• (F)
    Baada ya uchunguzi wa haraka, polisi walifukua miili kadhaa ya wagonjwa wa Shipman na kugundua kitu cha kutisha—miili yao ilikuwa na kiwango kikubwa cha morphine.

    Shipman alikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji ya wagonjwa 15, lakini uchunguzi wa kina ulionesha kuwa huenda alikuwa amewaua zaidi ya watu 250 kwa kipindi cha miaka 23!

    Alifungwa jela mwaka 2000, na mwaka 2004, alipatikana amejinyonga kwenye seli yake.
    (F) Baada ya uchunguzi wa haraka, polisi walifukua miili kadhaa ya wagonjwa wa Shipman na kugundua kitu cha kutisha—miili yao ilikuwa na kiwango kikubwa cha morphine. Shipman alikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji ya wagonjwa 15, lakini uchunguzi wa kina ulionesha kuwa huenda alikuwa amewaua zaidi ya watu 250 kwa kipindi cha miaka 23! Alifungwa jela mwaka 2000, na mwaka 2004, alipatikana amejinyonga kwenye seli yake.
    Like
    Love
    2
    0 Comments 0 Shares 75 Views
  • (B)
    Dr. Harold Frederick Shipman alizaliwa mnamo 1946 huko Nottingham, Uingereza.

    Alikua katika familia yenye maisha ya kawaida, lakini kitu kimoja kilimtofautisha na watoto wengine—upendo wake kwa mama yake.

    Mama yake, Vera, alikuwa kila kitu kwake. Lakini alipofikisha miaka 17, alishuhudia kitu ambacho pengine kingemuumba kuwa mtu wa kutisha zaidi katika historia ya madaktari.

    Mama yake aligunduliwa kuwa na saratani ya mapafu.

    Katika miezi ya mwisho ya ugonjwa wake, alikuwa akipewa dawa za kupunguza maumivu—morphine—na Harold kijana aliona jinsi dawa hizo zilivyomfanya mama yake awe mtulivu kabla ya kufariki.

    Ilikuwa ni tukio lililobadilisha maisha yake.

    Lakini hakuna aliyefikiria kwamba tukio hili lingekuwa chanzo cha wimbi la vifo visivyoelezeka.
    (B) Dr. Harold Frederick Shipman alizaliwa mnamo 1946 huko Nottingham, Uingereza. Alikua katika familia yenye maisha ya kawaida, lakini kitu kimoja kilimtofautisha na watoto wengine—upendo wake kwa mama yake. Mama yake, Vera, alikuwa kila kitu kwake. Lakini alipofikisha miaka 17, alishuhudia kitu ambacho pengine kingemuumba kuwa mtu wa kutisha zaidi katika historia ya madaktari. Mama yake aligunduliwa kuwa na saratani ya mapafu. Katika miezi ya mwisho ya ugonjwa wake, alikuwa akipewa dawa za kupunguza maumivu—morphine—na Harold kijana aliona jinsi dawa hizo zilivyomfanya mama yake awe mtulivu kabla ya kufariki. Ilikuwa ni tukio lililobadilisha maisha yake. Lakini hakuna aliyefikiria kwamba tukio hili lingekuwa chanzo cha wimbi la vifo visivyoelezeka.
    Like
    2
    0 Comments 0 Shares 106 Views
  • 10. DAMASCUS

    Sauli wa Tarso (ambaye baadaye alikuja kuwa Paulo) ndiye mtu anayekuja akilini kwa mara ya kwanza mtu anapofikiria Damasko.

    Ilikuwa ni njiani pale alipokutana na Kristo.

    Ajabu alikuwa njiani kuwatesa Wakristo kutoka Kanisa la kwanza.

    Katika Matendo sura ya 9 inasema, “Ikawa alipokuwa akienda zake, akikaribia Dameski, ghafula nuru kutoka mbinguni ilimwangazia pande zote.” Alianguka chini na kupoteza uwezo wake wa kuona. Sauli aliongoka baadaye na kuwa mmoja wa watetezi wa Kristo wenye shauku zaidi.
    10. DAMASCUS Sauli wa Tarso (ambaye baadaye alikuja kuwa Paulo) ndiye mtu anayekuja akilini kwa mara ya kwanza mtu anapofikiria Damasko. Ilikuwa ni njiani pale alipokutana na Kristo. Ajabu alikuwa njiani kuwatesa Wakristo kutoka Kanisa la kwanza. Katika Matendo sura ya 9 inasema, “Ikawa alipokuwa akienda zake, akikaribia Dameski, ghafula nuru kutoka mbinguni ilimwangazia pande zote.” Alianguka chini na kupoteza uwezo wake wa kuona. Sauli aliongoka baadaye na kuwa mmoja wa watetezi wa Kristo wenye shauku zaidi.
    Like
    Love
    2
    0 Comments 0 Shares 96 Views
  • Katika hatua mpya ya mzozo unaoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , kundi la Waasi wa M23 likishirikiana na Muungano wa Mto Congo (AFC) limetangaza kuwa Wanajeshi wa zamani wa Jeshi la DR Congo (FARDC) waliokamatwa au kujisalimisha wamehitimu mafunzo ya kiitikadi na mbinu za kijeshi.

    Katika taarifa ya Kundi la M23 kwenye mtandao wao wa X leo Februari 18, picha zilionyesha Wanajeshi hao wakiwa na sare na silaha rasmi za wanamgambo hao. Ujumbe uliambatana na chapisho hilo ulieleza:

    "Wanajeshi wa zamani wa FARDC, waliokamatwa au kujisalimisha, wamemaliza mafunzo ya kiitikadi na mbinu huko Rumangabo Mjini Goma chini ya AFC/M23. Sasa wakiwa na vifaa kamili na wanaolipwa, wametumwa Lubero, ambako wanashiriki kikamilifu muungano wa serikali."

    Wakati huo huo, Uganda imetangaza kuwa vikosi vyake vya kijeshi vimeanza kuelekea Bunia, DRC, ikiwa ni siku chache baada ya Jeshi la Uganda kutoa muda wa saa 24 kwa Askari waliopo eneo hilo kujisalimisha.

    Taarifa nyingine kuwa, hapo jana Kundi la Waasi hao wa M23 wamefanikiwa kuteka eneo la Kamanyola na sasa hivi wanajipanga kuelekea Uvira, Fizi kisha Mkoa wa Tanganyika (Kalemie) kabla ya kwenda Mjini Lubumbashi. Kwa mujibu wa Wananchi wa Kamanyala wanasema kuwa Kundi la Wapiganaji wa Wazalendo ambao wanapigana kwa upande wa Serikali waliibwa Silaha zao kisha wakakimbia na kuwaachia M23 kuichukua Kamanyola.

    Katika hatua mpya ya mzozo unaoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 馃嚚馃嚛, kundi la Waasi wa M23 likishirikiana na Muungano wa Mto Congo (AFC) limetangaza kuwa Wanajeshi wa zamani wa Jeshi la DR Congo (FARDC) waliokamatwa au kujisalimisha wamehitimu mafunzo ya kiitikadi na mbinu za kijeshi. Katika taarifa ya Kundi la M23 kwenye mtandao wao wa X leo Februari 18, picha zilionyesha Wanajeshi hao wakiwa na sare na silaha rasmi za wanamgambo hao. Ujumbe uliambatana na chapisho hilo ulieleza: "Wanajeshi wa zamani wa FARDC, waliokamatwa au kujisalimisha, wamemaliza mafunzo ya kiitikadi na mbinu huko Rumangabo Mjini Goma chini ya AFC/M23. Sasa wakiwa na vifaa kamili na wanaolipwa, wametumwa Lubero, ambako wanashiriki kikamilifu muungano wa serikali." Wakati huo huo, Uganda imetangaza kuwa vikosi vyake vya kijeshi vimeanza kuelekea Bunia, DRC, ikiwa ni siku chache baada ya Jeshi la Uganda kutoa muda wa saa 24 kwa Askari waliopo eneo hilo kujisalimisha. Taarifa nyingine kuwa, hapo jana Kundi la Waasi hao wa M23 wamefanikiwa kuteka eneo la Kamanyola na sasa hivi wanajipanga kuelekea Uvira, Fizi kisha Mkoa wa Tanganyika (Kalemie) kabla ya kwenda Mjini Lubumbashi. Kwa mujibu wa Wananchi wa Kamanyala wanasema kuwa Kundi la Wapiganaji wa Wazalendo ambao wanapigana kwa upande wa Serikali waliibwa Silaha zao kisha wakakimbia na kuwaachia M23 kuichukua Kamanyola.
    0 Comments 0 Shares 163 Views
  • Privaldinho

    CEO wa Getafe si anachambua. Sasa na mimi nianze kuchambua.

    Nimetazama vikosi vya Singida mechi 4 za nyuma

    Makipa
    Vs Kagera - Metacha
    Vs JKT - Amas
    Vs KMC - Masalanga
    Vs Yanga - Masalanga
    Ndani ya mechi nne makipa watatu

    Beki ya kushoto Imoro amecheza mechi 2 kati ya 5, vs Makolo, Mechi za Kagera na KMC akacheza Malonga. Vs JKT akacheza Imoro, vs Yanga akacheza Gadiel. Mechi 5 mabeki wa kushoto 3.

    Mechi ya JKT mabeki wa kati alikuwa Assink na Kennedy (Tra bi ta hakuwepo), jana ameanzia benchi. Mechi ya KMC alianza Tra bita na Kennedy. Tra bi ta alitolewa dkk 46 akaingia Assink beki mpya ambaye ameanza jana.

    Mechi ya Kagera Kennedy hakucheza wakaanza Tra bita na Manyama, vs makolo Kennedy na tra bi na vs Ken Gold, Kennedy na Manyama. Maana yake, kuna Manyama, Tra, Kennedy na ongezeko la beki mpya Assink kutoka Ghana aliyecheza jana. Kiufupi hakuna mwenye uhakika wa namba eneo hilo.

    Viungo wa kati
    Vs Yanga (Damaro, Nashon, Gego) Chukwu akabadilishiwa majukumu)
    Vs JKT (Chukwu, Nashon, Arthur)
    Vs KMC (Damaro, Athur, Tchakei)
    Vs Kagera (Damaro, Chukwu, Athur)
    vs Kolo (Damaro, Gego, Keyekeh)
    Vs Ken Gold (Damaro, Gego, Keyekeh)

    Yanga vs Singida wameanza na viungo wakabaji kiasilia 3. Damaro aliyecheza mechi 5/6, Gego aliyeanza mechi 3/3 na kutokea sub mechi 2.

    NB: Eneo la ushambuliaji, Tchakae hajacheza vs JKT na Yanga. Jana wamelalamika hajacheza ila hawajajiuliza kwanini hakucheza vs JKt

    Vs Yanga - Pokou Rupia Adebayor (Sowah Sub)
    Vs JKT - Lyanga, Sowah, Pokou (Rupia top scorer out)
    Vs KMC - Sowah, Rupia, Pokou (timu ikakosa balance, nyuma yao yupo Tchake (luxury player) wakapoteza mechi.) Hii ni kwa wale mnafirikia Sowah na Rupia kuanza pamoja away. KMC waliongoza umiliki wa mchezo. Kidogo kipindi cha pili Singida walibadilika baada ya sub ya Rupia, Pokou na Tchakei, akaingia Gego na Tchukwu

    Vs Kagera -Sowah, Rupia, Tchakei (matokeo 2-2, kwa mara nyingine wanakuwa vulnerable kudefend. Mbaya zaidi wakiwa nyumbani.

    Vs Kolo - Tchakei, Rupia Athur
    Vs Ken Gold - Tchakei, Rupia, Adebayor
    Vs Prisons - Lyanga, Rupia Tchakei

    Ni wachache sana wenye uhakika wa namba. Agenda ya kikosi kubadilika sio habari mpya kwao labda kama wewe ni mgeni wa JIJI

    Privaldinho 鉁嶏笍 CEO wa Getafe si anachambua. Sasa na mimi nianze kuchambua. Nimetazama vikosi vya Singida mechi 4 za nyuma Makipa Vs Kagera - Metacha Vs JKT - Amas Vs KMC - Masalanga Vs Yanga - Masalanga Ndani ya mechi nne makipa watatu Beki ya kushoto Imoro amecheza mechi 2 kati ya 5, vs Makolo, Mechi za Kagera na KMC akacheza Malonga. Vs JKT akacheza Imoro, vs Yanga akacheza Gadiel. Mechi 5 mabeki wa kushoto 3. Mechi ya JKT mabeki wa kati alikuwa Assink na Kennedy (Tra bi ta hakuwepo), jana ameanzia benchi. Mechi ya KMC alianza Tra bita na Kennedy. Tra bi ta alitolewa dkk 46 akaingia Assink beki mpya ambaye ameanza jana. Mechi ya Kagera Kennedy hakucheza wakaanza Tra bita na Manyama, vs makolo Kennedy na tra bi na vs Ken Gold, Kennedy na Manyama. Maana yake, kuna Manyama, Tra, Kennedy na ongezeko la beki mpya Assink kutoka Ghana aliyecheza jana. Kiufupi hakuna mwenye uhakika wa namba eneo hilo. Viungo wa kati Vs Yanga (Damaro, Nashon, Gego) Chukwu akabadilishiwa majukumu) Vs JKT (Chukwu, Nashon, Arthur) Vs KMC (Damaro, Athur, Tchakei) Vs Kagera (Damaro, Chukwu, Athur) vs Kolo (Damaro, Gego, Keyekeh) Vs Ken Gold (Damaro, Gego, Keyekeh) Yanga vs Singida wameanza na viungo wakabaji kiasilia 3. Damaro aliyecheza mechi 5/6, Gego aliyeanza mechi 3/3 na kutokea sub mechi 2. NB: Eneo la ushambuliaji, Tchakae hajacheza vs JKT na Yanga. Jana wamelalamika hajacheza ila hawajajiuliza kwanini hakucheza vs JKt Vs Yanga - Pokou Rupia Adebayor (Sowah Sub) Vs JKT - Lyanga, Sowah, Pokou (Rupia top scorer out) Vs KMC - Sowah, Rupia, Pokou (timu ikakosa balance, nyuma yao yupo Tchake (luxury player) wakapoteza mechi.) Hii ni kwa wale mnafirikia Sowah na Rupia kuanza pamoja away. KMC waliongoza umiliki wa mchezo. Kidogo kipindi cha pili Singida walibadilika baada ya sub ya Rupia, Pokou na Tchakei, akaingia Gego na Tchukwu Vs Kagera -Sowah, Rupia, Tchakei (matokeo 2-2, kwa mara nyingine wanakuwa vulnerable kudefend. Mbaya zaidi wakiwa nyumbani. Vs Kolo - Tchakei, Rupia Athur Vs Ken Gold - Tchakei, Rupia, Adebayor Vs Prisons - Lyanga, Rupia Tchakei Ni wachache sana wenye uhakika wa namba. Agenda ya kikosi kubadilika sio habari mpya kwao labda kama wewe ni mgeni wa JIJI
    0 Comments 0 Shares 152 Views
  • Zakazakazi azidi kumshushia nondo Amri Kiemba.

    MUONGO!

    Amri Kiemba alicheza Simba kwa misimu mitano na nusu, kuanzia 2009/10 hadi Disemba 2014.

    Katika kipindi hicho, Azam FC na Simba zilikutana mara 10, Simba ikishinda mara tano na Azam FC mara tatu, na mara mbili sare...angalia picha ya pili.

    Katika hizo mara tano ambazo Simba ilishinda, mbili ni za msimu wa 2009/10.

    24/10/2009
    Simba 1-0 Azam FC

    14/3/2010
    Azam FC 0-2 Simba

    Huu ulikuwa msimu ambao Simba ilikuwa kwenye ubora mkubwa sana na ikamaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja.

    Walishinda mechi zote za mzunguko wa kwanza, wakaja kupata sare mbili tu mzunguko wa pili, dhidi ya Kagera Sugar na African Lyon.

    Kwa ubora huo, huwezi kuilamu Azam FC ilhali timu zote zilifungwa...kiungwana unawasifia Simba kwamba walikuwa kwenye ubora wa hali ya juu.

    Lakini baada ya msimu huo, Azam FC na Simba zililingana matokeo hadi Kiemba alipoondoka Simba kwenda Azam FC.

    Swali ni je, Kiemba anapata wapi uhalali wa kutilia shaka maandalizi yaliyoleta matokeo kama haya?

    Msimu wa 2013/14, Azam FC ikawa kwenye ubora mkubwa na kumaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja, ikiwemo kushinda nje ndani dhidi ya Simba ya Kiemba na maandalizi yao ya hali ya juu.

    28/10/2013
    Simba 1-2 Azam FC

    30/3/2014
    Azam FC 2-1 Simba

    Baada ya mechi hizi Kiemba akaenda Azam FC...na mechi yake ya kwanza ikaisha kwa sare ya 1-1.

    Ni vipi Kiemba hakuridhika na maandalizi ya Azam FC yaliyoleta sare lakini aliridhika na maandalizi ya Simba yaliyowafanya wafungwe nje ndani msimu mmoja tu nyuma yake?

    Msimu mmoja kabla Kiemba hajasajiliwa Simba, Azam FC ilishinda 2-0 na mashabiki wa Simba wakaenda kushusha kinyesi nyumbani kwa mwenyekiti wao Hassan Dalali.

    Ina maana maandalizi ya Azam FC yangekuwa hafifu yangewatoa kinyesi Simba kweli?

    Azam FC ilikuwa inaifunga Simba kabla yeye hajaenda, na ikaifunga akiwemo...kwa maandalizi yale yale...halafu anakuja hadharani leo, miaka zaidi ya 10 na kusema aliona maandalizi hafifu...sasa walikuwa wanashindaje kwa maandalizi hafifu?

    Ni mbaya sana kumuita mtu muongo...lakini Kiemba kwenye hili itoshe tu kusema kwamba WEWE NI MUONGO!

    Zakazakazi azidi kumshushia nondo Amri Kiemba. MUONGO! Amri Kiemba alicheza Simba kwa misimu mitano na nusu, kuanzia 2009/10 hadi Disemba 2014. Katika kipindi hicho, Azam FC na Simba zilikutana mara 10, Simba ikishinda mara tano na Azam FC mara tatu, na mara mbili sare...angalia picha ya pili. Katika hizo mara tano ambazo Simba ilishinda, mbili ni za msimu wa 2009/10. 24/10/2009 Simba 1-0 Azam FC 14/3/2010 Azam FC 0-2 Simba Huu ulikuwa msimu ambao Simba ilikuwa kwenye ubora mkubwa sana na ikamaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja. Walishinda mechi zote za mzunguko wa kwanza, wakaja kupata sare mbili tu mzunguko wa pili, dhidi ya Kagera Sugar na African Lyon. Kwa ubora huo, huwezi kuilamu Azam FC ilhali timu zote zilifungwa...kiungwana unawasifia Simba kwamba walikuwa kwenye ubora wa hali ya juu. Lakini baada ya msimu huo, Azam FC na Simba zililingana matokeo hadi Kiemba alipoondoka Simba kwenda Azam FC. Swali ni je, Kiemba anapata wapi uhalali wa kutilia shaka maandalizi yaliyoleta matokeo kama haya? Msimu wa 2013/14, Azam FC ikawa kwenye ubora mkubwa na kumaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja, ikiwemo kushinda nje ndani dhidi ya Simba ya Kiemba na maandalizi yao ya hali ya juu. 28/10/2013 Simba 1-2 Azam FC 30/3/2014 Azam FC 2-1 Simba Baada ya mechi hizi Kiemba akaenda Azam FC...na mechi yake ya kwanza ikaisha kwa sare ya 1-1. Ni vipi Kiemba hakuridhika na maandalizi ya Azam FC yaliyoleta sare lakini aliridhika na maandalizi ya Simba yaliyowafanya wafungwe nje ndani msimu mmoja tu nyuma yake? Msimu mmoja kabla Kiemba hajasajiliwa Simba, Azam FC ilishinda 2-0 na mashabiki wa Simba wakaenda kushusha kinyesi nyumbani kwa mwenyekiti wao Hassan Dalali. Ina maana maandalizi ya Azam FC yangekuwa hafifu yangewatoa kinyesi Simba kweli? Azam FC ilikuwa inaifunga Simba kabla yeye hajaenda, na ikaifunga akiwemo...kwa maandalizi yale yale...halafu anakuja hadharani leo, miaka zaidi ya 10 na kusema aliona maandalizi hafifu...sasa walikuwa wanashindaje kwa maandalizi hafifu? Ni mbaya sana kumuita mtu muongo...lakini Kiemba kwenye hili itoshe tu kusema kwamba WEWE NI MUONGO!
    0 Comments 0 Shares 136 Views
  • Mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu kutoka Nchini Liberia , George Weah, amekana kufanya mazungumzo yoyote na Mmiliki wa mtandao wa X Elon Musk kuhusiana na kununua tuzo yake ya Ballon D’or aliyoshinda mwaka 1995 kwa thamani ya Dola bilioni moja (1).

    Mchezaji huyo amesema kuwa Musk hakuwahi kutaka kununua tuzo hiyo kutoka kwake, kama ilivyoripotiwa mitandaoni hivi karibuni. Pamoja na hayo, Weah ameongeza kuwa Tuzo hiyo haiuzwi hata Watoto wake alishawaambia kuwa Tuzo hiyo ni mali ya Afrika, hata ikitokea wakapatwa na shida, haitakiwi kuuzwa kwa sababu ndio Tuzo pekee bara la Afrika inajivunia.

    Mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu kutoka Nchini Liberia 馃嚤馃嚪, George Weah, amekana kufanya mazungumzo yoyote na Mmiliki wa mtandao wa X Elon Musk kuhusiana na kununua tuzo yake ya Ballon D’or aliyoshinda mwaka 1995 kwa thamani ya Dola bilioni moja (1). Mchezaji huyo amesema kuwa Musk hakuwahi kutaka kununua tuzo hiyo kutoka kwake, kama ilivyoripotiwa mitandaoni hivi karibuni. Pamoja na hayo, Weah ameongeza kuwa Tuzo hiyo haiuzwi hata Watoto wake alishawaambia kuwa Tuzo hiyo ni mali ya Afrika, hata ikitokea wakapatwa na shida, haitakiwi kuuzwa kwa sababu ndio Tuzo pekee bara la Afrika inajivunia.
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 154 Views
  • Rais wa Senegal , Bassirou Diomaye Faye ametangaza mpango wa kubadilisha majina ya mitaa yenye majina ya enzi za ukoloni na kuyapa majina ya mashujaa wa kitaifa na matukio muhimu ya kihistoria ya Nchi ya Senegal. Mpango huo ulioanzishwa wakati wa mkutano wa hivi karibuni wa Baraza la Mawaziri ni sehemu ya juhudi za kurejesha utambulisho wa kitamaduni wa Nchi hiyo.

    Mpango huyo utahusu pia kubadilisha majina na kuandika upya historia ya Nchi ya Senegal katika kwa umma, alisema Rais huyo ambapo pia aliongeza kwa kusema “Lazima tuelimishe Vijana wetu kuhusu Watu na matukio yaliyounda na kuijenga Senegal"

    Rais wa Senegal 馃嚫馃嚦, Bassirou Diomaye Faye ametangaza mpango wa kubadilisha majina ya mitaa yenye majina ya enzi za ukoloni na kuyapa majina ya mashujaa wa kitaifa na matukio muhimu ya kihistoria ya Nchi ya Senegal. Mpango huo ulioanzishwa wakati wa mkutano wa hivi karibuni wa Baraza la Mawaziri ni sehemu ya juhudi za kurejesha utambulisho wa kitamaduni wa Nchi hiyo. Mpango huyo utahusu pia kubadilisha majina na kuandika upya historia ya Nchi ya Senegal katika kwa umma, alisema Rais huyo ambapo pia aliongeza kwa kusema “Lazima tuelimishe Vijana wetu kuhusu Watu na matukio yaliyounda na kuijenga Senegal"
    0 Comments 0 Shares 126 Views
  • Jay Z si mwanamuziki wa kawaida. Alianza maisha kwa shida mitaani, lakini leo ni bilionea, mjasiriamali na mmiliki wa makampuni makubwa duniani.

    Amemuoa Beyoncé, mmoja wa wasanii wenye nguvu na ushawishi mkubwa zaidi duniani.

    Anamiliki Tidal, kampuni ya muziki, ana mkataba na kampuni kubwa za mavazi, anamiliki klabu ya michezo, na ana mikataba ya uwekezaji kwenye teknolojia na mali zisizohamishika.

    Kwa mtu wa hadhi yake, Rockstar ni ishara ya mafanikio yake.

    Kwa Jay Z, hii ni ishara ya kuwa juu ya mfumo wa kawaida wa maisha.
    Ni alama ya kuwa kwenye mzunguko wa watu wenye nguvu duniani.

    Kwa kawaida, saa ni kifaa cha kuonesha muda, lakini kwa Jay Z, hii ni hadithi ya maisha. Ni hadithi ya kupanda kutoka chini kabisa hadi kileleni.

    Ni hadithi ya nguvu za akili na juhudi za kipekee. Lakini pia ni hadithi ya siri na mafumbo ya ulimwengu wa nguvu na ushawishi.

    Kwa wengi, ni saa tu.
    Lakini kwa wachache wenye macho ya ndani, ni ishara ya siri kubwa zaidi duniani.

    Hakuna anayejua kwa hakika, lakini kinachojulikana ni kwamba saa hii imeacha maswali mengi zaidi kuliko majibu.
    Jay Z si mwanamuziki wa kawaida. Alianza maisha kwa shida mitaani, lakini leo ni bilionea, mjasiriamali na mmiliki wa makampuni makubwa duniani. Amemuoa Beyoncé, mmoja wa wasanii wenye nguvu na ushawishi mkubwa zaidi duniani. Anamiliki Tidal, kampuni ya muziki, ana mkataba na kampuni kubwa za mavazi, anamiliki klabu ya michezo, na ana mikataba ya uwekezaji kwenye teknolojia na mali zisizohamishika. Kwa mtu wa hadhi yake, Rockstar ni ishara ya mafanikio yake. Kwa Jay Z, hii ni ishara ya kuwa juu ya mfumo wa kawaida wa maisha. Ni alama ya kuwa kwenye mzunguko wa watu wenye nguvu duniani. Kwa kawaida, saa ni kifaa cha kuonesha muda, lakini kwa Jay Z, hii ni hadithi ya maisha. Ni hadithi ya kupanda kutoka chini kabisa hadi kileleni. Ni hadithi ya nguvu za akili na juhudi za kipekee. Lakini pia ni hadithi ya siri na mafumbo ya ulimwengu wa nguvu na ushawishi. Kwa wengi, ni saa tu. Lakini kwa wachache wenye macho ya ndani, ni ishara ya siri kubwa zaidi duniani. Hakuna anayejua kwa hakika, lakini kinachojulikana ni kwamba saa hii imeacha maswali mengi zaidi kuliko majibu.
    0 Comments 0 Shares 201 Views
  • Kwa wapenzi wa saa, jina hili lina maana kubwa zaidi ya pesa. Richard Mille anajulikana kwa kutengeneza saa zenye muundo wa kipekee, teknolojia ya hali ya juu, na bei zinazoacha wengi wakishangaa.

    Richard Mille Rockstar, ndivyo saa hii inavyoitwa. Na jina hilo si la bahati mbaya.

    Ni saa iliyotengenezwa kwa ajili ya watu wenye hadhi ya kipekee, watu walio juu ya mfumo wa kawaida wa maisha, watu ambao majina yao ni alama ya mafanikio.

    Ili kuelewa thamani ya saa hii, inabidi uelewe falsafa ya Richard Mille mwenyewe.

    Anasema anapotengeneza saa, hatoi tu kifaa cha kuonesha muda, anatengeneza sanaa inayozungumza na nafsi ya aliyenayo.

    Ndiyo maana saa zake ni za kipekee, na zinavaliwa na watu wa kipekee kama Jay Z.

    Rockstar ni saa ya nadra sana. Duniani zipo mbili tu. Moja ipo kwa Jay Z, na nyingine iko kwa bilionea mmoja wa Asia ambaye jina lake linahifadhiwa kwa usiri mkubwa.

    Hili ndilo linawafanya watu wengi waamini kwamba Jay Z si mtu wa kawaida. Wengi wanasema, “Hii ni ishara ya hadhi ya juu, ishara ya kuwa kwenye mzunguko wa watu wenye nguvu duniani.”

    Shilingi bilioni 8.5. Hii si bei ya nyumba, wala si bei ya jumba la kifahari. Ni bei ya saa moja tu.
    Kwa wapenzi wa saa, jina hili lina maana kubwa zaidi ya pesa. Richard Mille anajulikana kwa kutengeneza saa zenye muundo wa kipekee, teknolojia ya hali ya juu, na bei zinazoacha wengi wakishangaa. Richard Mille Rockstar, ndivyo saa hii inavyoitwa. Na jina hilo si la bahati mbaya. Ni saa iliyotengenezwa kwa ajili ya watu wenye hadhi ya kipekee, watu walio juu ya mfumo wa kawaida wa maisha, watu ambao majina yao ni alama ya mafanikio. Ili kuelewa thamani ya saa hii, inabidi uelewe falsafa ya Richard Mille mwenyewe. Anasema anapotengeneza saa, hatoi tu kifaa cha kuonesha muda, anatengeneza sanaa inayozungumza na nafsi ya aliyenayo. Ndiyo maana saa zake ni za kipekee, na zinavaliwa na watu wa kipekee kama Jay Z. Rockstar ni saa ya nadra sana. Duniani zipo mbili tu. Moja ipo kwa Jay Z, na nyingine iko kwa bilionea mmoja wa Asia ambaye jina lake linahifadhiwa kwa usiri mkubwa. Hili ndilo linawafanya watu wengi waamini kwamba Jay Z si mtu wa kawaida. Wengi wanasema, “Hii ni ishara ya hadhi ya juu, ishara ya kuwa kwenye mzunguko wa watu wenye nguvu duniani.” Shilingi bilioni 8.5. Hii si bei ya nyumba, wala si bei ya jumba la kifahari. Ni bei ya saa moja tu.
    0 Comments 0 Shares 175 Views
  • Kulikuwa na kelele nyingi, kelele zilizotikisa uwanja mzima wakati wa fainali ya Super Bowl.

    Hii si tukio la kawaida ni tukio linalotazamwa na mamilioni ya watu duniani kote.

    Kila kitu kilikuwa kwenye kiwango cha juu muziki, burudani, mashabiki, na hata mavazi ya mastaa waliohudhuria.

    Lakini katikati ya yote hayo, Jay Z alivuta macho ya wengi kwa kitu kimoja tu saa aliyovaa mkononi.

    Hii haikuwa saa ya kawaida. Ilikuwa ni saa ya kipekee, saa iliyobeba stori ya siri, utajiri, na hadhi isiyoelezeka. Saa hii ilikuwa na thamani ya shilingi bilioni 8.5, na duniani kote zipo saa mbili tu za aina hii.

    Watazamaji wengi waliangalia kwa macho ya kawaida, lakini watazamaji wenye jicho la uchambuzi waliona kitu cha ajabu zaidi.

    Waliona alama ya vidole vya mikono vilivyowekwa kwa umakini, alama inayofanana na ishara za Freemason.

    Kundi linaloaminika kuwa na ushawishi mkubwa duniani katika mambo ya siri na nguvu za kiuchumi na kisiasa.

    Saa hii haikutengenezwa na kampuni ya kawaida. Ilitoka kwa mtengenezaji maarufu wa saa za kifahari duniani, Richard Mille.
    Kulikuwa na kelele nyingi, kelele zilizotikisa uwanja mzima wakati wa fainali ya Super Bowl. Hii si tukio la kawaida ni tukio linalotazamwa na mamilioni ya watu duniani kote. Kila kitu kilikuwa kwenye kiwango cha juu muziki, burudani, mashabiki, na hata mavazi ya mastaa waliohudhuria. Lakini katikati ya yote hayo, Jay Z alivuta macho ya wengi kwa kitu kimoja tu saa aliyovaa mkononi. Hii haikuwa saa ya kawaida. Ilikuwa ni saa ya kipekee, saa iliyobeba stori ya siri, utajiri, na hadhi isiyoelezeka. Saa hii ilikuwa na thamani ya shilingi bilioni 8.5, na duniani kote zipo saa mbili tu za aina hii. Watazamaji wengi waliangalia kwa macho ya kawaida, lakini watazamaji wenye jicho la uchambuzi waliona kitu cha ajabu zaidi. Waliona alama ya vidole vya mikono vilivyowekwa kwa umakini, alama inayofanana na ishara za Freemason. Kundi linaloaminika kuwa na ushawishi mkubwa duniani katika mambo ya siri na nguvu za kiuchumi na kisiasa. Saa hii haikutengenezwa na kampuni ya kawaida. Ilitoka kwa mtengenezaji maarufu wa saa za kifahari duniani, Richard Mille.
    0 Comments 0 Shares 130 Views
  • Mtengeneza maudhui (Content Creator) kwenye mtandao wa Tiktok, Fanuel John Masamaki maarufu Zerobrainer0, ameshinda kipengele cha mtengeneza maudhui bora wa michezo kwa mwaka 2024 barani Afrika, katika tuzo zilizofanyika Februari 8, 2025 Nchini Afrika Kusini.

    Zerobrainer0 ana Wafuasi zaidi ya milioni (12) kwenye mtandao wake wa TikTok huku TikToker huyo akjizoelea umaarufu kwa maudhui yake ya kuchekekesha kwenye mchezo wa mpira wa miguu. Pia anatajwa kama ‘TikToker’ wa kuangaliwa zaidi kwa mwaka 2025.

    Mtengeneza maudhui (Content Creator) kwenye mtandao wa Tiktok, Fanuel John Masamaki maarufu Zerobrainer0, ameshinda kipengele cha mtengeneza maudhui bora wa michezo kwa mwaka 2024 barani Afrika, katika tuzo zilizofanyika Februari 8, 2025 Nchini Afrika Kusini. Zerobrainer0 ana Wafuasi zaidi ya milioni (12) kwenye mtandao wake wa TikTok huku TikToker huyo akjizoelea umaarufu kwa maudhui yake ya kuchekekesha kwenye mchezo wa mpira wa miguu. Pia anatajwa kama ‘TikToker’ wa kuangaliwa zaidi kwa mwaka 2025.
    0 Comments 0 Shares 97 Views
  • Mfalme wa Nchi ya Jordan , Abdullah II amekataa pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump la kutaka kuwahamishia Wapalestina Nchini mwake baada ya mazungumzo na Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye alishauri Wakazi wa Gaza wapatao milioni mbili (2) kuondolewa kutoka katika eneo lililoharibiwa na vita.

    Katika mkutano na Rais Trump, Mfalme Abdullah alijitolea kuchukua hadi Watoto 2,000 kutoka Gaza, hasa wale wanaohitaji matibabu ya dharura, ikiwemo Watoto wa saratani. Kupitia mtandao wa X, Mfalme Abdullah alisema, "Msimamo wa Jordan ni msimamo wa pamoja wa mataifa ya Kiarabu."

    Sanjari na hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit, alikosoa pendekezo hilo, akisema kuwa ni lisilokubalika katika ukanda huo, huku Nchi ya China ikisisitiza kuwa Gaza ni ardhi ya Wapalestina.

    Mfalme wa Nchi ya Jordan 馃嚡馃嚧, Abdullah II amekataa pendekezo la Rais wa Marekani 馃嚭馃嚫 Donald Trump la kutaka kuwahamishia Wapalestina Nchini mwake baada ya mazungumzo na Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye alishauri Wakazi wa Gaza wapatao milioni mbili (2) kuondolewa kutoka katika eneo lililoharibiwa na vita. Katika mkutano na Rais Trump, Mfalme Abdullah alijitolea kuchukua hadi Watoto 2,000 kutoka Gaza, hasa wale wanaohitaji matibabu ya dharura, ikiwemo Watoto wa saratani. Kupitia mtandao wa X, Mfalme Abdullah alisema, "Msimamo wa Jordan ni msimamo wa pamoja wa mataifa ya Kiarabu." Sanjari na hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit, alikosoa pendekezo hilo, akisema kuwa ni lisilokubalika katika ukanda huo, huku Nchi ya China 馃嚚馃嚦 ikisisitiza kuwa Gaza ni ardhi ya Wapalestina.
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 135 Views
  • Hatua ya Rais wa Marekani , Donald Trump ya kusitisha misaada yote kwenye baadhi ya Nchi za Afrika ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliyokuwa ikitolewa na Marekani imeongeza hali ya wasiwasi Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako mamilioni ya Wakimbizi walikuwa wakitegemea misaada hiyo.

    Afisa kutoka Umoja wa Mataifa, Bruno Lemarquis, amenukuliwa akisema kuwa Nchi ya DR Congo ilikuwa ikipokea asilimia sabini (70) ya misaada ya kibinadamu kutoka Nchini Marekani. Uamuzi wa Trump umesababisha upungufu mkubwa wa mahitaji muhimu kwa Wakimbizi. Afisa huyo ameongeza kuwa kwa mwaka 2024 pekee, DR Congo ilipokea dola milioni 910 kutoka Nchini Marekani pamoja na misaada mingine kwa Waathirika wa mapigano kati ya Majeshi ya Serikali na Waasi Nchini humo.

    Hatua ya Rais wa Marekani 馃嚭馃嚫, Donald Trump ya kusitisha misaada yote kwenye baadhi ya Nchi za Afrika ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliyokuwa ikitolewa na Marekani imeongeza hali ya wasiwasi Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako mamilioni ya Wakimbizi walikuwa wakitegemea misaada hiyo. Afisa kutoka Umoja wa Mataifa, Bruno Lemarquis, amenukuliwa akisema kuwa Nchi ya DR Congo ilikuwa ikipokea asilimia sabini (70) ya misaada ya kibinadamu kutoka Nchini Marekani. Uamuzi wa Trump umesababisha upungufu mkubwa wa mahitaji muhimu kwa Wakimbizi. Afisa huyo ameongeza kuwa kwa mwaka 2024 pekee, DR Congo ilipokea dola milioni 910 kutoka Nchini Marekani pamoja na misaada mingine kwa Waathirika wa mapigano kati ya Majeshi ya Serikali na Waasi Nchini humo.
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 135 Views
  • #SportsElite TETESIArsenal, Chelsea na Liverpool wanavutiwa na mlinzi wa Bournemouth mwenye umri wa chini ya miaka 21 Dean Huijsen, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 55 katika mkataba wake. (TBR Football),

    Liverpool wana nia ya kumsajili winga wa England chini ya miaka 21 mzaliwa wa Ufaransa Mohamed-Ali Cho, 21, kutoka Nice. (TeamTalks)

    Chelsea wanaandaa dau la pauni milioni 58.3 (euro milioni 70) msimu ujao kwa ajili ya beki wa Atletico Madrid mwenye umri wa miaka 21 Pablo Barrios. (Fichajes)

    Klabu ya Saudi Pro-League Al-Nassr ilikaribia sana kufikia makubaliano ya mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez kutoka Liverpool mnamo Januari kabla ya Reds kukataa mpango wa mchezaji huyo wa miaka 25. (Givemesport),
    #SportsElite TETESI馃審Arsenal, Chelsea na Liverpool wanavutiwa na mlinzi wa Bournemouth mwenye umri wa chini ya miaka 21 Dean Huijsen, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 55 katika mkataba wake. (TBR Football), Liverpool wana nia ya kumsajili winga wa England chini ya miaka 21 mzaliwa wa Ufaransa Mohamed-Ali Cho, 21, kutoka Nice. (TeamTalks) Chelsea wanaandaa dau la pauni milioni 58.3 (euro milioni 70) msimu ujao kwa ajili ya beki wa Atletico Madrid mwenye umri wa miaka 21 Pablo Barrios. (Fichajes) Klabu ya Saudi Pro-League Al-Nassr ilikaribia sana kufikia makubaliano ya mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez kutoka Liverpool mnamo Januari kabla ya Reds kukataa mpango wa mchezaji huyo wa miaka 25. (Givemesport),
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 176 Views
  • Performance ya rapa Kendrick Lamar kwenye usiku wa kilele cha mashindano ya NFL Superbowl 2025 imevunja rekodi na kuwa performance ya Superbowl iliyotazamwa zaidi kuliko performance nyingine ndani ya muda mfupi.

    Mpaka sasa performance hiyo imejikusanyia jumla ya watazamaji Milioni 133.5 huku ikijikusanyia watazamaji zaidi kwa asilimia 3 kupita performance ya mwaka jana.

    Takwimu hizo zimetolewa na Roc Nation ambao ni hushirikiana na Apple Music katika kuandaa performance za Superbowl.
    Performance ya rapa Kendrick Lamar kwenye usiku wa kilele cha mashindano ya NFL Superbowl 2025 imevunja rekodi na kuwa performance ya Superbowl iliyotazamwa zaidi kuliko performance nyingine ndani ya muda mfupi. Mpaka sasa performance hiyo imejikusanyia jumla ya watazamaji Milioni 133.5 huku ikijikusanyia watazamaji zaidi kwa asilimia 3 kupita performance ya mwaka jana. Takwimu hizo zimetolewa na Roc Nation ambao ni hushirikiana na Apple Music katika kuandaa performance za Superbowl.
    0 Comments 0 Shares 127 Views
  • Kikundi cha misaada cha Denmark kimetoa dola trilioni moja (1) kwa ajili ya kulinunua Jimbo la California Nchini Marekani siku chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema anataka kulinunua eneo la Greenland lililoko Nchini Denmark. Raia Denmark hao ambao wameonesha kumkejeli Rais trump wamesema watasambaza keki za Denmark katika Jimbo hilo bila kikomo ikiwa wazo lao litapokelewa.

    Trump amekuwa akijadili mara kwa mara kuhusu ununuzi wa Greenland eneo lenye uhuru la Denmark akionyesha thamani yake ya kimkakati na kiuchumi kwa Marekani. Hata hivyo, Maafisa wa Denmark na Greenland wamepinga vikali wazo hilo.

    Trump amesisitiza anaweza kutumia nguvu za kijeshi na kiuchumi ili kupata eneo hilo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, alisisitiza mwezi uliopita kwamba ununuzi wa Greenland ni lengo la kweli na "si jambo la kuchekesha."

    Kikundi cha misaada cha Denmark 馃嚛馃嚢 kimetoa dola trilioni moja (1) kwa ajili ya kulinunua Jimbo la California Nchini Marekani 馃嚭馃嚫 siku chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema anataka kulinunua eneo la Greenland lililoko Nchini Denmark. Raia Denmark hao ambao wameonesha kumkejeli Rais trump wamesema watasambaza keki za Denmark katika Jimbo hilo bila kikomo ikiwa wazo lao litapokelewa. Trump amekuwa akijadili mara kwa mara kuhusu ununuzi wa Greenland eneo lenye uhuru la Denmark akionyesha thamani yake ya kimkakati na kiuchumi kwa Marekani. Hata hivyo, Maafisa wa Denmark na Greenland wamepinga vikali wazo hilo. Trump amesisitiza anaweza kutumia nguvu za kijeshi na kiuchumi ili kupata eneo hilo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, alisisitiza mwezi uliopita kwamba ununuzi wa Greenland ni lengo la kweli na "si jambo la kuchekesha."
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 139 Views
  • #SportsElite...Manchester United wako tayari kuwasilisha dau la £33.3m (euro 40m) kwa beki wa kushoto wa Barcelona mwenye umri wa miaka 21 Alejandro Balde msimu ujao. (El Nacional - Spanish)

    Newcastle wanapanga kutoa dau la pauni milioni 33.3 (euro milioni 40) msimu ujao kwa mshambuliaji wa PSV Eindhoven na Ubelgiji Johan Bakayoko, 21. (Tuttosport – In Italy)

    Newcastle pia wanatazamiwa kuzipiku Barcelona na Real Madrid katika usajili wa bure wa winga wa Uhispania chini ya umri wa miaka 19 Antonio Cordero, 18, ambaye mkataba wake wa Malaga unamalizika msimu huu wa joto. (Mail)

    Manchester United na Chelsea wanavutiwa na mshambuliaji wa Ipswich Mwingereza Liam Delap, 22. (Football Insider)
    #SportsElite馃審...Manchester United wako tayari kuwasilisha dau la £33.3m (euro 40m) kwa beki wa kushoto wa Barcelona mwenye umri wa miaka 21 Alejandro Balde msimu ujao. (El Nacional - Spanish) Newcastle wanapanga kutoa dau la pauni milioni 33.3 (euro milioni 40) msimu ujao kwa mshambuliaji wa PSV Eindhoven na Ubelgiji Johan Bakayoko, 21. (Tuttosport – In Italy) Newcastle pia wanatazamiwa kuzipiku Barcelona na Real Madrid katika usajili wa bure wa winga wa Uhispania chini ya umri wa miaka 19 Antonio Cordero, 18, ambaye mkataba wake wa Malaga unamalizika msimu huu wa joto. (Mail) Manchester United na Chelsea wanavutiwa na mshambuliaji wa Ipswich Mwingereza Liam Delap, 22. (Football Insider)
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 211 Views
  • Rais wa Marekani , Donald Trump ameonya kuwa kama kundi la Hamas (Gaza) hawatawaachilia mateka wote wa Nchi ya Israel kufikia Jumamosi ya Wiki hii basi Dunia itashuhudia mashambulizi halisi katika eneo hilo. Onyo la Trump linakuja siku moja baada ya Kundi la Wapiganaji wa Hamas kuvunja makubaliano ya usitishwaji vita na Israel kwa kugoma kuendelea na zoezi la kuwaachia huru mateka wa Israel mpaka watakapotoa taarifa nyingine.

    Uamuzi huo wa Hamas umekuja siku chache baada ya Viongozi wake Wakuu kufanya ziara Nchini Iran na kukutana na Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khemenei ambaye aliwapongeza kwa kuendelea kusimama imara dhidi ya Israel. Trump wiki iliyopita alionya kuwa Gaza haitofaa kuwa eneo la kuishi chini ya Uongozi wa Hamas na kupendekeza kwamba Marekani ingependa kulichukua eneo hilo na kulisimamia huku Wakazi wa eneo hilo wakihamishiwa Nchi za Misri na Jordan .

    Rais huyo wa Marekani alisema Marekani ipo tayari kulinunua eneo hilo na kulimiliki na kuahidi kwamba Marekani italijenga na kulifanya kuwa eneo zuri la mfano Mashariki ya Kati. Kiufupi kundi la Hamas wanacheza na moto kwa sasa, Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz ameviagiza Vikosi vya Israel kukaa tayari kwa mashambulizi mapya iwapo Kundi hilo la Hamas likigoma kutii maelekezo ya kuachia mateka.

    Marekani ndio imekuwa Nchi inayoipa misaada mikubwa ya kibinadamu na kiuchumi Gaza pamoja na kuizuia Israel kutokuifutilia mbali Gaza kwa miaka mingi sasa ambapo Hamas imekua ikifanya uchokozi. Ikumbukwe Trump ni kati ya Viongozi wa Marekani ambaye ana msimamo mkali mno dhidi ya kundi la Hamas na tokea kuanza kwa mapigano Oktoba 7 mwaka 2023 Trump alisema Israel inachopaswa kufanya ni kulifutilia mbali kundi hilo.

    Rais wa Marekani 馃嚭馃嚫, Donald Trump ameonya kuwa kama kundi la Hamas (Gaza) hawatawaachilia mateka wote wa Nchi ya Israel 馃嚠馃嚤 kufikia Jumamosi ya Wiki hii basi Dunia itashuhudia mashambulizi halisi katika eneo hilo. Onyo la Trump linakuja siku moja baada ya Kundi la Wapiganaji wa Hamas kuvunja makubaliano ya usitishwaji vita na Israel kwa kugoma kuendelea na zoezi la kuwaachia huru mateka wa Israel mpaka watakapotoa taarifa nyingine. Uamuzi huo wa Hamas umekuja siku chache baada ya Viongozi wake Wakuu kufanya ziara Nchini Iran 馃嚠馃嚪 na kukutana na Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khemenei ambaye aliwapongeza kwa kuendelea kusimama imara dhidi ya Israel. Trump wiki iliyopita alionya kuwa Gaza haitofaa kuwa eneo la kuishi chini ya Uongozi wa Hamas na kupendekeza kwamba Marekani ingependa kulichukua eneo hilo na kulisimamia huku Wakazi wa eneo hilo wakihamishiwa Nchi za Misri 馃嚜馃嚞 na Jordan 馃嚡馃嚧. Rais huyo wa Marekani alisema Marekani ipo tayari kulinunua eneo hilo na kulimiliki na kuahidi kwamba Marekani italijenga na kulifanya kuwa eneo zuri la mfano Mashariki ya Kati. Kiufupi kundi la Hamas wanacheza na moto kwa sasa, Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz ameviagiza Vikosi vya Israel kukaa tayari kwa mashambulizi mapya iwapo Kundi hilo la Hamas likigoma kutii maelekezo ya kuachia mateka. Marekani ndio imekuwa Nchi inayoipa misaada mikubwa ya kibinadamu na kiuchumi Gaza pamoja na kuizuia Israel kutokuifutilia mbali Gaza kwa miaka mingi sasa ambapo Hamas imekua ikifanya uchokozi. Ikumbukwe Trump ni kati ya Viongozi wa Marekani ambaye ana msimamo mkali mno dhidi ya kundi la Hamas na tokea kuanza kwa mapigano Oktoba 7 mwaka 2023 Trump alisema Israel inachopaswa kufanya ni kulifutilia mbali kundi hilo.
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 255 Views
  • Waziri Mkuu wa Israel , Benjamin Netanyahu, amefikishwa mbele ya mahakama Jijini Tel Aviv kujibu mashtaka ya muda mrefu ya rushwa. Waziri huyo aliwasili akiwa na Timu yake ya Mawakili inayoongozwa na Amit Hadad, baada ya kuamriwa kutoa ushahidi katika kesi tatu (3) za rushwa za mwaka 2019, zinazohusisha zawadi kutoka kwa Marafiki Mamilionea na madai ya kutafuta hisani kutoka kwa Matajiri wa vyombo vya habari kwa kubadilishana na fursa bora ya utangazaji.

    Hata hivyo, Netanyahu amekana mashtaka yote yanayomkabili. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu (75) ameweka rekodi ya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza Nchini humo kushtakiwa kwa uhalifu.

    Waziri Mkuu wa Israel 馃嚠馃嚤, Benjamin Netanyahu, amefikishwa mbele ya mahakama Jijini Tel Aviv kujibu mashtaka ya muda mrefu ya rushwa. Waziri huyo aliwasili akiwa na Timu yake ya Mawakili inayoongozwa na Amit Hadad, baada ya kuamriwa kutoa ushahidi katika kesi tatu (3) za rushwa za mwaka 2019, zinazohusisha zawadi kutoka kwa Marafiki Mamilionea na madai ya kutafuta hisani kutoka kwa Matajiri wa vyombo vya habari kwa kubadilishana na fursa bora ya utangazaji. Hata hivyo, Netanyahu amekana mashtaka yote yanayomkabili. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu (75) ameweka rekodi ya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza Nchini humo kushtakiwa kwa uhalifu.
    Love
    Wow
    2
    0 Comments 0 Shares 240 Views
More Results