kuna sheria ya Arkansas ya mwaka 2017 inayohitaji sanamu ya kuwekwa maeneo ya Serikali iwe na udhamini wa Mbunge ambaye atawasilisha mswada iidhinishwe kupitia Bunge. Sanamu hiyo ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilidhaminiwa na mwanasiasa wa Republican, Seneta Jason Rapert. Hata hivyo, chini ya saa 24 baada ya kuwekwa, mwanamume mmoja alivurumisha gari na kuugonga mnara huo na kuubomoa. Maandamano ya Satanic Temple Arkansas yalisababisha kuandaliwa kwa maandamano mengine ya kuwapinga yaliyoandaliwa na makundi ya Kikristo na Wanachama wa Republican. Wakristo walikuwa wamebeba karatasi zilizokuwa na ujumbe kutoka kwenye Biblia. Satanic Temple waliwasilisha ombi la kushirikishwa kwenye kesi ya kupinga mnara huo wa Amri Kumi za Mungu iliyowasilishwa na shirika la haki za kiraia la American Civil Liberties Union, lakini kundi hilo limewasilisha ombi kutaka wasishirikishwe kwenye kesi hiyo. Sanamu hiyo ya Baphomet ilizinduliwa mara ya kwanza katika mji wa Detroit, Michigan. Mipango ya kuuweka nje ya Makao Makuu ya jimbo la Oklahoma ambapo kulikuwa kumewekwa mnara mwingine wa Amri Kumi za Mungu mwaka 2015. Mnara huo ulizinduliwa Julai 25 Mwaka huo, ambapo kupitia taarifa yao, Satanic temple walisema: "Tulichagua Baphomet kwa sababu ni kiumbe ambaye huhusishwa na Shetani na maana inayohusishwa naye inafaa sana akiwekwa kando na Sanamu inayowakilisha dini nyingine." Sherehe ya kuizindua ilikuwa ya faragha, na ukumbi uliotumiwa uliwekwa siri kubwa kwani Wakristo walikuwa wameandamana awali kuipinga mjini. Picha zilizopakiwa kwenye Facebook zilionyesha uzinduzi wake ulifanyika karibu na Mto wa Detroit. Kabla ya uzinduzi huo kufanyika, waumini takriban 200 walihudhuria ibada ya misa katika kanisa la St. Joseph mjini humo kupinga sanamu hiyo. Wengine 50 walifanya maombi mjini katika eneo ambalo awali Satanic Temple walikuwa wamepanga kuuzindulia mnara huo hapo. Mwanamume yule yule aliyeuharibu mnara wa Arkansas anadaiwa kufanya vivyo hivyo na kuubomoa mnara mwingine kama huo wa Amri Kumi za Mungu nje ya Makao Makuu ya jimbo la Oklahoma. Satanic Temple walisitisha juhudi zao za kutaka kuweka sanamu ya Baphomet huko baada ya Mahakama ya Juu ya Oklahoma kuamua kwamba Sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilikuwa imewekwa kinyume cha sheria, hivyo wakawa wameshinda vita bila kupigana. Mahakama ilisema ni kinyume cha sheria kutumia mali ya umma kwa manufaa ya dini yoyote ile. Jina hili Baphomet, asili yake ni enzi ya kukomesha uasi katika Kanisa Katoliki katika miaka ya 1100, kwa Kiingereza "Inquisition", na kuteswa kwa wapiganaji wa kidini kwa jina la "Knights Templar" waliokuwa wanateswa ili wafichue siri zao na wakubali kuifuata dini kwa mujibu wa viongozi wa kanisa wa wakati huo. Kwa mujibu wa waandishi wa enzi za vita vya kidini maarufu kama Crusade, wapiganaji hao walikiri kumuabudu Mungu wa wapagani kwa jina la Baphometh. Baadhi ya wasomi hata hivyo huamini kwamba "Baphometh" ni upotoshaji wa jina "Mahomet" - ambalo hutumiwa kumrejelea Nabii Muhammad, jambo linalozua utata zaidi. Lakini kadiri miaka ilivyosonga na mafumbo na siri kuhusu Utata wa Knights Templar kuzidi, ndivyo ufafanuzi wa neno hilo na maana yake ulivyozidi kutofautiana. Moja ya tafsiri ya neno hilo inapatikana katika kitabu cha "Da Vinci Code" cha ,Dan Brown, ambapo, neno Baphomet limefafanuliwa na kutafsiriwa kama "Sophia" au busara. Picha maarufu zaidi ya Baphomet ilichorwa na mzungu wa Ufaransa aitwaye , Eliphas Levi, mwaka 1856 katika kitabu chake cha Transcendental Magic: Its Doctrine and Ritual. Alichora kiumbe mwenye mabawa na mwenye pembe na mwenge ulio katikati ya pembe hizo kichwani. Kuna mchoro pia wa pembe nane kwenye paji la uso. Mikononi kumeandikwa maneno ya Kilatino SOLVE (tenganishwa) na COAGULA (fungamanisha) - ambazo ni nguvu za kuunganisha na kutenganisha ambazo zilitwaliwa kutoka kwa Mungu. Mchoro wa Levi ulihamasisha zaidi sanamu inayotumiwa na Satanic Temple. Ni jinsia mbili kwa pamoja, nusu mnyama na nusu binadamu.anapiga saluti ya vidole viwili Sanamu hiyo ina vidole viwili vilivyoelekezwa juu mkono wa kulia na viwili vinavyoelekezwa chini mkono wa kushoto, maana yake "kama ilivyo juu, na chini iwe pia". Maneno hayo na ishara hiyo ya vidole ni maarufu miongoni mwa wenye kuamini katika mizungu na mafumbo. Chanzo chake ni kazi za kale za msomi Hermes Trismegistus, ambaye vitabu vyake vilikuwa maarufu sana enzi ya Kipindi cha mwamko wa sanaa na mageuzi ya kidini, maarufu kama "Renaissance and Reformation" barani Ulaya. Maneno hayo pia hutumiwa kuhusiana na sayansi, vitu vyote na Mungu, lakini Levi aliandika kwamba kwa kutumia ishara hiyo, Baphomet wake alikuwa anaashiria kuwiana sawa kwa fadhila na haki. Lakini maana yake halisi ni kwamba ,shetani anatawala duniani na Mungu anatawala juu. Lucien Greaves, msemaji wa Satanic Temple anasema "lengo lao ni kwamba watoto watatazama kazi hiyo ya sanaa kama kwa usalama, ni sanamu isiyofaa kuzua wasiwasi wowote. "Sura ya mbuzi huyo haioneshi chochote. Si ya kishetani wala ya kutisha - kama wanavyodai baadhi ya watu - ukiitazama bila kuongozwa na mzigo wa utamaduni." "Sifikiri watoto wanaokutana na sanamu hii watatiwa hofu na propaganda wanaweza wasione chochote cha kuwatia wasiwasi," anasema Greaves. "Lakini si kwamba tunapinga kuwaingiza watoto kwenye mitazamo ya kidini. Mara nyingi watoto hulazimishwa kuingia kwenye dini. Hilo ni jambo hatutaki kulifanya kamwe." Kwenye tumbo la Baphomet kuna ishara ya kale ya Kigiriki ya nyoka wawili walio kwenye fimbo - fimbo ambayo ilibebwa na Hermes na maafisa wa kueneza matangazo au kutoa matangazo rasmi waliotumiwa kutoa matamko rasmi. Ishara hiyo kwenye sanamu hiyo inaashiria biashara, mashauriano na kutendeana, na iliingizwa kwenye Baphomet na Levi. "Kwetu ni ishara ya maridhiano ya vitu viwili tofauti - kwa mfano kuwa na sanamu ya Kishetani karibu na sanamu ya Kikristo," anasema Greaves. "Tunafikiri ni ujumbe wenye nguvu sana kuwa na sanamu hii ikiwa karibu na sanamu ya Amri Kumi za Mungu. Unaweza kuwa na mambo mawili tofauti kwa pamoja bila mzozo." Baphomet wa Levi alikuwa ni mwenye maziwa, lakini "tuliyaondoa maziwa hayo" anasema Greaves. Anasema hatukutaka wajipachike kwenye mdahalo kuhusu jinsia ya kiumbe huyo wao jambo ambalo lingewafanya watu kupoteza maana halisi. Badala yake anasema watoto wawili, mvulana na msichana, ndio wanaowakilisha jinsia. Kwa maana iliyojificha Greaves anashindwa kusema kwamba watoto hao wawili wa kike na kiume wanawakilisha ulimwengu wote na hawa ni Adam na Hawa, Kwenye paji la uso la Baphomet na kwenye kiti cha enzi alichokikalia kuna mchoro wa nyota ya pembe tano, ishara ambayo mara nyingi hutambuliwa kama ishara ya shetani. Mara nyingi huonekana ikiwa imepinduliwa. Msalaba wa Peter pia hupinduliwa. Greaves anasema lengo lao ni kuwafanya watu wabadilishe mtazamo wao na kuacha kuongozwa na waliyofunzwa na utamaduni wao. Waangazie mambo kwa kuzingatia ushahidi uliopo. Anasema mtazamo huo huwazuia watu kuchukua msimamo huru kuhusu masuala kama vile ndoa za wapenzi wa jinsia moja na haki za kutoa mimba pamoja na huduma nyingine za uzazi wa mpango. "Mwenge wa maarifa ndio kama upembe wa kati na inatukuza juhudi za kutafuta elimu na maarifa. Tunathamini hilo sana," anasema Greaves. Levi mwenyewe aliandika kwamba mwenge wa maarifa uolikuwa unawaka katikati ya pembe za Baphomet ni mwanga wa kusawazisha vitu vyote. Ni taswira ya roho iliyo juu ya vitu vyote vinavyoonekana, kama zilivyo ndimi za moto, ingawa bado imeunganishwa na vitu hivyo, mfano moto unavyoendelea kung'aa juu ya mafuta au kijiti. Kulikuwa na mpango wa kuongeza maandiko kwenye mchoro wa nyota ya pembe tano ya moja ya nguzo saba kuu za Satanic Temple: "moyo wa huruma, busara na haki unafaa daima kuongoza zaidi ya neno lililoandikwa au kutamkwa." Nyuma ya sanamu hiyo, kutakuwa na nukuu kutoka kwa kitabu cha Cain chake Lord Byron unaosema: "Kisha, nani alikuwa Ibilisi? Yule hangekuruhusu wewe uishi milele, au yule ambaye angelikuumba uishi milele, katika raha na nguvu za elimu na maarifa?" Kwa mujibu wa tovuti yao Satanic Temple wanaamini kwamba "kimsingi watu kuteseka au kuumia ni vibaya, na chochote kile kinachopunguza madhila na mateso ni kizuri." Hawaamini katika kutenda mabaya. Wanasema: "Huwa tunakumbatia kukufuru kama njia halali ya kujieleza na kuonyesha uhuru wa mtu binafsi dhidi ya imani za kitamaduni zisizo na tija." "Msimamo wa Satanic Temple ni kwamba dini inaweza, na inafaa kutenganishwa na ushirikina. Hivyo basi, huwa hawaendelezi imani katika Shetani binafsi. "Kukumbatia jina la Shetani ni kukumbatia mtazamo wa kutumia fikira na kujiondoa kutoka katika mfumo wa kuamini katika nguvu za kipekee za kutoka nje ya dunia na utamaduni uliopitwa na wakati wenye msingi wake katika ushirikina."
    0 Comments ·0 Shares ·912 Views
  • JE UNAKIJUA CHUMBA MAARUFU NAMBA 39?...

    ROOM 39.....

    NIlipokuwa nikisoma kuhusu dada yake kiongozi wa Korea Kaskazini aitwae Kim Yo-jong nikapata kidogo ufahamu wa chumba kiitwacho Room 39 ambacho inasadikiwa kuwa mume wake dada huyo aitwae Chong Ryong-hae anafanya kazi ndani ya chumba hicho.

    Chumba hiki kina majina mengi kadhaa kama vile Bureau au Kitengo, Division au sehemu au pia Office 39.

    Chumba hiki kipo ndani ya jengo la chama cha wafanyakazi wa Korea kaskazini jengo ambalo halipo mbali na makazi rasmi ya kiongozi wa Korea Kaskazini bwana Kim Jong-un.

    Lakini kiukweli hiki ni kitengo maalum cha kijasusi ambacho kinafanya kazi zake ndani ya chama cha wafanyakazi wa Korea Kaskazni ambacho kina jukumu moja tu, kuhakikisha viongozi wa Korea Kaskazini wana fedha za kigeni za matumizi wakiwa nje ya nchi hiyo.

    Room 39 kipo chini ya usimamizi wa kamati kuu ya chama hicho lakini upande wa kamati ya kijeshi ambayo ina majukumu ya kupitisha matumizi ya fedha kwa jeshi kwenye ununuzi wa silaha na usimamzi wa maliasili za nchi hiyo madini yakiwemo.

    Inakisiwa kuwa kitengo hicho kinaingiza kati ya dola milioni 500 hadi bilioni 1 au zaidi kwa mwaka, na fedha hizo ni kutokana na biashara za aina zote tunazozifahamu duniani zikiwemo halali na haramu.

    Ukiangalia kazi za kitengo hiki waweza kukifananisha kwa mbali na jeshi maalum la Iran la IRGC ambalo pia linajitegemea na linahisiwa kuingiza kiasi cha dola hadi bilioni 12 kwa mwaka zinatotokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi.

    Tofauti iliyopo kidogo ni kwamba Chumba 39 au Room 39 kimejikita zaidi kwenye ujasusi wa nje ya Korea Kaskazini na kinaratibu ofisi na makampuni mbalimbali ndani na nje ya Korea Kaskazini huku wakibadilisha majina mara kwa mara.

    Mfano wa makampuni mbalimbali yanayoendesha shughuli zake nje ya Korea Kaskazini ni migahawa iitwayo Pyongyang ambayo ipo sehemu mbalimbali duniani.

    Kampuni ingine ni ile ya KNIC ambayo inashughulika na masuala ya bima na ina ofisi katika miji ya Hamburg nchini Ujerumani na London nchini Uingereza. Mwaka 2015 umoja wa Ulaya uliwahi kuifungia kampuni hii kutokana na kujishughulisha na biashara haramu na bima bandia na kujipatia fedha kutokana na kudai bima hewa.

    Chumba 39 kilianzishwa kwenye miaka ya 70 na Kim II Sung ambae ni babu yake Kim Jong-un na kukabidhiwa majukumu ya kuhakikisha utawala wa Korea kaskazini huishiwi fedha za kujiendesha pamoja na usimamizi wa uchumi wa nchi hiyo.

    Mahali kilipoanzia shughuli zake ni chumba kilichoitwa Office 39 na baadae kubatiza chumba hichi jina la Room 39 kikiwa nyuma ya chumba kingine kiitwacho room 36 ambacho kazi yake kubwa ni kusimamia fedha za utawala wa Korea Kakazini.

    Chumba hiki kina shughuli nyingi na kimesheheni majasusi wenye taaluma zote muhimu wakiwemo wakemia ambao hudaiwa kutengeneza madawa mbalimbali na kuyauza nchini China, Japan na sehemu zingine barani Asia.

    Pia majasusi wakemia wa chumba 39 wanasadikiwa kutengeneza dawa za kuongeza nguvu za kiume maarufu kama Viagra zenye vimelea mbalimbali kwenye viwanda vyake vilivyoko sehemu iitwayo Chonglin na kuuza kwenye nchi za Hong Kong, China na Mashariki ya kati.

    Kitengo hiki pia kina wataalam wa masuala ya fedha na watengenezaji noti bandia ziitwazo "Supernotes" ambazo huonekana kama fedha halali kwa matumizi na huwa na thamani ya hadi dola milioni 100.

    Kitengo hiki cha kipekee pia hutengeneza bidhaa ambazo baadae huwekwa nembo ya bidhaa za China na kupitishwa na kufanikiwa kufika kwenye masoko ya kimataifa kwenye nchi kama za Ufaransa, Italia na Korea Kusini.

    Bidhaa hizo ni pamoja na Eyelashes (kalamu ya urembo wa kope za macho), vifaa vya muziki na sigara ambavyo kwa pamoja vinasadikiwa kuiingizia nchi hiyo dola milioni 120 kwa mwaka.

    Kwa upande wa mauzo ya silaha nchi hiyo iliwekewa vikwazo kwenye uuzajiw a silaha zake lakini chumba namba 39 kikafanikwia na mwaka 2014 silaha za Korea kaskazini ziliuzwa kwa kutumia makampuni yake yenye majna halali kwa nchi za Syria, Myanmar, Eritrea, Tanzania, Ethiopia, Somalia na Iran.

    Kitengo hiki pia mwaka 2016 kwa kutumia majasusi wake wataalam wa teknolojia walifanikiwa kudukua hazina ya New York iitwayo Federal Reserve na kuchukua kiasi cha dola bilioni 1.

    Majasusi wa Marekani walipokuwa wakifuatilia wizi huo walikuja kugundua kasoro ya maandishi kwenye makaratasi ya kuombea kufanya mialama na ndipo walipogundua kasoro kwenye neno Foundation lililoandikwa "fandation" ndipo walipobaini kuwa wakorea kaskazini ndio walofanya uharibifu.

    Itakumbukwa kuwa mwaka huohuo wa 2016 ndio mwaka ambao kulitokea kirusi cha kompyuta cha "Wannacry" ambacho kilivamia mifumo mbalimbali ya kompyuta duniani.

    Pia majasusi hao wa Room 39 waliweza kuingiza kwenye mifumo ya ulinzi wa anga ya Korea Kusini na kufanikiwa kuiba ndege za kivita na kisha kuzirusha na kuzitua salama nchini Korea Kaskazini na zisipatikane hadi leo.

    Nchi nyingi zilizoendelea kwa sasa zimeamua kuwekeza kwenye utaalam wa masuala ya mitandao uitwao Cyber Security kwani inasadikiwa kuwa chumba namba 39 kina majasusi wengi walopikwa tayari kushambulia nchi yoyote ile duniani.

    Ama hakika chumba hiki kiitwacho Room 39 ni chumba hatari kuwahi kutokea duniani na hivi karibuni na kuendelea tuzidi kusikiliza kauli zinazotoka kwa utawala wa PyongYang khasa dada yake Kim Jong-un aitwae Kim Yo-jong ambae kiufundi anaonekana ndie kamanda wa Room 39.

    Hii inaweza kumfanya aonekane kuwa ni mwanamke hatari zaidi kuwahi kutokea duniani.

    NB: Ombi kwa MOds msiuunganishe uzi huu.

    Karibu.
    JE UNAKIJUA CHUMBA MAARUFU NAMBA 39?... ROOM 39..... NIlipokuwa nikisoma kuhusu dada yake kiongozi wa Korea Kaskazini aitwae Kim Yo-jong nikapata kidogo ufahamu wa chumba kiitwacho Room 39 ambacho inasadikiwa kuwa mume wake dada huyo aitwae Chong Ryong-hae anafanya kazi ndani ya chumba hicho. Chumba hiki kina majina mengi kadhaa kama vile Bureau au Kitengo, Division au sehemu au pia Office 39. Chumba hiki kipo ndani ya jengo la chama cha wafanyakazi wa Korea kaskazini jengo ambalo halipo mbali na makazi rasmi ya kiongozi wa Korea Kaskazini bwana Kim Jong-un. Lakini kiukweli hiki ni kitengo maalum cha kijasusi ambacho kinafanya kazi zake ndani ya chama cha wafanyakazi wa Korea Kaskazni ambacho kina jukumu moja tu, kuhakikisha viongozi wa Korea Kaskazini wana fedha za kigeni za matumizi wakiwa nje ya nchi hiyo. Room 39 kipo chini ya usimamizi wa kamati kuu ya chama hicho lakini upande wa kamati ya kijeshi ambayo ina majukumu ya kupitisha matumizi ya fedha kwa jeshi kwenye ununuzi wa silaha na usimamzi wa maliasili za nchi hiyo madini yakiwemo. Inakisiwa kuwa kitengo hicho kinaingiza kati ya dola milioni 500 hadi bilioni 1 au zaidi kwa mwaka, na fedha hizo ni kutokana na biashara za aina zote tunazozifahamu duniani zikiwemo halali na haramu. Ukiangalia kazi za kitengo hiki waweza kukifananisha kwa mbali na jeshi maalum la Iran la IRGC ambalo pia linajitegemea na linahisiwa kuingiza kiasi cha dola hadi bilioni 12 kwa mwaka zinatotokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi. Tofauti iliyopo kidogo ni kwamba Chumba 39 au Room 39 kimejikita zaidi kwenye ujasusi wa nje ya Korea Kaskazini na kinaratibu ofisi na makampuni mbalimbali ndani na nje ya Korea Kaskazini huku wakibadilisha majina mara kwa mara. Mfano wa makampuni mbalimbali yanayoendesha shughuli zake nje ya Korea Kaskazini ni migahawa iitwayo Pyongyang ambayo ipo sehemu mbalimbali duniani. Kampuni ingine ni ile ya KNIC ambayo inashughulika na masuala ya bima na ina ofisi katika miji ya Hamburg nchini Ujerumani na London nchini Uingereza. Mwaka 2015 umoja wa Ulaya uliwahi kuifungia kampuni hii kutokana na kujishughulisha na biashara haramu na bima bandia na kujipatia fedha kutokana na kudai bima hewa. Chumba 39 kilianzishwa kwenye miaka ya 70 na Kim II Sung ambae ni babu yake Kim Jong-un na kukabidhiwa majukumu ya kuhakikisha utawala wa Korea kaskazini huishiwi fedha za kujiendesha pamoja na usimamizi wa uchumi wa nchi hiyo. Mahali kilipoanzia shughuli zake ni chumba kilichoitwa Office 39 na baadae kubatiza chumba hichi jina la Room 39 kikiwa nyuma ya chumba kingine kiitwacho room 36 ambacho kazi yake kubwa ni kusimamia fedha za utawala wa Korea Kakazini. Chumba hiki kina shughuli nyingi na kimesheheni majasusi wenye taaluma zote muhimu wakiwemo wakemia ambao hudaiwa kutengeneza madawa mbalimbali na kuyauza nchini China, Japan na sehemu zingine barani Asia. Pia majasusi wakemia wa chumba 39 wanasadikiwa kutengeneza dawa za kuongeza nguvu za kiume maarufu kama Viagra zenye vimelea mbalimbali kwenye viwanda vyake vilivyoko sehemu iitwayo Chonglin na kuuza kwenye nchi za Hong Kong, China na Mashariki ya kati. Kitengo hiki pia kina wataalam wa masuala ya fedha na watengenezaji noti bandia ziitwazo "Supernotes" ambazo huonekana kama fedha halali kwa matumizi na huwa na thamani ya hadi dola milioni 100. Kitengo hiki cha kipekee pia hutengeneza bidhaa ambazo baadae huwekwa nembo ya bidhaa za China na kupitishwa na kufanikiwa kufika kwenye masoko ya kimataifa kwenye nchi kama za Ufaransa, Italia na Korea Kusini. Bidhaa hizo ni pamoja na Eyelashes (kalamu ya urembo wa kope za macho), vifaa vya muziki na sigara ambavyo kwa pamoja vinasadikiwa kuiingizia nchi hiyo dola milioni 120 kwa mwaka. Kwa upande wa mauzo ya silaha nchi hiyo iliwekewa vikwazo kwenye uuzajiw a silaha zake lakini chumba namba 39 kikafanikwia na mwaka 2014 silaha za Korea kaskazini ziliuzwa kwa kutumia makampuni yake yenye majna halali kwa nchi za Syria, Myanmar, Eritrea, Tanzania, Ethiopia, Somalia na Iran. Kitengo hiki pia mwaka 2016 kwa kutumia majasusi wake wataalam wa teknolojia walifanikiwa kudukua hazina ya New York iitwayo Federal Reserve na kuchukua kiasi cha dola bilioni 1. Majasusi wa Marekani walipokuwa wakifuatilia wizi huo walikuja kugundua kasoro ya maandishi kwenye makaratasi ya kuombea kufanya mialama na ndipo walipogundua kasoro kwenye neno Foundation lililoandikwa "fandation" ndipo walipobaini kuwa wakorea kaskazini ndio walofanya uharibifu. Itakumbukwa kuwa mwaka huohuo wa 2016 ndio mwaka ambao kulitokea kirusi cha kompyuta cha "Wannacry" ambacho kilivamia mifumo mbalimbali ya kompyuta duniani. Pia majasusi hao wa Room 39 waliweza kuingiza kwenye mifumo ya ulinzi wa anga ya Korea Kusini na kufanikiwa kuiba ndege za kivita na kisha kuzirusha na kuzitua salama nchini Korea Kaskazini na zisipatikane hadi leo. Nchi nyingi zilizoendelea kwa sasa zimeamua kuwekeza kwenye utaalam wa masuala ya mitandao uitwao Cyber Security kwani inasadikiwa kuwa chumba namba 39 kina majasusi wengi walopikwa tayari kushambulia nchi yoyote ile duniani. Ama hakika chumba hiki kiitwacho Room 39 ni chumba hatari kuwahi kutokea duniani na hivi karibuni na kuendelea tuzidi kusikiliza kauli zinazotoka kwa utawala wa PyongYang khasa dada yake Kim Jong-un aitwae Kim Yo-jong ambae kiufundi anaonekana ndie kamanda wa Room 39. Hii inaweza kumfanya aonekane kuwa ni mwanamke hatari zaidi kuwahi kutokea duniani. NB: Ombi kwa MOds msiuunganishe uzi huu. Karibu.
    0 Comments ·0 Shares ·805 Views
  • .KUTOKA KWENYE UKURASA WA MWANDISHI MICKJR TANZANIA HUENDA IKAONDOLEWA KWENYE AFCON 2025

    Hiki ndicho kilichotokea na sababu kwa nini Tanzania inaweza kuondolewa katika michuano ya AFCON 2025 nchini Morocco baada ya kufuzu.

    Dakika ya 73, Tanzania ilifanya mabadiliko na kumuingiza mchezaji aliyevaa jezi namba 26 Ibrahim Amme lakini kwenye karatasi ya timu waliyoiwasilisha CAF, hakuna mchezaji aliyesajiliwa na jezi namba 26.

    Ibarahim Amme alisajiliwa kwa jezi namba 24

    Hii inakiuka kanuni za CAF kuhusu utambulisho wa wachezaji.

    Guinea imewasilisha rasmi ripoti kwa CAF.

    Je unamaoni Gani kuhusu Hili swala ??
    .🚨KUTOKA KWENYE UKURASA WA MWANDISHI MICKJR TANZANIA HUENDA IKAONDOLEWA KWENYE AFCON 2025 Hiki ndicho kilichotokea na sababu kwa nini Tanzania inaweza kuondolewa katika michuano ya AFCON 2025 nchini Morocco baada ya kufuzu. 🚨🇹🇿 Dakika ya 73, Tanzania ilifanya mabadiliko na kumuingiza mchezaji aliyevaa jezi namba 26 Ibrahim Amme lakini kwenye karatasi ya timu waliyoiwasilisha CAF, hakuna mchezaji aliyesajiliwa na jezi namba 26. 😳👀 Ibarahim Amme alisajiliwa kwa jezi namba 24 Hii inakiuka kanuni za CAF kuhusu utambulisho wa wachezaji. Guinea imewasilisha rasmi ripoti kwa CAF. Je unamaoni Gani kuhusu Hili swala ??
    Like
    Love
    Sad
    4
    · 0 Comments ·0 Shares ·560 Views
  • Kama umefukia hela, muda wa kuzitoa umefika. Ukichelewa utatumia kama karatasi za kuwashia jiko la mkaa
    Kama umefukia hela, muda wa kuzitoa umefika. Ukichelewa utatumia kama karatasi za kuwashia jiko la mkaa
    Love
    Like
    Haha
    4
    · 30 Comments ·0 Shares ·256 Views

  • KAMA UNAELEWA SAYANSI YA MPIRA UTAMUELEWA FADLU, SIMBA YA JANA

    Sayansi ya mpira inasema kabla ya mechi msome sana mpinzani, wazungu wanaita game guiding, lakini pia wakati wa mchezo, ile mechi inaanza tu shika peni na karatasi noti vitu muhimu kwa mpinzani, amekuja kujaje.

    Itasaidia kukupa ABC kudili naye, kutambua ulipo ubora wake & ulipo udhaifu wake. Unaweza kuvunja mitego yake, vunja. Kuna eneo yeye ni bora sana, wewe boresha ilipo nguvu yako kwa lengo la kuudhibiti ubora wake.

    Davids Fadlu kaichukua Simba ambapo moja kati ya eneo lilikuwa linavuja sana ni safu ya ulinzi. Kutoruhusu goli mechi mbili za Ligi Kuu NBC haiwezi kutumika kama guarantee ya kwenda kujilipua ugenini mchezo wa CAF mtoano mbele ya Waarabu.

    Nidhamu ya kwanza ya kimbinu kama mpango kazi, inakulazimu plan A iwe ni kuziba mianya kwa namba kubwa. Sio tena kazi ya mabeki pekee hiyo bali kazi ya timu. System ni mid-block.

    Ilikuwa ni rahisi kumuona mtu kama deep playmaker Deborah Fernandes Mavambo akicheza zaidi chini kuliko ilivyozoeleka. Game Aproach ilimhitaji acheze hivyo.

    Plan A ya kuzima mashambulizi ya mpinzani ilitiki, Plan B ya counter attack ikakataa.Mutale&Balua wakimezwa. Kwenye football kawaida inatokea, kimoja kukubali, kingine kukataa.

    Take away:Bora nusu kitu kuliko kukosa kabisa.
    #paulswai
    KAMA UNAELEWA SAYANSI YA MPIRA UTAMUELEWA FADLU, SIMBA YA JANA Sayansi ya mpira inasema kabla ya mechi msome sana mpinzani, wazungu wanaita game guiding, lakini pia wakati wa mchezo, ile mechi inaanza tu shika peni na karatasi noti vitu muhimu kwa mpinzani, amekuja kujaje. Itasaidia kukupa ABC kudili naye, kutambua ulipo ubora wake & ulipo udhaifu wake. Unaweza kuvunja mitego yake, vunja. Kuna eneo yeye ni bora sana, wewe boresha ilipo nguvu yako kwa lengo la kuudhibiti ubora wake. Davids Fadlu kaichukua Simba ambapo moja kati ya eneo lilikuwa linavuja sana ni safu ya ulinzi. Kutoruhusu goli mechi mbili za Ligi Kuu NBC haiwezi kutumika kama guarantee ya kwenda kujilipua ugenini mchezo wa CAF mtoano mbele ya Waarabu. Nidhamu ya kwanza ya kimbinu kama mpango kazi, inakulazimu plan A iwe ni kuziba mianya kwa namba kubwa. Sio tena kazi ya mabeki pekee hiyo bali kazi ya timu. System ni mid-block. Ilikuwa ni rahisi kumuona mtu kama deep playmaker Deborah Fernandes Mavambo akicheza zaidi chini kuliko ilivyozoeleka. Game Aproach ilimhitaji acheze hivyo. Plan A ya kuzima mashambulizi ya mpinzani ilitiki, Plan B ya counter attack ikakataa.Mutale&Balua wakimezwa. Kwenye football kawaida inatokea, kimoja kukubali, kingine kukataa. Take away:Bora nusu kitu kuliko kukosa kabisa. #paulswai
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·869 Views
  • Kazi ya Sanaa. Mti unazungushiwa karatasi maalum
    Kazi ya Sanaa. Mti unazungushiwa karatasi maalum
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·277 Views
  • Kamera Mpya
    Inayoweza Kuona Kupitia Karatasi ya 1cm

    Wanasayansi wameunda kamera mpya inayoweza kuona kupitia vipande vya karatasi hadi unene wa 1 cm. Hii inamaanisha unaweza kuona kilicho upande wa pili wa karatasi bila kuiondoa karatasi, kama vile kuchunguza vitu vilivyofichwa nyuma ya karatasi au sanduku. Teknolojia hii inaruhusu uchunguzi kupitia vifaa vya kawaida vya kila siku, bila kutumia mionzi hatari kama X-ray.

    #Hora_Tech
    #camera #ugunduzi #Karatasi #XRay
    📷 Kamera Mpya Inayoweza Kuona Kupitia Karatasi ya 1cm 🚨 Wanasayansi wameunda kamera mpya inayoweza kuona kupitia vipande vya karatasi hadi unene wa 1 cm. Hii inamaanisha unaweza kuona kilicho upande wa pili wa karatasi bila kuiondoa karatasi, kama vile kuchunguza vitu vilivyofichwa nyuma ya karatasi au sanduku. Teknolojia hii inaruhusu uchunguzi kupitia vifaa vya kawaida vya kila siku, bila kutumia mionzi hatari kama X-ray. ➤ #Hora_Tech #camera #ugunduzi #Karatasi #XRay
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·1K Views
  • Achana na nguvu za giza,
    Nasoma yasiyo andikika,

    Naandika yasiyosomeka,
    Nakamua tumbo la nchi kutapisha elimu yaliyofichika,

    Nimebeba akili za wengi niite fuvu la wenye fikra napachika,
    Natembea kwenye contua za ubongo kuziunganisha zilizofutika,

    Tega sikio, unasikiliza hekaya za mpatashika,
    Mwelemewa wa mitungi mizito ya machozi ya wataabika,

    Damu iliyogeuka wino kwenye karatasi inamiminika,
    Kwa kalamu naandika,
    Mikono inavimba mchiz napigika,

    Hiphop fani inapozikwa nahuzunika kuliko msiba,

    Napata uchungu zaidi ya nyongo inayomwagika,

    Kichefuchefu nikitema mate wengi wanayazunguka wakizan yamemwagika,
    Tamaa ni kuyaokota wakidhani tiba imefika,

    Me ndo mc mpatashika,
    Naunganisha vipande vya Hekaya zilizochanika,
    Achana na nguvu za giza, Nasoma yasiyo andikika, Naandika yasiyosomeka, Nakamua tumbo la nchi kutapisha elimu yaliyofichika, Nimebeba akili za wengi niite fuvu la wenye fikra napachika, Natembea kwenye contua za ubongo kuziunganisha zilizofutika, Tega sikio, unasikiliza hekaya za mpatashika, Mwelemewa wa mitungi mizito ya machozi ya wataabika, Damu iliyogeuka wino kwenye karatasi inamiminika, Kwa kalamu naandika, Mikono inavimba mchiz napigika, Hiphop fani inapozikwa nahuzunika kuliko msiba, Napata uchungu zaidi ya nyongo inayomwagika, Kichefuchefu nikitema mate wengi wanayazunguka wakizan yamemwagika, Tamaa ni kuyaokota wakidhani tiba imefika, Me ndo mc mpatashika, Naunganisha vipande vya Hekaya zilizochanika,
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·629 Views
  • Nacho kifanya iga uone...
    Hakuna anae miliki ramani ya Money...
    Kama pesa makaratasi Yachane tuone...
    Miliki heshima speed Kwenye mapene...
    Zuga kama umenimiss....
    Pis kama unanipenda shusha kiss...
    Chata ya kilimanjaro mchaga halis...
    Tena munigga tiih tiih Mweus...
    Pambana maisha magumu yawe Hadith...
    Nacho kifanya iga uone... Hakuna anae miliki ramani ya Money... Kama pesa makaratasi Yachane tuone... Miliki heshima speed Kwenye mapene... Zuga kama umenimiss.... Pis kama unanipenda shusha kiss... Chata ya kilimanjaro mchaga halis... Tena munigga tiih tiih Mweus... Pambana maisha magumu yawe Hadith...
    Like
    3
    · 0 Comments ·0 Shares ·511 Views

  • kutokuajiriwa kulikuwa kipimo tosha cha elimu bora mliyoipata lkn kelele zenu zinatuonyesha jinsi mlivyojitahidi kujaza karatasi kwa maelezo yasiyojaa vitendo
    kutokuajiriwa kulikuwa kipimo tosha cha elimu bora mliyoipata lkn kelele zenu zinatuonyesha jinsi mlivyojitahidi kujaza karatasi kwa maelezo yasiyojaa vitendo
    0 Comments ·0 Shares ·274 Views
  • Je wajua?
    MUHAMMED IQBAL DAR ndiye aliyebuni jina la nchi ya TANZANIA?
    Muhammed Iqbal Dar ni mtanzania mwenye asili ya India mzaliwa wa mkoani Tanga mwaka 1944, dini yake ni Muislamu dhehebu la Ahmadiya, baba yake aitwaye Dokta Tufail Ahmad Dar alikuwa ni daktari wa binadamu aliyehamia Tanzania kutoka India mwaka 1930 na walikuwa wakiishi mkoani Morogoro.
    Mwandishi wa kituo cha Redio Safari ya mkoani Mtwara aitwae Alphonce Tonny Kapelah aliwahi kumhoji Muhammed ana kwa ana na ndipo Muhammed alianza kuhadithia jinsi alivyoweza kubuni jina TANZANIA kama ifuatavyo;
    Mnamo mwaka 1964 Tanganyika na Zanzibar zilipoungana serikali waliita muungano huo jina la "Republic of Tanganyika & Zanzibar" jina ambalo lilikuwa refu sana hivyo serikali ikatoa tangazo kwa raia kutoa mapendekezo ya majina ili kupata jina moja zuri litakalobeba maana ya Tanganyika na Zanzibar kwa pamoja na atakaeshinda atapewa zawadi ya Tsh 200, Mohammed anasema siku moja alikuwa maktaba akisoma gazeti la Tanganyika Standard ambalo kwa sasa linaitwa Daily News akaona tangazo hilo ndipo akaamua ashiriki shindano hilo, akachukua karatasi kisha akaandika maneno BISMILLAH RAHMAN RAHIM kisha akaandika TANGANYIKA kisha akaandika ZANZIBAR alafu akaandika jina lake IQBAL kisha akaandika dhehebu la dini yake AHMADIYA kisha akaomba Mungu amjaalie apate jina zuri litakalofaa, baada ya hapo akaandika herufi tatu za mwanzo kwenye neno TANGANYIKA akaunganisha na herufi tatu nyingine za mwanzo kutoka kwenye neno ZANZIBAR (TAN+ZAN) akapata neno TANZAN lakini akaona hili neno bado halijakamilika kuitwa muungano huo, akaweka herufi moja ya mwanzo kutoka kwenye jina lake IQBAL (TAN+ZAN+I) kisha akaongeza na herufi moja ya mwanzo ya neno AHMADIYA (TAN+ZAN+I+A) akapata neno TANZANIA kisha akahisi huenda hili likawa jina sahihi akaamua kufanya utafiti akagundua nchi nyingi za Afrika majina yake yanaishia na herufi IA nchi kama ETHIOPIA, ZAMBIA, NIGERIA, TUNISIA, SOMALIA, GAMBIA, NAMIBIA, LIBERIA, MAURITANIA ndipo akaona hili ndio jina sahihi.
    Baada ya hapo akatuma jina hilo kwa kamati ya kuratibu shindano hilo kisha alikaa miezi kadhaa baadae akapokea barua iliyoeleza kuwa ameshinda shindano hilo na aende ili apewe zawadi yake kisha akapewa pongezi, Muhammed alienda lakini kuna mtu mwingne aitwae Yusufal Pir Mohammed na yeye pia alienda akidai yeye ndie aliyeshinda lakini alipoambiwa aonyeshe barua ya uthibitisho na pongezi kama ya Muhammed hakuwa nayo hivyo Muhammed alipewa cheki yake ya Tsh 200 na zawadi ya ngao, Muhammed pia alisema kwamba washiriki walioshiriki shindano hilo walikuwa 16 lakini alishinda yeye.
    Kwa wakati huo ambao Muhammed alikuwa anahojiwa na Alphonce Muhammed alikuwa anaishi nchini Uingereza mjini Birmingham.
    Ahsante
    Je wajua? MUHAMMED IQBAL DAR ndiye aliyebuni jina la nchi ya TANZANIA? Muhammed Iqbal Dar ni mtanzania mwenye asili ya India mzaliwa wa mkoani Tanga mwaka 1944, dini yake ni Muislamu dhehebu la Ahmadiya, baba yake aitwaye Dokta Tufail Ahmad Dar alikuwa ni daktari wa binadamu aliyehamia Tanzania kutoka India mwaka 1930 na walikuwa wakiishi mkoani Morogoro. Mwandishi wa kituo cha Redio Safari ya mkoani Mtwara aitwae Alphonce Tonny Kapelah aliwahi kumhoji Muhammed ana kwa ana na ndipo Muhammed alianza kuhadithia jinsi alivyoweza kubuni jina TANZANIA kama ifuatavyo; Mnamo mwaka 1964 Tanganyika na Zanzibar zilipoungana serikali waliita muungano huo jina la "Republic of Tanganyika & Zanzibar" jina ambalo lilikuwa refu sana hivyo serikali ikatoa tangazo kwa raia kutoa mapendekezo ya majina ili kupata jina moja zuri litakalobeba maana ya Tanganyika na Zanzibar kwa pamoja na atakaeshinda atapewa zawadi ya Tsh 200, Mohammed anasema siku moja alikuwa maktaba akisoma gazeti la Tanganyika Standard ambalo kwa sasa linaitwa Daily News akaona tangazo hilo ndipo akaamua ashiriki shindano hilo, akachukua karatasi kisha akaandika maneno BISMILLAH RAHMAN RAHIM kisha akaandika TANGANYIKA kisha akaandika ZANZIBAR alafu akaandika jina lake IQBAL kisha akaandika dhehebu la dini yake AHMADIYA kisha akaomba Mungu amjaalie apate jina zuri litakalofaa, baada ya hapo akaandika herufi tatu za mwanzo kwenye neno TANGANYIKA akaunganisha na herufi tatu nyingine za mwanzo kutoka kwenye neno ZANZIBAR (TAN+ZAN) akapata neno TANZAN lakini akaona hili neno bado halijakamilika kuitwa muungano huo, akaweka herufi moja ya mwanzo kutoka kwenye jina lake IQBAL (TAN+ZAN+I) kisha akaongeza na herufi moja ya mwanzo ya neno AHMADIYA (TAN+ZAN+I+A) akapata neno TANZANIA kisha akahisi huenda hili likawa jina sahihi akaamua kufanya utafiti akagundua nchi nyingi za Afrika majina yake yanaishia na herufi IA nchi kama ETHIOPIA, ZAMBIA, NIGERIA, TUNISIA, SOMALIA, GAMBIA, NAMIBIA, LIBERIA, MAURITANIA ndipo akaona hili ndio jina sahihi. Baada ya hapo akatuma jina hilo kwa kamati ya kuratibu shindano hilo kisha alikaa miezi kadhaa baadae akapokea barua iliyoeleza kuwa ameshinda shindano hilo na aende ili apewe zawadi yake kisha akapewa pongezi, Muhammed alienda lakini kuna mtu mwingne aitwae Yusufal Pir Mohammed na yeye pia alienda akidai yeye ndie aliyeshinda lakini alipoambiwa aonyeshe barua ya uthibitisho na pongezi kama ya Muhammed hakuwa nayo hivyo Muhammed alipewa cheki yake ya Tsh 200 na zawadi ya ngao, Muhammed pia alisema kwamba washiriki walioshiriki shindano hilo walikuwa 16 lakini alishinda yeye. Kwa wakati huo ambao Muhammed alikuwa anahojiwa na Alphonce Muhammed alikuwa anaishi nchini Uingereza mjini Birmingham. Ahsante
    Like
    Love
    Yay
    4
    · 0 Comments ·0 Shares ·763 Views
  • KWAMFANO WEWE NDIO MWALIMU UNASIMAMIA MTIANI UKACHANA KARATASI YA MWANAFUNZI MMOJA NA WENGINE WOTE WALIOPO CHUMBA CHA MTIANI WAKACHANA NAZAKWAO WEWE KAMA MWALIMU UTAFANYAJE??
    KWAMFANO WEWE NDIO MWALIMU UNASIMAMIA MTIANI UKACHANA KARATASI YA MWANAFUNZI MMOJA NA WENGINE WOTE WALIOPO CHUMBA CHA MTIANI WAKACHANA NAZAKWAO WEWE KAMA MWALIMU UTAFANYAJE??
    Like
    Love
    2
    · 1 Comments ·0 Shares ·357 Views ·25