• Mpenzi wa zamani wa Israel Adesanya ambaye ni Msanii wa Sanaa za mapigano kutoka Nchini New Zealand mwenye asili ya Nigeria , Charlotte Powdrell amepigwa na butwaa kisha kulia machozi baada ya kumlipa "X" wake Israel dola laki tano (500.000) ambazo ni takribani Shilingi Bilioni 1.3 kwa kumpeleka Mahakamani baada ya kuachana kwao.

    Charlotte na lsreal hawakuwahi kuoana wala kuwa na Watoto, lakini walipoachana, Charlotte alimpeleka mahakamani akidai alistahili nusu ya mali ya Israel kwa sababu ya muda waliokaa kwenye uhusiano, akidai kwamba alistahili kuolewa naye. Makadirio ya utajiri wa Adesanya ulikadiriwa kuwa dola milioni 15 ambazo ni zaidi Shilingi Bilioni 39 .1 hivyo Charlotte alidai kwamba pesa hizo walipaswa kugawana baada ya kuachana.

    Mahakama baada ya kufuatilia na kuchunguza kesi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja toka mwaka 2023, Mahakama hiyo hatimaye ilipitisha uamuzi kwamba apewe nusu ya utajiri wa lsreal Adesanya, lakini ikagundulika kuwa thamani ya Isreal Adesanya ni sifuri yaani hana chochote anachomiliki wala hajawahi kumiliki akaunti ya benki maisha yake yote.

    Na kwa kuwa Charlotte ana thamani ya dola milioni moja na tajiri zaidi kuliko aliyekuwa Mpenzi wake Adesanya, pesa zake mwenyewe zilipaswa kugawanywa kati yao kwa usawa na kumuacha Israeli na kiasi cha dola laki tano (500.000). Inaripotiwa kuwa pesa zote za Israel Adesanya ambazo ni zaidi dola milioni 15 zinasimamiwa na Mama yake Mzazi, Taiwo na amekuwa akisimamia fedha zake tangu mwanzo wa kazi yake.
    Mpenzi wa zamani wa Israel Adesanya ambaye ni Msanii wa Sanaa za mapigano kutoka Nchini New Zealand 🇳🇿 mwenye asili ya Nigeria 🇳🇬, Charlotte Powdrell amepigwa na butwaa kisha kulia machozi baada ya kumlipa "X" wake Israel dola laki tano (500.000) ambazo ni takribani Shilingi Bilioni 1.3 kwa kumpeleka Mahakamani baada ya kuachana kwao. Charlotte na lsreal hawakuwahi kuoana wala kuwa na Watoto, lakini walipoachana, Charlotte alimpeleka mahakamani akidai alistahili nusu ya mali ya Israel kwa sababu ya muda waliokaa kwenye uhusiano, akidai kwamba alistahili kuolewa naye. Makadirio ya utajiri wa Adesanya ulikadiriwa kuwa dola milioni 15 ambazo ni zaidi Shilingi Bilioni 39 .1 hivyo Charlotte alidai kwamba pesa hizo walipaswa kugawana baada ya kuachana. Mahakama baada ya kufuatilia na kuchunguza kesi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja toka mwaka 2023, Mahakama hiyo hatimaye ilipitisha uamuzi kwamba apewe nusu ya utajiri wa lsreal Adesanya, lakini ikagundulika kuwa thamani ya Isreal Adesanya ni sifuri yaani hana chochote anachomiliki wala hajawahi kumiliki akaunti ya benki maisha yake yote. Na kwa kuwa Charlotte ana thamani ya dola milioni moja na tajiri zaidi kuliko aliyekuwa Mpenzi wake Adesanya, pesa zake mwenyewe zilipaswa kugawanywa kati yao kwa usawa na kumuacha Israeli na kiasi cha dola laki tano (500.000). Inaripotiwa kuwa pesa zote za Israel Adesanya ambazo ni zaidi dola milioni 15 zinasimamiwa na Mama yake Mzazi, Taiwo na amekuwa akisimamia fedha zake tangu mwanzo wa kazi yake.
    0 Comments ·0 Shares ·6 Views
  • Rais wa Marekani , Donald Trump ametoa siri kuwa Ofisi yake imepokea barua kutoka kwa Rais wa Ukraine , Volodymyr Zelensky, ikisema yuko tayari kwa mazungumzo na Russia na kusaini makubaliano ya madini adimu.

    “Ukraine iko tayari kukaa kwenye meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo ili kuleta amani ya kudumu. Hakuna anayetaka amani zaidi ya Waukraine,” Trump amesema katika hotuba yake bungeni usiku wa kuamkia leo huku akinukuu barua hiyo.

    “Mimi na timu yangu tuko tayari kufanya kazi chini ya uongozi thabiti wa Rais Trump ili kupata amani ya kudumu’,” Trump alinukuu maneno ya Zelenskyy.

    “Si hilo lingekuwa jambo zuri?” aliuliza. “Ni wakati wa kukomesha huu upuuzi. Ni wakati wa kusitisha mauaji. Ni wakati wa kumaliza vita hivi visivyo na maana. Ukitaka kumaliza vita, lazima uzungumze na pande zote mbili,” amesema Trump.

    Kauli hiyo ya Trump imekuja siku chache baada ya mvutano mkali kati yake na Zelenskyy katika Ofisi ya Oval iliyoko Ikulu ya White House, hali iliyosababisha Marekani kusitisha msaada muhimu wa kijeshi kwa Ukraine.

    Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump ametoa siri kuwa Ofisi yake imepokea barua kutoka kwa Rais wa Ukraine 🇺🇦, Volodymyr Zelensky, ikisema yuko tayari kwa mazungumzo na Russia 🇷🇺 na kusaini makubaliano ya madini adimu. “Ukraine iko tayari kukaa kwenye meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo ili kuleta amani ya kudumu. Hakuna anayetaka amani zaidi ya Waukraine,” Trump amesema katika hotuba yake bungeni usiku wa kuamkia leo huku akinukuu barua hiyo. “Mimi na timu yangu tuko tayari kufanya kazi chini ya uongozi thabiti wa Rais Trump ili kupata amani ya kudumu’,” Trump alinukuu maneno ya Zelenskyy. “Si hilo lingekuwa jambo zuri?” aliuliza. “Ni wakati wa kukomesha huu upuuzi. Ni wakati wa kusitisha mauaji. Ni wakati wa kumaliza vita hivi visivyo na maana. Ukitaka kumaliza vita, lazima uzungumze na pande zote mbili,” amesema Trump. Kauli hiyo ya Trump imekuja siku chache baada ya mvutano mkali kati yake na Zelenskyy katika Ofisi ya Oval iliyoko Ikulu ya White House, hali iliyosababisha Marekani kusitisha msaada muhimu wa kijeshi kwa Ukraine.
    0 Comments ·0 Shares ·22 Views
  • Nchi ya Ujerumani imepanda kusitisha misaada kwa Nchi ya Rwanda kutokana na kujihusisha kwao na Kundi la Waasi wa M23 ambao limefanikiwa kuiteka Miji ya Goma na Bukavu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo . Tayari Rwanda imeshafahamishwa na Ujerumani kuhusu mpango huo.

    Aidha, Nchi ya Rwanda imekuwa ikinufaika na misaada kutoka Nchini Ujerumani inayokadiriwa kufikia thamani ya wastani wa Dola za Kimarekani milioni 53 kwa mwaka ambayo imekuwa ikitolewa katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, uzalishaji wa chanjo na mabadiliko ya tabia Nchi.

    Nchi ya Ujerumani 🇩🇪 imepanda kusitisha misaada kwa Nchi ya Rwanda 🇷🇼 kutokana na kujihusisha kwao na Kundi la Waasi wa M23 ambao limefanikiwa kuiteka Miji ya Goma na Bukavu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Tayari Rwanda imeshafahamishwa na Ujerumani kuhusu mpango huo. Aidha, Nchi ya Rwanda imekuwa ikinufaika na misaada kutoka Nchini Ujerumani inayokadiriwa kufikia thamani ya wastani wa Dola za Kimarekani milioni 53 kwa mwaka ambayo imekuwa ikitolewa katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, uzalishaji wa chanjo na mabadiliko ya tabia Nchi.
    0 Comments ·0 Shares ·100 Views
  • Serikali ya Kinshasa (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ) imetangaza kuwa Bidhaa (Biashara) kutoka Miji ya Goma na Bukavu ambayo ni Miji inayopatikana Mashariki mwa DR Congo kulipa ushuru wa kuingia kwenye Mikoa mingine ambayo inasimamiwa na Serekali ya Kinshasa.

    Miji ya Goma na Bukavu inadhibitiwa na Waasi wa kundi la M23 na inachukuliwa kama Nchi nyingine ndani ya DR Congo huku Serekali ya Kinshasa ikizitaka Nchi nyingine Duniani kutotambua Miji hiyo kama sehemu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Waasi wa kundi la M23 wamesema kuwa wapo kwenye hatua za mwisho ya kutangaza Viongozi wao katika Miji hiyo ambapo wanasema kuwa wataanda uchaguzi ili kuwapata Viongozi wataongoza Miji hiyo ambayo ipo chini ya Uongozi wao.

    Hata hatua nyingine, Serekali ya Kinshasa imetangaza rasmi Mji wa Uvira kuwa ndiyo Mji Mkuu wa Serekali ya Mkoa wa Sud-Kivu na Makazi ya muda ya Gavana wa Mkoa huo wa Sud-Kivu baada ya Mji wa Bukavu kuvamiwa na kudhibitiwa na Waasi wa M23.

    Serikali ya Kinshasa (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩) imetangaza kuwa Bidhaa (Biashara) kutoka Miji ya Goma na Bukavu ambayo ni Miji inayopatikana Mashariki mwa DR Congo kulipa ushuru wa kuingia kwenye Mikoa mingine ambayo inasimamiwa na Serekali ya Kinshasa. Miji ya Goma na Bukavu inadhibitiwa na Waasi wa kundi la M23 na inachukuliwa kama Nchi nyingine ndani ya DR Congo huku Serekali ya Kinshasa ikizitaka Nchi nyingine Duniani kutotambua Miji hiyo kama sehemu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Waasi wa kundi la M23 wamesema kuwa wapo kwenye hatua za mwisho ya kutangaza Viongozi wao katika Miji hiyo ambapo wanasema kuwa wataanda uchaguzi ili kuwapata Viongozi wataongoza Miji hiyo ambayo ipo chini ya Uongozi wao. Hata hatua nyingine, Serekali ya Kinshasa imetangaza rasmi Mji wa Uvira kuwa ndiyo Mji Mkuu wa Serekali ya Mkoa wa Sud-Kivu na Makazi ya muda ya Gavana wa Mkoa huo wa Sud-Kivu baada ya Mji wa Bukavu kuvamiwa na kudhibitiwa na Waasi wa M23.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·63 Views
  • MTUNZI WA JINA LA 'TANZANIA' AFARIKI

    Hicho ni kipande cha gazeti la The Nationalist la Oktoba 30, 1964. Habari kubwa kwenye gazeti hili na Nchi kwa ujumla ni jina jipya la TANZANIA. Ni kwamba baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa April 26, 1964, jina la nchi mpya lilikuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Lakini jina hili lilikuwa refu sana na kuwa kero kwa Watumiaji.

    Serikali kupitia wizara ya habari na utalii chini ya waziri Dkt. Idrisa Abdul Wakili, ikaanzisha mchakato wa kutafuta jina jipya litakalokuwa fupi na rahisi. Ikatoa tangazo kupitia gazeti la Tanganyika Standard, ambalo sasa ni Daily News, kuwataka Watanzania wenye kuweza kubuni jina jipya la Nchi kufanya hivyo. Ndipo kijana wa miaka 18 kutoka Morogoro, Mohamed Iqbal Dar, Mwanafunzi wa Sekondari ya Aga Khan Morogoro, akaliona tangazo hilo na kushiriki.

    Akatunga jina la Tanzania na kulituma kwenye anwani iliyotangazwa. Baada ya muda kupita, akapata barua kutoka serikalini ikimtaja na kumpongeza yeye kama mmoja wa Washindi 16 na wakatakiwa kufika ofisi za wizara. Kwa pamoja watu hawa walitakiwa kugawana zawadi ya shilingi 200, wakati huo shilingi moja ilikuwa sawa na dola 8 za Marekani.

    Siku ilipofika, watu wawili tu walijitokeza; yeye Mohamed Iqbal Dar na Yusufal Pir Mohamed. Lakini huyo mwenzake hakuwa na ile barua ya kutajwa kama mshindi na kupongezwa... Serikali ikashindwa kumthibitisha hivyo kumtangaza Mohamed Iqbal Dar kama Mshindi pekee. Ndipo Jumatano ya Oktoba 29, 1964 serikali ikatangaza rasmi kwamba jina jipya la nchi ni Tanzania na gazeti la The Nationalist likaichapisha habari hii kubwa, Alhamisi ya Oktoba 30, 1964. Jina la Tanzania likaanza kutumika rasmi Novemba Mosi, 1964.

    - Alitungaje jina?

    TAN - kutoka Tanganyika
    ZAN - kutoka Zanzibar
    I - kutoka jina lake la Iqbal.
    A - kutoka dini yake ya Ahmadiya. Hii pia ikawa rahisi zaidi kwake kwani majina ya nchi nyingi za Afrika yaliishia na A kama Ethiopia, Zambia, Gambia nk.

    - Ni nani huyu Mohamed Iqbal Dar?

    Ni mtoto wa Dkt. Dar, ambaye alikuja Tanzania mwaka 1930 kutoka India. Alifikia Tanga, na ndiko alikozaliwa Mohamed, hakafu akahamia Morogoro. Mohamed amefarikia huko Birmingham Nchini Uingereza .
    MTUNZI WA JINA LA 'TANZANIA' AFARIKI Hicho ni kipande cha gazeti la The Nationalist la Oktoba 30, 1964. Habari kubwa kwenye gazeti hili na Nchi kwa ujumla ni jina jipya la TANZANIA. Ni kwamba baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa April 26, 1964, jina la nchi mpya lilikuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Lakini jina hili lilikuwa refu sana na kuwa kero kwa Watumiaji. Serikali kupitia wizara ya habari na utalii chini ya waziri Dkt. Idrisa Abdul Wakili, ikaanzisha mchakato wa kutafuta jina jipya litakalokuwa fupi na rahisi. Ikatoa tangazo kupitia gazeti la Tanganyika Standard, ambalo sasa ni Daily News, kuwataka Watanzania wenye kuweza kubuni jina jipya la Nchi kufanya hivyo. Ndipo kijana wa miaka 18 kutoka Morogoro, Mohamed Iqbal Dar, Mwanafunzi wa Sekondari ya Aga Khan Morogoro, akaliona tangazo hilo na kushiriki. Akatunga jina la Tanzania na kulituma kwenye anwani iliyotangazwa. Baada ya muda kupita, akapata barua kutoka serikalini ikimtaja na kumpongeza yeye kama mmoja wa Washindi 16 na wakatakiwa kufika ofisi za wizara. Kwa pamoja watu hawa walitakiwa kugawana zawadi ya shilingi 200, wakati huo shilingi moja ilikuwa sawa na dola 8 za Marekani. Siku ilipofika, watu wawili tu walijitokeza; yeye Mohamed Iqbal Dar na Yusufal Pir Mohamed. Lakini huyo mwenzake hakuwa na ile barua ya kutajwa kama mshindi na kupongezwa... Serikali ikashindwa kumthibitisha hivyo kumtangaza Mohamed Iqbal Dar kama Mshindi pekee. Ndipo Jumatano ya Oktoba 29, 1964 serikali ikatangaza rasmi kwamba jina jipya la nchi ni Tanzania na gazeti la The Nationalist likaichapisha habari hii kubwa, Alhamisi ya Oktoba 30, 1964. Jina la Tanzania likaanza kutumika rasmi Novemba Mosi, 1964. - Alitungaje jina? TAN - kutoka Tanganyika ZAN - kutoka Zanzibar I - kutoka jina lake la Iqbal. A - kutoka dini yake ya Ahmadiya. Hii pia ikawa rahisi zaidi kwake kwani majina ya nchi nyingi za Afrika yaliishia na A kama Ethiopia, Zambia, Gambia nk. - Ni nani huyu Mohamed Iqbal Dar? Ni mtoto wa Dkt. Dar, ambaye alikuja Tanzania mwaka 1930 kutoka India. Alifikia Tanga, na ndiko alikozaliwa Mohamed, hakafu akahamia Morogoro. Mohamed amefarikia huko Birmingham Nchini Uingereza 🇬🇧.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·135 Views
  • Ijumaa, tarehe 28 Februari, haikuwa siku rahisi kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alipofanya ziara katika Ikulu ya White House, Marekani. Kabla hata ya mzozo wa maneno kati yake na mwenyeji wake, Rais Donald Trump, pamoja na Makamu wa Rais JD Vance, tayari kulikuwa na ishara za mivutano.

    Trump alimkaribisha Zelensky mlangoni na kusema kwa utani: “Leo amevalia kweli kweli,” kauli ambayo iliwafanya baadhi ya waandishi wa habari kuiona kama kejeli badala ya pongezi. Wakati huo, Zelensky alikuwa amevalia fulana nyeusi ya mikono mirefu, vazi ambalo amekuwa akilivaa mara kwa mara tangu Ukraine ivamiwe na Urusi mwaka 2022.

    Baadaye, Trump alipompokea Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alionekana kutazama mavazi yake kwa makini kutoka juu hadi chini, kisha kunong’ona maneno yanayoweza kutafsiriwa kama pongezi kwa suti rasmi aliyovaa Starmer.

    Mjadala kuhusu mavazi ya Zelensky ulizidi kupamba moto wakati wa mkutano wa waandishi wa habari. Brian Glenn, mwandishi kutoka Real America’s Voice—chombo cha habari kinachopendelea mrengo wa kulia—alimtupia swali la moja kwa moja:

    “Kwa nini hauvai suti? Upo katika ofisi ya juu kabisa katika nchi hii, na umegoma kuvaa suti – je, unamiliki hata suti?”

    Kwa utulivu, Zelensky alijibu kwa mshangao mdogo:

    “Nitavaa suti vita hivi vitakapomalizika. Labda suti kama yako, labda bora zaidi, au pengine ya bei nafuu kuliko yako,” alisema kwa utani huku akionyesha msimamo wake wa kuendelea kuvaa mavazi ya kijeshi.

    Swali hilo la Glenn liliibua mjadala mkali mitandaoni. Wengine walimuunga mkono, wakisema kwamba kiongozi wa taifa anapaswa kuvaa mavazi rasmi anapokutana na viongozi wengine, ilhali wengine waliona swali hilo kuwa la dhihaka na lisilo na umuhimu.

    Miongoni mwa waliomkosoa Glenn ni mwandishi maarufu wa Uingereza, Piers Morgan, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Trump. Morgan aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter):

    “Swali la kipuuzi. Elon Musk havai suti anapoingia Ikulu.”

    Historia pia inaonyesha kuwa si Zelensky pekee aliyeingia Ikulu ya Marekani bila suti. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill, alifanya hivyo katika moja ya ziara zake rasmi.
    Ijumaa, tarehe 28 Februari, haikuwa siku rahisi kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alipofanya ziara katika Ikulu ya White House, Marekani. Kabla hata ya mzozo wa maneno kati yake na mwenyeji wake, Rais Donald Trump, pamoja na Makamu wa Rais JD Vance, tayari kulikuwa na ishara za mivutano. Trump alimkaribisha Zelensky mlangoni na kusema kwa utani: “Leo amevalia kweli kweli,” kauli ambayo iliwafanya baadhi ya waandishi wa habari kuiona kama kejeli badala ya pongezi. Wakati huo, Zelensky alikuwa amevalia fulana nyeusi ya mikono mirefu, vazi ambalo amekuwa akilivaa mara kwa mara tangu Ukraine ivamiwe na Urusi mwaka 2022. Baadaye, Trump alipompokea Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alionekana kutazama mavazi yake kwa makini kutoka juu hadi chini, kisha kunong’ona maneno yanayoweza kutafsiriwa kama pongezi kwa suti rasmi aliyovaa Starmer. Mjadala kuhusu mavazi ya Zelensky ulizidi kupamba moto wakati wa mkutano wa waandishi wa habari. Brian Glenn, mwandishi kutoka Real America’s Voice—chombo cha habari kinachopendelea mrengo wa kulia—alimtupia swali la moja kwa moja: “Kwa nini hauvai suti? Upo katika ofisi ya juu kabisa katika nchi hii, na umegoma kuvaa suti – je, unamiliki hata suti?” Kwa utulivu, Zelensky alijibu kwa mshangao mdogo: “Nitavaa suti vita hivi vitakapomalizika. Labda suti kama yako, labda bora zaidi, au pengine ya bei nafuu kuliko yako,” alisema kwa utani huku akionyesha msimamo wake wa kuendelea kuvaa mavazi ya kijeshi. Swali hilo la Glenn liliibua mjadala mkali mitandaoni. Wengine walimuunga mkono, wakisema kwamba kiongozi wa taifa anapaswa kuvaa mavazi rasmi anapokutana na viongozi wengine, ilhali wengine waliona swali hilo kuwa la dhihaka na lisilo na umuhimu. Miongoni mwa waliomkosoa Glenn ni mwandishi maarufu wa Uingereza, Piers Morgan, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Trump. Morgan aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter): “Swali la kipuuzi. Elon Musk havai suti anapoingia Ikulu.” Historia pia inaonyesha kuwa si Zelensky pekee aliyeingia Ikulu ya Marekani bila suti. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill, alifanya hivyo katika moja ya ziara zake rasmi.
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·176 Views
  • Tafsiri isiyo rasmi

    "Tulikuwa na mkutano wa maana sana leo (Jana) Ikulu (whilte house) Mengi yamefundishika ambayo yasingeweza kueleweka bila mazungumzo chini ya moto na shinikizo kama hilo. Inashangaza kinachotoka kupitia hisia, na nimeamua kuwa Rais Zelenskyy hayuko tayari kwa Amani ikiwa Amerika itahusika, kwa sababu anahisi kuhusika kwetu kunampa faida kubwa katika mazungumzo. Sitaki faida, nataka AMANI.
    Ameidharau Marekani katika Ofisi yake pendwa ya Oval. Anaweza kurudi pale atakapokuwa tayari kwa Amani.” - Donald J. Trump, Rais wa Marekani .

    Tafsiri isiyo rasmi "Tulikuwa na mkutano wa maana sana leo (Jana) Ikulu (whilte house) Mengi yamefundishika ambayo yasingeweza kueleweka bila mazungumzo chini ya moto na shinikizo kama hilo. Inashangaza kinachotoka kupitia hisia, na nimeamua kuwa Rais Zelenskyy hayuko tayari kwa Amani ikiwa Amerika itahusika, kwa sababu anahisi kuhusika kwetu kunampa faida kubwa katika mazungumzo. Sitaki faida, nataka AMANI. Ameidharau Marekani katika Ofisi yake pendwa ya Oval. Anaweza kurudi pale atakapokuwa tayari kwa Amani.” - Donald J. Trump, Rais wa Marekani 🇺🇸.
    0 Comments ·0 Shares ·166 Views
  • #Repost @georgejob_gj
    MASTER KI NI MVP TUSISAHAU.

    Tusisahau kua huyu Aziz Ki ndiye MVP wa ligi yetu Tanzania Bara msimu wa 2023/2024 haya anayo yafanya sio kwa Bahati Mbaya au kwa sababu Pamba ni wabovu Master Ki is a versatile player

    Goli la pili alilo piga ukiangalia mentality yake ilivyo change kwa haraka kutoka kutaka kutoa pasi na kufanya maamuzi ya kupiga shuti la kucave golini utagundua Azizi Ki ni mchezaji Mwenye akili kubwa sana ya Mpira.

    Pamba walizidiwa kimbinu kwenye kila sehemu Substitution walizo fanya ya Nakibinge na Habib Kyombo wallijaribu kutaka kubadilisha mchezo lakini mbinu ya Yanga bado iliendelea kutawala mchezo.

    Yona Amos moja ya Makipa Bora sana nchini bahati mbaya leo kakutana na Yanga iliyo Bora sana kimbinu karibu magoli yote aliyofungwa ni magoli ambayo sio ya kumlaumu ni magoii ya kiufundi.

    NB: Ikangalombo apewe muda au Mali ipo?
    (George Job, Mchambuzi)

    #Repost @georgejob_gj MASTER KI NI MVP TUSISAHAU. Tusisahau kua huyu Aziz Ki ndiye MVP wa ligi yetu Tanzania Bara msimu wa 2023/2024 haya anayo yafanya sio kwa Bahati Mbaya au kwa sababu Pamba ni wabovu Master Ki is a versatile player 🙌 Goli la pili alilo piga ukiangalia mentality yake ilivyo change kwa haraka kutoka kutaka kutoa pasi na kufanya maamuzi ya kupiga shuti la kucave golini utagundua Azizi Ki ni mchezaji Mwenye akili kubwa sana ya Mpira. Pamba walizidiwa kimbinu kwenye kila sehemu Substitution walizo fanya ya Nakibinge na Habib Kyombo wallijaribu kutaka kubadilisha mchezo lakini mbinu ya Yanga bado iliendelea kutawala mchezo. Yona Amos moja ya Makipa Bora sana nchini bahati mbaya leo kakutana na Yanga iliyo Bora sana kimbinu karibu magoli yote aliyofungwa ni magoli ambayo sio ya kumlaumu ni magoii ya kiufundi. NB: Ikangalombo apewe muda au Mali ipo? (George Job, Mchambuzi)
    0 Comments ·0 Shares ·263 Views
  • Uingereza imesitisha kutoa baadhi ya misaada ya moja kwa moja kwa Nchi ya Rwanda kufuatia kuendelea kwa machafuko ya yanayosababishwa na Vikundi huko Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kikiwemo Kikundi cha Waasi cha M23 ambacho kinadaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda.

    Uamuzi huo unakuja baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Lammy kukutana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame Jijini Kigali, Rwanda na Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi Jijini Kinshasa, DR Congo.

    Uingereza 🇬🇧 imesitisha kutoa baadhi ya misaada ya moja kwa moja kwa Nchi ya Rwanda 🇷🇼 kufuatia kuendelea kwa machafuko ya yanayosababishwa na Vikundi huko Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 kikiwemo Kikundi cha Waasi cha M23 ambacho kinadaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda. Uamuzi huo unakuja baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Lammy kukutana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame Jijini Kigali, Rwanda na Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi Jijini Kinshasa, DR Congo.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·179 Views
  • "Naona Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amefunga safari hadi Congo kumuona Rais Tshisekedi, sijui ni kipi hasa kinaendelea katika jumuiya ya Afrika mashariki lakini ni kama kuna muungano ndani ya muungano, eeeh kuna muungano kati ya Congo na Burundi ambao unalenga kupambana dhidi ya Rwanda

    Yaani ukiwatazama Congo na Burundi ni kama wameungana kupambana na Rwanda na M23 eeeh ipo wazi na tayari mapigano kati ya majeshi ya Congo Burundi dhidi ya Rwanda na M23 yameshuhudiwa, EAC wasipodhibiti hali ya Congo mzozo huu utaenda kutanuka na kuwa wa kikanda

    Ngoja tuone ila yajayo sio mazuri kwa diplomasia ya EAC , kiufupi ziara ya Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, nchini Congo inalenga kuonana na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi, huku lengo kuu ikiwa na mazungumzo kuhusu mzozo unaolikumba eneo la mashariki mwa Kongo" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.

    "Naona Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amefunga safari hadi Congo kumuona Rais Tshisekedi, sijui ni kipi hasa kinaendelea katika jumuiya ya Afrika mashariki lakini ni kama kuna muungano ndani ya muungano, eeeh kuna muungano kati ya Congo na Burundi ambao unalenga kupambana dhidi ya Rwanda Yaani ukiwatazama Congo na Burundi ni kama wameungana kupambana na Rwanda na M23 eeeh ipo wazi na tayari mapigano kati ya majeshi ya Congo Burundi dhidi ya Rwanda na M23 yameshuhudiwa, EAC wasipodhibiti hali ya Congo mzozo huu utaenda kutanuka na kuwa wa kikanda 😭 Ngoja tuone ila yajayo sio mazuri kwa diplomasia ya EAC , kiufupi ziara ya Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, nchini Congo inalenga kuonana na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi, huku lengo kuu ikiwa na mazungumzo kuhusu mzozo unaolikumba eneo la mashariki mwa Kongo" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.
    0 Comments ·0 Shares ·261 Views
  • Maskari wa Jeshi la Ulinzi la Afrika Kusini (SANDF) waliojeruhiwa katika mapigano Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , limeanza kurejea nyumbani kupitia Jijini Kigali, Rwanda baada ya kukwama katika kambi zao kwa takriban mwezi mmoja DR Congo.

    Wanajeshi hao ni miongoni mwa Askari wa (SANDF) walioko chini ya Kikosi cha Walinda Amani wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SAMIDRC), wanaoimarisha ulinzi Mashariki mwa DR Congo pamoja na kukabiliana na uovu wa Waasi wa kundi la M23 dhidi ya Raia wa DR Congo.

    Televisheni ya Afrika Kusini ya SABC imesema, Wanajeshi hao ambao walishindwa kupambana na Waasi wa kundi la M23 ambao waliitwaa Miji ya mashariki mwa Nchi hiyo, walionekana wakiondoka Mjini Goma kuanzia juzi jioni kwa barabara bila vifaa na sare zao za Kijeshi. Ripoti ya Jarida la Afrika Kusini la Rapport iliyochapishwa Jumapili ilieleza kuwa Wanajeshi wa Afrika Kusini waliojeruhiwa ni zaidi ya 189.

    Kwa mujibu wa Jarida hilo, miongoni mwa waliojeruhiwa ni Wanajeshi wawili (2) ambao ni Wajawazito, huku idadi ya Wanajeshi wa (SANDF) wanaoendelea kukwama Nchini DR Congo ikikadiriwa kuwa kati ya elfu moja (1,000) na elfu mbili (2,000).

    Maskari wa Jeshi la Ulinzi la Afrika Kusini 🇿🇦 (SANDF) waliojeruhiwa katika mapigano Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, limeanza kurejea nyumbani kupitia Jijini Kigali, Rwanda 🇷🇼 baada ya kukwama katika kambi zao kwa takriban mwezi mmoja DR Congo. Wanajeshi hao ni miongoni mwa Askari wa (SANDF) walioko chini ya Kikosi cha Walinda Amani wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SAMIDRC), wanaoimarisha ulinzi Mashariki mwa DR Congo pamoja na kukabiliana na uovu wa Waasi wa kundi la M23 dhidi ya Raia wa DR Congo. Televisheni ya Afrika Kusini ya SABC imesema, Wanajeshi hao ambao walishindwa kupambana na Waasi wa kundi la M23 ambao waliitwaa Miji ya mashariki mwa Nchi hiyo, walionekana wakiondoka Mjini Goma kuanzia juzi jioni kwa barabara bila vifaa na sare zao za Kijeshi. Ripoti ya Jarida la Afrika Kusini la Rapport iliyochapishwa Jumapili ilieleza kuwa Wanajeshi wa Afrika Kusini waliojeruhiwa ni zaidi ya 189. Kwa mujibu wa Jarida hilo, miongoni mwa waliojeruhiwa ni Wanajeshi wawili (2) ambao ni Wajawazito, huku idadi ya Wanajeshi wa (SANDF) wanaoendelea kukwama Nchini DR Congo ikikadiriwa kuwa kati ya elfu moja (1,000) na elfu mbili (2,000).
    Sad
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·212 Views
  • SOFTWARE ZINAZOTUMIKA KUFLASH SIMU ZA AINA ZOTE

    software hizo apo unaweza kutumia kutoa lock za simu, na lock z mordem zitumie line zote

    Hizo apo chini ndo list ya software zenyewe

    Softwares
    Miracle box
    Oss Client Pro
    Z3x Premium
    Gsm Alladin
    Infinix Box
    Octopus Samsung
    DC Unlocker
    NCK Box & Nck Dongle
    SP Flash Tool
    Infinity Best Dongle box
    Furious gold tool box
    Mtk Tool Box
    Octoplus Suite
    Volcano box
    Merapi tool
    Xt2 clip box
    SP Flash Tool
    Infinity Chinese miracle 2 Mtk box
    GbKEY Dongle
    Smart clip 2 tool
    CS Tool Dongle
    Medusa Pro Box
    BST dongle
    UFI Box International Version
    Atf box
    Avenger box
    Magma box
    Ultimate Multi Tool Box
    GPG Dragon
    Zamsung Crypter Advance Frp Tool Remover

    Je unatka kusoma na kupata izi link za program.
    🎉SOFTWARE ZINAZOTUMIKA KUFLASH SIMU ZA AINA ZOTE 🦠software hizo apo unaweza kutumia kutoa lock za simu, na lock z mordem zitumie line zote 🦠Hizo apo chini ndo list ya software zenyewe Softwares 💢Miracle box 💢Oss Client Pro 💢Z3x Premium 💢Gsm Alladin 💢Infinix Box 💢Octopus Samsung 💢DC Unlocker 💢NCK Box & Nck Dongle 💢SP Flash Tool 💢Infinity Best Dongle box 💢Furious gold tool box 💢Mtk Tool Box 💢Octoplus Suite 💢Volcano box 💢Merapi tool 💢Xt2 clip box 💢SP Flash Tool 💢Infinity Chinese miracle 2 Mtk box 💢GbKEY Dongle 💢Smart clip 2 tool 💢CS Tool Dongle 💢Medusa Pro Box 💢BST dongle 💢UFI Box International Version 💢Atf box 💢Avenger box 💢Magma box 💢Ultimate Multi Tool Box 💢GPG Dragon 💢Zamsung Crypter Advance Frp Tool Remover Je unatka kusoma na kupata izi link za program. 🥱🥱🥱
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·234 Views
  • PART 8

    Watu karibu 3,000 waangamia katika mashambulizi

    Mashambulizi haya manne, yaliyotekelezwa chini ya saa mbili, yaligharimu maisha ya watu 2,977, ikiwa ni pamoja na waokoaji 441 kutoka mji wa New York. Zaidi ya watu 6,000 walijeruhiwa na wengine waliumwa magonjwa yanayohusiana na mashambulio hayo, haswa kwa sababu walivuta chembe zenye sumu ambazo ziliendelea kwa wiki kadhaa baada ya mashambulio.
    PART 8 Watu karibu 3,000 waangamia katika mashambulizi Mashambulizi haya manne, yaliyotekelezwa chini ya saa mbili, yaligharimu maisha ya watu 2,977, ikiwa ni pamoja na waokoaji 441 kutoka mji wa New York. Zaidi ya watu 6,000 walijeruhiwa na wengine waliumwa magonjwa yanayohusiana na mashambulio hayo, haswa kwa sababu walivuta chembe zenye sumu ambazo ziliendelea kwa wiki kadhaa baada ya mashambulio.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·163 Views
  • PART 3

    Chini ya saa mbili, majengo muhimu ya nchi hii yenye nguvu duniani yalishambuliwa, na kuua karibu watu 3,000 na kujeruhi maelfu kadhaa. Mashambulio haya, ambayo ni mabaya zaidi katika historia ya kisasa, yaliuacha ulimwengu wote kwa mshtuko mkubwa.
    PART 3 Chini ya saa mbili, majengo muhimu ya nchi hii yenye nguvu duniani yalishambuliwa, na kuua karibu watu 3,000 na kujeruhi maelfu kadhaa. Mashambulio haya, ambayo ni mabaya zaidi katika historia ya kisasa, yaliuacha ulimwengu wote kwa mshtuko mkubwa.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·146 Views
  • PART 1

    Miaka ishirini iliyopita, asubuhi ya Septemba 11, 2001 katika pwani ya mashariki mwa Marekani, ndege nne za abiria zilitekwa nyara kwa wakati mmoja na magaidi 19 na kusababisha vifo vya maelfu ya watu baada ya kugonga minara pacha ya kituo cha bisahara cha World Trade Center nchini Marekani.
    PART 1 Miaka ishirini iliyopita, asubuhi ya Septemba 11, 2001 katika pwani ya mashariki mwa Marekani, ndege nne za abiria zilitekwa nyara kwa wakati mmoja na magaidi 19 na kusababisha vifo vya maelfu ya watu baada ya kugonga minara pacha ya kituo cha bisahara cha World Trade Center nchini Marekani.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·123 Views
  • Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo , Felix Tshisekedi ameitaka Nchi ya Marekani kununua madini moja kwa moja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiitaja ndio "mmiliki halisi" wa rasilimali hizo na sio Nchi Rwanda .

    Tshisekedi amesema kuwa anaanza kwa kutoa ofa hiyo kwa Marekani kwanza huku akitoa pendekezo hilo pia liko wazi kwa mataifa ya Umoja Ulaya (EU) na wanunuzi wengine wanaotafuta na kununua madini kutoka Nchini Rwanda kwa sasa.

    Rais huyo amewaonya Mataifa yanayonunua madini kutoka Nchini Rwanda kuwa wanachukua madini yaliyoibwa kutoka Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, kwahiyo wanatakiwa kununua kwa mmiliki halali. Ikumbukwe kwamba Nchi ya Rwanda ni moja ya kati ya Nchi zinauza madini mengi barani Afrika kwa Mataifa ya Ulaya, Marekani na Asia.

    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo 🇨🇩, Felix Tshisekedi ameitaka Nchi ya Marekani 🇺🇸 kununua madini moja kwa moja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiitaja ndio "mmiliki halisi" wa rasilimali hizo na sio Nchi Rwanda 🇷🇼. Tshisekedi amesema kuwa anaanza kwa kutoa ofa hiyo kwa Marekani kwanza huku akitoa pendekezo hilo pia liko wazi kwa mataifa ya Umoja Ulaya (EU) na wanunuzi wengine wanaotafuta na kununua madini kutoka Nchini Rwanda kwa sasa. Rais huyo amewaonya Mataifa yanayonunua madini kutoka Nchini Rwanda kuwa wanachukua madini yaliyoibwa kutoka Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, kwahiyo wanatakiwa kununua kwa mmiliki halali. Ikumbukwe kwamba Nchi ya Rwanda ni moja ya kati ya Nchi zinauza madini mengi barani Afrika kwa Mataifa ya Ulaya, Marekani na Asia.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·151 Views
  • Mkuu wa Muungano wa Waasi ikiwemo Kundi la M23, Corneille Nangaa amesema kuwa kama Nchi ya TChad itakubali ombi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo la kutuma Jeshi lake Nchini DR Congo, itakuwa ni uhaini kama ilivyo kwa Rais wa DR Congo Félix Tshisekedi.

    Nandaa ameimbia Tchad iachane na mpango huo kwasababu watakuwa wamefanya kosa kubwa maana wakifanya hivyo wajiandae kupokea Wanajeshi wake wakiwa wamepoteza maisha (wamekufa)

    Mkuu wa Muungano wa Waasi ikiwemo Kundi la M23, Corneille Nangaa amesema kuwa kama Nchi ya TChad 🇹🇩 itakubali ombi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 la kutuma Jeshi lake Nchini DR Congo, itakuwa ni uhaini kama ilivyo kwa Rais wa DR Congo Félix Tshisekedi. Nandaa ameimbia Tchad iachane na mpango huo kwasababu watakuwa wamefanya kosa kubwa maana wakifanya hivyo wajiandae kupokea Wanajeshi wake wakiwa wamepoteza maisha (wamekufa)
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·202 Views
  • HAKUNA MUHIMU ZAIDI YA HURUMA...

    Tunaishi katika ulimwengu unaotukuza mafanikio. Ulimwengu ambamo kazi zinaabudiwa, utajiri unaheshimiwa, akili inasifiwa, na hadhi inafuatiliwa kwa shauku isiyokoma. Lakini mwisho, tunapovua vyeo, ​​digrii, akaunti za benki, na marupurupu, ni nini kinachobaki? Ni nini hasa kinatufafanua? Si sifa tulizopata, wala mali tulizojilimbikizia, wala si nguvu tulizo nazo. Hapana, kipimo cha kweli cha mtu ni jinsi alivyohisi kwa undani wengine. Hakuna, hakuna kitu, ni muhimu zaidi kuliko huruma kwa mateso ya mwanadamu mwingine. Sio kazi yako, sio utajiri wako, sio akili yako, na hakika sio hali yako. Mambo haya ni ya kupita; hunyauka kama majani chini ya jua kali. Lakini huruma, uwezo wa kumtazama mwanadamu mwingine na kuhisi maumivu yake kana kwamba ni yako mwenyewe, ni ya milele. Siku hizi, tunasikia mengi kuhusu upendo. Upendo kwa wanadamu, upendo kwa wasio na upendeleo, upendo kwa wanaoteseka. Lakini acheni tusimame kwa muda na kujiuliza: Upendo ni nini ikiwa hauonyeshwa kwa vitendo? Mapenzi ambayo yanasalia kuwa tangazo tu, hotuba iliyobuniwa kwa uzuri, au chapisho la mitandao ya kijamii lililoandikwa kwa werevu ni unafiki tu. Ni unyongovu, onyesho tupu, la kujitolea la wema ambalo halimaanishi chochote unapokabiliwa na mateso halisi ya mwanadamu.

    Kwangu mimi, upendo wa kweli lazima uonekane. Ni lazima usikike. Ni lazima uonekane. Neno la fadhili ni zuri, lakini haliwezi kulisha mtoto mwenye njaa. Kupumua kwa huruma ni heshima, lakini hakuwezi kuwaweka wasio na makazi. Tweet iliyotungwa vyema kuhusu mshikamano haimaanishi chochote ikiwa tutapita mateso bila kujali. Tunaishi katika zama za unafiki mkubwa. Wakati ambapo watu huchangisha fedha kwa ajili ya maskini huku wakiwadharau mioyoni mwao. Wakati ambapo watu huzungumza kwa ufasaha kuhusu mapenzi huku wakiwakanyaga wengine ili kupanda ngazi ya mafanikio. Wakati ambapo watu hutabasamu hadharani lakini wanasaliti faraghani. Ikiwa tutaishi kwa heshima, ikiwa tunataka kuhifadhi asili ya ubinadamu, lazima tuache unafiki huu. Ni lazima tuache kudai upendo huku tukifanya ubinafsi. Ni lazima tuache kuhubiri wema huku tukitembea katika ukatili. Lazima tuache kupiga makofi kwa hisani hadharani huku tukipuuza mateso kwa faragha. Huruma sio huruma. Huruma inasimama kwa mbali na kusema, "Ninajisikia vibaya kwako." Huruma hupiga magoti kando ya mateso na kusema, “Maumivu yako ni maumivu yangu. Machozi yako ni machozi yangu.” Uelewa ndio unaotufanya kuwa wanadamu. Ndiyo unaotenganisha upendo na utendaji, wema na utangazaji, na unyoofu na unafiki. Jamii isiyo na huruma ni msitu, ambapo ni wenye nguvu pekee wanaosalia, na wanyonge huangamia kimya.

    Kwa maana mwisho, tunaposimama mbele ya Muumba, hatatuuliza tulipata kiasi gani, tulipanda juu kiasi gani, au tulipata umaarufu gani. Atatuuliza, “Je, ulipenda? Je, ulijali? Uliwahurumia wanadamu wenzako?” Tusisubiri siku hiyo ndio tujibu. Wacha maisha yetu yawe jibu.
    HAKUNA MUHIMU ZAIDI YA HURUMA... Tunaishi katika ulimwengu unaotukuza mafanikio. Ulimwengu ambamo kazi zinaabudiwa, utajiri unaheshimiwa, akili inasifiwa, na hadhi inafuatiliwa kwa shauku isiyokoma. Lakini mwisho, tunapovua vyeo, ​​digrii, akaunti za benki, na marupurupu, ni nini kinachobaki? Ni nini hasa kinatufafanua? Si sifa tulizopata, wala mali tulizojilimbikizia, wala si nguvu tulizo nazo. Hapana, kipimo cha kweli cha mtu ni jinsi alivyohisi kwa undani wengine. Hakuna, hakuna kitu, ni muhimu zaidi kuliko huruma kwa mateso ya mwanadamu mwingine. Sio kazi yako, sio utajiri wako, sio akili yako, na hakika sio hali yako. Mambo haya ni ya kupita; hunyauka kama majani chini ya jua kali. Lakini huruma, uwezo wa kumtazama mwanadamu mwingine na kuhisi maumivu yake kana kwamba ni yako mwenyewe, ni ya milele. Siku hizi, tunasikia mengi kuhusu upendo. Upendo kwa wanadamu, upendo kwa wasio na upendeleo, upendo kwa wanaoteseka. Lakini acheni tusimame kwa muda na kujiuliza: Upendo ni nini ikiwa hauonyeshwa kwa vitendo? Mapenzi ambayo yanasalia kuwa tangazo tu, hotuba iliyobuniwa kwa uzuri, au chapisho la mitandao ya kijamii lililoandikwa kwa werevu ni unafiki tu. Ni unyongovu, onyesho tupu, la kujitolea la wema ambalo halimaanishi chochote unapokabiliwa na mateso halisi ya mwanadamu. Kwangu mimi, upendo wa kweli lazima uonekane. Ni lazima usikike. Ni lazima uonekane. Neno la fadhili ni zuri, lakini haliwezi kulisha mtoto mwenye njaa. Kupumua kwa huruma ni heshima, lakini hakuwezi kuwaweka wasio na makazi. Tweet iliyotungwa vyema kuhusu mshikamano haimaanishi chochote ikiwa tutapita mateso bila kujali. Tunaishi katika zama za unafiki mkubwa. Wakati ambapo watu huchangisha fedha kwa ajili ya maskini huku wakiwadharau mioyoni mwao. Wakati ambapo watu huzungumza kwa ufasaha kuhusu mapenzi huku wakiwakanyaga wengine ili kupanda ngazi ya mafanikio. Wakati ambapo watu hutabasamu hadharani lakini wanasaliti faraghani. Ikiwa tutaishi kwa heshima, ikiwa tunataka kuhifadhi asili ya ubinadamu, lazima tuache unafiki huu. Ni lazima tuache kudai upendo huku tukifanya ubinafsi. Ni lazima tuache kuhubiri wema huku tukitembea katika ukatili. Lazima tuache kupiga makofi kwa hisani hadharani huku tukipuuza mateso kwa faragha. Huruma sio huruma. Huruma inasimama kwa mbali na kusema, "Ninajisikia vibaya kwako." Huruma hupiga magoti kando ya mateso na kusema, “Maumivu yako ni maumivu yangu. Machozi yako ni machozi yangu.” Uelewa ndio unaotufanya kuwa wanadamu. Ndiyo unaotenganisha upendo na utendaji, wema na utangazaji, na unyoofu na unafiki. Jamii isiyo na huruma ni msitu, ambapo ni wenye nguvu pekee wanaosalia, na wanyonge huangamia kimya. Kwa maana mwisho, tunaposimama mbele ya Muumba, hatatuuliza tulipata kiasi gani, tulipanda juu kiasi gani, au tulipata umaarufu gani. Atatuuliza, “Je, ulipenda? Je, ulijali? Uliwahurumia wanadamu wenzako?” Tusisubiri siku hiyo ndio tujibu. Wacha maisha yetu yawe jibu.
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·451 Views
  • Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeomba msaada wa kijeshi kutoka Nchini Chad katika jitihada zake za kupambana na Waasi wa kundi la M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda . Waziri anayeshughulikia masuala ya kikanda wa DR Congo alikutana na Rais wa Chad, Mahamat Idriss Deby Itno, Jumanne akimuwakilisha Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi, kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Rais wa Chad na kusasishwa kwenye wa mtandao wa Facebook.

    Maelezo ya kina ya mazungumzo yao hajawekwa wazi. Mmoja wa Maafisa wa Chad anayeyefahamu mazungumzo hayo alisema Chad inalibeba ombi la kuombwa msaada na DR Congo, lakini bado haijafanya maamuzi kuhusu ombi hilo. Chanzo kutoka Ofisi ya Rais DR Congo C kimeiambia BBC kuwa kuwa Nchi hiyo imeomba msaada wa kijeshi na kidiplomasia kutoka Nchini Chad.

    Hata hivyo chanzo hicho ambacho hakijataka kutambulishwa kwa sababu za ndani, hakijatoa maelezo zaidi. Msemaji wa Serikali ya Chad, Gassim Cherif, hakujibu ombi la kutoa maoni yake kuhusu hili, kwa mujibu wa Reuters. Kwa upande wake, Msemaji wa Rais Tshisekedi, Tina Salama, alisema hana taarifa yoyote kuhusu suala hilo.

    Wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad aliiambia Reuters kuwa kupeleka msaada wa kijeshi DR Congo ni "taarifa za tetesi" bado haijathibitishwa rasmi.
    (BBC)

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 imeomba msaada wa kijeshi kutoka Nchini Chad 🇹🇩 katika jitihada zake za kupambana na Waasi wa kundi la M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda 🇷🇼. Waziri anayeshughulikia masuala ya kikanda wa DR Congo alikutana na Rais wa Chad, Mahamat Idriss Deby Itno, Jumanne akimuwakilisha Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi, kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Rais wa Chad na kusasishwa kwenye wa mtandao wa Facebook. Maelezo ya kina ya mazungumzo yao hajawekwa wazi. Mmoja wa Maafisa wa Chad anayeyefahamu mazungumzo hayo alisema Chad inalibeba ombi la kuombwa msaada na DR Congo, lakini bado haijafanya maamuzi kuhusu ombi hilo. Chanzo kutoka Ofisi ya Rais DR Congo C kimeiambia BBC kuwa kuwa Nchi hiyo imeomba msaada wa kijeshi na kidiplomasia kutoka Nchini Chad. Hata hivyo chanzo hicho ambacho hakijataka kutambulishwa kwa sababu za ndani, hakijatoa maelezo zaidi. Msemaji wa Serikali ya Chad, Gassim Cherif, hakujibu ombi la kutoa maoni yake kuhusu hili, kwa mujibu wa Reuters. Kwa upande wake, Msemaji wa Rais Tshisekedi, Tina Salama, alisema hana taarifa yoyote kuhusu suala hilo. Wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad aliiambia Reuters kuwa kupeleka msaada wa kijeshi DR Congo ni "taarifa za tetesi" bado haijathibitishwa rasmi. (BBC)
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·323 Views
  • 10. DAMASCUS

    Sauli wa Tarso (ambaye baadaye alikuja kuwa Paulo) ndiye mtu anayekuja akilini kwa mara ya kwanza mtu anapofikiria Damasko.

    Ilikuwa ni njiani pale alipokutana na Kristo.

    Ajabu alikuwa njiani kuwatesa Wakristo kutoka Kanisa la kwanza.

    Katika Matendo sura ya 9 inasema, “Ikawa alipokuwa akienda zake, akikaribia Dameski, ghafula nuru kutoka mbinguni ilimwangazia pande zote.” Alianguka chini na kupoteza uwezo wake wa kuona. Sauli aliongoka baadaye na kuwa mmoja wa watetezi wa Kristo wenye shauku zaidi.
    10. DAMASCUS Sauli wa Tarso (ambaye baadaye alikuja kuwa Paulo) ndiye mtu anayekuja akilini kwa mara ya kwanza mtu anapofikiria Damasko. Ilikuwa ni njiani pale alipokutana na Kristo. Ajabu alikuwa njiani kuwatesa Wakristo kutoka Kanisa la kwanza. Katika Matendo sura ya 9 inasema, “Ikawa alipokuwa akienda zake, akikaribia Dameski, ghafula nuru kutoka mbinguni ilimwangazia pande zote.” Alianguka chini na kupoteza uwezo wake wa kuona. Sauli aliongoka baadaye na kuwa mmoja wa watetezi wa Kristo wenye shauku zaidi.
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·252 Views
More Results