Mvua zafichua makaburi ya pamoja yenye miili kadhaa Uvira, Sud-Kivu.
Mvua kubwa zilizonyesha katika Mji wa Uvira, Mkoani Sud-Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimesababisha kugunduliwa kwa angalau makaburi matatu ya pamoja yaliyokuwa yamefukiwa kwa siri.
Kaburi la kwanza liligunduliwa karibu na ofisi ya Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwenye barabara ya Kavinvira, ambapo miili takriban 35 ilipatikana. Mvua hizo zilifichua baadhi ya maiti zilizokuwa zimefunikwa kwa udongo, hali iliyosababisha harufu kali iliyowatahadharisha wakazi wa eneo hilo.
Mbali na eneo hilo, kaburi lingine la pamoja limeripotiwa kupatikana katika kitongoji cha Kilomoni ndani ya Mji huo huo.
Aidha, katika makaburi ya Mji, Wanaharakati wa kiraia wanasema pia kuna uwezekano wa kuwepo kwa miili kadhaa zaidi. Takriban kilomita 30 kutoka hapo, katika Mji wa Sange, kaburi jingine linadaiwa kuwa na takriban waathiriwa kumi.
Katika muktadha wa vita vinavyoendelea mashariki mwa nchi, baadhi ya vyanzo vya ndani vinayahusisha makaburi hayo na Waasi wa M23, wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, tuhuma ambazo zimekuwa zikijirudia mara kwa mara katika mgogoro huo. Hata hivyo, wengine wanawalaumu wanamgambo wa kujilinda wanaojulikana kama Wazalendo.
Afisa mmoja wa ngazi ya juu ndani ya M23 alikiri kupitia chapisho kwamba baadhi ya makaburi ya pamoja yaliyopo Mikoa ya Sud-Kivu na Nord-Kivu yanahusishwa na operesheni za Afisa mmoja wa Waasi.
Wakazi tayari wamewasiliana na mamlaka za Mkoa kuhusu tukio hilo. Timu maalum zimefika katika maeneo husika ili kuyahifadhi na kufunika miili, ingawa hadi sasa hakuna uchimbaji rasmi uliofanyika.
Hali hiyo imeibua wasiwasi mkubwa kuhusu uhifadhi wa ushahidi muhimu.
Mashirika kadhaa yanataka kufanyika kwa uchimbaji wa miili kwa utaratibu rasmi, kufunguliwa kwa uchunguzi wa kisheria usioegemea upande wowote, pamoja na kutambuliwa kwa waathiriwa. Pia wanasisitiza umuhimu wa mazishi ya heshima na kuwafikisha mahakamani wanaodaiwa kuhusika.
Wito huo unaangazia umuhimu wa haki ya mpito na mapambano dhidi ya utamaduni wa kutoadhibiwa katika eneo hilo linalokumbwa na mzozo wa muda mrefu.

0 Comentários
0 Compartilhamentos
2 Visualizações