Kutoka Nchini Qatar , Pande mbali hasimu katika mzozo wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa AFC/M23 wanaotuhumiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda wamekubaliana kusitisha mapigano mara moja, baada ya mazungumzo ya wiki moja yaliyoandaliwa Nchini Qatar. Makubaliano hayo, yaliyoelezwa kuwa ni hatua ya matumaini, yalitangazwa kupitia taarifa rasmi zilizotolewa na kila upande baada ya Wajumbe kurejea kutoka Qatar mapema wiki hii.
“Pande zote zimethibitisha dhamira yao ya kusitisha uhasama, kupinga matamshi ya chuki na vitisho, na kuhimiza jamii kutekeleza ahadi hizi,” ilisomeka sehemu ya taarifa. Hata hivyo, tarehe ya duru inayofuata ya mazungumzo haikutajwa.
Kundi la M23 ambalo limekuwa likijipatia nguvu upya tangu mwaka jana, limeshambulia na kuteka Miji kadhaa Mashariki mwa DR Congo, hali iliyosababisha vifo vya maelfu na kuwafanya mamilioni kuwa Wakimbizi. Hofu ya vita vikubwa vya kikanda imetanda, hasa kutokana na mvutano kati ya DR Congo na Nchi ya Rwanda. Rwanda imeendelea kukanusha kuhusika moja kwa moja na kundi la M23, ikisema Wanajeshi wake wapo kulinda mipaka dhidi ya mashambulizi ya Wanamgambo wa Kihutu waliokimbilia DR Congo baada ya mauaji ya kimbari ya 1994.
Juhudi hizi za upatanishi zinafuatia mkutano wa mwezi uliopita ulioandaliwa pia na Qatar, uliowakutanisha Rais wa DR Congo, Félix Tshisekedi na Rais wa Rwanda, Paul Kagame. Wito wa pamoja wa kusitisha mapigano ulitolewa, na sasa mazungumzo kati ya Serikali ya DR Congo na Kundi la M23 yanaonekana kuanza kupewa nafasi, licha ya DR Congo kulitambua Kundi hilo kama la kigaidi hapo awali.

Kutoka Nchini Qatar 🇶🇦, Pande mbali hasimu katika mzozo wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 na waasi wa AFC/M23 wanaotuhumiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda 🇷🇼 wamekubaliana kusitisha mapigano mara moja, baada ya mazungumzo ya wiki moja yaliyoandaliwa Nchini Qatar. Makubaliano hayo, yaliyoelezwa kuwa ni hatua ya matumaini, yalitangazwa kupitia taarifa rasmi zilizotolewa na kila upande baada ya Wajumbe kurejea kutoka Qatar mapema wiki hii.
“Pande zote zimethibitisha dhamira yao ya kusitisha uhasama, kupinga matamshi ya chuki na vitisho, na kuhimiza jamii kutekeleza ahadi hizi,” ilisomeka sehemu ya taarifa. Hata hivyo, tarehe ya duru inayofuata ya mazungumzo haikutajwa.
Kundi la M23 ambalo limekuwa likijipatia nguvu upya tangu mwaka jana, limeshambulia na kuteka Miji kadhaa Mashariki mwa DR Congo, hali iliyosababisha vifo vya maelfu na kuwafanya mamilioni kuwa Wakimbizi. Hofu ya vita vikubwa vya kikanda imetanda, hasa kutokana na mvutano kati ya DR Congo na Nchi ya Rwanda. Rwanda imeendelea kukanusha kuhusika moja kwa moja na kundi la M23, ikisema Wanajeshi wake wapo kulinda mipaka dhidi ya mashambulizi ya Wanamgambo wa Kihutu waliokimbilia DR Congo baada ya mauaji ya kimbari ya 1994.
Juhudi hizi za upatanishi zinafuatia mkutano wa mwezi uliopita ulioandaliwa pia na Qatar, uliowakutanisha Rais wa DR Congo, Félix Tshisekedi na Rais wa Rwanda, Paul Kagame. Wito wa pamoja wa kusitisha mapigano ulitolewa, na sasa mazungumzo kati ya Serikali ya DR Congo na Kundi la M23 yanaonekana kuanza kupewa nafasi, licha ya DR Congo kulitambua Kundi hilo kama la kigaidi hapo awali.
0 التعليقات
·0 المشاركات
·1 مشاهدة