• Isak aanza mazoezi na wachezaji wenzake wa Liverpool

    Mshambuliaji wa Liverpool, Alexander Isak, ameanza rasmi mazoezi na kikosi cha Liverpool.

    Mchezaji huyo wa Kiswidi alikamilisha usajili wa rekodi ya Uingereza wa £125 milioni kutoka Newcastle katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili, kisha akaungana na timu ya taifa ya Sweden kwa mechi za kimataifa za Septemba.

    Isak alicheza dakika 18 tu katika mechi mbili ambazo Sweden haikushinda dhidi ya Slovenia na Kosovo, lakini sasa ameonekana akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wapya wa klabu ya Liverpool.

    Huenda Isak akacheza mechi yake ya kwanza kwa Liverpool dhidi ya Burnley siku ya jumapili hii.
    👀Isak aanza mazoezi na wachezaji wenzake wa Liverpool 👉Mshambuliaji wa Liverpool, Alexander Isak, ameanza rasmi mazoezi na kikosi cha Liverpool. 👉Mchezaji huyo wa Kiswidi alikamilisha usajili wa rekodi ya Uingereza wa £125 milioni kutoka Newcastle katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili, kisha akaungana na timu ya taifa ya Sweden kwa mechi za kimataifa za Septemba. 👉Isak alicheza dakika 18 tu katika mechi mbili ambazo Sweden haikushinda dhidi ya Slovenia na Kosovo, lakini sasa ameonekana akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wapya wa klabu ya Liverpool. 👉Huenda Isak akacheza mechi yake ya kwanza kwa Liverpool dhidi ya Burnley siku ya jumapili hii.
    0 Commentarii ·0 Distribuiri ·193 Views
  • SAKATA LA JASUSI SERGEI SKRIPAL NA MWANAE NI UTEKELEZAJI WA OPERATION SARLISBURY ILIYOTEKELEZWA NA RUSSIA, KIMSIMGI NI VITA KATI YA URUSI NA NATO KUJIBU MAPIGO YA UCHAGUZI WA MAREKANI MWAKA 2016.

    Na mhariri wako Comred Mbwana Allyamtu

    Sakata la jaribio la mauaji ya jasusi au mpelelezi, ndumilakuwili wa Urusi na Uingereza, Sergei Skripal na binti yake Yulia katika kitongoji cha Salisbury jijini London nchini Uingereza linachukua sura mpya kila siku.

    Wawili hao walipatikana wakiwa hawajitambui katika eneo la maduka liitwalo Maltings mwanzoni mwa Machi.

    Taarifa kutoka kwa polisi wa Uingereza ambao hushughulikia matukio ya kigaidi wanaamini kuwa jasusi huyo na mwanaye, walivuta hewa iliyokuwa na kemikali yenye sumu iitwayo novichok.

    Kemikali hii hushambulia mfumo wa mfahamu na inasemekana ilitengenezwa katika maabara moja huko Urusi na ilitumika wakati wa Vita vya Pili vya Dunia mwaka 1935 hadi 1945. Kemikali hiyo iliachwa mlangoni mwa nyumba ambayo amekuwa akiishi jasusi huyo na mwanaye katika eneo hilo la Salisbury.

    Mashirika makubwa ya habari nchini Uingereza yameipa umuhimu habari hii ambapo Machi 30, yalitangaza kuwa binti wa Skripal, Yulia hakuwa katika hali tete kiafya.

    Kufuatia tukio hilo Serikali ya Uingereza chini ya Waziri Mkuu, Theresa May iliitupia lawama Serikali ya Urusi kwa kuhusika na uovu huo na ili kuonyesha kuwa imechukia iliamua kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi wapatao 23.

    Urusi imekanusha kuhusika na uovu huo na ikaahidi kuwa kwa kila hukumu itakayotolewa nayo itajibu kwa ukubwa huohuo au zaidi ya hapo, na ikajibu kwa kutoa hukumu ya kisasi kwa kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza na kufunga kituo cha Lugha na Utamaduni cha Uingereza, British Council na imeitaka Uingereza kuwaondoa wanadiplomasia wake wengine wapatao 50 katika kipindi cha mwezi mmoja.
    Ili kuonyesha mshikamano na Uingereza nchi nyingine za Ulaya Magharibi na Australia zimewafukuza wanadiplomasia wa Urusi wanaofikia 150 huku Marekani ikiongoza kwa kufunga ubalozi mdogo wa Urusi katika Jiji la Seattle na kuwafukuza wanadiplomasia 60 kutoka nchi hiyo.

    Urusi nayo haikubaki kimya, Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov ametangaza kuwafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani na vilevile kufunga ubalozi wa Marekani katika mji wa Saint Petersburg na kuahidi kuwa kila nchi iliyohusika na kufukuza wanadiplomasia wake itaadhibiwa vilivyo.

    Kwa ujumla nchi karibu 23 na Umoja wa Kujihami wa nchi za Ulaya Magharibi (Nato) kote ulimwenguni zimeonyesha kukerwa na vitendo vya Urusi kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi tofautitofauti, kama vile kuvamia Ukraine na kulichukua jimbo la Krimea, kuitungua ndege ya Malaysia na kuingilia uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka 2016.
    Siyo mara ya kwanza nchi hizi kuingia katika mzozo wa kidiplomasia kwani mwaka 1986 Ronald Reagan aliyekuwa Rais wa Marekani, aliamuru wanadiplomasia 80 wa Shirikisho la Urusi (USSR) wafukuzwe nchini humo na mwaka 2016, Rais Barak Obama aliwatimua wanadiplomasia 35 kutoka nchi hiyo kwa tuhuma za kudukua kompyuta za chama cha Democratic kwa nia ya kumhujumu mgombea wake wa Rais, Hillary Clinton.

    Mwaka 2006 Skripal alihukumiwa kifungo cha miaka 13, nchini Urusi katika kesi ambayo iliendeshwa katika mahakama ya siri, alipewa haki ya ukimbizi na ukazi nchini Uingereza mwaka 2010 baada ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa katika mtindo ambao ulitumika enzi za vita baridi kuhusiana na shughuli za kijasusi.

    Kulingana na nyaraka za kumbukumbu ambazo vyombo vya habari vya Uingereza vilizipata kutoka makumbusho ya taifa ya Uingereza mwaka 2015, zinaonyesha kuwa Serikali ya Urusi imekuwa ikiichunguza Uingereza muda mrefu lakini kisa kinachojulikana sana ni kile kilichopewa jina la Cambridge Four, ambapo kitengo cha ujasusi cha shirikisho la Urusi (USSR), KGB, katika miaka ya 1930 kabla ya vita vya pili vya dunia kiligundua kuwa Serikali ya Uingereza ilikuwa ikitumia Chuo Kikuu cha Cambridge kama sehemu maalumu ya kuwapata majasusi wachanga wakiwa masomoni. KGB waliwafuata wanafunzi wanne wa wakati huo ambao ni Anthony Blunt, Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess.
    Wasomi hao ambao kwa bahati nzuri kwao KGB walipomaliza masomo yao waliingia kufanya kazi katika Mashirika ya Ujasusi ya Uingereza, MI5 na MI6, na wakawa ni majasusi ndumilakuwili.

    Walifanya kazi yao hadi mwaka 1964 ambapo Anthony Blunt ambaye alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Ujasusi wa ndani, MI5, alikiri kuwa jasusi ndumilakuwili ili asishtakiwe na habari hiyo ilikuja kutolewa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo, Magreth Thatcher alipokuwa akihutubia Bunge mwaka 1979. Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess wao walitimkia Urusi na Serikali ya Uingereza ikawa imekubali yaiishe.

    Kwa hiyo Urusi imekuwa hailali usingizi wakati wote wa miaka ya vita baridi kati ya nchi za Ulaya Mashariki na Magharibi miaka ya 1945 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990, imekuwa ikiingiza wapelelezi wake maeneo mbalimbali katika nchi hizo ili kupata habari nyeti kuhusiana na masuala mbalimbali katika nyanja za uchumi, biashara hasa ya silaha na teknolojia yake na hivi karibuni kuingilia mambo ya siasa za uchaguzi huko Marekani.
    Ukiangalia kisa cha safari hii hakina tofauti sana kile alichofanyiwa Jasusi mwingine wa Urusi Novemba 2006, Alexander Litvinenko ambaye aliwekewa kemikali iitwayo Polonium 210 katika kikombe cha chai katika mgahawa mmoja jijini London.

    Litvinenko alitoroka Urusi baada ya kutofautiana na wenzake katika shirika la kijasusi la nchi hiyo FSB, ambapo aliutuhumu uongozi wa juu wa nchi hiyo kuigeuza nchi hiyo kuwa Taifa la kimafia. akiwa nchini Uingereza, alifanya kazi kama mwandishi wa habari, vitabu na mshauri wa mambo ya usalama.
    Akiwa Uingereza aliandika vitabu viwili, Blowing up Russia: Terror from within na Lubyanka Criminal Group ambapo aliituhumu idara hiyo ya kijasusi kwa vitendo vya mauaji na matumizi ya mabomu na mauaji ya mwandishi wa habari, Anna Politkovskaya kwa amri kutoka kwa Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin.

    Litvinenko akiwa mahututi kitandani hospitalini jijini London aliwatamkia ndugu zake kuwa alikuwa na uhakika kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin ndiye aliyeamuru auawe.
    Serikali ya Uingereza ya wakati huo chini ya Waziri Mkuu, Tony Blair ilifanya upelelezi na kugundua kuwa jasusi huyo siku chache kabla ya kupata mkasa huo alikuwa ametembelewa na jasusi mwingine mstaafu wa FSB ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara, Andrey Lugovoy.
    Serikali ya Uingereza iliitaka Urusi imsalimishe kwake ili afanyiwe mahojiano lakini Urusi ilikataa kwa maelezo kuwa Katiba ya nchi hiyo inakataza raia wake kupelekwa nchi nyingine kufanyiwa mashtaka ya jinai. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulififia kwa muda.

    Serikali ya Uingereza kwa matukio yote haya imekuwa ikiituhumu serikali ya Urusi kwa kile inachoeleza kuwa kemikali hizo haziwezi kuwa mikononi mwa mtu binafsi bila kuwa na kibari cha mamlaka za juu za nchi hiyo.

    Wakati Kim Phillby alipokimbilia Urusi baada ya kushtukia kuwa wenzake walikuwa wanaelekea kumgundua kuwa ni ndumilakuwili, Ofisa mmoja wa ngazi ya juu ndani ya KGB wakati huo alimsifu kuwa alikuwa jasusi mwenye thamani kubwa wa karne iliyopita.

    Urusi imekuwa ikitoa ulinzi wa kiwango cha juu kwa majasusi ndumilakuwili ambao wamefanikiwa kuingia nchini humo baada ya mambo kwenda kombo huko kwao.

    Marekani nayo haikuwahi kupona kwa taasisi zake za kijasusi kuingiliwa na wenzao wa Urusi. Mwaka 2001 Shirika la Ujasusi wa Ndani, FBI, lilimkamata Robert Hanssen ambaye alikuwa mtumishi wake kwa kupeleka taarifa za siri za nchi hiyo kwa Urusi tangu mwaka 1979 kwa kulipwa fedha na almasi.

    Kwa sehemu kubwa shughuli za ujasusi zimekuwa zikifanywa kwa njia ya teknolojia (Artificial Intelligence) ambapo mitambo ya kompyuta na setelaiti na kamera zenye nguvu za kunasa picha hutumika na pale ambapo haiwezekani, inabidi kutumia binadamu (human intelligence) ili kupata habari ambazo ni siri na mataifa karibu yote duniani yameuweka ujasusi kama ni kosa la uhaini kwa yeyote atakayejihusisha nao.
    SAKATA LA JASUSI SERGEI SKRIPAL NA MWANAE NI UTEKELEZAJI WA OPERATION SARLISBURY ILIYOTEKELEZWA NA RUSSIA, KIMSIMGI NI VITA KATI YA URUSI NA NATO KUJIBU MAPIGO YA UCHAGUZI WA MAREKANI MWAKA 2016. Na mhariri wako Comred Mbwana Allyamtu Sakata la jaribio la mauaji ya jasusi au mpelelezi, ndumilakuwili wa Urusi na Uingereza, Sergei Skripal na binti yake Yulia katika kitongoji cha Salisbury jijini London nchini Uingereza linachukua sura mpya kila siku. Wawili hao walipatikana wakiwa hawajitambui katika eneo la maduka liitwalo Maltings mwanzoni mwa Machi. Taarifa kutoka kwa polisi wa Uingereza ambao hushughulikia matukio ya kigaidi wanaamini kuwa jasusi huyo na mwanaye, walivuta hewa iliyokuwa na kemikali yenye sumu iitwayo novichok. Kemikali hii hushambulia mfumo wa mfahamu na inasemekana ilitengenezwa katika maabara moja huko Urusi na ilitumika wakati wa Vita vya Pili vya Dunia mwaka 1935 hadi 1945. Kemikali hiyo iliachwa mlangoni mwa nyumba ambayo amekuwa akiishi jasusi huyo na mwanaye katika eneo hilo la Salisbury. Mashirika makubwa ya habari nchini Uingereza yameipa umuhimu habari hii ambapo Machi 30, yalitangaza kuwa binti wa Skripal, Yulia hakuwa katika hali tete kiafya. Kufuatia tukio hilo Serikali ya Uingereza chini ya Waziri Mkuu, Theresa May iliitupia lawama Serikali ya Urusi kwa kuhusika na uovu huo na ili kuonyesha kuwa imechukia iliamua kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi wapatao 23. Urusi imekanusha kuhusika na uovu huo na ikaahidi kuwa kwa kila hukumu itakayotolewa nayo itajibu kwa ukubwa huohuo au zaidi ya hapo, na ikajibu kwa kutoa hukumu ya kisasi kwa kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza na kufunga kituo cha Lugha na Utamaduni cha Uingereza, British Council na imeitaka Uingereza kuwaondoa wanadiplomasia wake wengine wapatao 50 katika kipindi cha mwezi mmoja. Ili kuonyesha mshikamano na Uingereza nchi nyingine za Ulaya Magharibi na Australia zimewafukuza wanadiplomasia wa Urusi wanaofikia 150 huku Marekani ikiongoza kwa kufunga ubalozi mdogo wa Urusi katika Jiji la Seattle na kuwafukuza wanadiplomasia 60 kutoka nchi hiyo. Urusi nayo haikubaki kimya, Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov ametangaza kuwafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani na vilevile kufunga ubalozi wa Marekani katika mji wa Saint Petersburg na kuahidi kuwa kila nchi iliyohusika na kufukuza wanadiplomasia wake itaadhibiwa vilivyo. Kwa ujumla nchi karibu 23 na Umoja wa Kujihami wa nchi za Ulaya Magharibi (Nato) kote ulimwenguni zimeonyesha kukerwa na vitendo vya Urusi kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi tofautitofauti, kama vile kuvamia Ukraine na kulichukua jimbo la Krimea, kuitungua ndege ya Malaysia na kuingilia uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka 2016. Siyo mara ya kwanza nchi hizi kuingia katika mzozo wa kidiplomasia kwani mwaka 1986 Ronald Reagan aliyekuwa Rais wa Marekani, aliamuru wanadiplomasia 80 wa Shirikisho la Urusi (USSR) wafukuzwe nchini humo na mwaka 2016, Rais Barak Obama aliwatimua wanadiplomasia 35 kutoka nchi hiyo kwa tuhuma za kudukua kompyuta za chama cha Democratic kwa nia ya kumhujumu mgombea wake wa Rais, Hillary Clinton. Mwaka 2006 Skripal alihukumiwa kifungo cha miaka 13, nchini Urusi katika kesi ambayo iliendeshwa katika mahakama ya siri, alipewa haki ya ukimbizi na ukazi nchini Uingereza mwaka 2010 baada ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa katika mtindo ambao ulitumika enzi za vita baridi kuhusiana na shughuli za kijasusi. Kulingana na nyaraka za kumbukumbu ambazo vyombo vya habari vya Uingereza vilizipata kutoka makumbusho ya taifa ya Uingereza mwaka 2015, zinaonyesha kuwa Serikali ya Urusi imekuwa ikiichunguza Uingereza muda mrefu lakini kisa kinachojulikana sana ni kile kilichopewa jina la Cambridge Four, ambapo kitengo cha ujasusi cha shirikisho la Urusi (USSR), KGB, katika miaka ya 1930 kabla ya vita vya pili vya dunia kiligundua kuwa Serikali ya Uingereza ilikuwa ikitumia Chuo Kikuu cha Cambridge kama sehemu maalumu ya kuwapata majasusi wachanga wakiwa masomoni. KGB waliwafuata wanafunzi wanne wa wakati huo ambao ni Anthony Blunt, Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess. Wasomi hao ambao kwa bahati nzuri kwao KGB walipomaliza masomo yao waliingia kufanya kazi katika Mashirika ya Ujasusi ya Uingereza, MI5 na MI6, na wakawa ni majasusi ndumilakuwili. Walifanya kazi yao hadi mwaka 1964 ambapo Anthony Blunt ambaye alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Ujasusi wa ndani, MI5, alikiri kuwa jasusi ndumilakuwili ili asishtakiwe na habari hiyo ilikuja kutolewa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo, Magreth Thatcher alipokuwa akihutubia Bunge mwaka 1979. Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess wao walitimkia Urusi na Serikali ya Uingereza ikawa imekubali yaiishe. Kwa hiyo Urusi imekuwa hailali usingizi wakati wote wa miaka ya vita baridi kati ya nchi za Ulaya Mashariki na Magharibi miaka ya 1945 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990, imekuwa ikiingiza wapelelezi wake maeneo mbalimbali katika nchi hizo ili kupata habari nyeti kuhusiana na masuala mbalimbali katika nyanja za uchumi, biashara hasa ya silaha na teknolojia yake na hivi karibuni kuingilia mambo ya siasa za uchaguzi huko Marekani. Ukiangalia kisa cha safari hii hakina tofauti sana kile alichofanyiwa Jasusi mwingine wa Urusi Novemba 2006, Alexander Litvinenko ambaye aliwekewa kemikali iitwayo Polonium 210 katika kikombe cha chai katika mgahawa mmoja jijini London. Litvinenko alitoroka Urusi baada ya kutofautiana na wenzake katika shirika la kijasusi la nchi hiyo FSB, ambapo aliutuhumu uongozi wa juu wa nchi hiyo kuigeuza nchi hiyo kuwa Taifa la kimafia. akiwa nchini Uingereza, alifanya kazi kama mwandishi wa habari, vitabu na mshauri wa mambo ya usalama. Akiwa Uingereza aliandika vitabu viwili, Blowing up Russia: Terror from within na Lubyanka Criminal Group ambapo aliituhumu idara hiyo ya kijasusi kwa vitendo vya mauaji na matumizi ya mabomu na mauaji ya mwandishi wa habari, Anna Politkovskaya kwa amri kutoka kwa Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin. Litvinenko akiwa mahututi kitandani hospitalini jijini London aliwatamkia ndugu zake kuwa alikuwa na uhakika kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin ndiye aliyeamuru auawe. Serikali ya Uingereza ya wakati huo chini ya Waziri Mkuu, Tony Blair ilifanya upelelezi na kugundua kuwa jasusi huyo siku chache kabla ya kupata mkasa huo alikuwa ametembelewa na jasusi mwingine mstaafu wa FSB ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara, Andrey Lugovoy. Serikali ya Uingereza iliitaka Urusi imsalimishe kwake ili afanyiwe mahojiano lakini Urusi ilikataa kwa maelezo kuwa Katiba ya nchi hiyo inakataza raia wake kupelekwa nchi nyingine kufanyiwa mashtaka ya jinai. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulififia kwa muda. Serikali ya Uingereza kwa matukio yote haya imekuwa ikiituhumu serikali ya Urusi kwa kile inachoeleza kuwa kemikali hizo haziwezi kuwa mikononi mwa mtu binafsi bila kuwa na kibari cha mamlaka za juu za nchi hiyo. Wakati Kim Phillby alipokimbilia Urusi baada ya kushtukia kuwa wenzake walikuwa wanaelekea kumgundua kuwa ni ndumilakuwili, Ofisa mmoja wa ngazi ya juu ndani ya KGB wakati huo alimsifu kuwa alikuwa jasusi mwenye thamani kubwa wa karne iliyopita. Urusi imekuwa ikitoa ulinzi wa kiwango cha juu kwa majasusi ndumilakuwili ambao wamefanikiwa kuingia nchini humo baada ya mambo kwenda kombo huko kwao. Marekani nayo haikuwahi kupona kwa taasisi zake za kijasusi kuingiliwa na wenzao wa Urusi. Mwaka 2001 Shirika la Ujasusi wa Ndani, FBI, lilimkamata Robert Hanssen ambaye alikuwa mtumishi wake kwa kupeleka taarifa za siri za nchi hiyo kwa Urusi tangu mwaka 1979 kwa kulipwa fedha na almasi. Kwa sehemu kubwa shughuli za ujasusi zimekuwa zikifanywa kwa njia ya teknolojia (Artificial Intelligence) ambapo mitambo ya kompyuta na setelaiti na kamera zenye nguvu za kunasa picha hutumika na pale ambapo haiwezekani, inabidi kutumia binadamu (human intelligence) ili kupata habari ambazo ni siri na mataifa karibu yote duniani yameuweka ujasusi kama ni kosa la uhaini kwa yeyote atakayejihusisha nao.
    0 Commentarii ·0 Distribuiri ·2K Views
  • JINSI SHIRIKA LA KIJASUSI LA URUSI FSB {KGB} LILIVYO HATARI....

    Kama waswahili wasemavyo maisha ni safari ndefu na kifo ni Siri, pengine hili ni kweli kutokana na sintofahamu iliyochukua uhai wa Alexander Litvinenko, jasusi wa zamañi wa KGB na baadae FSB ya Urusi ya sasa.

    Tutarudi Sasa tuendelee mwishoni mwa wiki za mwezi wa kumi mwaka 2006 Alexander Litvinenko alipokuwa jijini London alipotorokea baada ya rabsha dhidi ya serikali mjini Moscow, siku hiyo Litvinenko alikuwa ametembelewa na marafiki zake wawili walikuwa wanausalama ndani ya FSB na iliyokuwa KGB Dmitri Kovtun na Andrei Lugovoi, asichokijua ni kwamba wale wawili walikuwa moja ya watu hatari na pia kama wasafirishaji mahiri wa msafiri kama Litvinenko kuliendelea kaburi

    Waliikutana hotelini jijini London wakinywa na kufurahi, siku hiyo Lugovoi na Kovtun wao waliagiza bia wakanywa wakifurahi, unajua nini Litvinenko ye aliagizwa chai ya rangi akanywa huku akiwachekea wasafirishaji wa ule msemo wa kiswahili " maisha ni safari"

    Maskinii Litvinenko alipojichanganya tu Lugovoi na Kovtun wakifanya kazi yao moja waliotumwa na FSB, kumnyamazisha " traitor of the mother Russia"

    Unajua walifanya Nini? Walichukua kemikali hatari sana duniani inayoua taratibu sana jina lake Polonium 210 wakatia katika chai ya Litvinenko. Inavyosemekana alivyorudi walimchekea na kufurahi zaidi kuona Litvinenko alikuwa amesahau mbinu muhimu kabisa ya wanaintelijensia kote duniani ! Kutomwamini mtu hata mama na baba yako.
    Litvinenko alikunywa chai ile

    **********
    Lugovoi na Kovtun walichukua ndege siku tatu baadae haoo Moscow, huko walifanyiwa sherehe ya uhakika wa kazi iliyofanyika isiyo na shaka, Kovtun aliamua kuwa mfanyabiashara mkubwa wakati Lugovoi alipandishwa cheo siku chache baadae.
    ******
    Maskini Litvinenko aliagana na wanyama wale wa kwenye barafu Kama wajiitavyo wao " "bear " lakini akiwapachika majina mazuri yaani marafiki, ndugu, wapenzi kutoka home Russia. Pia aliwauliza vipi watarudi lini kumuona, kimoyomoyo Kovtun na Lugovoi walikua wakicheka na kusikitika kiunafiki,wakijua huyu mtu hana mwezi duniani. Wiki tatu nyingi! atakufa kifo Cha mateso akiwa kitandani amelala.

    ***
    November 1 mwaka 2006 Litvinenko aliugua homa ya ghafla mwili ukiungua kwa namna ya kutisha sana, alipelekwa hospitali mjini London akaishi kwa wiki 3 akiwa hoi kitandani! Wakati akifa akitoa laana kwa Putin akamshutumu amemuua.

    Huo ukawa mwisho wa Litvinenko mtu aliyekuwa ameaminiwa kutunza siri za Russia yeye alizitoa hadharani kwa m16 . Pengine ni chafu sana zenye damu lakini bila shaka kulikuwa pigo kwa vitu hivyo kuwa hadharani. Putin alivuliwa nguo hata asiijifunike.

    Tuzungimzapo Leo ni miaka karibu 12 toka mnyama huyu atutoke.

    Mwaka fulani Putin aliulizwa na mwanahabari mmoja ni kitu gani asichoweza kuvumilia na kusamehe alisema hivi.. Ye ni ngumu sana kuwasamehe wasaliti wa mother Russia.

    Ohh ndo hivyo Litvinenko hakupata bahati ya kusamehewa na Putin hivyo alikwenda.

    Chanzo: na Google
    JINSI SHIRIKA LA KIJASUSI LA URUSI FSB {KGB} LILIVYO HATARI.... Kama waswahili wasemavyo maisha ni safari ndefu na kifo ni Siri, pengine hili ni kweli kutokana na sintofahamu iliyochukua uhai wa Alexander Litvinenko, jasusi wa zamañi wa KGB na baadae FSB ya Urusi ya sasa. Tutarudi Sasa tuendelee mwishoni mwa wiki za mwezi wa kumi mwaka 2006 Alexander Litvinenko alipokuwa jijini London alipotorokea baada ya rabsha dhidi ya serikali mjini Moscow, siku hiyo Litvinenko alikuwa ametembelewa na marafiki zake wawili walikuwa wanausalama ndani ya FSB na iliyokuwa KGB Dmitri Kovtun na Andrei Lugovoi, asichokijua ni kwamba wale wawili walikuwa moja ya watu hatari na pia kama wasafirishaji mahiri wa msafiri kama Litvinenko kuliendelea kaburi Waliikutana hotelini jijini London wakinywa na kufurahi, siku hiyo Lugovoi na Kovtun wao waliagiza bia wakanywa wakifurahi, unajua nini Litvinenko ye aliagizwa chai ya rangi akanywa huku akiwachekea wasafirishaji wa ule msemo wa kiswahili " maisha ni safari" Maskinii Litvinenko alipojichanganya tu Lugovoi na Kovtun wakifanya kazi yao moja waliotumwa na FSB, kumnyamazisha " traitor of the mother Russia" Unajua walifanya Nini? Walichukua kemikali hatari sana duniani inayoua taratibu sana jina lake Polonium 210 wakatia katika chai ya Litvinenko. Inavyosemekana alivyorudi walimchekea na kufurahi zaidi kuona Litvinenko alikuwa amesahau mbinu muhimu kabisa ya wanaintelijensia kote duniani ! Kutomwamini mtu hata mama na baba yako. Litvinenko alikunywa chai ile ********** Lugovoi na Kovtun walichukua ndege siku tatu baadae haoo Moscow, huko walifanyiwa sherehe ya uhakika wa kazi iliyofanyika isiyo na shaka, Kovtun aliamua kuwa mfanyabiashara mkubwa wakati Lugovoi alipandishwa cheo siku chache baadae. ****** Maskini Litvinenko aliagana na wanyama wale wa kwenye barafu Kama wajiitavyo wao " "bear " lakini akiwapachika majina mazuri yaani marafiki, ndugu, wapenzi kutoka home Russia. Pia aliwauliza vipi watarudi lini kumuona, kimoyomoyo Kovtun na Lugovoi walikua wakicheka na kusikitika kiunafiki,wakijua huyu mtu hana mwezi duniani. Wiki tatu nyingi! atakufa kifo Cha mateso akiwa kitandani amelala. *** November 1 mwaka 2006 Litvinenko aliugua homa ya ghafla mwili ukiungua kwa namna ya kutisha sana, alipelekwa hospitali mjini London akaishi kwa wiki 3 akiwa hoi kitandani! Wakati akifa akitoa laana kwa Putin akamshutumu amemuua. Huo ukawa mwisho wa Litvinenko mtu aliyekuwa ameaminiwa kutunza siri za Russia yeye alizitoa hadharani kwa m16 . Pengine ni chafu sana zenye damu lakini bila shaka kulikuwa pigo kwa vitu hivyo kuwa hadharani. Putin alivuliwa nguo hata asiijifunike. Tuzungimzapo Leo ni miaka karibu 12 toka mnyama huyu atutoke. Mwaka fulani Putin aliulizwa na mwanahabari mmoja ni kitu gani asichoweza kuvumilia na kusamehe alisema hivi.. Ye ni ngumu sana kuwasamehe wasaliti wa mother Russia. Ohh ndo hivyo Litvinenko hakupata bahati ya kusamehewa na Putin hivyo alikwenda. Chanzo: na Google
    0 Commentarii ·0 Distribuiri ·2K Views
  • Zana 10 Bora Za Ai Kwaajili yakuchuma pesa

    Momen: Unda programu za wavuti kwa kasi zaidi bila msimbo. momen.app

    2. Midjourney: Tengeneza picha za ubora wa juu ukitumia Midjourney. midjourney.com

    3. Figma: Figma ni programu shirikishi ya wavuti kwa muundo wa kiolesura. figma.com

    4. Tovuti ya Kutua: Mjenzi wa tovuti ya AI. landingsite.ai

    5. Mzinga wa Nyuki: Jukwaa la jarida la AI lililojengwa kwa ukuaji. beehiiv.com

    6. Claude AI: Claude ni msaidizi wa AI wa kizazi kijacho kwa kazi zako. claude.ai

    7. Looks: Jenereta bora ya nembo ya AI. looka.com

    8. Codeium: Nguvu kuu ya kisasa ya kusimba AI. codeium.com

    9. Picha: Pictory ni jenereta ya video ya AI. pictory.ai

    10. Lovo.ai: Lovo AI ni jenereta ya sauti inayotokana na AI iliyoshinda tuzo na jukwaa la maandishi-kwa-hotuba.

    #Ai
    #everyonefollowers
    #highlightseveryonefollowers2024
    Zana 10 Bora Za Ai Kwaajili yakuchuma pesa🌐 Momen: Unda programu za wavuti kwa kasi zaidi bila msimbo. 👉 momen.app 2. Midjourney: Tengeneza picha za ubora wa juu ukitumia Midjourney. 👉midjourney.com 3. Figma: Figma ni programu shirikishi ya wavuti kwa muundo wa kiolesura. 👉 figma.com 4. Tovuti ya Kutua: Mjenzi wa tovuti ya AI. 👉 landingsite.ai 5. Mzinga wa Nyuki: Jukwaa la jarida la AI lililojengwa kwa ukuaji. 👉 beehiiv.com 6. Claude AI: Claude ni msaidizi wa AI wa kizazi kijacho kwa kazi zako. 👉 claude.ai 7. Looks: Jenereta bora ya nembo ya AI. 👉 looka.com 8. Codeium: Nguvu kuu ya kisasa ya kusimba AI. 👉 codeium.com 9. Picha: Pictory ni jenereta ya video ya AI. 👉 pictory.ai 10. Lovo.ai: Lovo AI ni jenereta ya sauti inayotokana na AI iliyoshinda tuzo na jukwaa la maandishi-kwa-hotuba. #Ai #everyonefollowers #highlightseveryonefollowers2024
    Like
    Love
    2
    · 0 Commentarii ·0 Distribuiri ·2K Views
  • Rapa Kendrick Lamar ameachia video ya “Not Like Us” ambayo ni diss-track kwa rapa kutoka Canada Aubrey Drake Graham. Video hio imepata mapokezi makubwa kwani ndani ya masaa machache imefanikiwa kujikusanyia watazamaji milioni 17 kupitia chaneli yake ya Youtube.

    Licha ya mistari kuntu iliyo ndani ya wimbo huo kumchana vibaya Drake, Kendrick ameonyesha hasira yake wazi hata kupitia video hiyo baada ya kuonekana akipiga mfano wa bundi ambao ndege huyo hutumika kama logo ya lebo ya OVO ya mhasimu wake Drake.

    #CrownMuziki #HapaNiNyumbani
    Rapa Kendrick Lamar ameachia video ya “Not Like Us” ambayo ni diss-track kwa rapa kutoka Canada Aubrey Drake Graham. Video hio imepata mapokezi makubwa kwani ndani ya masaa machache imefanikiwa kujikusanyia watazamaji milioni 17 kupitia chaneli yake ya Youtube. Licha ya mistari kuntu iliyo ndani ya wimbo huo kumchana vibaya Drake, Kendrick ameonyesha hasira yake wazi hata kupitia video hiyo baada ya kuonekana akipiga mfano wa bundi ambao ndege huyo hutumika kama logo ya lebo ya OVO ya mhasimu wake Drake. #CrownMuziki #HapaNiNyumbani
    Like
    Love
    2
    · 0 Commentarii ·0 Distribuiri ·1K Views ·16
  • MECHI ZA LEO IJUMAA

    King Cup - Final:
    20:00 Al Hilal - Al Nassr

    Club Friendly:
    13:00 AS Roma - AC Milan

    Superliga - CL Final:
    19:00 FC Copenhagen - Randers FC

    Egypt Cup:
    16:00 Baladiyat El Mahalla - El Gouna
    16:00 National Bank Egypt - Petrojet

    Euro Women - Qualification:
    18:00 Austria - Iceland
    18:00 Norway - Italy
    18:30 Czech Republic - Belgium
    19:00 Denmark - Spain
    20:30 Germany - Poland
    20:30 Iceland - Sweden
    20:45 Netherlands - Finland
    21:00 England - France

    Euro Women - Qualification:
    17:00 Kosovo - Croatia
    18:00 Serbia - Slovakia
    19:00 Turkey - Azerbaijan
    19:30 Malta - Bosnia & Herzegovina
    20:00 Switzerland - Hungary
    20:05 Scotland - Israel
    20:15 Wales - Ukraine
    21:45 Portugal - Northern Ireland

    Euro Women - Qualification:
    15:00 Armenia - Kazakhstan
    17:00 Estonia - Albania
    17:00 Greece - Montenegro
    17:00 North Macedonia - Moldova
    17:45 Faroe Islands - Andorra
    18:00 Cyprus - Georgia
    18:00 Romania - Bulgaria
    18:00 Slovenia - Latvia

    #Sportsviews
    MECHI ZA LEO IJUMAA 🇸🇦 King Cup - Final: 20:00 Al Hilal - Al Nassr 🌎 Club Friendly: 13:00 AS Roma - AC Milan 🇩🇰 Superliga - CL Final: 19:00 FC Copenhagen - Randers FC 🇪🇬 Egypt Cup: 16:00 Baladiyat El Mahalla - El Gouna 16:00 National Bank Egypt - Petrojet 🇪🇺 Euro Women - Qualification: 18:00 🇦🇹 Austria - Iceland 🇮🇸 18:00 🇳🇴 Norway - Italy 🇮🇹 18:30 🇨🇿 Czech Republic - Belgium 🇧🇪 19:00 🇩🇰 Denmark - Spain 🇪🇸 20:30 🇩🇪 Germany - Poland 🇵🇱 20:30 🇮🇪 Iceland - Sweden 🇸🇪 20:45 🇳🇱 Netherlands - Finland 🇫🇮 21:00 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 England - France 🇫🇷 🇪🇺 Euro Women - Qualification: 17:00 🇽🇰 Kosovo - Croatia 🇭🇷 18:00 🇷🇸 Serbia - Slovakia 🇸🇰 19:00 🇹🇷 Turkey - Azerbaijan 🇦🇿 19:30 🇲🇹 Malta - Bosnia & Herzegovina 🇧🇦 20:00 🇨🇭 Switzerland - Hungary 🇭🇺 20:05 🏴󠁧󠁢󠁳󠁣󠁴󠁿 Scotland - Israel 🇮🇱 20:15 🏴󠁧󠁢󠁷󠁬󠁳󠁿 Wales - Ukraine 🇺🇦 21:45 🇵🇹 Portugal - Northern Ireland 🇬🇧 🇪🇺 Euro Women - Qualification: 15:00 🇦🇲 Armenia - Kazakhstan 🇰🇿 17:00 🇪🇪 Estonia - Albania 🇦🇱 17:00 🇬🇷 Greece - Montenegro 🇲🇪 17:00 🇲🇰 North Macedonia - Moldova 🇲🇩 17:45 🇫🇴 Faroe Islands - Andorra 🇦🇩 18:00 🇨🇾 Cyprus - Georgia 🇬🇪 18:00 🇷🇴 Romania - Bulgaria 🇧🇬 18:00 🇸🇮 Slovenia - Latvia 🇱🇻 #Sportsviews
    Like
    Love
    7
    · 3 Commentarii ·0 Distribuiri ·2K Views
  • Karibu ujipatie Laptops kuanzia Tsh.300,000/= nakuendelea.
    Hp,Dell,Macbook, Lenovo na Acer.
    Karibu ujipatie Laptops kuanzia Tsh.300,000/= nakuendelea. Hp,Dell,Macbook, Lenovo na Acer.
    Like
    Love
    5
    · 4 Commentarii ·0 Distribuiri ·1K Views