Usikubali kuanguka na kuendelea kukaa chini huku una UWEZO mkubwa ndani yako. Hakuna aliyewahi kufanikiwa moja kwa moja tena pasipo kupitia maanguko mengi. Kila mtu unayemwona amefanikiwa leo hii ni matokeo ya kuwa chini mara nyingi alikokutana nako.
Tofauti ni kuwa, watu waliofanikiwa wakianguka mahali hawachelewi kuinuka na wanatumia anguko lao kama sehemu ya kujiboresha zaidi kwenye safari ya maisha yao. Hii ni tofauti sana na watu wanaoshindwa katika maisha, wao wakianguka wanabaki chini wakisubiri watu wengine wawainue au kuwatia moyo, wakilia na kusononeka kwamba kwa nini wameanguka. Nataka nikuambie hata mwanafunzi wa Yesu aliyejulikana kwa jina la Petro aliwahi kuanguka kwa kuamkana Yesu mara tatu lakini alipogundua amekosea, aliinuka akatubu kisha akaendelea na safari yake dhidi ya kusudi aliloitiwa.
Usikubali kuanguka kwenye eneo lolote kwenye maisha yako ukakubali kubaki chini pasipo kuinuka. Acha kubaki ulipo ukijilaumu na kujisemea mengi mabaya dhidi yako. Acha kuendelea kulaumu wengine kwa anguko lako. Kumbuka mwenye jukumu la maisha yako 100% ni wewe mwenyewe, hivyo inakupasa kuinuka binafsi hapo ulipo pasipo kusubiri kuinuliwa na mtu mwingine. Unahitaji KUJITIA NGUVU na kuinuka ili uweze kuifaata ndoto yako na kuifanikisha.
Kama umeanguka kwenye masomo inuka na rudi shule tena kuendelea na masomo yako ili kufanya vizuri zaidi. Kama umeanguka kwenye biashara hakikisha unarudi kwenye biashara yako ili kuleta matokeo mapya yatakayobadilisha biashara yako. Usijikatie tamaa kwa sababu ya kushindwa mara moja. Kushindwa si kushindwa ila kukubali kushindwa ndio kushindwa. Inuka maana uwezo mkubwa wa kushinda upo ndani yako. Amini wewe ni mshindi.
Believe It's Possible!
#ishindotoyako

·199 Views