• "Nimetazama Interview ya Rais wa Marekani na Rais wa Ukraine pale Oval Office ndani ya Ikulu ya Marekani, nimekuja kugundua Rais wa Ukraine anahisi anajadiliana na Mwanasiasa mwenzake ila anachosahau Trump ni Mfanyabiashara na hawezi kufanya kitu cha bure ambacho Taifa lake Marekani halinufaiki na chochote, ndio maan anamsukumia sana kuwa amalizane na Urusi wasaini mkataba wa amani.

    Pale Ukraine kuna madini adimu sana duniani, Mrusi hapigani Kichwa kichwa ndio maana maeneo ya Donbass na Zaporizhia yanabaki kuwa maeneo ya Kimkakati sana kwa Mrusi, hata Marekani hawapo kichwa kichwa maana Secretary Rubio wa Marekani alimwambia Rais wa Ukraine akubali kusaini mkataba wa madini ili wao waendelee kumlinda, Mrusi na Mmarekani wapo rada sana eneo lile na kila mmoja yupo Kitalaam.

    Kwa akili ya kawaida Marekani hataki kuendelea kugharamikia vita hivyo bila faida.

    Juzi kuna website nilisoma ya taarifa za Kiuchunguzi ni kuwa Marekani, China na Urusi kwasasa wapo meza moja na wazo lao kubwa wamekubaliana juu ya MULTIPOLAR WORLD ORDER ambapo Mataifa zaidi ya mawili yanakuwa na nguvu sawa ama yanakaribiana, kwa ufupi sana mataifa haya matatu yanataka kuitawala dunia bila kugusana.

    Ndio maana Trump alivyoingia madarakani akapush agenda chap ya BRICS kuachana na wazo lao la kuibadili dola ya Marekani kuwa sio sarafu rasmi kwenye umoja wao, ndio maana alipoingia wamerudi mezani kwa mengi ikiwemo Trump na Putin wote kukiri kuwa watashirikiana na Trump atasafiri kuelekea Urusi kwenye sherehe za Mei 9, ambapo watakutana Marais wote watatu yani Putin, Xi Jinping na Trump.

    Kifupi sana Marekani ya Donald Trump ina Approach tofauti sana, ndio maana hata Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Stearmer alipofika White House kukutana na Trump kwenye mazungumzo yao akalisifia sana Jeshi la Uingereza ila kuna sehemu akampiga kwa kumwambia huwezi kuichukua Urusi peke yako, hata leo amesisitiza Ukraine wakubali amani nje na hapo bila msaada wake hawamuwezi Mrusi, huyo ndio Donald Trump" - Farhan JR, Mchambuzi.

    "Nimetazama Interview ya Rais wa Marekani na Rais wa Ukraine pale Oval Office ndani ya Ikulu ya Marekani, nimekuja kugundua Rais wa Ukraine anahisi anajadiliana na Mwanasiasa mwenzake ila anachosahau Trump ni Mfanyabiashara na hawezi kufanya kitu cha bure ambacho Taifa lake Marekani halinufaiki na chochote, ndio maan anamsukumia sana kuwa amalizane na Urusi wasaini mkataba wa amani. Pale Ukraine kuna madini adimu sana duniani, Mrusi hapigani Kichwa kichwa ndio maana maeneo ya Donbass na Zaporizhia yanabaki kuwa maeneo ya Kimkakati sana kwa Mrusi, hata Marekani hawapo kichwa kichwa maana Secretary Rubio wa Marekani alimwambia Rais wa Ukraine akubali kusaini mkataba wa madini ili wao waendelee kumlinda, Mrusi na Mmarekani wapo rada sana eneo lile na kila mmoja yupo Kitalaam. Kwa akili ya kawaida Marekani hataki kuendelea kugharamikia vita hivyo bila faida. Juzi kuna website nilisoma ya taarifa za Kiuchunguzi ni kuwa Marekani, China na Urusi kwasasa wapo meza moja na wazo lao kubwa wamekubaliana juu ya MULTIPOLAR WORLD ORDER ambapo Mataifa zaidi ya mawili yanakuwa na nguvu sawa ama yanakaribiana, kwa ufupi sana mataifa haya matatu yanataka kuitawala dunia bila kugusana. Ndio maana Trump alivyoingia madarakani akapush agenda chap ya BRICS kuachana na wazo lao la kuibadili dola ya Marekani kuwa sio sarafu rasmi kwenye umoja wao, ndio maana alipoingia wamerudi mezani kwa mengi ikiwemo Trump na Putin wote kukiri kuwa watashirikiana na Trump atasafiri kuelekea Urusi kwenye sherehe za Mei 9, ambapo watakutana Marais wote watatu yani Putin, Xi Jinping na Trump. Kifupi sana Marekani ya Donald Trump ina Approach tofauti sana, ndio maana hata Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Stearmer alipofika White House kukutana na Trump kwenye mazungumzo yao akalisifia sana Jeshi la Uingereza ila kuna sehemu akampiga kwa kumwambia huwezi kuichukua Urusi peke yako, hata leo amesisitiza Ukraine wakubali amani nje na hapo bila msaada wake hawamuwezi Mrusi, huyo ndio Donald Trump" - Farhan JR, Mchambuzi.
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·357 مشاهدة
  • Baada ya kujiondoa kwenye Umoja wa Nchi Magharibi (ECOWAS) na kuunda Umoja wao wa Mataifa wa Sahel (AES), Nchi za Niger , Mali , na Burkina faso , zimezindua rasmi Bendera yake mpya ya Umoja huo.

    Umoja huo wa (AES) baada ya kuanzisha Pasi ya kusafiria (Pasipoti) na Kikosi cha Wanajeshi Elfu wa pamoja tano (5000), umepanga pia kuanzisha (kuunda) sarafu moja inayotumika katika Mataifa hayo.

    Ikumbukwe kwamba Nchi hizo tatu (3) zinazoongozwa Kijeshi baada ya Majeshi ya Nchi hizo kupundua Kiongozi waliokuwepo madarakani

    Baada ya kujiondoa kwenye Umoja wa Nchi Magharibi (ECOWAS) na kuunda Umoja wao wa Mataifa wa Sahel (AES), Nchi za Niger 🇳🇪, Mali 🇲🇱, na Burkina faso 🇧🇫, zimezindua rasmi Bendera yake mpya ya Umoja huo. Umoja huo wa (AES) baada ya kuanzisha Pasi ya kusafiria (Pasipoti) na Kikosi cha Wanajeshi Elfu wa pamoja tano (5000), umepanga pia kuanzisha (kuunda) sarafu moja inayotumika katika Mataifa hayo. Ikumbukwe kwamba Nchi hizo tatu (3) zinazoongozwa Kijeshi baada ya Majeshi ya Nchi hizo kupundua Kiongozi waliokuwepo madarakani
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·241 مشاهدة
  • *VATICAN CITY......
    Nchi? Mji? Serikali au Kampuni?*

    Nadhani moja kati ya maeneo ambayo yamekuwa tata zaidi kuyaelewa basi ni mji wa Vatican… tukiachilia mbali kuhusu utata/ugumu wa kuelewa mfumo wake wa uendeshaji na historia yake lakini swali jepesi zaidi ambalo kila mtu huwa anahisi analifahamu jawabu lake ni kuhusu utambulisho wa Vatican.!! Ni swali jepesi ambalo karibia kila mtu anadhani ana jawabu sahihi lakini uhalisia ni kwamba asilimia kubwa ya watu wana jawabu lisilo sahihi… kila mtu atakueleza kwamba Vatican ni nchi inayojitegemea lakini hii ni robo tu au thelethi ya jawabu…

    Leo nami niandike kidogo kuhusu eneo hili… na kwenye andishi hili fupi nitaeleza utambulisho wa Vatican ukoje kwa usahihi wake kabisa!

    *Muhimu:* andishi hili halilengi kukosoa au kupinga imani ya mtu yeyote. Tahadhali zote zinazingatiwa ili kulinda heshima ya imani ya kila mtu.

    Tuendelee…

    Vatican City, ndio makao makuu ya Kanisa Katoliki na nyumba ya maisha ya Papa, kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki.
    Vatican ndio nchi ndogo zaidi duniani kiasi kwamba unaweza kuizunguka yote kwa mzingo (circumference) kwa muda wa dakika arobaini tu kwa kutembea kwa miguu.

    Ni ajabu sana kwa namna gani nchi ndogo kiasi hiki imetokea na je ni nchi kama nchi nyingine???

    Jibu la swali hili ni refu sana kiaisi kwamba unaweza hata kusoma darasani kwa mwaka mzima lakini nitajaribu kuweka katika maneno machache sana ya kueleweka kwa wepesi…

    Miaka ya kale sana Papa wa Kanisa Katoliki alikuwa ni mtawala wa nchi ambayo ilikuwa inajiita *Himaya ya Papa (Papal State)* ambayo inarandana kabisa na eneo la sasa la nchi nzima ya Italia. Hii ilikuwa takribani miaka ya 754 mpaka miaka ya 1870.
    Ni katika kipindi hiki ambacho Papa aliteua eneo ndani ya nchi yake Papal State ambalo likajengwa *St. Peters Basilica*, kanisa kubwa zaidi duniani na lenye nakshi adhimu zaidi. Eneo hili ambalo St. Peters Basilica ilijengwa ni eneo fulani hivi la muinuko ambako hapo hapo pia yalijengwa makazi ya Papa kuishi.

    Ikumbukwe kwamba katika kipindi hiki hiki cha uwepo wa himaya ya Papal State pia ilikuwa inapakana na Ufalme wa Italy (Kingdom of Italy) japo kila moja ilikuwa inajitegemea.

    Japokuwa himaya hizi mbili zilikuwa jirani lakini kulikuwa na uhasama fulani kati yao. Hii ilifanya Papa kujenga ukuta mkubwa kuzunguka makazi yake ya kuishi na kanisa la St. Peters Basilica.

    Kadiri miaka ilivyozidi kwenda uhasama kati ya Italy Kingdom na Papal State ulipanuka zaidi na ilifikia hatua Kingdom of Italy wakafanya uamuzi wa kuiteka Papal State na kuifanya makao makuu ya nchi yake (Rome ya sasa).

    Wakati na baada ya uvamizi huu wa Kingdom of Italy kuteka Papal State, Papa mwenyewe alikuwa amejificha ndani ya makazi yake yaliyozungushiwa ukuta ambao nimeeleza awali.
    Ikumbukwe kwamba hata kipindi hiki Kanisa Katoliki tayari lilikuwa na ushawishi mkubwa duniani kwa hiyo Kingdom of Italy walihofia kuingiza majeshi kwa nguvu ndani ya makazi ya Papa na kumkamata kuogopa umaarufu wao kimataifa kudondoka.

    Kwa hiyo majeshi ya Kingdom of Italy yalibakia nje mwa kuta za Vatican kwa miaka mingi sana wakiamini kwamba iko siku Papa atakata tamaa na kujisalimisha.
    Lakini hii haikufua dafu kwani miongo ilipita na Papa hakujisalimisha kwa kutoka nje ya kuta za Vatican. Takribani Mapapa watano kwa muda wa karibia miaka sitini waliishi ndani ya kuta za Vatican katika hali hii. Mapapa hao kwa majina yao walikuwa ni Papa Pius IX, Papa Leo XIII, Papa Pius X, Papa Benedict XV na Papa Pius XI.

    Hali hii ilisababisha Mapapa kutotambua Kingdom of Italy na pia kulalamika mara kwa mara kwa jamii ya kimataifa kwamba wanaishi kama wafungwa ndani ya kuta za Vatican kutokana na ukandamizaji wa Kingdom of Italy na hofu waliyonayo kutoka nje ya kuta za Vatican.

    Hii inatufikisha mpaka miaka ya 1920s wakati wa utawala wa Benito Mussolini akiwa Waziri Mkuu wa Italy.
    Mussolini alichoshwa na malalamiko haya ya Papa na majibizano ya kila mara huku Papa bado akishikilia msimamo wa kutoitambua Italy

    Mussolini mwanasiasa mahiri kama ajulikanavyo akaona fursa hapa ya kuandika jina lake kwenye vitabu vya historia.
    Akapendekeza makubaliano maalumu kwa Papa. Kwamba atafanya yafuatayo;

    1. Italy itatoa ardhi ya Vatican kwa Papa na iwe himaya/nchi iliyo chini ya utawala wa Papa.

    2. Italy itatoa fedha kama fidia kwa Papa kutokana na manyanyaso ya miaka yote.

    Mussolini alihitaji Papa kufanya yafuatayo;

    1. Papa atambue Italy kuwa ni nchi.

    2. Papa asijihusishe wala kutoa maoni yoyote kuhusu masuala ya kisiasa na vita.

    Papa na Mussolini wakafikia makubaliano na mikataba ikasainiwa na hapa ndipo taifa dogo zaidi duniani likazaliwa, Vatican.

    Vatican ikaanza kujiendesha kama taifa linalojitegemea kwa kuwa na sarafu yake, serikali yake, Polisi wake, jela yake (ndio kuna jela Vatican), Posta yake, Plate number zake, Passport zake na kadhalika na kadhalika.

    Vatican si kama nchi nyingine duniani kwa hiyo usidhani kwamba tayari umeielewa Vatican, hicho nilichoeleza ni theluthi tu mkanganyiko wa kuielewa Vatican kama nchi… kunywa tena glass ya maji and relax!! Nitaeleza tena kidogo…

    Ili kuielewa Vatican walau kiduchu kuna watu wawili tunapaswa kuwafahamu;

    1. Papa

    2. Mfalme wa Vatican

    Na pia kuna vitu viwili vya kuvielewa;

    1. The Holy See

    2. Vatican City

    Tuanze kimoja kimoja…

    *1. Papa*
    Hii sihitaji kueleza sana karibia wote tunafahamu. Lakini kwa msingi wa awali kabisa, Papa ni askofu wa Wakatoliki wote waliopo Rome/Vatican lakini kwa kuwa yeye pia ndiye kiongozi wa Wakatoliki wote duniani ndio sababu ya Uaskofu wake kuwa Papa.

    *2. The Holy See*
    Kabla sijaeleza chochote kuhusu Mfalme wa Vatican kwanza nieleze kuhusu The Holy See. Hili ni moja ya mambo magumu zaidi kuyaelewa kuhusu Vatican. Nitaeleza kwa lugha nyepesi na uchache ili tusipasue vichwa kwa mikanganyiko.

    Kwa tafsiri nyepesi Holy See ni 'Throne' ya Papa (nakosa neno zuri la kiswahili, sipendezwi sana na tafsiri ya 'Kiti cha Enzi').

    Ni kwamba, maaskofu wote ndani ya kanisa Katoliki wanakuwa na 'throne' lakini kwa kuwa 'throne' ya Papa ni maalumu (kiongozi wa Wakatoliki wote duniani) kwa hiyo throne yake inakuwa muhimu zaidi na inaitwa 'The Holy See'.
    Mapapa wanabadilika lakini The Holy See iko na itaendelea kuwepo siku zote.

    Yaani kwa mfano Papa anapofariki au kustaafu kama tulivyoona mwaka juzi, Makadinali wanapokusanyika Vatican kwa uhalisia wanaenda kumchagua Kadinali mwenzao ambaye atakalia 'throne' ya 'Holy See'.

    Kwa 'angle' nyingine tunaweza kusema kwamba 'The Holy See' ndiyo sheria na mamlaka yote inayofanya kanisa Katoliki kuwa namna lilivyo. Pia sheria zote za kanisa Katoliki na mfumo wake unatengenezwa na The Holy See (sio Papa).

    Pia tunaweza kusema kwamba Benito Mussolini alipofanya makubaliano na Vatican aliingia mkataba ule na 'The Holy See'.

    Pia unaweza usiamini lakini katika nyanja za sheria za kimataifa 'The Holy See' inatambulika kama mtu/kampuni halisi ambaye amesajiliwa kisheria.

    Labda nitumie lugha nyepesi zaidi ya mfano… ukitaka kuelewa The Holy See, chukulia mfano huu kwamba Holy See ni "Catholic Church Inc." alafu Papa ndiye CEO.

    Nimejitahidi kueleza kwa kifupi na kwa wepesi niwezavyo, kuielewa kwa undani zaidi The Holy See labda tunapaswa kuandaa andishi maalumu mahususi kwa ajili yake tu.

    *3. Mfalme wa Vatican*
    Mfalme wa Vatican ni mtawala mwenye mamlaka yote juu ya nchi ya Vatican na hii inaifanya Vatican kuwa moja kati ya nchi sita pekee duniani zenye wafalme wenye mamlaka kamili (absolute monarchy). Nchi nyingine tano ni Saudi Arabia, Brunei, Oman, Qatar, Oman na Swaziland.

    Hii ndio sababu kwanini Vatican hawawezi kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa sababu EU wanakubali nchi zenye mfumo wa kidemokrasia pekee.
    Japokuwa Vatican ina tawi la 'bunge' ambalo linaundwa na makadinali wa Vatican ambayo wanatunga sheria za 'nchi' lakini bado mfalme wa Vatican anauwezo wa kuveto maamuzi yoyote ambayo wamefikia.

    *Swali: Kwanini hatusikii chochote kuhusu Mfalme wa Vatican??*

    Ni kwa sababu Mfalme wa Vatican na Papa ni wajibu na mamlaka mbili tofauti lakini zinakaliwa na mtu mmoja, Papa wa Kanisa Katoliki.

    Hii inatupa kitu kingine cha kipekee kuhusu Vatican.

    Papa anachaguliwa na makadinali wenzake - Demokrasia.
    Lakini Mfalme hachaguliwi.

    Hii inafanya Vatican kuwa nchi pekee kwenye historia ya dunia kuwa na Mfalme mwenye mamlaka kamili ambaye si wa kurithi na anapatikana kidemokrasia (Elected non-heridetary absolute Monarchy).

    Kwa hiyo Papa kulingana na muktadha na mazingira ya suala husika kuna muda anatumia mamlaka yake kama Papa na muda mwingine inampasa kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Vatican.

    Bado kuna mkanganyiko???

    Zingatia mfano huu rahisi; tuseme kwamba kuna kampuni fulani kubwa ya kimataifa inaitwa Aman Enterprises (The Holy See kwa mada yetu). Aman Enterprises wakafanikiwa kuishwishi Tanzania kuwapatia kisiwa cha Mbudya na Bold Enterprises wanakibadilisha kisiwa cha Mbudya kuwa nchi inayojitegemea, labda iitwe Aman Land (Vatican City kwa mfano wetu).
    Sasa CEO wa kampuni Bwana Aman (Papa kwa mada yetu) anahamishiamanya makao makuu ya kampuni mpaka Aman Land. Kwa kuwa Aman Land sasa ni nchi, CEO wa kampuni anakuwa pia mtawala wa nchi hii, Mfalme.

    .
    Kwa hiyo kwa manufaa ya kampuni kutumia 'connection' zake za kimataifa kunufaisha taifa lake la Aman Land ni vyema kutumia mamlaka kama CEO wa Bold Enterprises na kuna muda akihitaji nchi yake ya Aman Land kutunga sheria na taratibu ambazo zitanufaisha kampuni izidi kushamiri ni vyema kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Aman Land.

    Haya ndio mamlaka mawili yaliyo chini ya mtu mmoja ndani ya vatican, Papa na Mfalme wa Vatican.

    Bado kuna mkanganyiko???

    Kama haujaelewa sawia usihofu kwa maana bado kuna hata nchi nyingine duniani bado hawaelewi sawa sawa mfumo mzima wa Vatican.

    Mfano, Umoja wa Mataifa wamekubali The Holy See (corporation) kama mwanachama wake lakini sio Vatican City nchi yenyewe.

    Passports za raia wa Vatican zinatolewa na The Holy See na sio Vatican na zinakubalika kwenye nchi nyingine japokuwa The Holy See kimataifa inatambulika kisheria kama Kampuni inayojitegemea.

    Na hapa tuongee kiduchu pia kuhusu raia wa Vatican. Katika nchi nyingine raia wa wanaongezeka kutokana na kuzaliana lakini hapa Vatican hakuna hilo kutokana na idadi ndogo ya wanaweka kiasi kwamba karibia ni asilimia sufuri. Namna pekee ya kuwa raia wa Vatican ni kwa kupewa uraia na Mfalme wa Vatican ili uishi Vatican kama moja wa wasaidizi wa Papa (ambaye ndiye mfalme). Kwa hiyo siku ukiacha kazi, yaani usaidizi wako kwa Papa ukifikia kikomo, Mfalme wa Vatican (ambayr ndiye Papa) anaondoa uraia wako na unarudi kwenu.

    Katika muda wowote ule raia wa nchi ya Vatican wanakadiriwa kuwa jumla karibia ya 500 ambao ndio idadi ndogo zaidi ya raia kwa nchi na ndogo kushinda hata idadi ya watu wanaoishi kwenye ghorofa moja kwenye nchi nyingi.
    Na raia wote hawa ni wafanyakazi wa Papa/The Holy See ambao wanapewa uraia na Mfalme (ambaye ndiye Papa) ambapo wanafanya kazi kama Makadinali, Wanadiplomasia, walinzi au kazi nyingine za kikanisa.

    Kwa ufupi sana hii ndio picha halisi ya nchi ya Vatican… na hapa ndipo ambapo maisha ya kiroho ya wafuasi zaidi ya Billioni 2 yanapoendeshwa…

    *VATICAN CITY...... Nchi? Mji? Serikali au Kampuni?* Nadhani moja kati ya maeneo ambayo yamekuwa tata zaidi kuyaelewa basi ni mji wa Vatican… tukiachilia mbali kuhusu utata/ugumu wa kuelewa mfumo wake wa uendeshaji na historia yake lakini swali jepesi zaidi ambalo kila mtu huwa anahisi analifahamu jawabu lake ni kuhusu utambulisho wa Vatican.!! Ni swali jepesi ambalo karibia kila mtu anadhani ana jawabu sahihi lakini uhalisia ni kwamba asilimia kubwa ya watu wana jawabu lisilo sahihi… kila mtu atakueleza kwamba Vatican ni nchi inayojitegemea lakini hii ni robo tu au thelethi ya jawabu… Leo nami niandike kidogo kuhusu eneo hili… na kwenye andishi hili fupi nitaeleza utambulisho wa Vatican ukoje kwa usahihi wake kabisa! *Muhimu:* andishi hili halilengi kukosoa au kupinga imani ya mtu yeyote. Tahadhali zote zinazingatiwa ili kulinda heshima ya imani ya kila mtu. Tuendelee… Vatican City, ndio makao makuu ya Kanisa Katoliki na nyumba ya maisha ya Papa, kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki. Vatican ndio nchi ndogo zaidi duniani kiasi kwamba unaweza kuizunguka yote kwa mzingo (circumference) kwa muda wa dakika arobaini tu kwa kutembea kwa miguu. Ni ajabu sana kwa namna gani nchi ndogo kiasi hiki imetokea na je ni nchi kama nchi nyingine??? Jibu la swali hili ni refu sana kiaisi kwamba unaweza hata kusoma darasani kwa mwaka mzima lakini nitajaribu kuweka katika maneno machache sana ya kueleweka kwa wepesi… Miaka ya kale sana Papa wa Kanisa Katoliki alikuwa ni mtawala wa nchi ambayo ilikuwa inajiita *Himaya ya Papa (Papal State)* ambayo inarandana kabisa na eneo la sasa la nchi nzima ya Italia. Hii ilikuwa takribani miaka ya 754 mpaka miaka ya 1870. Ni katika kipindi hiki ambacho Papa aliteua eneo ndani ya nchi yake Papal State ambalo likajengwa *St. Peters Basilica*, kanisa kubwa zaidi duniani na lenye nakshi adhimu zaidi. Eneo hili ambalo St. Peters Basilica ilijengwa ni eneo fulani hivi la muinuko ambako hapo hapo pia yalijengwa makazi ya Papa kuishi. Ikumbukwe kwamba katika kipindi hiki hiki cha uwepo wa himaya ya Papal State pia ilikuwa inapakana na Ufalme wa Italy (Kingdom of Italy) japo kila moja ilikuwa inajitegemea. Japokuwa himaya hizi mbili zilikuwa jirani lakini kulikuwa na uhasama fulani kati yao. Hii ilifanya Papa kujenga ukuta mkubwa kuzunguka makazi yake ya kuishi na kanisa la St. Peters Basilica. Kadiri miaka ilivyozidi kwenda uhasama kati ya Italy Kingdom na Papal State ulipanuka zaidi na ilifikia hatua Kingdom of Italy wakafanya uamuzi wa kuiteka Papal State na kuifanya makao makuu ya nchi yake (Rome ya sasa). Wakati na baada ya uvamizi huu wa Kingdom of Italy kuteka Papal State, Papa mwenyewe alikuwa amejificha ndani ya makazi yake yaliyozungushiwa ukuta ambao nimeeleza awali. Ikumbukwe kwamba hata kipindi hiki Kanisa Katoliki tayari lilikuwa na ushawishi mkubwa duniani kwa hiyo Kingdom of Italy walihofia kuingiza majeshi kwa nguvu ndani ya makazi ya Papa na kumkamata kuogopa umaarufu wao kimataifa kudondoka. Kwa hiyo majeshi ya Kingdom of Italy yalibakia nje mwa kuta za Vatican kwa miaka mingi sana wakiamini kwamba iko siku Papa atakata tamaa na kujisalimisha. Lakini hii haikufua dafu kwani miongo ilipita na Papa hakujisalimisha kwa kutoka nje ya kuta za Vatican. Takribani Mapapa watano kwa muda wa karibia miaka sitini waliishi ndani ya kuta za Vatican katika hali hii. Mapapa hao kwa majina yao walikuwa ni Papa Pius IX, Papa Leo XIII, Papa Pius X, Papa Benedict XV na Papa Pius XI. Hali hii ilisababisha Mapapa kutotambua Kingdom of Italy na pia kulalamika mara kwa mara kwa jamii ya kimataifa kwamba wanaishi kama wafungwa ndani ya kuta za Vatican kutokana na ukandamizaji wa Kingdom of Italy na hofu waliyonayo kutoka nje ya kuta za Vatican. Hii inatufikisha mpaka miaka ya 1920s wakati wa utawala wa Benito Mussolini akiwa Waziri Mkuu wa Italy. Mussolini alichoshwa na malalamiko haya ya Papa na majibizano ya kila mara huku Papa bado akishikilia msimamo wa kutoitambua Italy Mussolini mwanasiasa mahiri kama ajulikanavyo akaona fursa hapa ya kuandika jina lake kwenye vitabu vya historia. Akapendekeza makubaliano maalumu kwa Papa. Kwamba atafanya yafuatayo; 1. Italy itatoa ardhi ya Vatican kwa Papa na iwe himaya/nchi iliyo chini ya utawala wa Papa. 2. Italy itatoa fedha kama fidia kwa Papa kutokana na manyanyaso ya miaka yote. Mussolini alihitaji Papa kufanya yafuatayo; 1. Papa atambue Italy kuwa ni nchi. 2. Papa asijihusishe wala kutoa maoni yoyote kuhusu masuala ya kisiasa na vita. Papa na Mussolini wakafikia makubaliano na mikataba ikasainiwa na hapa ndipo taifa dogo zaidi duniani likazaliwa, Vatican. Vatican ikaanza kujiendesha kama taifa linalojitegemea kwa kuwa na sarafu yake, serikali yake, Polisi wake, jela yake (ndio kuna jela Vatican), Posta yake, Plate number zake, Passport zake na kadhalika na kadhalika. Vatican si kama nchi nyingine duniani kwa hiyo usidhani kwamba tayari umeielewa Vatican, hicho nilichoeleza ni theluthi tu mkanganyiko wa kuielewa Vatican kama nchi… kunywa tena glass ya maji and relax!! Nitaeleza tena kidogo… Ili kuielewa Vatican walau kiduchu kuna watu wawili tunapaswa kuwafahamu; 1. Papa 2. Mfalme wa Vatican Na pia kuna vitu viwili vya kuvielewa; 1. The Holy See 2. Vatican City Tuanze kimoja kimoja… *1. Papa* Hii sihitaji kueleza sana karibia wote tunafahamu. Lakini kwa msingi wa awali kabisa, Papa ni askofu wa Wakatoliki wote waliopo Rome/Vatican lakini kwa kuwa yeye pia ndiye kiongozi wa Wakatoliki wote duniani ndio sababu ya Uaskofu wake kuwa Papa. *2. The Holy See* Kabla sijaeleza chochote kuhusu Mfalme wa Vatican kwanza nieleze kuhusu The Holy See. Hili ni moja ya mambo magumu zaidi kuyaelewa kuhusu Vatican. Nitaeleza kwa lugha nyepesi na uchache ili tusipasue vichwa kwa mikanganyiko. Kwa tafsiri nyepesi Holy See ni 'Throne' ya Papa (nakosa neno zuri la kiswahili, sipendezwi sana na tafsiri ya 'Kiti cha Enzi'). Ni kwamba, maaskofu wote ndani ya kanisa Katoliki wanakuwa na 'throne' lakini kwa kuwa 'throne' ya Papa ni maalumu (kiongozi wa Wakatoliki wote duniani) kwa hiyo throne yake inakuwa muhimu zaidi na inaitwa 'The Holy See'. Mapapa wanabadilika lakini The Holy See iko na itaendelea kuwepo siku zote. Yaani kwa mfano Papa anapofariki au kustaafu kama tulivyoona mwaka juzi, Makadinali wanapokusanyika Vatican kwa uhalisia wanaenda kumchagua Kadinali mwenzao ambaye atakalia 'throne' ya 'Holy See'. Kwa 'angle' nyingine tunaweza kusema kwamba 'The Holy See' ndiyo sheria na mamlaka yote inayofanya kanisa Katoliki kuwa namna lilivyo. Pia sheria zote za kanisa Katoliki na mfumo wake unatengenezwa na The Holy See (sio Papa). Pia tunaweza kusema kwamba Benito Mussolini alipofanya makubaliano na Vatican aliingia mkataba ule na 'The Holy See'. Pia unaweza usiamini lakini katika nyanja za sheria za kimataifa 'The Holy See' inatambulika kama mtu/kampuni halisi ambaye amesajiliwa kisheria. Labda nitumie lugha nyepesi zaidi ya mfano… ukitaka kuelewa The Holy See, chukulia mfano huu kwamba Holy See ni "Catholic Church Inc." alafu Papa ndiye CEO. Nimejitahidi kueleza kwa kifupi na kwa wepesi niwezavyo, kuielewa kwa undani zaidi The Holy See labda tunapaswa kuandaa andishi maalumu mahususi kwa ajili yake tu. *3. Mfalme wa Vatican* Mfalme wa Vatican ni mtawala mwenye mamlaka yote juu ya nchi ya Vatican na hii inaifanya Vatican kuwa moja kati ya nchi sita pekee duniani zenye wafalme wenye mamlaka kamili (absolute monarchy). Nchi nyingine tano ni Saudi Arabia, Brunei, Oman, Qatar, Oman na Swaziland. Hii ndio sababu kwanini Vatican hawawezi kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa sababu EU wanakubali nchi zenye mfumo wa kidemokrasia pekee. Japokuwa Vatican ina tawi la 'bunge' ambalo linaundwa na makadinali wa Vatican ambayo wanatunga sheria za 'nchi' lakini bado mfalme wa Vatican anauwezo wa kuveto maamuzi yoyote ambayo wamefikia. *Swali: Kwanini hatusikii chochote kuhusu Mfalme wa Vatican??* Ni kwa sababu Mfalme wa Vatican na Papa ni wajibu na mamlaka mbili tofauti lakini zinakaliwa na mtu mmoja, Papa wa Kanisa Katoliki. Hii inatupa kitu kingine cha kipekee kuhusu Vatican. Papa anachaguliwa na makadinali wenzake - Demokrasia. Lakini Mfalme hachaguliwi. Hii inafanya Vatican kuwa nchi pekee kwenye historia ya dunia kuwa na Mfalme mwenye mamlaka kamili ambaye si wa kurithi na anapatikana kidemokrasia (Elected non-heridetary absolute Monarchy). Kwa hiyo Papa kulingana na muktadha na mazingira ya suala husika kuna muda anatumia mamlaka yake kama Papa na muda mwingine inampasa kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Vatican. Bado kuna mkanganyiko??? Zingatia mfano huu rahisi; tuseme kwamba kuna kampuni fulani kubwa ya kimataifa inaitwa Aman Enterprises (The Holy See kwa mada yetu). Aman Enterprises wakafanikiwa kuishwishi Tanzania kuwapatia kisiwa cha Mbudya na Bold Enterprises wanakibadilisha kisiwa cha Mbudya kuwa nchi inayojitegemea, labda iitwe Aman Land (Vatican City kwa mfano wetu). Sasa CEO wa kampuni Bwana Aman (Papa kwa mada yetu) anahamishiamanya makao makuu ya kampuni mpaka Aman Land. Kwa kuwa Aman Land sasa ni nchi, CEO wa kampuni anakuwa pia mtawala wa nchi hii, Mfalme. . Kwa hiyo kwa manufaa ya kampuni kutumia 'connection' zake za kimataifa kunufaisha taifa lake la Aman Land ni vyema kutumia mamlaka kama CEO wa Bold Enterprises na kuna muda akihitaji nchi yake ya Aman Land kutunga sheria na taratibu ambazo zitanufaisha kampuni izidi kushamiri ni vyema kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Aman Land. Haya ndio mamlaka mawili yaliyo chini ya mtu mmoja ndani ya vatican, Papa na Mfalme wa Vatican. Bado kuna mkanganyiko??? Kama haujaelewa sawia usihofu kwa maana bado kuna hata nchi nyingine duniani bado hawaelewi sawa sawa mfumo mzima wa Vatican. Mfano, Umoja wa Mataifa wamekubali The Holy See (corporation) kama mwanachama wake lakini sio Vatican City nchi yenyewe. Passports za raia wa Vatican zinatolewa na The Holy See na sio Vatican na zinakubalika kwenye nchi nyingine japokuwa The Holy See kimataifa inatambulika kisheria kama Kampuni inayojitegemea. Na hapa tuongee kiduchu pia kuhusu raia wa Vatican. Katika nchi nyingine raia wa wanaongezeka kutokana na kuzaliana lakini hapa Vatican hakuna hilo kutokana na idadi ndogo ya wanaweka kiasi kwamba karibia ni asilimia sufuri. Namna pekee ya kuwa raia wa Vatican ni kwa kupewa uraia na Mfalme wa Vatican ili uishi Vatican kama moja wa wasaidizi wa Papa (ambaye ndiye mfalme). Kwa hiyo siku ukiacha kazi, yaani usaidizi wako kwa Papa ukifikia kikomo, Mfalme wa Vatican (ambayr ndiye Papa) anaondoa uraia wako na unarudi kwenu. Katika muda wowote ule raia wa nchi ya Vatican wanakadiriwa kuwa jumla karibia ya 500 ambao ndio idadi ndogo zaidi ya raia kwa nchi na ndogo kushinda hata idadi ya watu wanaoishi kwenye ghorofa moja kwenye nchi nyingi. Na raia wote hawa ni wafanyakazi wa Papa/The Holy See ambao wanapewa uraia na Mfalme (ambaye ndiye Papa) ambapo wanafanya kazi kama Makadinali, Wanadiplomasia, walinzi au kazi nyingine za kikanisa. Kwa ufupi sana hii ndio picha halisi ya nchi ya Vatican… na hapa ndipo ambapo maisha ya kiroho ya wafuasi zaidi ya Billioni 2 yanapoendeshwa…
    Like
    2
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·853 مشاهدة
  • GEREZA LA GITARAMA: Jehenamu duniani!

    Jiji la Gitarama hupatikana katikati ya nchi ya Rwanda, kwa makadirio kilomita arobaini na tano toka kwenye jiji kubwa nchini humo; jiji la Kigali, jiji pekee lililoitangulia Gitarama kwa ukubwa.

    Kama haitoshi ni hapahapa katika jiji hili ndipo kuna historia kubwa ya makutano yaliyofanyika mwezi wa kwanza; mwaka 1961, Rwanda ikatangazwa rasmi kama jamhuri. Vilevile jiji hili (kipindi hicho mji) likatoa raisi wa kwanza wa Rwanda, bwana Gregoire Kayibanda, ambaye kumbukumbuye mpaka sasa imesimamishwa katikati ya eneo hili.

    Mazuri hayo hayakomei hapo, hapana! Bali pia hili jiji likabarikiwa na kutunukiwa vivutio kadha wa kadha vya utalii na taasisi lukuki za elimu ambazo aidha zaweza jaza ukumbi nikizianisha hapa. Na kwa namna moja ama nyingine nachelea kusema taasisi hizo zilijengwa (zimejengwa) kwa lengo chanya la kuwafanya watu wapate elimu na hatimaye kujikomboa kifikra na kimwili.

    Lakini mbali na taasisi hizo, na aidha vivutio na uzuri wa jiji hili, upande wa pili wa sarafu ukisikia jina hili ‘Gitarama’, yakupasa uhofie na hata kushikwa na huruma kwa namna binadamu kama wewe wanavyotendwa, tena bado wakiwa hai kabisa. Binadamu hao wakiwa wanaishi ndani ya eneo ambalo hakuna binadamu yeyote juu ya uso wa dunia angelipenda kuwamo kwa gharama yoyote ile!

    GITARAMA; ‘JEHANAMU DUNIANI’:

    Sehemu nyingi duniani zimewahi kuitwa jehanamu. Na jina hili lilishamiri zaidi baada ya vita vya pili vya dunia ambapo maeneo kadhaa yalipewa jina hili kuwakilisha maeneo yasiyokalika, hatari na yasiyo na afya stahiki kwa wanadamu. Maeneo hayo mathalani ni Blood Falls (Maanguko ya damu) huko Antarktika, Danakil Depression (bonde la Danakil) huko Ethiopia, Door to Hell (mlango wa kuzimu) huko Turkmenistan, Kamchatka Peninsula huko Russia na kadhalika, na kadhalika.

    Japokuwa sehemu hizo zipo nyingi zikipatikana maeneo mbalimbali, ni dhahiri kuna sifa ambazo hushirikiana na hivyo basi ndio maana huwekwa chini ya mwamvuli mmoja wa ‘jehanamu’.

    Upande wa kusini magharibi mwa jiji la Kigali, ndipo ilipo jela hii Gitarama. Kwa sasa inaitwa jela ya Muhanga ikichukua jina la wilaya ambayo ndiyo makazi yake mpaka sasa. Majengo ya jela hiyo yalikuwa yanamilikiwa na waingereza British housing complex mnamo mwaka 1960 yakiwa yamejengwa kama makazi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

    Pale kampuni ilipofungwa, eneo hilo likakodiwa na serikali ya kwanza ya Rwanda iliyokuwa imedhamiria kufanya majengo hayo kuwa jela ya kisiasa (political prison). Tangu hapo hakuna chochote kilichobadilika ndani ya jela hiyo isipokuwa tu serikali ya Rwanda ambapo kila serikali iliyoingia madarakani ilionekana kuipatia ama kuitafutia matumizi eneo hilo.

    Kwa mujibu wa gazeti la London Independent mwaka 1995, hii ndiyo jela mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani. Pia wanda za tovuti nyingi za mitandao, zinakiri na kuiweka jela hii kwenye kumi, ama tano, ama tatu bora zaidi ya jela hatari mno kuwahi kutokea duniani.

    Gitarama ilijengwa kwa ajili ya kumudu wafungwa mia nne tu, lakini mpaka sasa inabebelea wafungwa elfu saba! Mara kumi na nane kwa makadirio. Hali hii inapelekea mahesabu ya wafungwa wanne kurundikana katika eneo la hatua tatu (three feet). Hili laweza likawa la kawaida sana ukilisoma hapa, lakini ukijaribu kutoka nje ya bandiko hili na kujikuta ukiwa umekaa na watu wengine watatu ndani ya eneo la hatua tatu tu, kidogo waweza kuelewa.

    Hakuna mahali pa kulala, kujilaza, wala pa kuketi. Wafungwa husimama wakikung’utwa na jua na wakipoozwa na mvua kwakuwa jela hii kwa kiasi kikubwa haina paa la kuwakinga wafungwa na jua, mvua wala baridi.

    Kutokana na kutapakaa kwa wafungwa hao kwenye eneo hilo dogo, inakuwa ngumu sana kwa mfungwa kutaka kwenda chooni akafanikiwa kwa muda, hali hii inapelekea wafungwa kujisaidia popote pale na hivyo basi kujaza vinyesi, mikojo na harufu kila eneo. Wafungwa huozeshwa na kumomonywa miili na bakteria mpaka kufa kwasababu ya kujiweka karibu, aidha kwa kulala ama kusimama kwenye vinyesi na uchafu wa kila aina (gangrene).

    Wafungwa wengi hawana vidole, nyayo na miguu kwasababu ya kuoza wakiwa hai. Miguu hubadilika rangi na hata kutoa madonda. Ni kawaida kuona mtu ana wadudu miguuni huku wakitembea.

    Kati ya wafungwa kumi ndani ya jela hii, nane hufa kwa kukosa hewa ama magonjwa mbalimbali. Lakini wanapotoka kwenda kuzikwa, basi huingizwa wafungwa wengine ndani ya mlango mkubwa wenye kutu wenye kutoa malalamiko ya ukuukuu.

    Lakini ajabu na kweli ni kwamba, wafungwa waliomo humo ndani hakuna hata mmoja ambaye amepitia mahakamani akathibitishwa ya kwamba ana makosa na anastahili kufungwa.
    Wengi wao, kama si wote, ni wa Hutu. Na walianza kujazwa humo miaka ya 1990's wakituhumiwa kwa mauaji ya Kimbari yaliyokwapua maisha ya wana Rwanda zaidi ya milioni moja. Na hii huonekana ni sababu kubwa inayofanya serikali kutokujali kabisa jela hiyo achilia mbali aliye madarakani ni mtutsi.

    "Watu wanafanyana vitoweo."

    Si tu kwamba hakuna mahali pa kupumzikia, bali ndani ya jela hii kuna rekodi kadha wa kadha mfungwa kumuua mwenzake kisha kumla kama chakula.

    Mgawo wa chakula ni finyu sana. chakula na maji hutolewa mara moja tu kwa juma, tena kikiwa kibovu na hakitoshelezi; mara nyingine chakula kinakosekana kabisa na hivyo basi kuwalazimu wafungwa kumaliza siku kadha wa kadha pasipo kutia kitu tumboni.

    Kwakuwa kila mtu anataka kuishi, wafungwa wengine huamua kuchukua hatua ya kulinda uhai wao kwa kuwanyonga wenzao, kuwabamiza ukutani mpaka mauti kisha kuwatafuna wakiwa wabichi na wakivuja damu moto.

    Wengine hucheza kamari kabisa, ambapo wahusika huchaguliwa kwa kukurupushwa. Mwisho wa siku wahanga wa Kamari hiyo hupotea isijulikane wameenda wapi ndani ya jela, bali matumboni.

    Kumbuka kwamba yote haya yanawezekana tena kwa urahisi kwa sababu ndani ya jela hii hakuna hata mlinzi anayediriki kuingia, ni wafungwa wenyewe tu ndio ambao hujihudumia wenyewe. Chakula na maji vikiletwa, huachwa mlangoni kabla ya wafungwa wenyewe kunyakuwa na kuanza kujigawia. Ndio maana mtu anaweza akafa mpaka akaoza ndani ya jela hii kabla hajaja tolewa na kwenda kuzikwa kwenye makaburi ya pamoja.

    Kulana wenyewe kwa wenyewe si jambo geni wala la kushhtukiza kwa walinzi wa jela hiyo wala tawala husika.

    Juhudi za kubadilisha hali ya Gitarama:

    Kwa namna moja ama nyingine kuna watu na mashirika yaliyoguswa na hali ya kusikitisha kuhusu Gitarama. Japokuwa kweli waliomo humo wanaweza wakawa ni watu waliofanya makosa mbalimbali, ikiwemo hata kuua, lakini halibadilishi dhana ya kwamba na wao wanahitaji haki za binadamu kama wengineo.

    Shirika la Global Giving, likisukumwa na kiongozi wa projekti hii Karen Tse, ni moja ya shirika lisilonuwia faida lililoguswa na hata kuanzisha kampeni ya kutafuta pesa kwa ajili ya kuwasaidia wafungwa hao. Mpaka sasa shirika hili li wazi na unaweza ukawachangia.

    Pesa waliyoichangisha mpaka sasa ni dola za kimarekani 325 huku wakifadhiliwa na mashirika mawili fadhili na huu ukiwa ni mwaka wa sita sasa wapo moto (active).

    Mbali na hapo wanajitutumua kuwasaidia wafungwa hao kisheria ili kesi zao zipatwe kusikilizwa mahakamani. Japokuwa swala hili linaonekana ndoto zaidi ya uhalisia tangu mkono wa serikali unakuwa mzito sana kutingisha kidole.

    “Hiyo ndiyo Gitarama; jehanamu juu ya uso wa dunia. Ama tuseme tawi dogo la jehanamu duniani.”
    GEREZA LA GITARAMA: Jehenamu duniani! Jiji la Gitarama hupatikana katikati ya nchi ya Rwanda, kwa makadirio kilomita arobaini na tano toka kwenye jiji kubwa nchini humo; jiji la Kigali, jiji pekee lililoitangulia Gitarama kwa ukubwa. Kama haitoshi ni hapahapa katika jiji hili ndipo kuna historia kubwa ya makutano yaliyofanyika mwezi wa kwanza; mwaka 1961, Rwanda ikatangazwa rasmi kama jamhuri. Vilevile jiji hili (kipindi hicho mji) likatoa raisi wa kwanza wa Rwanda, bwana Gregoire Kayibanda, ambaye kumbukumbuye mpaka sasa imesimamishwa katikati ya eneo hili. Mazuri hayo hayakomei hapo, hapana! Bali pia hili jiji likabarikiwa na kutunukiwa vivutio kadha wa kadha vya utalii na taasisi lukuki za elimu ambazo aidha zaweza jaza ukumbi nikizianisha hapa. Na kwa namna moja ama nyingine nachelea kusema taasisi hizo zilijengwa (zimejengwa) kwa lengo chanya la kuwafanya watu wapate elimu na hatimaye kujikomboa kifikra na kimwili. Lakini mbali na taasisi hizo, na aidha vivutio na uzuri wa jiji hili, upande wa pili wa sarafu ukisikia jina hili ‘Gitarama’, yakupasa uhofie na hata kushikwa na huruma kwa namna binadamu kama wewe wanavyotendwa, tena bado wakiwa hai kabisa. Binadamu hao wakiwa wanaishi ndani ya eneo ambalo hakuna binadamu yeyote juu ya uso wa dunia angelipenda kuwamo kwa gharama yoyote ile! GITARAMA; ‘JEHANAMU DUNIANI’: Sehemu nyingi duniani zimewahi kuitwa jehanamu. Na jina hili lilishamiri zaidi baada ya vita vya pili vya dunia ambapo maeneo kadhaa yalipewa jina hili kuwakilisha maeneo yasiyokalika, hatari na yasiyo na afya stahiki kwa wanadamu. Maeneo hayo mathalani ni Blood Falls (Maanguko ya damu) huko Antarktika, Danakil Depression (bonde la Danakil) huko Ethiopia, Door to Hell (mlango wa kuzimu) huko Turkmenistan, Kamchatka Peninsula huko Russia na kadhalika, na kadhalika. Japokuwa sehemu hizo zipo nyingi zikipatikana maeneo mbalimbali, ni dhahiri kuna sifa ambazo hushirikiana na hivyo basi ndio maana huwekwa chini ya mwamvuli mmoja wa ‘jehanamu’. Upande wa kusini magharibi mwa jiji la Kigali, ndipo ilipo jela hii Gitarama. Kwa sasa inaitwa jela ya Muhanga ikichukua jina la wilaya ambayo ndiyo makazi yake mpaka sasa. Majengo ya jela hiyo yalikuwa yanamilikiwa na waingereza British housing complex mnamo mwaka 1960 yakiwa yamejengwa kama makazi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo. Pale kampuni ilipofungwa, eneo hilo likakodiwa na serikali ya kwanza ya Rwanda iliyokuwa imedhamiria kufanya majengo hayo kuwa jela ya kisiasa (political prison). Tangu hapo hakuna chochote kilichobadilika ndani ya jela hiyo isipokuwa tu serikali ya Rwanda ambapo kila serikali iliyoingia madarakani ilionekana kuipatia ama kuitafutia matumizi eneo hilo. Kwa mujibu wa gazeti la London Independent mwaka 1995, hii ndiyo jela mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani. Pia wanda za tovuti nyingi za mitandao, zinakiri na kuiweka jela hii kwenye kumi, ama tano, ama tatu bora zaidi ya jela hatari mno kuwahi kutokea duniani. Gitarama ilijengwa kwa ajili ya kumudu wafungwa mia nne tu, lakini mpaka sasa inabebelea wafungwa elfu saba! Mara kumi na nane kwa makadirio. Hali hii inapelekea mahesabu ya wafungwa wanne kurundikana katika eneo la hatua tatu (three feet). Hili laweza likawa la kawaida sana ukilisoma hapa, lakini ukijaribu kutoka nje ya bandiko hili na kujikuta ukiwa umekaa na watu wengine watatu ndani ya eneo la hatua tatu tu, kidogo waweza kuelewa. Hakuna mahali pa kulala, kujilaza, wala pa kuketi. Wafungwa husimama wakikung’utwa na jua na wakipoozwa na mvua kwakuwa jela hii kwa kiasi kikubwa haina paa la kuwakinga wafungwa na jua, mvua wala baridi. Kutokana na kutapakaa kwa wafungwa hao kwenye eneo hilo dogo, inakuwa ngumu sana kwa mfungwa kutaka kwenda chooni akafanikiwa kwa muda, hali hii inapelekea wafungwa kujisaidia popote pale na hivyo basi kujaza vinyesi, mikojo na harufu kila eneo. Wafungwa huozeshwa na kumomonywa miili na bakteria mpaka kufa kwasababu ya kujiweka karibu, aidha kwa kulala ama kusimama kwenye vinyesi na uchafu wa kila aina (gangrene). Wafungwa wengi hawana vidole, nyayo na miguu kwasababu ya kuoza wakiwa hai. Miguu hubadilika rangi na hata kutoa madonda. Ni kawaida kuona mtu ana wadudu miguuni huku wakitembea. Kati ya wafungwa kumi ndani ya jela hii, nane hufa kwa kukosa hewa ama magonjwa mbalimbali. Lakini wanapotoka kwenda kuzikwa, basi huingizwa wafungwa wengine ndani ya mlango mkubwa wenye kutu wenye kutoa malalamiko ya ukuukuu. Lakini ajabu na kweli ni kwamba, wafungwa waliomo humo ndani hakuna hata mmoja ambaye amepitia mahakamani akathibitishwa ya kwamba ana makosa na anastahili kufungwa. Wengi wao, kama si wote, ni wa Hutu. Na walianza kujazwa humo miaka ya 1990's wakituhumiwa kwa mauaji ya Kimbari yaliyokwapua maisha ya wana Rwanda zaidi ya milioni moja. Na hii huonekana ni sababu kubwa inayofanya serikali kutokujali kabisa jela hiyo achilia mbali aliye madarakani ni mtutsi. "Watu wanafanyana vitoweo." Si tu kwamba hakuna mahali pa kupumzikia, bali ndani ya jela hii kuna rekodi kadha wa kadha mfungwa kumuua mwenzake kisha kumla kama chakula. Mgawo wa chakula ni finyu sana. chakula na maji hutolewa mara moja tu kwa juma, tena kikiwa kibovu na hakitoshelezi; mara nyingine chakula kinakosekana kabisa na hivyo basi kuwalazimu wafungwa kumaliza siku kadha wa kadha pasipo kutia kitu tumboni. Kwakuwa kila mtu anataka kuishi, wafungwa wengine huamua kuchukua hatua ya kulinda uhai wao kwa kuwanyonga wenzao, kuwabamiza ukutani mpaka mauti kisha kuwatafuna wakiwa wabichi na wakivuja damu moto. Wengine hucheza kamari kabisa, ambapo wahusika huchaguliwa kwa kukurupushwa. Mwisho wa siku wahanga wa Kamari hiyo hupotea isijulikane wameenda wapi ndani ya jela, bali matumboni. Kumbuka kwamba yote haya yanawezekana tena kwa urahisi kwa sababu ndani ya jela hii hakuna hata mlinzi anayediriki kuingia, ni wafungwa wenyewe tu ndio ambao hujihudumia wenyewe. Chakula na maji vikiletwa, huachwa mlangoni kabla ya wafungwa wenyewe kunyakuwa na kuanza kujigawia. Ndio maana mtu anaweza akafa mpaka akaoza ndani ya jela hii kabla hajaja tolewa na kwenda kuzikwa kwenye makaburi ya pamoja. Kulana wenyewe kwa wenyewe si jambo geni wala la kushhtukiza kwa walinzi wa jela hiyo wala tawala husika. Juhudi za kubadilisha hali ya Gitarama: Kwa namna moja ama nyingine kuna watu na mashirika yaliyoguswa na hali ya kusikitisha kuhusu Gitarama. Japokuwa kweli waliomo humo wanaweza wakawa ni watu waliofanya makosa mbalimbali, ikiwemo hata kuua, lakini halibadilishi dhana ya kwamba na wao wanahitaji haki za binadamu kama wengineo. Shirika la Global Giving, likisukumwa na kiongozi wa projekti hii Karen Tse, ni moja ya shirika lisilonuwia faida lililoguswa na hata kuanzisha kampeni ya kutafuta pesa kwa ajili ya kuwasaidia wafungwa hao. Mpaka sasa shirika hili li wazi na unaweza ukawachangia. Pesa waliyoichangisha mpaka sasa ni dola za kimarekani 325 huku wakifadhiliwa na mashirika mawili fadhili na huu ukiwa ni mwaka wa sita sasa wapo moto (active). Mbali na hapo wanajitutumua kuwasaidia wafungwa hao kisheria ili kesi zao zipatwe kusikilizwa mahakamani. Japokuwa swala hili linaonekana ndoto zaidi ya uhalisia tangu mkono wa serikali unakuwa mzito sana kutingisha kidole. “Hiyo ndiyo Gitarama; jehanamu juu ya uso wa dunia. Ama tuseme tawi dogo la jehanamu duniani.”
    Like
    2
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·906 مشاهدة
  • VITA FUPI.

    Je unaifahamu vita fupi kuliko zote kuwahi kutokea duniani?.

    Kama hufahamu, basi leo inabidi ujue kwamba miaka 122 iliyopita, kulitokea vita iliyodumu kwa dakika 38 tu, na hivyo kuweka rekodi ya kuwa ndio vita fupi kuliko zote kuwahi kutokea duniani. Vita hiyo iliyojulikana kama 'Anglo- Zanzibar war' iliyotokea mwaka 1896 kati ya uingereza na Zanzibar, ikipiganwa katika ardhi ya Zanzibar iliyokuwa chini ya utawala wa kisultani.

    Kabla ya kuelezea vita hiyo, kwanza inabidi tufahamu jinsi historia ya Zanzibar hapo kabla ya mwaka 1698 ambapo ilikuwa chini ya utawala wa wareno waliotawala hapo kuanzia mwishoni mwa miaka 1490.

    Wareno hao waliondoka baada ya ujio wa waarabu kutoka Oman, waliokuja pwani ya Afrika Mashariki mnamo mwaka 1698. Hivyo kuanzia hapo, Zanzibar ikawa ni sehemu ya himaya ya Oman, ikiongozwa na masultani walioko mjini Muscat, Oman. Ilipofika mwaka 1804, Oman ikapata sultan mpya, aitwaye Sayyid Said ambaye aliweza kuanzisha mashamba ya mikarafuu huku akiwatumia watumwa kutoka Tanganyika wakitumika kama nguvu kazi katika mashamba hayo.

    Mwaka 1832, Sultan Sayyid Said alihamisha mji mkuu wa Omani kutoka Muskat kwenda Unguja. Hiyo ikapelekea ukuaji wa maendeleo katika mji wa Unguja kutokana na watu wengi kufurika hapo wakitoka sehemu mbalimbali ikiwemo Oman. Nchi mbalimbali zikaanza kujenga balozi zao hapo Zanzibar, mfano Marekani ilijenga balozi yake mwaka 1837, Uingereza mwaka 1841 kisha Ufaransa mwaka 1844.

    Ilipofika mwaka 1840, Sultani Sayyid said alihama kabisa mjini Muskat na kuja kuishi Zanzibar huku akiendelea kujulikana kama Sultan wa Oman na Zanzibar hadi mwaka alipofariki mwaka 1856. Baada ya kufariki Sayyid Said, waliokuwa watoto wake Majid bin Said na mwingine aliyeitwa Thuwaini bin Said, wakaanza mgogoro kuhusu nani wa kurithi kiti cha usultani wa Oman.

    Mgogoro huo ulipelekea himaya ya Oman kugawanyika katika sehemu mbili, Thuwaini bin Said alichukua Oman na hivyo kuwa Sultani wa Oman. Lakini Majid bin Said akiichukua Zanzibar na hivyo kuwa Sultani wa kwanza wa Zanzibar.

    Sultan Majid bin Said alitawala Zanzibar hadi mwaka 1870, akifuatiwa na sultan Barghash ambaye kwa kushirikiana na waingereza anakumbukwa kwa kusitisha biashara ya watumwa hapo Zanzibar mwaka 1876 japokuwa utumwa ulikuwa unaendelea.

    Mnamo mwaka 1890, kulisainiwa mkataba baina ya ujerumani na uingereza uliojulikana kama mkataba wa Heligoland uliopelekea Zanzibar kuwa chini ya uangalizi wa Uingereza huku ikiendelea kuongozwa na Sultani. Mwaka 1893 Uingereza 'ilifanya figisu' na hatimaye kumpandikiza kibaraka wao, Hamad bin Thuwaini kuwa sultani mpya wa Zanzibar, akitawala kwa miaka mitatu hadi tarehe 25 Agosti 1896 alipofariki ghafla akiwa ofisini kwake. Ingawa kuna tetesi kwamba aliyesababisha kifo chake ni binamu yake aitwaye Khalid bin Barghash ambaye inasemekana kuwa alimtilia sumu kwenye chakula.

    Tetesi hizo zilionekana ni kweli kutokana na kitendo cha Khalid bin Barghash kurithi kiti cha usultani punde tuu baada ya kifo cha nduguye akifanya hivyo bila ya kuthibitishwa na serikali ya uingereza.Maana ilikuwa ni kanuni kwamba serikali ya uingereza lazima ipitishe mchakato wa kumpata sultani.

    Kitendo cha Khalid bin Barghash kujitwalia madaraka ya kisultani, kiliwafanya waingereza kuchukia sana. Hivyo aliyekuwa balozi wa uingereza nchini Zanzibar, Basil Cave alimpa onyo kali sana sultan Khalid akitaka aachie madaraka. Waingereza walimpendelea Hamud bin Muhammed, awe sultani kwasababu waliona huyo ndiye wangeweza kufanya nae kazi vizuri kwani watamfanya kama kibaraka wao.

    Kitendo cha Khalid bin Barghash kujitwalia madaraka ya kisultani, kiliwafanya waingereza kuchukia sana. Hivyo aliyekuwa balozi wa uingereza nchini Zanzibar, Basil Cave alimpa onyo kali sana sultan Khalid akitaka aachie madaraka. Waingereza walimpendelea Hamud bin Muhammed, awe sultani kwasababu waliona huyo ndiye wangeweza kufanya nae kazi vizuri kwani watamfanya kama kibaraka wao.

    Mgogoro ulikuwa mkubwa baada ya Sultan Khalid bin Barghash kukaidi kuachia madaraka, badala yake akazidi kujiimarisha kiulinzi kwa kuongeza askari 3000 kwa ajili ya kulinda kasri yake.

    Wakati huohuo, uingereza nao walikuwa tayari wameshatega meli zao za kivita kwenye bandari huku wanajeshi wakisambazwa sehemu mbalimbali kwa ajili ya kujiandaa na lolote litakalotokea. Basil Cave aliwasiliana na makao makuu huko London akiomba aongezewe meli nyingine ya kivita. Hatimaye meli aina ya HMS Sparrow ikitia nanga katika bandari ya Zanzibar.

    Japokuwa alikuwa tayari kwa pambano, Basil Cave hakuwa na mamlaka ya kuanzisha vita pasipo kupokea amri kutoka makao makuu Uingereza. Akatuma ujumbe makao makuu akisema hivi;

    *_" Tumefanya njia zote za amani lakini zimeshindikana, sasa tunaruhusiwa kuanza mashambulizi??"*_

    Wakati anasubiria majibu kutoka makao makuu, Cave alituma tena ujumbe kwa Sultani akimtaka aachie madaraka, lakini Sultan hakujibu.

    Siku iliyofuata Cave alipokea majibu kutoka makao makuu ukisema kwamba, *" unaruhusiwa kufanya chochote unachodhani kinafaa na sisi tutakupa ushirikiano."*

    Wakati huohuo tuliona meli zingine za kivita zinaingia Zanzibar zikitokea uingereza.

    Usiku wa tarehe 26, Basil Cave akatuma Ujumbe wa mwisho kwa sultani akimtaka kuondoka ofisini kesho yake saa tatu asubuhi. Huku akiziamuru boti zote zisizo za kivita ziondolewe baharini ili kujiandaa na vita.

    Siku iliyofuata saa 2 asubuhi, Sultani Khalid akajibu, akasema hivi, *" Sina mpango wa kuachia madaraka na sitegemei kama mtaanzisha vita dhidi yetu"*

    Basil Cave naye akajibu akasema;
    "Hatuna haja ya kuanzisha vita, ila tutafanya hivyo kama ukikaidi maagizo yetu."

    Sultani hakujibu tena. Na ilipofika saa 3 kamili meli zote za kivita zilipokea amri ya kuanza kushambulia kasri ya sultani. Saa 3:02 asubuhi, majengo na silaha za Sultani zilianza kulipuliwa, huku majeshi ya sultani nayo yakijibu mashambulizi kwa kurusha makombora yao.

    Inaelezwa kwamba dakika chache tuu baada ya kuanza kwa mashambulizi, Sultan Khalid *alitoroka kupitia mlango wa nyuma* wa kasri hiyo akiwaacha wapiganaji wake wakiendelea na vita. Hadi kufikia saa 3:40, sehemu kubwa ya kasri ya sultani ilikuwa tayari imeshalipuliwa na bendera ya sultani ikashushwa.

    Na hapo ndipo ikawa mwisho wa vita hiyo fupi.

    Katika vita hiyo fupi, inaelezwa kwamba wapiganaji 500 wa sultani walifariki na kujeruhiwa huku mwanajeshi mmoja tuu wa kingereza alijeruhiwa lakini akapona baadae.

    Baada ya sultan Khalid kukimbia, ndipo Uingereza ikampitisha mtu wao *Hamud bin Muhammed,* kuwa sultani wa Zanzibar kwa miaka 6 iliyofuata.

    Inaelezwa kwamba Khalid alipotoroka kumbe alipewa hifadhi na balozi ya ujerumani hapo Zanzibar na kisha baadae akasafirishwa na meli za wajerumani kuja Tanganyika (koloni la ujerumani)

    Ilipofika mwaka 1916, wakati wa vita ya kwanza ya dunia tuliona majeshi ya Uingereza yanavamia makoloni ya ujerumani ikiwemo Tanganyika, ambapo *Khalid* alikamatwa na kupelekwa Seychelles , lakini baada ya miaka michache alirudishwa Mombasa ambapo alifariki Mwaka 1927.

    ***

    Na hiyo ndiyo vita fupi kuliko zote kuwahi kutokea Duniani.

    VITA FUPI. Je unaifahamu vita fupi kuliko zote kuwahi kutokea duniani?. Kama hufahamu, basi leo inabidi ujue kwamba miaka 122 iliyopita, kulitokea vita iliyodumu kwa dakika 38 tu, na hivyo kuweka rekodi ya kuwa ndio vita fupi kuliko zote kuwahi kutokea duniani. Vita hiyo iliyojulikana kama 'Anglo- Zanzibar war' iliyotokea mwaka 1896 kati ya uingereza na Zanzibar, ikipiganwa katika ardhi ya Zanzibar iliyokuwa chini ya utawala wa kisultani. Kabla ya kuelezea vita hiyo, kwanza inabidi tufahamu jinsi historia ya Zanzibar hapo kabla ya mwaka 1698 ambapo ilikuwa chini ya utawala wa wareno waliotawala hapo kuanzia mwishoni mwa miaka 1490. Wareno hao waliondoka baada ya ujio wa waarabu kutoka Oman, waliokuja pwani ya Afrika Mashariki mnamo mwaka 1698. Hivyo kuanzia hapo, Zanzibar ikawa ni sehemu ya himaya ya Oman, ikiongozwa na masultani walioko mjini Muscat, Oman. Ilipofika mwaka 1804, Oman ikapata sultan mpya, aitwaye Sayyid Said ambaye aliweza kuanzisha mashamba ya mikarafuu huku akiwatumia watumwa kutoka Tanganyika wakitumika kama nguvu kazi katika mashamba hayo. Mwaka 1832, Sultan Sayyid Said alihamisha mji mkuu wa Omani kutoka Muskat kwenda Unguja. Hiyo ikapelekea ukuaji wa maendeleo katika mji wa Unguja kutokana na watu wengi kufurika hapo wakitoka sehemu mbalimbali ikiwemo Oman. Nchi mbalimbali zikaanza kujenga balozi zao hapo Zanzibar, mfano Marekani ilijenga balozi yake mwaka 1837, Uingereza mwaka 1841 kisha Ufaransa mwaka 1844. Ilipofika mwaka 1840, Sultani Sayyid said alihama kabisa mjini Muskat na kuja kuishi Zanzibar huku akiendelea kujulikana kama Sultan wa Oman na Zanzibar hadi mwaka alipofariki mwaka 1856. Baada ya kufariki Sayyid Said, waliokuwa watoto wake Majid bin Said na mwingine aliyeitwa Thuwaini bin Said, wakaanza mgogoro kuhusu nani wa kurithi kiti cha usultani wa Oman. Mgogoro huo ulipelekea himaya ya Oman kugawanyika katika sehemu mbili, Thuwaini bin Said alichukua Oman na hivyo kuwa Sultani wa Oman. Lakini Majid bin Said akiichukua Zanzibar na hivyo kuwa Sultani wa kwanza wa Zanzibar. Sultan Majid bin Said alitawala Zanzibar hadi mwaka 1870, akifuatiwa na sultan Barghash ambaye kwa kushirikiana na waingereza anakumbukwa kwa kusitisha biashara ya watumwa hapo Zanzibar mwaka 1876 japokuwa utumwa ulikuwa unaendelea. Mnamo mwaka 1890, kulisainiwa mkataba baina ya ujerumani na uingereza uliojulikana kama mkataba wa Heligoland uliopelekea Zanzibar kuwa chini ya uangalizi wa Uingereza huku ikiendelea kuongozwa na Sultani. Mwaka 1893 Uingereza 'ilifanya figisu' na hatimaye kumpandikiza kibaraka wao, Hamad bin Thuwaini kuwa sultani mpya wa Zanzibar, akitawala kwa miaka mitatu hadi tarehe 25 Agosti 1896 alipofariki ghafla akiwa ofisini kwake. Ingawa kuna tetesi kwamba aliyesababisha kifo chake ni binamu yake aitwaye Khalid bin Barghash ambaye inasemekana kuwa alimtilia sumu kwenye chakula. Tetesi hizo zilionekana ni kweli kutokana na kitendo cha Khalid bin Barghash kurithi kiti cha usultani punde tuu baada ya kifo cha nduguye akifanya hivyo bila ya kuthibitishwa na serikali ya uingereza.Maana ilikuwa ni kanuni kwamba serikali ya uingereza lazima ipitishe mchakato wa kumpata sultani. Kitendo cha Khalid bin Barghash kujitwalia madaraka ya kisultani, kiliwafanya waingereza kuchukia sana. Hivyo aliyekuwa balozi wa uingereza nchini Zanzibar, Basil Cave alimpa onyo kali sana sultan Khalid akitaka aachie madaraka. Waingereza walimpendelea Hamud bin Muhammed, awe sultani kwasababu waliona huyo ndiye wangeweza kufanya nae kazi vizuri kwani watamfanya kama kibaraka wao. Kitendo cha Khalid bin Barghash kujitwalia madaraka ya kisultani, kiliwafanya waingereza kuchukia sana. Hivyo aliyekuwa balozi wa uingereza nchini Zanzibar, Basil Cave alimpa onyo kali sana sultan Khalid akitaka aachie madaraka. Waingereza walimpendelea Hamud bin Muhammed, awe sultani kwasababu waliona huyo ndiye wangeweza kufanya nae kazi vizuri kwani watamfanya kama kibaraka wao. Mgogoro ulikuwa mkubwa baada ya Sultan Khalid bin Barghash kukaidi kuachia madaraka, badala yake akazidi kujiimarisha kiulinzi kwa kuongeza askari 3000 kwa ajili ya kulinda kasri yake. Wakati huohuo, uingereza nao walikuwa tayari wameshatega meli zao za kivita kwenye bandari huku wanajeshi wakisambazwa sehemu mbalimbali kwa ajili ya kujiandaa na lolote litakalotokea. Basil Cave aliwasiliana na makao makuu huko London akiomba aongezewe meli nyingine ya kivita. Hatimaye meli aina ya HMS Sparrow ikitia nanga katika bandari ya Zanzibar. Japokuwa alikuwa tayari kwa pambano, Basil Cave hakuwa na mamlaka ya kuanzisha vita pasipo kupokea amri kutoka makao makuu Uingereza. Akatuma ujumbe makao makuu akisema hivi; *_" Tumefanya njia zote za amani lakini zimeshindikana, sasa tunaruhusiwa kuanza mashambulizi??"*_ Wakati anasubiria majibu kutoka makao makuu, Cave alituma tena ujumbe kwa Sultani akimtaka aachie madaraka, lakini Sultan hakujibu. Siku iliyofuata Cave alipokea majibu kutoka makao makuu ukisema kwamba, *" unaruhusiwa kufanya chochote unachodhani kinafaa na sisi tutakupa ushirikiano."* Wakati huohuo tuliona meli zingine za kivita zinaingia Zanzibar zikitokea uingereza. Usiku wa tarehe 26, Basil Cave akatuma Ujumbe wa mwisho kwa sultani akimtaka kuondoka ofisini kesho yake saa tatu asubuhi. Huku akiziamuru boti zote zisizo za kivita ziondolewe baharini ili kujiandaa na vita. Siku iliyofuata saa 2 asubuhi, Sultani Khalid akajibu, akasema hivi, *" Sina mpango wa kuachia madaraka na sitegemei kama mtaanzisha vita dhidi yetu"* Basil Cave naye akajibu akasema; "Hatuna haja ya kuanzisha vita, ila tutafanya hivyo kama ukikaidi maagizo yetu." Sultani hakujibu tena. Na ilipofika saa 3 kamili meli zote za kivita zilipokea amri ya kuanza kushambulia kasri ya sultani. Saa 3:02 asubuhi, majengo na silaha za Sultani zilianza kulipuliwa, huku majeshi ya sultani nayo yakijibu mashambulizi kwa kurusha makombora yao. Inaelezwa kwamba dakika chache tuu baada ya kuanza kwa mashambulizi, Sultan Khalid *alitoroka kupitia mlango wa nyuma* wa kasri hiyo akiwaacha wapiganaji wake wakiendelea na vita. Hadi kufikia saa 3:40, sehemu kubwa ya kasri ya sultani ilikuwa tayari imeshalipuliwa na bendera ya sultani ikashushwa. Na hapo ndipo ikawa mwisho wa vita hiyo fupi. Katika vita hiyo fupi, inaelezwa kwamba wapiganaji 500 wa sultani walifariki na kujeruhiwa huku mwanajeshi mmoja tuu wa kingereza alijeruhiwa lakini akapona baadae. Baada ya sultan Khalid kukimbia, ndipo Uingereza ikampitisha mtu wao *Hamud bin Muhammed,* kuwa sultani wa Zanzibar kwa miaka 6 iliyofuata. Inaelezwa kwamba Khalid alipotoroka kumbe alipewa hifadhi na balozi ya ujerumani hapo Zanzibar na kisha baadae akasafirishwa na meli za wajerumani kuja Tanganyika (koloni la ujerumani) Ilipofika mwaka 1916, wakati wa vita ya kwanza ya dunia tuliona majeshi ya Uingereza yanavamia makoloni ya ujerumani ikiwemo Tanganyika, ambapo *Khalid* alikamatwa na kupelekwa Seychelles , lakini baada ya miaka michache alirudishwa Mombasa ambapo alifariki Mwaka 1927. *** Na hiyo ndiyo vita fupi kuliko zote kuwahi kutokea Duniani.
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·817 مشاهدة
  • SARAFU YAOKOA MAISHA YA ASKARI VITANI.

    Optatius Buyssens mnamo Septemba 1914 wakati wa vita kuu ya kwanza ya Dunia ,alikua amebeba sarafu katika mfuko wake wa koti pasipokujua kuwa zinaenda kuokoa maisha yake hapo baadae.
    Hadithi ya kushangaza ya Buyssens, ambaye alinusurika vitani na kufariki baadae mwaka 1958, hadithi hii inasimuliwa na mjukuu wake Vincent Buyssens.

    Kwa kutumia picha ya sarafu, kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 alisema: 'Fedha hizi zilizuia risasi na kuokoa maisha ya babu yangu mkubwa wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia.'
    Vincent, anayeishi Antwerp Ubelgiji, alisema baba yake alipewa sarafu na Optatius pamoja na maelezo yake Baada ya kutoka vitani.

    "Kisa hiki kilitokea mwanzoni mwa vita katika mji wa Belbeke wa Ubelgiji.
    'Cha kushangaza zaidi sarafu hizo ndio zilizomfanya apigwe risasi kwa sababu zilipiga kelele kwenye mfuko wake wa shati.
    "Alikuwa na bahati sana kwani risasi ambayo ingemwua ilipiga rundo la sarafu, na hivyo kuokoa maisha yake.
    "Alipigwa kichwani kwa kitako cha bunduki na askari wa Ujerumani aliyempiga risasi, lakini alijifanya amekufa.
    "Wakati yule askari wa Ujerumani alipoondoka, yeye na mwenzake mwingine aliyejeruhiwa waliweza kutambaa na kuondoka salama kutoka katika uwanja wa vita'.
    Baada ya vita kuisha, baba na babu yake Vincent walihamia Uingereza, lakini walirudi Antwerp Ubelgiji baada ya WWII.
    Chanzo: Dailymail.
    -jbgw.
    SARAFU YAOKOA MAISHA YA ASKARI VITANI. Optatius Buyssens mnamo Septemba 1914 wakati wa vita kuu ya kwanza ya Dunia ,alikua amebeba sarafu katika mfuko wake wa koti pasipokujua kuwa zinaenda kuokoa maisha yake hapo baadae. Hadithi ya kushangaza ya Buyssens, ambaye alinusurika vitani na kufariki baadae mwaka 1958, hadithi hii inasimuliwa na mjukuu wake Vincent Buyssens. Kwa kutumia picha ya sarafu, kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 alisema: 'Fedha hizi zilizuia risasi na kuokoa maisha ya babu yangu mkubwa wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia.' Vincent, anayeishi Antwerp Ubelgiji, alisema baba yake alipewa sarafu na Optatius pamoja na maelezo yake Baada ya kutoka vitani. "Kisa hiki kilitokea mwanzoni mwa vita katika mji wa Belbeke wa Ubelgiji. 'Cha kushangaza zaidi sarafu hizo ndio zilizomfanya apigwe risasi kwa sababu zilipiga kelele kwenye mfuko wake wa shati. "Alikuwa na bahati sana kwani risasi ambayo ingemwua ilipiga rundo la sarafu, na hivyo kuokoa maisha yake. "Alipigwa kichwani kwa kitako cha bunduki na askari wa Ujerumani aliyempiga risasi, lakini alijifanya amekufa. "Wakati yule askari wa Ujerumani alipoondoka, yeye na mwenzake mwingine aliyejeruhiwa waliweza kutambaa na kuondoka salama kutoka katika uwanja wa vita'. Baada ya vita kuisha, baba na babu yake Vincent walihamia Uingereza, lakini walirudi Antwerp Ubelgiji baada ya WWII. Chanzo: Dailymail. -jbgw.
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·210 مشاهدة
  • MUONEKANO WA NABII ISSA MIAKA HIYO ULIKUWAJE ?

    Karibu kila mtu ana dhana fulani kuhusu muonekano wa Yesu Kristo.
    Ndiye mtu aliyechorwa zaidi katika sanaa ya Magharibi. Picha zake hutambuliwa kwa urahisi, ambapo huoneshwa akiwa na nywele na ndevu, akiwa amevalia vazi lefu lenye mikono mirefu linalofanana na kanzu ( la rangi nyeupe), na pia akiwa amejifunga joho (la rangi ya samawati). Muonekano wa Yesu umefahamika sana na wengi kiasi kwamba unaweza kutambuliwa ukiwa hata kwenye mikate au biskuti.

    Picha za sasa za Yesu zinatokana na enzi ya Byzantine, himaya iliyokuwa na mji mkuu wake Constantinople. Ni picha iliyoanza kutumika karne ya nne hivi. Michoro ya Yesu ya wakati wa utawala wa Byzantine ilikuwa ya ishara, na si muonekano wake. Wasanii waliangazia zaidi maana na si kumfananisha na Yesu mwenyewe.
    Picha zao ziliongozwa na dhana ya Yesu kama mtawala, kwenye kiti cha enzi, kama anavyoonyeshwa kwenye mchoro ulio kwenye altari ya kanisa la Santa Pudenziana jijini Roma.

    Yesu anaoneshwa akiwa amevalia mgolole wa rangi ya dhahabu.
    Ndiye mtawala wa dunia yote aliyetoka mbinguni, mfanano wa picha yake ni ule wa sanamu ya Zeus wa Olympus anayeonyeshwa akiwa na nywele ndefu za ndevu kwenye kiti cha enzi. Ni sanamu iliyokuwa maarufu sana wakati huo kiasi kwamba Mfalme Augustus wa Roma alishurutisha naye atengenezewe sanamu kama hiyo, lakini yake ikiwa bila nywele ndefu na ndevu, Wasanii wa Byzantine, walitaka kumuonyesha Kristo kama mtawala kutoka mbinguni, mfalme wa aina yake, na hivyo wakachora wakimuonyesha kama Zeus, lakini akiwa mdogo kidogo wa umri.

    Kilichotokea kadiri miaka ilivyosonga ni kwamba kuonyeshwa huku kwa Kristo kama mtawala kutoka mbinguni - ambapo wakati mwingine ameonyeshwa hata akiwa kama 'hippie' au 'superstar' (kama ilivyo kwenye mchoro huu hapa chini) - ndiko kumekuwa kama kigezo chetu cha Yesu alivyokuwa. Hebu tuchanganue kutoka kichwani hadi vidole vya miguuni. Wakristo wa nyakati za kwanza wakati walipokuwa wanamwonyesha Kristo si kama mtawala kutoka mbinguni, walimuonyesha kama binadamu wa kawaida tu - akiwa hana ndevu na hana nywele ndefu.

    Lakini pengine, kama msomi wa aina yake aliyekuwa akisafiri kutoka eneo moja hadi jingine, Yesu pengine alikuwa na ndevu, kwa sababu hakuwa akienda kwa vinyozi. Kwa kawaida, kuwa mchafu kiasi na kuwa na ndevu ndefu ni sifa ambazo zilihusishwa na wanafalsafa, wasomi wa ngazi ya juu, na kuwatenganisha na watu wa kawaida.
    Mwanafalsafa maarufu wa kundi la Stoic (Wanafalsafa wa Kigiriki waliofuata mafundisho ya mwanzilishi wao Zeno wa Citium mjini Athens mapema karne ya 3 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu) Epictetus aliamini "ilifaa hivyo kwa mujibu wa maumbile." Mambo yalibadilika katika karne ya 1 baada ya kuzaliwa kwa Yesu, wakati wa enzi za Warumi na Wagiriki, ambapo kuwa na nywele fupi na kunyoa ndefu ndiyo mambo yaliyochukuliwa kuwa yafaayo na ya kistaarabu.

    Kuwa na nywele ndefu na ndevu ni mambo ambayo yaliachiwa miungu pekee, si ya watu wa kawaida. Hata wanafalsafa enzi hizo walikuwa na nywele fupi. Ndevu pia hazikuwa sifa za kuwatambulisha Wayahudi enzi hizo. Ukweli ni kwamba moja ya changamoto ambazo waliotaka kuwatesa Wayahudi vipindi mbalimbali katika historia walihangaika sana kuwatofautisha na watu wengine. Hii ni kwa sababu wote walifanana (jambo ambalo limegusiwa katika kitabu cha Wamakabayo). Hata hivyo, picha za wanaume wa Kiyahudi zilizokuwa kwenye sarafu za Judea Capta ambazo zilitolewa na utawala wa Roma baada ya kutekwa kwa mji wa Yerusalemu mwaka 70 baada ya kuzaliwa kwa Yesu zinawaonesha wanaume wakiwa na ndevu, lakini nywele zao si ndefu.

    Kwa hivyo, Yesu, kama mwanafalsafa wa muonekano wa kawaida, kuna uwezekano alikuwa na ndevu lakini si ndefu sana, sawa na wanaume hao walioonyeshwa kwenye sarafu za Judaea Capta, lakini nywele zake basi hazikuwa ndefu sana pia.
    Kama ingetokea kwamba awe na nywele ndefu hata kidogo tu kuliko kawaida, basi angezua mtafaruku Wanaume wa Kiyahudi waliokuwa na ndevu ambazo hazikuwa zimetunzwa vyema na nywele ambazo zilikuwa ndefu kidogo kuliko kawaida walitambulika mara moja kama watu waliokuwa wamekula kiapo cha kuwa Wanazari (Nazarite).

    Hii ilikuwa na maana kwamba wangejitoa wakfu kwa Mungu kwa kipindi fulani, ambapo hawangekunywa vileo wala kuzikata nywele zao. Mwisho wa kipindi hicho, wangenyolewa nywele zao katika sherehe maalum hekaluni Jerusalem (kama inavyoelezwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Sura ya 21, aya ya 24).
    Lakini Yesu hakuwa amekula kiapo cha kuwa Mnazari, kwa sababu mara nyingi tunamsikia kwenye Biblia akinywa divai - wakosoaji wake hata wakati mwingine wanamshutumu kwa kunywa divai sana, kupita kiasi (Matayo Sura ya 11, aya ya 19). Kama angekuwepo na nywele ndefu, na kuonekana kama Mnazari, tungelitarajia basi kuwepo na tamko pahala fulani kuhusu tofauti ya muonekano wake na matendo aliyokuwa akiyafanya ambayo hayakuendana na Unazari. Hali kwamba alikuwa akinywa divai yenyewe ingekuwa tatizo kubwa.

    Wakati Yesu alipoishi, matajiri walizoea kuvalia kanzu na majoyo ya vitambaa vya thamani, kuonyesha hadhi yao katika jamii. Katika moja ya mahubiri yake, Yesu anasema : "Jihadharini na walimu wa sheria (waandishi). Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu (stolai), na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Pia wao hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kupewa nafasi za heshima katika karamu." Mafundisho haya ya Yesu kwa kawaida huchukuliwa kama yenye maelezo ya kuaminika zaidi kwenye Injili, hivyo tunaweza kuwa na msingi kuamini kwamba Yesu hakuvalia mavazi kama hayo marefu. Kwa jumla, mwanamume wakati huo wa Yesu angevalia gwanda au kanzu fupi hivi, na mwanamke angevalia vazi lililomfika kwenye kifundo cha mguu.

    Kwa hivyo, katika karne ya 2 kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume, Paul na Thecla, inapotokea kwamba Thecla ambaye ni mwanamke anavalia kanzu fupi kama mwanamume, hilo ni jambo linaloshangaza sana. Kanzu hizi kwa kawaida zingekuwa na ukanda au mstari wa rangi tofauti kutoka kwenye bega hadi kwenye pindo sehemu ya chini. Ni vazi ambalo lingeshonwa au kufumwa kama kipande kimoja cha vazi. Juu ya kanzu hiyo, ungejifunga joho au vazi jingine la nje, na tunajua kwamba Yesu alivalia vazi kama hilo kwa sababu ndilo lililoguswa na mwanamke aliyetaka kuponywa naye. (Marko 5:27): Alikuwa amesikia habari za Yesu, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, kwa maana alisema moyoni mwake, 'Kama nikiweza kuligusa vazi lake tu, nitaponywa.') Vazi hilo la nje lilifumwa kwa manyoya, lakini halikuwa zito sana na ndipo ili uhisi joto ingemlazimu mtu kuvalia mavazi mawili kama hayo.

    Vazi hilo lingevaliwa kwa njia nyingi, na wakati mwingine lingening'inia hadi chini ya magoti na kulifunika lile kanzu fupi la ndani. (Baadhi ya wanafalsafa walizoea kuvalia vazi hilo la nje pekee bila kuvalia ile kanzu ya ndani na kuacha sehemu ya bega au kifua ikiwa wazi). Mamlaka na hadhi ya mtu ni vitu ambavyo vilidhihirishwa kupitia ubora, ukubwa na rangi ya mavazi hayo ya nje. Rangi ya zambarau na baadhi ya aina za rangi ya buluu (samawati) ni rangi zilizoashiria utajiri, hadhi na kujionea fahari. Zilikuwa ni rangi za kifahari kwa sababu viungo vya kutengeneza rangi hizo vilikuwa adimu na ghali sana.

    Lakini rangi pia huashiria kitu kingine tofauti. Mwanahistoria Josephus, anawaeleza walokole waliofahamika kama Zealots (kundi la Wayahudi wa itikadi kali waliotaka kuwafurusha Warumi kutoka Judea) kama kundi la wahalifu wauaji waliovalia mavazi ya nje yaliyopakwa rangi kwa jina - mavazi anayoyaita chlanidia - kuashiria kwamba yalikuwa ni kama mavazi yaliyovaliwa na wanawake. Hii inaashiria kwamba wanaume kamili, kama hawakuwa na cheo cha juu zaidi katika jamii, walifaa kuvalia mavazi yasiyopakwa rangi.
    Yesu hakuvalia mavazi meupe hata hivyo. Haya yalikuwa mavazi ya kipekee na yalihitaji kupaushwa mara kwa mara (kufanywa meupe tena) au kupakwa chokaa. Judea, mavazi kama hayo meupe yalihusishwa na kundi lililofahamika kama Essenes - ambao ni watu waliofuata ufasiri mkali wa sheria za Kiyahudi. Tofauti kati ya mavazi ya Yesu na mavazi mengine ya rangi nyeupe ya kung'aa inaelezwa kwenye sura ya 9 ya Marko ambapo anaandamana na mitume watatu mlimani.

    Yesu aliwachukua "Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao. Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angaliweza kuyangʼarisha. Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu." Marko anaeleza kwamba mavazi ya Yesu yaligeuka rangi yakawa meupe sana, hapa anarejelea vazi la ndani na si la nje. Kabla ya kugeuka sura huku kwa Yesu, anaoneshwa na Marko kama mwanamume wa kawaida, aliyevalia mavazi ya kawaida, ambayo ni ya rangi ambayo haijapaushwa. Katika hali ambayo ndipo yang'ae na kuangaza unahitaji kumpelekea fundi.

    Tunaelezwa zaidi kuhusu mavazi ya Yesu wakati wa kusulubiwa kwake, pale wanajeshi wa Kirumi wanapoyakata mavazi yake ya nje vipande vinne (Yohana19:23: Askari walipokwisha kumsulubisha Yesu, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini.) Kuna uwezekano mavazi hayo ya nje yalikuwa mavazi mawili.

    Moja ya vazi hili huenda lilikuwa ni tallith, ambalo ni vazi la kujifunga Kiyahudi wakati wa maombi. Vazi hili lenye shada (tzitzith) limetajwa moja kwa moja na Yesu katika kitabu cha Mathayo 23:5 anapozungumza kuhusu walimu wa sheria na Mafarisayo (Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao). Lilikuwa ni vazi la nje lisilo zito, ambalo kawaida lilitengenezwa kwa kitambaa cha manyoya na lilikuwa la rangi ya malai hivi (krimu), na pengine lilikuwa na ukanda au mstari wa rangi ya nili (bluu iliyoiva).

    Miguuni, Yesu angevalia ndara (kandambili au malapa). Kila mtu wakati huo alivalia ndara. Katika mapango yaliyo jangwani karibu na Bahari ya Chumvi (Bahari Mfu) na Masada, ndara za wakati alipoishi Yesu zimegunduliwa, na tunaweza kutazama ndara ambazo huenda alivaa zilivyoonekana. Zilikuwa hazijafanyiwa kazi nyingi sana ya kiufundi. Soli (nyayo au kikanyagio) zake zilikuwa vipande vigumu vya ngozi vilivyoshonwa pamoja, na juu kulikuwa ni kanda za ngozi ambazo mbele zingeingizwa katikati ya vidole, kama malapa tu ya siku hizi.

    Yesu (Nabii Issa) Alikuwa Myahudi, na uso wake pia bila shaka ungefanana na Wayahudi wa wakati huo. Hali kwamba Yesu alikuwa Myahudi (au Mjudea) ni jambo linalorejelewa katika vitabu vingi, zikiwemo barua za Mtume Paulo. Na katika barua yake kwa Waebrania, anaandika: "Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda" (Sura ya 7:14) Kwa hivyo, Myahudi wa wakati huo, mwanamume wa miaka 30 hivi alipoanza kueneza Injili kwa mujibu wa Luka 3, pia akiwa ni mwenye ngozi nyeusi kama ilivyokuwa kwa wayahudi wengi zama zile waliokuwa wakitembeleana na ndugu zao wa Misri (Kushi) kemet.

    Mwaka 2001 mwanaantholopojia (mtaalamu wa elimu ya binadamu hasa elimu ihusuyo habari zinazohusu asili na maendeleo yake ya awali) Richard Neave alitengeneza mfano wa mwanamume wa Galilaya wa zama za Yesu ambao ulitumiwa kwa jina Son of God (Mwana wa Mungu). Alitumia fuvu lililopatikana katika eneo hilo. Hakusema kwamba huo ulikuwa muonekano wa uso wa Yesu. Mfano ulikuwa tu wa kuchochea hisia na kuwafanya watu kumfikiria Yesu kama mwanamume wa zama hizo na eneo hilo, kwa sababu hakuna mchoro wala maelezo yaliyopo ya kina kuhusu muonekano wake halisi.

    Ingawa tunaweza kupata viashiria kutoka kwa teknolojia na kutumia mifupa ya watu wa kale, kiashiria cha karibu sana kuhusu pengine Yesu alionekana vipi labda kinaweza kutokana na mchoro wa Musa kwenye ukuta wa sinagogi ya karne ya 3 ya Dura-Europos, kwani mchoro huo unaonesha jinsi Myahudi wa hekima alidhaniwa kuwa wakati wa utawala wa Wagiriki na Warumi. Musa anaoneshwa akiwa na mavazi ambayo hayajapaushwa, na moja ya vazi lake la nje ni tallith.

    Katika mchoro huo wa Dura wa Musa akitenganisha maji kwenye Bahari ya Sham ili Waisraeli wapite, unaweza kuziona shada (tzitzith) kwenye kona za vazi hilo. Kwa kiwango kikubwa, picha hiyo pengine inatoa msingi bora zaidi wa kumfikiria Yesu alivyokuwa badala ya picha za sasa zinazoongozwa na busara na mawazo ya enzi ya Byzantine - alikuwa na nywele fupi, ndevu fupi, na alikuwa amevalia kanzu fupi lenye mikono mifupi, na alikuwa na joho au vazi la nje.

    Makala hii chimbuko lake ni makala ya Kiingereza ya Joan Taylor ambaye ni profesa wa kitivo cha Asili ya Ukristo na Hekalu la Pili la Wayahudi katika Chuo Kikuu cha King's College London na ndiye mwandishi wa kitabu kwa jina The Essenes, the Scrolls and the Dead Sea.
    MUONEKANO WA NABII ISSA MIAKA HIYO ULIKUWAJE ? Karibu kila mtu ana dhana fulani kuhusu muonekano wa Yesu Kristo. Ndiye mtu aliyechorwa zaidi katika sanaa ya Magharibi. Picha zake hutambuliwa kwa urahisi, ambapo huoneshwa akiwa na nywele na ndevu, akiwa amevalia vazi lefu lenye mikono mirefu linalofanana na kanzu ( la rangi nyeupe), na pia akiwa amejifunga joho (la rangi ya samawati). Muonekano wa Yesu umefahamika sana na wengi kiasi kwamba unaweza kutambuliwa ukiwa hata kwenye mikate au biskuti. Picha za sasa za Yesu zinatokana na enzi ya Byzantine, himaya iliyokuwa na mji mkuu wake Constantinople. Ni picha iliyoanza kutumika karne ya nne hivi. Michoro ya Yesu ya wakati wa utawala wa Byzantine ilikuwa ya ishara, na si muonekano wake. Wasanii waliangazia zaidi maana na si kumfananisha na Yesu mwenyewe. Picha zao ziliongozwa na dhana ya Yesu kama mtawala, kwenye kiti cha enzi, kama anavyoonyeshwa kwenye mchoro ulio kwenye altari ya kanisa la Santa Pudenziana jijini Roma. Yesu anaoneshwa akiwa amevalia mgolole wa rangi ya dhahabu. Ndiye mtawala wa dunia yote aliyetoka mbinguni, mfanano wa picha yake ni ule wa sanamu ya Zeus wa Olympus anayeonyeshwa akiwa na nywele ndefu za ndevu kwenye kiti cha enzi. Ni sanamu iliyokuwa maarufu sana wakati huo kiasi kwamba Mfalme Augustus wa Roma alishurutisha naye atengenezewe sanamu kama hiyo, lakini yake ikiwa bila nywele ndefu na ndevu, Wasanii wa Byzantine, walitaka kumuonyesha Kristo kama mtawala kutoka mbinguni, mfalme wa aina yake, na hivyo wakachora wakimuonyesha kama Zeus, lakini akiwa mdogo kidogo wa umri. Kilichotokea kadiri miaka ilivyosonga ni kwamba kuonyeshwa huku kwa Kristo kama mtawala kutoka mbinguni - ambapo wakati mwingine ameonyeshwa hata akiwa kama 'hippie' au 'superstar' (kama ilivyo kwenye mchoro huu hapa chini) - ndiko kumekuwa kama kigezo chetu cha Yesu alivyokuwa. Hebu tuchanganue kutoka kichwani hadi vidole vya miguuni. Wakristo wa nyakati za kwanza wakati walipokuwa wanamwonyesha Kristo si kama mtawala kutoka mbinguni, walimuonyesha kama binadamu wa kawaida tu - akiwa hana ndevu na hana nywele ndefu. Lakini pengine, kama msomi wa aina yake aliyekuwa akisafiri kutoka eneo moja hadi jingine, Yesu pengine alikuwa na ndevu, kwa sababu hakuwa akienda kwa vinyozi. Kwa kawaida, kuwa mchafu kiasi na kuwa na ndevu ndefu ni sifa ambazo zilihusishwa na wanafalsafa, wasomi wa ngazi ya juu, na kuwatenganisha na watu wa kawaida. Mwanafalsafa maarufu wa kundi la Stoic (Wanafalsafa wa Kigiriki waliofuata mafundisho ya mwanzilishi wao Zeno wa Citium mjini Athens mapema karne ya 3 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu) Epictetus aliamini "ilifaa hivyo kwa mujibu wa maumbile." Mambo yalibadilika katika karne ya 1 baada ya kuzaliwa kwa Yesu, wakati wa enzi za Warumi na Wagiriki, ambapo kuwa na nywele fupi na kunyoa ndefu ndiyo mambo yaliyochukuliwa kuwa yafaayo na ya kistaarabu. Kuwa na nywele ndefu na ndevu ni mambo ambayo yaliachiwa miungu pekee, si ya watu wa kawaida. Hata wanafalsafa enzi hizo walikuwa na nywele fupi. Ndevu pia hazikuwa sifa za kuwatambulisha Wayahudi enzi hizo. Ukweli ni kwamba moja ya changamoto ambazo waliotaka kuwatesa Wayahudi vipindi mbalimbali katika historia walihangaika sana kuwatofautisha na watu wengine. Hii ni kwa sababu wote walifanana (jambo ambalo limegusiwa katika kitabu cha Wamakabayo). Hata hivyo, picha za wanaume wa Kiyahudi zilizokuwa kwenye sarafu za Judea Capta ambazo zilitolewa na utawala wa Roma baada ya kutekwa kwa mji wa Yerusalemu mwaka 70 baada ya kuzaliwa kwa Yesu zinawaonesha wanaume wakiwa na ndevu, lakini nywele zao si ndefu. Kwa hivyo, Yesu, kama mwanafalsafa wa muonekano wa kawaida, kuna uwezekano alikuwa na ndevu lakini si ndefu sana, sawa na wanaume hao walioonyeshwa kwenye sarafu za Judaea Capta, lakini nywele zake basi hazikuwa ndefu sana pia. Kama ingetokea kwamba awe na nywele ndefu hata kidogo tu kuliko kawaida, basi angezua mtafaruku Wanaume wa Kiyahudi waliokuwa na ndevu ambazo hazikuwa zimetunzwa vyema na nywele ambazo zilikuwa ndefu kidogo kuliko kawaida walitambulika mara moja kama watu waliokuwa wamekula kiapo cha kuwa Wanazari (Nazarite). Hii ilikuwa na maana kwamba wangejitoa wakfu kwa Mungu kwa kipindi fulani, ambapo hawangekunywa vileo wala kuzikata nywele zao. Mwisho wa kipindi hicho, wangenyolewa nywele zao katika sherehe maalum hekaluni Jerusalem (kama inavyoelezwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Sura ya 21, aya ya 24). Lakini Yesu hakuwa amekula kiapo cha kuwa Mnazari, kwa sababu mara nyingi tunamsikia kwenye Biblia akinywa divai - wakosoaji wake hata wakati mwingine wanamshutumu kwa kunywa divai sana, kupita kiasi (Matayo Sura ya 11, aya ya 19). Kama angekuwepo na nywele ndefu, na kuonekana kama Mnazari, tungelitarajia basi kuwepo na tamko pahala fulani kuhusu tofauti ya muonekano wake na matendo aliyokuwa akiyafanya ambayo hayakuendana na Unazari. Hali kwamba alikuwa akinywa divai yenyewe ingekuwa tatizo kubwa. Wakati Yesu alipoishi, matajiri walizoea kuvalia kanzu na majoyo ya vitambaa vya thamani, kuonyesha hadhi yao katika jamii. Katika moja ya mahubiri yake, Yesu anasema : "Jihadharini na walimu wa sheria (waandishi). Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu (stolai), na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Pia wao hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kupewa nafasi za heshima katika karamu." Mafundisho haya ya Yesu kwa kawaida huchukuliwa kama yenye maelezo ya kuaminika zaidi kwenye Injili, hivyo tunaweza kuwa na msingi kuamini kwamba Yesu hakuvalia mavazi kama hayo marefu. Kwa jumla, mwanamume wakati huo wa Yesu angevalia gwanda au kanzu fupi hivi, na mwanamke angevalia vazi lililomfika kwenye kifundo cha mguu. Kwa hivyo, katika karne ya 2 kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume, Paul na Thecla, inapotokea kwamba Thecla ambaye ni mwanamke anavalia kanzu fupi kama mwanamume, hilo ni jambo linaloshangaza sana. Kanzu hizi kwa kawaida zingekuwa na ukanda au mstari wa rangi tofauti kutoka kwenye bega hadi kwenye pindo sehemu ya chini. Ni vazi ambalo lingeshonwa au kufumwa kama kipande kimoja cha vazi. Juu ya kanzu hiyo, ungejifunga joho au vazi jingine la nje, na tunajua kwamba Yesu alivalia vazi kama hilo kwa sababu ndilo lililoguswa na mwanamke aliyetaka kuponywa naye. (Marko 5:27): Alikuwa amesikia habari za Yesu, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, kwa maana alisema moyoni mwake, 'Kama nikiweza kuligusa vazi lake tu, nitaponywa.') Vazi hilo la nje lilifumwa kwa manyoya, lakini halikuwa zito sana na ndipo ili uhisi joto ingemlazimu mtu kuvalia mavazi mawili kama hayo. Vazi hilo lingevaliwa kwa njia nyingi, na wakati mwingine lingening'inia hadi chini ya magoti na kulifunika lile kanzu fupi la ndani. (Baadhi ya wanafalsafa walizoea kuvalia vazi hilo la nje pekee bila kuvalia ile kanzu ya ndani na kuacha sehemu ya bega au kifua ikiwa wazi). Mamlaka na hadhi ya mtu ni vitu ambavyo vilidhihirishwa kupitia ubora, ukubwa na rangi ya mavazi hayo ya nje. Rangi ya zambarau na baadhi ya aina za rangi ya buluu (samawati) ni rangi zilizoashiria utajiri, hadhi na kujionea fahari. Zilikuwa ni rangi za kifahari kwa sababu viungo vya kutengeneza rangi hizo vilikuwa adimu na ghali sana. Lakini rangi pia huashiria kitu kingine tofauti. Mwanahistoria Josephus, anawaeleza walokole waliofahamika kama Zealots (kundi la Wayahudi wa itikadi kali waliotaka kuwafurusha Warumi kutoka Judea) kama kundi la wahalifu wauaji waliovalia mavazi ya nje yaliyopakwa rangi kwa jina - mavazi anayoyaita chlanidia - kuashiria kwamba yalikuwa ni kama mavazi yaliyovaliwa na wanawake. Hii inaashiria kwamba wanaume kamili, kama hawakuwa na cheo cha juu zaidi katika jamii, walifaa kuvalia mavazi yasiyopakwa rangi. Yesu hakuvalia mavazi meupe hata hivyo. Haya yalikuwa mavazi ya kipekee na yalihitaji kupaushwa mara kwa mara (kufanywa meupe tena) au kupakwa chokaa. Judea, mavazi kama hayo meupe yalihusishwa na kundi lililofahamika kama Essenes - ambao ni watu waliofuata ufasiri mkali wa sheria za Kiyahudi. Tofauti kati ya mavazi ya Yesu na mavazi mengine ya rangi nyeupe ya kung'aa inaelezwa kwenye sura ya 9 ya Marko ambapo anaandamana na mitume watatu mlimani. Yesu aliwachukua "Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao. Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angaliweza kuyangʼarisha. Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu." Marko anaeleza kwamba mavazi ya Yesu yaligeuka rangi yakawa meupe sana, hapa anarejelea vazi la ndani na si la nje. Kabla ya kugeuka sura huku kwa Yesu, anaoneshwa na Marko kama mwanamume wa kawaida, aliyevalia mavazi ya kawaida, ambayo ni ya rangi ambayo haijapaushwa. Katika hali ambayo ndipo yang'ae na kuangaza unahitaji kumpelekea fundi. Tunaelezwa zaidi kuhusu mavazi ya Yesu wakati wa kusulubiwa kwake, pale wanajeshi wa Kirumi wanapoyakata mavazi yake ya nje vipande vinne (Yohana19:23: Askari walipokwisha kumsulubisha Yesu, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini.) Kuna uwezekano mavazi hayo ya nje yalikuwa mavazi mawili. Moja ya vazi hili huenda lilikuwa ni tallith, ambalo ni vazi la kujifunga Kiyahudi wakati wa maombi. Vazi hili lenye shada (tzitzith) limetajwa moja kwa moja na Yesu katika kitabu cha Mathayo 23:5 anapozungumza kuhusu walimu wa sheria na Mafarisayo (Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao). Lilikuwa ni vazi la nje lisilo zito, ambalo kawaida lilitengenezwa kwa kitambaa cha manyoya na lilikuwa la rangi ya malai hivi (krimu), na pengine lilikuwa na ukanda au mstari wa rangi ya nili (bluu iliyoiva). Miguuni, Yesu angevalia ndara (kandambili au malapa). Kila mtu wakati huo alivalia ndara. Katika mapango yaliyo jangwani karibu na Bahari ya Chumvi (Bahari Mfu) na Masada, ndara za wakati alipoishi Yesu zimegunduliwa, na tunaweza kutazama ndara ambazo huenda alivaa zilivyoonekana. Zilikuwa hazijafanyiwa kazi nyingi sana ya kiufundi. Soli (nyayo au kikanyagio) zake zilikuwa vipande vigumu vya ngozi vilivyoshonwa pamoja, na juu kulikuwa ni kanda za ngozi ambazo mbele zingeingizwa katikati ya vidole, kama malapa tu ya siku hizi. Yesu (Nabii Issa) Alikuwa Myahudi, na uso wake pia bila shaka ungefanana na Wayahudi wa wakati huo. Hali kwamba Yesu alikuwa Myahudi (au Mjudea) ni jambo linalorejelewa katika vitabu vingi, zikiwemo barua za Mtume Paulo. Na katika barua yake kwa Waebrania, anaandika: "Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda" (Sura ya 7:14) Kwa hivyo, Myahudi wa wakati huo, mwanamume wa miaka 30 hivi alipoanza kueneza Injili kwa mujibu wa Luka 3, pia akiwa ni mwenye ngozi nyeusi kama ilivyokuwa kwa wayahudi wengi zama zile waliokuwa wakitembeleana na ndugu zao wa Misri (Kushi) kemet. Mwaka 2001 mwanaantholopojia (mtaalamu wa elimu ya binadamu hasa elimu ihusuyo habari zinazohusu asili na maendeleo yake ya awali) Richard Neave alitengeneza mfano wa mwanamume wa Galilaya wa zama za Yesu ambao ulitumiwa kwa jina Son of God (Mwana wa Mungu). Alitumia fuvu lililopatikana katika eneo hilo. Hakusema kwamba huo ulikuwa muonekano wa uso wa Yesu. Mfano ulikuwa tu wa kuchochea hisia na kuwafanya watu kumfikiria Yesu kama mwanamume wa zama hizo na eneo hilo, kwa sababu hakuna mchoro wala maelezo yaliyopo ya kina kuhusu muonekano wake halisi. Ingawa tunaweza kupata viashiria kutoka kwa teknolojia na kutumia mifupa ya watu wa kale, kiashiria cha karibu sana kuhusu pengine Yesu alionekana vipi labda kinaweza kutokana na mchoro wa Musa kwenye ukuta wa sinagogi ya karne ya 3 ya Dura-Europos, kwani mchoro huo unaonesha jinsi Myahudi wa hekima alidhaniwa kuwa wakati wa utawala wa Wagiriki na Warumi. Musa anaoneshwa akiwa na mavazi ambayo hayajapaushwa, na moja ya vazi lake la nje ni tallith. Katika mchoro huo wa Dura wa Musa akitenganisha maji kwenye Bahari ya Sham ili Waisraeli wapite, unaweza kuziona shada (tzitzith) kwenye kona za vazi hilo. Kwa kiwango kikubwa, picha hiyo pengine inatoa msingi bora zaidi wa kumfikiria Yesu alivyokuwa badala ya picha za sasa zinazoongozwa na busara na mawazo ya enzi ya Byzantine - alikuwa na nywele fupi, ndevu fupi, na alikuwa amevalia kanzu fupi lenye mikono mifupi, na alikuwa na joho au vazi la nje. Makala hii chimbuko lake ni makala ya Kiingereza ya Joan Taylor ambaye ni profesa wa kitivo cha Asili ya Ukristo na Hekalu la Pili la Wayahudi katika Chuo Kikuu cha King's College London na ndiye mwandishi wa kitabu kwa jina The Essenes, the Scrolls and the Dead Sea.
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·823 مشاهدة
  • JINSI SHIRIKA LA KIJASUSI LA URUSI FSB {KGB} LILIVYO HATARI....

    Kama waswahili wasemavyo maisha ni safari ndefu na kifo ni Siri, pengine hili ni kweli kutokana na sintofahamu iliyochukua uhai wa Alexander Litvinenko, jasusi wa zamañi wa KGB na baadae FSB ya Urusi ya sasa.

    Tutarudi Sasa tuendelee mwishoni mwa wiki za mwezi wa kumi mwaka 2006 Alexander Litvinenko alipokuwa jijini London alipotorokea baada ya rabsha dhidi ya serikali mjini Moscow, siku hiyo Litvinenko alikuwa ametembelewa na marafiki zake wawili walikuwa wanausalama ndani ya FSB na iliyokuwa KGB Dmitri Kovtun na Andrei Lugovoi, asichokijua ni kwamba wale wawili walikuwa moja ya watu hatari na pia kama wasafirishaji mahiri wa msafiri kama Litvinenko kuliendelea kaburi

    Waliikutana hotelini jijini London wakinywa na kufurahi, siku hiyo Lugovoi na Kovtun wao waliagiza bia wakanywa wakifurahi, unajua nini Litvinenko ye aliagizwa chai ya rangi akanywa huku akiwachekea wasafirishaji wa ule msemo wa kiswahili " maisha ni safari"

    Maskinii Litvinenko alipojichanganya tu Lugovoi na Kovtun wakifanya kazi yao moja waliotumwa na FSB, kumnyamazisha " traitor of the mother Russia"

    Unajua walifanya Nini? Walichukua kemikali hatari sana duniani inayoua taratibu sana jina lake Polonium 210 wakatia katika chai ya Litvinenko. Inavyosemekana alivyorudi walimchekea na kufurahi zaidi kuona Litvinenko alikuwa amesahau mbinu muhimu kabisa ya wanaintelijensia kote duniani ! Kutomwamini mtu hata mama na baba yako.
    Litvinenko alikunywa chai ile

    **********
    Lugovoi na Kovtun walichukua ndege siku tatu baadae haoo Moscow, huko walifanyiwa sherehe ya uhakika wa kazi iliyofanyika isiyo na shaka, Kovtun aliamua kuwa mfanyabiashara mkubwa wakati Lugovoi alipandishwa cheo siku chache baadae.
    ******
    Maskini Litvinenko aliagana na wanyama wale wa kwenye barafu Kama wajiitavyo wao " "bear " lakini akiwapachika majina mazuri yaani marafiki, ndugu, wapenzi kutoka home Russia. Pia aliwauliza vipi watarudi lini kumuona, kimoyomoyo Kovtun na Lugovoi walikua wakicheka na kusikitika kiunafiki,wakijua huyu mtu hana mwezi duniani. Wiki tatu nyingi! atakufa kifo Cha mateso akiwa kitandani amelala.

    ***
    November 1 mwaka 2006 Litvinenko aliugua homa ya ghafla mwili ukiungua kwa namna ya kutisha sana, alipelekwa hospitali mjini London akaishi kwa wiki 3 akiwa hoi kitandani! Wakati akifa akitoa laana kwa Putin akamshutumu amemuua.

    Huo ukawa mwisho wa Litvinenko mtu aliyekuwa ameaminiwa kutunza siri za Russia yeye alizitoa hadharani kwa m16 . Pengine ni chafu sana zenye damu lakini bila shaka kulikuwa pigo kwa vitu hivyo kuwa hadharani. Putin alivuliwa nguo hata asiijifunike.

    Tuzungimzapo Leo ni miaka karibu 12 toka mnyama huyu atutoke.

    Mwaka fulani Putin aliulizwa na mwanahabari mmoja ni kitu gani asichoweza kuvumilia na kusamehe alisema hivi.. Ye ni ngumu sana kuwasamehe wasaliti wa mother Russia.

    Ohh ndo hivyo Litvinenko hakupata bahati ya kusamehewa na Putin hivyo alikwenda.

    Chanzo: na Google
    JINSI SHIRIKA LA KIJASUSI LA URUSI FSB {KGB} LILIVYO HATARI.... Kama waswahili wasemavyo maisha ni safari ndefu na kifo ni Siri, pengine hili ni kweli kutokana na sintofahamu iliyochukua uhai wa Alexander Litvinenko, jasusi wa zamañi wa KGB na baadae FSB ya Urusi ya sasa. Tutarudi Sasa tuendelee mwishoni mwa wiki za mwezi wa kumi mwaka 2006 Alexander Litvinenko alipokuwa jijini London alipotorokea baada ya rabsha dhidi ya serikali mjini Moscow, siku hiyo Litvinenko alikuwa ametembelewa na marafiki zake wawili walikuwa wanausalama ndani ya FSB na iliyokuwa KGB Dmitri Kovtun na Andrei Lugovoi, asichokijua ni kwamba wale wawili walikuwa moja ya watu hatari na pia kama wasafirishaji mahiri wa msafiri kama Litvinenko kuliendelea kaburi Waliikutana hotelini jijini London wakinywa na kufurahi, siku hiyo Lugovoi na Kovtun wao waliagiza bia wakanywa wakifurahi, unajua nini Litvinenko ye aliagizwa chai ya rangi akanywa huku akiwachekea wasafirishaji wa ule msemo wa kiswahili " maisha ni safari" Maskinii Litvinenko alipojichanganya tu Lugovoi na Kovtun wakifanya kazi yao moja waliotumwa na FSB, kumnyamazisha " traitor of the mother Russia" Unajua walifanya Nini? Walichukua kemikali hatari sana duniani inayoua taratibu sana jina lake Polonium 210 wakatia katika chai ya Litvinenko. Inavyosemekana alivyorudi walimchekea na kufurahi zaidi kuona Litvinenko alikuwa amesahau mbinu muhimu kabisa ya wanaintelijensia kote duniani ! Kutomwamini mtu hata mama na baba yako. Litvinenko alikunywa chai ile ********** Lugovoi na Kovtun walichukua ndege siku tatu baadae haoo Moscow, huko walifanyiwa sherehe ya uhakika wa kazi iliyofanyika isiyo na shaka, Kovtun aliamua kuwa mfanyabiashara mkubwa wakati Lugovoi alipandishwa cheo siku chache baadae. ****** Maskini Litvinenko aliagana na wanyama wale wa kwenye barafu Kama wajiitavyo wao " "bear " lakini akiwapachika majina mazuri yaani marafiki, ndugu, wapenzi kutoka home Russia. Pia aliwauliza vipi watarudi lini kumuona, kimoyomoyo Kovtun na Lugovoi walikua wakicheka na kusikitika kiunafiki,wakijua huyu mtu hana mwezi duniani. Wiki tatu nyingi! atakufa kifo Cha mateso akiwa kitandani amelala. *** November 1 mwaka 2006 Litvinenko aliugua homa ya ghafla mwili ukiungua kwa namna ya kutisha sana, alipelekwa hospitali mjini London akaishi kwa wiki 3 akiwa hoi kitandani! Wakati akifa akitoa laana kwa Putin akamshutumu amemuua. Huo ukawa mwisho wa Litvinenko mtu aliyekuwa ameaminiwa kutunza siri za Russia yeye alizitoa hadharani kwa m16 . Pengine ni chafu sana zenye damu lakini bila shaka kulikuwa pigo kwa vitu hivyo kuwa hadharani. Putin alivuliwa nguo hata asiijifunike. Tuzungimzapo Leo ni miaka karibu 12 toka mnyama huyu atutoke. Mwaka fulani Putin aliulizwa na mwanahabari mmoja ni kitu gani asichoweza kuvumilia na kusamehe alisema hivi.. Ye ni ngumu sana kuwasamehe wasaliti wa mother Russia. Ohh ndo hivyo Litvinenko hakupata bahati ya kusamehewa na Putin hivyo alikwenda. Chanzo: na Google
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·970 مشاهدة
  • #JEWAJUA
    Jumba la Mfalme wa muziki wa Pop Michael Jackson ambalo alilinunua mwaka 1987 kwa USD milioni 19.5 limenunuliwa na Tajiri Ron Burkle kwa kiwango kinachotajwa kufika USD milioni 22 (USD milioni moja ni sawa na Tsh. Bilioni 2.3 )

    Jumba hilo ambalo lipo Los Olivos, California likijulikana kwa jina maarufu la ‘Neverland’ likiwa ndani ya hekari 2700 na humo ndani lina zoo ya Wanyama mbalimbali kama Tembo na Twiga.

    Ron Burkle ni miongoni mwa Wamiliki wa Team ya mchezo wa Magongo unaochezwa kwenye barafu ya Pittsburgh Penguins, Michael Jackson alifariki mwaka 2009 kwenye jumba jingine alilokua anaishi Los Angeles Marekani.
    #JEWAJUA Jumba la Mfalme wa muziki wa Pop Michael Jackson ambalo alilinunua mwaka 1987 kwa USD milioni 19.5 limenunuliwa na Tajiri Ron Burkle kwa kiwango kinachotajwa kufika USD milioni 22 (USD milioni moja ni sawa na Tsh. Bilioni 2.3 ) Jumba hilo ambalo lipo Los Olivos, California likijulikana kwa jina maarufu la ‘Neverland’ likiwa ndani ya hekari 2700 na humo ndani lina zoo ya Wanyama mbalimbali kama Tembo na Twiga. Ron Burkle ni miongoni mwa Wamiliki wa Team ya mchezo wa Magongo unaochezwa kwenye barafu ya Pittsburgh Penguins, Michael Jackson alifariki mwaka 2009 kwenye jumba jingine alilokua anaishi Los Angeles Marekani.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·491 مشاهدة
  • Paka Mapepe na Safari ya Shujaa

    Kulikuwa na paka mdogo mwenye jina la Mapepe, aliyejulikana kwa tabia yake ya kupenda kujua kila kitu. Mapepe alikuwa na manyoya meupe kama barafu na macho ya rangi ya kijani kibichi yaliyong’aa usiku kama nyota. Alikuwa akiishi kwenye kijiji kidogo kilichozungukwa na msitu mnene uliotisha, msitu ambao wanyama wote waliambiwa wasikaribie.

    Siku moja, Mapepe akiwa anachunguza pembe ya shamba, alisikia kelele za ajabu kutoka msituni. Ingawa paka wengine walikimbia, Mapepe alichomoa ushujaa wake na kuingia msituni. "Nani anaweza kunizuia?" aliwaza, akinyata kwa tahadhari.

    Baada ya kutembea kwa muda, Mapepe alikuta kijana wa ndege mdogo aliyejificha kwenye shimo la mti, akilia kwa uchungu. Ndege huyo alimwambia, "Nimepotea! Wazazi wangu wako ng'ambo ya mto mkubwa, lakini sijui njia ya kufika."

    Mapepe alitabasamu, akitumia mbinu zake za mpelelezi. Alimuambia ndege, "Usijali, nitakupeleka salama." Safari yao haikuwa rahisi. Walikabiliana na nyoka mwenye sumu, lakini Mapepe, kwa kuruka kwa ustadi, aliweza kumzidi ujanja. Walivuka mto kwa kutumia shina la mti lililoelea, huku Mapepe akihakikisha ndege mdogo hayumbishwi na mawimbi.

    Hatimaye, walipofika upande wa pili wa mto, ndege mdogo alilia kwa furaha alipowaona wazazi wake wakimsubiri. Wazazi wake walimshukuru Mapepe kwa moyo wa dhati. "Wewe ni shujaa wa kweli, Mapepe," walisema.

    Mapepe alirudi kijijini akiwa amechoka lakini mwenye furaha, akiendelea na maisha yake ya kawaida. Lakini kwa kijiji kizima, Mapepe hakuwahi kuwa paka wa kawaida tena. Alikuwa shujaa wa msitu, paka mapepe ambaye alithubutu kufanikisha yasiyowezekana.

    Na kwa kila usiku, akilala, nyota zilimwangazia kama kumbukumbu ya safari yake ya kishujaa.

    Paka Mapepe na Safari ya Shujaa Kulikuwa na paka mdogo mwenye jina la Mapepe, aliyejulikana kwa tabia yake ya kupenda kujua kila kitu. Mapepe alikuwa na manyoya meupe kama barafu na macho ya rangi ya kijani kibichi yaliyong’aa usiku kama nyota. Alikuwa akiishi kwenye kijiji kidogo kilichozungukwa na msitu mnene uliotisha, msitu ambao wanyama wote waliambiwa wasikaribie. Siku moja, Mapepe akiwa anachunguza pembe ya shamba, alisikia kelele za ajabu kutoka msituni. Ingawa paka wengine walikimbia, Mapepe alichomoa ushujaa wake na kuingia msituni. "Nani anaweza kunizuia?" aliwaza, akinyata kwa tahadhari. Baada ya kutembea kwa muda, Mapepe alikuta kijana wa ndege mdogo aliyejificha kwenye shimo la mti, akilia kwa uchungu. Ndege huyo alimwambia, "Nimepotea! Wazazi wangu wako ng'ambo ya mto mkubwa, lakini sijui njia ya kufika." Mapepe alitabasamu, akitumia mbinu zake za mpelelezi. Alimuambia ndege, "Usijali, nitakupeleka salama." Safari yao haikuwa rahisi. Walikabiliana na nyoka mwenye sumu, lakini Mapepe, kwa kuruka kwa ustadi, aliweza kumzidi ujanja. Walivuka mto kwa kutumia shina la mti lililoelea, huku Mapepe akihakikisha ndege mdogo hayumbishwi na mawimbi. Hatimaye, walipofika upande wa pili wa mto, ndege mdogo alilia kwa furaha alipowaona wazazi wake wakimsubiri. Wazazi wake walimshukuru Mapepe kwa moyo wa dhati. "Wewe ni shujaa wa kweli, Mapepe," walisema. Mapepe alirudi kijijini akiwa amechoka lakini mwenye furaha, akiendelea na maisha yake ya kawaida. Lakini kwa kijiji kizima, Mapepe hakuwahi kuwa paka wa kawaida tena. Alikuwa shujaa wa msitu, paka mapepe ambaye alithubutu kufanikisha yasiyowezekana. Na kwa kila usiku, akilala, nyota zilimwangazia kama kumbukumbu ya safari yake ya kishujaa.
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·473 مشاهدة
  • 𝗠𝗔𝗧𝗨𝗞𝗜𝗢 𝗠𝗔𝗧𝗔𝗡𝗢 (5) 𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗔𝗭𝗔 𝗞𝗨𝗠𝗨𝗛𝗨𝗦𝗨 𝗦𝗨𝗣𝗘𝗥 𝗠𝗔𝗥𝗜𝗢 𝗕𝗔𝗟𝗢𝗧𝗘𝗟𝗟𝗜

    haya ni matukio matano yaliyowafanya watu wamwone Mario ni kichaa

    Kwanza, akiwa na umri wa miaka 15 alienda kufanya majaribi katika klabunya Barcelona na alifuzu majaribio, shida ilikuja kwenye malipo, Super Balotelli alikuwa akihitaji malipo makubwa yaliyowashanganza Barcelona wakamwacha aende na akarudi kwao Italia.

    Pili, Balotelli alishawahi kuchoma nyumba anayoishi kisha akaenda kumwomba rafiki ya Richard waishi wote kwake, lakini Richard aligoma. Hata ungekuwa wewe ungekubali?

    Tatu, Wakati fulani Jose Morinho alikuwa kuwa akimsubiri Balotelli ili azungumze naye alipompigia simu Balotelli akamjibu nipo kuangalia mashindano ya FORMULA ONE ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka lakini wewe kila siku naiona sura yako.

    Nne, wakati akiwa anacheza Inter Milan wakiwa mazoezi alipewa jezi ya Ac Milan alivaa na akaingia mazoezi, wakati mazoezi yanaendelea alimfanyia rafu mchezaji mwenzake, kocha akamwambia aondoke lakini akagoma na mwisho mazoezi yenyewe yakaahirishwa.

    tano, Ni story za Manchini na Balotelli, kama kuna kitu watengeneza filamu wanafeli basi ni kutengeneza filamu ya Balotelli na mzee wake Manchini. Manchini alipofika Manchester City alimkataa kabisa Balotelli kwasababu ya tabia za ujuaji pia alikuwa hachukulii serious mechi za kirafiki.
    𝗠𝗔𝗧𝗨𝗞𝗜𝗢 𝗠𝗔𝗧𝗔𝗡𝗢 (5) 𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗔𝗭𝗔 𝗞𝗨𝗠𝗨𝗛𝗨𝗦𝗨 𝗦𝗨𝗣𝗘𝗥 𝗠𝗔𝗥𝗜𝗢 𝗕𝗔𝗟𝗢𝗧𝗘𝗟𝗟𝗜 haya ni matukio matano yaliyowafanya watu wamwone Mario ni kichaa Kwanza, akiwa na umri wa miaka 15 alienda kufanya majaribi katika klabunya Barcelona na alifuzu majaribio, shida ilikuja kwenye malipo, Super Balotelli alikuwa akihitaji malipo makubwa yaliyowashanganza Barcelona wakamwacha aende na akarudi kwao Italia. Pili, Balotelli alishawahi kuchoma nyumba anayoishi kisha akaenda kumwomba rafiki ya Richard waishi wote kwake, lakini Richard aligoma. Hata ungekuwa wewe ungekubali? Tatu, Wakati fulani Jose Morinho alikuwa kuwa akimsubiri Balotelli ili azungumze naye alipompigia simu Balotelli akamjibu nipo kuangalia mashindano ya FORMULA ONE ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka lakini wewe kila siku naiona sura yako. Nne, wakati akiwa anacheza Inter Milan wakiwa mazoezi alipewa jezi ya Ac Milan alivaa na akaingia mazoezi, wakati mazoezi yanaendelea alimfanyia rafu mchezaji mwenzake, kocha akamwambia aondoke lakini akagoma na mwisho mazoezi yenyewe yakaahirishwa. tano, Ni story za Manchini na Balotelli, kama kuna kitu watengeneza filamu wanafeli basi ni kutengeneza filamu ya Balotelli na mzee wake Manchini. Manchini alipofika Manchester City alimkataa kabisa Balotelli kwasababu ya tabia za ujuaji pia alikuwa hachukulii serious mechi za kirafiki.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·639 مشاهدة
  • Maana au ujumbe wa tattoo umewekwa kwa kuzingatia sehemu au mahali iliyochorwa hiyo tattoo, rangi iliyotumika kuichora hiyo tattoo, na mtindo uliotumika kuchora kwa tattoo husika
    Kabla hatujachambua orodha yetu ya tattoo maarafu na maana zake, unahitaji kujua mambo mengine ambayo ni muhimu
    1. Sehemu ambayo tattoo imechorwa au imekaa kwenye mwili ina maana kubwa, hasa kama ikiwa imewekwa au kuchorwa mahali fulani kwa ishara kama vile juu ya moyo, nyuma ya sikio au katika sehemu ya siri ya mwili.
    2. Rangi iliyotumika kuchora hiyo tattoo - rangi ya tattoo inaweza kubadilisha kabisa maana. Ua rose nyekundu inaashiria upendo wa kimapenzi na shauku, wakati Ua rose la bluu mara nyingi hutumika kuashiria upendo usioweza kupatikana.
    3. Mtindo uliotumika kuchora tattoo ina maana zaidi. Mfano tattoo ya simba dume kuwakilisha nguvu....au inaweza tu kuwa heshima.

    Huwezi kutambua maana halisi ya tattoo kwa kuiangalia pekee. Ni vyema ukauliza maana kwa mtu mwenye tattoo hiyo ilikupata majibu sahihi na maana sahihi.
    Ikiwa watajibu vyema, endelea na uulize kuhusu maana ya tattoo walizochora. Ikiwa hawaonekani na nia ya kuzungumza juu ya tattoo zao, usilazimishe zaidi.
    Tattoo zinaweza kushikilia maana na kumbukumbu za kina sana, na hata machungu ambayo watu wanapendelea kuweka faragha au siri.
    Maana au ujumbe wa tattoo umewekwa kwa kuzingatia sehemu au mahali iliyochorwa hiyo tattoo, rangi iliyotumika kuichora hiyo tattoo, na mtindo uliotumika kuchora kwa tattoo husika Kabla hatujachambua orodha yetu ya tattoo maarafu na maana zake, unahitaji kujua mambo mengine ambayo ni muhimu 1. Sehemu ambayo tattoo imechorwa au imekaa kwenye mwili ina maana kubwa, hasa kama ikiwa imewekwa au kuchorwa mahali fulani kwa ishara kama vile juu ya moyo, nyuma ya sikio au katika sehemu ya siri ya mwili. 2. Rangi iliyotumika kuchora hiyo tattoo - rangi ya tattoo inaweza kubadilisha kabisa maana. Ua rose nyekundu inaashiria upendo wa kimapenzi na shauku, wakati Ua rose la bluu mara nyingi hutumika kuashiria upendo usioweza kupatikana. 3. Mtindo uliotumika kuchora tattoo ina maana zaidi. Mfano tattoo ya simba dume kuwakilisha nguvu....au inaweza tu kuwa heshima. Huwezi kutambua maana halisi ya tattoo kwa kuiangalia pekee. Ni vyema ukauliza maana kwa mtu mwenye tattoo hiyo ilikupata majibu sahihi na maana sahihi. Ikiwa watajibu vyema, endelea na uulize kuhusu maana ya tattoo walizochora. Ikiwa hawaonekani na nia ya kuzungumza juu ya tattoo zao, usilazimishe zaidi. Tattoo zinaweza kushikilia maana na kumbukumbu za kina sana, na hata machungu ambayo watu wanapendelea kuweka faragha au siri.
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·489 مشاهدة
  • :dak 71'
    Kibu Denis anacheza rafu kwa mchezaji wa Congo DR
    #paulswai
    ⏳:dak 71' Kibu Denis anacheza rafu kwa mchezaji wa Congo DR #paulswai
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·149 مشاهدة
  • :dak 20'
    Henock Inonga anamchezea rafu mchezaji wa Tanzania
    ⏳:dak 20' Henock Inonga anamchezea rafu mchezaji wa Tanzania
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·143 مشاهدة
  • My business site: https://www.manarafurniture.com/
    another one: https://www.hanako.co.id/
    My business site: https://www.manarafurniture.com/ another one: https://www.hanako.co.id/
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·261 مشاهدة
  • Beki wa Al ahali Tripoli amuomba radhi DEBORA FERNANDES .

    Beki wa klabu ya Al AHLI TRIPOLI Thierry Manzi Raia wa Rwanda amemuomba radhi kiungo wa Simba Debora Fernandes

    Na hii ni baada ya yeye kumchezea rafu mbaya kwenye mchezo wa wikiend iliyopita.
    #paulswai
    Beki wa Al ahali Tripoli amuomba radhi DEBORA FERNANDES . Beki wa klabu ya Al AHLI TRIPOLI Thierry Manzi Raia wa Rwanda amemuomba radhi kiungo wa Simba Debora Fernandes Na hii ni baada ya yeye kumchezea rafu mbaya kwenye mchezo wa wikiend iliyopita. #paulswai
    Like
    3
    · 1 التعليقات ·0 المشاركات ·246 مشاهدة
  • Hello social Pop
    Napenda kuwatangazia kuhus pi network (sarafu za kimtandao) ambayo itaanza kutumika rasmi tarehe 31/12/2024 .
    Napenda kuwaambia kujiunga ni bure kabsa.
    Your most welcome
    Hello social Pop 👋 Napenda kuwatangazia kuhus pi network (sarafu za kimtandao) ambayo itaanza kutumika rasmi tarehe 31/12/2024 . Napenda kuwaambia kujiunga ni bure kabsa. Your most welcome 😊
    Love
    Like
    3
    · 3 التعليقات ·0 المشاركات ·262 مشاهدة
  • 52' Simba Sc 2-1 Al Adalah

    9' Steven Mukwala ( Fabrice Ngoma)
    32' Joshua Mutale

    Al Adalah wamepata bao kwa mkwaju wa penati baada ya Golikipa wa Simba Ally Salim kucheza rafu
    52' Simba Sc 🇹🇿 2-1 Al Adalah 🇸🇦 ⚽ 9' Steven Mukwala (🎯 Fabrice Ngoma) ⚽ 32' Joshua Mutale Al Adalah wamepata bao kwa mkwaju wa penati baada ya Golikipa wa Simba Ally Salim kucheza rafu
    Like
    2
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·273 مشاهدة
  • Na haya ni majukumu yakuteleza na hii rap...
    Ulie ndotoni ucjihukum you have to wake up...
    Huku majuu maisha magumu never give up...
    Tungo tata sio ngumu masela mmeketch it up...
    Life ni tough na hakuna was kupiga taff...
    kam nyambafu tafsiri zaid ya mkandala lufufu... mnyonge MPE dafu mbabe karate awe commando hio kwangu hafui dafu...
    hii ni tungo tata tafsiri hata ule nyamafu...
    utapiga kwata hata ukiwa unacheza rafu...
    nimemaliza kunielewa sio lazima mpk ule ndaf...
    Na haya ni majukumu yakuteleza na hii rap... Ulie ndotoni ucjihukum you have to wake up... Huku majuu maisha magumu never give up... Tungo tata sio ngumu masela mmeketch it up... Life ni tough na hakuna was kupiga taff... kam nyambafu tafsiri zaid ya mkandala lufufu... mnyonge MPE dafu mbabe karate awe commando hio kwangu hafui dafu... hii ni tungo tata tafsiri hata ule nyamafu... utapiga kwata hata ukiwa unacheza rafu... nimemaliza kunielewa sio lazima mpk ule ndaf...
    Like
    3
    · 1 التعليقات ·0 المشاركات ·475 مشاهدة
  • Nkaamua kuokoka kla day church..
    Nkapata rafk mtoto wa mchungaji..
    Aisee alinpenda pia alinfariji..
    Alkuwa mzur mtoto amenyooka sometimes namtamani..
    Ira dah nimeokoka alpenda matan achok kuniita my..
    Nkakaza kuulza achok kun sabayi..
    Ilkuwa jumapil baada ya ibada..
    Akaomba nimtoe lunch nkaduwaa mbaba..
    Mfukon ielewek nmebak na vchenchi..
    Nka mwambia ukwel akacheka kiucheshi..
    Alniaga kama utan ksha akasepa..
    Roho ikaniuma nkataman ata nwe ata bakressa..
    Juma3 npo geto mara naskia hodi..
    Karbu kufungua ni mtoto wa mchungaji..
    Bwana asifiwe akajbu amina..
    Nkamwabia karbu fasta geto akazama..
    Akawa ameinama anadai amechoka..
    Na pia anamawazo arafu kichwa knamuuma..
    Nkampa panado nkawasha na feni..
    Akasema anashukulu huku akivua eleni..
    Tulpiga stor nying alkuja na vileo tukamwagilia moyo mtoto kazdiwa na ulevi..
    Akaanza kunitomasa nyie shetani mshenzi..
    Mtoto wa mchungaji kama sio yeye..
    Na macho analembua ka kuku kaona mwewe..
    Kifuani akasogea ikabidi nijiongeze..
    Mm sio Yusufu mgalatia nichakaze..
    Nkaamua kuokoka kla day church.. Nkapata rafk mtoto wa mchungaji.. Aisee alinpenda pia alinfariji.. Alkuwa mzur mtoto amenyooka sometimes namtamani.. Ira dah nimeokoka alpenda matan achok kuniita my.. Nkakaza kuulza achok kun sabayi.. Ilkuwa jumapil baada ya ibada.. Akaomba nimtoe lunch nkaduwaa mbaba.. Mfukon ielewek nmebak na vchenchi.. Nka mwambia ukwel akacheka kiucheshi.. Alniaga kama utan ksha akasepa.. Roho ikaniuma nkataman ata nwe ata bakressa.. Juma3 npo geto mara naskia hodi.. Karbu kufungua ni mtoto wa mchungaji.. Bwana asifiwe akajbu amina.. Nkamwabia karbu fasta geto akazama.. Akawa ameinama anadai amechoka.. Na pia anamawazo arafu kichwa knamuuma.. Nkampa panado nkawasha na feni.. Akasema anashukulu huku akivua eleni.. Tulpiga stor nying alkuja na vileo tukamwagilia moyo mtoto kazdiwa na ulevi.. Akaanza kunitomasa nyie shetani mshenzi.. Mtoto wa mchungaji kama sio yeye.. Na macho analembua ka kuku kaona mwewe.. Kifuani akasogea ikabidi nijiongeze.. Mm sio Yusufu mgalatia nichakaze..
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·504 مشاهدة
الصفحات المعززة