• RASMI

    Fainali ya Saudi Arabia super cup itakuwa ni kati ya Al Nasr dhidi ya Al Ahli.

    Al Nasr alifanikiwa kumuondoa Al ittihad kwenye mchezo wa nusu fainali huku Al Ahli akimuondoa Al Qadsiah hii Leo.

    #SportsElite
    RASMI ✍️ Fainali ya Saudi Arabia super cup itakuwa ni kati ya Al Nasr dhidi ya Al Ahli. Al Nasr alifanikiwa kumuondoa Al ittihad kwenye mchezo wa nusu fainali huku Al Ahli akimuondoa Al Qadsiah hii Leo. #SportsElite
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·261 Views
  • Leon Bailey anaondoka Aston Villa miaka 28 na anaweza kujiunga na AS Roma au kwenda kuchukua pesa za Saudi Arabia.

    Mpaka sasa amekuwa na career nzuri japo ingeweza kuwa bora zaidi sababu uwezo anao lakini ni moja ya wachezaji muendelezo ni changamoto kwake kwa taifa alillotaka anabaki kuwa mchezaji wenye kipaji zaidi natumai Mason Greenwood akijunga rasmi na Jamaica watakuwa na taifa nzuri na shindani.

    #SportsElite
    🚨🚨Leon Bailey anaondoka Aston Villa miaka 28 na anaweza kujiunga na AS Roma au kwenda kuchukua pesa za Saudi Arabia. Mpaka sasa amekuwa na career nzuri japo ingeweza kuwa bora zaidi sababu uwezo anao lakini ni moja ya wachezaji muendelezo ni changamoto kwake kwa taifa alillotaka anabaki kuwa mchezaji wenye kipaji zaidi natumai Mason Greenwood akijunga rasmi na Jamaica watakuwa na taifa nzuri na shindani. #SportsElite
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·436 Views
  • Klabu ya NEOM ya Saudi Arabia inatarajia kumsajili aliyekuwa mchezaji wa Marseille , Pape Gueye, kulingana na taarifa za RMC Sport. Kiungo huyo wa Villarreal tayari amewasiliana kwa mara ya kwanza na viongozi wa klabu hiyo mpya iliyopanda daraja kwenye Saudi Pro League.

    #SportsElite
    💦Klabu ya NEOM ya Saudi Arabia 🇸🇦 inatarajia kumsajili aliyekuwa mchezaji wa Marseille 🇫🇷, Pape Gueye, kulingana na taarifa za RMC Sport. Kiungo huyo wa Villarreal 🇪🇸 tayari amewasiliana kwa mara ya kwanza na viongozi wa klabu hiyo mpya iliyopanda daraja kwenye Saudi Pro League. #SportsElite
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·293 Views
  • Barcelona imeumizwa na uhamisho wa Benjamin Sesko kwenda Manchester United.

    Kwani walitarajia kumuuza Robert Lewandowski kwenda Saudi Arabia ndio wamesajili Benjamin Sesko amesema Deco.

    (Source: Sport)

    #SportsElite
    🚨 Barcelona imeumizwa na uhamisho wa Benjamin Sesko kwenda Manchester United. Kwani walitarajia kumuuza Robert Lewandowski kwenda Saudi Arabia ndio wamesajili Benjamin Sesko amesema Deco. (Source: Sport) #SportsElite
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·209 Views
  • Robert Lewandowski ameifungulia milango Barcelona baada ya kupokea ofa kutoka Saudi Arabia yenye thamani ya €100M.

    (Source: El Nacional)

    #SportsElite
    🚨 Robert Lewandowski ameifungulia milango Barcelona baada ya kupokea ofa kutoka Saudi Arabia yenye thamani ya €100M. (Source: El Nacional) #SportsElite
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·199 Views
  • Ferran Torres ameikataa ofa kutoka Saudi Arabia.

    Anahitaji kusalia Barcelona.

    (Source: x/santiovalle)

    #SportsElite
    🚨 Ferran Torres ameikataa ofa kutoka Saudi Arabia. Anahitaji kusalia Barcelona. (Source: x/santiovalle) #SportsElite
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·112 Views
  • AC Milan yapigania kumsajili Darwin Núñez!

    Klabu hiyo ya Italia iko kwenye mazungumzo na mshambuliaji wa Liverpool kuhusu uhamisho kwenda San Siro , lakini inakumbana na ushindani mkali kutoka Al-Hilal ya Saudi Arabia ambao tayari wamewasilisha ofa rasmi .

    Liverpool wanahitaji karibu £70 milioni , huku Núñez akionekana kupendelea kubaki barani Ulaya .

    #ACMilan #Liverpool #DarwinNúñez #TransferNews #AlHilal #SanSiro

    #SportsElite
    🚨 AC Milan yapigania kumsajili Darwin Núñez! Klabu hiyo ya Italia iko kwenye mazungumzo na mshambuliaji wa Liverpool kuhusu uhamisho kwenda San Siro 🏟️, lakini inakumbana na ushindani mkali kutoka Al-Hilal ya Saudi Arabia 🇸🇦 ambao tayari wamewasilisha ofa rasmi 💰. Liverpool wanahitaji karibu £70 milioni 💸, huku Núñez akionekana kupendelea kubaki barani Ulaya 🌍. #ACMilan #Liverpool #DarwinNúñez #TransferNews #AlHilal #SanSiro #SportsElite
    Like
    Love
    2
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·693 Views
  • | BREAKING: Saudi Arabia iko tayari kutoa ofa ya €350M kwa Real Madrid ili kumsajili Vinicius Jr.

    Source Ben Jacobs

    #SportsElite
    🚨| BREAKING: Saudi Arabia iko tayari kutoa ofa ya €350M kwa Real Madrid ili kumsajili Vinicius Jr.🇸🇦 💰 Source Ben Jacobs #SportsElite
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·291 Views
  • ⚪️ RASMI: Lucas Vázquez Aondoka Real Madrid!

    Baada ya miaka mingi ya kujitoa kwa moyo wote, Lucas Vázquez hatakuwa mchezaji wa Real Madrid tena. Mkataba wake umeisha na sasa yupo huru (free agent) kujiunga na timu yoyote.

    Akiwa amehudumu kwa zaidi ya mechi 400, Lucas ametwaa mataji 23 yakiwemo: Champions League – 5
    La Liga – 4
    Supercopa, UEFA Super Cup na Club World Cup...

    Inaripotiwa kuwa Fenerbahçe ya Uturuki, klabu za MLS na Saudi Arabia tayari zimeanza mawasiliano naye.

    #SportsElite
    🇪🇸⚪️ RASMI: Lucas Vázquez Aondoka Real Madrid! Baada ya miaka mingi ya kujitoa kwa moyo wote, Lucas Vázquez hatakuwa mchezaji wa Real Madrid tena. Mkataba wake umeisha na sasa yupo huru (free agent) kujiunga na timu yoyote. 🗓️ Akiwa amehudumu kwa zaidi ya mechi 400, Lucas ametwaa mataji 23 yakiwemo: 🏆 Champions League – 5 🇪🇸 La Liga – 4 🎖️ Supercopa, UEFA Super Cup na Club World Cup... 🔜 Inaripotiwa kuwa Fenerbahçe ya Uturuki, klabu za MLS na Saudi Arabia tayari zimeanza mawasiliano naye. #SportsElite
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·440 Views
  • “Siku yangu ya kwanza nilipoenda kufanya majaribio nilichekwa sana, nilivalia suruali ndefu na viatu vyangu vilichanika sana, watu waliniona kama kituko, sikuonekana kama mcheza soka” - Sadio Mane, Mchezaji wa kimataifa wa Senegal na klabu ya Al Nasr ya Saudi Arabia .

    Rekodi yake.

    - Mechi : 686.
    - Mabao : 277.
    - "Assists" : 136.

    “Siku yangu ya kwanza nilipoenda kufanya majaribio nilichekwa sana, nilivalia suruali ndefu na viatu vyangu vilichanika sana, watu waliniona kama kituko, sikuonekana kama mcheza soka” - Sadio Mane, Mchezaji wa kimataifa wa Senegal 🇸🇳 na klabu ya Al Nasr ya Saudi Arabia 🇸🇦. Rekodi yake. - Mechi : 686. - Mabao : 277. - "Assists" : 136.
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·226 Views
  • Kikao cha mazungumzo ya kumaliza mzozo wa Nchi ya Ukraine na Nchi ya Urusi kinaendelea Nchini Saudi Arabia 🇸 ambapo Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Urusi chini ya Sergie Lavrov na Marekani chini ya Marco Rubio. Hata hivyo, Ukraine na Umoja wa Ulaya (EU) hawajashirikishwa huku Ukraine upande wake inapinga kikao hicho kuwa makubaliano yoyote haitayatambua.

    Katika kusisitiza hilo Ukraine imeendelea kusisitiza kwamba itaendelea kupigana vita kwa kutegemea Ulaya sio Marekani kama mwanzo huku Rais wa Nchi hiyo Volodmiry Zelensky akisema Ukraine ni Taifa huru, hivyo haliwezi kuamuliwa mambo yake na Marekani, itautetea uhuru wake hadi tone la mwisho. Marekani imejibu kwa kusema inaitaka Ukraine irejeshe haraka deni lote la usaidizi wa vita lililotolewa na Marekani tangu Februari 2022 Oparesheni ya Urusi ilipoanza.

    Kikao hiki kinachoendelea ni hatua muhimu kuelekea mkutano wa Rais Putin na Rais Trump uliopangwa mwezi Mei katika sherehe za Mashujaa wa Urusi utakaofanyika Jijini Moscow, Urusi ambapo pia mkutano huo utamwalika Rais wa China Xi Ping kama Mgeni mwalikwa muhimu.

    Kikao cha mazungumzo ya kumaliza mzozo wa Nchi ya Ukraine 🇺🇦 na Nchi ya Urusi 🇷🇺 kinaendelea Nchini Saudi Arabia 🇸 ambapo Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Urusi chini ya Sergie Lavrov na Marekani 🇺🇸 chini ya Marco Rubio. Hata hivyo, Ukraine na Umoja wa Ulaya (EU) hawajashirikishwa huku Ukraine upande wake inapinga kikao hicho kuwa makubaliano yoyote haitayatambua. Katika kusisitiza hilo Ukraine imeendelea kusisitiza kwamba itaendelea kupigana vita kwa kutegemea Ulaya sio Marekani kama mwanzo huku Rais wa Nchi hiyo Volodmiry Zelensky akisema Ukraine ni Taifa huru, hivyo haliwezi kuamuliwa mambo yake na Marekani, itautetea uhuru wake hadi tone la mwisho. Marekani imejibu kwa kusema inaitaka Ukraine irejeshe haraka deni lote la usaidizi wa vita lililotolewa na Marekani tangu Februari 2022 Oparesheni ya Urusi ilipoanza. Kikao hiki kinachoendelea ni hatua muhimu kuelekea mkutano wa Rais Putin na Rais Trump uliopangwa mwezi Mei katika sherehe za Mashujaa wa Urusi utakaofanyika Jijini Moscow, Urusi ambapo pia mkutano huo utamwalika Rais wa China 🇨🇳 Xi Ping kama Mgeni mwalikwa muhimu.
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·856 Views
  • Rais wa Marekani , Donald Trump, ameshitua Watu Duniani baada ya kutangaza nia yake ya kuchukua udhibiti wa Ukanda wa Gaza ulioharibiwa na vita na kuufanyia maendeleo ya kiuchumi baada ya Wapalestina kuhamishiwa maeneo mengine. Hatua hiyo inaweza kubadili sera za Marekani za miongo kadhaa kuhusu mgogoro wa Israel na Palestina.

    Katika mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, Rais huyo alitangaza mpango huu bila kutoa maelezo ya kina.

    Kabla ya tangazo hilo, Trump alipendekeza kuwa zaidi ya Wapalestina milioni mbili (2) wa Gaza wahamishiwe Nchi jirani. Alikitaja kisiwa hicho kidogo, ambacho kwa sasa kina makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas, kuwa “eneo la kubomolewa.”

    Pendekezo hili linakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Washirika na Wapinzani wa Marekani. Pia linaibua maswali kuhusu ikiwa Saudi Arabia itashiriki katika juhudi mpya za Marekani za kuleta uhusiano wa kawaida kati ya Israel na mataifa ya Kiarabu.

    - Hatua ya Marekani kuchukua ushawishi wa moja kwa moja Gaza itapingana na msimamo wa muda mrefu wa Washington na Jumuiya ya kimataifa, ambao unaona Gaza kama sehemu ya Taifa la baadaye la Palestina pamoja na Ukingo wa Magharibi.

    "Marekani itachukua Ukanda wa Gaza, na tutafanya nao kazi nzuri sana. Tutakuwa na umiliki wake na kuhakikisha tunasafisha mabomu na silaha zote hatari zilizobaki."

    "Tutaendeleza Gaza, kuunda maelfu ya ajira, na kuifanya iwe sehemu ambayo Mashariki ya Kati yote itajivunia. Ninaona umiliki wa muda mrefu na ninaamini italeta utulivu mkubwa katika eneo hilo." amesema Donald Trump.

    “nyumbani kwa watu wa dunia.” Aliielezea Gaza kama eneo lenye uwezo wa kuwa “Riviera ya Mashariki ya Kati.” - Donald Trump baada ya kuulizwa nani ataishi Gaza baada ya kuitengeneza

    Trump hakujibu moja kwa moja kuhusu mamlaka au mchakato wa kuchukua eneo hilo la Gaza baada ya kuulizwa Marekani ina mamlaka gani ya kuichukua Gaza, ambalo lina urefu wa maili 25 (km 45) na upana wa hadi maili 6 (km 10) na historia ya vurugu. Serikali za awali za Marekani, ikiwemo ile ya Trump katika muhula wake wa kwanza, ziliepuka kutuma Wanajeshi Gaza.

    Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump, ameshitua Watu Duniani baada ya kutangaza nia yake ya kuchukua udhibiti wa Ukanda wa Gaza ulioharibiwa na vita na kuufanyia maendeleo ya kiuchumi baada ya Wapalestina kuhamishiwa maeneo mengine. Hatua hiyo inaweza kubadili sera za Marekani za miongo kadhaa kuhusu mgogoro wa Israel na Palestina. Katika mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, Rais huyo alitangaza mpango huu bila kutoa maelezo ya kina. Kabla ya tangazo hilo, Trump alipendekeza kuwa zaidi ya Wapalestina milioni mbili (2) wa Gaza wahamishiwe Nchi jirani. Alikitaja kisiwa hicho kidogo, ambacho kwa sasa kina makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas, kuwa “eneo la kubomolewa.” Pendekezo hili linakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Washirika na Wapinzani wa Marekani. Pia linaibua maswali kuhusu ikiwa Saudi Arabia itashiriki katika juhudi mpya za Marekani za kuleta uhusiano wa kawaida kati ya Israel na mataifa ya Kiarabu. - Hatua ya Marekani kuchukua ushawishi wa moja kwa moja Gaza itapingana na msimamo wa muda mrefu wa Washington na Jumuiya ya kimataifa, ambao unaona Gaza kama sehemu ya Taifa la baadaye la Palestina pamoja na Ukingo wa Magharibi. "Marekani itachukua Ukanda wa Gaza, na tutafanya nao kazi nzuri sana. Tutakuwa na umiliki wake na kuhakikisha tunasafisha mabomu na silaha zote hatari zilizobaki." "Tutaendeleza Gaza, kuunda maelfu ya ajira, na kuifanya iwe sehemu ambayo Mashariki ya Kati yote itajivunia. Ninaona umiliki wa muda mrefu na ninaamini italeta utulivu mkubwa katika eneo hilo." amesema Donald Trump. “nyumbani kwa watu wa dunia.” Aliielezea Gaza kama eneo lenye uwezo wa kuwa “Riviera ya Mashariki ya Kati.” - Donald Trump baada ya kuulizwa nani ataishi Gaza baada ya kuitengeneza Trump hakujibu moja kwa moja kuhusu mamlaka au mchakato wa kuchukua eneo hilo la Gaza baada ya kuulizwa Marekani ina mamlaka gani ya kuichukua Gaza, ambalo lina urefu wa maili 25 (km 45) na upana wa hadi maili 6 (km 10) na historia ya vurugu. Serikali za awali za Marekani, ikiwemo ile ya Trump katika muhula wake wa kwanza, ziliepuka kutuma Wanajeshi Gaza.
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·930 Views
  • *VATICAN CITY......
    Nchi? Mji? Serikali au Kampuni?*

    Nadhani moja kati ya maeneo ambayo yamekuwa tata zaidi kuyaelewa basi ni mji wa Vatican… tukiachilia mbali kuhusu utata/ugumu wa kuelewa mfumo wake wa uendeshaji na historia yake lakini swali jepesi zaidi ambalo kila mtu huwa anahisi analifahamu jawabu lake ni kuhusu utambulisho wa Vatican.!! Ni swali jepesi ambalo karibia kila mtu anadhani ana jawabu sahihi lakini uhalisia ni kwamba asilimia kubwa ya watu wana jawabu lisilo sahihi… kila mtu atakueleza kwamba Vatican ni nchi inayojitegemea lakini hii ni robo tu au thelethi ya jawabu…

    Leo nami niandike kidogo kuhusu eneo hili… na kwenye andishi hili fupi nitaeleza utambulisho wa Vatican ukoje kwa usahihi wake kabisa!

    *Muhimu:* andishi hili halilengi kukosoa au kupinga imani ya mtu yeyote. Tahadhali zote zinazingatiwa ili kulinda heshima ya imani ya kila mtu.

    Tuendelee…

    Vatican City, ndio makao makuu ya Kanisa Katoliki na nyumba ya maisha ya Papa, kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki.
    Vatican ndio nchi ndogo zaidi duniani kiasi kwamba unaweza kuizunguka yote kwa mzingo (circumference) kwa muda wa dakika arobaini tu kwa kutembea kwa miguu.

    Ni ajabu sana kwa namna gani nchi ndogo kiasi hiki imetokea na je ni nchi kama nchi nyingine???

    Jibu la swali hili ni refu sana kiaisi kwamba unaweza hata kusoma darasani kwa mwaka mzima lakini nitajaribu kuweka katika maneno machache sana ya kueleweka kwa wepesi…

    Miaka ya kale sana Papa wa Kanisa Katoliki alikuwa ni mtawala wa nchi ambayo ilikuwa inajiita *Himaya ya Papa (Papal State)* ambayo inarandana kabisa na eneo la sasa la nchi nzima ya Italia. Hii ilikuwa takribani miaka ya 754 mpaka miaka ya 1870.
    Ni katika kipindi hiki ambacho Papa aliteua eneo ndani ya nchi yake Papal State ambalo likajengwa *St. Peters Basilica*, kanisa kubwa zaidi duniani na lenye nakshi adhimu zaidi. Eneo hili ambalo St. Peters Basilica ilijengwa ni eneo fulani hivi la muinuko ambako hapo hapo pia yalijengwa makazi ya Papa kuishi.

    Ikumbukwe kwamba katika kipindi hiki hiki cha uwepo wa himaya ya Papal State pia ilikuwa inapakana na Ufalme wa Italy (Kingdom of Italy) japo kila moja ilikuwa inajitegemea.

    Japokuwa himaya hizi mbili zilikuwa jirani lakini kulikuwa na uhasama fulani kati yao. Hii ilifanya Papa kujenga ukuta mkubwa kuzunguka makazi yake ya kuishi na kanisa la St. Peters Basilica.

    Kadiri miaka ilivyozidi kwenda uhasama kati ya Italy Kingdom na Papal State ulipanuka zaidi na ilifikia hatua Kingdom of Italy wakafanya uamuzi wa kuiteka Papal State na kuifanya makao makuu ya nchi yake (Rome ya sasa).

    Wakati na baada ya uvamizi huu wa Kingdom of Italy kuteka Papal State, Papa mwenyewe alikuwa amejificha ndani ya makazi yake yaliyozungushiwa ukuta ambao nimeeleza awali.
    Ikumbukwe kwamba hata kipindi hiki Kanisa Katoliki tayari lilikuwa na ushawishi mkubwa duniani kwa hiyo Kingdom of Italy walihofia kuingiza majeshi kwa nguvu ndani ya makazi ya Papa na kumkamata kuogopa umaarufu wao kimataifa kudondoka.

    Kwa hiyo majeshi ya Kingdom of Italy yalibakia nje mwa kuta za Vatican kwa miaka mingi sana wakiamini kwamba iko siku Papa atakata tamaa na kujisalimisha.
    Lakini hii haikufua dafu kwani miongo ilipita na Papa hakujisalimisha kwa kutoka nje ya kuta za Vatican. Takribani Mapapa watano kwa muda wa karibia miaka sitini waliishi ndani ya kuta za Vatican katika hali hii. Mapapa hao kwa majina yao walikuwa ni Papa Pius IX, Papa Leo XIII, Papa Pius X, Papa Benedict XV na Papa Pius XI.

    Hali hii ilisababisha Mapapa kutotambua Kingdom of Italy na pia kulalamika mara kwa mara kwa jamii ya kimataifa kwamba wanaishi kama wafungwa ndani ya kuta za Vatican kutokana na ukandamizaji wa Kingdom of Italy na hofu waliyonayo kutoka nje ya kuta za Vatican.

    Hii inatufikisha mpaka miaka ya 1920s wakati wa utawala wa Benito Mussolini akiwa Waziri Mkuu wa Italy.
    Mussolini alichoshwa na malalamiko haya ya Papa na majibizano ya kila mara huku Papa bado akishikilia msimamo wa kutoitambua Italy

    Mussolini mwanasiasa mahiri kama ajulikanavyo akaona fursa hapa ya kuandika jina lake kwenye vitabu vya historia.
    Akapendekeza makubaliano maalumu kwa Papa. Kwamba atafanya yafuatayo;

    1. Italy itatoa ardhi ya Vatican kwa Papa na iwe himaya/nchi iliyo chini ya utawala wa Papa.

    2. Italy itatoa fedha kama fidia kwa Papa kutokana na manyanyaso ya miaka yote.

    Mussolini alihitaji Papa kufanya yafuatayo;

    1. Papa atambue Italy kuwa ni nchi.

    2. Papa asijihusishe wala kutoa maoni yoyote kuhusu masuala ya kisiasa na vita.

    Papa na Mussolini wakafikia makubaliano na mikataba ikasainiwa na hapa ndipo taifa dogo zaidi duniani likazaliwa, Vatican.

    Vatican ikaanza kujiendesha kama taifa linalojitegemea kwa kuwa na sarafu yake, serikali yake, Polisi wake, jela yake (ndio kuna jela Vatican), Posta yake, Plate number zake, Passport zake na kadhalika na kadhalika.

    Vatican si kama nchi nyingine duniani kwa hiyo usidhani kwamba tayari umeielewa Vatican, hicho nilichoeleza ni theluthi tu mkanganyiko wa kuielewa Vatican kama nchi… kunywa tena glass ya maji and relax!! Nitaeleza tena kidogo…

    Ili kuielewa Vatican walau kiduchu kuna watu wawili tunapaswa kuwafahamu;

    1. Papa

    2. Mfalme wa Vatican

    Na pia kuna vitu viwili vya kuvielewa;

    1. The Holy See

    2. Vatican City

    Tuanze kimoja kimoja…

    *1. Papa*
    Hii sihitaji kueleza sana karibia wote tunafahamu. Lakini kwa msingi wa awali kabisa, Papa ni askofu wa Wakatoliki wote waliopo Rome/Vatican lakini kwa kuwa yeye pia ndiye kiongozi wa Wakatoliki wote duniani ndio sababu ya Uaskofu wake kuwa Papa.

    *2. The Holy See*
    Kabla sijaeleza chochote kuhusu Mfalme wa Vatican kwanza nieleze kuhusu The Holy See. Hili ni moja ya mambo magumu zaidi kuyaelewa kuhusu Vatican. Nitaeleza kwa lugha nyepesi na uchache ili tusipasue vichwa kwa mikanganyiko.

    Kwa tafsiri nyepesi Holy See ni 'Throne' ya Papa (nakosa neno zuri la kiswahili, sipendezwi sana na tafsiri ya 'Kiti cha Enzi').

    Ni kwamba, maaskofu wote ndani ya kanisa Katoliki wanakuwa na 'throne' lakini kwa kuwa 'throne' ya Papa ni maalumu (kiongozi wa Wakatoliki wote duniani) kwa hiyo throne yake inakuwa muhimu zaidi na inaitwa 'The Holy See'.
    Mapapa wanabadilika lakini The Holy See iko na itaendelea kuwepo siku zote.

    Yaani kwa mfano Papa anapofariki au kustaafu kama tulivyoona mwaka juzi, Makadinali wanapokusanyika Vatican kwa uhalisia wanaenda kumchagua Kadinali mwenzao ambaye atakalia 'throne' ya 'Holy See'.

    Kwa 'angle' nyingine tunaweza kusema kwamba 'The Holy See' ndiyo sheria na mamlaka yote inayofanya kanisa Katoliki kuwa namna lilivyo. Pia sheria zote za kanisa Katoliki na mfumo wake unatengenezwa na The Holy See (sio Papa).

    Pia tunaweza kusema kwamba Benito Mussolini alipofanya makubaliano na Vatican aliingia mkataba ule na 'The Holy See'.

    Pia unaweza usiamini lakini katika nyanja za sheria za kimataifa 'The Holy See' inatambulika kama mtu/kampuni halisi ambaye amesajiliwa kisheria.

    Labda nitumie lugha nyepesi zaidi ya mfano… ukitaka kuelewa The Holy See, chukulia mfano huu kwamba Holy See ni "Catholic Church Inc." alafu Papa ndiye CEO.

    Nimejitahidi kueleza kwa kifupi na kwa wepesi niwezavyo, kuielewa kwa undani zaidi The Holy See labda tunapaswa kuandaa andishi maalumu mahususi kwa ajili yake tu.

    *3. Mfalme wa Vatican*
    Mfalme wa Vatican ni mtawala mwenye mamlaka yote juu ya nchi ya Vatican na hii inaifanya Vatican kuwa moja kati ya nchi sita pekee duniani zenye wafalme wenye mamlaka kamili (absolute monarchy). Nchi nyingine tano ni Saudi Arabia, Brunei, Oman, Qatar, Oman na Swaziland.

    Hii ndio sababu kwanini Vatican hawawezi kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa sababu EU wanakubali nchi zenye mfumo wa kidemokrasia pekee.
    Japokuwa Vatican ina tawi la 'bunge' ambalo linaundwa na makadinali wa Vatican ambayo wanatunga sheria za 'nchi' lakini bado mfalme wa Vatican anauwezo wa kuveto maamuzi yoyote ambayo wamefikia.

    *Swali: Kwanini hatusikii chochote kuhusu Mfalme wa Vatican??*

    Ni kwa sababu Mfalme wa Vatican na Papa ni wajibu na mamlaka mbili tofauti lakini zinakaliwa na mtu mmoja, Papa wa Kanisa Katoliki.

    Hii inatupa kitu kingine cha kipekee kuhusu Vatican.

    Papa anachaguliwa na makadinali wenzake - Demokrasia.
    Lakini Mfalme hachaguliwi.

    Hii inafanya Vatican kuwa nchi pekee kwenye historia ya dunia kuwa na Mfalme mwenye mamlaka kamili ambaye si wa kurithi na anapatikana kidemokrasia (Elected non-heridetary absolute Monarchy).

    Kwa hiyo Papa kulingana na muktadha na mazingira ya suala husika kuna muda anatumia mamlaka yake kama Papa na muda mwingine inampasa kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Vatican.

    Bado kuna mkanganyiko???

    Zingatia mfano huu rahisi; tuseme kwamba kuna kampuni fulani kubwa ya kimataifa inaitwa Aman Enterprises (The Holy See kwa mada yetu). Aman Enterprises wakafanikiwa kuishwishi Tanzania kuwapatia kisiwa cha Mbudya na Bold Enterprises wanakibadilisha kisiwa cha Mbudya kuwa nchi inayojitegemea, labda iitwe Aman Land (Vatican City kwa mfano wetu).
    Sasa CEO wa kampuni Bwana Aman (Papa kwa mada yetu) anahamishiamanya makao makuu ya kampuni mpaka Aman Land. Kwa kuwa Aman Land sasa ni nchi, CEO wa kampuni anakuwa pia mtawala wa nchi hii, Mfalme.

    .
    Kwa hiyo kwa manufaa ya kampuni kutumia 'connection' zake za kimataifa kunufaisha taifa lake la Aman Land ni vyema kutumia mamlaka kama CEO wa Bold Enterprises na kuna muda akihitaji nchi yake ya Aman Land kutunga sheria na taratibu ambazo zitanufaisha kampuni izidi kushamiri ni vyema kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Aman Land.

    Haya ndio mamlaka mawili yaliyo chini ya mtu mmoja ndani ya vatican, Papa na Mfalme wa Vatican.

    Bado kuna mkanganyiko???

    Kama haujaelewa sawia usihofu kwa maana bado kuna hata nchi nyingine duniani bado hawaelewi sawa sawa mfumo mzima wa Vatican.

    Mfano, Umoja wa Mataifa wamekubali The Holy See (corporation) kama mwanachama wake lakini sio Vatican City nchi yenyewe.

    Passports za raia wa Vatican zinatolewa na The Holy See na sio Vatican na zinakubalika kwenye nchi nyingine japokuwa The Holy See kimataifa inatambulika kisheria kama Kampuni inayojitegemea.

    Na hapa tuongee kiduchu pia kuhusu raia wa Vatican. Katika nchi nyingine raia wa wanaongezeka kutokana na kuzaliana lakini hapa Vatican hakuna hilo kutokana na idadi ndogo ya wanaweka kiasi kwamba karibia ni asilimia sufuri. Namna pekee ya kuwa raia wa Vatican ni kwa kupewa uraia na Mfalme wa Vatican ili uishi Vatican kama moja wa wasaidizi wa Papa (ambaye ndiye mfalme). Kwa hiyo siku ukiacha kazi, yaani usaidizi wako kwa Papa ukifikia kikomo, Mfalme wa Vatican (ambayr ndiye Papa) anaondoa uraia wako na unarudi kwenu.

    Katika muda wowote ule raia wa nchi ya Vatican wanakadiriwa kuwa jumla karibia ya 500 ambao ndio idadi ndogo zaidi ya raia kwa nchi na ndogo kushinda hata idadi ya watu wanaoishi kwenye ghorofa moja kwenye nchi nyingi.
    Na raia wote hawa ni wafanyakazi wa Papa/The Holy See ambao wanapewa uraia na Mfalme (ambaye ndiye Papa) ambapo wanafanya kazi kama Makadinali, Wanadiplomasia, walinzi au kazi nyingine za kikanisa.

    Kwa ufupi sana hii ndio picha halisi ya nchi ya Vatican… na hapa ndipo ambapo maisha ya kiroho ya wafuasi zaidi ya Billioni 2 yanapoendeshwa…

    *VATICAN CITY...... Nchi? Mji? Serikali au Kampuni?* Nadhani moja kati ya maeneo ambayo yamekuwa tata zaidi kuyaelewa basi ni mji wa Vatican… tukiachilia mbali kuhusu utata/ugumu wa kuelewa mfumo wake wa uendeshaji na historia yake lakini swali jepesi zaidi ambalo kila mtu huwa anahisi analifahamu jawabu lake ni kuhusu utambulisho wa Vatican.!! Ni swali jepesi ambalo karibia kila mtu anadhani ana jawabu sahihi lakini uhalisia ni kwamba asilimia kubwa ya watu wana jawabu lisilo sahihi… kila mtu atakueleza kwamba Vatican ni nchi inayojitegemea lakini hii ni robo tu au thelethi ya jawabu… Leo nami niandike kidogo kuhusu eneo hili… na kwenye andishi hili fupi nitaeleza utambulisho wa Vatican ukoje kwa usahihi wake kabisa! *Muhimu:* andishi hili halilengi kukosoa au kupinga imani ya mtu yeyote. Tahadhali zote zinazingatiwa ili kulinda heshima ya imani ya kila mtu. Tuendelee… Vatican City, ndio makao makuu ya Kanisa Katoliki na nyumba ya maisha ya Papa, kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki. Vatican ndio nchi ndogo zaidi duniani kiasi kwamba unaweza kuizunguka yote kwa mzingo (circumference) kwa muda wa dakika arobaini tu kwa kutembea kwa miguu. Ni ajabu sana kwa namna gani nchi ndogo kiasi hiki imetokea na je ni nchi kama nchi nyingine??? Jibu la swali hili ni refu sana kiaisi kwamba unaweza hata kusoma darasani kwa mwaka mzima lakini nitajaribu kuweka katika maneno machache sana ya kueleweka kwa wepesi… Miaka ya kale sana Papa wa Kanisa Katoliki alikuwa ni mtawala wa nchi ambayo ilikuwa inajiita *Himaya ya Papa (Papal State)* ambayo inarandana kabisa na eneo la sasa la nchi nzima ya Italia. Hii ilikuwa takribani miaka ya 754 mpaka miaka ya 1870. Ni katika kipindi hiki ambacho Papa aliteua eneo ndani ya nchi yake Papal State ambalo likajengwa *St. Peters Basilica*, kanisa kubwa zaidi duniani na lenye nakshi adhimu zaidi. Eneo hili ambalo St. Peters Basilica ilijengwa ni eneo fulani hivi la muinuko ambako hapo hapo pia yalijengwa makazi ya Papa kuishi. Ikumbukwe kwamba katika kipindi hiki hiki cha uwepo wa himaya ya Papal State pia ilikuwa inapakana na Ufalme wa Italy (Kingdom of Italy) japo kila moja ilikuwa inajitegemea. Japokuwa himaya hizi mbili zilikuwa jirani lakini kulikuwa na uhasama fulani kati yao. Hii ilifanya Papa kujenga ukuta mkubwa kuzunguka makazi yake ya kuishi na kanisa la St. Peters Basilica. Kadiri miaka ilivyozidi kwenda uhasama kati ya Italy Kingdom na Papal State ulipanuka zaidi na ilifikia hatua Kingdom of Italy wakafanya uamuzi wa kuiteka Papal State na kuifanya makao makuu ya nchi yake (Rome ya sasa). Wakati na baada ya uvamizi huu wa Kingdom of Italy kuteka Papal State, Papa mwenyewe alikuwa amejificha ndani ya makazi yake yaliyozungushiwa ukuta ambao nimeeleza awali. Ikumbukwe kwamba hata kipindi hiki Kanisa Katoliki tayari lilikuwa na ushawishi mkubwa duniani kwa hiyo Kingdom of Italy walihofia kuingiza majeshi kwa nguvu ndani ya makazi ya Papa na kumkamata kuogopa umaarufu wao kimataifa kudondoka. Kwa hiyo majeshi ya Kingdom of Italy yalibakia nje mwa kuta za Vatican kwa miaka mingi sana wakiamini kwamba iko siku Papa atakata tamaa na kujisalimisha. Lakini hii haikufua dafu kwani miongo ilipita na Papa hakujisalimisha kwa kutoka nje ya kuta za Vatican. Takribani Mapapa watano kwa muda wa karibia miaka sitini waliishi ndani ya kuta za Vatican katika hali hii. Mapapa hao kwa majina yao walikuwa ni Papa Pius IX, Papa Leo XIII, Papa Pius X, Papa Benedict XV na Papa Pius XI. Hali hii ilisababisha Mapapa kutotambua Kingdom of Italy na pia kulalamika mara kwa mara kwa jamii ya kimataifa kwamba wanaishi kama wafungwa ndani ya kuta za Vatican kutokana na ukandamizaji wa Kingdom of Italy na hofu waliyonayo kutoka nje ya kuta za Vatican. Hii inatufikisha mpaka miaka ya 1920s wakati wa utawala wa Benito Mussolini akiwa Waziri Mkuu wa Italy. Mussolini alichoshwa na malalamiko haya ya Papa na majibizano ya kila mara huku Papa bado akishikilia msimamo wa kutoitambua Italy Mussolini mwanasiasa mahiri kama ajulikanavyo akaona fursa hapa ya kuandika jina lake kwenye vitabu vya historia. Akapendekeza makubaliano maalumu kwa Papa. Kwamba atafanya yafuatayo; 1. Italy itatoa ardhi ya Vatican kwa Papa na iwe himaya/nchi iliyo chini ya utawala wa Papa. 2. Italy itatoa fedha kama fidia kwa Papa kutokana na manyanyaso ya miaka yote. Mussolini alihitaji Papa kufanya yafuatayo; 1. Papa atambue Italy kuwa ni nchi. 2. Papa asijihusishe wala kutoa maoni yoyote kuhusu masuala ya kisiasa na vita. Papa na Mussolini wakafikia makubaliano na mikataba ikasainiwa na hapa ndipo taifa dogo zaidi duniani likazaliwa, Vatican. Vatican ikaanza kujiendesha kama taifa linalojitegemea kwa kuwa na sarafu yake, serikali yake, Polisi wake, jela yake (ndio kuna jela Vatican), Posta yake, Plate number zake, Passport zake na kadhalika na kadhalika. Vatican si kama nchi nyingine duniani kwa hiyo usidhani kwamba tayari umeielewa Vatican, hicho nilichoeleza ni theluthi tu mkanganyiko wa kuielewa Vatican kama nchi… kunywa tena glass ya maji and relax!! Nitaeleza tena kidogo… Ili kuielewa Vatican walau kiduchu kuna watu wawili tunapaswa kuwafahamu; 1. Papa 2. Mfalme wa Vatican Na pia kuna vitu viwili vya kuvielewa; 1. The Holy See 2. Vatican City Tuanze kimoja kimoja… *1. Papa* Hii sihitaji kueleza sana karibia wote tunafahamu. Lakini kwa msingi wa awali kabisa, Papa ni askofu wa Wakatoliki wote waliopo Rome/Vatican lakini kwa kuwa yeye pia ndiye kiongozi wa Wakatoliki wote duniani ndio sababu ya Uaskofu wake kuwa Papa. *2. The Holy See* Kabla sijaeleza chochote kuhusu Mfalme wa Vatican kwanza nieleze kuhusu The Holy See. Hili ni moja ya mambo magumu zaidi kuyaelewa kuhusu Vatican. Nitaeleza kwa lugha nyepesi na uchache ili tusipasue vichwa kwa mikanganyiko. Kwa tafsiri nyepesi Holy See ni 'Throne' ya Papa (nakosa neno zuri la kiswahili, sipendezwi sana na tafsiri ya 'Kiti cha Enzi'). Ni kwamba, maaskofu wote ndani ya kanisa Katoliki wanakuwa na 'throne' lakini kwa kuwa 'throne' ya Papa ni maalumu (kiongozi wa Wakatoliki wote duniani) kwa hiyo throne yake inakuwa muhimu zaidi na inaitwa 'The Holy See'. Mapapa wanabadilika lakini The Holy See iko na itaendelea kuwepo siku zote. Yaani kwa mfano Papa anapofariki au kustaafu kama tulivyoona mwaka juzi, Makadinali wanapokusanyika Vatican kwa uhalisia wanaenda kumchagua Kadinali mwenzao ambaye atakalia 'throne' ya 'Holy See'. Kwa 'angle' nyingine tunaweza kusema kwamba 'The Holy See' ndiyo sheria na mamlaka yote inayofanya kanisa Katoliki kuwa namna lilivyo. Pia sheria zote za kanisa Katoliki na mfumo wake unatengenezwa na The Holy See (sio Papa). Pia tunaweza kusema kwamba Benito Mussolini alipofanya makubaliano na Vatican aliingia mkataba ule na 'The Holy See'. Pia unaweza usiamini lakini katika nyanja za sheria za kimataifa 'The Holy See' inatambulika kama mtu/kampuni halisi ambaye amesajiliwa kisheria. Labda nitumie lugha nyepesi zaidi ya mfano… ukitaka kuelewa The Holy See, chukulia mfano huu kwamba Holy See ni "Catholic Church Inc." alafu Papa ndiye CEO. Nimejitahidi kueleza kwa kifupi na kwa wepesi niwezavyo, kuielewa kwa undani zaidi The Holy See labda tunapaswa kuandaa andishi maalumu mahususi kwa ajili yake tu. *3. Mfalme wa Vatican* Mfalme wa Vatican ni mtawala mwenye mamlaka yote juu ya nchi ya Vatican na hii inaifanya Vatican kuwa moja kati ya nchi sita pekee duniani zenye wafalme wenye mamlaka kamili (absolute monarchy). Nchi nyingine tano ni Saudi Arabia, Brunei, Oman, Qatar, Oman na Swaziland. Hii ndio sababu kwanini Vatican hawawezi kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa sababu EU wanakubali nchi zenye mfumo wa kidemokrasia pekee. Japokuwa Vatican ina tawi la 'bunge' ambalo linaundwa na makadinali wa Vatican ambayo wanatunga sheria za 'nchi' lakini bado mfalme wa Vatican anauwezo wa kuveto maamuzi yoyote ambayo wamefikia. *Swali: Kwanini hatusikii chochote kuhusu Mfalme wa Vatican??* Ni kwa sababu Mfalme wa Vatican na Papa ni wajibu na mamlaka mbili tofauti lakini zinakaliwa na mtu mmoja, Papa wa Kanisa Katoliki. Hii inatupa kitu kingine cha kipekee kuhusu Vatican. Papa anachaguliwa na makadinali wenzake - Demokrasia. Lakini Mfalme hachaguliwi. Hii inafanya Vatican kuwa nchi pekee kwenye historia ya dunia kuwa na Mfalme mwenye mamlaka kamili ambaye si wa kurithi na anapatikana kidemokrasia (Elected non-heridetary absolute Monarchy). Kwa hiyo Papa kulingana na muktadha na mazingira ya suala husika kuna muda anatumia mamlaka yake kama Papa na muda mwingine inampasa kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Vatican. Bado kuna mkanganyiko??? Zingatia mfano huu rahisi; tuseme kwamba kuna kampuni fulani kubwa ya kimataifa inaitwa Aman Enterprises (The Holy See kwa mada yetu). Aman Enterprises wakafanikiwa kuishwishi Tanzania kuwapatia kisiwa cha Mbudya na Bold Enterprises wanakibadilisha kisiwa cha Mbudya kuwa nchi inayojitegemea, labda iitwe Aman Land (Vatican City kwa mfano wetu). Sasa CEO wa kampuni Bwana Aman (Papa kwa mada yetu) anahamishiamanya makao makuu ya kampuni mpaka Aman Land. Kwa kuwa Aman Land sasa ni nchi, CEO wa kampuni anakuwa pia mtawala wa nchi hii, Mfalme. . Kwa hiyo kwa manufaa ya kampuni kutumia 'connection' zake za kimataifa kunufaisha taifa lake la Aman Land ni vyema kutumia mamlaka kama CEO wa Bold Enterprises na kuna muda akihitaji nchi yake ya Aman Land kutunga sheria na taratibu ambazo zitanufaisha kampuni izidi kushamiri ni vyema kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Aman Land. Haya ndio mamlaka mawili yaliyo chini ya mtu mmoja ndani ya vatican, Papa na Mfalme wa Vatican. Bado kuna mkanganyiko??? Kama haujaelewa sawia usihofu kwa maana bado kuna hata nchi nyingine duniani bado hawaelewi sawa sawa mfumo mzima wa Vatican. Mfano, Umoja wa Mataifa wamekubali The Holy See (corporation) kama mwanachama wake lakini sio Vatican City nchi yenyewe. Passports za raia wa Vatican zinatolewa na The Holy See na sio Vatican na zinakubalika kwenye nchi nyingine japokuwa The Holy See kimataifa inatambulika kisheria kama Kampuni inayojitegemea. Na hapa tuongee kiduchu pia kuhusu raia wa Vatican. Katika nchi nyingine raia wa wanaongezeka kutokana na kuzaliana lakini hapa Vatican hakuna hilo kutokana na idadi ndogo ya wanaweka kiasi kwamba karibia ni asilimia sufuri. Namna pekee ya kuwa raia wa Vatican ni kwa kupewa uraia na Mfalme wa Vatican ili uishi Vatican kama moja wa wasaidizi wa Papa (ambaye ndiye mfalme). Kwa hiyo siku ukiacha kazi, yaani usaidizi wako kwa Papa ukifikia kikomo, Mfalme wa Vatican (ambayr ndiye Papa) anaondoa uraia wako na unarudi kwenu. Katika muda wowote ule raia wa nchi ya Vatican wanakadiriwa kuwa jumla karibia ya 500 ambao ndio idadi ndogo zaidi ya raia kwa nchi na ndogo kushinda hata idadi ya watu wanaoishi kwenye ghorofa moja kwenye nchi nyingi. Na raia wote hawa ni wafanyakazi wa Papa/The Holy See ambao wanapewa uraia na Mfalme (ambaye ndiye Papa) ambapo wanafanya kazi kama Makadinali, Wanadiplomasia, walinzi au kazi nyingine za kikanisa. Kwa ufupi sana hii ndio picha halisi ya nchi ya Vatican… na hapa ndipo ambapo maisha ya kiroho ya wafuasi zaidi ya Billioni 2 yanapoendeshwa…
    Like
    2
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·2K Views
  • NDOTO YA MWANA MFALME WA SAUD ARABIA YA KUJENGA MJI UNAOJITEGEMEA KWA KILA KITU INAELEKEA KUTIMIA
    .
    .
    Mwana wa mfalme wa saud Arabia MOHAMMED BIN SALMAN alifikia uamuzi huo baada ya kutembelea ukanda wa kusinimagharibi mwa SAUDI ARABIA na kujionea eneo kubwa likiwa kame na lisilo na mvuto.Mradi huo utagharimu zaidi ya dola za kimarekani billioni miatano (500$) hii ni zaidi ya mara mia mbili ya bajeti ya Tanzania watu wanapesa bhana......
    .
    .
    Mradi huo utachukua maili za mraba elfu kumi (10,000 square miles) na katika huo mji vitu vingi vitakuwa ni BANDIA yaani vitu vingi vitakuwa ni vyakuundwa na binadamu kuanzia mchanga, mwezi nk.
    .
    .
    Amesema amekusudia kufanya hivyo kuonyesha na kuushangaza ulimwengu kwa kutoa wazo zuri na litakalo tukuzwa na kila mtu
    .
    .
    VITU VITAKAVYO KUWEPO HUMO
    .
    .
    MWEZI BANDIA (GIANT ARTIFICIAL MOON)
    Mwezi huo ndio utakuwa chanzo cha mwanga nyakati za usiku utakua ukiangaza na kutoa mwanga mkubwa kiasi kwamba usiku utakua ukionekana kama mchana.
    .
    MAGARI YANAYO PAA (FLYING CARS)
    katika mji huo kutakuwepo na magari yanayo paa ,yaani huduma nyingi za usafiri wa magari kama daladala na taxi zitakuwa zinatolewa na magari yanayopaa
    .
    MCHANGA BANDIA (ARTIFICIAL SHINNING SAND)
    Mwana mfalme huyo amekusudia kutengeneza mchanga ambao utakuwa unang'aa nyakati za mchana na usiku taswila ambayo itaongeza mvuto na uzuri wa mji huo
    .
    MVUA BANDIA (ARTIFICIAL RAIN)
    Pia amekusudia kutengeneza mvua mbadala yaani mvua ambayo itakuwa ikinyesha muda wowote anaotaka haijalishi ni kiangazi wala masika.Kumbuka mji huo utajengwa kwenye jangwa lililopo pembezoni mwa SAUDI ARABIA .
    .
    WAHUDUMU MAROBOTI (ROBOT WORKERS)
    Kumbuka mji huo utakuwa kama sehemu ya kiutalii hivyo amekusudia kuajiri wafanya maroboti.Maroboti hao watakuwa wakitoa huduma mbalimbali kama kuhudumia vinywaji kwenye bar chakuka kwenye hotel na hata kuendesha baadhi ya taxi.
    .
    .
    NB
    Teknolojia ya gari zinazopaa ilisha wekwa wazi na baadhi ya wasafiri wa kinadharia (TIME TRAVELERS) wengi wa time travelers wanasema mpaka kufikia mwaka 2030 teknolojia ya magari yanayopaa itakuwa ishaanza kushamiri katika miji mingi mikubwa duniani kama TEXAS,NEW YORK CITY,PARIS,BEIJING nk
    NDOTO YA MWANA MFALME WA SAUD ARABIA YA KUJENGA MJI UNAOJITEGEMEA KWA KILA KITU INAELEKEA KUTIMIA . . Mwana wa mfalme wa saud Arabia MOHAMMED BIN SALMAN alifikia uamuzi huo baada ya kutembelea ukanda wa kusinimagharibi mwa SAUDI ARABIA na kujionea eneo kubwa likiwa kame na lisilo na mvuto.Mradi huo utagharimu zaidi ya dola za kimarekani billioni miatano (500$) hii ni zaidi ya mara mia mbili ya bajeti ya Tanzania watu wanapesa bhana...... . . Mradi huo utachukua maili za mraba elfu kumi (10,000 square miles) na katika huo mji vitu vingi vitakuwa ni BANDIA yaani vitu vingi vitakuwa ni vyakuundwa na binadamu kuanzia mchanga, mwezi nk. . . Amesema amekusudia kufanya hivyo kuonyesha na kuushangaza ulimwengu kwa kutoa wazo zuri na litakalo tukuzwa na kila mtu . . VITU VITAKAVYO KUWEPO HUMO . . 🔴 MWEZI BANDIA (GIANT ARTIFICIAL MOON) Mwezi huo ndio utakuwa chanzo cha mwanga nyakati za usiku utakua ukiangaza na kutoa mwanga mkubwa kiasi kwamba usiku utakua ukionekana kama mchana. . 🔴MAGARI YANAYO PAA (FLYING CARS) katika mji huo kutakuwepo na magari yanayo paa ,yaani huduma nyingi za usafiri wa magari kama daladala na taxi zitakuwa zinatolewa na magari yanayopaa . 🔴MCHANGA BANDIA (ARTIFICIAL SHINNING SAND) Mwana mfalme huyo amekusudia kutengeneza mchanga ambao utakuwa unang'aa nyakati za mchana na usiku taswila ambayo itaongeza mvuto na uzuri wa mji huo . 🔴MVUA BANDIA (ARTIFICIAL RAIN) Pia amekusudia kutengeneza mvua mbadala yaani mvua ambayo itakuwa ikinyesha muda wowote anaotaka haijalishi ni kiangazi wala masika.Kumbuka mji huo utajengwa kwenye jangwa lililopo pembezoni mwa SAUDI ARABIA . . 🔴WAHUDUMU MAROBOTI (ROBOT WORKERS) Kumbuka mji huo utakuwa kama sehemu ya kiutalii hivyo amekusudia kuajiri wafanya maroboti.Maroboti hao watakuwa wakitoa huduma mbalimbali kama kuhudumia vinywaji kwenye bar chakuka kwenye hotel na hata kuendesha baadhi ya taxi. . . NB Teknolojia ya gari zinazopaa ilisha wekwa wazi na baadhi ya wasafiri wa kinadharia (TIME TRAVELERS) wengi wa time travelers wanasema mpaka kufikia mwaka 2030 teknolojia ya magari yanayopaa itakuwa ishaanza kushamiri katika miji mingi mikubwa duniani kama TEXAS,NEW YORK CITY,PARIS,BEIJING nk
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·2K Views
  • Je Wajua: Ikiwa na mtaji wa soko wa dola za Marekani trilioni 2.25 kufikia Aprili 2021, Apple ilikuwa kampuni kubwa zaidi duniani iliyo ingiza mapato mengi mwaka wa 2021. Kampuni nyingine zilizopo tano bora duniani kati ya hizo ni Microsoft, Saudi Arabian Oil Company (Saudi Aramco), Amazon, na Alfabeti ya kampuni kuu ya Google. Saudi Aramco iliongoza katika orodha ya makampuni yenye faida kubwa zaidi duniani mwaka 2019, ikiwa na mapato halisi ya dola za Marekani bilioni 88.21.
    Je Wajua: Ikiwa na mtaji wa soko wa dola za Marekani trilioni 2.25 kufikia Aprili 2021, Apple ilikuwa kampuni kubwa zaidi duniani iliyo ingiza mapato mengi mwaka wa 2021. Kampuni nyingine zilizopo tano bora duniani kati ya hizo ni Microsoft, Saudi Arabian Oil Company (Saudi Aramco), Amazon, na Alfabeti ya kampuni kuu ya Google. Saudi Aramco iliongoza katika orodha ya makampuni yenye faida kubwa zaidi duniani mwaka 2019, ikiwa na mapato halisi ya dola za Marekani bilioni 88.21.
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·145 Views
  • Cristiano Ronaldo: “Wakati wangu bora nikiwa na Al Nassr ni pindi tuliposhinda kombe langu la kwanza kwenye fainali dhidi ya Al Hilal.

    Nataka kushinda makombe mengi na Al Nassr, nataka kuwasaidia wachezaji wenzangu na Al Nassr kufanikiwa zaidi.

    Wazo la kuwa star wa kwanza kujiunga Ligi ya Saudi, ni heshima kubwa kwangu. Na natumai baada ya miaka 5-10 ligi itaendelea kukua. Sio ligi pekee na hata academies zilizopo Saudi Arabia na itaongeza kiwango cha ushindani. Hii ni ndoto yangu. Nataka kuisaidia ligi na nchi.

    Najua kwamba kila mtu anamwangalia Cristiano Ronaldo Kama mfano wa kuigwa. Sio uwanjani tu, mpaka nje ya uwanja pia. Najua hili, na kila mtu analijua hili, na Kama kuna mtu anasema tofauti basi anadanganya.

    Nina ndoto ya kushinda Asian Champions League na Al Nassr. Mwaka huu utakuwa ni mwaka mzuri kwa Al Nassr. Inshallah.”
    🔳Cristiano Ronaldo: “Wakati wangu bora nikiwa na Al Nassr ni pindi tuliposhinda kombe langu la kwanza kwenye fainali dhidi ya Al Hilal. Nataka kushinda makombe mengi na Al Nassr, nataka kuwasaidia wachezaji wenzangu na Al Nassr kufanikiwa zaidi. Wazo la kuwa star wa kwanza kujiunga Ligi ya Saudi, ni heshima kubwa kwangu. Na natumai baada ya miaka 5-10 ligi itaendelea kukua. Sio ligi pekee na hata academies zilizopo Saudi Arabia na itaongeza kiwango cha ushindani. Hii ni ndoto yangu. Nataka kuisaidia ligi na nchi. Najua kwamba kila mtu anamwangalia Cristiano Ronaldo Kama mfano wa kuigwa. Sio uwanjani tu, mpaka nje ya uwanja pia. Najua hili, na kila mtu analijua hili, na Kama kuna mtu anasema tofauti basi anadanganya. Nina ndoto ya kushinda Asian Champions League na Al Nassr. Mwaka huu utakuwa ni mwaka mzuri kwa Al Nassr. Inshallah.”
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·413 Views
  • Baada ya Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) kutangaza Nchi za Uhispania, Ureno na Morocco kuwa ndizo zitaandaa michuano ya kombe la Dunia la mwaka 2030 huku lile la mwaka 2034 likipangwa kufanyika Nchini Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo, Mitrovic na Ng'olo Kante wamezungumza yafuatayo:

    "Kombe la dunia mwaka 2034 nchini Saudia Arabia litakuwa bora zaidi kuwahi kutokea. " - Cristiano Ronaldo

    "Naamini kombe la dunia mwaka 2034 nchini Saudia Arabia litakuwa bora sana dunia kuwahi kushuhudia. " - Mitrovic

    "Naamini tutawaletea Kombe la Dunia la kipekee na na bora ambalo dunia inalisubiri kutoka ufalme wa Saudia Arabia. " - Ng'olo Kante.

    Baada ya Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) kutangaza Nchi za Uhispania, Ureno na Morocco kuwa ndizo zitaandaa michuano ya kombe la Dunia la mwaka 2030 huku lile la mwaka 2034 likipangwa kufanyika Nchini Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo, Mitrovic na Ng'olo Kante wamezungumza yafuatayo: "Kombe la dunia mwaka 2034 nchini Saudia Arabia litakuwa bora zaidi kuwahi kutokea. " - Cristiano Ronaldo "Naamini kombe la dunia mwaka 2034 nchini Saudia Arabia litakuwa bora sana dunia kuwahi kushuhudia. " - Mitrovic "Naamini tutawaletea Kombe la Dunia la kipekee na na bora ambalo dunia inalisubiri kutoka ufalme wa Saudia Arabia. " - Ng'olo Kante.
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·488 Views
  • VIKOSI VYA GUINEA VS TANZANIA

    1. GUINEA
    Camara -Simba (Tanzania)
    Diakite -Cerce Bruggle(Belgium)
    Ibrahim Conte-UTA Arad(Romania)
    Saidou Sow -Strasbourg (France)
    Issiaga Sylla -Montpellier (France)
    Mohamed Camara-PAOK (Greece)
    Abdoulaye Toure -Le Havre(France)
    Morlaye Sylla -Arouca(Portugal)
    Seydouba Cisse-Leganese(Spain)
    Francois Kamano-Damac(Saudi Arabia)
    Serhou Guirassy -Borussia Dortmund

    2. TANZANIA
    Manula-Simba(Tanzania)
    Kapombe-Simba(Tanzania)
    Hussein-Simba(Tanzania)
    Job-Yanga(Tanzania)
    Hamad-Yanga(Tanzania)
    Yahaya-Yanga(Tanzania)
    Bitegeko-Azam(Tanzania)
    Msuva-Al Talaba(Iraq)
    Salum-Azam(Tanzania)
    Mzize-Yanga(Tanzania)
    Samatta-PAOK(Greece)

    NB; TANZANIA WAMECHUKUA POINTS 6 KUTOKA KWA GUINEA. UMEJIFUNZA NINI?
    VIKOSI VYA GUINEA VS TANZANIA 1. GUINEA Camara -Simba (Tanzania) Diakite -Cerce Bruggle(Belgium) Ibrahim Conte-UTA Arad(Romania) Saidou Sow -Strasbourg (France) Issiaga Sylla -Montpellier (France) Mohamed Camara-PAOK (Greece) Abdoulaye Toure -Le Havre(France) Morlaye Sylla -Arouca(Portugal) Seydouba Cisse-Leganese(Spain) Francois Kamano-Damac(Saudi Arabia) Serhou Guirassy -Borussia Dortmund 2. TANZANIA Manula-Simba(Tanzania) Kapombe-Simba(Tanzania) Hussein-Simba(Tanzania) Job-Yanga(Tanzania) Hamad-Yanga(Tanzania) Yahaya-Yanga(Tanzania) Bitegeko-Azam(Tanzania) Msuva-Al Talaba(Iraq) Salum-Azam(Tanzania) Mzize-Yanga(Tanzania) Samatta-PAOK(Greece) NB; TANZANIA WAMECHUKUA POINTS 6 KUTOKA KWA GUINEA. UMEJIFUNZA NINI?
    Like
    Love
    Wow
    8
    · 1 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·858 Views
  • Leo saa 1:00 usiku tutakuwa tena uwanjani kuwakabili Al-Adalah FC ya nchini Saudi Arabia.
    Leo saa 1:00 usiku tutakuwa tena uwanjani kuwakabili Al-Adalah FC ya nchini Saudi Arabia.
    Like
    Love
    3
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·168 Views
  • Leo saa 1:00 usiku tutakuwa tena uwanjani kuwakabili Al-Adalah FC ya nchini Saudi Arabia.
    Leo saa 1:00 usiku tutakuwa tena uwanjani kuwakabili Al-Adalah FC ya nchini Saudi Arabia.
    Like
    Love
    3
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·172 Views
Arama Sonuçları