“…kila mara alikuwa akiniomba pesa, nampa… Akiniomba tena, nampa… Nilipomwambia ya kwamba sitaki tena uhusiano wa kifedha kati yetu, tuendelee na uhusiano kama ndugu, ndipo masahibu hayo yalinikuta…” - Paul Pogba akimzungumzia kaka yake, Mathias Pogba (pichani, mwenye fulana nyeupe)…
Kesi ya ulaghai ya Paul Pogba, imefungiliwa jana huko Mjini Paris Nchini Ufaransa. Katika kesi hiyo, Watu sita (6) wamefikishwa Mahakamani wakituhumiwa kwa ulaghai, kujaribu kupora Euro milioni (18) ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni (50) za Tanzania na kumshikilia Mchezaji huyo wa Timu ya Taifa ya Ufaransa huku wakiwa na silaha (Bunduki).
Kesi hiyo katika Mahakama ya jinai ya Paris, imewashangaza wengi kwa sababu Watuhumiwa ni Marafiki wa karibu wa Paul Pogba, waliokulia wote sehemu moja, Mitaa ya Roissy-en-Brie, Kaskazini mwa Jiji la Paris, lakini kubwa zaidi, wakishirikiana na Kaka wa Paul Pogba, Mathias Pogba ambaye ni mdogo wake.
Mmoja wa watuhumiwa hao, aliiambia Mahakama kuwa “alichukizwa kuona Paul Pogba, anawasahau marafiki zake wa ‘kitaa’ na kuwaacha masikini baada ya kupata mafanikio katika soka…”
Paul Pogba mwenyewe, ambaye wakati wa tukio alikuwa katika mafanikio makubwa Manchester United huku akijiandaa kuhamia Juventus ya Italia, hakuwepo Mahakamani hapo hiyo jana ambapo aliwakilishwa na Mawakili wake watatu (3): Wakili Pierre-Jean Douvier, Wakili Alexia Alfonsi na Wakili Carine Piccio.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa hadi Disemba 3, 2024, huku Watuhumiwa wote wakijiandaa kutumikia kifungo kati ya miaka saba (7) na miaka kumi (10) Jela endapo watakutwa na hatia.
“…kila mara alikuwa akiniomba pesa, nampa… Akiniomba tena, nampa… Nilipomwambia ya kwamba sitaki tena uhusiano wa kifedha kati yetu, tuendelee na uhusiano kama ndugu, ndipo masahibu hayo yalinikuta…” - Paul Pogba akimzungumzia kaka yake, Mathias Pogba (pichani, mwenye fulana nyeupe)…
Kesi ya ulaghai ya Paul Pogba, imefungiliwa jana huko Mjini Paris Nchini Ufaransa. Katika kesi hiyo, Watu sita (6) wamefikishwa Mahakamani wakituhumiwa kwa ulaghai, kujaribu kupora Euro milioni (18) ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni (50) za Tanzania ๐น๐ฟ na kumshikilia Mchezaji huyo wa Timu ya Taifa ya Ufaransa ๐ซ๐ท huku wakiwa na silaha (Bunduki).