• Mvua zafichua makaburi ya pamoja yenye miili kadhaa Uvira, Sud-Kivu.

    Mvua kubwa zilizonyesha katika Mji wa Uvira, Mkoani Sud-Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimesababisha kugunduliwa kwa angalau makaburi matatu ya pamoja yaliyokuwa yamefukiwa kwa siri.

    Kaburi la kwanza liligunduliwa karibu na ofisi ya Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwenye barabara ya Kavinvira, ambapo miili takriban 35 ilipatikana. Mvua hizo zilifichua baadhi ya maiti zilizokuwa zimefunikwa kwa udongo, hali iliyosababisha harufu kali iliyowatahadharisha wakazi wa eneo hilo.

    Mbali na eneo hilo, kaburi lingine la pamoja limeripotiwa kupatikana katika kitongoji cha Kilomoni ndani ya Mji huo huo.

    Aidha, katika makaburi ya Mji, Wanaharakati wa kiraia wanasema pia kuna uwezekano wa kuwepo kwa miili kadhaa zaidi. Takriban kilomita 30 kutoka hapo, katika Mji wa Sange, kaburi jingine linadaiwa kuwa na takriban waathiriwa kumi.

    Katika muktadha wa vita vinavyoendelea mashariki mwa nchi, baadhi ya vyanzo vya ndani vinayahusisha makaburi hayo na Waasi wa M23, wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, tuhuma ambazo zimekuwa zikijirudia mara kwa mara katika mgogoro huo. Hata hivyo, wengine wanawalaumu wanamgambo wa kujilinda wanaojulikana kama Wazalendo.

    Afisa mmoja wa ngazi ya juu ndani ya M23 alikiri kupitia chapisho kwamba baadhi ya makaburi ya pamoja yaliyopo Mikoa ya Sud-Kivu na Nord-Kivu yanahusishwa na operesheni za Afisa mmoja wa Waasi.

    Wakazi tayari wamewasiliana na mamlaka za Mkoa kuhusu tukio hilo. Timu maalum zimefika katika maeneo husika ili kuyahifadhi na kufunika miili, ingawa hadi sasa hakuna uchimbaji rasmi uliofanyika.

    Hali hiyo imeibua wasiwasi mkubwa kuhusu uhifadhi wa ushahidi muhimu.

    Mashirika kadhaa yanataka kufanyika kwa uchimbaji wa miili kwa utaratibu rasmi, kufunguliwa kwa uchunguzi wa kisheria usioegemea upande wowote, pamoja na kutambuliwa kwa waathiriwa. Pia wanasisitiza umuhimu wa mazishi ya heshima na kuwafikisha mahakamani wanaodaiwa kuhusika.

    Wito huo unaangazia umuhimu wa haki ya mpito na mapambano dhidi ya utamaduni wa kutoadhibiwa katika eneo hilo linalokumbwa na mzozo wa muda mrefu.
    Mvua zafichua makaburi ya pamoja yenye miili kadhaa Uvira, Sud-Kivu. Mvua kubwa zilizonyesha katika Mji wa Uvira, Mkoani Sud-Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimesababisha kugunduliwa kwa angalau makaburi matatu ya pamoja yaliyokuwa yamefukiwa kwa siri. Kaburi la kwanza liligunduliwa karibu na ofisi ya Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwenye barabara ya Kavinvira, ambapo miili takriban 35 ilipatikana. Mvua hizo zilifichua baadhi ya maiti zilizokuwa zimefunikwa kwa udongo, hali iliyosababisha harufu kali iliyowatahadharisha wakazi wa eneo hilo. Mbali na eneo hilo, kaburi lingine la pamoja limeripotiwa kupatikana katika kitongoji cha Kilomoni ndani ya Mji huo huo. Aidha, katika makaburi ya Mji, Wanaharakati wa kiraia wanasema pia kuna uwezekano wa kuwepo kwa miili kadhaa zaidi. Takriban kilomita 30 kutoka hapo, katika Mji wa Sange, kaburi jingine linadaiwa kuwa na takriban waathiriwa kumi. Katika muktadha wa vita vinavyoendelea mashariki mwa nchi, baadhi ya vyanzo vya ndani vinayahusisha makaburi hayo na Waasi wa M23, wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, tuhuma ambazo zimekuwa zikijirudia mara kwa mara katika mgogoro huo. Hata hivyo, wengine wanawalaumu wanamgambo wa kujilinda wanaojulikana kama Wazalendo. Afisa mmoja wa ngazi ya juu ndani ya M23 alikiri kupitia chapisho kwamba baadhi ya makaburi ya pamoja yaliyopo Mikoa ya Sud-Kivu na Nord-Kivu yanahusishwa na operesheni za Afisa mmoja wa Waasi. Wakazi tayari wamewasiliana na mamlaka za Mkoa kuhusu tukio hilo. Timu maalum zimefika katika maeneo husika ili kuyahifadhi na kufunika miili, ingawa hadi sasa hakuna uchimbaji rasmi uliofanyika. Hali hiyo imeibua wasiwasi mkubwa kuhusu uhifadhi wa ushahidi muhimu. Mashirika kadhaa yanataka kufanyika kwa uchimbaji wa miili kwa utaratibu rasmi, kufunguliwa kwa uchunguzi wa kisheria usioegemea upande wowote, pamoja na kutambuliwa kwa waathiriwa. Pia wanasisitiza umuhimu wa mazishi ya heshima na kuwafikisha mahakamani wanaodaiwa kuhusika. Wito huo unaangazia umuhimu wa haki ya mpito na mapambano dhidi ya utamaduni wa kutoadhibiwa katika eneo hilo linalokumbwa na mzozo wa muda mrefu.
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 219 Views
  • Washauri wamzuia Trump kushambulia Iran, lakini Lindsey Graham amsukuma aanzishe mashambulizi.

    Mvutano wa kisiasa umeibuka ndani ya kambi ya Rais wa Marekani, kufuatia taarifa kwamba baadhi ya Washauri wake wa karibu wamemtaka asichukue hatua ya kijeshi dhidi ya Iran. Hata hivyo, sauti kinzani imejitokeza kutoka kwa Seneta wa chama cha Republican, Lindsey Graham, ambaye amemtaka Rais huyo kupuuza ushauri huo na kuidhinisha mashambulizi.

    Kwa mujibu wa ripoti ya Axios, mjadala mkali umeendelea ndani ya duru za Ikulu ya White House kuhusu hatma ya sera ya Marekani dhidi ya Iran, wakati hali ya usalama Mashariki ya Kati ikiendelea kuwa tete.

    Taarifa zinaeleza kuwa baadhi ya Washauri wa karibu wa Rais Donald Trump wana hofu kuwa shambulio lolote la kijeshi dhidi ya Iran linaweza kusababisha mzozo mpana wa kikanda, na hata kuvuta mataifa mengine kuingia vitani. Wanaonya kuwa hatua hiyo inaweza kuathiri maslahi ya Marekani kimataifa, pamoja na uchumi wa dunia.

    Kwa mtazamo wao, njia ya diplomasia na vikwazo vya kiuchumi bado zinaweza kuwa mbinu mbadala ya kushinikiza Tehran bila kuingia kwenye mapambano ya wazi ya kijeshi.

    Kinyume chake, Seneta Lindsey Graham amesisitiza kuwa Marekani inapaswa kuonyesha nguvu na uthabiti dhidi ya Iran. Amedai kuwa kusita kuchukua hatua kunaweza kutafsiriwa kama udhaifu, na kuipa Iran nafasi ya kuendelea na kile anachokiona kama vitendo vya uchokozi katika ukanda huo.

    Kauli yake inaongeza presha ya kisiasa kwa Rais Trump, hasa kutoka kwa makundi ya wahafidhina wanaotaka msimamo mkali dhidi ya Tehran.

    Huku mjadala huo ukiendelea, macho ya jumuiya ya kimataifa yameelekezwa Washington. Uamuzi wowote wa Marekani unaweza kubadilisha mwelekeo wa siasa za Mashariki ya Kati na kuathiri usalama wa kimataifa.

    Kwa sasa, haijafahamika ni msimamo gani utachukuliwa rasmi na Ikulu, lakini kinachoonekana wazi ni kwamba mgawanyiko wa kimtazamo ndani ya uongozi wa Marekani umeibuka wazi katika suala la Iran.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Washauri wamzuia Trump kushambulia Iran, lakini Lindsey Graham amsukuma aanzishe mashambulizi. Mvutano wa kisiasa umeibuka ndani ya kambi ya Rais wa Marekani, kufuatia taarifa kwamba baadhi ya Washauri wake wa karibu wamemtaka asichukue hatua ya kijeshi dhidi ya Iran. Hata hivyo, sauti kinzani imejitokeza kutoka kwa Seneta wa chama cha Republican, Lindsey Graham, ambaye amemtaka Rais huyo kupuuza ushauri huo na kuidhinisha mashambulizi. Kwa mujibu wa ripoti ya Axios, mjadala mkali umeendelea ndani ya duru za Ikulu ya White House kuhusu hatma ya sera ya Marekani dhidi ya Iran, wakati hali ya usalama Mashariki ya Kati ikiendelea kuwa tete. Taarifa zinaeleza kuwa baadhi ya Washauri wa karibu wa Rais Donald Trump wana hofu kuwa shambulio lolote la kijeshi dhidi ya Iran linaweza kusababisha mzozo mpana wa kikanda, na hata kuvuta mataifa mengine kuingia vitani. Wanaonya kuwa hatua hiyo inaweza kuathiri maslahi ya Marekani kimataifa, pamoja na uchumi wa dunia. Kwa mtazamo wao, njia ya diplomasia na vikwazo vya kiuchumi bado zinaweza kuwa mbinu mbadala ya kushinikiza Tehran bila kuingia kwenye mapambano ya wazi ya kijeshi. Kinyume chake, Seneta Lindsey Graham amesisitiza kuwa Marekani inapaswa kuonyesha nguvu na uthabiti dhidi ya Iran. Amedai kuwa kusita kuchukua hatua kunaweza kutafsiriwa kama udhaifu, na kuipa Iran nafasi ya kuendelea na kile anachokiona kama vitendo vya uchokozi katika ukanda huo. Kauli yake inaongeza presha ya kisiasa kwa Rais Trump, hasa kutoka kwa makundi ya wahafidhina wanaotaka msimamo mkali dhidi ya Tehran. Huku mjadala huo ukiendelea, macho ya jumuiya ya kimataifa yameelekezwa Washington. Uamuzi wowote wa Marekani unaweza kubadilisha mwelekeo wa siasa za Mashariki ya Kati na kuathiri usalama wa kimataifa. Kwa sasa, haijafahamika ni msimamo gani utachukuliwa rasmi na Ikulu, lakini kinachoonekana wazi ni kwamba mgawanyiko wa kimtazamo ndani ya uongozi wa Marekani umeibuka wazi katika suala la Iran. Toa maoni yako #Habari
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 478 Views
  • Gianluca Prestianni ajibu baada ya kudaiwa kumtukana Vinicius Jr.

    Gianluca Prestianni ametoa taarifa rasmi baada ya kudaiwa kumkosea heshima Vinicius Jr. Prestianni ameeleza wazi: “Nataka kufafanua kwamba, sikuwahi kumtukana Mchezaji wa Real Madrid wowote ule, Vinicius Jr, kwa bahati mbaya alikosea kuelewa yale aliyoamini akinisikia nikisema.”

    Aidha, Mchezaji huyo wa Argentina ameongeza: “Sijawahi kumchukia Mtu kwa rangi na ninajuta kwa vitisho nilivyopokea kutoka kwa Wachezaji wa Real Madrid.”

    Taarifa hii inakuja baada ya kashfa ya madai ya ubaguzi wa rangi iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, na Prestianni ameonekana kujaribu kuondoa kashfa hiyo kwa uwazi wake.

    Hii ni hatua muhimu kwa Mchezaji huyo ili kulinda heshima yake na kuweka wazi msimamo wake dhidi ya ubaguzi wa rangi.

    Toa maoni yako
    #Sports
    #Habari
    Gianluca Prestianni ajibu baada ya kudaiwa kumtukana Vinicius Jr. Gianluca Prestianni ametoa taarifa rasmi baada ya kudaiwa kumkosea heshima Vinicius Jr. Prestianni ameeleza wazi: “Nataka kufafanua kwamba, sikuwahi kumtukana Mchezaji wa Real Madrid wowote ule, Vinicius Jr, kwa bahati mbaya alikosea kuelewa yale aliyoamini akinisikia nikisema.” Aidha, Mchezaji huyo wa Argentina ameongeza: “Sijawahi kumchukia Mtu kwa rangi na ninajuta kwa vitisho nilivyopokea kutoka kwa Wachezaji wa Real Madrid.” Taarifa hii inakuja baada ya kashfa ya madai ya ubaguzi wa rangi iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, na Prestianni ameonekana kujaribu kuondoa kashfa hiyo kwa uwazi wake. Hii ni hatua muhimu kwa Mchezaji huyo ili kulinda heshima yake na kuweka wazi msimamo wake dhidi ya ubaguzi wa rangi. Toa maoni yako #Sports #Habari
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 154 Views
  • UEFA kufungua uchunguzi wa tuhuma za ubaguzi wa rangi katika kesi ya Vinicius na Prestianni.

    UEFA imetangaza kuwa iko tayari kufungua uchunguzi rasmi kuhusiana na tuhuma za ubaguzi wa rangi zinazomhusisha Mchezaji wa Real Madrid, Vinícius Júnior, na wa Benfica, Gianluca Prestianni.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na kituo cha redio cha Hispania, Cadena SER kupitia kipindi cha michezo cha El Larguero, uchunguzi huo unatarajiwa kuanza kwa kuhoji Wachezaji wote waliokuwepo Uwanjani wakati wa tukio hilo.

    Chanzo hicho kimenukuliwa kikisema, “Kesi itafunguliwa kwa kuwaita Wachezaji wote ili waripoti mambo yote waliyosikia na kuyaona Uwanjani.”

    Hata hivyo, taarifa hiyo imeonya kuwa mchakato huo unaweza kuwa mgumu iwapo ushahidi wa moja kwa moja hautapatikana. Chanzo hicho kimeongeza kwa kusema, “Itakuwa vigumu kutoa uamuzi ikiwa tusi la kibaguzi na matusi ya moja kwa moja hayawezi kuthibitishwa.”

    Kwa mujibu wa taratibu za kinidhamu za UEFA, uchunguzi wa aina hii hulenga kukusanya ushahidi wa sauti, picha, pamoja na ushuhuda wa mashahidi ili kubaini iwapo kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni za maadili na nidhamu za mashindano ya Ulaya.

    Tukio hilo limeibua mjadala mpana katika ulimwengu wa soka, hasa katika kipindi ambacho juhudi za kupambana na ubaguzi wa rangi Viwanjani zimekuwa zikipewa kipaumbele katika mashindano ya kimataifa.

    Uamuzi wa mwisho wa UEFA utategemea uzito wa ushahidi utakao wasilishwa katika uchunguzi huo.

    Toa maoni yako
    #Sports
    #Habari
    UEFA kufungua uchunguzi wa tuhuma za ubaguzi wa rangi katika kesi ya Vinicius na Prestianni. UEFA imetangaza kuwa iko tayari kufungua uchunguzi rasmi kuhusiana na tuhuma za ubaguzi wa rangi zinazomhusisha Mchezaji wa Real Madrid, Vinícius Júnior, na wa Benfica, Gianluca Prestianni. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na kituo cha redio cha Hispania, Cadena SER kupitia kipindi cha michezo cha El Larguero, uchunguzi huo unatarajiwa kuanza kwa kuhoji Wachezaji wote waliokuwepo Uwanjani wakati wa tukio hilo. Chanzo hicho kimenukuliwa kikisema, “Kesi itafunguliwa kwa kuwaita Wachezaji wote ili waripoti mambo yote waliyosikia na kuyaona Uwanjani.” Hata hivyo, taarifa hiyo imeonya kuwa mchakato huo unaweza kuwa mgumu iwapo ushahidi wa moja kwa moja hautapatikana. Chanzo hicho kimeongeza kwa kusema, “Itakuwa vigumu kutoa uamuzi ikiwa tusi la kibaguzi na matusi ya moja kwa moja hayawezi kuthibitishwa.” Kwa mujibu wa taratibu za kinidhamu za UEFA, uchunguzi wa aina hii hulenga kukusanya ushahidi wa sauti, picha, pamoja na ushuhuda wa mashahidi ili kubaini iwapo kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni za maadili na nidhamu za mashindano ya Ulaya. Tukio hilo limeibua mjadala mpana katika ulimwengu wa soka, hasa katika kipindi ambacho juhudi za kupambana na ubaguzi wa rangi Viwanjani zimekuwa zikipewa kipaumbele katika mashindano ya kimataifa. Uamuzi wa mwisho wa UEFA utategemea uzito wa ushahidi utakao wasilishwa katika uchunguzi huo. Toa maoni yako #Sports #Habari
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 212 Views
  • Afghanistan yaipongeza Iran kwa “ushindi” wa vita vya siku 12.

    Msemaji wa serikali ya Afghanistan, Zabihullah Mujahid, amesema kuwa Iran iliibuka mshindi katika mapigano ya hivi karibuni yaliyodumu kwa siku 12, akieleza kuwa taifa hilo lina uwezo wa kujilinda dhidi ya tishio lolote la kijeshi.

    Akizungumza kuhusu mvutano huo, Mujahid alinukuliwa akisema kwamba, “Iran ilitoka kidedea katika vita vya hivi karibuni vilivyodumu kwa siku 12.”

    Alisisitiza zaidi uwezo wa kijeshi wa Tehran kwa kueleza kuwa, “Ina uwezo wa kushinda na kujilinda dhidi ya uvamizi wowote.”

    Kauli hiyo inaonekana kuashiria msimamo wa wazi wa Afghanistan kuhusu nafasi ya Iran katika mzozo huo, hasa katika kipindi ambacho hali ya usalama katika eneo la Mashariki ya Kati inaendelea kuwa tete.

    Katika hatua nyingine, Mujahid alieleza mshikamano wa watu wa Afghanistan iwapo Iran itakabiliwa na shambulio jingine.

    Alisema wazi kuwa, “Ikiwa Iran itashambuliwa, watu wa Afghanistan watasimama kwa umoja na kutoa msaada kamili kwa ndugu zao Wairani.”

    Tamko hilo linaashiria uhusiano wa karibu wa kisiasa na kidiplomasia kati ya Kabul na Tehran, huku likionyesha uwezekano wa ushirikiano wa karibu zaidi katika masuala ya usalama wa kikanda.

    Kauli ya Afghanistan inaweza kuongeza mjadala wa kimataifa kuhusu mizania ya nguvu katika eneo hilo, hasa ikizingatiwa mvutano unaoendelea kati ya Iran na mataifa yanayoihusisha na vitisho vya usalama.

    Wachambuzi wa siasa za kimataifa wanaona kuwa matamko ya aina hii yanaweza kuwa na athari kwa diplomasia ya kikanda, hasa katika kuunda miungano mipya au kuimarisha iliyopo.

    Kwa sasa, dunia inaendelea kufuatilia kwa karibu mwelekeo wa uhusiano kati ya Afghanistan na Iran, na jinsi yatakavyoathiri siasa za Mashariki ya Kati katika siku zijazo.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Afghanistan yaipongeza Iran kwa “ushindi” wa vita vya siku 12. Msemaji wa serikali ya Afghanistan, Zabihullah Mujahid, amesema kuwa Iran iliibuka mshindi katika mapigano ya hivi karibuni yaliyodumu kwa siku 12, akieleza kuwa taifa hilo lina uwezo wa kujilinda dhidi ya tishio lolote la kijeshi. Akizungumza kuhusu mvutano huo, Mujahid alinukuliwa akisema kwamba, “Iran ilitoka kidedea katika vita vya hivi karibuni vilivyodumu kwa siku 12.” Alisisitiza zaidi uwezo wa kijeshi wa Tehran kwa kueleza kuwa, “Ina uwezo wa kushinda na kujilinda dhidi ya uvamizi wowote.” Kauli hiyo inaonekana kuashiria msimamo wa wazi wa Afghanistan kuhusu nafasi ya Iran katika mzozo huo, hasa katika kipindi ambacho hali ya usalama katika eneo la Mashariki ya Kati inaendelea kuwa tete. Katika hatua nyingine, Mujahid alieleza mshikamano wa watu wa Afghanistan iwapo Iran itakabiliwa na shambulio jingine. Alisema wazi kuwa, “Ikiwa Iran itashambuliwa, watu wa Afghanistan watasimama kwa umoja na kutoa msaada kamili kwa ndugu zao Wairani.” Tamko hilo linaashiria uhusiano wa karibu wa kisiasa na kidiplomasia kati ya Kabul na Tehran, huku likionyesha uwezekano wa ushirikiano wa karibu zaidi katika masuala ya usalama wa kikanda. Kauli ya Afghanistan inaweza kuongeza mjadala wa kimataifa kuhusu mizania ya nguvu katika eneo hilo, hasa ikizingatiwa mvutano unaoendelea kati ya Iran na mataifa yanayoihusisha na vitisho vya usalama. Wachambuzi wa siasa za kimataifa wanaona kuwa matamko ya aina hii yanaweza kuwa na athari kwa diplomasia ya kikanda, hasa katika kuunda miungano mipya au kuimarisha iliyopo. Kwa sasa, dunia inaendelea kufuatilia kwa karibu mwelekeo wa uhusiano kati ya Afghanistan na Iran, na jinsi yatakavyoathiri siasa za Mashariki ya Kati katika siku zijazo. Toa maoni yako #Habari
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 303 Views
  • Serikali ya Kenya yachukua hatua kali dhidi ya tuhuma za Raia wa Urusi kusambaza video za faragha.

    Serikali ya Kenya imeibuka hadharani na kulaani vikali tuhuma zinazomhusu raia mmoja wa Urusi anayeshukiwa kurekodi na kusambaza video zenye maudhui ya faragha zikihusisha Wanawake wa Kenya bila ridhaa yao.

    Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa Jijini Nairobi, mamlaka za Kenya zimeeleza kuwa tukio hilo ni la kusikitisha na haliwezi kuvumiliwa katika jamii inayoheshimu utu na haki za binadamu.

    Katika tamko hilo, serikali imeeleza kuwa tukio hilo ni “kubwa na lisilokubalika”, ikisisitiza kuwa hatua zote muhimu zitachukuliwa ili ukweli ujulikane na haki itendeke. Aidha, imewahakikishia waathirika wanaodaiwa kuwa watapatiwa msaada stahiki wa kisheria na kisaikolojia.

    Vilevile, mamlaka hizo zimeweka bayana kuwa Wahusika wote watakaobainika kuhusika na kitendo hicho watawajibishwa kwa mujibu wa sheria. Serikali imeongeza kuwa haitasita kuchukua hatua kali dhidi ya yeyote anayekiuka faragha na heshima ya wananchi.

    Kashfa hiyo imezua hasira kubwa katika mitandao ya kijamii na miongoni mwa Wananchi, huku wengi wakitaka sheria kali zaidi zichukuliwe dhidi ya wanaosambaza maudhui ya faragha bila idhini. Tukio hili limeibua tena mjadala mpana kuhusu ulinzi wa maisha binafsi na mapambano dhidi ya usambazaji wa maudhui ya faragha bila ridhaa nchini Kenya.

    Mamlaka husika zimebainisha kuwa uchunguzi rasmi unaendelea, na matokeo yake yatatangazwa pindi yatakapokamilika.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Serikali ya Kenya yachukua hatua kali dhidi ya tuhuma za Raia wa Urusi kusambaza video za faragha. Serikali ya Kenya imeibuka hadharani na kulaani vikali tuhuma zinazomhusu raia mmoja wa Urusi anayeshukiwa kurekodi na kusambaza video zenye maudhui ya faragha zikihusisha Wanawake wa Kenya bila ridhaa yao. Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa Jijini Nairobi, mamlaka za Kenya zimeeleza kuwa tukio hilo ni la kusikitisha na haliwezi kuvumiliwa katika jamii inayoheshimu utu na haki za binadamu. Katika tamko hilo, serikali imeeleza kuwa tukio hilo ni “kubwa na lisilokubalika”, ikisisitiza kuwa hatua zote muhimu zitachukuliwa ili ukweli ujulikane na haki itendeke. Aidha, imewahakikishia waathirika wanaodaiwa kuwa watapatiwa msaada stahiki wa kisheria na kisaikolojia. Vilevile, mamlaka hizo zimeweka bayana kuwa Wahusika wote watakaobainika kuhusika na kitendo hicho watawajibishwa kwa mujibu wa sheria. Serikali imeongeza kuwa haitasita kuchukua hatua kali dhidi ya yeyote anayekiuka faragha na heshima ya wananchi. Kashfa hiyo imezua hasira kubwa katika mitandao ya kijamii na miongoni mwa Wananchi, huku wengi wakitaka sheria kali zaidi zichukuliwe dhidi ya wanaosambaza maudhui ya faragha bila idhini. Tukio hili limeibua tena mjadala mpana kuhusu ulinzi wa maisha binafsi na mapambano dhidi ya usambazaji wa maudhui ya faragha bila ridhaa nchini Kenya. Mamlaka husika zimebainisha kuwa uchunguzi rasmi unaendelea, na matokeo yake yatatangazwa pindi yatakapokamilika. Toa maoni yako #Habari
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 272 Views
  • Zambia Yawafukuza Zaidi ya Raia 80 wa Congo kwa tuhuma za kukaa kinyume cha sheria.

    Serikali ya Zambia imewafukuza zaidi ya Raia 80 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika operesheni maalum iliyolenga watu wanaodaiwa kuishi nchini humo bila vibali halali.

    Kwa mujibu wa mamlaka za Zambia, hatua hiyo ni sehemu ya zoezi pana la kukagua Wahamiaji wanaoshukiwa kuwa katika hali isiyo halali ndani ya mipaka ya taifa hilo. Vyanzo vya kiusalama vinaeleza kuwa operesheni hiyo ilifanyika baada ya uchunguzi wa kina kubaini kuwepo kwa idadi kubwa ya watu wasiokuwa na nyaraka sahihi.

    Afisa wa Zambia wamesema kuwa, "Zaidi ya watu 170 wa mataifa mbalimbali wanashukiwa kuwa katika hali isiyo halali nchini Zambia."

    Taarifa hiyo inaashiria kuwa si Raia wa Congo pekee waliolengwa katika msako huo, bali pia watu kutoka mataifa mengine ambao wanadaiwa kukiuka sheria za uhamiaji.

    Hatua ya kufukuzwa kwa Raia hao wa Congo inaelezwa kuwa ni utekelezaji wa sheria za uhamiaji za Zambia, ambazo zinataka Wageni wote kuwa na vibali halali vya kuishi au kufanya kazi nchini humo.

    Wachambuzi wa masuala ya kikanda wanasema kuwa operesheni za aina hii mara nyingi huibua mjadala kuhusu haki za Wahamiaji, hasa katika ukanda wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambako harakati za watu kuvuka mipaka ni jambo la kawaida kwa sababu za kiuchumi na kijamii.

    Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi kuhusu iwapo hatua hiyo itaathiri uhusiano wa kidiplomasia kati ya Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Serikali ya Zambia imeweka wazi kuwa itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kukaa nchini humo bila kufuata taratibu za kisheria.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Zambia Yawafukuza Zaidi ya Raia 80 wa Congo kwa tuhuma za kukaa kinyume cha sheria. Serikali ya Zambia imewafukuza zaidi ya Raia 80 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika operesheni maalum iliyolenga watu wanaodaiwa kuishi nchini humo bila vibali halali. Kwa mujibu wa mamlaka za Zambia, hatua hiyo ni sehemu ya zoezi pana la kukagua Wahamiaji wanaoshukiwa kuwa katika hali isiyo halali ndani ya mipaka ya taifa hilo. Vyanzo vya kiusalama vinaeleza kuwa operesheni hiyo ilifanyika baada ya uchunguzi wa kina kubaini kuwepo kwa idadi kubwa ya watu wasiokuwa na nyaraka sahihi. Afisa wa Zambia wamesema kuwa, "Zaidi ya watu 170 wa mataifa mbalimbali wanashukiwa kuwa katika hali isiyo halali nchini Zambia." Taarifa hiyo inaashiria kuwa si Raia wa Congo pekee waliolengwa katika msako huo, bali pia watu kutoka mataifa mengine ambao wanadaiwa kukiuka sheria za uhamiaji. Hatua ya kufukuzwa kwa Raia hao wa Congo inaelezwa kuwa ni utekelezaji wa sheria za uhamiaji za Zambia, ambazo zinataka Wageni wote kuwa na vibali halali vya kuishi au kufanya kazi nchini humo. Wachambuzi wa masuala ya kikanda wanasema kuwa operesheni za aina hii mara nyingi huibua mjadala kuhusu haki za Wahamiaji, hasa katika ukanda wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambako harakati za watu kuvuka mipaka ni jambo la kawaida kwa sababu za kiuchumi na kijamii. Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi kuhusu iwapo hatua hiyo itaathiri uhusiano wa kidiplomasia kati ya Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Serikali ya Zambia imeweka wazi kuwa itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kukaa nchini humo bila kufuata taratibu za kisheria. Toa maoni yako #Habari
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 183 Views
  • Denis Mukwege ataka “Mazungumzo ya Kitaifa” kutatua tatizo la uongozi DRC.

    Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Dkt. Denis Mukwege, amesema kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inahitaji haraka “Mazungumzo ya Kitaifa” ili kupata suluhisho la kudumu kwa changamoto zinazoikabili nchi hiyo, hususan katika eneo la uongozi.

    Akizungumza kuhusu hali ya sasa ya nchi yake, Dkt. Mukwege alieleza kuwa kiini cha matatizo mengi yanayoikumba Congo ni ukosefu wa uongozi bora.

    “Iwapo leo Congo inapitia mateso yote tunayoshuhudia, ni kwa sababu tu ya uwepo wa uongozi mbovu. Kama kungekuwa na uongozi mzuri, kwa kawaida Congo ingeweza kulinda raia wake na kusimamia ipasavyo rasilimali zake za madini ambazo kwa sasa zinavunwa na kila aina ya walafi wanaozunguka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.”

    Kauli hiyo imekuja wakati nchi hiyo ikiendelea kukabiliwa na changamoto za kiusalama, migogoro ya silaha katika maeneo ya mashariki, pamoja na lawama za muda mrefu kuhusu usimamizi wa rasilimali asilia.

    Kwa mujibu wa Dkt. Mukwege, suluhisho la kweli halitapatikana kwa hatua za juu juu, bali kupitia mchakato mpana wa kitaifa utakaowaleta pamoja wadau wote muhimu—serikali, vyama vya siasa, Asasi za kiraia na Wawakilishi wa wananchi.

    Anaamini kuwa kupitia jukwaa hilo, taifa linaweza kujadili kwa uwazi matatizo ya kiutawala, uwajibikaji wa Viongozi, pamoja na namna bora ya kusimamia utajiri mkubwa wa madini uliopo nchini humo.

    DRC ni miongoni mwa mataifa yenye utajiri mkubwa wa madini duniani, ikiwemo cobalt, dhahabu na coltan. Hata hivyo, kwa miaka mingi, rasilimali hizo zimehusishwa na migogoro, rushwa na uingiliaji wa maslahi ya ndani na nje ya nchi.

    Kauli ya Dkt. Mukwege inachukuliwa na Wachambuzi wengi kama wito wa mageuzi ya kina katika mifumo ya uongozi na uwajibikaji, ili kuhakikisha rasilimali za taifa zinawanufaisha Wananchi badala ya makundi machache yenye nguvu.

    Kwa sasa, macho ya wengi yanaelekezwa kuona iwapo wito huo wa “Mazungumzo ya Kitaifa” utapokelewa na mamlaka husika na kuwa mwanzo wa mabadiliko yanayohitajika nchini Congo.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Denis Mukwege ataka “Mazungumzo ya Kitaifa” kutatua tatizo la uongozi DRC. Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Dkt. Denis Mukwege, amesema kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inahitaji haraka “Mazungumzo ya Kitaifa” ili kupata suluhisho la kudumu kwa changamoto zinazoikabili nchi hiyo, hususan katika eneo la uongozi. Akizungumza kuhusu hali ya sasa ya nchi yake, Dkt. Mukwege alieleza kuwa kiini cha matatizo mengi yanayoikumba Congo ni ukosefu wa uongozi bora. “Iwapo leo Congo inapitia mateso yote tunayoshuhudia, ni kwa sababu tu ya uwepo wa uongozi mbovu. Kama kungekuwa na uongozi mzuri, kwa kawaida Congo ingeweza kulinda raia wake na kusimamia ipasavyo rasilimali zake za madini ambazo kwa sasa zinavunwa na kila aina ya walafi wanaozunguka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.” Kauli hiyo imekuja wakati nchi hiyo ikiendelea kukabiliwa na changamoto za kiusalama, migogoro ya silaha katika maeneo ya mashariki, pamoja na lawama za muda mrefu kuhusu usimamizi wa rasilimali asilia. Kwa mujibu wa Dkt. Mukwege, suluhisho la kweli halitapatikana kwa hatua za juu juu, bali kupitia mchakato mpana wa kitaifa utakaowaleta pamoja wadau wote muhimu—serikali, vyama vya siasa, Asasi za kiraia na Wawakilishi wa wananchi. Anaamini kuwa kupitia jukwaa hilo, taifa linaweza kujadili kwa uwazi matatizo ya kiutawala, uwajibikaji wa Viongozi, pamoja na namna bora ya kusimamia utajiri mkubwa wa madini uliopo nchini humo. DRC ni miongoni mwa mataifa yenye utajiri mkubwa wa madini duniani, ikiwemo cobalt, dhahabu na coltan. Hata hivyo, kwa miaka mingi, rasilimali hizo zimehusishwa na migogoro, rushwa na uingiliaji wa maslahi ya ndani na nje ya nchi. Kauli ya Dkt. Mukwege inachukuliwa na Wachambuzi wengi kama wito wa mageuzi ya kina katika mifumo ya uongozi na uwajibikaji, ili kuhakikisha rasilimali za taifa zinawanufaisha Wananchi badala ya makundi machache yenye nguvu. Kwa sasa, macho ya wengi yanaelekezwa kuona iwapo wito huo wa “Mazungumzo ya Kitaifa” utapokelewa na mamlaka husika na kuwa mwanzo wa mabadiliko yanayohitajika nchini Congo. Toa maoni yako #Habari
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 129 Views
  • Iran yafanya mazoezi ya kijeshi katika mlango wa Hormuz, njia muhimu ya mafuta Duniani.

    Serikali ya Iran imeendesha mazoezi ya kijeshi katika eneo la kimkakati la Strait of Hormuz, mojawapo ya njia muhimu zaidi za usafirishaji wa mafuta duniani.

    Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, mazoezi hayo yalihusisha vikosi vya majini, makombora ya masafa mbalimbali pamoja na ndege zisizo na rubani (drone). Hatua hiyo imekuja wakati kukiwa na mvutano wa kisiasa na kiusalama katika eneo la Mashariki ya Kati.

    Mlango wa Hormuz unaunganisha Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Oman, na ni njia ambayo sehemu kubwa ya mafuta ya dunia hupita kila siku. Inakadiriwa kuwa karibu theluthi moja ya mafuta yanayosafirishwa kwa njia ya bahari hupitia katika mkondo huo mwembamba lakini wenye umuhimu mkubwa kiuchumi.

    Afisa wa kijeshi wa Iran wamesema kuwa lengo la mazoezi hayo ni “kuimarisha uwezo wa kujilinda na kulinda mipaka ya majini ya taifa.” Aidha wameongeza kuwa “usalama wa eneo hili ni jukumu la mataifa ya ukanda huu, na si mataifa ya kigeni.”

    Hatua hiyo imeibua mjadala katika jumuiya ya kimataifa, hasa kwa kuzingatia umuhimu wa njia hiyo kwa uchumi wa dunia. Wataalamu wa masuala ya nishati wanaonya kuwa mvutano wowote katika eneo hilo unaweza kusababisha kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la kimataifa.

    Hadi sasa, hakujaripotiwa tukio lolote la moja kwa moja lililoathiri meli za kibiashara, lakini macho ya dunia yanaendelea kuelekezwa katika eneo hilo nyeti.

    Toa maoni yako
    #Habari
    #Iran #Military #Exercise #Oil #Route
    Iran yafanya mazoezi ya kijeshi katika mlango wa Hormuz, njia muhimu ya mafuta Duniani. Serikali ya Iran imeendesha mazoezi ya kijeshi katika eneo la kimkakati la Strait of Hormuz, mojawapo ya njia muhimu zaidi za usafirishaji wa mafuta duniani. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, mazoezi hayo yalihusisha vikosi vya majini, makombora ya masafa mbalimbali pamoja na ndege zisizo na rubani (drone). Hatua hiyo imekuja wakati kukiwa na mvutano wa kisiasa na kiusalama katika eneo la Mashariki ya Kati. Mlango wa Hormuz unaunganisha Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Oman, na ni njia ambayo sehemu kubwa ya mafuta ya dunia hupita kila siku. Inakadiriwa kuwa karibu theluthi moja ya mafuta yanayosafirishwa kwa njia ya bahari hupitia katika mkondo huo mwembamba lakini wenye umuhimu mkubwa kiuchumi. Afisa wa kijeshi wa Iran wamesema kuwa lengo la mazoezi hayo ni “kuimarisha uwezo wa kujilinda na kulinda mipaka ya majini ya taifa.” Aidha wameongeza kuwa “usalama wa eneo hili ni jukumu la mataifa ya ukanda huu, na si mataifa ya kigeni.” Hatua hiyo imeibua mjadala katika jumuiya ya kimataifa, hasa kwa kuzingatia umuhimu wa njia hiyo kwa uchumi wa dunia. Wataalamu wa masuala ya nishati wanaonya kuwa mvutano wowote katika eneo hilo unaweza kusababisha kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la kimataifa. Hadi sasa, hakujaripotiwa tukio lolote la moja kwa moja lililoathiri meli za kibiashara, lakini macho ya dunia yanaendelea kuelekezwa katika eneo hilo nyeti. Toa maoni yako #Habari #Iran #Military #Exercise #Oil #Route
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 403 Views
  • Karen Bujulu afunguka kuhusu Juma Jux: “Moyo wangu ni mweupe, sina kinyongo”.

    Mrembo Karen Bujulu, ambaye aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mkali wa RnB kutoka Tanzania, Juma Jux, amevunja ukimya na kueleza hisia zake kufuatia ndoa ya aliyekuwa Mpenzi wake huyo.

    Kupitia maelezo yake ya hivi karibuni, Karen amesisitiza kuwa hana chuki wala kinyongo chochote, licha ya watu wengi kudhani kuwa bado anaumizwa na uamuzi wa Jux kufunga ndoa.

    “Hadi leo watu wengi wanadhani moyo wangu unapitia maumivu makali mno kwa kitendo cha Ex wangu kufunga ndoa, hilo jambo halipo. Mnapaswa kujua kuwa moyo wangu ni mweupe na sina kinyongo chochote, nimeisha achilia kila kitu. Nimefungua ukurasa mpya kabisa na ninafurahia maisha haya mapya.”

    Kauli hiyo imeibua mjadala mpana mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimpongeza kwa ukomavu wa kiakili na kihisia, na wengine wakichambua kwa kina historia ya uhusiano wao.

    Ikumbukwe kuwa wakati uhusiano wao ulipovunjika, baadhi ya wanablogu waliibua madai kuwa chanzo kilikuwa ni Karen kuhusishwa kimapenzi na Ommy Dimpoz. Hata hivyo, Karen aliwahi kukanusha taarifa hizo na kueleza kuwa hazikuwa na ukweli wowote.

    Tangu wakati huo, kila mmoja ameendelea na maisha yake, huku Jux akiingia katika hatua mpya ya ndoa na Karen akisisitiza kuwa yeye pia ameanza safari mpya ya maisha.

    (Maoni Yangu)

    Kwa mtazamo wa kijamii na kisaikolojia, kauli ya Karen inaonyesha kiwango fulani cha ukomavu wa kihisia (emotional maturity). Katika uhusiano ya hadharani, mara nyingi presha ya mitandao ya kijamii huongeza maumivu au kuzalisha simulizi zisizo sahihi.

    Kukubali hali, kuachilia yaliyopita na kuendelea mbele ni ishara ya mtu aliyeamua kulinda amani yake ya ndani. Aidha, ni fundisho kwa jamii kuwa si kila uhusiano unaovunjika lazima uishe kwa chuki au visasi.

    Kwa upande mwingine, ni muhimu pia kutambua kuwa watu mashuhuri huishi chini ya lenzi ya umma, hivyo kila kauli au tukio huwa na tafsiri nyingi tofauti.

    Wewe unaonaje? Je, unaamini kweli hakuna maumivu yaliyobaki, au ni njia ya kulinda heshima yake mbele ya umma?

    Toa maoni yako
    #Udaku
    #Habari
    Karen Bujulu afunguka kuhusu Juma Jux: “Moyo wangu ni mweupe, sina kinyongo”. Mrembo Karen Bujulu, ambaye aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mkali wa RnB kutoka Tanzania, Juma Jux, amevunja ukimya na kueleza hisia zake kufuatia ndoa ya aliyekuwa Mpenzi wake huyo. Kupitia maelezo yake ya hivi karibuni, Karen amesisitiza kuwa hana chuki wala kinyongo chochote, licha ya watu wengi kudhani kuwa bado anaumizwa na uamuzi wa Jux kufunga ndoa. “Hadi leo watu wengi wanadhani moyo wangu unapitia maumivu makali mno kwa kitendo cha Ex wangu kufunga ndoa, hilo jambo halipo. Mnapaswa kujua kuwa moyo wangu ni mweupe na sina kinyongo chochote, nimeisha achilia kila kitu. Nimefungua ukurasa mpya kabisa na ninafurahia maisha haya mapya.” Kauli hiyo imeibua mjadala mpana mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimpongeza kwa ukomavu wa kiakili na kihisia, na wengine wakichambua kwa kina historia ya uhusiano wao. Ikumbukwe kuwa wakati uhusiano wao ulipovunjika, baadhi ya wanablogu waliibua madai kuwa chanzo kilikuwa ni Karen kuhusishwa kimapenzi na Ommy Dimpoz. Hata hivyo, Karen aliwahi kukanusha taarifa hizo na kueleza kuwa hazikuwa na ukweli wowote. Tangu wakati huo, kila mmoja ameendelea na maisha yake, huku Jux akiingia katika hatua mpya ya ndoa na Karen akisisitiza kuwa yeye pia ameanza safari mpya ya maisha. (Maoni Yangu) Kwa mtazamo wa kijamii na kisaikolojia, kauli ya Karen inaonyesha kiwango fulani cha ukomavu wa kihisia (emotional maturity). Katika uhusiano ya hadharani, mara nyingi presha ya mitandao ya kijamii huongeza maumivu au kuzalisha simulizi zisizo sahihi. Kukubali hali, kuachilia yaliyopita na kuendelea mbele ni ishara ya mtu aliyeamua kulinda amani yake ya ndani. Aidha, ni fundisho kwa jamii kuwa si kila uhusiano unaovunjika lazima uishe kwa chuki au visasi. Kwa upande mwingine, ni muhimu pia kutambua kuwa watu mashuhuri huishi chini ya lenzi ya umma, hivyo kila kauli au tukio huwa na tafsiri nyingi tofauti. Wewe unaonaje? Je, unaamini kweli hakuna maumivu yaliyobaki, au ni njia ya kulinda heshima yake mbele ya umma? Toa maoni yako #Udaku #Habari
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 390 Views
  • Trump: “Mabadiliko ya utawala Iran yangekuwa jambo bora zaidi”.

    Donald Trump, Rais wa Marekani, amesema kuwa mabadiliko ya utawala nchini Iran yanaweza kuwa suluhisho bora kufuatia kile alichokitaja kuwa ni miongo kadhaa ya mazungumzo yasiyozaa matunda kati ya pande hizo mbili.

    Kauli hiyo inakuja wakati mvutano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Iran ukiendelea kuongezeka, hasa kuhusu suala la makubaliano ya nyuklia na usalama wa kikanda.

    Akizungumza na Waandishi wa habari, Trump alisema: “Mabadiliko ya utawala nchini Iran yangekuwa jambo bora zaidi ambalo lingeweza kutokea. Kwa miaka 47, wamekuwa wakizungumza na kuzungumza. Wakati huo huo, tumepoteza maisha mengi huku wakizungumza. Miguu imepasuka, mikono imepasuka, nyuso zimepasuka. Tumekuwa tukiendelea kwa muda mrefu kwa hivyo hebu tuone kitakachotokea.”

    Kauli hiyo inaashiria msimamo mkali wa Washington kuhusu mwenendo wa mazungumzo na Tehran, huku Trump akionyesha kutoridhishwa na kile alichokiita historia ya ahadi zisizotekelezwa.

    Aliendelea kusisitiza kuwa Marekani iko tayari kwa suluhisho la kidiplomasia, lakini kwa masharti maalum: “Kama wakitupa makubaliano sahihi, hatutafanya hivyo lakini, unajua, kihistoria, hawajafanya hivyo. Nitasema wanataka kuzungumza lakini hadi sasa, wanazungumza sana na hakuna hatua.”

    Trump aliongeza kuwa suluhu ya kudumu ingekuwa mafanikio makubwa kwa pande zote: “Kama tungeweza kusuluhisha mambo mara moja na kwa wote, hilo lingekuwa jambo zuri.”

    Alipoulizwa ni nani angependa aongoze Iran iwapo mabadiliko ya utawala yangetokea, Trump alijibu kwa tahadhari: “Sitaki kuzungumzia hilo, kuna watu.”

    Kauli hizi zimezua mjadala mpana kimataifa, huku Wachambuzi wakitathmini iwapo msimamo huo utaongeza shinikizo la kisiasa dhidi ya Iran au kufungua mlango mpya wa mazungumzo ya moja kwa moja.

    Kwa sasa, macho ya dunia yanaelekezwa katika hatua zitakazochukuliwa na pande zote mbili, huku mustakabali wa uhusiano wa Marekani na Iran ukiwa katika mizani nyeti ya kidiplomasia.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Trump: “Mabadiliko ya utawala Iran yangekuwa jambo bora zaidi”. Donald Trump, Rais wa Marekani, amesema kuwa mabadiliko ya utawala nchini Iran yanaweza kuwa suluhisho bora kufuatia kile alichokitaja kuwa ni miongo kadhaa ya mazungumzo yasiyozaa matunda kati ya pande hizo mbili. Kauli hiyo inakuja wakati mvutano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Iran ukiendelea kuongezeka, hasa kuhusu suala la makubaliano ya nyuklia na usalama wa kikanda. Akizungumza na Waandishi wa habari, Trump alisema: “Mabadiliko ya utawala nchini Iran yangekuwa jambo bora zaidi ambalo lingeweza kutokea. Kwa miaka 47, wamekuwa wakizungumza na kuzungumza. Wakati huo huo, tumepoteza maisha mengi huku wakizungumza. Miguu imepasuka, mikono imepasuka, nyuso zimepasuka. Tumekuwa tukiendelea kwa muda mrefu kwa hivyo hebu tuone kitakachotokea.” Kauli hiyo inaashiria msimamo mkali wa Washington kuhusu mwenendo wa mazungumzo na Tehran, huku Trump akionyesha kutoridhishwa na kile alichokiita historia ya ahadi zisizotekelezwa. Aliendelea kusisitiza kuwa Marekani iko tayari kwa suluhisho la kidiplomasia, lakini kwa masharti maalum: “Kama wakitupa makubaliano sahihi, hatutafanya hivyo lakini, unajua, kihistoria, hawajafanya hivyo. Nitasema wanataka kuzungumza lakini hadi sasa, wanazungumza sana na hakuna hatua.” Trump aliongeza kuwa suluhu ya kudumu ingekuwa mafanikio makubwa kwa pande zote: “Kama tungeweza kusuluhisha mambo mara moja na kwa wote, hilo lingekuwa jambo zuri.” Alipoulizwa ni nani angependa aongoze Iran iwapo mabadiliko ya utawala yangetokea, Trump alijibu kwa tahadhari: “Sitaki kuzungumzia hilo, kuna watu.” Kauli hizi zimezua mjadala mpana kimataifa, huku Wachambuzi wakitathmini iwapo msimamo huo utaongeza shinikizo la kisiasa dhidi ya Iran au kufungua mlango mpya wa mazungumzo ya moja kwa moja. Kwa sasa, macho ya dunia yanaelekezwa katika hatua zitakazochukuliwa na pande zote mbili, huku mustakabali wa uhusiano wa Marekani na Iran ukiwa katika mizani nyeti ya kidiplomasia. Toa maoni yako #Habari
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 326 Views
  • “Tukiamua kuwashtaki na kuwafunga watu wote waliohusika kwenye mafaili ya Epstein, mfumo mzima utakufa”

    - Pam Bondi, Mwanasheria Mkuu wa Marekani.

    Toa maoni yako
    #Habari
    “Tukiamua kuwashtaki na kuwafunga watu wote waliohusika kwenye mafaili ya Epstein, mfumo mzima utakufa” - Pam Bondi, Mwanasheria Mkuu wa Marekani. Toa maoni yako #Habari
    0 Σχόλια 1 Μοιράστηκε 219 Views
  • Rais wa Senegal aagiza kuondolewa kwa picha zake katika ofisi za umma.

    Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, ametoa agizo rasmi linalowataka Afisa wote wa umma nchini humo kuondoa picha zake katika ofisi zote za serikali.

    Katika hotuba yake kwa taifa, Rais Faye anayehesabiwa miongoni mwa Viongozi vijana zaidi barani Afrika, alisisitiza kuwa nafasi yake ni ya kulitumikia taifa, si kuabudiwa au kupewa hadhi ya kipekee kupita kiasi.

    Akizungumza kwa msisitizo, Kiongozi huyo alisema: “Sitaki picha yangu katika ofisi zenu, kwa sababu mimi si Mungu wala mimi si sanamu bali mimi ni Mtumishi wa taifa.”

    Kauli hiyo imeibua mjadala mpana kuhusu mtazamo wake wa uongozi unaolenga unyenyekevu na uwajibikaji ndani ya utumishi wa umma.

    Mbali na kuagiza kuondolewa kwa picha zake, Rais Faye aliwataka Watumishi wa umma kuweka picha za Watoto wao katika ofisi zao kama njia ya kujikumbusha wajibu wao kwa familia na taifa. Kwa mujibu wake, hatua hiyo itasaidia kuongeza ari ya uwajibikaji kazini.

    Alisema: “Badala yake wekeni picha za Watoto wenu ili uweze kuziangalia wakati wowote unapotaka kuwa mvivu au kutowajibika.”

    Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona hatua hiyo kama ishara ya kujaribu kubadili utamaduni wa kisiasa unaoweka kiongozi katikati ya taasisi, na badala yake kuhimiza mfumo unaotanguliza misingi ya utumishi na uwajibikaji.

    Hatua ya Rais Faye inaonekana kuendana na ahadi zake za kampeni zilizolenga mageuzi, uwazi na kurejesha imani ya Wananchi kwa taasisi za umma nchini Senegal.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Rais wa Senegal aagiza kuondolewa kwa picha zake katika ofisi za umma. Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, ametoa agizo rasmi linalowataka Afisa wote wa umma nchini humo kuondoa picha zake katika ofisi zote za serikali. Katika hotuba yake kwa taifa, Rais Faye anayehesabiwa miongoni mwa Viongozi vijana zaidi barani Afrika, alisisitiza kuwa nafasi yake ni ya kulitumikia taifa, si kuabudiwa au kupewa hadhi ya kipekee kupita kiasi. Akizungumza kwa msisitizo, Kiongozi huyo alisema: “Sitaki picha yangu katika ofisi zenu, kwa sababu mimi si Mungu wala mimi si sanamu bali mimi ni Mtumishi wa taifa.” Kauli hiyo imeibua mjadala mpana kuhusu mtazamo wake wa uongozi unaolenga unyenyekevu na uwajibikaji ndani ya utumishi wa umma. Mbali na kuagiza kuondolewa kwa picha zake, Rais Faye aliwataka Watumishi wa umma kuweka picha za Watoto wao katika ofisi zao kama njia ya kujikumbusha wajibu wao kwa familia na taifa. Kwa mujibu wake, hatua hiyo itasaidia kuongeza ari ya uwajibikaji kazini. Alisema: “Badala yake wekeni picha za Watoto wenu ili uweze kuziangalia wakati wowote unapotaka kuwa mvivu au kutowajibika.” Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona hatua hiyo kama ishara ya kujaribu kubadili utamaduni wa kisiasa unaoweka kiongozi katikati ya taasisi, na badala yake kuhimiza mfumo unaotanguliza misingi ya utumishi na uwajibikaji. Hatua ya Rais Faye inaonekana kuendana na ahadi zake za kampeni zilizolenga mageuzi, uwazi na kurejesha imani ya Wananchi kwa taasisi za umma nchini Senegal. Toa maoni yako #Habari
    0 Σχόλια 1 Μοιράστηκε 326 Views
  • Sud-Kivu: DRC inalipa zawadi za motisha kwa Wanajeshi na Wapiganaji Wazalendo.

    Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeanza kutoa zawadi za motisha kwa Wanajeshi wa FARDC na Wapiganaji wa Wazalendo walioko mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya Waasi wa M23/RDF katika kusini mwa Mkoa wa Sud-Kivu.

    Chanzo cha Wizara ya Ulinzi kimesema kuwa, "Tumepeleka timu rasmi katika eneo hili na tangu wiki hii tumeanza kulipa moja kwa moja Wanajeshi walioko mstari wa mbele." Operesheni hii inahusisha miradi mbalimbali ya fronti ya kusini na inalenga kufikia Wanajeshi wote walioko katika operesheni za kijeshi zinazendelea.

    Mpango huu ni sehemu ya jitihada za serikali ya DRC kukuza morali na kuboresha hali ya Wanajeshi walioko Uwanjani, huku mapambano yakiendelea katika sehemu hii ya Mkoa.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Sud-Kivu: DRC inalipa zawadi za motisha kwa Wanajeshi na Wapiganaji Wazalendo. Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeanza kutoa zawadi za motisha kwa Wanajeshi wa FARDC na Wapiganaji wa Wazalendo walioko mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya Waasi wa M23/RDF katika kusini mwa Mkoa wa Sud-Kivu. Chanzo cha Wizara ya Ulinzi kimesema kuwa, "Tumepeleka timu rasmi katika eneo hili na tangu wiki hii tumeanza kulipa moja kwa moja Wanajeshi walioko mstari wa mbele." Operesheni hii inahusisha miradi mbalimbali ya fronti ya kusini na inalenga kufikia Wanajeshi wote walioko katika operesheni za kijeshi zinazendelea. Mpango huu ni sehemu ya jitihada za serikali ya DRC kukuza morali na kuboresha hali ya Wanajeshi walioko Uwanjani, huku mapambano yakiendelea katika sehemu hii ya Mkoa. Toa maoni yako #Habari
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 96 Views
  • WAKAZI WA PAKADJUMA WAKATAA KUONDOKA ENEO LILILOBOMOLEWA, WAKABILIA POLISI LIMETE.

    Hali ya wasiwasi na taharuki imetanda katika eneo la Pakadjuma, Wilaya ya Limete, Jijini Kinshasa, DR Congo, baada ya Wakazi wa eneo hilo kukataa kuondoka katika sehemu iliyobomolewa na mamlaka za Jiji. Hatua hiyo imesababisha makabiliano kati ya Wakazi na vikosi vya polisi vilivyotumwa kutekeleza agizo la kusafisha eneo hilo.

    Kwa mujibu wa mamlaka za Jiji la Kinshasa, Wakazi wa Pakadjuma waliondolewa katika eneo hilo kwa sababu kadhaa, ikiwemo madai kuwa makazi hayo yalijengwa bila kufuata mipango rasmi ya Mji, hali inayoyafanya kutambuliwa kama makazi yasiyo halali. Vilevile, eneo hilo limekuwa likitajwa kuwa hatarishi kiafya kutokana na uchafuzi wa mazingira, taka na mafuriko ya mara kwa mara, hali inayodaiwa kuhatarisha maisha ya Wakazi.

    Hatua ya ubomoaji pia inaelezwa kuwa ni sehemu ya mpango wa upangaji na usafi wa Jiji la Kinshasa, unaolenga kuondoa makazi yaliyojengwa kinyume cha sheria, kurejesha maeneo ya hifadhi na kuboresha miundombinu ya jiji pamoja na usalama wa Wakazi.

    Hata hivyo, Wakazi wa Pakadjuma wamepinga vikali uamuzi huo, wakisema hawajapewa makazi mbadala wala fidia ya kuridhisha. Wengi wao wameendelea kubaki katika eneo hilo licha ya ubomoaji, wakidai hawana sehemu nyingine ya kwenda.

    Mmoja wa wakazi hao amenukuliwa akisema, “Hatuwezi kuondoka hapa bila kupata uhakika wa mahali pa kuishi. Nyumba zetu zimebomolewa na hatujapewa suluhisho lolote.”

    Mvutano uliongezeka pale Polisi walipojaribu kuwasukuma Wakazi kuondoka katika eneo hilo, hali iliyopelekea makabiliano ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili. Mashuhuda wanasema hali ilikuwa ya vurugu kwa nyakati tofauti huku Wakazi wakionyesha hasira zao dhidi ya hatua za mamlaka.

    Kwa upande wake, Afisa mmoja wa usalama aliyekuwepo eneo la tukio amesema, “Tupo hapa kutekeleza maagizo ya kisheria na kuhakikisha usalama wa Raia wote. Tunawahimiza Wakazi kushirikiana na mamlaka ili kuepuka madhara.”

    Hadi sasa, hali bado ni tete katika eneo la Pakadjuma, huku Wakazi wakiendelea kushikilia msimamo wao na mamlaka za Jiji la Kinshasa zikiwa bado hazijatoa tamko rasmi kuhusu mpango wa makazi mbadala au fidia kwa Waathirika wa zoezi hilo.

    Toa maoni yako
    #Habari
    WAKAZI WA PAKADJUMA WAKATAA KUONDOKA ENEO LILILOBOMOLEWA, WAKABILIA POLISI LIMETE. Hali ya wasiwasi na taharuki imetanda katika eneo la Pakadjuma, Wilaya ya Limete, Jijini Kinshasa, DR Congo, baada ya Wakazi wa eneo hilo kukataa kuondoka katika sehemu iliyobomolewa na mamlaka za Jiji. Hatua hiyo imesababisha makabiliano kati ya Wakazi na vikosi vya polisi vilivyotumwa kutekeleza agizo la kusafisha eneo hilo. Kwa mujibu wa mamlaka za Jiji la Kinshasa, Wakazi wa Pakadjuma waliondolewa katika eneo hilo kwa sababu kadhaa, ikiwemo madai kuwa makazi hayo yalijengwa bila kufuata mipango rasmi ya Mji, hali inayoyafanya kutambuliwa kama makazi yasiyo halali. Vilevile, eneo hilo limekuwa likitajwa kuwa hatarishi kiafya kutokana na uchafuzi wa mazingira, taka na mafuriko ya mara kwa mara, hali inayodaiwa kuhatarisha maisha ya Wakazi. Hatua ya ubomoaji pia inaelezwa kuwa ni sehemu ya mpango wa upangaji na usafi wa Jiji la Kinshasa, unaolenga kuondoa makazi yaliyojengwa kinyume cha sheria, kurejesha maeneo ya hifadhi na kuboresha miundombinu ya jiji pamoja na usalama wa Wakazi. Hata hivyo, Wakazi wa Pakadjuma wamepinga vikali uamuzi huo, wakisema hawajapewa makazi mbadala wala fidia ya kuridhisha. Wengi wao wameendelea kubaki katika eneo hilo licha ya ubomoaji, wakidai hawana sehemu nyingine ya kwenda. Mmoja wa wakazi hao amenukuliwa akisema, “Hatuwezi kuondoka hapa bila kupata uhakika wa mahali pa kuishi. Nyumba zetu zimebomolewa na hatujapewa suluhisho lolote.” Mvutano uliongezeka pale Polisi walipojaribu kuwasukuma Wakazi kuondoka katika eneo hilo, hali iliyopelekea makabiliano ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili. Mashuhuda wanasema hali ilikuwa ya vurugu kwa nyakati tofauti huku Wakazi wakionyesha hasira zao dhidi ya hatua za mamlaka. Kwa upande wake, Afisa mmoja wa usalama aliyekuwepo eneo la tukio amesema, “Tupo hapa kutekeleza maagizo ya kisheria na kuhakikisha usalama wa Raia wote. Tunawahimiza Wakazi kushirikiana na mamlaka ili kuepuka madhara.” Hadi sasa, hali bado ni tete katika eneo la Pakadjuma, huku Wakazi wakiendelea kushikilia msimamo wao na mamlaka za Jiji la Kinshasa zikiwa bado hazijatoa tamko rasmi kuhusu mpango wa makazi mbadala au fidia kwa Waathirika wa zoezi hilo. Toa maoni yako #Habari
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 266 Views
  • FBI yafunga uchunguzi wa Epstein: Hakuna ushahidi wa mtandao wa Watu wenye nguvu.

    Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) limehitimisha rasmi uchunguzi wake kuhusu madai kuwa marehemu Jeffrey Epstein aliendesha mtandao wa usafirishaji haramu wa kingono uliowahusisha Wanaume wenye mamlaka na kutumia vitendo hivyo kama njia ya kuwatishia au kuwabana kwa siri.

    Kwa mujibu wa nyaraka za ndani zilizochunguzwa, FBI imebaini kuwa hakukuwa na ushahidi wowote wa kuaminika unaothibitisha madai hayo mazito yaliyozungumzwa kwa miaka mingi katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

    Chanzo cha karibu na uchunguzi huo kimenukuliwa kikisema kuwa, “Baada ya uchambuzi wa kina wa ushahidi wote uliokusanywa, hatukupata uthibitisho wa kuwepo kwa mtandao wa usafirishaji wa kingono unaowahusisha watu wenye nguvu au mpango wa kuwatumia kuwabana.”

    Ripoti hiyo inaeleza kuwa ingawa Jeffrey Epstein alihusishwa na makosa ya kingono dhidi ya Wasichana wadogo, madai ya kuwa Kiongozi wa mtandao mkubwa wa siri uliowahusisha Wanasiasa, Wafanyabiashara wakubwa na watu mashuhuri hayakuungwa mkono na ushahidi wa kisheria.

    Mtaalamu mmoja wa masuala ya sheria alieleza kuwa, “Ni muhimu kutenganisha makosa aliyothibitishwa Epstein binafsi na nadharia ambazo hazikuweza kuthibitishwa kwa ushahidi thabiti.”

    Hata hivyo, hitimisho hilo limeibua mjadala mpana miongoni mwa umma, hasa kwa wale wanaoamini kuwa ukweli kamili kuhusu kisiwa chake maarufu na Wageni wake haujawahi kuwekwa wazi kikamilifu.

    Kwa sasa, FBI imesisitiza kuwa faili zilizopo hazionyeshi kuwepo kwa mtandao wa siri wa kuhusisha watu wenye ushawishi, na hivyo kuweka rasmi mwisho wa uchunguzi huo katika mwelekeo huo.

    Toa maoni yako
    #Habarii
    FBI yafunga uchunguzi wa Epstein: Hakuna ushahidi wa mtandao wa Watu wenye nguvu. Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) limehitimisha rasmi uchunguzi wake kuhusu madai kuwa marehemu Jeffrey Epstein aliendesha mtandao wa usafirishaji haramu wa kingono uliowahusisha Wanaume wenye mamlaka na kutumia vitendo hivyo kama njia ya kuwatishia au kuwabana kwa siri. Kwa mujibu wa nyaraka za ndani zilizochunguzwa, FBI imebaini kuwa hakukuwa na ushahidi wowote wa kuaminika unaothibitisha madai hayo mazito yaliyozungumzwa kwa miaka mingi katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Chanzo cha karibu na uchunguzi huo kimenukuliwa kikisema kuwa, “Baada ya uchambuzi wa kina wa ushahidi wote uliokusanywa, hatukupata uthibitisho wa kuwepo kwa mtandao wa usafirishaji wa kingono unaowahusisha watu wenye nguvu au mpango wa kuwatumia kuwabana.” Ripoti hiyo inaeleza kuwa ingawa Jeffrey Epstein alihusishwa na makosa ya kingono dhidi ya Wasichana wadogo, madai ya kuwa Kiongozi wa mtandao mkubwa wa siri uliowahusisha Wanasiasa, Wafanyabiashara wakubwa na watu mashuhuri hayakuungwa mkono na ushahidi wa kisheria. Mtaalamu mmoja wa masuala ya sheria alieleza kuwa, “Ni muhimu kutenganisha makosa aliyothibitishwa Epstein binafsi na nadharia ambazo hazikuweza kuthibitishwa kwa ushahidi thabiti.” Hata hivyo, hitimisho hilo limeibua mjadala mpana miongoni mwa umma, hasa kwa wale wanaoamini kuwa ukweli kamili kuhusu kisiwa chake maarufu na Wageni wake haujawahi kuwekwa wazi kikamilifu. Kwa sasa, FBI imesisitiza kuwa faili zilizopo hazionyeshi kuwepo kwa mtandao wa siri wa kuhusisha watu wenye ushawishi, na hivyo kuweka rasmi mwisho wa uchunguzi huo katika mwelekeo huo. Toa maoni yako #Habarii
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 224 Views
  • Saadi Gaddafi afunguka kuhusu mauaji ya Kaka yake.

    Saadi Gaddafi, Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Libya Muammar Gaddafi, ametoa kauli yake kuhusu mauaji ya kaka yake huku akisisitiza umuhimu wa haki na uchunguzi wa kina. Saadi, ambaye pia ni Mwanajeshi, Mfanyabiashara na Mchezaji wa zamani wa soka, amesema: “…Hatuwezi kumtuhumu mtu yeyote kwa sasa, kuhusiana na mauaji ya kaka yangu…”

    Aidha, Saadi ameongeza kuwa familia ya Gaddafi inaendelea kusubiri ukweli kamili kubainika kabla ya kutoa lawama kwa upande wowote. Kauli yake hii imeibua hisia tofauti miongoni mwa wananchi na wafuasi wa familia hiyo, huku wengi wakisubiri kwa hamu matokeo ya uchunguzi wa kina.

    Saadi amesisitiza kuwa ni muhimu kuhakikisha haki inatendeka, na kwamba kutoa mashitaka bila ushahidi thabiti hakutasaidia katika kufanikisha mchakato wa kweli wa kisheria na kimaadili.

    Toa maoni yako
    Saadi Gaddafi afunguka kuhusu mauaji ya Kaka yake. Saadi Gaddafi, Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Libya Muammar Gaddafi, ametoa kauli yake kuhusu mauaji ya kaka yake huku akisisitiza umuhimu wa haki na uchunguzi wa kina. Saadi, ambaye pia ni Mwanajeshi, Mfanyabiashara na Mchezaji wa zamani wa soka, amesema: “…Hatuwezi kumtuhumu mtu yeyote kwa sasa, kuhusiana na mauaji ya kaka yangu…” Aidha, Saadi ameongeza kuwa familia ya Gaddafi inaendelea kusubiri ukweli kamili kubainika kabla ya kutoa lawama kwa upande wowote. Kauli yake hii imeibua hisia tofauti miongoni mwa wananchi na wafuasi wa familia hiyo, huku wengi wakisubiri kwa hamu matokeo ya uchunguzi wa kina. Saadi amesisitiza kuwa ni muhimu kuhakikisha haki inatendeka, na kwamba kutoa mashitaka bila ushahidi thabiti hakutasaidia katika kufanikisha mchakato wa kweli wa kisheria na kimaadili. Toa maoni yako
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 174 Views
  • Cristiano Ronaldo arejea Uwanjani baada ya mvutano Al Nassr na Saudi PIF.

    Ripoti zinazonukuliwa kutoka vyanzo mbalimbali nchini Saudi Arabia zinaeleza kuwa Staa wa soka duniani, Cristiano Ronaldo, amesitisha rasmi mgomo wake na yuko tayari kurejea Uwanjani kuitumikia klabu ya Al Nassr. Hatua hiyo inakuja baada ya Wafanyakazi wote wa klabu hiyo kulipwa mishahara yao pamoja na posho walizokuwa wakidai kwa muda.

    Kwa mujibu wa taarifa hizo, mgomo wa Ronaldo ulihusishwa na mvutano uliokuwepo kati yake na Tume ya Uwekezaji ya Saudi Arabia, maarufu kama Saudi PIF. Inadaiwa kuwa Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno alikuwa akilalamikia kile kilichoelezwa kuwa ni upendeleo kwa baadhi ya klabu, hususan katika masuala ya usajili wa Wachezaji na uwekezaji mkubwa unaofanywa kwenye timu fulani.

    Zaidi ya hayo, chanzo cha mgomo huo hakikujikita tu kwenye masuala ya usajili aliyoyaona kuwa hayaridhishi, bali pia katika kuhakikisha haki za Wafanyakazi wa klabu zinalindwa. Ronaldo alisisitiza kuwa Wafanyakazi wote, hasa wale wa ngazi za chini, walipaswa kulipwa stahiki zao kwa wakati na kwa ukamilifu.

    Hatua ya kulipwa kwa Wafanyakazi wote imeonekana kufungua ukurasa mpya ndani ya Al Nassr, na kurejesha hali ya utulivu kambini. Mashabiki wengi sasa wanasubiri kwa hamu kumuona Ronaldo akirejea Uwanjani, wakitumaini kuwa tukio hilo litaleta mabadiliko chanya ndani ya klabu hiyo na kwenye ligi kwa ujumla.

    Kwa kurejea kwake, Ronaldo anaonekana si tu kama Mchezaji mkubwa Uwanjani, bali pia kama sauti ya Wafanyakazi na mdau anayeonyesha kujali masuala ya haki na usawa ndani ya soka la kulipwa.

    Toa maoni yako
    #Tarifazauwakika
    Cristiano Ronaldo arejea Uwanjani baada ya mvutano Al Nassr na Saudi PIF. Ripoti zinazonukuliwa kutoka vyanzo mbalimbali nchini Saudi Arabia zinaeleza kuwa Staa wa soka duniani, Cristiano Ronaldo, amesitisha rasmi mgomo wake na yuko tayari kurejea Uwanjani kuitumikia klabu ya Al Nassr. Hatua hiyo inakuja baada ya Wafanyakazi wote wa klabu hiyo kulipwa mishahara yao pamoja na posho walizokuwa wakidai kwa muda. Kwa mujibu wa taarifa hizo, mgomo wa Ronaldo ulihusishwa na mvutano uliokuwepo kati yake na Tume ya Uwekezaji ya Saudi Arabia, maarufu kama Saudi PIF. Inadaiwa kuwa Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno alikuwa akilalamikia kile kilichoelezwa kuwa ni upendeleo kwa baadhi ya klabu, hususan katika masuala ya usajili wa Wachezaji na uwekezaji mkubwa unaofanywa kwenye timu fulani. Zaidi ya hayo, chanzo cha mgomo huo hakikujikita tu kwenye masuala ya usajili aliyoyaona kuwa hayaridhishi, bali pia katika kuhakikisha haki za Wafanyakazi wa klabu zinalindwa. Ronaldo alisisitiza kuwa Wafanyakazi wote, hasa wale wa ngazi za chini, walipaswa kulipwa stahiki zao kwa wakati na kwa ukamilifu. Hatua ya kulipwa kwa Wafanyakazi wote imeonekana kufungua ukurasa mpya ndani ya Al Nassr, na kurejesha hali ya utulivu kambini. Mashabiki wengi sasa wanasubiri kwa hamu kumuona Ronaldo akirejea Uwanjani, wakitumaini kuwa tukio hilo litaleta mabadiliko chanya ndani ya klabu hiyo na kwenye ligi kwa ujumla. Kwa kurejea kwake, Ronaldo anaonekana si tu kama Mchezaji mkubwa Uwanjani, bali pia kama sauti ya Wafanyakazi na mdau anayeonyesha kujali masuala ya haki na usawa ndani ya soka la kulipwa. Toa maoni yako #Tarifazauwakika
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 246 Views
  • Ukiona unafanya jambo usilo lipenda ni uhakika wa wazi kuwa kuna jambo bado ujalijua kuhusu zambi ,kwa lugha rahisi zambi imeikalia nafsi yako na kuiongoza.

    #Warumi 7:18-19
    [18]Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.

    [19]Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
    .
    Ndiyo sababu gheto unaenda kwa moyo wako wote ,nguo mnavua vizuri pamoja na ni wanakwaya mkimaliza kuzini unakuta mmoja anaanza kumlaumu mwenzake kuwa tamaa zako zimetuponza tumezini.

    Siyo kuwa tamaa zimewaponza ni kuwa either kuna jambo ujajua kuhusu zinaa ambalo ungelijua usinge thubutu kujitoa ufahamu kwenda getho la mtu na unaenda peke yako kabisa.

    #Chanzo ni nini ni kadiri unavyotaka kutumia akiri zako ndivyo unavyo fungua mlango wa shetani kukushanbulia kupitia ujinga wako.

    #Kumbe kama ungemuangalia Yusuph alicho fanya ungejua uzinzi hatuneni kwa lugha na kubakia hapo hapo tunakimbia mbali kabisa kwa kuwa usipo kimbia mwili wako utazidiwa na matokeo yako utaanguka.

    #Mwanzo 39:11-12
    [11]Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani;

    [12]huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje.

    Hii ndiyo sababu biblia inasema pia ikimbieni zinaa

    1 Wakorintho 6:18
    [18]Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.

    #Ukishindwa kukimbia shetani atakukamata .

    Lengo ni nini nimesema kila aliye shinda zambi au jambo furani kuna ufahamu anao ambao wewe una.

    Jitahidi kutafuta maarifa kuna aina ya zambi hazitoki kwa maombi peke yake bila kujua kanuni ya kushinda iyo zambi.

    Kitakacho tokea ni kuwa unaomba sana lakini ukitoka kuomba shetani anakuletea tena zambi ile ile na unaanguka tena

    #Shetani aogopi kipawa au karama uliyo nayo kuhusu kukushambulia ila anaogopa maarifa uliyo nayo kuhusu ilo jambo.Kadiri unavyo juuw siri nyingi juu ya jambo fulani ndivyo unavyo funga mlango wa mahambulizi ya shetani.

    Isaya amekuwa nabii lakini kila siku alikuwa nabii lakini pia ana midomo michafu mpaka siku alipo pata ufunuo ambao uliambatana na ukombozi ndio akaendelea kuwa mtu safi.

    Isaya 6:5-7
    [5]Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.

    [6]Kisha mmoja wa maserafi wale akaruka akanikaribia; naye alikuwa na kaa la moto mkononi mwake, ambalo alikuwa amelitwaa kwa makoleo toka juu ya madhabahu;

    [7]akanigusa kinywa changu kwa kaa hilo, akaniambia, Tazama, hili limekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa.

    Ukombozi wa Isaya ulitegemea sana na ufunuo alio pokea siku hiyi maana kila siku aliendelea kuwa nabii lakin kumbe kuna jambo liko nyuma ya pazia na ndicho kizuizi chake.

    MUNGU ALIYE MTOKEA ISAYA KATIKA ULE MWAKA WA KUFA KWA MFALME UZIA NDIO MUNGU AKAKUTOKEE NA WEWE NA MIMI PIA ILI ATUTIE UFUNUO WA KUJUA MAKOSA YETU NA UKOMBOZI WAKE UPITE MOJA KWA MOJA.

    Sylvester Mwakabende (0622625340)

    #2026_Sisi_ndio_wale_tunao_piganiwa_na_Bwana.
    Ukiona unafanya jambo usilo lipenda ni uhakika wa wazi kuwa kuna jambo bado ujalijua kuhusu zambi ,kwa lugha rahisi zambi imeikalia nafsi yako na kuiongoza. #Warumi 7:18-19 [18]Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. [19]Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. . Ndiyo sababu gheto unaenda kwa moyo wako wote ,nguo mnavua vizuri pamoja na ni wanakwaya mkimaliza kuzini unakuta mmoja anaanza kumlaumu mwenzake kuwa tamaa zako zimetuponza tumezini. Siyo kuwa tamaa zimewaponza ni kuwa either kuna jambo ujajua kuhusu zinaa ambalo ungelijua usinge thubutu kujitoa ufahamu kwenda getho la mtu na unaenda peke yako kabisa. #Chanzo ni nini ni kadiri unavyotaka kutumia akiri zako ndivyo unavyo fungua mlango wa shetani kukushanbulia kupitia ujinga wako. #Kumbe kama ungemuangalia Yusuph alicho fanya ungejua uzinzi hatuneni kwa lugha na kubakia hapo hapo tunakimbia mbali kabisa kwa kuwa usipo kimbia mwili wako utazidiwa na matokeo yako utaanguka. #Mwanzo 39:11-12 [11]Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani; [12]huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje. Hii ndiyo sababu biblia inasema pia ikimbieni zinaa 1 Wakorintho 6:18 [18]Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. #Ukishindwa kukimbia shetani atakukamata . Lengo ni nini nimesema kila aliye shinda zambi au jambo furani kuna ufahamu anao ambao wewe una. Jitahidi kutafuta maarifa kuna aina ya zambi hazitoki kwa maombi peke yake bila kujua kanuni ya kushinda iyo zambi. Kitakacho tokea ni kuwa unaomba sana lakini ukitoka kuomba shetani anakuletea tena zambi ile ile na unaanguka tena #Shetani aogopi kipawa au karama uliyo nayo kuhusu kukushambulia ila anaogopa maarifa uliyo nayo kuhusu ilo jambo.Kadiri unavyo juuw siri nyingi juu ya jambo fulani ndivyo unavyo funga mlango wa mahambulizi ya shetani. Isaya amekuwa nabii lakini kila siku alikuwa nabii lakini pia ana midomo michafu mpaka siku alipo pata ufunuo ambao uliambatana na ukombozi ndio akaendelea kuwa mtu safi. Isaya 6:5-7 [5]Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi. [6]Kisha mmoja wa maserafi wale akaruka akanikaribia; naye alikuwa na kaa la moto mkononi mwake, ambalo alikuwa amelitwaa kwa makoleo toka juu ya madhabahu; [7]akanigusa kinywa changu kwa kaa hilo, akaniambia, Tazama, hili limekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa. Ukombozi wa Isaya ulitegemea sana na ufunuo alio pokea siku hiyi maana kila siku aliendelea kuwa nabii lakin kumbe kuna jambo liko nyuma ya pazia na ndicho kizuizi chake. MUNGU ALIYE MTOKEA ISAYA KATIKA ULE MWAKA WA KUFA KWA MFALME UZIA NDIO MUNGU AKAKUTOKEE NA WEWE NA MIMI PIA ILI ATUTIE UFUNUO WA KUJUA MAKOSA YETU NA UKOMBOZI WAKE UPITE MOJA KWA MOJA. Sylvester Mwakabende (0622625340) #2026_Sisi_ndio_wale_tunao_piganiwa_na_Bwana.
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 1χλμ. Views
  • NENO LA SIKU.

    NAKUOMBEA SIKU YA LEO IKAWE SIKU YA KUFUJGULIWA KWA MALANGO YAKOPANDE ZOTE NNE ZA NCHI.

    BWANA AKAFUNGUE MALANGO YAKO YA FURSA ,MALANGO YAKO YA NDOA ,MALANGO YAKO YA UCHUMI,MALANGO YAKO YA BISHARA .

    Isaya 60:11
    [11]Malango yako nayo yatakuwa wazi daima;
    Hayatafungwa mchana wala usiku;
    Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa,
    Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.

    MALANGO YAKO YAWE WAZI WAKATI HUO HUO MUNGU AKUSOGEZEEE WATU SAHIHI AMBAO WATAKUJA KUKULETEA UTAJIRI KONA ZOTE ZA NCHI.

    MUNGU AKAKUFANYE KUWA SUMAKU INAYO WEZA KUVUTA WATU WA MAANA WAKATI MALANGO YAKO YAKO WAZI.

    Isaya 60:14

    [14]Na wana wa watu wale waliokutesa
    Watakuja kwako na kukuinamia;
    Nao wote waliokudharau
    Watajiinamisha hata nyayo za miguu yako;
    Nao watakuita, Mji wa BWANA,
    Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli.

    KILA ADUI YAKO ALIYE KUTESA ATAANGUKA MBELE YAKO NA WEWE UTASHUHUDIA WAZI WAZI NAWE UTASEMA BWANA KANILETEA MFALME WA SIHONI NIMPIGE MBELE YANGU

    NA BAADA TU YA KUMPIGA MALANGO YATAANZA KUWA WAZI WAKATI WOTE NA WAFALME KUTOKA MBALI YA NCHI WATAKUSANYANA WAKITAKA KUJUA KUKUONA WAKIAMBIANA YULE NDIYE BWANA ALIYE MBARIKI NA KUMPA MILKI YOTE YA NCHI HII.

    Sylvester Mwakabende
    0622625340
    #2026_SISI_NDOO_WALE_TUNAO PIGANIWA_NA _BWANA.
    NENO LA SIKU. NAKUOMBEA SIKU YA LEO IKAWE SIKU YA KUFUJGULIWA KWA MALANGO YAKOPANDE ZOTE NNE ZA NCHI. BWANA AKAFUNGUE MALANGO YAKO YA FURSA ,MALANGO YAKO YA NDOA ,MALANGO YAKO YA UCHUMI,MALANGO YAKO YA BISHARA . Isaya 60:11 [11]Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao. MALANGO YAKO YAWE WAZI WAKATI HUO HUO MUNGU AKUSOGEZEEE WATU SAHIHI AMBAO WATAKUJA KUKULETEA UTAJIRI KONA ZOTE ZA NCHI. MUNGU AKAKUFANYE KUWA SUMAKU INAYO WEZA KUVUTA WATU WA MAANA WAKATI MALANGO YAKO YAKO WAZI. Isaya 60:14 [14]Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa BWANA, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli. KILA ADUI YAKO ALIYE KUTESA ATAANGUKA MBELE YAKO NA WEWE UTASHUHUDIA WAZI WAZI NAWE UTASEMA BWANA KANILETEA MFALME WA SIHONI NIMPIGE MBELE YANGU NA BAADA TU YA KUMPIGA MALANGO YATAANZA KUWA WAZI WAKATI WOTE NA WAFALME KUTOKA MBALI YA NCHI WATAKUSANYANA WAKITAKA KUJUA KUKUONA WAKIAMBIANA YULE NDIYE BWANA ALIYE MBARIKI NA KUMPA MILKI YOTE YA NCHI HII. Sylvester Mwakabende 0622625340 #2026_SISI_NDOO_WALE_TUNAO PIGANIWA_NA _BWANA.
    0 Σχόλια 0 Μοιράστηκε 727 Views
Αναζήτηση αποτελεσμάτων