• Kwenye mahojiano na waandishi wa Habari , Fadlu alisema kuna uwezekano wa kuanza na washambuliaji wawili wa kati " UWEZEKANO " lakini akaona kama kikombe hakijpasuka kwanini ukitengeneze ? Kocha anajua muundo wake hauna shida bali ilibaki utekelezaji kwa wachezaji wake katika nyakati sahihi .

    Sehemu ambayo Fadlu alibadilisha ni ndogo sana katika muundo wake timu hasa ikiwa inashumbulia :

    1: Ni Position ya Kibu na Mpanzu . Mara nyingi huwa wanaombea mpira kwenye halfspace kabisa karibu na mabeki wa kati wa timu pinzani lakini leo walikuwa wanaanzia kupokea mpira katikati ya wingbacks na mabeki wa kati wa pembeni ( Outside CBs ) kwanini ?

    2: Ili kutengeneza sintofahamu kubwa ya kimaamuzi baina ya hao mabeki wa kati wa pembeni na wingbacks wao , kwa maana wingbacks wa Al Masry hofu yao ni fullbacks wa Simba wanaopanda juu .

    3: Fadlu alifanya hivyo ili kuwapa Kibu na Mpanzu " Shooting spaces" wawe katika nafasi bora za kupiga golini . Hii iliwezekana pia kwasababu ..

    4: Ahoua alikuwa anajaribu sana kuwa karibu na Mukwala asimuache peke yake dhidi ya beki wa kati wa Al Masry .

    5: Nafikiri hiki alichofanya Fadlu leo kimbinu kimeathiriwa sana na hali ya uwanja , vinginevyo ingekuwa jioni ndefu kwa Al Masry

    Al Masry mpango wao ulikuwa ambao umezoeleka

    1: Poteza sana muda kwa kucheza mechi ya taratibu

    2. Zuia sana kulinda mtaji wake

    3: Subiria , counter attack na mipira iliyokufa kupata goli la ugenini

    ✍🏻Kipindi cha pili , kasi ya mchezo ilipungua hasa kutoka kwa mwenyeji nafikiri pia ndio iliwapa Al Masry fursa na wao kuanza angalau kuunganisha hata pasi zao ( hapo nafikiri Simba walikuwa wanacheza moto , ni nafasi na kosa moja tu linaumua taswira nzima ya mechi )

    NOTE

    1: Siamini kama Al Masry waliamua kutaka penati bali hali ya mchezo iliwalazimisha , waliona kufunga kwao ngumu

    2: Hamza anacheza kwenye " GIA " yake mwenyewe anayotaka na hakuna kitu unamfanya

    3: Mukwala . Soma namba ya jezi ya beki basi beki yupo matatizoni

    4: Mpanzu , sio kwamba hawakufanya Homework yao Al Masry bali vitu vingine unakubali yaishe

    5: CAMARA. Unamuona tu golini hali ya kujiamini kubwa kwenye matuta

    FT: Simba 2-0 Al Masry
    (G. Ambangile )


    Kwenye mahojiano na waandishi wa Habari , Fadlu alisema kuna uwezekano wa kuanza na washambuliaji wawili wa kati " UWEZEKANO " lakini akaona kama kikombe hakijpasuka kwanini ukitengeneze ? Kocha anajua muundo wake hauna shida bali ilibaki utekelezaji kwa wachezaji wake katika nyakati sahihi . Sehemu ambayo Fadlu alibadilisha ni ndogo sana katika muundo wake timu hasa ikiwa inashumbulia : 1: Ni Position ya Kibu na Mpanzu . Mara nyingi huwa wanaombea mpira kwenye halfspace kabisa karibu na mabeki wa kati wa timu pinzani lakini leo walikuwa wanaanzia kupokea mpira katikati ya wingbacks na mabeki wa kati wa pembeni ( Outside CBs ) kwanini ? 2: Ili kutengeneza sintofahamu kubwa ya kimaamuzi baina ya hao mabeki wa kati wa pembeni na wingbacks wao , kwa maana wingbacks wa Al Masry hofu yao ni fullbacks wa Simba wanaopanda juu . 3: Fadlu alifanya hivyo ili kuwapa Kibu na Mpanzu " Shooting spaces" wawe katika nafasi bora za kupiga golini . Hii iliwezekana pia kwasababu .. 4: Ahoua alikuwa anajaribu sana kuwa karibu na Mukwala asimuache peke yake dhidi ya beki wa kati wa Al Masry . 5: Nafikiri hiki alichofanya Fadlu leo kimbinu kimeathiriwa sana na hali ya uwanja , vinginevyo ingekuwa jioni ndefu kwa Al Masry Al Masry mpango wao ulikuwa ambao umezoeleka 1: Poteza sana muda kwa kucheza mechi ya taratibu 2. Zuia sana kulinda mtaji wake 3: Subiria , counter attack na mipira iliyokufa kupata goli la ugenini ✍🏻Kipindi cha pili , kasi ya mchezo ilipungua hasa kutoka kwa mwenyeji nafikiri pia ndio iliwapa Al Masry fursa na wao kuanza angalau kuunganisha hata pasi zao ( hapo nafikiri Simba walikuwa wanacheza moto , ni nafasi na kosa moja tu linaumua taswira nzima ya mechi ) NOTE 1: Siamini kama Al Masry waliamua kutaka penati bali hali ya mchezo iliwalazimisha , waliona kufunga kwao ngumu 2: Hamza anacheza kwenye " GIA " yake mwenyewe anayotaka na hakuna kitu unamfanya 3: Mukwala . Soma namba ya jezi ya beki basi beki yupo matatizoni 🔥 4: Mpanzu , sio kwamba hawakufanya Homework yao Al Masry bali vitu vingine unakubali yaishe 5: CAMARA. Unamuona tu golini hali ya kujiamini kubwa kwenye matuta FT: Simba 2-0 Al Masry (G. Ambangile ✍️)
    0 Commenti ·0 condivisioni ·2 Views
  • Yanga walianza mchezo vizuri sana kwa kufanya kila kitu kwa usahihi pale wanapokuwa na mpira na wasipokuwa na mpira . Kivipi ?

    1: Wakati wanaanza build up wanakuwa na muundo mzuri wa 2-3-4-1 unawapa walinzi wao machaguo ya kupasia mipira (Job na Bakari wanakuwa nyuma then FBs wanakuwa mstari moja na Aucho , hapo Yanga wanapata msingi sahihi ya kufika kwenye eneo la mwisho kwa kupitia katikati na pembeni ya uwanja , rahisi kuishinda pressing ya Coastal ambayo hawakuwa na idadi nzuri ya wachezaji wakati wanaweka presha .

    2: Kwasababu Coastal Union hawakuweka presha vizuri kwenye mpira na positioning ya wachezaji wa Yanga ilikuwa nzuri , hapo ikawa rahisi kwa Yanga kufika eneo la mwisho baada ya hapo ni Yanga kuwa wafanisi mbele ya goli (unatumiaje nafasi kuimaliza game) .

    Maxi na Pacome waliuliza maswali magumu kwa walinzi wa Coastal walibadilishana nafasi kutokana na wapi mpira ulipo , nafasi zilikuwepo hasa kwenye zile “Half Spaces” na ndio maana pamoja na Coastal kuzuia wakiwa chini mda mwingi lakini Yanga waliwafungua kirahisi kwasababu wachezaji wao walikuwa mara nyingi wanachelewa kufika kwenye eneo la tukio .

    Nafikiri Coastal walijua kabisa hawawezi kupishana na Yanga kutokana na ubora wa mpinzani wake , wakaamua kuchagua vita yao ya kuzuia wakiwa chini na kuweka mtego wa kushambulia kwa kushtukiza . Lakini kuna nyakati wakivuka kwenye mstari wa kati wanachotegemea ni ubora wa mchezaji mmoja mmoja kufanya jambo kubwa .

    NOTE :

    1: Golikipa wa Coastal “FALESI” kafanya saves nyingi nzuri (kupunguza idadi ya magoli)

    2: Maxi na Pacome wamecheza game nzuri sana (Rotation ya nafasi , positioning zao zilikuwa sahihi )

    3: Lawi kacheza vizuri sana kwenye kiungo nimependa Energy ya Maabad

    4: Pacome goli la 8 kwenye NBCPL ( anakupa magoli na kufanya vitu vingine vitokee uwanjani kwa dribbling na Positioning yake )

    FT: Yanga 1-0 Coastal Union .
    (Kelvin Rabson).

    Yanga walianza mchezo vizuri sana kwa kufanya kila kitu kwa usahihi pale wanapokuwa na mpira na wasipokuwa na mpira . Kivipi ? 1: Wakati wanaanza build up wanakuwa na muundo mzuri wa 2-3-4-1 unawapa walinzi wao machaguo ya kupasia mipira (Job na Bakari wanakuwa nyuma then FBs wanakuwa mstari moja na Aucho , hapo Yanga wanapata msingi sahihi ya kufika kwenye eneo la mwisho kwa kupitia katikati na pembeni ya uwanja , rahisi kuishinda pressing ya Coastal ambayo hawakuwa na idadi nzuri ya wachezaji wakati wanaweka presha . 2: Kwasababu Coastal Union hawakuweka presha vizuri kwenye mpira na positioning ya wachezaji wa Yanga ilikuwa nzuri , hapo ikawa rahisi kwa Yanga kufika eneo la mwisho baada ya hapo ni Yanga kuwa wafanisi mbele ya goli (unatumiaje nafasi kuimaliza game) . ✍️ Maxi na Pacome waliuliza maswali magumu kwa walinzi wa Coastal walibadilishana nafasi kutokana na wapi mpira ulipo , nafasi zilikuwepo hasa kwenye zile “Half Spaces” na ndio maana pamoja na Coastal kuzuia wakiwa chini mda mwingi lakini Yanga waliwafungua kirahisi kwasababu wachezaji wao walikuwa mara nyingi wanachelewa kufika kwenye eneo la tukio . ✍️ Nafikiri Coastal walijua kabisa hawawezi kupishana na Yanga kutokana na ubora wa mpinzani wake , wakaamua kuchagua vita yao ya kuzuia wakiwa chini na kuweka mtego wa kushambulia kwa kushtukiza . Lakini kuna nyakati wakivuka kwenye mstari wa kati wanachotegemea ni ubora wa mchezaji mmoja mmoja kufanya jambo kubwa . NOTE : 1: Golikipa wa Coastal “FALESI” kafanya saves nyingi nzuri (kupunguza idadi ya magoli) 2: Maxi na Pacome wamecheza game nzuri sana (Rotation ya nafasi , positioning zao zilikuwa sahihi 🔥) 3: Lawi kacheza vizuri sana kwenye kiungo 👏 nimependa Energy ya Maabad ✅ 4: Pacome goli la 8 kwenye NBCPL ( anakupa magoli na kufanya vitu vingine vitokee uwanjani kwa dribbling na Positioning yake ) FT: Yanga 1-0 Coastal Union . (Kelvin Rabson).
    0 Commenti ·0 condivisioni ·205 Views
  • "Nafahamu wote kwa pamoja tuna hamu ya kupata matokeo katika mechi hii lakini matokeo haya kuyapata kwa kushinda na kufuzu. Sisi tumeweka mazingira mazuri ambayo yataiwezesha timu yetu kufuzu.”

    “Nipo hapa kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa alkini ningependa kutoa taarifa muhimu kwamba tunaendelea kushirikiana na serikali kuimarisha usalama wa siku hiyo. Tunawataka wapenzi wetu kuhakikisha kwamba wanazingatia mazingatio yote ambayo yatawekwa ya usalama. Hatutaruhusu mtu yeyote ambaye sio Mwanasimba kutuharibia shughuli yetu.”

    “Katika mchezo uliopita walisema maneno mengi kwamba kuna wazee wafupi, mbuzi lakini tuwatumie ujumbe kwamba kama mechi aikuhusu wabaki nyumbani na sisi tumejiandaa kuthibiti hilo kama klabu.”- Zubeda Sakuru, CEO wa klabu ya Simba SC.

    "Nafahamu wote kwa pamoja tuna hamu ya kupata matokeo katika mechi hii lakini matokeo haya kuyapata kwa kushinda na kufuzu. Sisi tumeweka mazingira mazuri ambayo yataiwezesha timu yetu kufuzu.” “Nipo hapa kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa alkini ningependa kutoa taarifa muhimu kwamba tunaendelea kushirikiana na serikali kuimarisha usalama wa siku hiyo. Tunawataka wapenzi wetu kuhakikisha kwamba wanazingatia mazingatio yote ambayo yatawekwa ya usalama. Hatutaruhusu mtu yeyote ambaye sio Mwanasimba kutuharibia shughuli yetu.” “Katika mchezo uliopita walisema maneno mengi kwamba kuna wazee wafupi, mbuzi lakini tuwatumie ujumbe kwamba kama mechi aikuhusu wabaki nyumbani na sisi tumejiandaa kuthibiti hilo kama klabu.”- Zubeda Sakuru, CEO wa klabu ya Simba SC.
    0 Commenti ·0 condivisioni ·185 Views
  • "Goli 8 Asisti 9 So Far .. Kabatini kwake kuna TUZO 6 za MAN OF THE MATCH. Tuzo 3 kazibeba kwenye mechi za ugenini, Tuzo 3 kazibeba kwenye mechi za Nyumbani

    Na kubwa zaidi, Tuzo 3 za Man of The Match kazibeba kwenye MECHI 3 MFULULIZO

    Mabibi na Mabwana .. Huyu sio mwingine ni EL PROFFESSSSOR @pacom_zouzoua .. HE IS ON FIRE🫡

    Mungu aendelee kumpa afya njema Tukamilishe Jambo letu Msimu huu" - Ali Kamwe, Msemaji wa klabu ya Yanga SC.

    "Goli 8 Asisti 9 So Far .. Kabatini kwake kuna TUZO 6 za MAN OF THE MATCH. Tuzo 3 kazibeba kwenye mechi za ugenini, Tuzo 3 kazibeba kwenye mechi za Nyumbani Na kubwa zaidi, Tuzo 3 za Man of The Match kazibeba kwenye MECHI 3 MFULULIZO Mabibi na Mabwana .. Huyu sio mwingine ni EL PROFFESSSSOR @pacom_zouzoua .. HE IS ON FIRE🫡 Mungu aendelee kumpa afya njema Tukamilishe Jambo letu Msimu huu👑" - Ali Kamwe, Msemaji wa klabu ya Yanga SC.
    0 Commenti ·0 condivisioni ·136 Views
  • Wakati mwingine, ninashangaa ikiwa unatambua jinsi ninavyokupenda, ikiwa unaelewa ni kiasi gani ninajali. Huenda usielewe kikamilifu maana ya kupendwa nami, na huenda nisipate kamwe maneno ya kueleza kujitolea kwangu.

    Tangu nilipokutana na wewe, maisha yangu yalibadilika kwa njia ambazo sikuwahi kufikiria. Uwepo wako unazijaza siku zangu na mwanga na usiku wangu kwa amani. Daima jua kwamba kila wakati unapotabasamu, unalia, kila chembe ya furaha unayohisi, na kila hisia unayopata, ninaihisi pia kwa sababu wewe ni moyo wangu, na kukutazama ni kuona roho yangu.

    Kuna wakati maneno hunishinda, ninachoweza kufanya ni kutazama macho yako na kutumaini unaweza kuona undani wa upendo wangu. Nataka ujue kwamba furaha yako ni furaha yangu, na maumivu yako ni maumivu yangu. Mioyo yetu inapiga kama kitu kimoja, iliyounganishwa katika dansi ya zamani kama wakati.

    Katika ulimwengu huu mkubwa, wewe ni nanga yangu, mara kwa mara, na nyumbani. Kila wakati tunaposhiriki ni hazina ninayothamini sana. Upendo wangu kwako hauna kikomo, hauna wakati, na hauteteleki. Ni upendo unaopita maneno, upendo ambao unaweza kuhisiwa tu katika nyakati tulivu tunazoshiriki.

    Jua kwamba mimi ni wako sasa na hata milele na kwamba upendo wangu kwako hautapungua kamwe. Wewe ni kila kitu changu, moyo wangu, roho yangu, mpenzi wangu.
    Wakati mwingine, ninashangaa ikiwa unatambua jinsi ninavyokupenda, ikiwa unaelewa ni kiasi gani ninajali. Huenda usielewe kikamilifu maana ya kupendwa nami, na huenda nisipate kamwe maneno ya kueleza kujitolea kwangu. Tangu nilipokutana na wewe, maisha yangu yalibadilika kwa njia ambazo sikuwahi kufikiria. Uwepo wako unazijaza siku zangu na mwanga na usiku wangu kwa amani. Daima jua kwamba kila wakati unapotabasamu, unalia, kila chembe ya furaha unayohisi, na kila hisia unayopata, ninaihisi pia kwa sababu wewe ni moyo wangu, na kukutazama ni kuona roho yangu. Kuna wakati maneno hunishinda, ninachoweza kufanya ni kutazama macho yako na kutumaini unaweza kuona undani wa upendo wangu. Nataka ujue kwamba furaha yako ni furaha yangu, na maumivu yako ni maumivu yangu. Mioyo yetu inapiga kama kitu kimoja, iliyounganishwa katika dansi ya zamani kama wakati. Katika ulimwengu huu mkubwa, wewe ni nanga yangu, mara kwa mara, na nyumbani. Kila wakati tunaposhiriki ni hazina ninayothamini sana. Upendo wangu kwako hauna kikomo, hauna wakati, na hauteteleki. Ni upendo unaopita maneno, upendo ambao unaweza kuhisiwa tu katika nyakati tulivu tunazoshiriki. Jua kwamba mimi ni wako sasa na hata milele na kwamba upendo wangu kwako hautapungua kamwe. Wewe ni kila kitu changu, moyo wangu, roho yangu, mpenzi wangu. ♥️💘
    0 Commenti ·0 condivisioni ·304 Views
  • “Kila siku Robo tu , Kocha naye amechangia Dakika ya kwanza tu toa Ateba weka Mukwala , Halftime toa Ngoma weka Mavambo mwarabu alikuwa anakufa” Mwisho wa kunukuu

    Kuna kibanda umiza nipo hapa nimenukuu maneno ya shabiki Ingawa sijafanikiwa kujua ni shabiki wa timu gani" - Shaffih Dauda, Mchambuzi

    “Kila siku Robo tu , Kocha naye amechangia Dakika ya kwanza tu toa Ateba weka Mukwala , Halftime toa Ngoma weka Mavambo mwarabu alikuwa anakufa” Mwisho wa kunukuu Kuna kibanda umiza nipo hapa nimenukuu maneno ya shabiki Ingawa sijafanikiwa kujua ni shabiki wa timu gani" - Shaffih Dauda, Mchambuzi ✍️
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·205 Views
  • "Goli mbili ni nyingi kwenye soka la Africa,tena kwa bahati mbaya ni 2-0,hivyo kwenye mechi ya pili Simba wanatakiwa kufunga goli tatu huku wakipambana kutoruhusu goli lolote….huu ni mlima mkubwa sana.

    Kuna mtu atakwambia Simba wamecheza vizuri,walikuwa na on target 7 na total shots 18 ila mwisho wa Siku hakuna goli.

    Narudia tena mechi za mtoano watu hawaangalii umiliki wa mpira bali matokeo ya mwisho,ndio maana ushangai kuona Al ahly anapaki Bus kwenye mechi za ugenini.

    Ni kweli Simba walikuwa na umiliki mkubwa ila nyuma hawakuwa na nidhamu,Al Masry walikuwa tishio kwenye counter na hata goli la pili limetokana na counter.

    Haya ni makosa ya miaka yote ya Simba kutaka umiliki mkubwa kuliko matokeo ya kupita.

    Nilitarajia Simba kupaki bus na kupiga counter ila imekuwa tofauti na goli mbili wamefungwa baada ya kuingia kwenye mtego wa Masry

    Simba wametengeneza mlima mkubwa sana" - Hans Rafael, Mchambuzi.

    "Goli mbili ni nyingi kwenye soka la Africa,tena kwa bahati mbaya ni 2-0,hivyo kwenye mechi ya pili Simba wanatakiwa kufunga goli tatu huku wakipambana kutoruhusu goli lolote….huu ni mlima mkubwa sana. Kuna mtu atakwambia Simba wamecheza vizuri,walikuwa na on target 7 na total shots 18 ila mwisho wa Siku hakuna goli. Narudia tena mechi za mtoano watu hawaangalii umiliki wa mpira bali matokeo ya mwisho,ndio maana ushangai kuona Al ahly anapaki Bus kwenye mechi za ugenini. Ni kweli Simba walikuwa na umiliki mkubwa ila nyuma hawakuwa na nidhamu,Al Masry walikuwa tishio kwenye counter na hata goli la pili limetokana na counter. Haya ni makosa ya miaka yote ya Simba kutaka umiliki mkubwa kuliko matokeo ya kupita. Nilitarajia Simba kupaki bus na kupiga counter ila imekuwa tofauti na goli mbili wamefungwa baada ya kuingia kwenye mtego wa Masry🥲 Simba wametengeneza mlima mkubwa sana" - Hans Rafael, Mchambuzi.
    Like
    2
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·250 Views
  • Mahakama Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imebatilisha hukumu ya kifo waliyopewa Raia watatu (3) wa Marekani kwa makosa ya jinai, ugaidi na kujaribu kuipindua Serikali ya Nchi hiyo.

    Shirika la Habari la Reuters, limeripoti leo Aprili 2,2025, kuwa taarifa ya Ikulu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeeleza watatu hao sasa hawatotumikia adhabu ya kifo badala yake watatumikia kifungo cha maisha jela. Walikuwa miongoni mwa Watu (37) waliohukumiwa kifo Septemba mwaka jana (2024) na Mahakama ya Kijeshi Nchini DR Congo katika mashitaka hayo ambayo hata hivyo waliyakanusha.

    Watatu hao ambao ni Mtoto wa Raia wa Marekani mwenye asili ya DR Congo, Christian Malanga, Marcel Malanga Malu, Rafiki zake Tylor Thomson na Zalman Polun Benjamin, walipewa msamaha kutoka kwa Rais Felix Tshisekedi. Walishtakiwa kwa kuongoza genge la uhalifu lililotekeleza shambulio dhidi ya ikulu na makazi ya Mshirika wa Rais wa Nchi nchi hiyo, Mei, 2024.

    Katika Taarifa iliyosomwa na Msemaji wa Rais Félix Tshisekedi, Tyna Salama kwenye Televisheni ya Taifa, imesema kuwa Rais Tshisekedi ametoa msamaha huo kwa kubatilisha hukumu ya kifo kwa Rais hao na kuwa ya kifungo cha maisha Jela kwa sababu ya kudumisha mahusiano mazuri kimataifa na Nchi ya Marekani.

    Kubatilishwa kwa hukumu hiyo kunakuja kabla ya ziara ya Mshauri mpya Mwandamizi wa Marekani barani Afrika, Massad Boulos. Ambapo ziara hiyo ililenga kwenda DR Congo.
    Mahakama Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 imebatilisha hukumu ya kifo waliyopewa Raia watatu (3) wa Marekani 🇺🇸 kwa makosa ya jinai, ugaidi na kujaribu kuipindua Serikali ya Nchi hiyo. Shirika la Habari la Reuters, limeripoti leo Aprili 2,2025, kuwa taarifa ya Ikulu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeeleza watatu hao sasa hawatotumikia adhabu ya kifo badala yake watatumikia kifungo cha maisha jela. Walikuwa miongoni mwa Watu (37) waliohukumiwa kifo Septemba mwaka jana (2024) na Mahakama ya Kijeshi Nchini DR Congo katika mashitaka hayo ambayo hata hivyo waliyakanusha. Watatu hao ambao ni Mtoto wa Raia wa Marekani mwenye asili ya DR Congo, Christian Malanga, Marcel Malanga Malu, Rafiki zake Tylor Thomson na Zalman Polun Benjamin, walipewa msamaha kutoka kwa Rais Felix Tshisekedi. Walishtakiwa kwa kuongoza genge la uhalifu lililotekeleza shambulio dhidi ya ikulu na makazi ya Mshirika wa Rais wa Nchi nchi hiyo, Mei, 2024. Katika Taarifa iliyosomwa na Msemaji wa Rais Félix Tshisekedi, Tyna Salama kwenye Televisheni ya Taifa, imesema kuwa Rais Tshisekedi ametoa msamaha huo kwa kubatilisha hukumu ya kifo kwa Rais hao na kuwa ya kifungo cha maisha Jela kwa sababu ya kudumisha mahusiano mazuri kimataifa na Nchi ya Marekani. Kubatilishwa kwa hukumu hiyo kunakuja kabla ya ziara ya Mshauri mpya Mwandamizi wa Marekani barani Afrika, Massad Boulos. Ambapo ziara hiyo ililenga kwenda DR Congo.
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·355 Views
  • Rais wa Marekani , DonaldTrump, ameibua mjadala mkali baada ya kusema kuwa kuna uwezekano wa yeye kuwania muhula wa tatu, licha ya Katiba ya Marekani kupiga marufuku jambo hilo kupitia Marekebisho ya 22. Katika mahojiano na NBCNews, Rais huyo hakutaka kufuta uwezekano wa kuwania tena Urais baada ya kumaliza mihula miwili, akidai kuwa kuna njia za kufanya hilo kutokea. Alisisitiza kuwa "hakuwa anatania," jambo ambalo limeibua hofu miongoni mwa Wachambuzi wa siasa na Wanaharakati wa demokrasia Nchini humo.

    Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, Rais haruhusiwi kutawala kwa zaidi ya mihula miwili ya miaka minne minne. Marekebisho ya 22 yaliwekwa ili kuzuia Mtu mmoja kuwa na mamlaka ya muda mrefu kama ilivyokuwa kwa Franklin D. Roosevelt, ambaye altawala kwa zaidi ya mihula miwili kabla ya marekebisho hayo kuidhinishwa mwaka 1951.

    Kauli ya Trump imeibua maswali kuhusu mbinu anazoweza kutumia kutafuta muhula wa tatu. Wachambuzi wa sheria wanabainisha kuwa ili hilo litokee, ama katiba ibadilishwe rasmi kwa marekebisho mapya, au ipatikane tafsiri mpya ya kisheria inayomruhusu kugombea tena. Hata hivyo, mchakato wa kubadili katiba ni mgumu na unahitaji ridhaa ya Bunge pamoja na Majimbo mengi ya Marekani.

    Baadhi ya Wafuasi wa Donald Trump wameunga mkono kauli yake, wakidai kuwa anastahili muda zaidi wa kuongoza Nchi. Hata hivyo, Wakosoaji wake wanasema kuwa hatua yoyote ya kupindua Marekebisho ya 22 inaweza kuwa tishio kwa demokrasia ya Marekani na kuweka msingi wa uongozi wa kiimla.

    Rais wa Marekani 🇺🇸, DonaldTrump, ameibua mjadala mkali baada ya kusema kuwa kuna uwezekano wa yeye kuwania muhula wa tatu, licha ya Katiba ya Marekani kupiga marufuku jambo hilo kupitia Marekebisho ya 22. Katika mahojiano na NBCNews, Rais huyo hakutaka kufuta uwezekano wa kuwania tena Urais baada ya kumaliza mihula miwili, akidai kuwa kuna njia za kufanya hilo kutokea. Alisisitiza kuwa "hakuwa anatania," jambo ambalo limeibua hofu miongoni mwa Wachambuzi wa siasa na Wanaharakati wa demokrasia Nchini humo. Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, Rais haruhusiwi kutawala kwa zaidi ya mihula miwili ya miaka minne minne. Marekebisho ya 22 yaliwekwa ili kuzuia Mtu mmoja kuwa na mamlaka ya muda mrefu kama ilivyokuwa kwa Franklin D. Roosevelt, ambaye altawala kwa zaidi ya mihula miwili kabla ya marekebisho hayo kuidhinishwa mwaka 1951. Kauli ya Trump imeibua maswali kuhusu mbinu anazoweza kutumia kutafuta muhula wa tatu. Wachambuzi wa sheria wanabainisha kuwa ili hilo litokee, ama katiba ibadilishwe rasmi kwa marekebisho mapya, au ipatikane tafsiri mpya ya kisheria inayomruhusu kugombea tena. Hata hivyo, mchakato wa kubadili katiba ni mgumu na unahitaji ridhaa ya Bunge pamoja na Majimbo mengi ya Marekani. Baadhi ya Wafuasi wa Donald Trump wameunga mkono kauli yake, wakidai kuwa anastahili muda zaidi wa kuongoza Nchi. Hata hivyo, Wakosoaji wake wanasema kuwa hatua yoyote ya kupindua Marekebisho ya 22 inaweza kuwa tishio kwa demokrasia ya Marekani na kuweka msingi wa uongozi wa kiimla.
    0 Commenti ·0 condivisioni ·390 Views
  • "Marekani mpaka sasa hawajasaini mkataba wa kuilinda Congo mchakato umekuwa mrefu. Jiulize vile vikwazo vya Magharibi walivyoiwekea Rwanda vimeishia wapi

    Kagame anajua anachokifanya ndio maana licha ya ripoti za UN , US na EU kuonyesha Rwanda wanaifadhili M23 plus Vikwazo hakuna kilichobadilika Congo

    Wanachokifanya wanaoibia Congo na Africa ni ile ile mbinu ya wakati wa ukoloni inaitwa "Divided and Rule " yaani wagawanywe uwatawale nakumbuka hii mbinu pia enzi hizo ndio iliyozaa utani wa jadi wa Yanga na Simba

    Oooh Africa " - Zungu, Mchambuzi wa Siasa na Mtangazaji.

    "Marekani mpaka sasa hawajasaini mkataba wa kuilinda Congo mchakato umekuwa mrefu. Jiulize vile vikwazo vya Magharibi walivyoiwekea Rwanda vimeishia wapi 😀😀😀😀 Kagame anajua anachokifanya ndio maana licha ya ripoti za UN , US na EU kuonyesha Rwanda wanaifadhili M23 plus Vikwazo hakuna kilichobadilika Congo 😭😭😭😭 Wanachokifanya wanaoibia Congo na Africa ni ile ile mbinu ya wakati wa ukoloni inaitwa "Divided and Rule " yaani wagawanywe uwatawale nakumbuka hii mbinu pia enzi hizo ndio iliyozaa utani wa jadi wa Yanga na Simba Oooh Africa🌍 😭" - Zungu, Mchambuzi wa Siasa na Mtangazaji.
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·407 Views
  • Najua umesalitiwa na wale uliowaamini, umeachwa ulipohitaji kupendwa, na umedhihakiwa wakati ulichotaka ni kuungwa mkono. Najua umechoka. Najua umepigana vita hakuna mtu aliyeona, kulia kimya, na kuvumilia maumivu ambayo maneno hayawezi kuelezea.

    Maisha hayajakuwa sawa kwako. Milango imegongwa usoni mwako. Umewatazama wengine wakiinuka huku wewe ukiwa umekwama katika sehemu moja. Umeomba, kutumaini, na kungoja, lakini hakuna kinachoonekana kubadilika. Inaumiza. Ni chungu. Inachosha.

    Lakini nisikilizeni, na nisikilize kwa makini: USIKATE TAMAA.

    Kila mtu mkubwa unayekuvutia leo alikuwa hapo ulipo sasa. Walihisi kile unachohisi. Walihangaika, walilia, na walitilia shaka wenyewe. Lakini hawakuacha. Hawakuruhusu maumivu yao yawafafanue. Waliendelea kusonga mbele, hata pale nguvu zao zilipopungua. Na ndio maana leo, ulimwengu unawaadhimisha.

    Lazima uelewe ukweli huu: Kadiri hatima yako inavyokuwa kubwa, ndivyo vita yako inavyokuwa kubwa. KILA KIWANGO KIPYA UNACHOFIKIA, KUNA SHETANI MPYA ANAKUSUBIRI. Ulipokuwa maskini, hakuna aliyekuonea wivu. Lakini unapoanza kufanya maendeleo, ghafla, watu wanaanza kukuchukia. Ulipokuwa huna kazi, hakuna aliyezungumza juu yako. Lakini mara tu unapopata kazi nzuri, wanaanza kueneza uvumi. Ulipokuwa ukihangaika, hakuna aliyejali. Lakini wakati unapoanza kufanikiwa, maadui huonekana kutoka popote.

    Ibilisi hapigani na watu ambao hawaendi popote. Sababu ya wewe kukabiliwa na vita vingi ni kwa sababu hatima yako ni kubwa; sababu ya maisha kukujaribu sana ni kwa sababu kesho yako ni kubwa. Huna mateso kwa sababu wewe ni dhaifu. Unateseka kwa sababu wewe ni IMARA, na maisha yanajua kwamba mara tu unapopitia, hautazuilika.

    Kwa hivyo, usikatishwe tamaa na vita unavyokabili sasa. Wao ni ishara kwamba unasonga mbele. Usiruhusu maumivu yakufanye uchungu. Usiruhusu tamaa kuua ndoto zako. Endelea kupigana. Endelea kusukuma. Endelea kuamini. Wakati wako utafika.

    Kuna toleo lako katika siku zijazo ambalo lina nguvu zaidi, busara, na mafanikio zaidi kuliko wewe sasa. Toleo hilo lako linasubiri. Lakini ili kuwa mtu huyo, lazima upitie moto huu. Sio rahisi, lakini nakuahidi, itafaa.

    Lia ikiwa ni lazima, lakini baada ya kulia, futa machozi yako na uendelee kusonga. Lalamika ikibidi, lakini baada ya kulalamika, simama na upigane tena. Jisikie dhaifu ikiwa ni lazima, lakini usiache kujaribu.

    Wakati wako unakuja. Ufanisi wako umekaribia. Maumivu hayatadumu milele. Siku moja, utaangalia nyuma na kugundua kuwa kila kitu ulichopitia kilikufanya kuwa mtu mwenye nguvu, aliyefanikiwa ambaye unakusudiwa kuwa.

    Kwa hivyo, endelea kusonga mbele. Ushindi wako uko njiani.

    Quadic Bangura
    Najua umesalitiwa na wale uliowaamini, umeachwa ulipohitaji kupendwa, na umedhihakiwa wakati ulichotaka ni kuungwa mkono. Najua umechoka. Najua umepigana vita hakuna mtu aliyeona, kulia kimya, na kuvumilia maumivu ambayo maneno hayawezi kuelezea. Maisha hayajakuwa sawa kwako. Milango imegongwa usoni mwako. Umewatazama wengine wakiinuka huku wewe ukiwa umekwama katika sehemu moja. Umeomba, kutumaini, na kungoja, lakini hakuna kinachoonekana kubadilika. Inaumiza. Ni chungu. Inachosha. Lakini nisikilizeni, na nisikilize kwa makini: USIKATE TAMAA. Kila mtu mkubwa unayekuvutia leo alikuwa hapo ulipo sasa. Walihisi kile unachohisi. Walihangaika, walilia, na walitilia shaka wenyewe. Lakini hawakuacha. Hawakuruhusu maumivu yao yawafafanue. Waliendelea kusonga mbele, hata pale nguvu zao zilipopungua. Na ndio maana leo, ulimwengu unawaadhimisha. Lazima uelewe ukweli huu: Kadiri hatima yako inavyokuwa kubwa, ndivyo vita yako inavyokuwa kubwa. KILA KIWANGO KIPYA UNACHOFIKIA, KUNA SHETANI MPYA ANAKUSUBIRI. Ulipokuwa maskini, hakuna aliyekuonea wivu. Lakini unapoanza kufanya maendeleo, ghafla, watu wanaanza kukuchukia. Ulipokuwa huna kazi, hakuna aliyezungumza juu yako. Lakini mara tu unapopata kazi nzuri, wanaanza kueneza uvumi. Ulipokuwa ukihangaika, hakuna aliyejali. Lakini wakati unapoanza kufanikiwa, maadui huonekana kutoka popote. Ibilisi hapigani na watu ambao hawaendi popote. Sababu ya wewe kukabiliwa na vita vingi ni kwa sababu hatima yako ni kubwa; sababu ya maisha kukujaribu sana ni kwa sababu kesho yako ni kubwa. Huna mateso kwa sababu wewe ni dhaifu. Unateseka kwa sababu wewe ni IMARA, na maisha yanajua kwamba mara tu unapopitia, hautazuilika. Kwa hivyo, usikatishwe tamaa na vita unavyokabili sasa. Wao ni ishara kwamba unasonga mbele. Usiruhusu maumivu yakufanye uchungu. Usiruhusu tamaa kuua ndoto zako. Endelea kupigana. Endelea kusukuma. Endelea kuamini. Wakati wako utafika. Kuna toleo lako katika siku zijazo ambalo lina nguvu zaidi, busara, na mafanikio zaidi kuliko wewe sasa. Toleo hilo lako linasubiri. Lakini ili kuwa mtu huyo, lazima upitie moto huu. Sio rahisi, lakini nakuahidi, itafaa. Lia ikiwa ni lazima, lakini baada ya kulia, futa machozi yako na uendelee kusonga. Lalamika ikibidi, lakini baada ya kulalamika, simama na upigane tena. Jisikie dhaifu ikiwa ni lazima, lakini usiache kujaribu. Wakati wako unakuja. Ufanisi wako umekaribia. Maumivu hayatadumu milele. Siku moja, utaangalia nyuma na kugundua kuwa kila kitu ulichopitia kilikufanya kuwa mtu mwenye nguvu, aliyefanikiwa ambaye unakusudiwa kuwa. Kwa hivyo, endelea kusonga mbele. Ushindi wako uko njiani. Quadic Bangura
    Love
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·464 Views
  • JE, UNAMLETEA UHAI MPENZI WAKO, AU UNALETA KISU?

    Upendo unakusudiwa kujenga, sio kuvunja. Uhusiano unakusudiwa kuwa patakatifu, sio kichinjio. Nafsi mbili zinapokutana, zinapaswa kuleta uhai kwa kila mmoja, sio majeraha, sio makovu, sio huzuni. Hata hivyo, ukweli wa kusikitisha ni kwamba watu wengi huingia kwenye mahusiano wakitarajia kupendwa lakini hupokea maumivu. Wanatazamia furaha lakini wanakutana na taabu. Badala ya mwenzi anayeleta uzima, wanajikuta wanaishi na mtu ambaye ana kisu, akipunguza ujasiri wao, amani na heshima. Kwa hiyo, unaleta uhai kwa mpenzi wako, au unaleta kisu? Upendo unakusudiwa kumpa uhai yule unayedai kumpenda. Katika Mwanzo Mungu alimpulizia Adamu pumzi ya uhai, naye akawa nafsi hai. Kwa njia hiyo hiyo, uhusiano unapaswa kupumua maisha ndani ya mtu, sio kukimbia maisha kutoka kwao. Unapomhimiza mwenzako kufuata ndoto zake, unaleta uzima. Unapozungumza maneno ya fadhili, heshima, na uthibitisho, unaleta uzima. Unapovumilia mapungufu yao na kutembea nao katika mapambano yao, unaleta uhai. Wakati uwepo wako ni chanzo cha amani na si chanzo cha msongo wa mawazo, unaleta uhai. Upendo haupaswi kamwe kuhisi kama kutembea kwenye uwanja wa vita, ambapo kila neno, kila kitendo na kila siku huhisi kama kupigania kuishi. Mpenzi wako hapaswi kujisikia salama nje kuliko ndani ya uhusiano. Ikiwa unampenda mtu, anapaswa kustawi chini ya upendo wako, sio kukauka.

    Kisu sio lazima kiwe cha mwili kila wakati. Vidonda vingine huenda zaidi kuliko mwili; wanachoma roho. Baadhi yetu, badala ya kuleta uhai, kuleta kisu. Tunaleta kisu cha maneno makali, kukata ndani ya kujithamini kwa mpenzi wetu. Tunaleta kisu cha kulinganisha, na kuwafanya wahisi kama hawatoshi vya kutosha. Tunakuja na kisu cha kupuuza, na njaa ya upendo na tahadhari wanayotamani. Kwa namna fulani, pia kuja na kisu cha usaliti, ambapo uaminifu wetu ni kwa maneno tu lakini si kwa vitendo. Watu wengine wanakufa kihisia na kiroho kwa sababu ya mtu wanayempenda. Furaha yao inafifia taratibu. Kujiamini kwao kunatoweka. Kicheko chao hakitoki tena moyoni. Kwa nini? Kwa sababu aliyekusudiwa kuwalisha sasa ndiye anayewaangamiza. Je, wewe ni mtoaji wa uzima au mleta maumivu? Je, watu hupata amani mbele yako au wasiwasi wako? Je, unainua au kubomoa? Ikiwa mtu unayempenda anafurahi zaidi wakati haupo kuliko wakati haupo, ni ishara kwamba unaweza kuwa unaleta kisu, sio maisha. Upendo unapaswa kuwa kama bustani ambayo watu wawili hukua pamoja. Lakini upendo unawezaje kukua ikiwa mwenzi mmoja anamwaga maji wakati mwingine anamwaga sumu? Ikiwa mmoja anapanda mbegu wakati mwingine anang'oa? Chagua kusema maneno ya uhai badala ya maneno yanayoua kujiamini. Chagua kukumbatia dosari badala ya kuzitumia kama silaha. Chagua kuunga mkono ndoto badala ya kuzikejeli. Chagua kuwa mahali salama, sio eneo la vita.

    Upendo unapaswa kuwa zawadi, sio mzigo. Baraka, si laana. Nguvu ya uponyaji, sio chanzo cha majeraha. Je, katika maisha ya mwenzako wewe ni mganga au mharibifu? Unaleta uhai au kisu?

    Credit
    Albert Nwosu
    JE, UNAMLETEA UHAI MPENZI WAKO, AU UNALETA KISU? Upendo unakusudiwa kujenga, sio kuvunja. Uhusiano unakusudiwa kuwa patakatifu, sio kichinjio. Nafsi mbili zinapokutana, zinapaswa kuleta uhai kwa kila mmoja, sio majeraha, sio makovu, sio huzuni. Hata hivyo, ukweli wa kusikitisha ni kwamba watu wengi huingia kwenye mahusiano wakitarajia kupendwa lakini hupokea maumivu. Wanatazamia furaha lakini wanakutana na taabu. Badala ya mwenzi anayeleta uzima, wanajikuta wanaishi na mtu ambaye ana kisu, akipunguza ujasiri wao, amani na heshima. Kwa hiyo, unaleta uhai kwa mpenzi wako, au unaleta kisu? Upendo unakusudiwa kumpa uhai yule unayedai kumpenda. Katika Mwanzo Mungu alimpulizia Adamu pumzi ya uhai, naye akawa nafsi hai. Kwa njia hiyo hiyo, uhusiano unapaswa kupumua maisha ndani ya mtu, sio kukimbia maisha kutoka kwao. Unapomhimiza mwenzako kufuata ndoto zake, unaleta uzima. Unapozungumza maneno ya fadhili, heshima, na uthibitisho, unaleta uzima. Unapovumilia mapungufu yao na kutembea nao katika mapambano yao, unaleta uhai. Wakati uwepo wako ni chanzo cha amani na si chanzo cha msongo wa mawazo, unaleta uhai. Upendo haupaswi kamwe kuhisi kama kutembea kwenye uwanja wa vita, ambapo kila neno, kila kitendo na kila siku huhisi kama kupigania kuishi. Mpenzi wako hapaswi kujisikia salama nje kuliko ndani ya uhusiano. Ikiwa unampenda mtu, anapaswa kustawi chini ya upendo wako, sio kukauka. Kisu sio lazima kiwe cha mwili kila wakati. Vidonda vingine huenda zaidi kuliko mwili; wanachoma roho. Baadhi yetu, badala ya kuleta uhai, kuleta kisu. Tunaleta kisu cha maneno makali, kukata ndani ya kujithamini kwa mpenzi wetu. Tunaleta kisu cha kulinganisha, na kuwafanya wahisi kama hawatoshi vya kutosha. Tunakuja na kisu cha kupuuza, na njaa ya upendo na tahadhari wanayotamani. Kwa namna fulani, pia kuja na kisu cha usaliti, ambapo uaminifu wetu ni kwa maneno tu lakini si kwa vitendo. Watu wengine wanakufa kihisia na kiroho kwa sababu ya mtu wanayempenda. Furaha yao inafifia taratibu. Kujiamini kwao kunatoweka. Kicheko chao hakitoki tena moyoni. Kwa nini? Kwa sababu aliyekusudiwa kuwalisha sasa ndiye anayewaangamiza. Je, wewe ni mtoaji wa uzima au mleta maumivu? Je, watu hupata amani mbele yako au wasiwasi wako? Je, unainua au kubomoa? Ikiwa mtu unayempenda anafurahi zaidi wakati haupo kuliko wakati haupo, ni ishara kwamba unaweza kuwa unaleta kisu, sio maisha. Upendo unapaswa kuwa kama bustani ambayo watu wawili hukua pamoja. Lakini upendo unawezaje kukua ikiwa mwenzi mmoja anamwaga maji wakati mwingine anamwaga sumu? Ikiwa mmoja anapanda mbegu wakati mwingine anang'oa? Chagua kusema maneno ya uhai badala ya maneno yanayoua kujiamini. Chagua kukumbatia dosari badala ya kuzitumia kama silaha. Chagua kuunga mkono ndoto badala ya kuzikejeli. Chagua kuwa mahali salama, sio eneo la vita. Upendo unapaswa kuwa zawadi, sio mzigo. Baraka, si laana. Nguvu ya uponyaji, sio chanzo cha majeraha. Je, katika maisha ya mwenzako wewe ni mganga au mharibifu? Unaleta uhai au kisu? Credit Albert Nwosu
    Love
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·447 Views
  • PICHA YA SIMBA HUYU NI FUNZO MAISHANI:
    ------------------------------------------------------

    Hivi ndivyo mfalme wa pori anavyoonekana akiwa kwenye siku za mwisho za maisha yake. Jinsi alivyokonda, kujua idadi ya mbavu zake hata huitaji msaada wa calculator.

    Hii picha ilipigwa na "Larry Pannell."

    Alifanikiwa kupata picha ya Simba aliyekuwa kwenye hitimisho la kuvuta pumzi za mwisho. Katika huu ulimwengu wenye mafungamano na dhambi.

    "Larry Pannell" anasema:

    Nilimkuta huyu simba amelala kwenye majani. Akiwa amechoka, miguu ikionekana kumnyima ushirikiano wa kutembea.

    Sikuwa na lakufanya zaidi ya kusimama mita kadhaa. Macho yakifanya ushuhuda wa kutazama, "King of savannah" akipoteza uhai chini ya kivuli cha mti.

    Nikiwa nimesimama kimya. Nilishusha chini camera yangu. Tulitazamana na simba, tukafumba macho yetu pamoja.

    Jinsi mfalme wa nyika alivyokuwa akihangaika kuhema. Pumzi zilionekana kuwa bidhaa hadimu kwenye duka la mapafu yake.

    Kifua chake kilikuwa kikipanda na kushuka. Ishara ya kuonyesha anavuta pumzi za mwisho, kabla ya kukipa ruhusa kifo kiondoke na roho yake.

    Ghafla eneo alilolala Simba ukazaliwa ukimya. Mfalme wa pori akawa haemi wala kutikisika. Mauti ikawa imehitimisha simulizi ya ubabe wake mbugani.

    Hakika maisha ya binadamu na wanyama ni simulizi fupi sana."

    Haijalishi una nguvu kiasi gani. Kuna nyakati zitafika nguvu zitafanya mgomo wa kuishi mwilini mwako. Zitaupisha udhaifu uchukue nafasi ya kukutawala. Udhaifu nao ukikutawala, utayaita maradhi. Bila hiyari utajikuta umekigeuza kitanda kuwa rafiki."

    Kuna shule ya bure hapa: Nguvu tulizonazo ni kitu cha kupita. Hata uzuri umpao kiburi mwanamke una ukomo. Licha ya kujidanganya kwa make up na wanja. Lakini hawezi kuzuia muanguko wa mashavu, uzee unapoanza kumuondoa kwenye kundi la warembo.

    "Chini ya jua kila kitu kina mwanzo na mwisho."

    Hivyo katika maisha tusisahau kuvipa kipaumbele vitu hivi. Utu, wema, ukarimu, heshima, na unyenyekevu.

    Tusaidie wenye maradhi, tuwajali wasiojiweza, na viongozi tusitumie madaraka vibaya.

    Tutende mema tukiamini. Kuna siku pumzi zitamaliza mkataba wa kuishi ndani ya matundu ya pua zetu. Baada ya hapo sisi wote tutalala mauti."

    Imeandikwa na Green Osward
    PICHA YA SIMBA HUYU NI FUNZO MAISHANI: ------------------------------------------------------ Hivi ndivyo mfalme wa pori anavyoonekana akiwa kwenye siku za mwisho za maisha yake. Jinsi alivyokonda, kujua idadi ya mbavu zake hata huitaji msaada wa calculator. Hii picha ilipigwa na "Larry Pannell." Alifanikiwa kupata picha ya Simba aliyekuwa kwenye hitimisho la kuvuta pumzi za mwisho. Katika huu ulimwengu wenye mafungamano na dhambi. "Larry Pannell" anasema: Nilimkuta huyu simba amelala kwenye majani. Akiwa amechoka, miguu ikionekana kumnyima ushirikiano wa kutembea. Sikuwa na lakufanya zaidi ya kusimama mita kadhaa. Macho yakifanya ushuhuda wa kutazama, "King of savannah" akipoteza uhai chini ya kivuli cha mti. Nikiwa nimesimama kimya. Nilishusha chini camera yangu. Tulitazamana na simba, tukafumba macho yetu pamoja. Jinsi mfalme wa nyika alivyokuwa akihangaika kuhema. Pumzi zilionekana kuwa bidhaa hadimu kwenye duka la mapafu yake. Kifua chake kilikuwa kikipanda na kushuka. Ishara ya kuonyesha anavuta pumzi za mwisho, kabla ya kukipa ruhusa kifo kiondoke na roho yake. Ghafla eneo alilolala Simba ukazaliwa ukimya. Mfalme wa pori akawa haemi wala kutikisika. Mauti ikawa imehitimisha simulizi ya ubabe wake mbugani. Hakika maisha ya binadamu na wanyama ni simulizi fupi sana." Haijalishi una nguvu kiasi gani. Kuna nyakati zitafika nguvu zitafanya mgomo wa kuishi mwilini mwako. Zitaupisha udhaifu uchukue nafasi ya kukutawala. Udhaifu nao ukikutawala, utayaita maradhi. Bila hiyari utajikuta umekigeuza kitanda kuwa rafiki." Kuna shule ya bure hapa: Nguvu tulizonazo ni kitu cha kupita. Hata uzuri umpao kiburi mwanamke una ukomo. Licha ya kujidanganya kwa make up na wanja. Lakini hawezi kuzuia muanguko wa mashavu, uzee unapoanza kumuondoa kwenye kundi la warembo. "Chini ya jua kila kitu kina mwanzo na mwisho." Hivyo katika maisha tusisahau kuvipa kipaumbele vitu hivi. Utu, wema, ukarimu, heshima, na unyenyekevu. Tusaidie wenye maradhi, tuwajali wasiojiweza, na viongozi tusitumie madaraka vibaya. Tutende mema tukiamini. Kuna siku pumzi zitamaliza mkataba wa kuishi ndani ya matundu ya pua zetu. Baada ya hapo sisi wote tutalala mauti." Imeandikwa na Green Osward
    Love
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·593 Views
  • Mchambuzi Farhan JR.

    Nimeona andiko la Waukae @zakazakazi kuhusu TFF kutengeneza Vijana ambalo lilipaswa kuwa jukumu la Klabu na akienda mbali kusema kwamba TFF ndio Shirikisho pekee duniani ambalo lina kituo ambacho kinazalisha na kulea vipaji vya vijana, kwanza kabla ya kupingana nae kuna kitu kwanza nataka kukiweka sawa kwenye eneo hilo.

    Duniani kote Mashirikisho kama TFF yamejikita zaidi kwenye DEVELOPMENT PROJECTS yaani Miradi ya maendeleo kisha wakaachia Mashindano kadhaa yasimamiwe na Bodi zao za Ligi kwa 90% bila kuyaingilia, TFF anachokifanya ni sahihi lakini pia sio sahihi sana kufanya yeye alipaswa kuwa na CLINICS tu ila kuna changamoto sehemu ambayo imeletwa na TFF wenyewe.

    Duniani Klabu zinaweza kuendesha miradi ya Vijana kwasababu kuna kitu kinaitwa FALSAFA ya nchi kwenye mpira, kuanzia mifumo, afya tiba, afya lishe na miundo yote ambayo portifolio hutoka Shirikisho (TFF) Klabu zinaenda kutekeleza mifumo hiyo na kuadjust baadhi ya maeneo halafu Vijana wakienda Clinics za Kitaifa wanaenda kukazia tu.

    Swali linakuja Je Waukaye @zakazakazi FALSAFA ya Tanzania kwenye mpira wa Miguu ni ipi? Iliwasilishwa lini? Anayo nani? Hilo ni Jukumu la TFF ambalo halijatekelezwa, kuna kitu kinaitwa TALENT ID FRAMEWORK ili kupata Vijana je tunayo? Ipoje, anayo nani? Inasemaje? Klabu hazina Mwongozo kutoka kwa TFF? Academy zote nchini zipite humo LAZIMA TFF wafanye wanachoweza, tupo katikati, TFF ASIMAMIE HILO KIKAMILIFU.

    TFF wasiende mbali waende tu hapo Uganda ilipo FUFA, wana Talent ID Framework ambayo Mashirikisho yoote yalipigwa huo Msasa sambamba na Kamati zao tendaji, ndio maana Uganda wapo mbali mno kwenye soka la Vijana kwenye Klabu zao na National Team, kwasababu wana ramani wanaifuata, wameintergrate mfumo wao na FIFA Talent Development Schemes (TDS) je sisi lini tutaforce Klabu zipite humo?

    TFF anajipa majukumu ambayo mengine sio ya kwake, kujadili mikataba ya kibiashara sio Jukumu lake bali Vilabu na Bodi yao, TFF anabaki kama Baba pekee, duniani kote TFF zao zina majukumu yao ukitoa michuano ya FA na Ngao basi Ligi Kuu sio mali yao, TFF ASIMAMIE HASWA JUKUMU LA MAENDELEO NI LAKE.

    Mchambuzi Farhan JR. Nimeona andiko la Waukae @zakazakazi kuhusu TFF kutengeneza Vijana ambalo lilipaswa kuwa jukumu la Klabu na akienda mbali kusema kwamba TFF ndio Shirikisho pekee duniani ambalo lina kituo ambacho kinazalisha na kulea vipaji vya vijana, kwanza kabla ya kupingana nae kuna kitu kwanza nataka kukiweka sawa kwenye eneo hilo. Duniani kote Mashirikisho kama TFF yamejikita zaidi kwenye DEVELOPMENT PROJECTS yaani Miradi ya maendeleo kisha wakaachia Mashindano kadhaa yasimamiwe na Bodi zao za Ligi kwa 90% bila kuyaingilia, TFF anachokifanya ni sahihi lakini pia sio sahihi sana kufanya yeye alipaswa kuwa na CLINICS tu ila kuna changamoto sehemu ambayo imeletwa na TFF wenyewe. Duniani Klabu zinaweza kuendesha miradi ya Vijana kwasababu kuna kitu kinaitwa FALSAFA ya nchi kwenye mpira, kuanzia mifumo, afya tiba, afya lishe na miundo yote ambayo portifolio hutoka Shirikisho (TFF) Klabu zinaenda kutekeleza mifumo hiyo na kuadjust baadhi ya maeneo halafu Vijana wakienda Clinics za Kitaifa wanaenda kukazia tu. Swali linakuja Je Waukaye @zakazakazi FALSAFA ya Tanzania kwenye mpira wa Miguu ni ipi? Iliwasilishwa lini? Anayo nani? Hilo ni Jukumu la TFF ambalo halijatekelezwa, kuna kitu kinaitwa TALENT ID FRAMEWORK ili kupata Vijana je tunayo? Ipoje, anayo nani? Inasemaje? Klabu hazina Mwongozo kutoka kwa TFF? Academy zote nchini zipite humo LAZIMA TFF wafanye wanachoweza, tupo katikati, TFF ASIMAMIE HILO KIKAMILIFU. TFF wasiende mbali waende tu hapo Uganda ilipo FUFA, wana Talent ID Framework ambayo Mashirikisho yoote yalipigwa huo Msasa sambamba na Kamati zao tendaji, ndio maana Uganda wapo mbali mno kwenye soka la Vijana kwenye Klabu zao na National Team, kwasababu wana ramani wanaifuata, wameintergrate mfumo wao na FIFA Talent Development Schemes (TDS) je sisi lini tutaforce Klabu zipite humo? TFF anajipa majukumu ambayo mengine sio ya kwake, kujadili mikataba ya kibiashara sio Jukumu lake bali Vilabu na Bodi yao, TFF anabaki kama Baba pekee, duniani kote TFF zao zina majukumu yao ukitoa michuano ya FA na Ngao basi Ligi Kuu sio mali yao, TFF ASIMAMIE HASWA JUKUMU LA MAENDELEO NI LAKE.
    Like
    2
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·396 Views
  • Rais wa Nchi ya Burundi , Evariste Ndayishimiye anasema kuwa Nchi ya Rwanda ina mpango wa kuivamia Burundi kupitia Congo ambapo anasema Nchi hiyo itakuwa imekosea sana.

    “Tunajua kwamba Rwanda inajaribu kutushambulia kupitia eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kupitia vuguvugu la Red-Tabara. Lakini tunawaambia kwamba ikiwa wanataka kushambulia Bujumbura kupitia Congo na sisi Kigali hatuko mbali kupitia Kirundo,” alisema Rais Evariste Ndayishimiye

    Baada ya kauli hiyo, Msemaji wa Serikali ya Rwanda Yolande Makolo amesema kuwa, ameshangazwa na kauli ya Rais Evariste Ndayishimiye huku akihoji Rais Ndayishimiye anaeleza kuwa ana taarifa za kuaminika kuwa Rwanda ina mpango wa kushambulia Burundi ?. Msemaji huyo alisema pia endapo hali hiyo ikitokea basi migogoro inaweza kuwa na maafa kwani inaweza kusambaa katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki na kati.

    Rais Ndayishimiye amemalizia kwa kusema kuwa tayari ameshatuma Wajumbe kadhaa kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame wa kumtaka atekeleze makubaliano ambayo yatazileta pamoja Nchi hizo mbili pamoja lakini hadi leo hii hakuna majibu yoyote yaliyotolewa na bado anayasubiri pia.

    Rais wa Nchi ya Burundi 🇧🇮, Evariste Ndayishimiye anasema kuwa Nchi ya Rwanda 🇷🇼 ina mpango wa kuivamia Burundi kupitia Congo ambapo anasema Nchi hiyo itakuwa imekosea sana. “Tunajua kwamba Rwanda inajaribu kutushambulia kupitia eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kupitia vuguvugu la Red-Tabara. Lakini tunawaambia kwamba ikiwa wanataka kushambulia Bujumbura kupitia Congo na sisi Kigali hatuko mbali kupitia Kirundo,” alisema Rais Evariste Ndayishimiye Baada ya kauli hiyo, Msemaji wa Serikali ya Rwanda Yolande Makolo amesema kuwa, ameshangazwa na kauli ya Rais Evariste Ndayishimiye huku akihoji Rais Ndayishimiye anaeleza kuwa ana taarifa za kuaminika kuwa Rwanda ina mpango wa kushambulia Burundi ?. Msemaji huyo alisema pia endapo hali hiyo ikitokea basi migogoro inaweza kuwa na maafa kwani inaweza kusambaa katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki na kati. Rais Ndayishimiye amemalizia kwa kusema kuwa tayari ameshatuma Wajumbe kadhaa kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame wa kumtaka atekeleze makubaliano ambayo yatazileta pamoja Nchi hizo mbili pamoja lakini hadi leo hii hakuna majibu yoyote yaliyotolewa na bado anayasubiri pia.
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·278 Views
  • "Najisikia vibaya namna watu wanavyoniona na kuanza kuniita Yesu, wanafikia hata kutundika picha zangu katika nyumba zao, mimi ni mwigizaji tu, mimi ni mtu" - Jonathan Roumie(50), mwigizaji wa Marekani

    Aidha, Jonathan Roumie katika mahojiano amesema maisha yake binafsi alikuwa na hali mbaya kiuchumi hakuwa na uhakika siku inayofuata atakula nini, alikuwa mwigizaji ila kiuchumi alikuwa bado hajafanikiwa. Baada ya mambo kuzidi kuwa magumu siku moja ni kama alikuwa anamuomba Mungu kuhusu hali anayopitia ili mambo yake yakae sawa

    Baada ya miezi kama mitatu ndio akapata nafasi ya kuigiza kama Yesu katika series ya "The Chosen" iliyoanza kuoneshwa 2017 ambayo imejipatia umaarufu mkubwa sana hadi sasa imetazamwa na watu zaidi ya milioni 250 na misimu mipya inafuata huku ikipongezwa kwa kinachoonekana kuigizwa

    Umaarufu wa uhusika wake kama Yesu umempa umaarufu mkubwa na fursa nyingi ikiwemo katika mikutano na makongamano makubwa ya kidini na app za dini ya kikiristo

    Jonathan ambaye ni mkatoliki, alipoulizwa na New York Times, je ni tukio gani gumu analokumbuka ambalo alishakutana nalo baada ya kuigiza kama Yesu, amejibu kwa kusema kuna kipindi alikuwa katika mkutano kwenye uwanja wenye watu takribani 40,000 baadaye alishuka stejini akaenda kwenye chumba fulani uwanjani hapo, mmoja wa walinzi alikuja akamwambia nje kuna mwanamke ana mtoto kwenye kiti cha magurudumu anaomba kusalimiana na wewe

    Jonathan alitoka akaonana na mwanamke husika na mwanae ambaye kwa ufupi alieleza jinsi Yesu alivyoponya mtu katika hiyo series ya "The Chosen" na kusema angependa mwanae pia apone yaani akimtaka Jonathan amponye mtoto wake. Ilibidi Jonathan amueleze ukweli kwamba yeye sio mponyaji wala mhubiri bali ni mwigizaji tu.

    Jonathan akamueleza wafanye maombi wote ilichukua kama dakika moja, walipomaliza maombi wakafurahi na kushukuru kisha Jonathan akarudi alipokuwa huku akitokwa na machozi akihisi amewaangusha matarajio waliyokuwa nayo kwake ila amesema ni bora waujue ukweli kuwa yeye sio Yesu wala mponyaji bali ni mwigizaji tu

    Ukiacha hayo ya uhusika wake wa Yesu na dini, Jonathan Roumie amegusia pia kwamba alishafika Tanzania na Rwanda sababu kuna watoto kadhaa wanaoishi katika mazingira magumu huwa anawasaidia na familia zao

    Jonathan Roumie pia ameweka wazi kwamba anatamani watu pia wawe wanamuona katika nyuma ya pazia(behind the scene) anayopitia katika kujiandaa na uigizaji wake kama Yesu ili watu wengine waelewe wajue kumtofautisha katika maisha halisi na kisanaa

    KUMBUKA, zipo filamu nyingine miaka ya nyuma kuhusu Yesu zilizohusisha waigizaji wengine kabla ya sasa Jonathan Roumie kupata umaarufu na uhusika wa Yesu katika series maarufu ya "The Chosen"
    (Swahili Word)

    "Najisikia vibaya namna watu wanavyoniona na kuanza kuniita Yesu, wanafikia hata kutundika picha zangu katika nyumba zao, mimi ni mwigizaji tu, mimi ni mtu" - Jonathan Roumie(50), mwigizaji wa Marekani Aidha, Jonathan Roumie katika mahojiano amesema maisha yake binafsi alikuwa na hali mbaya kiuchumi hakuwa na uhakika siku inayofuata atakula nini, alikuwa mwigizaji ila kiuchumi alikuwa bado hajafanikiwa. Baada ya mambo kuzidi kuwa magumu siku moja ni kama alikuwa anamuomba Mungu kuhusu hali anayopitia ili mambo yake yakae sawa Baada ya miezi kama mitatu ndio akapata nafasi ya kuigiza kama Yesu katika series ya "The Chosen" iliyoanza kuoneshwa 2017 ambayo imejipatia umaarufu mkubwa sana hadi sasa imetazamwa na watu zaidi ya milioni 250 na misimu mipya inafuata huku ikipongezwa kwa kinachoonekana kuigizwa Umaarufu wa uhusika wake kama Yesu umempa umaarufu mkubwa na fursa nyingi ikiwemo katika mikutano na makongamano makubwa ya kidini na app za dini ya kikiristo Jonathan ambaye ni mkatoliki, alipoulizwa na New York Times, je ni tukio gani gumu analokumbuka ambalo alishakutana nalo baada ya kuigiza kama Yesu, amejibu kwa kusema kuna kipindi alikuwa katika mkutano kwenye uwanja wenye watu takribani 40,000 baadaye alishuka stejini akaenda kwenye chumba fulani uwanjani hapo, mmoja wa walinzi alikuja akamwambia nje kuna mwanamke ana mtoto kwenye kiti cha magurudumu anaomba kusalimiana na wewe Jonathan alitoka akaonana na mwanamke husika na mwanae ambaye kwa ufupi alieleza jinsi Yesu alivyoponya mtu katika hiyo series ya "The Chosen" na kusema angependa mwanae pia apone yaani akimtaka Jonathan amponye mtoto wake. Ilibidi Jonathan amueleze ukweli kwamba yeye sio mponyaji wala mhubiri bali ni mwigizaji tu. Jonathan akamueleza wafanye maombi wote ilichukua kama dakika moja, walipomaliza maombi wakafurahi na kushukuru kisha Jonathan akarudi alipokuwa huku akitokwa na machozi akihisi amewaangusha matarajio waliyokuwa nayo kwake ila amesema ni bora waujue ukweli kuwa yeye sio Yesu wala mponyaji bali ni mwigizaji tu Ukiacha hayo ya uhusika wake wa Yesu na dini, Jonathan Roumie amegusia pia kwamba alishafika Tanzania na Rwanda sababu kuna watoto kadhaa wanaoishi katika mazingira magumu huwa anawasaidia na familia zao Jonathan Roumie pia ameweka wazi kwamba anatamani watu pia wawe wanamuona katika nyuma ya pazia(behind the scene) anayopitia katika kujiandaa na uigizaji wake kama Yesu ili watu wengine waelewe wajue kumtofautisha katika maisha halisi na kisanaa KUMBUKA, zipo filamu nyingine miaka ya nyuma kuhusu Yesu zilizohusisha waigizaji wengine kabla ya sasa Jonathan Roumie kupata umaarufu na uhusika wa Yesu katika series maarufu ya "The Chosen" (Swahili Word)
    Love
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·493 Views
  • Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi

    CPA Amos Makala kiongozi wa juu wa CCM amesema kuwa Chadema wana mpango wa kununua virusi via Ebola na Mpox ili kuzuia uchaguzi!!

    Maswali yangu kufuatia kauli ya CPA Amos Makala

    1. Hizi taarifa Makala amezipata wapi ?

    2. Idara ya usalama wa taifa (TISS) inataarifa za mpango huu ?, kama hakuna taarifa turejee kwenye swali la kwanza! Kama kuna taarifa hadi sasa ni hatua gani zimechukuliwa?

    3. Makala anatuambia kwa lugha nyingine baadhi ya viongozi wa Chadema wana mpango wa uhaini na kuhujumu uchumi wa nchi je kwanini vyombo vipo kimya kwa watu wenye tuhuma nzito kama hizi ?

    4. Je Makala amepima madhara ya kauli aliyoitoa hadharani ambayo huenda inazua taharuki na hofu kwa wananchi wa Tanzania na kwa wageni amabao wana mpango wa kuitembelea Tanzania kwa siku za usoni ?

    5. Ni hatua gani za kujibu ambazo Chadema wamezichukua hadi sasa ?

    6. Je ni kauli ya maksudi tu ili kuhamisha upepo na mjadala wa chadema ambao utashika kasi kwenye mikutano yao ya hadhara inayoanza hivi punde, kuhusu mpango wao wa no reform no election ?

    7. Je Makala anaweza kuthibitishaje kauli yake kwa Umma ?

    8.Je Chadema watanunulia wapi hivyo virusi, na kumbe vinauzwaga, Makala anaweza kuthibitisha ?

    Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi CPA Amos Makala kiongozi wa juu wa CCM amesema kuwa Chadema wana mpango wa kununua virusi via Ebola na Mpox ili kuzuia uchaguzi!! Maswali yangu kufuatia kauli ya CPA Amos Makala 👇👇👇👇 1. Hizi taarifa Makala amezipata wapi ? 2. Idara ya usalama wa taifa (TISS) inataarifa za mpango huu ?, kama hakuna taarifa turejee kwenye swali la kwanza! Kama kuna taarifa hadi sasa ni hatua gani zimechukuliwa? 3. Makala anatuambia kwa lugha nyingine baadhi ya viongozi wa Chadema wana mpango wa uhaini na kuhujumu uchumi wa nchi je kwanini vyombo vipo kimya kwa watu wenye tuhuma nzito kama hizi ? 4. Je Makala amepima madhara ya kauli aliyoitoa hadharani ambayo huenda inazua taharuki na hofu kwa wananchi wa Tanzania na kwa wageni amabao wana mpango wa kuitembelea Tanzania kwa siku za usoni ? 5. Ni hatua gani za kujibu ambazo Chadema wamezichukua hadi sasa ? 6. Je ni kauli ya maksudi tu ili kuhamisha upepo na mjadala wa chadema ambao utashika kasi kwenye mikutano yao ya hadhara inayoanza hivi punde, kuhusu mpango wao wa no reform no election ? 7. Je Makala anaweza kuthibitishaje kauli yake kwa Umma ? 8.Je Chadema watanunulia wapi hivyo virusi, na kumbe vinauzwaga, Makala anaweza kuthibitisha ?
    0 Commenti ·0 condivisioni ·427 Views
  • Historia ya Wazazi wa Jackie Chan inavutia zaidi hadi Jackie Chan aliamua kuandaa "Documentary" maalum kwa ajili ya kueleza Wazazi wake walivyokutana na walikuwa wanafanya kazi gani.

    Katika kipindi chote Jackie Chan alichoishi na Wazazi wake hakuwahi kufahamu Wazazi wake walikutana vipi pamoja na kazi halisi za awali za Wazazi wake mpaka hapo Baba yake alipokuwa ana umri wa miaka 80 akaamua kumwambia ukweli maana aliamini umri wake umeenda sana hivyo muda wowote anaweza kufariki bila kumueleza ukweli Jackie Chan.

    Baba Mzazi wa Jackie Chan, Charles Chan (1914 - 2008) siku moja akiwa barabarani kwenye gari na Jackie Chan alifunguka kuwa tangu zamani alikuwa Mpelelezi (Shushushu) kwenye Serikali ya China na Mama yake Jackie Chan, Lee-Lee Chan (1916-2002) alikuwa muuza madawa ya kulevya, siku moja katika "operation" ya kukamata Wauza madawa Charles Chan alimkamata Lee-Lee Chan lakini baada ya kumfikisha kwenye vyombo vya dola walijikuta wamependana na wakafunga ndoa.

    Hadithi hii ilimshitua sana Jackie Chan kwani amekua akijua kwamba Baba yake ni Mpishi na amewahi kuwa Mpishi kwenye ubalozi wa Ufaransa - Hong Kong, pamoja na ubalozi wa Marekani Nchini Australia .

    Taarifa nyingine iliyomshitua zaidi ni pale alipoambiwa kuwa kuwa jina la Baba yake sio Chan bali ni Fang Daolong, hivyo kama asingebadili jina, Jackie Chan hivi sasa angefahamika kama Jackie Fang, Baba Jackie Chan alikuwa "Spy" kwenye Serikali ya China iliyokuwa ikiundwa na Chama cha Kuomintang, mwaka 1949 baada ya vita kali ya wenyewe kwa wenyewe Chama cha Kikomunisti kikiongozwa na Mao Zedong kiliipindua Serikali ya Kuomintang kikachukua Nchi hapo ilibidi Baba Jackie Chan abadili jina kwa sababu ya kuficha utambulisho wake maana kulikuwa na vita kubwa baina ya vyama hivyo na baadhi ya makachero wa Kuomintang walikuwa wakikamatwa na kuuawa.

    Historia ya Wazazi wa Jackie Chan imeelezwa kwa urefu kwenye "Documentary" iliyoandaliwa na Jackie Chan "Traces of the Dragon: Jackie Chan and His Lost Family" (2003)

    "Baba alikua jasusi na Mama alikua Muuza madawa na mcheza kamari. Walikutana na wakaoana baada ya Baba yangu kumkamata Mama"

    "Tangu nilipokua Mdogo nilikua najua Baba yangu anafanya kazi ya upishi kwenye Ubalozi wa Marekani mpaka alipotimiza miaka 80 na akaniambia kazi yake ya kweli. Nilishtuka, nilishtuka"

    " Kwahiyo kuna siku moja nilikua naendesha gari nikiwa na Baba yangu ghafla, Baba akageuka na kusema: 'Jackie, Mimi ni Mzee sana na huenda nisiamke kesho. Kuna kitu lazima nikuambie, ni siri' kisha akasema: kwa kweli wewe sio Jackie Chan, jina lako unaitwa Fong.'

    "Nikahisi kupatwa na mshtuko, kwangu ilikua kitu cha kustaajabisha. Kwa haraka nikamuambia asiendelee kuongea nikampigia rafiki yangu ili tutengeneze documentary ya stori ya Baba yangu. Ilituchukua miaka 3 ya kumfata Baba yangu na kuongea nae kuhusu stori yote."

    " Nilihisi mimi ndiye Mwanae wa pekee lakini nilishtuka baada ya kujua kwamba nina ndugu zangu wanne kwa Wazazi wangu. Kaka zangu wawili, upande wa Baba na Dada zangu wawili upande wa Mama. Alilazimika kunificha yote hayo kwa sababu ya kazi yake, baba alikua jasusi. Nilivutiwa sana baada ya kujua kwamba Baba yangu alikua mpole sana. Miaka yote ile nilidhania ni Mpishi. Nimetengeneza movie kupitia hii stori." - Jackie Chan

    Historia ya Wazazi wa Jackie Chan inavutia zaidi hadi Jackie Chan aliamua kuandaa "Documentary" maalum kwa ajili ya kueleza Wazazi wake walivyokutana na walikuwa wanafanya kazi gani. Katika kipindi chote Jackie Chan alichoishi na Wazazi wake hakuwahi kufahamu Wazazi wake walikutana vipi pamoja na kazi halisi za awali za Wazazi wake mpaka hapo Baba yake alipokuwa ana umri wa miaka 80 akaamua kumwambia ukweli maana aliamini umri wake umeenda sana hivyo muda wowote anaweza kufariki bila kumueleza ukweli Jackie Chan. Baba Mzazi wa Jackie Chan, Charles Chan (1914 - 2008) siku moja akiwa barabarani kwenye gari na Jackie Chan alifunguka kuwa tangu zamani alikuwa Mpelelezi (Shushushu) kwenye Serikali ya China na Mama yake Jackie Chan, Lee-Lee Chan (1916-2002) alikuwa muuza madawa ya kulevya, siku moja katika "operation" ya kukamata Wauza madawa Charles Chan alimkamata Lee-Lee Chan lakini baada ya kumfikisha kwenye vyombo vya dola walijikuta wamependana na wakafunga ndoa. Hadithi hii ilimshitua sana Jackie Chan kwani amekua akijua kwamba Baba yake ni Mpishi na amewahi kuwa Mpishi kwenye ubalozi wa Ufaransa 🇫🇷 - Hong Kong, pamoja na ubalozi wa Marekani 🇺🇸 Nchini Australia 🇦🇺. Taarifa nyingine iliyomshitua zaidi ni pale alipoambiwa kuwa kuwa jina la Baba yake sio Chan bali ni Fang Daolong, hivyo kama asingebadili jina, Jackie Chan hivi sasa angefahamika kama Jackie Fang, Baba Jackie Chan alikuwa "Spy" kwenye Serikali ya China iliyokuwa ikiundwa na Chama cha Kuomintang, mwaka 1949 baada ya vita kali ya wenyewe kwa wenyewe Chama cha Kikomunisti kikiongozwa na Mao Zedong kiliipindua Serikali ya Kuomintang kikachukua Nchi hapo ilibidi Baba Jackie Chan abadili jina kwa sababu ya kuficha utambulisho wake maana kulikuwa na vita kubwa baina ya vyama hivyo na baadhi ya makachero wa Kuomintang walikuwa wakikamatwa na kuuawa. Historia ya Wazazi wa Jackie Chan imeelezwa kwa urefu kwenye "Documentary" iliyoandaliwa na Jackie Chan "Traces of the Dragon: Jackie Chan and His Lost Family" (2003) "Baba alikua jasusi na Mama alikua Muuza madawa na mcheza kamari. Walikutana na wakaoana baada ya Baba yangu kumkamata Mama" "Tangu nilipokua Mdogo nilikua najua Baba yangu anafanya kazi ya upishi kwenye Ubalozi wa Marekani mpaka alipotimiza miaka 80 na akaniambia kazi yake ya kweli. Nilishtuka, nilishtuka" " Kwahiyo kuna siku moja nilikua naendesha gari nikiwa na Baba yangu ghafla, Baba akageuka na kusema: 'Jackie, Mimi ni Mzee sana na huenda nisiamke kesho. Kuna kitu lazima nikuambie, ni siri' kisha akasema: kwa kweli wewe sio Jackie Chan, jina lako unaitwa Fong.' "Nikahisi kupatwa na mshtuko, kwangu ilikua kitu cha kustaajabisha. Kwa haraka nikamuambia asiendelee kuongea nikampigia rafiki yangu ili tutengeneze documentary ya stori ya Baba yangu. Ilituchukua miaka 3 ya kumfata Baba yangu na kuongea nae kuhusu stori yote." " Nilihisi mimi ndiye Mwanae wa pekee lakini nilishtuka baada ya kujua kwamba nina ndugu zangu wanne kwa Wazazi wangu. Kaka zangu wawili, upande wa Baba na Dada zangu wawili upande wa Mama. Alilazimika kunificha yote hayo kwa sababu ya kazi yake, baba alikua jasusi. Nilivutiwa sana baada ya kujua kwamba Baba yangu alikua mpole sana. Miaka yote ile nilidhania ni Mpishi. Nimetengeneza movie kupitia hii stori." - Jackie Chan
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·463 Views
  • Rais wa Nchi ya Iran , Ayatollah Ali Khamenei, amesema kuwa vitisho vya Nchi ya Marekani dhidi ya Taifa lake havisaidii lolote na havitaleta matokeo yoyote kama Rais Donald Tramp anavyofikiria. Kiongozi huyo amesema hayo baada ya Rais Trump kuonya uwezekano wa hatua za kijeshi kuchukuliwa dhidi ya Iran.

    "Wamarekani wanapaswa kuelewa kwamba vitisho havitafanikiwa wanapokabiliana na Iran. Wao (Marekani) na wengine wanapaswa kufahamu kuwa wakifanya lolote baya dhidi ya taifa la Iran, watajibiwa kwa nguvu kubwa." alisema Rais Khemenei

    Mnamo Machi 7, Rais Trump alisema kuwa alimwandikia barua Rais Khamenei, akimtaka kuanzisha mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, huku akionya kuwa kuna uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi iwapo Iran itakataa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, alisema Alhamisi wiki hii kuwa barua hiyo ilikuwa zaidi ya tishio, ingawa pia ilionesha uwezekano wa mazungumzo.

    "Tunachunguza kwa kina maudhui ya barua hiyo, na tutajibu rasmi katika siku chache zijazo” alisema Waziri huyo

    Kulingana na ripoti ya tovuti ya habari ya Marekani, Axios, ikimnukuu Afisa wa Serikali ya Trump na vyanzo vingine vikisema, barua hiyo inaweka muda wa miezi miwili wa kufikia makubaliano mapya ya nyuklia. Hata hivyo, haijabainishwa ni lini muda huo utaanza au kuisha. Kwa muda mrefu, Rais Khamenei amepuuza wito wa Rais Trump wa mazungumzo ya moja kwa moja, akisema kuwa Rais huyo wa Marekani anajaribu kudanganya ulimwengu kwa kuonesha kuwa Marekani iko tayari kwa mazungumzo huku Iran ikionekana kutotaka kushiriki.

    Ikumbukwe kwamba Trump ambaye alianza muhula wake wa pili Januari 2025, amerudisha sera yake ya shinikizo la juu dhidi ya Iran. Wakati wa kipindi chake cha kwanza, Trump aliiondoa Marekani kwenye makubaliano ya kihistoria ya nyuklia ya 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu ulimwenguni na akairejeshea Tehran vikwazo vikubwa vya kiuchumi.

    Rais wa Nchi ya Iran 🇮🇷, Ayatollah Ali Khamenei, amesema kuwa vitisho vya Nchi ya Marekani 🇺🇸 dhidi ya Taifa lake havisaidii lolote na havitaleta matokeo yoyote kama Rais Donald Tramp anavyofikiria. Kiongozi huyo amesema hayo baada ya Rais Trump kuonya uwezekano wa hatua za kijeshi kuchukuliwa dhidi ya Iran. "Wamarekani wanapaswa kuelewa kwamba vitisho havitafanikiwa wanapokabiliana na Iran. Wao (Marekani) na wengine wanapaswa kufahamu kuwa wakifanya lolote baya dhidi ya taifa la Iran, watajibiwa kwa nguvu kubwa." alisema Rais Khemenei Mnamo Machi 7, Rais Trump alisema kuwa alimwandikia barua Rais Khamenei, akimtaka kuanzisha mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, huku akionya kuwa kuna uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi iwapo Iran itakataa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, alisema Alhamisi wiki hii kuwa barua hiyo ilikuwa zaidi ya tishio, ingawa pia ilionesha uwezekano wa mazungumzo. "Tunachunguza kwa kina maudhui ya barua hiyo, na tutajibu rasmi katika siku chache zijazo” alisema Waziri huyo Kulingana na ripoti ya tovuti ya habari ya Marekani, Axios, ikimnukuu Afisa wa Serikali ya Trump na vyanzo vingine vikisema, barua hiyo inaweka muda wa miezi miwili wa kufikia makubaliano mapya ya nyuklia. Hata hivyo, haijabainishwa ni lini muda huo utaanza au kuisha. Kwa muda mrefu, Rais Khamenei amepuuza wito wa Rais Trump wa mazungumzo ya moja kwa moja, akisema kuwa Rais huyo wa Marekani anajaribu kudanganya ulimwengu kwa kuonesha kuwa Marekani iko tayari kwa mazungumzo huku Iran ikionekana kutotaka kushiriki. Ikumbukwe kwamba Trump ambaye alianza muhula wake wa pili Januari 2025, amerudisha sera yake ya shinikizo la juu dhidi ya Iran. Wakati wa kipindi chake cha kwanza, Trump aliiondoa Marekani kwenye makubaliano ya kihistoria ya nyuklia ya 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu ulimwenguni na akairejeshea Tehran vikwazo vikubwa vya kiuchumi.
    0 Commenti ·0 condivisioni ·407 Views
  • SIFA ZA WANAUME WENYE THAMANI KUBWA [ HIGH VALUE MEN ].

    Kama mwanaume wako ana sifa zifuatazo basi jua una mwanaume mwenye thamani kubwa sana, na mwanaume mwenye thamani kubwa maana yake ni mwanaume bora.

    1. Hazoeleki kiurahisi.
    Moja ya sifa za wanaume wenye thamani kubwa ni wao kutozoeleka kiurahisi, hadi kumzoea mtu wa aina hii ni lazima uwe na sababu maalumu.

    2. Wana roho nzuri ila wana maamuzi magumu sana.
    Siku zote watu wa aina hii huwa na roho nzuri sana, huwa na huruma lakini wapo vizuri kufanya maamuzi mazito pale inapobidi.

    3. Haishi maisha ya kuigiza.
    Siku zote huishi maisha yake halisi, haigizi maisha.

    4. Anajua vitu vingi.
    Watu wa aina hii huwa na uelewa wa vitu vingi sana, ni ngumu kumuuliza kitu fulani akawa hakijui kabisa.

    5. Anasimamia mipango yake bila kuyumbishwa.
    Akishaamua kufanya kitu huwa hayumbishwi tena, haijalishi anaambiwa na nani, kama anahisi ni muhimu kwake kukitekeleza basi atafanya kwa vyovyote vile.

    6. Haoni shida kuanza upya.
    Ni watu wepesi sana kuamua kuanza upya, kama ni mahusiano yakilegalega ni rahisi tu kuachana nayo na kuanza upya, kwenye chochote kile kama hakiende sawa huamua kuanza upya.

    7. Jasiri sana.
    Hawa huwa hawaogopi kitu, ni majasiri kwenye kila kitu, wanajiamini sana.

    8. Hawapendi mikopo.
    Huwa hawapendi mikopo na hawapendi watu wanaopenda mikopo pia.

    9. Hana cha kuongea na x wake.
    Kama hajazaa nae huwezi kumkuna ana muda na x wake, yakiisha yameisha kweli.

    10. Hawezi kuwa chawa.
    Huwezi kumkuta anatafuta ukaribu na mtu mwenye pesa au maarufu.

    11. Huwa hana cha kujadili na mwanamke msaliti.
    Huyu ni mtu ambaye ukimsaliti basi kwa asilimia kubwa hayo mahusiano yanavunjika.

    12. Hababaishwi na muonekano wa mwanamke au ufundi wake kitandani.
    Haijalishi wewe ni mrembo kiasi gani, haijalishi wewe ni fundi kitandani kwa kiasi gani, yeye ni mtu ambaye hababaishwi na vitu hivyo, kwa kifupi huwezi kumuendesha kwa uzuri wako.

    13. Haoni shida kuondoka.
    Iwe ni kazini wakimzingua ataacha hiyo kazi, iwe kwenye mahusiano ukimzingua ataondoka, kwa kifupi anapenda vitu vilivyonyooka, hataki longo longo.

    14. Hapendi mwanamke mwenye drama, mapicha picha mengi.
    Watu hawa huhitaji wanawake wanaojitambua na wasio na mambo mengi, yani hawataki mapicha picha kwenye mahusiano.

    15. Mwanamke ukikosea atakuwajibisha.
    Hawafumbii macho mambo, ukikosea atakuchana live kabisa bila kupepesa macho.

    16. Wanajiamini sana.
    Sababu ya kujiamini ni kwakuwa wanajua vitu vingi, wanajua kipi sahihi na kipi sio sahihi.

    17. Hawaoni shida kuwa wenyewe.
    Uwezo wao wa kuishi wenyewe bila kuhisi upweke ni mkubwa sana.

    18. Hapendi uonevu.
    Huweza kumsaidia hata mtu asiyemjua pale tu anapohisi mtu huyo anaonewa.

    19. Kwenye mahusiano sio watoaji sana ila atahakikisha anakupa mahitaji yako ya msingi.
    Huwa hawapendi kutoa toa hela bila mpangilio, na hii ni kutokana na mipango yao katika maisha, ila siku zote atajitahidi kukupa mahitaji yako muhimu.

    20. Huwa hawapo romantic.
    Hawa ni wanaume ambao wanalalamikiwa sana kwenye mahusiano, hawapo romantic ila ni wanaume bora sana, hasa kwenye kulea familia.

    21. Wana huruma sana.
    Muda pekee utakaojua wana huruma ni pale utakapokuwa na shida, kama ni mwanamke wake ni pale utakapokuwa unaumwa au unapitia jambo lolote gumu, hawa ni wanaume ambao wana uwezo wa kupika, kufua, kuogesha watoto, kulisha na kufanya kila kitu kuhakikisha wanakusaidia.

    22. Sio waongeaji sana.
    Moja ya sifa yao kuu ni ukimya, muda mwingi wanahitaji kuwa kimya wakifanya mambo yao, ukiwa mwanamke muongeaji sana muda mwingi atautumia kutabasamu unavyoongea na kukujibu kwa kifupi, na mara nyingi hunyamaza bila kujibu kama hiko ulichoongea atakiona hakina maana yoyote.

    23. Hana marafiki wengi.
    Tafiti zinaonyesha watu hawa huwa hawana marafiki wengi, wanachagua sana marafiki.

    24. Hupenda kukataza na kuonya mara nyingi.
    Kwa mwanamke ukiwa na mwanaume wa namna hii, jiandae kukutazwa na kupata maonyo kwa wingi, lakini jambo zuri kuhusu hilo huwa wanakukataza au kukuonya kwa jambo ambalo linaweza kukuletea shida. Mara nyingi ukifatilia vitu anavyokukutaza au kukuonya utagundua vitakuletea shida huko mbele.

    25. Anajua vitu vingi kukuhusu kuliko unavyodhani.
    Uwezo wao wa kukutafiti ni mkubwa mno, anajua mambo mengi kukuhusu ila hawezi kukwambia, na siku akikwambia utashangaa alijua lini? Na alijuaje?
    SIFA ZA WANAUME WENYE THAMANI KUBWA [ HIGH VALUE MEN ]. Kama mwanaume wako ana sifa zifuatazo basi jua una mwanaume mwenye thamani kubwa sana, na mwanaume mwenye thamani kubwa maana yake ni mwanaume bora. 1. Hazoeleki kiurahisi. Moja ya sifa za wanaume wenye thamani kubwa ni wao kutozoeleka kiurahisi, hadi kumzoea mtu wa aina hii ni lazima uwe na sababu maalumu. 2. Wana roho nzuri ila wana maamuzi magumu sana. Siku zote watu wa aina hii huwa na roho nzuri sana, huwa na huruma lakini wapo vizuri kufanya maamuzi mazito pale inapobidi. 3. Haishi maisha ya kuigiza. Siku zote huishi maisha yake halisi, haigizi maisha. 4. Anajua vitu vingi. Watu wa aina hii huwa na uelewa wa vitu vingi sana, ni ngumu kumuuliza kitu fulani akawa hakijui kabisa. 5. Anasimamia mipango yake bila kuyumbishwa. Akishaamua kufanya kitu huwa hayumbishwi tena, haijalishi anaambiwa na nani, kama anahisi ni muhimu kwake kukitekeleza basi atafanya kwa vyovyote vile. 6. Haoni shida kuanza upya. Ni watu wepesi sana kuamua kuanza upya, kama ni mahusiano yakilegalega ni rahisi tu kuachana nayo na kuanza upya, kwenye chochote kile kama hakiende sawa huamua kuanza upya. 7. Jasiri sana. Hawa huwa hawaogopi kitu, ni majasiri kwenye kila kitu, wanajiamini sana. 8. Hawapendi mikopo. Huwa hawapendi mikopo na hawapendi watu wanaopenda mikopo pia. 9. Hana cha kuongea na x wake. Kama hajazaa nae huwezi kumkuna ana muda na x wake, yakiisha yameisha kweli. 10. Hawezi kuwa chawa. Huwezi kumkuta anatafuta ukaribu na mtu mwenye pesa au maarufu. 11. Huwa hana cha kujadili na mwanamke msaliti. Huyu ni mtu ambaye ukimsaliti basi kwa asilimia kubwa hayo mahusiano yanavunjika. 12. Hababaishwi na muonekano wa mwanamke au ufundi wake kitandani. Haijalishi wewe ni mrembo kiasi gani, haijalishi wewe ni fundi kitandani kwa kiasi gani, yeye ni mtu ambaye hababaishwi na vitu hivyo, kwa kifupi huwezi kumuendesha kwa uzuri wako. 13. Haoni shida kuondoka. Iwe ni kazini wakimzingua ataacha hiyo kazi, iwe kwenye mahusiano ukimzingua ataondoka, kwa kifupi anapenda vitu vilivyonyooka, hataki longo longo. 14. Hapendi mwanamke mwenye drama, mapicha picha mengi. Watu hawa huhitaji wanawake wanaojitambua na wasio na mambo mengi, yani hawataki mapicha picha kwenye mahusiano. 15. Mwanamke ukikosea atakuwajibisha. Hawafumbii macho mambo, ukikosea atakuchana live kabisa bila kupepesa macho. 16. Wanajiamini sana. Sababu ya kujiamini ni kwakuwa wanajua vitu vingi, wanajua kipi sahihi na kipi sio sahihi. 17. Hawaoni shida kuwa wenyewe. Uwezo wao wa kuishi wenyewe bila kuhisi upweke ni mkubwa sana. 18. Hapendi uonevu. Huweza kumsaidia hata mtu asiyemjua pale tu anapohisi mtu huyo anaonewa. 19. Kwenye mahusiano sio watoaji sana ila atahakikisha anakupa mahitaji yako ya msingi. Huwa hawapendi kutoa toa hela bila mpangilio, na hii ni kutokana na mipango yao katika maisha, ila siku zote atajitahidi kukupa mahitaji yako muhimu. 20. Huwa hawapo romantic. Hawa ni wanaume ambao wanalalamikiwa sana kwenye mahusiano, hawapo romantic ila ni wanaume bora sana, hasa kwenye kulea familia. 21. Wana huruma sana. Muda pekee utakaojua wana huruma ni pale utakapokuwa na shida, kama ni mwanamke wake ni pale utakapokuwa unaumwa au unapitia jambo lolote gumu, hawa ni wanaume ambao wana uwezo wa kupika, kufua, kuogesha watoto, kulisha na kufanya kila kitu kuhakikisha wanakusaidia. 22. Sio waongeaji sana. Moja ya sifa yao kuu ni ukimya, muda mwingi wanahitaji kuwa kimya wakifanya mambo yao, ukiwa mwanamke muongeaji sana muda mwingi atautumia kutabasamu unavyoongea na kukujibu kwa kifupi, na mara nyingi hunyamaza bila kujibu kama hiko ulichoongea atakiona hakina maana yoyote. 23. Hana marafiki wengi. Tafiti zinaonyesha watu hawa huwa hawana marafiki wengi, wanachagua sana marafiki. 24. Hupenda kukataza na kuonya mara nyingi. Kwa mwanamke ukiwa na mwanaume wa namna hii, jiandae kukutazwa na kupata maonyo kwa wingi, lakini jambo zuri kuhusu hilo huwa wanakukataza au kukuonya kwa jambo ambalo linaweza kukuletea shida. Mara nyingi ukifatilia vitu anavyokukutaza au kukuonya utagundua vitakuletea shida huko mbele. 25. Anajua vitu vingi kukuhusu kuliko unavyodhani. Uwezo wao wa kukutafiti ni mkubwa mno, anajua mambo mengi kukuhusu ila hawezi kukwambia, na siku akikwambia utashangaa alijua lini? Na alijuaje?
    Love
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·464 Views
Pagine in Evidenza