• ASANTE SANA KWA MAUMIVU

    Ningetamani kuwa nawe katika maisha yote, nyakati zote, lakini upepo wa maisha na tamaa zimetuweka mbali.

    Nilitamani kuiweka dunia yangu kifuani mwako, lakini huenda dunia ninayoishi mimi ni tofauti na dunia yako.

    Dunia ya ufukara ninayoishi mimi dhidi ya dunia yako ya pesa na starehe za gharama.

    Nilishindwa mimi na ufukara wangu, nimedondoka, nimekuacha uende.

    Nimeamini kuwa, ukiwa huna pesa, kitu pekee unachoweza kumiliki kwa mwanamke mrembo ni picha zake tu na sio moyo wake.

    Moyo wa mwanamke ni kama mluzi wa ng'ombe mnadani, kadri miluzi inavyoongezeka ndivyo anavyozidi kupanda bei.

    Nasikitika kuyajua haya leo, ni kweli inauma sana, nimekubali.

    Nimeelewa nguvu ya ukimya wako, nimeelewa kwanini umeondoka kwangu, bora umeondoka tu, ni ngumu kusubiri ahadi zangu zisizotimia.

    Hongera kwa kumpata mtu wa maisha yako, bado natafuta maisha yangu, nimekubali uende kipepeo wangu wa zamani, japo kumbukumbu zetu zinauma.

    Kwaheri, Mungu akuongoze huko ulikochagua.

    Nashusha karamu yangu chini, ngoja niache kuwaza upuuzi wa mapenzi.
    ASANTE SANA KWA MAUMIVU 💔 Ningetamani kuwa nawe katika maisha yote, nyakati zote, lakini upepo wa maisha na tamaa zimetuweka mbali. Nilitamani kuiweka dunia yangu kifuani mwako, lakini huenda dunia ninayoishi mimi ni tofauti na dunia yako. Dunia ya ufukara ninayoishi mimi dhidi ya dunia yako ya pesa na starehe za gharama. Nilishindwa mimi na ufukara wangu, nimedondoka, nimekuacha uende. Nimeamini kuwa, ukiwa huna pesa, kitu pekee unachoweza kumiliki kwa mwanamke mrembo ni picha zake tu na sio moyo wake. Moyo wa mwanamke ni kama mluzi wa ng'ombe mnadani, kadri miluzi inavyoongezeka ndivyo anavyozidi kupanda bei. Nasikitika kuyajua haya leo, ni kweli inauma sana, nimekubali. Nimeelewa nguvu ya ukimya wako, nimeelewa kwanini umeondoka kwangu, bora umeondoka tu, ni ngumu kusubiri ahadi zangu zisizotimia. Hongera kwa kumpata mtu wa maisha yako, bado natafuta maisha yangu, nimekubali uende kipepeo wangu wa zamani, japo kumbukumbu zetu zinauma. Kwaheri, Mungu akuongoze huko ulikochagua. Nashusha karamu yangu chini, ngoja niache kuwaza upuuzi wa mapenzi.
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·56 Views
  • UNAJIUMIZA KWA KUJIDHARAU

    Sio maisha yanayo kunyima nafasi ila niwewe unaye jinyima thamani yako, kila wakati unajiona hustahili, unajiona kuwa hutoshi bila fulani una jiona kila wakati wewe ni fungu la kukosa, hujawahi kujiona katika hali ya ushindi kila wakati unajiweka katika hali ya kujijeruhi hali ambayo inafanya ukose nafasi

    Nafahamu unasema kwa sauti ya chini, lakini ni sauti ya chini iliyo jionia hivyo kila ikitoka inatoka kwa makali sana, kiasi kwamba unapo jiona si kitu inaingiza hofu mbele zako ,unapojitilia shaka inakupotezea thamani kimya kimya

    Acha kujificha kwa tabasamu ili watu wasione jinsi ambavyo una jidharau, katika nyakati za ukimya hali ya kujidharau inapo jirudia hukuumiza zaidi kwakua katika ukimya hujikumbusha mambo. Ulimwengu utakumulika kwa vile ambavyo wewe binafsi utavyo penda kujitazama

    Unafikiri kwakua umefahamu kusema samahani basi unaitoa kila sehemu na kila wakati, mpaka samahani inapoteza thamani yake, yote ni kwasababu wewe binafsi umepoteza thamani yako kwa kujidharau. Unaamua kujidharau kwasababu kila sehemu unaona hustahili

    Marcus Aurielius anasema

    " Una thamani si kwasababu watu wanasema, bali kwasababu upo"

    Naye Epictetus anasema

    "Jifahamu kwanza kisha jipambe na huo ukweli "

    Ndugu unapo jidharau unauonesha ulimwengu haukustahili kukuleta ili ulitimize kusudi kuu la wewe kuwapo, unajidhurumu mpangilio wa maisha unao kustahili. Unaamini kuna watu walio letwa dunia kuwa uthibitisho wako, ikiwa ndivyo basi unajidanganya hakuna aliye letwa kwasababu hiyo zaidi yako

    Acha, acha kujinyima kwa woga wa siwezi, siku zote thamani yako haisubiri sifa za dunia. Usiogope kuzungumza kwa hofu ya kukosea tu si kwakua hujapata cha kuongea.Lazima uamini kuwa sauti yako ina maana mbele ya yoyote yule ,acha kujidogodesha ili tu wengine wajivike vazi la ukubwa.

    Ulimwengu hautakupa mafanikio mpaka pale ambapo utaacha kujidharau, utakapo acha kujificha nyuma ya migongo ya wengine```
    UNAJIUMIZA KWA KUJIDHARAU Sio maisha yanayo kunyima nafasi ila niwewe unaye jinyima thamani yako, kila wakati unajiona hustahili, unajiona kuwa hutoshi bila fulani una jiona kila wakati wewe ni fungu la kukosa, hujawahi kujiona katika hali ya ushindi kila wakati unajiweka katika hali ya kujijeruhi hali ambayo inafanya ukose nafasi Nafahamu unasema kwa sauti ya chini, lakini ni sauti ya chini iliyo jionia hivyo kila ikitoka inatoka kwa makali sana, kiasi kwamba unapo jiona si kitu inaingiza hofu mbele zako ,unapojitilia shaka inakupotezea thamani kimya kimya Acha kujificha kwa tabasamu ili watu wasione jinsi ambavyo una jidharau, katika nyakati za ukimya hali ya kujidharau inapo jirudia hukuumiza zaidi kwakua katika ukimya hujikumbusha mambo. Ulimwengu utakumulika kwa vile ambavyo wewe binafsi utavyo penda kujitazama Unafikiri kwakua umefahamu kusema samahani basi unaitoa kila sehemu na kila wakati, mpaka samahani inapoteza thamani yake, yote ni kwasababu wewe binafsi umepoteza thamani yako kwa kujidharau. Unaamua kujidharau kwasababu kila sehemu unaona hustahili Marcus Aurielius anasema " Una thamani si kwasababu watu wanasema, bali kwasababu upo" Naye Epictetus anasema "Jifahamu kwanza kisha jipambe na huo ukweli " Ndugu unapo jidharau unauonesha ulimwengu haukustahili kukuleta ili ulitimize kusudi kuu la wewe kuwapo, unajidhurumu mpangilio wa maisha unao kustahili. Unaamini kuna watu walio letwa dunia kuwa uthibitisho wako, ikiwa ndivyo basi unajidanganya hakuna aliye letwa kwasababu hiyo zaidi yako Acha, acha kujinyima kwa woga wa siwezi, siku zote thamani yako haisubiri sifa za dunia. Usiogope kuzungumza kwa hofu ya kukosea tu si kwakua hujapata cha kuongea.Lazima uamini kuwa sauti yako ina maana mbele ya yoyote yule ,acha kujidogodesha ili tu wengine wajivike vazi la ukubwa. Ulimwengu hautakupa mafanikio mpaka pale ambapo utaacha kujidharau, utakapo acha kujificha nyuma ya migongo ya wengine```
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·101 Views
  • Mamia ya Raia wa Burkina Faso wanaoishi Ufaransa wameandamana nchini Ufaransa kushinikiza Rais wa mpito wa Burkina Faso, Ibrahim Traore aondoke madarakani kwani wanadai kiongozi huyo ni Dikteta.

    Baada ya sakata hili baadhi ya Watu wanadai huenda Waandamanaji hao wamepangwa na Serikali ya Ufaransa baada ya hivi karibuni Ibrahim Traore kukata urafiki na mazoea na nchi hiyo ambayo kwa muda mrefu inadaiwa ilikuwa ikiinyonya Burkina Faso hasa kwenye eneo la madini.

    Traore tangu aingie madarakani amekuwa akipingwa sana na baadhi ya mataifa yenye nguvu Duniani, na hivi sasa Marekani inamtuhumu kuwa anatumia Madini ya Burkina Faso kwa manufaa yake binafsi siyo ya Wananchi wote.
    Mamia ya Raia wa Burkina Faso wanaoishi Ufaransa wameandamana nchini Ufaransa kushinikiza Rais wa mpito wa Burkina Faso, Ibrahim Traore aondoke madarakani kwani wanadai kiongozi huyo ni Dikteta. Baada ya sakata hili baadhi ya Watu wanadai huenda Waandamanaji hao wamepangwa na Serikali ya Ufaransa baada ya hivi karibuni Ibrahim Traore kukata urafiki na mazoea na nchi hiyo ambayo kwa muda mrefu inadaiwa ilikuwa ikiinyonya Burkina Faso hasa kwenye eneo la madini. Traore tangu aingie madarakani amekuwa akipingwa sana na baadhi ya mataifa yenye nguvu Duniani, na hivi sasa Marekani inamtuhumu kuwa anatumia Madini ya Burkina Faso kwa manufaa yake binafsi siyo ya Wananchi wote.
    Like
    3
    · 0 Comments ·0 Shares ·91 Views
  • Maisha bila unafiki hayaendi kabisa, Leo hii Alex Sanchez anasema timu yake ya moyoni ni Arsenal.

    Hawezi kuisahau katukatu lakini jinsi alivyolazimisha kuondoka kipindi timu inamuhitaji, nazidi kuamini unafiki upo duniani kote .

    Babu Wenger alijitahidi sana kumbakisha lakini wapi

    Follow Neliud Cosiah
    Maisha bila unafiki hayaendi kabisa, Leo hii Alex Sanchez anasema timu yake ya moyoni ni Arsenal. Hawezi kuisahau katukatu lakini jinsi alivyolazimisha kuondoka kipindi timu inamuhitaji, nazidi kuamini unafiki upo duniani kote 😂. Babu Wenger alijitahidi sana kumbakisha lakini wapi 😀 Follow Neliud Cosiah
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·109 Views
  • KUWA KWENYE UHUSIANO NA MWANAUME MWENYE KAZI NGUMU

    Kuwa na mwanamume mchapakazi si jambo la kukata tamaa.
    Ni kwa ajili ya mwanamke ambaye anaelewa kwamba upendo hauji kila wakati na waridi na mashairi -
    Wakati mwingine, huja na usiku wa manane, macho yenye uchovu, na mikono iliyochoshwa na jukumu.
    Hawezi kuwa na saa za kutumia simu kila wakati au jioni ndefu za kimapenzi zilizopangwa,
    Sio kwa sababu hajali ...
    Lakini kwa sababu yuko huko akijenga siku zijazo - kwa ajili yako.
    Kwa nyinyi wawili.
    Mwanaume mwenye bidii hawezi kujibu mara moja,
    Lakini ukimya wake mara nyingi huzungumza juu ya dhabihu.
    Ni katika zamu hizo ndefu, saa za ziada, mapumziko yaliyoruka -
    Hapo ndipo upendo wake unaishi.
    Na ndio, kutakuwa na siku ambazo nishati yake pekee itatumika kurudi nyumbani,
    Kumbusu usiku mwema, na kugonga kitandani
    Ili tu kuamka na kuifanya tena.
    Lakini kamwe usichanganye uchovu na kutojali.
    Kamwe usichanganye utulivu na umbali.
    Kwa sababu uaminifu wake hauvai suti kila wakati na kuzungumza kwa maua -
    Wakati mwingine huvaa buti zilizovaliwa, mashati yenye rangi, na macho ambayo ndoto ya kukupa kila kitu.
    Ikiwa una mwanaume mwenye bidii,
    Mthamini.
    Ongea lugha yake ya upendo - uvumilivu, imani, kutia moyo.
    Simama karibu naye, sio nyuma yake -
    Mshangilie, sio kumshinikiza -
    Muunge mkono, usimdharau.
    Kwa sababu nyuma ya kila familia yenye nguvu, salama, na yenye mafanikio
    Ni mtu aliyeinuka kabla ya jua
    Na ilifanya kazi hadi ilipowekwa -
    Sio kwa pesa tu,
    Lakini kwa maisha aliyokuahidi.
    Basi hapa ni kwa wanaume wanaobeba uzito wa dunia mabegani mwao,
    Na wanawake wenye uwezo wa kutembea nao kwa neema.
    Kufanya kazi kwa bidii ni lugha yake ya upendo.
    Na ikiwa unasikiliza kwa makini -
    Utasikia "nakupenda"
    Katika kila juhudi anazofanya.

    #WeweNdiweMaishaYangu # #UmejengwaKwaSadaka# #UpendoHalisi Huzungumza Kwa Utulivu #
    KUWA KWENYE UHUSIANO NA MWANAUME MWENYE KAZI NGUMU Kuwa na mwanamume mchapakazi si jambo la kukata tamaa. Ni kwa ajili ya mwanamke ambaye anaelewa kwamba upendo hauji kila wakati na waridi na mashairi - Wakati mwingine, huja na usiku wa manane, macho yenye uchovu, na mikono iliyochoshwa na jukumu. Hawezi kuwa na saa za kutumia simu kila wakati au jioni ndefu za kimapenzi zilizopangwa, Sio kwa sababu hajali ... Lakini kwa sababu yuko huko akijenga siku zijazo - kwa ajili yako. Kwa nyinyi wawili. Mwanaume mwenye bidii hawezi kujibu mara moja, Lakini ukimya wake mara nyingi huzungumza juu ya dhabihu. Ni katika zamu hizo ndefu, saa za ziada, mapumziko yaliyoruka - Hapo ndipo upendo wake unaishi. Na ndio, kutakuwa na siku ambazo nishati yake pekee itatumika kurudi nyumbani, Kumbusu usiku mwema, na kugonga kitandani Ili tu kuamka na kuifanya tena. Lakini kamwe usichanganye uchovu na kutojali. Kamwe usichanganye utulivu na umbali. Kwa sababu uaminifu wake hauvai suti kila wakati na kuzungumza kwa maua - Wakati mwingine huvaa buti zilizovaliwa, mashati yenye rangi, na macho ambayo ndoto ya kukupa kila kitu. Ikiwa una mwanaume mwenye bidii, Mthamini. Ongea lugha yake ya upendo - uvumilivu, imani, kutia moyo. Simama karibu naye, sio nyuma yake - Mshangilie, sio kumshinikiza - Muunge mkono, usimdharau. Kwa sababu nyuma ya kila familia yenye nguvu, salama, na yenye mafanikio Ni mtu aliyeinuka kabla ya jua Na ilifanya kazi hadi ilipowekwa - Sio kwa pesa tu, Lakini kwa maisha aliyokuahidi. Basi hapa ni kwa wanaume wanaobeba uzito wa dunia mabegani mwao, Na wanawake wenye uwezo wa kutembea nao kwa neema. Kufanya kazi kwa bidii ni lugha yake ya upendo. Na ikiwa unasikiliza kwa makini - Utasikia "nakupenda" Katika kila juhudi anazofanya. #WeweNdiweMaishaYangu # #UmejengwaKwaSadaka# #UpendoHalisi Huzungumza Kwa Utulivu #
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·326 Views
  • Mkulima mmoja mwenye umri wa miaka 55 kutoka Mkoa wa Shandong Nchini China , ambaye ana ulemavu wa akili, alitumia miaka kadhaa kujenga Nyumba ya Ghorofa saba (7) kwa mkono. Alijenga Jengo hilo akiwa na matumaini kwamba Ndugu zake wawili (2) wangekuja na kuishi naye, licha ya kuambiwa mara nyingi na Wanakijiji kuwa kaka zake hao walikuwa wamefariki Dunia muda mrefu uliopita.

    Aidha, Jengo hilo lililojengwa kwa mawe, mbao, na udongo, linasimama kama ishara yenye nguvu ya kujitolea na upendo wake kwa familia yake. Hata hivyo, Serikali ya eneo hilo iliingilia kati kwa kumsaidia kumjengea Nyumbani nyingine ambayo ilijengwa na kijiji hicho kwa ajili ya ustawi wake kisha kumhamisha katika Nyumba hiyo mpya.

    Toa maoni yako
    Mkulima mmoja mwenye umri wa miaka 55 kutoka Mkoa wa Shandong Nchini China 🇨🇳, ambaye ana ulemavu wa akili, alitumia miaka kadhaa kujenga Nyumba ya Ghorofa saba (7) kwa mkono. Alijenga Jengo hilo akiwa na matumaini kwamba Ndugu zake wawili (2) wangekuja na kuishi naye, licha ya kuambiwa mara nyingi na Wanakijiji kuwa kaka zake hao walikuwa wamefariki Dunia muda mrefu uliopita. Aidha, Jengo hilo lililojengwa kwa mawe, mbao, na udongo, linasimama kama ishara yenye nguvu ya kujitolea na upendo wake kwa familia yake. Hata hivyo, Serikali ya eneo hilo iliingilia kati kwa kumsaidia kumjengea Nyumbani nyingine ambayo ilijengwa na kijiji hicho kwa ajili ya ustawi wake kisha kumhamisha katika Nyumba hiyo mpya. Toa maoni yako
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·259 Views
  • Miaka kadhaa iliyopita, hii ilikuwa nyumba nzuri zaidi katika mtaa huu. Mmiliki wake alikuwa mtu tajiri zaidi ambaye kila mmoja alimtegemea kwa msaada. Gari lake lilikuwa kivutio kwa macho ya kila mtu. Ilionekana kama ndoto kutimia pale alipoongeza nyumba na gari hilo katika orodha ya mali zake. Lakini leo, mali hizo zimezeeka, na kwa mujibu wa sheria ya asili, lazima ziporomoke ili nafasi ya nyumba mpya ipatikane.
    Kama mtu yeyote atapatikana akiishi ndani ya jengo hilo kwa hali lilivyo sasa, mtu huyo huonekana kama "mchizi" na huogopwa kama hatari.
    Hakuna kitu duniani kinachostahili kupiganiwa kwa udi na uvumba. Mavazi yako bora ni matambara ya mtu mwingine. Salio lako benki ni mchango wa mtu mwingine kwenye harusi. Mpenzi wako wa sasa ni ex wa mtu mwingine. Kila kahaba unayemuona hotelini au mtaani usiku, aliwahi kuwa bikira. Basi kuna sababu gani ya kugombana? Maisha ni mafupi mno kujiona bora au mkubwa kuliko wengine.
    “Tote tuko uchi mbele ya kifo,” alisema Steve Jobs. Hakuna kitu kinachoweza kutuokoa nacho. Sipendi kuona watu wanaojivuna kwa mali, uzuri, akili, elimu, umaarufu au vitu vya kidunia. Hakuna ulichofanikiwa maishani ambacho wengine hawajawahi kupata. Kitu kimoja tu kinachostahili kujivunia ni: “Maisha ndani ya Mungu Mwenyezi.” Kwa hiyo, kuwa mwema kwa wanadamu wenzako na jenga urafiki kila wakati. Kumbuka kwamba wale uliowakanyaga ukiwa unapaa juu, unaweza kuwakuta tena ukiwa unashuka.
    Hivyo, usiwasababishie wengine shida, maana siku moja, wao ndio watakuwa shida yako. Mwisho, hata mgomba hufikia kukauka na kuwa majani makavu. Usiongozwe na mali za dunia – huchakaa na kufa.

    KUWA MWEMA KILA WAKATI.
    Miaka kadhaa iliyopita, hii ilikuwa nyumba nzuri zaidi katika mtaa huu. Mmiliki wake alikuwa mtu tajiri zaidi ambaye kila mmoja alimtegemea kwa msaada. Gari lake lilikuwa kivutio kwa macho ya kila mtu. Ilionekana kama ndoto kutimia pale alipoongeza nyumba na gari hilo katika orodha ya mali zake. Lakini leo, mali hizo zimezeeka, na kwa mujibu wa sheria ya asili, lazima ziporomoke ili nafasi ya nyumba mpya ipatikane. Kama mtu yeyote atapatikana akiishi ndani ya jengo hilo kwa hali lilivyo sasa, mtu huyo huonekana kama "mchizi" na huogopwa kama hatari. Hakuna kitu duniani kinachostahili kupiganiwa kwa udi na uvumba. Mavazi yako bora ni matambara ya mtu mwingine. Salio lako benki ni mchango wa mtu mwingine kwenye harusi. Mpenzi wako wa sasa ni ex wa mtu mwingine. Kila kahaba unayemuona hotelini au mtaani usiku, aliwahi kuwa bikira. Basi kuna sababu gani ya kugombana? Maisha ni mafupi mno kujiona bora au mkubwa kuliko wengine. “Tote tuko uchi mbele ya kifo,” alisema Steve Jobs. Hakuna kitu kinachoweza kutuokoa nacho. Sipendi kuona watu wanaojivuna kwa mali, uzuri, akili, elimu, umaarufu au vitu vya kidunia. Hakuna ulichofanikiwa maishani ambacho wengine hawajawahi kupata. Kitu kimoja tu kinachostahili kujivunia ni: “Maisha ndani ya Mungu Mwenyezi.” Kwa hiyo, kuwa mwema kwa wanadamu wenzako na jenga urafiki kila wakati. Kumbuka kwamba wale uliowakanyaga ukiwa unapaa juu, unaweza kuwakuta tena ukiwa unashuka. Hivyo, usiwasababishie wengine shida, maana siku moja, wao ndio watakuwa shida yako. Mwisho, hata mgomba hufikia kukauka na kuwa majani makavu. Usiongozwe na mali za dunia – huchakaa na kufa. KUWA MWEMA KILA WAKATI.
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·382 Views
  • Mwanaume huyo pichani, anaitwa Ho Van Lang na picha hizo zilipigwa mara baada ya kugunduliwa mwaka 2013, akiwa ameishi katika msitu wa mbali Nchini Vietnam kwa miaka 41 pamoja na Baba yake, Ho Van Thanh. Walikimbia kijiji chao mwaka 1972 kufuatia mashambulizi ya mabomu ya Marekani wakati wa Vita ya Vietnam ambayo yaliwaua baadhi ya Wanafamilia wao.

    Kwa kuogopa usalama wao, Baba na Mwana walitoweka msituni katika mkoa wa Quang Ngai na wakabaki bila mawasiliano na Jamii kwa miongo kadhaa. Lang, ambaye alikuwa Mtoto mchanga walipotoweka, alitumia maisha yake yote akiwa katika hali ya kutengwa, bila kufahamu chochote kuhusu Dunia ya kisasa.

    Hakuwa na dhana ya Jamii, teknolojia, wala hata uwepo wa Wanawake, jambo alilolielewa tu baada ya kurejeshwa kwenye Jamii. Hadithi yake inaonyesha kwa kina uimara wa Mwanadamu na athari za kutengwa kwa muda mrefu katika maendeleo ya mtu binafsi na mtazamo wake wa Dunia.

    Mwanaume huyo pichani, anaitwa Ho Van Lang na picha hizo zilipigwa mara baada ya kugunduliwa mwaka 2013, akiwa ameishi katika msitu wa mbali Nchini Vietnam 🇻🇳 kwa miaka 41 pamoja na Baba yake, Ho Van Thanh. Walikimbia kijiji chao mwaka 1972 kufuatia mashambulizi ya mabomu ya Marekani 🇺🇸 wakati wa Vita ya Vietnam ambayo yaliwaua baadhi ya Wanafamilia wao. Kwa kuogopa usalama wao, Baba na Mwana walitoweka msituni katika mkoa wa Quang Ngai na wakabaki bila mawasiliano na Jamii kwa miongo kadhaa. Lang, ambaye alikuwa Mtoto mchanga walipotoweka, alitumia maisha yake yote akiwa katika hali ya kutengwa, bila kufahamu chochote kuhusu Dunia ya kisasa. Hakuwa na dhana ya Jamii, teknolojia, wala hata uwepo wa Wanawake, jambo alilolielewa tu baada ya kurejeshwa kwenye Jamii. Hadithi yake inaonyesha kwa kina uimara wa Mwanadamu na athari za kutengwa kwa muda mrefu katika maendeleo ya mtu binafsi na mtazamo wake wa Dunia.
    Like
    Haha
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·567 Views
  • kwa mujibu wa Jarida la Forbes, hii hapa orodha ya Jamii ya Watu Weusi wenye utajiri mkubwa Duniani kwa Mwaka 2025 ambapo wanakadariwa kumiliki utajiri wa dola bilioni 96.2. Wengi wao utajiri wao unatokana sekta za teknolojia, fedha, nishati na burudani, huku Mfanyabiashara Aliko Dangote wa Nigeria akiongoza kwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 23.9.

    1. Aliko Dangote (Nigeria) : $23.9B (Saruji, sukari)
    2. David Steward (Marekani) : $11.4B (Teknolojia)
    3. Robert F. Smith (Marekani) : $10.8B (Uwekezaji binafsi)

    4. Alexander Karp (Marekani) : $8.4B (Programu za uchambuzi wa data)
    5. Mike Adenuga (Nigeria) : $6.8B (Mawasiliano, mafuta)
    6. Abdulsamad Rabiu (Nigeria) : $5.1B (Saruji, sukari)

    7. Michael Jordan (Marekani) : $3.5B (Michezo, matangazo)
    8. Patrice Motsepe (Afrika Kusini) : $3B (Madini)
    9. Oprah Winfrey (Marekani) : $3B (Runinga)

    10. Jay-Z (Marekani) : $2.5B (Muziki, biashara)
    11. Adebayo Ogunlesi (Marekani) :$2.2B (Uwekezaji binafsi)
    12. Magic Johnson (Marekani) : $1.5B (Michezo, uwekezaji)

    13. Femi Otedola (Nigeria) : $1.5B (Nishati)
    14. Tope Awotona (Marekani) : $1.4B (Programu "Calendly")
    15. Tyler Perry (Marekani) : $1.4B (Filamu, Runinga)

    16. Tiger Woods (Marekani) : $1.4B (Gofu)
    17. Rihanna (Barbados) : $1.4B (Muziki, urembo)
    18. Mo Ibrahim (Uingereza) : $1.3B (Mawasiliano)

    19. LeBron James (Marekani) : $1.3B (Kikapu)
    20. Strive Masiyiwa (Zimbabwe) : $1.2B (Mawasiliano)
    21. Michael Lee-Chin (Canada) : $1.1B (Uwekezaji wa fedha)

    22. Herriot Tabuteau (Marekani) : $1.1B (Afya)
    23. Sheila Johnson (Marekani) : $1B (Runinga, hoteli)

    kwa mujibu wa Jarida la Forbes, hii hapa orodha ya Jamii ya Watu Weusi wenye utajiri mkubwa Duniani kwa Mwaka 2025 ambapo wanakadariwa kumiliki utajiri wa dola bilioni 96.2. Wengi wao utajiri wao unatokana sekta za teknolojia, fedha, nishati na burudani, huku Mfanyabiashara Aliko Dangote wa Nigeria 🇳🇬 akiongoza kwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 23.9. 1. Aliko Dangote (Nigeria) : $23.9B (Saruji, sukari) 2. David Steward (Marekani) : $11.4B (Teknolojia) 3. Robert F. Smith (Marekani) : $10.8B (Uwekezaji binafsi) 4. Alexander Karp (Marekani) : $8.4B (Programu za uchambuzi wa data) 5. Mike Adenuga (Nigeria) : $6.8B (Mawasiliano, mafuta) 6. Abdulsamad Rabiu (Nigeria) : $5.1B (Saruji, sukari) 7. Michael Jordan (Marekani) : $3.5B (Michezo, matangazo) 8. Patrice Motsepe (Afrika Kusini) : $3B (Madini) 9. Oprah Winfrey (Marekani) : $3B (Runinga) 10. Jay-Z (Marekani) : $2.5B (Muziki, biashara) 11. Adebayo Ogunlesi (Marekani) :$2.2B (Uwekezaji binafsi) 12. Magic Johnson (Marekani) : $1.5B (Michezo, uwekezaji) 13. Femi Otedola (Nigeria) : $1.5B (Nishati) 14. Tope Awotona (Marekani) : $1.4B (Programu "Calendly") 15. Tyler Perry (Marekani) : $1.4B (Filamu, Runinga) 16. Tiger Woods (Marekani) : $1.4B (Gofu) 17. Rihanna (Barbados) : $1.4B (Muziki, urembo) 18. Mo Ibrahim (Uingereza) : $1.3B (Mawasiliano) 19. LeBron James (Marekani) : $1.3B (Kikapu) 20. Strive Masiyiwa (Zimbabwe) : $1.2B (Mawasiliano) 21. Michael Lee-Chin (Canada) : $1.1B (Uwekezaji wa fedha) 22. Herriot Tabuteau (Marekani) : $1.1B (Afya) 23. Sheila Johnson (Marekani) : $1B (Runinga, hoteli)
    0 Comments ·0 Shares ·549 Views
  • Panya wa kutoka Nchini Tanzania mwenye jina la Ronin ambaye ni maalum kwa kunusa, amefanikiwa kunusa mabomu 109 yaliyotegwa ardhini Nchini Cambodia na kuvunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa mabomu mengi ya ardhini yaliyogunduliwa na Panya Duniani.

    Panya huyo mwenye umri wa miaka mitano (5) amepata vipande 15 vya ziada vya silaha ambazo hazijalipuka tangu kutumwa Nchini Cambodia na Shirila la APOPO, linalofundisha Panya na Mbwa kugundua mabomu ya ardhini na kifua kikuu.

    Ronin alivunja rekodi ya hapo awali, ya Magawa, ambaye aligundua mabomu 71 ya ardhini na vipande vya silaha ambazo hazijalipuka 38 wakati wa kazi yake ya miaka mitano, na alikufa baada ya kustaafu Januari 2022.

    Panya wa kutoka Nchini Tanzania 🇹🇿 mwenye jina la Ronin ambaye ni maalum kwa kunusa, amefanikiwa kunusa mabomu 109 yaliyotegwa ardhini Nchini Cambodia 🇰🇭 na kuvunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa mabomu mengi ya ardhini yaliyogunduliwa na Panya Duniani. Panya huyo mwenye umri wa miaka mitano (5) amepata vipande 15 vya ziada vya silaha ambazo hazijalipuka tangu kutumwa Nchini Cambodia na Shirila la APOPO, linalofundisha Panya na Mbwa kugundua mabomu ya ardhini na kifua kikuu. Ronin alivunja rekodi ya hapo awali, ya Magawa, ambaye aligundua mabomu 71 ya ardhini na vipande vya silaha ambazo hazijalipuka 38 wakati wa kazi yake ya miaka mitano, na alikufa baada ya kustaafu Januari 2022.
    0 Comments ·0 Shares ·453 Views
  • Muigizaji maarufu na Mkongwe Duniani, Jean-Claude Van Damme anakabiliwa na mashtaka ya kujibu baada ya kudaiwa kufanya ngono na Wanawake waliotekwa nyara Nchini Romania .

    Kwa mujibu wa CNN, Idara ya Romania ya Uchunguzi wa Uhalifu wa kupangwa na Ugaidi (DIICOT) imewasilisha malalamiko ya jinai dhidi ya Van Damme, ikidai alifanya ngono kwa kujua na Wanawake kadhaa waliokuwa wakitumiwa katika biashara haramu ya ngono.

    Kulingana na ripoti hiyo, Mwigizaji huyo Raia wa Ubelgiji anadaiwa kukutana na Watu kadhaa ambao pia wanachunguzwa kwa uhalifu wa usafirishaji wa Binadamu, ambao walimpa fursa ya kufanya ngono na Wanamitindo watano (5) wa Kiromania kama zawadi.

    Tukio hilo linaripotiwa kutokea Cannes Nchini Ufaransa hivyo, Serikali ya hiyo inapaswa kuidhinisha mashitaka hayo ya jinai lakini haikuwekwa wazi ni lini tukio hilo lilitokea hapo Ufaransa.

    Muigizaji maarufu na Mkongwe Duniani, Jean-Claude Van Damme anakabiliwa na mashtaka ya kujibu baada ya kudaiwa kufanya ngono na Wanawake waliotekwa nyara Nchini Romania 🇷🇴. Kwa mujibu wa CNN, Idara ya Romania ya Uchunguzi wa Uhalifu wa kupangwa na Ugaidi (DIICOT) imewasilisha malalamiko ya jinai dhidi ya Van Damme, ikidai alifanya ngono kwa kujua na Wanawake kadhaa waliokuwa wakitumiwa katika biashara haramu ya ngono. Kulingana na ripoti hiyo, Mwigizaji huyo Raia wa Ubelgiji 🇧🇪 anadaiwa kukutana na Watu kadhaa ambao pia wanachunguzwa kwa uhalifu wa usafirishaji wa Binadamu, ambao walimpa fursa ya kufanya ngono na Wanamitindo watano (5) wa Kiromania kama zawadi. Tukio hilo linaripotiwa kutokea Cannes Nchini Ufaransa 🇫🇷 hivyo, Serikali ya hiyo inapaswa kuidhinisha mashitaka hayo ya jinai lakini haikuwekwa wazi ni lini tukio hilo lilitokea hapo Ufaransa.
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·428 Views
  • Uongozi wa Ligi Kuu ya mpira wa miguu Nchini Marekani , Major League Soccer (MLS), umempiga marufuku Mlinzi binafsi (Bodyguard) wa Lionel Messi, Yassine Cheuko, kuwa kando na kuingia katikati ya Uwanja wakati wa mechi za Inter Miami kwa lengo lake la kumlinda Mwajiri wake Messi.

    Ikumbukwe kwamba Yassine Cheuko, ni Mwanajeshi wa zamani wa kikosi maalumu cha operesheni za kijeshi cha Jeshi la Majini la Marekani (U.S. Navy) kinachobobea katika vita visivyo vya kawaida, kupambana na ugaidi, mashambulizi ya moja kwa moja, na upelelezi wa kijeshi. Tangu Yessine Cheuko aanze kufanya kazi na Messi amejizolea umaarufu mkubwa Duniani kwani ameonekana mara nyingi akiwadhibiti Wavamizi mbalimbali ambao wengi lengo lao huwa sio baya, zaidi wanataka kupiga picha na Messi.

    Tayari uongozi wa Ligi hiyo umemzuia kuingia Uwanjani, sasa ataruhusiwa tu kuwa kwenye Vyumba vya kubadilishia nguo na maeneo ya Waandishi wa habari siku za mechi. Uamuzi huu ni sehemu ya mpango wa (MLS) wa kuchukua mamlaka kamili ya usalama wa mechi.

    Baada ya katazo, Yassine Cheuko ameonyesha kutoridhishwa na hatua hiyo, akisema kuwa Wavamizi wa Uwanja ni tatizo kubwa zaidi Nchini Marekani kuliko Ulaya. Kwa mujibu wake, katika miaka saba aliyofanya kazi Ulaya, kulikuwa na matukio sita pekee ya uvamizi Uwanjani, ilhali katika miezi 20 Nchini Marekani, tayari yameshuhudiwa matukio 16.

    Mlinzi huyo ameendelea kusema kuwa Uongozi wa Ligi Kuu ya Marekani haukutakiwa kumzuia kufanye kazi yake bali walitakiwa kumpa ushirikiano ili kazi hiyo waifanye kwa pamoja kwa sababu eti kipindi yupo barani Ulaya, alipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwenye Uongozi na alifanya kazi yake kwa uhuru. Pamoja na kuzuiliwa kuingia Uwanjani au kukaa kando ya Uwanja, Cheuko amesema kuwa ataendelea kufanya kazi yake kama kawaida bila kuvunja sheria au utaratibu uliopo kwenye mchezo wa mpira wa miguu.

    Uongozi wa Ligi Kuu ya mpira wa miguu Nchini Marekani 🇺🇸, Major League Soccer (MLS), umempiga marufuku Mlinzi binafsi (Bodyguard) wa Lionel Messi, Yassine Cheuko, kuwa kando na kuingia katikati ya Uwanja wakati wa mechi za Inter Miami kwa lengo lake la kumlinda Mwajiri wake Messi. Ikumbukwe kwamba Yassine Cheuko, ni Mwanajeshi wa zamani wa kikosi maalumu cha operesheni za kijeshi cha Jeshi la Majini la Marekani (U.S. Navy) kinachobobea katika vita visivyo vya kawaida, kupambana na ugaidi, mashambulizi ya moja kwa moja, na upelelezi wa kijeshi. Tangu Yessine Cheuko aanze kufanya kazi na Messi amejizolea umaarufu mkubwa Duniani kwani ameonekana mara nyingi akiwadhibiti Wavamizi mbalimbali ambao wengi lengo lao huwa sio baya, zaidi wanataka kupiga picha na Messi. Tayari uongozi wa Ligi hiyo umemzuia kuingia Uwanjani, sasa ataruhusiwa tu kuwa kwenye Vyumba vya kubadilishia nguo na maeneo ya Waandishi wa habari siku za mechi. Uamuzi huu ni sehemu ya mpango wa (MLS) wa kuchukua mamlaka kamili ya usalama wa mechi. Baada ya katazo, Yassine Cheuko ameonyesha kutoridhishwa na hatua hiyo, akisema kuwa Wavamizi wa Uwanja ni tatizo kubwa zaidi Nchini Marekani kuliko Ulaya. Kwa mujibu wake, katika miaka saba aliyofanya kazi Ulaya, kulikuwa na matukio sita pekee ya uvamizi Uwanjani, ilhali katika miezi 20 Nchini Marekani, tayari yameshuhudiwa matukio 16. Mlinzi huyo ameendelea kusema kuwa Uongozi wa Ligi Kuu ya Marekani haukutakiwa kumzuia kufanye kazi yake bali walitakiwa kumpa ushirikiano ili kazi hiyo waifanye kwa pamoja kwa sababu eti kipindi yupo barani Ulaya, alipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwenye Uongozi na alifanya kazi yake kwa uhuru. Pamoja na kuzuiliwa kuingia Uwanjani au kukaa kando ya Uwanja, Cheuko amesema kuwa ataendelea kufanya kazi yake kama kawaida bila kuvunja sheria au utaratibu uliopo kwenye mchezo wa mpira wa miguu.
    0 Comments ·0 Shares ·649 Views
  • Mke wa Mchezaji wa kimataifa wa Burkina Faso n'a klabu ya Yanga SC, Hamisa Mobetto (Tanzania ) ameingia kwenye orodha ya WAGS (Wives And Girlfriends of Footballers) ambao ni Wake (Wapenzi au Wachumba) wa Wachezaji wenye Wafuasi (followers) wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram Duniani.

    1. @georginagio (Mrs. Ronaldo) :+65.5M
    2. antonelaroccuzzo (Mrs. Messi) : +39.9M
    3. @iambeckyg (Mrs. Sebastian) : +37.2M
    4. @victoriabeckham (Mrs. Beckham) : +32.9M
    5. @perrieedwards (Mrs. Alex) :+19M

    6. @alishalehmann7 (Mrs. Douglas Luiz) : +16.6M
    7. @brunabiancardi (Mrs. Neymar Jr) : +13.6M
    8. @hamisamobetto (Mrs. Aziz Ki) : +12.1M
    9. @pilarrubio (Mrs. Sergio Ramos) : +11.1M
    10. @leighannepinnock (Mrs. Andre Gray) : +10M

    Mke wa Mchezaji wa kimataifa wa Burkina Faso 🇧🇫 n'a klabu ya Yanga SC, Hamisa Mobetto (Tanzania 🇹🇿) ameingia kwenye orodha ya WAGS (Wives And Girlfriends of Footballers) ambao ni Wake (Wapenzi au Wachumba) wa Wachezaji wenye Wafuasi (followers) wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram Duniani. 1. @georginagio (Mrs. Ronaldo) :+65.5M 2. antonelaroccuzzo (Mrs. Messi) : +39.9M 3. @iambeckyg (Mrs. Sebastian) : +37.2M 4. @victoriabeckham (Mrs. Beckham) : +32.9M 5. @perrieedwards (Mrs. Alex) :+19M 6. @alishalehmann7 (Mrs. Douglas Luiz) : +16.6M 7. @brunabiancardi (Mrs. Neymar Jr) : +13.6M 8. @hamisamobetto (Mrs. Aziz Ki) : +12.1M 9. @pilarrubio (Mrs. Sergio Ramos) : +11.1M 10. @leighannepinnock (Mrs. Andre Gray) : +10M
    0 Comments ·0 Shares ·675 Views
  • Jarida la Forbes toleo la mwaka huu wa 2025 limemtaja Manyabiashara wa Tanzania Mohamed Dewjl, kuwa miongoni mwa Watu Matajiri Duniani, akiwa na utajiri wa USD 2.2 bilioni sawa na Shilingi Trilioni 5.7 za Kitanzania. Mo Dewji, anakuwa tajiri namba 12 barani Afrika na namba moja Afrika Mashariki kwa kiwango hicho.

    2. Orodha ya mwaka huu inaonyesha utajiri wa Mo
    Dewji umeongezeka na kufikia, dola bilioni 2.2 kutoka dola bilioni 1.8 mwaka jana.

    3. Orodha ya Forbes ya Matajiri wa Afrika kwa mwaka 2024 ilibainisha kuwa utajiri wa Mo Dewji umeongezeka kutoka dola bilioni 1.5 hadi bilioni 1.8.

    4. Licha ya utajiri huo, MO Dewji kupitia kampuni ya Mohamed Entrprises Limited (MeTL) imezalisha ajira 40,000 kwa Watanzania, kupitia biashara 126 zinazofanywa na kampuni hiyo.

    5. Lengo la Mo Dewji ni kuongeza ajira hadi kufikia laki moja kwa Watanzania na wana-Afrika Mashariki.

    6. Mo Dewji kupitia MoDewjl Foundation, imeshirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Maji, kuchimba visima, kukarabati na kutibu maji mkakati uliosaidia Watu zaidi ya 15,000 kupata maji salama ya kunywa.

    7. Utajiri wa Mo Dewji haikushia kwenye maji na afya pekee, umekwenda zaidi na kuwekeza katika tasnia ya michezo ambako ni sehemu ya Mmiliki akiwekeza
    asilimia 49 kwenye klabu ya Simba SC.

    Jarida la Forbes toleo la mwaka huu wa 2025 limemtaja Manyabiashara wa Tanzania Mohamed Dewjl, kuwa miongoni mwa Watu Matajiri Duniani, akiwa na utajiri wa USD 2.2 bilioni sawa na Shilingi Trilioni 5.7 za Kitanzania. Mo Dewji, anakuwa tajiri namba 12 barani Afrika na namba moja Afrika Mashariki kwa kiwango hicho. 2. Orodha ya mwaka huu inaonyesha utajiri wa Mo Dewji umeongezeka na kufikia, dola bilioni 2.2 kutoka dola bilioni 1.8 mwaka jana. 3. Orodha ya Forbes ya Matajiri wa Afrika kwa mwaka 2024 ilibainisha kuwa utajiri wa Mo Dewji umeongezeka kutoka dola bilioni 1.5 hadi bilioni 1.8. 4. Licha ya utajiri huo, MO Dewji kupitia kampuni ya Mohamed Entrprises Limited (MeTL) imezalisha ajira 40,000 kwa Watanzania, kupitia biashara 126 zinazofanywa na kampuni hiyo. 5. Lengo la Mo Dewji ni kuongeza ajira hadi kufikia laki moja kwa Watanzania na wana-Afrika Mashariki. 6. Mo Dewji kupitia MoDewjl Foundation, imeshirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Maji, kuchimba visima, kukarabati na kutibu maji mkakati uliosaidia Watu zaidi ya 15,000 kupata maji salama ya kunywa. 7. Utajiri wa Mo Dewji haikushia kwenye maji na afya pekee, umekwenda zaidi na kuwekeza katika tasnia ya michezo ambako ni sehemu ya Mmiliki akiwekeza asilimia 49 kwenye klabu ya Simba SC.
    0 Comments ·0 Shares ·494 Views
  • Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) limetangaza zawadi zitakazotolewa kwa Washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu (FIFA CLUB WORLD CUP), ambapo bingwa wa michuano hiyo atapata dola milioni 125 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 300 za kitanzania huku kukitarajiwa kutolewa jumla ya dola bilioni 1 kwa klabu 32 zitakavyoshiriki na dola milioni 250 zitatolewa kwa mashirikisho kwa ajili kukuza mpira wa miguu kwa ngazi ya klabu Duniani.

    Shirikisho hilo limepanga kutoa dola milioni 250 ili kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu kwa kiwango cha kimataifa ambapo fedha hizi zitatumika kusaidia klabu ndogo, kuboresha miundombinu, kuwekeza katika mafunzo ya Wachezaji na Makocha pamoja na kuimarisha ushirikiano wa klabu kimataifa.

    Aidha, pango huu unalenga kuhakikisha kuwa maendeleo ya mpira wa miguu hayaishii kwa klabu kubwa pekee, bali pia yanawanufaisha hadi klabu dogo na kuinua mpira wa Duniani kote. FIFA pia imesisitiza kuwa, mapato yote ya mashindano haya yatasambazwa kwa klabu bila kugusa akiba yake, ambayo inatumiwa kwa maendeleo ya mpira wa miguu kupitia Vyama (211) Wanachama wa FIFA.

    Mfumo huu ni mkubwa zaidi katika historia ya mpira wa miguu, ukiwa na mechi saba (7) kwenye hatua ya makundi na mfumo wa mchujo.

    Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) limetangaza zawadi zitakazotolewa kwa Washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu (FIFA CLUB WORLD CUP), ambapo bingwa wa michuano hiyo atapata dola milioni 125 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 300 za kitanzania huku kukitarajiwa kutolewa jumla ya dola bilioni 1 kwa klabu 32 zitakavyoshiriki na dola milioni 250 zitatolewa kwa mashirikisho kwa ajili kukuza mpira wa miguu kwa ngazi ya klabu Duniani. Shirikisho hilo limepanga kutoa dola milioni 250 ili kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu kwa kiwango cha kimataifa ambapo fedha hizi zitatumika kusaidia klabu ndogo, kuboresha miundombinu, kuwekeza katika mafunzo ya Wachezaji na Makocha pamoja na kuimarisha ushirikiano wa klabu kimataifa. Aidha, pango huu unalenga kuhakikisha kuwa maendeleo ya mpira wa miguu hayaishii kwa klabu kubwa pekee, bali pia yanawanufaisha hadi klabu dogo na kuinua mpira wa Duniani kote. FIFA pia imesisitiza kuwa, mapato yote ya mashindano haya yatasambazwa kwa klabu bila kugusa akiba yake, ambayo inatumiwa kwa maendeleo ya mpira wa miguu kupitia Vyama (211) Wanachama wa FIFA. Mfumo huu ni mkubwa zaidi katika historia ya mpira wa miguu, ukiwa na mechi saba (7) kwenye hatua ya makundi na mfumo wa mchujo.
    0 Comments ·0 Shares ·568 Views
  • Rais wa Nchi Burkina Faso , Kapteni IbrahimTraoré (37) amekataa ongezeko lolote kwenye mshahara wake anaoupata kama kapteni, akisisitiza kuwa anajitolea kwa ajili ya Wananchi wa Nchi hiyo.

    Rais huyo kijana zaidi Duniani, ambaye alichukua madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi, alitangaza kuwa makadirio ya utajiri wake wote ni Shilingi milioni 340 za Kitanzania na ataendelea kupokea mshahara wake uleule wa kawaida kama kapteni wa Jeshi.

    Uamuzi huo wa kukataa ongezeko la mshahara ni tofauti kubwa na hatua za baadhi ya watangulizi wake, ambapo anaonyesha taswira ya Uongozi mpya kabisa katika Nchi ya Burkina Faso.

    Rais wa Nchi Burkina Faso 🇧🇫, Kapteni IbrahimTraoré (37) amekataa ongezeko lolote kwenye mshahara wake anaoupata kama kapteni, akisisitiza kuwa anajitolea kwa ajili ya Wananchi wa Nchi hiyo. Rais huyo kijana zaidi Duniani, ambaye alichukua madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi, alitangaza kuwa makadirio ya utajiri wake wote ni Shilingi milioni 340 za Kitanzania na ataendelea kupokea mshahara wake uleule wa kawaida kama kapteni wa Jeshi. Uamuzi huo wa kukataa ongezeko la mshahara ni tofauti kubwa na hatua za baadhi ya watangulizi wake, ambapo anaonyesha taswira ya Uongozi mpya kabisa katika Nchi ya Burkina Faso.
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·493 Views
  • Mchambuzi Farhan JR.

    Nimeona andiko la Waukae @zakazakazi kuhusu TFF kutengeneza Vijana ambalo lilipaswa kuwa jukumu la Klabu na akienda mbali kusema kwamba TFF ndio Shirikisho pekee duniani ambalo lina kituo ambacho kinazalisha na kulea vipaji vya vijana, kwanza kabla ya kupingana nae kuna kitu kwanza nataka kukiweka sawa kwenye eneo hilo.

    Duniani kote Mashirikisho kama TFF yamejikita zaidi kwenye DEVELOPMENT PROJECTS yaani Miradi ya maendeleo kisha wakaachia Mashindano kadhaa yasimamiwe na Bodi zao za Ligi kwa 90% bila kuyaingilia, TFF anachokifanya ni sahihi lakini pia sio sahihi sana kufanya yeye alipaswa kuwa na CLINICS tu ila kuna changamoto sehemu ambayo imeletwa na TFF wenyewe.

    Duniani Klabu zinaweza kuendesha miradi ya Vijana kwasababu kuna kitu kinaitwa FALSAFA ya nchi kwenye mpira, kuanzia mifumo, afya tiba, afya lishe na miundo yote ambayo portifolio hutoka Shirikisho (TFF) Klabu zinaenda kutekeleza mifumo hiyo na kuadjust baadhi ya maeneo halafu Vijana wakienda Clinics za Kitaifa wanaenda kukazia tu.

    Swali linakuja Je Waukaye @zakazakazi FALSAFA ya Tanzania kwenye mpira wa Miguu ni ipi? Iliwasilishwa lini? Anayo nani? Hilo ni Jukumu la TFF ambalo halijatekelezwa, kuna kitu kinaitwa TALENT ID FRAMEWORK ili kupata Vijana je tunayo? Ipoje, anayo nani? Inasemaje? Klabu hazina Mwongozo kutoka kwa TFF? Academy zote nchini zipite humo LAZIMA TFF wafanye wanachoweza, tupo katikati, TFF ASIMAMIE HILO KIKAMILIFU.

    TFF wasiende mbali waende tu hapo Uganda ilipo FUFA, wana Talent ID Framework ambayo Mashirikisho yoote yalipigwa huo Msasa sambamba na Kamati zao tendaji, ndio maana Uganda wapo mbali mno kwenye soka la Vijana kwenye Klabu zao na National Team, kwasababu wana ramani wanaifuata, wameintergrate mfumo wao na FIFA Talent Development Schemes (TDS) je sisi lini tutaforce Klabu zipite humo?

    TFF anajipa majukumu ambayo mengine sio ya kwake, kujadili mikataba ya kibiashara sio Jukumu lake bali Vilabu na Bodi yao, TFF anabaki kama Baba pekee, duniani kote TFF zao zina majukumu yao ukitoa michuano ya FA na Ngao basi Ligi Kuu sio mali yao, TFF ASIMAMIE HASWA JUKUMU LA MAENDELEO NI LAKE.

    Mchambuzi Farhan JR. Nimeona andiko la Waukae @zakazakazi kuhusu TFF kutengeneza Vijana ambalo lilipaswa kuwa jukumu la Klabu na akienda mbali kusema kwamba TFF ndio Shirikisho pekee duniani ambalo lina kituo ambacho kinazalisha na kulea vipaji vya vijana, kwanza kabla ya kupingana nae kuna kitu kwanza nataka kukiweka sawa kwenye eneo hilo. Duniani kote Mashirikisho kama TFF yamejikita zaidi kwenye DEVELOPMENT PROJECTS yaani Miradi ya maendeleo kisha wakaachia Mashindano kadhaa yasimamiwe na Bodi zao za Ligi kwa 90% bila kuyaingilia, TFF anachokifanya ni sahihi lakini pia sio sahihi sana kufanya yeye alipaswa kuwa na CLINICS tu ila kuna changamoto sehemu ambayo imeletwa na TFF wenyewe. Duniani Klabu zinaweza kuendesha miradi ya Vijana kwasababu kuna kitu kinaitwa FALSAFA ya nchi kwenye mpira, kuanzia mifumo, afya tiba, afya lishe na miundo yote ambayo portifolio hutoka Shirikisho (TFF) Klabu zinaenda kutekeleza mifumo hiyo na kuadjust baadhi ya maeneo halafu Vijana wakienda Clinics za Kitaifa wanaenda kukazia tu. Swali linakuja Je Waukaye @zakazakazi FALSAFA ya Tanzania kwenye mpira wa Miguu ni ipi? Iliwasilishwa lini? Anayo nani? Hilo ni Jukumu la TFF ambalo halijatekelezwa, kuna kitu kinaitwa TALENT ID FRAMEWORK ili kupata Vijana je tunayo? Ipoje, anayo nani? Inasemaje? Klabu hazina Mwongozo kutoka kwa TFF? Academy zote nchini zipite humo LAZIMA TFF wafanye wanachoweza, tupo katikati, TFF ASIMAMIE HILO KIKAMILIFU. TFF wasiende mbali waende tu hapo Uganda ilipo FUFA, wana Talent ID Framework ambayo Mashirikisho yoote yalipigwa huo Msasa sambamba na Kamati zao tendaji, ndio maana Uganda wapo mbali mno kwenye soka la Vijana kwenye Klabu zao na National Team, kwasababu wana ramani wanaifuata, wameintergrate mfumo wao na FIFA Talent Development Schemes (TDS) je sisi lini tutaforce Klabu zipite humo? TFF anajipa majukumu ambayo mengine sio ya kwake, kujadili mikataba ya kibiashara sio Jukumu lake bali Vilabu na Bodi yao, TFF anabaki kama Baba pekee, duniani kote TFF zao zina majukumu yao ukitoa michuano ya FA na Ngao basi Ligi Kuu sio mali yao, TFF ASIMAMIE HASWA JUKUMU LA MAENDELEO NI LAKE.
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·605 Views
  • Zungu

    Miaka miwili ya Rais Ibrahim Traore wa Burkina Faso: na hii ni Ripoti tangu kuchukua uongozi wa Taifa hilo la Afrika Magharibi

    1. GDP ya Burkina Faso iliongezeka kutoka karibu dola bilioni 18.8 hadi $ 22.1 bilioni.

    2. Alikataa mikopo kutoka kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, akisema, "Afrika haiitaji Benki ya Dunia, IMF, Ulaya, au Amerika."

    3. Alikata mishahara ya mawaziri na wabunge kwa 30% wakati akiinua mishahara ya wafanyikazi wa umma na 50%.

    4. Alisafisha deni la ndani la Burkina Faso.

    5. Alianzisha mimea ya kwanza ya usindikaji wa nyanya.

    6. Mnamo 2023, alizindua mgodi wa dhahabu wa kisasa ili kuimarisha uwezo wa usindikaji wa ndani.

    7. Alisimamisha usafirishaji wa dhahabu isiyo wazi kutoka Burkina Faso kwenda Ulaya.

    8. Aliunda mmea wa pili wa usindikaji wa pamba wa Burkina Faso, na kuongeza kwenye ile iliyopo.

    9. Alianzisha Kituo cha Msaada wa Kitaifa cha Usindikaji wa Pamba ya Artisanal, wa kwanza wa aina yake, kusaidia wakulima wa pamba wa ndani.

    10. Alikataza matumizi ya wigs za kisheria za Uingereza na gauni katika korti za mitaa, na kuzibadilisha na mavazi ya jadi ya burkinabé.

    11. Alitanguliza kilimo kwa kusambaza matrekta zaidi ya 400, viboreshaji 239, pampu 710 za gari, na pikipiki 714 ili kuongeza uzalishaji na kusaidia jamii za vijijini.

    12. Aliwezesha ufikiaji wa mbegu zilizoboreshwa na pembejeo zingine za kilimo ili kuongeza mavuno ya kilimo.

    Uzalishaji wa nyanya ulikua kutoka tani 315,000 za tani mnamo 2022 hadi tani 360,000 za tani mnamo 2024.

    Uzalishaji wa Millet uliongezeka kutoka tani 907,000 za tani 2022 hadi tani milioni 1.1 mnamo 2024.

    15. Uzalishaji wa mchele uliongezeka kutoka tani 280,000 za tani 2022 hadi tani 326,000 mnamo 2024.

    16. Alipiga marufuku shughuli za kijeshi za Ufaransa huko Burkina Faso.

    17. Alikataza vyombo vya habari vya Ufaransa kufanya kazi nchini.

    18. Aliwafukuza askari wa Ufaransa kutoka Burkina Faso.

    19. Serikali yake inaunda barabara mpya, kupanua zile zilizopo, na kubadilisha barabara za changarawe kuwa nyuso za lami.

    20. Anajenga kinu kikubwa cha nyuklia kwa ajili ya umeme wa uhakika wa nchi yake ya Burkina faso

    Zungu ✍️ Miaka miwili ya Rais Ibrahim Traore wa Burkina Faso: na hii ni Ripoti tangu kuchukua uongozi wa Taifa hilo la Afrika Magharibi 1. GDP ya Burkina Faso iliongezeka kutoka karibu dola bilioni 18.8 hadi $ 22.1 bilioni. 2. Alikataa mikopo kutoka kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, akisema, "Afrika haiitaji Benki ya Dunia, IMF, Ulaya, au Amerika." 3. Alikata mishahara ya mawaziri na wabunge kwa 30% wakati akiinua mishahara ya wafanyikazi wa umma na 50%. 4. Alisafisha deni la ndani la Burkina Faso. 5. Alianzisha mimea ya kwanza ya usindikaji wa nyanya. 6. Mnamo 2023, alizindua mgodi wa dhahabu wa kisasa ili kuimarisha uwezo wa usindikaji wa ndani. 7. Alisimamisha usafirishaji wa dhahabu isiyo wazi kutoka Burkina Faso kwenda Ulaya. 8. Aliunda mmea wa pili wa usindikaji wa pamba wa Burkina Faso, na kuongeza kwenye ile iliyopo. 9. Alianzisha Kituo cha Msaada wa Kitaifa cha Usindikaji wa Pamba ya Artisanal, wa kwanza wa aina yake, kusaidia wakulima wa pamba wa ndani. 10. Alikataza matumizi ya wigs za kisheria za Uingereza na gauni katika korti za mitaa, na kuzibadilisha na mavazi ya jadi ya burkinabé. 11. Alitanguliza kilimo kwa kusambaza matrekta zaidi ya 400, viboreshaji 239, pampu 710 za gari, na pikipiki 714 ili kuongeza uzalishaji na kusaidia jamii za vijijini. 12. Aliwezesha ufikiaji wa mbegu zilizoboreshwa na pembejeo zingine za kilimo ili kuongeza mavuno ya kilimo. Uzalishaji wa nyanya ulikua kutoka tani 315,000 za tani mnamo 2022 hadi tani 360,000 za tani mnamo 2024. Uzalishaji wa Millet uliongezeka kutoka tani 907,000 za tani 2022 hadi tani milioni 1.1 mnamo 2024. 15. Uzalishaji wa mchele uliongezeka kutoka tani 280,000 za tani 2022 hadi tani 326,000 mnamo 2024. 16. Alipiga marufuku shughuli za kijeshi za Ufaransa huko Burkina Faso. 17. Alikataza vyombo vya habari vya Ufaransa kufanya kazi nchini. 18. Aliwafukuza askari wa Ufaransa kutoka Burkina Faso. 19. Serikali yake inaunda barabara mpya, kupanua zile zilizopo, na kubadilisha barabara za changarawe kuwa nyuso za lami. 20. Anajenga kinu kikubwa cha nyuklia kwa ajili ya umeme wa uhakika wa nchi yake ya Burkina faso
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·628 Views
  • "Sijui kama mnaona jinsi Trump na Marekani yake wanavyocheza na Dunia kupitia ugomvi au migogoro ya Dunia ili kuipatia faida Marekani kwa kisingizio cha kutafuta amani huku nyuma ya pazia Marekani ikipata faida kupitia migogoro au vita.

    Tazama Makubaliano ya Madini pale Ukraine
    Ambapo Marekani watafaidika na Rasilimali za madini za Ukraine, yani ili Marekani waisadie Ukraine ni lazima Ukraine kuipatia madini yake Marekani

    Congo nayo inakaribia kusaini mkataba wa kuipatia Marekani madini ili Marekani iipatie ulinzi hapo tunazungumzia rasimali za Congo amabzo zinaenda kutumika kama faida kwa Marekani kisa tu ni ugomvi wa Afrika wenyewe kwa wenyewe na hapo hapo Trump katupiga Bao

    Huko Gaza napo mpango wa kuwahamisha wakazi wa Gaza kwa kisingizio cha kuijenga upya Gaza umeiva, Trump haijengi Gaza bure anafahamu fika kuwa chini ya ardhi ya Gaza kuna utajiri mkubwa wa maliasili ya Gesi na mafuta

    Huyo ndiye Trump mfanyabiashara kutoka White House ambaye anaenda sambamba na ule msemo unaosema "no free lunch in America" yaani hakuna chakula cha mchana cha bure Marekani, ukiona unapewa cha bure ujue badae utalipia tu!!" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.

    "Sijui kama mnaona jinsi Trump na Marekani yake wanavyocheza na Dunia kupitia ugomvi au migogoro ya Dunia ili kuipatia faida Marekani kwa kisingizio cha kutafuta amani huku nyuma ya pazia Marekani ikipata faida kupitia migogoro au vita. Tazama Makubaliano ya Madini pale Ukraine Ambapo Marekani watafaidika na Rasilimali za madini za Ukraine, yani ili Marekani waisadie Ukraine ni lazima Ukraine kuipatia madini yake Marekani Congo nayo inakaribia kusaini mkataba wa kuipatia Marekani madini ili Marekani iipatie ulinzi hapo tunazungumzia rasimali za Congo amabzo zinaenda kutumika kama faida kwa Marekani kisa tu ni ugomvi wa Afrika wenyewe kwa wenyewe na hapo hapo Trump katupiga Bao Huko Gaza napo mpango wa kuwahamisha wakazi wa Gaza kwa kisingizio cha kuijenga upya Gaza umeiva, Trump haijengi Gaza bure anafahamu fika kuwa chini ya ardhi ya Gaza kuna utajiri mkubwa wa maliasili ya Gesi na mafuta Huyo ndiye Trump mfanyabiashara kutoka White House ambaye anaenda sambamba na ule msemo unaosema "no free lunch in America" yaani hakuna chakula cha mchana cha bure Marekani, ukiona unapewa cha bure ujue badae utalipia tu!!" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.
    0 Comments ·0 Shares ·407 Views
  • Kwa mujibu wa Magazeti Nchini Burkina Faso , Aziz K alitoa sharti la kusafiri na Mke wake Hamisa Mobeto kwenda kuitumikia Timu ya Taifa (Les Étalons) na alipiwe gharama zote za safari hadi Nchini Burkina Faso. Lakini Jambo ambalo lilikaliwa na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Burkina Faso, Brama Traoré.

    Ikumbukwe kwamba Kocha Traoré alitangaza kikosi chake kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026 huku Aziz K hajaitwa. Timu ya Taifa ya Burkina Faso inajiandaa na mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Djibouti Machi 21, na baadae itacheza dhidi ya Timu ya Taifa ya Guinea-Bissau Machi 24, 2025

    Burkina Faso wapo nafasi ya 3 wakiwa na alama tano 5, katika kundi A linaloongozwa na Misri wenye alama 10.

    Kwa mujibu wa Magazeti Nchini Burkina Faso 🇧🇫, Aziz K alitoa sharti la kusafiri na Mke wake Hamisa Mobeto kwenda kuitumikia Timu ya Taifa (Les Étalons) na alipiwe gharama zote za safari hadi Nchini Burkina Faso. Lakini Jambo ambalo lilikaliwa na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Burkina Faso, Brama Traoré. Ikumbukwe kwamba Kocha Traoré alitangaza kikosi chake kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026 huku Aziz K hajaitwa. Timu ya Taifa ya Burkina Faso inajiandaa na mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Djibouti 🇩🇯 Machi 21, na baadae itacheza dhidi ya Timu ya Taifa ya Guinea-Bissau 🇬🇼 Machi 24, 2025 Burkina Faso 🇧🇫 wapo nafasi ya 3 wakiwa na alama tano 5, katika kundi A linaloongozwa na Misri 🇪🇬 wenye alama 10.
    0 Comments ·0 Shares ·271 Views
More Results