• KWENU MNAOJIITA WACHAMBUZI KWA KOFIA ZA USHABIKI NA CHUKI BINAFSI

    kuna kipindi Azam Fc iliwapa wachezaji 5 Simba sports club ili Simba ichukue Ubingwa

    Kuna kipindi kwenye mchezo mmoja Saido ntibanzokiza aliachiwa magoli matano kwenye mechi moja ili Amfikie Fiston kalala Mayele

    Kuna kipindi mchezaji wa Coastal Union alikwepa mpira uliopigwa na saido ili uwe goli

    Mzunguko wa kwanza michezo 2 ya kwanza ya Simba sc dhidi ya Tabora United na Fountain Gate fc wachezaji walifungiwa na kuonekana hawana vibali baada ya wote kucheza na Simba vibali vyao vilikuwepo na walicheza vema na kushinda

    Mzunguko huu wa pili vivyo hivyo Tabora United wachezaji wake Muhimu walikuwa majeruhi na wengine hawakuwa na vibali ila mara tu baada ya kucheza na Simba wachezaji wote walipata vibali na waliokuwa wanaumwa walipona

    Yanga sc ambayo jana imetufunga goli 2 kwa moja ni kikosi hiki hiki kama sikosei ndicho kilichowalamba Tano ni Yanga hii hii ambayo mtoto amezaliwa na amekuwa hajawahi kuona japo Simba ikipata walau Draw dhidi ya yanga kila siku ni vichapo tu

    Nilichogundua mashabiki wengi wa Simba wana wivu sana huwa wanataka wafungwe wao peke yao na Yanga

    Mkiona hapawafai mnaruhusiwa kuhama ligi ila kwa Taarifa za ndaaaaaaani Yanga wamesema popote mtakapohamia na wenyewe watakuja

    Asubuhi mbaya kwenu wabaya wetu
    KWENU MNAOJIITA WACHAMBUZI KWA KOFIA ZA USHABIKI NA CHUKI BINAFSI kuna kipindi Azam Fc iliwapa wachezaji 5 Simba sports club ili Simba ichukue Ubingwa Kuna kipindi kwenye mchezo mmoja Saido ntibanzokiza aliachiwa magoli matano kwenye mechi moja ili Amfikie Fiston kalala Mayele Kuna kipindi mchezaji wa Coastal Union alikwepa mpira uliopigwa na saido ili uwe goli Mzunguko wa kwanza michezo 2 ya kwanza ya Simba sc dhidi ya Tabora United na Fountain Gate fc wachezaji walifungiwa na kuonekana hawana vibali baada ya wote kucheza na Simba vibali vyao vilikuwepo na walicheza vema na kushinda Mzunguko huu wa pili vivyo hivyo Tabora United wachezaji wake Muhimu walikuwa majeruhi na wengine hawakuwa na vibali ila mara tu baada ya kucheza na Simba wachezaji wote walipata vibali na waliokuwa wanaumwa walipona Yanga sc ambayo jana imetufunga goli 2 kwa moja ni kikosi hiki hiki kama sikosei ndicho kilichowalamba Tano ni Yanga hii hii ambayo mtoto amezaliwa na amekuwa hajawahi kuona japo Simba ikipata walau Draw dhidi ya yanga kila siku ni vichapo tu Nilichogundua mashabiki wengi wa Simba wana wivu sana huwa wanataka wafungwe wao peke yao na Yanga Mkiona hapawafai mnaruhusiwa kuhama ligi ila kwa Taarifa za ndaaaaaaani Yanga wamesema popote mtakapohamia na wenyewe watakuja Asubuhi mbaya kwenu wabaya wetu
    0 Comments ·0 Shares ·144 Views
  • “Ukiwa Mwandishi wa Habari una vitu viwili muhimu vya kuchunga navyo ni Ulimi wako na Mikono yako, unapaswa kufahamu unaongea nini ama unaandika kitu gani, nyuma ya mauaji ya Kimbari yalikuwa ni matamshi ya Watangazaji pia ambao walieneza chuki, kwasasa kuna kazi mbili za hatari nazo ni Ualimu na Waandishi wa Habari, hawa wanaweza kutengeneza taifa la Wajinga ama Waelevu.

    Nataka kusema nini? Nataka kusema juu ya kelele na shutuma za Yanga na Singida bado hakuna aliyetupa picha kamili zaidi ni kuwa Mashabiki wanalalamika kwa hisia, Waandishi tunalalamika kwa hisia ila hakuna anayekuja mbele kutoa usahihi, inaitwa Proving beyond reasonable doubt! Nimeona Wadau wanasema TFF haifanyi chochote, lakini wewe umewapa tip gani? Taasisi haifanyi maamuzi kwa hisia, the corporate world works differently from streets.

    Bado kizazi chetu cha Uandishi kuna kitu kinamiss ni INVESTIGATIVE JOURNALISM, binafsi nakiri wazi TUMEFELI sana eneo hili, yaani sote tunalaumu Singida kufanya rotation tunaita kupanga matokeo, tangu lini duniani kubadili kikosi chako ni kupanga matokeo? Ikitokea Coastal kabadili kikosi, ikitokea Simba kabadili ama AZAM? Yani timu inalaumiwa kwa kutumia Wachezaji wake?

    Tunaweza kuwa na hoja ila mpaka sasa hazina mashiko zaidi tunaonekana tunalalama ila tukipelekwa Mahakamani hakuna ambaye atathibitisha chochote, kama kufungwa ni kupanga matokeo mara ya mwisho Simba kumfunga Yanga ndani ya dakika 90 ni lini? Kama kufungwa ni kupanga matokeo lini Singida kamfunga Simba? Kama kufungwa ni kupanga lini Namungo kamfunga Simba lini?

    Sisi WAANDISHI tuna homework tunapaswa kufanya, tutaharibu fikra za Watanzania! Wenzetu Ulaya walipoibua kashfa ya Casciopoli pale Italia walikuja na data, hata UEFA Heated Balls Scandal watu walikuwa na data! Yanga wakisema waende kisheria nani anaweza kuja na hoja za kueleweka? Kama hakuna taarifa sahihi, mifano hai basi tunaongelea hisia, TFF atareact endapo atajitokea Mtu akaattack matter not the subject" - Farhan JR, Mchambuzi.

    “Ukiwa Mwandishi wa Habari una vitu viwili muhimu vya kuchunga navyo ni Ulimi wako na Mikono yako, unapaswa kufahamu unaongea nini ama unaandika kitu gani, nyuma ya mauaji ya Kimbari yalikuwa ni matamshi ya Watangazaji pia ambao walieneza chuki, kwasasa kuna kazi mbili za hatari nazo ni Ualimu na Waandishi wa Habari, hawa wanaweza kutengeneza taifa la Wajinga ama Waelevu. Nataka kusema nini? Nataka kusema juu ya kelele na shutuma za Yanga na Singida bado hakuna aliyetupa picha kamili zaidi ni kuwa Mashabiki wanalalamika kwa hisia, Waandishi tunalalamika kwa hisia ila hakuna anayekuja mbele kutoa usahihi, inaitwa Proving beyond reasonable doubt! Nimeona Wadau wanasema TFF haifanyi chochote, lakini wewe umewapa tip gani? Taasisi haifanyi maamuzi kwa hisia, the corporate world works differently from streets. Bado kizazi chetu cha Uandishi kuna kitu kinamiss ni INVESTIGATIVE JOURNALISM, binafsi nakiri wazi TUMEFELI sana eneo hili, yaani sote tunalaumu Singida kufanya rotation tunaita kupanga matokeo, tangu lini duniani kubadili kikosi chako ni kupanga matokeo? Ikitokea Coastal kabadili kikosi, ikitokea Simba kabadili ama AZAM? Yani timu inalaumiwa kwa kutumia Wachezaji wake? Tunaweza kuwa na hoja ila mpaka sasa hazina mashiko zaidi tunaonekana tunalalama ila tukipelekwa Mahakamani hakuna ambaye atathibitisha chochote, kama kufungwa ni kupanga matokeo mara ya mwisho Simba kumfunga Yanga ndani ya dakika 90 ni lini? Kama kufungwa ni kupanga matokeo lini Singida kamfunga Simba? Kama kufungwa ni kupanga lini Namungo kamfunga Simba lini? Sisi WAANDISHI tuna homework tunapaswa kufanya, tutaharibu fikra za Watanzania! Wenzetu Ulaya walipoibua kashfa ya Casciopoli pale Italia walikuja na data, hata UEFA Heated Balls Scandal watu walikuwa na data! Yanga wakisema waende kisheria nani anaweza kuja na hoja za kueleweka? Kama hakuna taarifa sahihi, mifano hai basi tunaongelea hisia, TFF atareact endapo atajitokea Mtu akaattack matter not the subject" - Farhan JR, Mchambuzi.
    0 Comments ·0 Shares ·232 Views
  • Zakazakazi azidi kumshushia nondo Amri Kiemba.

    MUONGO!

    Amri Kiemba alicheza Simba kwa misimu mitano na nusu, kuanzia 2009/10 hadi Disemba 2014.

    Katika kipindi hicho, Azam FC na Simba zilikutana mara 10, Simba ikishinda mara tano na Azam FC mara tatu, na mara mbili sare...angalia picha ya pili.

    Katika hizo mara tano ambazo Simba ilishinda, mbili ni za msimu wa 2009/10.

    24/10/2009
    Simba 1-0 Azam FC

    14/3/2010
    Azam FC 0-2 Simba

    Huu ulikuwa msimu ambao Simba ilikuwa kwenye ubora mkubwa sana na ikamaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja.

    Walishinda mechi zote za mzunguko wa kwanza, wakaja kupata sare mbili tu mzunguko wa pili, dhidi ya Kagera Sugar na African Lyon.

    Kwa ubora huo, huwezi kuilamu Azam FC ilhali timu zote zilifungwa...kiungwana unawasifia Simba kwamba walikuwa kwenye ubora wa hali ya juu.

    Lakini baada ya msimu huo, Azam FC na Simba zililingana matokeo hadi Kiemba alipoondoka Simba kwenda Azam FC.

    Swali ni je, Kiemba anapata wapi uhalali wa kutilia shaka maandalizi yaliyoleta matokeo kama haya?

    Msimu wa 2013/14, Azam FC ikawa kwenye ubora mkubwa na kumaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja, ikiwemo kushinda nje ndani dhidi ya Simba ya Kiemba na maandalizi yao ya hali ya juu.

    28/10/2013
    Simba 1-2 Azam FC

    30/3/2014
    Azam FC 2-1 Simba

    Baada ya mechi hizi Kiemba akaenda Azam FC...na mechi yake ya kwanza ikaisha kwa sare ya 1-1.

    Ni vipi Kiemba hakuridhika na maandalizi ya Azam FC yaliyoleta sare lakini aliridhika na maandalizi ya Simba yaliyowafanya wafungwe nje ndani msimu mmoja tu nyuma yake?

    Msimu mmoja kabla Kiemba hajasajiliwa Simba, Azam FC ilishinda 2-0 na mashabiki wa Simba wakaenda kushusha kinyesi nyumbani kwa mwenyekiti wao Hassan Dalali.

    Ina maana maandalizi ya Azam FC yangekuwa hafifu yangewatoa kinyesi Simba kweli?

    Azam FC ilikuwa inaifunga Simba kabla yeye hajaenda, na ikaifunga akiwemo...kwa maandalizi yale yale...halafu anakuja hadharani leo, miaka zaidi ya 10 na kusema aliona maandalizi hafifu...sasa walikuwa wanashindaje kwa maandalizi hafifu?

    Ni mbaya sana kumuita mtu muongo...lakini Kiemba kwenye hili itoshe tu kusema kwamba WEWE NI MUONGO!

    Zakazakazi azidi kumshushia nondo Amri Kiemba. MUONGO! Amri Kiemba alicheza Simba kwa misimu mitano na nusu, kuanzia 2009/10 hadi Disemba 2014. Katika kipindi hicho, Azam FC na Simba zilikutana mara 10, Simba ikishinda mara tano na Azam FC mara tatu, na mara mbili sare...angalia picha ya pili. Katika hizo mara tano ambazo Simba ilishinda, mbili ni za msimu wa 2009/10. 24/10/2009 Simba 1-0 Azam FC 14/3/2010 Azam FC 0-2 Simba Huu ulikuwa msimu ambao Simba ilikuwa kwenye ubora mkubwa sana na ikamaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja. Walishinda mechi zote za mzunguko wa kwanza, wakaja kupata sare mbili tu mzunguko wa pili, dhidi ya Kagera Sugar na African Lyon. Kwa ubora huo, huwezi kuilamu Azam FC ilhali timu zote zilifungwa...kiungwana unawasifia Simba kwamba walikuwa kwenye ubora wa hali ya juu. Lakini baada ya msimu huo, Azam FC na Simba zililingana matokeo hadi Kiemba alipoondoka Simba kwenda Azam FC. Swali ni je, Kiemba anapata wapi uhalali wa kutilia shaka maandalizi yaliyoleta matokeo kama haya? Msimu wa 2013/14, Azam FC ikawa kwenye ubora mkubwa na kumaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja, ikiwemo kushinda nje ndani dhidi ya Simba ya Kiemba na maandalizi yao ya hali ya juu. 28/10/2013 Simba 1-2 Azam FC 30/3/2014 Azam FC 2-1 Simba Baada ya mechi hizi Kiemba akaenda Azam FC...na mechi yake ya kwanza ikaisha kwa sare ya 1-1. Ni vipi Kiemba hakuridhika na maandalizi ya Azam FC yaliyoleta sare lakini aliridhika na maandalizi ya Simba yaliyowafanya wafungwe nje ndani msimu mmoja tu nyuma yake? Msimu mmoja kabla Kiemba hajasajiliwa Simba, Azam FC ilishinda 2-0 na mashabiki wa Simba wakaenda kushusha kinyesi nyumbani kwa mwenyekiti wao Hassan Dalali. Ina maana maandalizi ya Azam FC yangekuwa hafifu yangewatoa kinyesi Simba kweli? Azam FC ilikuwa inaifunga Simba kabla yeye hajaenda, na ikaifunga akiwemo...kwa maandalizi yale yale...halafu anakuja hadharani leo, miaka zaidi ya 10 na kusema aliona maandalizi hafifu...sasa walikuwa wanashindaje kwa maandalizi hafifu? Ni mbaya sana kumuita mtu muongo...lakini Kiemba kwenye hili itoshe tu kusema kwamba WEWE NI MUONGO!
    0 Comments ·0 Shares ·141 Views
  • Zakazakazi amjibu Amri Kiemba.

    TUONGEE KWA FACT

    Ni kweli kwamba Amri Kiemba alicheza Azam FC kwa mkopo wa miezi 6 akitokea Simba, 2014/15.

    Alisajiliwa dirisha dogo lililofunguliwa Disemba 15, 2014, na walikuja wawili, yeye na Saad Kawemba kama mtendaji mku (CEO).

    Akiwa Azam FC, Kiemba alikutana na mechi mbili dhidi ya Simba,

    24/01/2015
    Azam FC 1-1 Simba

    Hii mechi ndiyo ile ambayo Aggrey Morris alimfanyia madhambi Okwi hadi akapoteza fahamu...akaenda kuzindukia hospitali.

    02/05/2015
    Simba 2-1 Azam FC

    Hii mechi kwa asilimia kubwa iliamuliwa na kadi nyekundu ya Salum Abubakar dakika 38, na kuumia kwa Frank Domayo dakika chache baadaye.

    Lakini hadi wakati huo, Azam FC ilikuwa imeushika mchezo hasa. Kipindi cha pili Simba wakapata goli, Azam FC ikiwa pungufu ikasawazisha...dakika za jioni Simba wakapata bao la pili.

    Hii ilikuwa mechi ya kwanza ya Simba kuifunga Azam FC tangu Oktoba 27, 2012 kwenye ile mechi ambayo Azam FC ilisimamisha wachezaji wanne ikiwatuhumu kuihujumu timu.

    Wachezaji hawa ni Agrey Morris, Erasto Nyoni, Dida na Said Morad...na walisimamishwa hadi Aprili 2013. Yaani timu ifanye maandalizi finyu halafu isimamishe wachezaji wanne kwa takribani miezi 6?

    Simba baada ya kushinda mchezo huo, hawakushinda tena ndiyo hadi 2015...na 2016...tena hadi 2018.

    Kuanzia 2013 hadi 2017 Simba walishinda mechi mbili tu dhidi ya Azam...halafu Kiemba anasema alikuwa haoni maandalizi...maandalizi gani?

    Kama adui yako anakufa kwa asali, kwanini umpige bunduki?

    Kiemba alikuwa Simba ambayo ilifungwa mfululizo na Azam FC kwa miaka mitatu...walikuwa wanajiandaaje huko?

    Kiemba anaheshimika sana, lakini huu ushuhuda wake wa kupika unamvunjia heshima.

    Eti maandalizi dhidi ya Yanga yalikuwa tofauti. Ok...akiwa Azam FC, Kiemba alikutana na mechi mbili dhidi ya Yanga.

    28/12/2014
    Yanga 2-2 Azam FC

    06/05/2015
    Azam FC 2-1 Yanga

    Hii mechi ndiyo ile ya siku ya mvua nyingi, Yanga wameshakuwa mabingwa.

    Coutinho anataka kupiga faulo, Ngassa anamnyang'anya mpira.

    Kwa wanaokumbuka, wataikumbuka mechi hii.

    Huu ulikuwa mchezo wa kwanza Azam FC kuifunga Yanga tangu 2013, lakini katika kipindi hicho, Simba akichomoka kwa Azam, ni sare!

    Zakazakazi amjibu Amri Kiemba. TUONGEE KWA FACT Ni kweli kwamba Amri Kiemba alicheza Azam FC kwa mkopo wa miezi 6 akitokea Simba, 2014/15. Alisajiliwa dirisha dogo lililofunguliwa Disemba 15, 2014, na walikuja wawili, yeye na Saad Kawemba kama mtendaji mku (CEO). Akiwa Azam FC, Kiemba alikutana na mechi mbili dhidi ya Simba, 24/01/2015 Azam FC 1-1 Simba Hii mechi ndiyo ile ambayo Aggrey Morris alimfanyia madhambi Okwi hadi akapoteza fahamu...akaenda kuzindukia hospitali. 02/05/2015 Simba 2-1 Azam FC Hii mechi kwa asilimia kubwa iliamuliwa na kadi nyekundu ya Salum Abubakar dakika 38, na kuumia kwa Frank Domayo dakika chache baadaye. Lakini hadi wakati huo, Azam FC ilikuwa imeushika mchezo hasa. Kipindi cha pili Simba wakapata goli, Azam FC ikiwa pungufu ikasawazisha...dakika za jioni Simba wakapata bao la pili. Hii ilikuwa mechi ya kwanza ya Simba kuifunga Azam FC tangu Oktoba 27, 2012 kwenye ile mechi ambayo Azam FC ilisimamisha wachezaji wanne ikiwatuhumu kuihujumu timu. Wachezaji hawa ni Agrey Morris, Erasto Nyoni, Dida na Said Morad...na walisimamishwa hadi Aprili 2013. Yaani timu ifanye maandalizi finyu halafu isimamishe wachezaji wanne kwa takribani miezi 6? Simba baada ya kushinda mchezo huo, hawakushinda tena ndiyo hadi 2015...na 2016...tena hadi 2018. Kuanzia 2013 hadi 2017 Simba walishinda mechi mbili tu dhidi ya Azam...halafu Kiemba anasema alikuwa haoni maandalizi...maandalizi gani? Kama adui yako anakufa kwa asali, kwanini umpige bunduki? Kiemba alikuwa Simba ambayo ilifungwa mfululizo na Azam FC kwa miaka mitatu...walikuwa wanajiandaaje huko? Kiemba anaheshimika sana, lakini huu ushuhuda wake wa kupika unamvunjia heshima. Eti maandalizi dhidi ya Yanga yalikuwa tofauti. Ok...akiwa Azam FC, Kiemba alikutana na mechi mbili dhidi ya Yanga. 28/12/2014 Yanga 2-2 Azam FC 06/05/2015 Azam FC 2-1 Yanga Hii mechi ndiyo ile ya siku ya mvua nyingi, Yanga wameshakuwa mabingwa. Coutinho anataka kupiga faulo, Ngassa anamnyang'anya mpira. Kwa wanaokumbuka, wataikumbuka mechi hii. Huu ulikuwa mchezo wa kwanza Azam FC kuifunga Yanga tangu 2013, lakini katika kipindi hicho, Simba akichomoka kwa Azam, ni sare!
    0 Comments ·0 Shares ·107 Views
  • "Watu wanaizungumza tu Singida na Yanga hata Simba kuna timu wanapata nazo fever, wakati ninachezea Azam maandalizi ya mchezo dhidi ya Yanga yalikuwa ya hali ya juu, lakini maandalizi ya mechi dhdi ya Simba yalikuwa ya kawaida ni kama maandalizi ya mechi ya Kengold" - Amri Kiemba, Mchezaji wa zamani wa klabu ya Azam FC na Mchambuzi.

    "Watu wanaizungumza tu Singida na Yanga hata Simba kuna timu wanapata nazo fever, wakati ninachezea Azam maandalizi ya mchezo dhidi ya Yanga yalikuwa ya hali ya juu, lakini maandalizi ya mechi dhdi ya Simba yalikuwa ya kawaida ni kama maandalizi ya mechi ya Kengold" - Amri Kiemba, Mchezaji wa zamani wa klabu ya Azam FC na Mchambuzi.
    0 Comments ·0 Shares ·102 Views
  • "Kwa mijadala ambayo nimeitazama inaendelea baada ya mchezo wa Yanga na Singida Black Stars inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu walikuwa na matokeo ya Singida kushinda kwenye mechi hiyo.

    Kikawaida mwalimu anaweza kupanga kikosi kulingana na mahitaji ya mchezo husika na namna ambavyo amewasoma wapinzani na sio mchezaji bora anaweza kuanza kwenye mechi.

    Kinachoendelea kwasasa ni kuzinyima uhuru hizi timu za madaraja ya chini kuamua wachezaji zitakazowatumia kwenye michezo yake dhidi ya Simba na Yanga.

    Hii pia ni aina moja wapo ya kudumaza soka letu. Yanga kwenye ubora wao kila timu imepata ilichokitegemea, kila timu imevuna ilichokipanda.Ili timu isiwe imepanga matokeo lazima iifunge Yanga? Na ikifungwa tu basi imepanga matokeo?

    Tuwape uhuru makocha wa kuamua nyota watakaocheza kwenye michezo husika kulingana na mbinu za wapinzani wao." - Lameck Shabahanga Mwandishi wa habari.

    "Kwa mijadala ambayo nimeitazama inaendelea baada ya mchezo wa Yanga na Singida Black Stars inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu walikuwa na matokeo ya Singida kushinda kwenye mechi hiyo. Kikawaida mwalimu anaweza kupanga kikosi kulingana na mahitaji ya mchezo husika na namna ambavyo amewasoma wapinzani na sio mchezaji bora anaweza kuanza kwenye mechi. Kinachoendelea kwasasa ni kuzinyima uhuru hizi timu za madaraja ya chini kuamua wachezaji zitakazowatumia kwenye michezo yake dhidi ya Simba na Yanga. Hii pia ni aina moja wapo ya kudumaza soka letu. Yanga kwenye ubora wao kila timu imepata ilichokitegemea, kila timu imevuna ilichokipanda.Ili timu isiwe imepanga matokeo lazima iifunge Yanga? Na ikifungwa tu basi imepanga matokeo? Tuwape uhuru makocha wa kuamua nyota watakaocheza kwenye michezo husika kulingana na mbinu za wapinzani wao." - Lameck Shabahanga Mwandishi wa habari.
    0 Comments ·0 Shares ·124 Views
  • "Wakati tunazilaumu Simba Sports na Azam Football Club Kuukosa Ubingwa,tukumbuke pia Mazingira Yao Magumu ya Kushindana

    Parameters za Simba Sports na Azam Fc Kuchukua Ubingwa zimebadilika Kabisa na ni tofauti Washindani wenzao Kwenye Ligi

    Kuna hoja Lazy sana eti Mbona Simba Sports alicheza na Tabora United Dhaifu?

    Kwenye Mechi zote 2 Tabora wana uwezo wa Ku justifie Kwanini walichezesha Vikosi vile na ukawaelewa vizuri tu.

    Mechi ya Kwanza n issue ya Vibali,na mechi ya Pili Heritier Makambo alikuwa na Kadi 3 za njano. Yacouba Sogne alikuwa ni Majeruhi..

    Kuna hoja Lazy nyingine Kwamba mbona Kikosi bora cha Singida Black Stars Kilifungwa 2-0 na KMC ambayo ilifungwa 6-1 na Yanga?

    Kwanza Kwenye hiyo hoja hapo wote tumekubaliana Kwamba Singida Black Stars wamepanga Kikosi Dhaifu

    Pili, Sisi hatusemi Singida Black Stars angepanga Kikosi bora lazima angeshinda dhidi ya Yanga au asingepoteza mechi

    Mbona ile Mechi ya Kwanza Kule Amani Complex Zanzibar Singida Black Stars waliweka Full Mkoko na bado Yanga alishinda 1-0 bao la Paccome ?

    Swali ni Sababu ipi ya Singida Black Stars Kubadilisha wachezaji 6 Kutoka Kwenye Kikosi Kilichomfunga Jkt Tanzania 1-0?

    Mbaya zaidi Kuna wachezaji walichezeshwa Kabisa nje ya Maeneo ya ya asili na wachezaji wenye nafasi zao wakiwa bench

    Singida black stars Dhaifu ilipigwa 2-0 Kipindi Cha Kwanza na Stars bora ilishinda 1-0 Kipindi cha Pili.

    Ligi yetu tukufu inachezewa na watu ambao hawana nia njema na Mpira wetu na Kama tusipotwanga sasa hivi tutakuja Kuula Mbichi" - Wilson Orumo, Mchambuzi.

    "Wakati tunazilaumu Simba Sports na Azam Football Club Kuukosa Ubingwa,tukumbuke pia Mazingira Yao Magumu ya Kushindana Parameters za Simba Sports na Azam Fc Kuchukua Ubingwa zimebadilika Kabisa na ni tofauti Washindani wenzao Kwenye Ligi Kuna hoja Lazy sana eti Mbona Simba Sports alicheza na Tabora United Dhaifu? Kwenye Mechi zote 2 Tabora wana uwezo wa Ku justifie Kwanini walichezesha Vikosi vile na ukawaelewa vizuri tu. Mechi ya Kwanza n issue ya Vibali,na mechi ya Pili Heritier Makambo alikuwa na Kadi 3 za njano. Yacouba Sogne alikuwa ni Majeruhi.. Kuna hoja Lazy nyingine Kwamba mbona Kikosi bora cha Singida Black Stars Kilifungwa 2-0 na KMC ambayo ilifungwa 6-1 na Yanga? Kwanza Kwenye hiyo hoja hapo wote tumekubaliana Kwamba Singida Black Stars wamepanga Kikosi Dhaifu Pili, Sisi hatusemi Singida Black Stars angepanga Kikosi bora lazima angeshinda dhidi ya Yanga au asingepoteza mechi Mbona ile Mechi ya Kwanza Kule Amani Complex Zanzibar Singida Black Stars waliweka Full Mkoko na bado Yanga alishinda 1-0 bao la Paccome ? Swali ni Sababu ipi ya Singida Black Stars Kubadilisha wachezaji 6 Kutoka Kwenye Kikosi Kilichomfunga Jkt Tanzania 1-0? Mbaya zaidi Kuna wachezaji walichezeshwa Kabisa nje ya Maeneo ya ya asili na wachezaji wenye nafasi zao wakiwa bench Singida black stars Dhaifu ilipigwa 2-0 Kipindi Cha Kwanza na Stars bora ilishinda 1-0 Kipindi cha Pili. Ligi yetu tukufu inachezewa na watu ambao hawana nia njema na Mpira wetu na Kama tusipotwanga sasa hivi tutakuja Kuula Mbichi" - Wilson Orumo, Mchambuzi.
    0 Comments ·0 Shares ·162 Views
  • Miaka miwili mingine ya kuitumikia Simba
    Miaka miwili mingine ya kuitumikia Simba
    Love
    1
    · 1 Comments ·0 Shares ·32 Views
  • Zambro Traore wakala wa wachezaji wa kigeni waliopo Yanga, Simba na Singida Black Stars
    Zambro Traore wakala wa wachezaji wa kigeni waliopo Yanga, Simba na Singida Black Stars 🔥
    Like
    1
    · 1 Comments ·0 Shares ·38 Views
  • Kipa wa Simba, MOUSSA CAMARA amefikisha clean sheet ya 14 kwenye ligi msimu huu akicheza mechi 18 akiendelea kuongoza.
    .
    Clean Sheet hizo zinalingana na zile ambazo Djigui Diarra wa Yanga alizomaliza nazo msimu uliopita alipocheza mechi 21, huku pia akibakisha moja kuzifikia za Ley Matampi aliyekuwa Coastal Union ambaye aliibuka kinara msimu uliopita kwenye mechi zake 25 kati ya 30.


    #paulswai
    🚨 Kipa wa Simba, MOUSSA CAMARA amefikisha clean sheet ya 14 🧤 kwenye ligi msimu huu akicheza mechi 18 akiendelea kuongoza. . Clean Sheet hizo zinalingana na zile ambazo Djigui Diarra wa Yanga alizomaliza nazo msimu uliopita alipocheza mechi 21, huku pia akibakisha moja kuzifikia za Ley Matampi aliyekuwa Coastal Union ambaye aliibuka kinara msimu uliopita kwenye mechi zake 25 kati ya 30. #paulswai
    Like
    Yay
    3
    · 1 Comments ·0 Shares ·244 Views
  • SHEREHEKEENI PAMOJA SIKU YENU

    Picha inaiieleza kwamba ni ya mwaka 1948, waasisi wa klabu ya Yanga wakiwa na wenzao wa Africa Sports ya Zanzibar.

    Picha hii inatufundisha kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haukuwa mwaka 1964 bali zamani sana...mwaka 1964 ulikuwa mkataba tu.

    Na hata kutengana kuliletwa na wakoloni, wakaweka mipaka na kuigawana ardhi...mjerumani akachukua Bara na mwingereza akachukua Zanzibar.

    Lakini kabla ya mipaka yao, hii nchi ilikuwa moja tu, na hata mji wa Dar es Salaam ulianzishwa na Sultan Majid wa Zanzibar.

    Yaani aliamua tu kutoka sehemu moja ya nchi yake na kwenda kuanzisha mji sehemu nyingine ya nchi yake.

    Lakini hilo lengo la andiko hili...

    Lengo la kuandika hapa ni kutaka kuwakumbusha watu kwamba waliopo kwenye picha ni waasisi wa Yanga, na pia hawa ndiyo waasisi wa Simba.

    Na hii ni kwa sababu walioanzisha Simba ni wale wale walioanzisha Yanga, lakini wakajitenga na wenzao.

    Ni hivi

    Kulikuwa na timu iliyoitwa New Young, ambayo ilianzishwa mwaka 1935 na kuanza kushiriki ligi mwaka huo huo.

    Wakati huo ligi ilikuwa moja tu, ya Dar es Salaam...na Dar es Salaam yenyewe ilikuwa wilaya ya jimbo la Mashariki.

    Hakukuwa na ligi nyingine yoyote nchini, japo miaka michache baadaye wilaya zingine nazo zikaanzisha ligi...ikianza wilaya ya Iringa. Stori yake itakuja siku nyingine.

    Ligi ya Dar es Salaam ambayo ilianza 1929 ikiwa na daraja moja tu, la kwanza...ilikua na kuongeza daraja la pili kwenye miaka ya 1930.

    Kwa hiyo New Young ilipojiunga na ligi mwaka 1935, ikaanzia daraja la pili.

    Ikashinda ubingwa na kupanda daraja la kwanza, mwaka 1936. Hata hivyo ilicheza ligi kwa mtindo wa VIEW ONCE kwani ilishuka mwaka huo huo.

    Kushuka kwao ndiko kulikoleta mpasuko na wengine kujitenga.

    Waliojitenga ndiyo hawa ambao sasa ni Simba, na waliobaki wakabadili jina kutoka New Young na kujiita Young Africans ambao ndiyo Yanga.

    Lakini hawa watu walikuwa pamoja mwaka mmoja tu uliopita...na ndiyo waliopo kwenye picha hii.

    Kwa hiyo leo inatakiwa hii sherehe iwe yao wote! Happy Birthday Yanga na Simba. Furahieni siku yenu kwa amani. Sisi tunajua nyinyi ni ndugu ila mnatuzuga tu!
    (Zakazakazi )

    SHEREHEKEENI PAMOJA SIKU YENU Picha inaiieleza kwamba ni ya mwaka 1948, waasisi wa klabu ya Yanga wakiwa na wenzao wa Africa Sports ya Zanzibar. Picha hii inatufundisha kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haukuwa mwaka 1964 bali zamani sana...mwaka 1964 ulikuwa mkataba tu. Na hata kutengana kuliletwa na wakoloni, wakaweka mipaka na kuigawana ardhi...mjerumani akachukua Bara na mwingereza akachukua Zanzibar. Lakini kabla ya mipaka yao, hii nchi ilikuwa moja tu, na hata mji wa Dar es Salaam ulianzishwa na Sultan Majid wa Zanzibar. Yaani aliamua tu kutoka sehemu moja ya nchi yake na kwenda kuanzisha mji sehemu nyingine ya nchi yake. Lakini hilo lengo la andiko hili... Lengo la kuandika hapa ni kutaka kuwakumbusha watu kwamba waliopo kwenye picha ni waasisi wa Yanga, na pia hawa ndiyo waasisi wa Simba. Na hii ni kwa sababu walioanzisha Simba ni wale wale walioanzisha Yanga, lakini wakajitenga na wenzao. Ni hivi Kulikuwa na timu iliyoitwa New Young, ambayo ilianzishwa mwaka 1935 na kuanza kushiriki ligi mwaka huo huo. Wakati huo ligi ilikuwa moja tu, ya Dar es Salaam...na Dar es Salaam yenyewe ilikuwa wilaya ya jimbo la Mashariki. Hakukuwa na ligi nyingine yoyote nchini, japo miaka michache baadaye wilaya zingine nazo zikaanzisha ligi...ikianza wilaya ya Iringa. Stori yake itakuja siku nyingine. Ligi ya Dar es Salaam ambayo ilianza 1929 ikiwa na daraja moja tu, la kwanza...ilikua na kuongeza daraja la pili kwenye miaka ya 1930. Kwa hiyo New Young ilipojiunga na ligi mwaka 1935, ikaanzia daraja la pili. Ikashinda ubingwa na kupanda daraja la kwanza, mwaka 1936. Hata hivyo ilicheza ligi kwa mtindo wa VIEW ONCE kwani ilishuka mwaka huo huo. Kushuka kwao ndiko kulikoleta mpasuko na wengine kujitenga. Waliojitenga ndiyo hawa ambao sasa ni Simba, na waliobaki wakabadili jina kutoka New Young na kujiita Young Africans ambao ndiyo Yanga. Lakini hawa watu walikuwa pamoja mwaka mmoja tu uliopita...na ndiyo waliopo kwenye picha hii. Kwa hiyo leo inatakiwa hii sherehe iwe yao wote! Happy Birthday Yanga na Simba. Furahieni siku yenu kwa amani. Sisi tunajua nyinyi ni ndugu ila mnatuzuga tu! (Zakazakazi ✍️)
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·254 Views
  • Mpinzani wa SimbaSC hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB ni TMA FC.

    #paulswai
    Mpinzani wa SimbaSC hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB ni TMA FC. #paulswai
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·231 Views
  • "Ni mambo mawili yakitokea mchambuzi utamlaumu Ladarck Chasambi, moja, ni kama umesahau, mbili, kama haufahamu moja ya msingi wa mpira wa miguu ambao ni kuutunza mpira, na hasa kwa kuutoa mpira sehemu yenye vurugu na kuupeleka palipotulia.

    Kama unafahamu kanuni au principle hii hauwezi kumlaumu Chasambi kupita kiasi, angalia hao wachezaji wa FG niliowawekea mishale, wote wanatoa shinikizo kwa Chasambi, wamefunga njia karibu pande zote na kuacha chaguo moja kubwa la kucheza na golikipa wake.

    Na golikipa Camara alitambua kuwa Chasambi ana chaguo moja tu la kumrudishia yeye mpira na Camara akaonesha utayari wa kuucheza mpira, wanaocheza mpira na walimu wataungana na mimi kuwa mpira una lugha yake na Camara aliitumia kuonesha utayari.

    Kitu pekee ninachoweza kumkumbusha Chasambi ni kuwa wazo lake lilikua sahihi lakini mguso wake kwa mpira ulikuwa mzito na kuufanya mpira uende mbali na kwa kasi zaidi wenzetu wanasema “heavy touch”
    Kitu pekee ninachoweza kumkumbusha Camara ni alitakiwa kusogea kushoto kwa haraka kukutana na boli, ni kama alichelewa kidogo kushiriki mchezo, na misstiming kwa Camara imewai kutokea pia katika mechi ambayo Coastal Union wanasawazisha dhidi ya Simba SC" - Amri Kiemba, Mchambuzi.

    "Ni mambo mawili yakitokea mchambuzi utamlaumu Ladarck Chasambi, moja, ni kama umesahau, mbili, kama haufahamu moja ya msingi wa mpira wa miguu ambao ni kuutunza mpira, na hasa kwa kuutoa mpira sehemu yenye vurugu na kuupeleka palipotulia. Kama unafahamu kanuni au principle hii hauwezi kumlaumu Chasambi kupita kiasi, angalia hao wachezaji wa FG niliowawekea mishale, wote wanatoa shinikizo kwa Chasambi, wamefunga njia karibu pande zote na kuacha chaguo moja kubwa la kucheza na golikipa wake. Na golikipa Camara alitambua kuwa Chasambi ana chaguo moja tu la kumrudishia yeye mpira na Camara akaonesha utayari wa kuucheza mpira, wanaocheza mpira na walimu wataungana na mimi kuwa mpira una lugha yake na Camara aliitumia kuonesha utayari. Kitu pekee ninachoweza kumkumbusha Chasambi ni kuwa wazo lake lilikua sahihi lakini mguso wake kwa mpira ulikuwa mzito na kuufanya mpira uende mbali na kwa kasi zaidi wenzetu wanasema “heavy touch” Kitu pekee ninachoweza kumkumbusha Camara ni alitakiwa kusogea kushoto kwa haraka kukutana na boli, ni kama alichelewa kidogo kushiriki mchezo, na misstiming kwa Camara imewai kutokea pia katika mechi ambayo Coastal Union wanasawazisha dhidi ya Simba SC" - Amri Kiemba, Mchambuzi.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·258 Views
  • "Rasmi leo ndio umekua mtu mzima wa kimpira, ingekua kimaumbile tungesema umebaleghe hii leo

    Matusi, kejeli, na dhihaka zote utakazopokea leo ni ukaribisho kwenye ukubwa wako, yasikutishe tamaa na wala yasikuvunje moyo, KARIBU UKUBWANI

    Umeumiza mioyoo ya Wana Simba, lakini wewe sio wa kwanza kwenye mpira, wapo wenzio makosa yao yaliwanyima Kombe la Dunia

    Kosa hili linakuongezea ukomavu

    Ndugu zangu Wana Simba najua tunahisira na kijana wetu lakini kila mtu kazini kwake anakosea

    Na tukumbuke kabla ya kujifunga alishaisaidia timu kupata goli hivyo sukari na chumvi vimechanganyikana hii leo na bahati mbaya chumvi imezidi

    Tukasirike lakini tusimchukie, na kama haitoshi tumsamehe na tuanze kumtia moyo

    Kipindi hiki anatuhitaji zaidi sisi familia yake kumtetea na kumpigania ili arejee kwenye utulivu wake wa kiakali na aendelee kuipigania Simba yetu

    Tunapatia pamoja, tunakosea pamoja, tunajisahihisha pamoja tunasonga mbele" - Ahmed Ally, Msemaji wa klabu ya Simba SC.

    "Rasmi leo ndio umekua mtu mzima wa kimpira, ingekua kimaumbile tungesema umebaleghe hii leo Matusi, kejeli, na dhihaka zote utakazopokea leo ni ukaribisho kwenye ukubwa wako, yasikutishe tamaa na wala yasikuvunje moyo, KARIBU UKUBWANI Umeumiza mioyoo ya Wana Simba, lakini wewe sio wa kwanza kwenye mpira, wapo wenzio makosa yao yaliwanyima Kombe la Dunia Kosa hili linakuongezea ukomavu Ndugu zangu Wana Simba najua tunahisira na kijana wetu lakini kila mtu kazini kwake anakosea Na tukumbuke kabla ya kujifunga alishaisaidia timu kupata goli hivyo sukari na chumvi vimechanganyikana hii leo na bahati mbaya chumvi imezidi Tukasirike lakini tusimchukie, na kama haitoshi tumsamehe na tuanze kumtia moyo Kipindi hiki anatuhitaji zaidi sisi familia yake kumtetea na kumpigania ili arejee kwenye utulivu wake wa kiakali na aendelee kuipigania Simba yetu Tunapatia pamoja, tunakosea pamoja, tunajisahihisha pamoja tunasonga mbele" - Ahmed Ally, Msemaji wa klabu ya Simba SC.
    Sad
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·281 Views
  • SIMBA SAFARI MUMEIMALIZA
    PUMZIKA KWA AMANI..HEBU ONA KILELENI KULIVYO KWA BARIDI ...AHSANTE SANA FOUNTAIN GATE ...
    SIMBA SAFARI MUMEIMALIZA PUMZIKA KWA AMANI..HEBU ONA KILELENI KULIVYO KWA BARIDI ...AHSANTE SANA FOUNTAIN GATE ...🤣🤣
    0 Comments ·0 Shares ·137 Views
  • Hawa simba wanatukwamisha watu tumebeti uku na hiyo beti tunaitegemea kwenye kulipa kodi dah.
    Hawa simba wanatukwamisha watu tumebeti uku na hiyo beti tunaitegemea kwenye kulipa kodi dah. 😭😭😭
    0 Comments ·0 Shares ·102 Views
  • Wana Simba apewe zawadi gani huyu jamaa? maana kaokoa jahazi.
    Wana Simba apewe zawadi gani huyu jamaa? maana kaokoa jahazi.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·102 Views
  • Goaaaaaal..! Ateba

    Fountain Gate 0️⃣ 1️⃣ Simba Sc

    Chasambi

    #paulswai
    Goaaaaaal..! Ateba ⚽ Fountain Gate 0️⃣ 🆚 1️⃣ Simba Sc 🎯 Chasambi #paulswai
    Like
    Love
    3
    · 1 Comments ·0 Shares ·373 Views
  • Klabu zinazofanya vizuri katika Ligi Kuu zao barani Afrika kwa Wiki (14) zilizopita.

    3. Simba SC
    8. Yanga SC

    Klabu zinazofanya vizuri katika Ligi Kuu zao barani Afrika kwa Wiki (14) zilizopita. 3. Simba SC 8. Yanga SC
    0 Comments ·0 Shares ·136 Views

  • "Tumejipanga kubeba ubingwa msimu huu Hatutaki maneno mengi " MCHUNGAJI WA SIMBA

    #paulswai
    "Tumejipanga kubeba ubingwa msimu huu Hatutaki maneno mengi " MCHUNGAJI WA SIMBA #paulswai
    Like
    Love
    Wow
    3
    · 0 Comments ·0 Shares ·448 Views ·7
More Results