Kim Jong Un ampandisha Binti yake Kim Ju Ae kuwa Mrithi wa uongozi wa Korea Kaskazini.
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, anatarajiwa kumtangaza rasmi Binti yake, Kim Ju Ae, kuwa Mrithi wake wa uongozi wa taifa hilo lenye utawala wa kifamilia unaodumu kwa miongo kadhaa.
Hatua hiyo, iwapo itathibitishwa rasmi, itaashiria mabadiliko makubwa katika siasa za Pyongyang, ambako uongozi umekuwa ukirithishwa ndani ya familia ya Kim tangu kuanzishwa kwa taifa hilo mwaka 1948.
Kwa mujibu wa taarifa zinazoibuka kutoka duru za kisiasa na Wachambuzi wa masuala ya Korea Kaskazini, Kim Jong Un anaelekea kumpa Binti yake nafasi ya juu katika mfumo wa uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Korea, hatua itakayomuweka wazi kama Mrithi halali wa madaraka.
Chanzo kimoja cha kisiasa kimenukuliwa kikisema: "Maandalizi ya kumtambulisha Kim Ju Ae kama Mrithi yamekuwa yakifanyika kimyakimya kwa muda sasa."
Katika miezi ya hivi karibuni, Kim Ju Ae ameonekana mara kadhaa katika hafla za kijeshi na kitaifa akiwa sambamba na Baba yake, jambo lililotafsiriwa na Wachambuzi kama ishara ya maandalizi ya kisiasa.
Mchambuzi mmoja wa siasa za Asia Mashariki amesema: "Kuonekana kwake hadharani katika matukio ya kijeshi ni ujumbe wa wazi kwa ndani na nje ya nchi kwamba anajengwa kama kiongozi ajaye."
Iwapo Kim Ju Ae atatangazwa rasmi kuwa Mrithi, atakuwa Mwanamke wa kwanza katika historia ya Korea Kaskazini kurithi uongozi wa taifa hilo linaloongozwa kwa mfumo wa kifalme wa kisiasa.
Hata hivyo, serikali ya Korea Kaskazini bado haijatoa tamko rasmi kuthibitisha hatua hiyo.
Wachambuzi wanaamini kuwa tangazo rasmi linaweza kuwa na athari kubwa kwa siasa za ndani ya nchi pamoja na uhusiano wa kimataifa, hasa kwa mataifa yenye mvutano wa muda mrefu na Pyongyang.
Kwa sasa, dunia inasubiri kuona ikiwa hatua hiyo itathibitishwa rasmi na mamlaka za Korea Kaskazini.
Toa maoni yako
#Habari

0 Commenti
0 condivisioni
3 Views