Upgrade to Pro

  • Yule Mwamba kasimama
    Yule Mwamba kasimama 🤔
    Like
    3
    1 Comments ·30 Views
  • Nadhani hii Sasa Imevuka kwenye Quality .......

    Khalid Aucho anaweza akawa siyo yule tena in terms of Physically lakin Whenever Aucho is in the Pitch Yanga Africans are safe .

    -Akili ya Mpira
    -Composure
    -Technical Ability
    -Game Passing

    Huyu Mganda anatawala sana Dimba la kati ...Hilal wana watu wagumu na wana kasi lakin Fundi alikua anaokota moja moja pakihitajika Kuvunja kuni anavunja kweli kweli ...

    Juzi Kuna Mashabiki Kutoka Uganda Walicomment kwenye post yake wakimtakia kheri na mechi bora wakaenda mbali zaidi na Kusema ,

    "Tunaomba walau nusu ya Kiwango chako Ndani ya Yanga Sc utuonyeshe Ukiwa na timu yetu ya Uganda Cranes "

    Wanamtambua kama moja ya Viungo bora ambao wamewahi Kuwashuhudia .....Binafsi huyu ni Kipimo halisi cha Kiungo wa Chini au holding Mid ndani ya Ligi yetu .

    THE TANK FOR REASON .

    #neliudcosiah
    Nadhani hii Sasa Imevuka kwenye Quality ....... Khalid Aucho anaweza akawa siyo yule tena in terms of Physically lakin Whenever Aucho is in the Pitch Yanga Africans are safe 🤝. -Akili ya Mpira -Composure -Technical Ability -Game Passing Huyu Mganda anatawala sana Dimba la kati ...Hilal wana watu wagumu na wana kasi lakin Fundi alikua anaokota moja moja pakihitajika Kuvunja kuni anavunja kweli kweli ... Juzi Kuna Mashabiki Kutoka Uganda Walicomment kwenye post yake wakimtakia kheri na mechi bora wakaenda mbali zaidi na Kusema , "Tunaomba walau nusu ya Kiwango chako Ndani ya Yanga Sc utuonyeshe Ukiwa na timu yetu ya Uganda Cranes " Wanamtambua kama moja ya Viungo bora ambao wamewahi Kuwashuhudia .....Binafsi huyu ni Kipimo halisi cha Kiungo wa Chini au holding Mid ndani ya Ligi yetu . THE TANK FOR REASON ✅. #neliudcosiah
    Like
    1
    ·75 Views
  • MOYO SAFI WA SADIO MANÉ NDIO SILAHA YA MAFANIKIO YAKE.

    Sadio Mané amesaidia mambo mengi sana katika Kijiji alichotoka mara Baada ya kupata mafanikio katika soka.

    Sadio Mané amezaliwa katika Kijiji Cha Bambali nchini Senegal,amekulia huko na wanakijiji wengi walimsapoti na kumuombea sana Dua za mafanikio kipindi anaenda rasmi ulaya kujaribu bahati yake katika kazi ya kucheza mpira wa miguu.

    Mungu Si Athumani wala Mzee Nkumilwa kijana akatoboa na maisha yakaanza kuwa safi kwa upande wake,lakini pamoja na yote hakuwasahau watu waliomfanya awe hapo Leo.

    Alianza kukata fungu kwenye Kila mshahara wake wa mwezi kwa ajili ya kusaidia Kijiji chake kutoka kuwa Cha kimasikini mpaka kuwa Cha maisha ya kati kabla ya kuwa Cha kitajiri kabisa.

    Baadae zile pesa alizokuwa anahifadhi kutoka kwenye Kila mshahara wake zilianza kufanya kazi vyema na kufanikisha kukamklisha vitu vifuatavyo:

    1. Alijenga hospital yenye thamani ya €530K sawa na pesa za kitanzania Billion Moja,million mia tatu sabini na mbili,laki tano na Elfu tisini na nne.

    2. Alijenga Shule yenye thamani ya €270K sawa na pesa za kitanzania Million mia sita tisa tisa,laki mbili na Elfu Arobaini na sita.

    3. Pia huwa anatoa kiasi Cha €70 Kwa Kila kaya iliyopo Katika Kijiji hicho kwa mwezi ambayo ni sawa na pesa za kitanzania Laki moja,Elfu themanini na Moja,mia mbili themanini na sita.

    4. Kutoa nguo za bure Kwa watoto wote waliopo ndani ya Kijiji hicho.

    5. Kufanikisha kupeleka internet yenye Kasi ya 4G katika Kijiji hicho.

    6. Kufanikisha kupeleka vituo vya gas katika Kijiji hicho akishirikiana na kampuni ya Oryx.

    7. Kajenga uwanja wa soka pia.

    NDIO MAANA ANAFANIKIWA KILA ANAPOENDA HATA KAMA AKISEMEWA MABAYA KUNA WENGI WAPO NYUMA YAKE WANAMUOMBEA MEMA

    #neliudcosiah
    MOYO SAFI WA SADIO MANÉ NDIO SILAHA YA MAFANIKIO YAKE. Sadio Mané amesaidia mambo mengi sana katika Kijiji alichotoka mara Baada ya kupata mafanikio katika soka. Sadio Mané amezaliwa katika Kijiji Cha Bambali nchini Senegal,amekulia huko na wanakijiji wengi walimsapoti na kumuombea sana Dua za mafanikio kipindi anaenda rasmi ulaya kujaribu bahati yake katika kazi ya kucheza mpira wa miguu. Mungu Si Athumani wala Mzee Nkumilwa kijana akatoboa na maisha yakaanza kuwa safi kwa upande wake,lakini pamoja na yote hakuwasahau watu waliomfanya awe hapo Leo. Alianza kukata fungu kwenye Kila mshahara wake wa mwezi kwa ajili ya kusaidia Kijiji chake kutoka kuwa Cha kimasikini mpaka kuwa Cha maisha ya kati kabla ya kuwa Cha kitajiri kabisa. Baadae zile pesa alizokuwa anahifadhi kutoka kwenye Kila mshahara wake zilianza kufanya kazi vyema na kufanikisha kukamklisha vitu vifuatavyo: 1. Alijenga hospital yenye thamani ya €530K sawa na pesa za kitanzania Billion Moja,million mia tatu sabini na mbili,laki tano na Elfu tisini na nne. 2. Alijenga Shule yenye thamani ya €270K sawa na pesa za kitanzania Million mia sita tisa tisa,laki mbili na Elfu Arobaini na sita. 3. Pia huwa anatoa kiasi Cha €70 Kwa Kila kaya iliyopo Katika Kijiji hicho kwa mwezi ambayo ni sawa na pesa za kitanzania Laki moja,Elfu themanini na Moja,mia mbili themanini na sita. 4. Kutoa nguo za bure Kwa watoto wote waliopo ndani ya Kijiji hicho. 5. Kufanikisha kupeleka internet yenye Kasi ya 4G katika Kijiji hicho. 6. Kufanikisha kupeleka vituo vya gas katika Kijiji hicho akishirikiana na kampuni ya Oryx. 7. Kajenga uwanja wa soka pia. NDIO MAANA ANAFANIKIWA KILA ANAPOENDA HATA KAMA AKISEMEWA MABAYA KUNA WENGI WAPO NYUMA YAKE WANAMUOMBEA MEMA ♥️📌 #neliudcosiah
    Like
    1
    ·100 Views
  • "SPACE SHUTTLE AU ORBITER " CHOMBO KINACHO KWENDA MWENDO MKALI MARA TISA ZAIDI YA RISASI NA MARA ISHIRINI YA SPIDI YA SAUTI "

    > Hiki chombo kina mwendo mkali, mara 9 zaidi ya risasi au mara20 ya spidi ya sauti pindi kinapotoka hapa duniani.

    Hapa tunaongelea chombo cha anga za mbali au kile kiendacho nje ya dunia. "Space shuttle" au "Orbiter" ambayo ni aina ya ndege maalum.

    "HAPO AWALI"

    Nakumbuka baadhi yetu tulipokuwa tunaona chombo kinapita umbali wa juu huku kikiacha moshi mweupe nyuma tunasema "rocket" lakini leo tunafahamu kuwa ile ni ndege ya kawaida ya abiria na ule moshi mweupe tunao uona nyuma ni matokeo ya kukutana hewa yenye joto itokayo kenye injini na hali ya hewa ya baridi iliyopo usawa ule ambapo "condensation trail" vikikutana vinaganda na kutengeneza lile wingu moshi tulionalo nyuma.
    wanasema hata mawingu yanapatikana kwa njia inayofanana kidogo na hiyo, Kwa mujibu wa wataalam.
    (kumbuka pia hata 'rocket' ina tabia ya kuacha moshi nyuma pale inapokuwa imewashwa).

    "UZITO"

    Chombo hiki 'space shuttle' mara nyingi huwa kinabeba wataalam mbalimbali wa masuala ya anga za juu "Astronauts", vifaa mbalimbali vya ujenzi wa maabara ya nje ya dunia, spare, satelite n.k
    Pia kinabeba hewa yake yenyewe ya oxygen kwasababu ya uhai wa watu waliomo ndani kwaajili ya kuendesha injini zake kinapokuwa nje ya dunia kwasababu huko hakuna hewa."vacuum space"
    Mara nyingi kinafikia jumla ya uzito wa hadi tani 2000 au kg 2,000,000 pindi kinapoondoka hapa duniani.

    "NGUVU"

    Chombo hiki kimeundwa na injini tatu lakini kinaongezewa injini mbili za ziada "Solid Rocket Booster" 'SRB' na ndiyo jina la rocket lilipozaliwa, (picha chini inaonesha rocket booster hizo mbili nyeupe) ambazo ndani hubeba mafuta ya aina yake.

    Lakini pia inabeba tank kubwa la mafuta tumboni lenye rangi ya Orange, ambalo nalo linabeba mamilioni ya lita za mafuta ambayo yote huwa yanaisha ndani ya dakika8 tangu ikianza safari.

    Kutokana na uzito na umbali wa safari yake kwa ujumla injini hizo mbili za Solid Rocket Booster "SRB" zinazalisha nguvu kufikia horse power million44 au linganisha nguvu ya vichwa vya train 14,000.

    Rocket injini hizi na tank la mafuta zikifika umbali fulani hujiachia na kurudi duniani hasa pale yanapoisha mafuta yake na kukiacha chombo kinaendelea chenyewe na injini zake ambapo kinakuwa kimefikishwa umbali ambao hakihitaji tena nguvu kubwa.

    Umbali wa kufikia anga za huko kwenye "Space" au anga za mbali uanzia kilometa 100 kutoka hapa duniani kwenda angani wanasema wataalam wa mambo ya anga.

    "MWENDO"

    Wakati kinawashwa kuondoka kutoka katika sehemu yake "launch pad" ndani ya dakika 8 huwa kinafikia mwendo wa 25000 M/hr au 40,000 k/hr hivyo kufanya kwenda kasi mara9 zaidi ya risasi au mara10 ya kasi ya sauti.
    Mwendo wa sauti ni zaidi ya 1200 k/h.

    "GHARAMA"

    Chombo hiki huwa akiruki mara kwa mara isipokuwa kwa misheni maalum tu.
    Mara nyingi, mara moja kwa miezi miwili au zaidi ya hapo.

    NASA ambao ndiyo Mamlaka ya Usafiri wa Anga za karibu na mbali huko Marekani ndiyo wahusika wakuu kwenye kurusha chombo hiki.

    Pia alikuwa anarusha Mrusi na kuna taarifa za Mchina pia alikuwa na program ya kwenda.

    Marekani ameviita majina vyombo hivyo,
    >Enteprise-kimestaafu zamani
    >Colombia-kilipata ajali kikaua wote
    >Discovery-2011
    >Atlantis-2011
    >Endeavour- 2011 kiliziba nafasi ya challenger
    >Challenge-kilipata ajali kikaua wote

    Mrusi aliita
    >Buran-na kilienda safari moja tu.

    Gharama waliyotoa NASA mwaka 2011 kurusha chombo hiki kwa safari moja ni sawa na bei ya kununua Boeing 787 Dreamliner mbili hadi Tano inategemea na misheni husika.
    Tukumbuke pia sio kila "rocket launch" roketi inayorushwa ni lazima ihusishe chombo hiki, zipo misheni nyengine za anga za mbali ambazo zinapeleka mizigo tu kama satelite n.k pasipo kuwemo watu katika chombo na huwa kinaendeshwa kwa remote control.
    "SPACE SHUTTLE AU ORBITER " CHOMBO KINACHO KWENDA MWENDO MKALI MARA TISA ZAIDI YA RISASI NA MARA ISHIRINI YA SPIDI YA SAUTI " > Hiki chombo kina mwendo mkali, mara 9 zaidi ya risasi au mara20 ya spidi ya sauti pindi kinapotoka hapa duniani. Hapa tunaongelea chombo cha anga za mbali au kile kiendacho nje ya dunia. "Space shuttle" au "Orbiter" ambayo ni aina ya ndege maalum. "HAPO AWALI" Nakumbuka baadhi yetu tulipokuwa tunaona chombo kinapita umbali wa juu huku kikiacha moshi mweupe nyuma tunasema "rocket" lakini leo tunafahamu kuwa ile ni ndege ya kawaida ya abiria na ule moshi mweupe tunao uona nyuma ni matokeo ya kukutana hewa yenye joto itokayo kenye injini na hali ya hewa ya baridi iliyopo usawa ule ambapo "condensation trail" vikikutana vinaganda na kutengeneza lile wingu moshi tulionalo nyuma. wanasema hata mawingu yanapatikana kwa njia inayofanana kidogo na hiyo, Kwa mujibu wa wataalam. (kumbuka pia hata 'rocket' ina tabia ya kuacha moshi nyuma pale inapokuwa imewashwa). "UZITO" Chombo hiki 'space shuttle' mara nyingi huwa kinabeba wataalam mbalimbali wa masuala ya anga za juu "Astronauts", vifaa mbalimbali vya ujenzi wa maabara ya nje ya dunia, spare, satelite n.k Pia kinabeba hewa yake yenyewe ya oxygen kwasababu ya uhai wa watu waliomo ndani kwaajili ya kuendesha injini zake kinapokuwa nje ya dunia kwasababu huko hakuna hewa."vacuum space" Mara nyingi kinafikia jumla ya uzito wa hadi tani 2000 au kg 2,000,000 pindi kinapoondoka hapa duniani. "NGUVU" Chombo hiki kimeundwa na injini tatu lakini kinaongezewa injini mbili za ziada "Solid Rocket Booster" 'SRB' na ndiyo jina la rocket lilipozaliwa, (picha chini inaonesha rocket booster hizo mbili nyeupe) ambazo ndani hubeba mafuta ya aina yake. Lakini pia inabeba tank kubwa la mafuta tumboni lenye rangi ya Orange, ambalo nalo linabeba mamilioni ya lita za mafuta ambayo yote huwa yanaisha ndani ya dakika8 tangu ikianza safari. Kutokana na uzito na umbali wa safari yake kwa ujumla injini hizo mbili za Solid Rocket Booster "SRB" zinazalisha nguvu kufikia horse power million44 au linganisha nguvu ya vichwa vya train 14,000. Rocket injini hizi na tank la mafuta zikifika umbali fulani hujiachia na kurudi duniani hasa pale yanapoisha mafuta yake na kukiacha chombo kinaendelea chenyewe na injini zake ambapo kinakuwa kimefikishwa umbali ambao hakihitaji tena nguvu kubwa. Umbali wa kufikia anga za huko kwenye "Space" au anga za mbali uanzia kilometa 100 kutoka hapa duniani kwenda angani wanasema wataalam wa mambo ya anga. "MWENDO" Wakati kinawashwa kuondoka kutoka katika sehemu yake "launch pad" ndani ya dakika 8 huwa kinafikia mwendo wa 25000 M/hr au 40,000 k/hr hivyo kufanya kwenda kasi mara9 zaidi ya risasi au mara10 ya kasi ya sauti. Mwendo wa sauti ni zaidi ya 1200 k/h. "GHARAMA" Chombo hiki huwa akiruki mara kwa mara isipokuwa kwa misheni maalum tu. Mara nyingi, mara moja kwa miezi miwili au zaidi ya hapo. NASA ambao ndiyo Mamlaka ya Usafiri wa Anga za karibu na mbali huko Marekani ndiyo wahusika wakuu kwenye kurusha chombo hiki. Pia alikuwa anarusha Mrusi na kuna taarifa za Mchina pia alikuwa na program ya kwenda. Marekani ameviita majina vyombo hivyo, >Enteprise-kimestaafu zamani >Colombia-kilipata ajali kikaua wote >Discovery-2011 >Atlantis-2011 >Endeavour- 2011 kiliziba nafasi ya challenger >Challenge-kilipata ajali kikaua wote Mrusi aliita >Buran-na kilienda safari moja tu. Gharama waliyotoa NASA mwaka 2011 kurusha chombo hiki kwa safari moja ni sawa na bei ya kununua Boeing 787 Dreamliner mbili hadi Tano inategemea na misheni husika. Tukumbuke pia sio kila "rocket launch" roketi inayorushwa ni lazima ihusishe chombo hiki, zipo misheni nyengine za anga za mbali ambazo zinapeleka mizigo tu kama satelite n.k pasipo kuwemo watu katika chombo na huwa kinaendeshwa kwa remote control.
    ·177 Views
  • DUNIA NA MAAJABU YAKE
    (Muundo wa Dunia na Maajabu Yaliyomo)

    1. UMRI WA DUNIA

    HII Dunia yetu ina historia ndefu mno tangu ilipojiunda angani, miaka takribani bilioni 4.5 iliyopita.

    Tarakimu za umri huo wa miaka bilioni 4.5 ni 4,500,000,000, yaani miaka milioni elfu nne na mia tano iliyopita.

    Dunia ambayo kwa lugha ya Kiingereza inafahamika vyema kwa jina la 'Earth', pia hujulikana kama 'the World', ikimaanishwa ulimwengu.

    Aidha, Dunia ni sayari pekee kwenye himaya ya sayari zilizopo chini ya jua ambayo jina lake halitokani na majina ya "Miungu wa Dola" ya Kigiriki au ya Kirumi.

    Asili ya jina la 'earth' ni 'erde' lenye asili ya nchini Ujerumani, na maana yake ni udongo au ardhi.

    Mpaka kuweza kupata umri huo wa dunia wanasayansi walifanya kazi ya kutafiti na kisha kuwasilisha matokeo yao kwenye makongamano ya kisayansi duniani, ambapo matokeo hayo yalijadiliwa kwa kina na hatimaye kukubalika kama hivi.

    Kumbuka katika majadiliano hayo huwepo mivutano mikali miongoni mwa wanasayansi waalikwa, ambapo pia jopo la wanasayansi wanaowasilisha utafiti husika hujikuta wakitakiwa kujibu hoja mbalimbali za wanasayansi wenzao.

    Kuna wakati baadhi ya matokeo ya tafiti kadhaa hukataliwa, huku watafiti husika wakitakiwa kurejea upya tafiti zao.

    Wanasayansi hupata umri wa sayari kwa kupima umri wa miamba ya sayari husika, ambapo mwamba wenye umri mkubwa zaidi kuliko miamba yote ndiyo huchukuliwa kuwa umri wa sayari husika.

    Itakumbukwa kuwa Msahafu wa Biblia (Sura ya Mwanzo 1) husimulia jinsi Mwenyezi Mungu alivyoumba "mbingu na nchi na vyote vilivyomo kwa siku 6," lakini pia Msahafu huohuo kwenye aya zingine hueleza kuwa miaka elfu moja ya duniani yaweza kuwa sawa na siku moja kwenye ya Makazi ya Mwenyezi Mungu.

    Ni dhahiri kuwa binadamu tukiwa hatuna hoja sahihi kwa maelezo ya aina hiyo, ndipo tunaona ni vyema mambo ya Mwenyezi Mungu kumwachia Yeye Mwenyewe Mwenyezi Mungu.

    2. KUUMBIKA DUNIA, SAYARI, JUA, NYOTA

    Kimsingi, Dunia kama zilivyo sayari zingine zote ilijiunda kutokana na mabaki ya vitu vilivyotumika kuunda Jua.

    Jua ambalo ni nyota kama zilivyo nyota zote angani, lilijiunda lenyewe kwenye eneo la anga lijulikanalo kama 'Pillars of Creation' (nguzo za uumbaji) katika ukanda wa anga wenye upana ambao huonekana kutokuwa na mwisho.

    Ukanda huo ujulikanao kama 'Solar Nebula,' umegubikwa na mawingu ya vumbi la huko angani pamoja na aina mbalimbali za gesi na hewa, ikiwemo haidrojeni na heliumu.

    'Solar' ni jina la nishati itokanayo na joto la jua, na 'Nebula' kwa lugha ya Kilatini ni "wingu" au vumbi la gesi asilia mithili ya ukungu.

    Hivyo, 'Solar Nebula' ni ukanda katika anga ya mbali wenye mawingu yaliyosheheni nishati yenye joto, sawa na nishati ya joto la jua.

    Sasa basi, tunafahamu vyema kuwa jua hutoa mionzi hatari yenye joto kali mithili ya moto mkali, na ambayo ikiboreshwa kisayansi pia huweza kutoa nishati ya umeme.

    Hivyo, kwa muktadha huo, hebu ngoja sasa tuleta pamoja hewa za gesi, zikiwemo haidrojeni na heliumu, mawingu yenye nishati ya umeme wa jua, vumbi la angani na tufani itokanayo na mchafuko mbaya wa hali ya hewa huko anga za mbali.

    Na ili kuweza kupata matokeo yanayotakiwa, hebu pia tutambue uwepo wa nguvu kubwa ya asili katika kiwango kijulikanacho kwa jina la "Supernatural Power", ambayo ndiyo huwa kisababishi cha mambo yote.

    Kisayansi, "Supernatural Power" ni nguvu kubwa ya asili ambayo huendesha mifumo mbalimbali ya asili, ambapo duniani nguvu hiyo hujulikana kama Nguvu ya Mungu.

    Nguvu asili hiyo, yaani Supernatural Power, husababisha tufani ambayo huvurumisha kwa pamoja vitu vyote hivyo, (gesi, hewa, mawingu yenye nishati ya joto na vumbi la angani) ili kuunda tufani yenye umbo la duara.

    Duara hiyo ni kama ile itokanayo na kimbunga kikali duniani, na ambacho sasa tutaona kikifungamanisha pamoja vitu vyote hivyo katika mchafuko mkubwa wa hali mbaya ya hewa.

    Natumia maneno ya msisitizo kuelezea "ukubwa" wa mchafuko huo wa hali ya hewa katika eneo hilo la anga, kwani katika kuunda sayari au nyota nguvuasili kubwa hutumika.

    Aidha, tufani hiyo ya duara itakayoanza kidogo kidogo kama kimbunga kikali, itazidi kukua hadi kuwa na kipenyo cha takribani kilomita 10 hadi 200 au zaidi na kwendelea.

    Tufani hiyo ndiyo itavurumisha kwa pamoja gesi na hewa za naitrojeni na heliumu, mawingu ya nishati ya joto na vumbi la angani (kama kifanyavyo kimbunga kikali katika eneo tambarare la duniani).

    Pia, wakati mchafuko huo wa hali mbaya ya hewa ukiendelea, hebu ngoja sisi watazamaji tujibanze mahali fulani kwa mbali kushuhudia duara hiyo ya tufani ikijizungusha yenyewe bila kukoma kwa kipindi cha miaka mingi.

    Kitakachofuata ni kuanza kuona kiini cha moto kikianza kujiunda katikati ya duara hiyo ya tufani kali, huku pia nje ya duara hiyo vitu kibao vikivutwa kujiunga na mzunguko wa hiyo tufani ya duara.

    Vitu hivyo ni pamoja na vumbi zaidi la angani, na gesi zaidi zenye joto kali.

    Wakati huohuo kipenyo na mzingo wa duara hiyo vitazidi kuongezeka upana na ukubwa, mfano wa duara yenye umbo sawa na la mpira mkubwa wa miguu.

    Hivyo, baada ya miaka takribani milioni moja tutashangaa kuona lile vumbi likigeuka taratibu kuwa miamba ya moto ndani ya kiini cha tufani hiyo ya duara.

    Miamba hiyo ni kutokana na lile vumbi la angani ambalo hatimaye limeshikamana pamoja mithili ya zege, na hatimaye kuwa miamba ndani ya tufani ya duara.

    Sanjari na kuundika huko ndani ya kitovu cha hiyo tufani ya duara, pia kwelekea nje ya duara hiyo utaundika udongo ambao ardhi, mchanga na mawe.

    Kimsingi, vitu hivyo pia ni matokeo ya lile vumbi la angani ambalo lilikusanywa pamoja na kuvutwa na kasi ya mzunguko wa tufani.

    Hatua hiyo mpya inatokana na kuwepo mshikamano na mgandamizo wa zile chembechembe za lile vumbivumbi ndani ya tufani.

    Vurumai hiyo ya mzunguko wa hiyo tufani ya duara yenye vumbi, itazidi kukua hadi kuunda sumaku ya asili ndani ya kile kitovu cha duara ya tufani.

    Kutokana na duara hiyo ya tufani kuongezeka ukubwa, hatimaye sumaku iliyopo kwenye kitovu cha duara hiyo itaishiwa nguvu ya kwendelea kunasa vumbi zaidi kuja kwenye mzingo wa hiyo duara ya tufani.

    Kumbuka kuwa wakati huo hiyo duara pia itaunda kimo kutoka kwenye usawa wa ardhi yake kwenda ndani kwenye kitovu chake, na hivyo kuwa duara ya mviringo kama umbo mfano wa mpira mchezo wa miguu.

    Baada ya kupita maelfu ya miaka mingi, duara hiyo ambayo hapo awali ilianza kama umbo la tufani na kuzidi kukua huko angani, sasa itakuwa na joto kali kupita kiasi na kuanza kung'aa kama jua.

    Jua hilo, ndiyo nyota mojawapo ya zile ambazo huonekana usiku ziking'aa angani.

    Lakini pia wakati wa kujiunda nyota hiyo, kama tulivyoona hapo awali, baadhi ya mabaki yake yaliyokuwa yakitawanyika angani wakati ile tufani ya duara ikijizungusha, huweza kujikusanya pamoja na kuunda sayari ambazo huzunguka baadhi ya hizo nyota.

    Hivyo ndivyo zilivyojiunda sayari zote ambazo huelea kwa kulizunguka jua letu.

    Mathalani, sayari zote ambazo hulizunguka jua, ikiwemo dunia zilijiunda kutokana na mabaki ya vitu kama gesi, michanga na mawe ambavyo vilitawanyika angani wakati jua likijiunda (kama ambavyo imeelezwa hapo awali).

    3. KIINI CHA DUNIA

    Dunia yetu ambayo wastani wa nusu kipenyo cha umbo lake la duara ni kilomita 6,371, mzingo wake ni kilomita takribani 40,041.

    Kama zilivyo sayari zote katika himaya ya jua, dunia nayo ilijiunda wakati jua likijiunda lenyewe.

    Yaani kwamba sayari ni mabaki ya vitu vilivyotumika kuliunda jua.

    Kadhalika kama zilivyo sayari zingine zote, dunia nayo ina kiini chake ambacho kipo katikati ya ardhi yake.

    Kiini hicho kina nguvu kubwa ya sumaku ambayo, pamoja na mambo mengineyo, 'huvuta' umbo hilo la duara kutoka juu ya ardhi kwenda katikati ya kiini hicho.

    Muundo huo ndio hulifungamanisha pamoja umbo la duara la dunia, na hivyo kuzuia umbo hilo lisifumke kutoka ardhini na kusambaratika.

    Hiyo ni sawa na mpira wa miguu unavyoweza kupasuka na kusambaratika, kama utajazwa upepo kupita kiasi chake.

    Kiini hicho ambacho kipo katikati kabisa ya dunia, kinajulikanacho kwa jina la kisayansi la 'Inner Core.'

    Kiini hicho kina joto kali la sentigredi 6,230 ambacho ndio kiasi cha joto la jua.

    Kiini hicho kina umbo la duara lenye nusu kipenyo cha kilomita 1,250.

    Kama ingetokea kuchimba ardhi wima kwenda kwenye kiini hicho, mchimbaji angeanza kukutana na joto la kiini hicho kuanzia kimo cha umbali wa kilomita 5,150 kutoka usawa wa juu ya ardhi tunayotembea.

    Katika historia ya uchimbaji ardhi, kina kirefu kilichowahi kuchimbwa ardhini ni mita 12,345 (kilomita 12.345) huko Sakhalini, nchini Urusi, kwa ajili ya uvunaji wa mafuta ya petroli.

    Kiini cha dunia kinaundwa na madini mchanganyiko wa nikeli (nickle), chuma (iron) na dhahabu.

    Kwa mujibu wa utafiti, inakadiriwa kuwa kama dhahabu hiyo ingechimbwa na kuchomwa mpaka kuwa kimiminika sawa na uji na kisha kumwagwa chini, ingeweza kuifunika dunia yote kwa unene wa sentimeta 45.

    Kiini hicho muhimu kwa uhai wa sayari hii ya dunia kiligunduliwa mwaka 1936 na mtaalamu wa matetemeko ya ardhi wa nchini Denmark, mwanamama Dkt. Inge Lehmann.

    Dkt. Lehmann alihitimu shahada yake ya kwanza katika fani ya Hisabati mwaka 1910, ya Uzamili mwaka 1920 (zote kutoka Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini mwake), na ile ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza.

    Alifariki kwa uzee mwaka 1993 akiwa na umri wa miaka 104.

    4. MAJI DUNIANI

    Kupatikana maji kwenye dunia yetu, ni mojawapo ya miundo ambayo haipo katika sayari zingine ambazo tuna taarifa za kitafiti kuzuhusu.

    Maji ni muhimili muhimu kwa ajili ya uhai wa viumbe wote na mimea, ambavyo kwa pamoja havipo katika sayari zingine za himaya ya jua.

    Kwa mujibu wa tafiti nyingi ambazo zimefanyika kwa miongo mingi ya miaka kujaribu kubaini nini chanzo cha kuwepo maji duniani, hakuna hata utafiti mmoja ulioonesha kwa usahihi matokeo ya kuridhisha.

    Miongoni mwa tafiti hizo ni pamoja na ule wa mwaka 2005, ambapo Mkuu wa Idara ya Masomo ya Sayari na Mwezi katika Chuo Kikuu cha Arizona nchini Marekani, Profesa Michael Julian Drake, na mwenzake ambaye ni mtaalamu wa Vimondo, Dkt. Huberto Campins, wa Chuo Kikuu cha Central Florida, walitafiti nini chanzo cha kuwepo maji duniani.

    Katika mawasilisho yao kwenye kongamano la kisayansi la Chama cha Wanataaluma wa Maarifa ya Anga za Juu (IAU), watafiti hao walikanusha madai ya uwezekano wa dunia hapo kale kugongwa na kimondo kikubwa na kusababisha maji kulipuka kutoka ardhini.

    Wakiwasilisha matokeo ya utafiti wao kwenye mkutano wa kongamano hilo, magwiji hao wa masuala ya sayari walieleza kwenye waraka wao uitwao "Origin of water on the terrestial planets" (chanzo cha kuwepo maji kwenye sayari).

    Walidai kuwa maji yaliyopo duniani yaliumbika kwenye ardhi ya dunia tangu mwanzo, wakati ikijiunda angani.

    Ikumbukwe kuwa eneo la uso wa dunia likiwa ni jumla ya kilomita za mraba milioni 510, asilimia 70.8 ya eneo hilo imefunikwa na maji na asilimia 29.2 ni nchi kavu, ikiwemo milima, mabonde na ardhi tambarare.

    5. HEWA YA OKSIJENI

    Muundo mwingine muhimu katika sayari hii ya dunia ni hewa ambazo ni tawala, yaani Naitrojeni ambayo kwa usahihi imeenea kwa asilimia 78.08 ya hewa yote ya dunia, Oksijeni asilimia 20.95, 'Argon' asilimia 0.93, hewa ya Ukaa (Carbon dioxide) asilimia 0.039, na asilimia moja ni hewa mithili ya mvuke wa maji (water vapour).

    Hewa ya Oksijeni ambayo ni nguzo muhimu kwa ajili ya uhai wa viumbe wote na pia haipatikani kwenye sayari nyingine chini ya jua, inadhaniwa ilianza kupatikana duniani miaka takribani bilioni 2.5 iliyopita kufuatia "kukomaa kwa kiini cha dunia."

    Kwa mujibu wa matokeo ya tafiti mbalimbali na nadharia za kisayansi, inaoneshwa kuwa kukomaa kwa kiini hicho cha dunia hatimaye ndiko kulisababisha kuzuka duniani milipuko ya volikano ambayo pia ilisababisha kuzuka mabonde na milima.

    Inaoneshwa kuwa tayari wakati huo maji yaliishakuwepo duniani, na kuwezesha kuzuka chembechembe ndogo sana za kibakteria zijulikanazo kwa jina la kisayansi la 'cyanobacteria' au 'blue-green algae'.

    Kwa kutumia mwanga wa jua, maji na hewa ya ukaa, chembechembe hizo ziliweza kuzalisha hewa mbalimbali, ikiwemo 'Carbonhydrates' na Oksijeni.

    Kwa kuwa hizo chembechembe ndogo za kibakteria huishi baharini, ilikuwa rahisi kwa oksijeni kutokea baharini kupepea na kuenea katika anga ya dunia na kuzuiliwa hapo na nguvu asili ya uvutano ya dunia ili pia ibaki ikienea pote duniani.

    Mpaka wakati wa kuzuka duniani mimea na viumbe hai miaka takribani bilioni 3.5 iliyopita, tayari oksijeni ilikwa ni tele duniani; na hivyo kutumika kudumisha uhai wa viumbe hadi wakati huu.

    6. UKANDA WA 'OZONE'

    Muundo mwingie muhimu wa asili kwa dunia ni ukanda wa anga ujulikanao kwa jina la 'ozone' ambao umetanda kama 'mwavuli' kwenye anga ya dunia, na kuikinga isidhuriwe na mionzi hatari ya sumu kutoka kwenye Jua.

    Ukanda huo maarufu kama 'ozone layer' umetanda kuanzia usawa wa kilometa 15 kutoka ardhini kwenda juu angani mpaka ukomo wa kilomita takribani 50, ambapo huchuja asilimia kati ya 97 na 99 ya mionzi hatari kwenye miale ya joto la jua.

    Miongoni mwa matatizo yanayosababishwa na mionzi hiyo hatari kutoka kwenye jua, ni pamoja na magonjwa ya saratani ya ngozi kwa bianadamu.

    Pia juu ya ukanda wa tabaka la ozone kuna ukanda mwingine uitwao "atmosphere" ambao ni madhubuti kiasi kwamba vitu vinavyotoka anga za juu na kujaribu kuupenya ili kufika duniani, hukumbana na joto kali na kusambaratishwa kwa kuunguzwa.

    Si kwamba tabaka hilo lina joto, isipokuwa kasi ya "kuanguka" vitu hivyo kutoka juu angani kuja dunia husababisha msuguano na chembechembe za gesi katika eneo hilo na kuzalisha joto mithili ya ndimi za moto.

    Picha za video za vyombo vya 'Apollo' vikirejea duniani kutoka mwezini vikiwa na wanaanga ndani yake na kupenya tabaka hilo kwa kasi ya kilomita 39,000 kwa saa, huonekana kughubikwa na ndimi za moto wa rangi ya njano na bluu.

    Rangi hizo ni ishara ya ukali wa moto huo, lakini kutokana na waundaji wa vyombo hivyo kutumia mchanganyiko wa mabati na plastiki ngumu visivyopenywa na joto, Apollo huonekana kulichana tabaka hilo na kutokea upande wa pili ambao ni anga ya dunia.

    Hivyo basi, mfano huo mdogo unaonesha uimara wa tabaka hilo la 'ozone', ambalo kama ambavyo tumeona huchuja mionzi ya sumu kutoka kwenye mwanga wa jua ili kutolete madhara kwa viumbe duniani.

    Mwanga huo ukisafiri kutoka juani umbali wa kilomita milioni 150 kwa kasi ya kilomita 299,793, hutua duniani ndani ya dakika 8 na sekunde 19 ukiwa tayari umechujwa wakati ukipenya tabaka hilo.

    'Ozone' iligunduliwa mwaka 1913 na wanasayansi wawili wa nchini Ufaransa, Charlest Fabry na Henri Buisson, ambapo kipimo cha kasi ya mwanga kiligunduliwa na mwanasayansia wa anga za juu wa nchini Denmark, Ole Roemer, mwaka 1676.

    7. NGUVU ASILI YA UVUTANO

    Muundo mwingine wa dunia ni nguvu ya asili ya uvutano ya dunia, maarufu kama 'gravitation', ambayo huvuta vitu kuvirejesha chini duniani pale vinaporushwa kwenda juu au vile vinavyoanguka kutoka juu angani.

    Nguvu hiyo ina manufaa makubwa, kwani bila kuwepo duniani binadamu na viumbe wengine wangepeperuka kama karatasi kwenda juu wakati wakitembea juu ya ardhi ya hii.

    Kadhalika, nguvu hiyo husaidia kuvuta hewa ya oksijeni na kuiweka karibu na ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

    Pia, nguvu hiyo husaidia kuiweka dunia, mwezi, jua na sayari zingine katika uwiano wa umbali usio na madhara kutoka kila moja.

    Nguvu hiyo ya asili ndiyo huliweka joto la jua duniani na kubaki kuwa katika kiwango kinachotakiwa, na hivyo kuwezesha viumbe kupata joto la wastani na pia katika kiwango mwanana.

    Nguvu hiyo huvuta mvua kuja duniani na kuwezesha maji ya bahari, maziwa na mito kutulia duniani.

    Mathalani, bila nguvu asili hiyo kuwepo duniani, maji 'yangemwagika' kutoka duniani kwa kutawanyika kama upepo na kupaa kwenda juu angani na kutoweka kabisa.

    Na ndio maana ukirusha maji kwenda juu, hurudi chini ardhini.

    Hebu angalia mfano huu kwamba wanaanga waliokwenda mwenzini walilazimika kuvaa mavazi yenye uzito wa kilo 80 hapa duniani, lakini mavazi hayo kule mwezini yakawa na uzito wa kilo 3.

    Mavazi hayo, yaani viatu, koti, suruali, na kofia nzito yenye miwani maalumu ya kukinga macho dhidi ya mionzi hatari ya jua, vyote kwa pamoja viliunganishwa na kuwa mfano wa sare za 'ovaroli' za mafundi wa magari.

    Mavazi hayo pia mgongoni yakiwa yameunganishwa kwa pamoja na mtungi wa hewa ya oksijeni kwa ajili ya kupumua, yalivaaliwa mahsusi muda mfupi baada ya chombo kutua mwezini.

    Hivyo, msomaji wangu tafakari nini kilisababisha mavazi kuwa mazito hapa duniani, lakini yawe mepesi kule mwezini?

    Jibu ni kwamba nguvu asili ya uvutano hapa duniani ni kubwa kuliko ya kule mwezini.

    Na ndipo tunaona umuhimu wa muundo huo wa nguvu asili ya uvutano, ambapo hapa duniani huvuta vitu kuja chini kwa kasi ya mita 9.81 kwa sekunde, lakini kwa kuwa nguvu ya mwezi ni hafifu, huvuta vitu kwa kasi ndogo ya mita 1.62 kwa sekunde.

    Ingawa nguvu hiyo ya asili iligunduliwa kuwepo duniani miaka mingi iliyopta, mwanafizikia bingwa wa Uingereza, Sir Isaac Newton (1642-1727), ndiye anatambulika kama mgunduzi wa hesabu hizo za nguvu asili hiyo.

    Anaeleza kuwa vitu vyote vyenye maumbo asili, ikiwemo jua, sayari, dunia, mwezi, na vimondo, kila kimoja kina nguvu hiyo katika viwango tofauti.

    Kanuni hiyo, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wake, hueleza kuwa nguvu hiyo ndiyo hufanya jua kuvuta sayari zake ili kulizunguka, huku pia kila sayari ikitumia nguvu 'binafsi' (na kwa uwiano maalumu) kujihami isivutwe hadi kwenda kuligonga jua au kugongana na sayari zingine au vimondo.

    Nguvuasili ya jua ni mita 274 kwa sekunde, ikiwa ni zaidi ya kiasi cha nguvuasili ya kila sayari.

    Muundo huo wa kila sayari kujihami kivyake katika mstari wa njia yake hufahamika kisayansi kama "sayari kuhami mazingira ya njia yake"; yaani kwamba 'a planet has to clear the neighbourhood around its orbit.'

    Newton akiwa amezaliwa 'mtoto-njiti' na baadaye kuibuka kuwa mwenye akili nyingi kiasi cha kukaribia kuwa sawa na mtu wa miujiza, hakuwahi kuoa kutokana na kinachoelezwa kuwa ni " kutokana na kutingwa na shughuli za kimasomo."

    Huoneshwa kuwa muda mwingi alikuwa maabara akifanya tafiti mbalimbali za kisayansi, au akiwa maktaba akijisomea, ama akiandika kitabu, au akifundisha wanafunzi wake.

    Alikuwa bingwa mwenye kipaji cha taaluma nyingi, ikiwemo Fizikia, Kemia, Hisabati, Maarifa ya Anga za Juu, Uchumi, Falsafa, na Theolojia ambayo ni taaluma ya masuala ya kiroho.

    Kwa mujibu wa historia, mwanasayansi huyo gwiji wa kuigwa alihitimu shahada zake zote mbili za sayansi, yaani 'Bachelor' na 'Masters', mwaka 1665 na 1668 katika Chuo Kikuu cha Cambridge, nchini Uingereza.

    Akiwa na umri wa miaka 84, mwanasayansi huyo anayedhaniwa na wengi kuwa bingwa wa hesabu za kisayansi kuliko wote duniani, alifariki mwaka 1727 akiwa usingizini.

    Ripoti ya uchunguzi wa mwili wake huonesha kuwa alikuwa na tatizo la figo, lakini pia alikutwa na kiasi kingi cha zebaki.

    Zebaki hiyo, yamkini, ni kutokana na kudumu mno kwenye maabara za Kemia na Fizikia, ambazo hutumia kemikali aina mbalimbali, zikiwemo hewa za gesi, katika kufanya majaribio ya kisayansi.
    DUNIA NA MAAJABU YAKE (Muundo wa Dunia na Maajabu Yaliyomo) 1. UMRI WA DUNIA HII Dunia yetu ina historia ndefu mno tangu ilipojiunda angani, miaka takribani bilioni 4.5 iliyopita. Tarakimu za umri huo wa miaka bilioni 4.5 ni 4,500,000,000, yaani miaka milioni elfu nne na mia tano iliyopita. Dunia ambayo kwa lugha ya Kiingereza inafahamika vyema kwa jina la 'Earth', pia hujulikana kama 'the World', ikimaanishwa ulimwengu. Aidha, Dunia ni sayari pekee kwenye himaya ya sayari zilizopo chini ya jua ambayo jina lake halitokani na majina ya "Miungu wa Dola" ya Kigiriki au ya Kirumi. Asili ya jina la 'earth' ni 'erde' lenye asili ya nchini Ujerumani, na maana yake ni udongo au ardhi. Mpaka kuweza kupata umri huo wa dunia wanasayansi walifanya kazi ya kutafiti na kisha kuwasilisha matokeo yao kwenye makongamano ya kisayansi duniani, ambapo matokeo hayo yalijadiliwa kwa kina na hatimaye kukubalika kama hivi. Kumbuka katika majadiliano hayo huwepo mivutano mikali miongoni mwa wanasayansi waalikwa, ambapo pia jopo la wanasayansi wanaowasilisha utafiti husika hujikuta wakitakiwa kujibu hoja mbalimbali za wanasayansi wenzao. Kuna wakati baadhi ya matokeo ya tafiti kadhaa hukataliwa, huku watafiti husika wakitakiwa kurejea upya tafiti zao. Wanasayansi hupata umri wa sayari kwa kupima umri wa miamba ya sayari husika, ambapo mwamba wenye umri mkubwa zaidi kuliko miamba yote ndiyo huchukuliwa kuwa umri wa sayari husika. Itakumbukwa kuwa Msahafu wa Biblia (Sura ya Mwanzo 1) husimulia jinsi Mwenyezi Mungu alivyoumba "mbingu na nchi na vyote vilivyomo kwa siku 6," lakini pia Msahafu huohuo kwenye aya zingine hueleza kuwa miaka elfu moja ya duniani yaweza kuwa sawa na siku moja kwenye ya Makazi ya Mwenyezi Mungu. Ni dhahiri kuwa binadamu tukiwa hatuna hoja sahihi kwa maelezo ya aina hiyo, ndipo tunaona ni vyema mambo ya Mwenyezi Mungu kumwachia Yeye Mwenyewe Mwenyezi Mungu. 2. KUUMBIKA DUNIA, SAYARI, JUA, NYOTA Kimsingi, Dunia kama zilivyo sayari zingine zote ilijiunda kutokana na mabaki ya vitu vilivyotumika kuunda Jua. Jua ambalo ni nyota kama zilivyo nyota zote angani, lilijiunda lenyewe kwenye eneo la anga lijulikanalo kama 'Pillars of Creation' (nguzo za uumbaji) katika ukanda wa anga wenye upana ambao huonekana kutokuwa na mwisho. Ukanda huo ujulikanao kama 'Solar Nebula,' umegubikwa na mawingu ya vumbi la huko angani pamoja na aina mbalimbali za gesi na hewa, ikiwemo haidrojeni na heliumu. 'Solar' ni jina la nishati itokanayo na joto la jua, na 'Nebula' kwa lugha ya Kilatini ni "wingu" au vumbi la gesi asilia mithili ya ukungu. Hivyo, 'Solar Nebula' ni ukanda katika anga ya mbali wenye mawingu yaliyosheheni nishati yenye joto, sawa na nishati ya joto la jua. Sasa basi, tunafahamu vyema kuwa jua hutoa mionzi hatari yenye joto kali mithili ya moto mkali, na ambayo ikiboreshwa kisayansi pia huweza kutoa nishati ya umeme. Hivyo, kwa muktadha huo, hebu ngoja sasa tuleta pamoja hewa za gesi, zikiwemo haidrojeni na heliumu, mawingu yenye nishati ya umeme wa jua, vumbi la angani na tufani itokanayo na mchafuko mbaya wa hali ya hewa huko anga za mbali. Na ili kuweza kupata matokeo yanayotakiwa, hebu pia tutambue uwepo wa nguvu kubwa ya asili katika kiwango kijulikanacho kwa jina la "Supernatural Power", ambayo ndiyo huwa kisababishi cha mambo yote. Kisayansi, "Supernatural Power" ni nguvu kubwa ya asili ambayo huendesha mifumo mbalimbali ya asili, ambapo duniani nguvu hiyo hujulikana kama Nguvu ya Mungu. Nguvu asili hiyo, yaani Supernatural Power, husababisha tufani ambayo huvurumisha kwa pamoja vitu vyote hivyo, (gesi, hewa, mawingu yenye nishati ya joto na vumbi la angani) ili kuunda tufani yenye umbo la duara. Duara hiyo ni kama ile itokanayo na kimbunga kikali duniani, na ambacho sasa tutaona kikifungamanisha pamoja vitu vyote hivyo katika mchafuko mkubwa wa hali mbaya ya hewa. Natumia maneno ya msisitizo kuelezea "ukubwa" wa mchafuko huo wa hali ya hewa katika eneo hilo la anga, kwani katika kuunda sayari au nyota nguvuasili kubwa hutumika. Aidha, tufani hiyo ya duara itakayoanza kidogo kidogo kama kimbunga kikali, itazidi kukua hadi kuwa na kipenyo cha takribani kilomita 10 hadi 200 au zaidi na kwendelea. Tufani hiyo ndiyo itavurumisha kwa pamoja gesi na hewa za naitrojeni na heliumu, mawingu ya nishati ya joto na vumbi la angani (kama kifanyavyo kimbunga kikali katika eneo tambarare la duniani). Pia, wakati mchafuko huo wa hali mbaya ya hewa ukiendelea, hebu ngoja sisi watazamaji tujibanze mahali fulani kwa mbali kushuhudia duara hiyo ya tufani ikijizungusha yenyewe bila kukoma kwa kipindi cha miaka mingi. Kitakachofuata ni kuanza kuona kiini cha moto kikianza kujiunda katikati ya duara hiyo ya tufani kali, huku pia nje ya duara hiyo vitu kibao vikivutwa kujiunga na mzunguko wa hiyo tufani ya duara. Vitu hivyo ni pamoja na vumbi zaidi la angani, na gesi zaidi zenye joto kali. Wakati huohuo kipenyo na mzingo wa duara hiyo vitazidi kuongezeka upana na ukubwa, mfano wa duara yenye umbo sawa na la mpira mkubwa wa miguu. Hivyo, baada ya miaka takribani milioni moja tutashangaa kuona lile vumbi likigeuka taratibu kuwa miamba ya moto ndani ya kiini cha tufani hiyo ya duara. Miamba hiyo ni kutokana na lile vumbi la angani ambalo hatimaye limeshikamana pamoja mithili ya zege, na hatimaye kuwa miamba ndani ya tufani ya duara. Sanjari na kuundika huko ndani ya kitovu cha hiyo tufani ya duara, pia kwelekea nje ya duara hiyo utaundika udongo ambao ardhi, mchanga na mawe. Kimsingi, vitu hivyo pia ni matokeo ya lile vumbi la angani ambalo lilikusanywa pamoja na kuvutwa na kasi ya mzunguko wa tufani. Hatua hiyo mpya inatokana na kuwepo mshikamano na mgandamizo wa zile chembechembe za lile vumbivumbi ndani ya tufani. Vurumai hiyo ya mzunguko wa hiyo tufani ya duara yenye vumbi, itazidi kukua hadi kuunda sumaku ya asili ndani ya kile kitovu cha duara ya tufani. Kutokana na duara hiyo ya tufani kuongezeka ukubwa, hatimaye sumaku iliyopo kwenye kitovu cha duara hiyo itaishiwa nguvu ya kwendelea kunasa vumbi zaidi kuja kwenye mzingo wa hiyo duara ya tufani. Kumbuka kuwa wakati huo hiyo duara pia itaunda kimo kutoka kwenye usawa wa ardhi yake kwenda ndani kwenye kitovu chake, na hivyo kuwa duara ya mviringo kama umbo mfano wa mpira mchezo wa miguu. Baada ya kupita maelfu ya miaka mingi, duara hiyo ambayo hapo awali ilianza kama umbo la tufani na kuzidi kukua huko angani, sasa itakuwa na joto kali kupita kiasi na kuanza kung'aa kama jua. Jua hilo, ndiyo nyota mojawapo ya zile ambazo huonekana usiku ziking'aa angani. Lakini pia wakati wa kujiunda nyota hiyo, kama tulivyoona hapo awali, baadhi ya mabaki yake yaliyokuwa yakitawanyika angani wakati ile tufani ya duara ikijizungusha, huweza kujikusanya pamoja na kuunda sayari ambazo huzunguka baadhi ya hizo nyota. Hivyo ndivyo zilivyojiunda sayari zote ambazo huelea kwa kulizunguka jua letu. Mathalani, sayari zote ambazo hulizunguka jua, ikiwemo dunia zilijiunda kutokana na mabaki ya vitu kama gesi, michanga na mawe ambavyo vilitawanyika angani wakati jua likijiunda (kama ambavyo imeelezwa hapo awali). 3. KIINI CHA DUNIA Dunia yetu ambayo wastani wa nusu kipenyo cha umbo lake la duara ni kilomita 6,371, mzingo wake ni kilomita takribani 40,041. Kama zilivyo sayari zote katika himaya ya jua, dunia nayo ilijiunda wakati jua likijiunda lenyewe. Yaani kwamba sayari ni mabaki ya vitu vilivyotumika kuliunda jua. Kadhalika kama zilivyo sayari zingine zote, dunia nayo ina kiini chake ambacho kipo katikati ya ardhi yake. Kiini hicho kina nguvu kubwa ya sumaku ambayo, pamoja na mambo mengineyo, 'huvuta' umbo hilo la duara kutoka juu ya ardhi kwenda katikati ya kiini hicho. Muundo huo ndio hulifungamanisha pamoja umbo la duara la dunia, na hivyo kuzuia umbo hilo lisifumke kutoka ardhini na kusambaratika. Hiyo ni sawa na mpira wa miguu unavyoweza kupasuka na kusambaratika, kama utajazwa upepo kupita kiasi chake. Kiini hicho ambacho kipo katikati kabisa ya dunia, kinajulikanacho kwa jina la kisayansi la 'Inner Core.' Kiini hicho kina joto kali la sentigredi 6,230 ambacho ndio kiasi cha joto la jua. Kiini hicho kina umbo la duara lenye nusu kipenyo cha kilomita 1,250. Kama ingetokea kuchimba ardhi wima kwenda kwenye kiini hicho, mchimbaji angeanza kukutana na joto la kiini hicho kuanzia kimo cha umbali wa kilomita 5,150 kutoka usawa wa juu ya ardhi tunayotembea. Katika historia ya uchimbaji ardhi, kina kirefu kilichowahi kuchimbwa ardhini ni mita 12,345 (kilomita 12.345) huko Sakhalini, nchini Urusi, kwa ajili ya uvunaji wa mafuta ya petroli. Kiini cha dunia kinaundwa na madini mchanganyiko wa nikeli (nickle), chuma (iron) na dhahabu. Kwa mujibu wa utafiti, inakadiriwa kuwa kama dhahabu hiyo ingechimbwa na kuchomwa mpaka kuwa kimiminika sawa na uji na kisha kumwagwa chini, ingeweza kuifunika dunia yote kwa unene wa sentimeta 45. Kiini hicho muhimu kwa uhai wa sayari hii ya dunia kiligunduliwa mwaka 1936 na mtaalamu wa matetemeko ya ardhi wa nchini Denmark, mwanamama Dkt. Inge Lehmann. Dkt. Lehmann alihitimu shahada yake ya kwanza katika fani ya Hisabati mwaka 1910, ya Uzamili mwaka 1920 (zote kutoka Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini mwake), na ile ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza. Alifariki kwa uzee mwaka 1993 akiwa na umri wa miaka 104. 4. MAJI DUNIANI Kupatikana maji kwenye dunia yetu, ni mojawapo ya miundo ambayo haipo katika sayari zingine ambazo tuna taarifa za kitafiti kuzuhusu. Maji ni muhimili muhimu kwa ajili ya uhai wa viumbe wote na mimea, ambavyo kwa pamoja havipo katika sayari zingine za himaya ya jua. Kwa mujibu wa tafiti nyingi ambazo zimefanyika kwa miongo mingi ya miaka kujaribu kubaini nini chanzo cha kuwepo maji duniani, hakuna hata utafiti mmoja ulioonesha kwa usahihi matokeo ya kuridhisha. Miongoni mwa tafiti hizo ni pamoja na ule wa mwaka 2005, ambapo Mkuu wa Idara ya Masomo ya Sayari na Mwezi katika Chuo Kikuu cha Arizona nchini Marekani, Profesa Michael Julian Drake, na mwenzake ambaye ni mtaalamu wa Vimondo, Dkt. Huberto Campins, wa Chuo Kikuu cha Central Florida, walitafiti nini chanzo cha kuwepo maji duniani. Katika mawasilisho yao kwenye kongamano la kisayansi la Chama cha Wanataaluma wa Maarifa ya Anga za Juu (IAU), watafiti hao walikanusha madai ya uwezekano wa dunia hapo kale kugongwa na kimondo kikubwa na kusababisha maji kulipuka kutoka ardhini. Wakiwasilisha matokeo ya utafiti wao kwenye mkutano wa kongamano hilo, magwiji hao wa masuala ya sayari walieleza kwenye waraka wao uitwao "Origin of water on the terrestial planets" (chanzo cha kuwepo maji kwenye sayari). Walidai kuwa maji yaliyopo duniani yaliumbika kwenye ardhi ya dunia tangu mwanzo, wakati ikijiunda angani. Ikumbukwe kuwa eneo la uso wa dunia likiwa ni jumla ya kilomita za mraba milioni 510, asilimia 70.8 ya eneo hilo imefunikwa na maji na asilimia 29.2 ni nchi kavu, ikiwemo milima, mabonde na ardhi tambarare. 5. HEWA YA OKSIJENI Muundo mwingine muhimu katika sayari hii ya dunia ni hewa ambazo ni tawala, yaani Naitrojeni ambayo kwa usahihi imeenea kwa asilimia 78.08 ya hewa yote ya dunia, Oksijeni asilimia 20.95, 'Argon' asilimia 0.93, hewa ya Ukaa (Carbon dioxide) asilimia 0.039, na asilimia moja ni hewa mithili ya mvuke wa maji (water vapour). Hewa ya Oksijeni ambayo ni nguzo muhimu kwa ajili ya uhai wa viumbe wote na pia haipatikani kwenye sayari nyingine chini ya jua, inadhaniwa ilianza kupatikana duniani miaka takribani bilioni 2.5 iliyopita kufuatia "kukomaa kwa kiini cha dunia." Kwa mujibu wa matokeo ya tafiti mbalimbali na nadharia za kisayansi, inaoneshwa kuwa kukomaa kwa kiini hicho cha dunia hatimaye ndiko kulisababisha kuzuka duniani milipuko ya volikano ambayo pia ilisababisha kuzuka mabonde na milima. Inaoneshwa kuwa tayari wakati huo maji yaliishakuwepo duniani, na kuwezesha kuzuka chembechembe ndogo sana za kibakteria zijulikanazo kwa jina la kisayansi la 'cyanobacteria' au 'blue-green algae'. Kwa kutumia mwanga wa jua, maji na hewa ya ukaa, chembechembe hizo ziliweza kuzalisha hewa mbalimbali, ikiwemo 'Carbonhydrates' na Oksijeni. Kwa kuwa hizo chembechembe ndogo za kibakteria huishi baharini, ilikuwa rahisi kwa oksijeni kutokea baharini kupepea na kuenea katika anga ya dunia na kuzuiliwa hapo na nguvu asili ya uvutano ya dunia ili pia ibaki ikienea pote duniani. Mpaka wakati wa kuzuka duniani mimea na viumbe hai miaka takribani bilioni 3.5 iliyopita, tayari oksijeni ilikwa ni tele duniani; na hivyo kutumika kudumisha uhai wa viumbe hadi wakati huu. 6. UKANDA WA 'OZONE' Muundo mwingie muhimu wa asili kwa dunia ni ukanda wa anga ujulikanao kwa jina la 'ozone' ambao umetanda kama 'mwavuli' kwenye anga ya dunia, na kuikinga isidhuriwe na mionzi hatari ya sumu kutoka kwenye Jua. Ukanda huo maarufu kama 'ozone layer' umetanda kuanzia usawa wa kilometa 15 kutoka ardhini kwenda juu angani mpaka ukomo wa kilomita takribani 50, ambapo huchuja asilimia kati ya 97 na 99 ya mionzi hatari kwenye miale ya joto la jua. Miongoni mwa matatizo yanayosababishwa na mionzi hiyo hatari kutoka kwenye jua, ni pamoja na magonjwa ya saratani ya ngozi kwa bianadamu. Pia juu ya ukanda wa tabaka la ozone kuna ukanda mwingine uitwao "atmosphere" ambao ni madhubuti kiasi kwamba vitu vinavyotoka anga za juu na kujaribu kuupenya ili kufika duniani, hukumbana na joto kali na kusambaratishwa kwa kuunguzwa. Si kwamba tabaka hilo lina joto, isipokuwa kasi ya "kuanguka" vitu hivyo kutoka juu angani kuja dunia husababisha msuguano na chembechembe za gesi katika eneo hilo na kuzalisha joto mithili ya ndimi za moto. Picha za video za vyombo vya 'Apollo' vikirejea duniani kutoka mwezini vikiwa na wanaanga ndani yake na kupenya tabaka hilo kwa kasi ya kilomita 39,000 kwa saa, huonekana kughubikwa na ndimi za moto wa rangi ya njano na bluu. Rangi hizo ni ishara ya ukali wa moto huo, lakini kutokana na waundaji wa vyombo hivyo kutumia mchanganyiko wa mabati na plastiki ngumu visivyopenywa na joto, Apollo huonekana kulichana tabaka hilo na kutokea upande wa pili ambao ni anga ya dunia. Hivyo basi, mfano huo mdogo unaonesha uimara wa tabaka hilo la 'ozone', ambalo kama ambavyo tumeona huchuja mionzi ya sumu kutoka kwenye mwanga wa jua ili kutolete madhara kwa viumbe duniani. Mwanga huo ukisafiri kutoka juani umbali wa kilomita milioni 150 kwa kasi ya kilomita 299,793, hutua duniani ndani ya dakika 8 na sekunde 19 ukiwa tayari umechujwa wakati ukipenya tabaka hilo. 'Ozone' iligunduliwa mwaka 1913 na wanasayansi wawili wa nchini Ufaransa, Charlest Fabry na Henri Buisson, ambapo kipimo cha kasi ya mwanga kiligunduliwa na mwanasayansia wa anga za juu wa nchini Denmark, Ole Roemer, mwaka 1676. 7. NGUVU ASILI YA UVUTANO Muundo mwingine wa dunia ni nguvu ya asili ya uvutano ya dunia, maarufu kama 'gravitation', ambayo huvuta vitu kuvirejesha chini duniani pale vinaporushwa kwenda juu au vile vinavyoanguka kutoka juu angani. Nguvu hiyo ina manufaa makubwa, kwani bila kuwepo duniani binadamu na viumbe wengine wangepeperuka kama karatasi kwenda juu wakati wakitembea juu ya ardhi ya hii. Kadhalika, nguvu hiyo husaidia kuvuta hewa ya oksijeni na kuiweka karibu na ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Pia, nguvu hiyo husaidia kuiweka dunia, mwezi, jua na sayari zingine katika uwiano wa umbali usio na madhara kutoka kila moja. Nguvu hiyo ya asili ndiyo huliweka joto la jua duniani na kubaki kuwa katika kiwango kinachotakiwa, na hivyo kuwezesha viumbe kupata joto la wastani na pia katika kiwango mwanana. Nguvu hiyo huvuta mvua kuja duniani na kuwezesha maji ya bahari, maziwa na mito kutulia duniani. Mathalani, bila nguvu asili hiyo kuwepo duniani, maji 'yangemwagika' kutoka duniani kwa kutawanyika kama upepo na kupaa kwenda juu angani na kutoweka kabisa. Na ndio maana ukirusha maji kwenda juu, hurudi chini ardhini. Hebu angalia mfano huu kwamba wanaanga waliokwenda mwenzini walilazimika kuvaa mavazi yenye uzito wa kilo 80 hapa duniani, lakini mavazi hayo kule mwezini yakawa na uzito wa kilo 3. Mavazi hayo, yaani viatu, koti, suruali, na kofia nzito yenye miwani maalumu ya kukinga macho dhidi ya mionzi hatari ya jua, vyote kwa pamoja viliunganishwa na kuwa mfano wa sare za 'ovaroli' za mafundi wa magari. Mavazi hayo pia mgongoni yakiwa yameunganishwa kwa pamoja na mtungi wa hewa ya oksijeni kwa ajili ya kupumua, yalivaaliwa mahsusi muda mfupi baada ya chombo kutua mwezini. Hivyo, msomaji wangu tafakari nini kilisababisha mavazi kuwa mazito hapa duniani, lakini yawe mepesi kule mwezini? Jibu ni kwamba nguvu asili ya uvutano hapa duniani ni kubwa kuliko ya kule mwezini. Na ndipo tunaona umuhimu wa muundo huo wa nguvu asili ya uvutano, ambapo hapa duniani huvuta vitu kuja chini kwa kasi ya mita 9.81 kwa sekunde, lakini kwa kuwa nguvu ya mwezi ni hafifu, huvuta vitu kwa kasi ndogo ya mita 1.62 kwa sekunde. Ingawa nguvu hiyo ya asili iligunduliwa kuwepo duniani miaka mingi iliyopta, mwanafizikia bingwa wa Uingereza, Sir Isaac Newton (1642-1727), ndiye anatambulika kama mgunduzi wa hesabu hizo za nguvu asili hiyo. Anaeleza kuwa vitu vyote vyenye maumbo asili, ikiwemo jua, sayari, dunia, mwezi, na vimondo, kila kimoja kina nguvu hiyo katika viwango tofauti. Kanuni hiyo, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wake, hueleza kuwa nguvu hiyo ndiyo hufanya jua kuvuta sayari zake ili kulizunguka, huku pia kila sayari ikitumia nguvu 'binafsi' (na kwa uwiano maalumu) kujihami isivutwe hadi kwenda kuligonga jua au kugongana na sayari zingine au vimondo. Nguvuasili ya jua ni mita 274 kwa sekunde, ikiwa ni zaidi ya kiasi cha nguvuasili ya kila sayari. Muundo huo wa kila sayari kujihami kivyake katika mstari wa njia yake hufahamika kisayansi kama "sayari kuhami mazingira ya njia yake"; yaani kwamba 'a planet has to clear the neighbourhood around its orbit.' Newton akiwa amezaliwa 'mtoto-njiti' na baadaye kuibuka kuwa mwenye akili nyingi kiasi cha kukaribia kuwa sawa na mtu wa miujiza, hakuwahi kuoa kutokana na kinachoelezwa kuwa ni " kutokana na kutingwa na shughuli za kimasomo." Huoneshwa kuwa muda mwingi alikuwa maabara akifanya tafiti mbalimbali za kisayansi, au akiwa maktaba akijisomea, ama akiandika kitabu, au akifundisha wanafunzi wake. Alikuwa bingwa mwenye kipaji cha taaluma nyingi, ikiwemo Fizikia, Kemia, Hisabati, Maarifa ya Anga za Juu, Uchumi, Falsafa, na Theolojia ambayo ni taaluma ya masuala ya kiroho. Kwa mujibu wa historia, mwanasayansi huyo gwiji wa kuigwa alihitimu shahada zake zote mbili za sayansi, yaani 'Bachelor' na 'Masters', mwaka 1665 na 1668 katika Chuo Kikuu cha Cambridge, nchini Uingereza. Akiwa na umri wa miaka 84, mwanasayansi huyo anayedhaniwa na wengi kuwa bingwa wa hesabu za kisayansi kuliko wote duniani, alifariki mwaka 1727 akiwa usingizini. Ripoti ya uchunguzi wa mwili wake huonesha kuwa alikuwa na tatizo la figo, lakini pia alikutwa na kiasi kingi cha zebaki. Zebaki hiyo, yamkini, ni kutokana na kudumu mno kwenye maabara za Kemia na Fizikia, ambazo hutumia kemikali aina mbalimbali, zikiwemo hewa za gesi, katika kufanya majaribio ya kisayansi.
    ·253 Views
  • "INJINI MOJA YA BOEING787 DREAMLINER INASUKUMA TANI MOJA NA ROBO YA HEWA KWA SEKUNDE IKIWA KATIKA 'FULL POWER'
    (Hesabu inasema, inachukua takribani miezi isiyopungua mitatu kwa binaadam wa kawaida kutumia kiwango hiki cha hewa)

    Leo si vibaya kama tukifahamu juu juu kuhusu aina ya injini za ndege ili kila mmoja wetu asibaki nyuma sana.

    Zipo ndege zenye injini 1,2,3,4,6 hadi 8 katika ndege moja.
    Ndege nyingi zinaendeshwa na injini za aina 2 kwa muonekano tuliozoea.

    (1)-Injini za Jeti (Zenye mfano wa pipa lililolazwa)

    (2)-Injini za Propeller (Maarufu Mapangaboi)

    1> MFUMO WA INJINI ZA JETI
    Huu umegawanyika kutokana na 'modification' ya ufanisi na matumizi yake ambazo pia zipo katika makundi mbalimbali mfano,

    *Turbojet 'PureJet'(Mfumo wa ndege nyingi za awali)

    *Turbofan(Mfumo wa ndege nyingi za sasa)

    *Turboshaft(Mfumo wa baadhi ya ndege za sasa mfano Helicopter n.k

    *Scramjet.(Mfumo ulio katika ndege za majaribio za mwendokasi mara nyingi ufanisi wake uanzia mara tano ya kasi ya sauti 'Hypersonic')

    Injini za jeti zinafanya kazi kwa:

    1-Kunyonya hewa mbele (suck)
    2-Kukandamiza (compression)
    3-Kulipua hewa iliyokandamizwa kwa kuchanganya na mafuta(Ignition)
    4-Kisha inatoka/kupulizwa nyuma kwa kasi kubwa na kuisukuma ndege mbele.(Thrust)
    Mfano mzuri kazi ya injini hizi ni kama Puto lililopulizwa na kuachiwa hewani pasipo kuzibwa mdomo wake.(Action and reaction)

    Ndege nyingi za kisasa zinatumia injini aina ya 'Turbofan' (Gas driven) katika kundi la jeti ambazo zinasemakana kuwa na nguvu kubwa na ulaji mdogo wa mafuta.
    (Unaweza kutambua injini hizi kwa haraka kwa kuona feni kubwa lililo mbele ya injini kwa ndani kidogo..usifananishe na mapangaboi)

    Injini za 'Turbojet/Purejet' ambazo moja kwa moja zinanyonya hewa mbele zinakandamiza,kulipua na kuitoa hewa moja ya moto kwa kasi nyuma ambayo ndiyo nguvu pekee inayosukuma ndege kwenda mbele, hutumia mafuta mengi kuliko
    Injini ya 'Turbofan' ambayo ni tofauti kidogo kwani feni lake linavuta na kusukuma hewa mbili nyuma huku hewa ya kwanza ikiwa ile inayoingia kwenye mfumo wa ndani ya injini ambayo unyonywa,kukandamizwa na kulipuliwa na hewa ya pili ni pale hewa ya kwanza iliyolipuliwa kabla ya kufika nje inazungusha visahani maalum 'turbine' zilizoungwa na 'shaft' kwenda kwenye feni lake mbele ambapo huzunguka pamoja na feni na kufanya livute na kusukuma nyuma hewa ya pili yenye nguvu zaidi inayopita nje ya mfumo wa injini(Bypass air) hivyo kuleta nguvu zaidi kwa kutumia mafuta kidogo.

    2-MFUMO WA INJINI ZA MAPANGABOI
    Mapangaboi au 'Propeller'nazo zinafanya kazi kwa kutumia mapanga yake kuchota hewa mbele na kuisukuma nyuma kwa kasi na kuifanya ndege kwenda mbele.

    *Pangaboi linaweza kuwa linazungushwa na 'propeller' iliyoungwa na piston za injini,

    *Au kwa mapangaboi yenye injini ya 'turbo' (turbopropeller)yanazungushwa na hewa iliyolipuliwa (hii aina ya jeti engine yenye mapangaboi)kupitia visahani 'turbine' vilivyo ungwa na propela ya mapangaboi kupitia mfumo wa gear(Geared turboprop)au yanayozunguka kupitia mkandamizo 'pressure' ya hewa iliyolipuliwa pasipo kuungana na chochote (free turbine).

    *Pia 'turboshaft' Mapangaboi yanayozungushwa na hewa iliyolipuliwa kupitia visahani 'turbine' vilivyoungana na propela ya mapangaboi moja kwa moja,pia yaweza kuwa 'Geared' au ila si 'free turbine'

    Mifumo ya injini za kisasa ya mapangaboi inafanya kazi sawa na jeti (Ukiacha za piston)katika mfumo wa ufuaji wa nishati na kuzitofautisha tu katika muonekano wa nje wa injini.

    Injini zenye mfumo ya jeti ni fanisi zaidi kwa ndege zinazopaa anga za juu ambapo hewa ni hafifu,masafa marefu na mwendokasi hasa unaozidi spidi ya sauti 'supersonic'
    Wakati,
    Injini za mfumo wa Mapangaboi ni fanisi zaidi katika mwendo ulio chini ya spidi ya sauti 'subsonic',anga za chini na kati na masafa mafupi kwenda ya kati.

    Tukumbuke pia injini za ndege hazina mahusiano wala kiunganishi chochote na tairi za ndege.
    Tairi za ndege ni 'freewheel' na zimeunganishwa na mfumo wa 'brake' na kona tu.
    Hakuna kinachozungusha tairi kutoka kwenye injini bali zinafuata uelekeo wa kule ndege inaposukumwa.

    Crdts: Online,Aero book,wikimedia.
    "INJINI MOJA YA BOEING787 DREAMLINER INASUKUMA TANI MOJA NA ROBO YA HEWA KWA SEKUNDE IKIWA KATIKA 'FULL POWER' (Hesabu inasema, inachukua takribani miezi isiyopungua mitatu kwa binaadam wa kawaida kutumia kiwango hiki cha hewa) Leo si vibaya kama tukifahamu juu juu kuhusu aina ya injini za ndege ili kila mmoja wetu asibaki nyuma sana. Zipo ndege zenye injini 1,2,3,4,6 hadi 8 katika ndege moja. Ndege nyingi zinaendeshwa na injini za aina 2 kwa muonekano tuliozoea. (1)-Injini za Jeti (Zenye mfano wa pipa lililolazwa) (2)-Injini za Propeller (Maarufu Mapangaboi) 1> MFUMO WA INJINI ZA JETI Huu umegawanyika kutokana na 'modification' ya ufanisi na matumizi yake ambazo pia zipo katika makundi mbalimbali mfano, *Turbojet 'PureJet'(Mfumo wa ndege nyingi za awali) *Turbofan(Mfumo wa ndege nyingi za sasa) *Turboshaft(Mfumo wa baadhi ya ndege za sasa mfano Helicopter n.k *Scramjet.(Mfumo ulio katika ndege za majaribio za mwendokasi mara nyingi ufanisi wake uanzia mara tano ya kasi ya sauti 'Hypersonic') Injini za jeti zinafanya kazi kwa: 1-Kunyonya hewa mbele (suck) 2-Kukandamiza (compression) 3-Kulipua hewa iliyokandamizwa kwa kuchanganya na mafuta(Ignition) 4-Kisha inatoka/kupulizwa nyuma kwa kasi kubwa na kuisukuma ndege mbele.(Thrust) Mfano mzuri kazi ya injini hizi ni kama Puto lililopulizwa na kuachiwa hewani pasipo kuzibwa mdomo wake.(Action and reaction) Ndege nyingi za kisasa zinatumia injini aina ya 'Turbofan' (Gas driven) katika kundi la jeti ambazo zinasemakana kuwa na nguvu kubwa na ulaji mdogo wa mafuta. (Unaweza kutambua injini hizi kwa haraka kwa kuona feni kubwa lililo mbele ya injini kwa ndani kidogo..usifananishe na mapangaboi) Injini za 'Turbojet/Purejet' ambazo moja kwa moja zinanyonya hewa mbele zinakandamiza,kulipua na kuitoa hewa moja ya moto kwa kasi nyuma ambayo ndiyo nguvu pekee inayosukuma ndege kwenda mbele, hutumia mafuta mengi kuliko Injini ya 'Turbofan' ambayo ni tofauti kidogo kwani feni lake linavuta na kusukuma hewa mbili nyuma huku hewa ya kwanza ikiwa ile inayoingia kwenye mfumo wa ndani ya injini ambayo unyonywa,kukandamizwa na kulipuliwa na hewa ya pili ni pale hewa ya kwanza iliyolipuliwa kabla ya kufika nje inazungusha visahani maalum 'turbine' zilizoungwa na 'shaft' kwenda kwenye feni lake mbele ambapo huzunguka pamoja na feni na kufanya livute na kusukuma nyuma hewa ya pili yenye nguvu zaidi inayopita nje ya mfumo wa injini(Bypass air) hivyo kuleta nguvu zaidi kwa kutumia mafuta kidogo. 2-MFUMO WA INJINI ZA MAPANGABOI Mapangaboi au 'Propeller'nazo zinafanya kazi kwa kutumia mapanga yake kuchota hewa mbele na kuisukuma nyuma kwa kasi na kuifanya ndege kwenda mbele. *Pangaboi linaweza kuwa linazungushwa na 'propeller' iliyoungwa na piston za injini, *Au kwa mapangaboi yenye injini ya 'turbo' (turbopropeller)yanazungushwa na hewa iliyolipuliwa (hii aina ya jeti engine yenye mapangaboi)kupitia visahani 'turbine' vilivyo ungwa na propela ya mapangaboi kupitia mfumo wa gear(Geared turboprop)au yanayozunguka kupitia mkandamizo 'pressure' ya hewa iliyolipuliwa pasipo kuungana na chochote (free turbine). *Pia 'turboshaft' Mapangaboi yanayozungushwa na hewa iliyolipuliwa kupitia visahani 'turbine' vilivyoungana na propela ya mapangaboi moja kwa moja,pia yaweza kuwa 'Geared' au ila si 'free turbine' Mifumo ya injini za kisasa ya mapangaboi inafanya kazi sawa na jeti (Ukiacha za piston)katika mfumo wa ufuaji wa nishati na kuzitofautisha tu katika muonekano wa nje wa injini. Injini zenye mfumo ya jeti ni fanisi zaidi kwa ndege zinazopaa anga za juu ambapo hewa ni hafifu,masafa marefu na mwendokasi hasa unaozidi spidi ya sauti 'supersonic' Wakati, Injini za mfumo wa Mapangaboi ni fanisi zaidi katika mwendo ulio chini ya spidi ya sauti 'subsonic',anga za chini na kati na masafa mafupi kwenda ya kati. Tukumbuke pia injini za ndege hazina mahusiano wala kiunganishi chochote na tairi za ndege. Tairi za ndege ni 'freewheel' na zimeunganishwa na mfumo wa 'brake' na kona tu. Hakuna kinachozungusha tairi kutoka kwenye injini bali zinafuata uelekeo wa kule ndege inaposukumwa. Crdts: Online,Aero book,wikimedia.
    ·124 Views
  • "MFUMO ULIOANGUSHA B737MAX"

    Mara baada ya uchunguzi wa awali kutoa ripoti inayoonesha kuwa ajali ya ndege ya Ethiopia Airline na Lion Air B737 Max iliyotokea mapema miezi michache iliyopita haikusababishwa na makosa ya kiurubani bali ni mfumo wao mpya wa"Software" iitwayo 'MCAS' waliouweka katika ndege hiyo kwa lengo la kuzuia ndege ku'STALL.
    'STALL' ni kitendo ambacho hutokea pale mbawa za ndege zinapobinuka na kufikia 'angle' ambayo hushindwa kuendelea kuzalisha 'lift' ya kutosha na kupelekea ndege kushindwa kuendelea kupaa na kurudi chini (mda mwengine mithili ya jiwe).
    'Stall' mara nyingi inatokea pale ambapo ndege inapokuwa inapaa na kunyanyua pua yake juu kupita kiasi na katika mwendo mdogo isivyo kawaida na kupelekea hewa inayopita kwenye mbawa zake ili kuipaisha ndege kuvurugika.
    Software hii mpya ya "MCAS' (Inayosemekana kuwa na makosa) imewekwa kwenye B737Max ili kuzuia ndege hizo ku'stall na inafanya kazi 'automatic' ya kuinamisha pua ya ndege chini ili kuipa kasi na kurudisha hewa iliyovurugika kwenye mbawa katika hali yake ya kawaida ili ndege iendelee kupaa.
    Lakini wachambuzi wanasema, software hii mda mwengine inafanya kazi kimakosa pale inapoinamisha pua ya ndege chini hata kama ndege haikuwa katika ya hali hiyo ya kunyanyua pua yake hivyo kuanza kushindana na Rubani na kupelekea ndege kudaivu kurudi ardhini mithili ya mkuki.
    Inasemekana Boeing wameweka Software hii mpya kwenye B737Max ili kuzuia tabia hiyo mpya ya ndege hizo ya kunyanyua pua yake juu zaidi pale inapokuwa inapaa hali inayosababishwa na kubachikwa kwa injini nyengine kubwa mpya ambazo zilishindwa kufiti katika sehemu yake ya kawaida kutokana na ndege hizo kuwa chichini hivyo waka'modify kwa kuzisogeza mbele na kuzipandisha juu kidogo ya mbawa.
    Modification' hiyo inapelekea ndege kuwa na tabia hiyo ya kunyanyua pua yake yenyewe wakati wa urukaji hivyo kujitofautisha na Boeing 737 nyengine za awali katika urukaji hivyo Boeing wakaamua kuweka mfumo huu ili kuepuka gharama za kufundisha marubani upya juu ya hali hiyo.
    (Picha kwa hisani ya mtandao)
    #Ndege #Ajali #Boeing #Max #Ethiopian #Airline #Lion #Air #MCAS
    "MFUMO ULIOANGUSHA B737MAX" Mara baada ya uchunguzi wa awali kutoa ripoti inayoonesha kuwa ajali ya ndege ya Ethiopia Airline na Lion Air B737 Max iliyotokea mapema miezi michache iliyopita haikusababishwa na makosa ya kiurubani bali ni mfumo wao mpya wa"Software" iitwayo 'MCAS' waliouweka katika ndege hiyo kwa lengo la kuzuia ndege ku'STALL. 'STALL' ni kitendo ambacho hutokea pale mbawa za ndege zinapobinuka na kufikia 'angle' ambayo hushindwa kuendelea kuzalisha 'lift' ya kutosha na kupelekea ndege kushindwa kuendelea kupaa na kurudi chini (mda mwengine mithili ya jiwe). 'Stall' mara nyingi inatokea pale ambapo ndege inapokuwa inapaa na kunyanyua pua yake juu kupita kiasi na katika mwendo mdogo isivyo kawaida na kupelekea hewa inayopita kwenye mbawa zake ili kuipaisha ndege kuvurugika. Software hii mpya ya "MCAS' (Inayosemekana kuwa na makosa) imewekwa kwenye B737Max ili kuzuia ndege hizo ku'stall na inafanya kazi 'automatic' ya kuinamisha pua ya ndege chini ili kuipa kasi na kurudisha hewa iliyovurugika kwenye mbawa katika hali yake ya kawaida ili ndege iendelee kupaa. Lakini wachambuzi wanasema, software hii mda mwengine inafanya kazi kimakosa pale inapoinamisha pua ya ndege chini hata kama ndege haikuwa katika ya hali hiyo ya kunyanyua pua yake hivyo kuanza kushindana na Rubani na kupelekea ndege kudaivu kurudi ardhini mithili ya mkuki. Inasemekana Boeing wameweka Software hii mpya kwenye B737Max ili kuzuia tabia hiyo mpya ya ndege hizo ya kunyanyua pua yake juu zaidi pale inapokuwa inapaa hali inayosababishwa na kubachikwa kwa injini nyengine kubwa mpya ambazo zilishindwa kufiti katika sehemu yake ya kawaida kutokana na ndege hizo kuwa chichini hivyo waka'modify kwa kuzisogeza mbele na kuzipandisha juu kidogo ya mbawa. Modification' hiyo inapelekea ndege kuwa na tabia hiyo ya kunyanyua pua yake yenyewe wakati wa urukaji hivyo kujitofautisha na Boeing 737 nyengine za awali katika urukaji hivyo Boeing wakaamua kuweka mfumo huu ili kuepuka gharama za kufundisha marubani upya juu ya hali hiyo. (Picha kwa hisani ya mtandao) #Ndege #Ajali #Boeing #Max #Ethiopian #Airline #Lion #Air #MCAS
    ·113 Views
  • *FAHAMU MAAJABU YA WANAWAKE YALIYOWASHINDA HATA WANA FALSAFA KUELEWA*

    Wanawake ni binadamu wa ajabu sana katika uso huu wa Dunia yaani hawa watu ni next level, Manabii na busara zao zote walishindwa kuwaelewa wakaishia kushauri ya kwamba tuishi nao kwa akili. Sasa najiuliza ni jambo gani unaweza kufanya nao bila kutumia akili?, hapa ndipo napata ushahidi kwamba kumbe wanawake walishindikana tangu zama za mwanzo kabisa!.

    Wanasaikolojia wanasema kuwa kama utamuoa/kuishi na mwanamke mwenye miaka 25 basi itakuchukua miaka 25 mingine kumuelewa huyo mwanamke angalau kwa 90% maana hawa kila siku hubadilika na kuwa wapya kimatendo na kifikra.

    Mwanamke unaweza mnunulia BMW X6 akatoka nayo kwenda kutembea, akiwa njiani akaombwa lift na kijana akampa akipitia sheli hela ya mafuta ikawa haitoshi, yule kijana akaamua kumuongeza ata elfu 20 basi mwanamke huweza kubadili mawazo na kumuona yule kijana ni bora kisa tu kachangia mafuta kuliko wewe uliyenunua BMW X6.

    Mfano akitoka hapo akapitia supermarket kununua bidhaa labda akapungukiwa kiasi mfano anadaiwa elfu 20, na yule kijana akasema hiyo ntalipa mimi basi basi hapo atasahau zile zawadi zote huwa unambebea na hiyo elfu 20 inaweza kumfanya awaze kumtunuku yule kijana penzi.

    Mwanamke unaweza mpa hela akanunue nyama kilo 5 buchani, mwenye bucha akimuongeza robo tu hilo litamfurahisha kiasi kwamba anaweza kumpa mwenye bucha penzi na akusahau wewe ulieyota hela ya nyama kilo 5.

    Mwanamke unaweza kumnunulia nguo, weaving, mafuta, perfume na urembo mzuri akavutia ila akipita mtaani akasifiwa na mwanaume kuwa kapendeza inaweza kuwa chanzo cha kumtunuku penzi na akakusahu wewe uliyegharamika na kufanya asifiwe!.

    Mwanamke unaweza kumpa mimba na ukamhudumia mwanzo mwisho na familia ukalea kwa juhudi zako zote ila siku mkikosana anakwambia niache na watoto wangu, apo ashasahau kuwa wewe ndiye uliyempa mimba na kumlea yeye na watoto!.

    Mchukue rafiki yako mwende bar, wewe uwe na laki 5 na yeye awe na elfu 30 kisha mkae meza moja na muagize unywaji, wewe agiza soda na yeye aagize bia. halafu baada ya nusu saa iteni warembo utaona wewe na laki 5 yako unapitwa tu ila yeye mwenye slfu 30 anaibuka kidedea kisa kaweza kumudu gharama ya bia, Hao ndio wanawake ndugu!

    Mwanamke ndiye kiumbe pekee anayeweza kukupenda bila sababu ama kukuchukia bila sababu tofauti na viumbe wengine.
    Mwanamke ndiye mwigizaji mkubwa ulimwenguni, anaweza kulia kwa furaha na akacheka kwa huzuni, bado hujawajua tu wanawake!

    Mwanamke akisema ndio humaanisha hapana, na akisema hapana humaanisha ndio, pia anaweza kucheka bila kujua sababu lakini pia anaweza kulia pasipo sababu ya msingi ya kumfanya alie, hivyo chunga sana usijejichanganya!.

    Mwanamke hupendi vutu vigumu na vyenye hatari mfano wanaume wenye nguvu, mlevi, muhuni (playboy), jambazi, mgomvi anayeogopwa hata na wanaume wenzie ila ukimuuliza anakuambia mie napenda kuwa na mwanaume mpole mwenye hofu ya Mungu tifauti na sisi wanaume tunavyopenda vitu vipole na vinyenyekevu na vyenye ukarimu, sasa wewe jifanye kumuamini mwanamke!

    Jinsi unavyozidi kumpenda na kumthibutishia upendo wa dhati ndivyo unavyozidi kujiweka mbali nayeye, mwanamke hupenda migogoro isiyo na maana, ukijua hili ndoa haitokusumbua. Mwanamke hupendi utulivu kamwe!, usipomchokoa atakuchokoa tuu na usipomuendesha lazima akuendeshe yeye, Hawa viumbe hawana hiyana aisee!.

    Mwanamke hupendi vitu vikubwa wala vidogo, kiufupi hana chaguo maalumu. Ukimnunulia gari sio garantii ya yeye kutulia nawewe bali anaweza kukusaliti hata na muosha gari wako. Ukimjengea nyumba nzuri na kumuwekea kila kitu sio njia ya kumteka kimahaba kwani anaweza kumtunuku penzi ata mtunza bustani wa nyumba yako.

    Mwanamke hapendi ukweli, Ukimpa ukweli akija mwenye uongo basi we andika maumivu. Unaweza kuwa na elfu 50 ukamueleza ukweli kuwa "mke wangu leo hali mbaya chukua hii elfu 30,"... akatokea jamaa akamuongopea kuwa "Chukua hii elfu 15 ngoja nimesahau ATM card yangu nyumbani ikifuka saa 10 jioni ntakutumia laki 2 kwenye simu", Usishangae mkeo akakusaliti hata kabla ya hiyo saa 10 na iyo laki 2 asiione katu!.

    Unamuoa hana ishu akiwa kwao amekaa tu, unaamua kumfungulia biashara hata ya duka unamjazia kila kitu. anatokea mshikaji mmoja kumuunga pale dukani kila siku na kumuachia soda tu na hicho kinakuwa kigezo tosha cha kuona mshikaji anamjali kwa kumuachia ya soda kila siku kuliko wewe uliyemfungulia duka zima na kinachofuata ni usaliti tu.
    Yapo mengi mno kuliko hayo ila kwa leo naishia hapo... ukiweza shea kwenye groups zingine.

    🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽
    Wamekuwa viumbe walioshindikana kwa Maana nyingine
    *ni mawazo tu wadau msijenge chuki*🏃🏽
    *FAHAMU MAAJABU YA WANAWAKE YALIYOWASHINDA HATA WANA FALSAFA KUELEWA* Wanawake ni binadamu wa ajabu sana katika uso huu wa Dunia yaani hawa watu ni next level, Manabii na busara zao zote walishindwa kuwaelewa wakaishia kushauri ya kwamba tuishi nao kwa akili. Sasa najiuliza ni jambo gani unaweza kufanya nao bila kutumia akili?, hapa ndipo napata ushahidi kwamba kumbe wanawake walishindikana tangu zama za mwanzo kabisa!. Wanasaikolojia wanasema kuwa kama utamuoa/kuishi na mwanamke mwenye miaka 25 basi itakuchukua miaka 25 mingine kumuelewa huyo mwanamke angalau kwa 90% maana hawa kila siku hubadilika na kuwa wapya kimatendo na kifikra. Mwanamke unaweza mnunulia BMW X6 akatoka nayo kwenda kutembea, akiwa njiani akaombwa lift na kijana akampa akipitia sheli hela ya mafuta ikawa haitoshi, yule kijana akaamua kumuongeza ata elfu 20 basi mwanamke huweza kubadili mawazo na kumuona yule kijana ni bora kisa tu kachangia mafuta kuliko wewe uliyenunua BMW X6. Mfano akitoka hapo akapitia supermarket kununua bidhaa labda akapungukiwa kiasi mfano anadaiwa elfu 20, na yule kijana akasema hiyo ntalipa mimi basi basi hapo atasahau zile zawadi zote huwa unambebea na hiyo elfu 20 inaweza kumfanya awaze kumtunuku yule kijana penzi. Mwanamke unaweza mpa hela akanunue nyama kilo 5 buchani, mwenye bucha akimuongeza robo tu hilo litamfurahisha kiasi kwamba anaweza kumpa mwenye bucha penzi na akusahau wewe ulieyota hela ya nyama kilo 5. Mwanamke unaweza kumnunulia nguo, weaving, mafuta, perfume na urembo mzuri akavutia ila akipita mtaani akasifiwa na mwanaume kuwa kapendeza inaweza kuwa chanzo cha kumtunuku penzi na akakusahu wewe uliyegharamika na kufanya asifiwe!. Mwanamke unaweza kumpa mimba na ukamhudumia mwanzo mwisho na familia ukalea kwa juhudi zako zote ila siku mkikosana anakwambia niache na watoto wangu, apo ashasahau kuwa wewe ndiye uliyempa mimba na kumlea yeye na watoto!. Mchukue rafiki yako mwende bar, wewe uwe na laki 5 na yeye awe na elfu 30 kisha mkae meza moja na muagize unywaji, wewe agiza soda na yeye aagize bia. halafu baada ya nusu saa iteni warembo utaona wewe na laki 5 yako unapitwa tu ila yeye mwenye slfu 30 anaibuka kidedea kisa kaweza kumudu gharama ya bia, Hao ndio wanawake ndugu! Mwanamke ndiye kiumbe pekee anayeweza kukupenda bila sababu ama kukuchukia bila sababu tofauti na viumbe wengine. Mwanamke ndiye mwigizaji mkubwa ulimwenguni, anaweza kulia kwa furaha na akacheka kwa huzuni, bado hujawajua tu wanawake! Mwanamke akisema ndio humaanisha hapana, na akisema hapana humaanisha ndio, pia anaweza kucheka bila kujua sababu lakini pia anaweza kulia pasipo sababu ya msingi ya kumfanya alie, hivyo chunga sana usijejichanganya!. Mwanamke hupendi vutu vigumu na vyenye hatari mfano wanaume wenye nguvu, mlevi, muhuni (playboy), jambazi, mgomvi anayeogopwa hata na wanaume wenzie ila ukimuuliza anakuambia mie napenda kuwa na mwanaume mpole mwenye hofu ya Mungu tifauti na sisi wanaume tunavyopenda vitu vipole na vinyenyekevu na vyenye ukarimu, sasa wewe jifanye kumuamini mwanamke! Jinsi unavyozidi kumpenda na kumthibutishia upendo wa dhati ndivyo unavyozidi kujiweka mbali nayeye, mwanamke hupenda migogoro isiyo na maana, ukijua hili ndoa haitokusumbua. Mwanamke hupendi utulivu kamwe!, usipomchokoa atakuchokoa tuu na usipomuendesha lazima akuendeshe yeye, Hawa viumbe hawana hiyana aisee!. Mwanamke hupendi vitu vikubwa wala vidogo, kiufupi hana chaguo maalumu. Ukimnunulia gari sio garantii ya yeye kutulia nawewe bali anaweza kukusaliti hata na muosha gari wako. Ukimjengea nyumba nzuri na kumuwekea kila kitu sio njia ya kumteka kimahaba kwani anaweza kumtunuku penzi ata mtunza bustani wa nyumba yako. Mwanamke hapendi ukweli, Ukimpa ukweli akija mwenye uongo basi we andika maumivu. Unaweza kuwa na elfu 50 ukamueleza ukweli kuwa "mke wangu leo hali mbaya chukua hii elfu 30,"... akatokea jamaa akamuongopea kuwa "Chukua hii elfu 15 ngoja nimesahau ATM card yangu nyumbani ikifuka saa 10 jioni ntakutumia laki 2 kwenye simu", Usishangae mkeo akakusaliti hata kabla ya hiyo saa 10 na iyo laki 2 asiione katu!. Unamuoa hana ishu akiwa kwao amekaa tu, unaamua kumfungulia biashara hata ya duka unamjazia kila kitu. anatokea mshikaji mmoja kumuunga pale dukani kila siku na kumuachia soda tu na hicho kinakuwa kigezo tosha cha kuona mshikaji anamjali kwa kumuachia ya soda kila siku kuliko wewe uliyemfungulia duka zima na kinachofuata ni usaliti tu. Yapo mengi mno kuliko hayo ila kwa leo naishia hapo... ukiweza shea kwenye groups zingine. 😂🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽 Wamekuwa viumbe walioshindikana kwa Maana nyingine 😅👀 *ni mawazo tu wadau msijenge chuki*🏃🏽
    ·196 Views
  • KWANINI WAARABU HUWA HAWATEKI RAIA WA KUTOKA URUSI!????

    Mkwara wa kibabe: Majasusi wa KGB walivyowafanya magaidi wa Hezbollah waliowateka diplomats wao wanne.

    Picha za video za hivi karibuni zilizokuwa zikionesha jinsi wanahabari wa kimarekani bwana James Foley pamoja na Steven sotloff wakikatwa vichwa na magaidi wa ISIS inanikumbusha stori ambayo ilitokea nchini Lebanon mnamo mwaka 1985.

    Mnamo mwezi wa tisa, tarehe 30, mwaka 1985, kundi la watu wenye silaha lilifanikiwa kuwateka nyara wanadiplomasia wanne wa Urusi pamoja na wafanyakazi wa ubalozi wa Urusi nchini Lebanon (Arkady Katkov, Valery Myrikov, Oleg Spirin pamoja na Nikolai Svirsky) katika mji mkuu wa Beirut.

    Wakati wa tukio zima la utekaji nyara huo nje kabisa ya majengo ya ubalozi huo, bwana Katkov alijeruhiwa sehemu ya mguu wake wa kushoto.

    Watekaji nyara hao walijiita ni "Jeshi la Khaled Al-Walid" pamoja na "Islamic Liberation Organization" (ILO). Kulingana na taarifa za idara ya ujasusi wa nje ya Urusi, kanali Yuri Perfilyev, ambaye kwa wakatu huo ndiye aliyekuwa shushushu mkazi (resident spy ama station chief) wa KGB nchini Lebanon, tukio zima la utekaji nyara lilipangwa na kuratibiwa kwa umakini mkubwa na jasusi katili sana wa magaidi wa Hezbollah bwana Imad Mugniyeh kama kujibu mapigo ya wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali ya Syria katika mji wa Tripoli uliopo humo nchini Lebanon. Baada ya kuchukua mateka, magaidi hao wa kishiha wakaitaka kwa nguvu zote serikali ya Urusi kuilazimisha Syria kuacha mara moja kufanya mashambulizi ya kijeshi katika mji wa Tripoli na kuufunga haraka sana ubalozi wake uliopo mjini Beirut.

    Ili kudhihirisha ya kwamba hawakuwa na masihara katika kutaka matakwa yao kutekelezwa, ndani ya siku mbili tu, gaidi mkuu Mugniyeh akamuua bila huruma mwanadiplomasia wa Urusi aliyekuwa amejeruhiwa bwana Katkov kwa kummiminia risasi za kutosha kwa SMG na kisha kuutupa mwili wake kwenye dampo la takataka hapo hapo jijini Beirut.

    KGB station chief bwana Perfilyev kisha akaamua kukutana na bwana mkubwa Ayatollah Muhammad Fadlallah, kiongozi wa kidini wa washiha waishio nchini Lebanon kisha akamwambia;

    "Taifa kubwa kamwe haliwezi kusubiri milele. Tutaacha kusubiri na kutazama na kuamua kuchukua hatua kali zitakazokuwa na madhara yasiyotabirika (mkwara huu......)

    Baada ya kuona ayatollah Fadlallah bado tupo kimya, KGB station chief akazungumza kwa ukali sana safari hii akimwambia;

    " Hatuzungumzii tu kuhusu watu wa Beirut. Ninazungumza kuhusu miji ya Tehran na Qom ambao ni mji mtakatifu wa washiha pamoja na makazi ya Ayatollah Khomeini, ambayo haipo mbali na mpaka wa Urusi.

    Qom ipo karibu sana na Russia na makosa yanaweza kujitokeza na kombora linarusha kwa bahati mbaya. Makosa ya kiufundi yanaweza kutokea kwa bahati mbaya sana na tunaomba Mungu aepushie mbali janga hili"

    Ayatollah Fadlallah ambaye alionekana anatetemeka sana kutokana na mkwara ule wa boss wa KGB akajibu baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu akisema "ninafikiri mambo yote yataenda sawa sawia"

    Baadaye mshauri wa karibu wa Ayatollah Fadlallah bwana Hassan akamwambia KGB boss ya kwamba hakuna mtu aliyewahi kuongea na kiongozi wetu mkuu wa dini kwa ukali wa namna hiyo.

    Kutumia mbinu ya kutishia kushambulia moja kati ya miji kitakatifu sana ya watu wa dhehebu la shiha ilikuwa ni moja tu kati ya mikakati lukuki ya Urusi katika kutaka kuwakomboa diplomats wake, ila baada ya ukimya kuzidi kushika kasi KGB wakaamua kutoa somo la milele kwa magaidi wote wa kiarabu pale mashariki ya kati. Wanaume wa KGB walifanya ushenzi huu mpaka leo wanaogopwa sana na waarabu;

    KGB walimteka mtu waliyejua fika alikuwa ni ndugu wa karibu saaaaana na kiongozi mashuhuri wa Hezbollah. Walimkata vipandevipande vya nyama, kisha wakaweza nyama zile kwenye mfuko na kisha kuvituma kwa viongozi wa juu wa Hezbollah.

    Siku iliyofuata KGB wakakamata ndugu mwingine wa karibu sana wa kiongozi wa Hezbollah, wakamfumua ubongo wake kwa risasi, wakaweka kwenye kiroba, kisha wakapeleka mwili wake kwa viongozi wa magaidi hao.

    Kama hio haitoshi kuonesha ya kwamba wapo serious sana na kazi zao, wababe wa KGB wakawaambia viongozi wa Hezbollah ya kwamba tunajua walipo ndugu zenu wengine wa karibu kabisa na kwamba wategemee vifurushi zaidi vya maiti ndani ya mifuko ya viroba kama wanadiplomasia hao watatu hawataachiwa huru mara moja.

    Baada ya kuonea sasa wamegusa pabaya pasipogusika, viongozi wa Hezbollah wakachukua gari mpya na za kisasa sana aina ya BMW zinazokimbia kwa kasi kubwa sana, wakawabeba wanadiplomasia wale waliobaki hai, kisha kiwapeleka katika ubalozi wa Urusi mjini Beirut.

    Tangia siku hiyo, hakuna mwanadiplomasia wala raia wa Urusi aliyewahi kutekwa nchini Lebanon.

    Hivi ndivyo KGB ilivyokuwa ilifanya kazi. Walikuwa hawaongei mara mbili mbili.

    ****MWISHO****
    KWANINI WAARABU HUWA HAWATEKI RAIA WA KUTOKA URUSI!???? Mkwara wa kibabe: Majasusi wa KGB walivyowafanya magaidi wa Hezbollah waliowateka diplomats wao wanne. Picha za video za hivi karibuni zilizokuwa zikionesha jinsi wanahabari wa kimarekani bwana James Foley pamoja na Steven sotloff wakikatwa vichwa na magaidi wa ISIS inanikumbusha stori ambayo ilitokea nchini Lebanon mnamo mwaka 1985. Mnamo mwezi wa tisa, tarehe 30, mwaka 1985, kundi la watu wenye silaha lilifanikiwa kuwateka nyara wanadiplomasia wanne wa Urusi pamoja na wafanyakazi wa ubalozi wa Urusi nchini Lebanon (Arkady Katkov, Valery Myrikov, Oleg Spirin pamoja na Nikolai Svirsky) katika mji mkuu wa Beirut. Wakati wa tukio zima la utekaji nyara huo nje kabisa ya majengo ya ubalozi huo, bwana Katkov alijeruhiwa sehemu ya mguu wake wa kushoto. Watekaji nyara hao walijiita ni "Jeshi la Khaled Al-Walid" pamoja na "Islamic Liberation Organization" (ILO). Kulingana na taarifa za idara ya ujasusi wa nje ya Urusi, kanali Yuri Perfilyev, ambaye kwa wakatu huo ndiye aliyekuwa shushushu mkazi (resident spy ama station chief) wa KGB nchini Lebanon, tukio zima la utekaji nyara lilipangwa na kuratibiwa kwa umakini mkubwa na jasusi katili sana wa magaidi wa Hezbollah bwana Imad Mugniyeh kama kujibu mapigo ya wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali ya Syria katika mji wa Tripoli uliopo humo nchini Lebanon. Baada ya kuchukua mateka, magaidi hao wa kishiha wakaitaka kwa nguvu zote serikali ya Urusi kuilazimisha Syria kuacha mara moja kufanya mashambulizi ya kijeshi katika mji wa Tripoli na kuufunga haraka sana ubalozi wake uliopo mjini Beirut. Ili kudhihirisha ya kwamba hawakuwa na masihara katika kutaka matakwa yao kutekelezwa, ndani ya siku mbili tu, gaidi mkuu Mugniyeh akamuua bila huruma mwanadiplomasia wa Urusi aliyekuwa amejeruhiwa bwana Katkov kwa kummiminia risasi za kutosha kwa SMG na kisha kuutupa mwili wake kwenye dampo la takataka hapo hapo jijini Beirut. KGB station chief bwana Perfilyev kisha akaamua kukutana na bwana mkubwa Ayatollah Muhammad Fadlallah, kiongozi wa kidini wa washiha waishio nchini Lebanon kisha akamwambia; "Taifa kubwa kamwe haliwezi kusubiri milele. Tutaacha kusubiri na kutazama na kuamua kuchukua hatua kali zitakazokuwa na madhara yasiyotabirika (mkwara huu......) Baada ya kuona ayatollah Fadlallah bado tupo kimya, KGB station chief akazungumza kwa ukali sana safari hii akimwambia; " Hatuzungumzii tu kuhusu watu wa Beirut. Ninazungumza kuhusu miji ya Tehran na Qom ambao ni mji mtakatifu wa washiha pamoja na makazi ya Ayatollah Khomeini, ambayo haipo mbali na mpaka wa Urusi. Qom ipo karibu sana na Russia na makosa yanaweza kujitokeza na kombora linarusha kwa bahati mbaya. Makosa ya kiufundi yanaweza kutokea kwa bahati mbaya sana na tunaomba Mungu aepushie mbali janga hili" Ayatollah Fadlallah ambaye alionekana anatetemeka sana kutokana na mkwara ule wa boss wa KGB akajibu baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu akisema "ninafikiri mambo yote yataenda sawa sawia" Baadaye mshauri wa karibu wa Ayatollah Fadlallah bwana Hassan akamwambia KGB boss ya kwamba hakuna mtu aliyewahi kuongea na kiongozi wetu mkuu wa dini kwa ukali wa namna hiyo. Kutumia mbinu ya kutishia kushambulia moja kati ya miji kitakatifu sana ya watu wa dhehebu la shiha ilikuwa ni moja tu kati ya mikakati lukuki ya Urusi katika kutaka kuwakomboa diplomats wake, ila baada ya ukimya kuzidi kushika kasi KGB wakaamua kutoa somo la milele kwa magaidi wote wa kiarabu pale mashariki ya kati. Wanaume wa KGB walifanya ushenzi huu mpaka leo wanaogopwa sana na waarabu; KGB walimteka mtu waliyejua fika alikuwa ni ndugu wa karibu saaaaana na kiongozi mashuhuri wa Hezbollah. Walimkata vipandevipande vya nyama, kisha wakaweza nyama zile kwenye mfuko na kisha kuvituma kwa viongozi wa juu wa Hezbollah. Siku iliyofuata KGB wakakamata ndugu mwingine wa karibu sana wa kiongozi wa Hezbollah, wakamfumua ubongo wake kwa risasi, wakaweka kwenye kiroba, kisha wakapeleka mwili wake kwa viongozi wa magaidi hao. Kama hio haitoshi kuonesha ya kwamba wapo serious sana na kazi zao, wababe wa KGB wakawaambia viongozi wa Hezbollah ya kwamba tunajua walipo ndugu zenu wengine wa karibu kabisa na kwamba wategemee vifurushi zaidi vya maiti ndani ya mifuko ya viroba kama wanadiplomasia hao watatu hawataachiwa huru mara moja. Baada ya kuonea sasa wamegusa pabaya pasipogusika, viongozi wa Hezbollah wakachukua gari mpya na za kisasa sana aina ya BMW zinazokimbia kwa kasi kubwa sana, wakawabeba wanadiplomasia wale waliobaki hai, kisha kiwapeleka katika ubalozi wa Urusi mjini Beirut. Tangia siku hiyo, hakuna mwanadiplomasia wala raia wa Urusi aliyewahi kutekwa nchini Lebanon. Hivi ndivyo KGB ilivyokuwa ilifanya kazi. Walikuwa hawaongei mara mbili mbili. ****MWISHO****
    ·201 Views
  • WATU 10 AMBAO WALIPOTEA NA HAWAJAWI ONEKANA
    #1
    Kupotea kwa mwanasiasa Ben Saanane takribani miaka miwili iliyopita pamoja na kupotea kwa mwanahabari Azory Agwanda mwaka mmoja uliopita,kuliwashtua Watanzania walio wengi na kuibua minong'ono juu ya mahali walipo watu hao. Mpaka leo hatujui walipo Ben Saanane pamoja na Azory Agwanda. Miaka ya nyuma, aliwahi kupotea mwanasiasa mahiri wa miaka hiyo hapa nchini Abdallah Kassim Hanga, ambaye mpaka leo hajulikani alipelekwa wapi licha ya kuwa mpaka kupotea kwake alikuwa kwenye mikono ya dola. Hayo ni machache.

    Leo tujionee watu maarufu ambao walipotea, hawajulikani walipo na hawakuwahi kuonekana tena hapa Duniani. Baadhi yao ni viongozi, wahalifu na watu wa kawaida tu.

    10.Jim Sullivan

    Huyu alikuwa ni mwanamuziki wa kimarekani. Mwaka 1969 alitoa albamu iliyoitwa U.F.O. Ndani ya albamu hiyo kulikuwa na vibao vyenye utata wa majina, kama vile Aliens, I"never die na vinginevyo vingi. Alitoweka mwaka 1975 na mpaka leo hajulikani ni wapi alipo.

    9.Bison Dele

    Alikuwa ni mchezaji wa mpira wakikapu katika ligi ya NBA na alichezea vilabu kadhaa vikiwemo Detroit Pistons, Chicago bulls nk. Alitoweka mwaka 2002 wakati akiwa na mchumba wake kwenye boti yao huko Tahiti katika bahari ya Pacific. Vyanzo mbalimbali vinadai kuwa Bison Dele alikuwa na kaka yake siku ya safari katika boti, pia aligombana na kaka yake hivyo walipigana wakiwa katika boti na kupelekea kuuliwa na bastola yeye pamoja na mchumba wake. Boti yao ilikuja kupatikana ikiwa haina mtu yoyote ndani yake.

    8.Frank Morris

    Huyu alikuwa ni mfungwa aliyekuwa anatumikia kifungo cha miaka 10 katika gereza la Alcatraz huko nchini Marekani. Alipelekwa katika gereza Alcatraz baada ya kutoroka gereza la Louisiana. Hivyo baada ya kukamatwa alipelekwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali na lililopo kisiwani Alcatraz, gereza hilo limezungukwa ma maji yenye kina kirefu na eneo lenye samaki wengi aina ya papa.

    Mwanaume huyu na mapacha wawili walifanikiwa kutoroka mwaka 1962 na mpaka leo hajulikani alipo licha ya msako mkali wa FBI. Kuna wanaoamini huenda Frank aliuwawa na papa ndani ya bahari lakini hakuna aliyethibitisha. Mpaka leo jalada la kesi yake bado lipo wazi.

    7. Mapacha John and Clarence Anglin

    Hawa ni mapacha ambao kwa pamoja waliungana na Jambazi Frank Morris kutoroka katika jela yenye ulinzi mkali na iliyozungukwa na maji ya Alcatraz. Walitoroka mwaka 1962 na mpaka leo hawajwahi kuonekana tena. Inasemekana baada ya kutoroka walikimbilia nchini Brazil ambapo wamekuwa wakiishi na kwasiliana na familia zao kwa siri lakini hakuna aliyewahi kuthibitisha madai hayo. Sasa ni zaidi ya miaka 56 toka watoroke jela hawajawahi kuonekana tena na jalada lao lipo wazi bado halijafungwa.

    6.Oscar Zeta Acosta

    Alikuwa ni mwanasiasa, mwanafasihi na mwanasheria nguli kutoka nchini Marekani ambapo alikuwa ni mkosoaji mkubwa sana wa biashara ya madawa ya kulevya. Alipotea mwaka 1974 alipokuwa anaelekea Mexico. Inaaminika Acosta aliuwawa na wafanya biashara wa madawa ya kulevya na kuna wanaoamini Acosta aliuwawa kwasababu za kisiasa lakini mpaka leo hakuwahi kupatikana tena.

    5.Amelia Earhart

    Alikuwa ni rubani mahiri wa ndege huko Marekani. Pia alikuwa ni mwalimu, mwanamitindo na Mhariri wa majarida mbalimbali. Alikuwa mwanamke wa kwanza kurusha ndege peke yake na kuzunguka bahari ya Pacific.

    Alitoweka na ndege yake mwaka 1937 akiwa angani na mpaka leo hajulikani alipo. Japo kuna wanaoamini kuwa alipewa kazi ya ujasusi na utawala wa Rais wa kipindi hiko Marekani ndugu Franklin D. Roosevelt ya kwenda kuichunguza Japan. Pia wapo wanaoamini kuwa aliamua kujibadilisha kimwili na jina na kuishi maisha yake nje ya awali. Mpaka leo hajawahi kupatikana tena.

    4.Camilo Cienfuegos

    Ni mwanamapinduzi wa Cuba aliyeshiriki kikamilifu Mapinduzi ya Nchi hiyo akiwa sambamba na akina Fidel castro, Che Guevara na wengineo. Ndege aliyopanda akitokea Camaguey alikotoka kumkamata mwanamapinduzi mwenzake aliyeasi Huber Matos, ilipotea angani na haijaonekana tena mpaka leo hii. Wengi wanadai Camilo alifanyiwa faulo na wenzake hasa Fidel Castro ili kuizima nyota yake iliyokuwa inang'aa kwa kasi.

    3.Jimmy Hoffa

    Alikuwa ni kiongozi wa chama cha wafanyakazi nchini Marekani. Pia alikuwa anajihusisha na makundi ya kihalifu. Anajulikana kama kiongozi mtata, mpendwa rushwa na mwizi ambapo kuna wakati alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela kwa kosa la utakatishaji pesa. Aliachiwa kwa msamaha wa Rais wa kipindi hiko wa Marekani Richard Nixon.

    Mchana wa july 30 mwaka 1975 katika parking ya Mgahawa wa Red Fox, Jimmy hoffa alitoweka na hakuonekana tena mpaka leo. Haijulikani ni akina nani haswa walihusika katika kumteka, kuna wanaosema Serikali, kuna wanaosema Mafia. Licha ya msako mkali wa FBI kiongozi huyo hakuwahi kupatikana tena.

    2. Harlod Holt

    Alikuwa ni Waziri Mkuu wa 17 wa Australia mpaka kupotea kwake. Jioni ya 17 december mwaka 1967 wananchi wa Australia hawatoisahau katika kumbukumbu zao baada ya kupotea kwa Waziri Mkuu wao.

    Waziri Mkuu Holt alipotea alipokuwa anaogelea baharini huko Portsea, Victoria nchini Australia alipokuwa katika likizo ya mwisho wa mwaka.Licha ya msako mkali wa kwenye maji, mwili wa Waziri Mkuu Holt hakuwahi kuoekana tena. Minong'ono ilizuka kuwa Waziri mkuu huyo alitekwa na Submarine (nyambizi) ya China kwakuwa alikuwa ni jasusi wao lakini hakuna aliyethibitisha. Kuna wanaosema Harold Holt alifeki kifo chake ili aishi kwa uhuru mara baada ya kuchoshwa na maisha ya siasa ikiwa ni miaka miwili tu toka achaguliwe kuwa Waziri Mkuu. Mpaka leo mwili wake haukuwahi kupatikana tena.

    1.D.B Cooper

    D.B.Cooper ni jina linalotumika kumrejelea mwanaume mmoja wa makamo ambaye jioni ya November 24, mwaka 1971 alichukua kiasi cha Dola za Kimarekani 200,000 kama malipo mara baada ya kuiteka ndege huko portland nchini Marekani.

    Licha ya msako mkali wa zaidi ya miaka 45 uliofanywa na FBI kwa kushirikiana na idara nyingine za kiusalama nchini Marekani, bado D.B Cooper hafahamiki ni wapi alipo wala pesa alizopewa hazikuwahi kuingia kwenye mzunguko wala kupatikana. kuna wanaoamini kuwa D.B Cooper alitengenezwa na kusaidiwa na FBI wenyewe ili wajipatie pesa. Kuna wanaoamini Cooper alifariki mara baada ya kuruka toka kwenye ndege angani lakini mbona pesa hazijapatikana? D.B Cooper ameacha maswali mengi kuliko majibu na mpaka leo hajawahi kuonekana tena baada ya jioni ile ya mwaka 1971.

    MWISHO
    WATU 10 AMBAO WALIPOTEA NA HAWAJAWI ONEKANA #1 Kupotea kwa mwanasiasa Ben Saanane takribani miaka miwili iliyopita pamoja na kupotea kwa mwanahabari Azory Agwanda mwaka mmoja uliopita,kuliwashtua Watanzania walio wengi na kuibua minong'ono juu ya mahali walipo watu hao. Mpaka leo hatujui walipo Ben Saanane pamoja na Azory Agwanda. Miaka ya nyuma, aliwahi kupotea mwanasiasa mahiri wa miaka hiyo hapa nchini Abdallah Kassim Hanga, ambaye mpaka leo hajulikani alipelekwa wapi licha ya kuwa mpaka kupotea kwake alikuwa kwenye mikono ya dola. Hayo ni machache. Leo tujionee watu maarufu ambao walipotea, hawajulikani walipo na hawakuwahi kuonekana tena hapa Duniani. Baadhi yao ni viongozi, wahalifu na watu wa kawaida tu. 10.Jim Sullivan Huyu alikuwa ni mwanamuziki wa kimarekani. Mwaka 1969 alitoa albamu iliyoitwa U.F.O. Ndani ya albamu hiyo kulikuwa na vibao vyenye utata wa majina, kama vile Aliens, I"never die na vinginevyo vingi. Alitoweka mwaka 1975 na mpaka leo hajulikani ni wapi alipo. 9.Bison Dele Alikuwa ni mchezaji wa mpira wakikapu katika ligi ya NBA na alichezea vilabu kadhaa vikiwemo Detroit Pistons, Chicago bulls nk. Alitoweka mwaka 2002 wakati akiwa na mchumba wake kwenye boti yao huko Tahiti katika bahari ya Pacific. Vyanzo mbalimbali vinadai kuwa Bison Dele alikuwa na kaka yake siku ya safari katika boti, pia aligombana na kaka yake hivyo walipigana wakiwa katika boti na kupelekea kuuliwa na bastola yeye pamoja na mchumba wake. Boti yao ilikuja kupatikana ikiwa haina mtu yoyote ndani yake. 8.Frank Morris Huyu alikuwa ni mfungwa aliyekuwa anatumikia kifungo cha miaka 10 katika gereza la Alcatraz huko nchini Marekani. Alipelekwa katika gereza Alcatraz baada ya kutoroka gereza la Louisiana. Hivyo baada ya kukamatwa alipelekwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali na lililopo kisiwani Alcatraz, gereza hilo limezungukwa ma maji yenye kina kirefu na eneo lenye samaki wengi aina ya papa. Mwanaume huyu na mapacha wawili walifanikiwa kutoroka mwaka 1962 na mpaka leo hajulikani alipo licha ya msako mkali wa FBI. Kuna wanaoamini huenda Frank aliuwawa na papa ndani ya bahari lakini hakuna aliyethibitisha. Mpaka leo jalada la kesi yake bado lipo wazi. 7. Mapacha John and Clarence Anglin Hawa ni mapacha ambao kwa pamoja waliungana na Jambazi Frank Morris kutoroka katika jela yenye ulinzi mkali na iliyozungukwa na maji ya Alcatraz. Walitoroka mwaka 1962 na mpaka leo hawajwahi kuonekana tena. Inasemekana baada ya kutoroka walikimbilia nchini Brazil ambapo wamekuwa wakiishi na kwasiliana na familia zao kwa siri lakini hakuna aliyewahi kuthibitisha madai hayo. Sasa ni zaidi ya miaka 56 toka watoroke jela hawajawahi kuonekana tena na jalada lao lipo wazi bado halijafungwa. 6.Oscar Zeta Acosta Alikuwa ni mwanasiasa, mwanafasihi na mwanasheria nguli kutoka nchini Marekani ambapo alikuwa ni mkosoaji mkubwa sana wa biashara ya madawa ya kulevya. Alipotea mwaka 1974 alipokuwa anaelekea Mexico. Inaaminika Acosta aliuwawa na wafanya biashara wa madawa ya kulevya na kuna wanaoamini Acosta aliuwawa kwasababu za kisiasa lakini mpaka leo hakuwahi kupatikana tena. 5.Amelia Earhart Alikuwa ni rubani mahiri wa ndege huko Marekani. Pia alikuwa ni mwalimu, mwanamitindo na Mhariri wa majarida mbalimbali. Alikuwa mwanamke wa kwanza kurusha ndege peke yake na kuzunguka bahari ya Pacific. Alitoweka na ndege yake mwaka 1937 akiwa angani na mpaka leo hajulikani alipo. Japo kuna wanaoamini kuwa alipewa kazi ya ujasusi na utawala wa Rais wa kipindi hiko Marekani ndugu Franklin D. Roosevelt ya kwenda kuichunguza Japan. Pia wapo wanaoamini kuwa aliamua kujibadilisha kimwili na jina na kuishi maisha yake nje ya awali. Mpaka leo hajawahi kupatikana tena. 4.Camilo Cienfuegos Ni mwanamapinduzi wa Cuba aliyeshiriki kikamilifu Mapinduzi ya Nchi hiyo akiwa sambamba na akina Fidel castro, Che Guevara na wengineo. Ndege aliyopanda akitokea Camaguey alikotoka kumkamata mwanamapinduzi mwenzake aliyeasi Huber Matos, ilipotea angani na haijaonekana tena mpaka leo hii. Wengi wanadai Camilo alifanyiwa faulo na wenzake hasa Fidel Castro ili kuizima nyota yake iliyokuwa inang'aa kwa kasi. 3.Jimmy Hoffa Alikuwa ni kiongozi wa chama cha wafanyakazi nchini Marekani. Pia alikuwa anajihusisha na makundi ya kihalifu. Anajulikana kama kiongozi mtata, mpendwa rushwa na mwizi ambapo kuna wakati alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela kwa kosa la utakatishaji pesa. Aliachiwa kwa msamaha wa Rais wa kipindi hiko wa Marekani Richard Nixon. Mchana wa july 30 mwaka 1975 katika parking ya Mgahawa wa Red Fox, Jimmy hoffa alitoweka na hakuonekana tena mpaka leo. Haijulikani ni akina nani haswa walihusika katika kumteka, kuna wanaosema Serikali, kuna wanaosema Mafia. Licha ya msako mkali wa FBI kiongozi huyo hakuwahi kupatikana tena. 2. Harlod Holt Alikuwa ni Waziri Mkuu wa 17 wa Australia mpaka kupotea kwake. Jioni ya 17 december mwaka 1967 wananchi wa Australia hawatoisahau katika kumbukumbu zao baada ya kupotea kwa Waziri Mkuu wao. Waziri Mkuu Holt alipotea alipokuwa anaogelea baharini huko Portsea, Victoria nchini Australia alipokuwa katika likizo ya mwisho wa mwaka.Licha ya msako mkali wa kwenye maji, mwili wa Waziri Mkuu Holt hakuwahi kuoekana tena. Minong'ono ilizuka kuwa Waziri mkuu huyo alitekwa na Submarine (nyambizi) ya China kwakuwa alikuwa ni jasusi wao lakini hakuna aliyethibitisha. Kuna wanaosema Harold Holt alifeki kifo chake ili aishi kwa uhuru mara baada ya kuchoshwa na maisha ya siasa ikiwa ni miaka miwili tu toka achaguliwe kuwa Waziri Mkuu. Mpaka leo mwili wake haukuwahi kupatikana tena. 1.D.B Cooper D.B.Cooper ni jina linalotumika kumrejelea mwanaume mmoja wa makamo ambaye jioni ya November 24, mwaka 1971 alichukua kiasi cha Dola za Kimarekani 200,000 kama malipo mara baada ya kuiteka ndege huko portland nchini Marekani. Licha ya msako mkali wa zaidi ya miaka 45 uliofanywa na FBI kwa kushirikiana na idara nyingine za kiusalama nchini Marekani, bado D.B Cooper hafahamiki ni wapi alipo wala pesa alizopewa hazikuwahi kuingia kwenye mzunguko wala kupatikana. kuna wanaoamini kuwa D.B Cooper alitengenezwa na kusaidiwa na FBI wenyewe ili wajipatie pesa. Kuna wanaoamini Cooper alifariki mara baada ya kuruka toka kwenye ndege angani lakini mbona pesa hazijapatikana? D.B Cooper ameacha maswali mengi kuliko majibu na mpaka leo hajawahi kuonekana tena baada ya jioni ile ya mwaka 1971. MWISHO
    Like
    2
    ·262 Views
  • MAMBO 8 YA KUSHANGAZA YANAYOFANYWA NA MWILI WAKO KUKULINDA PASIPO WEWE KUJUA.

    C&P

    Mwili wa binadamu unafanya mambo mengi ya kibaiolojia ambayo mara nyingi ni vigumu kuyaelewa.

    Mwili una mifumo mbalimbali ya ulinzi ambayo inatulinda na hatari zinazoweza kutudhuru. Mifumo hiyo inatulinda masaa 24 ya siku, Siku zote 7 za wiki, katika mambo yote yanayoweza kuhatarisha maisha yetu.

    Yafuatayo ni mambo yanayofanywa na mwili ambayo ni kati ya hiyo mifumo ya ulinzi wa mwili wa binadamu.

    1. KUPIGA MIAYO (YAWNING)
    Lengo kubwa la kupiga muayo ni kuupoza ubongo baada ya joto kuzidi kwenye ubongo au baada ya ubongo kuchoka kufanya kazi.

    Vile vile kama ukiwa umechoka au una njaa husabababisha oxygen kupungua kwenye damu na kwenye mapafu, hii hupelekea tatizo la kupumua, hivyo kupiga miayo husaidia kuingiza oxygen ya ziada mwilini ili irudishe mwili katika hali yake ya kawaida.

    2. KUPIGA CHAFYA (SNEEZING)
    Mara nyingi tunapiga chafya pale pua zetu zinapokua zimejaa bakteria wa magonjwa ambao hawahitajiki mwilini, Vumbi pamoja na takataka mbali mbali zilizoingia kupitia pua.

    Hivyo kupiga chafya ni kitenda cha mwili kujisafisha kwa kuyatoa hayo matakataka nje yaliyoingia mwilini.

    3. KUJINYOOSHA (STRETCHING)
    Kuninyoosha mwili ni kitendo kisicho cha hiari ambacho lengo lake ni kuuandaa mwili kwa ajili ya kazi mbalimbali za kutumia nguvu utakazokabiliana nazo kwa siku nzima. Lakini pia kujinyoosha kunaipa misuli ya mwili mazoezi na kuiweka sawa vilevile kunarudisha mzunguko wa damu katika hali yake ya kawaida na kumtoa mtu katika uchovu.

    4. KWIKWI (HICCUPING)
    Najua umewahi kupata kwikwi, na mara nyingi mara baada ya kumaliza kula chakula. Je umeshawahi kujiuliza ile sauti ya ajabu ya kwikwi inasababishwa na nini au kwa sabababu gani watu hushikwa na kwikwi?

    Hiyo yote husababishwa na DIAPHRAGM (tamka DAYA - FRAM) kiungo kinachopatikana ndani ya mwili wa binadamu chini kabisa ya kifua baada ya mapafu(lungs). Kazi kubwa ya diaphragm ni kusaidia katika upumuaji, (inhale) na (exhale). Pale unapoingiza hewa ndani (inhale) diaphragm hushuka chini ili kusaidia kuivuta hewa ifike kwenye mapafu. Na unapotoa hewa nje (exhale) diaphragm hutulia kwa kubakia sehem yake ili kuwezesha hewa chafu kutoka nje kupitia pua na mdomo.

    Sasa basi, kuna wakati diaphragm kubugudhiwa na kuisababisha kushuka chini kwa kasi sana jambo linalosababisha wewe kuvuta hewa (inhale) kwa kasi isiyo ya kawaida kupitia koromeo la sauti, hewa ikifika kwenye box la sauti (larynx), sehem hiyo hujifunga kwa haraka sana ili kuzuia hewa isipite huko na ndipo KWIKWI hutokea.

    Mambo mengine yanayoweza kuibugudhi diaphragm na kuisababisha kufanya kazi vibaya mpaka kupelekea kwikwi ni kitendo cha kula haraka haraka au kuvimbewa.

    5. KUJIKUNJA KWA NGOZI YA VIDOLE VYA MIKONO BAADA YA KULOWA AU KUKAA MUDA MREFU KWENYE MAJI.
    Je umewahi shuhudia jinsi ngozi ya vidole vyako inavyojikunja baada ya kufua nguo muda mrefu au kushika maji muda mrefu? Unajua ni kwa sababu gani ngozi hujikunja kama ya mtu aliyezeeka angali yu kijana mara baada ya kukaa sana kwenye maji?

    Watu wengi kabla walizani kwamba kujikunja kwa ngozi hiyo hutokana na maji kuingia kwenye ngozi na hivyo ngozi hujikunja baada ya kulowa.

    Lakini wanasayansi baada ya kufanya utafiti kwa muda merefu juu ya nini hasa hupelekea ngozi kujikunja? Walisema HAPANA si kwa sababu ya ngozi kulowana. Na walikuja na majibu haya.

    Mwili unapokutana na majimaji mara moja hupeleka taarifa na kutafsiri kwamba mazingira hayo yana UTELEZI (Slippery) hivyo kutasababisha mikono kushindwa kushika (Grip) au kukamata vitu kwa urahisi kutokana na utelezi huo. Hapo mwili huchukua hatua ya haraka kuikunja ngozi ya mikono yako ili kurahisisha ushikaji wa vitu vinavyoteleza ndani ya maji pamoja na kutembea kwenye utelezi.

    6. VIPELE VIPELE VYA BARIDI KWENYE NGOZI (GOOSEBUMPS)
    Kazi kubwa ya vipele hivi ni kupunguza kiasi cha joto la mwili linalopotea kupitia matundu ya ngozi. Hivyo kwa kufanya hivi humfanya binadamu kutunza joto la mwili hata katika mazingira ambayo hali yake ya hewa si rafiki kwa mwili wa mwanadamu au ni yenye baridi sana.

    7. MACHOZI (TEARS)
    Zaidi ya kuwa majimaji (MUCOUS MEMBRANE ) yanayopatikana kwenye Macho ambayo kazi zake ni kulilinda jicho dhidi ya kitu chochote kigeni kinachoingia jichoni (mfano unapokata vitunguu au mdudu anapoingia jichoni huwa unatoa machozi mengi eeeh!! Pia dhidi ya upepo na moshi) na pia hutumika kama kilainishi cha jicho pale linapokuwa linazunguka zunguka (blink).

    Vilevile machozi yana kazi ya kupunguza HISIA ZA HUDHUNI zinazozalishwa mwilini. Wanasayansi wanaamini kuwa mtu anapokua mwenye msongo wa mawazo (stress) mwili hutengeneza kitu kipya ili kwenda kubugudhi na kuharibu maumivu yote ambayo mtu anajisikia. Hivyo machozi yanayozalishwa hapa huwa na kemikali na yanafahamika kama NATURAL PAINKILLER. Machozi haya ni tofauti na machozi ya kawaida, lengo lake hasa la kuzalishwa ni kwa ajili ya kuondoa kabisa maumivu yaliyozalishwa mwilini

    Hivyo mpaka hapa tumeona kua kuna machozi ya aina tatu ambayo ni
    i. Basal tears (vilainishi)
    ii. Reflex tears (mlinzi)
    iii. Emotion tears (mtuliza maumivu)

    8. KUSHTUKA USINGIZINI (MYOCLONIC JERKS or HYPNIC JERK).
    Je! Ushawahi kutokewa na hali hii? umelala halafu ghafla unashtuka usingizini kwa mguvu nyingi kama umepigwa na shoti ya umeme na akili inakurudi ghafla huku mapigo ya moyo yakikuenda mbio? Na hali hii ikakutokea pasipo hata kuota ndoto yoyote?

    Basi usiogope au kuwasingizia watu uchawi, hii ni hali ya sayansi ya mwili.na ni njia moja wapo katika ile mifumo ya mwili kujilinda.

    Je hutokeaje?

    Hii ni hali ya ajabu sana isiyofanywa kwa hiari ambayo huwatokea watu mara tu wamejinyoosha kitandani na kupitiwa na usingizi, mwili hutetemeshwa na kusukumwa kwa nguvu na mtu hushtuka katika hali kama vile kapigwa na shoti ya umeme. Hali hii inaweza kupelekea mtu hata kuanguka kitandani na humwamsha mara moja kutoka usingizini.

    Wanasayansi wanatuambia kua, pale tu unapopata usingizi kiwango cha upumuaji kinashuka ghafla, mapigo ya moyo nayo taratibu yanapungua, misuli inatulia kwa ku-relax, Kitu cha AJABU hapa ubongo unatafsiri hali hii kama ni DALILI ZA KIFO (brain's misinterpretation of muscle relaxation), hivyo huchukua hatua za haraka za kuushtua mwili kwa kuutetemesha au kuuskuma kwa nguvu, hali ambayo humfanya mtu kuamka kutoka usingizini kwa KURUKA kitu ambacho ni hali isiyo ya kawaida.

    Hali hii ikimtokea mtu huambatana na kuongezeka kwa mapigo ya moyo (rapid heartbeat), kuhema haraka haraka, na wakati mwingine mtu hutokwa na jasho jingi.

    Wakati mwingine mtu huamka ametoa macho na kama ukimwangalia, nae huishia hukuangalia tu huku akikosa la kukujibu endapo utamuuliza vipi kuna tatizo gani?

    MWILI WAKO NI ZAIDI YA UNAVYOUJUA. JAMBO LA MSINGI NI KUONDOA HOFU KWANI MWILI WAKO UNAJUA NINI UFANYE NA WAKATI GANI ILI KUKULINDA USIKU NA MCHANA KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO.

    Share pia wengine wajue sio kila kitu ni uchawi
    MAMBO 8 YA KUSHANGAZA YANAYOFANYWA NA MWILI WAKO KUKULINDA PASIPO WEWE KUJUA. C&P Mwili wa binadamu unafanya mambo mengi ya kibaiolojia ambayo mara nyingi ni vigumu kuyaelewa. Mwili una mifumo mbalimbali ya ulinzi ambayo inatulinda na hatari zinazoweza kutudhuru. Mifumo hiyo inatulinda masaa 24 ya siku, Siku zote 7 za wiki, katika mambo yote yanayoweza kuhatarisha maisha yetu. Yafuatayo ni mambo yanayofanywa na mwili ambayo ni kati ya hiyo mifumo ya ulinzi wa mwili wa binadamu. 1. KUPIGA MIAYO (YAWNING) Lengo kubwa la kupiga muayo ni kuupoza ubongo baada ya joto kuzidi kwenye ubongo au baada ya ubongo kuchoka kufanya kazi. Vile vile kama ukiwa umechoka au una njaa husabababisha oxygen kupungua kwenye damu na kwenye mapafu, hii hupelekea tatizo la kupumua, hivyo kupiga miayo husaidia kuingiza oxygen ya ziada mwilini ili irudishe mwili katika hali yake ya kawaida. 2. KUPIGA CHAFYA (SNEEZING) Mara nyingi tunapiga chafya pale pua zetu zinapokua zimejaa bakteria wa magonjwa ambao hawahitajiki mwilini, Vumbi pamoja na takataka mbali mbali zilizoingia kupitia pua. Hivyo kupiga chafya ni kitenda cha mwili kujisafisha kwa kuyatoa hayo matakataka nje yaliyoingia mwilini. 3. KUJINYOOSHA (STRETCHING) Kuninyoosha mwili ni kitendo kisicho cha hiari ambacho lengo lake ni kuuandaa mwili kwa ajili ya kazi mbalimbali za kutumia nguvu utakazokabiliana nazo kwa siku nzima. Lakini pia kujinyoosha kunaipa misuli ya mwili mazoezi na kuiweka sawa vilevile kunarudisha mzunguko wa damu katika hali yake ya kawaida na kumtoa mtu katika uchovu. 4. KWIKWI (HICCUPING) Najua umewahi kupata kwikwi, na mara nyingi mara baada ya kumaliza kula chakula. Je umeshawahi kujiuliza ile sauti ya ajabu ya kwikwi inasababishwa na nini au kwa sabababu gani watu hushikwa na kwikwi? Hiyo yote husababishwa na DIAPHRAGM (tamka DAYA - FRAM) kiungo kinachopatikana ndani ya mwili wa binadamu chini kabisa ya kifua baada ya mapafu(lungs). Kazi kubwa ya diaphragm ni kusaidia katika upumuaji, (inhale) na (exhale). Pale unapoingiza hewa ndani (inhale) diaphragm hushuka chini ili kusaidia kuivuta hewa ifike kwenye mapafu. Na unapotoa hewa nje (exhale) diaphragm hutulia kwa kubakia sehem yake ili kuwezesha hewa chafu kutoka nje kupitia pua na mdomo. Sasa basi, kuna wakati diaphragm kubugudhiwa na kuisababisha kushuka chini kwa kasi sana jambo linalosababisha wewe kuvuta hewa (inhale) kwa kasi isiyo ya kawaida kupitia koromeo la sauti, hewa ikifika kwenye box la sauti (larynx), sehem hiyo hujifunga kwa haraka sana ili kuzuia hewa isipite huko na ndipo KWIKWI hutokea. Mambo mengine yanayoweza kuibugudhi diaphragm na kuisababisha kufanya kazi vibaya mpaka kupelekea kwikwi ni kitendo cha kula haraka haraka au kuvimbewa. 5. KUJIKUNJA KWA NGOZI YA VIDOLE VYA MIKONO BAADA YA KULOWA AU KUKAA MUDA MREFU KWENYE MAJI. Je umewahi shuhudia jinsi ngozi ya vidole vyako inavyojikunja baada ya kufua nguo muda mrefu au kushika maji muda mrefu? Unajua ni kwa sababu gani ngozi hujikunja kama ya mtu aliyezeeka angali yu kijana mara baada ya kukaa sana kwenye maji? Watu wengi kabla walizani kwamba kujikunja kwa ngozi hiyo hutokana na maji kuingia kwenye ngozi na hivyo ngozi hujikunja baada ya kulowa. Lakini wanasayansi baada ya kufanya utafiti kwa muda merefu juu ya nini hasa hupelekea ngozi kujikunja? Walisema HAPANA si kwa sababu ya ngozi kulowana. Na walikuja na majibu haya. Mwili unapokutana na majimaji mara moja hupeleka taarifa na kutafsiri kwamba mazingira hayo yana UTELEZI (Slippery) hivyo kutasababisha mikono kushindwa kushika (Grip) au kukamata vitu kwa urahisi kutokana na utelezi huo. Hapo mwili huchukua hatua ya haraka kuikunja ngozi ya mikono yako ili kurahisisha ushikaji wa vitu vinavyoteleza ndani ya maji pamoja na kutembea kwenye utelezi. 6. VIPELE VIPELE VYA BARIDI KWENYE NGOZI (GOOSEBUMPS) Kazi kubwa ya vipele hivi ni kupunguza kiasi cha joto la mwili linalopotea kupitia matundu ya ngozi. Hivyo kwa kufanya hivi humfanya binadamu kutunza joto la mwili hata katika mazingira ambayo hali yake ya hewa si rafiki kwa mwili wa mwanadamu au ni yenye baridi sana. 7. MACHOZI (TEARS) Zaidi ya kuwa majimaji (MUCOUS MEMBRANE ) yanayopatikana kwenye Macho ambayo kazi zake ni kulilinda jicho dhidi ya kitu chochote kigeni kinachoingia jichoni (mfano unapokata vitunguu au mdudu anapoingia jichoni huwa unatoa machozi mengi eeeh!! Pia dhidi ya upepo na moshi) na pia hutumika kama kilainishi cha jicho pale linapokuwa linazunguka zunguka (blink). Vilevile machozi yana kazi ya kupunguza HISIA ZA HUDHUNI zinazozalishwa mwilini. Wanasayansi wanaamini kuwa mtu anapokua mwenye msongo wa mawazo (stress) mwili hutengeneza kitu kipya ili kwenda kubugudhi na kuharibu maumivu yote ambayo mtu anajisikia. Hivyo machozi yanayozalishwa hapa huwa na kemikali na yanafahamika kama NATURAL PAINKILLER. Machozi haya ni tofauti na machozi ya kawaida, lengo lake hasa la kuzalishwa ni kwa ajili ya kuondoa kabisa maumivu yaliyozalishwa mwilini Hivyo mpaka hapa tumeona kua kuna machozi ya aina tatu ambayo ni i. Basal tears (vilainishi) ii. Reflex tears (mlinzi) iii. Emotion tears (mtuliza maumivu) 8. KUSHTUKA USINGIZINI (MYOCLONIC JERKS or HYPNIC JERK). Je! Ushawahi kutokewa na hali hii? umelala halafu ghafla unashtuka usingizini kwa mguvu nyingi kama umepigwa na shoti ya umeme na akili inakurudi ghafla huku mapigo ya moyo yakikuenda mbio? Na hali hii ikakutokea pasipo hata kuota ndoto yoyote? Basi usiogope au kuwasingizia watu uchawi, hii ni hali ya sayansi ya mwili.na ni njia moja wapo katika ile mifumo ya mwili kujilinda. Je hutokeaje? Hii ni hali ya ajabu sana isiyofanywa kwa hiari ambayo huwatokea watu mara tu wamejinyoosha kitandani na kupitiwa na usingizi, mwili hutetemeshwa na kusukumwa kwa nguvu na mtu hushtuka katika hali kama vile kapigwa na shoti ya umeme. Hali hii inaweza kupelekea mtu hata kuanguka kitandani na humwamsha mara moja kutoka usingizini. Wanasayansi wanatuambia kua, pale tu unapopata usingizi kiwango cha upumuaji kinashuka ghafla, mapigo ya moyo nayo taratibu yanapungua, misuli inatulia kwa ku-relax, Kitu cha AJABU hapa ubongo unatafsiri hali hii kama ni DALILI ZA KIFO (brain's misinterpretation of muscle relaxation), hivyo huchukua hatua za haraka za kuushtua mwili kwa kuutetemesha au kuuskuma kwa nguvu, hali ambayo humfanya mtu kuamka kutoka usingizini kwa KURUKA kitu ambacho ni hali isiyo ya kawaida. Hali hii ikimtokea mtu huambatana na kuongezeka kwa mapigo ya moyo (rapid heartbeat), kuhema haraka haraka, na wakati mwingine mtu hutokwa na jasho jingi. Wakati mwingine mtu huamka ametoa macho na kama ukimwangalia, nae huishia hukuangalia tu huku akikosa la kukujibu endapo utamuuliza vipi kuna tatizo gani? MWILI WAKO NI ZAIDI YA UNAVYOUJUA. JAMBO LA MSINGI NI KUONDOA HOFU KWANI MWILI WAKO UNAJUA NINI UFANYE NA WAKATI GANI ILI KUKULINDA USIKU NA MCHANA KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO. Share pia wengine wajue sio kila kitu ni uchawi
    ·213 Views
  • MANSA MUSA
    .
    Mansa Musa alizaliwa 1280 katika familia ya watawala. Nduguye , Mansa Abu-Bakr, alitawala ufamle huo hadi 1312, wakati alipoamua kwenda safari. Kulingana na mwanahistoria wa karne ya 14 Shibab al-Umari, Abu-Bakr alipendelea sana kuiona bahari ya Atlantic na kile ilichokuwa nacho. Aliripotiwa kuanza safari na msafara wa meli 2000 na maelfu ya wanaume na wanawake pamoja na watumwa. Walienda na hawakurudi tena. Wengine kama vile mwanahistoria wa Marekani Ivan Van Sertima anadai kwamba waliwasili Marekani Kusini. Lakini hakuna ushahidi. Ukweli ni kwamba Mansa Musa alirithi ufalme ulioachwa nyuma na nduguye. Chini ya uongozi wake ufalme wa Mali uliimarika kwa kiwango kikubwa.
    Watag marafk zako waje wapate kufahamu mengi wasiyo yajua kuhusu Mansa Musa pia isisahau ku follow hawa watu.
    .
    .
    .
    Mfalme huyo aliripotiwa kuondoka Mali na msafara wa watu 60,000. Alibeba ufalme wake wote na maafisa wake , wanajeshi, watumbuizaji , madereva wa ngamia na watumwa 12,000 mbali na idadi kubwa ya mbuzi , kondoo na chakula. Ulikuwa mji uliokuwa ukipitia katika jangwa. Mji ambao wakaazi wake hadi watumwa wake walikuwa wamevalia dhahabu na nguo za hariri. Kulikuwa na ngamia 100 ambao kila mmojawao alikuwa akibeba mamia ya pauni za dhahabu. Utajiri huo ulionekana zaidi wakati msafara huo ulipowasili mjini Cairo ambapo ulionekana.
    .
    .
    Kampuni ya kiteknolojia ya Marekani SmartAsset.com inakadiria kwamba kutokana na kuanguka kwa bei ya dhahabu, Hija ya Mansa Musa ilisababisha hasara ya $1.5bn (£1.1bn) katika uchumi wa eneo la mashariki ya kati. Alipokuwa akirudi nyumbani, Mansa Musa alpitia tena Misri na kulingana wachache akajaribu kusaidia uchumi wa taifa hilo kwa kuondoa dhahabu iliokuwepo kupitia kuiomba kwa kiwango cha juu kutoka kwa wafanyibiashara wa Misri. Wengine wanasema kuwa aligharamika sana hadi dhahabu alizokuwa nazo zikaisha. Lucy Duran wa Shule ya African and Oriental Studies mjini London anasema kwamba wanahistoria wa Mali walikasirishwa naye. ''Alitoa dhahabu nyingi ya Mali hali ambayo iliwafanya wanahistoria hao kutomsifu katika nyimbo zao na hadithi kwa kuwa wanaona kwamba alipoteza mali nyingi ya taifa hilo nje ya ufalme wake'', alisema.


    .
    SHUKRANI
    MANSA MUSA . Mansa Musa alizaliwa 1280 katika familia ya watawala. Nduguye , Mansa Abu-Bakr, alitawala ufamle huo hadi 1312, wakati alipoamua kwenda safari. Kulingana na mwanahistoria wa karne ya 14 Shibab al-Umari, Abu-Bakr alipendelea sana kuiona bahari ya Atlantic na kile ilichokuwa nacho. Aliripotiwa kuanza safari na msafara wa meli 2000 na maelfu ya wanaume na wanawake pamoja na watumwa. Walienda na hawakurudi tena. Wengine kama vile mwanahistoria wa Marekani Ivan Van Sertima anadai kwamba waliwasili Marekani Kusini. Lakini hakuna ushahidi. Ukweli ni kwamba Mansa Musa alirithi ufalme ulioachwa nyuma na nduguye. Chini ya uongozi wake ufalme wa Mali uliimarika kwa kiwango kikubwa. Watag marafk zako waje wapate kufahamu mengi wasiyo yajua kuhusu Mansa Musa pia isisahau ku follow hawa watu. . . . Mfalme huyo aliripotiwa kuondoka Mali na msafara wa watu 60,000. Alibeba ufalme wake wote na maafisa wake , wanajeshi, watumbuizaji , madereva wa ngamia na watumwa 12,000 mbali na idadi kubwa ya mbuzi , kondoo na chakula. Ulikuwa mji uliokuwa ukipitia katika jangwa. Mji ambao wakaazi wake hadi watumwa wake walikuwa wamevalia dhahabu na nguo za hariri. Kulikuwa na ngamia 100 ambao kila mmojawao alikuwa akibeba mamia ya pauni za dhahabu. Utajiri huo ulionekana zaidi wakati msafara huo ulipowasili mjini Cairo ambapo ulionekana. . . Kampuni ya kiteknolojia ya Marekani SmartAsset.com inakadiria kwamba kutokana na kuanguka kwa bei ya dhahabu, Hija ya Mansa Musa ilisababisha hasara ya $1.5bn (£1.1bn) katika uchumi wa eneo la mashariki ya kati. Alipokuwa akirudi nyumbani, Mansa Musa alpitia tena Misri na kulingana wachache akajaribu kusaidia uchumi wa taifa hilo kwa kuondoa dhahabu iliokuwepo kupitia kuiomba kwa kiwango cha juu kutoka kwa wafanyibiashara wa Misri. Wengine wanasema kuwa aligharamika sana hadi dhahabu alizokuwa nazo zikaisha. Lucy Duran wa Shule ya African and Oriental Studies mjini London anasema kwamba wanahistoria wa Mali walikasirishwa naye. ''Alitoa dhahabu nyingi ya Mali hali ambayo iliwafanya wanahistoria hao kutomsifu katika nyimbo zao na hadithi kwa kuwa wanaona kwamba alipoteza mali nyingi ya taifa hilo nje ya ufalme wake'', alisema. . SHUKRANI 🙏🙏🙏🙏🙏
    Like
    1
    ·153 Views
  • ELIMU; HISTORIA NA SIFA ZA ZIWA VICTORIA .
    _______________________________

    Ziwa hili kabla ya kuitwa Victoria, lilikuwa na majina mengi yaliyotokana na wakazi walioishi kando kando yake, mfano; Kule Uganda liliitwa "Nnalubaale" kwa lugha ya Luganda, Nchini Kenya Waluo wao waliliita "Nam Lolwe" na huku Tanzania lilijulikana kama "Nyanza" kwa lugha za makabila ya wabantu.

    Baadae lilipewa jina la Malkia wa Uingereza aliyeitwa Alexandrina Victoria aliyeitawala Uingereza kuanzia mwaka 1837 hadi 1901.

    Wakati wa Ukoloni, Malkia huyu alituma wapelelezi wake kuja Afrika na ndipo Bw. John Hanning Speke na Richard Francis Burton waliamua kufanya chunguzi wa kina dhidi ziwa hili lote toka kasikazini hadi wakafanikiwa kufika katika fukwe za ng'ambo ya kusini mwaka 1858, Na wakawa ndio wazungu wa kwanza kuandika taarifa juu ya ziwa hili.
    Baada ya uchunguzi waliwasilisha ripoti kwa Malkia ambaye ndiye aliyewezesha shughuli nzima ya upelelezi na serikali ya Uingereza ikaamua kuliita kwa jina la Victoria kama sehemu ya heshima ya kumuenzi Kiongozi huyo kama ilivyo kwa maeneo mengine yanavyopewa majina ya viongozi na watu mashuhuri.


    SIFA ZAKE:
    1. Ziwa hili lina upana wa kilomita za mraba 69, 584 Japo eneo lote linalopatikana maji ni kilomita za Mraba 169, 858

    2. Victoria inakadiriwa kuwa na Urefu wa kina kuanzia mita 80 hadi mita 84 ambazo ni sawa na futi 262 hadi futi 276. Lakini maeneo mengi yana wastani wa kina cha mita 40 ambazo ni sawa na futi 130.

    3. Ziwa Victoria limegawanyika katika Nchi tatu; Tanzania, Kenya na Uganda.
    Upande wa Tanzania ziwa lina ukubwa wa kilomita za mraba 33,700 sawa na 49% ya ziwa lote, Nchini Uganda ziwa lina ukubwa wa kilomita za mraba 31, 000 sawa na 45% ya ziwa lote na Nchini Kenya ziwa lina ukubwa wa kilomita za mraba 4,100 sawa na 6% ya ziwa lote.

    4. Ziwa Victoria linakadiriwa kuwa na aina zaidi ya 500 za Samaki japo tafiti zinasema kwamba 40% ya aina zote za Samaki ziko mbioni kutoweka kabisa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kibinadamu na zile za asili.

    5. Ziwa hili lina zaidi ya visiwa 100 ambavyo hukaliwa na watu na vingine hatukaliwi na watu

    5. Ziwa hili ni la kwanza kwa ukubwa Barani Afrika na la pili kwa eneo lenye maji baridi Duniani baada ya Ziiwa Superior la Marekani, Lakini pia ni la tatu kwa ukubwa katika maziwa yote Duniani

    6. Shughuli kuu zifanyikazo katika ziwa hili ni Uvuvi, Usafirishaji, Utalii, Uvunaji wa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali n.k.

    7. Ziwa hili hupokea maji kutoka mito mikubwa kama vile Mto Kagera, Mto Mara n.k. mbali na hapo Ziwa hili humwaga maji yake katika Mto Nile.
    ELIMU; HISTORIA NA SIFA ZA ZIWA VICTORIA . _______________________________ Ziwa hili kabla ya kuitwa Victoria, lilikuwa na majina mengi yaliyotokana na wakazi walioishi kando kando yake, mfano; Kule Uganda liliitwa "Nnalubaale" kwa lugha ya Luganda, Nchini Kenya Waluo wao waliliita "Nam Lolwe" na huku Tanzania lilijulikana kama "Nyanza" kwa lugha za makabila ya wabantu. Baadae lilipewa jina la Malkia wa Uingereza aliyeitwa Alexandrina Victoria aliyeitawala Uingereza kuanzia mwaka 1837 hadi 1901. Wakati wa Ukoloni, Malkia huyu alituma wapelelezi wake kuja Afrika na ndipo Bw. John Hanning Speke na Richard Francis Burton waliamua kufanya chunguzi wa kina dhidi ziwa hili lote toka kasikazini hadi wakafanikiwa kufika katika fukwe za ng'ambo ya kusini mwaka 1858, Na wakawa ndio wazungu wa kwanza kuandika taarifa juu ya ziwa hili. Baada ya uchunguzi waliwasilisha ripoti kwa Malkia ambaye ndiye aliyewezesha shughuli nzima ya upelelezi na serikali ya Uingereza ikaamua kuliita kwa jina la Victoria kama sehemu ya heshima ya kumuenzi Kiongozi huyo kama ilivyo kwa maeneo mengine yanavyopewa majina ya viongozi na watu mashuhuri. SIFA ZAKE: 1. Ziwa hili lina upana wa kilomita za mraba 69, 584 Japo eneo lote linalopatikana maji ni kilomita za Mraba 169, 858 2. Victoria inakadiriwa kuwa na Urefu wa kina kuanzia mita 80 hadi mita 84 ambazo ni sawa na futi 262 hadi futi 276. Lakini maeneo mengi yana wastani wa kina cha mita 40 ambazo ni sawa na futi 130. 3. Ziwa Victoria limegawanyika katika Nchi tatu; Tanzania, Kenya na Uganda. Upande wa Tanzania ziwa lina ukubwa wa kilomita za mraba 33,700 sawa na 49% ya ziwa lote, Nchini Uganda ziwa lina ukubwa wa kilomita za mraba 31, 000 sawa na 45% ya ziwa lote na Nchini Kenya ziwa lina ukubwa wa kilomita za mraba 4,100 sawa na 6% ya ziwa lote. 4. Ziwa Victoria linakadiriwa kuwa na aina zaidi ya 500 za Samaki japo tafiti zinasema kwamba 40% ya aina zote za Samaki ziko mbioni kutoweka kabisa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kibinadamu na zile za asili. 5. Ziwa hili lina zaidi ya visiwa 100 ambavyo hukaliwa na watu na vingine hatukaliwi na watu 5. Ziwa hili ni la kwanza kwa ukubwa Barani Afrika na la pili kwa eneo lenye maji baridi Duniani baada ya Ziiwa Superior la Marekani, Lakini pia ni la tatu kwa ukubwa katika maziwa yote Duniani 6. Shughuli kuu zifanyikazo katika ziwa hili ni Uvuvi, Usafirishaji, Utalii, Uvunaji wa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali n.k. 7. Ziwa hili hupokea maji kutoka mito mikubwa kama vile Mto Kagera, Mto Mara n.k. mbali na hapo Ziwa hili humwaga maji yake katika Mto Nile.
    Like
    1
    ·127 Views
  • HII KITAALAMU TUNAIITAJE

    Mnamo 1993, Sevilla walipoteza uongozi wao mbele ya Barcelona baada ya kuruhusu mabao mawili ndani ya dakika moja. Kocha wa Sevilla, Bilardo, alikasirika na alitaka kuwafundisha somo wachezaji wake.

    Asubuhi iliyofuata, Bilardo alileta watoto 11 kutoka timu ya chini ya miaka 10 na kuwataka kucheza dhidi ya wachezaji wake. Aliwaambia wachezaji wake wacheze kwa umakini, kana kwamba wanakabiliana na timu ya watu wazima. Baada ya chini ya dakika moja, timu ya wakubwa ilifunga bao. Dakika ya kwanza ilipomalizika, Bilardo akapuliza kipyenga chake na kumaliza mechi.

    Aliipongeza timu ya watoto na kisha akawakusanya wachezaji wake katikati ya duara, akisema kwa hasira: "Umeona, nyie wahuni?! Hata timu ya watoto hairuhusu mabao mawili kwa dakika moja!"

    HII KITAALAMU TUNAIITAJE😀 🔙 Mnamo 1993, Sevilla walipoteza uongozi wao mbele ya Barcelona baada ya kuruhusu mabao mawili ndani ya dakika moja. Kocha wa Sevilla, Bilardo, alikasirika na alitaka kuwafundisha somo wachezaji wake. Asubuhi iliyofuata, Bilardo alileta watoto 11 kutoka timu ya chini ya miaka 10 na kuwataka kucheza dhidi ya wachezaji wake. Aliwaambia wachezaji wake wacheze kwa umakini, kana kwamba wanakabiliana na timu ya watu wazima. Baada ya chini ya dakika moja, timu ya wakubwa ilifunga bao. Dakika ya kwanza ilipomalizika, Bilardo akapuliza kipyenga chake na kumaliza mechi. Aliipongeza timu ya watoto na kisha akawakusanya wachezaji wake katikati ya duara, akisema kwa hasira: "Umeona, nyie wahuni?! Hata timu ya watoto hairuhusu mabao mawili kwa dakika moja!" 😂💀
    Like
    1
    ·70 Views
  • Bombardier Q400 Next Generation.
    #Dash8 #Q400 #NextGen

    Uundaji: Canada
    Kampuni: De Havilland Canada/Bombardier Aeropace
    Abiria: 74-90
    Urefu: mita 32
    Kimo: futi 6.40
    Upana: futi 8
    Nguvu/Injini: Hp 10,142
    Mwendokasi: 666.7 km/h
    Umbali iendapo: km 2522
    Umbali wa juu: futi 27,000
    Uwezo/Ubebaji: tani 8.7
    Ubebaji Mafuta: lita 6617
    Barabara/kuruka: mita 1067
    Barabara/kutua: mita 1286
    Ulaji mafuta: lita 14/dakika
    Bei: U$d 27-33 Milion

    #Note:
    Mchanganuo mwepesi wa makadirio ya chini, kati, au juu kwa ndege husika.

    #karibu #Mwanza #BombardierQ400
    #TGFA #ATCL #TANZANIA #GOVERNMENT
    Bombardier Q400 Next Generation. #Dash8 #Q400 #NextGen Uundaji: Canada Kampuni: De Havilland Canada/Bombardier Aeropace Abiria: 74-90 Urefu: mita 32 Kimo: futi 6.40 Upana: futi 8 Nguvu/Injini: Hp 10,142 Mwendokasi: 666.7 km/h Umbali iendapo: km 2522 Umbali wa juu: futi 27,000 Uwezo/Ubebaji: tani 8.7 Ubebaji Mafuta: lita 6617 Barabara/kuruka: mita 1067 Barabara/kutua: mita 1286 Ulaji mafuta: lita 14/dakika Bei: U$d 27-33 Milion #Note: Mchanganuo mwepesi wa makadirio ya chini, kati, au juu kwa ndege husika. #karibu #Mwanza #BombardierQ400 #TGFA #ATCL #TANZANIA #GOVERNMENT
    ·472 Views
  • MJUE MNYAMA MAMBA KIUNDANI

    Mamba ni moja ya mnyama alaye nyama, maisha yake ni majini na nchi kavu tuu, watu wengi hufikiri mamba ni mnyama anayezaa, lakini sivyo mamba ni mnyama anayetaga na hutaga mayai kwa wastani wa 35 mpaka 50, najua utajiuliza sasa huyu kiumbe anaatamia vipi wakati maisha yake ni ya heka heka, ukweli ni huu hutengeneza kiota kwa kuchimba pembezoni mwa mto, na kisha kufukia mayai yake mpaka hapo ambapo mayai yatakapokuwa tayari.

    Mayai yake yanapokuwa tayari kwa kutoa watoto, mamba husikia sauti na akiyatoa mayai hayo katika kiota watoto wake hujitoa wenyewe, yaani watoto hutumia nguvu binafsi na kuvunja gamba la yai, kisha hutoka katika ulimwengu mpyaa, kazi ya mama kwa wakati huo itakuwa ni kuhakikisha anawachukua wanaye na kuwapeleka majini, ambapo huwabeba kwa kutumia mdomo wake.

    Wakati huu wanyama wote ambapo huliwa na mamba ndio wakati ambapo hulipiza kisasi, mfano kenge, mijusi wakubwa pamoja na ndege, humtegea anapopeleka watoto wa awamu ya kwanza wale wanaosaria hujeruhiwa vibaya, au kubebwa kama chakula na wanyonge wa Mamba, na mamba hujisikia tabu sana kiasi kwamba anapoibuka katika maji huwatizama kwa jicho la Shari sana.
    Watoto wa Mamba ukiwaona katika udogo wao ni wanashangaza sana, hutokaa ufikirie kwamba ndio hao wafikapo ukubwani hufikia urefu wa futi 13 na zaidi, na uzito wa kilo zaidi ya 1000, ni viumbe ambao huonekana wadogo sana unaweza hisi labda ni kenge tuu.

    Kwa taarifa yako Mamba ni miongoni mwa wanyama wakubwa sana duniani, meno yake yamejipanga kama msumeno, ana macho makubwa, ngozi ngumu na mkia mrefu ambao humsaidia katika kuwinda, hupendelea sana kukaa kwenye maji lakini jua lichomozapo na likaribiapo kuzama hupendelea sana kwenda kuchukua vitamin.

    Ajabu la mnyama huyu ni moja, pamoja kwamba wanyama wanaokula nyama tuu ndio huishi muda mfupi, lakini yeye maisha yake ni marefu anaweza kugonga miaka 50 na zaidi kabisa, muone vile na sura yake mbaya vile vile lakini ni mnyama ambaye anafahamu anafanya nini na kwa wakati gani, Dume huwa refu na zito kuliko jike.

    CHAKULA CHAKE

    Chakula kikuu cha Mamba ni nyama tuu, hutafuna samaki, wanyama wadogo wadogo nk, hapo ni wakati umri ukiwa bado Mdogo, lakini umri unapoongezeka mnyama mamba humuwinda moja kwa moja nyumbu, hawa huwakamata kiurahisi kwa sababu ya ujinga wao wanapovuka MAJI au kunywa maji, Twiga anapofata maji, Nyati pia anapoenda kunywa MAJI , wakati mwingine hujaribu hata kumuwinda tembo Mdogo, lakini anapotokea mama wa tembo zoezi hill huishia hapo.

    SIFA ZAKE ZA KIPEKEE

    1. Jamaa ni fundi wa kuogelea vibaya mno, ana kasi kubwa sana ndani ya maji.
    2. Anaweza kuishi majini na nchi kavu.
    3. Mashambulizi yake ni ya kishitukiza.
    4. Ana akili na mjanja sana anapomuona mnyama ambaye hana uwezo wa kucheza naye hujifanya amelala usingizi ili uingie katika maji.
    5. Ndio mnyama pekee ambaye amewatafuna sana binadamu.
    6. Anapoiona hatari hukimbilia katika maji haraka sana, na akifika huko anakukaribisha.
    7. Hapatani na simba kabisa kwakuwa ndiye mnyama, ambaye hupenda kumbughuzi awapo mapumzikoni, hivyo wawili hawa wanapokutana ni kama watani.
    8. Mamba anajua sana kuzira, hupenda kuachana na vitu vinavyomuumiza kichwa.
    9. Wakati mwingine huigiza amekufa ili kuwakamata samaki wakubwa kwa urahisi, akiwa majini utaona anazunguka tuu kama anapelekwa na maji, samaki wakubwa hubaki kumshangaa.
    10. Ngozi yake ni dili sana, ila ukikamatwa nayo popote duniani utashughulikiwa maana anarindwa na Sharia umoja wa mataifa.
    11. Aonapo hatari hukimbilia majini na akifika tuu hugeuza kichwa chake alikotoka.
    12. Mkia wake pia huutumumia kumsukumia kiumbe anayejaribu kumshangaa nchi kavu, na ukishaingia kwenye naye huja.
    13.:huwa na nguvu zaidi akiwa kwenye maji, kuliko nchi kavu.
    14. Ni mnyama anayeua haraka sana, tofauti na wanyama wengine walao nyama, hivyo kifo chake sio cha mateso sana kama kwa simba au chui, ila kwa mtizamaji atapata hofu Mara dufu kuliko akiona mauaji ya wanyama wengine.
    15. Anaweza kunyata katika maji na kiumbe aliyepo pembeni asishituke kabisa, akiwa mwanadamu ndio kabisa atakosa habari.
    16. Mamba jike hapendi mambo ya mahaba, Mara nyingi hutumia muda mwingi kulikimbia dume.
    17. Madume kwa sababu ya ukubwa wao na uzito, wakati mwingine hutumia ubabe kulipanda jike lake.
    18. Dume LA mamba lina msaada mdogo sana kwa jike, msaada huo hutoa pindi linapokuwa na muda wa ziada.
    19. Kutafuta chakula huweza kushirikiana.
    20. Ni mnyama pekee anayekula nyama na anaishi umri mrefu, tofauti na wanyama wengine ambao hula nyama umri wao wa kuishi ni mfupi, hii ni kwasababu moja tuu mfumo wake wa mmeng'enyo wa chakula upo vizuri anaweza kula hata mifupa pasina kuchagua steki tuu.
    21. Wakati mwingine mamba humeza mawe lakini bado sijapata uhakika mawe hayo sababu ya kumeza ni IPI, baadhi ya watu hudai mawe hayo humsaidia katika mfumo wa umeng'enyaji wa chakula na wengine hudai humsaidia katika kuogelea.

    UKIKUTANA NAYE UFANYE NINI

    Ushauri wa pekee ni kukimbia tuu, kwani hakuna namna yoyote inayoweza kukufanya utoke salama, mnyama huyu ana nguvu kubwa ya mwili na ni kiumbe ambaye huwezi pambana naye hata ukiwa na silaha kwa sababu ya ngozi yake ngumu.
    Epuka kukaa sehemu ambazo kuna uwezekano wa uwepo wa kiumbe huyu ni hatari sana, sehemu hizo ni kama mito iliyopo vijijini au mbugani, kaa mbali kabisa na fukwe za mito hiyo, wala usidiriki kunawa au kutaka kunywa maji yake bila ruhusa ya anayewaongoza.

    Like na Follow t
    MJUE MNYAMA MAMBA KIUNDANI Mamba ni moja ya mnyama alaye nyama, maisha yake ni majini na nchi kavu tuu, watu wengi hufikiri mamba ni mnyama anayezaa, lakini sivyo mamba ni mnyama anayetaga na hutaga mayai kwa wastani wa 35 mpaka 50, najua utajiuliza sasa huyu kiumbe anaatamia vipi wakati maisha yake ni ya heka heka, ukweli ni huu hutengeneza kiota kwa kuchimba pembezoni mwa mto, na kisha kufukia mayai yake mpaka hapo ambapo mayai yatakapokuwa tayari. Mayai yake yanapokuwa tayari kwa kutoa watoto, mamba husikia sauti na akiyatoa mayai hayo katika kiota watoto wake hujitoa wenyewe, yaani watoto hutumia nguvu binafsi na kuvunja gamba la yai, kisha hutoka katika ulimwengu mpyaa, kazi ya mama kwa wakati huo itakuwa ni kuhakikisha anawachukua wanaye na kuwapeleka majini, ambapo huwabeba kwa kutumia mdomo wake. Wakati huu wanyama wote ambapo huliwa na mamba ndio wakati ambapo hulipiza kisasi, mfano kenge, mijusi wakubwa pamoja na ndege, humtegea anapopeleka watoto wa awamu ya kwanza wale wanaosaria hujeruhiwa vibaya, au kubebwa kama chakula na wanyonge wa Mamba, na mamba hujisikia tabu sana kiasi kwamba anapoibuka katika maji huwatizama kwa jicho la Shari sana. Watoto wa Mamba ukiwaona katika udogo wao ni wanashangaza sana, hutokaa ufikirie kwamba ndio hao wafikapo ukubwani hufikia urefu wa futi 13 na zaidi, na uzito wa kilo zaidi ya 1000, ni viumbe ambao huonekana wadogo sana unaweza hisi labda ni kenge tuu. Kwa taarifa yako Mamba ni miongoni mwa wanyama wakubwa sana duniani, meno yake yamejipanga kama msumeno, ana macho makubwa, ngozi ngumu na mkia mrefu ambao humsaidia katika kuwinda, hupendelea sana kukaa kwenye maji lakini jua lichomozapo na likaribiapo kuzama hupendelea sana kwenda kuchukua vitamin. Ajabu la mnyama huyu ni moja, pamoja kwamba wanyama wanaokula nyama tuu ndio huishi muda mfupi, lakini yeye maisha yake ni marefu anaweza kugonga miaka 50 na zaidi kabisa, muone vile na sura yake mbaya vile vile lakini ni mnyama ambaye anafahamu anafanya nini na kwa wakati gani, Dume huwa refu na zito kuliko jike. CHAKULA CHAKE Chakula kikuu cha Mamba ni nyama tuu, hutafuna samaki, wanyama wadogo wadogo nk, hapo ni wakati umri ukiwa bado Mdogo, lakini umri unapoongezeka mnyama mamba humuwinda moja kwa moja nyumbu, hawa huwakamata kiurahisi kwa sababu ya ujinga wao wanapovuka MAJI au kunywa maji, Twiga anapofata maji, Nyati pia anapoenda kunywa MAJI , wakati mwingine hujaribu hata kumuwinda tembo Mdogo, lakini anapotokea mama wa tembo zoezi hill huishia hapo. SIFA ZAKE ZA KIPEKEE 1. Jamaa ni fundi wa kuogelea vibaya mno, ana kasi kubwa sana ndani ya maji. 2. Anaweza kuishi majini na nchi kavu. 3. Mashambulizi yake ni ya kishitukiza. 4. Ana akili na mjanja sana anapomuona mnyama ambaye hana uwezo wa kucheza naye hujifanya amelala usingizi ili uingie katika maji. 5. Ndio mnyama pekee ambaye amewatafuna sana binadamu. 6. Anapoiona hatari hukimbilia katika maji haraka sana, na akifika huko anakukaribisha. 7. Hapatani na simba kabisa kwakuwa ndiye mnyama, ambaye hupenda kumbughuzi awapo mapumzikoni, hivyo wawili hawa wanapokutana ni kama watani. 8. Mamba anajua sana kuzira, hupenda kuachana na vitu vinavyomuumiza kichwa. 9. Wakati mwingine huigiza amekufa ili kuwakamata samaki wakubwa kwa urahisi, akiwa majini utaona anazunguka tuu kama anapelekwa na maji, samaki wakubwa hubaki kumshangaa. 10. Ngozi yake ni dili sana, ila ukikamatwa nayo popote duniani utashughulikiwa maana anarindwa na Sharia umoja wa mataifa. 11. Aonapo hatari hukimbilia majini na akifika tuu hugeuza kichwa chake alikotoka. 12. Mkia wake pia huutumumia kumsukumia kiumbe anayejaribu kumshangaa nchi kavu, na ukishaingia kwenye naye huja. 13.:huwa na nguvu zaidi akiwa kwenye maji, kuliko nchi kavu. 14. Ni mnyama anayeua haraka sana, tofauti na wanyama wengine walao nyama, hivyo kifo chake sio cha mateso sana kama kwa simba au chui, ila kwa mtizamaji atapata hofu Mara dufu kuliko akiona mauaji ya wanyama wengine. 15. Anaweza kunyata katika maji na kiumbe aliyepo pembeni asishituke kabisa, akiwa mwanadamu ndio kabisa atakosa habari. 16. Mamba jike hapendi mambo ya mahaba, Mara nyingi hutumia muda mwingi kulikimbia dume. 17. Madume kwa sababu ya ukubwa wao na uzito, wakati mwingine hutumia ubabe kulipanda jike lake. 18. Dume LA mamba lina msaada mdogo sana kwa jike, msaada huo hutoa pindi linapokuwa na muda wa ziada. 19. Kutafuta chakula huweza kushirikiana. 20. Ni mnyama pekee anayekula nyama na anaishi umri mrefu, tofauti na wanyama wengine ambao hula nyama umri wao wa kuishi ni mfupi, hii ni kwasababu moja tuu mfumo wake wa mmeng'enyo wa chakula upo vizuri anaweza kula hata mifupa pasina kuchagua steki tuu. 21. Wakati mwingine mamba humeza mawe lakini bado sijapata uhakika mawe hayo sababu ya kumeza ni IPI, baadhi ya watu hudai mawe hayo humsaidia katika mfumo wa umeng'enyaji wa chakula na wengine hudai humsaidia katika kuogelea. UKIKUTANA NAYE UFANYE NINI Ushauri wa pekee ni kukimbia tuu, kwani hakuna namna yoyote inayoweza kukufanya utoke salama, mnyama huyu ana nguvu kubwa ya mwili na ni kiumbe ambaye huwezi pambana naye hata ukiwa na silaha kwa sababu ya ngozi yake ngumu. Epuka kukaa sehemu ambazo kuna uwezekano wa uwepo wa kiumbe huyu ni hatari sana, sehemu hizo ni kama mito iliyopo vijijini au mbugani, kaa mbali kabisa na fukwe za mito hiyo, wala usidiriki kunawa au kutaka kunywa maji yake bila ruhusa ya anayewaongoza. Like na Follow t
    ·193 Views
  • Kuna wakati lazima tukubali kuwa sisi ni dhaifu sana hatuna tunachomiliki zaidi ya kinyesi kwenye matumbo yetu.

    Hii ni California sehemu ambayo wanakaa watu wenye ukwasi na wadhifa. Watu ambao wanajua kutumia hela zaidi kuliko kuongea kuhusu hela.

    Sehemu ambayo fukara harusiwi kuishi. Sehemu. ambayo watu wanaishi na bank chini ya majumba yao. Lakini licha ya heshima yote ya sehemu hio Mungu kapitisha makadara yake kumekuwa kama nyika inayoandaliwa kuwa makaazi.

    Mungu anae badilisha usiku kuwa mchana ndio Mungu huyo huyo alieifanya California kuwa jivu. Mungu hazihakiwi. Mungu akasirikiwi. Mungu hajaribiwi na uwezo wa Mungu ni mkubwa kushinda neno uwezo.

    Utajiri wa mtu au wadhifa wa mtu mbele ya Mungu huwa si kitu cha maana kama mtu huyo ataishi kinyume na matakwa ya Mungu. Hela haimfanyi mtu kuwa na amani bali amani inayotoka kwa Mungu ndie inayomfanya binadamu kuwa na amani. MUOGOPE SANA MUNGU.
    (CC: Abdulrazaki issa)
    Kuna wakati lazima tukubali kuwa sisi ni dhaifu sana hatuna tunachomiliki zaidi ya kinyesi kwenye matumbo yetu. Hii ni California sehemu ambayo wanakaa watu wenye ukwasi na wadhifa. Watu ambao wanajua kutumia hela zaidi kuliko kuongea kuhusu hela. Sehemu ambayo fukara harusiwi kuishi. Sehemu. ambayo watu wanaishi na bank chini ya majumba yao. Lakini licha ya heshima yote ya sehemu hio Mungu kapitisha makadara yake kumekuwa kama nyika inayoandaliwa kuwa makaazi. Mungu anae badilisha usiku kuwa mchana ndio Mungu huyo huyo alieifanya California kuwa jivu. Mungu hazihakiwi. Mungu akasirikiwi. Mungu hajaribiwi na uwezo wa Mungu ni mkubwa kushinda neno uwezo. Utajiri wa mtu au wadhifa wa mtu mbele ya Mungu huwa si kitu cha maana kama mtu huyo ataishi kinyume na matakwa ya Mungu. Hela haimfanyi mtu kuwa na amani bali amani inayotoka kwa Mungu ndie inayomfanya binadamu kuwa na amani. MUOGOPE SANA MUNGU. (CC: Abdulrazaki issa)
    ·43 Views
  • Kuna wakati lazima tukubali kuwa sisi ni dhaifu sana hatuna tunachomiliki zaidi ya kinyesi kwenye matumbo yetu.

    Hii ni California sehemu ambayo wanakaa watu wenye ukwasi na wadhifa. Watu ambao wanajua kutumia hela zaidi kuliko kuongea kuhusu hela.

    Sehemu ambayo fukara harusiwi kuishi. Sehemu. ambayo watu wanaishi na bank chini ya majumba yao. Lakini licha ya heshima yote ya sehemu hio Mungu kapitisha makadara yake kumekuwa kama nyika inayoandaliwa kuwa makaazi.

    Mungu anae badilisha usiku kuwa mchana ndio Mungu huyo huyo alieifanya California kuwa jivu. Mungu hazihakiwi. Mungu akasirikiwi. Mungu hajaribiwi na uwezo wa Mungu ni mkubwa kushinda neno uwezo.

    Utajiri wa mtu au wadhifa wa mtu mbele ya Mungu huwa si kitu cha maana kama mtu huyo ataishi kinyume na matakwa ya Mungu. Hela haimfanyi mtu kuwa na amani bali amani inayotoka kwa Mungu ndie inayomfanya binadamu kuwa na amani. MUOGOPE SANA MUNGU.
    (CC: Abdulrazaki issa)

    Kuna wakati lazima tukubali kuwa sisi ni dhaifu sana hatuna tunachomiliki zaidi ya kinyesi kwenye matumbo yetu. Hii ni California sehemu ambayo wanakaa watu wenye ukwasi na wadhifa. Watu ambao wanajua kutumia hela zaidi kuliko kuongea kuhusu hela. Sehemu ambayo fukara harusiwi kuishi. Sehemu. ambayo watu wanaishi na bank chini ya majumba yao. Lakini licha ya heshima yote ya sehemu hio Mungu kapitisha makadara yake kumekuwa kama nyika inayoandaliwa kuwa makaazi. Mungu anae badilisha usiku kuwa mchana ndio Mungu huyo huyo alieifanya California kuwa jivu. Mungu hazihakiwi. Mungu akasirikiwi. Mungu hajaribiwi na uwezo wa Mungu ni mkubwa kushinda neno uwezo. Utajiri wa mtu au wadhifa wa mtu mbele ya Mungu huwa si kitu cha maana kama mtu huyo ataishi kinyume na matakwa ya Mungu. Hela haimfanyi mtu kuwa na amani bali amani inayotoka kwa Mungu ndie inayomfanya binadamu kuwa na amani. MUOGOPE SANA MUNGU. (CC: Abdulrazaki issa)
    ·68 Views
  • HIVI UNAJUA: India nchi ya saba kwa ukubwa duniani kwa eneo na nchi ya pili kwa watu wengi , nyuma ya Uchina; hata hivyo, inakadiriwa kuwa India itaipiku China kuwa nchi yenye watu wengi zaidi duniani katika mwaka wa 2023. Mnamo mwaka wa 2021, India ina wakazi bilioni 1.39, na mji mkuu wake, New Delhi, unakadiriwa kuwa na karibu milioni 20. wenyeji. Licha ya ukweli kwamba idadi ya watu wa India imeongezeka kwa kasi, kiwango cha uzazi nchini kinapungua, na hivi karibuni kitashuka chini ya kiwango cha uingizwaji (watoto 2.1 kwa kila mwanamke).
    HIVI UNAJUA: India nchi ya saba kwa ukubwa duniani kwa eneo na nchi ya pili kwa watu wengi , nyuma ya Uchina; hata hivyo, inakadiriwa kuwa India itaipiku China kuwa nchi yenye watu wengi zaidi duniani katika mwaka wa 2023. Mnamo mwaka wa 2021, India ina wakazi bilioni 1.39, na mji mkuu wake, New Delhi, unakadiriwa kuwa na karibu milioni 20. wenyeji. Licha ya ukweli kwamba idadi ya watu wa India imeongezeka kwa kasi, kiwango cha uzazi nchini kinapungua, na hivi karibuni kitashuka chini ya kiwango cha uingizwaji (watoto 2.1 kwa kila mwanamke).
    Like
    1
    ·91 Views
  • KHALID AUCHO WABONGO WAMEKUITA DAKTARI!!!

    Aucho amecheza soka katika vilabu mbalimbali, kama vile Halmashauri ya Manispaa ya Jinja F.C. kutoka 2009 hadi 2010, Water F.C kutoka Uganda kutoka 2010 hadi 2012, Simba FC kutoka Uganda, Tusker kutoka Kenya, Gor Mahia kutoka Kenya, na Baroka kutoka Ligi Kuu ya Soka ya Afrika Kusini.

    Kipindi kile anasajiliwa jangwani, mwaka mmoja nyuma alikuwa anawindwa na klabu moja kubwa hapa nchini lakini dili lake halikukaa sawa na panapo muda kuwadia, akatua mizigo yake Jangwani!

    Mpaka hivi sasa ndiye kiungo wa kati wa Kigeni aliyedumu nchini kwa Ubora usiomithilika licha ya sasa kasi yake kuonekana inapungua na hii ni changamoto ya kucheza michezo msimu mzima bila kupata msaidizi halisi!..

    Kabla Hujaniuliza kwanini nimemsifia huyu AUCHO kutoka kwa Wananchi njoo apa uniambie kwani Aucho kijana wa watu Aliwahi kukukosea wapi ili Tujue kabla hatujakutafsiri kama mtu mwenye nongwa binafsi!

    Yess,, Utani upo lakini sio kila wakati!

    Unyamani namuona akija FABRICE NGOMA licha naye bado hajajisimika vizuri kwenye mwendelezo bora wa kila msimu...!!!

    SEMA "WABONGO" KILA MTU KWAO #DAKTARI
    Khalid Aucho8
    #UkweliUnaumaSana🫴
    #neliudcosiah

    KHALID AUCHO WABONGO WAMEKUITA DAKTARI!!! 🤏 Aucho amecheza soka katika vilabu mbalimbali, kama vile Halmashauri ya Manispaa ya Jinja F.C. kutoka 2009 hadi 2010, Water F.C kutoka Uganda kutoka 2010 hadi 2012, Simba FC kutoka Uganda, Tusker kutoka Kenya, Gor Mahia kutoka Kenya, na Baroka kutoka Ligi Kuu ya Soka ya Afrika Kusini. Kipindi kile anasajiliwa jangwani, mwaka mmoja nyuma alikuwa anawindwa na klabu moja kubwa hapa nchini lakini dili lake halikukaa sawa na panapo muda kuwadia, akatua mizigo yake Jangwani! Mpaka hivi sasa ndiye kiungo wa kati wa Kigeni aliyedumu nchini kwa Ubora usiomithilika licha ya sasa kasi yake kuonekana inapungua na hii ni changamoto ya kucheza michezo msimu mzima bila kupata msaidizi halisi!.. Kabla Hujaniuliza kwanini nimemsifia huyu AUCHO kutoka kwa Wananchi njoo apa uniambie kwani Aucho kijana wa watu Aliwahi kukukosea wapi ili Tujue kabla hatujakutafsiri kama mtu mwenye nongwa binafsi! Yess,, Utani upo lakini sio kila wakati! Unyamani namuona akija FABRICE NGOMA licha naye bado hajajisimika vizuri kwenye mwendelezo bora wa kila msimu...!!! SEMA "WABONGO" KILA MTU KWAO #DAKTARI 🤣✍️ Khalid Aucho8🇺🇬 #UkweliUnaumaSana🫴🤔 #neliudcosiah
    Like
    2
    ·268 Views
More Results