Aliyetiwa hatiani kuwa Mhalifu wa kivita na Mahakama ya kimataifa ya (ICC) kwa makosa mbalimbali, Thomas Lubanga, ametangaza kuunda kundi jipya la Waasi lenye lengo la kuiangusha Serikali ya Jimbo la Ituri, lililopo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo .
Nchi ya DR Congo imekuwa ikikabiliwa na tishio la kiusalama katika Mikoa ya mashariki ambapo makundi ya Waasi ikiwemo Muungano wa Waasi wa AFC/M23 unaoshikilia Miji ya Goma, Bukavu, Nyabibwe na Walikale.
Hata hivyo, uamuzi wa Thomas Lubanga ambaye ni Mzaliwa wa Mkoa wa Ituri Nchini DR Congo na anayeishi Nchini Uganda , kutangaza kuanzisha Kundi lake la Waasi alilolipa jina Convention for the Popular Revolution (CPR) ambalo litaongeza hofu ya machafuko Nchini humo wakati huu ambao Serikali ya Rais Felix Tshisekedi inatafuta maridhiano na M23 kwa njia ya mazungumzo.
Shirika la Habari la Reuters, limeripoti leo Jumanne Aprili Mosi, 2025, kuwa Lubanga ambaye ni Mzaliwa wa Ituri, alihukumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mwaka 2012 kwa makosa ya kuwasajili Watoto kama Askari na akapewa kifungo cha miaka 14 Gerezani, baadaye aliachiliwa mwaka 2020 na Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi kisha akamteua kuwa sehemu ya kikosi kazi cha kuleta amani Jimboni Ituri.
Hata hivyo, mwaka 2022 alitekwa nyara kwa miezi miwili na kundi la Waasi, tukio analodai kupangwa na Serikali ya DR Congo kwa lengo kumpoteza ila kwa sasa anaishi Nchini Uganda.

Aliyetiwa hatiani kuwa Mhalifu wa kivita na Mahakama ya kimataifa ya (ICC) kwa makosa mbalimbali, Thomas Lubanga, ametangaza kuunda kundi jipya la Waasi lenye lengo la kuiangusha Serikali ya Jimbo la Ituri, lililopo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩.
Nchi ya DR Congo imekuwa ikikabiliwa na tishio la kiusalama katika Mikoa ya mashariki ambapo makundi ya Waasi ikiwemo Muungano wa Waasi wa AFC/M23 unaoshikilia Miji ya Goma, Bukavu, Nyabibwe na Walikale.
Hata hivyo, uamuzi wa Thomas Lubanga ambaye ni Mzaliwa wa Mkoa wa Ituri Nchini DR Congo na anayeishi Nchini Uganda 🇺🇬, kutangaza kuanzisha Kundi lake la Waasi alilolipa jina Convention for the Popular Revolution (CPR) ambalo litaongeza hofu ya machafuko Nchini humo wakati huu ambao Serikali ya Rais Felix Tshisekedi inatafuta maridhiano na M23 kwa njia ya mazungumzo.
Shirika la Habari la Reuters, limeripoti leo Jumanne Aprili Mosi, 2025, kuwa Lubanga ambaye ni Mzaliwa wa Ituri, alihukumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mwaka 2012 kwa makosa ya kuwasajili Watoto kama Askari na akapewa kifungo cha miaka 14 Gerezani, baadaye aliachiliwa mwaka 2020 na Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi kisha akamteua kuwa sehemu ya kikosi kazi cha kuleta amani Jimboni Ituri.
Hata hivyo, mwaka 2022 alitekwa nyara kwa miezi miwili na kundi la Waasi, tukio analodai kupangwa na Serikali ya DR Congo kwa lengo kumpoteza ila kwa sasa anaishi Nchini Uganda.
0 Commentarios
·0 Acciones
·46 Views