• Katika hatua mpya ya mzozo unaoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , kundi la Waasi wa M23 likishirikiana na Muungano wa Mto Congo (AFC) limetangaza kuwa Wanajeshi wa zamani wa Jeshi la DR Congo (FARDC) waliokamatwa au kujisalimisha wamehitimu mafunzo ya kiitikadi na mbinu za kijeshi.

    Katika taarifa ya Kundi la M23 kwenye mtandao wao wa X leo Februari 18, picha zilionyesha Wanajeshi hao wakiwa na sare na silaha rasmi za wanamgambo hao. Ujumbe uliambatana na chapisho hilo ulieleza:

    "Wanajeshi wa zamani wa FARDC, waliokamatwa au kujisalimisha, wamemaliza mafunzo ya kiitikadi na mbinu huko Rumangabo Mjini Goma chini ya AFC/M23. Sasa wakiwa na vifaa kamili na wanaolipwa, wametumwa Lubero, ambako wanashiriki kikamilifu muungano wa serikali."

    Wakati huo huo, Uganda imetangaza kuwa vikosi vyake vya kijeshi vimeanza kuelekea Bunia, DRC, ikiwa ni siku chache baada ya Jeshi la Uganda kutoa muda wa saa 24 kwa Askari waliopo eneo hilo kujisalimisha.

    Taarifa nyingine kuwa, hapo jana Kundi la Waasi hao wa M23 wamefanikiwa kuteka eneo la Kamanyola na sasa hivi wanajipanga kuelekea Uvira, Fizi kisha Mkoa wa Tanganyika (Kalemie) kabla ya kwenda Mjini Lubumbashi. Kwa mujibu wa Wananchi wa Kamanyala wanasema kuwa Kundi la Wapiganaji wa Wazalendo ambao wanapigana kwa upande wa Serikali waliibwa Silaha zao kisha wakakimbia na kuwaachia M23 kuichukua Kamanyola.

    Katika hatua mpya ya mzozo unaoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, kundi la Waasi wa M23 likishirikiana na Muungano wa Mto Congo (AFC) limetangaza kuwa Wanajeshi wa zamani wa Jeshi la DR Congo (FARDC) waliokamatwa au kujisalimisha wamehitimu mafunzo ya kiitikadi na mbinu za kijeshi. Katika taarifa ya Kundi la M23 kwenye mtandao wao wa X leo Februari 18, picha zilionyesha Wanajeshi hao wakiwa na sare na silaha rasmi za wanamgambo hao. Ujumbe uliambatana na chapisho hilo ulieleza: "Wanajeshi wa zamani wa FARDC, waliokamatwa au kujisalimisha, wamemaliza mafunzo ya kiitikadi na mbinu huko Rumangabo Mjini Goma chini ya AFC/M23. Sasa wakiwa na vifaa kamili na wanaolipwa, wametumwa Lubero, ambako wanashiriki kikamilifu muungano wa serikali." Wakati huo huo, Uganda imetangaza kuwa vikosi vyake vya kijeshi vimeanza kuelekea Bunia, DRC, ikiwa ni siku chache baada ya Jeshi la Uganda kutoa muda wa saa 24 kwa Askari waliopo eneo hilo kujisalimisha. Taarifa nyingine kuwa, hapo jana Kundi la Waasi hao wa M23 wamefanikiwa kuteka eneo la Kamanyola na sasa hivi wanajipanga kuelekea Uvira, Fizi kisha Mkoa wa Tanganyika (Kalemie) kabla ya kwenda Mjini Lubumbashi. Kwa mujibu wa Wananchi wa Kamanyala wanasema kuwa Kundi la Wapiganaji wa Wazalendo ambao wanapigana kwa upande wa Serikali waliibwa Silaha zao kisha wakakimbia na kuwaachia M23 kuichukua Kamanyola.
    0 Comments ·0 Shares ·165 Views
  • wananchi Kwa mara nyingne Tena
    🔥🤟🤟🤟wananchi Kwa mara nyingne Tena
    0 Comments ·0 Shares ·103 Views
  • Wananchi kuzisaka point tatu ijumaa hii zid ka kmc hatok mtu
    Venue; kmc complex
    Time:10:15 jion
    Wananchi kuzisaka point tatu ijumaa hii zid ka kmc hatok mtu Venue; kmc complex Time:10:15 jion
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·108 Views
  • Habari iliyobamba kwa sasa kwenye vyombo vya habari ni ndoa ya Stephane Aziz Ki na Hamisa Mobetto, ingawa wapo waliofika mbali na kudai ni kiki tu kwa ajili ya matangazo ya bidhaa fulani na wanatumika tu.

    Baada ya vuta nkuvute ya stori hii hatimaye mama yake Hamisa, Shufaa Rutanga amefunga na anathibitisha kuwepo kwa ndoa hiyo na kuhusu posa ya Aziz Ki, amesema hakuna posa yoyote iliyofika kwake kutoka kwa nyota huyo wa kimataifa wa Burkina Faso ingawa amepokea nyingi kutoka kwa wanaume tofauti wanaotaka kumuoa mwanaye.

    “Sasa ngoja nikuambie ukweli, maana nilikuwa nashindwa kutoa majibu sahihi kutokana na baadhi ya ya vitu kuhusu ndoa hii vilikuwa havijakamilika, sasa vimekamilika na ndoa ipo. Kiukweli namshukuru Mungu maombi yangu kwa mwanagu yameitika, nilikuwa kila kukicha naomba apate mtu sahihi watakayependana ili aolewe, kuwa kwenye ndoa ni heshima kubwa sana" - Mama Mobetto

    Mama Hamisa anasema hekaheka za ndoa hiyo zitaanza Jumamosi Februari 15 na ndiyo siku mahari itatolewa na sherehe itafanyika Februari 19, The Superdome, Masaki, jijini Dar es Salaam.

    “Kutoka moyoni nimewapa baraka zote mkwe wangu AziZ Ki na mwanagu Hamisa na upendo mwingi sana kwake Aziz Ki kwa kupenda watoto wa Hamisa. Hiki ndiyo sababu kuu iliyonifanya nimpende zaidi Aziz Ki, maana kwa hali ya sasa hivi upate mwanamume atakayekubali kuoa mwanamke mwenye watoto ni wachache sana ila Aziz Ki ameonyesha upendo wa dhati kwa mwanangu Hamisa, kapenda boga na maua yake.” - Mama Mobetto

    Wakati huohuo mmoja wa viongozi wa Yanga, amethibitisha ni kweli wawili hao watafunga ndoa Ijumaa na kwasasa Aziz yupo kwenye maandalizi ya Ndoa ingawa atakuwepo kwenye mchezo wa Ijumaa.
    (Mwananchi)

    Habari iliyobamba kwa sasa kwenye vyombo vya habari ni ndoa ya Stephane Aziz Ki na Hamisa Mobetto, ingawa wapo waliofika mbali na kudai ni kiki tu kwa ajili ya matangazo ya bidhaa fulani na wanatumika tu. Baada ya vuta nkuvute ya stori hii hatimaye mama yake Hamisa, Shufaa Rutanga amefunga na anathibitisha kuwepo kwa ndoa hiyo na kuhusu posa ya Aziz Ki, amesema hakuna posa yoyote iliyofika kwake kutoka kwa nyota huyo wa kimataifa wa Burkina Faso ingawa amepokea nyingi kutoka kwa wanaume tofauti wanaotaka kumuoa mwanaye. “Sasa ngoja nikuambie ukweli, maana nilikuwa nashindwa kutoa majibu sahihi kutokana na baadhi ya ya vitu kuhusu ndoa hii vilikuwa havijakamilika, sasa vimekamilika na ndoa ipo. Kiukweli namshukuru Mungu maombi yangu kwa mwanagu yameitika, nilikuwa kila kukicha naomba apate mtu sahihi watakayependana ili aolewe, kuwa kwenye ndoa ni heshima kubwa sana" - Mama Mobetto Mama Hamisa anasema hekaheka za ndoa hiyo zitaanza Jumamosi Februari 15 na ndiyo siku mahari itatolewa na sherehe itafanyika Februari 19, The Superdome, Masaki, jijini Dar es Salaam. “Kutoka moyoni nimewapa baraka zote mkwe wangu AziZ Ki na mwanagu Hamisa na upendo mwingi sana kwake Aziz Ki kwa kupenda watoto wa Hamisa. Hiki ndiyo sababu kuu iliyonifanya nimpende zaidi Aziz Ki, maana kwa hali ya sasa hivi upate mwanamume atakayekubali kuoa mwanamke mwenye watoto ni wachache sana ila Aziz Ki ameonyesha upendo wa dhati kwa mwanangu Hamisa, kapenda boga na maua yake.” - Mama Mobetto Wakati huohuo mmoja wa viongozi wa Yanga, amethibitisha ni kweli wawili hao watafunga ndoa Ijumaa na kwasasa Aziz yupo kwenye maandalizi ya Ndoa ingawa atakuwepo kwenye mchezo wa Ijumaa. (Mwananchi)
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·263 Views
  • Kwa mujibu wa wa kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un , migogoro inayochochewa na Marekani katika sehemu mbalimbali za dunia, "inazidi kuongeza hatari ya kuzuka kwa vita vya dunia vipya vyenye athari kubwa sio tu kwa amani na usalama wa kimataifa bali pia nyanja nyingine zote za shughuli za binadamu."

    Pia Kim alitoa maoni kwamba mwaka 2025, mzozo wa Ukraine utasalia kuwa moja ya "mhimili mkuu wa hali ya wasiwasi ya kimataifa," nyingine ikiwa hali katika Ukanda wa Gaza na Syria "ambayo imekuwa uwanja wa migogoro ya kijiografia na makabiliano ya kimataifa mwaka jana."

    Katika hatua nyingine Kim alisema Marekani na nchi za Magharibi zinaelezea mzozo wa Ukraine kwa kushindwa kuishinda Urusi kimkakati, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alisema, kama ilivyonukuliwa na Shirika la Habari la Korea (KCNA).

    Katika mkutano katika Wizara ya Ulinzi, kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 77 ya Jeshi la Wananchi wa Korea, alidai kwamba Marekani imepofushwa na tamaa mbaya huku akiionyesha wasiwasi mkubwa juu ya tabia ya kutojali ya Marekani na kundi la Magharibi kwa makusudi kuendeleza vita vya muda mrefu kwa ndoto isiyoweza kutekelezwa ili kukabiliana na kurudi kwa kimkakati kwa Urusi," shirika la habari lilibainisha.

    Kim alidokeza kuwa Pyongyang imekuwa ikipinga kila mara "kitendo chochote cha kunyima haki ya kimataifa na kuvuruga amani na usalama duniani." Aliongeza kuwa nchi yake "itaunga mkono kila wakati na kuhimiza sababu ya haki ya jeshi la Urusi na watu kutetea uhuru wao, usalama na uadilifu wa eneo kwa kuzingatia ari ya mkataba juu ya ushirikiano wa kimkakati wa kina kati ya DPRK na Urusi."
    (Zungu)

    Kwa mujibu wa wa kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un , migogoro inayochochewa na Marekani katika sehemu mbalimbali za dunia, "inazidi kuongeza hatari ya kuzuka kwa vita vya dunia vipya vyenye athari kubwa sio tu kwa amani na usalama wa kimataifa bali pia nyanja nyingine zote za shughuli za binadamu." Pia Kim alitoa maoni kwamba mwaka 2025, mzozo wa Ukraine utasalia kuwa moja ya "mhimili mkuu wa hali ya wasiwasi ya kimataifa," nyingine ikiwa hali katika Ukanda wa Gaza na Syria "ambayo imekuwa uwanja wa migogoro ya kijiografia na makabiliano ya kimataifa mwaka jana." Katika hatua nyingine Kim alisema Marekani na nchi za Magharibi zinaelezea mzozo wa Ukraine kwa kushindwa kuishinda Urusi kimkakati, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alisema, kama ilivyonukuliwa na Shirika la Habari la Korea (KCNA). Katika mkutano katika Wizara ya Ulinzi, kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 77 ya Jeshi la Wananchi wa Korea, alidai kwamba Marekani imepofushwa na tamaa mbaya huku akiionyesha wasiwasi mkubwa juu ya tabia ya kutojali ya Marekani na kundi la Magharibi kwa makusudi kuendeleza vita vya muda mrefu kwa ndoto isiyoweza kutekelezwa ili kukabiliana na kurudi kwa kimkakati kwa Urusi," shirika la habari lilibainisha. Kim alidokeza kuwa Pyongyang imekuwa ikipinga kila mara "kitendo chochote cha kunyima haki ya kimataifa na kuvuruga amani na usalama duniani." Aliongeza kuwa nchi yake "itaunga mkono kila wakati na kuhimiza sababu ya haki ya jeshi la Urusi na watu kutetea uhuru wao, usalama na uadilifu wa eneo kwa kuzingatia ari ya mkataba juu ya ushirikiano wa kimkakati wa kina kati ya DPRK na Urusi." (Zungu)
    0 Comments ·0 Shares ·375 Views
  • Kuhusu mkutano mkubwa wa Makundi ya Waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo uliofanyika Jijini Goma leo hii ambapo mambo mengi yamezungumzwa pamoja na kuwateua Viongozi wapya wa Mji huo baada ya kuutwaa.

    Mkutano huo umefanyika katika Uwanja mkubwa wa Stade De L'Unite uliopo Jijini hapo na kuhudhuriwa na Viongozi wakuu wa Makundi ya Waasi hao akiwemo Kiongozi Mkuu Corneille Nangaa ambaye ni Kiongozi Congo River Allience na Muungano wao, Bertrand Bisimwa ambaye ni Kiongozi Mkuu wa M23 na Luteni Kanali Willy Ngoma ambaye ni Msemaji wa M23.

    Mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya Wananchi wa Goma huku wakiushangilia kwa nderemo na vifijo ambapo baadhi ya Watu nje na ndani ya DR Congo wameshangaza kwamba kumbe Wananchi wengi pia wanaunga mkono Waasi hao na wapo pamoja nao. Lugha ya Kiswahili ilitumika Viongozi hao na kutoa mipango yao ya kuichukua Nchi nzima kutoka kwa Serikali iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais Felix Tshisekedi.

    Msemaji wa M23, Willy Ngoma akiwa Jukwaani aliwauliza Wananchi "mnataka tuishie hapa Goma tu? " Wananchi kwa shangwe kubwa wakajibu "hapana".

    Kuhusu mkutano mkubwa wa Makundi ya Waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 uliofanyika Jijini Goma leo hii ambapo mambo mengi yamezungumzwa pamoja na kuwateua Viongozi wapya wa Mji huo baada ya kuutwaa. Mkutano huo umefanyika katika Uwanja mkubwa wa Stade De L'Unite uliopo Jijini hapo na kuhudhuriwa na Viongozi wakuu wa Makundi ya Waasi hao akiwemo Kiongozi Mkuu Corneille Nangaa ambaye ni Kiongozi Congo River Allience na Muungano wao, Bertrand Bisimwa ambaye ni Kiongozi Mkuu wa M23 na Luteni Kanali Willy Ngoma ambaye ni Msemaji wa M23. Mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya Wananchi wa Goma huku wakiushangilia kwa nderemo na vifijo ambapo baadhi ya Watu nje na ndani ya DR Congo wameshangaza kwamba kumbe Wananchi wengi pia wanaunga mkono Waasi hao na wapo pamoja nao. Lugha ya Kiswahili ilitumika Viongozi hao na kutoa mipango yao ya kuichukua Nchi nzima kutoka kwa Serikali iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais Felix Tshisekedi. Msemaji wa M23, Willy Ngoma akiwa Jukwaani aliwauliza Wananchi "mnataka tuishie hapa Goma tu? " Wananchi kwa shangwe kubwa wakajibu "hapana".
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·268 Views
  • Je, nini kinaweza kuwa suluhisho la kudumu kwa Kivu Kaskazini na DRC kwa ujumla?

    Mazungumzo ya kina na makundi ya waasi – Kupitia majadiliano yanayojumuisha waasi, serikali, na wadau wa kikanda ili kufikia makubaliano ya amani.

    Kushughulikia mizizi ya mgogoro – Mgogoro wa DRC unahusiana na rasilimali, ukabila, na siasa za kikanda. Ni lazima kuwe na suluhisho la kisera linalozingatia haya yote.

    Msaada wa kimataifa wenye ufanisi – Umoja wa Mataifa na jumuiya za kikanda kama AU na EAC wanapaswa kushirikiana kuhakikisha kuwa msaada wa kijeshi na diplomasia unakwenda sambamba.

    Marekebisho ya kijeshi na kiuchumi – Kuimarisha jeshi la DRC na kupunguza utegemezi wa wanajeshi wa kigeni, pamoja na kuweka mikakati ya maendeleo ili wananchi wa Kivu Kaskazini wapate ajira na fursa badala ya kushawishika kujiunga na makundi ya waasi.

    Kwa sasa, swali kubwa linabaki:

    Je, Tshisekedi atachagua vita au diplomasia?

    Na je, nini kingekuwa suluhisho la kudumu kwa mgogoro wa Kivu Kaskazini na DRC kwa ujumla?
    Je, nini kinaweza kuwa suluhisho la kudumu kwa Kivu Kaskazini na DRC kwa ujumla? Mazungumzo ya kina na makundi ya waasi – Kupitia majadiliano yanayojumuisha waasi, serikali, na wadau wa kikanda ili kufikia makubaliano ya amani. Kushughulikia mizizi ya mgogoro – Mgogoro wa DRC unahusiana na rasilimali, ukabila, na siasa za kikanda. Ni lazima kuwe na suluhisho la kisera linalozingatia haya yote. Msaada wa kimataifa wenye ufanisi – Umoja wa Mataifa na jumuiya za kikanda kama AU na EAC wanapaswa kushirikiana kuhakikisha kuwa msaada wa kijeshi na diplomasia unakwenda sambamba. Marekebisho ya kijeshi na kiuchumi – Kuimarisha jeshi la DRC na kupunguza utegemezi wa wanajeshi wa kigeni, pamoja na kuweka mikakati ya maendeleo ili wananchi wa Kivu Kaskazini wapate ajira na fursa badala ya kushawishika kujiunga na makundi ya waasi. Kwa sasa, swali kubwa linabaki: Je, Tshisekedi atachagua vita au diplomasia? Na je, nini kingekuwa suluhisho la kudumu kwa mgogoro wa Kivu Kaskazini na DRC kwa ujumla?
    Wow
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·228 Views
  • Huyu hapa kocha mpya wa Yanga alietambulishwa na hiyo ni profile yake mwananchi weka kama haupo kinyonge
    Huyu hapa kocha mpya wa Yanga alietambulishwa na hiyo ni profile yake💚💛 mwananchi weka ✅ kama haupo kinyonge
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·228 Views
  • TAARIFA KWA UMMA Mwananchi umeipokeaje je Uongozi wa Yanga wamefeli ua wapo sawa
    TAARIFA KWA UMMA Mwananchi umeipokeaje je Uongozi wa Yanga wamefeli ua wapo sawa💚💚💛💛
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·279 Views
  • Rais wa Marekani , Donald Trump ameendelea na msimamo wake na kuweka mkazo kuhusu kuifanya Nchi ya Canada kuwa jimbo la (51) la Nchi ya Marekani. Kupitia ukurasa wake wa mtandao X, Rais huyo amesema kuwa Nchi yake ya Marekani inatumia mabilioni ya fedha na punguzo za ushuru kuihudumia Canada hivyo hakuna haja Nchi hiyo kuendelea kuifaidi Marekani wakati ingeweza kuwa sehemu ya Marekani na kupata unafuu bila kuinyonya Nchi ya Marekani.

    Donald Trump amesema iwapo Nchi ya Canada itakataa mpango huo basi tozo na ushuru wa bidhaa kwa Taifa hilo utapanda mara dufu na kulingana mataifa mengine. Trump amesema iwapo Canada ikijiunga na Marekani hakutakuwa na tozo wala mazuio ya maelfu ya Raia wa Canada wanaoingia Marekani kufanya kazi.

    Ikumbukwe kwamba Nchi za Canada na Mexico ni kati ya mataifa yenye Raia wengi wanaofanya kazi za kujiingizia kipato Nchini Marekani ambao hawana vibali halali vya kazi na uhamiaji (Wahamiaji haramu). Tayari Donald Trump ameshaongea na Viongozi wakuu wa mataifa hayo na kuwapa muda wa siku thelathini (30) kuchukua hatua kwa mapendekezo yake ama utozaji wa tozo na ushuru wa asilimia (25) kwa bidhaa zao uanze mara moja.

    Viongozi wa Nchi hizo wamekiri kupokea maelekezo ya Trump na kuahidi kuchukua hatua ikiwemo kuzuia mipaka yao kuwa njia za Wahamiaji haramu. Waziri Mkuu wa Canada, Justin Tradeau amesema Canada kuwa sehemu ya Marekani haitawezekana licha ya kwamba huenda wakakutana rungu la kiuchumi kisha Wananchi wakaamua wenyewe kupitia uchunguzi (kura).

    Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump ameendelea na msimamo wake na kuweka mkazo kuhusu kuifanya Nchi ya Canada 🇨🇦 kuwa jimbo la (51) la Nchi ya Marekani. Kupitia ukurasa wake wa mtandao X, Rais huyo amesema kuwa Nchi yake ya Marekani inatumia mabilioni ya fedha na punguzo za ushuru kuihudumia Canada hivyo hakuna haja Nchi hiyo kuendelea kuifaidi Marekani wakati ingeweza kuwa sehemu ya Marekani na kupata unafuu bila kuinyonya Nchi ya Marekani. Donald Trump amesema iwapo Nchi ya Canada itakataa mpango huo basi tozo na ushuru wa bidhaa kwa Taifa hilo utapanda mara dufu na kulingana mataifa mengine. Trump amesema iwapo Canada ikijiunga na Marekani hakutakuwa na tozo wala mazuio ya maelfu ya Raia wa Canada wanaoingia Marekani kufanya kazi. Ikumbukwe kwamba Nchi za Canada na Mexico 🇲🇽 ni kati ya mataifa yenye Raia wengi wanaofanya kazi za kujiingizia kipato Nchini Marekani ambao hawana vibali halali vya kazi na uhamiaji (Wahamiaji haramu). Tayari Donald Trump ameshaongea na Viongozi wakuu wa mataifa hayo na kuwapa muda wa siku thelathini (30) kuchukua hatua kwa mapendekezo yake ama utozaji wa tozo na ushuru wa asilimia (25) kwa bidhaa zao uanze mara moja. Viongozi wa Nchi hizo wamekiri kupokea maelekezo ya Trump na kuahidi kuchukua hatua ikiwemo kuzuia mipaka yao kuwa njia za Wahamiaji haramu. Waziri Mkuu wa Canada, Justin Tradeau amesema Canada kuwa sehemu ya Marekani haitawezekana licha ya kwamba huenda wakakutana rungu la kiuchumi kisha Wananchi wakaamua wenyewe kupitia uchunguzi (kura).
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·343 Views
  • Ni tetesi

    Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga SC, S. Ramovic anatarajiwa kujiunga na klabu ya CR Belouizdad. Klabu hiyo ya Algeria ilituma ofa kwa Ramovic na kukubali kulipa fidia ya kuvunja mkataba na klabu ya Yanga SC huku klabu ya Yanga SC ikikubali kumuachia Ramovic na wamempa baraka zote.

    Inasemekana kuwa leo hii Ramovic amewaaga Wachezaji wake mazoezini alafu Mashabiki wa klabu ya Yanga SC (Wananchi) wanatarajiwa kuagwa kwenye mchezo wa Yanga SC dhidi ya klabu ya Kengold FC.

    @
    Ni tetesi Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga SC, S. Ramovic anatarajiwa kujiunga na klabu ya CR Belouizdad. Klabu hiyo ya Algeria ilituma ofa kwa Ramovic na kukubali kulipa fidia ya kuvunja mkataba na klabu ya Yanga SC huku klabu ya Yanga SC ikikubali kumuachia Ramovic na wamempa baraka zote. Inasemekana kuwa leo hii Ramovic amewaaga Wachezaji wake mazoezini alafu Mashabiki wa klabu ya Yanga SC (Wananchi) wanatarajiwa kuagwa kwenye mchezo wa Yanga SC dhidi ya klabu ya Kengold FC. @
    0 Comments ·0 Shares ·260 Views
  • "Tutaboresha uwezo wetu kwenye mchezo huu unaofuata na michezo inayokuja, Ligi si rahisi timu nyingi zinazokuja kwenye huu mzunguko wa pili wanajilinda sana kutokufungwa kwa hiyo nyingi zinaona bora kupata sare kuliko kupoteza alama zote tatu, walimu wanaliona hilo na wanalifanyia kazi" Mshery

    #timuyawananchi
    #daimambelenyumamwiko
    "Tutaboresha uwezo wetu kwenye mchezo huu unaofuata na michezo inayokuja, Ligi si rahisi timu nyingi zinazokuja kwenye huu mzunguko wa pili wanajilinda sana kutokufungwa kwa hiyo nyingi zinaona bora kupata sare kuliko kupoteza alama zote tatu, walimu wanaliona hilo na wanalifanyia kazi" Mshery #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko
    0 Comments ·0 Shares ·448 Views
  • 𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒

    "Maandalizi yetu kwa ujumla yapo vizuri,tumejiandaa vizuri kwenda kucheza mchezo wetu dhidi ya KenGold"

    "Wamesajili wachezaji wengi wazoefu ukilinganisha na mzunguko wa kwanza, na kwetu sisi hiki ni kitu kizuri maana mechi itakuwa nzuri sana maana wana wachezaji wazoefu na wachezaji wanaojua" Mshery

    #timuyawananchi
    #daimambelenyumamwiko
    𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒💬 "Maandalizi yetu kwa ujumla yapo vizuri,tumejiandaa vizuri kwenda kucheza mchezo wetu dhidi ya KenGold" "Wamesajili wachezaji wengi wazoefu ukilinganisha na mzunguko wa kwanza, na kwetu sisi hiki ni kitu kizuri maana mechi itakuwa nzuri sana maana wana wachezaji wazoefu na wachezaji wanaojua" Mshery #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·453 Views
  • 𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒

    "Jonathan ni mchezaji mzuri sana, jambo la kwanza tunalopaswa kufanya, bila shaka, ni kumfikisha kwenye kiwango cha utimamu wa mwili tunachotaka. Kwa sababu si tu kuhusu utimamu wa mwili, bali pia kuhakikisha kwamba hapati majeraha. Ikiwa hana utimamu wa kutosha na anahitaji kukimbia kwa kasi kwenye mechi, kuna uwezekano mkubwa wa kuumia, na hilo ndilo tunalotaka kuepuka.

    Lakini bila shaka yeye ni mchezaji mzuri na katika siku zijazo atatusaidia sana" Sead Ramovic

    #timuyawananchi
    #daimambelenyumamwiko
    𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒💬 "Jonathan ni mchezaji mzuri sana, jambo la kwanza tunalopaswa kufanya, bila shaka, ni kumfikisha kwenye kiwango cha utimamu wa mwili tunachotaka. Kwa sababu si tu kuhusu utimamu wa mwili, bali pia kuhakikisha kwamba hapati majeraha. Ikiwa hana utimamu wa kutosha na anahitaji kukimbia kwa kasi kwenye mechi, kuna uwezekano mkubwa wa kuumia, na hilo ndilo tunalotaka kuepuka. Lakini bila shaka yeye ni mchezaji mzuri na katika siku zijazo atatusaidia sana" Sead Ramovic #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·466 Views
  • 𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒

    "Nadhani tumeboresha mambo mengi tangu nilipokuja, na bila shaka tunahitaji kuwa makini zaidi katika safu ya ushambuliaji. Katika mechi za mwisho, tulifunga mabao mengi na tulipata nafasi nyingi mbele ya goli. Hii ni moja ya nguvu zetu, lakini tunapaswa kuwa na umakini zaidi katika kumalizia na kujaribu kufunga mabao zaidi, kwa sababu tunataka kuwa bora katika kila kitu tunachofanya" Sead Ramovic

    #timuyawananchi
    #daimambelenyumamwiko
    𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒💬 "Nadhani tumeboresha mambo mengi tangu nilipokuja, na bila shaka tunahitaji kuwa makini zaidi katika safu ya ushambuliaji. Katika mechi za mwisho, tulifunga mabao mengi na tulipata nafasi nyingi mbele ya goli. Hii ni moja ya nguvu zetu, lakini tunapaswa kuwa na umakini zaidi katika kumalizia na kujaribu kufunga mabao zaidi, kwa sababu tunataka kuwa bora katika kila kitu tunachofanya" Sead Ramovic #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·482 Views
  • 𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒

    "Tunahitaji kujaribu kucheza kati ya mistari. Tunapaswa kucheza katika nafasi ndogo nyuma ya safu ya ulinzi. Tunahitaji kuwasambaza ili tuweze kupata nafasi kati ya mistari. Kwa ujumla, itakuwa mechi ngumu tena, lakini kama ninavyosema kila wakati, sisi ni timu bora zaidi nchini Tanzania. Tumeshinda taji mara tatu, na tunataka kushinda tena" Sead Ramovic

    #timuyawananchi
    #daimambelenyumamwiko
    𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒💬 "Tunahitaji kujaribu kucheza kati ya mistari. Tunapaswa kucheza katika nafasi ndogo nyuma ya safu ya ulinzi. Tunahitaji kuwasambaza ili tuweze kupata nafasi kati ya mistari. Kwa ujumla, itakuwa mechi ngumu tena, lakini kama ninavyosema kila wakati, sisi ni timu bora zaidi nchini Tanzania. Tumeshinda taji mara tatu, na tunataka kushinda tena" Sead Ramovic #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·490 Views
  • 𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒

    "Kesho tutakabiliana na timu ambayo imepata wachezaji wapya wengi. Pia Kocha wao ana mtindo wake wa kucheza, na itakuwa mechi ngumu kwa sababu hatujui jinsi wanavyocheza na wachezaji wapya wote kwenye timu. Lakini huenda, kama tulivyokabiliana na wapinzani wa mwisho, watacheza kwa kujilinda zaidi. Hiyo inamaanisha tunapaswa kutafuta nafasi na mianya ili tuweze kupata matokeo" Sead Ramovic

    #timuyawananchi
    #daimambelenyumamwiko
    𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒💬 "Kesho tutakabiliana na timu ambayo imepata wachezaji wapya wengi. Pia Kocha wao ana mtindo wake wa kucheza, na itakuwa mechi ngumu kwa sababu hatujui jinsi wanavyocheza na wachezaji wapya wote kwenye timu. Lakini huenda, kama tulivyokabiliana na wapinzani wa mwisho, watacheza kwa kujilinda zaidi. Hiyo inamaanisha tunapaswa kutafuta nafasi na mianya ili tuweze kupata matokeo" Sead Ramovic #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·416 Views
  • #PART9

    Baada ya miaka mitatu ya utulivu, ghafla 2006 Jenerali Laurent Nkunda, aliasi jeshi kwa madai serikali imeshindwa kutekeleza Mkataba wa Amani wa SunCity. Ikumbukwe kabla ya kujiunga na Jeshi, alikua mpiganaji wa RCD - Goma, kundi lililoungwa mkono na Rwanda. Baada ya mkataba wa Suncity waasi wote waliingizwa jeshini akiwemo Nkunda.

    Lakini Juni 29, 2006, Nkunda akaasi jeshi na kuunda kundi la Congrès National pour la Défense du Peuple (CNDP). Madai yake:
    - Askari wa vikundi vya waasi walioingizwa jeshini hawakupewa vyeo.
    - Serikali ya Congo kushindwa kuwatanbua Watutsi (Banyamulenge) waishio mashariki mwa nchi hiyo kama raia wa Congo.
    - Serikali ya Congo kushindwa kuwakamata wanamgambo wa kihutu wa FDLR (Intarahanwe) waliojificha Congo baada ya kufanya mauaji ya kimbari Rwanda 1994.

    Nkunda akasema lengo la kuanzisha kundi la waasi la CNDP ni kupigania haki za Watutsi waishio mashariki mwa Congo (Banyamulenge) na kukabiliana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR. Nkunda akaungwa mkono na Rwanda na Uganda, akapewa silaha, vita ikaanza upyaaaaa (tamka kwa sauti ya mbunge Bwege).

    CNDP ikaua raia wengi wenye asili ya Kihutu ikiwatumu kuwa wafuasi wa FDLR. Serikali ya Burundi ikiongozwa na Piere Nkurunzinza (Mhutu) ikaingiza jeshi Congo kupambana na CNDP ili kulinda raia wake waliokua Congo. Kwa miaka mitatu kukawa na mapigano makali sana mashariki mwa Congo.

    January 2009 Waasi wa CNDP wakazidiwa. Laurent Nkunda akakimbilia Rwanda. Alipofika akakamatwa na kuwekwa kizuizini. Mpaka leo, bado anashikiliwa bila kufikishwa mahakamani. Jenerali Bosco Ntaganda, Mtutsi (Banyamulenge) wa Kivu akateuliwa kuongoza CNDP. Akafanya vitendo vingi vya kikatili kwa raia kuliko mtangulizi wake, kama ubakaji, mauaji ya halaiki, na kutumikisha watoto jeshini.

    Machi 23, 2009 serikali ya Congo na CNDP wakasaini Mkataba wa Amani, ulioitwa "March 23 Agreement" wenye masharti yafuatayo:
    - Kusitisha mapigano kwa pande zote.
    - Kuingiza askari wa CNDP kwenye jeshi la Congo.
    - Kutowashtaki askari wa CNDP kwa makosa waliyofanya wakati wa vita.
    - Wananchi wa Kivu wanufaike na rasilimali zao
    - Kulinda haki za binadamu Kivu
    (Malisa GJ)

    #PART9 Baada ya miaka mitatu ya utulivu, ghafla 2006 Jenerali Laurent Nkunda, aliasi jeshi kwa madai serikali imeshindwa kutekeleza Mkataba wa Amani wa SunCity. Ikumbukwe kabla ya kujiunga na Jeshi, alikua mpiganaji wa RCD - Goma, kundi lililoungwa mkono na Rwanda. Baada ya mkataba wa Suncity waasi wote waliingizwa jeshini akiwemo Nkunda. Lakini Juni 29, 2006, Nkunda akaasi jeshi na kuunda kundi la Congrès National pour la Défense du Peuple (CNDP). Madai yake: - Askari wa vikundi vya waasi walioingizwa jeshini hawakupewa vyeo. - Serikali ya Congo kushindwa kuwatanbua Watutsi (Banyamulenge) waishio mashariki mwa nchi hiyo kama raia wa Congo. - Serikali ya Congo kushindwa kuwakamata wanamgambo wa kihutu wa FDLR (Intarahanwe) waliojificha Congo baada ya kufanya mauaji ya kimbari Rwanda 1994. Nkunda akasema lengo la kuanzisha kundi la waasi la CNDP ni kupigania haki za Watutsi waishio mashariki mwa Congo (Banyamulenge) na kukabiliana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR. Nkunda akaungwa mkono na Rwanda na Uganda, akapewa silaha, vita ikaanza upyaaaaa (tamka kwa sauti ya mbunge Bwege). CNDP ikaua raia wengi wenye asili ya Kihutu ikiwatumu kuwa wafuasi wa FDLR. Serikali ya Burundi ikiongozwa na Piere Nkurunzinza (Mhutu) ikaingiza jeshi Congo kupambana na CNDP ili kulinda raia wake waliokua Congo. Kwa miaka mitatu kukawa na mapigano makali sana mashariki mwa Congo. January 2009 Waasi wa CNDP wakazidiwa. Laurent Nkunda akakimbilia Rwanda. Alipofika akakamatwa na kuwekwa kizuizini. Mpaka leo, bado anashikiliwa bila kufikishwa mahakamani. Jenerali Bosco Ntaganda, Mtutsi (Banyamulenge) wa Kivu akateuliwa kuongoza CNDP. Akafanya vitendo vingi vya kikatili kwa raia kuliko mtangulizi wake, kama ubakaji, mauaji ya halaiki, na kutumikisha watoto jeshini. Machi 23, 2009 serikali ya Congo na CNDP wakasaini Mkataba wa Amani, ulioitwa "March 23 Agreement" wenye masharti yafuatayo: - Kusitisha mapigano kwa pande zote. - Kuingiza askari wa CNDP kwenye jeshi la Congo. - Kutowashtaki askari wa CNDP kwa makosa waliyofanya wakati wa vita. - Wananchi wa Kivu wanufaike na rasilimali zao - Kulinda haki za binadamu Kivu (Malisa GJ)
    0 Comments ·0 Shares ·470 Views
  • #PART7

    Baada ya kundi la RCD kuvunjika, yalizaliwa makundi mawili ambayo ni RCD Goma (liliungwa mkono na Rwanda) na RCD Kisangani (likiungwa mkono na Uganda). Aliyekua Kiongozi wa RCD Ernest Wamba Dia Wamba akaamua kukaa pembeni baada ya kugundua wanatumika kupigana kwa maslahi ya watu wengine.

    Kwahiyo makundi haya yakapata viongozi wapya. RCD-Goma ikaongozwa na Kanali Emile Ilunga na RCD-Kisangani, ikaongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi. Ikumbukwe kabla kundi la RCD halijavunjika, lilikuwa limeshikilia maeneo mengi ya migodi huko Goma, Bukavu, na Katanga. Sasa baada ya kuvunjika, ukatokea mgogoro wa kugawana maeneo. Mgodi upi uende RCD Goma na upi uende RCD Kisangani.

    Kwa hiyo wakaanza kupigana tena wao kwa wao. Ikapigwa vita moja kali sana pale Kisangani, ikabatizwa jina la ‘Six Day War’ maana ilipiganwa kwa siku sita. RCD-Goma, ikawatandika vibaya sana RCD-Kisangani. Tar.10 June 2000 RCD Kisangani ikaachia migodi yote na kukimbia. RCD-Goma wakataka RCD-Kisangani wabadili jina lao maana mji wa Kisangani haukuwa chini yao tena. Hatimaye, RCD-Kisangani wakabadili na kujiita RCD-ML, yaani Rally for Congolese Democracy - Liberation Movement.

    RCD - ML walikimbilia kwenye milima Mikeno karibu na hifadhi ya Virunga kujipanga upya. RCD-Goma wakaendeleza mapigano kuelekea Kinshasa. Lakini kufika Bukavu wakakumbana na upinzani kutoka wanamgambo wa Maï-Maï waliokua wamepewa silaha na serikali za majimbo kupigana na askari yoyote mgeni kwenye ardhi yao.

    Maï-Maï waliongozwa na Kanali Musa Sindi upande wa Kivu Kusini na Sheikh Ntabo Ntaberi kwa Kivu Kaskazini. Kwa hiyo safari ya RCD Goma kwenda Kinshasa kumng’oa Laurent Kabila ikakutana na kizuizi cha Maï-Maï. Wakachapana sana. Watu zaidi ya 1,000 wakapoteza maisha.

    Kwahiyo vita ya kumng'oa Laurent Kabila ikawa ngumu maana vikundi vingi vya waasi vilianza kupigana vyenyewe kwa vyenyewe. Hali hiyo ilifanya vita kuwa ngumu zaidi, maana watu walipigana bila mpangilio. Risasi zikafyatuliwa hovyo hovyo na wananchi wengi wakapoteza maisha.
    (Malisa GJ)

    #PART7 Baada ya kundi la RCD kuvunjika, yalizaliwa makundi mawili ambayo ni RCD Goma (liliungwa mkono na Rwanda) na RCD Kisangani (likiungwa mkono na Uganda). Aliyekua Kiongozi wa RCD Ernest Wamba Dia Wamba akaamua kukaa pembeni baada ya kugundua wanatumika kupigana kwa maslahi ya watu wengine. Kwahiyo makundi haya yakapata viongozi wapya. RCD-Goma ikaongozwa na Kanali Emile Ilunga na RCD-Kisangani, ikaongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi. Ikumbukwe kabla kundi la RCD halijavunjika, lilikuwa limeshikilia maeneo mengi ya migodi huko Goma, Bukavu, na Katanga. Sasa baada ya kuvunjika, ukatokea mgogoro wa kugawana maeneo. Mgodi upi uende RCD Goma na upi uende RCD Kisangani. Kwa hiyo wakaanza kupigana tena wao kwa wao. Ikapigwa vita moja kali sana pale Kisangani, ikabatizwa jina la ‘Six Day War’ maana ilipiganwa kwa siku sita. RCD-Goma, ikawatandika vibaya sana RCD-Kisangani. Tar.10 June 2000 RCD Kisangani ikaachia migodi yote na kukimbia. RCD-Goma wakataka RCD-Kisangani wabadili jina lao maana mji wa Kisangani haukuwa chini yao tena. Hatimaye, RCD-Kisangani wakabadili na kujiita RCD-ML, yaani Rally for Congolese Democracy - Liberation Movement. RCD - ML walikimbilia kwenye milima Mikeno karibu na hifadhi ya Virunga kujipanga upya. RCD-Goma wakaendeleza mapigano kuelekea Kinshasa. Lakini kufika Bukavu wakakumbana na upinzani kutoka wanamgambo wa Maï-Maï waliokua wamepewa silaha na serikali za majimbo kupigana na askari yoyote mgeni kwenye ardhi yao. Maï-Maï waliongozwa na Kanali Musa Sindi upande wa Kivu Kusini na Sheikh Ntabo Ntaberi kwa Kivu Kaskazini. Kwa hiyo safari ya RCD Goma kwenda Kinshasa kumng’oa Laurent Kabila ikakutana na kizuizi cha Maï-Maï. Wakachapana sana. Watu zaidi ya 1,000 wakapoteza maisha. Kwahiyo vita ya kumng'oa Laurent Kabila ikawa ngumu maana vikundi vingi vya waasi vilianza kupigana vyenyewe kwa vyenyewe. Hali hiyo ilifanya vita kuwa ngumu zaidi, maana watu walipigana bila mpangilio. Risasi zikafyatuliwa hovyo hovyo na wananchi wengi wakapoteza maisha. (Malisa GJ)
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·653 Views
  • Kazi ya Bando la Wananchi wa Kenya
    Kazi ya Bando la Wananchi wa Kenya 🇰🇪 😳
    Wow
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·368 Views
More Results