• Habari ya usiku ndugu zangu ni siku ya nne leo japo kwa kuchelewe tunaendelea na mwendelezo wa fasiri za ndoto kiblia .

    *Ungana nami Sylvester Mwakabende kwa ufafanuzi zaidi kadiri roho wa Bwana Atakavyo niongoza*

    *Je umewai kuota unafukuzwa na mbwa ? nini maana yake*? .


    Zaburi 22:16
    *[16]Kwa maana mbwa wamenizunguka Kusanyiko la waovu wamenisonga;
    Wamenizua mikono na miguu*
    For dogs have compassed me: the assembly of the wicked have inclosed me: they pierced my hands and my feet.

    1.Kufuatiliwa na roho chafu kama zinaa na uasherati

    Mithali26:11 SUV

    *Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena.*

    Kutoka 22:31 BHN
    *Nyinyi mtakuwa watu waliowekwa wakfu kwangu. Kwa hiyo hamtakula nyama ya mnyama aliyeuawa na mnyama wa porini. Nyama hiyo mtawatupia mbwa.*

    Chochote kile kilicho kichafu upaswi kukila .

    Torati 23:18 BHN
    *Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yoyote; kwani haya ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako, yote mawili.*
    2wafalme 9;10

    Zaburi 22;20 BHN
    *Iokoe nafsi yangu mbali na upanga, yaokoe maisha yangu makuchani mwa mbwa hao!*

    *Mbwa ana nguvu maana yake mbwa anawakilisha roho chafu za zinaa, uasherati na machafu yote ya shetani .*
    .
    2.kuiacha njia ya bwana kama kuhani.

    Isaya 56:11 BHN
    *Hao ni kama mbwa wenye uchu sana, wala hawawezi kamwe kutoshelezwa. Wachungaji hao hawana akili yoyote; kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe.*

    Naombaje ?NAMNA YA KUOMBA

    1.Toba ya kweli kwa sababu ya kufungua mlango .

    2.kuhalibu kila njia ya uovu inayo kufuatilia

    3.Muone kuhani kwa ajiri ya ukombozi .

    4.kataa kabisa roho za uharibifu kwa kusimamisha madhabau ya Mungu kwa sadaka.

    Zingatia :Ndoto ni mlango Mungu anao utumia kupitisha ujumbe wake na shetani naye anatumia hivyo hivyo jifunze kuomba uongozi wa roho mtakatifu katika fasiri sahiii japo zingine uja kwa uchovu na shughuli nyingi.

    Ok naitwa Sylvester Mwakabende wa (Build new eden)
    Unaweza share somo hili kwa rafiki wengine.
    Simu no :0622625340
    Habari ya usiku ndugu zangu ni siku ya nne leo japo kwa kuchelewe tunaendelea na mwendelezo wa fasiri za ndoto kiblia . *Ungana nami Sylvester Mwakabende kwa ufafanuzi zaidi kadiri roho wa Bwana Atakavyo niongoza* *Je umewai kuota unafukuzwa na mbwa ? nini maana yake*? . Zaburi 22:16 *[16]Kwa maana mbwa wamenizunguka Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenizua mikono na miguu* For dogs have compassed me: the assembly of the wicked have inclosed me: they pierced my hands and my feet. 1.Kufuatiliwa na roho chafu kama zinaa na uasherati Mithali26:11 SUV *Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena.* Kutoka 22:31 BHN *Nyinyi mtakuwa watu waliowekwa wakfu kwangu. Kwa hiyo hamtakula nyama ya mnyama aliyeuawa na mnyama wa porini. Nyama hiyo mtawatupia mbwa.* Chochote kile kilicho kichafu upaswi kukila . Torati 23:18 BHN *Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yoyote; kwani haya ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako, yote mawili.* 2wafalme 9;10 Zaburi 22;20 BHN *Iokoe nafsi yangu mbali na upanga, yaokoe maisha yangu makuchani mwa mbwa hao!* *Mbwa ana nguvu maana yake mbwa anawakilisha roho chafu za zinaa, uasherati na machafu yote ya shetani .* . 2.kuiacha njia ya bwana kama kuhani. Isaya 56:11 BHN *Hao ni kama mbwa wenye uchu sana, wala hawawezi kamwe kutoshelezwa. Wachungaji hao hawana akili yoyote; kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe.* Naombaje ?NAMNA YA KUOMBA 1.Toba ya kweli kwa sababu ya kufungua mlango . 2.kuhalibu kila njia ya uovu inayo kufuatilia 3.Muone kuhani kwa ajiri ya ukombozi . 4.kataa kabisa roho za uharibifu kwa kusimamisha madhabau ya Mungu kwa sadaka. Zingatia :Ndoto ni mlango Mungu anao utumia kupitisha ujumbe wake na shetani naye anatumia hivyo hivyo jifunze kuomba uongozi wa roho mtakatifu katika fasiri sahiii japo zingine uja kwa uchovu na shughuli nyingi. Ok naitwa Sylvester Mwakabende wa (Build new eden) Unaweza share somo hili kwa rafiki wengine. Simu no :0622625340
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·1 Views
  • Habari ya jion tena .leo tunaendelea tena na tafsiri ya ndoto kiroho kwa kutumia biblia .

    Ukiota ndoto umekaa na viongozi wakuu wanchi ,unawawakilisha au hata unashare nao majukumu au company ywko ndotoni nini maana yake.?

    Mithali 18:16

    1.Ndoto hii inaashiria karama au kibali kinacho kuja mbele yako au uwezo wako wa ndani rohoni jinsi unavyo tizamwa.

    2.Inawakilisha kuwa kuna msimu mpya unakuja na nafasi mpya njema katika maisha yako.

    3. Inaonyesha pia unaweza ukawa unashare naye destiny huyo kiongozi yaani rohoni mko level moja sasa inategemea huyo uongozi wake msingi wake ni upi?


    Mwanzo 40:9-23 wote waliota ndoto zinazo elekeana lakini hazikufanana

    4.Unaukuu ndani yako wa kiuongozi ni vile tu umejisahau sana .anza kuliishi kusudi lako ili uifikie hatma yako.
    Zaburi 113:7-8

    Maana ya jumla .
    Viongozi katika ndotocwanawakilisha roho yenye mamlaka ya kutawala na yenye nguvu wakutawala na kumiliki juu ya nchi.

    Unapo wakilisha wakuu au kuona nafasi ya ukuu ndani yako wanawakikisha kutiwa mafuta kwa nafsi yako ili upate kuwa mtu fulani katika nchi.

    Ndoto za ukuu mara nyingi zinakuwaga na vita sana zinataka kusimama sana na Mungu kwani ukitaka kuona msome yusuph katika mwanzo 37

    NB .Kuota swala moja na kutimia swala moja ili litimie lazima ujifunze namna ya kuomba Mungu.

    Namna ya kuomba .

    1.kuwa mtu wa imani amini anza kuomba rehema na shukrani.

    2.Omba Mungu aifanikishe isibaki kuwa ndoto tu (ndoto iliyo zuiwa rohoni)

    3.Chuchumilia mbele za Mungu mpaka itimie kwa mifungo mingi na maombi mengi sana.

    4.Kama kuna nafasi chuku hatua ya kuomba Mungu akusogezee watu sahii ambao wanaweza kuwa wakuu.

    Ok naitwa sylvester kutoka (build new eden.
    Habari ya jion tena .leo tunaendelea tena na tafsiri ya ndoto kiroho kwa kutumia biblia . Ukiota ndoto umekaa na viongozi wakuu wanchi ,unawawakilisha au hata unashare nao majukumu au company ywko ndotoni nini maana yake.? Mithali 18:16 1.Ndoto hii inaashiria karama au kibali kinacho kuja mbele yako au uwezo wako wa ndani rohoni jinsi unavyo tizamwa. 2.Inawakilisha kuwa kuna msimu mpya unakuja na nafasi mpya njema katika maisha yako. 3. Inaonyesha pia unaweza ukawa unashare naye destiny huyo kiongozi yaani rohoni mko level moja sasa inategemea huyo uongozi wake msingi wake ni upi? Mwanzo 40:9-23 wote waliota ndoto zinazo elekeana lakini hazikufanana 4.Unaukuu ndani yako wa kiuongozi ni vile tu umejisahau sana .anza kuliishi kusudi lako ili uifikie hatma yako. Zaburi 113:7-8 Maana ya jumla . Viongozi katika ndotocwanawakilisha roho yenye mamlaka ya kutawala na yenye nguvu wakutawala na kumiliki juu ya nchi. Unapo wakilisha wakuu au kuona nafasi ya ukuu ndani yako wanawakikisha kutiwa mafuta kwa nafsi yako ili upate kuwa mtu fulani katika nchi. Ndoto za ukuu mara nyingi zinakuwaga na vita sana zinataka kusimama sana na Mungu kwani ukitaka kuona msome yusuph katika mwanzo 37 NB .Kuota swala moja na kutimia swala moja ili litimie lazima ujifunze namna ya kuomba Mungu. Namna ya kuomba . 1.kuwa mtu wa imani amini anza kuomba rehema na shukrani. 2.Omba Mungu aifanikishe isibaki kuwa ndoto tu (ndoto iliyo zuiwa rohoni) 3.Chuchumilia mbele za Mungu mpaka itimie kwa mifungo mingi na maombi mengi sana. 4.Kama kuna nafasi chuku hatua ya kuomba Mungu akusogezee watu sahii ambao wanaweza kuwa wakuu. Ok naitwa sylvester kutoka (build new eden.
    Share on WhatsApp
    w.app
    WhatsApp Messenger: More than 2 billion people in over 180 countries use WhatsApp to stay in touch with friends and family, anytime and anywhere. WhatsApp is free and offers simple, secure, reliable messaging and calling, available on phones all over the world.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·37 Views
  • .KIDNEY CARE
    DAWA YA FIGO
    Dawa hii ni unga na imeandaliwa maalum kwa kutibu maradhi yafuatayo.
    1.Huboresha figo katika kufanya kazi.
    2.Huondosha vijiwe katika figo
    3.Huondosha matatizo ya mkojo.
    4.Kuvimba kwa miguu,maumivu na uchovu wa mwili
    5.Husaidia kuboresha kazi ya ubongo.
    6.Huboresha mfumo wa chakula na kinga ya mwili.
    ✦Hakika Mungu ni mponyaji na atakusaidia.
    MATUMIZI.
    Mkubwa:Tumia kijiko 1 cha chakula katika maji moto,maziwa au uji.
    Mtoto:Atumie kijiko 1 cha chai katika mchanganyiko huo.

    KIDNEY CARE
    Herbal Powder
    Powder medicine and has been specially prepared to treat the following diseases.
    1.Improves kidney function.
    2.Removes kidney stones
    3.Eliminates urinary problems.
    4.Swelling of the feet, pain and fatigue
    5.Helps improve brain function.
    6.Improves the digestion system and body immunity.
    ✦Surely God is a healer and will help you.
    USAGE.
    Adult: Use 1X2 tablespoon in hot water, milk or porridge.
    Child: Use 1x2 teaspoon in the mixture.
    ✦𝐝𝐚𝐰𝐚 𝐦𝐩𝐲𝐚 𝐡𝐢𝐢 𝐧𝐚 𝐢𝐥𝐢𝐲𝐨 𝐛𝐨𝐫𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐮𝐰𝐞𝐳𝐨 𝐰𝐚 𝐌𝐮𝐧𝐠𝐮
    .KIDNEY CARE DAWA YA FIGO Dawa hii ni unga na imeandaliwa maalum kwa kutibu maradhi yafuatayo. 1.Huboresha figo katika kufanya kazi. 2.Huondosha vijiwe katika figo 3.Huondosha matatizo ya mkojo. 4.Kuvimba kwa miguu,maumivu na uchovu wa mwili 5.Husaidia kuboresha kazi ya ubongo. 6.Huboresha mfumo wa chakula na kinga ya mwili. ✦Hakika Mungu ni mponyaji na atakusaidia. MATUMIZI. Mkubwa:Tumia kijiko 1 cha chakula katika maji moto,maziwa au uji. Mtoto:Atumie kijiko 1 cha chai katika mchanganyiko huo. KIDNEY CARE Herbal Powder Powder medicine and has been specially prepared to treat the following diseases. 1.Improves kidney function. 2.Removes kidney stones 3.Eliminates urinary problems. 4.Swelling of the feet, pain and fatigue 5.Helps improve brain function. 6.Improves the digestion system and body immunity. ✦Surely God is a healer and will help you. USAGE. Adult: Use 1X2 tablespoon in hot water, milk or porridge. Child: Use 1x2 teaspoon in the mixture. ✦𝐝𝐚𝐰𝐚 𝐦𝐩𝐲𝐚 𝐡𝐢𝐢 𝐧𝐚 𝐢𝐥𝐢𝐲𝐨 𝐛𝐨𝐫𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐮𝐰𝐞𝐳𝐨 𝐰𝐚 𝐌𝐮𝐧𝐠𝐮🙏
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·95 Views
  • Nilidanganya na kusema nilikuwa bize.
    Nilikuwa na shughuli nyingi;
    lakini si kwa njia ambayo watu wengi wanaelewa.

    Nilikuwa bize nikivuta pumzi zaidi.
    Nilikuwa bize kunyamazisha mawazo yasiyo na mantiki.
    Nilikuwa bize kutuliza moyo uendao mbio.
    Nilikuwa busy kujiambia niko sawa.

    Wakati mwingine, hii ni shughuli yangu -
    na sitaomba msamaha kwa hilo.

    Nilidanganya na kusema nilikuwa bize. Nilikuwa na shughuli nyingi; lakini si kwa njia ambayo watu wengi wanaelewa. Nilikuwa bize nikivuta pumzi zaidi. Nilikuwa bize kunyamazisha mawazo yasiyo na mantiki. Nilikuwa bize kutuliza moyo uendao mbio. Nilikuwa busy kujiambia niko sawa. Wakati mwingine, hii ni shughuli yangu - na sitaomba msamaha kwa hilo.
    Love
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·33 Views
  • Maisha bila unafiki hayaendi kabisa, Leo hii Alex Sanchez anasema timu yake ya moyoni ni Arsenal.

    Hawezi kuisahau katukatu lakini jinsi alivyolazimisha kuondoka kipindi timu inamuhitaji, nazidi kuamini unafiki upo duniani kote .

    Babu Wenger alijitahidi sana kumbakisha lakini wapi

    Follow Neliud Cosiah
    Maisha bila unafiki hayaendi kabisa, Leo hii Alex Sanchez anasema timu yake ya moyoni ni Arsenal. Hawezi kuisahau katukatu lakini jinsi alivyolazimisha kuondoka kipindi timu inamuhitaji, nazidi kuamini unafiki upo duniani kote 😂. Babu Wenger alijitahidi sana kumbakisha lakini wapi 😀 Follow Neliud Cosiah
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·79 Views
  • Watumiaji wa halotel hakikisha una hii app kwenye simu yako, kwa wageni. Mtapewa G1 na kuendelea

    Pia kila siku fungua tu hio app kaa kidogo alf angalia salio lako. Utapewa MBS kadhaa kila siku

    Download hii app hapa
    https://halotelsuperapp.page.link/QX58cnP5ebgAYQf49


    Enjoy


    #Duduumendez
    #Duduu_mendez
    #Dml_Tech
    Watumiaji wa halotel hakikisha una hii app kwenye simu yako, kwa wageni. Mtapewa G1 na kuendelea Pia kila siku fungua tu hio app kaa kidogo alf angalia salio lako. Utapewa MBS kadhaa kila siku Download hii app hapa 👉👉 https://halotelsuperapp.page.link/QX58cnP5ebgAYQf49 Enjoy 😃 😉 #Duduumendez #Duduu_mendez #Dml_Tech
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·61 Views
  • 3. "Pesa hazileti furaha, lakini furaha inahitaji pesa." - Nukuu hii inaonyesha uhusiano kati ya fedha na furaha
    3. "Pesa hazileti furaha, lakini furaha inahitaji pesa." - Nukuu hii inaonyesha uhusiano kati ya fedha na furaha
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·50 Views
  • Miaka kadhaa iliyopita, hii ilikuwa nyumba nzuri zaidi katika mtaa huu. Mmiliki wake alikuwa mtu tajiri zaidi ambaye kila mmoja alimtegemea kwa msaada. Gari lake lilikuwa kivutio kwa macho ya kila mtu. Ilionekana kama ndoto kutimia pale alipoongeza nyumba na gari hilo katika orodha ya mali zake. Lakini leo, mali hizo zimezeeka, na kwa mujibu wa sheria ya asili, lazima ziporomoke ili nafasi ya nyumba mpya ipatikane.
    Kama mtu yeyote atapatikana akiishi ndani ya jengo hilo kwa hali lilivyo sasa, mtu huyo huonekana kama "mchizi" na huogopwa kama hatari.
    Hakuna kitu duniani kinachostahili kupiganiwa kwa udi na uvumba. Mavazi yako bora ni matambara ya mtu mwingine. Salio lako benki ni mchango wa mtu mwingine kwenye harusi. Mpenzi wako wa sasa ni ex wa mtu mwingine. Kila kahaba unayemuona hotelini au mtaani usiku, aliwahi kuwa bikira. Basi kuna sababu gani ya kugombana? Maisha ni mafupi mno kujiona bora au mkubwa kuliko wengine.
    “Tote tuko uchi mbele ya kifo,” alisema Steve Jobs. Hakuna kitu kinachoweza kutuokoa nacho. Sipendi kuona watu wanaojivuna kwa mali, uzuri, akili, elimu, umaarufu au vitu vya kidunia. Hakuna ulichofanikiwa maishani ambacho wengine hawajawahi kupata. Kitu kimoja tu kinachostahili kujivunia ni: “Maisha ndani ya Mungu Mwenyezi.” Kwa hiyo, kuwa mwema kwa wanadamu wenzako na jenga urafiki kila wakati. Kumbuka kwamba wale uliowakanyaga ukiwa unapaa juu, unaweza kuwakuta tena ukiwa unashuka.
    Hivyo, usiwasababishie wengine shida, maana siku moja, wao ndio watakuwa shida yako. Mwisho, hata mgomba hufikia kukauka na kuwa majani makavu. Usiongozwe na mali za dunia – huchakaa na kufa.

    KUWA MWEMA KILA WAKATI.
    Miaka kadhaa iliyopita, hii ilikuwa nyumba nzuri zaidi katika mtaa huu. Mmiliki wake alikuwa mtu tajiri zaidi ambaye kila mmoja alimtegemea kwa msaada. Gari lake lilikuwa kivutio kwa macho ya kila mtu. Ilionekana kama ndoto kutimia pale alipoongeza nyumba na gari hilo katika orodha ya mali zake. Lakini leo, mali hizo zimezeeka, na kwa mujibu wa sheria ya asili, lazima ziporomoke ili nafasi ya nyumba mpya ipatikane. Kama mtu yeyote atapatikana akiishi ndani ya jengo hilo kwa hali lilivyo sasa, mtu huyo huonekana kama "mchizi" na huogopwa kama hatari. Hakuna kitu duniani kinachostahili kupiganiwa kwa udi na uvumba. Mavazi yako bora ni matambara ya mtu mwingine. Salio lako benki ni mchango wa mtu mwingine kwenye harusi. Mpenzi wako wa sasa ni ex wa mtu mwingine. Kila kahaba unayemuona hotelini au mtaani usiku, aliwahi kuwa bikira. Basi kuna sababu gani ya kugombana? Maisha ni mafupi mno kujiona bora au mkubwa kuliko wengine. “Tote tuko uchi mbele ya kifo,” alisema Steve Jobs. Hakuna kitu kinachoweza kutuokoa nacho. Sipendi kuona watu wanaojivuna kwa mali, uzuri, akili, elimu, umaarufu au vitu vya kidunia. Hakuna ulichofanikiwa maishani ambacho wengine hawajawahi kupata. Kitu kimoja tu kinachostahili kujivunia ni: “Maisha ndani ya Mungu Mwenyezi.” Kwa hiyo, kuwa mwema kwa wanadamu wenzako na jenga urafiki kila wakati. Kumbuka kwamba wale uliowakanyaga ukiwa unapaa juu, unaweza kuwakuta tena ukiwa unashuka. Hivyo, usiwasababishie wengine shida, maana siku moja, wao ndio watakuwa shida yako. Mwisho, hata mgomba hufikia kukauka na kuwa majani makavu. Usiongozwe na mali za dunia – huchakaa na kufa. KUWA MWEMA KILA WAKATI.
    Like
    Love
    2
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·365 Views
  • Kwenye mahojiano na waandishi wa Habari , Fadlu alisema kuna uwezekano wa kuanza na washambuliaji wawili wa kati " UWEZEKANO " lakini akaona kama kikombe hakijpasuka kwanini ukitengeneze ? Kocha anajua muundo wake hauna shida bali ilibaki utekelezaji kwa wachezaji wake katika nyakati sahihi .

    Sehemu ambayo Fadlu alibadilisha ni ndogo sana katika muundo wake timu hasa ikiwa inashumbulia :

    1: Ni Position ya Kibu na Mpanzu . Mara nyingi huwa wanaombea mpira kwenye halfspace kabisa karibu na mabeki wa kati wa timu pinzani lakini leo walikuwa wanaanzia kupokea mpira katikati ya wingbacks na mabeki wa kati wa pembeni ( Outside CBs ) kwanini ?

    2: Ili kutengeneza sintofahamu kubwa ya kimaamuzi baina ya hao mabeki wa kati wa pembeni na wingbacks wao , kwa maana wingbacks wa Al Masry hofu yao ni fullbacks wa Simba wanaopanda juu .

    3: Fadlu alifanya hivyo ili kuwapa Kibu na Mpanzu " Shooting spaces" wawe katika nafasi bora za kupiga golini . Hii iliwezekana pia kwasababu ..

    4: Ahoua alikuwa anajaribu sana kuwa karibu na Mukwala asimuache peke yake dhidi ya beki wa kati wa Al Masry .

    5: Nafikiri hiki alichofanya Fadlu leo kimbinu kimeathiriwa sana na hali ya uwanja , vinginevyo ingekuwa jioni ndefu kwa Al Masry

    Al Masry mpango wao ulikuwa ambao umezoeleka

    1: Poteza sana muda kwa kucheza mechi ya taratibu

    2. Zuia sana kulinda mtaji wake

    3: Subiria , counter attack na mipira iliyokufa kupata goli la ugenini

    ✍🏻Kipindi cha pili , kasi ya mchezo ilipungua hasa kutoka kwa mwenyeji nafikiri pia ndio iliwapa Al Masry fursa na wao kuanza angalau kuunganisha hata pasi zao ( hapo nafikiri Simba walikuwa wanacheza moto , ni nafasi na kosa moja tu linaumua taswira nzima ya mechi )

    NOTE

    1: Siamini kama Al Masry waliamua kutaka penati bali hali ya mchezo iliwalazimisha , waliona kufunga kwao ngumu

    2: Hamza anacheza kwenye " GIA " yake mwenyewe anayotaka na hakuna kitu unamfanya

    3: Mukwala . Soma namba ya jezi ya beki basi beki yupo matatizoni

    4: Mpanzu , sio kwamba hawakufanya Homework yao Al Masry bali vitu vingine unakubali yaishe

    5: CAMARA. Unamuona tu golini hali ya kujiamini kubwa kwenye matuta

    FT: Simba 2-0 Al Masry
    (G. Ambangile )


    Kwenye mahojiano na waandishi wa Habari , Fadlu alisema kuna uwezekano wa kuanza na washambuliaji wawili wa kati " UWEZEKANO " lakini akaona kama kikombe hakijpasuka kwanini ukitengeneze ? Kocha anajua muundo wake hauna shida bali ilibaki utekelezaji kwa wachezaji wake katika nyakati sahihi . Sehemu ambayo Fadlu alibadilisha ni ndogo sana katika muundo wake timu hasa ikiwa inashumbulia : 1: Ni Position ya Kibu na Mpanzu . Mara nyingi huwa wanaombea mpira kwenye halfspace kabisa karibu na mabeki wa kati wa timu pinzani lakini leo walikuwa wanaanzia kupokea mpira katikati ya wingbacks na mabeki wa kati wa pembeni ( Outside CBs ) kwanini ? 2: Ili kutengeneza sintofahamu kubwa ya kimaamuzi baina ya hao mabeki wa kati wa pembeni na wingbacks wao , kwa maana wingbacks wa Al Masry hofu yao ni fullbacks wa Simba wanaopanda juu . 3: Fadlu alifanya hivyo ili kuwapa Kibu na Mpanzu " Shooting spaces" wawe katika nafasi bora za kupiga golini . Hii iliwezekana pia kwasababu .. 4: Ahoua alikuwa anajaribu sana kuwa karibu na Mukwala asimuache peke yake dhidi ya beki wa kati wa Al Masry . 5: Nafikiri hiki alichofanya Fadlu leo kimbinu kimeathiriwa sana na hali ya uwanja , vinginevyo ingekuwa jioni ndefu kwa Al Masry Al Masry mpango wao ulikuwa ambao umezoeleka 1: Poteza sana muda kwa kucheza mechi ya taratibu 2. Zuia sana kulinda mtaji wake 3: Subiria , counter attack na mipira iliyokufa kupata goli la ugenini ✍🏻Kipindi cha pili , kasi ya mchezo ilipungua hasa kutoka kwa mwenyeji nafikiri pia ndio iliwapa Al Masry fursa na wao kuanza angalau kuunganisha hata pasi zao ( hapo nafikiri Simba walikuwa wanacheza moto , ni nafasi na kosa moja tu linaumua taswira nzima ya mechi ) NOTE 1: Siamini kama Al Masry waliamua kutaka penati bali hali ya mchezo iliwalazimisha , waliona kufunga kwao ngumu 2: Hamza anacheza kwenye " GIA " yake mwenyewe anayotaka na hakuna kitu unamfanya 3: Mukwala . Soma namba ya jezi ya beki basi beki yupo matatizoni 🔥 4: Mpanzu , sio kwamba hawakufanya Homework yao Al Masry bali vitu vingine unakubali yaishe 5: CAMARA. Unamuona tu golini hali ya kujiamini kubwa kwenye matuta FT: Simba 2-0 Al Masry (G. Ambangile ✍️)
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·607 Views
  • Rais wa zamani wa Marekani , Barack Obama katika mahojiano na chuo cha Hamilton College Nchini humo aliongea kuhusu hali ya Nchi chini ya muhula wa pili wa Rais wa sasa Donald Trump na alikosoa vikali hatua za hivi karibuni za utawala huo.

    Rais huyo Mstaafu ambaye alitangulia muhula wa kwanza wa Trump, alimkosoa vikali Trump kwa juhudi zake za kubadilisha mfumo wa Serikali ya Shirikisho, kukandamiza uhamiaji na upinzani, pamoja na kuwatisha Wanahabari na Taasisi ya sheria.

    “Hivyo basi, hii ndio mara yangu ya kwanza kuzungumza hadharani kwa muda sasa,” Obama alisema wakati wa mahojiano jukwaani katika Chuo cha Hamilton. “Nimekuwa nikitazama kwa muda.”

    "Hebu fikiria kama ningekuwa nimefanya chochote kati ya haya,”

    “Ni jambo lisilowezekana kufikirika kwamba vyama vilevile vinavyonyamaza sasa vingevumilia tabia kama hiyo kutoka kwangu, au hata kutoka kwa baadhi ya walionitangulia.” alisema Obama

    Obama aliendelea kusema kuwa haamini tangazo jipya la ushuru lililotolewa na Trump “litakuwa zuri kwa Marekani.” Hata hivyo, alieleza kuwa anahofia zaidi kile alichokiita kama uvunjaji wa haki unaofanywa na Ikulu.

    Rais wa zamani wa Marekani 🇺🇸, Barack Obama katika mahojiano na chuo cha Hamilton College Nchini humo aliongea kuhusu hali ya Nchi chini ya muhula wa pili wa Rais wa sasa Donald Trump na alikosoa vikali hatua za hivi karibuni za utawala huo. Rais huyo Mstaafu ambaye alitangulia muhula wa kwanza wa Trump, alimkosoa vikali Trump kwa juhudi zake za kubadilisha mfumo wa Serikali ya Shirikisho, kukandamiza uhamiaji na upinzani, pamoja na kuwatisha Wanahabari na Taasisi ya sheria. “Hivyo basi, hii ndio mara yangu ya kwanza kuzungumza hadharani kwa muda sasa,” Obama alisema wakati wa mahojiano jukwaani katika Chuo cha Hamilton. “Nimekuwa nikitazama kwa muda.” "Hebu fikiria kama ningekuwa nimefanya chochote kati ya haya,” “Ni jambo lisilowezekana kufikirika kwamba vyama vilevile vinavyonyamaza sasa vingevumilia tabia kama hiyo kutoka kwangu, au hata kutoka kwa baadhi ya walionitangulia.” alisema Obama Obama aliendelea kusema kuwa haamini tangazo jipya la ushuru lililotolewa na Trump “litakuwa zuri kwa Marekani.” Hata hivyo, alieleza kuwa anahofia zaidi kile alichokiita kama uvunjaji wa haki unaofanywa na Ikulu.
    Love
    Like
    3
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·491 Views
  • "Nafahamu wote kwa pamoja tuna hamu ya kupata matokeo katika mechi hii lakini matokeo haya kuyapata kwa kushinda na kufuzu. Sisi tumeweka mazingira mazuri ambayo yataiwezesha timu yetu kufuzu.”

    “Nipo hapa kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa alkini ningependa kutoa taarifa muhimu kwamba tunaendelea kushirikiana na serikali kuimarisha usalama wa siku hiyo. Tunawataka wapenzi wetu kuhakikisha kwamba wanazingatia mazingatio yote ambayo yatawekwa ya usalama. Hatutaruhusu mtu yeyote ambaye sio Mwanasimba kutuharibia shughuli yetu.”

    “Katika mchezo uliopita walisema maneno mengi kwamba kuna wazee wafupi, mbuzi lakini tuwatumie ujumbe kwamba kama mechi aikuhusu wabaki nyumbani na sisi tumejiandaa kuthibiti hilo kama klabu.”- Zubeda Sakuru, CEO wa klabu ya Simba SC.

    "Nafahamu wote kwa pamoja tuna hamu ya kupata matokeo katika mechi hii lakini matokeo haya kuyapata kwa kushinda na kufuzu. Sisi tumeweka mazingira mazuri ambayo yataiwezesha timu yetu kufuzu.” “Nipo hapa kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa alkini ningependa kutoa taarifa muhimu kwamba tunaendelea kushirikiana na serikali kuimarisha usalama wa siku hiyo. Tunawataka wapenzi wetu kuhakikisha kwamba wanazingatia mazingatio yote ambayo yatawekwa ya usalama. Hatutaruhusu mtu yeyote ambaye sio Mwanasimba kutuharibia shughuli yetu.” “Katika mchezo uliopita walisema maneno mengi kwamba kuna wazee wafupi, mbuzi lakini tuwatumie ujumbe kwamba kama mechi aikuhusu wabaki nyumbani na sisi tumejiandaa kuthibiti hilo kama klabu.”- Zubeda Sakuru, CEO wa klabu ya Simba SC.
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·559 Views
  • kwa mujibu wa Jarida la Forbes, hii hapa orodha ya Jamii ya Watu Weusi wenye utajiri mkubwa Duniani kwa Mwaka 2025 ambapo wanakadariwa kumiliki utajiri wa dola bilioni 96.2. Wengi wao utajiri wao unatokana sekta za teknolojia, fedha, nishati na burudani, huku Mfanyabiashara Aliko Dangote wa Nigeria akiongoza kwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 23.9.

    1. Aliko Dangote (Nigeria) : $23.9B (Saruji, sukari)
    2. David Steward (Marekani) : $11.4B (Teknolojia)
    3. Robert F. Smith (Marekani) : $10.8B (Uwekezaji binafsi)

    4. Alexander Karp (Marekani) : $8.4B (Programu za uchambuzi wa data)
    5. Mike Adenuga (Nigeria) : $6.8B (Mawasiliano, mafuta)
    6. Abdulsamad Rabiu (Nigeria) : $5.1B (Saruji, sukari)

    7. Michael Jordan (Marekani) : $3.5B (Michezo, matangazo)
    8. Patrice Motsepe (Afrika Kusini) : $3B (Madini)
    9. Oprah Winfrey (Marekani) : $3B (Runinga)

    10. Jay-Z (Marekani) : $2.5B (Muziki, biashara)
    11. Adebayo Ogunlesi (Marekani) :$2.2B (Uwekezaji binafsi)
    12. Magic Johnson (Marekani) : $1.5B (Michezo, uwekezaji)

    13. Femi Otedola (Nigeria) : $1.5B (Nishati)
    14. Tope Awotona (Marekani) : $1.4B (Programu "Calendly")
    15. Tyler Perry (Marekani) : $1.4B (Filamu, Runinga)

    16. Tiger Woods (Marekani) : $1.4B (Gofu)
    17. Rihanna (Barbados) : $1.4B (Muziki, urembo)
    18. Mo Ibrahim (Uingereza) : $1.3B (Mawasiliano)

    19. LeBron James (Marekani) : $1.3B (Kikapu)
    20. Strive Masiyiwa (Zimbabwe) : $1.2B (Mawasiliano)
    21. Michael Lee-Chin (Canada) : $1.1B (Uwekezaji wa fedha)

    22. Herriot Tabuteau (Marekani) : $1.1B (Afya)
    23. Sheila Johnson (Marekani) : $1B (Runinga, hoteli)

    kwa mujibu wa Jarida la Forbes, hii hapa orodha ya Jamii ya Watu Weusi wenye utajiri mkubwa Duniani kwa Mwaka 2025 ambapo wanakadariwa kumiliki utajiri wa dola bilioni 96.2. Wengi wao utajiri wao unatokana sekta za teknolojia, fedha, nishati na burudani, huku Mfanyabiashara Aliko Dangote wa Nigeria 🇳🇬 akiongoza kwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 23.9. 1. Aliko Dangote (Nigeria) : $23.9B (Saruji, sukari) 2. David Steward (Marekani) : $11.4B (Teknolojia) 3. Robert F. Smith (Marekani) : $10.8B (Uwekezaji binafsi) 4. Alexander Karp (Marekani) : $8.4B (Programu za uchambuzi wa data) 5. Mike Adenuga (Nigeria) : $6.8B (Mawasiliano, mafuta) 6. Abdulsamad Rabiu (Nigeria) : $5.1B (Saruji, sukari) 7. Michael Jordan (Marekani) : $3.5B (Michezo, matangazo) 8. Patrice Motsepe (Afrika Kusini) : $3B (Madini) 9. Oprah Winfrey (Marekani) : $3B (Runinga) 10. Jay-Z (Marekani) : $2.5B (Muziki, biashara) 11. Adebayo Ogunlesi (Marekani) :$2.2B (Uwekezaji binafsi) 12. Magic Johnson (Marekani) : $1.5B (Michezo, uwekezaji) 13. Femi Otedola (Nigeria) : $1.5B (Nishati) 14. Tope Awotona (Marekani) : $1.4B (Programu "Calendly") 15. Tyler Perry (Marekani) : $1.4B (Filamu, Runinga) 16. Tiger Woods (Marekani) : $1.4B (Gofu) 17. Rihanna (Barbados) : $1.4B (Muziki, urembo) 18. Mo Ibrahim (Uingereza) : $1.3B (Mawasiliano) 19. LeBron James (Marekani) : $1.3B (Kikapu) 20. Strive Masiyiwa (Zimbabwe) : $1.2B (Mawasiliano) 21. Michael Lee-Chin (Canada) : $1.1B (Uwekezaji wa fedha) 22. Herriot Tabuteau (Marekani) : $1.1B (Afya) 23. Sheila Johnson (Marekani) : $1B (Runinga, hoteli)
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·520 Views
  • Nchi ya Marekani imeunda sera mpya inayozuia Wafanyakazi wa Serikali, Wanafamilia, na Wakandarasi walio na vibali vya usalama kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi au kingono na Raia wa China . Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Habari la Associated Press.

    Sera hiyo imewekwa na aliyekuwa Balozi wa Marekani, Nicholas Burns mnamo Januari, ikiwa ni uondoaji mkubwa kutoka kwa miongo ya awali, ambayo ilizuia uhusiano na Raia wa China wanaofanya kazi katika majukumu maalum, kama vile Walinzi wa ubalozi. Inaripotiwa kuwa uamuzi huo umechukuliwa kutokana na hofu kwamba Mawakala wa China wanaweza kuchukua taarifa za siri za Serikali ya Marekani na kuziwasilisha kwa Serikali ya China.

    Sera hiyo inatumika kwa Wafanyakazi wa Marekani walioko China Bara, ikiwa ni pamoja na ubalozi wa Beijing na balozi ndogo huko Guangzhou, Shanghai, Shenyang na Wuhan, pamoja na ubalozi mdogo wa Marekani huko Hong Kong. Pia haitumiki kwa Wafanyakazi wa Marekani walioko nje ya China ambao wana uhusiano uliokuwepo hapo awali na Raia wa China ingawa wanaweza kutuma maombi ya misamaha, lakini wakikataliwa, lazima wasitishe uhusiano huo au waache nafasi zao.

    Ikiwa sera hiyo itakiukwa, Wafanyakazi wanaohusika wataamriwa kuondoka China mara moja. Hata hivyo, Sera hiyo inaashiria mabadiliko makubwa katika mtazamo wa Serikali ya Marekani kuhusu usalama Nchini China, ikionyesha mvutano unaoongezeka kati ya Washington na Beijing kuhusu biashara, teknolojia na ushindani wa kijiografia na kisiasa.

    Kwaupande wa Wizara ya mambo ya nje ya China imekataa kutoa maoni yake kuhusu sera hiyo, ikisema kwamba "ni sahihi zaidi kuuliza Marekani kuhusu swali hilo." imekadiriwa ikisema Wizara hiyo ya China.

    Nchi ya Marekani 🇺🇸 imeunda sera mpya inayozuia Wafanyakazi wa Serikali, Wanafamilia, na Wakandarasi walio na vibali vya usalama kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi au kingono na Raia wa China 🇨🇳. Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Habari la Associated Press. Sera hiyo imewekwa na aliyekuwa Balozi wa Marekani, Nicholas Burns mnamo Januari, ikiwa ni uondoaji mkubwa kutoka kwa miongo ya awali, ambayo ilizuia uhusiano na Raia wa China wanaofanya kazi katika majukumu maalum, kama vile Walinzi wa ubalozi. Inaripotiwa kuwa uamuzi huo umechukuliwa kutokana na hofu kwamba Mawakala wa China wanaweza kuchukua taarifa za siri za Serikali ya Marekani na kuziwasilisha kwa Serikali ya China. Sera hiyo inatumika kwa Wafanyakazi wa Marekani walioko China Bara, ikiwa ni pamoja na ubalozi wa Beijing na balozi ndogo huko Guangzhou, Shanghai, Shenyang na Wuhan, pamoja na ubalozi mdogo wa Marekani huko Hong Kong. Pia haitumiki kwa Wafanyakazi wa Marekani walioko nje ya China ambao wana uhusiano uliokuwepo hapo awali na Raia wa China ingawa wanaweza kutuma maombi ya misamaha, lakini wakikataliwa, lazima wasitishe uhusiano huo au waache nafasi zao. Ikiwa sera hiyo itakiukwa, Wafanyakazi wanaohusika wataamriwa kuondoka China mara moja. Hata hivyo, Sera hiyo inaashiria mabadiliko makubwa katika mtazamo wa Serikali ya Marekani kuhusu usalama Nchini China, ikionyesha mvutano unaoongezeka kati ya Washington na Beijing kuhusu biashara, teknolojia na ushindani wa kijiografia na kisiasa. Kwaupande wa Wizara ya mambo ya nje ya China imekataa kutoa maoni yake kuhusu sera hiyo, ikisema kwamba "ni sahihi zaidi kuuliza Marekani kuhusu swali hilo." imekadiriwa ikisema Wizara hiyo ya China.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·577 Views
  • Msemaji wa klabu ya Yanga SC, Ali Kamwe alikamatwa na Jeshi Polisi baada ya mchezo wao dhidi ya klabu ya Tabora United majira ya saa saba na nusu usiku wa kuamkia leo hii. Ali Kamwe alipelekwa kituo kikubwa cha Polisi cha Mkoa na amelala ndani hapo na hadi sasa bado hajaachiwa.

    Viongozi wa Yanga SC bado wanaendelea kufanya jitihada za kumtoa Ali Kamwe hapo haijawekwa bayana makosa aliyoyafanya Msemaji huyo. Taarifa iliyopo ni kuwa, inadaiwa Ali Kamwe alitoa kauli isiyokuwa nzuri kipindi anamjibu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha kabla ya mechi kama sehemu ya utani baada ya Mkuu huyo kutoa ahadi ya Shilingi milioni sitini (60) endapo klabu ya Tabora United ikimfunga Yanga SC ambapo mchezo ulimalizika kwa ushindi wa Yanga SC wa mabao matatu kwa bila (0-3).

    Msemaji wa klabu ya Yanga SC, Ali Kamwe alikamatwa na Jeshi Polisi baada ya mchezo wao dhidi ya klabu ya Tabora United majira ya saa saba na nusu usiku wa kuamkia leo hii. Ali Kamwe alipelekwa kituo kikubwa cha Polisi cha Mkoa na amelala ndani hapo na hadi sasa bado hajaachiwa. Viongozi wa Yanga SC bado wanaendelea kufanya jitihada za kumtoa Ali Kamwe hapo haijawekwa bayana makosa aliyoyafanya Msemaji huyo. Taarifa iliyopo ni kuwa, inadaiwa Ali Kamwe alitoa kauli isiyokuwa nzuri kipindi anamjibu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha kabla ya mechi kama sehemu ya utani baada ya Mkuu huyo kutoa ahadi ya Shilingi milioni sitini (60) endapo klabu ya Tabora United ikimfunga Yanga SC ambapo mchezo ulimalizika kwa ushindi wa Yanga SC wa mabao matatu kwa bila (0-3).
    Like
    Wow
    2
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·403 Views
  • "Simba SC wamepoteza lakini HII WANAVUKA, NO DOUBT. Sioni Al Masry wakileta ubishi kwa Mkapa, dhahiri watatii Sheria iwe kwa shuruti au bila shuruti. Heads up boys, come finish your job. TANZANIA KWANZA" - Jemedari Said, Mchambuzi.

    "Simba SC wamepoteza lakini HII WANAVUKA, NO DOUBT. Sioni Al Masry wakileta ubishi kwa Mkapa, dhahiri watatii Sheria iwe kwa shuruti au bila shuruti. Heads up boys, come finish your job. TANZANIA 🇹🇿 KWANZA" - Jemedari Said, Mchambuzi.
    Like
    2
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·474 Views
  • Pamoja na uwezo wa ugomvi wa Mashabiki ambao ulitokea kwenye mchezo wa jana kati ya Mamelodi Sundowns dhidi ya Esperence kwenye mchezo wa klabu bingwa barani Afrika (CAF Champions League) lakini hiki kitendo kimesisimua zaidi Mashabiki wengi.

    Picha hii inaeleza sababu milioni ya upendo ambao unatakiwa pindi Mashabiki wawapo Uwanjani. Mpira wa miguu unatufanya kuwa ndugu hii ndio maana unaitwa Football kwa kiingereza.

    Pamoja na uwezo wa ugomvi wa Mashabiki ambao ulitokea kwenye mchezo wa jana kati ya Mamelodi Sundowns 🇿🇦dhidi ya Esperence 🇹🇳 kwenye mchezo wa klabu bingwa barani Afrika (CAF Champions League) lakini hiki kitendo kimesisimua zaidi Mashabiki wengi. Picha hii inaeleza sababu milioni ya upendo ambao unatakiwa pindi Mashabiki wawapo Uwanjani. Mpira wa miguu unatufanya kuwa ndugu hii ndio maana unaitwa Football kwa kiingereza.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·372 Views
  • Rais wa Nchi ya Burkina Faso , Kapteni Ibrahim Traoré ametoa msamaha kwa Wanajeshi (21) waliojaribu kufanya mapinduzi ya Serikali ya Septemba mwaka 2015. Katika amri iliyosainiwa Machi 24 na kuwekwa hadharani Jumapili hii, Kapteni Traore aliweka masharti ya msamaha huu, ambao ulipigiwa kura na Bunge la Nchi hiy Desemba iliyopita.

    Wanajeshi hao (21), wakiwemo Maafisa, Maafisa wasio na kamisheni na Vyeo vingine, walifikishwa mahakamani na kutiwa hatiani kwa matendo yaliyofanywa Septemba 15 na 16, 2015, inasema amri iliyotiwa saini na Rais wa Nchi hiyo Kapteni Ibrahim Traore. Amri hii iliyopitishwa na Bunge mwishoni mwa Desemba 2024 ya msamaha na masharti ya kutoa msamaha kwa Watu waliopatikana na hatia kuhusiana na mapinduzi yaliyofeli ya 2015.

    Sheria hii pia imeweka wazi kwamba Askari waliotiwa hatiani au kufunguliwa mashtaka kuhusiana na kesi hii, wakionyesha kujitolea katika mapambano dhidi ya ugaidi Nchini humo, wanaweza kupata fursa ya neema ya msamaha ili kupandishwa cheo kazini.

    Rais wa Nchi ya Burkina Faso 🇧🇫, Kapteni Ibrahim Traoré ametoa msamaha kwa Wanajeshi (21) waliojaribu kufanya mapinduzi ya Serikali ya Septemba mwaka 2015. Katika amri iliyosainiwa Machi 24 na kuwekwa hadharani Jumapili hii, Kapteni Traore aliweka masharti ya msamaha huu, ambao ulipigiwa kura na Bunge la Nchi hiy Desemba iliyopita. Wanajeshi hao (21), wakiwemo Maafisa, Maafisa wasio na kamisheni na Vyeo vingine, walifikishwa mahakamani na kutiwa hatiani kwa matendo yaliyofanywa Septemba 15 na 16, 2015, inasema amri iliyotiwa saini na Rais wa Nchi hiyo Kapteni Ibrahim Traore. Amri hii iliyopitishwa na Bunge mwishoni mwa Desemba 2024 ya msamaha na masharti ya kutoa msamaha kwa Watu waliopatikana na hatia kuhusiana na mapinduzi yaliyofeli ya 2015. Sheria hii pia imeweka wazi kwamba Askari waliotiwa hatiani au kufunguliwa mashtaka kuhusiana na kesi hii, wakionyesha kujitolea katika mapambano dhidi ya ugaidi Nchini humo, wanaweza kupata fursa ya neema ya msamaha ili kupandishwa cheo kazini.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·367 Views
  • "Marekani mpaka sasa hawajasaini mkataba wa kuilinda Congo mchakato umekuwa mrefu. Jiulize vile vikwazo vya Magharibi walivyoiwekea Rwanda vimeishia wapi

    Kagame anajua anachokifanya ndio maana licha ya ripoti za UN , US na EU kuonyesha Rwanda wanaifadhili M23 plus Vikwazo hakuna kilichobadilika Congo

    Wanachokifanya wanaoibia Congo na Africa ni ile ile mbinu ya wakati wa ukoloni inaitwa "Divided and Rule " yaani wagawanywe uwatawale nakumbuka hii mbinu pia enzi hizo ndio iliyozaa utani wa jadi wa Yanga na Simba

    Oooh Africa " - Zungu, Mchambuzi wa Siasa na Mtangazaji.

    "Marekani mpaka sasa hawajasaini mkataba wa kuilinda Congo mchakato umekuwa mrefu. Jiulize vile vikwazo vya Magharibi walivyoiwekea Rwanda vimeishia wapi 😀😀😀😀 Kagame anajua anachokifanya ndio maana licha ya ripoti za UN , US na EU kuonyesha Rwanda wanaifadhili M23 plus Vikwazo hakuna kilichobadilika Congo 😭😭😭😭 Wanachokifanya wanaoibia Congo na Africa ni ile ile mbinu ya wakati wa ukoloni inaitwa "Divided and Rule " yaani wagawanywe uwatawale nakumbuka hii mbinu pia enzi hizo ndio iliyozaa utani wa jadi wa Yanga na Simba Oooh Africa🌍 😭" - Zungu, Mchambuzi wa Siasa na Mtangazaji.
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·593 Views
  • Amesema Steve Nyerere.

    "Mstafuuu ,,, Ivi Mama Akipenda kwenda kuangalia Dabi,....Pale uwanja wa Taifa pamoja na Watanzania na mashabiki wa Simba na Yanga Si Itapendeza sana,......Naimani Timu zote zitafurahia kuazimisha Miaka 4 Ya Rais wetu Mpendwa kwa Kucheza Dabi,...Maana ndani ya Miaka 4 Ya Mh @samia_suluhu_hassan Soka Limekuwa kivutio kikubwa sana Na Muanko wa Soka umekuwa mkubwa Baada ya Mh Rais kuhakikisha sekta hii Inapiga hatua,......

    Kuazimisha Miaka 4 Ya kipenzi cha Watanzania Dr Samia Suluhu Hassan Dabi halafu mgeni Rasmi Mama Itapendeza Tutajaaaa balaaa,...Apo vipi.,.," - Steve Nyerere, Mwigizaji wa filamu Tanzania.

    Amesema Steve Nyerere. "Mstafuuu ,,, Ivi Mama Akipenda kwenda kuangalia Dabi,....Pale uwanja wa Taifa pamoja na Watanzania na mashabiki wa Simba na Yanga Si Itapendeza sana,......Naimani Timu zote zitafurahia kuazimisha Miaka 4 Ya Rais wetu Mpendwa kwa Kucheza Dabi,...Maana ndani ya Miaka 4 Ya Mh @samia_suluhu_hassan Soka Limekuwa kivutio kikubwa sana Na Muanko wa Soka umekuwa mkubwa Baada ya Mh Rais kuhakikisha sekta hii Inapiga hatua,...... Kuazimisha Miaka 4 Ya kipenzi cha Watanzania Dr Samia Suluhu Hassan Dabi halafu mgeni Rasmi Mama Itapendeza Tutajaaaa balaaa,...Apo vipi.,.," - Steve Nyerere, Mwigizaji wa filamu Tanzania.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·479 Views
  • PICHA YA SIMBA HUYU NI FUNZO MAISHANI:
    ------------------------------------------------------

    Hivi ndivyo mfalme wa pori anavyoonekana akiwa kwenye siku za mwisho za maisha yake. Jinsi alivyokonda, kujua idadi ya mbavu zake hata huitaji msaada wa calculator.

    Hii picha ilipigwa na "Larry Pannell."

    Alifanikiwa kupata picha ya Simba aliyekuwa kwenye hitimisho la kuvuta pumzi za mwisho. Katika huu ulimwengu wenye mafungamano na dhambi.

    "Larry Pannell" anasema:

    Nilimkuta huyu simba amelala kwenye majani. Akiwa amechoka, miguu ikionekana kumnyima ushirikiano wa kutembea.

    Sikuwa na lakufanya zaidi ya kusimama mita kadhaa. Macho yakifanya ushuhuda wa kutazama, "King of savannah" akipoteza uhai chini ya kivuli cha mti.

    Nikiwa nimesimama kimya. Nilishusha chini camera yangu. Tulitazamana na simba, tukafumba macho yetu pamoja.

    Jinsi mfalme wa nyika alivyokuwa akihangaika kuhema. Pumzi zilionekana kuwa bidhaa hadimu kwenye duka la mapafu yake.

    Kifua chake kilikuwa kikipanda na kushuka. Ishara ya kuonyesha anavuta pumzi za mwisho, kabla ya kukipa ruhusa kifo kiondoke na roho yake.

    Ghafla eneo alilolala Simba ukazaliwa ukimya. Mfalme wa pori akawa haemi wala kutikisika. Mauti ikawa imehitimisha simulizi ya ubabe wake mbugani.

    Hakika maisha ya binadamu na wanyama ni simulizi fupi sana."

    Haijalishi una nguvu kiasi gani. Kuna nyakati zitafika nguvu zitafanya mgomo wa kuishi mwilini mwako. Zitaupisha udhaifu uchukue nafasi ya kukutawala. Udhaifu nao ukikutawala, utayaita maradhi. Bila hiyari utajikuta umekigeuza kitanda kuwa rafiki."

    Kuna shule ya bure hapa: Nguvu tulizonazo ni kitu cha kupita. Hata uzuri umpao kiburi mwanamke una ukomo. Licha ya kujidanganya kwa make up na wanja. Lakini hawezi kuzuia muanguko wa mashavu, uzee unapoanza kumuondoa kwenye kundi la warembo.

    "Chini ya jua kila kitu kina mwanzo na mwisho."

    Hivyo katika maisha tusisahau kuvipa kipaumbele vitu hivi. Utu, wema, ukarimu, heshima, na unyenyekevu.

    Tusaidie wenye maradhi, tuwajali wasiojiweza, na viongozi tusitumie madaraka vibaya.

    Tutende mema tukiamini. Kuna siku pumzi zitamaliza mkataba wa kuishi ndani ya matundu ya pua zetu. Baada ya hapo sisi wote tutalala mauti."

    Imeandikwa na Green Osward
    PICHA YA SIMBA HUYU NI FUNZO MAISHANI: ------------------------------------------------------ Hivi ndivyo mfalme wa pori anavyoonekana akiwa kwenye siku za mwisho za maisha yake. Jinsi alivyokonda, kujua idadi ya mbavu zake hata huitaji msaada wa calculator. Hii picha ilipigwa na "Larry Pannell." Alifanikiwa kupata picha ya Simba aliyekuwa kwenye hitimisho la kuvuta pumzi za mwisho. Katika huu ulimwengu wenye mafungamano na dhambi. "Larry Pannell" anasema: Nilimkuta huyu simba amelala kwenye majani. Akiwa amechoka, miguu ikionekana kumnyima ushirikiano wa kutembea. Sikuwa na lakufanya zaidi ya kusimama mita kadhaa. Macho yakifanya ushuhuda wa kutazama, "King of savannah" akipoteza uhai chini ya kivuli cha mti. Nikiwa nimesimama kimya. Nilishusha chini camera yangu. Tulitazamana na simba, tukafumba macho yetu pamoja. Jinsi mfalme wa nyika alivyokuwa akihangaika kuhema. Pumzi zilionekana kuwa bidhaa hadimu kwenye duka la mapafu yake. Kifua chake kilikuwa kikipanda na kushuka. Ishara ya kuonyesha anavuta pumzi za mwisho, kabla ya kukipa ruhusa kifo kiondoke na roho yake. Ghafla eneo alilolala Simba ukazaliwa ukimya. Mfalme wa pori akawa haemi wala kutikisika. Mauti ikawa imehitimisha simulizi ya ubabe wake mbugani. Hakika maisha ya binadamu na wanyama ni simulizi fupi sana." Haijalishi una nguvu kiasi gani. Kuna nyakati zitafika nguvu zitafanya mgomo wa kuishi mwilini mwako. Zitaupisha udhaifu uchukue nafasi ya kukutawala. Udhaifu nao ukikutawala, utayaita maradhi. Bila hiyari utajikuta umekigeuza kitanda kuwa rafiki." Kuna shule ya bure hapa: Nguvu tulizonazo ni kitu cha kupita. Hata uzuri umpao kiburi mwanamke una ukomo. Licha ya kujidanganya kwa make up na wanja. Lakini hawezi kuzuia muanguko wa mashavu, uzee unapoanza kumuondoa kwenye kundi la warembo. "Chini ya jua kila kitu kina mwanzo na mwisho." Hivyo katika maisha tusisahau kuvipa kipaumbele vitu hivi. Utu, wema, ukarimu, heshima, na unyenyekevu. Tusaidie wenye maradhi, tuwajali wasiojiweza, na viongozi tusitumie madaraka vibaya. Tutende mema tukiamini. Kuna siku pumzi zitamaliza mkataba wa kuishi ndani ya matundu ya pua zetu. Baada ya hapo sisi wote tutalala mauti." Imeandikwa na Green Osward
    Love
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·900 Views
Αναζήτηση αποτελεσμάτων